Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1155 | 1156 | (Page 1157) | 1158 | 1159 | .... | 1898 | newer

  0 0

   


  0 0
  Mkurugenzi wa Taasisi ya Binti Foundation, Johari Sadiq, akimkabidhi vifaa vya shule Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Mwananyamala Kisiwani, Tuwaje Mohamed kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma shuleni hapo ambao wanatoka katika familia duni. Wa pili kulia ni Caroline Magoti.

  Mkurugenzi wa Taasisi ya Binti Foundation, Johari Sadiq, akimkabidhi sare za shule, Esther Amon.

  Wanafunzi wakiwa darasani.

  Mkurugenzi wa Taasisi ya Binti Foundation, Johari Sadiq, akizungumza na waandishi habari wakati wa hafla hiyo.

  Mkurugenzi wa Binti Foundation, Johari Sadiq, akimkabidhi sare za Shule mwanafunzi wa Shule ya Msingi, Mwananyamala Kisiwani, Esther Amon, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo ya kusaidia wanafunzi wanaotoka katika familia duni ili waweze kupata vifaa vya shule.

  Mkurugenzi wa Binti Foundation, Johari Sadiq akikabidhi sare za Shule kwa baadhi ya wanafunzi wa naotoka katika familia duni wanaosoma katika Shule ya Msingi, Mwananyamala Kisiwani jijini Dar es Salaam.

  Pokeeni vifaa vya Shule.

  Mkurugenzi wa Taasisi ya Binti Foundation, Johari Sadiq, akiwakabidhi sare za shule baadhi ya wanafunzi wanaosoma katika Shule ya Msingi Mwananyamala Kisiwani jijini Dar es Salaam, wanafunzi hao wanatoka katika familia duni.

  Mkurugenzi wa Taasisi ya Binti Foundation, Johari Sadiq, akiwaonesha kitu wanafunzi wa darasa la tatu Shule ya Msingi Mwananyamala.

  Wanafunzi wakipokea zawadi.
  Wanafunzi waliopata vifaa vya Shule wakiwa katika picha ya pamoja.

  0 0


  Na Karama Kenyunko, blog ya jamii

  Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), amewataka wananchi kuzibua mitaro ili kuepuka mafuriko yanayoweza kutokea katika mvua za masika za mwezi Machi hadi Mei Mwaka huu.

  Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dk. Agnes Kijazi amesema licha ya kwamba mvua hizo zinatarajiwa kuwa za wastani na nyingeni juu ya wastani katika maeneo mingi nchini ni vema wananchi wakachukua tahadhari mapema.

  Amesema kuwa, taadhari hizo zitasaidia wananchi kuondokana na kukumbwa na mafuriko kwa baadhi ya maeneo nchini, kuepuka vifo na magonjwa ya mlipuko.

  Aidha amewataka wananchi kutunza maji katika mvua hizo zinazoanza kunyesha ili kuepuka athari za upungufu wa maji uliojitokeza

  Aliongeza kuwa, msimu wa mvua za November hadi Aprili mwaka huu ni mahususi kwa maeneo ya Magharibi mwanchi, kanda ya kati, nyanda za juu kusini-magharibi, kusini mwa nchi na pwani ya kisini.

  Amesema mvua katika mikoa ya Njombe, Songwe Ruvuma, Mtwara, Lindi, pamoja na eneo la Morogoro Kusini (Mahenge) zinatarajiwa kuwa za wastani.

  Aidha aliongeza kuwa katika mvua zinazoendelea katika mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi na Rukwa zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani na pia zinatarajiwa kuisha katika wiki ya pili na ya tatu ya mwezi Aprili mwaka huu

  "Mikoa ya Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, kusini mqa Morogoro na ile ya kusini na pwani ya kusini inatarajiwa kuwa na mvua za wastani.

  Dk Kijazi Aliongeza kuwa mvua za msimu huu zinatatarajia kuisha katika wiki ya nne ya mwezi Ap. rili hadi wiki ya kwanza ya mwezi Mei mwaka hui.
  Mkurugenzi wa Mkuu wa TMA Dk. Agnes Kijazi akizungumza na wanahabari juu ya mwelekeo wa mvua za masika za mwezi Machi  hadi Mei mwaka huu.Leo jijini Dar es Salaam.
  Wanahabari wakimsikiliza Dk. kijazi kwenye  mkutano wa Uelekeo wa mvua za Masika mwezi Machi hadi Mei mwaka huu Leo jijini Dar Es Salaam.
  Mkurugenzi wa utafiti wa Mamlaka ya Hali ya Hewa, Ladislaus Chan'ga akifafanua jambo mbele ya wanahabari Leo jijini, kulia ni Mkurugenzi Mkuu Dk. Kijazi

  0 0

   Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko, akihutubia wananchi baada ya kufungua rasmi  daraja linalounganisha Kata ya Bonyokwa na Kata ya Kinyerezi katika Manispaa ya Ilala, jijini Dar es salaam.
   Mbunge wa Viti Maalumu, Anatropia Theonesti (Chadema) akihutubia wakati wa ufunguzi wa daraja hilo
   Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko, akikiwa amekata utepe ikiwa ni ishara ya  kufungua rasmi  daraja linalounganisha Kata ya Bonyokwa na Kata ya Kinyerezi katika Manispaa ya Ilala, jijini Dar es salaam.

  Mwandishi wetu
  MSTAHIKI MEYA wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko jana alifungua rasmi daraja linalounganisha Kata ya Bonyokwa na Kata ya Kinyerezi katika Manispaa ya Ilala, jijini Dar es salaam.

  Awali akizungumza katika hafla hiyo Mhandisi wa Manispaa ya Ilala ndugu Benjamin Maziku alisema  daraja hili limejengwa kwa takribani mwaka mmoja na kugharimu Tsh.million  478 hadi kukamilika kwake leo hii. Ujenzi wa daraja hili umesua sua kwa siku nyingi kutokana na sababu mbali mbali lakini kutokana na usimamizi imara wa Mstahiki Meya wa Ilala Mhe. Charles Kuyeko sasa historia imebadilika.

  Meya Kuyeko akizungumza na umati wa wananchi waliokusanyika kushuhudia ufunguzi huo amewasitiza kulilinda na kulitunza vyema daraja hilo kwani limejengwa kwa kodi zao.

  Awali, Meya akitoa historia ya daraja hilo amesema kuwa, waliokuwa wanatakiwa kujenga daraja hilo ni wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad) lakini kutokana na kusuasua kwao, Mimi (Meya)  niamua kuingilia kati kwa Manispaa kutenga Fedha kujenga daraja la muda ili kuwasaidia wananchi wa Bonyokwa kuondokana na atha ya kuwa Kisiwa hususani wakati wa Mvua.

  Kuyeko ambaye pia ni Diwani wa kata ya bonyokwa amewaambia wananchi hao waliofurika kwenye uzifunguzi huo kuwa huo ni mwanzo tu wa utekelezaji wa ahadi zake katika kutatua kero za wananchi na wapiga kura wake. "Nawahakikishia kuwa hamtajutia kunipa kura zenu kwani daraja hili imekuwa kero ya miaka nenda rudi lakini Mimi nimeimaliza kwa muda mfupi kwa kushirikiana na watendaji wangu hivyo mtarajie mengi kabla mwaka huu kuisha hata daladala zitakuwa zinafika hadi kisiwani".

  Mbali na hayo,Meya amewaahidi wananchi hao muda mfupi ujao atatatua kero ya maji na barabara kama ambavyo aliahidi kutekeleza wakati wa kampeni.

  Ufunguzi huo ulihudhuliwa na viongozi mbali mbali wa kiserikali na kisiasa akiwemo mbunge wa Viti Maalum Mhe. Anatropia Theonest, madiwani wa kata mbalimbali na viongozi wa vyama vya siasa.

  Akitoa salam kwa niaba ya viongozi wa vyama vya siasa, Dk.Makongoro Milton Mahanga mbunge wa zamani jimbo la Segerea ambaye kwa sasa ni, Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Ilala alisema, "Tangu niwe kiongozi sijawahi kuona kiongozi mahiri kama Meya Kuyeko. 

  Ameweza kuwaunganisha viongozi wa Manispaa yake na kuwa kitu kimoja, na hadi sasa ameshafanya vitu vingi ambavyo awali vilishindikana nakupongeza sana Meya Kuyeko.

  Dkt. Mahanga  aliwasisitiza wananchi kuwaamini viongozi wanaotokana na UKAWA kwani ni wazuri jifunzeni kwa Kuyeko mambo makubwa anayoyafanya. Kwa niaba ya Chadema nampongeza sana Meya Kuyeko kwa kukiwakirisha vyema  chama kwa wananchi.

  Naye Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Segerea ndugu Gango Kidera aliwataka wananchi wa Bonyokwa  waendelee kumwamini na kumuunga mkono Meya Kuyeko, Baraza lake la Madiwani kwani amekuwa mfano bora kwa kutekeleza ahadi zake zinazotokana na ilani na Sera za Chadema/UKAWA. 

  Chadema imemtuma Kuyeko kuwatumikia wananchi wa Bonyokwa na Manispaa nzima ya Ilala kwa kuhakikisha anatatua kero zao kwa spidi ya mwendokasi na leo tumeona anatenda kwa maslahi ya wananchi. Nakupongeza sana Meya Kuyeko, alisema Kidera

  Viongozi wengine waliozungumza katika ufunguzi huo ni Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Anatropia Theonest ambaye aliwapongeza wananchi wa Bonyokwa kwa kumchagua Kuyeko, wananchi wa Bonyokwa mlifanya maamuzi sahihi kuchagua Chadema kwa sababu bila Chadema Meya Kuyeko tusingempata. 

  Anatropia pia alimpongeza Meya Kuyeko kwa kuendelea kutatua kero za wapiga kura wa Bonyokwa siku hadi siku na Ilala kwa ujumla. UKAWA kwa Manispaa ya Ilala chini ya Meya Kuyeko imeleta matumaini makubwa kwani wakazi wa Manispaa wapatao 1,415,443 walikuwa wamekata tamaa kabisa kwani viongozi waliopita walishindwa kutatua kero za wananchi, hivyo UKAWA chini ya Meya Kuyeko ni mfariji mkuu wa wananchi, alisema Anatropia.

  Diwani wa Buguruni Mhe. Penza wa CUF akizungumza kwa niaba ya Madiwani wa Ilala alisema ilani ya UKAWA imeweka vipaumbele kwenye Barabara, maji, afya, elimu, na masoko na mitaji hivi vyote vinafanyika.

  Meya Kuyeko aliwashukuru wananchi kwa kuendelea kumwamini na kumpa ushirikiano wa karibu hali ambayo inampa ari ya kuwatumikia kwa nguvu zake zote. Pia amekishukuru chama chake Chadema, viongozi, Madiwani na watendaji wote wa Manispaa ya Ilala wakiongozwa na Mkurugenzi kwa kumpa ushirikiano wa hali na Mali katika kuwatumikia wananchi.


  0 0


   Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Ally Mwakababu akizungumza wakati wa kikao cha pamoja baina yao na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkinga kuhusu umuhimu wa kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ili waweze kunufaika na huduma zitolewazo
   Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkinga,kushoto ni Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)Ally Mwakababu kulia ni Mratibu wa CHF wilaya ya Mkinga,Rashid Gembe
   Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kushoto akifuarahia jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkinga,Rashid Gembe mara baada ya kufungua kikao cha pamoja baina ya Mfuko huo na watumishi wa Halmashauri hiyo kuhusu umuhimu wa kujiunga na mfuko huo ili kuweza kunufaika na huduma zinazotolewa.
  Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Miraji Kisile akieleza umuhimu wa watumishi wa halmashauri hiyo kujiunga  na mfuko huo ili kuweza kunufaika na huduma zinazotolewa wakati wa kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
  Kutoka kushoto ni Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu akiteta jambo na Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga,Miraji Kisile katikati kushoto ni Mratibu wa CHF wilaya ya Mkinga Elizaberth Dickson kabla ya kuanza semina hiyo ya uhamasishaji wa watumishi kujiunga na mfuko huo
  Daktari akiwapima baadhi ya watumishi wa halmashauri huo
   Daktari akiwapima baadhi ya watumishi wa halmashauri huo
  Afisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Juliana Mathias wa pili kulia akiwapima baadhi ya watumishi wa Halmashauri hiyo uzito wakati wa uhamasishaji huo 
   Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkinga wakifuatilia kikao hicho
  Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkinga wakifuatilia kikao hicho
  Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka aliyemtembelea Makamu wa Rais ofisini kwake leo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwake, Ikulu jijini Dar es salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwake ,Ikulu jijini Dar es Salaam.

  (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

  0 0   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye, ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

  0 0

  Na Chalila Chibuda wa Blogu ya Jamii.

  Baadhi ya wasanii walioshiriki katika kampeni 2015 (Mama ongea na mwanao) wamepinga uvumi ulioenea kuwa wasanii hao waliofanya kampeni  nchi nzima na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassani hawakulipwa.

  Akizungumza leo na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam,msemaji wa Mama Ongea na Mwanao,Ndumbago Misayo (Thea) amesema taarifa hizo za kutokulipwa katika kampeni sio za kweli na kinachofanyika ni kumchafua Makamu wa Rais ,Mama Samia pamoja na kikundi cha wasanii walioshiriki kampeni za uchaguzi 2015.

  Kwa upande wake mwenyekiti wa muda wa kundi hilo, Yobnesh Yussuf (Baturi) amesema shutuma hizi zinatokana na baadhi ya wasanii kushawishiwa kuongea uongo kwa masilahi yao.

  "Wasanii wote tumelipwa na mikataba ipo na haiwezekani mtu mwenye jina ukajitokeza mbele ya vyombo vya habari kuzungumza uongo wakati wewe ndio uliokuwa unalipa wenzio hicho kitu hakiwezekani" amesema.

  Aliongeza kuwa kundi la Ongea na Mwanao bado lipo na linaendelea vizuri chini ya Makamu wa Rais , Mama Samia Hassan Suluhu.

  "Msanii aliotangaza kuwa sisi wasanii hatujalipwa ni Wema Sepetu wakati yeye ndio alikuwa mlipaji wa kundi hilo.
   Msemaji wa Mama Ongea na Mwanao,Ndumbago Misayo (Thea) akizungumza na waandishi wa habari juu ya taarifa katika mitandao ya kijamii  inayodai kuwa wasaanii waliozunguka na Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu hawakulipwa  leo jijini Dar es Salaam.kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Mama Ongea na Mwanao, Yobnesh Yussuf (Baturi). Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
   Makamu Mwenyekiti wa Mama Ongea na Mwanao, Yobnesh Yussuf (Baturi) akizungumza katika mkutano  na waandishi habari juu ya madai ya kutolipwa katika kampeni za mwaka 2015  leo jijni Dar es Salaam. kulia ni Msemaji wa Mama Ongea na Mwanao, Ndumbago Misayo (Thea)
  Baadhi ya wasanii wakiwa katika picha ya pamoja leo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Mamkamba. (MB) akitoa Taarifa kwa Umma kuhusu marufuku ya uzalishaji, uingizaji , usambazaji,na matumizi ya vifungashio vya plastiki maarufu kama viroba vinavyotumika kufungashia pombe kali, alipozungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Mtaa wa Luthuli Jijini Dare es Salaam Leo.
  Katikati Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba. (MB) akitoa Taarifa kwa Umma kuhusu marufuku ya uzalishaji, uingizaji , usambazaji,na matumizi ya vifungashio vya plastiki maarufu kama viroba vinavyotumika kufungashia pombe kali, kulia ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Profesa Faustin Kamuzora na Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mazingira, Waziri Makamba alizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake mtaa wa Luthuli Jijini Dare es Salaam Leo.
  Mtakumbuka tarehe 20 Februari 2017 Ofisi ya Makamu wa Rais ilitoa tamko la Serikali la utaratibu utakaotumika kutekeleza agizo la kusitisha utengenezaji, uuzaji na matumizi ya pombe kali zinazofungashwa kwenye vifungashio vya plastiki (viroba)kuanzia tarehe 1 Machi 2017. Utekelezaji wa katazo hili utazingatia Ibara ya 8(1) (b) na 14, Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 na Kanuni zake zilizotungwa kupitia kifungu 230 (2) (f) cha sheria hiyo, na Sheria ya Leseni za Vileo Namba 28 ya mwaka 1968 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2012.


  Napenda kusisitiza na kuujulisha umma wa Tanzania kuwa utekelezaji wa maamuzi haya ya Serikali kuhusu usitishaji uingizaji, uzalishaji, uuzaji na matumizi ya vifungashio vya plastiki vya kufungia pombe kali utaanza rasmi tarehe 01 Machi, 2017, katika Mikoa yote ya Tanzania Bara. 

  Operesheni ya kukagua utekelezaji wa agizo la serikali la usitishaji utengenezaji, uuzaji na matumizi ya pombe zinazofungashwa kwenye vifungashio vya plastiki itaendeshwa nchini kote kuanzia tarehe 2 Machi 2017 kwa kupitia Kamati za Ulinzi na Usalama na Kamati za Mazingira katika ngazi ya Mkoa, Wilaya, Tarafa, Kata, Vijiji na Mtaa. Kamati hizi zitawajibika kuwasilisha taarifa za operesheni wakati na baada ya operesheni hiyo Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na nakala Ofisi ya Makamu wa Rais.


  Mnamo terehe 24 Februari 2017, kiliitishwa kikao cha Mawaziri na viongozi wa taasisi za Serikali kujadili mpango wa utekelezaji wa zuio hili. Katika kikao hicho, Wizara na taasisi za Serikali zilipewa majukumu mbalimbali, kama ifuatavyo: 

  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa kuzingatia umuhimu wa ujazo katika utozaji kodi, imeanzisha mfumo wa stempu za Kielektroniki ili kudhibiti ujazo wakati wa uzalishaji kwa ajili ya kupata mapato stahiki. Aidha, Mamlaka itahakikisha kwamba wazalishaji na waingizaji nchini wa malighafi ya pombe kali (ethanol) wamesajiliwa na kwamba mfumo wa ufuatiliaji wa usambazaji malighafi hiyo unawekwa. 

  Wazalishaji na waingizaji wa malighafi hiyo watawauzia wale tu ambao wamepewa kibali na pia watatakiwa kutoa taarifa kila baada ya miezi mitatu (3) ya kiasi cha ujazo kilichouzwa na wateja waliouziwa ambao wamesajiliwa. Uuzaji wa malighafi kwa watengezaji wa pombe kali ambao hawajasajiliwa itakuwa ni kosa la jinai kulingana na Sheria. 

  Mkemia Mkuu wa Serikali ambaye ndiye msajili wa kemikali za viwandani na majumbani, atasajili makampuni na taasisi zinazoingiza kemikali za viwandani na majumbani nchini ikiwa ni pamoja na Ethanol. Msajili atawajibika kutoa taarifa sahihi za majina ya makampuni na watu binafsi na taasisi zinazohusika, kiasi kilichoingizwa na kimetumika, pamoja na madhumuni ya matumizi. 

  Kulingana na sheria ya Leseni ya Vileo Na 28 ya Mwaka 1968 na marekebisho yake ya mwaka 2012, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa katika operesheni hii itaratibu zoezi hili katika mikoa, wilaya, tarafa, kata, vijiji na mitaa yote Tanzania bara kwa kuhakikisha kuwa wanaofanya biashara ya pombe ya kawaida na pombe kali (spirit) na watumiaji kinyume na masharti ya leseni za vileo wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria. 

  Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kupitia Shirika la Viwango Tanzania (TBS), katika operesheni hii watakukagua viwanda vyote vinavyojihusisha na uzalishaji wa vileo na vifungashio vya aina mbalimbali vya kufungia pombe kali kama vimekidhi viwango vya kitaifa Ukaguzi katika viwanda vya plastiki utachunguza kama kuna mitambo ya kuzalisha vifungashio vya plastiki kwa ajili ya pombe kali. 

  Mitambo ya kuzalisha vifungashio vya plastiki kama haitumiki kwa kuzalisha bidhaa zingine katika kiwanda husika, mwenye kiwanda atalazimika kutoa ufafanuzi wa hatima ya mitambo hiyo. Mitambo ya kuzalisha vifungashio vya plastiki itakayokutwa inaendelea kuzalisha pombe kali na kufungashia vifungashio vya plastiki itakamatwa na kutaifishwa na wahusika watashtakiwa. 

  Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Watoto na Wazee, kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na mabwana afya katika operesheni hii watatoa elimu kwa umma na kukagua maeneo yote yanayotumika kuhifadhia, kuuza na kusambaza vileo vya aina zote, na kushiriki kukamata vileo ambavyo vipo kinyume cha sheria na kanuni. 

  Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, kupitia Idara ya Habari Maelezo, itasaidia kutoa elimu kwa umma kuhusu suala hili. 
  Wizara ya Mambo ya Ndani, kupitia Jeshi la Polisi, na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, itashiriki katika operesheni, ikiwemo kwenye masuala ya inteligensia. 

  Ofisi ya Makamu wa Rais na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira, wataratibu operesheni. 


  Kama tangazo letu la tarehe 20/2/2017 lilivyoonesha muda wa nyongeza unaweza kutolewa kwa wazalishaji halali ambao wataonyesha ushahidi wa kuelekea kuhamia kwenye teknolojia ya chupa, na kwamba watahitaji muda mchache kufanya hivyo, na ambao watatimiza masharti kadhaa na kupata kibali maalum kabla ya tarehe 28/2/2017. Hadi sasa Serikali imepokea maombi ya wazalishaji 9. Tutangaza kesho iwapo kuna ambao wamekidhi masharti au la. Kanuni za upigaji marufuku pombe hizi zipo tayari.


  Pia tumepokea malalamiko kwa wazalishaji wengi kwamba zoezi hili limekuja ghafla na wengine wana malighafi na bidhaa kwenye maghala. Ukweli ni kwamba Serikali ilitoa taarifa Bungeni, kuanzia mwezi Mei 2016, na mara kadhaa baada ya hapo, na rekodi zipo, kuhusu hatua hizi. Vilevile, taarifa ya Serikali iliyotangaza kupiga marufuku pombe za viroba ziliripotiwa kwa ukubwa stahiki kwenye vyombo vya habari, ikiwemo kwenye ukurasa wa kwanza wa gazeti la Mwananchi, mwezi Agosti 2016. Katika taarifa zote za nyuma, Serikali ilitangaza kwamba hatua hiyo itaanza tarehe 1 Januari 2017. Hatua hizi zimechelewa kwa miezi miwili. Iwapo, baada ya taarifa hizo za Serikali, kuna mzalishaji ameagiza malighafi au kutengeneza au kuhifadhi pombe za viroba, au kuchukua mkopo kwa ajili hiyo, atakuwa amefanya hivyo akijua madhara yake.


  Mwisho napenda kutoa wito kwa wananchi wote kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa zoezi hili la upigaji marufuku matumizi ya pombe zinazofungashwa katika vifungashio vya plastiki (viroba) kwa kutoa taarifa kwa vyombo husika ili wale wanaozalisha na kuuza au kuhifadhi waweze kuchukuliwa hatua stahiki. Zawadi itatolewa kwa watakaotoa taarifa zitakazowezesha kukamatwa kwa watakaokiuka zuio hili.


  OFISI YA MAKAMU WA RAIS

  28/02/2017

  0 0

  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

  Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifamba amekana kuhusika na utumaji wa ujumbe katika mitandao ya kijamii juu ya kuitisha mkutano na waandishi wa habari. 

  Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Rais wa Shirikisho hilo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya ujumbe huo uliokuwa ukisambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii na kumuhusisha Rais wa Shirikisho hilo. 

  Mwakifamba amesema kuwa ujumbe huo umeeleza kuwa Rais wa shirikisho hilo atakuwa na mkutano na waandishi wa habari utakaohusu wasanii waliokipigia kampeni Chama cha Mapinduzi (CCM) na kutolipwa fedha zao pamoja na kuunga mkono jitihada za msanii Wema Sepetu kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

  “Kiukweli sikushiriki kwa namna yoyote katika kuuandika ujumbe huo na nimesikitishwa kuona kwamba huo ujumbe unasambazwa ukiwa na jina langu hivyo umeniletea picha mbaya kwani ni kinyume na taratibu na sheria za Shirikisho,”alisema Mwakifamba.

  Amefafanua kuwa Shirikisho hilo sio chama cha siasa na hawajasajiliwa na msajili wa vyama vya siasa bali wamejisajiliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na kazi zote zinafanyika kwa Sheria Na. 4 ya mwaka 1976 ambayo iko chini ya Bodi ya Filamu Tanzania.

  Ameongeza kuwa mwanachama wa shirikisho hilo hafungwi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa lakini kwa mujibu wa katiba ya vyama na shirikisho ni marufuku siasa kuletwa katika shirikisho au vyama vyake.

  Kwa upande wake Afisa Mipango wa Chama cha Waigizaji, Saimon Mwapagaja ametoa rai kwa wananchi wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii kwa lengo la kuchafua majina ya watu kuacha tabia hiyo kwani inashusha hadhi ya mtu husika na sio utaratibu mzuri.

  “Changamoto tulizonazo katika tasnia ya filamu ni nyingi sana hivyo ifike wakati wasanii tuanze kuangalia vitu vya msingi na vyenye tija vitakavyomaliza changamoto hizo, pia wananchi wapunguze kujiamulia kufanya mambo ambayo baadae yanaweza kumsababishia muhusika matatizo mabukwa,” alisema Mwapagaja.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri  akizugumza na Wakazi wa kijiji cha Mbori, Kata ya Matomondo Wilayani Mpwapwa wakati wa uzinduzi wa Mnara wa Matomondo. Aidha Airtel pamoja na USCAF ilizindua minara minne wilayani hapo na kuwawezesha wakazi katika vijjiji 49 kupata huduma za mawasiliano ya uhakika.
  Meneja wa Kampuni ya Simu ya Airtel, Mkoa wa Dodoma Paschal Bikomagu akizugumza na Wakazi wa kijiji cha Mbori,  Kata ya Matomondo Wilayani Mpwapwa wakati wa uzinduzi wa Mnara wa Matomondo. Aidha Airtel pamoja na USCAF ilizindua minara minne wilayani hapo na kuwawezesha wakazi katika vijjiji 49 kupata huduma za mawasiliano ya uhakika.
  Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Jabir Shekimweri akisalimiana na mchezaji wa timu ya Manchester United ya Mbori Wilayani Mpwapwa, Juma Athmani katika mchezo wa fainali iliochezwa juzi katika uwanja wa Ikulu kata ya Matomondo Wilayani Mpwapwa. Mchezo huo ulikuwa madhumuni kwa ajili ya uzinduzi wa mnara wa simu wa Matomondo uliojengwa na Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na USCAF ili kufikisha huduma mawasiliano kwa wananchi waishio maeneo ya pembezoni mwa nchi. Manchester ilishinda kwa mabao 4-3 dhidi ya Liverpool.
  Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri akisalimiana na wachezaji wa timu ya Liverpool ya Mbori Wilayani Mpwapwa katika mchezo wa fainali uliochezwa juzi katika uwanja wa Ikulu kata ya Matomondo Wilayani Mpwapwa. mchezo huo ulikuwa na madhumuni kwa ajili ya uzinduzi wa Mnara wa simu wa Matomondo,uliojengwa Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na USCAF ili kufikisha huduma mawasiliano kwa wananchi waishio maeneo ya pembezoni mwa nchi. Manchester ilishinda kwa mabao 4-3 dhidi ya Liverpool.


  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel katika mpango wake wa kufikisha huduma za mawasiliano kwenye maeneo ya pembezoni imeshirikiana na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) kwa kujenga na kukamilisha miundombinu ya mawasiliano katika kata 10 zilizoko katika maeneo ya vijijini ili kutoa huduma bora ya mawasiliano.

  Katika kufanikisha mkakati huo, Airtel na UCSAF leo imefanya uzinduzi wa kwanza wa minara minne iliyoko katika kata za Matomondo, Mbuga and Ipera wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma ambapo uzinduzi huo utawawezesha wakazi zaidi ya  38,000 katika vijiji 49 kuunganishwa na huduma za mawasiliano toka Airtel na kufurahia huduma na bidhaa mbalimbali ikiwemo huduma za intaneti, kupiga simu pamoja na huduma ya Airtel money ili kutatua changamoto zao

  Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma za mawasiliano katika kata ya Matomondo Dodoma,  Meneja wa mauzo wa Airtel Dodoma, Bwn Pascal Bikomagu alisema” Airtel imejipanga katika kuboresha na kupanua upatikanaji wa huduma za mawasilino  ili kuchochea kukua kwa shughuli za kijamii na kiuchumi katika maeneo yaliyo na changamoto hususani vijijini

  “Kufatia uzinduzi huu leo tunawashauri wakazi wa kata ya Matomondo na vijiji vya jirani kutumia huduma za Airtel Money katika kufanya miamala ya kifedha. Huduma hii ya Airtel Money itawawezesha kutuma na kupokea pesa, kulipia ankra mbalimbali kwa urahisi na gharama nafuu, na pia kutumiaka kama mfumo rasmi wa huduma za  kifedha kwani upatikanaji wa huduma zingine za kibenki katika maeneo hayo bado ni changamoto.” Aliongeza Bikomagu

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Mh. Jabir Shekimweli Alisema “ mawasiliano ya simu ni nyenzo muhimu katika kukuza uchumi wa jamii na nchi kwa ujumla, nachukua fursa hii kuwahimiza wakazi wa kata za Ipera,Matomondo na Mbuga kutumia mawasiliano hayo katika kuboresha shughuli zao za kilimo na biashara ili kuinua kipato.

  Naye Mkuu wa Huduma za Ununuzi na Ugavi UCSAF, John Munkondya alisema  “Tunawapongeza Airtel kwakumaliza ujenzi wa minara hii yakutoa mawasiliano bora, leo hii tumeanza kuzindua huduma za mawasilino katika mkoa wa Dodoma. ni matumaini yetu tutaendelea kushirikiana na kuboresha huduma hizi za mawasiliano ili kuwafika watanzania wengi zaidi.

  Airtel ilisaini makubaliano na Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote UCSAF kwa lengo la kufikisha mawasilino katika maeneo ya pembezoni mwa nchi. Kupitia mpango huu kata 28 nchini zimeweza kufikiwa na hivyo kuongeza idadi ya minara ya mawasiliano ya Airtel kufikia 2,210 ndani ya miji zaidi 128 na hivyo kuwafikishia huduma za mawasiliano wakazi zaidi ya  asilimia 85 nchini.

  0 0

  Kamishna wa Ardhi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mary Makondo(aliyesimama) akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa ardhi hapa nchini Tanzania ambao utajumuisha mradi wa majaribio katika mikoa mbalimbali kuona kama utawezekana maana swala la upatikanaji wa ardhi imekuwa ni changamoto kubwa sana hapa nchini.
  Mkurugenzi wa Jumuiko la Maliasili Tanzania( TNRF), Joseph Olila akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa ardhi hapa nchini Tanzania uliodhaminiwa na Jumuiko la Maliasili Tanzania ili kuweza kupatikana kwa ardhi hasa maeneo ya vijijini .
  Mkurugenzi Mtendani wa Taasisi ya MVUWATA ya Morogoro, Steven Ruvuga akizungumza jinsi wanavyoweza kuhamasisha watu kwenye matumizi mazuri yaardhi pamoja na kutatua migogoro ya ardhi kwenye mkutano uliofanyika kwneye ukumbi wa Hotel ya Wanyama jijini Dar es Salaam.
  Bwana Alain Essimi  Biloa  akitoa mada juu ya matumizi mazuri ya ardhi kwenye jamii hasa kwa wananchi waishio vijijini
  Baadhi ya wadau wakichangia mada kwenye kongamano lililofanyika leo katika Hotel ya Wanyama jijini Dar es Salaam leo
  Baadhi ya wadau wakiwa kwenye mkutano wa uzinduzi wa mpango mkakati wa ardhi unaoratibiwa na Jumuiko la Maliasili Tanzania( TNRF).
  Meneja Program wa Jumuiko la Maliasili Tanzania( TNRF), Zakaria Faustine akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa uzinduzi wa mpango mkakati wa ardhi hapa nchini Tanzania ambao utajumuisha mradi wa majaribio katika mikoa mbalimbali 
  Afisa Program za Ardhi Jumuiko la Maliasili Tanzania( TNRF),Godfrey Massay akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkakati waliojiwekea kama Jumuiko la Maliasili Tanzania(TNRF) ili kufikia malengo  waliyojiwekea.
  Kamishna wa Ardhi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mary Makondo akizungumza na waandishi wa habari leo baada ya kufanya uzinduzi wa mpango mkakati wa ardhi utakaoleta tija kwa wananchi hasa vijijini.
  Picha ya Pamoja

  0 0


  0 0

   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akitoa hotuba yake ya ufunguzi katika mkutano wa Wakuu wa Mashirika ya Umma uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam mapema leo. Mkutano huo uliandaliwa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Hazina.
   Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza katika mkutano wa Wakuu wa Mashirika ya Umma ambao ulikuwa na lengo ya kujadili nafasi za Mashirika ya Umma katika utekelezaji wa Mpango wa II wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano.
   Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Profesa Joseph Semboja akitoa ukaribisho kwa Watendaji Wakuu na Wenyeviti wa Bodi za Mashirika ya Umma kwa niaba ya waandaji wa mkutano huo uliofanikiwa kuleta pamoja wakuu wa mashirika zaidi ya 70 nchini.
  Sehemu ya Wenyeviti na Wakurugenzi Watendaji wa Mashirika ya Umma wakifuatilia mkutano wa Wakuu wa Mashirika ya Umma ulioandaliwa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na Tume ya Mipango na kufanyika Ikulu, Dar es Salaam mapema leo.
   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (aliyeketi katikati), Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (wapili kutoka kulia), Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Profesa Joseph Semboja (wapili kushoto), Kaimu Msajili wa Hazina Bw. Mihalale Mwakibinga (kushoto) na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Tume ya Mipango Maduka Kessy (kulia) katika picha ya pamoja na Wenyeviti wa Bodi wa Mashirika ya Umma.
   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (aliyeketi katikati), Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (wapili kutoka kulia), Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Profesa Joseph Semboja (wapili kushoto), Kaimu Msajili wa Hazina Bw. Mihalale Mwakibinga (kushoto) na Naibu Mtendaji Mkuu wa Tume ya Mipango Maduka Kessy (kulia) katika picha ya pamoja na Wakurugenzi Watendaji wa Mashirika ya Umma.

  0 0

   Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji Ashaji amesema kwamba Mfumo jumuishi wa kifedha ni muhimu katika kujenga uchumi wa Taifa la Tanzania. 

  Dkt.Kijaji ameyasema hayo jana wakati wa mkutano wa tatu wa Kitaifa juu ya huduma rasmi za kifedha kwa vikundi vya hisa na mjadala wa masuala ya kisera na Sheria katika uhusishwaji wa kifedha.

  Alisema kuwa ili kuhakikisha swala hili linafanyiwa kazi, Serikali imeandaa sera ya mwaka 2006 inayohakikisha mifumo isiyo rasmi ya kifedha inakuwa rasmi na watu wote wanakuwa wamejumuishwa katika mfumo sahihi wa matumizi ndani ya sekta ya kifedha.

  Dkt. Kijaju alisema kuwa moja ya changamoto katika mfumo usio rasmi wa kifedha ni kukopeshwa kwa riba kubwa na watu wanaofanyakazi katika mifumo hiyo, lakini hawajarasmishwa rasmi,hali inayouwaumiza Wafanyabiashara na watanzania kwa ujumla.Dkt Kijaji akaongeza kuwa kutokana namfumo huo, Serikali sasa inaandaa sheria kwa ajili ya huduma ndogo za kifedha ilikuwekea mazingira rafiki ya kufanya kazi zao. 

  Pia aliongeza kuwa Care international amekuwa mdau mkubwa katika maendeleo ya uchumi nchini Tanzania, sio kifedha tu lakini pia sekta ya afya,Kilimo na maeneo mbalimbali,hivyo  aliwasihi wananchi waendelee kuwapa ushirikiano ili kuleta maendeleo zaidi nchini.

  Nae Mkurugenzi Mkazi wa Asasi ya Kiraia Care International Nchini Tanzania Bw. Paul Daniel alisema kuwa lengo la mkutano huo ni muendelezo wa utamaduni wa Care kutoa Fulsa ya kupeana taarifa kwa wadau walio ndani ya sekta hiyo,lengo kubwa ni kuongeza umoja na ushirikiano katika kuhamasisha uhusishwaji wa kifedha katika vikundi vya hisa.

  Mkutano huu ulihusisha wadau mbalimbali wa Serikali wakiwemo Wizara ya Fedha na Mipango,Benki kuu ya Tanzania,TAMISEMI na Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) pia Taasisi za kifedha na Sekta mbalimbali,ikiwa ni juhudi za Care nchini Tanzania ambazo zimelenga katika kutoa Fursa kwa jamii kuhamasisha usawa wa kijinsia kwa ubia wakiwahusisha sekta binafsi, Serikali,wabia wa maendeleo na asasi za Kiraia (CSO's) .Mkutano huo uliandaliwa na Asasi ya kiraia ya Care International ya Nchini Tanzania.
   Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Ashatu Kijaji akizungumza na wadau mbalimbali wa sekta za Serikali na Sekta binafsi katika hafla hiyo iliyofanyika mapema jana jijini Dar es salaam.
   Baadhi ya Wadau waliohudhuria katika mkutano huo.
   Mmiliki wa Vikundi vya Kifedha (VIKOBA) Mwalim  Monica akitoa ufafanuzi zaidi namna gani alivofaidika kupitia Care International pamoja na taasisi za kifedha. Picha na Yasir Adam Globu ya Jamii
    Mkurugenzi Mkazi wa  Asasi ya Kiraia wa Care International Nchini Tanzania Ndugu Paul Daniel akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo mbele ya Wadau,huku akielezea kwa ufupi lengo la na Mafanikio ya Care International
  Mkurugenzi Muendeshaji  wa Mfuko wa Kuendeleza Huduma za Fedha (FSDT) Bi,Irene Mlola akizungumza namna walivyo panua wigo na mafanikio yao katika vikundi mbalimbali vyenye uhitaji wa kifedha nchini Tanzania
   Baadhi ya Wadau waliohudhuria katika mkutano huo
   Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara Bw. Deo Kwiyakwa akizungumza kuhusu  Sera,sheria zinavyokwamisha Maendeleo katiaka Taasisi za Kifedha
  Mkurugenzi wa Programu (GEWE) Bi Mwanahamisi Singano akizungumza jambo katika Mkutano huo ulio wakutanisha Sekta za kiserikali na sekta binafsi

  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akizungumza katika ziara ya  Naibu Waziri wa TAMISEMI Suleiman Jafo,alipotembelea Shule ya Sekondari ya Mboga kukagua ujenzi unaondelea shuleni hapo.
  Mheshimiwa Naibu Waziri Suleiman Jaffo alitazama Ujenzi wa Maabara Tatu za Sayansi zinazojengwa , ujenzi wa madarasa mawili, Jiko la kisasa na Bwalo na Mwisho Hostel ambazo zitachukua wanafunzi 796
   Mbunge Kikwete akitoa maelezo juu ya ujenzi wa Hostel unavyoendelea kwa Naibu Waziri Jafo . 
  Mbunge akimshukuru Naibu Waziri kwa kukagua ujenzi unaoendelea katika kshule ya Sekondari Mboga.
  Naibu Waziri Jaffo akiwa na wenyeji wake wa pili upande wa kushoto ni  Mkuu wa Wilaya Bagamoyo Alhaj Majid Mwanga, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri Ndg Zikatimu  na wa tatu ni Naibu Waziri wa TAMISEMI Suleiman Jafo na Mhehimiwa Mbunge Ridhiwani Kikwete wa walipokwenda kukagua ujenzi shule ya Sekondari ya Mboga
  Mheshimiwa Naibu Waziri Jafo akiingia kwenye kikao cha kuzungumza na wadau wa maendeleo na watumishi wa Halmashauri
  Dada Mkuu wa shule ya Mboga sekondari wa kwanza kulia  kakizungumza neno kumshukuru Mbunge kwa msaada wa kuwatafutia Hostel na kukamilisha Maabara na kumuahidi kuwa watasoma kwa bidii ili asife moyo kusaidia elimu jimboni humo.

  0 0


   Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  Msafara wa mwanamuziki wa bongo fleva, Ally Kiba amesimamisha wakazi wa jiji la Dar es Salaam kwa zaidi ya saa tatu mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam akitokea nchini Afrika kusini kuchukua tunzo yake ya Msanii bora barani Afrika.

  Kiba ambaye aliwasili katika uwanja wa kimataifa wa JNA majira ya saa nane mchana na kulakiwa na wapenzi lukuki ambao aliambatana nao katika mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam. 

  Msafara huo ambao ulianzia katika barabara ya pugu kasha kuingia katika barabara ya Mandela na kuwapa fursa wakazi wa buguruni na viunga vyake vya malapa na bungoni kushuhudia msanii huyo akiwa katika gari ya wazi huku akionyesha tunzo  yake huku wakazi hao wa jiji wakimshangilia.
  Kiba alipita katika eneo alilozaliwa la Kariakoo mtaa wa Muheza na kumkabidhi mama yake tunzo hiyo na majirani zake ambao walipiga shangwe ya kutosha kutokana na mafanikio ya msanii huyo. 

  Msafara wa msani huyo ulitoka kariakoo na kupita katika mitaa ya Msimbazi, Upanga na barabra ya Sarenda kasha kuelekea moja kwa moja katika hotel ya Double Tree Masaki kwa ajili ya mahojiano na waandishi wa habari.
   
   Ally Kiba akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere  akitokea nchini Afrika Kusini mara baada ya kukabidhiwa tunzo yake ya MTV kama msanii bora wa kiume Afrika
   Kiba kielekea kwenye gari maalum aliyoandaliwa mara baada ya kuzngumza na mashabiki wake.
   Ally Kiba akiwa na ndugu yake Abdul Kiba juu ya gari la wazi katika mita ya Buguruni
   Ally Kiba akimkabidhi Tunzo yake Mama yake mzazi maarufu kama Mama k
   Mama K ambaye ni mama mzazi wa Ally Kiba akionyesha Tunzo ya msani huyo juu. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  0 0


  Na Anthony John Glob ya Jamii.

  Mkuu wa wilaya ya kinondoni Alli  Hapi ametoa muda wa siku saba kwa wachimba kokoto wa eneo la Boko chama kuondosha mawe yao yaliyopo kwenye eneo hilo, ili kupisha ujenzi wa dampo la kisasa.

  Kauli hiyo ya DC Hapi imekuja baada ya kutembelea na kukagua eneo hilo ambalo awali wachimbaji wake walipewa amri ya kutokuendelea na uchimbaji wa kokoto, lakini baadhi wamekaidi amri hiyo na kuendelea.

  Akielezea zaidi Hapi amewataka kutokuendelea kuchimba na hasa katika kipindi hiki cha mvua, kwani wanaweza kujisababishia madhara ya kufukiwa na kifusi na kupoteza uhai.

  Amesema amewaelekeza maafisa mazingira na mipango miji wa manispaa waunde timu ,waangalie uwezekano wa kuweka dampo kwenye eneo hilo, kwani eneo la dampo lililopo ni moja Pugu Kinyamwezi, ambako ni mbali.

  Aidha amesema dampo hilo lifanywe la kisasa ili uwe mradi ambao utasaidia kuingiza mapato kwa manispaa.

  Aidha HAPI ameeleza kuwa pindi eneo hilo litakapoanza kutengenezwa watu waliokuwa wakichimba hapo waandae orodha ya majina ili mawe yatakayotolewa hapo wapewe wao.

  Kwa upande wake afisa mazingira wilaya ya kinondoni Mohamed Msangi amesema, eneo hilo likifanywa dampo litarahisisha utupaji taka kwa wakazi wa eneo la boko, mabwepande, bunju,  kawe na mwenge.
   Eneo linalochimbwa kokoto na baadhi ya Wakazi wa Boko chama,ambalo kwa sasa utaratibu wake umesitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Mh.Ally Hapi
   Mkuu wa wilaya  ya Kinondoni Ally Hapi akiwa na wakazi wa Boko chama katika eneo la uchimbaji wa kokoto
    Mkuu wa wilaya  ya Kinondoni  Ally Hapi  akizungumza  na watendaji wa Kata pamoja na wenyeviti wa Serikali za Mitaa jana katika Ofisi ya Afisa mtendaji wa Kata ya Bunju katika ziara yake ya siku kumi.
   Wenyeviti wa Serikali za mitaa na watendaji katika Kata ya bunju  wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Kinondoni  Ally Hapi jana katika ziara yake.

   

  0 0

  Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga.Alhaji Mustapha Selebosi akisisitiza jambo kwenye kikao cha baraza la madiwani leo kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga,Daudi Mayeji kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga,Kassim Mbughuni
  Naibu Meya wa Jiji la Tanga,Mohamed Haniu akizungumza kwenye kikao hicho cha Baraza la Madiwani 
  Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akizungumza kwenye kikao hicho cha Baraza la Madiwani kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga,Daudi Mayeji 
  Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku akizunguza kwenye kikao cha baraza la Madiwani leo kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga,Kassim Mbughuni 
  Baadhi ya Wataalamu wa Halmashauri ya Jiji la Tanga nao wakiwa makini kuchukua baadhi ya hoja zilizokuwa zikiwasilishwa na madiwani kwenye kikao hicho cha baraza la madiwani 
  Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga (DAS) Faidha Salim akifuatilia kwa umakini kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika leo kwenye ukumbi wa Halmashauri Jijini Tanga. 
  Baadhi ya Madiwani wakifuatilia kwa umakini kikao hicho kulia ni Diwani wa Kata ya Central Jijini Tanga,Khalid Mohamed wakifuatilia kwa umakini kikao hicho
  Wakuu wa Idara kwenye Halmashauri ya Jiji la Tanga wa kwanza kulia ni Mratibu wa Ukimwi Jiji la Tanga,Moses Kisibo anayefuatia ni Meneja Mkuu wa kituo cha Television ya Jiji la Tanga (TATV) Mussa Labani wakifuatilia kwa umakini majadiliano ya kikao hicho
  Baadhi ya Madiwani wakifuatilia kwa umakini kikao hicho
  Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku kulia akiteta jambo na Diwani wa Kata ya Marungu (CCM) Mohamed Mambea mara baada ya kumalizika kikao cha Baraza la Madiwani.
  Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga (CCM).Alhaji Mustapha Selebosi kushoto akiteta jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Daudi Mayeji nyuma yao ni Naibu Meya wa Jiji la Tanga (CUF) Mohamed Haniu mara baada ya kumalizika kikao cha Baraza la Madiwani leo. Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

older | 1 | .... | 1155 | 1156 | (Page 1157) | 1158 | 1159 | .... | 1898 | newer