Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1132 | 1133 | (Page 1134) | 1135 | 1136 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ataongoza mazishi ya viongozi wa CCM, waliofariki juzi, kwa ajali ya gari wakati wakitoka kwenye maadhimisho ya miaka 40 ya CCM, mkoani Kilimanjaro.

  " Misiba hii ni mikubwa sana na yenye kuhuzunisha, kwa hiyo nitakiwakilisha Chama, katika mazishi yote ya viongozi wetu hawa kuonyesha jinsi walivyokuwa muhimu kwa Chama", amesema Kinana wakati akisafiri kutoka Mjini Dodoma kwenda Arusha ambako atalala na kesho kwenda mkoani Kilimanjaro kuanza kuongoza mazishi hayo.

  Kulingana na taratibu ilizopatiwa ofisi ya Katibu Mkuu wa CCM kutoka CCM mkoa wa Kilimanjaro, mazishi ya viongozi hao yatafanyika kwa siku tatu tofauti kuanzia kesho ambapo Mjumbe wa NEC wilaya ya Same, marehem Ally Mbaga atazikwa Usangi, Mwanga kesho  Februari 8, 2017 kuanzia saa tisa alasiri.

  Taarifa ya taratibu hizo imesema, aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (VCCM) Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Anold Swai, atazikwa Masama Mashariki katika kijiji cha Mboyera, Februari 10, 2017, kuanzia saa 8 mchana na aliyekuwa Katibu wa Hamasa wa Shirikisho la Vyuo Vikuu Mkoa wa Kilimanjaro, Edwin Msele atazikwa eneo la Ukaoni Moshi Vijijini Februari 11, 2017 kuanzia saa tisa alasiri.

  Kulingana na taarifa hiyo ya taratibu za mazishi ya viongozi hao, mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa UWT Tawi la Chuo Kikuu cha Ushirika (Moshi) Anastazia Mslamsha, utaagwa kesho Februari 9, 2017, kuanzia asubuhi kwenye Chuo hicho na baadaye kwenda kuzikwa Rombo siku hiyo hiyo alasiri.

  Katika ajali hiyo, watu saba wakiwemo viongozi hao na wanachama wanne wa CCM, walikufa baada ya gari aina ya Toyota Hilux walilokuwemo kugongwa kwa nyuma na gari la mizigo la aina Fuso, lililokosa breki katika eneo la Mwika, Wilaya ya Moshi Vijijini, Mkoa wa Kilimanjaro, siku ya Jumapili ya Februari 5,  2017.

  Viongozi na wanachama hao walikuwa wakitoka katika kutekeleza majukumu ya Chama ya Maadhimisho ya Miaka 40 ya Kuzaliwa kwa CCM yaliyofanyika kimkoa Wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro.

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam,Paul Makonda amewataja watuhumiwa 65 wa Dawa za Kulevya,katika majia hayo ametajwa Freeman Mbowe,Mchungaji Gwajima,Yusuf Manji,Idd Azzan.
   
  Akizungumza na waandishi wa habari Ofisi kwake mapema leo jijini Dar,RC Makonda ameingia katika awamu ya pili ya kutaja majina hayo na kuyaweka hadharani,huku akieleza kuwa watuhumiwa hao watatakiwa kufika kituo cha polisi kati siku ya Ijumaa,saa tano asubuhi kwa mahojiano zaidi.

  Katika hatua nyingine RC Makonda amekiri kukamatwa kwa Mmiliki wa kituo cha Radio ya EFM,ajulikanae kwa jina la Francis Ciza,almaarufu kwa jina la Dj Majay."tulipokuwa tukifanya opereseheni ya kuwakamata Wahusika weote wa Dawa za kulevya juzi usiku nae akakamatwa kw mahojiano zaidi;"alisema Makonda.

  Makonda amejibu habari za kukamatwa kwa Dj Majay mara baada ya kuulizwa swali na mmoja wa waandishi wa habari,kufuatia tetesi nyingi zilizokuwa zikisambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii 


  0 0

  Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

  Serikali imetolea ufafanuzi juu ya swala la michezo ya kubahatisha kuwa  ni moja ya shughuli za kiuchumi, zinazoendeshwa kwa mujibu wa sheria kama shughuli zingine. Aidha michezo yote ya kubahatisha ikiwemo Kamari (slots machines) inaendeshwa kwa mujibu wa Sheria ya Bodi ya Michezo ya Kubahatiba Namba 4 ya mwaka 2003, Sura 41 pamoja na Kanuni zake.

  Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt Ashatu Kijaji, wakati akijibu maswali ya Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Asha Abdullah Juma, aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa kudhibiti mchezo wa kamari ambao amesema huwakosesha amani wazazi na jamii nzima, kwa kuchangia uvunjifu wa maadili na nguvu kazi ya vijana inayopotea kwa kucheza kamari badala ya kushiriki katika uzalishaji.

  Aidha, Dkt Kijaji, amesema kuwa kwa mujibu wa sheria, hakuna mtu au taasisi inayoruhusiwa kuendelesha biashara ya Michezo ya Kubahatisha bila kuwa na leseni kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha pamoja na vibali vingine vinavyotolewa na mamlaka zingine za biasahra. Vilevile , sheria inakataza watoto wenye umri chini wa miaka 18 kushiriki, kuingia, kukaa au kuzururazurura karibu na maeneo ya michezo ya kubahatisha.

  “Mtu yeyote atakaye ruhusu mtoto chini ya miaka 18 kushiriki, kuingia au kukaa karibu na eneo la Mchezo wa Kubahatisha, anahesabika kafanya kosa na anastahili kulipia faini ya shilingi 500,000/- au kifungo  kisichopungua miezi mitatu au vyote kwa pamoja” aliongeza Dkt. Kijaji

  “endapo kosa hilo litafanywa na mwendesha mchezo wa kubahatisha, Bodi ina mamlaka kisheria kumfutia leseni. Hivyo basi, wajibu wa Serikali ni kuzuia watoto na vijana walio chini ya miaka 18 kucheza michezo ya kubahatisha. Natoa rai kwa wazazi na walezi kuwazuia wao kucheza michezo hiyo” alisisitiza Dkt. Kijaji

  Amewataka wote wanaoendesha michezo ya kubahatisha wazingatie sheria na kanuni zilizowekwa, huku akiwaangaliza wazazi na walezi na jamii kwa ujumla ihakikishe kuwa vijana  wanazingatia mila na desturi zinazolinda maadili ya Kitanzania kwa kujishughulisha na shughuli halali za kiuchumi.

  0 0

  Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa kuhusu mfumuko wa bei wa mwezi Januari 2017 jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Meneja Idara ya Takwimu za Ajira na Bei, Ruth Minja.
  Waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.
  Wanahabari wakiwa kazini.
  Mkutano na wanahabari ukiendelea.  Na Dotto Mwaibale


  MFUMUKO wa Bei wa mwezi Januari 2017 unaopimwa kwa kipimo cha mwezi umeongezeka kwa asilimia 0.8 ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 0.7 ilivyokuwa mwezi Desemba 2016.

  Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakati akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

  "Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 105.92 mwezi Januari 2017 kutoka 1-05.04 mwezi Desemba 2016" alisema Kwesigabo.Alisema kuongeza kwa fahirisi za bei kumechangiwa na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula.

  Alitaja baadhi za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi ni pamoja na mahindi kwa asilimia 6.3, ndizi za kupika kwa asilimia 5.8, magimbi kwa asilimia 5.3 na viazi vitamu kwa asilimia 6.5.

  Alisema kwa upande mwingine baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilichochangia kuongezeka kwa fahirisi ni pamoja na mkaa kwa asilimia 3.2 na majokofu kwa asilimia 2.4.Kwesigabo alisema thamani ya shilingi ya Tanzania hupima badiliko la uwezo wa shilingi ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma zilezile za mlaji ambazo shilingi ya Tanzania ingeweza kununua katikavipindi tofauti.

  "Ikiwa fahirisi za bei za Taifa zinaongezeka, uwezo wa shilingi ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma hupungua" alisema Kwesigabo.Alisema uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia shilingi 94 na senti 42 mwezi Januari, 2017 ikilinganisha na shilingi 95 na senti 20 ilivyokuewa mwezi Desemba 2016.

  0 0


  JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
  KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO

  Simu ya Upepo  : “N G O M E”        Makao Makuu ya Jeshi,
  Simu ya Mdomo: DSM 22150463    Sanduku la Posta 9203,
  Telex                   : 41051                      DAR ES SALAAM, 07 Februari, 2017.
  Tele Fax              : 2153426
  Barua pepe       : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
  Tovuti                  : www.tpdf.mil.tz


  Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linapenda kutoa ufafanuzi kuhusu uvaaji wa sare za Jeshi kwa viongozi wanajeshi wanaoteuliwa na kupewa madaraka mbalimbali nje ya Jeshi. Hivi karibuni kumekuwa na mjadala juu ya uhalali wa uvaaji wa sare hizo.

  Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linapenda kuwataarifu wananchi kuwa kulingana na kanuni za Majeshi ya Ulinzi juzuu ya kwanza, viongozi hao wanaruhusiwa kisheria kuvaa sare za Jeshi wanapokuwa wakitekeleza majukumu maalum, hivyo wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa viongozi hao waliopo katika maeneo yao.


  Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Uhusiano
  Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
  S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.
  Kwa Mawasiliano zaidi: 0756-716085

  0 0

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amekabidhi hati miliki za ardhi 1,361 kwa wakazi wa vijiji vya Hembeti na Dihombo wilayani Mvomero mkoani Morogoro.

  Waziri Lukuvi amegawa hati hizo na kuwasisitiza wananchi wa wilaya ya Mvomero kuhakikisha wanapata hati za umiliki wa ardhi pamoja na kuwataka viongozi wa vijiji kote nchini kuhakikisha wanakuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi ili kuepusha migogoro ya wakulima na wafugaji kuendelea katika maeneo yao.

  Pia amesema ili mwananchi aweze kujikimu kimaisha ahakikishe anazitumia hati miliki hizo za kimila kujiletea maendeleo na anaweza kuomba mkopo benki kwa kutumia hati hiyo ili kuendesha shughuli zake za kujipatia kipato kupitia eneo analomiliki kisheria.

  Nae Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe amewataka wananchi kuzitunza hati hizo walizokabidhiwa na kuyatumia mashamba yao waliyomilikishwa kwa kuyalima na sio kuyauza au kukodisha kwa watu wengine na wao kubaki masikini.

  Waziri Lukuvi pia alimtaka Mkuu wa mkoa wa Morogoro ayaainishe mashamba mengine makubwa yasiyoendelezwa na kugeuka kuwa mashamba pori ili amshauri Rais kuyafutia umiliki wa mashamba hayo na kurudishwa kwao ili kuweza kuwapa kaya maskini ambazo zinaishi katika maeneo ya hayo.

  Kazi hii ya upimaji wa maeneo na kutoa hati kwa wananchi ni katika mpango wa nchi wa matumizi bora ya ardhi,ambapo serikali imechangua Mkoa wa Morogoro kuwa wa Mfano katika upimaji wa ardhi na utahusisha nchi nzima kwa wapimaji wa ardhi kutumia vipimo vya kisasa zaidi ambavyo kwa kiasi kikubwa vipimo hivyo vitaweza kupima ardhi kwa kipindi kifupi na kila mtu kumiliki kipande cha eneo lake.

  Lukuvi alisema kuwa wakati wa kampeni mwaka 2015,Rais Dkt. John Magufuli alihaidi wazi kuwa kipindi cha miaka 10 kutakuwa na upimaji katika maeneo yote ya nchi kwa utaratibu wa mpango mzuri na wa kisasa, na kwa miaka mitano takribani vijiji 7,500  vitapimwa kwa kupangwa kila halmashauri 25 ambapo na kila mwaka vitapimwa vijiji 1,500 na kutoa hati. Alisema kuwa zoezi la upimaji linaloendelea hivi sasa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM)kwa wananchi katika kuondoa migogoro inayojitokeza.

  Na Hassan Mabuye (Kitengo cha Mawasiliano Serikalini - Wizara ya Ardhi)
      Mzee Ali Juma mkazi wa kijiji cha Hembeti wilayani Mvomero mkoani Morogoro akimshukuru Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi kumuwezesha kupata hati ya kumuliki ardhi yake ambayo amekuwa nayo kwa miaka mingi bila kupewa hati hiyo, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi ya Ardhi (NLUPC), Dkt. Stephen Nindi anayemsaidia kwa kumshika mkono.
    Bi. Zaina Hussein mkazi wa kijiji cha Dihombo wilayani Mvomero mkoani Morogoro akipokea hati ya kumuliki ardhi kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe.
    Bibi. Magret Hamis mkazi wa kijiji cha Hembeti akipokea hati ya kumuliki ardhi kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe.
    Baadhi wa wakazi wa vijiji vya Hembeti na Dihombo wilayani Mvomero mkoani Morogoro wakiwa hati zao za kumuliki ardhi mbele Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe.
   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiongea na wakazi wa vijiji vya Hembeti na Dihombo  na kuwataka wahakikishe wanazitumia hati miliki hizo za kimila kwa kujiletea maendeleo.
   Baadhi wa wakazi wa vijiji vya Hembeti na Dihombo wilayani Mvomero mkoani Morogoro wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi.
  Mwenyekiti wa Kijiji cha Hembeti wilayani Mvomero mkoani Morogoro Bwana Limbena Madela akimshukuru Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi kuwezesha wakazi wa kijiji chake kupata hati miliki hizo za kimila.

  0 0

  Katibu wa chama cha Walimu mkoa wa Ruvuma Shaibu Omary.

  Chama cha walimu mkoa wa Ruvuma kimepanga malengo mbalimbali ya mwaka huu wa 2017 ikiweo kutatua matatizo ambayo yanawakuta walimu pamoja na kuwawezesha kupata mikopo bila masharti yeyote.

  Hayo yamesemwa na katibu mkuu wa chama hicho SHAIBU OMARY wakati akizungumza na Ruvuma tv ofisini kwake.


  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  Matumizi ya simu ya mkononi huku akiwa ameshikiliwa na jeshi la Polisi ni moja ya mambo yalitajwa mtuhumiwa wa kesi ya Dawa za kulevya Wema Sepetu kuendelea kusota rumande.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,Mkuu wa Mkoa RC Makonda amesema kuwa, moja ya makosa katika nchi hii ni mtu akiwa yupo chini ya ulinzi halafu kuendelea kutumia simu ya mkononi.

  Amesema kuwa mrembo huyo ambaye alikuwa akituma Video na sauti mbalimbali kuhusu hali ya maisha akiwa mahabusu ya kituo cha kati huku akimkejeli mkuu wa mkoa huenda akaendelea kuwa katika wakati mgumu zaidi kutokana na kitendo hicho cha kutumia simu akiwa mahabusu.

  Makonda amesema kuwa  amezungumza na wakuu wa Magereza yote yaliyopo Dar es Salaam na wakuu wa mikoa juu ya vitendo vya watu kuingia na simu katika vituo vya Polisi.

  Pia amesema kuwa matumizi ya simu hizo watu wakiwa gerezani yamekuwa yakitumika kuendeleza biashara zao za dawa za kulevya kwa njia ya mawasiliano hata kama wakiwa ndani.

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bibi. Zamaradi Kawawa akizungumza wakati wa Mkutano baina ya waandishi wa habari, wawakilishi kutoka Kituo cha Utamduni cha Irani pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo leo jijini Dar es Salaam.Kituo cha utamaduni cha Iran kimeaandaa maonyesho ya utamaduni yatakayofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, kuanzia terehe 10 - 12 Februari kwa kuonyesha tamaduni kutoka Iran. Kutoka kulia Kutoka kushoto ni Msaidizi wa Kituo cha Utamaduni wa Iran nchini Tanzania Bibi. Fatma Ally, Mshauri wa Masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa Iran nchini Ali Bagheni na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Hajjat Shani Kitogo.
  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Hajjat Shani Kitogo (wa pili kutoka kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maonyesho ya Utamaduni wa Iran leo jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yanatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, kuanzia na terehe 10 - 12 Februari kwa kuonyesha tamaduni kutoka Iran. Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bibi. Zamaradi Kawawa, Mshauri wa Masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa Iran nchini Ali Bagheni na Msaidizi wa Kituo cha Utamaduni wa Iran nchini Tanzania Bibi. Fatma Ally.
  Mshauri wa Masuala ya Utamaduni kutoka Ubalozi wa Iran nchini Ali Bagheni akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya wiki ya utamaduni wa Iran inayotarajiwa kufanyika kuanazia tarehe 10 – 12 Februari leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Msaidizi wa Kituo cha Utamaduni wa Iran nchini Tanzania Bibi. Fatma Ally na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Hajjat Shani Kitogo.
  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bibi. Zamaradi Kawawa akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi kutoka Kituo cha Utamduni cha Iran walioambatana na wasanii kutoka Irani pamoja na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. 


  Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO.

  0 0


  Ofisa Mawasiliano ya Umma wa Benki ya KCB Tanzania Aziza Mkwizu, (aliyekaa kulia), Ofisa biashara wa benki ya KCB Tawi la Stone Town Zanzibar Lutfy Said (aliyekaa wapili kulia), Ofisa biashara wa Tawi la Stone Town Zanzibar wa Benki ya KCB, Rashid Mshana (aliyekaa wapili kushoto) na Ofisa mawasiliano ya Umma wa Benki hiyo Margaret Makere (aliyekaa watatu kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanawake wajasiriamali wa Zanzibar.
  Ofisa Biashara wa Tawi la Stone Town Zanzibar wa Benki ya KCB Tanzania, Rashid Mshana akimkabidhi mmoja wa wanawake wajasiriamali Bi. Rayyan Khelef cheti cha kushiriki semina ya mafunzo hayo. Meneja wa Tawi la Stone Town Zanzibar wa Benki ya KCB Tanzania Iddy Mwacha, akizungumza na wanawake wajasiriamali waliohudhuria semina ya mafunzo ya siku tatu kwa ajiri ya wanawake wajasiriamali inayoitwa 2JIAJIRI iliyoandaliwa na benki hiyo Kisiwani Zanzibar.
  Mwalimu wa ujasiriamali wa Kituo cha Uwezeshaji na Ushindani Tanzania (TECC) Seif Abdullah akizungumza na wanawake wajasiriamali wa Zanzibar.
  Mkurugenzi msaidizi wa Kituo cha Uwezeshaji na Ushindani Tanzania (TECC) Daniel Mghwira akitoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wajasiriamali Kisiwani Zanzibar.

  0 0

   Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea hati za utambulisho toka kwa Balozi wa Saudi Arabia nchini Mhe. Mohamed Ben Mansour Al Malek Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Fenruari 8, 2017.
   Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea hati za utambulisho toka kwa Balozi wa Morocco Mhe Abdellah Benryane Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Fenruari 8, 2017
    Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea hati za utambulisho toka kwa Balozi wa Zambia Mhe. Benson Keith Chali  Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Fenruari 8, 2017. 
   Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea hati za utambulisho toka kwa Balozi wa Cuba Mhe. Lucas Dominingo Hermandes Polledo  Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Fenruari 8, 2017
   Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea hati za utambulisho toka kwa Balozi wa Iran Mhe Mousa Farhang  Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Fenruari 8, 2017.
  Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea hati za utambulisho toka kwa Balozi wa  Burundi  nchini Mhe. Gervais Abayeho Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumatano Fenruari 8, 2017.PICHA NA IKULU

  0 0

  Vodacom Tanzania tunapenda kuwajulisha wateja wetu na wananchi wote kwa ujumla kuwa bado tunaendelea na zoezi letu la kuwapatia wateja wetu malipo ya faida ya kutumia M-Pesa ambayo tulianza mwezi Januari nakufanya yanaufanya mwanzo wa mwaka mpya kuwa mzuri zaidi kwa mamilioni ya wateja wetu na mawakala wa M-Pesa kwa ujumla.

  Akiongea na mtandao huu Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Jacquiline Materu alisema Mpaka sasa tumeweza kuwagawia wateja wetu kiasi cha shilingi Bilioni 6/- ikiwa hii ni awamu ya kwanza ya malipo ya faida ya utumiaji wa M-Pesa kutakuwa na awamu tatu za ugawaji wa fedha hizo ambapo awamu ya kwanza tayari imefanyika na awamu zingine zitaendelea mpaka mwezi wa tatu na kukamilisha zoezi zima la ugawaji wa billionii 32 kwa wateja wetu,Alisema Materu

  “Napenda kuwahakikishia wateja wetu wote kwa ujumla ya kana kwamba Malipo haya yanafanyika kwa awamu kwa hiyo wasiwe na wasiwasi kwani yatawanufaisha wateja na mawakala wa M-Pesa waliopo kila kona ya Tanzania,Ugawaji huu wa faida ya kutumia M-Pesa kwa wateja na mawakala wetu ni muendelezo wa dhana kuu ya mtandao wetu tuliojiwekea”,Alisema Materu.

  0 0

  Na Anthony John, Globu ya Jamii

  Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam , limesema Jalada la kesi ya kukutwa na bangi Msanii maarufu na Mlimbwende , Wema Sepetu bado linapitiwa na Mwanasheria wa Serikali na baada ya kukamilika kwa upelelezi atapelekwa mahakamani.

  Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi Simon Sirro amesema jeshi la polisi limeshafanya kazi yake hivyo taratibu za kisheria za kesi ya Msanii huyo zinaandaliwa kwa ajili ya kumfikisha mahakamani.

  Amesema katika mapambano ya dawa kulevya, wananchi na raia wema wameaswa kuacha kutoa habari za uvunjifu wa amani katika mkoa wa Dar es salaam,badala yake wajikite kutoa taarifa zilizokuwa za kweli.

  "Unapotoa taarifa ambazo si za kweli haumdanganyi kamishina Sirro ,unakuwa unalidanganya Jeshi la polisi ,kwa ujumla naomba raia wema waendelee kutoa taarifa lakini watoe taarifa za uhakika"amesema Sirro.

  Pia Siro ameongeza kuwa Jeshi la polisi limejipanga vizuri kwa kuwapokea watakao fika siku ya ijumaa lakini kikubwa wafike waje waripoti.

  0 0

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na Wajumbe wa Bodi aliyoizindua leo (hawapo pichani) pamoja na wageni waalikwa kwenye hafla ya Uzinduzi wa Bodi hito iliyofanyika Hospital ya Mirembe Mkoani Dodoma 08/02/2017. 
  Mwenyekiti wa Bodi Hospitali ya Mirembe, Prof. Gadi Kilonzo akiongea na Wajumbe wa Bodi ya Hospitali hiyo (hawapo pichani) pamoja na wageni waalikwa kwenye hafla ya Uzinduzi wa Bodi hito iliyofanyika Hospital ya Mirembe Mkoani Dodoma 08/02/2017. 
  Mganga Mkuu na Katibu wa Bodi ya Hospitali ya Miremb, Erasmus Mndeme akiongea na Wajumbe wa Bodi aliyoizindua leo (hawapo pichani) pamoja na wageni waalikwa kwenye hafla ya Uzinduzi wa Bodi hito iliyofanyika Hospital ya Mirembe Mkoani Dodoma 08/02/2017. 
  Mkurugenzi Msaidizi Hospitali ya Mirembe, Bibi. Doroth Gwajima akiongea na Wajumbe wa Bodi leo (hawapo pichani) pamoja na wageni waalikwa kwenye hafla ya Uzinduzi wa Bodi hito iliyofanyika Hospital ya Mirembe Mkoani Dodoma 08/02/2017. 
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimuakiwakabidhi vitendea kazi baadhi ya Wajumbe wa Bodi aliyoizindua leo wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Bodi hito iliyofanyika Hospital ya Mirembe Mkoani Dodoma 08/02/2017. 
  Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Hospitali ya Mirembe wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi leo 08/02/2017 mkoani Dodoma. 
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Hospitali ya Mirembe kwenye hafla ya Uzinduzi wa Bodi hito iliyofanyika Hospital ya Mirembe Mkoani Dodoma 08/02/2017. (PICHA/HABARI NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM)  SERIKALI imesema kwamba tatizo la maradhi yasiyoambukiza yakiwemo magonjwa ya akili yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku huku vyanzo vyake vikiwa ni pamoja na urithi, matumizi ya madawa ya kulevya, pombe, matatizo ya kisaikolojia pamoja na hali ngumu ya maisha.

  Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipokuwa akizindua Bodi ya Hospitali ya Mrembe Mkoani hapo.

  Akiongea na mbele ya Watendaji wa Bodi hiyo, wageni waalikwa pamoja na Viongozi wa hospitalini hapo, Waziri Ummy amesema kuwa, kundi lililoathirika Zaidi na kdhai hiyo ni vijana ambao ni nguvu kazi ya Taifa, ambapo alitaja taarifa ya Shirikala Afya Ulimwenguni (WHO) ya mwaka 2016n inayoonyesha takribani watu milioni 15.3 Duniani wanapata matatizo ya kiafya yatokanayo na matumizi ya dawa za kulevya pamoja na matumizi ya pombe kupita kiasi.

  “Matatizo haya yamekuwa yakisababisha vifo milioni 3.3 kila mwaka Duniani kote, hata hivyo taarifa ya Wizata yangu inaonyesha kwamba idadi ya watu wanaougua magonjwa ya akili inaongezeka kwa kasi kubwa kutoka wagonjwa 136,710 mwaka 2011/2012 hado wagonjwa 448,997 mwaka 2015/2016”, alisema Ummy.

  Ameongeza kuwa, takwimu za hospitali ya Mirembe zinaonyesha kuwa, katika kipindi cha miaka mine kuanzia mwaka 2012 hadi 2016, jumla ya wagonjwa Zaidi ya 60,000 wenye magonjwa ya akili na waathirika wa dawa za kulevya walipatiwa huduma za afya na utengamao.

  Aidha, kwa kutambua majukumu makubwa ya hospitali hiyo na kutatua changamoto zinazohusiana na magonjwa hayo, Serikali imeamua kuunda Bodi ya hospitalini hapo lengo likiwa ni kutekeleza dhana ya Utawala Bora na Utoaji wa Huduma Bora za Afya ya Akili kwa mujibu wa mapango mkakati na sera za nchi.

  “Ninayo furaja leo kushiriki nanyi katika uzinduzi wa Bodi hii ya Hospitali ya Afya ya Akili Mirembe, na bodi hii itaongozwa na Mwenyekiti pamoja na Wajumbe waliouteuliwa kutoka maeneo mbaimbali ya kiujuzi hapa nchini”, alisema Waziri Ummy.

  Amesema kuwa, bodi hiyo itakuwa na majukumu mbalimbali yakiwemo kusimamia utendaji wa hospitali hiyo na Taasisi ya Isanga, kuhakikisha kuwa Sheria ya uanzishwaji wa hospitali inapatikana kwa wakati, kushauri kuhusu muundo wa hospitali, kuunda kamati ndogo ndogo, kushauri kuhusu mpango wa muda mrefu ili kuboresha huduma pamoja na kushauri jinsi ya kupunguza gharama za uendeshaji hospitalini hapo.

  Sambamba na kuzindua bodi hiyo, Waziri Ummy ameitaka jamii kushirikiana na Serikali katika kupiga vita matumizi ya madawa ya kulevya hususan kwa vijana ili nguvu kazi ya Taifa isizidi kupotea.Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Profesa Gadi Kilonzo amempongeza Waziri Ummy na kwa kuzindua bodi hiyo na amemuhakikishia kuwa bodi hiyo itatekeleza maagizo yote pamoja na majukumu iliyopewa ili kuboresha utendaji kazi hospitakini hapo.

  “Dhama uliyotupa sisi Wajumbe wa Bodi ni kubwa, tunaieheshimu sana na pia nakuahidi kuwa, tutatekeleza kwa bidii majukumu yote ya kuisimamia hospitali hii, tutajitahidi kwa uwezo wetu wote kutatua changamoto za hospitali hii kwa kushirikiana na wadau wengine wa afya kupitia Wizara yako, pia tunashukuru kwa vifaa vya kazi ulivyotupatia kwa ajili ya kutumia wakati wa utendaji wetu”, alisem Kilonzo.

  Wajumbe waliochaguliwa kuunda bodi hiyo ni Profesa Gadi Kilonzo ambaye ndio Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Dkt. Erasmus Mndeme ambaye ni Katibu wa Bodi na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mirembe, Dkt. Mpona Boniventura ambaye ni Mwakilishi kutoka chuo Kikuu cha Dodoma, Profesa Joseph Mbatia, Ndugu John Sipendi, Ndugu Ernest Kabohola, Ndugu Jane Magembe pamoja na Ndugu Clavery Lyela.

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (wa sita kulia) akishiriki kuswalia  jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa NEC, Mwalimu Ali Mbaga wakati wa mazishi yaliyofanyika leo Feb 8, 2017, katika kijiji cha Kighare, Usangi wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro, leo. Mbaga ni miongoni mwa viongozi wanne wa CCM, waliofariki kwa ajali ya gari wakati  wakitoka kwenye maadhimisho ya miaka 40 ya CCM katika mkoa huo.(Picha  na Bashir Nkoromo)

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  BENKI ya DCB imeendelea kufanya droo ya pili ya bahati nasibu ya pili ya kampeni ya kuweka Amani inayoitwa Boresha maisha na DCB huku Mkaguzi wa michezo ya kubahatisha (Bahati nasibu) Taifa Bakari Maggid na kufurahishwa kwa juhudi zinazofanywa na benki hiyo katika kuwapata washindi.

  Droo hiyo iliyoanza mwezi Januari iliweza kuwapata washindi wa wa kwanza 20 waliopata tisheti, watatu waliopata fedha taslimu na wawili wakiopata simu za mkononi

  Akizungumza kabla ya kuanza kwa droo hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Steven Dede amesema kampeni hiyo ilianza Novemba 28,2016 na droo hii ya pili ni kwa wateja walioekwa pesa kwenye akaunti zao kuanzia Desemba 28 hadi Januari 31.

  Dede amesema akaunti zitakazohusika ni akaunti ya akiba binafsi, akaunti ya watoto na akaunti ya WAHI na kuwataka wateja wa benki hiyo na wasio wateja , watu binafsi, wajasirimalina taasisi mbalimbali kunendelea kujitokeza kwa wingi kushiriki shindano hilo kwa kufungua akaunti na kuweka amana.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Steven Dede akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na droo ya pili inatochezwa na benki hiyo ya weka amana na DCB na Boresha maisha na DCB
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa DCB akibonyeza kitufe kuashiria kuanza kwa droo hiyo akishuhudiwa na mkaguzi wa michezo ya kubahatisha( bahati nasibu) Taifa Bakari Maggid (wa pili kulia).

  0 0  Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma.

  Ugunduzi wa gesi asilia nchini umepelekea kushuka kwa gharama za umeme kwa asilimia 33.26 kwa mwaka 2014 hadi 2016.

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani ameyasema hayo leo Bungeni, Mjiji Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge viti Maalum Maida Hamad Abdallah kuhusu faida zilizopatikana tangu kugundulika kwa gesi asilia.

  “Faida kubwa iliyopatikana kutokana na ugunduzi na matumizi ya gesi asilia nchini ni uzalishaji wa umeme wa bei nafuu kwa kutumia Gesi Asilia ikilinganishwa na mafuta. Uzalishaji umeme kwa kutumia Gesi Asilia umeongezeka kutoka uniti 2,714.25 milioni kwa mwaka 2014 hadi uniti 4,196.4 milioni mwaka 2016 sawa na ongezeko la asilimia 54.61,” alifafanua Dkt. Kalemani.

  Aliendelea kwa kusema kuwa kuongezeka kwa uzalishaji wa umeme wa Gesi Asilia umepelekea kushuka kwa bei ya umeme kutoka wastani wa shilingi 188.56 kwa uniti mwaka 2014 hadi wastani wa shilingi 125.85 kwa uniti mwaka 2016.

  Akitolea ufafanuzi zaidi juu ya faida zinazopatikana kutokana na matumizi ya Gesi Asilia, Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo amesema kuwa maeneo ya Mikocheni, Jijini Dar es Salaam zikiwemo nyumba za Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wanatumia Gesi Asilia ambapo gharama wanayoitumia kwa mwezi haizidi shilingi elfu 25,000, na wanatumia kwa kupikia aina zote za vyakula hata vile vinavyotumia muda mrefu kuiva kama vile maharage na makongoro.

  Aliendelea kwa kusema kuwa, mpaka sasa jumla ya viwanda 37 vinatumia nishati inayotokana na Gesi Asilia, ambayo gharama yake ni nafuu ukilinganisha na gharama ya nishati nyingine.Aidha, amesema kuwa Wizara yake imepata ufadhili wa Dola Mil. 150 kutoka Afrikan Development Bank kwa ajili ya kusambaza gesi katika mikoa Dar es Salaam, Mtwara na Lindi.

  Prof. Muhongo amesema kuwa usambazaji huo utakapoanza na kufika maeneo ya Kinyerezi, Jijini Dar es Salaam yatafungwa mabomba mengine kwa ajili ya kupeleka gesi katika mikoa mingine kama vile Morogoro, Mbeya na Iringa.Aidha amesema gesi ambazo zinatumika kwa sasa ni gesi salama ambazo hazilipuki ukilinganisha na gesi za miaka ya nyuma.

  Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) lilianza utafiti wa masuala ya mafuta na Gesi Asilia nchini mwaka 1950, ikihusisha utafiti katika maeneo ya bahari ya kina kirefu, maziwa na nchi kavu. Gesi Asilia iliyogundulika katika maeneo ya bahari ya kina kirefu ni futi za ujazo trilioni 47.08 na katika nchi kavu ni futi za ujazo trilioni 10.17 hivyo kuwa na jumla ya futi za ujazo trilioni 57.25 za Gesi Asilia inayojulika kama “sweet gas” yaani gesi yenye kiwango kidogo sana cha salfa (sulphur).

  0 0

  Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma

  Mtu yeyote atakaye ruhusu mtoto chini ya miaka 18 kushiriki, kuingia au kukaa karibu na eneo la mchezo wa kubahatisha (kamari) anahesabiwa kufanya kosa.

  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji ameyasema hayo leo Bungeni, Mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge Viti Maalum Asha Abdullah Juma juu ya kuongezeka kwa maduka ya kucheza Kamari yanayojulikana kama Jack Pot katika miji mingi hapa nchini hivyo kusababisha uvunjifu wa maadili na nguvu kazi ya vijana.

  “Michezo yote ya kubahatisha ikiwemo kamari (slots machines) inaendeshwa kwa mujibu wa sheria ya Bodi ya Michezo ya kubahatisha namba 4 ya mwaka 2003, sura 41 pamoja na Kanuni zake,” alifafanua Dkt. Kijaji.

  Aliendelea kwa kusema kuwa, kwa mujibu wa sheria hiyo hakuna mtu au taasisi inayoruhusiwa kuendesha biashara ya michezo ya kubahatisha bila kuwa na leseni kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha pamoja na vibali vingine vinavyotolewa na mamlaka nyingine za biashara.

  Vile vile sheria hiyo inakataza watoto wenye umri chini ya miaka 18 kushiriki, kuingia, kukaa au kuzururazurura karibu na maeneo ya michezo ya kubahatisha.Aidha mtu yoyote ambaye atamruhusu mtoto chini ya miaka 18, kushiriki, kuingia au kukaa karibu na eneo la mchezo wa kubahatisha anahesabika kufanya kosa na anastahili kulipa faini ya shilingi 500,000 au kifungo kisichopungua miezi mitatu au vyote kwa pamoja.

  Dkt. Kijaji amesema kuwa ikiwa kosa hilo litafanywa na mwendesha mchezo wa kubahatisha, Bodi inamamlaka ya kumfutia leseni.Hivyo basi, wajibu wa Serikali ni kuzuia watoto na vijana walio chini ya miaka 18 kucheza michezo ya kubahatisha.Pia, Dkt. Kijaji ametoa rai kwa wazazi na walezi kuwazuia vijana wao kucheza michezo ya kubahatisha pale wanapoona kuwa uchezaji wao unakuwa na matokeo hasi.

  Hata hivyo amesema kuwa, michezo hiyo inaendeshwa kwa mujibu na sheria kama shughuli nyingine. Jambo la msingi ni kuhakikisha kuwa, wanaoendesha michezo hiyo wanazingatia sheria na kanuni zilizowekwa pamoja na wazazi, walezi na jamii kuhakikisha vijana wanazingatiia mila na desturi zinazolinda maadili ya Kitanzania wanapokuwa wanajishughulisha na shughuli halali za kiuchumi.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipofanya ziara ya kustukiza katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa Terminal III kuona maendeleo ya ujenzi unaondelea leo Jumatano February 8, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipofanya ziara ya kustukiza katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa Terminal III kuona maendeleo ya ujenzi unaondelea leo Jumatano February 8, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipofanya ziara ya kustukiza katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa Terminal III kuona maendeleo ya ujenzi unaondelea leo Jumatano February 8, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipofanya ziara ya kustukiza katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa Terminal III kuona maendeleo ya ujenzi unaondelea leo Jumatano February 8, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  katika picha ya pamoja na baadhi ya wahandisi na makadrasai alipofanya ziara ya kustukiza katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa Terminal III kuona maendeleo ya ujenzi unaondelea leo Jumatano February 8, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipofanya ziara ya kustukiza katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa Terminal III kuona maendeleo ya ujenzi unaondelea leo Jumatano February 8, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipofanya ziara ya kustukiza katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa Terminal III kuona maendeleo ya ujenzi unaondelea leo Jumatano February 8, 2017.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipofanya ziara ya kustukiza katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa Terminal III kuona maendeleo ya ujenzi unaondelea leo Jumatano February 8, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akisalimiana na wafanyakazi wa ujenzi alipofanya ziara ya kustukiza katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa Terminal III kuona maendeleo ya ujenzi unaondelea leo Jumatano February 8, 2017
  0 0


older | 1 | .... | 1132 | 1133 | (Page 1134) | 1135 | 1136 | .... | 1898 | newer