Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46329 articles
Browse latest View live

Hakuta Kuja Kutokea Upungufu wa Sukari Nchini – Waziri Mkuu

$
0
0
Na: Lilian Lundo – MAELEZO - Dodoma

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema kwamba Tanzania haitapata upungufu wa sukari kutokana na kuanza kwa uzalishaji wa sukari kwa viwanda vya ndani.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo Bungeni, Mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge  Suleiman Ahmed Sadick  alipotaka ufafanunuzi namna ambavyo Serikali ya Awamu ya Tano imejipanga ikiwa tatizo la upungufu wa sukari litajirudia tena.

“Tayari Viwanda vya ndani vimeanza uzalishaji wa sukari ambapo kufikia mwisho wa mwezi Machi mwaka huu ambao ndio mwisho wa msimu tutakuwa tumefikia lengo la uzalishaji wa sukari kwa nchi nzima,” alifafanua Majaliwa.

Aidha, Waziri Mkuu amewataka wafanyabiashara kutoweka vyakula ndani ili kuviuza kwa bei ya juu baadae, badala yake amewataka kuuza vyakula hivyo ili kuongeza upatikanaji wa chakula nchini, kwani uongezaji wa bei wa vyakula unaumiza wananchi wa kipato cha chini na kati.

Katika kukabiliana na tatizo la ukame kwa baadhi ya maeneo hapa nchini, Waziri Mkuu amewataka wakulima kutumia kipindi hiki ambacho baadhi ya maeneo yanapata mvua kwa kupanda mazao ya muda mfupi ambayo pia mazao hayo yataweza kutumika kwa msimu ujayo.


KAMATI YA UTENDAJI, BARAZA LA WADHAMINI SIMBA LAMALIZA TOFAUTI ZAO

$
0
0
Mwenyekiti wa Baraza La Wadhamini wa Simba Mzee Hamis Kilomoni (katikati) akiwa ameshikana mikono na viongozi wa kamati ya utendaji wa Simba, Rais wa Klabu ya Simba Evance Aveva, Mkuu wa kitengo wa habari na mawasiliano Haji Manara, Mjumbe wa kamati ya utendaji na mwenyekiti wa kamati ya usajili Zacharia Hanspope.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Baraza la Wadhamini wa Klabu ya Simba limekubali yaishe baada ya kukutana leo na na Kamati ya utendaji ya Klabu hiyo na kuwataka wapeleke mpango kazi wa mabadiliko ili kufikia maamuzi yatakayokuwa na manufaa ndani ya klabu hiyo kongwe hapa nchini.

Mwenyekiti wa Baraza hilo, Mzee Hamis Kilomoni alisema wanatambua kila binadamu anafanya makosa na kama mtu akifanya kosa hakuna budi kumsamehe na kushirikiana kufanya mambo mbalimbali ambayo yataleta maendeleo.

Alisema Kamati hiyo ilifanya vikao vyake na kugundua Uongozi wa Simba kwa ujumla ulikosea kufanya maamuzi yake na kuamua kuwasamehe kwa yote waliyoyakosea ili kukamilisha mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu hiyo kutoka kumilikiwa na wanachama na kuelekea kwa mwekezaji mmoja. Ikumbukwe kuwa baraza hilo liligomea hatua za mabadiliko ya uendeshaji wa klabu hiyo yaliyotangazwa kufanywa na kamati tendaji tangu mwaka jana kwa madai ya kutotimiza matakwa mbalimbali ya kisheria ikiwemo kupuuzia baraza hilo linalotambulika kisheria.

"Niwajulishe mashabiki wa Simba kwa ujumla kwamba sisi hatuna ugomvi na Kamati tendaji ya Simba lakini kilichokuwa kikifanyika ni kuwashtua watekeleze matakwa yale tuliyokuwa tukiwaeleza kwa muda mrefu na wao walikuwa hawajayatekeleza kikubwa zaidi hakuna mtu anayekataa mabadiliko na sisi kama bodi ya wadhamini ya Simba SC ambao tunapenda kuona mafanikio ya klabu tumewaagiza hawa viongozi watuletee mpango kazi ili tujue ni namna gani mabadiliko hayo yatakavyokuwa na msaada kwa klabu kiujumla," alisema Kilomoni.

Kilomoni aliendelea kusisitiza kuwa licha ya kuwataka viongozi wa klabu hiyo kupeleka mpango kazi ili wafanye mabadiliko, Viongozi hao wanapaswa kutambua mali zilizopo katika klabu hiyo ni za Simba hazitokwenda kwa yeyote badala yake zitaendelea kubaki chini ya baraza la wadhamini kama ilivyokuwa kipindi chote na mali za klabu hiyo sio za mchezo wa mpira wa miguu pekee bali zinauhusiano na michezo mingine licha ya kuwa kwa sasa haipo katika klabu hiyo.

Wakati huo huo, Rais wa Klabu hiyo, Evans Aveva alisema kumekuwa na taarifa za kutokuwepo kwa maelewano chanya kati ya Uongozi wa klabu hiyo na baraza la wadhamini jambo ambalo limemsukuma na kujitokeza kulizungumzia ili kuwajuza watanzania kwamba hakuna tatizo lolote.

Alisema kilichokuwa kikitokea katika klabu hiyo ni changamoto za kufanya kazi kwa pamoja na sehemu zote zinazowakutanisha watu mbalimbali kutokea kwa baadhi ya watu kukubali jambo fulani na wengine kutokubali ni lakawaida na halishangazi sana kwa kuwa Simba sio ya kwanza kupitia hilo.

Alisema uongozi wa Simba umekuwa ukifanya kazi kwa ushirikiano na mamlaka zote zilizopo katika klabu hiyo ili kuhakikisha inapata mafanikio yale waliyoyapata kwa wakati waliojipangia na kuahidi kufanyia kazi kwa wakati maelezo yaliyotolewa na baraza la wadhamini.
Rais wa Klabu ya Simba Evance Aveva akizungumza na waandishi wa habari juu ya mustakabali wa uhalali wa Simba na bodi ya wadhamini na kukubaliana kuweka wazi michakato yote ya mabadiliko ya klabu hiyo, kulia ni Mwenyekiti wa Baraza La Wadhamini wa Simba Mzee Hamis Kilomoni.
Mwenyekiti wa Baraza La Wadhamini wa Simba Mzee Hamis Kilomoni akizungumza na waandishi wa habari juu ya mustakabali wa uhalali wa Simba na bodi ya wadhamini na kukubaliana kuweka wazi michakato yote ya mabadiliko ya klabu hiyo.

MAKONDA ATAJA LIST YA WAUZA MADAWA YA KULEVYA,WEMA SEPETU,TID,MR BLUE WATAKIWA KUJISALIMISHA POLISI

$
0
0

MKUU wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewataja baadhi ya Maafisa wa Jeshi la polisi wanao shirikiana na Wasanii wanaojihusisha na uuzwaji wa Madawa ya kulevya.

 Akizungumza na waandishi wa Habari mapema leo hii jijini hapa amesema Serikali ya awamu ya Tano haito vumilia vitendo vya uuzwaji wa dawa za kulevya na kutoa agizo kwa jeshi la polisi kuwakamata Maafisa wote wa jeshi la polisi waliotajwa kushirikiana na wauza madawa ya kulevya mpaka pale uchunguzi utakapo kamilika.


RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA MWAKA MPYA WA KIMAHAKAMA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamisi Juma wakati wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017.

Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamisi Juma akihutubia wakati wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017 wakati wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akihutubia wakati wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipokea ripoti ya mahakama kuhusu kesi za uchaguzi kutoka kwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamisi Juma wakati wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017. Kulia ni Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiagana na majaji wa Mahakama ya Rufaa na wa Mahakama kuu baada ya sherehe za uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiaga baada ya sherehe za uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipeana mikono na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu baada ya sherehe za uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017. PICHA NA IKULU




























Taarifa ya Mauaji ya Kondakta Tanga

$
0
0
 

JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO

Simu ya Upepo  : “N G O M E”        Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo: DSM 22150463     Sanduku la Posta 9203,
Telex                   : 41051                       DAR ES SALAAM, 31 Januari, 2017.
Tele Fax              : 2153426
Barua pepe       : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti                  : www.tpdf.mil.tz


Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limesikitishwa na taarifa iliyotolewa na gazeti la Tanzania Daima toleo Nambari 4438 la tarehe 28 Januari 2017, Habari leo   la tarehe 29 Januari 2017 na baadhi ya vyombo vya habari vikihusisha mauaji ya kondakta wa daladala na Wanajeshi Mkoani Tanga.

Tunapenda  kuwataarifu wananchi kwamba kwa mujibu wa jeshi la polisi watuhumiwa wanaoshikiliwa na Jeshi hilo ni wanne (4),mmoja kati yao ni Mwanajeshi ambaye ni mzazi wa msichana anayetuhumiwa kusababisha tukio hilo. 

Hivyo Mwanajeshi huyo anashikiliwa kwa ajili ya kulisaidia Jeshi la Polisi katika uchunguzi kwa kuwa tukio hilo lilifanyika nyumbani kwake. Hakuna Wanajeshi waliohusika katika tukio hilo kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari, kambi za Jeshi wanaishi Wanajeshi pamoja na familia zao hivyo kuhusisha moja kwa moja mauaji hayo na Wanajeshi  mkoani Tanga ni kuupotosha umma.

Wito unatolewa kwa vyombo vya habari kuripoti habari zenye ukweli.Habari zisizo za kweli zinapotosha umma na kujenga taswira potofu kwa wananchi dhidi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.  

Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0756-716085

BARAZA LA TATU LA WAFANYAKAZI MOI LAFUNGULIWA

$
0
0
Makamu mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MOI Prof Bakari Lembariti akihutubia wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa MOI wakati wa Uzinduzi wa Kikao cha Tatu cha Baraza Hilo.
Kaimu Mkurugenzi wa MOI Dkt Othman Kiloloma akiwasilisha ripoti ya Utendaji ya Mwaka 2015/2016.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa MOI wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi Prof Bakari Lembariti
Makamu mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi MOI Prof Bakari Lembariti akimkabidhi cheti Mfanyakazi bora wa MOI kwa Mwaka 2015/2016 Bwana Robert Sere

…………………………………………………………………

Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MOI Profesa Bakari Lembariti leo amezindua vikao vya Baraza la Tatu la Wafanyakazi wa MOI katika ukumbi wa IDDI NYUNDO katika halmashauri ya Temeke jijini Dar es Salaam. Vikao vimehudhuriwa na zaidi ya wajumbe 50 kutoka katika kila idara, vitengo na chama cha wafanyakazi wa MOI (TUGHE) na wajumbe wa TUGHE mkoa.

Akizindua Baraza hilo Profesa Lembariti alisema anampongeza Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli. Alisema ” Kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini MOI Mh Zakia Meghji natumia Fursa hii kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa uongozi wake uliotukuka na jitihada zake za kuboresha huduma za afya hapa nchini, sote ni mashahidi“.

Aidha, Profesa Lembariti aliwakumbusha wafanyakazi wa MOI kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia maadili ya utumishi wa Umma ili kujenga imani kwa watanzania walio wengi ambao wanaitegemea MOI kama Taasisi pekee inayotoa Tiba ya kiwango cha juu cha rufaa kwenye Tiba ya Mifupa, upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu.

Pia Profesa Lembariti alisema ni vyema wajumbe wa Baraza la MOI wakatumia vikao vya Baraza kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili Taasisi ya MOI na kutafuta muarobaini ili Taasisi ya MOI iendelee kutoa huduma bora

Kwa upande mwingine Profesa Lembariti aliwakabidhi zawadi wafanyakazi Bora wa MOI kwa mwaka 2015/2016 ambapo Bwana Robert Sere aliibuka kidedea na kuwa mfanyakazi Bora wa MOI na kujipatia cheti na fedha taslimu kiasi cha Tshs Milioni 4, nafasi ya pili ikishikwa na Bwana Lucas Machage akijipatia cheti na kiasi cha Tshs Milioni 2 na nafasi ya tatu ikishikwa na Bi Betty Shila ambaye alijipatia cheti na kiasi cha Tshs Milioni 1.5

Kwa upande wake ,akiwasilisha ripoti ya utendaji wa Taasisi ya Kaimu Mkurugenzi wa MOI Dkt Othman Kiloloma alisema kutokana na ongezeko kubwa la ajali ambazo zimepelekea ongezeko kubwa la wagonjwa MOI, Taasisi ya MOI iko kwenye mpango mkakati kabambe wa kushirikiana na baadhi ya hospitali za rufaa za pembezoni kwa kuwapeleka wataalamu kutoa huduma katika hospitali hizo na kupunguza kama si kuondoa kabisa wimbi la wagonjwa wanaopokelewa MOI

Dkt Kiloloma alisema kwamba Taasisi ya MOI imeendelea kuwa Kitovu cha Weledi katika matibabu ya Mifupa ,Ajali ,Ubongo na Mishipa ya Fahamu katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati ambapo mwaka 2015 MOI ilitoa utafiti bora wa mfupa mrefu wa paja duniani ,ambapo utafiti uliwasilishwa katika Taasisi ya kimataifa ya upasuaji wa mifupa duniani ya Marekani (AOTA)

Vilevile, Dkt Kiloloma aliwaomba wajumbe wa Baraza la MOI kutoa michango yenye tija ili kupata matibabu ya changamoto mbalimbali zinazoikabili Taasisi ili Taasisi iendelee kutoa huduma bora kwa watanzania

SERIKALI ITAOKOA SH.BILIONI 900 KWA MWAKA ENDAPO IKIFANIKIWA KUTEKELEZA MKAKATI WA UWAZI KATIKA UJENZI NCHINI.

$
0
0
Kaimu Mtendaji Mkuu Baraza la Taifa la Ujenzi,Elias Kissamo akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa mchakato wa utoaji wa taarifa za miradi ya ujenzi wa miundombinu ya umma katika ukumbi wa Holiday Inn jijini Dar es Salaam jana. (PICHA NA ELISA SHUNDA)
Katibu Mkuu kutoka Ofisi ya Rais Ikulu,Peter Ilomo,akifungua mkutano wa mchakato wa utoaji wa taarifa za miradi ya ujenzi wa miundombinu ya umma katika ukumbi wa Holiday Inn jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mwenyekiti wa Sekta ya Uwazi na Uwajibikaji katika Ujenzi (Cost Tanzania),Mhandisi Kazungu Magili na Kaimu Mtendaji Mkuu Baraza la Taifa la Ujenzi,Elias Kissamo.
Wadau wa masuala ya ujenzi wakifuatilia kwa umakini wakati mkutano huo ukiendelea.


Mwenyekiti wa Baraza la Ujenzi la Taifa (Cost Tanzania),Mhandisi Kazungu Magili,akizungumza katika mkutano huo.
Katibu Mkuu kutoka Ofisi ya Rais Ikulu,Peter Ilomo akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Baraza la Taifa la Ujenzi Tanzania na wadau wa masuala ya ujenzi nchini.(www.elisashunda.blogspot.com)


SERIKALI itaokoa angalau Sh.bilioni 900 kwa mwaka endapo itafanikiwa katika utekelezaji wa Mkakati Uwazi katika Ujenzi (CoST).

Aidha kupitia mkakati huo, miradi mbalimbali ya mashirika ya umma 10 inatarajiwa kufanyiwa tathmini itakayokamilika ifikapo Julai mwaka huu.

Akizungumza katika mkutano wa mashauriano ya utoaji wa taarifa za miradi ya ujenzi wa miundombinu ya umma wa baraza la wajenzi, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ikulu, Peter Ilomo alisema kuwa mkakati huo utapunguza rushwa na upotevu wa fedha za Serikali.

Ilomo alisema CoST itaisaidia Serikali na umma kujua fedha zinavyotumika katika ujenzi wa miundombinu, kuokoa fedha za umma kwa kupunguza rushwa na kuboresha usimamiaji wa utekelezaji wa miundombinu.

Mwenyekiti wa CoST, Kazungu Magili alitaja mashirika yatakayofanyiwa tathmini na kuweka wazi miradi yake kuwa ni, Wakala wa Majengo (TBA), Wakala wa Barabara (Tanroads) na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)/.

Mashirika mengine ni mifuko wa Taifa wa hifadhi ya jamii ya NSSF, GEPF, LAPF, Wizara ya Elimu na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii jinsia Wazee na Watoto na kutoa taarifa kwa umma ambapo utaweza kuitumia kufuatilia utekelezaji wa miradi husika.

Alisema kupitia tathmini hiyo, CoST itapata fursa ya kutambua majengo yaliyojengwa kwa mujibu wa vigezo ama chini ya kiwango halisi cha fedha zilizotolewa na thamani ya jengo husika.

Magili alisema ikitokea kuna baadhi ya miradi imejengwa chini ya kiwango itafikishwa katika mamlaka mbalimbali ikiwemo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA) na Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) ili hatua mbalimbali zichukuliwe.

Aidha alisema kuwa awali kabla ya kuanzishwa mkakati huo mambo mengi yalikuwa hayawekwi wazi hali ambayo imekuwa ikisababisha upotevu wa fedha.

WIZARA YA AFYA KWA KUSHIRIKIANA NA MRADI WA GLOBAL HEALTH SUPPLY CHAIN YAANDAA WARSHA YA SIKU MOJA YA KUBORESHA MIUNDO MBINU YA USAMBAZAJI DAWA NA VIFAA TIBA.

$
0
0

Mfamasia Mkuu wa Serikali Habib Ali Shariff akifungua warsha ya siku moja ya kuandaa mikakati ya kuboresha miundo mbinu ya usambazaji dawa, vifaa tiba na huduma za afya iliyofanyika Bohari kuu ya dawa Maruhubi Mjini Zanzibar. Baadhi ya washiriki wa warsha ya kuandaa mikakati ya kuboresha huduma za usambazaji dawa wakifuatilia mwendo wa mafunzo hayo. Mkurugenzi wa mafunzo wa Mradi wa Global Health Supply Chain (GHS) Matiko Mhoni Machagge akiwaeleza washiriki wa warsha hiyo malengo ya mradi katika kufanikisha huduma za afya.
Washiriki wa warsha wakiwa katika mazoezi ya vikundi ili kuweza kutoa mapendekezo na maoni yao yatakayosaidia kufanikisha mpango huo.
Picha ya pamoja ya washiriki wa mafunzo ya siku moja ya kuandaa mikakati ya pamoja ya kuboresha miundo mbinu ya usambazaji dawa na vifaa tiba katika wilaya na vituo vya afya Zanzibar.

Picha na Makame Mshenga Maelezo.

Rais Magufuli ateua Mkuu wa Majeshi na Mnadhimu Mkuu

$
0
0





Luteni Jenerali Venance Mabeyo ambaye ameteuliwa na Rais Dkt Magufuli kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania




VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 3,2017

Wafanyabiashara wa Tanzania tupo tayari kwa ubia- Dkt Mengi

$
0
0
 Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Dkt. Reginald Mengi (katikati) akifurahi jambo na Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda Nchini (CTI) Dr. Samwel Nyantahe (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bw. Godfrey Simbeye (kushoto) mara baada ya kuwasili kwenye hafla ya chakula cha mchana na kuwapongeza mabalozi wapya wa Tanzania nje ya nchi iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bw. Godfrey Simbeye akiwasilisha 'presentation' iliyoainisha maeneo muhimu ya fursa za kibiashara kwenye masoko ya kimataifa kwa mabalozi wapya wa Tanzania nje ya nchi walioapishwa hivi karibuni wakati wa hafla ya chakula cha mchana kwa mabalozi hao iliyoandaliwa na TPSF jijini Dar es Salaam
  Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Dkt. Reginald Mengi akizungumza na mabalozi wapa wa Tanzania nje ya nchi kwenye hafla ya chakula cha mchana na kuwapongeza mabalozi hao watakaoiwakilisha Tanzania katika nchi za Uturuki, Italy, China, UN Geneva na Brazil iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Dkt. Reginald Mengi akisisitiza jambo kwa mabalozi wapya watakaoiwakilisha Tanzania kwenye nchi za Uturuki, Italy, China, Brazil na UN Geneva (hawapo pichani) katika hafla ya chakula cha mchana na kuwapongeza mabalozi hao iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda nchini–CTI Dr. Samwel Nyantahe akisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika uwekezaji, kutafuta masoko mapya, kubadilishana bidhaa na utafutaji fursa za biashara kwenye masoko ya kimataifa kwa wafanyabiashara katika hafla ya chakula cha mchana na kuwapongeza mabalozi wapya watakaoiwakilisha Tanzania kwenye nchi za Uturuki, Italy, China, Brazil na UN Geneva iliyoandaliwa na TPSF katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam
 Mwenyekiti wa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs (TASWE - SACCOSS), Anna Matinde akizungumzia umuhimu wa kumshirikisha mwanamke katika ukuzaji wa biashara kubwa na ndogo ndogo, ambapo amesema wanawake ni nguzo muhimu katika ukuaji wa sekta binafsi nchini kutokana na uchapaji kazi wao katika sekta mbalimbali.
 Balozi mpya wa Tanzania nchini Uturuki, Prof Elizabeth Kiondo  akitoa shukrani kwa TPSF kwa kuandaa hafla fupi kama hiyo ya kubadilishana mawazo kwa jinsi gani wanaweza kukuza diplomasia ya kiuchumi katika vituo vyao vya kazi walipopangiwa.
 Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki, akizungumza kwenye hafla hiyo  ambapo amesisitiza wafanyabiashara kutoka Tanzania watumie fursa adimu ambayo ipo kati ya Tanzania na China ambapo mahusiano na ushirikiano ulianza tangu enzi za Mao na Mwalimu Nyerere.
 Balozi wa Tanzania, Geneva, Dkt. James Msekela akisisitiza jambo kwa bodi ya TPSF kwenye hafla ya chakula cha mchana kwa mabalozi hao wapya iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Wafanyabiashara wa Tanzania wamesema wapo tayari kwa kufanya ushirikiano wa kibiashara wa ubia na wafanyabiashara kutoka nje ili kukuza diplomasia ya kiuchumi na mataifa mengine.

Akizungumza katika hafla ya chakula cha mchana na mabalozi wa Tanzania nje ya nchi kilichoandaliwa na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) nchini, Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Dkt. Reginald Mengi amesema wafanyabiashara watanzania si omba omba na wapo tayari kwa kufanya biashara ya ubia na wenzao.

“Napenda kusisitiza kwamba sisi watanzania si omba omba kwa wafanyabishara wa nje, tuna nia uwezo, ujuzi na tunajiamini kwa kufanya biashara za kimataifa kwa ubia ili kukuza uchumi wa nchini zetu,” amesema Dkt. Mengi.

Amesema kwamba fursa za uwekezaji zipo nchini kwenye sekta za kilimo, mafuta, gesi, usindikaji na mawasiliano ila ni muhimu kuunganisha nguvu za wafanyabiashara ili kuweza kupata matokeo chanya.

Dkt. Mengi alilisisitiza kwamba sekta binafsi nchini ina imani kubwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli katika adhma yake ya kukuza sekta ya viwanda ili kutatua tatizo la ajira na kuongeza mapato ya nchini.

“Ni muhimu kuimarisha sekta binafsi ili iweze kutoa mchango mkubwa katika uanzishwaji wa viwanda hapa nchini, kwa vyovyote vile sekta hii binafsi ndio itakayojenga viwanda hapa Tanzania,” aliongeza

Kwa Upande wa Mabalozi, Dkt. Emmanuel Nchimbi ambaye anakwenda kuiwakilisha nchi huko Brazil, amesema kwamba mabalozi ni kiungo muhimu kati ya wananchi wa mataifa husika katika kukuza mahusiano na ushirikiano wa kimataifa.

“Sisi ni wawakilishi wenu huko kwenye mataifa ya nje na zaidi na kukuza mahusiano au diplomasia ya kiuchumi kwa maslahi ya wananchi wetu,” amesema Dkt. Nchimbi

Naye Balozi wa Tanzania, Geneva, Dkt. James Msekela amesema kwamba ni muhimu kuanzisha mawasiliano ya mara kwa mara kati ya wafanyabishara na mabalozi ili kusaidia upatikanaji wa taarifa za fursa mbalimbali za uwekezaji au masoko kutoka kwenye bidhaa za nyumbani.

“fursa zipo kwenye kila sekta ni muhimu wafanyabishara wa ndani wakajenga uaminifu na kujiamini ili kuweza kuingia katika ushindani wa kibiashara katika soko la kimataifa,” amesema Dkt. Msekela.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi, Geofrey Simbeye amesema wataanzisha mawasiliano ya kudumu na mabalozi wa Tanzania nje ya nchi ili kuweza kubadilishana mawazo na taarifa juu ya fursa za kibiashara katika nchi wanazokwenda kuwakilisha.

Alifafanua kwamba serikali imefungua milango kwa sekta binafsi kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kukuza uchumi wa Tanzania na kuondoa tatizo la umaskini.
Kikao hicho kati ya sekta binafsi na mabalozi wa Tanzania wanaokwenda kuwakilisha nchi katika mataifa matano ambapo mabalozi hao ni Dkt Emmanuel Nchimbi-Brazil, Dkt. James Msekela-Geneva, Profesa Elizabeth Kinyondo-Uturuki, Mbelwa Kairuki-China na Balozi George Madafa- Italy

FEMINA HIP YAWAJENGEA VIJANA NCHINI UWEZO WA UONGOZI NA KUJIAMINI.

$
0
0

Mkurugenzi na mwanzilishi wa FeminaHip Dr. Minou Fuglesanga kizungumza wakati wa Kongamano la mwaka la Vijana leo jijini Dar es Salaam.
Jopo la washiriki wa mjadala katika kongamano la vijana wa FeminaHip 2017 (Kushoto: Lyen Charles-Kiongozi wa Team ya Feminahip Nguvu ya binti, Mwakilishi wa One UN Tanzania –Alvaro Rodriguez, Mkurugenzi na mwanzilishi wa FeminaHip Dr. Minou Fuglesang, Naibu Kamishna wa elimu Tz (Nicholaus Burreta), Balozi wa Denmark Tanzania (Einar Jensen) na Mwakilishi kutoka ubalozi wa Sweden-Helena Reutersward . Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
Mshindi wa tuzo ya mlezi bora wa Fema Club Network – Christopher Mavunde akipokkea tuzo kutoka kwa Mkurugenzi na mwanzilishi wa FeminaHip Dr. Minou Fuglesang na Balozi wa Denmark Tanzania (Einar Jensen) leo jijini Dar es Salaam. 


Na: Frank Shija – MAELEZO

FEMINA Hip yatoa tuzo tano za mwaka kwa Klabu za Fema ambazo zimefanya vizuri katika Nyanja mbalimbali.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la Femina Hip Dkt. Minou Fuglesang wakati wa Kongamano la mwaka la Vijana leo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi huyo amesema kuwa tuzo hizo zinatolewa ili kutia chachu kwa vijana kuongeza bidi katika kutatua changamoto zao kwa kujiamnini huku wakiwa na ujuzi mwepesi utakaowaomgezea umakini katika shughuli zao.

“Tmezigawa tuzo hizi katika makundi makuu matano ambayo ni Mtandao Bora wa Klabu ya Fema ambayo imekwenda kwa Mwanza Federation Fema Clubs, Mshindi wa Pili wa Mtandao Bora wa Klabu za Fema iliyochukuliwa na Dodoma Students and Teachers”.Alisema Fuhlesang.

Tuzo zingine kuwa ni Mhamasishaji Bora wa Mtandao wa Klabu za Fema wa mwaka iliyokwenda kwa Mwalimu Christopher Mavunde, Mhamasishaji Bora wa Klabu za Fema wa mwaka iliyochukuliwa na Mwalimu Bryson Paul kutoka Ngweli FEMA Klabu – Shule ya Sekondari Ngweli wilayani Sengerema pamoja na Klabu bora ya FEMA kwa mwaka ambayo ni Kisihigh Fema Club kutoka Shule ya Sekondari Kisimiri mkoani Arusha.

Akizungumza katika mkutano huo Mkurugenzi huyo amesema kuwa FEMINA Hip imekuwa ikiendesha program za kuwakutanisha vijana ili kuwajengea uwezo katika Nyanja za mabalimabali ikiwemo uongozi kwa manufaa ya sasa na baadae. Ujuzi ambaa vijana wamekuwa wakipatiwa kutoka kwa wataalamu wa Shirika hilo ni pamoja na mawasiliano,

Kwa upande wake mshindi wa tuzo Mhamasishaji Bora wa Klabu za Fema wa mwaka 2017 Mwalimu Bryson Paul amesema kuwa Klabu za FEMA zimekuwa msingi imara wa kuwajengea uwezo wa kujitambua vijana wengi nchini hivyo ni vyema watanzania wakatambua umuhimu wa vijana wao kushiriki katika vikundi hivyo ambavyo vimekuwa na lengo la kuwajengea uwezo kwa kuwapa elimu na ujuzi mbalimbali ikiwemo stadi za maisha.

Aliongeza kuwa binafsi amefarijika kwa kuibuka kuwa mshindi katika kipengele hicho na kusisitiza kuwa siri pekee ni nidhamu na moyo wa kujifunza Zaidi kwa kushirikiana na wenzako.

FEMINA Hip imewakutanisha vijana walikatika Klabu za FEMA kutoka pande zote za nchi katika Kongamono lililofanyika katika hoteli ya Belinda Jijini Dar es Salaam, ambalo pamoja na utoaji wa tuzo pia vijana walipata fursa ya kujadiliana mambo mbalimbali kuhusu elimu na masuala mtambuka kwa vijana.  

SIKU YA SHERIA NI SIKU AMBAYO WANANCHI HUPATA MSAADA WA KISHERIA

$
0
0
Na Pamela Mollel,Arusha


Imeelezwa kuwa siku ya sheria ni siku ambayo wananchi wanapata fursa ya kupata msaada wa kisheria ambayo kila mwananchi anapaswa kuwa chini ya shieria na sio juu ya sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake wakili wa kujitegemea Mruma aShabibu kutoka kampuni IRM Legal alisema kuwa siku hii ni maalum kwa mawakili kutoa huduma za kisheria kwa jamii bila malipo yeyote.

Alisema kuwa kwa siku hii watu wengi ufaidika kwa kutatuliwa baadhi ya matatizo yao bila kutozwa gharama yeyote ikiwa ni pamoja na kupata elimu ya kisheria sanjari na kupata fursa ya kubadilishana mawazo na mawakili.

Alidai kuwa wananchi wanapaswa kuheshimu katiba lakini pia na kukaa chini ya sheria ili haki iweze kutendekea kwani baadhi ya wananchi wanakaa juu ya sheria hali ambayo inawafanya kujiona hawatendewi haki.

Hata hivyo alifafanua kuwa lengo la kuanzishwa kwa siku hii ni kuangalia umuhimu wa sheria katika jamii na kuona jinsi inavyofanya kazi katika kukuza uchumi wa nchi .

Wakili wa kujitegemea Mruma aShabibu kutoka kampuni IRM Legal alisema kuwa siku hii ni maalum kwa mawakili kutoa huduma za kisheria kwa jamii bila malipo yeyote.

WABUNGE WANAWAKE WAJUMUIKA KUFANYA MAZOEZI YA PAMOJA UWANJA WA JAMHURI MJINI DODOMA

$
0
0
Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiongea na Wabunge (hawapo pichani) pamoja na Waandishi wa Habari kuhusu umuhimu wa kufanya mazoezi kwa ajili ya kulinda afya leo katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.
Naibu Waziri, Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura (Mb) akiongea na Wabunge wenzake (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa kufanya mazoezi kwa ajili ya kulinda afya ya miili pamoja na matarajio ya Uzinduzi wa Mazoezi yanayotarajiwa kuzinduliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo yatatangazwa hivi karibuni.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mhe. Ritta Kabati akiongea na Wabunge wenzake pamoja na Waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa kufanya mazoezi kwa ajili ya kulinda afya ya miili wakati wa mazoezi ya pamoja kwa Wabunge hao wanawake yaliyofanyika leo 03/02/2017 Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.


Mbunge wa Jimbo la Ilemela Jijini Mwanza (CCM), Mhe. Angeline Mabula akiongea na Wabunge wenzake pamoja na Waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa kufanya mazoezi kwa ajili ya kulinda afya ya miili wakati wa mazoezi ya pamoja kwa Wabunge hao wanawake yaliyofanyika leo 03/02/2017 Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Baadhi ya Wabunge wanawake wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa wameongozana na Spika wa Bunge (wa pili kushoto) wakifanya mazoezi (Jogging) ikiwa ni sehemu ya kufanya mazoezi ya pamoja kwa ajili ya kuweka sawa miili, mazoezi hayo yamefanyika leo 03/02/2017 katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Baadhi ya Wabunge wanawake wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa wakifanya mazoezi ikiwa ni sehemu ya kufanya mazoezi ya pamoja kwa ajili ya kuweka sawa miili, mazoezi hayo yamefanyika leo 03/02/2017 katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (wa pili kushoto) akifanya mazoezi ya mwili ikiwa ni sehemu ya ya kuweka sawa mwili, mazoezi hayo yamefanyika leo 03/02/2017 katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

(Picha zote na Benedict Liwenga).

BENKI KUU YA TANZANIA (BOT) HAINA MAMLAKA YA KUZIPANGIA TAASISI ZA FEDHA VIWANGO VYA RIBA ZA MIKOPO-SERIKALI

$
0
0
Benny Mwaipaja-WFM, Dodoma
SERIKALI imesema kuwa Benki Kuu ya Tanzania haina mamlaka kisheria ya kuweka ukomo wa riba au riba elekezi itakayotumiwa na taasisi za fedha nchini zikiwemo benki katika kutoa mikopo.
Kauli hiyo imetolewa Bungeni mjini Dodoma, Februari 3, 2017 na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, wakati akijibu maswali ya msingi yaliyoulizwa na Mbunge wa Jimbo la Mbagala, Mhe. Issa Ali Mangungu, aliyetaka kujua kama serikali inaweza kuandaa utaratibu maalumu wa riba elekezi itakayowawezesha wanawake na vijana kupata mikopo kwenye benki kwa riba nafuu ili waweze kujikwamua kiuchumi
Aidha Mbunge huyo alitaka kufahamu kama Serikali inaweza kuziagiza benki za biashara kulegeza masharti ya dhamana kwa vijana na wanawake ambayo amedai yanarefusha mchakato wa upatikanaji wa mikopo kwa makundi hayo.
Dkt. Kijaji amesema kuwa viwango vya riba katika benki na taasisi nyingine za fedha hupangwa na taasisi husika kwa kutegemea mambo mengi ikiwemo nguvu ya soko, sifa za mkopaji, ushindani katika soko, gharama za upatikanaji wa fedha, mwenendo wa riba za dhamana za serikali, gharama za uendeshaji na matarajio ya mfumuko wa bei.
Amesema kuwa Benki Kuu imepewa mamlaka kisheria kusimamia Benki na Taasissi nyingine za fedha hivyo haiwezi kuingilia upangaji wa riba za mikopo kwenye taasisi hizo kwakuwa jambo hilo linapingana na mfumo wa uchumi wa soko huria.
“Kutoa maelekezo kwa benki na taasisi za fedha kutumia viwango fulani vya riba katika biashara zao, kutaifanya Benki Kuu kukosa nguvu na mamlaka ya kuzichukulia hatua endapo zitapata hasara kwa kutumia riba iliyopangwa ama kuelekezwa na Benki Kuu” alisisitiza Dkt. Kijaji
Naibu Waziri huyo wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amesema kuwa Benki Kuu imeendelea na jukumu lake la msingi la kuhakikisha kuwa mfumo huo unaendeshwa kwa kuzingatia sheria zilizowekwa ili kulinda maslahi ya Taifa na uchumi kwa kusimamia ongezeko la ujazi wa fedha ili kuhakikisha linakwenda sambamba na mahitaji halisi ya uchumi ili kudhibiti mfumuko wa bei.
Ameyataja majukumu mengine ya BOT kuwa ni kuhakikisha kuwa ongezeko la mikopo ya benki haliathiri uzalishaji mali kulingana na malengo ya ujazi wa fedha, kuhakikisha kuwa soko la dhamana la serikali linaendeshwa kwa ufanisi ili liweze kutoa riba elekezi kulingana na hali ya soko na uchumi kwa ujumla.

MAKALA: MAFANIKIO YA KUKABILIANA NA UJANGILI KIMKAKATI YAANZA KUONEKANA

$
0
0
NA HAMZA TEMBA - WMU

"Haiwezekani maliasili yetu ikawa inapotea hovyo hovyo kwasababu ya watu wachache wenye tamaa ya kupata utajiri wa harakaharaka, hakuna wa kumbakiza, awe mkubwa, awe nani, shikeni, wala msijali mtu cheo chake, umri wake, dini yake, kabila lake, umaarufu wake, sheria ni msumeno, watafuteni wote mpaka wakiona tembo wawe wanakimbia wenyewe".

Hiyo ilikua ni kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alipofanya ziara ya kushtukiza katika makao makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii (Mpingo House)  Jijini  Dar es Salaam tarehe 29 Oktoba, 2016 kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa operesheni ya kukabiliana na ujangili inayofanywa na kikosi kazi kilichoundwa na Wizara hiyo.

Katika ziara hiyo, Rais Magufuli akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Gaudence Milanzi alishuhudia meno ya tembo 50 yaliyokuwa yamekamatwa katika kipindi cha siku mbili zilizopita Jijini Dar es Salaam, alioneshwa pia gari lililokuwa limebeba meno hayo na watuhumiwa wanane wanaotuhumiwa kujihusisha na mtandao wa biashara haramu ya meno ya tembo.

Rais Magufuli aliwapongeza askari wote waliopo katika kikosi cha kupambana na ujangili pamoja na raia wema wanaotoa ushirikiano katika mapambano hayo na kwamba anatambua kazi nzuri wanayofanya na anawaunga mkono.

Katika hotuba yake ya kwanza ya kulihutubia bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma, Rais Magufuli alitoa vipaombele kadhaa vya kutekelezwa na wizara zake huku Wizara ya Maliasili na Utalii akiipa majukumu makuu matatu; kupambana na ujangili, kutatua migogoro ya mipaka kwenye maeneo ya hifadhi na kuongeza mapato ya Serikali.

Wizara hiyo inayoongozwa na Waziri Prof. Jumanne Maghembe; Naibu Waziri, Mhandisi Ramo Makani; Katibu Mkuu, Meja Generali Gaudence Milanzi na Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Aloyce Nzuki imejipanga kutekeleza majukumu yake makuu ya uhifadhi wa Maliasili, Malikale na Kuendeleza Utalii pamoja na vipaombele ilivyoelekezwa.

Mara tu alipoteuliwa kuingoza wizara hiyo, Prof. Maghembe alitangaza vita na majangili na kubainisha kuwa kipaumbele chake kikubwa kitakuwa ni kupambana nao. “Niwaambie majangili sasa wakafanye kazi nyingine ama wakae nyumbani, kiama kinakuja huko”, alisema.

Alisema kuwa atasimamia kwa uhakika maliasili za Watanzania kwa sababu mambo ya maliasili ndiyo eneo alilobobea kwenye usomi wake.
“Tutajitahidi pia kutangaza utalii na kuongeza mapato ya sekta hii kama tulivyofanya kwenye miaka ya 2006 hadi 2008, tuliongeza bei za vitalu na ada kwa mnyama mmoja mmoja anayewindwa,”  alisema Profesa Maghembe siku aliyoapishwa.

Mikakati ya Wizara kukabiliana na ujangili

Ni takribani mwaka mmoja na miezi miwili tangu uongozi wa Serikali ya awamu ya tano uingie madarakani, taarifa iliyotolewa na Idara ya Wanyamapori ya Wizara ya Maliasili na Utalii, inaonyesha kuwa katika kipindi cha mwezi Novemba, 2015 hadi mwezi Oktoba 2016 Wizara hiyo imefanikiwa kuweka mikakati mbalimbali ya kukabiliana na ujangili ikiwemo kuanzisha kikosi kazi maalum cha kupambana na ujangili.

Kikosi kazi hicho cha kudhibiti uhalifu wa Misitu na Wanyamapori nchini(Wildlife and Forest Crime Unit),kinasimamiwa na Watendaji wa Sekta ya Wanyamapori kwa ajili ya kukabiliana na majangili katika ngazi za juu za uwezeshaji (Facilitators) kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama nchini.

Kikosi hicho kiliundwa mwezi Julai, 2016 na Katika kipindi cha miezi mitatu (Agosti hadi Oktoba, 2016) kimefanikiwa kukamata majangili 107 na kesi 9 ziko mahakamani, upelelezi wa kesi nyingine unaendelea. Nyara mbali mbali, silaha na vifaa vya kufanyia ujangili pia vimekamatwa na kikosi kazi hicho.

Wizara imefanikiwa kuimarisha Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) ambayo ilizinduliwa rasmi mwezi Novemba, 2015 na Rais wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na kuanza majukumu yake rasmi tarehe 1 Julai, 2016.

Mamlaka hii yenye jukumu la kuendeleza shughuli za ulinzi na uhifadhi wa wanyamapori nchini kwa maeneo yote yaliyopo nje ya Hifadhi za Taifa na Eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhibiti ujangili kwenye maeneo hayo.

Mabadiliko ya mfumo wa utendaji kutoka ule wa kiraia kwenda wa Jeshi Usu umenzishwa na Wizara kwa ajili ya kuimarisha nidhamu, ufanisi wa utendaji kazi za uhifadhi pamoja na mapambano dhidi ya ujangili. Katika kipindi hicho mafunzo kadhaa yametolewa kwa watumishi 425 wa TANAPA katika kuelekea mabadiliko hayo.

Watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania pia pia wamepatiwa mafunzo hayo. Lengo ni kutoa mafunzo hayo kwa watumishi wote wa taasisi za uhifadhi nchini zikiwemo za wanyamapori na misitu.

Pamoja na mafunzo hayo, matumizi ya teknolojia ya ndege zisizokuwa na rubani (drones) kwa ajili ya doria na ulinzi wa mipaka na wanyamapori yamepewa kipaombele katika hifadhi mbalimbali za taifa na Pori la Akiba la Selous kama mkakati wa kukabiliana na ujangili.

Mkakati mwingine ulioanzishwa na kuimarishwa ni ukaguzi wa nyara katika viwanja vya ndege na bandari kwa kutumia mbwa maalum wa kunusa ili kutambua nyara na kufuatilia majangili.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa ushirikiano na nchi jirani katika kutatua changamoto za uhifadhi na biashara haramu ya ujangili umeimarishwa. Katika eneo hili Tanzania inashirikiana na nchi ya Msumbiji, Zambia, Uganda na Kenya kukabili ujangili unaovuka mipaka ya nchi hizo.

Ushirikishwaji wa wananchi katika uhifadhi na vita dhidi ya ujangili ni moja ya mkakati uliowekwa na wizara. Elimu ya uhifadhi kwa wananchi  imeendelea kutolewa katika  wilaya 11 na vijiji 57 vinavozunguka Pori la Akiba la Selous, Mapori ya Akiba  ya Lukwika/Lumesule na Msanjesi na eneo la Ardhioevu la Ziwa Natron.

Miongoni mwa hatua zilizochukuliwa;

Katika kipindi cha mwezi Novemba, 2015 hadi Oktoba 2016, taarifa ya Idara ya Wanyamapori inaeleza kuwa Sekta ya Wanyamapori imefanikiwa kukamata jumla ya watuhumiwa 5,894 kwa makosa mbalimbali ya uvunjaji wa Sheria za Uhifadhi na kuwafungulia mashitaka. Jumla ya kesi 859 zilifunguliwa. Kesi 136 zenye watuhumiwa 248 zilihukumiwa kifungo cha jumla ya miezi 8,295 na kesi 198 zenye watuhumiwa 234 walilipa faini jumla ya shilingi 387,985,063/=.

Imeeleza kuwa silaha 254 za aina mbalimbali zilikamatwa katika kipindi hicho, Nyara za aina mbalimbali zilikamatwa ikiwemo meno ya tembo vipande 848 vyenye uzito wa kilo 2,664.48, nyamapori yenye uzito wa kilo 7,790 za wanyama mbalimbali, meno 8 ya kiboko, magunia 67 ya magamba ya kakakuona, ngozi 16 na mikia 33 ya wanyamapori mbalimbali.

Miongoni mwa watuhumiwa waliokamatwa katika kipindi hicho ni watu sita akiwemo mfanyabiashara Yusuf Ally (34) aliyewahi kutajwa na Rais John Magufuli kwa jina maarufu la ‘Mpemba’ kuwa ni kinara wa ujangili, watuhumiwa hao ambao kesi yao bado inaendelea walifikishwa mahakamani wakikabiliwa na mashtaka ya kujihusisha na biashara ya meno ya tembo yenye thamani ya shilingi milioni 785.6.

Mtuhumiwa mwingine maarufu wa ujangili aliyewahi kukamatwa nchini ni mwanamke wa China anayedaiwa kuongoza genge kubwa zaidi la usafirishaji wa pembe za ndovu barani Afrika. Akipewa jina la utani “Ivory Queen”, Yang Feng Glan anadaiwa kusafirisha pembe za ndovu 706 kutoka nchini kwenda Mashariki ya mbali. Glan, 66, anadaiwa kuwa na ukaribu na majangili wa Afrika Mashariki na walanguzi wa China, kesi yake bado ipo mahakamani.

Ujangili waripotiwa kuanza kupungua;

Januari 17 mwaka huu (2017), akizungumza kwenye kikao cha kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii mkoani morogoro, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Generali, Gaudence Milanzi alisema ujangili hapa nchini kwa sasa umepungua kwa kiasi kikubwa na kwamba nyara zinazokamatwa kwa sasa ikiwemo meno ya tembo ni za zamani zilizokuwa zikisubiria kusafirishwa kwenda nje ya nchi.

Aliongeza kuwa mizoga ya wanyamapori imepungua ikilinganishwa na kipindi cha nyuma ambapo ni dalili pia ya kupungua kwa ujangili nchini, “mafanikio hayo yametokana na kazi kubwa inayofanywa na vikosi maalum vya Askari wa wanyamapori vya kudhibiti ujangili kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama nchini”, alisema Milanzi.

Katika hatua nyingine alieleza kuwa kitendo cha Serikali ya China kupiga marufuku biashara ya meno ya tembo nchini humo ni jambo la kupongezwa na kwamba uamuzi huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza msukumo wa vitendo vya ujangili nchini kwa kuwa nchi hiyo ni miongoni mwa masoko makubwa ya meno hayo duniani.

Ujangili haukubaliki kwa kuwa unatishia kuathiri faida kubwa inayopatikana kupitia sekta ya utalii ambayo kwa kiasi kikubwa inategemea uwepo wa wanyamapori katika hifadhi zetu, Sekta hii inachangia asilimia 17.5 ya pato la taifa na ni sekta inayoongoza kwa miaka mitatu mfululizo kwa kutoa mchango wa asilimia 25 ya mapato yote ya fedha za kigeni nchini.

Ni jukumu la kila Mtanzania kuona umuhimu wa rasilimali hizi na kuunga mkono juhudi za Serikali kuhakikisha kuwa Maliasili zetu zinaendelea kuwepo kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo, Tanzania bila Ujangili inawezekana, kila mmoja akitimiza wajibu wake.
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi alipofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya hiyo (MPINGO HOUSE) jijini Dar es salaam Oktoba 29, 2016. (Picha na Ikulu)
Rais Dkt John Pombe Magufuli akikagua pembe za ndovu 50 zilizokamatwa katika operesheni maalum ya kusaka majangili alipofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii (MPINGO HOUSE) jijini Dar es salaam Oktoba 29, 2016. (Picha na Ikulu)

HALMASHAURI YA WILAYA YA KISARAWE YATENGA KATA 10 KWA AJILI YA KILIMO CHA MKATABA

$
0
0

Dotto Mwaibale, Kisarawe

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani imetenga Kata 10 kwa ajili ya kilimo cha mkataba kitakachoendeshwa na Taasisi ya Winamwanga Cultural Heritage Association.

Mratibu wa mradi huo kutoka taasisi hiyo, Saidi Simkonda akizungumza juzi katika uzinduzi wa mafunzo ya kilimo hai na mafunzo ya ufugaji wa kuku chotara na mafunzo ya utunzaji wa mazingira kwa kutumia vikundi vya ufugaji wa nyuki yaliyofanyika wilayani humo juzi alisema mradi huo umelenga kuwainua kiuchumi wananchi wa Kisarawe na Mkoa wa Pwani kiujumla.

Alisema taasisi hiyo imepanga kuanzisha vikundi vya kuweka na kukopa ili kuinua uchumi wa wananchi kupitia vikundi vya ujasiriamali wa kilimo hai na ufugaji wa kuku chotara pamoja na kuwawezesha kupata fursa za mikopo katika asasi za kifedha zilizopo wilayani humo.

"Taasisi yetu imejipanga kuanzisha kilimo cha mkataba ambapo mazao yatakayopatikana itayanunua na tayari serikali ya Kijiji cha Kuluwi imetoa ghala la kuhifadhia mazao hayo.

Mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo ambaye ni Ofisa Maendeleo ya Jamii, Wanchoke Chinchibera alisema mradi huo utawasaidia wananchi na kuwa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe imetenga kata kadhaa kwa ajili ya mradi huo ambazo ni Maluwi, Vikumburu, Kuluwi na Mafizi.

Alisema kwa sababu mradi huo ni mpya katika wilaya yao na utafanya shughuli zake kwa kilimo cha mkataba aliishauri taasisi hiyo kujenga ushirikiano mkubwa na wananchi kupitia vikundi ambavyo tayari vimesajili na majina yake kuwepo katika daftari ofisini kwa mkurugenzi wa halmshauri hiyo.
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi wa kilimo cha mkataba kupitia Taasisi ya Winamwanga Cultural Heritage Association kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, ambaye ni Ofisa Maendeleo ya Jamii, Wanchoke Chinchibera akihutubia wadau wa kilimo wa wilaya hiyo wakati wa semina ya siku moja iliyohusu kilimo cha mkataba iliyofanyika juzi wilayani humo. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa mradi huo, Mwajuma Motto, Ofisa Kilimo na Umwagiliaji wa wilaya hiyo, Elliot Mwasabwite na Mwenyekiti wa Bodi wa Taasisi hiyo, Esabela Luoga. 
Semina ikiendelea.
Meza kuu.
Mmoja wa maofisa wa Taasisi hiyo, Wilson Kibugu akitoa maelezo kwa wadau wa kilimo wa wilaya hiyo wakati wa semina hiyo ya siku moja iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Wilaya hiyo.
Ofisa Utawala wa Taasisi hiyo, Fatma Shaib (kushoto), akisoma lisala.
Mgeni rasmi Wanchoke Chinchibera akipokea lisala kutoka kwa Ofisa Utawala wa Taasisi hiyo, Fatma Shaib.
Mratibu Mradi wa Kilimo wa Taasisi ya Winamwnga Cultural Heritage Association, Saidi Simkonda (katikati), akitoa mada katika uzinduzi wa mafunzo ya kilimo hai na mafunzo ya ufugaji wa kuku chotara na mafunzo ya utunzaji wa mazingira yaliyofanyika wilayani Kisarawe mkoani Pwani juzi. 
Ofisa Mauzo wa Kampuni ya Syngeta Tanzania Limited, John Ngoma akielezea ubora wa mbegu aina ya Sy 514 inayosambazwa na kampuni hiyo kupitia miradi ya kilimo ya taasisi hiyo.
Mkurugenzi wa Mradi wa kilimo wa Taasisi ya Winamwnga Cultural Heritage Association, Mwajuma Motto (katikati), akizungumza katika uzinduzi wa mafunzo ya kilimo hai na mafunzo ya ufugaji wa kuku chotara na mafunzo ya utunzaji wa mazingira kwa kutumia vikundi vya ufugaji wa nyuki yaliyofanyika wilayani Kisarawe mkoani Pwani jana. Kulia ni Mwezeshaji, Filbert Luoga na kushoto ni mratibu wa miradi wa taasisi hiyo, Saidi Simkonda. 
Ofisa Kilimo na Umwagiliaji wa wilaya hiyo, Elliot Mwasabwite akichangia jambo kwenye semina hiyo.

SPIKA WA BUNGE JOB NDUGAI AMJULIA HALI MKURUGENZI WA TEHAMA WA BUNGE

$
0
0
Daktari Bingwa Upasuaji wa Mgongo na Mishipa ya Fahamu MOI, Nicephorus Rutabasibwa (kulia) akifafanua jambo kwa Spika wa Bunge Job Ndugai  (wa tatu kushoto) Dar es Salaam jana wakati alipofika kumjulia hali Mkurugenzi Msaidizi wa Tehama (ICT)  wa Bunge, Lily Mraba aliyelazwa katika Taasisi hiyo 
 Muuguzi Mwandamizi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (MOI), Zaituni Bembe (kushoto) akiagana na Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai  Dar es Salaam jana mara baada ya kutoka katika Taasisi hiyo, wakati alipokwenda kumjulia hali Mkurugenzi Msaidizi wa Tehama (ICT) wa Bunge, Lily Mraba.
Daktari wa Mishipa ya Fahamu katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI)  Hamisi Kinyerero akiagana na maofisa wa Bunge walioongozana na Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai wakati alipofika kumjulia hali Mkurugenzi Msaidizi wa Tehama (ICT) wa Bunge, Lily Mraba. aliyelazwa katika Taasisi ya Mifupa MOI. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA )

AIRTEL YAZINDUA KAMPENI YAKE MPYA YA MR MONEY IJULIKANAYO KAMA RELAX.. AIRTEL MONEY

$
0
0


Meneja Uhusiano wa Airtel akitambulisha kampeni  kabambe  ya Mr Money ijulikanayo kama Relax.. Airtel Money ndio mambo yote. Kupitia huduma ya Airtel Money wateja wetu wanafaidika na huduma nyingi zenye faida zaidi kwa kupiga tu *150*60#

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia huduma yake inayokuwa kwa kasi ya Airtel Money imezindua na  kuitambulisha kampeni  kabambe  ya Mr Money ijulikanayo kama Relax.. Airtel Money ndio mambo yote.

Akiongea kuhusu Kampeni hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando aliseme “Kupitia huduma ya Airtel Money wateja wetu wanafaidika na mambo lukuki ikiwemo

Kutuma pesa kwenda mitandoa yote kwa bei nafuu wateja wetu wanaweza kutuma pesa kwenda mitandao mingine kwa tozo ileile wakati wowote mahali popote pale nchini. Haya ni mapinduzi ya kipekee katika huduma za kifedha ambapo tumewezesha wateja wetu kufanya miamala hiyo kwa urahisi zaidi bila kujali gharama.

Kupata vifurushi  bora kupitia Airtel Money OFA KABAMBE vyenye ujazo zaidi kuliko vifurushi vya mitandao mingingine yote: Kupata hii piga *150*60# kisha nunua kifurushi kupia Airtel Money kwa kuchagua No.6 OFA KABAMBE  , Pia vipo vifurushi vya UNI packs sasa vinapatikana kupitia huduma ya Airtel Money hivyo kuwawezesha wanafunzi kujiunga na vifurushi hivyo kwa urahisi zaidi

Kutuma pesa kwenda benki na kutoa pesa kutoka kwenye akaunti yako ya Airtel Money kwenda Benki-  sasa wateja wa Airtel Money wanaweza kufanya miamala hiyo kwenye benki 38 ambazo tayari tunaushirikiano nazo. Kadhalika wateja waweza kutumia ATM za umoja switch na CRBD zaidi ya 1105 nchini kwa kutoa pesa kwenye akaunti zao za Airtel Money masaa 24 kila siku. ushirikiano huu umeongeza idadi ya mawakala na kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha kupitia simu za mkononi

Na pia tunawewezesha wateja wetu kupata mikopo ya Timiza isiyo na dhamana  kwa wateja wetu na mawakala nchini, Mteja anaweza kuomba mkopo wa hadi laki 5 na kujipangia yeye mweye alipe lini SIKU, WIKI au baada ya  MWEZI. Airtel Timiza ni suluhisho kwa mahitaji ya mikopo ya haraka ya kutatua changamoto za kijamii lakini pia inawawezesha wajasiriamali wadogo wadogo kupata mitaji kwaajili ya biashara  zao papo hapo.

“Ndio maana tunaseme? Relax Airtel Money mambo yote” alisisitiza Mmbando

Huduma ya Airtel Money, kwa sasa imefanikiwa kwa kufanya mihamala mingi ya kifedha nchini hasa  katika maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma za kibenki. Mwezi uliopita Airtel Money pia ilifanikiwa kugawa gawio la shilingi bilioni 3.5 kwa watejawake wote wanaotumia huduma ya Airtel Money.
 

DKT PALLANGYO AKUTANA NA WASIMAMIZI WA MIRADI YA NISHATI

$
0
0
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kushoto) akiongoza kikao kazi na wasimamizi wa miradi ya nishati kilichofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 03 February, 2017 lengo likiwa ni kujadili maendeleo na changamoto za miradi hiyo.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kushoto) akiongoza kikao kazi na wasimamizi wa miradi ya nishati kilichofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 03 February, 2017 lengo likiwa ni kujadili maendeleo na changamoto za miradi hiyo.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kushoto) akiongoza kikao kazi na wasimamizi wa miradi ya nishati kilichofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 03 February, 2017 lengo likiwa ni kujadili maendeleo na changamoto za miradi hiyo.
 Sehemu ya wasimamizi wa miradi na watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Wakala wa Nishati Vijijini (REA), wakifuatilia maelekezo  yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi  Juliana Pallangyo (hayupo pichani)
 Kutoka kushoto, Milka Digha,  Alika Ilomo na Costa Mosha kutoka Idara ya Sera na Mipango, Wizara ya Nishati na Madini  wakinukuu maelekezo  mbalimbali yaliyokuwa yanatolewa katika kikao hicho.

Viewing all 46329 articles
Browse latest View live




Latest Images