Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

WANACHAMA PSPF SASA RASMI KUPATA MIKOPO KUPITIA BENKI YA CRDB

0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, (kushoto), akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dkt. Charels Kimei, wakati wa uzinduzi wa ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili ambapo CRDB sasa itawakopesha Wanachama wa PSPF kwenye maeneo ya elimu, viwanja na pesa za kuanzia maisha kwa watumishi wa serikali. Uzinduzi huo umefanyika Februari 27, 2017 makao makuu ya PSPF jijini Dar es Salaam.

NA K-VIS BLOG
WANACHAMA wa mfuko wa pensheni wa PSPF sasa wataanza kupata mikopo yao kupitia benki ya CRDB mara baada ya kuzinduliwa kwa  mpango  huo  baina ya taasisi hizo mbili jana jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwenye hafla ya utiaji saini mpango huo  , Mkurugenzi Mkuu  wa PSPF, Bw Adam Mayingu , alisema kuwa mpango huo wa kutoa mikopo kwa wanachama ulianza tangu Desemba 2014 kwa kupitia taasisi nyingine za kifedha.
Alisema kuwa PSPF na benki ya CRDB wamekubaliana  kushirikiana katika kuendesha kwa pamoja huduma ya mikopo.Mikopo hiyo ni pamoja na mkopo wa elimu(education loan scheme), mkopo wa kuanzia maisha( startup life loan scheme) na mkopo wa viwanja(Nipo site na PSPF).
Alisema kuwa kwa upande wa mkopo wa elimu , mwanachama anaweza kukopa kwa ajili ya kujiendeleza kielimu katika ngazi yeyote ya elimu .Ngazi hiyo ni  stashahada, shahada, shahada ya uzamili na hata mafunzo ya ufundi.
Kwa upande wa mkopo wa kuanzia maisha, alisema mwanachama aliyepata ajira kwa mara ya kwanza huwa na mahitaji yake muhimu  na kwa kutambua hilo, PSPF kwa kushirikiana na CRDB wameanzisha  mpango huu ambapo mwanachama anaruhusiwa kukopa mishahara yake ya miezi miwili ili awaeze kujipanga na maisha mapya ya ajira.
Kuhusu mkopo wa viwanja  kwa wanachama, alisema  kuwa  huduma hii itawawezesha wanachama wa PSPF kukopa na kumiliki viwanja vya makazi ambavyo vinapataikana  maeneo mbali mbali ya nchi.
“Lengo  kubwa hapa ni kuwawezesha wanachama wa PSPF kumiliki viwanja vya makazi vilivyopimwa iii kuwaepusha dhdi ya ujenzi katika makazi holela, ambayo yamekuwa na gharama kubwa kuliko makazi yaliyopangiliwa”,alisema.
Alifafanua kuwa lengo kubwa la kuanzisha mikopo hiyo ni kuhakikisha kila mtanzania anatimiza ndoto  yake ikiwa ni katika masomo kupitia mkopo wa  elimu , ndoto yake nyingine kupitia mkopo wa kuanzia maisha au mkopo wa viwanja.
Hadi kufikia tarehe 17 Mwezi huu idadi ya wanachama walionufaika na mikopo  hiyo na idadi kwenye mabano ni  Elimu  (1,432)), mkopo wa kuanzia maisha ( 847), mkopo wa viwanja (58).
“Kwa kushirikiana na benki ya CRDB ambayo ina mtandao mkubwa wa matawi hapa nchini tunaamini watanzania wengi watanufaika na mikopo hii na kwa kufanya hivyo tutakuwa tunatakeleza juhudi za serikali ya awamu ya tano ya kuhakikisha watanzania wengi zaidi wananufaika na huduma mbali mbali za Mifuko ya Hifadhi ya jamii”, alieleza.
Kw a upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk Charles Kimei, alisema azma yao ni kuhakikisha kuwa ushirikiano na wadau wanamkomboa kiuchumi mwananchi  hususan mwenye kipato cha chini  kwa kumpatia  mkopo wenye riba ya asilimia 14 tu kwa mwaka. Kuhusu marejesho alisema ni kuanzia mwaka mmoja hadi miaka mitano.
Ushirikiano wetu na PSPF  bado una muendeleo ulio mpana kwani kwa pamoja tunadhamiria hapo baadae kuingiza sokono mikopo kwa ajili ya wastaafu ‘pensioners’.
Alisema mpango huu wa utoaji wa mikopo kw wastaafu una lengo la kuleta faraja na kuwasaidia wastaafu katika kukidhi mahitaji yao mbali mbali ya kimaisha ikiwamo kulipia gharama za matibabu, ada za shule za watoto au wajukuaa  na kuendesha biashara ndogo ndogo zitakazosaidia kupunguza ukali wa maisha ya kila siku.
Dk Kimei alifafanua kuwa  nia yao ni kujenga mazingira mazuri kwa wastaafu walio wanachama wa PSPF ili kustaafu kusiogopwe na kuonekana ni mwanzo wa kuanza kwa kipindi cha maisha ya shida yasiyokuwa na  matumaini.
“Tunataka kujenga tabia ya kuwafanya wafanyakazi wanapopata barua za kustaafu wasihuzunike kama ilivyozoeleka”,alidokezaAlisema kuwa mwanachama wa PSPF anayetaka mkopo anatakiwa aende kwenye tawi lolote la benki ya CRDB ililopo karibu naye ili kupata huduma.
 Bw. Mayingu akitoa hotuba yake kuelezea ushirikiano huo ambao lengo lake kubwa ni kupanuan wigo wa huduma kwa Wanachama wa Mfuko huo

 Dkt. Charles Kimei, akitoa hotuba yake kueleza jinsi benki yake ilivyofurahishwa na ushirikiano huo

 Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, akitoa hotuba ya ukaribisho
 Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo, (katikati), na Msaidizi Mtendaji wa Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Bw.Keneth Kasigila, wakimsikiliza Mkurugenzi wa Wateja wa Mashirika wa CRDB, Bw.Goodluck Nkini, (kushoto), wakati wa hafla hiyo.
 Bw. Mayingu, (kushoto) na Dkt. Kimei, wakibadilishana mawazo muda mfupi kabla ya kufanyika kwa uzinduzi huo
 Viongozi wa juu wa PSPF, wakipiga makofi wakati wa hafla hiyo
 Baadhi ya maafisa wa CRDB waliohudhuria hafla hiyo
 Baadhi ya maafisa wa PSPF
 Baloziwa PSPF, Mrisho Mpoto, (kushoto), akiongoza kuimba wimbo wa taifa
 Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dkt. Charles Kimei, (kushoto) na Balozi wa PSPF, Bw. Mrisho Mpoto (katikati), wakimsikiliza Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi kabla ya kuanza kwa hafla hiyo
 Baadhi ya maafisa wa PSPF waliohudhuria hafla hiyo
 Mkurugenzi wa Mipangona Uwekezaji wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo, akitoa neno la shukrani mwishoni mwa hafla hiyo
 Anna Lukando wa kampuni ya Ardhi Plan Limited, yenye ushirikiano na PSPF, akizungumzia jinsi wanachamawa Mfuko huo wanavyoweza kufaidika naupatikanajiwa viwanja vilivyopimwa kisheria
 Maafisa wa PSPF na CRDB wakifuatilia hafla hiyo
Maafisa wa CRDB

 Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS), wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Bi.Mwanjaa Sembe, (kulia), akimkabidhi kadi ya kujiunga na mpango huo, mfanyakazi wa CRDB, Bi. Fausta Urassa


 Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, (kulia), akimkabidhi kadi ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS),  mfanyakazi wa CRDB, Bw.Alfred Kessy.
Balozi wa PSPF, Bw. Mrisho Mpoto, (kulia),akimkabidhi kadi ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS),  mfanyakazi wa CRDB, Bi. Flora Munisi.

Picha ya pamoja ya wanachama wapya wa PSPF na maafisa wa Mfuko huo akiwemo Balozi Mpoto.
Uzinduzi rasmi ukifanyika

Wizara ya Mambo ya Nje yahamishia Ofisi zake Dodoma Rasmi

0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Ofisini kwake Mjini Dodoma. Waziri Mahiga leo ameutangazi Umma wa Watanzania kuwa Wizara imehamia rasmi Dodoma. 
Waandishi wa habari wakifuatilia hotuba ya Mhe. Waziri Balozi Dkt. Mahiga 
Walio keti ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (katika), Naibu Katibu Mkuu Balozi Ramadhani Mwinyi (wa kwanza kulia) Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu Bw. Nigel Msangi (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Usimamizi Rasilimali Watu Bw.Hamid Mbegu wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara Mjini Dodoma 



KUHUSU WIZARA KUHAMIA DODOMA

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuufahamisha Umma kuwa tayari imeshahamia Dodoma kuanzia tarehe 17 Februari, 2017. Hatua hiyo imehusisha Awamu Mbili, Awamu ya kwanza imetekelezwa tarehe 28 Januari, 2017 na Awamu ya Pili imetekelezwa tarehe 17 Februari, 2017. 

Miongoni mwa Watumishi waliohamia Dodoma katika awamu hii ya kwanza (Awamu ndogo ya kwanza tarehe 28 Januari, 2017) nipamoja na Viongozi Wakuu na Watumishi wa Wizara wakiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Augustine P.Mahiga na Naibu Waziri Mhe. Dkt. Susan A. Kolimba pamoja na Watumishi Kumi (10) waliofuatana nao. Awamu ndogo ya kwanza ilifuatiwa na (Awamu ndogo ya Pili tarehe, 17 Februari, 2017) iliyoongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara, Balozi Dkt. Aziz P.Mlima na Naibu Katibu Mkuu Balozi Ramadhan M.Mwinyi wa kiongozana na Watumishi 33 wa Wizara ya Mambo ya Njena Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 

Katika Uhamisho huo wa Awamu ya Kwanza, jumla ya Watumishi 43 wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wameungana na Viongozi wao Wakuu.

Mawasiliano ya Wizara yatakayotumika kuanzia sasa nikama ifuatavyo:

Katibu Mkuu,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,

Barabara ya Makole,
S.L.P 2933,
Jengo la LAPF, Ghorofaya6,
DODOMA.

Namba za Simu: +255 (0) 262323201-7,
Nukushi : +255-26-2323208,
Barua pepe : nje@nje.go.tz Tovuti : www.foreign.go.tz

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dodoma, 27 Februari, 2017.

WAKAZI WA MIJINI WANAOMILIKI MAENEO YASIYO NA HATI KUTOZWA KODI

0
0

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akionyesha baadhi ya nyaraka za ardhi wakati akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaaml,kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Angelina Mabula na kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Yamungu Kayandabila. 


Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.


Serikali imejipanga kuwatoza kodi wakazi wanaomiliki maeneo yaliyopo mijini ambayo hayana hati wala ofa kwa viwango vile vile ambavyo wakazi wenye hati wanatozwa.

Tamko hilo limetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya ulipaji wa kodi za ardhi.

Waziri Lukuvi amesema kuwa wizara hiyo inaendelea na ukaguzi wa ardhi ambapo mwanzoni ilianza na ukaguzi wa mashamba yanayomilikiwa bila kuendelezwa lakini kwa sasa imegundulika kuwa kuna maeneo makubwa mijini yasiyokuwa na hati yanamilikiwa na wananchi na kusababisha eneo kubwa la ardhi kutumika bila kulipiwa kodi.

“Kwa muda wote huo Serikali imekuwa haiwatozi kodi wananchi wanaomiliki maeneo mijini bila kuwa na hati hivyo, kuanzia sasa Serikali kupitia wizara yangu itawatoza kodi watu wote nchini wanaomiliki maeneo ndani ya miji hata kama hawana hati au ofa ili mradi wana karatasi za mauziano ya ardhi,”alisema Lukuvi.

Ameongeza kuwa watu wote waliopo mjini ambao wana ardhi lakini hawana hati wala ofa wapeleke taarifa zao za maeneo wanayoyamiliki kwa maafisa wateule wa ardhi kwenye halmashauri zao ili yaweze kujulikana ili kuanza kulipiwa kodi.

Amefafanua kuwa kila mwananchi lazima aende na kielelezo kinachoonyesha umiliki wake katika eneo husika na akatamke mwenyewe ukubwa wa eneo alilonalo ili kama itatokea amedanganya ukubwa wa eneo lake na wizara ikagundua basi eneo hilo lililozidi litamilikiwa na Serikali bila kulipa fidia yoyote.

Aidha, Waziri Lukuvi amesema kuwa kuanzia mwezi Julai mwaka huu wizara itaanza kuwatoza kodi wananchi wote waliojenga mjini katika maeneo ambayo viwanja vyake havijapangwa wala kupimwa kwani watu hao wanaishi mjini na wanatumia miundombinu ya umma inayojengwa kwa kutumia kodi za wananchi.

“Ardhi ya Tanzania inayotumika ni zaidi ya asilimia 70 lakini eneo linalolipiwa kodi halizidi asilimia 11 na wengi wao wanaitumia isivyo rasmi na hawalipi kodi kwa Serikali hivyo kila mtu mwenye ardhi awe na nyaraka rasmi au isiyo rasmi wote wanatakiwa kulipa kodi ya ardhi na baada ya miezi 6 kutoka sasa, eneo ambalo halitakuwa limesajiliwa litachukuliwa na kumilikiwa na Serikali,”alimalizia Lukuvi.

Ni lazima kuwatambua watu wote wanaomiliki ardhi kisheria, kimila au kwa namna nyingine yoyote ili kufahamu ardhi inamilikiwa na nani na inatumika kwa matumizi gani.

WASANII WATAKIWA KUACHA KUTUMIA MADAWA AMA VILEO KABLA YA KUFANYA KAZI ZAO

0
0
Na Ripota wa globu ya jamii

Wito umetolewa kwa wasanii kuacha kutumia dawa za kulevya na vileo kabla ya kuanza kufanya kazi zao,ili waweze kuongeza weledi wa sanaa kwa hadhira.

Wito huo umetolewa na mwandishi mwandamizi wa Michuzi blog Humphrey Shao, alipokuwa akizungumza na wasanii pamoja na waandishi wa habari katika jukwaa la Sanaa lililoandaliwa na Baraza la Sanaa Tanzania(BASATA).

Akizungumza katika jukwaa hilo ,Shao amesema kuwa amefanikiwa kuandika makala nyingi,zinazousu matatizo ya dawa za kulevya kwa wasani tangu mwaka 2014 lakini mwaka huu 2017 ndipo mambo yote yamekuwa hadharani.

“tatizo la dawa za kulevya kwa wasanii halijaanza leo, na wengi wao huanzia na kilevi cha bangi na kupelekea kujiingiza kwenye dawa za kulevya hali inayo hatarisha maisha yao na kazi zao za sanaa”amesema Shao.

Kwa upande wake msanii wa muziki wa Bongo Fleva Snura Mushi amesema kuwa, amekuwa akishuhudia wasanii wengi ambao hawawezi kupanda jukwaani mpaka walewe, hali inayopelekea wengi wao kuharibu kazi na kupoteza mashabiki.

Ametaja kuwa mtu ukitumia madawa yakulevya au pombe katika kazi yako inakufanya upoteze umakini ambao unaweza kukupoteza katika ramani ya sanaa na heshima yako kushuka.

Nae katibu mkuu wa BASATA, Godfrey Mwingereza ametoa onyo kwa wasanii wote ambao wanatumia dawa za kulevya na wale ambao hupendelea kunywa pombe kupita kiasi na kupanda katika majukwaa ya muziki.

Mwingereza amesema kuwa kitendo cha msanii kupanda jukwaani akiwa amelewa ni kudhalilisha kazi ya sanaa ambayo ni kazi kama ilivyo kazi nyingine na kutaja kuwa ni mara chache sana kuona wakandarasi au madaktari kuona wakiwa katika kazi zao wamelewa kama wasanii wetu.
Mwandishi wa habari Mwandamizi kutoka Michuzi Blog , Humphrey Shao akiongea na wasanii na Waandishi wa habari katika jukwaa la sanaa lililoandaliwa na BASATA juu ya tatizo la Dawa za kulevya kwa wasanii kulia kwake ni Snura Mushi na kushoto kwake ni Msanii wa Mizengwe Hemed maliyaga(Mkwere Original) na katibu mkuu wa basata , Godfrey Mwingereza .
Katibu mkuu wa BASATA, Godfrey Mwingereza akizungumza na wasanii na waandishi habari juu ya kujikwamua katika tatizo la dawa za kulevya

wadau wa wasanaa na waandishi wa habari wakifatilia
Katibu mkuu wa Baraza la Sanaa Basata akizungumza na wasanii wa filamiu na muziki kabla ya kuingiakatika mkutano.

MKUU WA JESHI LA ULINZI TANZANIA NA MNADHIMU MKUU WALA KIAPO CHA UADILIFU KWA VIONGOZI WA UMMA

0
0
 Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Tanzania (CDF), Jenerali Venance Salvatory Mabeyo akila Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma leo Jijini Dar es Salaam. Kulia anayeshuhudia ni Kamishna wa Maadili wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela leo Jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Tanzania (CDF), Jenerali Venance Salvatory Mabeyo akitia saini katika Hati ya Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma leo Jijini Dar es Salaam. Kulia anayeshuhudia ni Kamishna wa Maadili wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela leo Jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Tanzania (CDF), Jenerali Venance Salvatory Mabeyo akipokea Hati ya Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma kutoka kwa Kamishna wa Maadili wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela leo Jijini Dar es Salaam.
 Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Tanzania, Luteni Jenerali James Alois Mwakibolwa akila Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma leo Jijini Dar es Salaam. Kulia anayeshuhudia ni Kamishna wa Maadili wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela leo Jijini Dar es Salaam.
 Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Tanzania, Luteni Jenerali James Alois Mwakibolwa akitia saini katika Hati ya Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma leo Jijini Dar es Salaam. Kulia anayeshuhudia ni Kamishna wa Maadili wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela leo Jijini Dar es Salaam.
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Tanzania, Luteni Jenerali James Alois Mwakibolwa akipokea Hati ya Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma kutoka kwa Kamishna wa Maadili wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela leo Jijini Dar es Salaam.  

 Kamishna wa Maadili kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela akimpokea Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Tanzania(CDF), Jenerali Venance Salvatory Mabeyo alipowasili katika Ofis za Sekretari hiyo kwa ajili ya kula kiapo cha Uadilifu leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na Frank Shija – MAELEZO.

TAARIFA KWA UMMA: WIZARA YA MALIASILI NA UTALII YAFUNGUA RASMI OFISI ZAKE ZA DODOMA LEO

0
0

WAZIRI NAPE ATUMA SALAMU ZA POLE KWA SHIRIKISHO LA RIADHA NCHINI

0
0

TAASISI YA SEKTA BINAFSI YAJIPANGA KUWAJENGEA UWEZO WAHITIMU WA VYUO VIKUU NCHINI

0
0


Na Jovina Bujulu MAELEZO Dar es Salaam

TAASISI ya sekta binafsi nchini (TPSF) imetoa wito kwa wahitimu na vijana waliopo vyuoni kuchangamkia fursa ya mpango maalum uliobuniwa baina yake na Serikali ambao umekusudia kuwajengea ujuzi kabla ya kuajiriwa ili waweze kufanya kazi kwa weledi.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye wakati alipokuwa akichangia mada kuhusu wahitimu wa vyuo vikuu kushindwa kuonyesha ujuzi baada ya kuajiriwa.

“Upo upungufu mkubwa wa mafunzo ya vitendo kwa wahitimu wengi wanaomaliza vyuo vikuu nchini na imedhihirika kuwa wahitimu hao hushindwa kufanya kazi kwa weledi wanapokuwa wameajiriwa na sekta mbali mbali.

Alisema kuwa mpango huo maalum umeanzishwa kwa lengo la kuwatayarisha wahitimu wa vyuo kupata mafunzo ya muda mfupi ili kuondoa changamoto wanazokabiliana nazo pindi wanapoajiriwa au kutaka kujiajiri.

Simbeye alisema Mpango huo pia umekusudia kuwapunguzia gharama waajiri, hasa wa sekta binafsi kwa kuwa wengi wao wamekuwa wakitumia pesa nyingi kwa kuwapeleka waajiriwa wapya katika mafunzo ili waweze kumudu kazi zao.

Akifafanua zaidi alisema katika mpango huo waajiriwa wataweza kupata mafunzo mtambuka na gharama zote za mafunzo zinagharimiwa na Serikali.

“Chini ya mpango huu, wahitimu na vijana walioko vyuoni wanatakiwa kujiandikisha kwa hiari, na baada ya mafunzo inakuwa rahisi kwao kupata ajira kupitia katika sekta binafsi au makampuni” aliongeza Bwana Simbeye.

Aidha Bwana Simbeye alisema kuwa mpango huo pia utawawezesha wahitimu kutengeneza mazingira ya kuanzisha biashara nyingi na kupanua biashara zilizopo ili waweze kupata fursa nyingi za kuajiriwa na kujiajiri hasa katika wakati huu ambao nchi inaelekea katika uchumi wa viwanda.

Akizungumzia mpango huo, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana, na Walemavu), Anthony Mavunde alisema kuwa mpango wa Serikali ni kuhakikisha kuwa kila chuo kinajitengenezea mwongozo wake unaomwezesha kila mwanafunzi kupata nafasi ya kufanya mafunzo kwa vitendo.

Aidha aliongeza kuwa Serikali itahakikisha kuwa mpango huo unakuwa endelevu na unafanya kazi kama ilivyokusudiwa na kutoa wito kwa sekta binafsi na waajiri kutoa maoni yao ili kuboresha mpango huo.

Halmashauri Nchini Zaagizwa Kuwasilisha Taarifa Kuhusu Maendeleo ya Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Nchini.

0
0
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace Simbachawene akizungumza wakati wa mkutano baina yake na wajumbe wa Kamati ya Uongozi wa MKURABITA Ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuwasilisha taarifa ya tathimini ya utekelezaji wa Mpango wa Urasimishaji wa Rasilimali na Biashara katika Halmashauri nchini.Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mkurabita Kapteni Mstaafu John Chiligati.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA) Mhe. Kapteni Mstaafu John Chiligati akielezea jambo wakati wa kikao baina ya kamati hiyo na TAMISEMI kuhusu tathmini ya utekelezaji wa mpango huo katika Halmashauri mbalimbali nchini leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace Simbachawene, Mratibu wa MKURABITA Bibi. Seraphia Mgembe na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa MKURABITA Profesa. Aldo Lupala.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA) Mhe. Kapteni Mstaafu John Chiligati akielezea jambo wakati wa kikao baina ya kamati hiyo na TAMISEMI kuhusu tathmini ya utekelezaji wa mpango huo katika Halmashauri mbalimbali nchini leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace Simbachawene, Mratibu wa MKURABITA Bibi. Seraphia Mgembe na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa MKURABITA Profesa. Aldo Lupala.
Mratibu wa MKURABITA Bibi. Seraphia Mgembe akifafanua jambo wakati wa kikao baina ya Kamati ya Uongozi ya MKURABITA na TAMISEMI kuhusu tathmini ya utekelezaji wa mpango huo katika Halmashauri mbalimbali nchini leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace Simbachawene, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA) Mhe. Kapteni Mstaafu John Chiligati na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa MKURABITA Profesa. Aldo Lupala.
 Watendaji kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambao ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Miji Dkt. Mkuki Hante pamoja na Mkurugenzi wa Utawala kwa Serikali za Mitaa Bibi. Miriam Mmbaga wakifuatilia mjadala wakati wa kikao baina ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI na MKURABITA kuhusu tathmini ya utekelezaji wa mpango huo leo Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace Simbachawene akipokea taarifa ya tathmini kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kurasimisha rasilimali na biashara uliofanyika katika Halmashauri 52 na Miji 9 nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mkurabita Kapteni Mstaafu John Chiligati leo Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace Simbachawene akisoma taarifa ya tathmini kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kurasimisha rasilimali na biashara uliofanyika katika Halmashauri 52 na Miji 9 nchini mara baada ya kuipokea kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mkurabita Kapteni Mstaafu John Chiligati(hayupo pichani) leo Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace Simbachawene akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mkurabita Kapteni Mstaafu John Chiligati (katikati) Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa MKURABITA Profesa. Aldo Lupala mara baada ya  mkutano baina yake na wajumbe wa Kamati ya hiyo Ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam.
Na: Mpiga Picha Wetu.

PSPF,CRDB BENKI ZAZINDUA HUDUMA YA MIKOPO YA ELIMU,VIWANJA NA KUANZA MAISHA

0
0

PROF. MBARAWA AKUTANA NA BODI YA AfDB

0
0
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ameiomba Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo Africa (AfDB), kuendelea kuiunga mkono Tanzania katika mkakati wake wa kukuza uchumi kwa kuwekeza katika sekta ya miundombinu.

Akizungumza na Wakurugenzi wa Bodi ya AfDB waliomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo Prof. Mbarawa ameishukuru benki hiyo kwa ushirikiano inaoipa Serikali ya Tanzania katika miradi mingi ya ujenzi wa barabara na kuiomba kuiunga mkono katika uwekezaji mkubwa inaoufanya katika miradi ya usafiri wa anga na reli.

“Tumejipanga kukuza uchumi kwa kuimarisha sekta za barabara,anga,reli na bandari hivyo tunaomba ushirikiano wenu kadri tunavyouhitaji ili kufikia malengo yetu kwa wakati”, amesema Prof. Mbarawa.

Ameitaja baadhi ya miradi ya barabara ambayo Tanzania imenufaika na AfDB kuwa ni barabara ya Kibondo-Kasulu-Manyovu Km 250, Makutano-Nata-Mugumu-Mto wa Mbu hadi Loliondo Km 213, Makurunge-Saadani-Pangani-Tanga KM 178 na barabara za pete jijini Dar es Salaam Km 34.

“Kuimarika kwa Sekta ya miundombinu nchini hasa sekta ya anga, reli na barabara, kutaimarisha sekta za utalii na kilimo na hivyo kuongeza ajira na kukuza uchumi wa taifa”, amesisitiza Prof. Mbarawa.

Naye mjumbe wa Bodi ya AfDB Dkt. Weggoro Nyamajeje Calleb amezungumzia umuhimu wa miradi ya ujenzi inayoanzishwa hapa nchini kutoa fursa za ajira kwa wananchi na kuwekewa mazingira endelevu ili ilete mabadiliko chanya katika maisha ya watu na taifa kwa ujumla.

Dkt. Calleb amesisitiza umuhimu wa ushirikishwaji wa sekta binafsi katika ujenzi wa miundombinu ili kuiwezesha nchi kuwa na miundombinu bora na yakutosha na hivyo kuchochea maendeleo.

Ujumbe wa AfDB upo hapa nchini ambapo pamoja na mambo mengine leo umepata fursa ya kubadilishana uzoefu na viongozi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ili kujua mikakati yake katika kuboresha miundombinu hapa nchini na namna inavyoweza kutoa ushirikiano katika kuiwezesha.

Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
 Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto), akimsikiliza kwa makini mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Maendeleo Africa (AfDB), Bi, Lekhethe Mmakgoshi (wa pili kushoto), wakati alipokutana na Bodi hiyo jijini Dar es salaam leo kujadiliana namna ya kushirikiana kuboresha sekta ya miundombinu ya uchukuzi hapa nchini.
 Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto), akimsikiliza kwa makini mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Maendeleo Africa (AfDB), Bi, Lekhethe Mmakgoshi (wa pili kushoto), wakati alipokutana na Bodi hiyo jijini Dar es salaam leo kujadiliana namna ya kushirikiana kuboresha sekta ya miundombinu ya uchukuzi hapa nchini.
 Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa kwanza kushoto ), akifafanua jambo kwa wajumbe wa  Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo Africa (AfDB), bi, Lekhethe Mmakgoshi, Dkt. Weggoro Nyamajeje na Dkt. Bright Okogu (wa kwanza kulia), alipokutana na Bodi hiyo jijini Dar es Salaam leo kujadiliana namna ya kushirikiana kuboresha sekta ya miundombinu ya uchukuzi hapa nchini.
Picha ya pamoja kati ya viongozi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Maendeleo ya Africa (AfDB) walipokutana Jijini Dar es salaam leo.Imetolewa Na Kitengo cha Habari Na Mawasiliano Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na mawasiliano.

SERIKALI YAISHUKURU AfDB KUKUBALI KUFADHILI MIRADI YA UJENZI WA B

0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam

Waziri wa Fedha na Mipango ameishukuru Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kukubali kuendelea kufadhili miradi ya maendeleo ya kipaumbele hususani ya ujenzi wa barabara na usafirishaji wa umeme ili kufungua fursa za kiuchumi katika kanda ya Magharibi.

Dkt. Mpango ametoa shukrani hizo alipokutana na Wakurugenzi Watendaji 12 wanaowakilisha nchi zao katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), jijini Dar es salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) ameiomba Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kuharakisha kazi za upembuzi yakinifu na hatimaye kutoa fedha ili utekelezaji wa miradi ya Maendeleo kuanza mapema iwezekanavyo.

Amesema kuwa Benki hiyo iliahidi kutoa fedha ili kujenga barabara ya Nyakanazi, kupitia Kibondo, Kasulu hadi Manyovu, kwa kiwango cha lami na kwamba mradi huo ukipatiwa fedha na kukamilika kwa wakati kutasaidia kuchochea biashara ya wakazi wa maeneo hayo na Nchi jirani ya Burundi.

Pia mradi wa North – West grid wa kusafirisha Nishati ya Umeme kutoka Shinyanga hadi Mbeya kupitia Kigoma Katavi na Rukwa. Mradi huu utawezesha Mikoa ya ukanda wa Magharibi kupata Nishati ya uhakika ya umeme na kufungua fursa za Maendeleo mbalimbali yakiwemo ya ujenzi wa Viwanda vidogo na vya kati.

“Katika kikao hicho tumewaeleza Wakurugenzi hao wa AfDB hatua mbalimbali ambazo Serikali inazichukua katika kutatua changamoto ya Miundombinu ya Umeme na Barabara, kupanua fursa za Ajira, na kuharakisha maendeleo ya ukuaji wa Sekta ya Kilimo ambayo inategemewa na wananchi wengi” Alifafanua Waziri Mpango.

Aidha amewaeleza wageni juu ya jitihada za Serikali ya Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli za kukusanya mapato ya kodi na yasiyo ya kodi, kupambana na rushwa na biashara haramu ya madawa ya kulevya.

Waziri Mpango ametumia fursa hiyo kuomba AfDB kusaidia kujenga uwezo wa Tanzania kukabiliana na majanga yakiwemo ya matetemeko ya ardhi, ajali kubwa za majini na kwenye migodi. Maeneo mengine ambayo AfDB imeombwa kuisaidia Tanzania ni uvunaji wa rasilimali za bahari (blue economy), kuelekeza mitaji katika Sekta ya kilimo na kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabia nchi.

Naye Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ameipongeza Benki ya AfDB kwa kuwa mdau mkubwa wa Maendeleo ya nchi za Afrika na hasa Tanzania kwa kuwa imekuwa mnufaika mkubwa wa program/ miradi inayofadhiliwa na Benki hiyo.

Amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa wageni hao watakapokuwa wakitembelea miradi mbalimbali inayogharamiwa na AfDBi katika siku takribani tano ambazo watakuwepo nchini.

Kwa upande wa Wakurugenzi Watendaji wa AfDB wanaoziwakilisha nchi zao, wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji kutoka Afrika ya Kusini Bi. Elizabeth Mmakgoshilekethe, wameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa mafanikio ya kiuchumi kwa kuwa Tanzania imekuwa na viashiria vingi ambavyo vinaonesha uchumi wa Taifa ni imara ukilinganisha na nchi nyingine katika bara la Afrika kusini mwa jangwa la Sahara.

Aidha wameitaka Tanzania kuendeleza jitihada za kupambana na Umaskini hasa katika maeneo ya vijijini na kuongeza fursa za ajira ili kuharakisha maendeleo. Pia wameipongeza Serikali kwa mikakati waliyonayo kupitia Mpango wa Pili wa Maendeleo wa miaka mitano kwa kuwa unaendana na vipaumbele vya Benki hiyo.



Benki hiyo imeitaka pia Tanzania kushiriki na kuchangamkia fursa za miradi ya kikanda hasa katika Nishati ya Umeme, Barabara na Reli na pia kuhakikisha utawala bora.

PINDA AZINDUA KONGAMANO LA WADAU WA SUA NA KUTEMBELEA BANDA LA TADB

0
0
 Wadau waliojitokeza kutembelea Banda la Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) wakipitia majarida na vipeperushi vilivyokuwa vikitolewa na wafanyakazi wa Benki hiyo. 
 Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda (Kulia) akikaribishwa kutembelea Banda la TADB na Afisa Mahusiano na Masoko Mkuu wa Benki hiyo, Bw. Saidi Mkabakuli (Kushoto). 
 Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda (Kulia) akisalimiana na wafanyakazi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania waliokuwa wakitoa huduma wakati wa Kongamano la Wadau la SUA linaloendelea Mkoani Morogoro. Kushoto ni Afisa Maendeleo ya Biashara Mwandamizi, Bw. George Nyamrunda na Afisa Mipango na Sera Mkuu wa Benki hiyo, Bw. Mzee Kilele (wa pili kushoto).
 Kaimu Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA), Prof. Deogratias Lutatora (Kushoto) na Mkuu wa Chuo cha Kilimo, Prof. Susan Nchimbi-Msolla (Wapili Kushoto) wakimuongoza Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda (Mwenye tai nyekundu) kufungua Kongamano la Wadau la SUA. Kushoto kwa Mhe. Pinda ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda (Katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la Wadau la SUA mara baada ya kufungua Kongamano hilo. Wengine waliokaa ni  Kushoto kwa Mhe. Pinda ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe. Kaimu Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA), Prof. Deogratias Lutatora (Kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe  (Kulia).

WASHIRIKI WA MISS UTALII SONGEA WATEMBELEA VIVUTIO NA UTALII VILIVYOPO WILAYA YA NYASA

0
0

Washiriki wa miss utalii Songea mkoani Ruvuma watembelea utalii uliopo katika wilaya ya nyasa ili kujionea vivutio vilivyopo katika ziwa nyasa na wilaya hiyo, ambapo wametembelea jiwe POMONDI lilipo LIULI na kisiwa cha LUNDO cha MBAMBABY.

Mtoto Latifa aliyeibwa asubuhi saa 2 leo Iringa Mjini apatikana usiku huu kijiji cha Mkungugu

0
0
Leo mida ya saa mbili  asubuhi katika maeneo ya Stand kuu ya mabasi ya Iringa aliibiwa mtoto mchanga mweney umri wa miezi 5. Mtoto huyo inasadikwia aliibwa na binti ambaye alikuwa amekuja kutafuta kazi. 

Akieleza tukio hilo Mama yake Bi Asha Shaban Lauza alisema " nikiwa naosha vyombo binti huyu ambaye toka jana alikuwa anatafuta kazi alianza kumpa maziwa mtoto yaliyo kwenye chupa mpaka mtoto akamaliza. Baadae mtoto akajinyea basi bila wasiwasi nikampa shilingi elfu kumi ili akanunue pampasi duka la pili tu akanyanyuka na mtoto kwenda dukani toka  asubuhi mpaka sasa usiku hautja muona" . 

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela alifika eneo la tukio baada ya kumhoji mzazi akagundua walichelewa kutoa taarifa polisi. Baada ya msako wa muda was saa 3 usiku mtoto alipatikana eneo la Mkungugu km 33 kutoka Iringa Mjini. 

Binti wa miaka 14 (Jina linahifadhiwa) alikuwa akitoroka na mtot huyo gari la polisi la doria likishirikiana na wananchi wa kijiji cha Mkungugu lilifanikiwa kumuweka chini ya ulinzi mtuhumiwa huyo wa wizi  wa mtoto. 

Mkuu wa Wilaya alifika akiongozana na mama Mzazi wa mtoto pamoja na Diwani wa kata ya Kisinga Mh Ritha Mlagala. Binti mwizi yupo kituo cha polisi akiendelea kuhojiwa na mama mzazi baada ya kuandika maelezo alipewa fomu ya matibabu na kumpeleka mtoto hospitali.

 Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela amekemea vikali kitendo cha uzembe wa mama huyu na wazazi kwa ujumla "pamoja na mama huyu kuwa na uchungu wa mtoto bado ana mashtaka ya kujibu ya uzembe, watu tusiowajua tusiwape watoto wetu hata kidogo huu ni uzembe wa hali ya juu" alisisitiza Mkuu wa wilaya.
Mkuu wa Wilaya ya iringa Mhe. Richard Kasesela akiwa eneo la kijiji cha Mkungugu barabani alipokamatwa binti mwizi akiwa na mtoto usiku wa saa 3 usiku huu.​
Mtoto Latifa akiwa ambebwa na Mkuu wa wilaya walipofika kituo cha polisi.
Mtoto Latifa akiwa ambebwa na Mkuu wa wilaya walipofika kituo cha polisi.


SERIKALI YAISHUKURU AfDB KUKUBALI KUFADHILI MIRADI YA UJENZI WA BARABARA NA USAFIRISHAJI WA UMEME ILI KUFUNGUA KANDA YA MAGHARIBI

0
0
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Mpango (Mb), akiongoza mkutano ulio wakutanisha Wakurugenzi Watendaji wanaoziwakilisha nchi zao katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kuhusu hali ya uchumi wa Tanzania huku ahadi zilizotolewa na Benki hiyo zikijadiliwa katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam. 
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kulia)na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Doto James (kushoto) wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), (hayupo pichani) alipokuwa akielezea umuhimu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) wakati akizungumza na Wakurugenzi 12 wanaoziwakilisha nchi zao katika Benki hiyo Mkutano uliofanyika jijini Dar es salaam. 
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Mpango (Mb) akizungumza na Wakurugenzi Watendaji 12 wanaoziwakilisha nchi zao katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kuhusu hali ya uchumi wa Tanzania, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es Salaam.
 Maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango wakisikiliza kwa Makini Maelezo ya Mkurugenzi Mtendaji kutoka Afrika ya Kusini anayeiwakilisha nchi hiyo (AfDB) Bi. Elizabeth Mmakgoshilekethe (hayupo) pichani wakati wa mkutano kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji kutoka Afrika ya Kusini anayeiwakilisha nchi hiyo (AfDB) Bi. Elizabeth Mmakgoshilekethe (kulia) akiipongeza Serikali kwa kuweka vipaumbele vya maendeleo vinavyoendana na vile vya Benki ya Maendeleo ya Afrika katika Mkutano na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Mpango (Mb) (kushoto) katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es Salaam.
 Mmoja wa Wakurugenzi anayeiwakilisha nchi yake katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) akipongeza juhudi za Serikali katika kuwataulia wananchi wake matatizo ya kiuchumi wakati wa Mkutano kati ya Wakurugenzi hao na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) jijini Dar es salaam.
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akifafanua jambo wakati wa Mkutano wake na Mkurugenzi Mtendaji kutoka Afrika ya Kusini anayeiwakilisha nchi hiyo (AfDB) Bi. Elizabeth Mmakgoshilekethe (kulia)  katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dar es salaam.

 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Mpango (Mb), (katikati) na Kiongozi wa Ujumbe wa AfDB, Bi. Elizabeth Mmakgoshilekethe, kutoka Afrika Kusini (wa pili kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wengine wanaowakilisha nchi zao katika Benki ya AfDB baada ya kumalizika kwa Mkutano katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Mpango (Mb) (kulia) na Naibu wake Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji kutoka Afrika ya Kusini anayeiwakilisha nchi hiyo (AfDB) Bi. Elizabeth Mmakgoshilekethe (katikati) wakibadilishana mawazo baada ya kumalizika kwa Mkutano kuhusu Hali ya uchumi nchini Tanzania katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dar es salaam.

KITIME ATAHADHARISHA BENDI KUPIGA KWENYE BAR

0
0


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Wasanii na vikundi vinavyopiga muziki wa bendi wametakiwa kujitazama upya juu ya muziki huo kutumika kama chombo cha kuuzia bia kwenye Bar.

Hayo yamesemwa na msanii nguli wa muziki wa dansi hapa nchini John Kitime alipokuwa akizungumza na wasanii pamoja na waandishi wa habari katika jukwaa la sanaa lililoandaliwa na Baraza la Sanaa nchini (BASATA).

“kuna vitu tunafanya tunaona kama vya kawaida lakini ndio vinaua muziki wetu kama leo hii, bendi zinapiga kwenye bar kwa ajili ya kuuza bia na watu wanaangalia bure, hivyo inamaanisha bendi zetu ndio kichocheo cha kuuza pombe katika mabaa yote mjini”amesema Kitime.

Kitime ametoa wito kwa wasanii kuanza kubadilisha mtindo wa maisha kwani kitendo cha bendi zote kuhamia kwenye bar ni moja ya anguko kubwa la muziki wa dansi nchini

HATIMAYE meli ya kwanza kati ya tatu zinazojengwa Bandari ya Itungi yaingizwa Ziwa Nyasa

0
0

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMANNE FEB 28,2017

0
0

UNESCO KUENDELEA KUSAIDIA REDIO JAMII KUKUZA DEMOKRASIA

0
0
Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limeahidi kuendelea kuzisaidia redio jamii kwa lengo la kuhakikisha sauti za wanyonge zinapazwa na kusikika ili kukuza demokrasia nchini. Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania (COMNETA), Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues alisema UNESCO alisema kuwa wakati umefika kwa wadau wa sekta ya habari kufikiri kwa kina namna ya kuhabarisha umma kwa kuangalia namna ya uwasilishaji ambapo kwa sasa changamoto kubwa ni kasi ya ukuaji wa teknolojia ya habari na namna ambapo redio zinaweza kushindana na vyombo vingine. 

Alisema kwa wanahabari wanapaswa kuwa makini na taarifa wazitoazo kwa jamii kwani kumekuwa na mazoea ya baadhi yao kuripoti habari bila kufanya uchuinguzi wa kina huku wakitumia chanzo kimoja cha habari badala ya kujiuliza maswali mengi ili kupata taarifa sahihi. 

Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Habari wa UNESCO, Ofisi za Tanzania, Christophe Legay akizungumza machache wakati wa mkutano mkuu wa wajumbe wa Bodi ya Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania (COMNETA) unaoendelea katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.

Aliwashauri wanachama wa COMNETA, wawe na umoja, mshikamano na kupendana ili kuepuka migogoro inayoweza kuyumbisha ustawi wa mtandao huo. “Ninawaomba sana, COMNETA, muwe mfano wa kuigwa kwa kuepuka migongano ya wenyewe kwa wenyewe ikiwamo kugombea madaraka ili kuwa umoja wa mfano kwa katika tasnia ya vyombo vya habari hapa nchini’.
‘Vipindi mbalimbali vya kuhamasisha maendeleo vinavyorushwa na redio hii vimesaidia sana kuhamasisha wananchi na sasa mwamko wa maendeleo umekuwa mkubwa hapo Micheweni” alisema Zulmira Rodrigues
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya COMNETA, Mohamed Tibanyendera akizungumza na wadau mbalimbali wa vyombo vya habari jamii waliokutana kwenye mkutano mkuu ili kujadili changamoto na kufanya uchaguzi wa viongozi wapya uliodhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).

Mwenyekiti wa Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania-COMNETA, Prosper Kwigize alisema kuwa ipo changamoto kwa baadhi ya maafisa habari mikoani na wilayani kuleta urasimu mkubwa katika utoaji wa taarifa zinazohitajika kwa waandishi wa habari hivyo kukwamisha upatikanaji wa habri kwa umma. Pia kuna changamoto mbalimbali kwenye chama hicho hivyo ni vyema kuzitafutia suluhiso la msingi ili mtandao huwe imara.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya COMNETA, Mohamed Tibanyendera alisema kuwa kwa siku za nyuma redio ilikuwa ni chombo cha kuaminika katika utoaji wa habari hivyo kujijengea umaarufu na kuaminika zaidi tofauti na ilivyo sasa ambapo kuna upotoshaji mkubwa. Pia aliweza kuyatolea majibu maswali yaliyoulizwa na wajumbe wa bodi ya COMNETA ili kuimarisha uwajibikaji katika Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania-COMNETA.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania (COMNETA), Prosper Kwigize akizungumza na viongozi wa vyombo vya habari jamii wakati wa mkutano mkuu wa COMNETA unaondelea katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Bodi ya Udhamini ya COMNETA, Balozi Christopher Liundi akizungumza jambo wakati wa mkutano mkuu Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania (COMNETA) unaofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam chini ya udhamini wa UNESCO.
Katibu wa Bodi ya Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania (COMNETA), Marco Mipawa akisoma marejesho kwenye mkutano mkuu unaondelea OUT jijini Dar es Salaam. Pichani juu na chini ni Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya COMNETA ambao pia ni Mameneja na wawakilishi wa vituo vya redio jamii nchini wakishiriki kutoa maoni kwenye mkutano mkuu wa COMNETA unaoendelea katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
     
 Kutoka kushoto ni Afisa Programu wa Mawasiliano na Habari wa UNESCO, Nancy Kaizilege na Mkufunzi wa Redio Jamii UNESCO, Rose Haji Mwalimu wakirekodi mambo muhimu katika mkutano mkuu wa COMNETA unaoendelea jijini Dar es Salaam.
Mkutano ukiendelea.
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images