Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 111 | 112 | (Page 113) | 114 | 115 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Kiungo wa timu ya Garden, Juma Masoud (kulia) akiwania mpira na beki wa Mapambano, Said Ally katika mchezo wa fainali mashindano ya Vijana U-17 Airtel Rising Stars,kwenye Uwanja wa Tualipo Dar es Salaam,Garden waliibuka mabingwa wa Mkoa ya Temeke kwa ushindi wa goli 4-1.
  Mshambuliaji wa timu ya Garden, Roma David (kulia) akiwania mpira na mshambuliaji wa Mapambano, Jacobo Widon katika mchezo wa fainali mashindano ya Vijana U-17 Airtel Rising Stars, kwenye Uwanja wa Tualipo Dar es Salaam, Garden waliibuka mabingwa wa Mkoa wa Temeke kwa ushindi wa goli 4-1.
  Alliance Schools Academy ikiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabithiwa kombe na kuibuka washindi wa Airtel Rising stars katika mkoa wa Mwanza.

  Mashindano ya vijana chini ya umri wa mika 17 ya Airtel Rising Stars ngazi ya mkoa yamefikia tamati mwishoni mwa wiki kwa timu za Moro Kids, Alliance Schools Academy na Garden kutangazwa mabingwa katika mikoa ya Morogoro, Mwanza na Temeke.

  Moro Kids imetwaa uchampioni baada ya kujikusanyia pointi nne sawa na wapinzani wao wakubwa timu ya Techfort lakini Moro Kids wakatangazwa washindi kwa kuwa na magoli mengi ya kufunga. Techfort walihitimisha michuano hiyo kwa kuifunga timu dhaifu ya Anglikana 2-1 katika uwanja wa shule ya sekondari Morogoro. Magoli yao yalipatikana kupitia kwa washambuliaji Alobogast Mtalemwa na Octatus Lupekenya wakati Anglikana walifunga goli lao pekee kupitia kwa Kessy Khamis.

  Hadithi ya mkoani Morogoro vile vile ilitokea huko jijini Mwanza ambapo timu ya Mwanza Alliance Schools Academy ilimemaliza ligi ikiwa na pointi nne sawa na timu ya Marsh Athletical lakini Alliance wakanyakuwa ubingwa wa mkoa kwa kuwa na magoli mengi ya kufunga.

  Katika mchezo wa kufunga dimba uliopigwa kwenye uwanja mkongwa wa Nyamagana Ijumaa jioni, Alliance Schools Academy na Marsh Athletical walipambana vikali katika mchezo uliovuta hisia za watazamaji wengi ambapo wachezaji wa pande zote mbili walionyesha vipaji vya hali ya juu ya kusakata kabumbu.

  Mchezo mwingine wa kufunga dimba ulipigwa katika uwanja wa Twalipo katika mkoa wa kisoka wa Temeke jijini Dar es Salaam, ambapo timu ya Garden wallibukwa mabingwa baada ya kuiadhibu bila huruma timu ya Mapambano 4-1. Washindi walipata magoli yao kupitia kwa Badili Salum, Bona David, Juma Masudi na Said Mohamed wakati Mapambano walipaga goli lao la kufutia machozi kupitia kwa Said Hassan.

  Wakati huo huo, chama cha soka mkoa wa Morogoro kimetangaza kikosi chake kitakacho uwakilisha mkoa huo katika fainali za taifa za Airtel Rising Stars zinazotarajiwa kuanza kutimua vumbi katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 2 hadi Julai 7.

  Kikosi chao kinajumuisha washambuliaji mapacha Evance na Robert Roshan. Wengine ni Fadhili Kamwenda, Juma Shaban, Boniface Myowela, Majid Musisi, Ramadhani Kondo, Rotan Nkamwa, Dickson Mwesa, Alphonce Lukani, Octatus Lupekenya, George Chota, Salum Kiibwa, Shafii Ngesa na Petro Mgaya.

  Mashindano ya Airtel Rising Stars ngazi ya taifa mwaka huu yanashirikisha timu za wasichana na wavulana kutoka mikoa tisa – Kinondoni, Ilala, na Temeke itakayoleta timu za wasichana na wavulana wakati Tanga, Kigoma na Ruvuma zitashirikisha wasichana pekee huku mikoa ya Morogoro, Mwanza na Mbeya ikiwa na timu za wavulana tu.

  Maandalizi kwa ajili ya mtanange huo wa taifa yamekamilika na timu kutoka mikoani zinatarajiwa kuanza kuwasili jijini Dar es Salaam mwishoni wa wiki tayari kwa mashindano hayo. Fainali za ARS Taifa vile vile zilifanyika katika uwanja huo mwaka jana ambapo Temeke waliibuka washindi.

  0 0

   Picha ya pamoja na viongozi wa Halmashauri ya jiji la Mwanza.
   Sehemu ya vyandarua vilivyotolewa msaada vikiwa tayari vimefungwa na wasanii wa filamu hapa nchini,mara baada ya kutoa msaada wa vyandarua hivyo ndani ya wodi ya wazazi kwenye hospitali ya Mkoa wa jiji la Mwanza-Sekou-toure  mapema leo asubuhi kwa udhamini mkubwa wa kinywaji kisicho na kilevi cha Grandmalt..
   Msanii wa Bongo Movie,Jacline Wolper akiwa katika wodi ya wazazi ,Hospital ya Mkoa wa Mwanza Sekou-toure akifunga chandarua kwenye moja ya vitanda hospitalini hapo,ikiwa ni sehemu ya vyandarua vilivyotolewa na wasanii hao kupitia kinywaji cha Grandmalt
   Wasanii Irine Uwoya na Shamsa Ford wakiwa na mmoja wazazi akiwa amembeba mtoto aliezaliwa kwenye hospitali hiyo ya Mkoa wa Mwanza, Sekou-toure  mara baada ya wasanii hao kutembelea Hospitali hiyo na kutoa vyandarua kwenye wodi Wazazi.
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Mwanza,Halifa Hassan Hida akizungumza machache (mbele ya wasanii wa Bongo Movie (hawapo pichani) ikiwemo na kuwashukuru wasanii hao wa filamu kwa kitendo cha kiungwana kabisa katika suala zima la kuisaidia jamii yao inayowazunguka kwa njia moja ama nyingine na pia amewataka kuwasaidia wasanii wachanga wa jiji la Mwanza na kuwaelekeza njia sahihi za mafanikio katika tasnia hiyo ambayo kwa sasa imezidi kushika kasi siku siku. 
   Meneja wa kinywaji cha Grandmalt Consolata Adam akipokea mkono wa shukurani  kutoka kwa katibu wa Afya hospitali ya Sekou-toure Bwa.Daniel Temba,mara baada ya kabidhi msaada wa vyandarua sanjari na wasanii mbalimbali wa filamu,makabidhiano hayo yamefanyika mapema leo kwenye hospitali ya mkoa wa Mwanza Sekou-toure,ikiwa ni sehemu ya wasanii hao kuwa karibu na wananchi, kisha baadae kuonyesha kazi zao mbalimbali kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
  Wasanii mbalimbali wakiongozwa na Raymond Kigosi  wakikabidhi msaada wa vyandarua kwenye hospitali ya mkoa wa Mwanza Sekou-toure, kwa katibu wa afya wa Hospitali  hiyo Bwa.Daniel Temba ikiwa ni sehemu ya wasanii hao kuwa karibu na wananchi, kisha baadae kuonyesha kazi zao mbalimbali kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
   wasanii wakiendelea na zoezi la  wakikabidhi msaada wa vyandarua kwenye hospitali ya mkoa wa Mwanza Sekou-toure kwa katibu wa afya wa Hospitali  hiyo ikiwa ni sehemu ya wasanii hao kuwa karibu na wananchi, kisha baadae kuonyesha kazi zao mbalimbali kwenye  uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.
   Baadhi ya wasanii wa Filamu hapa nchini a.k.a Bongo Movie Unity wakiwasili kwenye hospitali ya Sekou-toure tayari kwa kushiriki zoezi la kugawa vyandarua kwenye wodi ya wazazi kwa udhamini mkubwa wa kinywaji kisicho na kilevi cha GrandMalt mapema leo asubuhi.
   Mlezi wa Bongo Movie Unity,Jacob Steven a.k.a JB a.k.a Bonge la Bwana wakisalimiana na Afisa mhausiano wa Halmashauri ya jiji la Mwanza,Bwa.Joseph Mlinzi,pichani kati ni msanii wa filamu Singo Mtambalike.
   Baadhi ya Wasanii hao wa Bongo Movie Unit wakitoka kwenye wodi ya Wazazi mara baada ya kukabidhi msaada wa vyandarua vilivyotolewa kwa hisani kubwa ya kinywaji kisicho na kilevi cha Grandmalt.


  ======  =======  =========
  Wasanii Tamasha la Filamu Grand Malt watoa msaada
  Na Mwandishi Wetu, Mwanza

  WASANII maarufu wa Bongo Movie hapa nchini, ambao wapo hapa kwa ajili ya Tamasha la Wazi la Filamu Tanzania, maarufu kama ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’ jana walikabidhi vyandarua kwa Halmashauri ya Jiji la Mwanza pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Sekou Toure.
   Akizungumza na wasanii hao, Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Halifa Hassan Hida, aliwashukuru wasanii hao kwa msaada huo na kuwataka wawasaidie pia wasanii wachanga wa jijini hapa ili nao waweze kutoka.
  “Nimefarijika na msaada huu pamoja na ujio wenu, ila kimoja ninachokiomba kutoka kwenu ni kuwasaidia wasanii wa Mwanza ili nao waweze kutoka, naamini ujio wenu ni changamoto kubwa kwao,” alisema Hida.
  Kaimu Meya wa Jiji la Mwanza, Dismas Masuni naye alitoa shukrani kwa msaada huo na kusema wapo ni vema zaidi kwa wasanii hao pia kufikiria kuwekeza jijini hapa kwa ajili ya maendeleo yao.
   Meneja wa kinyawaji cha Grand Malt, Consolata Adam, alisema nia kubwa ya kuamua kudhamini tamasha hilo ni kuwaendeleza zaidi vijana kwani wengi wako katika ajira hiyo na kutaka wakazi wa Mwanza kufika kwa wingi wakati wote wa tamasha hilo.
   Wakati walipokabidhi msaada wa vyandarua katika hospitali ya rufaa ya Sekou Toure na kuvifunga katika wadi ya wazazi, wasanii hao walionekana kuguswa zaidi na hali ilivyo na kusema wana jukumu kubwa la kuisaidia jamii.  Katibu wa Afya wa hospitali hiyo, aliye pia kaimu Katibu wa Afya wa Mkoa, Danny Temba alishukuru kwa msaada huo na kusema umekuja wakati muafaka kutokana na mahitaji yaliyopo.
   “Tunashukuru mno kwa msaada wenu na kwa kutaka kuwadhihirishia tuna mahitaji makubwa na vyandarua hasa katika kupambana na malaria, naomba mkavifunge wenyewe,” alisema Temba, ombi lililoridhiwa na wasanii hao na kuomba wavifunge katika wadi ya mzazi na mtoto.
   Wasanii walionekana kuguswa zaidi walipoingia katika wadi hiyo, huku Jacqueline Wolper, Shamsa Ford, Chuchu Hans, Aunty Ezekiel, Vicent Kigosi ‘Ray’, Hashim Kambi na wengineo wakionekana kuguswa zaidi na mahitaji ya wadi hiyo.
   “Kuna mahitaji makubwa katika hospitali hii, kuna kitu kimenigusa mno kwa kuja hapa,” alisema Jacob Steven ‘JB’, huku akiungwa mkono na Single Mtambalike ‘Ritchie Ritchie’ na Steve Nyerere.
  Mratibu wa Tamasha hilo, Musa Kissoky, ambalo lilizinduliwa rasmi jana katika Uwanja wa Nyamagana alisema, kutakuwa na filamu za aina mbalimbali zitakazoonyeshwa wakati wote wa tamasha hilo. 


  Kissoky alisema, tamasha hilo ambalo litakuwa la bure kwa watu wote na kushirikisha mastaa wa filamu hapa nchini, litakuwa la aina yake na kuwataka wakazi wa Mwanza wajitokeze kwa wingi kushuhudia mambo yanayoendelea.


  Meneja wa kinywaji cha Grand Malt walio wadhamini wakuu wa tamasha hilo, Consolata Adam, alisema wameamua kufanya kweli zaidi kwani wanataka kuona Watanzania wanapata kitu chenye uhakika. “Tumejipanga katika hili na wala hatutanii. Tunawakaribisha watu wote wenye mapenzi na filamu zetu za Tanzania kufika na kushuhudia tamasha hili ambalo mwaka huu limeboreshwa zaidi,” alisema Consolata.


  Tamasha hilo la filamu limedhaminiwa na kinywaji cha Grand Malt kisicho na kilevi ambacho kinazalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

  0 0

  Chegge akiwadatisha wapenzi wa burudani wa Dar Live katika Usiku wa Tudd Thomas.
  Izzo B akiongea na Mshua ndani ya Dar Live.
  Mwanamuziki Marlaw akiwabembeleza mashabiki wa Dar Live.
  Tundaman akiwarusha mashabiki.
  Mhe. Temba akifanya makamuzi katika Usiku wa Tudd Thomas.
  Wanadada kutoka Scorpion Girls, Jini Kabula (kulia) na Isabela Mpanda wakiwadatisha mashabiki.


  Mashabiki wakifuatilia burudani ndani ya Dar Live.
  Linex akisema na mashabiki wake....Akijichanganya na mashabiki.
  Makomandoo wakionyesha umahiri wao stejini.
  Msanii Amin akitoa burudani stejini.
  Queen Darleen akifanya vitu vyake.
  Sehemu ya mashabiki waliohudhuria shoo hiyo.
  Quick Lacka akipagawisha.
  Baghdad akiwapa raha mashabiki.
  Madansa wa Tundaman wakilishambulia jukwaa la Dar Live.
  Wasanii mbalimbali wakiwemo Marlaw, Izzo B, Chegge, Tundaman, Mhe. Temba, Amin, Queen Darleen, Quick Lacka, Baghdad, Scorpion Girls, Makomandoo na wengineo usiku wa kuamkia leo walifanya makamuzi ya nguvu katika Tamasha la Usiku wa Prodyuza Tudd Thomas lililofanyika kwenye Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo pande za Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam.
  (PICHA NA ISSA MNALLY / GPL)

  0 0

   Rais Barack Obama wa Marekani na mkewe Michelle Obama akipokewa kwa Shangwe Ikulu, Dar es salaam na baadaye akaongea na wanahabari.PICHA YA IKULU NA ISSA MICHUZI

    

  Rais Kikwete akiwa ameambatana na mgeni wake,Rais wa Marekani,Barack Obama,wakati wakielekea kuzungumza na wanahabari Ikulu,jioni ya leo. 


  0 0


  Na Mwandishi Wetu
  SIYO siri, Julai 7, mwaka huu (Siku ya Sabasaba), anga lote la Jiji la Dar es Salaam litasimama kwa muda wa saa 16. Burudani mfululizo pamoja na matukio ambayo hayajawahi kushuhudiwa, mengine ni adimu sana, yatachukua nafasi pana siku hiyo kwenye Uwanja wa Taifa.  Diamond.
  Ni saa 16 za maajabu! Tafakari Mbunge wa Kigoma Mjini (Chadema), Zitto Kabwe, ataonesha uwezo wake wa kucheza masumbwi na kuchapana na staa wa filamu Tanzania, Vincent Kigosi ‘Ray’. Je, ni vigumu kuamini?  Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee, atakuwa na kibarua chake katika mchezo wa ndondi, atakapopanda ulingoni kuzipiga na malkia wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper. Uheshimiwa na usupastaa kando, zitapigwa ngumi tu kwa raundi nne.

  Prezzo.
  Vilevile, Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mkoa wa Mara, Ester Bulaya, siku hiyo atakuwa na kazi moja tu ya kukong’otana na mrembo nyota wa sanaa za maigizo nchini, Aunt Ezekiel. Ni burudani ambazo awali hazikuwahi kufikiriwa kwamba zingewezekana lakini ndani ya Usiku wa Matumaini, imewezekana.

  Kila mmoja anatamba kivyake kumchapa mpinzani wake lakini mwisho wa ubishi ni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwenye Usiku wa Matumaini, Dar es Salaam.

  JB.

  JB YEYE ANAMTAKA AZZAN
  Kuonesha kwamba homa ya Tamasha la Usiku wa Matumaini imepanda juu sana, staa mkubwa wa filamu Tanzania, Jacob Steven ‘JB’, amemtaka Mbunge wa Kinondoni (CCM), Idd Azzan, wakutane Uwanja wa Taifa, amuoneshe kazi.  “Idd Azzan asiogope, namtaka aje tukutane ulingoni. Ila kiukweli ndani ya sekunde 35, itakuwa nimeshampiga na atakuwa ameshalala,” alisema JB na kuongeza: “Nakuomba Azzan, njoo nikuoneshe mchezo. Inawezekana uzito wa ngumi zangu hujaujua, kwa hiyo lengo langu ni kukuchapa makonde mazito halafu baada ya hapo, nitaanza kufukuzia mapambano ya kimataifa, maana naona hapa nchini sitakuwa na mpinzani.”

  Ester Bulaya.
  Upande mwingine, JB alisema kuwa anaamini kuwa pambano la Zitto na Ray litakuwa na upinzani mkali kwa sababu wote wana mazoezi ya kutosha. “Naamini mdogo wangu Ray yupo vizuri ila upinzani utakuwa mkali sana dhidi ya Zitto. Vilevile nawatakia kila la heri Jacqueline Wolper ambaye bila shaka atamchakaza mheshimiwa Halima Mdee na Aunt Ezekiel sina shaka naye kwamba atampiga mheshimiwa Ester Bulaya,” alisema JB.

  Wabunge: Simba vs Yanga.


  MAAJABU YAAENDELEA
  Mechi kali yenye ushindani mkubwa, itakuwa ni Simba na Yanga. Waheshimiwa wabunge wanaoshabikia timu hizo mbili, watachuana wao kwa wao kumtafuta Bingwa wa Kombe la Matumaini mwaka 2013.

  Mechi kama hiyo, ilipigwa mwaka jana, Uwaja wa Taifa, Dar es Salaam kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini na Simba iliibuka mshindi kwa changamoto ya mikwaju ya penalti. Mambo yatanoga kwa mara nyingine mwaka huu, kuonesha kuwa Yanga wanataka kurejesha heshima yao, wameogeza wachezaji wanaocheza kikosi A.

  Mashali.
  Mmoja wa viongozi wa timu ya wabunge wanaoshabikia Yanga, Abbas Mtemvu, amesema kuwa wameamua kuongeza wachezaji wanne kutoka kwenye kikosi A cha Yanga ili kuhakikisha ushindi unapatikana. 

  “Tumewaogeza Mrisho Ngassa, Ally Mustapha ‘Barthez’, Kelvin Yondan na Athuman Idd ‘Chuji’. Watacheza kuhakikisha Yanga inashinda. Hatuna utani katika mechi, sisi tunakweda kulinda heshima,” alisema Mtemvu.

  Upande mwigine, nahodha wa timu ya wabunge wa Simba, Amos Makalla, amesema kuwa ameshajua hila ya Yanga, kwa hiyo nao wanajipanga kuongeza wachezaji wengine kutoka Simba A ili kuhakikisha Yanga hawatoki siku hiyo taifa. “Mpaka sasa tumeshawaongeza Shomari Kapombe na Amri Kiemba, tunatarajia kuongeza wengine baada ya kocha wetu kutoa mwongozo. Siku hiyo watake wasitake, tutawapiga tu Yanga, hawana ujanja. Mwaka huu tunawatengeneza ndani ya dakika 90,” alisema Makalla.

  Miyeyusho.
  MAKONGO VS JITEGEMEE
  Katika tamasha hilo, kivutio kingine ni mechi ya soka kati ya timu za kombaini ya Makongo Sekondari na Jitegemee. Inaeleweka kuwa Jitegemee na Makongo ni shule zenye upinzani wa jadi kimichezo, kwa hiyo siku hiyo bingwa atajulikana na kukabidhiwa kikombe.

  BONGO MOVIE VS BONGO FLEVA
  Hii ni mechi inayokutanisha mastaa watupu. Wale wa filamu, Bongo Movie FC, wataoneshana umwamba kwa dakika 90 na wakali wa muziki, Bongo Fleva FC.  Mwaka jana katika Tamasha la Usiku wa Matumaini, mechi hii ilifanyika na Bongo Movie walishinda bao 1-0, kwa hiyo mwaka huu Bongo Fleva wanataka kurejesha heshima yao.

  Bongo Fleva vs Bongo Movie.
  Nahodha wa Bongo Fleva FC, Hamis Ramadhan ‘H. Baba’, amesema kuwa wao kama timu, wanajua mbinu ambazo Bongo Movie walizitumia kushinda mwaka jana, kwa hiyo mwaka huu wasitegemee mazingira yaleyale.

  “Tutawafunga kwa urahisi sana mwaka huu. Hatutaki kurejea makosa ya mwaka jana. Hili naomba hao Bongo Movie walijue. Mimi binafsi lazima niwafunge, nina usongo nao sana wale jamaa,” alisema H. Baba. Naye Mwenyekiti wa Bongo Movie, Vincent Kigosi ‘Ray’, alisema kwamba hana shaka na timu yake, kwani watashinda kama ilivyokuwa mwaka jana.


  “Lile kombe ni letu, Bongo Fleva wataendelea kuwa wateja wetu tu. Tunaendelea kufanya mazoezi makali, tupo vizuri sana. Bongo Fleva wasubiri kichapo kingine. Tunatarajia mwaka huu tutawafunga zaidi ya mabao mawili,” alisema Ray.

  Kiongozi wa Jahazi Modern Taarab, Mzee Yusuf.
  MUZIKI
  Siku haitakamilika bila burudani ya muziki, Nasibu Abdul ‘Diamond’ wa Tanzania na Rapa Jackson Makini ‘Prezzo’, watabadilishana mic, kuoneshana ni nani mkali zaidi ukanda wa Afrika Mashariki.
  Bendi hasimu na kongwe zaidi, Msondo na Mlimani Park Orchestra ‘Sikinde’, watapishana kwenye jukwaa moja kisha mashabiki wataamua nani mkali kuliko wengine.


  Mfalme wa Taarab, Mzee Yusuf akiwa na kundi zima la Jahazi Modern Taarab, watafanya muziki mzuri siku hiyo na kukamilisha shangwe za wapenda mambo ya Pwani hususan muziki wa mwambao.
  Mwanza Suspastaa, Hamis Ramadha ‘H. Baba’, atakuwa na timu yake ya shoo, yote ni kuhakikisha kwamba anafanya muziki utakaoacha historia kubwa siku hiyo.


  Kundi la TMK Wanaume Family linaloongozwa na mastaa, Amani James Temba ‘Mheshimiwa Temba’ na Saidi Juma ‘Chegge’, litakuwepo na lile la TMK Wanaume Halisi ambalo kinara wake ni Juma Kassim Kiroboto ‘Sir Nature’.

  Flora Mbasha.

  INJILI
  Muziki wa Injili, utakutanisha mchuano wa nguvu kwa wanamuziki wa Tanzania kuchuana na wale wa Kenya. Kenya itaongozwa na Anastazia Mukabwa, Solomoni Mukubwa, Sara K na 24 Elders ambao wameahidi kutoa ushindani mkubwa kwa Watanzania. Kwa upande wa Tanzania, watakuwepo waimbaji mahiri kama Upendo Nkone, Flora Mbasha, Martha Mwaipaja, Edson Masabwite, Ambwene Mwasongwe, Glorious Worship Team, Enock Jackson, Kundi la The Voice, Jesca na Kundi la The Voice. Viingilio vya tamasha hilo ambalo litasheheni matukio kibao ya kusisimua kwa lengo la kuchangia Mfuko wa Mamlaka ya Elimu nchini (TEA), vitakuwa ni shilingi 20,000 kwa V.I.P, 10,000 viti vya bluu na 5,000 viti vya kawaida.

  0 0

   Wazira wa Afya Juma Duni Haji, akifungua Mkutano wa Wauguzi  wa Afrika Mashariki kulia Clavery Mpandana Muguzi Mkuu Tanzania ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Uuguzi Afrika Mashariki kushoto Katibu Mkuu Wizara ya Afya Muhamed Saleh Jidawi. Mkutano huo uliofanyika Hoteli ya Oceanview nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. 
   Badhi ya Wajumbe wa Mkutano wa Wauguzi wa Afrika Mashariki wakifuatilia hutuba ya ufunguzi iliyotolewa na Waziri wa Afya Juma Duni Haji, huko Hoteli ya Ocean view nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. 
  Waziri wa Afya Juma Duni, katikati waliokaa akiwa katika Picha ya pamoja na Wajumbe wa Mkutano wa Wauguzi wa Afrika Mashariki uliofanyika katika Hoteli ya Ocean view nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Picha na Makame Mshenga- Maelezo Zanzibar.

  0 0

    Mshindi wa droo ya pili ya Winda na Ushindeinayoendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti, Mwl. Michael Mbuya, akiongea na vyombo vya habari mwishoni mwa wiki mara baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya shilingi milioni 1katika bar aliyopatia kizibo cha ushindi New Mashilingi Bar iliopo Tabata- Kisukuru jijini Dar es Salaam.
  Meneja muendeshaji wa kanda ya Dar es Salaam kutoka Kampuni ya Bia ya Serengeti Joseph Silumbe(kushoto) na Meneja mauzo wa eneo Benson Bwanga wakikabidhi mfano wa hudi ya shilingi milioni 1 kwa mshindi wa droo ya pili ya Winda na Ushinde Michael Mbuya, 29,(kulia) mwishoni mwa wiki katika hafla iliyofanyika New Mashilingi Bar iliopo Tabata- Kisukuru jijini Dar es Salaam.
   Akiendelea kujipongeza kwa kunywa Serengeti baridi, Mshindi wa droo ya pili ya Winda na Ushinde inayoendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti, Mwl. Michael Mbuya wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 1 kwa mshindi huyo tabata jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Maadhimisho ya siku ya serikali za mitaa katika mkoa wa IRINGA yamefanyika  hii leo katika viwanja vya mwembetogwa vilivyopo manispaa ya Iringa,  huku mgeni rasmi akiwa ni mkuu wa wilaya DR. RETICIA WARIOBA.

  Katika maadhimisho hayo  DR.WARIOBA  amesema kuwa siku  ya leo ni  muhimu kuienzi kwa kufanya maadhimisho ikiwa ni kuuenzi utaratibu uliowekwa na  waasisi wa taifa  la Tanzania.

  WARIOBA pia amezitaka mamlaka za serikali za mitaa, kutambua umuhimu wa wananchi kushirikishwa katika utendaji kwa lengo la kuleta maendeleo bila kuweka udini na ukabila.

  Kwa upande wake mbunge wa jimbo la iringa mjini mchungaji PETER MSIGWA amesema kuwa kuwepo kwa serikali za mitaa kutasaidia kuweka democrasia kwa wananchi na watakuwa huru katika kudai kile kinachowastaili kutoka kwa viongozi ikiwemo maisha bora kwa kila mwananchi.

  Hata hivyo msigwa amesema kuwa viongozi wanapaswa kuwa wachapakazi na wabunifu ili kuweza kuboresha shughuli mbalimbali zinazowazunguka katika jamii. Maadhimisho ya serikali za mitaa huazimishwa kila mwaka july mosi na mwaka huu kitaifa yamefanyika mkoani morogoro.

  0 0


  Waziri Mkuu , Mizengo  Pinda akimwongoza Mfalme Muswati  wa Swaziland kutembelea abanda ya maonyesho baada ya mfalme huyo kufungua maoinyesho ya kimataifa ya Biashara kwenye uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam Julai 1, 2013. 
  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
   IMG_0139IMG_0146
  IMG_0167 
  Mfalme Muswati wa Swazilanda (kulia) na Waziri Mkuu , Mizengo Pinda wakitazama dawa za aina mbali mbali wakati walipotembelea banda la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya mfalme huyo kufungua maonyesho ya Biashara ya Kimataifa kwenye uwanja wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Julai 1, 2013. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

    
  Rais Obama akipanda mti aina ya mpingo katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam leo.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa maelezo ya mti wa mpingo anaotaka kuupanda katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam leo.
  Rais Jakaya Mrisho kikwete akimsindikiza mgeni wake baada ya kumpatia mapokezi ya kihistoria leo Ikulu,PICHA YA IKULU NA ISSA MICHUZI.

  0 0


  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na mfalme Mswati wa Swaziland ambaye aliondoka nchini baada ya kufungua maonyesho ya Kiataifa ya Biashara kwenye uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam Julai 1, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Mfalme Mswati wa Swaziland akisindikizwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipoondoka kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam kurejea nyumbani baada ya kufungua maonyesho ya Biashara ya Kimataifa kwenye uwanja wa Mwalimu Nyerere Julai 1,2013.

  0 0
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mommmed Gharib Bilal, akifunga  Mkutano wa siku tatu wa Viongozi wa  Kimataifa  wenye  lengo la  kutokomeza  njaa Barani Afrika .Mkutano huo ulimazika jana jioni mjini Addis Ababa Ethiopia. 


  Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiongoza Ujumbe wa Tanzania kwenye  Mkutano wa Kimataifa   kuzungumzi  juu ya   kutokomeza tatizo la njaa Barani Afrika uliomalizika  mjini Addis Ababa Ethiopia leo.


  Ujumbe wa Tanzania uliofuatana na Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal wakifuatilia kwa makini mkutano wa Afrika uliozungumzia juu ya kutokomeza tatizo la njaa Barani Afrika . Mkutano huo ulimalizika  jana  jioni July 01-2013  mjini Addis Ababa Ethiopia.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mwenyekiti wa  AUC  Dk.  Nkosazana  Dlamina Zuma, kwenye ukumbi wa Mikutano wa umoja huo baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Viongozi wa Kimataifa uliozungumzia juu ya kutokomeza tatizo la njaa Barani Afrika  mjini Addis Ababa Ethiopia jana jioni July  01-2013


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal wa pili kushoto akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Viongozi wa kimataifa waliohudhuria Mkutano wa  Kimataifa  uliozungumzia juu ya kutokomeza tatizo la njaa Barani Afrika mjini Addis Ababa  Ethiopia    July 01-2013.


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mommmed Gharib Bilal na ujumbe wake, wakiingia kwenye ukumbi wa mkutano wa Viongozi wa kimataifa uliozungumzia juu ya kutokomeza tatizo la njaa Barani Afrika . Mkutano huo ulimalizika jana jioni mjini Addis Ababa Ethiopia.(Picha na OMR).

  =======  ======= ==========
  MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA UMOJA WA AFRIKA KUHUSU KUDHIBITI NJAA
  ADDIS ABABA, ETHIOPIA
   JULAI 02, 2013.

  Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal ameiwakilisha Tanzania katika Mkutano wa Umoja wa Afrika unaojadili namna ya kumaliza Baa la Njaa katika nchi za Afrika. Mkutano huo wa siku moja umefanyika jijini Addis Ababa, Ethiopia Jumatatu Julai Mosi, 2013 ambapo nchi washiriki wamekumbusha kuhusu Azimio la Maputo walilolitoa miaka 10 iliyopita yaani mwaka 2003, azimio lililolenga kukabiliana na Njaa na Utapiamlo.

  Azimio hilo lililenga kuzitaka nchi za Afrika kukabiliana na Baa la Njaa sambamba na kuhakikisha kuwa wananchi wa Bara hili, si tu kwamba wanapata uhakika wa chakula, bali kula chakula bora chenye virutubisho vinavyohitajika katika kulinda afya za binadamu na hivyo kuwa na uwezo wa kukabiliana na magonjwa. Pia azimio hilo lilizitaka nchi wanachama wa Umoja wa Afrika kuhakikisha zinatanua bajeti zake za Kilimo ili zifikia asilimia 10 ya Bajeti Kuu na pia kukifanya Kilimo kuchangia kwa asimilia 6 katika ukuaji wa uchumi wa nchi za Afrika.

  Katika mkutano huo, Mheshimiwa Makamu wa Rais alieleza kuwa Tanzania inashirikiana bega kwa bega na nchi za Afrika katika kuhakikisha kuwa Bara hili linakabiliana vilivyo  na baa la njaa na hivyo kutokomeza Baa hilo kama nchi hizo zilivyokubaliana katika mkutano uliofanyika Maputo mwaka 2003 uliopendekeza pia kuwa nchi za Afrika ziwe zimefanikiwa kukabiliana na Baa la Njaa na Utapiamlo ifikapo mwaka 2025.

  Katika maelezo yake, Mheshimiwa Makamu wa Rais alifafanua kuwa Tanzania imepiga hatua katika kilimo kupitia mpango wa Kilimo Kwanza na pia mpango wa kukuza uzalishaji kwa kutumia kanda maalum maarufu kama SAGGOT (unaojumuisha mikoa iliyo na uwezo wa kuzalisha chakula kwa wingi) umeanza kukubalika na kuwa mpango wa nchi nyingi za Afrika. Hata hivyo Mheshimiwa Makamu wa Rais alifafanua pia kuwa, ukuzaji wa Kilimo unapaswa kuambatana na sekta nyingine kama Nishati, Miundombinu, Viwanda na Biashara.

  Umuhimu wa kukuza sekta hizo unatokana na ukweli kuwa, zinachangia kukuza kilimo, kukifanya kuwa na tija na pia kutoa unafuu wa uzalishaji kwa wakulima. Tena kwa kukuza sekta hizo, Afrika inaweza kupiga hatua kubwa kwani tatizo la uzalishaji halitokani na upungufu wa uzalishaji tu, bali hata pale panapokuwa na uzalishaji mkubwa, kuna maeneo ambayo mazao yameshindwa kulifikia soko ama kufikishwa kwa watu wenye mahitaji.

  Awali akichagia katika mkutano huo, Rais Mstaafu wa Brazil Lula da Silva alisema njaa ni jambo la kijamii, linalochangiwa kwa kiasi kikubwa na binadamu wenyewe hasa pale mtaji na kipato kinapobakia kuwa katika mikono ya wachache wakati wengi wakiambulia patupu.

  Rais Lula pia alimnukuu Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kusema; “kama mnataka maendeleo lazima mshirikishe wananchi wote.” Kwa kutumia nukuu hii, Rais Lula anasisitiza kuwa, Afrika inapaswa kuwa na mipango inayoshirikisha wananchi ili iwasaidie kukua kiuchumi na kukabiliana na matatizo yanayowakabili katika maisha yao.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamisheni ya Afrika Dkt. Nkosazana Zuma alisema barani Afrika kuna changamoto kubwa inayowakabili akina mama na moja ni kubwa ni kukosa fursa ya kumiliki ardhi hali inayofanya uzalishaji kuwa duni. “Jambo hili linaweza kubadilishwa na sisi, tunaweza kubadili tamaduni zetu kwa kuwa tunatambua mchango mkubwa wa akina mama katika Kilimo. Hata hivyo, kama hatutafanya mabadiliko akina mama watabakia nyuma na bara la Afrika litazidi kukabiliana na Baa la Njaa,” alisema.

  Naye Rais Mstaafu wa Nigeria Olesegun Obasanjo aliueleza mkutano huo kuwa, zipo tamaduni barani Afrika ambazo zinawabagua wanawake japokuwa ndio wazalishaji zaidi. Pia akaongeza kuwa, wanawake wasitumike katika shughuli za kisiasa tu bali wawezeshwe ili kufanikisha azma ya Afrika kukabiliana na njaa.

  Makamu wa Rais katika mkutano huo ameambatana na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Injinia Christopher Chiza pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mahadhi Juma Maalim. Katika Mkutano huo pia viongozi mbalimbali wamehudhuria akiwemo Rais Mstaafu wa Brazil Lula da Silva, Rais Mstaafu wa Nigeria Olesegun Obasanjo, Rais Mstaafu wa Ghana John Kuofor. 

  Viongozi wengine waliohudhuria mkutano huo ni Mkurugenzi wa Shirika la Chakula Duniani, Jose Graziano da Silva, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Afrika Dkt. Nkosazana Zuma, Rais wa Sudan, Benin na wawakilishi wa nchi mbalimbali ambazo ni wajumbe wa Umoja wa Afrika.

  Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais
                Ethiopia Julai 02, 2013

  0 0

   Kijana anayetuhumiwa kukwapua simu(aliyeshikwa) ndani ya maonesho ya 37 ya Biashara jijini Dar es Salaam akipelekwa kwenye vyombo vya usalama.
  Kijana huyo akisindikizwa kwenda kwenye kituo cha polisi, ndani ya maonesho ya 37 ya Biashara jijini Dar es Salaam akipelekwa kwenye vyombo vya usalama.

  0 0

  Afisa Mtendaji Mkuu wa Twiga Bancorp Limited, Hussein Mbululo, akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiana na huduma mbalimbali za kibenki zinazopatikana katika katika Banda la Benki hiyo lililopo katika viwanja vya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ambayo yanaendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere barabara ya Kilwa Dar es Salaam. 

  0 0

   Meneja wa Mradi  wa kuwawezesha wananawake wa  “MWEI”  Grace Lyon  akiwaelimisha baadhi ya wateja waliotembelea banda la Vodacom katika maonesho ya 37 ya sabasaba ,namna ya mradi huo unavyofanya kazi  kwa kuwawezesha wajasiriamali  wadogo wanawake kupata mikopo isiyokuwa na riba mradi huo hadi sasa umewawezesha wanawake zaidi ya 7,000. 
   Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania walioko katika maonesho ya 37 ya sabasaba jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja tayari kabisa kwa kutoa huduma kibandani hapo.
    Afisa wa Vodacom akimueleimisha moja ya wateja waliojitokeza kupata huduma katika banda la Vodacom lililopo katika maonesho ya 37 ya sabasaba jijini Dar es Salaam, Kampuni hiyo sasa imewawezesha wateja wake kulipia bidhaa kupitia huduma ya M pesa katika maonyesho hayo.
  Hili ndilo Banda la Vodacom linavyo onekana kwa nje katika viwanja vya Sabasaba.

  0 0

    Rais Barack Obama wa Marekani na mkewe Michelle wakiangalia ngoma za utamaduni pamoja na bendi ya polisi wakati wa dhifa ya kitaifa  aliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho kikwete. Kushoto ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Serikali ya Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein. PICHA NA IKULU
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Rais Barak Obama wa Marekani kwa Mawaziri wakuu wastaafu pamoja na viongozi wengine wakati wa dhifa ya kitaifa aliyomwandalia mgeni huyo Jumatatu usiku Ikulu jijini Dar es salaam.
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete na wageni wake Rais Barack Obama wa Marekani na mkewe Michelle wakati wa dhifa ya kitaifa aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Usiku. Kushoto ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein na Kulia ni Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda  0 0

   
   Mgeni rasmi na muasisi wa Cherie Blair Foundation for Women(CBFW) Bi. Cherie Blair katika uzinduzi wa Mpango wa Maendeleo ya Wanawake kupitia Tigo Pesa. Pembeni ni Mkurugenzi wa Tigo Tanzania bw. Diego Guitierrez. 
  Mgeni rasmi na muasisi wa Cherie Blair Foundation for Women(CBFW) Bi. Cherie Blair (katikati) katika uzinduzi wa Mpango wa Maendeleo ya Wanawake kupitia Tigo Pesa. Wa karibu kushoto ni Mkurugenzi wa Tigo Tanzania bw. Diego Guitierrez akifuatiwa na Mkuu wa Huduma za Kibenki wa FINCA Adrian Ochieno na Mkurugenzi Mkuu wa FINCA Tanzania Bw. Tom Kocsis. Kutoka kulia ni Meneja Maendeleo ya Kibiashara wa Tigo Bi. Catherine Rutinge na Mkuu wa Huduma za Kibenki wa FINCA Adrian Ochieno.

  0 0

   Wasanii Raymond Kigosi na Steven nyerere wakiwafurahisha washabiki wao kwenye uzinduzi wa Tamasha la filamu la Grandmalt Tanzania Open Fillim Festival jijini Mwanza ambalo liliwashirikisha wasanii wote wa filamu nchini na kuanza jana kwenye kiwanja cha Nyamagana chini ya udhamini wa kinywaji cha Grandmalt na Isamilo Lodge ya Mwanza
   Wasanii wakibadilishana mawazo na baadhi ya wasanii chipukizi wa jiji la Mwanza kwenye uzinduzi wa Tamasha la filamu la Grandmalt Tanzania Open Fillim Festival jijini Mwanza ambalo liliwashirikisha wasanii wote wa filamu nchini na kuanza jana kwenye kiwanja cha Nyamagana chini ya udhamini wa kinywaji cha Grandmalt na Isamilo Lodge ya Mwanza.

   
   Wananchi mbalimbali wa jiji la Mwanza wakishangilia kwa nguvu kwenye uzinduzi wa Tamasha la filamu la Grandmalt Tanzania Open Fillim Festival jijini Mwanza ambalo liliwashirikisha wasanii wote wa filamu nchini na kuanza jana kwenye kiwanja cha Nyamagana chini ya udhamini wa kinywaji cha Grandmalt na Isamilo Lodge ya Mwanza
   Wasanii wakiwa katika picha ya pamoja kwenye uzinduzi wa Tamasha la filamu la Grandmalt Tanzania Open Fillim Festival jijini Mwanza ambalo liliwashirikisha wasanii wote wa filamu nchini na kuanza jana kwenye kiwanja cha Nyamagana chini ya udhamini wa kinywaji cha Grandmalt na Isamilo Lodge ya Mwanza
   mashabiki wakiwa katika nyuso za furaha kwenye uzinduzi wa Tamasha la filamu la Grandmalt Tanzania Open Fillim Festival jijini Mwanza ambalo liliwashirikisha wasanii wote wa filamu nchini na kuanza jana kwenye kiwanja cha Nyamagana chini ya udhamini wa kinywaji cha Grandmalt na Isamilo Lodge ya Mwanza.


  ======== ======    ======== ===========

  Uzinduzi Tamasha la Filamu Grand Malt  lawakuna wakazi wa jiji la mwanza
  Na Mwandishi Wetu, Mwanza

  WAKAZI wa Mwanza na vitongoji vyake juzi walishuhudia vitu tofauti wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Filamu la Wazi la Granda Malt Tanzania, ulioongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Busega, Paul Mzindakaya, lililofanyika kwenye Uwanja wa Nyamagana, jijini hapa.
  Tamasha hilo maarufu kama ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’ lilinogeshwa zaidi na burudani kali kutoka kwa bendi ya Extra Bongo, waliokuwa wakiongozwa na Ally Choki.
  Shamrashamra za uzinduzi huo zilionekana toka mapema alfajiri, wakati wasanii wa Bongo Movie walipojikuta wakibanwa kila mahali walipokuwa wakipita kutambulisha ujio wao.
  Wakati wa uzinduzi huo, wasanii waliokuwepo uwanjani hapo wakiongozwa na Hashima Kambi, walijikuta wakizongwa kwa muda wote, huku mashabiki wakitaka kuwashika au kupiga nao picha.
  Aunty Ezekiel, Irene Uwoya, Jacqueline Wolper, Vicent Kigosi ‘Ray’ na Jacob Steven ‘JB’ walijikuta wakishangiliwa muda wote kama ilivyokuwa kwa Hashim Kambi, Isa Musa ‘Cloud’ na Steve Nyerere.
  Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Busega, Paul Mzindakaya, alisema amefurahishwa mno na tamasha hilo na hasa watu waliokuwa wamejitokeza kwa wingi kushuhudia wasanii wao.
  “Serikali itaendelea kuthamini kwa kiasi kikubwa wasanii wetu na huu ni wakati wa wasanii wa Mwanza kujifunza kutoka kwa mastaa wetu hawa,” alisema.
  Meneja wa kinywaji cha Grand Malt, Consolata Adam alisema, wameamua kulidhamini tamasha hilo kwani wanajua watu wengi kwa sasa wanapenda kutazama filamu za Tanzania.
  “Pia tunapenda kuwashauri muendelee kutumia kinywaji cha Grand Malt ambacho hakina kilevi, badala ya kumpa mtoto vinywaji ambavyo manufaa unaweza pia kumfungashia kinywaji hiki katika matumizi yake,’ alisema.
  Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wasanii hao walisema wamefurahishwa mno na mapokezi waliyoyapata na hawakutarajia kukutana na mashabiki waliowakubali kama hao.
  “Nimefurahishwa mno na hiki kitu, kusema kweli Mwanza tutaendelea kupakumbuka,” alisema JB akiungwa mkono na Ray, huku Wolper akidai lazima atarejea tena. Mratibu wa Tamasha hilo aliye pia Mkurugenzi wa Sophia Records, Musa Kissoky, alisema tamasha hilo litaendelea kwa muda wa wiki moja ambapo filamu mbalimbali zitaonyeshwa.
  Kissoky alisema, tamasha hilo ambalo ni la bure kwa watu wote na kushirikisha mastaa wa filamu hapa nchini, litakuwa la aina yake kwani vitu vitakavyofanyika vitakuwa si vya kawaida.
  Tamasha la Filamu la Grand Malt limeanza rasmi juzi na litamalizika mwishoni mwa wiki huku kukiwa na filamu mbalimbali zitakazooneshwa katika kipindi hicho. Filamu zote hizo ni kutoka Tanzania.
  Tamasha hilo la filamu limedhaminiwa na kinywaji cha Grand Malt kisicho na kilevi ambacho kinazalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) na Isamilo Lodge na Club Lips zote za jiji la Mwanza

  %%%%

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Mstaafu wa Marekani Mhe George W. Bush na Mkewe Laura na Mama Salma Kikwete wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wake wa marais wa Afrika Mashariki leo July 3, 2013 katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mkutano wa wake wa marais wa Afrika Mashariki leo July 3, 2013 katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
  Wageni wakimsikiliza Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mkutano wa wake wa marais wa Afrika Mashariki leo July 3, 2013 katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam. PICHA NA IKULU .

older | 1 | .... | 111 | 112 | (Page 113) | 114 | 115 | .... | 1897 | newer