Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46193 articles
Browse latest View live

WAZIRI MAKAMBA AWATAKA WACHIMBAJI MCHANGA NA WALIMA BUSTANI ZA MBOGAMBOGA KUONDOKA MARA MOJA KATIKA BONDE LA MTO MSIMBAZI HUKO VINGUNGUTI

0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba amewataka wachimbaji mchanga na walimaji wa bustani katika bonde la mto msimbazi katika kata vingunguti iliyopo katika Manispaa ya Ilala, kuondoka mara moja na kuacha shughuli hizo.

Ameyasema hayo alipokua katika ziara ya siku moja ya kutembelea kata ya Vingunguti na kujionea athari mbalimbali za kimazingira katika kata hiyo.
Wakiongea mbele ya Waziri Makamba, Wananchi wamelalamika kero mbalimbali zinazowakabili ikiwemo bonde hilo kuzidi kumong'onyoka na kusogelea makazi ya watu pamoja na eneo la makaburi. 

Hivyo basi kusababisha nyumba zao kuanguka na makaburi kumong'onyoka hali amabayo inahatrisha maisha yao na kuwafanya kuishi kwa hofu.
Akijibu kero hiyo Waziri Makamba aliwaambia kuwa atayafanyia kazi maombi yao na atakaa na viongozi wa Manispaa na wa Ofisi yake ili kupata suluhu ya matatizo yao. 

Pamoja na hayo alisema kuwa kwa hatua za awali anawataka  wachimbaji na wakulima wa bustani kuacha mara moja shughuli hizo wanazofanya katika maeneno ya bonde hilo. (Habari na picha toka Kitengo caha mawasiliano Serikalini OMR)
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiangalia bonde la mto Msimbazi katika kata ya Vingunguti lilivyoharibika kwa shughuli za kila siku za Wananchi ikiwemo kilimo cha mbogamboga na uchimbaji wa mchanga. Waziri Mkamba yupo katika ziara kutembelea kata ya Vingunguti kukagua athari za mazingira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba pamoja na Mbunge wa jimbo la Segerea Mh. Bonnah Klauwa wakiskiliza kero mbalimbali zinazotolewa ana Wananchi wakati Mh. Waziri alipofanya ziara katika kata ya Vingunguti  kukagua athari mbalimbali za mazingira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiongea na Wananchi waliojikusanya kumsikiliza wakati wa ziara yake katika kata ya Vingunguti katika wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akipata maelezo, toka kwa vijana wa kata ya Vingunguti  juu ya utenegenezaji wa majiko ya mkaa ambayo ni rafiki wa mazingira na ambayo hayatumii mkaa mwingi.

SERIKALI KUANZISHA MPANGO WA MIAKA 5 KUWASAIDIA VIJANA KUPATA MAFUNZO KWA VITENDO ILI KUONGEZA SIFA YA KUAJIRIWA NA KUJIAJIRI

0
0
Asilimia 61 ya wanafunzi wanaomaliza elimu ya juu katika vyuo mbalimbali nchini hawana ujuzi na sifa za kuajiriwa kwenye sekta binafsi ili kukuza uchumi na kufikia kiwango cha kati .

Hayo yamebainishwa leo na Naibu waziri wa kazi,vijana na ajira Anthony Mavunde wakati akizungumza na wadau wa makampuni ya sekta binafsi jijin Dar es salaam na kusema kuwa baada ya kugundua changamoto hiyo serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi wameanzisha mpango wa miaka 5 wa kuwasaidia vijana kupata mafunzo kwa vitendo ili kuongeza sifa ya kuajiriwa na kujiajiri.

''Tumeamua kuanzisha programu hiyo ili kuhakikisha wanasaidia nguvu kazi ya nchi kupata ujuzi wa kuweza kujiajiri lakini pia kuajiriwa katika makampuni mbalimbali yenye uhitaji wa wafanyakazi walio bora katika utendaji kazi" alisema Mavunde.

Mheshimiwa mavunde akaongeza kuwa programu hiyo ya miaka 5 iliyoanza mwaka 2016 na kutegewa kumalizika na kufikia mwaka 2021 unatarajiwa kuwafikia watu milioni 4 ili kuwasaidia kukuza ujuzi na kufikia uchumi wa kati kwa kuwepo nguvu kazi ya juu ya asilimia 34.

''Mpaka sasa tumeweza kuwafikia vijana elfu 2000 ambapo wamepata nafasi ya kujiunga katika mafunzo na kupata ujuzi katika kiwanda vya nguo EPZA pamoja na vijana elfu 1000 kupata mafunzo ya kutengeneza bidhaa zitokanazo na ngozi katika mikoa mbalimbali ikiwemo morogoro .'' Aliongeza Mheshimiwa Mavunde.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa sekta binafsi Tpsf ameeleza kuwa sababu za kukosa ujuzi ni sababu kubwa inayosababisha waajiri kuajiri watu kutoka nchi za nje kutokana na wazawa kukosa viwango vya utendaji kazi.

''Kuna haja ya kuwepo kwa mafunzo yatakayosaidia kuwapa ujuzi wa kufanya kazi pindi wanapoajiriwa japokuwa tatizo hili haliko tanzania pekee hata kea nchi jirani kama kenya.''alieleza simbeye.

Hata hivyo MKurugenzi huyo amewataka waajiri wa sekta binafsi kutoa kipaumbele za ajira kwa vijana wa kitanzania ili kuendelea kuunga mkono kazi inayofanywa na serikali kwa kuwa inatumia kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kutoa mafunzi.
Naibu wazir wa kazi,vijana na watu wenye ulemavu Mh,Anthony Mavunde akizungumza na wadau Mbalimbali sekta binafsi katika mkutano uliohusisha serikali na sekta Binafsi uliozungumzia Mafunzo ya miaka mitano ya kuwapatia ujuzi wa kuajiriwa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu.
Mkurugenzi mtendaji Bw Godfrey Simbeye akitoa ufafanuzi katika Mkutano huo uliokutanisha Serikali na Sekta Binafsi
Baadhi ya Wadau waliohudhuria Mkutano huo leo Jijini Dar es salaam.Picha na Yasir Adam Blogu ya Jamii

Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Tanzania jenerali Venance Mabeyo amtembelea Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Zuberi ofisini kwake

0
0
Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Tanzania (CDF ),Jenerali Venance Mabeyo akiwa katika picha ya pamoja na vingozi wa dini ya Kiislam, alipomtembelea Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Zuberi ofisini kwake mapema leo.Waliokaa kuanzia kushoto sheikh wa mkoa wa Dar es salaam Alhd Mussa .Jenerali Venance Mabeyo .Sheikh Mkuu Muft Zuberi, waliosimama kuanzia kushoto Katibu Mstaafu Suleiman Lolila,Haidari Kambili,Sheikh Mussa Hemed, Katibu wa dini Mohammed Hamisi pamoja na Tabu kawambwa

viongozi wa kata na mitaa wilaya ya Kinondoni watoke maofisini wakasikilize kero za wananchi-dc Ally Hapi

0
0
Viongozi wa kata na mitaa wilaya ya kinondoni jijini Dar es salaam,wametakiwa kutoka nje ya ofisi zao ili kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

Akizungumza na wananchi wa kata ya Kinondoni katika ziara yake ya siku kumi, mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Hapi amesema viongozi wote wakitaifa akiwemo raisi, waziri mkuu na mawaziri wanafanya ziara za kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

Hatahivyo mkuu huyo wa wilaya amewataka viongozi wa kata na mitaa kuwa wabunifu na kuwashirikisha wadau ili kuweza kutatua changamoto ndogondogo tofauti na kuzipeleka kwa ofisi ya mkuu wa wilaya.

Aidha amesema serekali ya awamu ya tano imejipanga kikamilifu kutatua kero za wananchi nakutekeleza kikamalifu ilani ya chama cha mapinduzi kwa mwaka 2015/2020.


Mkuu wa wilaya ya Kinondoni akitoka katika ofisi ya mtendaji wa Kata ya Kinondoni akielekekea kukagua miradi mbambali na Kinondoni leo hii katika Ziara yake
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni ally hapi akiwashukuru wafanya biashara katika soko la mtambani lililo kinondo ni Jijini Dar es salaam leo hii.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni wilaya ya Kinondoni Ally Hapi Akizungumza na viongozi wa Kata na mitaa wilaya ya Kinondoni Jijini dar es salaam leo hii katika Ziara yake ya kukagua miradi mbambali na kusikiliza kero za wakazi wa Kinondoni Pembeni Kushoto ni Diwani wa Kata ya Kinondoni Mustapha Muro

Waziri Mahiga apokea ujumbe wa Mhe. Rais kutoka kwa Mfalme wa Qatar

0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akipokea ujumbe wa Mfalme wa Qatar, Mtukufu Sheikh Tamim Hamad Bin Khalifa Al-Thani kwenda kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Ujumbe huo uliwasilishwa leo katika ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam na Balozi wa Qatar nchini, Mhe. Abdullah Jassim Al Maadadi. 
Waziri Mahiga akizungumza na Mhe. Jassim Al Maadadi ambapo pamoja na kuzungumzia masuala ya ushirikiano Waziri alimpongeza kwa hatua nzuri za maandalizi ya Kombe la Dunia linalotarajiwa kufanyika nchini Qatar mwaka 2022. Vilevile alimuarifu kuhusu hatua iliyofikiwa na Serikali ya Tanzania katika kukamilisha ufunguzi wa Ofisi za Ubalozi mjini Doha, Qatar. 
Mhe. Jassim Al Maadadi alitumia fursa hiyo kuwasisitiza Watanzania kuzichangamkia fursa za ajira zilizopo nchini Qatar wakati huu wa maandalizi ya Kombe la Dunia kwa kuwa nchi hizi zilikwisha saini mkataba wa ushirikiano kwenye kazi na ajira mwaka 2013. 
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga, Afisa Mambo ya Nje, Bw. Hangi Mgaka na Katibu wa Waziri, Bw. Gerald Mbwafu wakifuatilia mazungumzo. 
Mazungumzo yakiendelea 
Picha ya pamoja.

KAMPUNI YA KUFUGA SUNGURA YA "THE RABBIT BLISS" SASA YAHAMIA DAR

0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya The Rabbit Blill inayohusika na ufugaji wa kisasa wa Sungura pamoja na uuzaji wake, Payas Ruben akizngumza na Ripota maalum wa Globu ya Jamii alietembelea makao makuu mapya ya Kampuni hiyo, yaliyopo eneo la Majohe, jijini Dar es salaam. Kampuni hiyo hivi sasa ipo Dar es salaam ikitokea Jijini Arusha kulikokuwa na makazi yake ya awali baada ya mmiliki wa sasa kununua hisa zote zilizokuwa zikimilikiwa na mmiliki wa awali. Akizungumza katika eneo hilo, Bw. Ruben alisema kuwa ufugaji wa Sungura ni mzuri sana na unafaida kubwa kwa mfugaji, kwani unaweza kumuingia kipato kikubwa kama atazingitia taratibu zote za ufugani, hivyo ametoa wito kwa wale wote wanaotaka kufuga au kujifunza ufugaji wa Sungura wasisite kufika kwenye ofisi zao zilizopo Majohe, Jijini Dar es salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya The Rabbit Blill inayohusika na ufugaji wa kisasa wa Sungura pamoja na uuzaji wake, Payas Ruben (kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi Mwena wa Kampuni hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya The Rabbit Republic ya nchini Kenya, Moses Mutua wakati wakimuangalia mmoja wa Sungura anaefugwa kisasa katika Shamba ya Sungura, lililopo Majohe, jijini Dar es salaam.

 Sehemu ya Mabanda ya kisasa kabisa ya kufugia Sungura.
 Baadhi ya Sungura wanaofugwa na Kampuni ya The Rabbit Blill.
 Moses Mutua a.k.a Mr. Rabbit akiwa kabeba mabox maalum ya Sungura wanaokuwa katika hali kuzaa.
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya The Rabbit Blill wakiwa wamebeba baadhi ya Sungura wafugwao hapo.
Furaha ya kufuga Sungura kwa faida.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO ALHAMIS FEB 23,2017

0
0

DC SHINYANGA ATOA MBINU KWA WANAWAKE KUJINASUA NA MFUMO DUME

0
0
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ametoa mbinu kwa wanawake kujinasua na mfumo dume kwa kuachana na tabia tegemezi, ambayo husababisha kukithiri kwa manyanyaso kwao kutoka kwa waume zao.
Amewataka wajikite kwenye vikundi vya ujasiriamali ambavyo vitawaondoa kwenye mfumo huo kwa kujikwamua kiuchumi.
Matiro ameyasema leo mjini Shinyanga wakati wa hafla fupi ya ugawaji baiskeli 36 kwa wawezeshaji elimu ya ujasiriamali kutoka shirika lisilo la kiserikali (Rafiki-Sido ) mkoani Shinyanga linalojihusisha na mradi wa uwezeshaji wa vijana wa kike hususani wanaoishi katika mazingira magumu ili kuwainua kiuchumi.
Matiro amesema matatizo ya manyanyaso kwa wanawake kutoka kwa waume zao husabishwa na wao wenyewe kutokana na kutojishughulisha na biashara mbalimbali na kubaki kuwa tegemezi kwa mme wake na hivyo kuishi kama mtumwa.
“Ili kuondokana na tatizo la mfumo dume ndani ya jamii ni lazima wanawake wajishughulishe na biashara mbalimbali ambazo zitaondoa dhana ya utegemezi,kama mitaji ipo mnatakiwa mjiunge kwenye vikundi vya ujasiriamali ndipo serikali itoe pesa kwenu zile asilimia tano”,amesema Matiro.
Aidha amelipongeza shirika hilo la Rafiki kwa kuendelea kushirikiana na serikali katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii hususani kwenye suala la kumtetea mwanamke na kumuinua kiuchumi, huku akitoa wito kwa wanufaika na mradi huo kuyatumia mafunzo hayo vizuri ili kuondokana na hali ya umaskini.
Naye mkurugenzi wa shirika hilo, Geradi Ngong’a amesema mradi huo wa kumwezesha kijana wa kike kiuchumi, ulianza mwaka 2015 na kutarajiwa kuisha 2018 ambapo mpaka sasa wameshaunda vikundi vya ujasiriamali 180 kutoka katika kata 15 za manispaa ya Shinyanga sawa na vijana 3,833 .
Hata hivyo Ngong’a amesema, mradi huo unahusisha vijana wa kike ambao wapo nje ya shule kuanzia miaka 15-24 wakiwemo waliobebeshwa mimba,kuolewa ndoa za utotoni, kuishi maisha magumu kwa kuwapatia elimu ya ujasiriamali pamoja na kuwaunga kwenye vikundi vya vikoba ili wajikwamue kiuchumi.
Kwa upande wake mmoja wa waathirika wa mimba hizo za utotoni Christina Charles ambaye alipata ujauzito mwaka jana mara baada ya kuhitimu elimu ya darasa la saba ,amesema kabla ya kujiunga na shirika hilo alikuwa na maisha magumu, lakini sasa ana uwezo kwa kujihudumia mwenyewe kwa kuuza mboga mboga.
Nao baadhi ya wawezeshaji waliopewa baiskeli hizo Rose Noel na Getruda Ishengoma wamesema baiskeli hizo zitawasaidia kutembelea vikundi hivyo vya ujasiriamali kwa urahisi pamoja na kushauri vijana wengine wa kike kujiunga na shirika hilo ili wapate kujikomboa na umaskini.
Na Marco Maduhu-Malunde1 blog

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza katika hafla hiyo
Mkurugenzi wa shirika la Rafiki  Geradi Ngong’a akizungumza
Mkurugenzi wa shirika la Rafiki Geradi Ngong’a akizungumza
Baiskeli zikiwa eneo la tukio
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga akikabidhi baiskeli kwa wawezeshaji
Mwezeshaji akijaribu kuendesha baiskeli

KAIMU MKUU WA MKOA WA TANGA AIPONGEZA TAYODEA KWA KUSAIDIA KUWAINUA VIJANA KIUCHUMI

0
0

Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati wa uzinduzi wa akibadhi vifaa vya vijana wa mradi wa WEKEZA (Wezesha Ustawi Endelevu kiwango cha Elimu Kuzuia Ajira kwa watoto) kulia ni Mkurugenzi wa Tayodea, David Chanyegea na kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga,Faidha Salim.
 Mkurugenzi wa Tayodea, David Chanyege akizungumza wakati wa halfa hiyo kushoto kwake ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza.
Mwenyekiti wa Tayodea Stephen Kiama Mwaimu akizungumza wakati wa halfa hiyo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Muheza akizungumza kwenye halfa hiyo
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza kushoto akionyeshwa baadhi ya vifaa vya ushonaji waliokabidhiwa vijana kupitia mradi wa WEKEZA
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza kushoto akionyeshwa kitu na Meneja wa Mradi wa WEKEZA wa Tayodea Michael Mchomvu wakati wa halfa hiyo
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza akitazama vifaa mbalimbali vya ushonaji wa kwanza kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Tayodea ,David Chanyegea
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza akimsikiliza kwa umakini Mkurugenzi wa Tayodea,David Chanyegea kulia wakati wa halfa ya kukabidhiwa vifaa vya ushonaji kwa vijana kupitia mradi wa WEKEZA.

 Meneja wa Mradi wa WEKEZA wa Tayodea Michael Mchomvuwa kwanza kulia akifuatilia hotuba ya Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Mwanasha Tumbo wakati wa kukabidhiwa vifaa kwa vijana.

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

VIFAA VYA OFISI VYA WATUMISHI WA MALIASILI WANAOHAMIA DODOMA AWAMU YA KWANZA VYASAFIRISHWA LEO

0
0
 Moja ya gari la jeshi lililokuwa limebeba vifaa vya ofisi vya watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii likiondoka rasmi makao makuu ya wizara hiyo leo kuelekea mjini Dodoma. (Picha na Hamza Temba - WMU)
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akiaga msafara wa magari yaliyobeba vifaa vya ofisi vya kundi la kwanza la watumishi wa wizara hiyo wanaohamia Makao Makuu ya Nchi Mjini Dodoma nje ya jengo kuu la Wizara hiyo (Mpingo House) Jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Hamza Temba - WMU)

ASKOFU GADI AMPONGEZA RAIS DK. MAGUFULI KUMTEUA KAMISHNA WA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA, AMUOMBEA PAMOJA NA NCHI

0
0
Askofu Ernest Sumisumi (wa pili kushoto) wa Kanisa la Baptist akiiombea ramani ya Tanzania pamoja na picha ya Rais Dk. John Magufuli.
Askofu wa Good News  for All Ministry,  Dkt. Charles Gadi na Askofu Filbert Mbepera (kuli), wakiyabariki mafuta ya kupaka picha ya Rais, Dk. Magufuli.
Askofu Hezron Mwamsemba wa Kanisa la Baptist akiipaka mafuta picha ya Rais Dk. John Magufuli.
Maaskofu wa madhehebu mbalimbali wa dini ya Kikristo, wakiinyanyua juu picha ya Rais Magufuli, baada ya kuipaka mafuta na kuiombea.
Askofu John Sambuki (wa pili kulia) wa Victory Gospel Assemble a.k.a Furahini Katika Bwana, akiiombea bendera, wakati wa hafla hiyo.
Maaskofu na baadhi ya watumishi wa madhehebu hayo ya dini ya Kikristo wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa maombi hayo.

Askofu wa Good News  for All Ministry,  Dkt. Charles Gadi  akizungumza na waandishi wa habari wakati madhehebu mbalimbali hapa nchini walipomuombea Rais Dkt. John Pombe Magufuli, nchi, pamoja na kumpongeza kwa kumteua Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Dar es Salaam leo. Kushoto ni Askofu Hezron Mwamsemba wa Kanisa la Baptist jijini na katikati ni Askofu Ernest Sumisumi wa kanisa hilo.(Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Baadhi ya waandishi wa habari, wakimsikiliza Askofu wa Good News  for All Ministry,  Dkt. Charles Gadi  wakati alipokuwa akizungumza.
Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini ya Kikristo, wakiongozwa na Askofu wa Good News  for All Ministry,  Dkt. Charles Gadi (katikati), wakiimba wimbo wa amani wakati wa kumuombea Rais Dk. Magufuli na Taifa.
Askofu Filbert Mbepera (wa pili kuli) wa Kanisa la EAGT, akiombea amani nchi.


Na Lilian Lundo – Maelezo
ASKOFU wa Good News  for All Ministry  Dkt. Charles Gadi  kwa niaba ya dini na madhehebu mbalimbali hapa nchini wamempongeza  Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumteua Kamishna wa Mamlaka ya Kuthibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya.

Dkt. Gadi ametoa pongezi hizo leo, Jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na vyombo vya habari katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO).

“Tunamshukuru Mungu kwa kumuinua Rais ambaye ameonyesha nia na kuwa mstari wa mbele  kupigana na biashara hiyo haramu, ni ukweli usiopingika kwamba tatizo la dawa  ya kulevya ni kubwa na lenye madhara makubwa sana kwa watanzania  wengi haswa vijana ambao ni nguvu kazi  ya Taifa,” alifafanua Dkt. Gadi.

Aliendelea kwa kusema kuwa, Vijana wengi wamepoteza maisha , kuharibika akili, kupata magonjwa ya kuambukiza, kupoteza malengo ya kimaisha kwa sababu ya dawa hizo. Vile vile dawa hizo zimeleta fedheha kwa Taifa kutokana na Vijana wengi wa Kitanzania kuwepo katika magereza mbalimbali Duniani huku wengine wakisubiri  adhabu  ya kunyongwa.

Aidha amempongeza Rais Dkt. Magufuli kwa kuimarisha Mamlaka ya Kuthibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa  kumteua Kamishna ambaye atasimamia Mamlaka hiyo na anaamini kwamba kwa neema ya Mungu ataweza kumsaidia kikamilifu  Rais Magufuli katika kutimiza azma yake ya kukomesha  biashara hiyo.

Wakati huo huo, Dkt. Gadi amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuianzisha vita hiyo dhidi ya matumizi ya dawa kulevya katika mkoa wa Dar es Salaam. Vile vile amewapongeza waandishi wa habari na vyombo mbalimbali vya habari kwa kutoa habari zinazosaidia katika upambanaji wa  biashara hiyo.

Dkt. Gadi amewataka viongozi wa Dini kuungana bega kwa bega na Rais Magufuli kwa kuendelea kutoa maadili kwa vijana ili kuepukana na uovu wa dawa za kulevya nchini.

ZIARA YA MKURUGENZI WA NAMAINGO KUIMARISHA UJASIRIAMALI MIKOANI

0
0
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Namaingo Business Agency, Ubwa Ibrahim akiwa katika moja ya ,ya mikoa kukagua na kuimarisha shughuli za Wajasiriamali wanachama wa kampuni hiyo katika mikoa mbalimbali nchini. Tayari hadi leo ameshafanya ziara katika mikoa ya Iringa, Tabora, Kigoma, Manyara, Arusha na Kilimanjaro.

Mafunzo yanayotolewa na kampuni hiyo kwa wajasiriamali zaidi ya 400,000 nchini ni. ufugaji wa kuku wa chotara, sungura, samaki pamoja na kilimo bishara cha mbogamboga na matunda.

Pia husaidia kupatika kwa masoko ya bidhaa hizo, pamoja na kuwaunganisha katika taasisi mbalimbali za kifedha ili kupata mikopo kirahisi. Imeandaliwa na Richard Mwaikenda; Kamanda wa Matukio Blog























VIJIJI VITATU PERAMIHO VYA NUFAIKA NA MIRADI YA MAJI YENYE THAMANI YA MILIONI 21 RUVUMA.

0
0

Mkurugezi wa Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu JOSEPH PERAMIHO, iliyopo halimashauri ya wilaya ya peramiho mkoani Ruvuma, BRUDA ASGARI STUFE ,amezindua miradi mitatu ya mabomba ya maji safi yenye thamani ya shilingi milioni 21 katika vijiji vya Mgazini,Peramiho B na Kiwulungi katika tarafa ya Ruvuma.

DC MTATURU ATOA MWEZI MMOJA WAFANYABIASHARA WA ASALI KANDO YA BARABARA SINGIDA-DODOMA KUHAMIA JENGO JIPYA.

0
0
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akionyesha moja ya kifungashio bora cha asali katika uzinduzi wa vifungashio hivyo.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akizungumza na wadau wa asali wakiwemo wazalishaji na wafanyabiashara katika uzinduzi wa vifungashio vya asali wilayani humo.
Mkurugenzi wa wilaya ya Ikungi Rustika Turuka akitoa salam kwenye uzinduzi wa vifungashio vya asali uliofanyika katika kijiji cha Issuna wilayani humo.

…………………………………………………………………………..

MKUU wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida Miraji Mtaturu ametoa mwezi mmoja kuanzia leo kwa wafanyabiashara wote wanaouza asali pembezoni mwa barabara kuu ya Singida-Dodoma kuhamia katika jengo lililojengwa na serikali ili kuongeza thamani na kurahisha upatikanaji wake.

Akizungumza katika uzinduzi wa vifungashio vya asali uliofadhiliwa na wakala wa misitu Tanzania(TFS)leo katika kijiji cha Issuna A wilayani humo Mtaturu amesema serikali iliwekeza kwa makusudi katika jengo hilo ili kuwainua wazalishaji wa asali lakini ni zaidi ya miaka mitatu sasa toka likamilike na halijaanza kutumika.

“Kauli mbiu yetu ni asali bora, maisha bora na hii inaenda sambamba na mikakati ya serikali katika kuboresha maisha ya wananchi na dira ya maendeleo ya Taifa 2025 lakini pia inaunga mkono Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020 iliyoahidi kuendeleza program ya ufugaji nyuki ili kuwajengea uwezo wadau,”alisema Mtaturu.

Aliwapongeza TFS kwa juhudi zao katika uhifadhi wa misitu na kutoa mafunzo kwa kamati za mazingira karibu vijiji vyote wilayani humo lakini pia kwa hatua yao ya kuleta vifungashio na kwa wadau kuendelea na ushirikiano waliouonyesha.

Alisema vifungashio hivyo vitatumika kufungashia asali bora ya Ikungi na hivyo kuondokana na vifungashio ambavyo vimezoeleka ambavyo kiafya sio salama huku akiwaasa wazalishaji na wafanyabiashara kuwa pamoja ili kupata fursa mbalimbali na kuboresha uzalishaji wenye tija zaidi kiuchumi.

“Sekta hii ikipewa kipaumbele ikiwemo kutatua changamoto zake inayo nafasi kuchangia kwa kiasi kikubwa katika uhifadhi wa mazingira ,itapunguza umaskini na kuongeza pato la mwananchi na Taifa kwa ujumla kwa kuwa soko la bidhaa hii na nta lipo ndani nan je ya nchi,”aliongeza Mtaturu.

Alieleza mpango wa wilaya kuwa ni kusaidia uanzishwaji wa vikundi vya ufugaji nyuki vya wanawake na vijana na kuvijengea uwezo ili hatimaye viongeze uzalishaji na kupelekea kuwa na kiwanda cha kuchakata asali wilayani humo hatua ambayo itasaidia kuongeza thamani ya zao hilo na kumuagiza mkurugenzi wa halamshauri hiyo kuongeza bidii ya uundaji wa vikundi ili kuvijengea uwezo na kufikia malengo mapema.

Mtaturu aliwanunulia vikundi viwili vifungashio 200 vya kuanzia na kuahidi kuwapelekea mizinga 20 kama chachu ya kutumia mizinga ya kisasa ambayo uvunaji mmoja unapata lita 18 kwa mzinga tofauti na ile ya kienyeji inayovunwa kiwango kidogo kisichofikia lita 5 kwa mzinga.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na kaimu meneja wa TFS wilaya Samson Lyimo zinaonyesha kuwa kila mwaka uzalishji wa asali unaongezeka ambapo mwaka 2014/2015 ilikuwa tani 3.6 na 2015/2016 tani 4.617 na kusisitiza kufuatwa kwa kanuni za kuwa na mizinga bora,uvunaji bora na kutumia vifungashio vinavyotakiwa kwa mujibu wa sheria ambapo ameeleza changamoto waliyokuwa wanaipata ya kushindwa kuwafikia wafanyabiashara kutokana na kutokuwa na eneo maalum.

Akimkaribisha mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo meneja wa TFS kanda ya kati Mathew kiondo aliahidi kuendelea kutoa vifungashio vya kutosha ili asali Ikungi iongezeke ubora kwa kifungashio cha lita moja wachangie shilingi mia 500 na cha nusu lita wachangie shilingi 300 na kueleza lengo lao ni kuwaweka pamoja ili kuwapatia fursa ya mikopo kupitia program ya kopa mzinga lipa asali.

Katika uzinduzi huo alichangia madawati 50 katika kusaidia mkakati wa wilaya uliotangazwa na mkurugenzi wa halamshauri Rustika Turuka wa kumaliza tatizo la madawati uliopewa jina la “changia dawati umnusuru dogo wa Ikungi asikae chini”.

NHIF YAKUTANA NA WADAU NA KUAHIDI UBORESHAJI WA HUDUMA ZA AFYA MKOANI GEITA

0
0
Mwenyekiti wa Bodi NHIF na Spika mstaafu wa Bunge mama Anna Makinda akisisitiza juu ya kuboreshwa huduma katika mfuko wa Bima ya afya wa Taifa. 
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akiwa na mwenyekiti wa Bodi ya NIHF wakisikiliza kwa makini taarifa ya Mkoa wa Geita juu ya mfuko wa bima ya afya .
Mbunge wa Geita Mjini Constatine Kanyasu na Mbunge wa Jimbo la Busanda  Lorencia Bukwimba wakifuatilia mkutano .
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akifungua mkutano wa wadau wa Mfuko wa Bima wa Taifa Mkoani Humo.
Mbunge wa Geita Mjini Constatine Kanyasu,akielezea namna ambavyo kumekuwepo na changamoto za huduma ya afya katika jimbo ambalo analiongoza.
Mbunge wa Bukombe Dotto Biteko akichangia swala la huduma ambazo zinatolewa na mfuko wa Bima ya afya wa NHIF.
Baadhi ya wajumbe wakiwa kwenye mkutano huo wakisikiliza taarifa ya utekelezaji wa shughuli za NHIF.
Kaimu Mkurugenzi wa NHIF Angela Mziray akifafanua namna ambavyo NHIF imekuwa ikisaidia wa gonjwa wenye magonjwa yasiyoambukiza.
Meneja wa NHIF Mkoani Geita Mathias Sweya akielezea namna ambavyo shughuli za kuandikisha wanachama wapya jinsi zikifanyika Mkoani Geita .
Wajumbe wakiendelea kufatilia mkutano.
Mwenyekiti wa Bodi NHIF na Spika mstaafu wa Bunge mama Anna Makinda,akiwashkuru wajumbe ambao wamehudhuria Mkutano huo.
Picha ya pamoja mwenyekiti wa Bodi ya NHIF pamoja na wajumbe ambao wameshiriki mkutano huo.

RC MRISHO GAMBO AENDELEA NA ZIARA YAKE WILAYANI MONDULI

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo, jana  february 22,2017 ameendelea na ziara yake ya kikazi kwa siku ya tatu katika Wilaya ya Monduli ambapo yupo wilayani humo kwa ziara ya siku tano ambapo ijumaa ya wiki hii atakamilisha ziara hiyo.

Akiwa kwenye ziara hiyo leo ametembelea Zahanati ya Mswakini Juu iliyopo Wilayani humo na kujionea utendaji kazi,na maendeleo ya zahanati hiyo pamoja na kusikiliza kero zinazowakabili wananchi waishio jirani na kituo hicho cha Afya.
Pichani Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, Akiwasili kwenye Zahanati ya Mswakini Juu Wilayani Monduli .
Picha na msumbanews blog
kutoka kushoto Mkuu wa mkoa akikagua maendeleo ya zahanati,Aliyeshika fimbo ni Mbunge wa Monduli Julius Kalanga,kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo ( Chadema ) akiwa ameambatana na wajumbe wake.Picha na msumbanews blog



Mkuu wa Mkoa wa Arusha Akigagua baadhi ya mashine katika kwenye zahanati hiyo. Picha na Msumbanews blog




Mkuu wa Mkoa Akisalimiana na wananchi wa Mswakini juu waliohudhuria kwenye ziara hiyo. Picha na Msumbanews blog .
Mbunge wa Monduli Julius Kalanga Akihutubia wananchi wa Mswakini juu. Picha na Msumbanews blog



Mkuu wa Mkoa Akikagua baadhi ya nyumba za wauguzi wa Zahanati hiyo ya Mswakini juu. Picha na Msumbanews blog.

WENGI WAJITOKEZA KUPIMA AFYA BURE KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA.

0
0
Zoezi la upimaji wa Afya Bure kwa wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani linalofanyika kwa siku tangu kuanzia jana, linaendelea katika viwanja vya Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu la Sabasaba Ilemela.

Mchungaji wa kanisa hilo, Dkt.Daniel Moses Kulola (kulia) amebainisha kwamba jana zaidi ya wananchi 150 walijitokeza kupima afya zao ambapo zaidi ya 70 walihudumiwa na kurejea nyumba.

Alisema zoezi hilo limejikita kwenye uchunguzi wa afya ya uzazi, kisukari, presha pamoja na uzito likiongozwa na wataalamu wa afya kutoka Canada wanaosaidizana na wataalamu wazawa.
#BMGHabari
Umati wa akina mama waliojitokeza kwenye zoezi la upimaji afya bure katika viunga vya kanisa la EAGT Lumala Mpya
Zoezi la kuchukua taarifa likiendelea kwa umakini
Zoezi hilo la upimaji afya bure linafanyika kwa siku mbili kuanzia jana
Zoezi hilo la upimaji afya bure linafanyika kwa siku mbili kuanzia jana na linasimamiwa na wataalamu wa afya kutoka Canada
Zoezi hilo la upimaji afya bure linafanyika kwa siku mbili kuanzia jana
Kwa wale watakaobainika kuwa katika hali ya uchunguzi zaidi watasaidiwa kufikishwa kwenye hospitali za rufaa ili kuhudumiwa.

Ujenzi wa Ubungo interchange kuanza mara moja

0
0
Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), jana umetiliana saini na kampuni ya M/S China Civil Engeneering Construction Cooperation kutoka China (CCECC) mkataba wa ujenzi wa barabara za Juu ‘Interchange’ katika makutano ya barabara ya Sam Najoma na Mandela Ubungo jijini Dar es salaam.

Mkataba huo unamtaka Mkandarasi kampuni ya CCECC kutoka China kuanza ujenzi huo mara moja na ujenzi huo unatarajiwa kutumia takriban miezi 30 hadi kukamilika kwake.Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Eng. Patrick Mfugale amesema zaidi ya shilingi Bilioni 177.4 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi huo utakaowekewa jiwe la msingi mwezi machi mwaka huu.

“Hakikisheni mnaanza ujenzi mara moja kwani Serikali imeshakamilisha taratibu zote na tayari kiasi cha shilingi bilioni 2.1 kimelipwa kwa ajili ya fidia kwa wananchi walioguswa na mradi huo”. Amesema Eng. Mfugale.Ujenzi wa Ubungo interchange unajengwa kwa fedha ya mkopo kutoka Benki ya Dunia ambapo Serikali kwa upande wake imeshalipa fidia ya zaidi ya shilingi bilioni 2.1

“Zaidi ya magari 65,000 yanapita kila siku katika katika makutano ya barabara za morogoro,Mandela na sam nujoma eneo la Ubungo hali inayosababisha msongamano katika barabara ya Morogoro ambayo ndio lango kuu la kuingia jijini Dar es salaam hivyo ufanisi wa mradi huo utahuisha hali ya usafirishaji katika jiji la Dar es salaam na kuchochea ukuaji wa uchumi” amesisitiza Eng. Mfugale.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CCECC Bw, Jiang Yigao amemhakikishia Eng. Mfugale kuwa wataanza maandalizi ya ujenzi huo mara moja na watafanya kazi hiyo kwa wakati.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya M/S China Civil Engeneering Construction Cooperation kutoka China (CCECC) Jiang Yigao wakibadilisha hati za mikataba mara baada ya kusaini ujenzi wa barabara za juu eneo la ubungo (Interchange).
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya M/S China Civil Engeneering Construction Cooperation kutoka China (CCECC) Jiang Yigao wakisaini mkataba wa ujenzi wa barabara za juu eneo la ubungo (Interchange).
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya M/S China Civil Engeneering Construction Cooperation kutoka China (CCECC) Jiang Yigao (Katikati) wakisaini mkataba wa ujenzi wa barabara za juu eneo la ubungo (Interchange).Kushoto ni Meneja Mradi wa ujenzi huo Li Haiquan.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale akifafanua jambo wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa ujenzi wa barabara za juu eneo la ubungo (Interchange) utakaotekelezwa na kampuni M/S China Civil Engeneering Construction Cooperation kutoka China (CCECC).
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale akitoa maelezo wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa ujenzi wa barabara za juu eneo la ubungo (Interchange) utakaotekelezwa na kampuni M/S China Civil Engeneering Construction Cooperation kutoka China (CCECC).
Baadhi ya wawakilishi wa Mkandarasi wa kampuni ya M/S China Civil Engeneering Construction Cooperation kutoka China (CCECC) wakifuatilia hafla ya utiaji saini ya ujenzi wa Ubungo interchange Jijin Dar es salaam.

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA HOYCE TEMU

0
0
 Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania akimkaribisha ofisini kwake  Mkuu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Nchini Hoyce Temu, Ikulu jijini Dar es Salaam (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
 Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza na  Mkuu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Nchini Hoyce Temu (kushoto) aliyemtembelea Makamu leo ofisini kwake, Ikulu jijini Dar es Salaam (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Nchini Hoyce Temu mara baada ya mazungumzo, Ikulu jijini Dar es Salaam (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI

0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkaribisha ofisini kwake Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Mwigulu Nchemba tayari kwa mazungumzo Ikulu jijini Dar Es Salaam. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na  Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Mwigulu Nchemba , Ikulu jijini Dar Es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na  Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Mwigulu Nchemba , Ikulu jijini Dar Es Salaam ( Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Viewing all 46193 articles
Browse latest View live




Latest Images