Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1127 | 1128 | (Page 1129) | 1130 | 1131 | .... | 1896 | newer

  0 0

  Jacquiline Mrisho – MAELEZO

  The Permanent Secretary in President’s Office, Honorable Peter Ilomo has commended the Construction Sector Transparency Initiatives (CoST - Tanzania) for enlightening the Government on the use of public money due to their focus on enhancing transparency.

  Hon. Ilomo said this in a meeting involving various stakeholders in the construction industry held at the Holiday Inn auditorium in Dar es Salaam on behalf of Minister of State, Public Service Management and Good Governance, Honorable Angellah Kairuki.
    
  Hon. Ilomo said that, CoST’s activities focuses on enhancing transparency in construction industry through disclosing information on delivery of public infrastructure something which will help to identify potential efficiency savings which complements Public financial management together with procurement reforms.
                        
  “The work being done by CoST – Tanzania is an opportunity for the Government and the Public in general to track on how Public money is being spent on infrastructure delivery, such tracking will definitely save the country’s money through reduced corruption, improved management and delivery of better performing infrastructure,” Hon. Ilomo said.

  Hon. Ilomo added that, the information included in its Infrastructure Data Standard is required to be disclosed by law to Regulatory Authorities so, CoST is actually helping Procuring Entities to comply with already existing legal and regulatory requirements so as to help them on fulfilling their obligations.
    
  Hon. Ilomo has encouraged CoST and the National Construction Council (NCC) to broaden their efforts and to undertake more disclosure activities especially in Procuring Entities because the output from those activities  will be used by oversight organs to expand their data sources.

  Meanwhile, CoST’s Chairman, Eng. Kazungu Magili explained that, disclosure  of information benefits related to Public financed construction projects will allow the public to know the perfomance of  certain projects so as to raise Government reputation to its citizen.

  “Through this transparency we expect to support the better management of Public finances, prevent corruption and to be used as a catalyst by bringing the disclosed information to the Public which shall help other Government’s Anti-corruption Instruments to make follow up,” Eng. Magili said.

   In this year, CoST intends to evaluate at least ten construction projects including the construction of flyovers, buildings built by Tanzania Buildings Agency (TBA) especially the construction of the new University of Dar es Salaam hostels also buildings built by National Social Security Funds (NSSF) together with National Housing Construction (NHC).

  0 0

  Meneja wa Tawi la Morogoro wa Benki ya KCB Tanzania Emmanuel Mnzava, (aliyekaa katikati) na afisa biashara wa benki ya KCB tawi la morogoro, Lela Kisinda (aliyekaa kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanawake wajasiriamali waliohudhuria na kumaliza mafunzo ya ujasiriamali yalitolewa na benki hiyo katika mkoa wa Morogoro.
  Baadhi ya wanawake wajasiriamali waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa na Benki ya KCB mkoani Morogoro.
  Meneja wa Tawi la Morogoro wa Benki ya KCB Tanzania Emmanuel Mnzava, akizungumza na wanawake wajasiriamali waliohudhuria semina ya mafunzo ya siku tatu kwa ajiri ya wanawake wajasiriamali inayoitwa 2JIAJIRI iliyoandaliwa na benki hyo jijini Morogoro 
  Mwalimu wa Ujasiriamali wa Kituo cha Uwezeshaji na Ushindani Tanzania (TECC) Allen Mhidze akitoa mafunzo ya ujasiriamali yaliyoandaliwa na Benki ya KCB Tanzania kwa wanawake wajasiriamali wa mkoa wa Morogoro. 
  Mwalimu wa Ujasiriamali wa Kituo cha Uwezeshaji na Ushindani Tanzania (TECC) Grace Makoye akitoa mafunzo ya ujasiriamali yaliyoandaliwa na Benki ya KCB Tanzania kwa wanawake wajasiriamali wa mkoa wa Morogoro.

  0 0


  Mkufunzi kutoka tasisi wa masuala ya sheria juu manunuzi ya Umma , Hamis Tika akizungumza na watumishi wa taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete.
  Baadhi ya wafanyakazi wa tasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete wakisikiliza kwa makini juu ya mafunzo ya masuala ya manunuzi.

  Mkurugenzi wa Maendeleo ya taaluma PSPTB, Ally Songoro akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete .

  Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Profesa Mohamed Janabi, akizungumza kabla ya kumkaribisha kaimu mkurugenzi mkuu wa PSPTB .


  .Kaimu Mtendaji mkuu wa PSPTB,Godfred Mbanyi akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya maofisa manunuzi na watendaji wa tasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete, Muhimbili jijini Dar es Salaam.
  Afisa Mwanadamizi wa Mahusiano ya Umma na Masoko Shamimu Mdee na mratibu mkuu wa utafiti na ushauri PSPTB Amos Kazinza wakifuatilia mafunzo


  0 0


   Wananchi wakimuangalia dereva wa teksi aliyejeruhiwa baada ya gari lake lenye namba za usajili T 625 AWS kugongana na gari dogo lenye namba usajili T 214 CFX wakati likiingia barabara ya Nyerere likitokea Jengo la Kibiashara la Quality Centre Dar es Salaam leo asubuhi.
   Mwonekano wa Teksi hiyo namba T 625 baada ya kugongana.
   Wananchi wakiangalia ajali hiyo.
   Wananchi wakiangalia gari dogo aina ya Toyota Corolla lenye namba T 214 CFX baada ya kuyagonga magari namba T 741 DEK na T 596 BCG katika eneo hilo la Mtava.
   Askari wa Usalama Barabarani akipima ajali hiyo.
   Gari dogo aina ya Toyota Corolla lenye namba T 214 CFX likiwa eneo la ajali kabla ya kuondolewa.

  Na Dotto Mwaibale

  DEREVA wa gari dogo teksi yenye namba za usajili T 625 AWS amenusurika kufa baada ya gari lake alilokuwa akiliendesha kutoka mjini akielekea Uwanja wa Ndege kugongana na gari dogo lenye namba T 214 CFX aina ya Corolla lililokuwa likiingia Barabara ya Nyerere likitokea Jengo la Biashara la Quality Centre eneo la Mtava jijini Dar es Salaam leo asubuhi.

  Mashuhuda wa ajali hiyo wakizungumza na waandishi wa habari eneo la ajali walisema ajali hiyo ilisababishwa na gari hilo dogo aina ya Corolla lililokuwa likiingia barabara ya Nyerere bila kuchukua tahadhari.

  "Chanzo cha ajali hii ni gari hilo dogo aina ya corolla ambalo liliingia barabara ya Nyerere bila ya dereva wake kuchukua tahadhari na kama dereva wa gari namba T 625 AWS angekuwa katika mwendo wa kawaida madhara yake yasingekuwa makubwa kiasi hicho" alisema shuhuda aliyejitambulisha kwa jina la Mlugulu.

  Mlugulu alisema baada ya magari hayo kugongana gari hilo aina ya Corolla liligeuka na kwenda kuyagonga magari mengine namba T 596 BCG na T 741 DEK yaliyokuwa yamesimama yakisubiri kuingia upande ambao lipo Jengo la Kibiashara la Quality Centre.

  Katika ajali hiyo gari namba T 625 AWS liliacha njia na kuhamia upande wa pili wa barabara ya kutoka Tazara kwenda mjini.

  Baada ya ajali askari wa usalama barabarani walifika na kupima ajali hiyo na kuchukua maelezo ya madereva wote wanne ambapo magari mawili T 214 CFX na T 625 AWS yakiondolewa na  magari ya kukokota magari mabovu (Breck Down) na kupelekwa kituo cha Polisi cha Chang'ombe Temeke jijini Dar es Salaam kwa hatua zingine za kisheria.

  0 0  0 0  JPCC kati ya Tanzania na Malawi ni chachu ya kuimarisha mahusiano

  Wajumbe wanaoshiriki katika Kikao cha 4 cha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPCC) kati ya Tanzania na Malawi kilichofunguliwa leo jijini Lilongwe, Malawi wamehimizwa katika majadiliano yao ya siku tatu kubuni mkakati utakaowezesha kutatua changamoto zinazojitokeza kutokana na muingiliano mkubwa wa ngazi mbalimbali za ushirikiano baina ya wananchi wa mataifa hayo mawili.

  Kauli hiyo imetolewa na Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania katika ngazi ya Wataalam, Balozi Ramadhan Mwinyi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alipokuwa anasoma hotuba ya ufunguzi.

  "Kama mnavyofahamu kunapokuwa na maingiliano makubwa ya wananchi wa nchi mbili kama zilivyo nchi zetu, changamoto haziwezi kukosa kujitokeza. Hivyo ni jukumu letu sisi wataalamu kubuni mkakati wa kuhakikisha kuwa changamoto hizo zinashughulikiwa haraka iwezekanavyo".

  Balozi Mwinyi alieleza kuwa kikao hicho ni fursa nzuri kwa Serikali za Tanzania na Malawi kujadili masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya nchi zao katika maeneo tofauti ikiwemo uchumi, uwekezaji, biashara, kutunza mazingira, elimu, Tehama, kilimo, uhamiaji, uchukuzi na masuala ya ulinzi na usalama, Hivyo alihimiza wajumbe wa pande zote mbili kuwa wabunifu katika majadiliano yao ili watoke na mipango inayotekelezeka kwa kuwa wananchi wanachohitaji ni maendeleo na sio mikakati inayoishia katika makabrasha. 

  Aidha, Balozi Mwinyi aliekeza kuwa watu wengi walistaajabu kusikia ujumbe wa Tanzania unakuja Malawi kushiriki kikao hiki kama walivyostaajabu kuona Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipofanya mazungumzo hivi karibuni na Rais wa Malawi, Mhe. Prof. Peter Mutharika pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa, Ethiopia. Alisema hakuna cha kustaajabisha hapo, isipokuwa ifahamike lengo kuu la pande zote mbili ni kuona uhusiano kati ya Tanzania na Malawi unaimarishwa na kwamba mkutano huo ni ushahidi kuwa nchi hizi mbili zipo karibu zaidi kuliko hapo awali.

  Naibu Katibu Mkuu aliihakikishia Serikali ya Malawi kuwa Serikali ya Tanzania imedhamiria kushirikiana na nchi hiyo katika kuboresha mahusiano ya kidiplomasia, uchumi na kijamii, hivyo alisisitiza umuhimu wa yale yote yatakayoafikiwa katika mkutano huo yanatekelezwa katika muda uliopangwa. Alishauri iundwe timu ya ngazi ya Makatibu Wakuu ambayo itakuwa inakutana kila baada ya miezi sita kutathmini utekelezaji wa maazimio ya kikao hicho.

  Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Malawi, Dkt. Dalitso Kabambe alisisitiza umuhimu wa nchi hizi mbili kuweka mikakati itakayorahisisha wananchi kufanya biashara bila vikwazo. "Bisahara ni jambo muhimu lazima tuhakikishe kuwa Serikali zetu zinaweka mazingira mazuri ili wananchi wafanye biashara kwa wepesi". 

  Kikao hicho kinatarajiwa kufungwa rasmi na Mawaziri wa Mambo ya Nje siku ya Jumapili tarehe 05 Februari 2017 ambapo Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anatarajiwa kuwasili Malawi tarehe 04 Februari 2017. Mawaziri hao pia wataweka saini Mikataba mitatu ya ushirikiano katika mashauriano ya kisiasa na kidiplomasia, usafiri wa anga na utalii.

  Wajumbe wa Tanzania katika kikao hicho wanatoka katika sekta mbalimbali wakiwemo wajumbe kutoka mikoa miwili ya Mbeya na Ruvuma inayopakana na Malawi ambao wanaongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Amos Makalla.

  Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Malawi na Mwenyekiti Mwenza wa Kikao cha JPCC kati ya Tanzania na Malawi, Dkt. Kalitso Kabambe akisoma hotuba ya iufunguzi na ukaribisho. 
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Mwinyi akisoma houtuba ya ufunguzi wa kikao cha Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JPCC) kati ya Tanzania na Malawi. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Malawi, Dkt. Dalitso Kabambe. Kikao hicho kinafanyika Lilongwe, Malawi kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe 03 Februari 2017. 
  Wajumbe wa Tanzania wakisikiliza hotuba za Makatibu Wakuu. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Amos Makalla, Mkurugenzi Msaidizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Suleiman Salehe na Kaimu Mkurugenzi kutoka Mamlka ya Viwanja vya Ndege. 
  Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga, Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Ali Ubwa na mjumbe mwingine ambaye jina lake halikupatikana. 

  Bw. Kalitso Kabambe akiwa na Balozi wa Malawi nchini Tanzania. 
  Sehemu ya ujumbe wa Malawi ukifuatilia hotuba za ufunguzi 
  Wajumbe wa pande zote mbili wakiwa katika kikao cha JPCC 
  Naibu Katibu Mkuu, Balozi Mwinyi akihojiwa na Mwandishi wa TBC, Bw. Hosea Cheo 
  Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Victoria Mwakasege akihojiwa na Mwandishi wa TBC 
  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Amos Makalla akifanya mahojiano na Mwandishi wa TBC

  0 0


  Timu ya Taifa ya Tanzania ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 "Serengeti Boys" imefuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri huo.

  Taarifa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), imethibitisha hilo pasi na shaka kwamba Tanzania ndiyo yenye nafasi ya kucheza fainali hizo zitakazofanyika kuanzia Aprili 2, mwaka huu huko Gabon baada ya Madagascar kuenguliwa kutokana na kutoandaa vema fainali hizo.

  Taarifa hizo za CAF kutoka Libreville, nchini Gabon zinathibitisha kwamba Kamati ya Utendaji ya CAF imeipa ushindi Tanzania dhidi ya timu ya Jamhuri ya Congo ambayo katika michuano ya kufuzu, ilimchezesha mchezaji Langa Lesse Bercy aliyezidi umri kinyume cha kanuni za kanuni za michuano hiyo.

  Katika michezo hiyo ya kirafiki na ushindani, Serengeti Boys ilipoteza mchezo wa 16 tu dhidi ya Congo ilihali kulikuwa na rufaa kuhusu mmoja wa wachezaji wa Congo ambaye alionekana kuwa na umri mkubwa. Mchezaji huyo ni Langa Lesse Bercy.

  CAF, kwa nyakati tofauti ikiwamo Novemba 10, 2016 na Desemba 15, mwaka jana walitoa agizo kwa Congo Brazzaville kumpeleka kijana huyo Cairo, Misri kwa ajili ya vipimo vya MRI ili kuthibitisha au kupangua madai ya Tanzania. Congo Brazzaville hawakupeleka.

  Januari 12, mwaka huu 2017 iliamriwa kwa mara nyingine kijana huyo kupelekwa jijini Libreville, Gabon ili kufanyiwa vipimo vya MRI, lakini hakupelekwa na katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya CAF, kimeamua kumaliza suala hilo na kuipa ushindi Tanzania.

  Siku 10 ziliisha Januari 23, mwaka huu lakini tangu hapo kumekuwa na maswali ya kutosha kuhoji nafasi ya Tanzania yakitoka kwa Watanzania kupitia wanahabari, lakini TFF ilisimama kidete kutangaza kuwa tunasubiri uthibitisho wa CAF ambayo leo Februari 3, mwaka huu imetangaza rasmi kuwa Tanzania itacheza fainali hizo.

  0 0


  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bw. Bernard Konga (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jana jini Dar es salaam (hawapo pichani) kuhusu maboresho yaliyofanywa na Mfuko. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uhai wa Mfuko Bw. Baraka Maduhu.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Bernard Konga akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Bi. Angela Mziray na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uhai wa Mfuko Bw. Baraka Maduhu.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bw. Bernard Konga (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu ushiriki wa Mfuko katika kupunguza magonjwa yasiyoambukiza . Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Bi. Angela Mziray.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bw. Bernard Konga (wa pili kutoka kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu ongezeko la usajili wa vituo vya kutolea huduma kwa wanachama wa Mfuko. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uhai wa Mfuko Bw. Baraka Maduhu. 
  Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia maelezo ya Kaimu Mkurugenzi wa NHIF Bw. Bernard Konga .(Picha na Frank Mvungi-Maelezo)

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi wa Kuwait nchini Mhe.Jasem Ibrahim Al Najem walipokutana kwa mazungumzo Wizarani Jijini Dar es Salaam. Mazungumzo hayo yalijikita katika kujadili namna ya kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo nchini itakayo fadhiliwa na serikali ya Kuwait ikiwemo uchimbaji visima vya maji, miradi ya kuendeleza elimu na kuboresha sekta ya afya. 
  Waziri Mhe. Mahiga akimsikiliza Balozi wa Kuwait nchini Mhe.Najem 
  Waziri Mahiga na Balozi wa Kuwait nchini wakifurahia jambo

  0 0

   Daktari Bingwa wa magonjwa ya macho Dk. Mustafa Yusufali akimpima macho, Alphonce Joseph mmoja wa wagonjwa waliofika katika Hospitali ya Kairuki Mikocheni jijini Dar es Salaam, ikiwa sehemu ya maadhimisho ya 18 ya Kumbukizi  ya  Hayati Prof. Hubert Kairuki, ambapo upimaji wa awali wa afya ya macho umefanyika kuanzia Februari 3-4 kwa gharama za hospitali hiyo pamoja na utoaji wa miwani ya kusomea na upasuaji mdogo bure.

   Daktari Bingwa wa magonjwa ya macho Dk. Mustafa Yusufali akimpima macho, Alphonce Joseph mmoja wa wagonjwa waliofika katika Hospitali ya Kairuki Mikocheni jijini Dar es Salaam, ikiwa sehemu ya maadhimisho ya 18 ya Kumbukizi  ya  Hayati Prof. Hubert Kairuki. 
  Muuguzi wa Hospitali ya Kairuki Mikochezni jijini Dar es Salaam, Athuma Makolela akichukua maelezo ya mmoja wa wagonjwa wa macho waliofika hospitalini hapo kupata huduma zilizokuwa zikitolewa kwa gharama za hospitali hiyo. 
   Dk. Kenneth Munanu akimpima macho mgonjwa aliyefika katika hospitali ya Kairuki Mikocheni jijini Dar es Salaam.
   Dk. Kenneth Munanu akimpima macho mgonjwa aliyefika katika hospitali ya Kairuki Mikocheni jijini Dar es Salaam.
   Dk. Kenneth Munanu akimpima macho mgonjwa aliyefika katika hospitali ya Kairuki Mikocheni jijini Dar es Salaam.
   Dk. Kenneth Munanu akimpima macho mgonjwa aliyefika katika hospitali ya Kairuki Mikocheni jijini Dar es Salaam.
   Dk. Kenneth Munanu akimpima macho mgonjwa aliyefika katika hospitali ya Kairuki Mikocheni jijini Dar es Salaam.
  Wananchi wakipata hudumza za matibabu ya Afya ya Macho katika hospitali ya Kiruki Mikocheni. Huduma hizo zimegharamiwa na hosptali hiyo.   
   Wagonjwa wakisubiri kupata huduma.
   Mgonjwa akipima macho.
   Regina Shadrack akipimwa macho.
   Huduma zikiendelea.
  wananchi wakisubiri kupata huduma.

  0 0


  Na: Frank Shija – MAELEZO

  Wataalamu wa Tathmini ya Athari za Mazingira nchini wametahadharishwa kuwepo kwa matapeli wanaingilia taaluma hiyo kwa lengo la kufanya udanganyifu na kujipatia kipato.

  Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba wakati akifungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wataalamu wa Tathmini ya Athari za Mazingira Tanzania (TEEA) leo Jijini Dar es Saalam.

  Makamba amesema kuwa taaluma ya tathmini ya Athari za Mazingira ni ya shughuli ambayo inahitaji mkubwa sana na ni kwa mujibu wa sheria za nchi lakini kumekuwapo na makanjanja ambao wamekuwa wakifanya uraghai kwa wawekezaji na kutia doa tasnia nzima ya taaluma ya uthamini wa athari za mazingira.

  “Serikali inakusudia kubadilisha kanuni na taratibu ili kuongeza udhibiti wa udanganyifu katika eneo la Tathmini ya Athari za Mazingira(IAE) kwa kuweka viwango stahiki kwa wataalamu wa tathmini ya athari za mazingira vitakavyozingatia elimu na uzoefu,” alisema Makamba.

  Aliongeza kuwa ni vyema sasa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kushirikiana na Chama cha Wataalumu hao kushirikiana kuhakikisha taaluma hiyo haingiliwi na makanjanja ili kufanikisha utoaji wa huduma zenye viwango stahiki na vya kuridhisha.

  Awali akiwasilisha salamu za Bodi ya Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Profesa Ruben Mwamakimbullah amesema amemshukuru Waziri Makamba kwa kukubali kujumuika na wataalamu hao katika mkutano huo muhimu na kuongeza kuwa wao kama Bodi watafanyia kazi ushauri wote alioutoa na kuahidi kuongeza ufanisi katika kutekeleza majukumu yao ili kuleta heshi kwa tasnia ya tathmini ya athari za mazingira na taifa kwa ujumla.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Mhandisi Bonaventure Baya amesema kuwa mkutano huo umekuwa ukiwakutanisha Wataalamu wa Tathmini ya Athari za Mazingira nchini ambapo utumia fursa hiyo kukumbushana mambo yanayohusu weledi na majukumu yao.

  Mkurugenzi huyo amesema kuwa mkutano huo ni wa tatu kufanyika ambapo umetanguliwa na mikutano iliyofanyika februari 2011 na Machi 2015 na kuongeza kuwa NEMC imekuwa ikiratibu mkutano huo kwa lengo la kuwakutanisha Wataalamu wa Tathmini ya Athari za Mazingira nchini ili kujadili changamoto zao na kupeana uzoefu.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January Yusuph Makamba akiongea na wataalamu wa Mazingira katika Mkutano wa Tatu wa Chama cha Wataalam wa Tathminiya Athari za Mazingira nchini Dar es Salaam jana (leo) ).
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January Yusuph Makamba akiongea na wataalamu wa Mazingira katika Mkutano wa Tatu wa Chama cha Wataalam wa Tathminiya Athari za Mazingira jijini Dar es Salaam jana (leo) ).
  Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Mwandisi Bonaventure Baya akiongea na wataalamu wa Mazingira katika Mkutano wa Tatu wa Chama cha Wataalam wa Tathmini ya Athari za Mazingira nchini Dar es Salaam jana (leo)
  Mjumbe wa Bodi wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Prof. Ruben Mwamakimbullah akitoa salamu za Bodi kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya Mazingira Prof. Salome Misana katika Mkutano wa Tatu wa Chama cha Wataalam waTathmini ya Athari za Mazingira Dar es Salaam jana (leo))
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mh. January Yusuph Makamba akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa Mazingira katika Mkutano wa Tatu wa Chama cha Wataalam wa Tathmini ya Athari za Mazingira nchini Dar es Salaam jana (leo).(Pichazotena Benjamin Sawe)

  0 0

  Hapa ni katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga ambako leo Ijumaa Februari 03,2017 kumefanyika Kongamano la wafanyabiashara kutoka wilaya ya Shinyanga lililoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo(TCCIA) kwa kushirikiana na mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro.
  Kongamano hilo lililokutanisha wafanyabishara kutoka Shinyanga Mjini na Vijijini na nje ya mkoa wa Shinyanga  lililenga la kuibua na kujadili fursa za uwekezaji zilizopo mkoani Shinyanga na kujadili changamoto zinazowakabili wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo.
  Mgeni rasmi katika Kongamano hilo ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro.Mwandishi wetu Kadama Malunde, ametuletea picha za matukio yaliyojiri katika kongamano hilo lililoanza majira ya saa 11:25 jioni na kumalizika saa 4:06 usiku…Tazama hapa chini
  Kushoto ni mgeni rasmi katika kongamano la wafanyabiashara ,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo mkoa wa Shinyanga,(TCCIA) Mchungaji Dr. Kulwa Ezekiel Meshack wakiwa katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga leo Ijumaa Februari 3 2017Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
  Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
  Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
  Tunafuatilia kinachoendelea
  Sekretariati wakiwa ukumbini
  Afisa Tawala wilaya ya Shinyanga Charles Maugira aliyemwakilisha katibu tawala wa wilaya hiyo akitambulisha viongozi wa serikali waliohudhuria kongamano hilo
  Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
  Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Geofrey Ramadhan Mwangulumbi akiwasalimia wafanyabiashara
  Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Geofrey Ramadhan Mwangulumbi akiwasalimia wafanyabiashara,kulia ni naibu meya wa manispaa ya Shinyanga Agnes Machiya
  Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo mkoa wa Shinyanga Mchungaji Dr. Kulwa Ezekiel Meshack akizungumza wa kufungua kongamano hilo ambapo alisema wameamua kukutana ili kujadili fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo mkoani Shinyanga.
  Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo mkoa wa Shinyanga Mchungaji Dr. Kulwa Ezekiel Meshack alitumia fursa hiyo kumpongeza rais John Pombe Magufuli kwa kuhimiza uchumi wa viwanda na kuahidi kuwa wafanyabiashara mkoa wa Shinyanga wapo tayari kumuunga mkono
  Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo mkoa wa Shinyanga Mchungaji Dr. Kulwa Ezekiel Meshack pia aliiomba serikali kupunguza rundo la kodi kwawafanyabiashara kwani kodi hioz zinawakatisha tamaa kuendelea kufanya biashara
  Meneja wa Benki ya Maendeleo -TIB Kanda ya ziwa Zacharia Kicharo akitoa mada wakati wa kongamano hilo
  Meneja Miradi kutoka Tanzania Local Enterprise Development (TLED) Stanley Magese akitoa mada wakati wa kongamano hilo
  Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
  Kongamano linaendelea
  Mwalimu wa walipa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Shinyanga Anthony Faustine akitoa mada kuhusu ulipaji kodi
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwahutubia wafanyabiashara wilaya ya Shinyanga waliohudhuria kongamano hilo ambapo aliwaasa kujitokeza kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo viwanda kwani serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais John Pombe Magufuli inataka watanzania kuwekeza katika viwanda
  Mkuu huyo wa wilaya Josephine Matiro alisema serikali ya wilaya ya Shinyanga ipo tayari kushirikiana na wafanyabishara katika kukuza uchumi wa mkoa wa Shinyanga
  Matiro aliwapongeza wafanyabiashara waliojitokeza kwa wingi katika kongamano hilo na kuwaomba kuendelea kuwekeza
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga akizungumza
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisisitiza jambo
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza ukumbini
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro(kushoto) akiteta jambo na mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Shinyanga Mchungaji Dr. Kulwa Ezekiel Meshack na katibu wa Katibu wa TCCIA mkoa wa Shinyanga Marcelina Saulo
  Mc Mama Sabuni anayeongoza Kongamano hilo akiwa ukumbini
  Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
  Wafanyabiashara wakifuatilia kinachoendelea ukumbini
  Wafanyabisahara wakiwa ukumbini.Kulia ni mkurugenzi wa Vigimark Hotel bi Victoria Majige
  Tunafuatilia kinachoendelea
  Kulia ni Katibu wa TCCIA mkoa wa Shinyanga Marcelina Saulo,kushoto ni Afisa tawala wilaya ya Shinyanga Charles Maugira wakifuatilia kinachoendelea ukumbini
  Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga Said Pamui akitoa mada wakati wa kongamano hilo ambapo aliwasisitiza wafanyabiashara kujenga mazingira ya kukopesheka,kuwa waaminifu na kulipa madeni yao kwa wakati kama wanavyokubaliana na benki 
  Pamui alitumia fursa hiyo kuwapongeza wafanyabiashara wilaya ya Shinyanga kujitokeza kwa wingi katika kongamano hilo na kuwataka kujenga utamaduni wa kujitokeza katika vikao na mikutano mbalimbali ili kubadilishana uzoefu na kupeana mbinu mpya za kufanya biashara.
  Wafanyabiashara wakifuatilia yanaliyokuwa yanajiri ukumbini
  Mkurugenzi wa Vigimark Hotel iliyopo mjini Shinyanga Victoria Majige akizungumzia changamoto ya ubovu wa barabara inayoelekea katika hoteli hiyo ambapo aliiomba serikali kutengeneza barabara hiyo walau kwa kiwango cha moramu 
  Mfanyabshara wa Uyoga wilayani Shinyanga Hamisa Nuhu akichangia hoja wakati wa kongamano hilo
  Meneja wa shule ya Msingi Little Treasures Mwita Nchagwa akichangia hoja ukumbini
  Wafanyabiashara wakiwa ukumbini
  Tunafuatilia kinachoendelea
  Katibu wa Wachimbaji wadogo wa madini mkoa wa Shinyanga Gregory Kigusi akichangia hoja ukumbini
   Katibu wa TCCIA Marcelina Saulo akielezea kuhusu namna wafanyabishara wanavyokerwa na bei kubwa ya mabango ya matangazo na kuiomba serikali kuangalia namna ya kupunguza gharama za matangazo kwani inawakatisha tamaa wafanyabishara na kuamua kuondoa matangazo
  Afisa Biashara wa manispaa ya Shinyanga Sunday akieleza namna serikali inavyofanya kuhakikisha kuwa gharama za matangazo inapungua

  Mkuu wa Polisi wilaya ya Shinyanga Dotto Mdoe akijitambulisha kwa wafanyabishara ambapo alisema serikali itaendelea kuwalinda wafanyabiashara katika kuuweka mji wa Shinyanga salama
  MC Mama Sabuni akifanya yake ukumbini
  Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga Gasto Mkono akizungumza wakati kufunga kongamano hilo ambapo aliwaomba wafanyabiashara kujitokeza kutoa taarifa za watumishi ama idara yoyote inayowaomba rushwa katika biashara zao.

  Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

  0 0

  Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama ametangaza mbio za kuelekea Tamasha la Pasaka ambalo linataraji kufanyika April 16 Mwaka huu

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Alex Msama amesema kuwa Tamasha hilo la kusifu na kuabudu,ambalo ni kubwa nchini kuliko matamasha yote litakuwa la aina yake katika mwaka huu wa 2017.
  Msama amesema kuwa kauli mbiu ya Tamasha la Pasaka mwaka huu itakuwa ni ''Umoja na upendo kudumisha amani ndani ya nchi yetu'' ,Lengo ikiwa ni kudumisha amani ndani ya nchi yetu  katika kipindi chote
   
  “Napenda kuchukua fursa hii kuwaambia wapenzi wa muziki wa injili kuwa Msama Promotion imejipanga vyema kwa mwaka huu kuhakikisha kuwa inawaleta watu pamoja katika sehemu ambayo walikuwa wanaipenda ya kumtukuza mungu kila wakati wa pasaka kwa kuimba pamoja katika Tamasha la Pasaka wakiwa na wanamuziki maharufu wa muziki wa injili nchini”amesema Msama.

  Msama ameweka wazi kuwa kutokuwepo kwa Tamasha la Krissmas kumezidi kuongeza ari ya watu kutaka kushiriki tamasha la Pasaka na kujionea mambo mbalimbali yanayolijumuisha tamasha hilo ambalo huandaliwa kwa umakini mkubwa.
   
  Msama ametoa wito kwa wapenzi wa muziki wa injili kujitokeza kwa wingi katika Tamasha hili ili kuweza kumsifu Mungu kwa njia ya uimbaji. 
   
  Amesema kuwa tamasha hilo kwa mwaka huu litafanyika katika mikoa mitano ili kuwapa fursa watu wa mikoani kushuhudia waimbaji wa nyimbo za injili na kusema kuwa tamasha hilo litaanza katika mkoa wa Dar es Salaaam.
   
  Msama alimaliza kusema kuwa kwa sasa yupo katika hatua za kukamilisha vibali mbalimba vkiwemo vya Baraza Sanaa nchini (BASATA),yote hiyo ni kuhakikisha mambo yote yanakwenda katika mstari ulionyooka

  0 0

  Sio kila unachosoma ndio ndoto yako ya baadae, unaweza ukasoma Udaktari au Sheria lakini pia ukawa na kipaji cha zaidi ya ulichosomea na kujikuta unavutiwa kukitumia kipaji hicho kwa ajili ya jamii inayokuzunguka.

  The Beauty TV ilizungumza mambo mengi na Sheria Ngowi na unaweza kumtazama hapa na usisahau ku-subscribe kwa ajili ya taarifa zaidi kutoka The Beauty TV.

  0 0

  Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar H. Jensen (kulia) akimkabidhi mmoja wa wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi yake. Msaada huo ulitolewa na Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) unaofadhiliwa na Shirika la DANIDA la nchini Denmark na Shirika la DFID kutoka Uingereza. Kushoto ni Mkurugenzi wa LSF, Kees Groenendijk akishuhudia. Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar H. Jensen (kulia) akimkabidhi mmoja wa wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi yake. Msaada huo ulitolewa na Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) unaofadhiliwa na Shirika la DANIDA la nchini Denmark na Shirika la DFID kutoka Uingereza. Kushoto ni Mkurugenzi wa LSF, Kees Groenendijk akishuhudia.Mshauri Kiongozi wa DFID Tanzania, Helen Barnes (kulia) akimkabidhi mmoja wa wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi yake. Msaada huo ulitolewa na Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) unaofadhiliwa na Shirika la DANIDA la nchini Denmark na Shirika la DFID kutoka Uingereza. Mshauri Kiongozi wa DFID Tanzania, Helen Barnes (kulia) akimkabidhi mmoja wa wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi yake. Msaada huo ulitolewa na Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) unaofadhiliwa na Shirika la DANIDA la nchini Denmark na Shirika la DFID kutoka Uingereza.Mjumbe wa Bodi ya LSF, Dk. Benson Bana (kulia) akimkabidhi mmoja wa wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi yake. Msaada huo ulitolewa na Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) unaofadhiliwa na Shirika la DANIDA la nchini Denmark na Shirika la DFID kutoka Uingereza. Katikati akishuhudia ni, Mkurugenzi wa LSF, Kees Groenendijk. Mjumbe wa Bodi ya LSF, Dk. Benson Bana (kulia) akimkabidhi mmoja wa wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi yake. Msaada huo ulitolewa na Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) unaofadhiliwa na Shirika la DANIDA la nchini Denmark na Shirika la DFID kutoka Uingereza. Katikati akishuhudia ni, Mkurugenzi wa LSF, Kees Groenendijk.Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar H. Jensen akizungumza katika hafla ya Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) kuwakabidhi wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi zao zinazotoa msaada wa kisheria kwa jamii. Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar H. Jensen akizungumza katika hafla ya Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) kuwakabidhi wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi zao zinazotoa msaada wa kisheria kwa jamiiMshauri Kiongozi wa DFID Tanzania, Helen Barnes akizungumza katika hafla ya Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) kuwakabidhi wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi zao zinazotoa msaada wa kisheria kwa jamii. Mshauri Kiongozi wa DFID Tanzania, Helen Barnes akizungumza katika hafla ya Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) kuwakabidhi wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi zao zinazotoa msaada wa kisheria kwa jamii.Mjumbe wa Bodi ya LSF, Dk. Benson Bana akizungumza katika hafla ya Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) kuwakabidhi wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi zao zinazotoa msaada wa kisheria kwa jamii. Mjumbe wa Bodi ya LSF, Dk. Benson Bana akizungumza katika hafla ya Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) kuwakabidhi wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi zao zinazotoa msaada wa kisheria kwa jamiiBaadhi ya laptop zilizotolewa kwa wasaidizi hao wa kisheria kwa jamii. Baadhi ya laptop zilizotolewa kwa wasaidizi hao wa kisheria kwa jamii.Viongozi hao wakiwa katika hafla hiyo leo jijini Dar es Salaam. Viongozi hao wakiwa katika hafla hiyo leo jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi wa LSF, Kees Groenendijk (kulia) akimkabidhi mmoja wa wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi yake. Msaada huo ulitolewa na Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) unaofadhiliwa na Shirika la DANIDA la nchini Denmark na Shirika la DFID kutoka Uingereza. Mkurugenzi wa LSF, Kees Groenendijk (kulia) akimkabidhi mmoja wa wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria laptop kwa niaba ya taasisi yake. Msaada huo ulitolewa na Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) unaofadhiliwa na Shirika la DANIDA la nchini Denmark na Shirika la DFID kutoka Uingereza.

  MFUKO wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF) umekabidhi laptop 170 kwa asasi mbalimbali zinazotoa msaada wa kisheria kwa wananchi wahitaji katika mikoa anuai nchini Tanzania. Akizungumza kabla ya kukabidhi vitendea kazi hivyo kwa wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa wa kisheria, Mjumbe wa Bodi ya LSF, Dk. Benson Bana aliwataka sema shirika hilo linaamini zitatumika katika kutatua changamoto anuai kwa asasi husika ikiwa ni chachu ya kuongeza ufanisi kwa kazi zao
  Laptop hizo 170 zimekabidhiwa leo jijini Dar es Salaam na Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar H. Jensen huku akizitaka asasi hizo muhimu kuendelea kuisaidia jamii inayoitaji msaada wa kisheria popote walipo kwani zipo familia hasa wajane wanaitaji na wanashindwa namna ya kupata. LSF ni mfuko huru wa msaada wa kisheria unaotoa msaada kwa mashirika watoa msaada wa kisheria, kitaasisi na kiufundi ili kuongeza uwazi na uwajibikaji katika sekta ya sheria chini ya ufadhili wa Shirika la DANIDA la nchini Denmark na Shirika la DFID la Uingereza.Afisa Ufuatiliaji na Matokeo wa Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF), Saada Mkangwa (kushoto mbele) akiwasilisha mada ya kuwajengea uwezo wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria leo jijini Dar es Salaam. Afisa Ufuatiliaji na Matokeo wa Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF), Saada Mkangwa (kushoto mbele) akiwasilisha mada ya kuwajengea uwezo wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria leo jijini Dar es Salaam.Meneja Ufuatiliaji na Matokeo wa Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF), Said Chitong (kulia) akiwasilisha mada ya kuwajengea uwezo wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria leo jijini Dar es Salaam. Meneja Ufuatiliaji na Matokeo wa Mfuko wa Fedha za Msaada wa Kisheria (LSF), Said Chitong (kulia) akiwasilisha mada ya kuwajengea uwezo wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria leo jijini Dar es Salaam.Sehemu ya wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria wakiwa katika semina ya kuwajengea uwezo. Sehemu ya wawakilishi wa mikoa wa mashirika washauri wa msaada wa kisheria wakiwa katika semina ya kuwajengea uwezo.

  0 0


  Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

  Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma imevuna jumla ya wanachama wapya 102 kutoka chama cha Act Wazalendo na Chama cha Wananchi Cuf.

  Wanachama hao ambao wamepokelewa na mjumbe wa halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kigoma Prof Joyce Ndalichako ambaye aliwakabidhi wanachama hao wapya kadi 102 , akiwemo Mwenyekiti wa Chama cha ACT wazalendo Wilaya ya Kakonko pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha wananchi CUF Wilayani humo .

  Zoezi hilo alilifanya jana katika Sherehe za maadhimisho ya Miaka 40 ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kakonko, ambapo Wanachama kutoka katika Vyama vya ACT wazalendo, NSSR Mageuzi, CHADEMA na Chama cha Wananchi CUF ambao waliamua kuvihamba Vyama hivyo kutokana na Waanzilishi wa Vyama hivyo kukosa uzalendo kwa Nchi yao kwa kuwashawishi viongozi walio chaguliwa na vyama hivyo kuipinga Serikali katika masuala ya Maendeleo.

  Sambamba na zoezi hilo Ndalichako aliwaomba Wanachama Wa CCM Wilayani humo katika uchaguzi wa viongozi wa Chama 2017 kuhakikisha Wanachagua viongozi wazalendo Wanaoweza kukijenga chama katika Misingi ya Uzalendo, amani na mshikamano kama Waanzilishi wa Chama hicho walivyo kijenga Chama hicho ambacho kinazidi kuwa ni Chama kinacho wajali wanyonge.

  Alisema Kauli mbiu ya maadhimisho ya Miaka 40 ya Chama Cha mapinduzi ni CCM mpya na Tanzania mpya .kauli hiyo haiwezi kukamilika endapo chama hicho kitapata viongozi wasaliti wasio na mapenzi na Chama ambao wengi wao wametumika kununuliwa na vyama vya upinzani katika kipindi cha uchaguzi wa mwaka 2015 ambapo CCM imepoteza majimbo wengi kutokana na viongozi hao waliokisaliti Chama.

  "Nianze kwa kuwapongeza Wanachama walio amua kurudi katika Chama cha Mapinduzi wamefanya jambo zuri sana, CCM ni chama ambacho kikitoa ahadi zake lazima zikamilike na ni chama chenye misingi ya uwajibikaji, uzalendo amani na ushirikiano ndio maana Wananchi wengi wanaendelea kukiamini chama chetu kutokana nuwaombe Wanachama Wenzangu tusikubali kurubuniwa na baadhi ya watu wasio kipenda chama kikiuka Misingi ya Waanzilishi Wa chama chetu walioiweka ambayo inatusaidia Chqma hiki kuwa na Amani na mshikamano tofauti na Vyama vingine", alisema Ndalichako.

  Kwa upande wake Katibu Wa Chama cha Mapinduzi Mkoa Wa Kigoma,Naomi Kapambala aliwashukuru Wanachama hao kwa kukiamini Chama hicho na kuamia kujiunga! Aliwaahidi Wanachama hao kuwa Chama hicho kitaendelea kutenda haki na kuwatumikia Wananchi katika misingi ya uwajibikaji na kujitegemea ilikuhakikisha Chama hicho kirudisha misingi yake ya zamani.

  Hata hivyo Kapambala aliwaomba wanachama wote kuendelea kudumisha Umoja na mshikamano katika kuhakikisha Shughuli za chama hicho zinasonga mbele na Kwa kipindi cha uchaguzi wa mwaka 2017 wahakikishe Wanachagua viongozi Waadilifu,wasio penda rushwa na wanaotumiwa katika kukidhohofisha chama kutokana na maslahi ya baadhi ya Watu wasio penda Maendeleo ya Chama hicho.

  Nao baadhi ya Wanachama walio hamia CCM, akiwemo Mwenyekiti wa ACT wazalendo Nikolaus Weslaus alisema ameamua kukihama chama hicho kutokana na Mapungufu yaliyomo katika Chama hicho, alisema kunamambo aliyo yagundu katika chama hicho ni kitu kimoja kinaanzia kwa viongozi wa Juu wavyama vya upinzani unaoleta msukumo Mkubwa kwa wanasiasa wake na wananchi ili Nchi hii isiweze kutawaliwa ikiwemo zoezi la kuwashawishi madiwani na Wabunge kupinga kila kitu kinachoendelea katika Serikali hata kama ni cha maendeleo bila sababu ya Msingi.

  Alisema Ameamua kuhamia CCM kutokana na Rais aliyepo madarakani anasisitiza suala la uwajibikaji na vita dhidi ya rushwa ambavyo vimekuwa vikwazo vikubwa vya kuzuia maendeleo ya Nchi hii na Zoezi hilo linaendelea Kukamilika bila shida yoyote na serikali inaendelea kuwahudumia wananchi wote kwa usawa bila kuangalia chama.

  Amana Ramadhani ni Mwenyekiti wa Chama cha wananchi CUF Wilaya ya Kakonko alisema ameingia kwenye chama hicho tangu mwaka 1997 kutokana na chama hicho kuwa na sera nzuri na kwakuwa na malengo mazuri ya kuisaidia Serikali katika kupata Suqla zima la Demokrasia pamoja na maendeleo, lakini mpaka sasa kitu alicho kitalajia katika Chama hicho hajakiona.

  Na kilicho mfanya kuhamia CCM ni baada ya kuona Serikali ya Awamu ya Tano inavyo tekeleza Ilani yake kama ilivyo ahidi kipindi cha Kampeni na Sasa wanaendelea kuitekeleza kauri ya hapa Kazi tuu ambayo faida yake wanaiona mpaka sasa , ambapo kila idara ya Serikali inafanya kazi yake ipasavyo tofauti na Vyama vya upinzani hakuna kazi nyingine wanayo ifanya zaidi ya malumbano.

  Katika Sherehe za kuadhimisha miaka 40 Wilaya ya Kakonko ilifanya shughuli za Kufanya usafi Wa Zahanati ya Wilaya hiyo, kufungua ujenzi wa Ofisi ya Chama cha Wilaya pamoja na kikao cha Wanachama kilicho husisha upokeaji wa Kadi kutoka kwa Wananchama wapya wa CCM .
  mjumbe wa halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kigoma Prof Joyce Ndalichako na baadhi ya wanachama wa chama hicho wakishirika kufanya usafi katika kuadhimisha miaka 40 ya CCM .
  Wajumbe na wanachama mbalimbali wa chama CCM katika kuadhimisha miaka 40 ya kuzaliwa kwake,walishiriki kwenye kazi mbalimbali za kijamii ikiwemo ujenzi na kufanya usafi
  Baadhi ya ya wanachama wapya 102 kutoka chama cha Act Wazalendo na Chama cha Wananchi Cuf wakila kiapo.

  0 0

  Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania kwa kushirikiana na Wakifu  wa Taasisi Huru za Uwazi Afrika (OSIEA) wamefanya semina ya siku moja na waandishi wa habari  mkoani Dodoma katika  ukumbi wa Hazina  Ndogo, iliyolenga kuboresha utendaji katika kazi zao.

  Mjadala huu umelenga kuwajengea wanahabari uwezowa utendaji wao wa kazi.Waandishi wa habari hao wamejengewa uwezo kuhusu sheria ya huduma zavyombo vya habari ili kuleta ufanisi katika majukumu yao. Mkutano huu umefanyika katika ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma.
   Mhariri mtendaji wa Jamhuri Media, Deodatus Balile akitoa mada kwa wanahabari waliofika kwenye semina iliyokuwa ikihusu utendaji kazi wao wa kila siku.

  Wakili wa Mahakama Kuu na Mhariri wa Zamani, James Marenga akitoa mada inayohusisha sheria mbalimbali zinazohusiana na waandishi wa habari na namna ya kufanya kazi bila kuvunja sheria zilizowekwa.

    Afisa Habari na Utafiti wa MISA-Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa akizungumza jambo kwenye semina ya Wanahabari uliofanyika katika ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma leo.
   Mhariri Mtendaji wa The Guardian Ltd, Jesse Kwayu akizungumza jambo kwenye semina iliyowakutanisha wanahabari mbalimbali waliokutanishwa na Misa Tanzania ili kujadili changamoto zinazowapata katika kazi zaohasa za bungeni. 
  Baadhi ya waandishi wa habari wakichangia mada pamoja na kuuliza maswali kwa watoa mada waliowasilisha mada mbalimbali katika ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma.

  Baadhi ya waandishi wa habari waliofika katika semina iliyoandaliwa na Misa Tanzania kujadili namna ya kufanyakazi kifanisi katika majukumu yao ya kila siku
  Picha ya pamoja

  0 0
  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

  KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt.Tito E. Mwinuka, (pichani kushoto), amefanya ziara ya kutembelea vituo vitatu vya kupoza na kusambaza umeme wa msongo wa Kilovoti 132, (132Kv), vya Mbagala, Kurasini Wilayani Temeke na Kariakoo Wilayani Ilala jijini Dar es Salaam leo Februari 4, 2016 na kuwaomba wateja wa Shirika hilo kuwa wavumilivu wakati juhudi za kukamilisha mradi wa uboreshaji umeme ukiwa unakaribia kukamilika.

  Dkt. Mwinuka alisema, ongezeko la watu na shughuli za kiuchumi katika maeneo ya Mbagala, Kigamboni na Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani, kumepelekea upatikanaji wa umeme kwenye maeneo hayo kuwa na matatizo kidogo kwani vituo vinavyosambaza umeme kwenye maeneo hayo vilikuwa na ukubwa wa kupoza umeme wa Kilovoti 33 tu, na ndio maana TANESCO kupitia Mradi wa uboreshaji umeme jijini Dar es Salaam unakaribia kukamilisha ujenzi wa vituo vilivyotajwa hapo juu ili view na uwezo mkubwa wa Kilovoti 132 na hivyo kuondoa kabisa tatizo hilo.

  “Barabra zinapozidiwa na magari ni rahisi sana kubaini kutokana na ongezeko la magari yanayotumia barabara hizo, lakini ongezeko la watumiaji umeme na shughuli za kiuchumi inakuwa vigumu kubaini kwa haraka, kwa hivyo niwaombe wateja wetu kuwa wavumilivu kwani tatizo hilo litakuwa limepatiwa ufumbuzi katika kipindi kifupi kijacho.” Alisema Dkt. Mwinuka.


  Dkt. Mwinuka pia aibainisha, kuwa kazi ya kuongeza ukubwa wa vituo vya kupoza na kusambaza umeme inaendelea kwenye mikoa ya Mtwara na Lindi ambako nako vituo vya sasa vya ukubwa wa Kilovoti 33, vinabadilishwa na kuwa na uwezo wa Kilovolti 132.

  Dkt. Mwinuka amewapongeza wakandarasi kwa juhudi kubwa wanazofanya katika kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa haraka ili kuwaondolea adha wateja wa Shirika hilo wa upatikanaji wa umeme ulio bora na wa uhakika.

  Dkt. Mwinuka (kulia), akipatiwa maelezo ya litaalamu na Mkuu wa miradi (anayeshughulikia usafirishaji) wa TANESCO, Mhandisi Frank Mashalo, alipotembelea kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mbagala, Wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, Februari 4, 2017. Wakwanza kushoto ni Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji.
  Mitambo ya kupoza na kusafirisha umeme kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kurasini jijini Dar es Salaam, kikiwa katika hatua za mwisho ukamilika
  Dkt. Mwinuka, (wapili kulia), akimsikiliza mkandarasi kutoka kampuni ya FICHTNER, ambaye ndiyo Menenja mradi, Mathias Alby, wakati alipotembelea kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mbagala, Wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.
  Meneja wa TANESCO Mkoa wa Temeke, Mhandisi Jahulula Maendeleo, (kushoto), akitoa maelezo ya kiutendaji kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Dkt. Tito E.Mwinuka, wakati wa ziara yake ya kutembelea vituo vya kupoza na kusambaza umeme vya Mbagala na Kurasini vilivyoko Wilayani Temeka. Katikati ni Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi Mhandisi Mahende Mgaya.
  Dkt. Mwinuka (mbele), baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Kurasini jijini Dar es Salaam.

  Dkt. Mwinuka, (wapili kulia) akimsikiliza Meneja Mwandamizi wa TANESCO anayeshughulikia miradi ya usafirishaji na usambazaji umeme, Mhandisi Gregory Chegere, (kushoto), wakati alipotembelea kituo cha Kurasini. Kulia ni Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi Mhandisi Mahende Mgaya.
  Muhandisi mwandamizi wa miradi wa TANESCO, Mhandisi Rosmystice Luteganya, (kushoto), akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito E. Mwinuka, kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kariakoo jijini Dar es Salaam.


  Dkt. Mwinuka, (kulia), akikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kariakoo jijini Dar es Salaam.
  Fundi akiwa kazini kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kariakoo


  Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi Mhandisi Mahende Mgaya, (aliyesimama), akizungumza wakati wa majumuisho ya ziara hiyo, kwenye chuo cha TANESCO jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Dkt. Mwinuka, Mhandisi Chegere na Mhandisi Mashalo.


  Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji (aliyesimama), akizungumza wakati wa kikao hicho.
  Jengo la kituo cha bkupoza na kusambaza umeme wa msongo wa Kilovolti 132 cha Mbagala jijini Dar es Salaam, likiwa limekamilika
  Meneja wa TANESCO Wilayani Temeke, Mhandisi, Jahulula Maendeleo, (kulia), akizungumza na maafisa wa TANESCO wakati wakimsibiri Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Dkt. Rito E. Mwinuka kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mbagala jijini Dar es Salaam.

  0 0

      Diwani wa Viti Maalum Chadema, Debora Sanga (kulia) akipokea zawadi ya vitabu kutoka kwa Naibu Mkurugenzi wa na Mwanasheria  WLAC, Wigayi Kisandu, wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya ‘TUNAWEZA’  kwa Wilaya ya Ilala, iliyofanyika leo Feb 4, 2017 kwenye Uwanja wa Tabata Shule. Picha na Muhidin Sufiani  Mafoto Blog
  Diwani wa Viti Maalum Chadema, Debora Sanga (kushoto) akimkabidhi  zawadi ya vitabu Consoler Eliya kutoka New Hope for Girls Orphan,  wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya ‘TUNAWEZA’  kwa Wilaya ya Ilala, iliyofanyika leo Feb 4, 2017 kwenye Uwanja wa Tabata Shule.
  Diwani wa Viti Maalum Chadema, Debora Sanga (kushoto) akiwakabidhi  zawadi ya vitabu Wanafunzi wa Shule ya Sekondari  Zawadi,  wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya ‘TUNAWEZA’  kwa Wilaya ya Ilala, iliyofanyika leo Feb 4, 2017 kwenye Uwanja wa Tabata Shule.
   Mgeni rasmi Diwani wa Viti Maalum Chadema, Debora Sanga, akizungumza wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya ‘TUNAWEZA’  kwa Wilaya ya Ilala, iliyofanyika leo Feb 4, 2017 kwenye Uwanja wa Tabata Shule. 
  Wasanii wa Kikundi cha Msimamo Sanaa Group,wakiigiza mbele ya mgeni rasmi na wananchi wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya ‘TUNAWEZA’  kwa Wilaya ya Ilala, iliyofanyika leo Feb 4, 2017 kwenye Uwanja wa Tabata Shule. 
   Wasanii wa Kikundi cha Msimamo Sanaa Group,wakiigiza mbele ya mgeni rasmi na wananchi wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya ‘TUNAWEZA’  kwa Wilaya ya Ilala, iliyofanyika leo Feb 4, 2017 kwenye Uwanja wa Tabata Shule. 
  Consoler Eliya kutoka New Hope for Girls Orphan, akizungumza wakati akitoa ushuhuda wa Vitendo vya Unyanyasaji kwa Wanawake alivyowahi kuvipitia. Consoler alikuwa kitoa ushuhuda huo wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya ‘TUNAWEZA’  kwa Wilaya ya Ilala, iliyofanyika leo Feb 4, 2017 kwenye Uwanja wa Tabata Shule.
    Baadhi ya wananchi waliojitokeza wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya ‘TUNAWEZA’  kwa Wilaya ya Ilala, iliyofanyika leo Feb 4, 2017 kwenye Uwanja wa Tabata Shule.

  Baadhi ya viongozi waliohudhuria uzinduzi huo wakiwa meza kuu.
   Baadhi ya Wanafunzi wa Shule mbalimbali za Sekondari  waliojitokeza wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya ‘TUNAWEZA’  kwa Wilaya ya Ilala, iliyofanyika leo Feb 4, 2017 kwenye Uwanja wa Tabata Shule.
  Baadhi ya Wanafunzi wa Shule mbalimbali za Sekondari  waliojitokeza wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya ‘TUNAWEZA’  kwa Wilaya ya Ilala, iliyofanyika leo Feb 4, 2017 kwenye Uwanja wa Tabata Shule.
    Baadhi ya wananchi waliojitokeza wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya ‘TUNAWEZA’  kwa Wilaya ya Ilala, iliyofanyika leo Feb 4, 2017 kwenye Uwanja wa Tabata Shule.
    Baadhi ya wananchi waliojitokeza wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya ‘TUNAWEZA’  kwa Wilaya ya Ilala, iliyofanyika leo Feb 4, 2017 kwenye Uwanja wa Tabata Shule.
   Baadhi ya wananchi waliojitokeza wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya ‘TUNAWEZA’  kwa Wilaya ya Ilala, iliyofanyika leo Feb 4, 2017 kwenye Uwanja wa Tabata Shule.
  Wasanii wa Kikundi cha Msimamo Sanaa Group,washambulia jukwaa wakati wa sherehe za uzinduzi wa Kampeni ya ‘TUNAWEZA’  kwa Wilaya ya Ilala, iliyofanyika leo Feb 4, 2017 kwenye Uwanja wa Tabata Shule. 

older | 1 | .... | 1127 | 1128 | (Page 1129) | 1130 | 1131 | .... | 1896 | newer