Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1136 | 1137 | (Page 1138) | 1139 | 1140 | .... | 1897 | newer

  0 0


  0 0


  Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya igunga,mkoani tabora wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo

  Mbunge wa jimbo la Manonga,wilayani Igunga,mkoani Tabora,Mhe.Hamisi Gullamali(wa kwanza kulia) wakiteta jambo na katibu wake wakati wa mkutano wa kawaida wa baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)
  Jengo la ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Igunga,Mkoani Tabora, mahali kulikofanyikia mkutano wa kawaida wa baraza la madiwani.
  Katibu Tawala Mkoa wa Tabora,Dk.Thea Ntala akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumza na madiwani,watendaji wa Halmashauri ya wilaya pamoja na viongozi wa chama na serikali waliohudhuria mkutano huo wa kawaida wa Baraza la madiwani uliofanyika hivi karibuni kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.


  KATIBU Tawala wa Mkoa wa Tabora,amewaagiza waganga wakuu wa wilaya za Mkoa huo kuhakikisha kwamba wanaume wote watakaougua na kulazwa Hospitalini kwa ugonjwa wowote ule,wawaambie kuwa ugonjwa huo unatokana na uchafu unaotoka kwenye sehemu za siri za mwanaume huyo kutokana na kutofanyiwa tohara.

  Katibu Tawala huyo,Dk.Thea Ntala alitoa agizo hilo alipokuwa akiongea na madiwani pamoja na watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga kwenye mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo uliofanyika hivi karibuni kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.

  “Nimewaagiza waganga wakuu wote wa wilaya kuwa mgonjwa yeyote mwanaume akiwepo Mheshimiwa diwani,akiwepo mheshimiwa mbunge wakilazwa pale Hospitali awe anaumwa jino,awe anaumwa sikio,awe anaumwa mkono mwambie hivi hili tatizo lako linatokana na uchafu unaotoka kwenye sehemu za siri kwa kutofanyiwa tohara”alisisitiza katibu tawala huyo.

  Kwa mujibu wa Dk.Ntala haiwezekani katika Mkoa wa Tabora wakaendelea kukaa na wanaume ambao mpaka sasa bado hawajafanyiwa tohara kwani kuendelea kukaa na watu wa aina hiyo kunachangia kwa namna moja au nyingine ongezeko la maambukizi mapya ya ugonjwa wa Ukimwi.

  “Hatuwezi kukaa Tabora,hatuwezi kukaa na hicho kitu na ndiyo maana ugonjwa huu wa Ukimwi unaendelea kutokana na sababu za kuendelea kuwepo kwa watu wasiofanyiwa tohara,nimewaagiza MADMO,RMO hili nimewaagiza wote Tabora kuhakikisha wanawafanyia uchunguzi wanaume wote wanaolazwa iwapo wamefanyiwa tohara”alifafanua huku akiwaacha waliohudhuria mkutano huo wakiangua kicheko.

  Hata hivyo Dk.Ntala alibainisha kwamba hivi sasa baadhi ya wanaume wamekuwa wakihudhuria kwenye semina kupatiwa elimu ya juu ya umuhimu wa kufanyiwa tohara huku wengine wakiamua kwenda kwa hiyari yao kufanyiwa tohara hiyo kwenye maeneo yanayotoa huduma hizo.

  Akizungumzia kuhusu ugonjwa wa mabusha,Dk.Ntala alitumia fursa hiyo kuwashauri wanawake kumeza dawa kwani dawa za ugonjwa huo zinatakiwa kumezwa na wanaume pamoja na wanawake na kuonya dhana potofu iliyojengeka miongoni mwa jamii ya kuamini kwamba ugonjwa wa mabusha hauwahusu wanawake bali unawahusu wanaume peke yao.

  “Madiwani mnisaidie kwenye mikutano wanawake wanafikiri ukiongelea ugonjwa wa mabusha ni wanaume,aah mwanamke anapata mabusha kwenye matiti yaani badala ya kuwa na saizi ya kawaida kama ya RAS anakuwa na saizi kubwa kama tikitimaji fulani hivi…sijui kama kuna watu wanapenda magodoro makubwa”alibainisha katibu huyo tawala.

  0 0


  0 0

   Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Omary Kumbilamoto akizungumza na wafanyabishara wa soko la Ilala
   Wafanyabiahsra wakimsikiliza Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto katika mkutano wa halmashauri ya Ilala na wadau wa soko hilo.
   Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akiwa ameongozana na mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa hiyo.

  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa kukabidhi matembezi ya Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa wananchi wote ya kupambana na magonjwa yasioambukiza, Makao Makuu ya nchi Dodoma.

  Makamu wa Rais Mh.Samia Suluhu Hassan akishiriki mazoezi mapema leo asubuhi mjini Dodoma ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa wananchi wote ya kupambana na magonjwa yasioambukiza, mjini Dodoma.Pichani kushoto ni Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Mh.Nape Nnauye.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ashiriki kumuunga mkono Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa katika Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa wananchi wote ya kupambana na magonjwa yasioambukiza, mjini Dodoma.Mbali ya Makamu wa Rais kuunga mkono tukio hilo pia walikuwepo viongozi mbalimbali wa Serikali,akiwemo Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Mh.Nape Nnauye ,Naibu Spika wa Bunge,Tulia Ackson,Waziri wa Mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba,Naibu waziri wa Afya.Maendeleo ya Jamii,Ustawi wa Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt Khamis Kigwangalla na wengineo sambamba na Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Mji wa Dodoma.

  Makamu wa Rais Mh.Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Waziri wa Mambo ya Ndani,Mwigulu Nchemba kabla ya kuanza mazoezi ya kumuunga mkono Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa katika Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa wananchi wote ya kupambana na magonjwa yasioambukiza, mjini Dodoma

  Wananchi kutoka vitongoji mbalimbali vya mji wa Dodoma wakishiriki mazoezi mapema leo asubuhi ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa katika Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa wananchi wote ya kupambana na magonjwa yasioambukiza, mjini Dodoma.

  0 0


  Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa  mwalimu  Amina Masenza (wa tatu kushoto) akiongoza  mazoezi ya viungo katika  uwanja wa  samora  Leo wa  pili kushoto ni katibu  tawala wa mkoa  wa Iringa wamoja Ayubu

  DC  Iringa  Richard  Kasesela wa kwanza  kulia  akishiriki mazoezi ya  riadha kutoka  uwanja  wa Samora

  Washiriki wa  mazoezi  wakiwasili  ufisi ya  RC Iringa wakitokea  uwanja  wa  Samora

  Afisa  michezo mkoa wa Iringa Kenedy Komba  akiorodhesha  majina  ya wakuu wa Idara  walioshiriki mazoezi leo ni  kuwabana wamnaokwepa mazoezi


  Wanamazoezi  wakitoka  uwanja wa  samora


  Mkazi  wa Iringa  akiwa amebeba  pombe aina ya  komoni asubuhi ya  leo pombe  hii inatengenezwa kwa mahindi jambo  ambalo  serikali  ya  mkoa imepiga marufuku matumizi mabaya ya  chakula

  Mkazi  wa Iringa  akipishana na washiriki wa mazoezi huku  akiwa amebeba pombe ya  komoni inayotengenezwa  kwa mahindi

  RAS  Iringa na RC Masenza kulia  wakiwa katika mazoezi

  RC Iringa Amina Masenza  kulia  akiongoza mazoezi saa 12 asubuhi ya  leo

  Afisa  habari Manispaa ya  Iringa  Sima Bingilengi kushoto  akiwajibika

  Mwanahabari Manispaa ya  Iringa Janeth Matondo kulia pia  akishiriki mazoezi


  DC  Kasesela katikati wa  pili  kulia akiwa na wadau  wa  kwanza  kulia ni Geofrey  Mungai
  Mzee Vitus Mushi  akiwajibika mazoezini

  DC  Iringa  Richard Kasesela  wa  tatu katikati  kulia akiwa na mkurugenzi Manispaa ya  Iringa Dr  Wiliam na mwanasheria  wa  Iringa wa  pili kulia

  Na MatukiodaimaBlog.

  MKUU  wa  mkoa  wa  Iringa mwalimu  Amina Masenza amewaonya  watumishi  wa serikali ambao wanakwepa  kushiriki mazoezi ya  pamoja katika  uwanja  wa  Samora  na  kuwa kuanzia sasa mtumishi atakayekwepa kushiriki  kubanwa .

  Alisema pamoja na kuwa mazoezi  hayo ni kwa ajili ya afya za kila mmoja kujikinga na maradhi  yanayosababishwa na  kutofanya mazoezi ila  bado mazoezi hiyo  ni  utekelezaji wa agizo la makamu  wa Rais kwa  kila mtanzania .

  Hivyo  alisema kutokana na baadhi ya  watumishi hasa  wanawake  kukwepa mazoezi hayo anaandaa mkakati wa kuwabana  watumishi  wote  wanaokwepa mazoezi kwa  kuitisha mazoezi  siku ya kazi ili wale  ambao  watashindwa  kufika watawajibishwa .

  "Naangalia  ni  siku gani  ambayo  itakuwa ni  siku ya kazi kama ijumaa ama siku  nyingine  yeyote  ambayo  nitaitisha mazoezi kuanzia ofisi  yangu  hadi  Samora kwa  kila mtumishi kushiriki na siku hiyo hata ofisini  watumishi  wakichelewa ni  sawa lengo  kuweza  kufanya mazoezi na kutekeleza agizo la  serikali ......nashangazwa  sana  awali  wanawake  ndio  ambao  walikuwa  wakifika kwa  wingi mazoezini  ila leo  hii idadi ya  wanawake  imepungua ukilinganisha na  wanaume ....nawashangaa sana wanawake  wanaokwepa mazoezi  wakati  ndio ambao  wanakula vitu  vyenye mafuta "

  Hivyo  alisema  kuanza sasa  kila mtumishi  wa serikali  lazima  kufika katika mazoezi na  utawekwa  utaratibu  wa  kuorodhesha majina kila idara  ya  watu  wanaoshiriki mazoezi .


  0 0

   The Tanzania Revenue Authority (TRA) Commissioner General Mr. Alphayo Kidata (right) welcomes the World Customs Organisation (WCO) Secretary General Dr. Kunio Mikuriya when he paid a courtesy call to TRA in order to discuss issues pertaining to customs projects implemented by TRA in collaboration  with WCO
   The World Customs Organisation (WCO) Secretary General Dr. Kunio Mikuriya appreciating a book of Tanzania History handed to him by the Tanzania Revenue Authority (TRA) Commissioner General Mr. Alphayo Kidaya as a symbol of remembrance of his visit in Tanzania. Dr. Mikuriya paid a courtesy call to TRA in order to discuss issues pertaining to customs projects implemented by TRA in collaboration with WCO.
   The World Customs Organisation (WCO) Secretary General Dr. Kunio Mikuriya stressing  a point during a joint meeting with the Tanzania Revenue Authority (TRA) Commissioner General Mr. Alphayo Kidaya (right) when he paid a courtesy call to TRA in order to discuss issues pertaining to customs projects implemented by TRA  in collaboration  with WCO.
  ·       The Tanzania Revenue Authority (TRA) Manager for Customs Automation Systems Mr. Felix Tinkasimile (standing) making a presentation on how the Tanzania Customs Integrated System (TANCIS) operates to the World Customs Organisation (WCO) Secretary General Dr. Kunio Mikuriya (seated center). Looking on are the WCO Regional Development Manager for East and Southern Africa Mr. Patrick Gyan (left) and the Commissioner for Customs and Excise Mr. Jocktan Kyamuhanga. The WCO Secretary General paid a courtesy call to TRA in order to discuss issues pertaining to customs projects implemented by TRA in collaboration with WCO.

  0 0

   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiongoza matembezi yaliyoshirikisha  Mawaziri, Wabunge pamoja na wananchi walioshiriki mazoezi hayo ambayo yamehitimishwa katika Uwanja wa Jamuhuri Dodoma yakiwa na
  lengo la kupambana na maradhi yasiyo ambukizika.  Mazoezi hayo yamefanyika kitaifa Mkoani Dodoma
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiongoza mazoezi ya viungo kwa Mawaziri Wabunge pamoja na wananchi waliouhudhiria katika kushiriki mazoezi hayo ambayo yamefanyika katika Uwanja wa Jamuhuri Dodoma yakiwa na lengo la kupambana na maradhi yasiyo ambukizika Mazoezi hayo yamefanyika kitaifa Mkoani Dodoma
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwahutubia Mawaziri Wabunge Watumishi na Wananchi wa Mkoa wa Dodoma ambao wajitokeza katika kushiriki Mazoezi ya Viungo yenyelengo la Kupambana na Magonjwa yasiyo ambukizika Mazoezi hayo Kitaifa yamefanyika katika Uwanja wa Jamuhuri Mkoani Dodoma. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (aliyevaa traksuti nyeusi) akiwa ameongozana na Viongozi mbalimbali kuelekea Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kwenye Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa Wananchi wote yaliyofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo 11/02/2017.

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (aliyevaa traksuti nyeupe) akiwa ameongozana na Viongozi mbalimbali kuelekea Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kwenye Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa Wananchi wote yaliyofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo 11/02/2017.

  Kikosi cha Bendi ya Matarumbeta ycha Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakiongoza matembezo kuelekea Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kwenye Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa Wananchi wote yaliyofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo 11/02/2017.

  Umati wa watu pamoja na Jeshi la Wananchi Tanzania wakiwa katika matembezi kuelekea Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kwenye Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa Wananchi wote yaliyofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo 11/02/2017.

  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (wa pili kulia), Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wa pili kushoto) pamoja na Viongozi wengine wakifanya mazoezi kuelekea Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kwenye Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa Wananchi wote yaliyofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo 11/02/2017.


  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (aliyevaa traksuti nyeupe) akiongoza mazoezi ya viungo wakati wa Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa Wananchi wote yaliyofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo 11/02/2017.

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akiwahutubia baadhi ya Viongozi wa Serikali pamoja na wananchi (hawapo pichani) waliohudhuria Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa Wananchi wote yaliyofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo 11/02/2017.

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akitoa neno la shukrani mbele ya Viongozi wa Serikali pamoja na wananchi waliohudhuria Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa Wananchi wote yaliyofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo 11/02/2017.

  Waziri Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiongelea kuhusu umuhimu wa mazoezi katika kulinda afya, mbele ya Viongozi wa Serikali pamoja na wananchi waliohudhuria Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa Wananchi wote yaliyofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo 11/02/2017.

  Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu(Vijana, Kazi na Ajira), Mhe. Anthony Mavunde, akiongea jambo akiwa kama Kiongozi mwakilishi wa Mkoa wa Dodoma, mbele ya Viongozi wa Serikali pamoja na wananchi waliohudhuria Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa Wananchi wote yaliyofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo 11/02/2017.

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kulia) akiongea na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo leo mara baada ya kumalizika kwa Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa Wananchi wote yaliyofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo 11/02/2017.
  (PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM)

  Na. Lilian Lundo-Dodoma.


  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ameziagiza Halmashauri, Manispaa na Majiji yote nchini kutenga maeneo kwa ajili ya wananchi kufanya mazoezi na kupumzika.  Kassim Majaliwa ametoa agizo hilo leo, Mjini Dodoma wakati wa Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa Wananchi wote yaliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri.  "Ni muhimu kufanya mazoezi kila siku, mazoezi yanasaidia kuchangamsha mwili, kufahamiana, kujenga urafiki pamoja na kuwa na afya bora," alisema Mhe. Majaliwa.  Waziri Mkuu amesema kwamba, muitikio wa ufanyaji mazoezi wa viungo ni mkubwa, ambapo watu wengi wamejiunga na vikundi mbalimbali vya kufanya mazoezi ya viungo.  Aidha, amezitaka Halmashauri, Manispaa na Majiji yote nchini kutenga maeneo kwa ajili ya watu kufanya mazoezi na kumpuzika.  Ameongeza kuwa, watu wasilazimishwe kufanya mazoezi bali iwe ni hiari ya yao na kusiwe na gharama kwa ajili ya mtu kufanya mazoezi.  Vile vile amewataka Maafisa Utamaduni na Michezo nchini kuhamasisha mazoezi ya viungo katika maeneo yao pamoja na kuanzisha vikundi vya mazoezi ya viungo ambapo watakuwa wanakutana na kufanya mazoezi kwa muda ambao watajipangia.  Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amemshukuru Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuhamasisha mazoezi ya viungo na kuitangaza rasmi Jumamosi ya pili ya kila mwezi kuwa ni siku ya mazoezi ya viungo Kitaifa.  Aliendelea kwa kusema kuwa, mazoezi ya viungo yanamuepusha mtu na kupata magonjwa yasiyoambukiza kama vile magonjwa ya moyo, kisukari pamoja na saratani.  Naye Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye amesema kwamba, mazoezi ya viungo yanaratibiwa na Wizara ya Habari, Wizara ya Afya pamoja na TAMISEMI. Hivyo kwa pamoja watahamasisha uanzishwaji wa vikundi vya mazoezi ya viungo katika Halmashauri zote nchini kwa kuanza na watumishi wa Umma.  Aidha amewataka viongozi wanapokuwa mikoani katika siku ya mazoezi ya viungo wawahamasishe wananchi kufanya mazoezi ya viungo kwa ajili ya kulinda afya zao.  Uzinduzi wa Kitaifa wa mazoezi ya viungo ulianza kwa matembezi yaliongozwa na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan kuanzia viwanja vya Bunge na baadaye alimkabidhi Waziri Mkuu kuanzia Nyerere Square mpaka Uwanja wa Jamhuri. Uzinduzi huo umehusisha viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri, Wabunge, Viongozi wa Mkoa wa Dodoma pamoja na Wananchi wa Mkoa huo.

  0 0


  Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akizindua mazoezi ya viungo kwa kuonyesha kwa mfano kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid kuitikia wito wa Makamu wa Rais,Mh.Samia Suluhu Hassan wa kufanya mazoezi kila wiki ya pili ya mwezi kwa lengo kuzuia magonjwa yasiyoambukizwa na kuiweka miili katika hali ukakamavu.
  Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akipiga Push-Up za kutosha.

  Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha,Charles Mkumbo(kushoto) na Mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Daqarro nao hawakua nyumba katika kuonyesha ukakamavu wao.Picha zote na Filbert Rweyemamu
  Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo(katikati) akiongoza mazoezi mepesi akiwa na viongozi wengine.


  Umati uliojitokeza kushiriki mazoezi ya viungo kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
  Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha,Charles Mkumbo(kati)akipasha pamoja na wananchi
  Furaha ya ushindi wa kuvuta kamba
  Wadau katika halmashauri ya Jiji la Arusha walioshiriki mazoezi ya viungo.
  Furaha ya ushindi wa kuvuta kamba
  Mazoezi ya wanafunzi yakiendelea na mwalimu
  Mashindano ya kukimbia Yai likiwa kwenye Kijiko yamevutia wengi

  0 0

  BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma limewafukuza kazi watumishi wake wanne, kutokana na makosa mbalimbali yakiwemo ya utoro kazini na kuisababishia halmashauri hiyo hasara ya shilingi milioni 46,680,000.

  Waliofukuzwa kazi ni Mosta Ndunguru ambaye ni Afisa tabibu na Bapara Mwang’ombe Mhudumu wa afya ambapo wote kwa pamoja wamefukuzwa kwa makosa ya utoro kazini. Walioisababishia hasara halmashauri hiyo ya shilingi milioni 46,680,000 ni maofisa misitu wasaidizi, Kelvin Haulle na Ally Almasi. Msikilize mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Ambrose Nchimbi


  0 0

  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

  MWIMBAJI wa muziki wa taarab nchini Tanzania, Bi Khadija Kopa, amewataka wanawake kuendelea kujikwamua kiuchumi wao wenyewe bila kusubiri kuwezeshwa na wanaume.

  Khadija aliyasema hayo jana katika ufunguzi wa duka kubwa la kisasa la urembo na nguo za wanawake linalojihusisha pia na kupamba maharusi, kukodisha na kuuza nguo za maharusi, linalojulikana kama Taiba Beauty, linalomilikiwa na mjasiriamali Twaiba Ahmed Ally.
  Mwimbaji mkongwe wa muziki wa taarabu nchini, Bi Khadija Kopa, akizungumza na waandishi hawapo pichani katika uzinduzi wa duka la nguo za wanawake na za harusi linalomilikiwa na mwanamama Twaiba Ahmed Ally.

  Alisema kwamba wapo wanawake wanaoamini kuwa hawawezi kuendelea hadi wawezeshwe, jambo linalohitaji kupingwa vikali ili wanawake waweze kupiga hatua kiuchumi na kujikomboa wao wenyewe.
  Mmiliki wa duka la nguo za maharusi lililopo mtaa wa Livingstone na Mkunguni, Bi Twaiba Ahmed Ally, katikati akikata keki ya uzinduzi wa duka hilo jana. Kulia ni mwimbaji wa taarabu nchini, Khadija Kopa akilishwa keki kama mgeni rasmi. Kushoto ni mtangazaji wa kipindi cha Ng'ari Ng'ari kutoka Clouds Tv, Sakina Lyoka.
  Twaiba akimlisha keki Khadija Kopa katika tukio la uzinduzi huo jana.
  Bi Twaiba akimlisha keki Sakina Lyoka jana.
  Bi Sakika Lyoka akimlisha keki mmiliki wa duka hilo, bi Twaiba Ahmed. Kushoto ni Khadija Kopa.
  “Naomba wanawake tuache dhana kuwa hatuwezi kuendelea hadi tuwezeshwe na wanaume, ukizingatia kuwa Dunia imebadilika na wapo wenzetu wanaofanya kazi nzuri kiasi cha kutufanya tuige nyendo zao ili tusonge mbele, akiwamo Bi Twaiba Ahmed,” Alisema Kopa.

  Akizungumzia hilo, Bi Twaiba alisema ni jukumu lao kuhakikisha kwamba wanawake wanasonga mbele kiuchumi, akisisitiza namna ya ujihusishaji na masuala yote ya ujasiriamali na kazi nyingine.


  “Nashukuru kwa sapoti kubwa ninayoipata, akiwamo Bi Khadija Kopa, hivyo nitaendelea kufanya juhudi ili nizidi kupiga hatua kubwa kibiashara kwa kusimamia changamoto zote zinazonikabili. “Katika duka langu nafanya shughuli zote zinazomhusu mwanamke, wakiwamo wale wanaofunga ndoa kwa kuwapamba, kuwakodisha vifaa vya harusi bila kusahau wale wanaotaka kununua kwa fedha taslimu, ofisi yangu ikipatikana katika mtaa wa Mkunguni na Livingstone, Kariakoo, jijini Dar es Salaam,” Alisema.

  Mbali na kuuza vifaa vya maharusi na nguo za kawaida za wanawake, pia Twaiba anajihusisha na ufundishaji wa upambaji kwa wanawake, shughuli inayomfanya aheshimiwe na wengi wanaojihusisha na sekta hiyo ya mitindo na urembo.
  Baadhi ya nguo za maharusi zinavyoonekana katika duka la urembo na mitindo lililozinduliwa rasmi jana, huku mgeni rasmi akiwa ni mwimbaji wa muziki wa taarabu nchini Tanzania, Bi Khadija Kopa.

  0 0


  Na. Lilian Lundo - MAELEZO - Dodoma.


  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameziagiza Halmashauri, Manispaa na Majiji yote nchini kutenga maeneo kwa ajili ya watu kufanya mazoezi na kupumzika.

  Kassim Majaliwa ametoa agizo hilo leo, Mjini Dodoma katika uzinduzi wa Kitaifa wa mazoezi ya viungo kwa wananchi wote yaliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri.

  "Ni muhimu kufanya mazoezi kila siku, mazoezi yanasaidia kuchangamsha mwili, kufahamiana, kujenga urafiki pamoja na kuwa na afya bora," alifafanua Kassim Majaliwa. Aidha, Majaliwa amesema kwamba muitikio wa ufanyaji mazoezi ya viungo ni mkubwa, watu wengi wamejiunga na vikundi mbalimbali vya kufanya mazoezi ya viungo.

  Hivyo basi amezitaka Halmashauri, Manispaa na Majiji yote nchini kutenga maeneo kwa ajili ya watu kufanya mazoezi na kumpizika. Aidha, amesema kuwa, watu wasilazimishwe kufanya mazoezi bali iwe ni hiari ya mtu na kusiwe na gharama kwa ajili ya mtu kufanya mazoezi.

  Amewataka Maafisa Utamaduni na Michezo kuhamasisha mazoezi ya viungo katika maeneo yao pamoja na kuanzisha vikundi vya mazoezi ya viungo ambapo watakuwa wanakutana na kufanya mazoezi kwa muda ambao watajipangia.

  Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amemshukuru Makamu wa Rais Samia Suluhu kwa kuhamasisha mazoezi ya viungo na kuitangaza rasmi Jumamosi ya pili ya mwezi kuwa ni siku ya mazoezi ya viungo Kitaifa.

  Aliendelea kwa kusema kuwa mazoezi ya viungo yanamuepusha mtu na kupata magonjwa yasiyoambukiza kama vile magonjwa ya moyo, kisukari na saratani.

  Nae, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye amesema kuwa mazoezi ya viungo yanaratibiwa na Wizara ya Habari, Wizara ya Afya na TAMISEMI. Hivyo kwa pamoja watahamasisha uanzishwaji wa vikundi vya mazoezi ya viungo katika Halmashauri zote nchini kwa kuanza na watumishi wa Umma.

  Aidha, Nape amewataka viongozi wanapokuwa mikoani katika siku ya mazoezi ya viungo kuhamasisha mazoezi ya viungo kwa kufanya mazoezi na wananchi.

  Uzinduzi wa Kitaifa wa mazoezi ya viungo ulianza kwa matembezi yaliongozwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu kuanzia viwanja vya Bunge na baadae alimkabidhi Waziri Mkuu kuanzia Nyerere Square mpaka Uwanja wa Jamhuri. Uzinduzi huo umehusisha viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri, Wabunge, Viongozi wa Mkoa wa Dodoma na Wananchi wa Mkoa huo.

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk Julieth Magandi akikata utepe kuzindua sehemu ya kuchezea watoto wanaotibiwa Muhimbili. Dk Magandi amezindua sehemu ya kuchezea watoto kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Tiba Muhimbili, Dk Hedwiga Swai na mwakilishi wa Human Welfare Trust, Bi. Veena Jog.
  WATO 1
  Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk Julieth Magandi akizungumza kabla ya kuzindua sehemu ya watoto kuchezea. Kushoto ni Ofisa Mkuu Mtendaji wa Benki M, Anil Verma.

  WATO 2
  Baadhi ya wageni waliofika Muhimbili kushuhudia uzinduzi huo wakimsikiliza mgeni rasmi Dk Magandi.

  WATO 3
   Baadhi ya watoto, wauguzi, madaktari na wageni wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Dk Magandi leo.

  WATO 4
   Mwakilishi kutoka Human Welfare Trust, Bi. Veena Jog akizungumza kabla ya uzinduzi huo.
  WATO 5
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa hospitali hiyo, Aminiel Aligaesha akishiriki kuimba na watoto hao leo.

  WATO 6

  Watoto wakicheza baada ya sehemu ya kuchezea kuzinduliwa leo katika hospitali hiyo.
  ……………


  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto leo imezindua sehemu ya kuchezea watoto wanaolazwa  na wale wanaofika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili ya kupatiwa matibabu mbalimbali.

  Sehemu ya kuchezea watoto imezinduliwa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa hospitali hiyo, Dk Julieth Magandi kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Mpoki Ulisubisya.

  Akizindua sehemu ya kuchezea watoto, Dk Magandi amesema kuwapo kwa sehemu ya kuchezea kutaongeza chachu ya watoto kuacha kuogopa hospitali kwani watavutiwa na kutambua kwamba wapo katika mazingira salama na rafiki wakati wakipatiwa huduma za matibabu.

  “Nawapongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili licha ya kufungua sehemu hii ya michezo leo bado ndani ya jengo mmeweka vivutio vingi kwenye kuta zote za jengo la watoto ili kuhakikisha watoto wanafurahi,” amesema Dk Magandi.

  Dk Magandi amesema kuwa sehemu hiyo ya michezo ambako pamefungwa vifaa vya kisasa vya kuchezea itawasaidia watoto wanaokaa muda mrefu hospitalini kuanzia mwezi mmoja hadi mwaka mmoja kupata faraja.

   “Nina imani kuwa sehemu hii itawapa uhuru wa kucheza kwa nafasi na usalama zaidi ukilinganisha na hali ilivyokuwa awali.  Ni kweli ndani ya jengo  kuna michoro ya wanyama mbalimbali na katuni zinazotoa taswira rafiki kwa watoto na kuondoa mawazo ya kwamba hospitali ni sehemu ya maumivu muda wote, lakini kuongezeka kwa sehemu hii ya michezo itachochea zaidi hali ya watoto kupenda kutibiwa na kujisikia huru zaidi,” amesema.

  Pia, Dk Magandi amewashukuru Human Welfare Trust Fund kwa kujenga sehemu ya kuchezea watoto kwani wameonyesha wanawajali watoto wetu.

  Naye Mkurugenzi wa Tiba katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk Hedwiga Swai akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Museru amesema kwamba watoto wanaolazwa katika Jengo la Watoto ni wale wanaohitaji tiba za upasuaji, wenye majeraha ya moto, utapiamlo, matatizo ya moyo, wenye matatizo ya mishipa ya fahamu, figo, magonjwa ya tezi na kisukari, magonjwa ya mfumo wa damu, macho na watoto wanaohitaji ushauri wa lishe bora.

  “Sehemu hii ya michezo itatumika kwa watoto wanaokuja kliniki kwa ajili ya uchunguzi wa magonjwa mbalimbali, wale wanaofatiliwa maendeleo yao baada ya kupata nafuu na wale wanaopata ruhusa ya kurudi nyumbani na watoto waliolazwa wodini,” amesema Dk Swai.

  0 0

  Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini na Mbunge wa Simanjiro, Mhe.James Millya, wametembelea baadhi ya maduka yanayouza madini ya Tanzanite jijini Arusha ili kujionea shughuli za biashara na uongezaji thamani wa madini hayo zinavyofanyika. Ziara hiyo ni moja ya majukumu waliyopanga kuyafanya jijini Arusha, jukumu kuu likiwa ni kushuhudia jinsi Mnada wa Pili wa Kimataifa wa Madini ya Tanzanite unavyofanyika katika kituo cha Jemolojia jijini Arusha. 

  Moja ya duka lililotembelewa na Wabunge hao ni The Tanzanite Experience ambalo hujishughulisha na kukata Tanzanite ili kuiweka katika maumbo mbalimbali na kuing’arisha. Duka la The Tanzanite Experience pia hutoa elimu bure kwa wanafunzi na wageni mbalimbali kuhusu madini ya Tanzanite ikiwemo historia yake. 

  Ndani ya duka hilo pia kumejengwa mgodi wa mfano wa Tanzanite ambao hutumika kutoa elimu kwa wageni mbalimbali kuhusu shughuli za uchimbaji wa Tanzanite. 

  Baadhi ya Wajumbe waliofanya ziara hiyo ni pamoja na Mhe. John Heche, Mbunge wa Tarime Vijijini (CHADEMA), Mhe. Mwantakaje Juma Mbunge wa Bububu (CCM) na Mhe. Dunstan Kitandula Mbunge wa Mkinga (CCM). 
  Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. John Heche, Mbunge wa Tarime Vijijini (CHADEMA),(wa pili kulia), Mhe. Mwantakaje Juma Mbunge wa Bububu (CCM) (wa pili kushoto) na Mbunge wa Simanjiro, Mhe. James Millya (wa kwanza kulia) wakiwa ndani ya Mgodi wa mfano wa Tanzanite uliopo ndani ya duka la The Tanzanite Experience jijini Arusha. Mgodi huo hutumika kutoa elimu kwa wageni mbalimbali kuhusu shughuli za uchimbaji wa Tanzanite. Wa kwanza kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Madini, Kanda ya Kaskazini, Adam Juma.
  Mbunge wa Simanjiro, Mhe. James Millya (wa nne kulia) na Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Dunstan Kitandula, Mbunge wa Mkinga (CCM), (wa pili kulia), Mhe. Mwantakaje Juma Mbunge wa Bububu (CCM) (wa Tatu kulia) na wakipata maelezo kuhusu biashara ya Tanzanite ndani ya duka la The Tanzanite Experience jijini Arusha. Anayetoa maelezo ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Hasnain Sajan. Wa kwanza kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Madini, Kanda ya Kaskazini, Adam Juma.
  Mbunge wa Simanjiro, Mhe. James Millya (wa nne kulia) na Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. John Heche, Mbunge wa Tarime Vijijini (CHADEMA),(wa pili kulia), Mhe. Dunstan Kitandula, Mbunge wa Mkinga (CCM), (wa tatu kulia), Mhe. Mwantakaje Juma Mbunge wa Bububu (CCM) (wa kwanza kulia), wakiwa ndani ya duka la The Tanzanite Experience jijini Arusha ili kupata maelezo kuhusu biashara ya Tanzanite na shughuli za uongezaji thamani madini hayo. Wengine katika picha ni Afisa Madini Mkazi Merelani, Mhandisi Elias Mutelani (wa tano kulia) na wa Sita kulia ni Kamishna Msaidizi wa Madini, Kanda ya Kaskazini, Adam Juma.

  0 0


  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akitoa salam za rambirambi zake binafsi, CCM na za Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli wakati wa mazishi hayo.mara baada ya kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Katibu wa Hamasa wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu mkoa wa Kilimanjarona Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, Edwin Mselle, wakati wa ibada na kuaga mwili, wakati wa mazishi, yaliyofanyika leo Wilayani Kibosho, mkoani Kilimanjaro. Edwin ambaye pia alikuwa mwanafunzi wa udaktari, mwaka wa nne katika Chuo Kikuu Kishiriki cha KCMC, ni miongoni mwa viongozi wanne wa CCM waliofariki kwa ajali ya gari, wakati waitoka kwenye maadhimisho ya miaka 40 ya CCM, Februari 5, 2017 ambapo Kinana ameongoza kwenye mazishi yao wote. 

  Taratibu zikifanywa na Padre kabla ya kuingiza jeneza kaburini 


  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiweka udongo kaburini  

  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadick akimwaga udongo kaburini wakati wa maziko

  Kinana akikabidhi rambirambi kutoka CCM na Jumuia zake kwa Baba wa Marehemu Edwin, Christopher Mselle wakati wa mazishi hayo


  Kinana akimpa pole Padre Dackshen Hangai wakati wa mazsihi hayo.
  Vijana wa UVCCM wakiwa wamebeba jeneza kwenda eneola maziko, wakati wa mazishi hayo
  Vijana wa UVCCM wakiwasili na jeneleza lenye mwili wa marehemu katika eneo la maziko
  Kinana akiwasili eneo la maziko wakati wa mazishi hayo
  Huyu kuku naye alihudhuria mazihi hayo, na wengi kutafsiri kwamba, Marehemu amezikwa kwa baraka sana
  Padre akisoma maandiko matakatifu ya biblia kabla ya mwili kuingizwa kaburini

  Jeneza lenye mwili wa marehemu likiingizwa kaburini
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiweka udongo kaburini
  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadick akimwaga udongo kaburini wakati wa maziko
  Baba na Mama wa marehemu wakiweka udogo kaburini. TAFADHALI ENDELEA KUTAZAMA PICHA ZAIDI ZA MSIBA HUU. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Katibu wa Hamasa wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu mkoa wa Kilimanjarona Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, Edwin Mselle, wakati wa ibada na kuaga mwili, wakati wa mazishi, yaliyofanyika leo Wilayani Kibosho, mkoani Kilimanjaro. Edwin ambaye pia alikuwa mwanafunzi wa udaktari, mwaka wa nne katika Chuo Kikuu Kishiriki cha KCMC, ni miongoni mwa viongozi wanne wa CCM waliofariki kwa ajali ya gari, wakati waitoka kwenye maadhimisho ya miaka 40 ya CCM, Februari 5, 2017 ambapo Kinana ameongoza kwenye mazishi yao wote.
  Mkuu wa mkoawa Kilimanjaro Said Mecky Sadick akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Katibu wa Hamasa wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu mkoa wa Kilimanjarona Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, Edwin Mselle, wakati wa ibada na kuaga mwili, wakati wa mazishi, yaliyofanyika leo.


  Marehemu Edwin Mselle enzi za uhai wake


  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Saidi Mecky Sadick kwenye mazishi hayo


  Waombolezaji


  waombolezaji
  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisaliiana na Paroko wa Kanisa Katoliki Mwika, Emmanuel tumaini wakati wa mazishi hayo
  Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana akia na viongozi na waombolezaji wengie kwenye mazishi hayo


  Upande wa wa Ndugu wa Marehemu wakiwa kwenye mazishi hayo


  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahma Kinana akiwa amesimama na viongozi na waombolezaji wengine wakati wa ibada ya kuomea marehemu wakati wa mazishi hayo
  Wanakwaya wakiimba nyimbo za maombolezo kwenye mazishi hayo


  Ibada ya kuombea marehemu ikifanyika wakati wa mazishi hayo


  Waombolezaji


  Waombolezaji


  Muombolezaji


  Waombolezaji wakilachakula

  0 0

  Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akipata maelezo ya matumizi ya huduma za uzazi wa mpango kutoka kwa mhamasishaji wa Shirika la Engender Health Joyce Ishengoma alipotembelea banda la maonyesho wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha huduma hiyo iliyofanyika kijiji cha Mkwajuni Wilaya Kaskazini A.
  Mwakilishi wa Shirika la Engender Health Dkt. Martha Kisanga akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Kaskazini A wakati wa uzinduzi wa kampeni maalumu ya uhamasishaji wa uzazi wa mpango katika kijiji cha Mkwajuni.
  Wananchi waliojitokeza katika uzinduzi wa kampeni maalum ya uzazi wa mpango wakifuatilia uzinduzi huo uliofanyika Mkwajuni Wilaya ya Kaskazini A Unguja.
  Baadhi ya watoto walioshiriki uzinduzi wa kampeni maalum ya kuwahamasisha wazazi wao kujiunga na uzazi wa mpango wakifuatilia uzinduzi huo uliofanyika kijiji cha Mkwajuni.
  Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na wananchi na wageni waalikwa katika uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji uzazi wa mpango uliofanyika Mkwajuni Wilaya ya Kasakazi A Unguja.
  Picha na Makame Mshenga-Maelezo  Na Ramadhani Ali/Maelezo 

  Zaidi ya akinamama 236 kati ya laki moja wanaofika hospitali na vituo vya afya kujifungua Zanzibar wanafariki kila mwaka kutokana na sababu mbali mbali zikiwemo kuacha kutumia huduma za uzazi wa mpango.

  Kutokana na tatizo hilo Wizara ya Afya imeanzisha kampeni maalum ya wiki moja ya kuwahamasisha akina mama na akinababa kujiunga na uzazi wa mpango katika juhudi za kuokoa maisha ya wazazi na watoto.

  Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo alizindua kampeni hiyo katika kijiji cha Mkwajuni Wilaya ya Kaskazini ‘A’ na kuwashauri akinababa kuwaruhusu wake zao kujiunga na uzazi wa mpango .

  Alisema hidi sasa wanawake wanaostahiki kujiunga na uzazi wa mpango Zanzibar ni asilimia 14 tu waliojiunga na juhudi inatakiwa ifanywe ili iweze kufikia asilimia 20 ifikapo mwaka 2020 ili kulinda afya ya mama na mtoto.

  Waziri Mahmoud alisema idadi ya akinamama wanaofariki ni kubwa zaidi ya takwimu zilizopo kwani wanaojifungulia hospitali ni asilimia hamsini tu na asilimia iliyobaki wanajifungulia majumbani na hakuna takwimu zao. 

  Aliongeza kuwa Serikali imefanya juhudi kubwa za kusambaza huduma za uzazi wa mpango katika vituo vyote vya afya mijini na vijijini ili kuwaondoshea usumbufu wananchi hivyo amewashauri kuvitumia.

  Akizungumzia vifo vya watoto chini ya miaka mitano, Waziri wa Afya alisema bado ni tatizo kubwa Zanzibar watoto 56 kati ya 1000 wanaozaliwa wakiwa hao hufariki dunia.Alisema sababu kubwa ya vifo hivyo inatokana na wazazi kucheleweshwa kupelekwa hospitali ama kutopelekwa kabisa na kupelekea kujifungua katika mazingira yasiyo salama.

  Kutokana na matatizo mengi yanayowapata akinamama wajawazito na watoto wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua, Waziri Mahmoud Thabit Kombo ameagiza kuundwa Kamati ya kitaifa itakayowashirikisha viongozi kutoka kada mbali mbali na washirika wa maendeleo kukabiliana nalo.

  Mwakilishi wa Shirika la Engender Health Dkt. Martha Kisanga alisema ushiriki mdogo wa akinababa katika huduma ya uzazi wa mpango unachangia wanawake wengi kutojiunga na huduma hizo.

  Katika risala ya wananchi wa Wilaya Kaskazini A iliyosomwa na Tatu Khamis Kombo walisema pamoja na vituo vingi vya afya kutoa huduma za uzazi wa mpango, mwamko bado ni mdogo na kufanyika kwa kampeni hiyo katika wilaya yao itasaidia wananchi wengi kujiunga.

  Wilaya Kaskazini A na Wilaya ya Micheweni Pemba ndizo zenye asilimia ndogo zaidi ya akinamama waliojiunga na huduma ya uzazi wa mpango Zanzibar.


  IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR

  0 0  0 0

  Hapa ni katika viwanja vya Ofisi ya Mtendaji Kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga ambapo leo Jumamosi Februari 11,2017 Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amekabidhi vifaa tiba kwa mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kuvisambaza katika zanahati na hospitali zilizopo katika manispaa hiyo.
   
  Vifaa tiba hivyo vimetolewa na Watanzania waishi nchini Denmark ambapo upatikanaji wa vifaa hivyo unatokana ushirikiano wa Diwani wa kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi (CHADEMA) na shirika la AGAPE la Mjini Shinyanga kuwasiliana Watanzania waishio nchini Denmark kisha kuleta vifaa hivyo.
  Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo,Mkurugenzi wa shirika la AGPAE John Myola alisema wazo la kutafuta vifaa tiba lilitolewa na diwani wa kata ya Ngokolo Diwani Emmanuel Ntobi ambaye anajuana na watanzania waishio nchini Denmark.
  “Diwani huyu alitupatia mawasiliano ya watu hao wanaojulikana Denish Relief Group kisha sisi kama shiriki tukaandika andiko tukiomba kupewa vifaa tiba kwa ajili ya kupunguza uhaba wa vifaa tiba katika zahanati na hospitali za manispaa ya Shinyanga”,alisema Myola.
  Myola alitumia fursa hiyo kuiomba ofisi ya mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga kuhakikisha kuwa vifaa tiba hivyo vinatumika kama inavyotakiwa na kuhakikisha vinatunzwa.
  Naye Diwani wa kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi alisema watanzania waishio Denmark wametoa vifaa tiba hivyo bure kwa ajili ya watanzania huku akiishukuru serikali kuruhusu vifaa hivyo kuingia nchini bila kulipiwa kodi.
  “Hili jambo la kidiplomasia kwa nchi hizi mbili Tanzaia na Denmark,Denish Relief Group ni kundi la watu la kwanza kutoa msaada mkubwa nchini,huu ni kama mwanzo tu,wamesema wataendelea kutoa msaada na wamesema wapo tayari kutujengea zahanati katika kata hii ya Ngokolo ambayo haina zahanati”,alisema Ntobi.
  “Tumepokea vifaa tiba aina 26,vimo vitanda,magodoro,viti vya kisasa vya wagonjwa,mashine ya Utra sound,mashine ya Incubation na vifaa vingine vingi ambavyo vitatumika katika kutoa huduma za afya kwa wananchi wa manispaa ya Shinyanga”,aliongeza Ntobi.
  Hata hivyo diwani huyo aliomba vifaa hivyo vitumike vizuri na vitumike kwa wananchi wenye kipato cha hali ya chini.Alisema pamoja na kutoa vifaa tiba,pia watanzania hao waishio nchini Denmark wametoa baiskeli kwa watu wenye ulemavu na nguo kwa makundi ya watu wasiojiweza wakiwemo wazee wanaolelewa katika kituo cha Kolandoto kilichopo katika manispaa ya Shinyanga.
  Kwa upande wake mgeni rasmi katika makabidhiano hayo,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro alipongeza jitihada zilizofanywa na shirika la AGAPE na diwani wa kata ya Ngokolo katika kupatikana kwa vifaa hivyo.
  “Hili ni tukio kubwa na la busara sana,limetutia moyo ,nawapongeza sana watanzania waishio Denmark na wote mliofanikisha kupatikana kwa vifaa hivi ambavyo vitakuwa msaada mkubwa kwa wananchi,huu siyo muda wa kufanya siasa,kinachotakiwa ni kuwaletea maendeleo wananchi bila kujali itikadi za kichama”,alieleza Matiro.
  “Katika suala la maendeleo,serikali ipo tayari kushirikiana na shirika,kundi lolote la watu na hata mtu binafsi,tusitumie majukwaa ya maendeleo kufanya siasa,nimpongeze diwani wa kata hii kwa ushirikiano aliotuonesha katika kuwasaidia wananchi”,aliongeza Matiro.
  Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo wakati wa makabidhiano hayo ametuletea picha 30 za matukio..Tazama hapa chini
  Vifaa tiba vilivyotolewa na watanzania waishio nchini Denmark kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma za afya katika zahanati na hospitali zilizopo katika manispaa ya Shinyanga
  Vifaa vya kufanyia mazoezi na viti vya kubebea wagonjwa
  Vifaa tiba mbalimbali ikiwemo magongo,viti vya kuogea 
  Vifaa tiba vikiwa katika viwanja vya ofisi ya Afisa mtendaji kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga
  Baiskeli za wagonjwa na vifaa tiba vingine vya kisasa
  Vitanda vya wagonjwa 
  Vitanda vikiwa na magodoro yake
  Afisa Mtendaji wa kata ya Ngokolo William Ndila akitambulisha wageni mbalimbali waliohudhuria hafla fupi ya kukabidhi vifaa tiba vilivyotolewa na watanzania waishio nchini Denmark "Denish Relief Group" kutokana na jitihada zilizofanywa na diwani wa kata hiyo Emmanuel Ntobi na Shirika la AGAPE
  Mkurugenzi wa shirika la AGAPE la Mjini Shinyanga John Myola akizungumza katika hafla hiyo
  Wananchi wakiwa eneo la tukio
  Aliyesimama ni Mkurugenzi wa shirika la AGAPE la Mjini Shinyanga John Myola akielezea namna vifaa tiba vilipatikana kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma za afya kwa wananchi wa manispaa ya Shinyanga
  Diwani wa kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga Emmanuel Ntobi(Chadema) akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba hivyo.Kushoto ni diwani wa viti maalum Zainab Heri (Chadema).Kulia ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro
  Wananchi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
  Diwani wa kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga Emmanuel Ntobi(Chadema) aliwashukuru viongozi wa serikali kwa kuruhusu vifaa tiba hivyo kuingia nchini bila kodi huku akiomba serikali kuwapatia eneo kwa ajili ya kujenga zahanati katika kata hiyo ambayo haina zahanati kutokana na kushindwa kujenga baada ya kuibuka mgogoro kwenye eneo ambapo kulitakiwa pajenge zahanati 
  Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Magendi Magenzi ambaye ni afisa utumishi wa manispaa hiyo,akizungumza katika hafla hiyo ambapo kwa namna ya pekee alimpongeza diwani wa kata ya Ngokolo kwa jitihada alizofanya katika upatikanaji wa vifaa tiba hivyo.
  Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Ngokolo John Nangi akizungumza wakati wa hafla hiyo
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa hafla hiyo ambapo alisema serikali inaunga mkono jitihada zinazofanywa na wadau mbalimbali katika kuwaletea maendeleo wananchi
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza katika hafla hiyo
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisisitiza umuhimu wa kuendeleza siasa kwenye masuala ya maendeleo
  Diwani wa kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi akimwonesha mkuu wa wilaya vifaa tiba hivyo ikiwemo vifaa vya kubebea watoto na vifaa vya kufanyia mazoezi
  Diwani wa kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi akiendelea kumwonesha mkuu wa wilaya ya Shinyanga vifaa tiba,pichani ni meza za kulia chakula na kabati
  Diwani wa kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi akionesha vifaa tiba
  Diwani wa kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi akiwa ameshikilia fimbo za watu wasioona
  Baada ya kukabidhi baiskeli kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa viungo,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akishikana mkono na Richard ambaye ni mlemavu wa viungo.
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisalimiana na kijana mwenye ulemavu wa viungo baada ya kumkabidhi baiskeli
  Wananchi wenye ulemavu wa viungo wakiwa wamekaa kwenye baiskeli
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na mkurugenzi wa shirika la AGAPE John Myola wakiwasindikiza wananchi wenye ulemavu wa viungo baada ya kuwapatia baiskeli hizo.Baiskeli hizo zinaendelea kutolewa kwa wananchi mbalimbali wenye ulemavu wa viungo
  Mashine ya Utra Sound ambayo pia imetolewa na watanzania waishio Denmark 
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza baada ya kuona mashine mbili Utra Sound kwa ajili ya akina mama wajawazito na Mashine ya kukuzia watoto njiti
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza baada ya kuona mashine za kisasa za kutolea huduma za afya
  Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

  0 0

   

  Kongamano hilo limefanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga na kuhudhuriwa na wanafunzi wa vyuo mbalimbali mkoani Shinyanga,viongozi wa vyuo na dini,wanakwaya,wanafunzi wa shule za sekondari na watu mbalimbali wenye mapenzi mema.
  Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.
  Kongamano hilo ambalo ni la kwanza kufanyika mkoani Shinyanga limetokea baada ya Mtumishi wa Mungu Happiness Mwaja Kihama kutamani kuwepo kwa kongamano ndipo wanafunzi kwa pamoja wakakubali kuunganisha nguvu hatimaye kufanikisha kufanyika kwa kongamano hilo.
  Miongoni mwa malengo ya Kongamano hilo lenye kauli mbiu ya “Kumcha Bwana ni Chanzo cha Maarifa –Mithali 1:7”ni kuwaleta pamoja wanafunzi na kuwafanya wafahamiane,kuunganisha nguvu katika kumuomba mungu kwa ajili ya kuendelea ustawi wa kielimu katika mkoa wa Shinyanga.
  Pamoja na kuuombea mkoa wa Shinyanga kielimu,kongamano hilo pia lililenga kuwaombea wanafunzi ili mungu awasaidie kufanya vizuri katika masomo yao sambamba na kuwajengea uwezo vijana uwezo wa kumjua mungu na kusababisha hofu ya mungu ndani yao ili kuisadia serikali katika kupunguza vitendo viovu katika jamii.
  Wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali mkoani Shinyanga ikiweo Shycom,Mocu ,wakiwa ukumbini wakati wa kongamano Maalum la Maombi kwa wanavyuo
  Mchungaji Goodluck Mosha akizungumza wakati wa Kongamano hilo ambapo alisema ni mara ya kwanza kufanyika mkoani Shinyanga.Mchungaji Mosha aliwasisitiza vijana hao kumtanguliza Mungu katika maisha yao 
  Shija Simon akisoma risala ambapo alisema wameamua kukutana pamoja ili kuunganisha nguvu ya pamoja katika kumuomba mungu kwani wanaamini kuwa maomi hayo yatasababisha mabadiliko ya kielimu mkoani Shinyanga kwani ukilinganisha na mikoa mingine mkoa wa Shinyanga bado upo chini kielimu 
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na mchungaji Emmanuel Mboje wakiwa ukumbini wakati wa kongamano hilo 
  Mwalimu wa Injili/Mwinjilisti Happiness Mwaja Kihama ambaye ni mlezi wa wanafunzi walioandaa kongamano hilo akizungumza ukumbini jinsi alivyopata maono na kuamua kuhamasisha wanafunzi wa vyuo mkoani Shinyanga kupitia kwa wakuu wa wakuu wa vyuo kuungana ili kufanikisha kongamano hilo 
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimsikiliza kwa makini mwalimu wa Injili Happiness Mwaja Kihama 
  Mwalimu wa Injili/Mwinjilisti Happiness Mwaja Kihama alisema lengo la kongamano hilo ni kutengeneza umoja wa wanavyuo mkoani Shinyanga,kuomba kwa ajili ya elimu mkoani humo na kuwaombea wanafunzi wote mkoani Shinyanga 
  Mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akitoa somo kuhusu "Funguo za Kiagano za Kupata Majibu ya Maombi yetu"
  Wanafunzi wa vyuo wakiwa ukumbini
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiendelea kutoa somo ambapo aliwataka wanafunzi kumtegemea mungu ili kufanikiwa katika masomo na maisha yao 
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro aliwapongeza wanafunzi hao kuungana pamoja kuuombea mkoa wa Shinyanga kwani yatasababisha wawe na hofu ya mungu ili kusaidia kupunguza vitendo vya uovu katika jamii
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro aliwasisitiza wanafunzi hao kujitahidi kusoma na kuachana na tamaa zisizofaa 
  Mchungaji Goodluck Mosha akiomba ukumbini wakati wa kongamano maalum la maombi kwa wanafunzi wa vyuo mkoani Shinyanga 
  Wanakwaya ya Haleluya kuu ya Ndala katika manispaa ya Shinyanga wakicheza ukumbini 
  Uimbaji unaendelea
  Wanachuo wakiimba na kucheza 
  Vijana wakicheza
  Kijana Gabriel akiimba 
  Vijana wakimwimbia bwana 
  Uimbaji unaendelea
  Wanavyuo wakiwa ukumbini
  Tunafuatilia kinachoendelea ukumbini
  Wanachuo wakiwa ukumbini
  Kongamano linaendelea
  Wanachuo wakiimba ukumbini 
  Vijana wa TYCS wakiimba ukumbini 
  Washiriki wa kongamano hilo wakicheza ukumbini 
  Kongamano linaendelea 
  Tunafuatilia kinachoendelea 
  Mwalimu wa Injili Happiness Mwaja Kihama akiongoza maombi kuuombea mkoa wa Shinyanga kielimu kwani hali ya kitaaluma ipo chini ukilinganisha na mikoa mingine 
  Wanafunzi wakiwa wamenyoosha mikono wakati wa maombi 
  Washiriki wa kongamano wakiwa wamenyoosha mikono 
  Mwalimu wa Injili Happiness Mwaja Kihama akiomba wakati wa kongamano hilo la maombi maalum kwa wanafunzi wa vyuo vya mkoa wa Shinyanga 
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro(kulia) akiwa katika maombi 
  Maombi yanaendelea 
  Wanafunzi wakiwa katika maombi 
  Maombi yanaendelea 
  Maombi yanaendelea 
  Maombi yakiwa yamekolea kuombea mkoa wa Shinyanga 
  Watumishi wa mungu wakiwa katika maombi 
  Mwalimu wa Injili Happiness Mwaja Kihama akiendelea kuomba 
  Maombi yanaendelea 
  Maombi yakiendelea 
  Mwalimu wa Injili Happiness Mwaja Kihama akiombea wanafunzi wa vyuo na wanafunzi wa shule za sekondari waliohudhuria kongamano hilo 
  Maombi yanaendelea 
  Wanachuo wakiendelea kumsifu bwana Yesu kwa nyimbo 
  Kulia ni mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Kongamano hilo Jepherson Jackson akizungumza wakati wa kufunga kongamano hilo ambapo aliwashukuru watu wote waliofanikisha kongamano hilo na kuongeza kuwa wataendelea kushirikiana na mlezi wao Happiness Mwaja Kihama ili kuandaa kongamano jingine
  Mchungaji Emmanuel Mboje akizungumza wakati wa kufunga kongamano hilo ambapo aliwataka wanafunzi hao kupendana na kuhakikisha wanakwenda kusali na kumuomba mungu 
  Picha ya pamoja mgeni rasmi na kamati iliyofanikisha kongamano hilo 
  Kamati iliyofanikisha kongamano hilo ikiongozwa na mwalimu wa Injili Happiness Mwaja Kihama ambaye pia ni mkurugenzi wa EasyFlex Production wakiwa katika picha ya pamoja baada kumalizika kwa kongamano hilo.
  Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

older | 1 | .... | 1136 | 1137 | (Page 1138) | 1139 | 1140 | .... | 1897 | newer