Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1157 | 1158 | (Page 1159) | 1160 | 1161 | .... | 1896 | newer

  0 0  MOSHI SHABANI MALLEMA

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewataka wasimamizi wa miradi ya matengenezo ya barabara kuzingatia taaluma na weledi husika ili kupata thamani ya fedha kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu husika bila kukiuka taratibu za manunuzi.
  RC Makonda ameyasema hayo alipokuwa anafungua kikao cha bodi ya barabara ya mkoa wa Dar es Salaam kilichofanyika katika ukumbi wa Arnautoglo na kuwaomba mameya, madiwani, wakuu wa wilaya na wakurugenzi kuifuatilia miradi hii kwa karibu, huku akishauri kuwa ni vyema miradi hii ikafanyika kwa gharama nafuu, kwa muda mfupi na kwa viwango, kwani fedha za wananchi ndiyo zinatumika wanapaswa kutendewa haki kwa kuona matokeo chanya kwenye miradi ya maendeleo.
  Huku akisisitiza kuwa katika maslahi ya wananchi hatoangalia anagombana na wangapi, atahakikisha anatimiza wajibu wake.
  Katika hatua nyingine kampuni ya ujenzi ya IBRA Contractors Limited kupitia Mkurugenzi wake Maida Waziri ameeleza kuhusu ujenzi wa barabara zinazotumia teknolojia ya kisasa kwa udongo wa kawaida ni bora na huweza kudumu zaidi ya miaka 10, haina vumbi wala uterezi na ujenzi wake hutumia muda mfupi na kuishauri serikali kutumia ujenzi huo wa gharama nafuu kwa takribani asilimia 50, huku akizitolea mfano Australia na Algeria kuanza kutumia ujenzi huo, hivyo hiyo ni suluhu ya lawama za muda mrefu kuhusu barabara mbovu nchini.
  Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa ujenzi huo wa kibunifu utakuwa njia ya kuvifanya vijiji kuwa miji kupitia barabara.

  Bwana Fabian Campagnolo kutoka kampuni ya ujenzi ya IBRA Contractors Limited , akitoa maelezo kwa wajumbe wa kikao hicho cha barabara , kuhusu ujenzi wa barabara zinazotumia teknolojia ya kisasa kwa udongo wa kawaida ni bora na huweza kudumu zaidi ya miaka 10, katika ukumbi wa Arnautoglo

  0 0  0 0


  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

  Utekelezaji wa operesheni hiyo umeanza kufanyika leo baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba alipotangaza marufuku hiyo Februari 20 juu ya vileo vilivyo katika vifungashio viondoke katika mzunguko wa biashara na watengenezaji wahamie katika mfumo wa chupa kwa kuanzia milimita 250.

  Operesheni ya kukamata viroba imeanza leo jijini Dar es Salaam ikisimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais Katika Kiwanda cha Kampun ya nyati spirit kilichopo Vingunguti ambapo katoni za viroba 7067 aina ya nyati  zimekutwa katika kiwanda hicho.

  Akizungumza katika operesheni Meneja wa Kanda ya Magharibi wa Mamlaka ya Dawa na Chakula (TFDA ), Emmanuel Alphonce amesema operesheni imeanzia jiji la Dar es Salaam na kesho itaendelea nchi nzima chini ya Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya na Mikoa

  Mkurugenzi wa kiwanda hicho Rupa Suchik amesema hatatengeneza tena viroba ikiwa ni agizo la serikali na vilivyopo watateketeza . Amesema kuanzia jana ameshapunguza wafanyakazi 150 kutoka 300 kutokana na agizo hilo na hao wataingia katika mfumo wa uzalishaji vileo katika mfumo wa Chupa.
  Meneja wa Kanda ya Magharibi wa Mamlaka ya Dawa na Chakula (TFDA ), Emmanuel Alphonce akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya operesheni ya viroba katika kiwanda cha nyati sprit leo Vingunguti jijini Dar es Salaam.
  Vijana wakipanga Viroba katika boksi walipokutwa na timu ya operesheni viroba iliyofika katika kiwanda cha Nyati Spirit leo jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
  Sehemu ya Katoni za Viroba vilivyokutwa katika kiwanda cha nyati sprit leo jijini Dar es Salaam.
  Mafisa wa serikali wakikagua nyaraka mbalimbali za kiwanda cha Nyati Sprit ikiwa ni uhalali wake wa kuendelea kufanya biashara katika mfumo mpya kutoendelea.

  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Professa Jumanne Maghembe(wa pili kutoka kushoto) akizungumza na wafanyabiashara kwenye mkutano wa majadiliano kati ya Serikali na Sekta binafsi katika kulinda na kuhifadhi Maliasili hasa za wanyama pori kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar leo.(Picha na Karama Kenyunko wa Blogu ya Jamii)
  Mwenyekiti wa Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF), Dk. Reginald Mengi akizungumza na wafanyabiashara pamoja na viogozi juu ya uhifadhi wa wanayamapori leo kwenye ukumbi wa mkutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar. katika mkutano huo wafanyabiashara wameahidi kuipatia serikali uwezo zaidi  wa kupambana na ujangili dhidi ya wanyamapori.
  Balozi wa Uhifadhi wanyamapori, Jacqueline Mengi akizungumza kuhusu uzuiaji wa ujangili kwa wanyamapori kwenye ukumbi wa mkutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar
   Baadhi ya wadau wakiwa kwenye mkutano wa majadiliano kati ya Serikali na Sekta binafsi katika kulinda na kuhifadhi Mali asili hasa za wanyamapori.
  Waziri wa Maliasili na utalii, Prof. Jumanne Maghembe akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari mara baada ya kumaliza mkutano wa majadiliano kati ya Serikali na Sekta binafsi katika kulinda na kuhifadhi Mali asili hasa za wanyama pori.

  0 0

  Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Richard Muyungi akimuhoji mmoja wa Wamiliki wa kiwanda cha Afro African Company kilichopo Mwenge jijini Dar es Salaam ambao ni wazalishaji na watengenezaji wa pombe mbalimbali aina ya viroba. Ofisi ya Makamu wa Raisi inaongoza uendeshaji wa ukaguzi wa viwanda vyote jijini Dar es Salaam vinavyozalisha na kutengeneza pombe kali(viroba) na kufunga kwa vifungashio vya plastiki.
  Mwanasheria wa Baraza la Usimamizi wa Mazingira NEMC , Heche Suguti akiwaonyesha waandishi wa habari aina mojawapo ya pombe kali (kiroba) inayozalishwa na kampuni hiyo pasipo kufuata kanuni za TFDA wala pasipo kuweka stika za TRA.
  Mrundikano wa maboksi uliopo kiwandani hapo ambapo ndani yake tayari kumejazwa pombe za aina mbalimbali aina ya viroba tayari kwa kuuza.
  Mashine zinazotumiwa na kiwanda cha Afro African Company kuzalisha pombe kali aina ya viroba pamoja na kutengenezea vifungashio vya plastiki vya kufungashia pombe hizo.

  0 0  Mfuko wa Pensheni wa LAPF unatarajia kufanya mkutano wa tisa wa wadau tarehe 9 na 10 Machi, 2017 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC Jijini Arusha. Mgeni rasmi katika mkutano huu anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb).
   
  LAPF imekuwa ikifanya mikutano hii ili kutoa taarifa za undeshaji wa Mfuko na kuwapa fursa wadau kutoa maoni mbali mbali ili kuboresha utendaji wa Mfuko. Aidha mikutano hii hufanyika ili kutekeleza maagizo ya mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa mifuko ya Hifadhi ya jamii nchini (SSRA).

  Kauli mbiu ya mkutano wa mwaka huu ni “Kuibua Fursa Endelevu za Ajira kwa maendeleo ya Hifadhi ya Jamii Tanzania”. Pamoja na mambo mengine kwenye mkutano huu mada mbali mbali zitawasilishwa ikiwemo mada inayohusu kauli mbiu jatwa hapo juu. Mada nyingine zitahusu Utendaji wa Mfuko kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2015/2016, Taarifa ya uwekezaji pamoja na Taarifa ya Hesabu za Mfuko kwa mwaka 2015/2016.

  Kadhalika katika siku ya kwanza ya ufunguzi wa mkutano LAPF itazindua huduma ya Mkopo wa Kujikimu ijulikanayo kwa jina la Maisha Popote na LAPF) kwa kushirikiana na benki ya CRDB. Huduma hii imewanufaisha sana wanachama wa Mfuko wanaoanza ajira kwa kuwapa fursa ya kukopa mara tatu ya mshahara wao ili kukidhi mahitaji ya awali kama kulipa pango, nk kwa riba nafuu.

  Vilevile siku ya ufunguzi wa mkutano tarehe 09 Machi, 2017 itakuwa ni siku ya maadhimisho ya figo duniani hivyo basi LAPF itatumia siku hii kuwapa fursa wadau wote watakao shiriki mkutano huu kupima figo kwa kushirikiana na wataalamu kutoka hospitali ya KCMC.

  LAPF inatarajia kupata washiriki zaidi ya 600 katika mkutano huu kwa kuzingatia idadi ya waalikwa. Waalikwa wanaweza kuthibitisha ushiriki wao na kujisajili kwa kutembelea tovuti ya Mfuko www.lapf.or.tz . LAPF inawahamasisha wadau wote kujisajili kupitia tovuti ili kupunguza msongamano siku ya mkutano.

  Aidha, siku ya pili ya mkutano tarehe 10 Machi, 2017, LAPF pamoja na washiriki wote wa mkutano wakiongozwa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa wanatarajia kushiriki katika mazoezi ya kutembea ikiwa ni kuunga mkono utekelezaji wa tamko la Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan.

  Karibuni waalikwa wote kwa ustawi wa Mfuko.

    Meneja Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, James Mlowe (katikati), akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini kuhusu mkutano na wa tisa wa wadau wa LAPF utakaofanyika jijini Arusha Machi 9-10.kushoto ni  Ofisa Masoko na Mawasiliano, Rehema Mkamba na kulia ni Meneja Takwimu, Hadhari na Tathmini, Abubakar Ndwata.
   Waandishi wa habari wakimsikiliza Meneja Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, James Mlowe.
  Pichani kulini ni Meneja Takwimu, Hadhari na Tathmini, Abubakar Ndwata akielezea mafanikio mbalimbali yaliyopatikana kupitia mfuko huo wa Pensheni wa LAPF,Kushoto ni   Meneja Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, James Mlowe

  Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo mapema leo,jijini dar
  Waandishi wa habari wakimsikiliza Meneja Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF, James Mlowe.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga ofisini kwake, Ikulu jijini  Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais). 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga (kulia) mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwake, Ikulu jijini  Dar es Salaam. 

  0 0

  Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusions Africa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Manjano Foundation Mama Shekha Nasser akieleza Matumizi Sahihi ya Vipodozi vya Luv Touch Manjano Kwenye Semina ya Ujasiriamali kwa Wanawake wa Mkoa wa Dar es Salaam. 

  Mafunzo ya Ujasiriamali Awamu ya kwa Katika Msimu wa Pili wa Mradi wa Taasisi ya Manjano Foundation ya Mafunzo ya Ujarisiamali kwa wanawake 32 kutoka Mkoa wa Dar es Salaam Yamemalizika. Wanawake 32 wa mkoa wa Dar es salaam ni miongoni mwa wanawake walionufaika na mafunzo ya ujasiriamali na namna ya kupamba kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano. Mafunzo hayo yaliendeshwa na wataalamu wa mambo ya Biashara wakishirikiana na maofisa wa Taasisi ya Manjano. 

  Mafunzo hayo yalilenga kumwezesha mwanamke wa Kitanzania kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira kwa kujikita katika kujiajiri ndani ya Tasnia ya Urembo na vipodozi. Mafunzo hayo yatafanyika kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya,Mtwara,Tabora na Kigoma.Image may contain: 12 people, people sitting and outdoor
  Baada yanawake hawa kuhitimu mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation itawaunganisha na Taasisi za Fedha zinazotoa mikopo bila riba waweze kupata mtaji wa kununua bidhaa za vipodozi kwa ajili ya kuwawezesha kuanzisha biashara wakiwa chini ya uangalizi maalum wa 
  Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha kila mhitimu wa mafunzo haya anapiga hatua na kuweza kujitegemea.
  Washiriki walionufaika kwenye Mafunzo hayo wakiwa katika Picha ya Pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusions Africa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Manjano Foundation Mama Shekha Nasser.Wanawake wa mji wa Dar es Salaam walionufaiki na mafunzo ya ujasiriamali na urembo wamemshukuru Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions na Mkurugenzi wa Taasisi ya Manjano Foundation kwa moyo wa kujitolea na kuwajali wanawake wengine hususani wakazi wa Dar es Salaam .
  Image may contain: 8 people, people smiling, people standing and sunglasses
  Wakiongea zaidi wanawake hao ambao wamepatiwa elimu ya biashara kutambua nafasi yao katika jamii inayowazunguka pamoja na namba ya kupamba maharusi na matumizi ya vipodozi. Wamemshukuru mama Shekha Nasser kwa moyo wenye kuwajali na kuwabeba wanawake wenzake na kutoa elimu ya bure aliyokuwa nayo kwa wengine ili waweze nao kujiongezea kipato na kupunguza ukali wa maisha. Wamemshukuru na wameahidi kuyatumia mafunzo hayo kwa lengo la kujikwamua na tatizo la ukosefu wa ajira kwa wanawake na pia kujiongezea kipato.

  0 0  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe mara baada ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd. kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani leo.Kutoka kulia ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo, Balozi wa China nchini Dkt. Lu Youqing,  Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd Fang Habibi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru(wapili kushoto).
    Jiwe la msingi la kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd kama linavyooneka mara baada ya baada ya kuwekwa rasmi leo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd mara baada ya kuweka jiwe la msingi leo Wilayani Mkuranga, Pwani. Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 8000 za Vigae kwa siku.Kushoto kwake ni Balozi wa China nchini Tanznia Dkt.Lu Youqing na kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd mara baada ya kuweka jiwe la msingi leo Wilayani Mkuranga, Pwani. Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 8000 za Vigae kwa siku.Kushoto kwake ni Balozi wa China nchini Tanznia Dkt.Lu Youqing na kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd leo Wilayani Mkuranga, Pwani. Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 8000 za Vigae kwa siku.Kushoto kwake ni Balozi wa China nchini Tanznia Dkt.Lu Youqing na kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru (kulia) akimsikiliza kwa makini Naibu Mkurugenzi wa kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd, Robin Huang (kushoto) wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda hicho leo Wilayani, Mkuranga.Katikati ni Mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda hicho jina lake(limehifadhiwa).
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi na wafanyakazi wa  kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani mara baada ya kuweka jiwe la msingi leo wilayani Mkuranga, Pwani.
  Baadhi ya wananchi wakitawanyika mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (hayupo pichani) kuondoka  baada ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd kilichopo Mkuranga, Pwani.

  Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO.

  0 0


  NA BASHIR NKOROMO.

  Ikiwa sasa ni takriban miaka miwili tangu aliyekuwa Mkurugenzi wa Tanzania One Theatre (TOT), Kampteni John Komba, kufariki Dunia, Mtoto wake Gerald John Komba, ameibuka na kutoa wimbo wa kuiunga mkono Serikali katika mapambano yake mapya dhidi ya dawa za kulenya nchini Tanzania.

  Gerald aliyezaliwa mwaka 1986 jijini Dar es salaam, amesema, ameamua kutoa wimbo huo wenye maudhi ya kwaya, ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya kifo cha Baba yake, Marehemu John Komba aliyefariki  Dunia, Februari 28, 2015 katika Hospitali ya TMJ, Mikocheni jijini Dar e Salaam, alikopelekwa baada ya kuzidiwa ghafla akiwa nyumbani kwake, Tangibovu kwa Komba.

  Mtoto huyo wa Jihn Komba aliyekuwa mwanamuziki nguri wa utunzi na uimbaji wa nyimbo za kwaya, amesema, wimbo aliotoa nimarejeo ya wimbo ambao ulitungwa na nguri huyo, kukemea usambazaji na matumizi ya dawa za kulevya miaka zaidi ya kumi iliyopita, lakini baada ya kuurekodi haukuwahi kuimbwa na TOT wala kuchezwa kwenye vituo vya Radio au Televisheni.

  Gerald ambaye amesomea Sheria katika Chuo Kikuu cha Saint Augustine kilichopo Mwanza,  Tanzania,  baada ya masomo ya shule ya Msingi katika shule ya Kawe "A" na shule yasekondari Mbezi Beach High school, anasema katika kuutoa wimbo huo, hakubabaisha kwa kuwa na yeye anacho kipaji cha kuimba japo amekuwa hakitumii sana. Zamani Shule ya Kawe A' ilifahamika kwa jina la Tanganyika Packers, lakini baada ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi kubaini kuwa kiwanda cha kusindika nyama cha Tanganyika Packers kimeshakufa, akaamua shule hiyo kubadilishwa jina.

  "Nimeanza kupenda sanaa ya muziki tangu nilipokuwa mtoto, kwa kuwa nilikuwa naenda na Baba (John Komba) kwenye maonesho yake na kundi la TOT,  na nilikuwa navutiwa sana na namna baba yangu alivyokuwa akitamba jukwaani wakati akiimba", alisema Gerald.

  "Tangu wakati huo, nilikuwa napenda kukariri nyimbo zote za Baba, na hakuna wimbo nisioujua kuanzia ala hadi mpangilio wa mashairi, lakini pia pia shuleni nilikuwa naimba kwenye kwaya ya shule, na siku za karibuni nimekuwa pia nikiimba kwaya kwenye Kanisa la Praise team, hapa jijini Dar es Salaam", aliongeza.

  Anasema, ameambua  kuurudia wimbo wa Marehemu Baba yake kwa sababu, kwanza yeye binafsi anachukia mamia ya vijana wanavyoharibika kwa matumizi ya dawa za kulevya kwa namna ambavyo wanatumiaji wengi wa dawa hizo hukatishwa ndoto zao mbalimbali za kuwa watu muhimu katika ujenzi wa taifa la Tanzania.

  "Kwanza ukizingatia hakuna aliyezaliwa teja, wengi  wanaokuwa hivyo wanakutana na hili balaa wanapoingia kwenye jamii kwa hiyo nikaona nifanye kitu ili jamii iweze kutoa mchangu wangu katika kuelimisha jamisha jamii ili izinduke na kuelewa namna dawa hizi za kulevya zilivyo za hatari.

  Pili niliamua kuurudia wimbo huu kwa sababu, watu wengine hasa Walimu na Wazazi wengi wao wanajisahau katika kusimamia malezi ya vijana. Wazazi wanamwachia Mwalimu jukumu la kutazama mwanafunzi akiwa shule bila kujua mtoto anaharibika katikati ya shule na nyumbani wakati wa kwenda na kurudi nyumbani, kwa hiyo Mwalimu na mzazi  ni Watu muhimu wa kuchunga mwanafunzi", alisema Gerald.

  Anasema, sababu yake ya tatu ya kuamua kuurudia na kuongeza vionjo kwenye wimbo huo ni kusisitiza kuwa mapambano hayo ni ya Watanzania wote ambapo anasema ameweka baadhi ya majina ya wakuu wa mikoa kwenye wimbo huo kwa kuwa vita hii ya mapambano dhi ya dawa za kulevya ni ya Watanzania wote na hao ndiyo wawakilishi wa Rais kwenye kila mkoa.

  "Nimeongeza vionjo kwa kutaja hawa wakuu wa mikoa kwa kuwa najua hawa ndiyo waakilishi wa Rais, na Rais Dk. John Magufuli hawezi kukabiliana nayo peke yake hivyo unahitajika ushirikiano na wananchi kuanzia ngazi ya Kaya, Vijiji, Kata, wilaya hadi mkoa.

  Na mwisho niliamua kuurudia kama Kumbukumbu ya miaka miwili ya kifo cha Marehemu Baba, ukiuusikiliza wimbo huu utangua kuwa sauti yangu na yake zimefanana kwa karibu sana katika uimbaji, hivyo itaweza kuashiria kuwa yale alyolenga kuyakemea kwenye nyimbo zake, hata baada ya kufariki dunia lakini bado kuna mtu mwingine ambaye ni mtoto wake atakayeendelea nyimbo hizo kufanya lengo lake la kuionya jamii ibaki pale pale", alisema Gerald

  "Mtindo nilioutumia kwenye wimbo huu ni uleule wa kwaya aliotumia Baba, na nimeuimba upya kwa kushirikiana na Mama yangu Mzazi, Jane Mkondwa ambaye ni mwimbaji wa miaka mingi katika Kundi la TOT, Nimeurekodi katika Studio za PM Records chini ya Mtayarishaji anayefahamika kwa jina la Testimony.

  "Baadhi ya maneno yaliyomo kwenye wimbo huu ni maneno ambayo ambayo hutumiwa zaidi na mateja na nimefanya hivyo kwa kuwa ni miongoni mwa walegwa katika vita hii. Hivyo, nikaona nitumie maneno wanayoweza kuyaelewa haraka kama;  'nywele misumari', 'twende kilioni', 'Macho kufutuka', 'akili inayeya' ambapo neno kama akili inayeya kwa teja humaanisha anavyokuwa baada ya kulewa dawa za kulevya yaani ufahamu katika akili zake unapotea.

  "Maneno mengine ni Gheto na Washkaji (nyumba wanapoishi vijana wa kiume au wa kike, lakini neno mshkaji au washkaji unategemea na umri, wale wa miaka ya 1960 walimaanisha wanawake wao lakini wa sasa wanamaanisha marafiki wao ingawa maana zote mbili zina maana sawa", anafafanua Gerald.

  Anasema, kwa sasa wimbo huo bado upo katika sauti tu (Audi), kwa kuwa hajapata uwezo wa kuurekodi katika video, ingawa yupo katika jitihada za kutafuta uwezo ili kuhakikisha anaurekodi katika video ili ujumbe uweze kufika kwa urahisikwa walengwa wote.

  Gerald anatoa mwito kwa Watanzania kuungana ili tulitokomeza usambazaji na matumizi ya dawa za kulevya bila kujali itikadi za vyama, kabila, jinsia kwa kuwa ni janga linaloweza kuingia katika familia, Taasisi, Chama cha siasa, kabila au jinsia yoyote.

  "Watanzania wenzangu naomba kila atakayepata fursa ausikilize kwa makini wimbo wangu huu,  ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Rais Dk. John Magufuli katika mapambano haya mapaya dhidi ya usambazaji na matumizi ya dawa za kulevya katika nchi yetu ya Tanzania", anasema Geral

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ARKADIA Ltd. Dr. Ezio Copat walipokutana kwa mazungumzo ofisini kwake mjini Dodoma 

  Waziri Mhe. Balozi Dkt. Mahiga akimsikiliza Dr. Copat walipokutana kwa mazungumzo mjini Dodoma 
  Waziri Mhe. Balozi Dkt. Mahiga akifafanua jambo wakati wa mazungumzo 
  Mazungumzo yakiendelea

  0 0

   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa Kampuni ya  BAM International inayojenga Jengo la Tatu la Abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa timu ya usimamizi wa ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Jijini Dar es Salaam, Eng. Julius Ndyamukama (kushoto) akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa ramani ya miundombinu katika jengo hilo alipofanya ukaguzi mapema leo.
  Muonekano wa jengo la Tatu la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam likiwa katika hatua za mwisho za ujenzi. Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini , Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

  0 0

  KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhandisi Mwanasha Tumbo ameziagiza wilaya zote za mkoa huu kuunda majukwaa ya wanawake kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo ili yaweze kuwa chachu ya kuwakomboa kimaendeleo na kiuchumi.

  Mhandisi Mwanasha ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza aliyasema hayo hivi karibuni  wakati akizindua jukwaa la wanawake mkoani Tanga ambalo litakuwa na malengo makuu ya kuwainua na kuwawezesha wanawake kiiuchumi lililofanyika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga.

  Alisema uwepo wa majukwaa hayo itasaidia kutoa fursa kwa wanawake kuweza kushiriki kikamilifu kwenye masuala mbalimbali ikiwemo kuwepo na majukumu ya kuwawezesha wanawake kuweza kujiinua kiuchumi kutokana na shughuli wanazozifanya zikiwemo za ujasiriamali.

  Aidha pia aliwataka wanawake kuwa mstari wa mbele kuzalisha bidhaa bora na wenye kiwango cha kimataifa ili waweze kupata nafasi ya kuziuza ndani na nje ya nchi ili kuwasaidia kuongeza pato lao na Taifa kwa ujumla.

  “Wajasariamali warasimishe biashara zao ili ziweze kutambulika
  kisheria ikiwemo kulipa kodi lakini pia muachane na suala la
  kujiingiza kwenye biashara haramu ambazo zinaweza kukatisha ndoto zenu “Alisema.

  “Kupitia Jukwaa hili mnaweza mnalitumia kusaidia wanawake kujikwamua kiuchumi na kuweza kufia sera ya asilimia 50 kwa 50 hivyo ili kufikia huko jukumu lenu kuonyesha uwezo lakini pia wekezeni kwenye elimu kupitia mkusanyiko huu “Alisema.

  Awali akizungumza Mjasiriamali wa kampuni ya kutengeneza Fenicha, za majumbani na maofisini mkoani Tanga Edna Boimanda aliwashauri wanawake kuunganisha nguvu za pamoja ili kuona namna ya kuanzisha benki ya wanawake kwani hiyo ndio fursa ya kipekee wanayoweza kujikwamua kiuchumi.

  Alisema kupitia benki hiyo itawawezesha waanawake kujiletea maendeleo kwa kupata mikopo itakayokuwa chachu ya kufikia malengo yao ya kupata mafanikio.
  Mmmoja wa Wajasiriamali kushoto akimuonyesha Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tangaa,Mhandisi Mwanasha Tumbo ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza akiangalia moja kati ya bidhaa wanazozalisha wakati wa kongamano la wanawake wajasiriamali mkoani Tanga lililofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga hivi karibuni.
   Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo kushoto aliyevaa hijabu ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza akipata maelekezo kutoka kwa mmoja wa wanawake wajasiriamali wakati alipofungua jukwaa la wanawake mkoani Tanga hivi karibuni.

  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza kulia akipata maelekezo kutoka kwa mmoja wa wanawake wajasiriamali wakati alipofungua jukwaa la wanawake mkoani Tanga hivi karibuni.
  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza kulia akipata maelekezo kutoka kwa mmoja wa wanawake wajasiriamali wakati alipofungua jukwaa la wanawake mkoani Tanga hivi karibuni.
  Picha na habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

  0 0


  Naibu Waziri Mpina (katikati) akiwa na ujumbe wake, akisisita jambo wakati wa ukaguzi wa mradi wa upandaji na utunzaji mikoko katika Delta ya Rufiji kaskazini.
   Naibu Waziri Mpina  (kaikati) na Ujumbe wake katika picha wakitembea kukagua mikoko iliyopandwa katika Delta ya Kaskazini Rufiji.
   Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina na ujumbe wake wakiwa katika boti  wakielekea katika ukaguzi wa upandaji na utunzaji wa Mikoko, pamoja na uharibifu wa Mazingira katika Delta ya Rufiji Kaskazini.
  Naibu Waziri Mpina akiwaasa wasimamizi wa mradi wa upandaji na utunzaji mikoko katika delta ya kaskazini Rufiji hawapo pichani wamueleze ukweli kuhusu matumizi ya fedha na hali halisiya mradi kabla ya kwenda kukagua upandaji, utunzaji wa mikoko na uharibifu wa mazingira.


  NA EVELYN MKOKOI -RUFIJI 

  NAIBU Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina amebaini madudu katika matumizi ya sh. milioni 396 za ufadhili wa Mfuko wa nchi maskini zaidi duniani (LDCF) chini ya mkataba wa dunia mabadiliko ya tabianchi katika utekelezaji wa mradi wa upandaji na uendelezaji wa mikokokatika delta ya kaskazi mto Rufiji.

  Katika mradi huo matumizi ya zaidi ya sh. milioni 364  mchanganuo wake
  hauridhishi huku vikundi vinavyodaiwa kulipwa fedha hizo vikikana kulipwa na kusema hawakuwa na mkataba bali walifanya kazi kama vibarua kwa posho ya sh. 10000 kila wanapomaliza kazi na hawakuwa na mkataba.

  Kutokana na hatua hiyo Mpina amemuagiza Mkaguzi wa ndani Ofisi ya Makamu wa Rais, Mwatano Maganga kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja anafanya uhakiki wa matumizi ya fedha hizo za mradi na kuelekeza hatua za kuchukua kwakuwa.

  vielelezo alivyokabidhiwa na Msimamizi wa mradi kutoka Halmashauri ya
  Rufiji Sabastian Gaganijas vina mashaka. “Naagiza ukaguzi ufanyike, lazima kuna ubadhilifu umefanyika katika utekelezaji wa mradi, baada ya ukaguzi makini, tutajua ukweli na kubaini hatua gani zitachukuliwa.” Alisisitiza Mpina.

  1000 zilizodaiwa zimepandwa ni udanganyifu wa wazi.
  Hata hivyo, baada ya zoezi zima la kukagua Delta hiyo yenye kilomota zaidi ya 5 Naibu Waziri Mpina, alisema amesikitishwa na jutekelezaji wa  mradi huo unaotumia  fedha za wafadhili zaidi ya sh.milioni 396 kuwa na madudu na amejionea mwenyewe  kuwa, mradi hauna usimamizi na kusema kuwa,  kuna dalili ya fedha hizo kutumika ndivyo sivyo kwakuwa hata hekta 792 kati ya 


  “Huu ni uhuni ambao haukubali kwa serikali hii awamu ya tano tuliposema
  hapa kazi tu tulimaanisha kuwa hatuwezi kudanganywa watu wamezoea kuona  Waziri hawezi kuja kwenye mazingira kama haya nimejionea mwenyewe mikoko iliyopandwa haendani na thamani ya matumizi ya fedha hizo na sehemu kubwa imevamiwa na kupandwa mpunga badala ya mikoko,”alisema.


  Alisema katika mchanganuo aliokabidhi na msimamizo wa mradi fedha hizo
  zaidi ya  sh.milioni  364 zimedaiwa matumizi yake ni pamoja na kulipa
  vikundi 28 vilivyokabidhiwa mradi ambavyo sasa havipo.

  Alisema cha kushangaza katika fedha hizo kipo kikundi kimelipwa zaidi ya
  milioni 30 kwa kupanda hekta 3 huku kingine kikilipwa milioni 3 kwa hekta
  hizo hizo.

  Baadhi ya wakazi wa rufiji wakizungumza katika ziara ya Naibu Waziri Mpina, wametoa changamoto zao katika kukabiliana na uharibifu huo wa Mazingira   na kuiomba Serikali kuongeza usimamizi madhubuti katika mradi huo ili kukubaliana na uharibifu huo wa hifadhi hiyo ya mikoko,
  Awali Imeelezwa na mtaalam wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu  wa Rais Bw. Cretus Shengena kuwa, uharibifu huo waMikoko unaweza kusababisha kupotea kwa uoto asili na baiyonuwai katika eneo hilo kama udhibiti wa dhati usipo chukuliwa kwa haraka kuinusuru eneo hilo la Delta ya Rufiji kaskazini.

  Mradi huo wa hifadhi ya taifa ya Delta ya Rufiji kaskazini unafadhiliwa na Mfuko wa kundi la nchi maskini zaidi duniani (LDCF) kupitia Shirika la umoja wa Mataifa ya Mazingira chini ya usimamizi wa Ofisi ya Makamu wa Rais.


  0 0

  MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia mbali maombi yaliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ya kutaka asikamatwe hadi kesi yake ya kikatiba dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda itakapomalizika.

  Maombi hayo yalitupwa kwa sababu kifungu cha sheria kilichotumika kuyafungua si sahihi na kwamba hutumika pale ambapo sheria ziko kimya.

  Uamuzi huo wa majaji umefikiwa kutokana na pingamizi la jamhuri lililowasilishwa na Wakili wa Serikali Mkuu Gabriel Malata kuiomba kuyatupilia mbali maombi hayo kwani hayana msingi kisheria.

  Katika hatua nyingine, mwanahabari nguli nchini Jenerali Ulimwengu, ameungana na jopo la mawakili Tundu Lissu, Peter Kibatala na John Malya katika kumtetea Mbowe.

  Mbowe amefungua kesi hiyo ya kikatiba namba 1, ya mwaka 2017 dhidi ya wadaiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam na Ofisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalumu ya Dar es Salaam. Kesi hiyo itasikilizwa tena Machi 8, mwaka huu.
  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akitafakari jambo ndani ya Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam akiwa na wakili wake Jenarali Ulimwengu (kati),na Meya wa Ubungo Boniface Jacob .


  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu You qing mara baada ya kuweka jiwe la Msingi katika Kiwanda kikubwa cha kutengeneza Vigae(Tiles ) cha Good Will kilichopo katika kijiji cha Mkiwa, Mkuranga mkoani Pwani. Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha vigae laki nane kwa siku na mwekezaji ametumia zaidi ya Dola mil.50 katika uwekezaji huo.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu You qing   akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Kiwanda hicho cha vigae kilichopo Mkiwa Mkuranga mkoani Pwani.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akihutubia kabla ya kuweka jiwe la Msingi katika Kiwanda kikubwa cha kutengeneza Vigae(Tiles ) cha Good Will kilichopo katika kijiji cha Mkiwa, Mkuranga mkoani Pwani.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Ikwiriri mkoani Pwani wakati alipokuwa akielekea mkoani Lindi na Mtwara katika ziara yake ya kikazi ya siku nne.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwakilishi wa Kiwanda hicho cha y Vigae cha Good Will, Huang Heng Chao  kutoka kwa Kiwandani hapo.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa anapata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kuhusu matumizi ya Gesi katika Kiwanda cha Vigae cha Good Will kutoka kwa Kiwandani hapo.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Somanga mkoani Lindi wakati akiwa ziarani lkuelekea mikoa ya Kusini(Lindi na Mtwara).
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mbunge wa Kilwa Kusini Suleiman Bungara(Bwege ) kutoka CUF katika eneo la Somanga wakati alipokuwa akielekea Nangulukulu katika ziara yake ya mikoa ya Kusini.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mbunge wa Kilwa Kusini Suleiman Bungara(Bwege ) kutoka CUF katika eneo la Nangulukulu, Kilwa mkoani Lindi wakati akiwa katika ziara ya mikoa ya kusini.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa  Nangulukulu  mkoani Lindi.
   Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Nape Nnauye akifurahia hotuba iliyokuwa ikitolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika eneo la Nangulukulu mkoani Lindi.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Nape Nnauye mara baada ya kuhutubia wananchi wa Nangulukulu mkoani Lindi.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimian na mbunge wa Kilwa Kaskazini Vedasto Ngombale (CUF) mara baada ya kuhutubia wananchi wa Nangulukulu mkoani Lindi.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wananchi mara baada ya kuhutubia wananchi wa Nangulukulu mkoani Lindi.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpatia msaada wa Shilingi milioni moja kijana Abdulrahman Khalid ambaye ni mlemavu wa miguu katika eneo la Mchinga-1 mkoani Lindi, Katikati(Mwenye shati la maua) ni Mbunge wa Mchinga Hamidu Bobali kupitia chama cha (CUF) ambaye ameahidi kumpatia mlemavu huyo kiasi cha Shilingi Milioni moja pia.
  .
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd mara baada ya kuweka jiwe la msingi leo Wilayani Mkuranga, Pwani. Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 8000 za Vigae kwa siku.Kushoto kwake ni Balozi wa China nchini Tanznia Dkt.Lu Youqing na kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd leo Wilayani Mkuranga, Pwani. Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 8000 za Vigae kwa siku.Kushoto kwake ni Balozi wa China nchini Tanznia Dkt.Lu Youqing na kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru (kulia) akimsikiliza kwa makini Naibu Mkurugenzi wa kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd, Robin Huang (kushoto) wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda hicho leo Wilayani, Mkuranga.Katikati ni Mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda hicho jina lake(limehifadhiwa).
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi na wafanyakazi wa  kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani mara baada ya kuweka jiwe la msingi leo wilayani Mkuranga, Pwani.
  Baadhi ya wananchi wakitawanyika mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (hayupo pichani) kuondoka  baada ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd kilichopo Mkuranga, Pwani.

  PICHA NA IKULU

  0 0

   Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata (kulia) akimkaribisha Naibu Kamishna Mkuu wa Shirika la Huduma za Forodha la Korea (Korea Customs Service-KCS) Dk. Jong-Yeul Kim alipotembelea TRA tarehe 1 Machi 2017 ili kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya taasisi hizo. Baadhi ya mambo waliyojadili ni pamoja na  utekelezaji wa mradi wa Dirisha Moja la Huduma (Electronic Single Window Systems) kufuatia makubaliano ya ushirikiano  yaliyofanyika baina ya taasisi hizo mbili.
  Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata (kulia) akimuelezea jambo Naibu Kamishna Mkuu wa Shirika la Huduma za Forodha la Korea (Korea Customs Service - KCS) Dk. Jong-Yeul Kim alipotembelea TRA tarehe 1 Machi 2017 ili kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya Taasisi hizo mbili.
    Naibu Kamishna Mkuu wa Shirika la Huduma za Forodha la Korea (Korea Customs Service-KCS) Dk. Jong-Yeul Kim  (aliyeshika picha kushoto) akifurahia moja ya zawadi aliyokabidhiwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata (kulia) mara baada ya kumaliza mkutano wa pamoja  uliofanyika katika ofisi ya TRA Makao Makuu wakati wa ziara ya Dk. Kim nchini Tanzania.
  Timu ya  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) (kulia) ikiongozwa na Kamishna Mkuu Bw. Alphayo Kidata   pamoja na Timu ya Shirika la Huduma za Forodha la Korea (Korea Customs Service-KCS)  ikiongozwa na  Naibu Kamishna Mkuu Dk. Jong-Yeul Kim walipokutana katika ofisi ya TRA Makao Makuu ili kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili.
   Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Alphayo Kidata (wa nne kulia)  pamoja na Naibu Kamishna Mkuu wa Shirika la Huduma za Forodha la Korea (Korea Customs Service-KCS) Dk. Jong-Yeul Kim (wa tano kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kikao cha pamoja kilichowakilisha taasisi hizo mbili.

  0 0

  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

  Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wamenunua mtambo mpya wa kisasa unaojulikana kama ‘Energy Dispersive X-Ray Fluorescence Spectrometer’ (EDXRF) kwa ajili ya kurahisisha uchunguzi wa kimaabara.

  Mtambo huo uliogharimu kiasi cha shilingi 101,785,200 umesimikwa katika Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Kanda ya Nyanda za Juu Kusini mkoani Mbeya kuanzia Februari 21 hadi 23 mwaka huu.

  Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Mkemia Mkuu wa Serikali. Prof. Samwel Manyele alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu matumizi ya mtambo huo.

  Prof. Manyele amesema kuwa mtambo huo umesimikwa mkoani mbeya ikiwa ni moja ya hatua za kuboresha maabara za Kanda zilizopo Arusha, Dodoma, Mbeya, Mtwara na Mwanza, kusogeza shughuli za uchunguzi karibu na wananchi ili kupunguza gharama za kusafirisha sampuli kuja mkoani Dar es Salaam kwa ajili ya uchunguzi.

  “Kuwepo kwa mtambo huo ni suluhisho kwa Serikali, Wizara, Viwanda, Mashirika, Wachimbaji wa madini, wajasiriamali na wananchi kwa ujumla ambao walikuwa wanahitaji kufahamu ubora na usalama wa bidhaa mbalimbali za viwandani na mashambani, kutambua uwepo wa madini ya thamani kwenye udongo na bidhaa za vito pamoja na sampuli zinazohusiana na usalama wa afya na mazingira,”alisema Prof. Manyele.

  Ameyataja matumizi mengine ya mtambo huo kuwa ni kufanya uchunguzi wa sampuli za migodini, kupima bidhaa za mbao ili kubaini kiwango cha kemikali zinazotumika kutibu mbao, kupima sampuli za mafuta ya kula kwa kuangalia kiwango cha madini ya phosphorus, kupima sampuli za pembejeo za kilimo pamoja na kufanya uchunguzi wa sampuli na vielelezo vinavyohusiana na makosa ya jinai.

  Prof. Manyele amefafanua hoja zitakazojibiwa na matumizi ya mtambo huo zikiwemo za kufahamu dhahabu kiasi gani ipo katika udongo unaohitaji kuchenjuliwa, kufahamu mbogamboga zinazolimwa bondeni zina kiasi gani cha madini yanayoathiri watumiaji, kufahamu kiasi cha uranium katika ardhi na vyanzo vya maji pamoja na kufahamu athari za aina ya madini yaliyopo katika maji ya visima virefu na vifupi kwa watumiaji.

  Aidha, Mkemia Mkuu amebainisha kuwa baada ya kuzinduliwa kwa mradi huo, Maabara ya Nyanda za juu kusini itakua na majukumu ya kukusanya sampuli za vinasaba vya binadamu (DNA) pamoja na kuwa kituo rasmi cha kukusanyia sampuli nyingine mbalimbali.

  Maabara hiyo kwa sasa ipo Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya ambapo kuanzia mwezi Aprili mwaka huu itahamia katika eneo la Lwambi lililopo mkoani humo.
  Mkemia Mkuu wa Serikali, Prof. Samwel Manyele (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu kuanza kazi kwa mtambo mpya wa kisasa wa Energy Dispersive X Ray Fluorescence (EDXRF) kwa ajili ya kufanyia uchunguzi wa kimaabara.Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Huduma za Ubora wa Bidhaa, Bw. Daniel Ndiyo, Mkurugenzi Idara ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali Nchini, Bw. Sabanitho Mtega kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Biashara Bw. George Kasinga pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi Jinai na Huduma za Vinasaba,Bw. David Elias.
  Baadhi ya watumishi wa Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mkemia Mkuu wa Serikali, Prof. Samwel Manyele (hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza kuhusu kuanza kazi kwa mtambo mpya wa kisasa wa Energy Dispersive X Ray Fluorescence (EDXRF) kwa ajili ya kufanyia uchunguzi wa kimaabara. Mtambo huo umefungwa kwenye Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Mkoani Mbeya.
  Mtambo wa Energy Dispersive X – Ray Fluorescence (EDXRF) kushoto unaotumika kupima sampuli mbalimbali zenye asili ya yabisi na vimiminika kama vile vyakula, bidhaa za mafuta, maji, simenti, makaa ya mawe, bidhaa za chuma ili kutambua kiwango cha madini kilichomo ndani ya sampuli hizo. Mtambo huo umefungwa kwenye Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Mkoani Mbeya.

  0 0older | 1 | .... | 1157 | 1158 | (Page 1159) | 1160 | 1161 | .... | 1896 | newer