Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

NAPE: Nitahakikisha Timu za Dodoma zinacheza Ligi Kuu.

$
0
0

Na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amewahakikishia wapenzi wa Mpira Mjini Dodoma kuwa timu za Mpira Mkoani humo zitashiriki Ligi Kuu ili kuwapa raha ya Ligi hiyo mashabiki wa mpira na michezo kwa ujumla.

Amezungumza hayo mara baada ya kukutana na kufanya mazoezi na Vijana kutoka Jogging Club mbalimbali Mjini Dodoma ikiwa ni ishara rasmi ya Wizara yake kuhamia katika Makao Makuu ya nchi.

Mhe. Nape Nnauye amesema kuwa haitawezekana Serikali ikahamia Dodoma na kusiwe na timu inayoshiriki Ligi kuu ya Mpira wa Miguu Tanzania Bara hivyo yeye kama Waziri anayehusika na Michezo kwa kushirikiana na wadau wa Michezo atahakikisha Timu zinafanya vizuri na kushiriki Ligi hiyo.

“Haiwezekani Rais akawa hapa na Makamu wa Rais na Mawaziri tukakosa ladha na furaha ya Ligi kuu hapa Dodoma nitahakikisha timu za hapa zinashiriki Ligi kuu”alisistiza Mhe. Nnauye.

Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu kazi Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde amewapongeza vijana wa Jogging club na wakazi wa Dodoma kwa kushiriki michezo na kuhimiza kujituma zaidi kwa timu za michezo hasa mpira wa miguu ili kushiriki Ligi kuu Tanzania Bara.


Naye Katibu Mkuu Wizara wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel amewaomba wakazi wa Dodoma kufanya michezo kuwa ni Utamaduni wao wa kila siku ili kujenga Taifa la wapenda michezo kwa nia ya kuimarisha afya na kuendeleza michezo nchini.

Aidha Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Nchini Bw. Omary Singo amewahakikishia wakazi na wapenzi wa Michezo ushirikiano katika kuendeleza na kukuza michezo hasa katika makao makuu ya nchi Dodoma.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na vijana wa Jogging club Mjini Dodoma mara baada ya kufanya mazoezi ya pamoja yenye nia ya kuimarisha afya na kuendeleza michezo nchini yaliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma leo March 1, 2017.


RHINO CEMENT TANGA YAKABIDHI MADAWATI 350 SHULE MSINGI KANGE TANGA

$
0
0
Tanga, MKUU wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwalapwa, amekishukuru kiwanda cha Saruji cha Rhino cha Tanga kwa msaada wake wa madawati 350 kwa shule ya Msingi ya Kange na mabenchi 10 kwa Zahanati iliyopo ndani ya kata hiyo.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano, Mwalapwa alisema msaada huo utaondosha kero ya wanafunzi darasani kukaa chini hivyo kutaka makampuni mengine kufuata nyayo za kiwanda hicho cha Rhino.

Amesema mabenchi 10 kwa Zahanati pia itaondosha kero kwa wagonjwa wanaofika kituoni na kuondosha kero ya foleni ya kukaa chini kusubiri huduma.

“Niseme kutoka moyoni nimepata faraja kubwa kwa ndugu zetu kutukumbuka jiwe moja kwa ndege wawili, madawati 350 kwa shule na mabenchi 10 kwa Zahanati, hili ni tukio jema la faraja” alisema Mwailapwa

Kwa upande wake Mkuu wa Kiwanda cha Saruji cha Rhino, Girish Gumar, amesema msaada huo wa madawati 350 na mabenchi kwa Zahanati uko na thamani zaidi ya milioni 45.

Alisema kiwanda cha Rhino kimekuwa kikisaidia katika Nyanja mbalimbali zikiwemo za Elimu, Afya, Mazingira na huduma nyengine za kijamii.
Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Saruji cha Rinho, Girish Kumar akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwalapwa moja ya madawati 350 kwa shule ya msingi ya Kange kupunguza kero ya uhaba wa madawati kwa shule hiyo ambayo awali wanafunzi walikuwa wakisomea chini.







Wanafunzi wa shule ya msingi ya Kange Tanga wakipeleka madawati madarasani kati ya madawati 350 yaliyotolewa na kiwanda cha Saruji cha Rinho jana. Shule hiyo ilikuwa ikikabiliwa na uhaba wa madawati na baadhi ya wanafunzi kulazimika kukaa chini
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tangakumekucha

OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAHAMIA RASMI DODOMA

$
0
0
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora akipokewa na watumishi wa Ofisi yake mjini Dodoma mara baada ya kuwasili katika Ofisi zilizopo `Area D` Dodoma. Kulia ni Bi. Oigenia Mpanduji Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora akisalimiana na Bw. Isaya Kisiri Afisa Ugavi Mwandamizi mara baada ya kuwasili katika Ofisi zilizopo `Area D` Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Ngosi Mwihava (kushoto) akiongea na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais mjini Dodoma.

RAIS DKT. MAGUFULI ASALI IBADA YA JUMATANO YA MAJIVU KATIKA KANISA KATOLIKI LA MTAKATIFU PETRO (ST PETER) OYSTERBAY JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisali katika Ibada ya Jumatano ya Majivu pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini Wiliam Mkapa, Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa na Mke wake Mama Janeth Magufuli katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini Wiliam Mkapa wakiwatakia heri ya Masista katika Ibada ya Jumatano ya Majivu iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokiya ya Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisali katika Ibada ya Jumatano ya Majivu pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini Wiliam Mkapa, Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa na Mke wake Mama Janeth Magufuli katika Kanisa Katoliki Parokiya ya Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisali katika Ibada ya Jumatano ya Majivu pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini Wiliam Mkapa katika Kanisa Katoliki Parokiya ya Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Paroko Msaidizi wa Kanisa la Mtakatifu Petro Father Asis akijiandaa Kumpaka majivu kichwani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Ibada ya Jumatano ya Majivu iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokiya ya Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Paroko Msaidizi wa Kanisa la Mtakatifu Petro Father Asis akimpaka majivu kichwani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Ibada ya Jumatano ya Majivu iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokiya ya Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Paroko Msaidizi wa Kanisa la Mtakatifu Petro Father Asis akimpaka majivu kichwani Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli katika Ibada hiyo ya Jumatano ya majivu.
Paroko Msaidizi wa Kanisa la Mtakatifu Petro Father Asis akimpaka majivu kichwani Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini Wiliam Mkapa katika Ibada hiyo ya Jumatano ya majivu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini Wiliam Mkapa mara baada ya Ibada hiyo ya jumatano ya Majivu iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.

KITUO CHA EATV NA HAWA FOUNDATION WAZINDUA KAMPENI YA KUCHANGISHA FEDHA KUWASAIDIA WASICHANA WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI WAKATI WA HEDHI

$
0
0


Kituo cha televisheni cha EATV kwa kushirikiana na taasisi ya haki za wanawake (HAWA), wamezindua kampeni ya kuchangisha fedha kwa ajili ya wasichana na wanafunzi wa shule za sekondari nchini Tanzania,kununulia taulo za hedhi (pedi) ili kuwasitiri na kulinda utu wao.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari,jijini Dar leo, Afisa Masoko wa EATV,Brendansoa Kileo amesema kuwa Kampeni hiyo inazinduliwa wakati tukielekea siku ya Wanawake Duniani Machi 8.


"Nasi kama kituo cha habari kinachofanya biashara zake nchini,tumeona kuwa tuna wajibu wa kutumia vituo vyetu vya EATV na East Africa Radio kuhamasisha jamii kuwachangia watoto wetu wa kike kutatua tatizo",alisema  Brendansoa.

Amesema kuwa kumekuwepo na tatizo la wanafunzi wa kike kukosa kuhudhuria shule kati ya siku tano hadi saba kwa kukosa pedi za kujisitiri wakati wa hedhi .“kwa mwaka inakadiriwa mwanafunzi wa kike hukosa kuhudhuria shule kwa siku 60 hadi 70 kutokana na kukosa pedi tu , hali ambayo imekuwa ikichangia kutofanya vizuri katika masomo yao”amesema Brendansoa.

Amesema kuwa wanafunzi wengi wamekuwa wakihatarisha afya zao kwa kutumia matambara kwa ajili ya kujisitiri wakati wa hedhi na kusababisha aibu pale ambapo vitambaa vinapovujisha damu.

Wakati huo huo Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki  za Wanawake (HAWA) , Joyce Kiria ameongeza kusema kuwa ili kuchangia kampeni hiyo,wanatarajia kila Mwananchi atakayeguswa na tatizo hilo basi anaombwa kuchangia kuanzia kiasi cha shilingi Elfu Tano (5,000/=),ili
 kuwasaidia watoto wa kike kupata pedi na kuhudhuria shule. 

"Katika kampeni hiyo EATV na East Afrika Radio itahamasisha uchangiaji wa fedha na taasisi ya Haki za Wanawake (HAWA FOUNDATION),iliyosajiliwa kwa mujibu wa taratibu za nchi mwaka 2011,itahusika na kupokea na kusimamia fedha zote zitakazochangishwa na kusimamia ununuzi na usambazaji wa pedi hizo mashuleni",alisema Joyce Kiria.


Kiria aliongeza kwa kueleza taratibu za uchangiaji kuwa,unaweza kutuma fedha hizo kwa M-Pesa kupitia namba 5530307 ama kupitia akaunti ya CRDB namba 0150258750600.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki  za Wanawake (HAWA) , Joyce Kiria akifafanua jambo kuhusiana na uzinduzi wa  kampeni ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasaidia wasichana na wanafunzi wa shule za sekondari nchini Tanzania,kuwanunulia taulo za hedhi (pedi) ili kuwasitiri na kulinda utu wao.

Pichani kulia ni  Afisa Masoko wa EATV,Brendansoa Kileo akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar,kuhusiana na uzinduzi wa  kampeni ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasaidia wasichana na wanafunzi wa shule za sekondari nchini Tanzania,kuwanunulia taulo za hedhi (pedi) ili kuwasitiri na kulinda utu wao.Pichani kati ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki  za Wanawake (HAWA) , Joyce Kiria  pamoja na Afisa Masoko wa East Afrika Radio Basilisa Biseko.

Wa pilia kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki  za Wanawake (HAWA) , Joyce Kiria akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu uzinduzi wa  kampeni ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasaidia wasichana na wanafunzi wa shule za sekondari nchini Tanzania,kuwanunulia taulo za hedhi (pedi) ili kuwasitiri na kulinda utu wao.


Baadhi ya Wanahabari wakifuatilia yaliyokuwa yakizungumza kwenye mkutano huo.

WAFANYAKAZI WA ZANTEL-ZANZIBAR WACHANGIA DAMU KUISAIDIA BENKI YA DAMU SALAMA NCHINI

$
0
0

Mkurugenzi wa Ofisi Kuu ya Kampuni ya Zantel-Zanzibar Mohamed Musa Baucha akijiandaa kuchangia damu wakati wa zoezi la uchangiaji damu kwa hiari lilloandaliwa na kampuni hiyo ikiwa ni njia ya kuhamasisha jamii kuchangia damu kwa hiari. Zoezi hilo limefanyika jana mjini Unguja. Kushoto ni ofisa kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama-Zanzibar Gabriel Laurent.
Mfanyakazi wa kampuni ya Zantel -Zanzibar Mohammed Ali akichangia damu wakati wa zoezi lililowahusisha wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa upande wa Zanzibar ikiwa ni njia ya kuokoa maisha ya watanzania wenye uhitaji mkubwa wa huduma hiyo. Zoezi hilo limefanyika jana mjini Unguja. Kushoto ni Khairia Ali Hamad, mtoaji damu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama-Zanzibar.
Afisa mdhibiti wa Rasilimali watu wa kampuni ya Zantel -Zanzibar Said Habibu akichangia damu wakati wa zoezi lililowahusisha wafanyakazi wa kampuni hiyo ikiwa ni njia ya kuhamasisha jamii kuchangia damu kwa hiari. Zoezi hilo limefanyika jana mjini Unguja. Kushoto ni Khairia Ali Hamad, mtoaji damu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama-Zanzibar.
Mfanyakazi wa kampuni ya Zantel -Zanzibar Kassim Bakari Zuberi akichangia damu wakati wa zoezi lililowahusisha wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa upande wa Zanzibar ikiwa ni njia ya kuokoa maisha ya watanzania wenye uhitaji mkubwa wa huduma hiyo. Zoezi hilo limefanyika jana mjini Unguja. Kushoto ni ofisa kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama-Zanzibar Gabriel Laurent.
Afisa mdhibiti wa Rasilimali watu wa kampuni ya Zantel -Zanzibar Said Habibu akichangia damu wakati wa zoezi lililowahusisha wafanyakazi wa kampuni hiyo ikiwa ni njia ya kuhamasisha jamii kuchangia damu kwa hiari. Zoezi hilo limefanyika jana mjini Unguja. Kushoto ni Khairia Ali Hamad, mtoaji damu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama-Zanzibar.

 
Katika kuisaidia benki ya damu hapa nchini, wafanyakazi wa Zantel-Zanzibar wamejitokeza kwa wingi na kujitolea kuchangia damu katika kuendeleza mwitikio huo kwa jamii ulioanzishwa na Kampuni hiyo wiki iliyopiata katika makao makuu yake jijini Dar es Salaam.

Zoezi hili ambalo linaratibiwa na Kitengo cha uwajibikaji kwa jamii (CSR) cha Kampuni hiyo, limelenga kusambaza upendo kupitia shughuli hii ya uchangiaji damu ili kuiwezesha benki ya damu sambamba na kuokoa maisha ya Watanzania wenzetu.

Shughuli hiyo ya uchangiaji iliyofanyika katika makao makuu ya Ofisi za Zantel-Zanzibar, ilishuhudia mwitikio mkubwa kutokana na wingi wa wafanyakazi wa Zantel kujitokeza, pamoja na baadhi ya wananchi wakishiriki kuchangia damu.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo la uchangiaji damu, Mkurugenzi wa Ofisi kuu ya Zantel-Zanzibar, Bw. Mohamed Musa Baucha aliwashukuru watu wote walioshiriki na kutoa rai kwa makampuni mbalimbali pamoja na wananchi kuwa tayari kujitolea kwenye shughuli kama hizo wanapotakiwa kufanya hivyo.

“Tunayo furaha kwa mwitikio huu wa kukubali kuokoa maisha ya Watanzania wenzetu kwa kuonyesha upendo hususan wafanyakazi wa Zantel Zanzibar. Niwaombe muendelee na moyo huu huu wa kujitolea pindi mnapohitajika kushiriki kwenye shughuli nyingine kama hizi,”alisema.

Kwa upande wake, Afisa Uhamasihaji wa Mpango wa damu salama Zanzibar Bw. Omar Said Omar alisema kwamba zoezi la uchangiaji damu limefanyika kwa mafanikio makubwa na amefurahishwa na moyo wa kujitolea ulioonyeshwa na wafanyakazi wa Zantel-Zanzibar. Hata hivyo aliongeza kuwa, bado mahitaji ya damu ni makubwa ikilinganishwa na kiwango kilichokusanywa ambapo kwa mwaka huu wa 2017 walijiwekea lengo la kukusanya chupa 12,000.

Alisema kwamba shughuli ya kukusanya damu ni zoezi endelevu la kujitolea, benki ya damu imekuwa ikiomba makampuni na jamii kwa jumla kutambua umuhimu wa kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wananchi.

“Ni watu wachache sana ambao wamekuwa wakijitokeza kuchangia damu, hivyo tunaamini kuwa zoezi hili litaendelea kuwahamasisha watu wengi kujitokeza kushiriki,” alisema.

BUNDUKI KUMI ZIKIWEMO SMG SITA RISASI 59 ZAKAMATWA ARUSHA

$
0
0
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha.

Jeshi la Polisi mkoani hapa limefanikiwa kupata jumla ya bunduki kumi za aina nne tofauti zikiwemo Sub-Machine Gun sita baada ya operesheni ya wiki mbili iliyoanza tarehe 15.02.2017 katika wilaya ya Ngorongoro. 

Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari leo asubuhi, Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo alisema silaha hizo zilipatikana katika vijiji vya Olorieni Magaiduru, Oldonyosambu na Sale vilivyopo katika tarafa za Loliondo na Sale.

Alisema mafanikio hayo yalitokana na taarifa ambazo zilibainisha kwamba kuna baadhi ya watu wanamiliki silaha za kivita hivyo mahojiano makali baina ya askari wa Jeshi la Polisi na Viongozi wa Kimila na kuwataka wasalimishe silaha popote pale ambapo walikuwa wanaamini kwamba silaha hizo zitawafikia Jeshi la Polisi.

Akibainisha vijiji ambavyo silaha hizo zilipatikana kuwa ni Olorieni Magaiduru zilipatikana silaha aina ya Chinese 56 SMG moja yenye namba MT. 70B 1 2730021 na risasi 21 pamoja na silaha aina ya Semi Automatic Rifle (S.A.R) yenye namba KN 250374 ikiwa na risasi nne.

Katika kijiji cha Oldonyasambu ilipatikana silaha aina ya Mark IV yenye namba ZKK 5602 pamoja na silaha nne aina ya Chinese 56 Sub-Machine Gun (SMG) zikiwa na risasi 19. Silaha hizo nne ni Chinese 56 SMG yenye namba RT 7663, bunduki ya pili namba yake ni 563631144 na bunduki mbili nyingine hazikuwa na namba.

Kamanda Mkumbo alisema katika kijiji cha Sale silaha aina ya Chinese 56 SMG yenye namba 89020539 ikiwa na risasi 15 kwenye magazine ilipatikana pamoja na silaha nyingine mbili tofauti ambazo ni S.A.R yenye namba 25032534 na Mark III yenye namba 263126.

Aidha kamanda Mkumbo aliwataka wananchi wanaomiliki silaha za moto kinyume cha sheria wazisalimishe mara moja kwenye ofisi za mitaa, vijiji na hata vituo vya Polisi vyovyote vilichopo karibu huku akitoa onyo kwa wale ambao watakaidi na wakikutwa nazo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao. Alisema Operesheni hiyo ni endelevu na itakuwa katika maeneo tofauti ya mkoa huu na si wilaya ya Ngorongoro pekee.
 Silaha mbalimbali zikiwemo SMG 6 pamoja na risasi 59 zilizopatikana katika operesheni iliyofanyika katika wilaya ya Ngorongoro.
 Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna Charles Mkumbo akionyesha silaha mbalimbali zilizopatikana katika operesheni iliyofanyika wilayani Ngorongoro iliyofanyika wiki mbili zilizopita.
 Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo akionesha waandishi wa habari baadhi ya silaha  zilizopatikana katika operesheni iliyofanyika wilayani Ngorongoro.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha akiwaonesha waandishi wa habari moja ya silaha ya kivita aina ya Chinese 56 Sub Machine Gun (SMG) iliyopatikana kwenye operesheni iliyofanyika wilayani Ngorongoro.

NYUMBA ZA MAGOMENI COTTERS KUKAMILIKA MWEZI SEPTEMBA

$
0
0
 Eng. Athu Chulla akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani (wa pili kulia), mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba zinazojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), katika eneo la Magomeni jijini Dar es Salaam. Pembeni kwa Naibu Waziri ni Mratibu wa Ujenzi wa nyumba hizo, Arch. Christina Shayo.
 Mratibu wa Ujenzi wa nyumba  zinazojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Arch. Christina Shayo (wa kwanza kushoto), akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani,  mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba katika eneo la Magomeni jijini Dar es Salaam.
 Muonekano wa moja ya nyumba za wananchi zinazojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) katika eneo la Magomeni ikiwa katika hatua ya msingi, Nyumba hizo zinatarajiwa kuhudumia kaya 656 zitakapokamilia Septemba mwaka huu.
Mafundi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), wakiendelea na ujenzi wa nyumba za wananchi katika eneo la Magomeni. Nyumba hizo zinatarajiwa kuhudumia kaya 656 zitakapokamilia Septemba mwaka huu.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Naibu Waziri Mambo ya Nje akutana na Balozi wa Singapore nchini

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (kulia) akizungumza na Balozi wa Singapore nchini, Mhe. Tan Puay Hiang, alipomtembelea Wizarani Jijini Dar es salaam. Katika mazungumzo yao Mhe. Dkt. Kolimba alisisitiza umuhimu wa ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili sambamba na kutambua mchango wa Serikali ya Singapore kwa Tanzania katika sekta ya Elimu sambamba na kuwajengea uwezo Watumishi wa Umma. 
Mhe. Tan Puay Hiang nae akizungumza ambapo alieleza Serikali ya Singapore itaendelea kudumisha ushirikiano wa kidiplomasia uliopo baina ya Tanzania na Singapore pamoja na kuongeza maeneo ya ushirikiano hususan uwekezaji katika masuala ya nishati na miundombinu. 
Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje wakifuatilia mazungumzo. Kulia ni Bw. Charles Faini na pembeni yake ni Bw. Emmanuel Luangisa. 
Mazungumzo yakiendelea.Kushoto ni ujumbe alioambatana nao Mhe. Tan Puay Hiang. 
Picha ya pamoja.

NGOMA AWEKA WAZI MADUDU YA VIONGOZI WA YANGA

$
0
0
MSHAMBULIAJI wa Yanga wa kimataifa kutoka nchini Mzimbabwe Donald Ngoma amesema ataondoka katika klabu hiyo kukwepa mambo ya ovyo ya uongozi.

Ngoma amesema hayo wakati akizungumzia tuhuma dhidi yake juu ya kutocheza mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Simba Jumamosi, Yanga ikichapwa mabao 2-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Amesema kwamba ataondoka Yanga baada ya kuchoshwa na 'madudu' ya uongozi wa timu, mchezaji huyo amesema kwamba mashabiki na wapenzi wa Yanga wamekuwa wakimshutumu na kumtukana kutokana na taarifa zisizo za kweli zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu yeye. 
  
“Nimekuwa kimya wakati wote nikitukanwa juu ya sababu za kutocheza, wakati ukweli ni kwamba mimi nina maumivu ya goti. Taarifa nyingi zimekuwa zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba sitaki kucheza kwa sababu ninataka kuondoka katika timu, nashangaa wapi wanapata hizo taarifa,”amesema Ngoma.

Amesema Daktari ambaye Yanga walimtumia kumtibu yeye alikuwa ‘tapeli’ na ameilia fedha klabu bila kufanya kazi yoyote. “Daktari alikula fedha za viongozi wa klabu na kuwadanganya kwamba alikuwa ananitibu amenipeleka hospitali, wakati ukweli ni kwamba nilikuwa ninatibiwa katika hospitali nyingine kwa gharama zangu mwenyewe,”amesema Ngoma.

Mchezaji huyo mrefu mwenye nguvu na kasi uwanjani, amesema kwamba baadaye Daktari huyo alipoulizwa alisema kwamba niko fiti kucheza, wakati ukweli ni kwamba sikuwa tayari kabisa kucheza.

“Alikuwa anawaambia watu kwamba maumivu yangu yanaweza kupona ndani ya wiki mbili, wakati Daktari halisi aliyekuwa ananitibu alisema ninahitaji kati ya wiki sita hadi nane kupona. Tazama huyu Daktari feki alivyoleta mtafaruku kati yangu na timu,”amelalamika Ngoma.
Donald Dombo Ngoma anaelekea kukamilisha msimu wake wa pili tangu ajiunge na Yanga akitokea Platinums FC ya Zimbabwe mwaka 2015.

Ngoma ameweka wazima kuwa kwa sasa yeye na klabu wamefikia katika hatua ambayo atachukua maamuzi muda si mrefu na atatoa taarifa sahihi za kuondoka kwake kutokana na mambo ya ovyo ya viongozi wa klabu,”ameandika Ngoma katika akaunti yake ya Instagram leo asubuhi.

TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE IKSHIRIKIANA NA TAASISI YA SAVE CHILD HEART YA NCHINI ISRAEL YAWAPELEKA WATOTO NANE KUTIBIWA MAGONJWA YA MOYO NCHINI HUMO

$
0
0
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Godwin Sharau akiongea na waandishi wa habari kuhusu watoto nane wanaokwenda  nchini Israel kwa ajili ya matibabu ya moyo. Hili ni kundi la nne la watoto kwenda kutibiwa nchini humo tangu mwaka 2015 ambapo JKCI ilianza ushirikiano  na Taasisi ya Save Child Heart  ya kuwapeleka wagonjwa nchini Israel hadi sasa watoto 40 wameshatibiwa na wanaendelea vizuri. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma ya Uuguzi   Robert Mallya.
 Baadhi ya wazazi ambao watoto wao wamekwenda nchini Israel kwa ajili ya matibabu ya magonjwa ya moyo wakifuatilia kwa karibu mkutano wa waandishi wa Habarai uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).
  Kaimu Mkurugenzi wa Huduma ya Uuguzi  kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Mallya akiwaongoza watoto wanaokweda kutibiwa magonjwa ya moyo  nchini Israel kuingia kwenye gari kwa ajili ya kwenda uwanja wa ndege kuanza safari ya kuelekea nchini humo. Serikali kupitia JKCI  kwa kushirikiana na Serikali ya Israel kupitia Taasisi ya Save Child Heart imewapeleka watoto nane (8) nchini humo kwa ajili ya matibabu ya moyo.
 Wataalamu wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) , ndugu na watoto wanaokwenda kutibiwa nchini Israel wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa safari ya watoto hao ya kuelekea nchini humo kwa ajili ya matibabu ya moyo.

Picha na Anna Nkinda - JKCI

SSRA YAZINDUA MFUMO MPYA WA KURAHISISHA MAWASILIANO

$
0
0
  Na. Georgina Misama – MAELEZO

Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) imeanzisha mfumo wa TEHAMA utakaowawezesha wanachama kutuma na kufuatilia malalamiko yao moja kwa moja kwa mamlaka hiyo.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo Cha Mahusiano na Uhamasishaji kutoka mamlaka hiyo Sarah Kibonde alisema Mfumo huo utaiwezesha SSRA kupokea na kushughulikia malalamiko ya wanachama moja kwa moja.

“Mfumo huu unapatikana katika simu za mkononi (mobile app), unapatikana kwa watumiaji wa simu za mkononi zinazotumia mfumo wa android na unatambuliwa kwa jina la SSRA” alisema Sarah.

Akitoa maelezo ya namna ya kutumia mfumo huo, Afisa TEHAMA wa SSRA Bw.Ernest Masaka alisema mara baada ya mwanachama kuingiza taarifa zake ambazo ni majina matatu, anwani ya posta, namba ya simu, pamoja na namba ya uanachama na makazi, mfumo utampa namba ya kumbukumbu ya lalamiko husika.

Aidha, taarifa hizi husaidia kumtambua muhusika na Mamlaka kufanya mawasiliano na mwanachama mwenye malalamiko pamoja na kushughulikia malalamiko husika moja kwa moja.

“Mfumo huu umeweka utaratibu wa mlalamikaji kufuatilia  hatua za utatuzi wa malalamiko yake kwa kumbukumbu za mlalamikaji” alisema Bw.Masaka.
  
Akizungumzia faida zinazopatikana kwa wanachama kutumia mfumo huo Bw.Masaka alisema ni pamoja uwekaji mzuri wa kumbukumbu kwa Mamlaka,kutoa mrejesho wa idadi na hatua za utekelezaji pamoja na mwanachama kupata mrejesho kwa haraka bila kujali mahali alipo ambayo itasaidia kupunguza ghara za fedha na muda.

Mamlaka inatoa wito kwa wanachama na wananchi wote kwa ujumla kutumia mfumo huu kwasababu unarahisisha mawasiliano kati ya mlalamikaji na Mamlaka.


Afisa Mwandamizi wa TEHAMA wa Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), David Ngh’ambi akielezea jinsi ya kutuma malalamiko kwa njia ya simu wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es Salaam,kushoto ni Afisa TEHAMA wa Mamlaka hiyo, Ernest Masaka na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Uhamasishaji cha Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (Kulia), Sarah Msika.
Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Uhamasishaji cha Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (Kulia), Sarah Msika akiwaelekeza waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mfumo wa kupokea malalamiko kwa njia ya TEHAMA wakati wa mkutano na waandishi hao uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Afisa TEHAMA wa Mamlaka hiyo, Ernest Masaka pamoja na Afisa Mwandamizi wa TEHAMA wa Mamlaka hiyo, David Ngh’ambi.

PROF. MBARAWA AZINDUA SCANNER MPYA

$
0
0
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (wa nne kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa scanner mpya ambazo zimezinduliwa leo jijini Dar es Salaam. Wa tatu kushoto ni Balozi wa China Nchini, Dk. Lu Youqing.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (katikati), akitilia saini na Balozi wa China Nchini, Dk. Lu Youqing (kulia) ya kukabidhiana scanner mpya ambazo zimezinduliwa leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Eng. Deusdedit Kakoko.
 Muonekano wa Scanner Mpya ambazo zimenunuliwa kwa msaada kutoka Jamhuri ya Watu wa China. Scanner hizo mpya moja imefungwa katika bandari ya Dar es Salaam na nyingine itafungwa katika bandari ya Tanga.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (wa pili kushoto) na Balozi wa China Nchini, Dk. Lu Youqing (wa kwanza kushoto) wakipata maelezo kutoka kwa mtaalam wa  Scanner, mara baada ya kuzindua scanner mpya zitakazotumika katika Bandari za Dar es Salaam na Tanga.  

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

IFC yazindua kampeni ya kukuza uelewa kwa watumiaji wa simu, kutuma na kupokea pesa moja kwa moja kutoka mitandao yote

$
0
0
Taasisi tanzu ya Benki ya Dunia, IFC imezindua kampeni ya Huduma ya kutumia fedha kwenda mtandao wowote bila garama.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo ya Taifa kutoka  Benki Kuu Tanzania,  Bernard Dadi amesema   huduma hiyo mpya itawanufaisha  wananchi kupunguza garama za kutumia fedha kwenda mitandao mingine.

Amesema kuwa kampeni hiyo itaongeza uelewa wa watumiaji simu za mkononi nchini juu ya namna ya kutuma na kupokea pesa kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine bila garama.

"Uwezekano huu wa huduma ya kutuma na kupokea pesa kutoka kwenye mitandao mingine moja kwa moja kwenda kwenye akaunti ya mtumiaji, unatarajiwa kuongeza idadi ya watu wanaofaidika na huduma za kifedha nchini", amesema Dafi

Amesema kuwa kufanikiwa kwa Huduma hii ambayo kampeni yake ina lengo la kufikia watu milioni moja katika kipindi cha miezi sita kutaifanya Tanzania kuwa nchi ya Kwanza duniani ambako makampuni ya simu yamekubaliana  na wateja wao kutumiana fedha moja kwa moja.
Kampeni hiyo inayoongozwa na FEM Tanzania Ltd,  inafanikishwa kwa msaada wa BOT, Taasisi ya Bill & Gates na Shirika la the Financial Sector Deepening.

Amesema, uchunguzi iliofanywa na IFC imebaini ukosefu wa uelewa wa Huduma hiyo miongoni mwa watumiaji kwa kukosa kuaminiana miongoni mwa makampuni ya simu na ushindani kwenye masoko.
Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo ya Taifa, BOT, Bernard Dadi akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari,hawapo pichani juu ya Huduma ya kutuma na kupokea pesa kutoka mtandao wowote bila garama.
 Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo y Taifa, BOT Bernard Dadi wa nne kutoka kushoto na wadau mbali mbali wa kampuni za simu nchini, wakiangalia onyesho la uzinduzi kutoka kwa Vijana wanaofanya kampeni ya kuhamasisha matumizi ya Huduma ya kutuma fedha kwenda mitandao yote.
 Mkurugenzi Bernard Dadi wa pili kulia, Mkuu wa Masoko wa Tigo, Temitope Ayedun na wadau wengine mbali mbali kutoka katika makampuni ya simu wakifuatilia kampeni za uzinduzi wa Huduma za fedha kwa njia ya simu bila garama yoyote.

Article 2

$
0
0
Make your Car  look new and stylish all the time.Meet the PIMP Cars Specialists in MacAutoAccessories @ Sinza Mori for genuine car parts and accessories ie Car Audio Systems| Car Security Alarms Installations | Wheels & Tyres |Leather Seat Covers | Batteries |Car Perfumes | American tinteds installations | HID Lights & Bulbs| Riverts | Pimpin Cars | Call our Hotlines 24/7 ::::::::::::☎️ 0715000890 or 0767 120 111 or 0767 120 222/0767120444

RIWAYA KUPATIKANA KUPITIA PROGRAMU MAALUM NCHINI

$
0
0
 Katibu wa Umoja wa waandishi wa Riwaya wenye Dira(UWARIDI) Bw.Ibrahim Gama akizungumza na waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa programu(App)  ya kuuza ,kununua na kusoma riwaya kwa njia ya simu iitwayo “UWARIDI APP” iliyozinduliwa na Umoja huo leo Jijini Dar es Salaam.Kulia kwake ni Rais wa UWARIDI Bw.Hussein Tuwa.
 Rais wa Umoja wa waandishi wa Riwaya wenye Dira(UWARIDI) Bw.Hussein Tuwa akizungumzia uanzishwaji wa programu(App)  ya kuuza ,kununua na kusoma riwaya kwa njia ya simu iitwayo “UWARIDI APP” iliyozinduliwa na Umoja huo leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Katibu wa Umoja wa umoja huo Bw.Ibrahim Gama na Abdillahi Muna kutoka Dau Technology ltd.
 Mwakilishi kutoka Dau Technology Limited Bw.Abdillahi Muna(wa kwanza kulia) akieleza jinsi program ya “UWARIDI APP” iliyozinduliwa leo na Umoja wa waandishi wa Riwaya wenye Dira(UWARIDI) kwa ajili ya kuuza ,kununua na kusoma riwaya kwa njia ya simu.Dau Technology ndio watengenezaji wa App hiyo.Wengine ni Rais wa Umoja huo Bw.Hussein Tuwa na katibu wake Bw.Ibrahim Gama.
Viongozi wa Umoja wa waandishi wa Riwaya wenye Dira(UWARIDI)Rais wa umoja huo  Bw.Hussein Tuwa na Katibu wake  Bw.Ibrahim Gama wakionyesha  waandishi wa nembo ya program yao mpya waliyoizindua leo Jijini Dar es Salaam.

Picha na Daudi Manongi-MAELEZO.

Na Daudi Manongi-MAELEZO
Umoja wa waandishi wa Riwaya wenye Dira (UWARIDI) umezindua mfumo maalum wa kuuza,kununua na kusoma riwaya kwa njia ya simu iitwayo “UWARIDI APP” leo Jijini Dar es Salaam.

Akizindua Programu hiyo Katibu Mkuu wa Umoja huo Bw. Bw.Ibrahim Gama amesema kuwa wameamua kuanzisha programu hii ili kuwawezesha wanachama wa UWARIDI kuweka riwaya zao kwa ajili ya kuuzwa na wao kujipatia malipo kutoka kwa mtengenezaji wa app hiyo.

“Kwa miaka mingi waandishi wa riwaya wamekuwa wakijaribu kutafuta njia mbalimbali za kunadi kazi zao ili kuwafikia wasomaji wao kwa urahisi,na tukaona changamoto wanazopata katika kuzipata kazi zetu na hivyo tukaamua kuandaa program hii itakayowawezesha kupata riwaya zetu kwa urahisi zaidi kwani utahitaji kuwa na programu hii tu kwenye simu yako ili kusoma muda wowote”,Aliongeza Bw.Gama.

Katika mfumo huo kutapatikana riwaya za waandishi mchanganyiko ikijumuisha waandishi nguli na wachanga  ambapo mpaka sasa zaidi ya waandishi 20 wameweka riwaya zao katika mfumo huo na zinaendelea kuongezeka kila siku.

Aidha sababu kuu za kuanzisha mfumo huu ni wauzaji wa vitabu vya riwaya wamekuwa hawapati malipo ya vitabu vyao kwa wakati wanapozikabidhi kwa wachuuzi wa vitabu kwa utaratibu wa kupata malipo baada ya kuuza vitabu hivyo, pia kukosekana kwa maduka rasmi ya vitabu vya riwaya nchini na wasanii wachanga na wanaochipukia kutokuwa  na uwezo wa kifedha wa kuchapa vitabu.

Kwa upande wake Rais wa UWARIDI Bw.Hussein Tuwa alieleza faida za mfumo huo kwa watumiaji wake kwa kusisitiza kuwa kazi zitakazokuwa katika mfumo huo zitakuwa salama kwa kutoweza kunakiliwa na kuuzwa nje ya mfumo,pia waandishi wake watapata pesa kwa wakati,waandishi wachanga ambao hawajaweza kuchapisha vitabu vyao wataweza kuweka kazi zao kwa urahisi tofauti na kusubiri kuzi kuchachapwa kitabuni pamoja na wasomaji walioko mbali na maeneo walipo waandishi watazipata riwaya hizi kwa urahisi na wakati wowote.

UWARIDI ni umoja uliosajiliwa rasmi serikalini mwaka 2016 ukiwa unaundwa na mchanganyiko wa waandishi mahiri na wale wanaochipukia katika uandishi wa riwaya nchini.

ALI KIBA KUTIMKA KESHO MAREKANI,KUPIGA SHOO TANO

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii


Siku moja mara baada ya kuwasili nchini akiwa na tuzo ya MTV base msanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Kiba, ameondoka nchini kwenda Marekani kwa ajili ya maonyesho yake ya kimuziki katika nchi hiyo.

Akizungumza na mwandishi wa globu ya jamii ,mdogo wa msanii huyo Abdul Kiba amesema kuwa kiba amerudi nchini kwa ajili ya kuleta tunzo kwa Watanzania na hivyo kesho jioni tunaondoka kwenda marekani.

“tunaondoka kwenda marekani na tutafanya maonyesho matano katika miji tofauti ya nchi hiyo hivyo mashabiki wetu waendele kutegemea kupata makubwa kutoka kwetu” amesema Abdul Kiba.

Amesema kuwa  kwa sasa ratiba yao ipo taiti katika kufanya maonyesho ya kimataifa na wakirejea watafanya kitu kikubwa kwa watanzania na Afrika kwa ujumla.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Kiba.

JUMUIA YA WAZAZI WATAKIWA KUUUNGA MKONO SERIKALI KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA

$
0
0
 Katibu wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Stanley Mkandawile akizungumza na baadhi ya viongozi wa Jumuia hiyo kutoka katika Kata mbalimbali za wilaya ya Ilala, alipokutana nao katika kikao maalum cha kujitambulisha kwao, kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM wilaya ya Ilala. Kulia ni Katibu wa Jumuia hiyo wilaya ya Ilala, Lugano Mwafongo. 

Akizungumza kwenye kikao hicho, pamoja na mambo mbalimbali Mkandawile ameitaka Jumuia ya Wazazi katika mkoa wake na maeneo mengine nchini, kuunga mkono hatua ya serikali kuingia katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya.

Mkandawile amesema, Kama sehemu ya Wanana CCM, Jumuia hiyo haiba budi kuunga mkono mabambano hayo kwa kuwa Serikali inatekeleza ilani ya CCM, ibaraya 118 hadi 119.
Katibu wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Stanley Mkandawile akiwasili ukumbini. Kushoto ni Katibu wa Jumuia hiyo wilaya ya Ilala, Lugano Mwafongo na kulia ni Katibu wa Jimbo la Ilala Christopher Lugemalila.
 Wajumbe wakiwa ukumbini
Wajumbe wakishangilia jambo ukumbini
Katibu wa CCM Jimbo la Ilala, Said Dogo akitoa maneno ya utangulizi kabla ya kikao kuanza. Kulia ni Mkandawile na Lugano Mwafongo
Wajumbe ukumbini wakifuatilia mazungumzo katika kikao hicho
Mjumbe akiwa kwenye kikao hicho cha Jumuia ya Wazazi huku akiendelea na malezi ya mwanae ukumbini
Mwenyekiti wa CCM, Jimbo la Ilala Christopher Lugemalila akizungumza wakati wa kikao hicho
Katibu wa Jumuia ya Wazazi wilaya ya Ilala, akizungumza wakati wa kikao hicho
Katibu wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Stanley Mkandawile akizungumza na baadhi ya viongozi wa Jumuia hiyo kutoka katika Kata mbalimbali za wilaya ya Ilala, alipokutana nao katika kikao maalum cha kujitambulisha kwao, kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM wilaya ya Ilala.
Wajumbe wakimsikiliza Mkandawile
Wajumbe wakimsikiliza Mkandawile wakati akizungumza na watendaji na viongozi wa Jumuia ya Wazazi Wilaya ya Ilala. Picha zote na Bashir Nkoromo

TRA NA WASHAURI WA KODI 100 WAJADILIANA SHERIA ZA KODI

$
0
0
 Mkurugenzi wa Divisheni ya Mashauri ya Madai na Usuluhishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,  Obadia Kameya akifungua semina ya  elimu ya sheria za kodi iliyofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ambapo washauri wa masuala ya kodi walijadili namna ya utekelezaji wa mabadiliko mbalimbali katika sheria za kodi nchini.
 Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo akizungumza wakati wa semina ya  kujadili namna bora ya utekelezaji wa mabadiliko katika sheria za kodi iliyofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania.
 Washauri wa masuala ya Kodi (Tax Consultants) walioshiriki katika semina ya kujadili namna bora ya utekelezaji wa mabadiliko ya sheria za kodi nchini iliyotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na kampuni ya ushauri wa masuala ya kodi ya Hanif Habib & Co.Semina hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Benki Kuu jijini dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Divisheni ya Mashauri ya Madai na Usuluhishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,  Obadia Kameya akiwa katika picha ya pamoja na Washauri wa masuala ya kodi (Tax Consultants) baada ya semina ya majadiliano ya namna bora ya utekelezaji wa mabadiliko na maboresho katika sheria za kodi nchini kuisha.Semina hiyo ilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa benki kuu ya Tanzania.

OPERESHENI YA KUSAKA WASAMBAZAJI WA POMBE ZA VIROBA YAANZA RASMI LEO

$
0
0
 Mwanasheria toka Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw. Manchare Heche akikagua moja ya pombe aina ya Kiroba Original mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati wa operesheni ya kusaka wasambazaji wa kinywaji hicho ambacho Serikali imepiga marufuku kutumika.
 Mwanasheria toka Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw. Manchare Heche (kulia) akipata maelekezo toka kwa msimamizi wa ghala lanalohifadhi pombe aina ya kiroba original Bw. Mhina Rashid (kushoto) Original mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati wa operesheni ya kusaka wasambazaji wa kinywaji hicho ambacho Serikali imepiga marufuku kutumika, katikati ni Mkaguzi wa Chakula toka TFDA Bw. John Nzila.
Sehemu ya Shehena ya maboksi ya pombe aina ya Kiroba Original ilikutwa katika ghala lililopo  Mabibo jijini Dar es Salaam.
 Mwanasheria toka Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw. Manchare Heche akizungumza na waandishi wa habari katika ghala la kuhifadhi pombe aina viroba  lililopo Mabibo jijini Dar es Salaam wakati wa operesheni ya kusaka wasambazaji wa kinywaji hicho ambacho Serikali imepiga marufuku kutumika.
 Msimamizi wa Kiwanda cha Afro American Industries ambacho kinatengeneza pombe aina ya Viroba akitoa maelezo kwa Mwanasheria wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw. Manchare Heche wakati wa operesheni ya kusaka wasambazaji wa kinywaji hicho ambacho Serikali imepiga marufuku kutumika.
 Mwanasheria toka Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw. Manchare Heche akikagua baadhi ya nyara za Kiwanda cha Afro American Industries ambacho kinatengeneza pombe aina ya Viroba wakati wa operesheni ya kusaka wasambazaji wa kinywaji hicho ambacho Serikali imepiga marufuku kutumika.
Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira toka Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Mayungi (Kushoto) akisisitiza jambo kwa Msimamizi wa Kiwanda cha Afro American Industries ambacho kinatengeneza pombe aina ya Viroba mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati wa operesheni ya kusaka wasambazaji wa kinywaji hicho ambacho Serikali imepiga marufuku kutumika.

Picha zote na Eliphace Marwa - Maelezo
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images