Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1135 | 1136 | (Page 1137) | 1138 | 1139 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akizungumza na Wafanyakazi wa Wizara yake wa Fungu 51 kuhusu masuala mbalimbali ya kiutendaji. Kikao hicho ambacho kinafanyika mara mbili kwa mwaka kimeandaliwa na Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE), (hawapo pichani). Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi  Simba Yahya na Mwenyekiti wa chama hicho, William Mkombozi. 
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya, akizungumza na Wafanyakazi wa Wizara yake wa Fungu 51 kuhusu masuala mbalimbali ya kiutendaji. Kikao hicho ambacho kinafanyika mara mbili kwa mwaka kimeandaliwa na Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE), (hawapo pichani). Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira.
   Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE), Tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, William Mkombozi akizungumza na Wafanyakazi wenzake wa tawi hilo (hawapo pichani), wakati wa mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya.
   Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa akijibu baadhi ya hoja zilizoelekezwa kwenye idara yake wakati wa mkutano wa Wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE), katika mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam.
  Mjumbe  wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE), Tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwanaidi Shabaani akiuliza swali kwa Katibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (hayupo pichani), wakati wa mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO
  SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.


  0 0


  0 0


  0 0

   Mkurugenzi kinga na elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Fadhil Mohammed Abdalla akizungumza na wandishi wa Habari kuhusu kampeni ya wiki moja ya kuhamasisha utumiaji wa huduma za uzazi wa mpango itakayoanza kesho tarehe 11 Kivunge Mkoa Kaskazini “A” Unguja, (kushoto) Afisa muhamasishaji kitengo shirikishi Afya ya Uzazi na Mtoto Wizara ya Afya Zanzibar Kasim Issa Kirobo.
   Wandishi wa Habari kutoka vyombo tofauti wakisikiliza tarifa juu ya kampeni ya wiki moja ya kuhamasisha utumiaji wa huduma za uzazi wa mpango zitakayoanza kesho tarehe 11 Kivunge Mkoa Kaskazini “A” Unguja.
  Mwandishi wa habari Mariyam Ame Chum kutoka ZBC TV akiuliza swali kwa Mkurugenzi kinga na elimu ya Afya Zanzibar Dkt. Fadhil (hayupo pichani) kuhusu dawa za uzazi wa mpango na athari zake katika Mkutano uliofanyika Wizara ya Afya Zanzibar. Picha na Makame Mshenga.

  0 0

  Benny Mwaipaja-WFM, Dodoma.

  WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amezitaka Kampuni kubwa na za kati kuchangamkia fursa ya uwepo wa Sekta ya Soko la Mipaji, kwa kujiorodhesha katika soko la hisa la Dar es salaam ili kushiriki moja kwa moja katika umiliki wa uchumi wa nchi.

  Dkt. Mpango ametoa rai hiyo Bungeni Mjini Dodoma, wakati akijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Jimbo la Magomeni, Mhe. Jamal Kassim Ali, aliyetaka kujua mchango wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) na Soko la Hisa la Dar es saam (DSE), kwa wafanyabiashara wazawa.

  Alifafanua kuwa kampuni kadhaa, ikiwemo Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), TOL Gases, Kiwanda cha Sigara (TCC), Kiwanda cha Saruji Tanga, Wakala wa Huduma za Mizigo kwenye viwanja vya ndege-Swissport na Benki ya NMB, ni baadhi ya kampuni zinazouza hisa zake katika Soko la Hisa la Dar es salaam.

  Dkt. Mpango alisema kuwa kampuni hizo zimechangia kukuza uchumi wa nchi ikiwemo ajira, kutoa gawiwo kwa Serikali na wanahisa, lakini pia ni miongoni mwa walipa kodi wakubwa.

  “Kwa mfano kwa mwaka 2015 NMB, ilitoa gawiwo Serikalini kiasi cha shilingi bilioni 16.5 na TCC shilingi billion 1.4 kwa hisa zinazomilikiwa na Serikali huku mapato yatokanayo na kodi pamoja na gawiwo, hutumiwa katika kutoa huduma mbalimbali ambazo jamii ikijumuisha wafanyabiashara wadogo hunufaika nazo”alisema Dkt. Mpango

  “Vilevile, Serikali imekuwa ikitumia masoko ya mitaji kama chanzo cha upatikanaji wa fedha za bajeti (Treasury Bonds), Miradi inayotekelezwa na fedha hizi, pamoja na mambo mengine, imekuwa ikitoa ajira na fursa za kibiashara kwa wafanyabiashara wazawa; wadogo na wa kati” aliongeza Dkt. Mpango

  Dkt. Mpango, alibainisha kuwa Serikali inatambua mchango mkubwa wa kampuni ndogo ndogo katika kukuza uchumi wa nchi ndio maana mwaka 2013 Soko la Hisa la Dar es Salaam lilianzisha dirisha linaloziwezesha kampuni ndogo na za kati za wazawa zisizokidhi vigezo vya kujiunga na soko hilo kupitia dirisha kuu, kutumia Soko la Hisa katika kupata mitaji kutoka kwa umma wa watanzania.

  Dkt. Mpango alibainisha kuwa watanzania wengi wananufaika na uwepo wa soko la hisa, na kushiriki moja kwa moja katika umiliki wa uchumi wa nchi huku akizitaja baadhi ya kampuni zilizonufaika na utaratibu huo wa dirisha dogo la hisa  kuwa ni Benki ya Mwalimu Commercial Bank, Swala Oil and Gas Tanzania, Maendeleo Bank PLC, Yetu Microfinance na Mkombozi Commercial Bank, ambazo zina jumla ya mitaji isiyopungua shilingi bilioni 120.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha Mhe Alexzender Mnyeti akisaini kitabu cha maombolezo kijijini Misasi
   Dc Mnyeti, MD Kayombo na familia nzima ya Mzee Kayombo walipotembelea kaburi la Mzee Kayombo
   Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Alexzender Mnyeti (Kushoto), na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo wakiwa katika mazungumzo
   Dc Mnyeti akitoa salamu za pole kwa familia ya Marehemu Mzee Kayombo
   Wakati wa sala kwenye kaburi la Marehemu Mzee Kayombo
   Maombi ni muhimu katika kila jambo

  Mazungumzo na Ndegu, jamaa na rafiki

  Na Mathias Canal, Mwanza

  Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha Mhe Alexzender Pastory Mnyeti amezuru kijiji cha Misasi, Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza kutoa pole kwa familia ya Marehemu Mzee Kayombo aliyefariki Dunia siku ya saa mbili usiku katika Hospitali ya Rufaa Bugando, Mkoani Mwanza.

  Mhe Mnyeti ametoa salamu za pole kwa wakazi wa Kijiji cha Misasi kwa kumpoteza mshauri katika kijiji hicho ambaye amekuwa nguzo kwa maendeleo ya kijiji sawia na utaratibu wake wa kuhamasisha wananchi kupanda miti ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

  Mnyeti ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Misungwi kabla ya uteuzi wake kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru ameeleza jinsi alivyomfahamu Mzee Kayombo katika kuhakikisha jamii inasonga mbele katika maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

  Mnyeti alisema kuwa Mkoa wa Mwanza umepoteza mtu muhimu ambaye pia atakumbukwa kwa kazi njema alizozifanya wakati wa uhai wake.

  Dc Mnyeti ametoa pole kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndugu John Lipesi Kayombo kwa kuondokewa na Mzee wake ambaye ni Mlezi wake tangu akiwa mdogo sambamba na kuisihi familia ya Marehemu Mzee Kayombo kuendeleza mshikamano na kupendana.

  Marehemu Mzee Kayombo atakumbukwa kwa mambo mbalimbali aliyoyafanya wakati wa uhai wake pindi alipokuwa kazini ikiwa ni pamoja na kupanda miti katika shule zote alizofundisha, Ujenzi wa shule wakati huo, pia atakumbukwa kwa kuhamasisha ujenzi wa Zahanati ya Misasi.

  Marehemu Mzee Antony Raphael Kayombo alifariki saa mbili usiku, siku ya Jumamosi ambapo hadi mauti inamkuta alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kibofu cha mkojo ambao ulianza ghafla tarehe 29/1/2017 na kupelekwa katika hospitali ya Misasi, Baadae hospitaliti ya Sekou Ture na mwishowe Hospitali ya Bugando ambapo alifanyiwa upasuaji ambapo hata hivyo hali yake iliendelea kudhoofika mpaka mauti ilipomkuta.

  INNALILAH WAINNAH ILAIHI RAJIUN

  0 0

    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa , Spika wa Bunge Job Ndugai (wapili kushoto) na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na  Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa wakibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa   Mtandao wa 4G LTE  wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Februari 10, 2017. Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi  Edwin Ngonyani, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Huawei Tanzania, Zhang Yongquan na kulia ni Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza wakati alipozindua mtandao wa 4G LTE wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Februari 10, 2017.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa , Spika wa Bunge Job Ndugai (wapili kushoto) na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na  Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa wakibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa   Mtandao wa 4G LTE  wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Februari 10, 2017. Kushoto ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi  Edwin Ngonyani na kulia ni Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai wakizungumza  kwa simu  ikiwa ni uzinduzi wa mtandao wa 4G LTE wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), kwenye  viwanja vya Bunge mjini Dodoma Februari 10, 2017.

     Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana  na Spika wa Bunge, Job Ndugai baada ya kuzindua Mtandao wa 4G LTE  kwenye viwanja vya Bunge Februari 10, 2017.

  Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amezitaka Taasisi zote za Umma ambazo zinadaiwa na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kuhakikisha zinalipa madeni yao kabla ya Juni 30, 2017.

  Waziri Mkuu ametoa rai hiyo leo, Mjini Dodoma katika viwanja vya Bunge wakati wa uzinduzi wa huduma ya 4G LTE za kampuni hiyo ya simu kwa Mkoa wa Dodoma.

  “Kuhusu shilingi Bil. 11.5 ambazo TTCL inazidai Taasisi mbalimbali za Umma, Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, kaa na wadaiwa sugu wote, thibitisheni madeni husika kisha mkubaliane namna ya kulipa madeni hayo. Nijuavyo kila Wizara inatenga bajeti kwa ajili ya ankara za simu, sasa hayo malimbikizo yanatoka wapi?” alisema Kassim Majaliwa.

  Aidha amezitaka Taasisi hizo zinazodaiwa na TTCL kuhakikisha zinakamilisha madeni yao kabla ya kufikia Juni 30, 2017 ili kampuni hiyo iweze kufanya kazi ipasavyo na kuendana na ushindani wa kibiashara uliopo.

  Pia, ameitaka kampuni hiyo kujifunza kutoka kwenye makampuni binafsi namna yanavyoendeshwa na kuiga baadhi ya mbinu zao, hususan katika kupunguza gharama za uendeshaji. 

  Kassim Majaliwa amesema kwamba, Serikali ina matarajio makubwa kutoka katika kampuni hiyo kutokana na kuwa na imani kwamba kampuni hiyo ina maarifa ya kujifunza kutoka kwa waliofanikiwa kwenye sekta hiyo.

  Vile vile ameitaka kampuni hiyo kujifunza kutoka katika mashirika ya Umma ya Simu kwenye nchi nyingine ambayo yanajiendesha kwa faida, kwa kuiga mbinu ambazo wanazitumia na kuziweka katika muktadha wa nchi ya Tanzania.

  Waziri Mkuu amempongeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa pamoja na timu yake kwa hatua ambayo kampuni hiyo imefikia. Aidha amemtaka Waziri huyo kufuatilia kwa karibu kampuni hiyo ili iweze kutoa ushindani wa kutosha kibiashara, ijiendeshe kwa faida, itoe gawiwo stahiki kwa Serikali, ilipe kodi na zaidi ya yote fedha za Umma zilizowekezwa ziweze kutumika vizuri.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma leo.
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipitia baadhi ya ajenda wakati  kikao cha Baraza la Mawaziri mjini Dodoma.
   Mawaziri wakijadiliana jambo kabla kikao cha Baraza la Mawaziri hakijaanza kutoka kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako, Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage.

  Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba(kushoto),Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (katikati) wakizungumza jambo na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango muda mfupi kabla ya kuanza kikao cha Baraza la Mawaziri mjini Dodoma.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akijadiliana jambo na Mawaziri wenzake muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha Baraza la Mawaziri mjini Dodoma.

  0 0

  Na Rhoda Ezekiel-Globu ya Jamii, Kigoma.

  JESHI la polisi Mkoani Kigoma  linamshikilia mtu Mmoja kwa kosa la kukutwa na vipande vitatu vya Pembe za ndovu  vyenye uzito wa kilo 15  vyenye thamani ya shilingi za kitanzania Milioni 500 akivisafirisha kutoka Katavi kuvileta kigoma kwa ajili ya kuviuza.

  Sambamba na tukio hilo jeshi la polisi linawashikilia Wahamiaji halamu 231, Bangi keye 220, mtambo Mmoja wa kutengenezea pombe ya moshi na watuhumiwa 10 wakiwa na  lita 217 , watuhjmiwa hao ni wauzaji na wapikaji kitendo ambacho ni kinyume na sheria za Nchi.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari jana ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa Wa Kigoma Naibu kamishina Wa Jeshi la polisi , Fredinandi Mtu alisema mnamo tarehe februali6 mwaka majira ya saa sita huko katika Kijiji Cha Kazuramimba Wilayani Uvinza Askari walipokea taarifa kuwa kuna wizi umetokea  Katika Gari ya Saratoga Iliyokuwa ikitokea Tabora kuja  Kigoma , askari Walifanya upekuzi na kukamata begi la abiria mmoja jina lake limehifadhiwa kwaajili ya upelelezi  likiwa na  vipande vitatu vya meno ya tembo.

  Kamanda Mtui alisema Upelelezi wa tukio hilo unaendelea ilikufahamu mahali mtuhumiwa alipotoa vipande hivyo vya meno ya tembo , Mtuhumiwa atafikishwa  mahakamani pindi upelelezi utakapo kamilika kwa hatua zaidi za kisheria.

  "Jeshi la polisi Mkoani Kigoma tunawaomba Wananchi Kuendelea kuunga Mkono jitihada za vita dhidi ya uhalifu kwa kutoa taarifa za watu wanao jihusisha na   vitendo hivyo ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao na kukomesha vitendo hivyo.

  Kwa upande wake Afisa Wanyamapori Wilaya ya Kigoma, Iddi Salumu alisema katika Mapori ya Kigoma hakuna pembe za ndivu za aina hiyo zilizo kamatwa vipande hivyo vinaweza kuwa vimetokea katika Mkoa Wa Katavi au katika hofadhi ya TANAPA ya Seruu .

  Alisema Kigoma Ndio njia kuu ya Kupitishoa mozigo hiyo na biashara kubwa inafanyikia Bchini Burundi , kwa Nchi ya Burundi biashara hiyo imeruhusiwa na majangiri wengi wanatumia Njia ya Mkoa Wa Kigoma kupitishia mizigo hiyo.

  Salumu alisema katika kuhakikisha biashara hiyo inadhibitiwa wameamua kuboresha Doria kwa kushirikiana na Jeshi la polisi na polisi waliopo Mipakani ilikuweza kudhibiti na kufanya ukaguzi wa mizigo yote inayopita kuelekea Nchini Burundi.

  0 0

   Kamishna wa Makao Makuu wa Tanzania Girl Guides Association (TGGA), Rosaldina Majuva alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya chama hicho wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam, kutoka kulia Kamishna Mkuu wa chama hicho Symphorosa Hangi na Katibu wa chama hicho, Grace Shaba.
  Katibu wa chama cha Tanzania Girl Guides Association (TGGA), Grace Shaba akifafanua kuhusu malengo ya chama hicho wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam, kulia ni  Kamishna Mkuu wa chama hicho Symphorosa Hangi, kushoto ni  Kamishna wa Makao Makuu wa chama hicho, Rosaldina Majuva.

  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
   Tanzania Girl Guides Association (TGGA) wanategemea kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa chama hicho kwa njia ya kufanya shughuli mbalimbali za kuisaidia jamii.

  Maadhimisho hayo yanayojulikana kama ‘thinking day’ yatafanyika Februari 22 mwaka huu ambapo shughuli za kuisaidia jamii zitaanza Februari 10 mwaka huu.

  Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Kamishna wa Makao Makuu wa Chama hicho, Rosaldina Majuva alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho hayo.

  Bi. Rosaldina amesema kuwa siku ya maadhimisho ya chama hicho inaambatana na siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa waasisi wao akiwemo Lord Baden Powell ambaye alikuwa kiongozi wa Boy Scout pamoja na Kamishna Mkuu wa Girl Guides na Girl Scouts, Lady Olave Baden Powell (mkewe).

  “Tumepanga kuadhimisha siku hii muhimu kwa kufanya shughuli za kijamii zikiwemo za kutoa misaada kwa wahitaji, kutunza mazingira kwa kufanya usafi katika eneo la Coco Beach na Magomeni na kupanda miti, kutoa elimu ya kujithamini, kujitambua na kukataza unyanyasaji pamoja na kutembelea kituo cha wazee wa Kigamboni,”alisema Bi. Rosaldina.

  Kwa upande wake Katibu wa chama hicho, Grace Shaba amefafanua kuwa chama hicho kimelenga kupanua uelewa wa wanawake kwa ujumla kuhusu uzalendo, majukumu ya nchi yao, kujenga ushirikiano wa kitaifa na kimataifa kupitia kambi za mafunzo, kutembelea na kuwasiliana kwa njia za teknohama pamoja na kuwa tayari kufanya kazi kwa manufaa yao na ya Taifa.

  “Dira yetu ni kuwa na jamii yenye wasichana na wanawake waliowezeshwa kufikia uwezo wa juu kabisa katika kutimiza malengo yao na kuwa rasilimali bora ya Taifa,”alisema Bi. Grace.

  Nae Kamishna Mkuu wa Tanzania Girl Guides Association, Symphorosa Hangi amesisitiza wanawake na watoto wa kike kujiunga na chama hicho kwani kinatoa elimu ya masuala ya kijamii na kiuchumi yatakayosaidia kuwainua wanawake na watoto pamoja na taifa kwa ujumla.

  Mpaka sasa kwa Tanzania,chama hicho kipo katika mikoa 22 kikiwa na jumla ya wanachama 101,824.

  0 0

   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akiwasisitiza watumishi wa umma nchini kutumia Tovuti ya Watumishi (Watumishi Portal)  alipokuwa akizindua Tovuti hiyo mkoani Dodoma leo.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) pamoja na Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Mhe. Mhandisi Stella Manyanya (Mb) wakifurahia uzinduzi wa Tovuti ya Watumishi (Watumishi Portal) mkoani Dodoma leo.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akifuatilia maelezo kuhusu Tovuti ya Watumishi (Watumishi Portal) baada ya kuizindua rasmi mkoani Dodoma leo. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Mhe. Mhandisi  Stella Manyanya (Mb) na kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura (Mb) na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Dkt. Laurean Ndumbaro.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na baadhi ya watumishi wa umma waliohudhuria uzinduzi wa Tovuti ya Watumishi (Watumishi Portal) mkoani Dodoma leo.
   Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro akitoa neno la utangulizi wakati wa uzinduzi wa Tovuti ya Watumishi (Watumishi Portal) mkoani Dodoma leo. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) na Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji Sera Ofisi ya Rais - UTUMISHI, Bw. Mathias Kabunduguru.
   Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) kuzungumza na watumishi waliohudhuria uzinduzi wa Tovuti ya Watumishi (Watumishi Portal) mkoani Dodoma leo.
   Baadhi ya watumishi wa umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (Hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Tovuti ya Watumishi (Watumishi Portal) mkoani Dodoma leo.
   Baadhi ya watumishi wa umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) (Hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Tovuti ya Watumishi (Watumishi Portal) mkoani Dodoma leo. 

  0 0

  Na Karama Kenyunko.

  Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Ephraim Mgawe amehukumiwa kulipa faini ya shilingi milioni tano au akishindwa atatumikia kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka.

  Hukumu hiyo imesomwa leo na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Cyprian Mkeha.

  Hata hivyo, mshtakiwa Mgawe alifanikiwa kulipa faini hiyo na kuwa huru.
  Mahakama pia imemuachia huru naibu wake aliyekuwa anashughulikia huduma, Hamad Koshuma baada ya upande wa mashtaka kushindwa kudhibitisha mashataka dhidi yake.

  Akisoma huku hiyo, hakimu Mkeha alisema, upande wa mashtaka kupitia ushahidi wa mashahidi watano uliowasilishwa mahakamani hapo umeweza kuthibitisha pasipo na shaka kuwa mshtakiwa Mgawe alitenda kosa hilo la matumizi mabaya ya madaraka.

  Alisema katika ushahidi inaonesha wazi kuwa mshtakiwa  Mgawe alisaini  mkataba huo wa kibiashara na Kampuni ya China Communications Construction Company Ltd (CCCC), kwa ajili ya kuifaidisha kampuni hiyo.

  Katika utetezi wake, Mgawe alisema kuwa, yeye hakuwahi kusaini mkataba wa kibiashara kwa ajili ya ujenzi wa gati bali alisaini mkataba kwa ajili ya kupata mkopo ambao alipata baraka kutoka katika bodi ya wakurugenzi wa mamlaka hiyo na kuwa kitendo hicho hakikuipaatia serikali hasara yoyote.
  Hakimu Mkeha alisema kuwa haiwezi kubishaniwa kuwa, Mgawe alisaini mkataba kati ya TPA na CCCC   Desemba 5, 2011.

  Aliongeza kuwa mkataba huo ulikuwa kwa ajili  ya matumizi ya huduma za uhandisi, manunuzi pamoja na  ujenzi wa gati 13 na 14 .Kwa upande wa mashtakiwa wa pili, Koshuma Hakimu Mkeha alimuachia huru akidai kuwa mtuhumiwa alikuwa akituhumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka ambayo hakuwa nayo.

  Katika ushahidi na vielelezo vilivyoletwa na mshtakiwa huyo inaonyesha kuwa aliteuliwa kuwa naibu Mkurugenze  Juni 1, 2012 huku upande wa mashtaka ukileta tuhuma kuwa mshtakiwa nae alisaini mkataba huo tarehe  Desemba 5, 2011.

  Aliwataka upande wa Jamuhuri kuhakikisha wanapeleleza  vya kutosha tuhuma zinazomkabili mtu  ili hata kama  ataachiwa na mahakama basi aachiwe kwa kuwa hana kosa siyo kwa mapungufu ya upelelezi.

  Awali ilidaiwa kuwa Desemba 5, mwaka 2011 Mgawe na mwenzake walitumia madaraka yao vibaya kwa kutoa zabuni ya upanuzi wa gati namba 13 na 14, katika Bandari ya Dar es Salaam, kwa Kampuni ya China Communications Construction Company Ltd (CCCC), bila kufuata taratibu za sheria ya manunuzi.

  Inadaiwa washitakiwa hao walitenda kosa hilo wakati wakitekeleza majukumu yao ya utumishi wa mamlaka hiyo kwa nafasi ya mkurugenzi mkuu na naibu wake.

  Aidha, katika hati ya mashtaka, watuhumiwa hao wanadaiwa kuweka saini mkataba wa kibiashara na kampuni hiyo ya kichina bila zabuni shindanishi, ambapo ni kinyume cha sheria ya manunuzi ya umma namba 21 ya 2004, ambapo walitumia dola za kimarekani milioni 600. 
   Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Ephraim Mgawe baada ya kukutwa na hatia ya kifungo ambacho kina faini sh.milioni tano ambapo ameweza kulipa faini hiyo na kuachiwa kuwa huru leo katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
  Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Ephraim Mgawe akipongezana na aliyekuwa Naibu wa Mamlaka  ya Bandari  anashughulikia huduma, Hamad Koshuma ambaye   Mahakama pia imemuachia huru  leo   katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimfariji Baba wa aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Hai, marehemu Arnold Swai, Jonathan Swai, baada ya kumkabidhi rambirambi za CCM na Jumuia zake, wakati wa ibada na kuaga mwili wa marehemu, katika Kanisa la KKKT Usharika wa Masama, Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro, leo.  Arnold alifariki dunia katika ajali ya gari wakati akitoka kwenye maadhimisho ya miaka 40 ya CCM mkoa wa Kilimanjaro, Februari 5, 2017.
  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimfariji Baba wa aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Hai, marehemu Arnold Swai, Jonathan Swai, baada ya kumkabidhi rambirambi za CCM na Jumuia zake, wakati wa ibada na kuaga mwili wa marehemu, katika Kanisa la KKKT Usharika wa Masama, Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro, leo. 
  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimfariji Baba wa aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Hai, marehemu Arnold Swai, Jonathan Swai, baada ya kumkabidhi rambirambi za CCM na Jumuia zake, wakati wa ibada na kuaga mwili wa marehemu, katika Kanisa la KKKT Usharika wa Masama, Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro, leo.
  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiifariji familia ya aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Hai, marehemu Arnold Swai, kutoa salam za rambirambi zake binafsi, za CCM na za Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli wakati wa ibada na kuaga mwili wa marehemu, katika Kanisa la KKKT Usharika wa Masama, Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro, leo.
  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimshukuru Nchungaji Andrew Munishi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Magharibi, Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, baada ya kuendesha misa ya kumuombea aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Hai, marehemu Arnold Swai, kabla ya mazishi yaliyofanyka leo katika kijiji cha Mbweere, Kata ya Miasama wilayani humo.
  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akitoa salam za rambirambi zake binafsi, za CCM na za Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. JohnMagufuli, wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Hai, marehemu Arnold Swai, kutoa salam za rambirambi zake binafsi, za CCM na za Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli wakati wa ibada na kuaga mwili wa marehemu, katika Kanisa la KKKT Usharika wa Masama, Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro, leo.
  Mwakilishi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali ya TSN,  Isaya Mwaisembe atoa maneno ya rambirambi wakati wa kuagwa mwili wa marehemu Arnold Swai katika Kanisa la KKKT Usharika wa Masama, Hai mkoani Kilimanjaro. Arnold alikuwa Mwandishi wa habari wa TSN. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Kilimanjaro,  Bahati Nyakiraria.
  Nchungaji Andrew Munishi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Magharibi, Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, akitoa neno la kiroho,baada ya kuendesha misa ya kumuombea aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Hai, marehemu Arnold Swai, kabla ya mazishi yaliyofanyka leo katika kijiji cha Mbweere, Kata ya Miasama wilayani humo.
  Muombolezaji akionyesha huzuni
  Waziri wa Maliasili na Utalii Jumanne Magembe akimsalimia Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana wakati wa misa hiyo
  Mwenyekiti wa zamani wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Vick Nsilo Swai, akimsalimia Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana wakati wa misa hiyo. TAFADHALI ENDELEA KUTAZAMA PICHA ZAIDI ZA MSIBA HUU
  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwa na viongozi mbalimbali wa CCM na Waziri Magemebe wakati wa misa hiyo. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka, na kutokakulia ni Mkuu wa Wilaya ya Hai Gelasius Byakanwa, Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Deogratius Rutta, Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo, Iddi Juma na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadick

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia Mabalozi wanaziwakilisha nchi mbalimbali nchi Tanzania na wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kuanza mwaka mpya ya Sherry Party iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam
  Kutoka kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Augustine Mahiga na Katibu Mkuu wa Wizara Balozi Dkt.Aziz P. Mlima wakifuatilia hotuba ya Mhe. Rais Magufuli 
  Sehemu ya Waheshimiwa Mabalozi wakifuatilia hotuba
  Sehemu nyingine ya Waheshimiwa Mabalozi wakifuatilia hotuba
  Hotuba ikiendelea
  Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa China nchini Tanzania Mhe.Lu Youqing
  Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Mhe. Jasem Ibrahim Al Najem 
  Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mratibu Mkazi wa Mashika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maaendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP)  nchini Tanzania, Bw. Alvaro Rodriguez
  Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo nchini Mhe. Jean Pierre Tshampanga Mutamba
  Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika Balozi Joseph Sokoine kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
  Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Celestine Mushy
  Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Baraka Luvanda
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji wa Wizara Bi. Mindi Kasiga akizungumza katika hafla hiyo
  Rais Mhe. Dkt. Magufuli na Waziri Mhe. Balozi Dkt. Mhiga wakiwa katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Mabalozi
  Rais Mhe. Dkt. Magufuli na Waziri Mhe. Balozi Dkt. Mahiga wakiwa katika picha ya pamoja Wawakilishi wa Mashirika mbalimbali ya Kimataifa nchini Tanzania
  Rais Mhe. Dkt. Magufuli na Waziri Mhe. Balozi Dkt. Mahiga wakiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
  Rais Magufuli akutana na Mabalozi na wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amewashukuru Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa kwa ushirikiano na mchango wao kwa Serikali ya Tanzania ambao umesaidia kufikia malengo ya Serikali kwa mwaka uliopita wa 2016. Rais Magufuli aliwasihi Waheshimiwa Mabalozi waendelee kuisaidia Serikali ili kufikia malengo iliyojiwekea kwa mwaka 2017.

  Mhe. Rais Magufuli ametoa shukrani hizo leo wakati wa hafla ya kuukaribisha mwaka mpya (Diplomatic Sherry Party) iliyofanyika Ikulu,  Dar es Salaam kati yake, Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa  yaliyopo nchini.

  Katika hotuba yake, Mhe. Rais Magufuli alisema kuwa mwaka 2016 ambao ulikuwa mwaka wake wa kwanza tangu achaguliwe kuwa Rais wa Awamu ya Tano umekuwa wa mafanikio makubwa ambapo nchi imendelea kudumisha amani, mshikamano, umoja na Muungano umeimarika. Aidha katika mwaka huo,  Serikali  imeongeza jitihada za kuimarisha demokrasia, kupiga vita rushwa, ujangili na ufisadi.

  Mhe. Rais Magufuli aliongeza kusema kuwa, Serikali ya Tanzania imefanikiwa kiuchumi na kuwa nchi ya pili yenye uchumi unaokua kwa kasi barani Afrika ikitanguliwa na Ivory Coast. Uchumi wa Tanzania ulitarajiwa kukua kwa asilimia 7.2 mwaka jana kutoka asilimia 7.0 mwaka uliotangulia. Pia kiwango cha mfumuko wa bei kilipungua kutoka asilimia 6.5 mwezi Januari 2016 hadi kufikia asilimia 2.5 mwezi Oktoba mwaka huohuo.

  Akizungumzia suala la ukusanyaji mapato, Mhe. Rais Magufuli alisema kwamba Serikali inasimamia kikamilifu suala hilo ambapo kwa sasa  kiwango cha ukusanyaji wa mapato kimeongezeka kutoka shilingi bilioni 850 hadi kufikia shilingi trilioni 1.2 kwa mwezi.

  Kuhusu mpango wa maendeleo wa miaka mitano 2016/2021, Rais Magufuli aliwaeleza Mabalozi hao kuwa, mpango huu unalenga kujenga Uchumi wa Viwanda ili kuiwezesha Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 kama Dira ya Maendeleo ya Taifa inavyoelekeza.

  Alieleza kuwa katika kutekeleza Mpango huo kiasi cha shilingi Trilioni 107 kinahitajika na kati ya hizo  Serikali itatoa shilingi trilioni 59 ambazo ni wastani wa shilingi trilioni 11.8 kila mwaka kwa kipindi cha miaka mitano ijayo. Utekelezaji wa mpango huo umeshaanza ambapo Serikali katika Bajeti yake ya mwaka 2016 imetenga kiasi cha shilingi trilioni 29.5  ambazo ni sawa na asilimia 40 ya Bajeti ya Serikali kwa ajili ya Bajeti ya Maendeleo. Kiwango hicho ni cha juu zaidi kuwahi kutengwa kwenye bajeti ya maendeleo katika historia ya Tanzania.

  Fedha hizo zimeelekezwa kwenye ujenzi wa miundombinu wezeshi kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda kama vile nishati, barabara, reli  na maji. Aliongeza kusema kuwa Kati ya fedha hizo shilingi trilioni 5.5 zimetengwa kwa ajili ya miundombinu ya usafirishaji na shilingi trilioni 1.2 zimetengwa kwa ajili ya nishati ya umeme. “Hii imetuwezesha kuendelea au kuanza utekelezaji wa miradi mikubwa ya usafiri ikiwemo reli, barabara, anga, maji pamoja na miradi ya umeme. Tuliweza pia kununua ndege mpya sita ambazo bila shaka zitasaidia kukuza sekta ya utalii nchini”

  Kwa muktadha huo, Rais Magufuli aliwaomba Mabalozi kushawishi wawekezaji kuja kuwekeza katika ujenzi wa Reli wa kiwango cha kimataifa kutoka Dar Es Salaam hadi Mwanza na Kigoma na kuunganisha hadi nchi za Burundi, DRC na Rwanda. Serikali kwa kutumia fedha zake za ndani itaanza kujenga kilomita 300 kuanzia Dar  Es Salaam hadi Morogoro.

  Vile vile, Serikali imeweka kipaumbele kwenye kuboresha huduma za jamii ikiwemo sekta ya elimu iliyotengewa trilioni 4.8  na sekta ya afya kiasi cha trilioni 1.9. Kupitia mpango huu wa kuboresha sekta ya elimu, kiwango cha udahili kwa watoto wanaojiunga na darasa la kwanza na kidato cha kwanza na wale wanaopokea ufadhili wa masomo ya juu kimeongezeka mara dufu ikilinganishwa na miaka iliyopita.

  Akizungumzia masuala ya Diplomasia, Mhe. Rais Magufuli aliwaeleza Mabalozi na Wawakilishi hao wa Mashirika ya Kimatifa kuwa mahusiano ya kidiplomasia kati ya Tanzania na nchi ningine  yameimarika ambapo Viongozi Wakuu kutoka nchi mbalimbali wamefanya ziara nchini Tanzania.

   Aidha, yeye binafsi, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Viongozi wengine Serikalini wamefanya ziara za kuimarisha ushirikiano kwenye nchi mbalimbali. Katika ziara hizo, Tanzania imesaini mikataba mbalimbali ya ushirikiano. Mhe. Rais aliahidi kuwa Tanzania itaendelea kuwa mwanachama mwaminifu kwenye Mashirika ya Kimataifa na Kikanda ikiwemo Umoja wa Afrika (AU), Umoja wa Mataifa (UN), Jumuiya ya Madola, Jumuiya ya Afrika Mashariki na mengine.

  “Tunawashukuru sana Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa na Kikanda kwa kazi nzuri mnayoifanya hapa nchini kwetu. Mafanikio yote haya niliyoainisha yamewezeshwa na ushirikiano wenu na naahidi Serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwenu ili muweze kufanya kazi zenu vizuri” alisema Rais Magufuli.

  Vilevile aliwaomba Mabalozi hao kuendelea kushirikiana na Tanzania ili kuiwezesha kufikia malengo yake na aliwakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza nchini na kutumia fursa za malighafi, nguvukazi na soko kubwa lililopo nchini.

  Halikadhalika, Mhe. Rais Magufuli alianisha changamoto zinazochangia kukwamisha jitihada mbalimbali za Serikali ikiwa ni pamoja na Mabadiliko ya Tabianchi na kuiomba Jumuiya ya Kimataifa kushirikiana katika kukabiliana na changamoto hii ili kuziwezesha jamii zetu kufikia maendeleo na ustawi. Pia kupitia Mabalozi hao alizipongeza nchi zilizoridhia Mkataba wa Paris kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi na kueleza kuwa Tanzania imeanza mchakato wa kuridhia Mkataba huo tangu mwezi Aprili, 2016.

  Katika hatua nyingine, Mhe. Rais aliwaeleza rasmi Mabalozi hao azma ya Serikali ya kuhamishia Makao Makuu mjini Dodoma katika kipindi cha miaka mitano ya utawala wake na kuwaomba Mabalozi hao nao waanze mchakato wa kuhamia Dodoma.

  “Mwaka jana wakati nakabidhiwa uenyekiti wa Chama cha Mapinduzi niliahidi ndani ya miaka mitano Serikali itahamia Dodoma. Tayari Waziri Mkuu na baadhi ya Wizara zipo Dodoma. Nawaomba Mabalozi nanyi muanze kufikiria kuhamia Dodoma kwani Serikali imekwishatenga viwanja kwa ajili yenu, alisisitiza Rais Magufuli.

  Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Mabalozi ambaye pia ni Balozi wa Zimbabwe hapa nchini, Mhe. Edzai Chimonyo alisema kuwa anaipongeza Serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Rais Magufuli kwa hatua kubwa  ya maendeleo iliyopiga katika kipindi cha mwaka mmoja wa utawala wake. Alisema kuwa katika kipindi hiki wameshuhudia uchumi ukikua, nidhamu katika utumishi wa umma, ukusanyaji wa mapato kuongezeka, na kiwango cha mfumuko wa bei kupungua.

  Aidha, aliongeza kuwa wanaunga mkono mpango wa Serikali wa kujenga miundombinu wezeshi ikiwemo Reli kwa vile kutawezesha kukuza biashara na nchi jirani na mataifa mengine kwa ujumla. Pia alipongeza jitihada za Serikali katika kukuza ushirikiano na Sekta Binafsi ambayo ina mchango mkubwa kwenye maendeleo na kupongeza juhudi za Tanzania kwenye usuluhishi wa migogoro kwenye Ukanda wa Maziwa Makuu na kuitaja Tanzania kuwa ni Kisiwa cha Amani.

  Kuhusu Mabalozi kuhamia Dodoma, Balozi Chimonyo alisema Jumuiya ya Mabalozi inaunga mkono wazo hilo na wapo tayari kuhamia Dodoma kama ilivyopangwa.
                                                               -Mwisho-
  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
  Dar es Salaam, 10 Februari, 2017

  0 0


  HOTUBA YA MHESHIMIWA KASSIM M. MAJALIWA (MB), WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, WAKATI WA KUAHIRISHA MKUTANO WA SITA WA BUNGE LA KUMI NA MOJA LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA TAREHE 10 FEBRUARI, 2017


  UTANGULIZI:

  1.           Mheshimiwa Spika, awali ya yote, naomba kutumia fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu mwenye wingi wa rehma kwa kutujaalia afya njema na kutufikisha siku ya leo tunapohitimisha Mkutano wa Sita wa Bunge lako Tukufu tuliouanza tarehe 31 Januari, 2017. Mwenyezi Mungu ameendelea kuitikia Dua ya kuliombea Bunge lako Tukufu kwa kutuongezea hekima na maono kwa ajili ya kuwatumikia Watanzania. Tumshukuru kwa Baraka hiyo!

  MAJANGA MBALIMBALI

  2.           Mheshimiwa Spika, wakati mkutano huu ukiendelea, wapo Watanzania wenzetu waliokutwa na masahibu mbalimbali kama vile mafuriko yaliyotokea wilayani Mpwapwa, kimbunga huko Njombe, Ileje na Nyamagana, ajali ya treni eneo la Ruvu mkoani Pwani. Aidha, zimekuwepo ajali mbalimbali za barabarani. Hivyo, napenda kutumia fursa hii kutuma salamu zangu za pole kwa wale wote waliopoteza wapendwa wao na kuwaombea uponaji wa haraka kwa wale waliopata majeraha kwenye ajali hizo.

  3.           Mheshimiwa Spika, aidha itakumbukwa kuwa tarehe 26 Januari, 2017 ilitokea ajali ya kuporomoka kwa kifusi katika machimbo ya dhahabu ya Nyarugusu, mkoani Geita ambapo vijana wetu 15 waliofukiwa na kifusi kwenye machimbo hayo waliokolewa. Ninawashukuru na kuwapongeza kwa ujasiri na uzalendo wa hali ya juu waliofanikisha uokoaji huo. Yapo mambo mengi tunayoweza kujifunza kutokana na ajali hiyo, na hususan hatua za kuchukua kuzuia ajali kama hizo kujitokeza siku zijazo na jinsi ya kufanya uokoaji pindi zikitokea. Natoa rai, kwa kila Taasisi inayohusika, ifanyie kazi funzo ililolipata kwenye zoezi hili, ili kuepuka ajali za migodini, na endapo zikitokea, kuwepo na utayari katika uokoaji.

  Pongezi na teuzi mbalimbali

  4.           Mheshimiwa Spika, kwenye Mkutano huu, Bunge lako Tukufu limepokea na kuwaapisha Wabunge wapya wanne, ambao ni Mheshimiwa Abdallah Majura Bulembo (Mb), Mheshimiwa Anne Killango Malecela (Mb), Mheshimiwa Juma Ali Juma (Mb) na Mheshimiwa Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi (Mb). Ninawapongeza sana Waheshimiwa Wabunge wapya kwa heshima waliyoipata ya kujumuika nasi kwenye Bunge lako Tukufu. Kama ilivyo ada, naamini wote tutatoa ushirikiano unaotarajiwa kwa Waheshimiwa Wabunge wapya ili watekeleze majukumu yao kwa ufanisi na tija.

  5.           Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii pia kumpongeza Mheshimiwa Prof. Ibrahim Juma, kwa kuteuliwa na Mheshimiwa Rais, kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania. Sina shaka Mheshimiwa Jaji Prof. Juma ataendeleza uhusiano mzuri uliopo kati ya mhimili wa mahakama na mihimili mingine ya dola, kama alivyokuwa mtangulizi wake Mheshimiwa Jaji Mstaafu Mohammed Chande Othman. Serikali inaahidi kumpa ushirikiano unaostahili ili aendeleze maboresho kwenye mhimili huo yaliyoanzishwa na mtangulizi wake.

  6.           Mheshimwa Spika, tarehe 2 Februari 2017, Mheshimiwa John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, alimteua Jenerali Venance S. Mabeyo kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali Davis Mwamunyange ambaye amestaafu. Nitumie fursa hii kumpongeza Jenerali Mabeyo kwa uteuzi huo na kumshukuru Jenerali Mwamunyange kwa kulitumikia Taifa kwa uzalendo na uadilifu mkubwa.

  SHUGHULI ZA BUNGE

  7.           Mheshimiwa Spika, tunapohitimisha mkutano huu, tumeweza kukamilisha mjadala wa miswada miwili, kupokea Kauli za Mawaziri mbili na taarifa 14 za Kamati za Kudumu za Bunge. Itakumbukwa kuwa, awali Serikali ilipanga kuwasilisha miswada mitatu ikiwemo Muswada wa Sheria ya Madaktari, Madaktari wa Meno, na Wataalamu wa Afya Shirikishi wa Mwaka 2016 (the Medical, Dental and Allied Health Professionals Bill, 2016), lakini tukaomba kuuondoa ili tuendelee kujipanga vizuri zaidi. Hivyo, miswada iliyojadiliwa na kupitishwa na Bunge lako tukufu kwenye mkutano huu ni ifuatayo:-

  (i)         Muswada wa Sheria ya Huduma ya Msaada wa Kisheria wa Mwaka 2016 (The Legal Aid Bill, 2016) na

  (ii)        Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali Na. 4 wa Mwaka 2016 [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (Na.4) Bill, 2016].

  8.           Mheshimiwa Rais, Miswada hii ni muhimu sana kwa ustawi wa nchi yetu, hivyo nawapongeza sana Waheshimiwa Wabunge kwa michango yenu mizuri kwa maslahi ya Taifa letu. Aidha, nitumie fursa hii kumpongeza Mwanasheria Mkuu wa Serikali na watendaji wote kwa kazi nzuri ya maandalizi ya Miswada hiyo. Nawasihi Waheshimiwa Mawaziri wanaohusika na Miswada iliyopitishwa, wasimamie utayarishaji wa kanuni za sheria hizo zilizopitishwa pindi Mheshimwa Rais atakaporidhia, ili utekelezaji uanze mara moja.  

  9.           Mheshimiwa Spika, katika Mkutano huu jumla ya maswali ya msingi, ya nyongeza na ya papo kwa papo yaliulizwa na Waheshimiwa Wabunge na kujibiwa na Serikali.

  10.        Mheshimiwa Spika, Mkutano huu pia ulipokea na kujadili taarifa mbalimbali za Kamati za Kudumu za Bunge; na kutolewa kauli mbili za Mawaziri kuhusu hali ya chakula nchini na deni la Taifa na hali ya uchumi. Napenda kutumia fursa hii kuwapongeza Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge kwa kuwasilisha kwa umakini na umahiri mkubwa taarifa za kamati zao pamoja na kuzihitimisha. Aidha, nawashukuru Waheshimiwa Wabunge kwa michango, maoni na ushauri wao mzuri walioutoa wakati wa mijadala yote ya taarifa hizo.

  11.        Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kukushukuru wewe binafsi Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Naibu Spika, Wenyeviti wa Bunge, Waheshimiwa Mawaziri na Naibu Mawaziri, Waheshimiwa Wabunge na Wataalam wetu kwa kufanikisha kazi zote zilizokuwa zimepangwa kwenye mkutano huu tena kwa ufanisi mkubwa. Nawashukuru na kuwapongeza sana! Nawapongeza pia na kuwashukuru Waheshimiwa Mawaziri na Naibu Mawaziri kwa maelezo mazuri ya ufafanuzi waliyotoa katika kujibu baadhi za Kamati za Kudumu za Bunge na zile zilizotolewa na Waheshimiwa Wabunge binafsi au kwa ujumla wao. Napenda kuahidi kuwa Serikali itazingatia maoni na ushauri wa Waheshimiwa Wabunge pamoja na mapendekezo mliyotoa kwenye kamati husika.

  HOJA ZA KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE

  12.        Mheshimiwa Spika, naomba nami uniruhusu nitumie fursa hii kutoa maelezo mafupi ya msisitizo kuhusu baadhi ya hoja zilizojitokeza katika Mkutano huu wa Bunge.

  Vita dhidi ya Dawa za Kulevya

  13.        Mheshimiwa Spika, moja ya eneo lililojadiliwa na kuibua hisia kali ni kuhusu vita inayoendelea Nchini dhidi ya dawa za kulevya. Watanzania wote ni mashahidi kwamba vijana wetu wengi wameendelea kudhoofisha afya zao kutokana na matumizi ya dawa za kulevya. Dawa za kulevya ni hatari sana kwa usalama na ustawi wa Taifa letu. Vita hii inayopiganwa sasa dhidi uagizaji, uzalishaji, usambazaji na matumizi ya dawa za kulevya ni kubwa. Sote tunapaswa kuunga mkono jitihada hizo.

  14.        Mheshimiwa Spika, Kitaalamu, madhara ya kiafya yanayosababishwa na matumizi ya dawa za kulevya ni mengi ikiwa ni pamoja na kuathirika kwa mfumo wa fahamu kwa mtumiaji ikiwamo kuchanganyikiwa, kuwa na ulevi usioponyeka kirahisi na kusababisha kifo kama mtumiaji atazidisha matumizi ya dawa za kulevya. Madhara ya kiuchumi ni pamoja na gharama kubwa za kuwatibu waathirika wa dawa za kulevya, gharama kubwa za uchunguzi wa kimaabara kwenye Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na watumiaji wa dawa za kulevya kushindwa kujisimamia na kuendesha maisha yao wao wenyewe.

  Aidha, takwimu za jumla za Watanzania waliokamatwa na kufungwa gerezani katika nchi mbalimbali kwa makosa ya kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya ni kama ifuatavyo:-
  ·         Nchini China Watanzania walio magerezani ni zaidi ya 200;
  ·         Nchini Brazil Watanzania 12;
  ·         Nchini Iran Watanzania 63;
  ·         Nchini Ethiopia Watanzania 7; na
  ·         Nchini Afrika Kusini Watanzania 296.

  Madawa ya kulevya hapa nchini, huingia zaidi kutumia njia za bandari bubu kupitia Bahari ya Hindi na mipaka yetu kwa njia ya magari binafsi na mabasi kupitia nchi za Kenya, Uganda na mpaka wa Tunduma.

  15.        Mheshimiwa Spika, lengo la Serikali ni kuwasaidia walioathirika na dawa za kulevya na kuwachukulia hatua kali wale waliowaathiri kwa maana ya wauzaji na wasambazaji. Tunashukuru kwamba Watanzania wengi na Waheshimiwa Wabunge pia mmetoa mchango mkubwa na ushauri wa namna nzuri zaidi ya kupambana na janga hili. Dhamira ya Serikali ni kupambana na janga hili kwa dhahiri na kwa dhati bila kumuonea mtu yeyote na kwa kuzingatia misingi ya sheria na haki.

  Utaratibu wa utoaji Mikopo ya Elimu ya Juu

  16.        Mheshimiwa Spika, hoja nyingine iliyovuta hisia za Waheshimiwa Wabunge wengi ni kuhusu utaratibu wa utoaji wa Mikopo ya Elimu ya Juu. Mheshimiwa Spika, suala hili ni pana na linagusa familia nyingi za Watanzania, na hususan walio maskini. Hivyo, Serikali imeunda Kamati ya Wataalam ambao wanaupitia upya utaratibu wa sasa kwa lengo la kupendekeza vigezo muafaka kwa kuzingatia changamoto zilizopo. Azma ya Serikali ni kuanza utekelezaji wa vigezo vilivyoboreshwa katika upangaji na utoaji wa mikopo kuanzia mwaka wa masomo wa 2017/18. Aidha, Serikali itaendelea kuimarisha urejeshwaji mikopo hii kwa wakopaji ili kuongeza fedha kwa ajili ya kugharamia wanufaika wapya wa mikopo ya elimu ya juu ili kupunguza utegemezi kutoka katika bajeti ya Serikali.

  Uhakiki wa Watumishi na madai ya Watumishi

  17.        Mheshimiwa Spika, kulikuwa pia na hoja kuhusu uhakiki wa watumishi na madai ya watumishi. Mheshimiwa Spika, napenda kulifahamisha Bunge lako Tukufu kwamba, zoezi la uhakiki wa watumishi hewa limekamilika, kinachoendelea sasa ni uhakiki wa vyeti vya kitaaluma. Kuhusu madeni, Mkaguzi wa Ndani wa Serikali amefanya uhakiki wa madai mbalimbali ya watumishi wa umma ya hadi kufikia tarehe 30 Juni, 2016. Katika mwaka wa fedha 2016/17, Serikali imeanza kulipa madeni hayo ambapo hadi sasa Serikali imelipa shilingi bilioni 42.35 kwa watumishi wasiokuwa walimu. Aidha, kwa upande wa walimu, Serikali imelipa jumla ya shilingi bilioni 23.458 kwa walimu 63,955 kwa kipindi cha mwaka 2015/16 na mwaka 2016/17. Serikali itaendelea kulipa madeni yote ya waumishi wa umma yaliyohakikiwa.

  18.        Mheshimiwa Spika, hoja nyingine muhimu iliyojadiliwa sana na Waheshimiwa Wabunge ni kuhusu utawala bora hususan mipaka ya kimadaraka kati ya mihimili mikuu ya nchi yaani Serikali, Bunge na Mahakama. Mheshimiwa Spika, dhana ya mgawanyo wa madaraka baina ya mihimili ya dola imewekwa wazi kwa mujibu wa Ibara ya 4(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Utekelezaji wa majukumu ya mihimili hiyo unategemea sana viongozi na watendaji wake kuheshimiana, kuvumiliana na kufanya kazi zao kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa. Shabaha kuu ni kuwaletea wananchi maendeleo hivyo tuepuke misuguano isiyo na tija ambayo inatuondoa katika lengo la kufanya shughuli za maendeleo.

  SEKTA YA AFYA

  Hali ya Upatikanaji wa Dawa Nchini

  19.        Mheshimiwa Spika, hali ya upatikanaji wa dawa nchini inaendelea kuimarika kufuatia kutolewa kwa wakati fedha kwa ajili ya ununuzi wa dawa. Mathalan, kiasi cha shilingi bilioni 91 kimeshatolewa, kati ya shilingi bilioni 251 zilizotengwa, sawa na wastani wa shilingi bilioni 20 kila mwezi. Haya ni mafanikio makubwa na ni dhamira njema ya Serikali katika kuboresha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba nchini. Mafanikio haya ni tofauti na miaka ya nyuma ambako tulipeleka chini ya shilingi bilioni 10.

  Ununuzi wa Dawa kutoka wa Wazalishaji

  20.        Mheshimiwa Spika, kama ambavyo tumekuwa tukieleza kuhusu dhamira ya Serikali ya kununua madawa na vifaa tiba moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji badala ya mawakala. Napenda kuliarifu Bunge lako tukufu kwamba, utaratibu huo umeanza na tayari Serikali imekamilisha taratibu za kimkataba na wazalishaji watano (5) wakubwa wa ndani kwa ajili ya kununua baadhi ya dawa kutoka ndani ya nchi, wakati mikataba mingine 76 ya wazalishaji wa nje iko katika hatua za mwisho. Matarajio yetu ni kwamba, utekelezaji wa mikataba ya nje utaanza katika mwaka wa fedha 2017/18.

  21.        Mheshimiwa Spika, dhamira ya Serikali ya kusambaza dawa kwa wakati kwenye Halmashauri zetu haitafanikiwa endapo Halmashauri zitachelewa kuwasilisha maoteo ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi. Hivyo, Halmashauri zote nchini, zinaagizwa kufanya maoteo na kuyawasilisha Bohari Kuu ya Dawa kabla au ifikapo tarehe 05 Machi 2017. Aidha, naomba kutoa rai yangu kwa Waheshimiwa Wabunge, kupata wasaa wa kufuatilia mchanganuo wa usambazaji dawa katika Halmashauri zenu ambao hutolewa na Mheshimiwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Jitihada za usambazaji dawa pia zinafanywa na Maduka ya Dawa yanayoendelea kujengwa sehemu mbalimbali nchini. Shabaha yetu ni kwamba, ifikapo mwezi Juni, 2017 usambazaji wa dawa muhimu nchini kote uwe umefikia asilimia 85.

  Bima ya Afya kwa wote

  22.        Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na maboresho kwenye Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), ambayo yatamwezesha mwanachama kupata huduma kutoka ngazi ya Zahanati hadi ngazi ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa. Katika maboresho hayo, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) utabaki na jukumu la kununua huduma (Purchaser) wakati Halmashauri zitakuwa na jukumu la kutoa huduma (Provider) tofauti na ilivyo sasa. Kwa kuanzia, Mpango huu utatekelezwa katika Halmashauri 50 katika Mikoa ya Ruvuma, Kagera, Mwanza, Mara, Singida, Tabora na Pwani ambapo Mpango huu utazinduliwa rasmi mwishoni mwa mwezi Februari, mwaka 2017.

  23.        Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia mwelekeo huo wa Serikali, ni vema sasa Waheshimiwa Wabunge kupitia Halmashauri zetu mkaanza kuwaandaa wananchi kupokea mpango huu wa bima ya afya kwa kila mwananchi. Aidha, anzeni kutafakari namna bora zaidi ya kutekeleza mpango huo katika muktadha na mazingira ya nchi yetu.

  Uhaba wa Watumishi Katika Sekta ya Afya

  24.        Mheshimiwa Spika, kuna kilio kikubwa cha uhaba wa watumishi kwenye sekta ya afya. Jambo hili tunalifahamu na kwa hakika linatugusa sote. Kama ambavyo tumeanza kwa kutangaza ajira 4,348 za walimu wa masomo ya sayansi pia tutaajiri Watumishi wa kada ya afya na kada zingine.

  SEKTA YA ELIMU

  Uandikishaji wa wanafunzi kwa mwaka 2017

  25.        Mheshimiwa Spika, huu ni mwanzo wa mwaka 2017, tunayo matarajio ya uandikishaji wa wanafunzi wa awali, Msingi na pia kwa Sekondari, Kidato cha Kwanza. Zoezi la uandikishaji katika Kidato cha Kwanza linaendelea na linatarajiwa kufungwa tarehe 28 Februari, 2017. Naomba nitumie fursa hii, kuziagiza Halmashauri zote nchini, kuongeza kasi ya uandikishaji kwa shule za sekondari, usajili wa darasa la kwanza na pia ujenzi wa vyumba vya madarasa ili wanafunzi wote wanaostahili kuandikishwa au kuendelea na ngazi inayofuata katika shule wasipoteze fursa hiyo kutokana na ukosefu wa vyumba vya madarasa.

  Elimu kwa Wanafunzi wenye Mahitaji Maalum
  26.        Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu wa kutoa elimu bora kwa watoto wote wenye umri wa kwenda shule. Kutokuwepo kwa vifaa vya kufundishia na kujifunzia kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu imekuwa ni changamoto kwao katika kujifunza kwa ufanisi. Ili kuboresha upatikanaji, ushiriki na usawa katika elimu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum, Serikali imenunua vifaa vya kielimu na visaidizi kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia, kuona na wenye ulemavu wa akili. Vifaa hivyo vinajumuisha mashine 932 za maandishi ya nukta nundu, rimu za karatasi za breli zipatazo 2,548 na shime sikio (hearing aids) 1,150. Aidha, katika kuhakikisha kwamba tunatekeleza dhana ya elimu jumuishi, Serikali imenunua pia vifaa kwa ajili ya upimaji ili kubaini mahitaji mbalimbali ya ujifunzaji kabla na baada ya usajili wa watoto katika shule za msingi. Vifaa hivyo vinajumuisha pia vifaa vya upimaji kwa ajili ya masikio; vifaa vya upimaji wa macho; na vifaa vya upimaji wa mtindio wa ubongo.
  27.        Mheshimiwa Spika, napenda kulifahamisha Bunge lako Tukufu kuwa vifaa vya watoto wenye mahitaji maalum ambavyo vimegharimu kiasi cha Shilingi bilioni 3.6 vimekwishapokelewa na vitasambazwa katika shule zenye wanafunzi wenye mahitaji hayo kuanzia tarehe 1 Machi, 2017.

  Natoa wito kwa Maafisa Elimu na walimu wote wanaofundisha wanafunzi wetu wenye mahitaji maalum kutumia ipasavyo vifaa hivyo. Aidha, wazazi wa watoto wenye mahitaji maalum wawapeleke watoto wao shule, badala ya kuwaficha majumbani.

  Upatikanaji wa Vitabu vya Elimu ya Msingi na Sekondari

  28.        Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na jitihada zake za kuhakikisha upatikanaji wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia na hadi sasa Serikali imefanikiwa kusambaza Nakala 6,862,800 kwa vitabu vya kiada kwa Darasa la kwanza vya Mtaala ulioboreshwa kwa shule zote za msingi Tanzania Bara. Aidha, uchapaji wa vitabu vya Darasa la pili Nakala 6,862,800 unaendelea na uchapishaji wa Nakala 6,818,181 za Darasa la Tatu umekamilika. Nakala hizo za Darasa la Tatu zitasambazwa sambamba na Vifaa vya Darasa la Pili.

  Kwa upande wa shule za Sekondari, Nakala 2,109,683 zimechapishwa na usambazaji umeanza tarehe 07 Februari, 2017. Natoa wito kwa Walimu wote Nchini na Wanafunzi kutunza vizuri vitabu hivyo ili vitumike kwa muda mrefu.

  Usambazaji wa vifaa vya maabara

  29.        Mheshimiwa Spika, Serikali inatekeleza Mpango Maalum wa kukuza na kuimarisha ufundishaji wa masomo ya sayansi nchini. Ili kutekeleza azma hiyo, Serikali ilihamasisha ujenzi wa maabara kwa ajili ya masomo ya sayansi. Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba, Serikali imeagiza vifaa vya Maabara kwa ajili ya Shule 1,625 za Sekondari nchini. Hadi sasa Asilimia 70 ya vifaa hivyo imekwishawasili nchini na usambazaji wake umeanza hivi karibuni katika Kanda ya Dar es Salaam. Natoa wito kwa Wakuu wa Shule kuweka utaratibu mzuri wa kutunza vifaa hivyo ili viweze kudumu. Aidha, ni matumaini yangu kwamba vifaa hivyo vitakuwa ni chachu ya wanafunzi kuchangamkia masomo ya sayansi na hivyo kulifanya Taifa letu kutengeneza wanasayansi wengi zaidi.


  ELIMU YA JUU

  Ubora wa Elimu ya Juu

  30.        Mheshimiwa Spika, mwishoni mwa mwaka 2016, Serikali, kupitia Tume ya Vyuo Vikuu, ilifanya uhakiki wa ubora wa elimu kwa Vyuo Vikuu vyote nchini. Matokeo ya uhakiki huo yatatumika katika kuchukua hatua mbalimbali za kuboresha elimu ya juu ili kupandisha viwango vya taaluma ya wahitimu. Uhakiki huo utakuwa unafanyika kila baada ya miaka mitatu ili kuhakikisha ubora wa elimu inayotolewa unalingana kote nchini.

  31.        Mheshimiwa Spika, sanjari na jitihada hizo, kuanzia mwaka wa fedha 2017/18, Serikali itaweka Viwango vya Ulingalifu (Benchmark Standards) vya kuainisha kozi zinazotakiwa kusomwa katika nyanja za ualimu, udaktari wa binadamu, sheria na biashara. Matarajio yetu ni kwamba jitihada hizi na nyingine zitakazokuwa zinaendelea kufanyika zitasaidia kuboresha elimu ya juu kwa kiasi kikubwa.

  SEKTA YA KILIMO

  Hali ya Upatikanaji wa chakula nchini

  32.        Mheshimiwa Spika, kama ilivyoelezwa katika Kauli ya Serikali kuhusu hali ya chakula na lishe hapa nchini kwa mwaka 2016/2017, baadhi ya maeneo katika Halmashauri 55 yana upungufu wa chakula na bei za vyakula hasa nafaka kwenye masoko katika Halmashauri hizo imeendelea kupanda. Mheshimiwa Spika, leo sikusudii kurudia maelezo yaliyotolewa na Mheshimiwa Waziri mwenye dhamana na sekta ya kilimo bali kuwaagiza Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuwahamasisha wananchi kulima mazao yanayokomaa mapema kwa kutumia mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mengi hapa nchini. Pili, kuwashauri wananchi kutumia vizuri chakula walicho nacho na kuwasihi wafanyabishara wasifiche chakula bali wasaidie kuchukua chakula kutoka kwenye maeneo yenye chakula cha ziada na kukisafirisha kwenda kuuza kwenye maeneo yenye upungufu.

  SEKTA YA MIFUGO
  Upatikanaji na Usambazaji wa Mbegu Bora za Mifugo
  33.        Mheshimiwa Spika, ili kukabiliana na changamoto ya migogoro baina ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi, Serikali inahimiza wananchi kuondokana na mazoea ya uchungaji na kujikita zaidi katika ufugaji wa kisasa ambao utawawezesha kuwa na mifugo michache yenye ubora ambayo itawaongezea tija katika uzalishaji wa nyama na maziwa mengi zaidi kwa ng’ombe mmoja. Hivyo, Serikali kupitia mashamba ya mifugo na vituo vya taasisi za Serikali vilivyoko katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu itaendelea kuhakikisha kuwa mbegu bora za mifugo zinazalishwa kwa ajili ya uhamilishaji, na mitamba na madume bora yanazalishwa kwa wingi na kusambazwa ili kukidhi mahitaji ya wafugaji wetu.

  34.        Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kuimarisha Taasisi zinazoagiza mbegu za mifugo kutoka nje ya nchi kama vile Heifer Project International (HPI) na SAGCOT - Catalytic Trust Fund (CTF) na kwa kushirikiana na mashamba makubwa ya kisasa ya sekta binafsi ili wafugaji wawe na wigo mpana wa kuchagua aina bora zaidi za mifugo. Hivyo, natoa rai kwa wananchi kuchangamkia fursa hiyo kwa kushiriki katika ufugaji wa kisasa.

  Upatikanaji na Usambazaji wa Mbegu Bora za Malisho

  35.        Mheshimiwa Spika, kuna uhusiano mkubwa kati ya ufugaji bora na upatikanaji wa malisho bora. Hivyo, Serikali itaendelea kuboresha na kuendeleza mashamba ya mbegu za malisho ya mifugo yaliyo chini ya Serikali katika maeneo mbalimbali nchini. Mheshimiwa Spika, naomba kutumia fursa hii kuwaagiza Maafisa Ugani wa mifugo katika Halmashauri zote nchini, kufungua mashamba darasa ya kuzalisha mbegu hizo na kuhamasisha wafugaji kupanda malisho katika maeneo yao na kutoa stadi za ufugaji bora na wa kisasa. Baada ya miaka mitatu Wizara husika ifanye tathmini ya utekelezaji wa agizo hili na kuwasilisha taarifa kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu.

  SEKTA YA ARDHI

  Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi
  36.        Mheshimiwa Spika, katika kuongeza juhudi za kudhibiti migogoro ya matumizi ya ardhi inayojitokeza katika maeneo mbalimbali nchini, katika Mwaka Fedha 2016/17, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Matumizi ya Ardhi imeandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi ya vijiji 50 katika Wilaya 19 na kuandaa Hatimiliki za Kimila 1,361 katika Wilaya ya Mvomero; hatimiliki 2,943 katika wilaya za Mkuranga (297); Ikungi (957); Karagwe (1,099) na Nachingwea (590). Aidha, Serikali imeandaa hatimiliki za kimila 44 za nyanda za malisho za wilaya za Monduli, Ngorongoro, Hanang, Simanjiro na Karatu. Hadi sasa jumla ya vijiji 1,690 vimeandaliwa mipango ya matumizi ya ardhi ambayo imeainisha pia matumizi ya kilimo na ufugaji ikilinganishwa na vijiji 12,545 vilivyopo nchini. Vilevile, upimaji wa mipaka ya vijiji 53 umefanyika katika Wilaya ya Kilombero (Vijiji 7) na Ulanga (Vijiji 5).

  Upimaji na Utoaji wa Hati katika Maeneo yote ya Umma

  37.        Mheshimiwa Spika, ili kulinda maeneo ya umma, ikiwemo sehemu za huduma kama vile Shule, Zahanati, Vituo vya Afya, Hospitali, Vyuo, Ofisi, Vituo vya Polisi, Mahakama, Maeneo ya Majeshi, Mashamba ya serikali, Hifadhi za Misitu na Wanyama Pori, Maeneo ya Makumbusho na kadhalika dhidi ya uvamizi, Serikali inaendelea na upimaji wa maeneo hayo na kuyapatia hati miliki. Aidha, Wizara zote Tanzania bara zinaagizwa kuhakikisha kuwa maeneo wanayoyamiliki na yale yaliyoko chini ya taasisi zao yanapimwa na kuandaliwa hatimiliki.

  38.        Mheshimiwa Spika, ili kuharakisha zoezi la upimaji, upangaji na utoaji wa Hatimilki za maeneo ya umma, Serikali imeelekeza Wizara/taasisi za umma kutumia wapima wa Serikali au wapima binafsi waliosajiliwa na Bodi ya Wapima Ardhi nchini, yaani National Council of Professional Surveyors (NCPS) kupima maeneo yao kwa kugharimia upimaji wa maeneo hayo. Nitumie fursa hii kuzipongeza baadhi ya taasisi ambazo zimeanza kutekeleza maelekezo hayo, ambazo ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mahakama Kuu ya Tanzania na baadhi ya sekretarieti za mikoa.

  Mpango wa Uwekaji Mawe/Alama za Mipaka Kwenye Hifadhi na Mapori ya Akiba

  39.        Mheshimiwa Spika, Serikali inatekeleza mpango wa kulinda usalama wa maeneo ya hifadhi na mapori ya akiba kwa kuweka mawe ya mipaka yanayoonekana, yaani Pillars, ili kuzuia uvamizi na uharibifu wa maeneo hayo kwa kushirikisha wadau wa mipaka hiyo. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inashirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii kuhakiki mipaka ya maeneo ya hifadhi na kuweka alama za mipaka.

  40.        Mheshimiwa Spika, aidha Serikali imeendelea kushughulikia migogoro ya mipaka ya vijiji, wakulima na wafugaji, wanavijiji na hifadhi na mapori ya akiba inayoibuka hapa nchini. Ili kukabiliana na changamoto hii, Serikali iliunda Kamati Maalum ya kisekta ya kushughulikia migogoro ikijumuisha watendaji wa sekta mbalimbali zinazohusika kwa njia moja au nyingine kwenye masuala ya migogoro ya ardhi. Kamati hiyo tayari imepokea na kuchambua migogoro yote iliyowasilishwa kutoka Halmashauri mbalimbali nchini; na kutembelea wilaya zenye viashiria vya migogoro. Baada ya zoezi hilo kukamilika, Serikali itawasilisha taarifa ya hali ya migogoro na hatua iliyofikiwa ya utatuzi wa migogoro hiyo nchini.

  41.        Mheshimiwa Spika, nimekwishatoa maelekezo mahsusi kwa Halmashauri mbalimbali na ninaomba kutumia Bunge lako Tukufu kurejea maelekezo yangu kuhusu migogoro ya mipaka kati ya Kijiji na Kijiji, Vijiji na Hifadhi, au Wilaya na Wilaya. Kwa migogoro ya mpaka kati ya Kijiji na Kijiji, maelekezo ya Serikali ni kwamba, migogoro hiyo imalizwe kupitia vikao vya vijiji husika na wataalamu wa Halmashauri wasaidie katika kumaliza migogoro hiyo. Migogoro kati ya vijiji na Hifadhi, au Wilaya na Wilaya, migogoro hiyo itatuliwe kwa kuangalia Mipaka halali inayotambuliwa na Government Notice (GN) na Wataalamu wa Upimaji na Ramani wa Halmashauri au wale wa Wizara ya Ardhi wasaidie kubainisha mipaka hiyo iliyowekwa na Serikali miaka iliyopita na kusuluhisha pande zote mbili. Nazisihi Halmashauri zote nchini zizingatie mwongozo huo ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima.

  KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO YA WANANCHI
  42.          Mheshimiwa Spika, katika ziara mbalimbali ninazofanya Mikoani, nimebaini uwepo wa malalamiko mengi ya wananchi ambayo hayashughulikiwi kwa wakati katika ngazi za Vijiji, Mitaa na Kata. Aidha, nimebaini kuwa mikutano ya Vijiji, Kata na Mitaa imekuwa haifanyiki kama inavyotakiwa kisheria na hivyo kufanya kero nyingi kutopatiwa ufumbuzi.

  43.          Mheshimiwa Spika, suala la kutotatua kero za wananchi katika ngazi ya Serikali za Mitaa ni kinyume na dhamira ya Serikali ya kuwatumikia wananchi wote bila ubaguzi. Aidha, ni kinyume na msimamo wa Ibara ya 146 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  inayotamka kama ifuatavyo, naomba kunukuu;
  “Madhumuni ya kuwapo Serikali za Mitaa ni kupeleka madaraka kwa wananchi. Na vyombo vya Serikali za Mitaa vitakuwa na haki na mamlaka ya kushiriki na kuwashirikisha wananchi katika mpango wa shughuli za utekelezaji wa maendeleo katika Serikali zao na nchi kwa ujumla”. Mwisho wa kunukuu.
  44.        Mheshimiwa Spika, Sheria ya Serikali za Mitaa inaelekeza kuitishwa kwa Mikutano Mikuu ya Vijiji kila baada ya miezi mitatu. Sheria pia inatoa fursa ya kuitishwa kwa mikutano ya dharura, endapo ipo haja ya kufanya hivyo.

  45.      Mheshimiwa Spika, kutokana na msimamo huo wa kisheria na kutokana na dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kutatua kero za wananchi, suala la utatuzi wa kero za wananchi halitakiwi kuendelea kusubiri ziara za viongozi, badala yake, kero hizo zitatuliwe kwenye ngazi zinazohusika na zitatuliwe kwa wakati. Kwa muktadha huo, naomba kutumia Bunge lako Tukufu kusisitiza mambo yafuatayo:-

   Mosi:          Watendaji wa Kata, Vijiji na Mitaa wanakumbushwa kuitisha Mikutano ya kisheria ya Viijiji na Kata na Mitaa na kusoma taarifa za mapato na matumizi ya miradi ya maendeleo katika maeneo yao. Wakurugenzi wa Halmashauri nao wanaagizwa kusimamia kikamilifu uitishaji wa Mikutano Mikuu ya Vijiji na Mitaa kwa mujibu wa Sheria na kuchukua hatua dhidi ya Viongozi wote watakaoshindwa kutekeleza sharti hilo la kisheria. Tembeleeni vijiji kusikiliza kero za wananchi.
  Pili:             Viongozi na Watendaji katika ngazi ya Mkoa, Wilaya na Halmashauri wajenge utamaduni wa kuwatembelea Wananchi Vijijini kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi wa papo kwa papo.
  HALI YA ULINZI NA USALAMA

  46.        Mheshimiwa Spika, hali ya ulinzi na usalama nchini ni ya kuridhisha. Vyombo vya ulinzi na usalama viko imara na katika hali ya utayari katika kulinda amani na utulivu. Operesheni za kupambana na uhalifu kama vile unyang’anyi wa kutumia silaha/nguvu, kuteka magari na matishio mengine ya kiusalama vimefanyika katika jitihada za kupambana na uhalifu nchini. Mathalan, katika kipindi cha Julai, 2016 hadi Desemba, 2016, Operesheni Kamata Magendo ilifanyika katika mikoa mbalimbali na kufanikiwa kukamata watuhumiwa 109 na mali zenye thamani ya Shilingi 388,271,000.

  Usalama wa Barabarani

  47.        Mheshimiwa Spika, Kikosi cha Usalama Barabarani kinaendelea na kusimamia usalama barabarani. Pamoja na operesheni hizo, bado kuna ripoti za vifo vinavyotokana na ajali. Licha ya takwimu kuonesha vifo vinavyotokana na ajali kupungua, bado jitihada za makusudi pamoja na umakini katika matumizi ya vyombo vya moto inabidi viongezeke.
  Kila mtumia chombo cha moto, aendeshe kwa uangalifu, na Askari wa Usalama Barabarani waendelee kuchukua hatua stahiki kwa wanaovunja sheria za Usalama barabarani ili kuokoa maisha yetu na ya watumiaji wengine wa barabara.


  48.        Mheshimiwa Spika, misako na doria zilizofanyika kati ya Julai, 2016 na Desemba 2016 ziliwezesha kukamatwa kwa Watanzania na wageni 6,916 kwa makosa mbalimbali ya kiuhamiaji ikilinganishwa na Watanzania na wageni 3,119 waliokamatwa katika kipindi kama hiki mwaka 2015. Hili ni ongezeko la asilimia 55. Takwimu hizi zinaonesha ama kuongezeka kwa jitihada za kuwasaka wahamiaji haramu na kuwachukulia hatua za kisheria au changamoto hii imeongezeka duniani. Hata hivyo, lazima Idara iendelee kujizatiti. Haiingii akilini kundi la wahamiaji linapita kwenye mikoa zaidi ya mitatu bila kukamatwa!. Ni lazima Idara ya Uhamiaji iendelee kujitathmini na kujipanga vizuri zaidi.

  Udhibiti wa Silaha

  49.        Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuwakamata wahalifu wanaojihusisha na uhalifu wa kutumia silaha haramu. Aidha, imeweka utaratibu wa kuteketeza silaha zote zinazokamatwa ili zisiweze kurudi tena kutumika katika uhalifu. Hivi karibuni jumla ya silaha 5,608 ziliharibiwa huko mkoani Kigoma. Kwa upande mwingine, katika juhudi za kudhibiti uzagaaji holela wa silaha haramu, Serikali inaendelea kufuatilia mpaka ya Kigoma na Kagera ili kudhibiti silaha na uhamiaji haramu. Serikali ilifanya zoezi la kuhakiki silaha zote zinazomilikiwa kihalali, ambapo asilimia 65 ya wamiliki wa silaha walihakikiwa. Natoa rai kwa wamiliki wote wa silaha nchini, ambao bado hawajahakiki silaha zao, wafanye hivyo kabla au ifikapo tarehe 30/06/2017 vinginevyo watapoteza leseni ya umiliki kwa kukiuka Sheria.

  50.        Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, jukumu la ulinzi na usalama wa nchi yetu, ni la kila mwananchi. Hivyo, natoa wito kwa wananchi wote kuendelea kutekeleza jukumu hili kwa kuepuka kushiriki hujuma dhidi ya nchi yetu na kwa kutoa taarifa za watu wenye nia mbaya ya kuhatarisha amani na usalama wa nchi yetu.

  51.        Mheshimiwa Spika, kabla ya kuhitimisha hotuba yangu, niruhusu nibainishe masuala matano ya msisitizo, ambayo ninawaomba Waheshimiwa Wabunge na wananchi kwa jumla wayazingatie na wahamasishane katika kuyatekeleza. Masuala hayo ni haya yafuatayo:-

  Mosi:       Usalama wa chakula unaanzia katika ngazi ya kaya, kila kaya inatakiwa iwe na utaratibu wa kuwa na chakula cha akiba. Wakati Serikali inaendelea na wajibu wake wa kuwa na hifadhi ya chakula, na kuweka utaratibu wa kutoa chakula penye upungufu, kila mwananchi anao wajibu wa kujiwekea akiba ya chakula cha kaya yake.

  Pili:         Dhamira ya kuwa na Bajeti ya kujitegemea kwa asilimia 100 inategemea jitihada zetu za makusanyo ya kodi. Hivyo, kila mwananchi ana wajibu wa kulipa kodi stahiki bila kushurutishwa, na kila mnunuzi anao wajibu wa kudai stakabadhi kwa kila bidhaa anayonunua.  Aidha, kila mwananchi anao wajibu wa kufichua vitendo vya ukwepaji kodi pale anapo pata fununu za vitendo hivyo. Tulipe kodi kwa maendeleo ya nchi yetu.

  Tatu:       Tunapoendelea kuhamasisha ujenzi wa viwanda na kuvutia mitaji kwa ajili ya biashara mbalimbali hapa nchini, atakayefanya viwanda na biashara hizi ziwe endelevu ni sisi Watanzania. Hivyo, pamoja na kusisitiza uzalishaji bora, tunalo jukumu la kulinda viwanda na biashara za Tanzania kwa kununua bidhaa zinazozalishwa hapa nchini. Unaponunua bidhaa zilizozalishwa hapa nchini, sio tu unasaidia viwanda hivyo viendelee kuongeza ubora wa bidhaa zao, bali pia unavifanya vizidi kuimarika na kutoa ajira nyingi kwa vijana wa Kitanzania.

  Nne:        Azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kumtumikia kila Mtanzania popote pale alipo. Kama nilivyoeleza awali, nimebaini baadhi ya kero za wananchi ambazo zingeweza kutatuliwa katika ngazi za Wilaya, zinaletwa kwenye Ofisi za Viongozi wa Kitaifa, au zinasubiri ziara za viongozi hao.

                  Nawasihi Viongozi wa Mikoa na Halmashauri, tena tembeleeni vijijini na mtatue kero za wananchi huko vijijini, aidha, hakikisheni Mikutano ya Vijiji iliyowekwa kwa mujibu wa Sheria inasimamiwa utendaji wake na maazimio yake yanafika kwenye vikao halali vya Maamuzi. Waheshimiwa Wabunge, ninyi ni sehemu ya Halmashauri zenu, nawasihi toeni msukumo unaostahili kwa suala hili.

  Mwisho: Mipango ya maendeleo nchini na jitihada za wananchi kujikwamua na umaskini, vitafanikiwa endapo tutaendelea kuwa na umoja na kudumisha amani na utulivu. Hivyo, kila mmoja wetu aendelee kuwa mlinzi wa amani na kuhamasisha ufanyaji kazi kwa bidii na maarifa;

  HITIMISHO:

  52.        Mheshimiwa Spika, tunaahirisha Bunge lako Tukufu tukiwa na habari njema kwenye tasnia ya michezo ambazo zinatupa nguvu na hamasa ya kuendelea kufuatilia na kuhamasisha uwekezaji kwenye shughuli za michezo na burudani kama moja ya maeneo ya kutengeneza ajira kwa vijana wetu. Kwanza, mwezi Januari, 2017 Mtanzania mwenzetu Alphonce Felix Simbu, aliibuka mshindi kwa kunyakua medali ya dhahabu kwenye mashindano ya riadha ya Dunia ya Mumbai Marathon. Pili, Mtanzania Nasib Abdul, maarufu kama Diamond Platnumz, alipata heshima ya kutumbuiza kwenye ufunguzi wa Fainali za Kombe la Afrika lililomalizika hivi karibuni nchini Gabon, na mwisho, lakini sio mwisho kwa umuhimu, Timu ya Taifa ya Vijana walio chini ya umri wa miaka 17 (Serengeti Boys) imefuzu kwenye Fainali za Kombe la Afrika kwa vijana walio chini ya Umri wa Miaka 17 zitakazofanyika nchini Gabon tarehe 2 – 16 April, 2017. Nitambue juhudi za Bunge Sports Club kuwa ni miongoni mwa timu zilizoshiriki mashindano nchini Kenya. Tuwapongeze waheshimiwa wabunge kwa ushiriki na ushindi wenu na makombe mliyoyaleta.  Ikumbukwe kuwa mwaka huu 2017, Tanzania tutakuwa wenyeji wa mashindani ya mabunge ya Afrika Mashariki. Tupate nafasi ya kujiandaa vizuri na niwaombe wabunge wote tushiriki na hatimaye tuunde timu imara ya Bunge letu. Nitumie Bunge lako Tukufu kuwapongeza wachezaji, Benchi la Ufundi la Bunge Sports Club na Serengeti, TFF na wengine wote waliofanikisha timu zote hiyo kufikia hatua hiyo.

  53.        Mheshimiwa Spika vijana wa Serengeti Boys wametimiza wajibu wao na kwa hakika wametutoa kimasomaso kwa kufikia hatua hiyo. Natoa rai kwa Watanzania wote kote ulimwenguni kuiunga mkono timu yetu ili iweze kushindana kikamilifu. Nalishauri Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) liwe na maandalizi mazuri na ya mapema, ili Serengeti Boys isiwe mshiriki tu, bali itoe ushindani na kuchukua kombe hilo. Aidha, TFF itumie mashindano hayo kama chachu ya kuongeza msukumo katika soka nchini. Binafsi sifurahishwi sana kuona Taifa letu lenye vipaji lukuki vya michezo ikiwemo soka na riadha ikiwa nyuma Afrika Mashariki.

  54.        Mheshimiwa Spika, nihitimishe hotuba yangu, kwa kuwaombea Waheshimiwa Wabunge muwe na safari njema mnaporejea majimboni kwenu. Mwenyezi Mungu awajaalie na siha njema katika kipindi chote mtakachokuwa majimboni ili muweze kuchukua maoni ya wananchi mnaowawakilisha kwa lengo la kufikisha maoni yao kwenye Mkutano ujao, ambao utakuwa ni mahsusi kwa ajili ya Bajeti.  

  55.        Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo, napenda kutoa hoja kuwa Bunge lako Tukufu sasa liahirishwe hadi tarehe 4 Aprili, 2017, siku ya Jumanne, Saa 3:00 asubuhi litakapokutana katika ukumbi huu hapa Dodoma.


  56.        Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

  0 0


  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro(kulia) akimkabidhi Kompyuta mpakato bwana Buyamba Ngogeja kwa niaba ya wasaidizi wa kisheria katika kituo cha usaidizi wa kisheria wilaya ya Kishapu.Laptop hizo zimetolewa na shirika mama la Usaidizi wa Kisheria la Legal Service Facility (LSF) la lenye makao makuu yake jijini Dar es salaam.

  Mgeni rasmi katika kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mradi wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia na Elimu Kwa Watoa Msaada wa Kisheria katika wilaya ya Shinyanga na Kishapu mkoani Shinyanga,Josephine Matiro akizungumza katika kikao hicho.
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza katika kikao hicho cha wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia wilaya ya Shinyanga na Kishapu ambapo aliwataka wananchi kuwa wanajitokeza kutoa ushahidi katika kesi kutokana na kuwepo taarifa kuwa kesi nyingi zimekuwa zikishindwa kuendelea kutokana na ushahidi kukosekana.
  Mkurugenzi wa shirika la PACESH Perpetua Magoke akizungumza wakati wa kikao hicho ambapo alisema shirika lake limekuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa mkoa wa Shinyanga dhidi ya ukatili wa kijinsia.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la PACESH,Mchungaji Paul Mpanda akizungumza katika kikao hicho ambapo alisema ni wakati mzuri sasa wananchi wakabadilika na kutoa taarifa kuhusu vitendo vya ukatili vinavyofanyika katika familia zao na jamii kwa ujumla
  Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la PACESH,Mchungaji Paul Mpanda akisisitiza jambo ukumbini Wadau wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea


  0 0   Mkurugenzi wa Fedha na Utawala (PSPTB) Bw. Paul Bilabaye akifunga mafunzo ya wanafunzi waliofikia  Level 5 wanaotarajiwa kufanya mitihani ya Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi kwa niaba ya Kaimu  Mkurugenzi Mtendaji  wa bodi hiyo Godfred Mbanyi  katika Warsha ya siku tano ya Mafunzo  ya  Utafiti iliyondaliwa na Bodi hiyo, ambapo kila mwanafunzi amepangiwa msimamizi wa utafiti wake na baadaye utafiti wao utapimwa kitaalaam na  utawawezesha kufuzu katika taaluma ya Ununuzi na Ugavi wa Umma baada ya Kupata cheti cha kitaaluma cha (CPSP)
  Mafunzo hayo yalikuwa yakifanyika kwenye jengo la Taasisi ya Elimu ya watu wazima jijini Dar es salaam ambapo wanafunzi hao sasa watakwenda kufanya utafiti wao katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
  0001
  01
  Mkurugenzi wa Fedha na Utawala (PSPTB) Bw. Paul Bilabaye akimkabidhi zawadi ya kikombe mmoja wa wanafunzi Sosera Mokiri aliyeshinda bahati nasibu katika ufungaji wa mafunzo hayo Katikati  Amani Ngonyani Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo (PSPTB)
  1
  Mkurugenzi wa Fedha na Utawala (PSPTB) Bw. Paul Bilabaye akimkabidhi zawadi ya kikombe mmoja wa wanafunzi Grace Peter  aliyeshinda bahati nasibu katika ufungaji wa mafunzo hayo, Kulia ni Shamim Mdee Afisa Mwandamizi  Mahusiano ya Umma na Masoko. (PSPTB) na katikati ni Amani Ngonyani Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo (PSPTB)
  3
  Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakipokea vyeti vyao kutoka kwa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala (PSPTB) Bw. Paul Bilabaye katikati ni Amani Ngonyani Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo (PSPTB) na kushoto ni Bi. Shamim Mdee Afisa Mwandamizi  Mahusiano ya Umma na Masoko. PSPTB
  456
  Mkurugenzi wa Fedha na Utawala (PSPTB) Bw. Paul Bilabayekatikati  akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa zawadi hizo kutoka kulia ni Grace Peter , Gastor Masawe na kushoto ni Sosera Mokiri.
  07
  Mkurugenzi wa Fedha na Utawala (PSPTB) Bw. Paul Bilabaye katikati na Amani Ngonyani Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo (PSPTB) wakifurahia jambo wakati Bi. Shamim Mdee Afisa Mwandamizi  Mahusiano ya Umma na Masoko (PSPTB) alipokua akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo.
  7
  Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza Mkurugenzi wa Fedha na Utawala (PSPTB) Bw. Paul Bilabaye.
  8910
  Amani Ngonyani Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo (PSPTB) akitoa shukurani zake kwa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala (PSPTB) mara baada ya kufunga mafunzo hayo kulia ni Bi. Shamim Mdee Afisa Mwandamizi  Mahusiano ya Umma na Masoko. (PSPTB)

  0 0

  Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma.

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kwamba vita inayopiganwa sasa dhidi ya uagizaji, uzalishaji, usambazaji na matumizi ya dawa ya kulevya ni kubwa na kila Mtanzania anapaswa kuunga mkono jitihada hizo.

  Kassim Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Bungeni, Mjini Dodoma katika hotuba yake ya kuahirisha mkutano wa sita wa Bunge la Kumi na Moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  “Moja ya eneo lililojadiliwa na kuibua hisia kali ni kuhusu vita inayoendelea nchini dhidi ya dawa za kulevya. Watanzania wote ni mashahidi kwamba vijana wetu wengi wameendelea kudhoofisha afya zao kutokana na matumizi ya madawa ya kulevya. Dawa za kulevya ni hatari kwa usalama na ustawi wa Taifa,” alifafanua Waziri Mkuu.

  Aliendelea kwa kusema kuwa kitaalamu madhara ya kiafya yanayosababishwa na matumizi ya dawa za kulevya ni pamoja na kuathirika kwa mfumo wa fahamu kwa mtumiaji ikiwemo kuchanganyikiwa, kuwa na ulevi usioponyeka kirahisi na kusababisha vifo ikiwa mtumiaji atazidisha matumizi ya dawa hizo.

  Aidha Waziri Mkuu amesema kuwa madhara ya kiuchumi yanayosababishwa na magonjwa hayo ni pamoja na kuwatibu waathirika wa dawa za kulevya, gharama kubwa za uchunguzi wa kimaabara kwenye maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali pamoja na watumiaji wa dawa za kulevya kushindwa kujisimamia na kuendesha maisha yao.

  Amesema kuwa madawa hayo huingia nchini kwa kutumia bandari bubu kupitia Bahari ya Hindi na kwa njia ya magari binafsi kupitia mipaka ya nchi ya Kenya, Uganda na mpaka wa Tunduma.

  Kassim Majaliwa amesema kuwa lengo la Serikali ni kuwasaidia walioathirika na dawa hizo na kuwachukulia hatua kali wale waliowaathiri kwa maana ya wauzaji na wasambazaji.

  Amewashukuru wabunge kwa kutoa mchango mkubwa na ushauri wa namna nzuri zaidi ya kupambana na janga hilo ikiwa dhamira ya Serikali ni kupambana na janga hilo kwa dhati bila kumuonea mtu yeyote na kwa kuzingatia misingi ya sheria na haki.

  Kassim Majaliwa ametoa takwimu ya Watanzania ambao wamefungwa katika magereza mbalimbali nje ya Tanzania, ikiwa ni pamoja na Watanzania 200 ambao wamefungwa China, Watanzania 12 nchini brazil, Watanzania 63 nchini Iran, Watanzania 7 nchini Ethiopia na Watanzania 296 ambao wamefungwa Afrika ya Kusini.

  0 0


  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  Timu ya Azam FC, imetia nanga mkoani Pwani, tayari kabisa kwa ajili ya mchezo wa kesho wapinzani wao Ruvu Shooting utakaofanyika kesho katika Uwanja wa Mabatini mkoani humo.

  Mchezo huo nunaotarajiwa kupigwa majira ya saa 10 Alasiri utakuwa wanushindani mkubwa sana hasa baada ya Azam kukumbuka sare ya mechi ya awali iliyomalizika kwa goli 2-2.

  Kikosi cha Azam FC kimeondoka jana kikiwa na morali kubwa ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo kutokana na mazoezi makali wanayopewa chini ya benchi la ufundi linaloongozwa na Mromania, Aristica Cioaba, Msaidizi wake, Idd Cheche na Kocha Makipa, Idd Abubakar.

  Akizungumza kuelekea mchezo huo, Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Nassor Cheche, amesema kuwa wanakwenda huko kuendeleza wimbi lao la ushindi kwa kuichapa Ruvu Shooting.

  “Tunawaheshimu wapinzani wetu, tunajua upinzani wanaotuonyeshaga kila tunapokutana, lakini tumejipanga kufanya vizuri, rungu lililotumika kuua tembo ndilo litakalotumika kuua sisimizi, tunawaomba mashabiki wetu wasubirie kufurahi,” alisema.

  Hadi hivi sasa Azam FC imefanikiwa kujikusanyia jumla ya pointi 37 katika nafsi ya tatu kwenye msimamo ikilingana kwa pointi na Kagera Sugar iliyochini yake, inazidiwa pointi 12 na kinara Yanga aliyejikusanyia 49 na Simba iliyonafasi ya pili nazo 48.

  Msafara wa Azam FC umeondoka na jumla ya wachezaji 21, ambao ni makipa Aishi Manula, Mwadini Ally, Metacha Mnata, mabeki ni Aggrey Morris, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Yakubu Mohammed, Bruce Kangwa, Gadiel Michael, Ismail Gambo, Abdallah Kheri. 

  Viungo ni Nahodha Msaidizi Himid Mao, Frank Domayo, Mudathir Yahya, Masoud Abdallah, mawinga Joseph Mahundi, Khamis Mcha, Ramadhan Singano na washambuliaji Yahaya Mohammed, Samuel Afful na Shaaban Idd.

  Wachezaji wengine waliobakia wameachwa kwa sababu mbalimbali, nahodha John Bocco, Salum Abubakar, Stephan Kingue, Daniel Amoah, wakiwa ni wagonjwa, huku winga Enock Atta Agyei kibali chake cha uhamisho kikiwa bado hakijawasili nchini.

older | 1 | .... | 1135 | 1136 | (Page 1137) | 1138 | 1139 | .... | 1897 | newer