Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

BREAKING NEWZ: RAIS MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA UJENZI WA TERMINAL III UWANJA WA NDEGE WA JULIUS NYERERE JIJINI DAR JIONI HII


UKAGUZI WA MABASI KATIKA I KITUO CHA UBUNGO WAPAMBA MOTO , ABIRIA WAPONGEZA UKAGUZI WA MABASI

$
0
0
Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii.

Abiria wa walioshushwa  katika basi la Shukurani Coach linalofanya safari zake Dar kuelekea mikoa ya Kusini wamesema ukaguzi unaofanyika katika kituo cha mabasi ubungo ni mzuri kwani safari yao isingekuwa  nzuri kama wangeweza kupita bila kukaguliwa.

Akizungumza na Michuzi Blog, Shinza Lymo amesema kuwa utaratibu wa ukaguzi kabla ya basi kondoka uendelee kwa wamiliki watakuwa hawapeleki basi katika kituo hicho na kuwa wameweepusha abiria na ajali zinazotokana na uzembe.

Nae Halima Bakari amesema kuwa katika siku ambayo hatasahau ni kuzuiwa kwa basi hilo ambapo leo kitu ambacho kingetokea ni makosa ya watu kushindwa kufanya matengenezo ya mabasi wakati yanaingia katika kituo hicho .

Amesema jeshi la polisi wamekuwa makini katika kuhakikisha wanaokoa roho za watu ambao wanasafiri na vyombo vya moto hasa mabasi ya mikoani ambayo basi moja linabeba roho 100.

Kwa upande wa dereva Simwanzi Minja amesema kuwa jeshi la polisi limenyoosha wamiliki wa mabasi ambao hawataki kupeleka mabasi  yao Gereji na kituo  cha ukaguzi wa mabasi  cha ubungo kinazua safari.
Amesema kuwa kutokana na ukaguzi huo ajali zimepungua zinazotokana na mabasi mabovu kubaki matatizo ya kibinadamu ambayo nayo yamedhibitiwa ipasavyo.

Chami amesema kuna siku alimwambia mmiliki wa basi kuwa basi lake linamatatizo alikata na kuamuka kuita polisi kufanya ukaguzi ili walizuie kufanya safari kabla hajafanyiwa ukaguzi akiwa na abiria.
Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Geita Mponjoli Mwabulambo akipata maelezo  kwa Mkuu wa Usalama Barabarani  Kituo cha Mabasi ya Mikoani cha  Ubungo, Ibrahim Samwix a juu ya ukaguzi wanaofanya kabla ya mabasi hayo kuondoka kuelekea mikoani  alipofika kituo hicho kwa shughuli za kawaida.Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
 Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo akimueleza Mkuu wa Usalama Barabarani  Kituo cha Mabasi ya Mikoani cha  Ubungo, Ibrahim Samwix  juu ya utaratibu wanaoufanya katika ukaguzi wa magari na kuwapongeza kwa hatua wanazozichukua kwa basi itakayoonekana na tatizo leo jijini Dar es Salaam.
 Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Geita ,Mponjoli Mwabulambo akiangalia ukaguzi unaofanywa katika kituo cha mabasi ubungo kabla ya mabasi hayo hayajaanza safari leo jijini Dar es Salaam na Basi hilo ni Shukrani  Coach ambalo limezuiliwa kufanya safari zake leo baada ya kubaini usukani wake hauko leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Usalama Barabarani  Kituo cha Mabasi ya Mikoani cha  Ubungo, Ibrahim Samwix akikagua injini ya basi kabla halijaanza safari zake leo ubungo jijini Dar es Salaam.
 .Abiria akilalamikia kurudishiwa nauli katika basi alilotaka kusafiri nalo leo ambalo limerudishwa kituoni  kutokana na kuwa na matatizo  kwenye injini yake kabla halijaanza safari zake leo ubungo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Usalama Barabarani  Kituo cha Mabasi ya Mikoani cha  Ubungo, Ibrahim Samwix aking’oa namba za usajili katika basi CM  Millenium  linalofanya safari za Dar es Salaam  kuelekea Mtwara baada ya kubaini basi hilo linatatizo  na baadae baadae limekufa injini yake kabla halijaanza safari zake leo ubungo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Usalama Barabarani  Kituo cha Mabasi ya Mikoani cha  Ubungo, Ibrahim Samwix   (katikati) akitoa maelekezo kwa askari wake leo katika kituo cha ubungo jijini Dar es Salaam.







NIC WAPIGANA MSASA MOROGORO

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikala Bima la Taifa (NIC) Sam Kamanga akizungumza katika mkutano wa Mameneja wa NIC uliofanyika Morogoro jana.Kushoto ni Romanious Hokororo, Kaimu Mkurugenzi wa Bima za Ajali na Mali .
Baadhi ya Mameneja wa Shirika la Bima la Taifa NIC wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Sam Kamanga (hayupo Pichani) wakati wa mkutano wa Mameneja wa NIC uliofanyika Morogoro jana.

SERIKALI YA UHOLANZI YAAGIZA AINA 14 ZA MBEGU ZA VIAZI NCHINI

$
0
0
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Programu ya Kuendeleza Kilimo Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT), Bw.Geoffrey Kirenga  akisisitiza  jambo wakati wa warsha ya siku moja juu ya zao la viazi nchini na namna ya kuliongezea thamani. Kushoto ni Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT, Bi. Jennifer Baarn, wapili kushoto ni Mshauri Mwandamizi wa Kimataifa  wa maswala ya Mbegu toka Uholanzi,Bw.Jos van Meggelen na kulia ni Kaimu Mthibiti Mkuu wa Mbegu toka Taasisi ya Udhibiti wa Mbegu nchini(TOSCI),Dr.George Swella. Warsha hiyo iliwakutanisha wadau wa kilimo cha viazi toka Tanzania na Serikali ya Uholanzi.
 Baadhi ya washiriki waWarsha  iliyowakutanisha wadau wa kilimo cha viazi toka Tanzania na Serikali ya Uholanzi wakifurahi kwa kushikana mikono kuashiria ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika kukuza na kuliongezea thamani zao la viazi nchini. Warsha hiyo ilifanyika Mkoani Morogoro katika ukumbi wa Taasisi ya Uthibiti wa Mbegu Nchini(TOSCI).
 Afisa kilimo toka ubalozi wa Uholanzi Nchini,Bi.Theresia Mcha(kulia) akijadiliana jambo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Programu ya Kuendeleza Kilimo Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT), Bw.Geoffrey Kirenga mara baada ya kumaliza warsha ya siku moja juu ya zao la viazi nchini na namna ya kuliongezea thamani. Kushoto ni Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT, Bi.Jennifer Baarn na wapili kushoto ni Mkuu wa maendeleo ya kongani toka SAGCOT, Bi. Maria Ijumba. Warsha hiyo iliwakutanisha wadau wa kilimo cha viazi toka Tanzania na Serikali ya Uholanzi.
Baadhi ya washiriki wa Warsha iliyowakutanisha wadau wa kilimo cha viazi toka Tanzania na Serikali ya Uholanzi wakiwa katika picha ya pamoja. Walijadili pia namna ya kukuza na kuliongezea thamani zao la viazi nchini. Warsha hiyo ilifanyika Mkoani Morogoro katika ukumbi wa Taasisi ya Uthibiti wa Mbegu Nchini(TOSCI).

Na Mwandishi Wetu, Morogoro.

SERIKALI ya Uholanzi imeingiza nchini aina 14 ya mbegu za viazi kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa zao hilo na kuboresha maisha ya wakulima kupitia mradi wa kuboresha zao la viazi nchini.

Akizungumza katika kikao cha ufunguzi wa mradi huo kilichofanyika mkoani Morogoro katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) jana, Mshauri wa Kilimo wa Ubalozi kwa nchi za Kenya na Tanzania, Bw. Bert Rikken alisema nchi yake imeona Tanzania ina nafasi kubwa ya kuongoza uzalishaji wa viazi kutokana na ukubwa wa ardhi na hali ya hewa.

Bw. Rikken alibainisha wameamua kuingiza mbegu hizo ili kuongeza uzalishaji kwa sababu wakulima wanazalisha chini ya tani nane hadi 10 kwa hekta, hivyo ujio wa mbegu hizi utasaidia kuongeza uzalishaji na kufikia tani 40 kwa hekta.

“Mbegu hizi ni nzuri kwa matumizi mengi, viazi vyake vina ladha nzuri na vinaweza kutumika kutengeneza chips au bidhaa nyingine zitokanazo na viazi ambazo zinaweza kusafirishwa nje ya nchi. Mradi huu ulianza kwa kutiliana saini mawaziri wa kilimo kutoka Tanzania na Uholanzi mwaka 2016 ili kuruhusu mbegu kuingia nchini ili kupata ithibati,” alisema Rikken.

Mradi huo wa miaka mitatu utakaogharimu kiasi cha Euro 388,000 sawa na Sh milioni 700, utahakikisha Tanzania inapata mbegu mpya za zao hilo na kutoa mafunzo kwa taasisi zinazojihusisha na kilimo nchini ili kuongeza uzalishaji.

Kwa upande wake Kaimu Mthibiti Mkuu wa Mbegu kutoka Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu (TOSCI), Dkt. George Swella kazi yao kubwa ni kuhakikisha mradi unafanikiwa kwa kusimamia mchakato wa kupima mbegu zilizoingizwa nchini kutoka Uholanzi ili kujua kama zinaendana na mazingira ya Tanzania.

“Awali tulipokea mbegu tatu ambazo zilipitia mchakato mzima wa maabara hadi shambani, majibu ni mazuri na sasa zimeshasambazwa kwa wakulima tunasubiri uzalishaji. Mbegu hizo majina yake ni Jelly, Rumba na Sagitta. Baada ya matokeo hayo tumeletewa mbegu nyingine 11 ambazo bado zipo kwenye mchakato, jumla inakua mbegu 14 kutoka Uholanzi,” alisema Dkt. Swella.
Akizungumzia faida za ujio wa mbegu hizo Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao kutoka Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi, Twahir Nzallawahe alisema kwa sasa Tanzania imekua na matumizi makubwa ya viazi hasa kwa Chips, hivyo haja ya kuongeza uzalishaji ni wazo muafaka kwa kipindi hiki.

“Viazi mviringo ni zao muhimu kwa uchumi na mustakabali wa usalama wa chakula nchini, mchango wa viazi mviringo kwa Watanzania wa Nyanda za Juu Kusini na Kaskazini ni mkubwa hasa katika mnyororo wa kuongeza thamani kwa sababu mahitaji ya zao hili ni makubwa kutokana na ongezeko la walaji wa chips mayai na chips kuku.

“Tumeona ipo haja ya kuwekeza kwenye ulimaji na utayarishaji wa zao hilo ili kuongeza wingi na ubora, mwanzo wa zao lolote ili uongeze wingi na ubora kwa haraka tunaanza na mbegu. Kwa hiyo huu mradi mzima ambao leo tunauzindua unaangalia uwezekano wa kuingiza mbegu kutoka Uholanzi, wenzetu wamepiga hatua katika kilimo cha vaizi mviringo na hasa ni wasafirishaji wakubwa wa mbegu za viazi duniani,” alisema Nzallawahe na kuongeza:

“Uzalishaji ukiwa mkubwa maana yake tunakaribisha wawekezaji zaidi kutoka nje, mfano mdogo mgahawa wa Mc Donald hauwezi kuwekeza katika nchi isiyokuwa na uhakika wa upatikanaji wa viazi bora, hivyo hatuna sababu ya hoteli kubwa kuendelea kuagiza viazi kutoka nje ikiwa uwezo wa kuzalisha zao hilo kwa wingi na ubora wa hali ya juu tunao.”

Kwa upande wake Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mpango wa Kuendeleza Kilimo Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT), Jennifer Baarn aliwahakikisha wajumbe waliohudhuria mkutano huo wanaahidi kutoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha mradi unafanikiwa.

“Tumevutiwa na mradi huu na upo ndani ya uwezo wetu kuhakikisha unafanikiwa, bila kuchelewa tutaitisha kikao cha wadau wa kilimo kujadiliana kuhusiana na viazi lakini pia tutawasiliana na taasisi za kifedha ili kutafuta namna ya kuwawezesha wakulima wadogo kupata mitaji ya kulima viazi,” alisema Jennifer.

Kwa muda mrefu wakulima wa viazi nchini wamekuwa wakitegemea mbegu zilizoandaliwa kienyeji hadi ilipofika mwaka 2013 Serikali ya Finland ilipofanikiwa kuingiza aina nne ya mbegu ambazo ni Asante, Sherehekea, Tengeru na Meru.

BREAKING NEWZZZ:ASKOFU GWAJIMA ATII AGIZO LA MAKONDA,ATINGA KITUO CHA POLISI KATI NA WAFUASI WAKE MCHANA HUU

$
0
0
 Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,Mchungaji Gwajima akiwasili kituo cha polisi kati majira ya saa 7:30 mchana akiwa ameongoza na wafuasi wake,kutii agizo la Mkuu wa Mkoa Paul Makonda,ambaye watuhumiwa wote 65 aliowataja jana katika sakata la dawa za kulevya,aliwataka kufika kesho Ijumaa saa 5 asabuhi kituo cha Polisi kati kwa mahojiano zaidi.
 Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,Mchungaji Gwajima akiwasili kituo cha polisi kati majira ya saa 7:30 mchana akiwa ameongoza na wafuasi wake,kutii agizo la Mkuu wa Mkoa Paul Makonda,ambaye watuhumiwa wote 65 aliowataja jana katika sakata la dawa za kulevya,aliwataka kufika kesho Ijumaa saa 5 asabuhi kituo cha Polisi kati kwa mahojiano zaidi.
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,Mchungaji Gwajima akionekana kufurahia jambo wakati akiwasili kituo cha polisi kati majira ya saa 7:30 mchana akiwa ameongoza na wafuasi wake,kutii agizo la Mkuu wa Mkoa Paul Makonda,ambaye watuhumiwa wote 65 aliowataja jana katika sakata la dawa za kulevya,aliwataka kufika kesho Ijumaa saa 5 asabuhi kituo cha Polisi kati kwa mahojiano zaidi.
 Wafuasi wa Askofu Gwajima wakiwa wanawasili kituo cha Polisi kati 
 Polisi wakiwatawanya wafuasi hao wa Askofu Gwajima na kuwataka  kukaa umbali wa mita 100 kutoka kituo cha Polisi 
Wafuasi wa Askofu Gwajima wakiwa wamekaa umbali wa mita 100 kutoka kituo cha Polisi kama walivyoamriwa na Polisi.

CAG KUCHUNGUZA MAPATO YA SHIRIKA LA NDEGE TANZANIA-MAJALIWA

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema atamuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuchunguza ukusanyaji wa mapato ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL).

Ametoa kauli hiyo leo (Alhamis, Februari 9, 2017) alipotembelea Makao Makuu ya shirika hilo Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujionea mwenendo wa uendeshaji wake.

“Nitamuagiza CAG aje aangalie mwenendo wa ukusanyaji wa mapato ya shirika hili kuanzia mwaka jana lilipoanza kufanya kazi hadi sasa,” amesema.

Waziri Mkuu amesema Serikali haiko tayari kuona shirika hilo linakufa tena, hivyo amewataka viongozi wake wahakikishe linaendeshwa kwa mafanikio kwa manufaa ya Taifa. 

Pia amewataka waache kukusanya mapato kwa kutumia risiti za kuandika kwa mkono na badala yake waanze kutumia mfumo wa kieletroniki ili kuzuia upotevu wa mapato hayo.

“Vitu vingi vinavyoenda manual ni rahisi kufa. Serikali tumeagiza malipo yote yafanyike kielektroniki na kote tunakotumia mfumo huu tumepata mafanikio,”amesema.

Katika hatua nyinginre, Waziri Mkuu amemtaka Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Bi. Witness Mbaga ajiridhishe na fedha zinazokusanywa katika eneo la mizigo kama ziko sahihi, lengo ni kudhibiti upotevu wa mapato.

Hata hivyo Waziri Mkuu amewataka viongozi wa shirika hilo kuhakikisha wanazingaria ratiba ya njia na muda wa safari ili wasipoteze wateja.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
S. L. P. 980,
DODOMA.
ALHAMIS, FEBRUARI 9, 2017

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) wakati alipokwenda kwenye Ofisi kuu ya ATCL kufuatilia mwenendo wa uendeshaji wa Shirika na usimamizi wa mapato , Februari 9, 2017. Kushoto kwake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano, Profesa Makame Mbarawa na kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa ATCL, Mhandisi Ladislaus Matindi (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) wakati alipokwenda kwenye Ofisi kuu ya ATCL kufuatilia mwenendo wa uendeshaji wa Shirika na usimamizi wa mapato , Februari 9, 2017. Kushoto kwake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano, Profesa Makame Mbarawa na kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa ATCL, Mhandisi Ladislaus Matindi (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) wakati alipokwenda kwenye Ofisi kuu ya ATCL kufuatilia mwenendo wa uendeshaji wa Shirika na usimamizi wa mapato , Februari 9, 2017. Kushoto kwake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano, Profesa Makame Mbarawa na kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa ATCL. Mhandisi Ladislaus Matindi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Regini Masoud (kulia) kuhusu mfumo mpya wa ukusanyaji mapato kwa njia ya kielektroniki wakati alipotembelea ofisi kuu ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) jijini Dar es salaam kufuatilia mwenendo wa uendeshaji wa Shirika na usimamizi wa mapato, Februari 9, 2017. Kushoto kwake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano, Profesa Makame Mbarawa na kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa ATCL, Mhandisi Ladislaus Matindi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Regini Masoud (kulia) kuhusu mfumo mpya wa ukusanyaji mapato kwa njia ya kielektroniki wakati alipotembelea ofisi kuu ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) jijini Dar es salaam kufuatilia mwenendo wa uendeshaji wa Shirika na usimamizi wa mapato, Februari 9, 2017. Kushoto kwake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano, Profesa Makame Mbarawa na kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa ATCL, Mhandisi Ladislaus Matindi (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NEWZ ALERT: WATUHUMIWA 17 WA DAWA ZA KULEVYA WAKAMATWA SHINYANGA,MAJINA MENGINE ZAIDI YA 20 YAPO KWA DC SHINYANGA

$
0
0
Vita dhidi ya dawa za kulevya imetua mkoani Shinyanga ambapo jumla ya watu 17 wanaotuhumiwa kuwa ni watumiaji wa dawa hizo ikiwemo unga na mirungi wanashikiliwa na jeshi la polisi wilaya ya Shinyanga. 

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro,ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya hiyo amesema mbali na watu 17 kushikiliwa na polisi pia ofisi yake imepokea majina zaidi ya 20 ya watu wanaodaiwa kujihusisha na dawa za kulevya. 

“Mheshimiwa Rais ametangaza kuwa hii ni vita ya nchi nzima,baada ya wananchi kusikia vita ya dawa za kulevya ikiendelea mkoani Dar es salaam,wametuletea majina zaidi ya 20 ya watu wanaojihusisha na dawa za kulevya,wanasema wanaunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali kupiga vita dawa hizi”,amesema Matiro. 

“Wananchi wenyewe kwa moyo mweupe kabisa ndiyo wametuletea majina ya watu wanaotumia na kuuza dawa za kulevya ikiwemo unga na mirungi,kamati ya ulinzi na usalama tumeunda kikosi kazi cha kushughulikia majina yanayoletwa ili kubaini kama ni kweli wanajihusisha na dawa za kulevya”,alisema Matiro. 

Ametumia fursa hiyo kulipongeza jeshi la polisi kwa jitihada zake dhidi ya dawa za kulevya na kufanikisha kukamata watuhumiwa 17 huku akikisisitiza kuwa vita hiyo siyo ya Dar es salaam pekee bali inatakiwa kufanyika nchi nzima kwani watumiaji na wauzaji wa dawa hizo wapo kila mahali nchini. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akitoa taarifa kwa waandishi wa habari leo (hawapo pichani) Alhamis Februari 9,2017 kuhusu kukamatwa kwa watuhumiwa wa dawa za kulevya katika wilaya ya Shinyanga-Picha na Kadama  Malunde-Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akielezea jinsi wananchi wa wilaya hiyo waliamua kuchukua hatua ya kupeleka majina ya watumiaji na wauzaji wa dawa za kulevya wilayani humo
Mkuu wa polisi wilaya ya Shinyanga Dotto Mdoe akielezea kuhusu kikosi kasi walichounda kufuatilia majina ya watu wanaotajwa kuhusika na dawa za kulevya wilayani humo
******
Msikilize hapa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumzia watuhumiwa wa dawa za kulevya wilayani Shinyanga.

BARAZA LA VIONGOZI WA DINI LAUNGA MKONO JITIHADA ZA MAKONDA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Na Dotto Mwaibale

BARAZA la Viongozi wa dini la kupambana na dawa za kulevya Tanzania ambalo liko chini ya Tume ya kupambana na dawa za kulevya  limeunga mkono jitihada zinazofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda za kupambana na watu mbalimbali wanaotumia dawa za kulevya.

Katika hatua nyingine baraza hilo limeiomba serikali  kumuongezea ulinzi Makonda  kwa kuthubutu kutaja watu wanaojihusisha kwa namna moja au nyingine na dawa hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum ,alisema Makonda anapaswa kuongezewa ulinzi kutokana na ujasiri aliouonesha wa kuthubutu kuwataja kwa majina watu hao.

"Sisi kama baraza tunapinga vita na kulaani hatua yoyote ya kushiriki katika biashra au utimiaji wa dawa za kulevya kwa kuwa matumizi ya dawa hizo yamekuwa ni kikwazo kikubwa cha maendeleo katika nchi yetu na yanapotokea nguvu kazi ya Taifa kwa vile wahanga wakubwa wa matumizi ya dawa hizi ni vijana"alisema.

Alisema kutokana na ugumu wa kazi hiyo aliyoianzisha baraza hilo linamuombea kwa mwenyezi mungu ili ampe ulinzi wake na kinga yake na azidi kumpa moyo wa ujasiri wa kupambana na maovu yote yanayo haribu sifa ya Taifa letu na vijana kwa ujumla.

Salum alisema hivi sasa Makonda ameshanza kutengenezewa majungu, fitina na uzushi mbalimbali ili kumkatisha tamaa na aonekane mbaya kwa watanzania lakini hawatafanikiwa endapo atamtanguliza mwenyezi mungu katika mapambano hayo.

Alisema inawezekana wanaopinga au kubeza juhudi hizo ni kwa sababu tu madhara ya dawa za kulevya hayajawagusa wao na familia zao hivyo hawana uchungu na watanzania wenzao walioathirika hivyo wapuuzwe badala yake wasimame pamoja kama watanzania dhidi ya vita hiyo.

Mwenyekiti huyo wa baraza hilo alitumia fursa hiyo kuwaomba viongozi wengine waige mfano wa Makonda wa kupambana na uovu huo mkubwa ambao ni janga kwa Taifa kwani Tanzania bila dawa za kulevya inawezekana.
 Mwenyekiti wa Baraza la Viongozi wa Dini la Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania, Sheikh Alhad Mussa Salum.
 Mwenyekiti wa Baraza la Viongozi wa Dini la Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania, Sheikh Alhad Mussa Salum (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu baraza hilo kuunga mkono jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda za  kupambana na wanaojihusisha na dawa za kulevya. Kulia ni Katibu wa Baraza hilo, Padre John Solomon.
 Baadhi ya viongozi wa dini (waliokaa), wakiwa kwenye mkutano huo. Wengine ni wanahabari.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.

ASKOFU GWAJIMA ALIPOZUNGUMZA NA WANAHABARI JUU YA KUTAJWA KWAKE SAKATA LA DAWA ZA KULEVYA

$
0
0


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
ASKOFU wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josepahat Gwajima amesema kuwa ameokoka na anamtumikia mungu hivyo kutajwa katika orodha ya wanaojihusisha na dawa za kulevya iliyotangazwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ni jambo ovu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Askofu  Gwajima amesema kuwa Mkoa wa Dar es Salaam anafanya kazi vizuri lakini suala la kiutawala hawezi na kumuomba Rais Dk. John Pombe Magufuli ambadilishie kazi.

Amesema yeye alikuwa Mpwapwa  katika kazi zake aliposikia kutajwa kwa jina lake na kumlazimu arudi na kuwasili pale alipoitwa bila kusubiri siku iliyopangwa ya kukutana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Askofu  Gwajima amesema kuwa kuhusu mali anazomiliki ni kutokana na kazi anazofanya ikiwa kuwa na kampuni mbalimbali pamoja na kufundisha masuala ya farsasafa nje nchi na kulipwa dola za kimarekani 1000 kwa saa.

Aidha amesema kuwa kulindwa kwake ni kutokana na kuwa na usalama wake hata papa ana gari ambayo haipiti risasi wakati ni mtakatifu.
Askofu Gwajima amesema Makonda anachuki na wivu dhidi yake ndio maana anamhusisha na jambo ovu ambalo linamchafu mbele ya mungu.
Amesema kuwa yuko radhi kukaa ndani miaka 40 kutokana na kupigania suala la uovu ni jambo halitawe za kuvumiliwa.
 Askofu  wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josepahat Gwajima akizungumza na waandishi wa habari juu ya  kutajwa kwao kujihusisha na dawa za kulevya leo jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
 Katibu Mkuu wa Kanisa  la Ufufuo na Uzima, Gwandu Mwangasa akizungumza na waandishi wa habari juu watavyopambana na katika kupigania Askofu wake Josephat Gwajima leo jijini Dar es Salaam.
 Asikofu  wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josepahat Gwajima akitoka katika mkuna na kuelekea kituo  Kikuu cha polisi leo jijini Dar es Salaam.
Asikofu  wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josepahat Gwajima akiagana na waumini wa kanisa hilo leo jijini Dar es Salaam.

BAADA YA KUSOTA NDANI SIKU 7 WEMA AACHIWA KWA DHAMANA

$
0
0
Wema Sepetu akishuka katika gari ya Polisi huku pembeni Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu akipunga mkono akitokea katika gari hiyo kwa mbele.

Na Karama Kenyunko,Globu ya Jamii.

Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu imewaachia kwa dhamana msanii maarufu nchini Wema Sepetu na wenzake wawili baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili ambaye kila mmoja atasaini bondi ya Sh milioni tano.

Baada ya kutimiza masharti hayo, Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo Thomas Simba aliwataka washitakiwa kuhakikisha hawaruki dhamana waliyotakiwa na kuhakikisha wanafika mahakamani hapo kila wanapohitajika.

Hata hivyo, aliwataka mawakili wa serikali kukamilisha upelelezi haraka ili kesi hiyo ifike mwisho. Mbali na wema washtakiwa wengine ni Angelina Msigwa ambaye ni mfanyakazi wa ndani na Matrida selemani Abas ambaye ni Mkulima.

Wote watatu wanashtakiwa na kosa la kukutwa na kiasi kidogo cha madawa ya kulevya chini ya kifungu cha sheria namba 17 (1)(b) cha sheria inayodhibiti matumizi ya dawa za kulevya.

Kwa mujibu wa kifungu hicho, iwapo Wema na wenzake watapatikana na hatia basi watatakiwa kulipa faini isiyozidi sh.laki tano au kwenda jela.

Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa serikali Nassoro Katuga aliyekuwa akisaidiana na Wakili Pamela Shinyambala walidai kuwa Wema na wenzake watatu walitenda kosa hilo tarehe 4 February mwaka huu, huko nyumbani kwao Kunduchi Ununio.

Ilidaiwa kuwa, siku hiyo walikutwa wakiwa na msokoto mmoja pamoja na vipisi viwili vya banfi vyenye gramu 1.80. Hata hivyo washtakiwa wote wamekana mashtaka.

Akielezea hali ya upelelezi wakili Katuga alidai "mheshimiwa Hakimu, upelelezi wa shauri hili bado haujakamilika tunasubiri taarifa kutoka kwa Mkemia Mkuu ambayo tunategemea kuipata hivi karibuni".

Hakimu Simba aliwapa washtakiwa masharti ya dhamana ambapo mahakama ilimtaka kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili watakao weka dhamana na milioni tano. Mshtakiwa Wema na Wenzake walitimiza masharti ya dhamana na kesi hiyo itatajwa tena mahakamani hapo February 22 mwaka huu.

Nje ya Mahakama Umati wa watu na wasanii mbali mbali walijaa nje kumlaki Wema akitoka mahakamani baada ya kutimiza masharti ya dhamana.
Wema Sepetu akitolewa kutoka mahabusu ya Hakimu Mkazi Kisutu
Wema Sepetu akishuka katika ngazi za Mahakama ya Hakimu mkazi kisutu mara baada ya kuamuriwa apte dhamana ya mahakama.
Weme sepetu akipanda kwenda kusaini hati ya Dhamana kwa hakimu mkazi wa Mahakama ya Kisutu
Wema akishuka katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu 
Wema Sepetu akiwa nje na kwa dhama akiwa ameongozana na wakili 
Wema akirudi mahabusu ya hakimu mkazi kisutu akiwa chini ya ulinzi
Meneja wa Wema, Martin Kadinda  akitoka mahakamani
Baadhi ya wasanii waliofika mahakamani hapo
Mama wema akiwa naingia mahakamani

MKUU WA MKOA WA MWANZA AONGOZA MAZISHI YA MZEE ANTON R. KAYOMBO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe John Mongela akizungumza wakati wa mazishi
 Marehemu Mzee Antony Raphael Kayombo wakati wa uhai wake
 Rc Mongela akimpa pole Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda akimpa pole MD Kayombo.

Na Mathias Canal, Mwanza

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe John Mongela ameongoza mamia ya wananchi waliojitokeza kijijini Misasi, Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza kwa ajili ya kusindikiza safari ya mwisho ya kurejea mavumbini kwa utimilifu wa vitabu vitakatifu vya Dini Mzee Anton Raphael Kayombo.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe John Mongela akiteta jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Ndg Eliud Mwaiteleke kulia ni Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda akisaini kitabu cha wageni kabla ya mazishi
  Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Ally Happi akisaini kitabu cha wageni kabla ya mazishi
 Rc Makonda akiaga mwili wa marehemu Mzee Kayombo

Rc Mongela alisema kuwa kifo cha Mzee Kayombo kimeacha alama kubwa Duniani kwa ufanisi mkubwa alioufanya akiwa hai ambapo pia ni alama kubwa ya taswira ya fikra huru zitakazoishi kwa Yale aliowaasa wananchi katika maelekezo mbalimbali ikiwemo ushauri katika serikali.

Mongela aliyeambatana na mkewe katika mazishi hayo amewapongeza wananchi wote kwa kujitokeza mwenye mazishi hayo sambamba na kuwasihi kuendelea kutoa mshikamano kwa serikali katika majukumu mbalimbali ikiwemo kusimamia na kudumisha umoja waliouonyesha katika mazishi ya Mzee Kayombo.

 Dc Happi akiaga mwili wa marehemu Mzee Kayombo
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe Benjamini Sitta akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kijijini Misasi
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda alisema kuwa Mkoa wa Mwanza umepoteza mtu muhimu ambaye atakumbukwa kwa kazi njema alizozifanya wakati wa uhai wake ikiwemo kuwa mlezi bora wa familia yake na hatimaye kupatikana kwa kiongozi bora na mwenye weledi katika utendaji kazi. 


Akizungumza kwa niaba ya kundi la mtandaoni (Watsup) la The Impossible is Impossible Bwana Steve Nyerere ametoa pole kwa Mkurugenzi wa Ubungo Ndugu John Lipesi Kayombo kwa kuondokewa na Mzee wake ambaye ni Mlezi wake tangu akiwa mdogo sambamba na kuwasihi wananchi kuendeleza mshikamano na kupendana.
 Rc Makonda akitoa salamu za pole kwa niaba ya Viongozi wengine alioambatana nao kutoka Jijini Dar es salaam
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akitoa salamu za shukrani akiwa na Mkewe

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo alisema kuwa Mzee wake Hugo atakumbukwa kwa mambo mbalimbali aliyoyafanya wakati wa uhai wake pindi alipokuwa kazini ikiwa ni pamoja na kupanda miti katika shule zote alizofundisha, Ujenzi wa shule wakati huo, pia atakumbukwa kwa kuhamasisha ujenzi wa Zahanati ya Misasi.

Ameeleza kuwa Marehemu Mzee Antony Raphael Kayombo alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kibofu cha mkojo ambao ulianza ghafla tarehe 29/1/2017 na kupelekwa katika hospital ya Misasi, Baadae hospitaliti ya Sekou Ture na mwishowe Hospitali ya Bugando ambapo alifanyiwa upasuaji ambapo hata hivyo hali yake iliendelea kudhoofika mpaka mauti ilipomkuta tarehe 4/2/2017 majira ya saa mbili usiku.
 Mkurugenzi wa Asasi isiyokuwa ya Kiserikali ya METDO Tanzania (Mining and Environmental Transformation for Development  Organization) Bw Ashraf Omaryakisaini kitabu cga wageni

Muwakilishi wa kundi la mtandaoni (Watsup) la The Impossible is Impossible Bwana Steve Nyerere akitoa salamu za pole kwa niaba ya wajumbe wa kundi hilo

 Rc Mongela akiaga mwili wa marehemu Mzee Kayombo
Akizungumza kwa niaba ya wakurugenzi wote nchini Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Kiyomondi Kibamba alisema kuwa msiba huo umekuwa pigo kwa familia ya Kayombo na ukoo mzima lakini pia ni pigo kwa wananchi wote wa Kijiji cha Misasi na Mkoa wa Mwanza kwa ujumla kwa kumpoteza mlezi na mshauri mzuri.

MD Kayombo amewashukuru madaktari wa hospitali zote waliojaribu kuokoa uhai wa Mzee Raphael Kayombo hata hivyo ameeleza kuwa idadi kubwa ya watu waliohudhuria Kwenye mazishi imeonyesha kwamba Marehemu Mzee Kayombo alikuwa na mahusiano na kuishi vizuri na majiraji zake.

Marehemu Mzee Antony Raphael Kayombo ameacha watoto10, Wajukuu 60 na Vitukuu 30 huku kukiwa na idadi kubwa ya vilembwe.




Wizara yapokea msaada wa vifaa vya kufanyia mkutano kwa njia ya video.

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz P. Mlima akipokea baadhi ya vifaa vya kuwezesha kufanya Mkutano kwa njia ya video kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bi. Awa Dabo Wizarani Jijini Dar es Salaam 
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz P. Mlima akiwa katika mzungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja Bi. Awa Dabo mara baada ya makabidhiano ya vifaa vya kufanyia mkutano kwa njia ya video 
Kutoka kulia, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji wa Wizara Bi. Mindi Kisiga, Mkurugenzi wa Kitengo cha Ugavi Bw. Manyama M. Mapesi na Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy wakifuatilia zoezi la makabidhiano 
Zoezi la Makabidhiano likiendelea .


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Wizara yapokea msaada wa vifaa vya kufanyia mkutano kwa njia ya video.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz P. Mlima leo amepokea msaada wa vifaa vya kufanyia mkutano kwa njia ya video (Video Conference Facilities) kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (United Nations Development Programme – UNDP). 

Baada ya kupokea msaada huo, Balozi Mlima aliishukuru UNDP kwa msaada huo ambao alieleza kuwa utasaidia shughuli za Wizara katika ofisi mpya ya Wizara mjini Dodoma. Alisema msaada huo ni wa pili kwa Wizara katika muda mfupi ambapo awali UNDP ilitoa ngamizi, printers na cameras. 

“Tunamshukuru Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy ambaye ndio alianzisha suala hili na kuongea nanyi na kulisimamia bila kuchoka hadi leo vifaa vinapatikana” “Kwa kweli ni mtu ambaye wakati wote anapenda mambo anayoyasimamia yanatokea” Katibu Mkuu alimwambia Mkurugenzi wa UNDP nchini Tanzania, Bi. Awa Dabo. 

Kwa upande wake Bi. Dabo baada ya kukabidhi msaada huo, alisema kuwa mazungumzo kuhusu maombi ya msaada huo yalianza tokea mwaka 2014 lakini kwa uwezo wa mungu vifaa hivyo leo vimekabidhiwa rasmi Wizarani. Alielezea matumani yake kuwa vifaa hivyo vitachangia kwa kiasi kikubwa utendaji kazi wa Wizara na pia utaboresha na kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano kati ya Serikali na UNDP.


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 09 Februari 2017.
 

TCRA YAZIPIGA PINI MICHUZI TV, AYO TV NA GLOBAL TV, YAANDAA KANUNI ZAA USAJILI WA TV MTANDAO ZOTE

$
0
0
Na Sultani Kipingo, Globu ya Jamii.
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezitaka Michuzi TV, AYO TV na Global TV kusitisha huduma zao za TV mtandaoni hadi hapo kanuni za usajili rasmi ambazo mamlaka hiyo imesema inaandaa  kwa huduma hizo zitapokuwa tayari. 
Barua hiyo, iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu Mhandisi James Kilaba tarehe 30 January mwaka huu, imevitaka vyombo hivyo ambavyo vinapendwa sana nchini na nje ya nchi kuacha mara moja kutoa huduma za TV mtandaoni.
"Kwa mujibu wa section 13 (1) of the electronic and postal communications Act Cap 306, sheria za Tanzania zinahitaji watoa huduma zozote za aina hiyo wanahitaji leseni kutoka mamlaka ya mawasiliano", imesema barua hiyo.

Wamiliki wa mitandao hiyo - Millard Ayo, Ankal Issa Michuzi na Abdallah Mrisho -  wameeleza kushtushwa kwao kwa agizo hilo la ghafla, tena wakati hata kanuni zenyewe hazijawekwa.     
         
"Gloval TV ipo tayari hata leo kukamilisha taratibu za usajili - kama zingekuwepo - na kwa sababu bado kukamilika tunaomba kupewa muda zaidi chini ya uangalizi wakati tunasubiria kanuni hizo mpya," alisema Abdallah Mrisho, Meneja Mkuu wa Global Publishers.
Ankal Michuzi na Millard  Ayo waliunga mkono kauli hiyo na kwa pamoja watatu hao wameomba kuonana na mkurugenzi wa TCRA ili kuwasilisha maombi rasmi ya kuruhusiwa kuendelea kutoa huduma hiyo kwa muda wakati kanuni zikisubiriwa. 
Bahati mbaya Mhandisi Kilaba alikuwa safari na swala hilo limepangwa kushughuliwa ataporejea wiki ijayo."Ukizingatia kwamba tumekuwa tunatoa huduma hii kwa muda mrefu na haijulikani kanuni zitakuwa tayari lini tunaomba TCRA iangalie namna ya kufanya ili wananchi wanaotutegemea sana wasikose huduma hii", alisema Ankal. 

Hata hivyo vituo hivyo vitatu vinaendelea kuhudumu nje ya mchakato wa TV mtandao.
Ayo TV, Michuzi TV na Global TV,  ambazo zinaongoza kwa mbali kwa kutazamwa na watu wengi nchini na nje ya nchi, ni TV mtandao pekee zilizoitikia mwito wa TCRA, kati ya vituo mtandao  takriban 51 vilivyopata barua hiyo.

Ankal Issa Michuzi wa Michuzi TV, Millard Ayo na Askofu wa Ayo TV na Abdallah Mrisho wa Global TV wakitoka makao makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano walikoitwa kuchukua barua zao zinazowazuia kuendelea kutoa huduma za TV mtandao hadi hapo kanuni za usajili na leseni utapokamilika.

LADY IN RED 2017 KUTIKISA JIJI LA DAR, NDANI YA KING SOLOMONI HALL JUMAMOSI HII!

$
0
0

Ni siku chache tu! zimesalia kuikamata Tarehe 11 mwizi huu 2017, kumbuka siku hiyo ni siku pendwa ya Wanamitindo wa hapa Tz, coz wanategemea kukutatishwa kwenye Big Fashion Show ambayo hufanyika kila mwaka yaani hapa naizungumzia “Lady In Red”.


Muandaaji wa show hiyo Mama wa mitindo maarufu kama Asya Idarous Khamsin, akizungmza na wabahabari Jana Tarehe 8/2/2017 huku akiwa ameambatana na wanamitindo wengine amesema kuwa,

“Kwanza Show hii ni yakipekee pia inafaida kubwa sana kwa upcoming Designers, Lady in red huwa inatoa kipaumbele kwa upcoming Designers kuweza kuonesha kazi zao jukwaani, hivyo mwaka huu 11/2/2017 mambo yatakuwa mazuri sana ndani ya King Solomoni Hall”.

Hivyo kwa wadau wote wapenzi wa mitindo mnaombwa kuhudhuria usiku huo ili sanaa ya mitindo iweze kukua zaidi Asante.
Wanamitindo wakiwa kwenye Press ya Lady In Red 2017


Asya Idarous
Picha ya pamoja ya wanamitindo baada ya Press ya Lady In Red 2017























WAKURUGENZI, WATENDAJI WAKUU SERIKALINI KUELEZA UTEKELEZAJI


WAZIRI UMMY MWALIMU ALIPOZINDUA BODI YA HOSPITALI YA MIREMBE-DODOMA

MHANDISI WA UJENZI MKOA ASIMAMISHWA KAZI

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa huo wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya awali ya uchunguzi gharama za ujenzi wa Hospitali ya Mkoa
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini akizungumza na watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa huo wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya awali ya uchunguzi wa gharama za ujenzi wa Hospitali ya Mkoa.
Baadhi ya Watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Katibu Tawala Mkoa huo, Ndg.Jumanne Sagini wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya awali ya uchunguzi wa gharama za ujenzi wa Hospitali ya Mkoa.


Na Stella Kalinga

Mhandisi wa Ujenzi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Simiyu, Deusdedit Mshuga amesimamishwa kazi kwa kukabiliwa na mashtaka matatu.

Akizungumza na watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa, Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg. Jumanne Sagini amesema Mhandisi huyo anashtakiwa kwa kushindwa kutekeleza majukumu aliyopewa kwa kiwango cha kuridhisha.

Amesema akiwa mtumishi wa umma kinyume na kipengele cha 8 cha sehemu"A" ya jedwali la kwanza la kanuni za Utumishi wa Umma, Tangazo la Serikali Na.168/2003; mtumishi huyo alishindwa kuandaa makadirio ya gharama za ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa yenye uhalisia.

Aidha , Aliandaa makadirio ya Tsh46,106,456,000 yaliyosomwa mbele ya Mhe. Rais tarehe 11 Januari,2017 ambayo ni ya juu kuliko uhalisia. 

Shtaka la pili linalomkabili ni kufanya uzembe mkubwa wakati wa utekelezaji wa majukumu ya kazi iliyopewa kinyume na kipengele cha 13 cha sehemu "A" ya jedwali la kwanza la Kanuni za Utumishi wa Umma,Tangazo la Serikali na 168/2003;

Alitaja (1) kuandaa makadirio ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa Tshs.46,106,456,000 hali iliyosababisha Mhe Rais kusomewa taarifa ya gharama zisizo na uhalisia na(2) Kuandaa michoro ya taswira (3 D)isiyoendana na michoro halisi ya Hospitali ya Mkoa iliyooneshwa mbele ya Mhe.Rais

Shtaka la tatu ni kufanya kazi kwa kukiuka maadili ya taaluma yake wakati wa utekelezaji ya kazi aliyopewa kinyume na kipengele cha 14 cha Sehemu "A" ya Jedwali la kwanza la Kanuni za Utumishi wa Umma, Tangazo la Serikali Na.168/2003:- kwa (1) Kuandaa makadirio ya shilingi 46,106,456,000 ya gharama za ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa bila kuzingatia mita za mraba za eneo, michoro na kusababisha gharama kubwa zisizo na uhalisia

(2) Kuandaa makadirio ya shilingi 3,009,640,000 yasiyo na uhalisia ili kugharamia ujenzi wa majengo ya msingi kuwezesha Hospitali kuwa "functional" kwa kupiga simu Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida.

Katibu Tawala wa Mkoa, Ndg..Jumanne Sagini ametoa wito kwa watumishi wa Umma mkoani humo kutekeleza majukumu waliyopewa kwa bidii, weledi na uadilifu ili kuepuka makosa ambayo husababisha watumishi kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

“Nikiwa kama mwajiri nimesikitishwa na kufadhaishwa na wataalam walioajiriwa ngazi ya mkoa kuishauri Sekretarieti ya Mkoa na kuzisimamia Mamlaka za Serikali za Mitaa na kuzishauri kitaalam, kutenda matendo yanayodhihirisha upungufu wa weledi, kushindwa kutekeleza majukumu na uzembe mkubwa” alisema.

Naye Mkuu wa Mkoa huo,Mhe. Anthony Mtaka amesema gharama zilizowasilishwa awali na wataalam hazikuwa na mchanganuo toshelevu na makisio hayakuwa na uhalisia, hivyo amemwomba radhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli, kwa taarifa za upotoshaji zilizotolewa na wataalam wakati wa ziara yake Mkoani humo. 

“....kuna vitu vingine vilivyopachikwa kwenye ramani, wenye taaluma yao walipokutana ili kujustify hiyo bilioni 46.1 walishindwa kujustify kwenye ramani, kwa hiyo hatukuwa na uhalisia; baada ya mapitio ya kazi zote ilionekana Hospitali ya Mkoa wa Simiyu inaweza kujengwa kwa gharama ya bilioni 11.4 mule mule alimosema Rais” alisema Mtaka.

Makadirio ya awali ya Ujenzi wa Hospitali ya Mkoa yalikuwa ni shilingi bilioni 46.1 na gharama hii haikukubaliwa na Mhe.Rais na badala yake akaagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa kutembelea TBA Makao Makuu, ili kujifunza na kuona jinsi walivyoweza kujenga majengo ya hosteli ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa gharama ndogo ya shilingi bilioni 10 na akaahidi kutoa bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali hiyo.

Agizo la Rais Magufuli la kuendelea kwa ujenzi wa jengo jipya la Uwanja wa Ndege latekelezwa

$
0
0
 Shughuli za Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 3) ukiendelea mbele ya Jengo jipya la Abiria kama inavyoonekana pichani kufatia ziara ya kushtukiza  ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyofanya hapo jana na kutoa Maagizo kwa Mkandarasi wa Uwanja huo kuanza kazi mara moja kuanzia leo.
 Kazi ya Umwagiliaji ikiendelea katika sehemu ya mbele ya ya Jengo jipya la Abiria kama inavyoonekana pichani.
 Mmoja wa Mafundi akiendelea kazi ndani ya jengo hilo la Abiria uwanjani hapo.
 Mafundi Umeme wakiendelea na kazi ndani ya jengo hilo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 3).
 Mafundi wakiendelea na ujenzi wa Moja ya nguzo katika jengo hilo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 3).
 Mafundi wakiendelea na ujenzi wa sehemu ya chini ya maegesho ya ndege kama inavyoonekana.
 Mafundi wakiendelea na ujenzi sehemu ya juu ya jengo hilo la Abiria kama inavyoonekana.
Sehemu ya mbele ya jengo hilo la Abiria kama linavyoonekana. 

MAKONDA AONGEZEWE ULINZI-SHEIKH ALHAD MUSSA SALUM

RAIS SHEIN AONGOZA SHEREHE ZA KILELE CHA SIKU YA SHERIA ZANZIBAR

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu (kushoto) mara alipowasili katika viwanja vya ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi  Mnazi mmoja Mjini Unguja leo katika sherehe za Siku ya Sheria Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizindua kitabu cha Sheria ya Mwaka 2015 katika sherehe za Siku ya Sheria Zanzibar zilizofanyika leo katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi  Mnazi mmoja Mjini Unguja,(kushoto) Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akinyanyua kitabu cha Sheria ya Mwaka 2015 baada ya kukizindua   rasmi leo katika sherehe za Siku ya Sheria Zanzibar zilizofanyika katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi  Mnazi mmoja Mjini Unguja,(kulia) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora (kushoto) makamo wa Pili wa Rais balozi Seif Ali Iddi akifuatiwa na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake kwa Majaji,Mahakimu na wafanyakazi wakati wa sherehe za Siku ya Sheria Zanzibar zilizofanyika leo katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi  Mnazi mmoja Mjini Unguja,ambapo ujumbe wa mwaka huu unasema "SIMAMIA SHERIA NA MAADILI KATIKA UTENDAJI HAKI" (Picha na Ikulu).
  Baadhi ya Mahakimu na wafanyakazi wa idara ya Maahakama Zanzibar wakiwa katika sherehe ya kilele cha Siku ya Sheria Zanzibar zilizofanyika leo katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi  Mnazi mmoja Mjini Unguja,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)
 Baadhi ya Viongozi mbali mbali waliohudhuria katika sherehe ya kilele cha Siku ya Sheria Zanzibar zilizofanyika leo katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi  Mnazi mmoja Mjini Unguja,akiwepo jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania Mohamed Chande Othman (wa pili kulia)
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images