Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1125 | 1126 | (Page 1127) | 1128 | 1129 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Taasisi ya Global Peace Foundation (GPF) Tanzania, imemteua mshindi wa Big Brother Africa Hotshots 2014) Idris Sultan, kuwa balozi wa amani kwa vijana duniani.

  Mkurugenzi Mkazi wa GPF Tanzania, Martha Nghambi alisema kuwa wameamua kumtumia Idris kutokana na mvuto wake kwa vijana na kutokana na hilo atafikisha ujumbe kirahisi kwa vijana ambao ni zaidi ya asilimia 60 ya idadi ya watu Tanzania.

  Alisema kuwa bado kuna changanoto nyingi za kudumisha amani duniani kwani mpaka sasa kuna baadhi ya nchi zipo katika matatizo makubwa yaliyosababishwa na uvunjifu wa amani.
  Martha alisema kuwa Idris ni mtu sahihi katika kampeni yao na wanaamini kuwa kupitia yeye vijana na watu wengine watapata ujumbe wa kuhamaisha kudumisha amani duniani.

   “Kuna baadhi ya nchi zina matatizo ya amani, waswahili wanasema, ukiona kwa mwenzako kunawaka moto… kwako andaa maji, sisi tumeamua kuchukua tahadhari mapema ili kulinda amani yetu,”
  Kwa upande wake, Idris alifurahi sana kupewa nafasi hiyo ambayo ni kubwa sana katika maisha yake.

  “Wamenithamini na kuniona ninafaa katika kampeni hii, ni kweli, amani inatakiwa kuanzia kwenye familia mpaka juu ambako wengi wanadhani vita tu ndiyo inatakiwa kupigiwa kelele,  vijana ndiyo nguvu kazi ya ya taifa na hivyo tunatakiwa kuwa na mawazo yaliyopanuka ili kujipatia vipato na kuachana na lawama kutokana na kukosa soko la ajira,” alisema Idris.

  Alifafanua kuwa kuwa balozi ni jukumu zito na atalitumikia ipasayo ili kufikia malengo yaliyowekwa. “Amani ni  kazi ya kila siku na ni muhimu, leo hii wasanii wanaigiza na wanamuziki wanafanya kazi zao bila kuwa na woga, hii yote inatokana na amani,” alisema.

  Global Peace Foundation ni shirika lisilo la kiserikali na lisilo tengeneza faida lenye makao yake makuu, mjini Washington DC, Marekani. Shughuli kubwa la shirika hili ni kuhamasisha amani duniani kupitia matawi yake mbalimbali duniani.

  Mbali ya Tanzania, matawi mengine katika bara la Afrika ni Kenya, Uganda na Nigeria. Kauli mbiu ya shirika hilo ni “We are all  “One family under God”(sisi wote ni familia moja kwa Mungu).
  Kwa sasa Global Peace Tanzania inaendesha kampeni ya kuhamsisha amani kuanzia ngazi ya familia ijulikanyo kama “Vijana na Amani”. Kupitia kampeni hii, GPF Tanzania inahamasisha amani kwa kutoa elimu katika shule, vyuo na jamii kwa ujumla.

   Mshindi wa Big Brother Africa Hotshots 2014) Idris Sultan (kulia), akipokea cheti cha utambulisho  wa kuwa balozi wa Amani kutoka kwa Mkurugenzi Mkazi Taasisi ya Global Peace Foundation (GPF) Martha Nghambi.
  Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Global Peace Foundation (GPF) Tanzania, Martha Nghambi (wa pili kushoto) na mshindi wa Big Brother Africa Hotshots 2014) Idris Sultan (wa tatu kulia) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutangazwa kuwa balozi wa amani kwa vijana Tanzania


  0 0


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela wakati alipomtembelea nyumbani kwake, Kilimani mjini Dodoma Februari 1, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela wakati alipomtembelea nyumbani kwake, Kilimani mjini Dodoma Februari 1, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela wakati alipomtembelea nyumbani kwake, Kilimani mjini Dodoma Februari 1, 2017. baada ya kuzungumza naye (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0


  0 0

   Kaimu Jaji  Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahimu Juma akimkabidhi laptop Hakimu  Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo Kimara, Mhe. Asia Mjemah kwa ajili ya uchapishaji nakala za hukumu jana  jijini Dar es Salaam.

   Kaimu Jaji  Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahimu Juma akizungumza katika ufungaji wa maonesho ya wiki ya sheria katika viwanja vya Mnazi  mmoja jana jijini  Dar es Salaam.

   Baadhi ya viongozi mbalimbali na wananchi wakimsikiliza Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahimu Juma katika ufungaji wa maonesho ya wiki ya sheria katika viwanja vya Mnazi  mmoja jana jiji Dar es Salaam

  Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa,Ibrahimu Juma akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mblimblia katika viwanja vya Mnazi  mmoja leo jiji Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

  Mahakama kuu ya Tanzania imesema itafanya mpango wa kuongeza kasi ya utoaji wa haki kwa watu wote ikiwemo kupunguza  kesi za zamani katika ngazi zote za mahakama nchini.

  Hayo yamesemwa  jijini Dar es salaam na Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma katika kilele cha maonyesho ya wiki ya sheria, akisisitiza watongeza vitendea kazi na watumishi wa mahakama ili kuwepo na urahisi katika mfumo wa kusikiliza kesi na kuzitolea hukumu.

  Akizungumzia baadhi ya malalamiko yaliyotolewa na mmoja wa wananchi Profesa Juma amesema kuwa wamepokea malalamiko juu ya mahakama moja ambayo hakuitaja jina lake ambayo watumishi wake wamekuwa wakitoa lugha chafu,uzembe,kuchelewesha haki,kutumika kama vishoka sambamba na kuongea lugha za jazba hali ambayo ilimkwaza mwananchi huyo.

  ‘’Natoa rai kwa mahakama kuhakikisha wanatoa takwimu nawakumbusha kwamba kuna waraka wa Jaji Mkuu wa mwaka 2013  ambao aliwataka Majaji wafawidhi,Majaji wafawidhi na watendaji kuona kila baada ya miezi mitatu kuanzia Julai 2013 kuwasilisha mashauri ya  muda mrefu’’.amesema Profesa Juma.

   Pia ametoa rai kwa wadau wote kuendeleza yale mazuri yaliyojitokeza katika wiki ya huduma za kisheria katika viwanja vya mnazi mmoja ikiwemo kusikiliza kero za kisheria zinazowakabili wananchi hata watakapofika katika ofisi za


  0 0  2 FEBRUARY 2017– STONE TOWN, ZANZIBAR: Next Thursday on the 9th of February Sauti za Busara 2017 festival will kick-off in Stone Town, Zanzibar and the local tourism industry can breathe a sigh of relief. After a year-long hiatus, Sauti za Busara is back to business promoting local culture, building technical capacities and boosting the local economy with employment and training for East Africans.

  More than just a festival, Sauti za Busara has generated over 70 million USD in revenue for Zanzibar since it began in 2004. Every year, the small team of ten expands to 150 crew members directly employed in the festival, always prioritizing local people for crucial roles in Artists Management, Administration, Press Relations, Tickets and Merchandise, Venue & Technical and Security.

  A focus on training and skills-building enhances Busara’s sustainability while increasing economic impact for the local community. In 2016, Busara Promotions hosted training programs in stage management, sound engineering, stage lighting, press and marketing skills. In partnership with festivals such as Bushfire in Swaziland and Oya Festival in Norway, the Busara team benefited from hands-on learning experiences by joining other festival crews, where skills, knowledge and contacts are shared across borders.

  Sauti za Busara has helped put Zanzibar on the cultural tourism map as a premiere destination that goes beyond the ‘sun & sand’ cliché. Trish Dhanak, owner of Upendo hotel and restaurant explains, “As a business investor, it’s our job to show travellers the best of Zanzibar, to learn about the island’s deep cultural roots. Sauti za Busara is a vital link to travellers from around the world and mainland Africa -- it’s the music that brings them to Zanzibar and while they’re here, we hope they’ll discover a plethora of reasons to return.”

  February is now the highest month in the year for arrivals to Zanzibar with over 40,000 visitors. At this time, local flights and ferries are full; hotels and restaurants are abuzz with festival energy.

  As the festival continues to grow and attract more international visitors every year, keeping it accessible to local and regional guests is a priority for Busara. This year, the four-day Festival Pass for Tanzanians is only 20,000 TZS or 6,000 TZS per day. African passport holders pay 120,000 TZS (60 USD) or 50,000 TZS per day (25 USD). Tickets will be available at the Old Fort starting Tuesday 7th February, from 10:00am.

  Zanzibar’s weather forecast predicts highs of 34 degrees Celsius with blue skies for everyone. Sauti za Busara, mentioned by CNN as one of 7 top African music festivals that are too good miss, will take place in Stone Town, Zanzibar during 9th to 12th February, 2017.

  Sauti za Busara 2017 is generously powered by: Norwegian Embassy, Swiss Agency for Development & Cooperation (SDC), ZANTEL, Africalia, Embassy of Germany, Zanlink, Memories of Zanzibar, Ethiopian Airlines, Mozeti, Coastal Aviation, Ikala Zanzibar Stone Town Lodge, Music in Africa, Chuchu FM Radio, Tifu TV and Zanzibar Media Corporation.

  0 0

   Waziri wa Fedha na Mipango, mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akifafanua baadhi ya vipengele vya Muswada wa marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 4 ya Mwaka 2016, kuhusu marekebisho ya Sheria ya Mikopo, Misaada na Dhamana. Muswada huo ulipitishwa kuwa Sheria na Bunge Februari Mosi, 2017.
   Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. George Masaju, akihitimisha mjadala wa Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 4 ya Mwaka 2016, uliopitishwa na wabunge kuwa Sheria Februari Mosi, 2017, Mjini Dodoma
   Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) na Naibu Waziri wake, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wakipitia nyaraka za Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 4 ya Mwaka 2016, Bungeni Mjini Dodoma, Muswada ambao tayari Bunge limeupitisha kwa kishindo kuwa Sheria Februari Mosi, Mjini Dodoma.
   Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akitoka nje ya ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma baada ya kutetea na kufafanua vipengele kadhaa vya Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 4 ya Mwaka 2016, husani eneo la Sheria ya Mikopo, Misaada na Dhamana,  na baadaye Muswada huo kupitishwa na Bunge ili uwe Sheria, Februari Mosi, 2017, Bungeni Mjini Dodoma.
   Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akimweleza jambo Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhe. Dkt. Medard Kalemani (Mb), nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma, baada ya Bunge kupitisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 4 ya Mwaka 2016, Februari Mosi, 2017.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)
    Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb), akimpongeza Mkurugenzi wa Idara ya Sheria wa Wizara hiyo Bi. Suzana Mkapa, Nje ya Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma, kwa namna alivyoshirikiana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. George Masaju, kufanikisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 4 ya Mwaka 2016, uliopitishwa na wabunge Februari Mosi, 2017.
   Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb), akifurahia jambo na maafisa waandamizi wa masuala ya Sheria na Uchumi wa Wizara yake baada ya Bunge kupitisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 4 ya Mwaka 2016, uliopitishwa Februari Mosi, 2017, mjini Dodoma.
   Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa waandamizi wa masuala ya Sheria na Uchumi wa Wizara yake, nje ya ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma, baada ya kupitishwa kwa marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 4 ya Mwaka 2016, ikiwemo Sheria ya Mikopo, Misaada na Dhamana.
   Maafisa Waandamizi wa  masuala ya Sheria na Uchumi wakiambatana na Mkurugenzi wa Idara ya Sheria wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Suzana Mkapa (kulia), wakiwasili kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma, kusikiliza mjadala wa Bunge kuhusu Muswada wa  Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 4 ya Mwaka 2016, uliopitishwa na wabunge kuwa Sheria Februari Mosi, 2017.

  0 0


  0 0


  0 0

  NA Beatrice Lyimo-MAELEZO.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA Dkt. John Pombe Magufuli ametoa wito kwa Mahakama kukusanya Shilingi Trillioni 7.3 ambazo ni matokeo ya serikali kushinda kesi mbalimbali za ukwepaji kodi.

  Rais Magufuli ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya Sheria na Mwaka mpya wa Mahakama iliyobeba kauli Mbiu isemayo Utoaji haki kwa wakati kuwezesha ukuaji wa uchumi.

  Alisema  kuwa Takwimu zinaonesha kuwa kumekuwa na baadhi ya kesi za pingamizi za kodi ambapo  Serikali imeshinda kesi hizo japo  fedha hizo hazijakusanywa mpaka sasa.“Kukwepa au kutolipa kodi ni kosa kubwa sana, kila mtu anawajibu wa kulipa kodi nchini kwa maendeleo ya nchi” nalifafanua Dkt Magufuli.

  Aidha, Rais Magufuli alisema kuwa katika kuelekea ukuaji wa uchumi, Mahakama iwe sehemu ya chanzo cha pato la taifa kwa kwa kuhakikisha wale wanaotakiwa kulipa fidia baada ya kushindwa kesi wanafanya hivyo pamoja na kuwabana wakwepa kodi kwani kutimiza hilo kutaleta mabadiliko katika uchumi wa nchi.

  Katika hatua nyingine Rais Magufuli alisema kuwa Maendeleo ya nchi hayaangalii chama chochote, hivyo amevitaka vyombo vya utoaji haki kutoa haki kwa usawa.Kwa upande wake Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma alisema kuwa Mahakama imeandaa Mpango mkakati uliolenga kufanya maboresho ndani ya Mahakama.

  Alisema kuwa mpango mkakati huo umelenga masuala makuu matatu ikiwemo Utawala bora, uwajibikaji na usimamizi wa rasilimali, upatikanaji wa haki na kwa wakati, uimarishaji wa amani kwa wananchi na ushirikishwaji wa wadau katika shughuli za mahakama.

  Aidha Kaimu Jaji Mkuu alisema kuwa Mahakama imefanikiwa kusikiliza mashauri ya kesi za uchaguzi kwa asilimia 100.“kati ya mashauri ya kesi 249 ikiwemo 53 za ubunge na 196 za madiwani ya waliopinga uchaguzi kati ya kesi hizo, kesi 52 za ubunge zilikamilishwa na kesi zote za madiwani zilikamilishwa” alifafanua Kaimu Jaji Mkuu.

  Naye Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju amesema kuwa Katiba imeanisha bayana Kanuni ambazo zinapaswa kuzingatiwa na Mahakama wakati ikitekeleza mamlaka yake ya utoaji haki.“utoaji haki mapema ipasavyo ni moja ya Kanuni ambazo Mahakama inapaswa kuzingatia katika utekelezaji wa majukumu yake kama inavyoelekezwa katika Katiba” alifafanua Mwanasheria Mkuu.

  Alisema kuwa Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na kufanya biashara katika nchi ya Tanzania hivyo kuchochea maendeleo ya kiuchumi.Siku ya Sheria nchini ilioanzishwa mwaka 1996 ikiwa ni siku muhimu ya kuombea Majaji na Mahakimu ili kuweza kusikiliza kesi.

  0 0

  Wahe,Waandishi wa Habari,nimewaiteni hapa leo kwa ajili ya kuwapa Taarifa za hujuma zinazopangwa kufanywa dhidi ya chama chetu.

  Kama mnavyofahamu kwamba,Chama chetu kiko katika sintofahamu ya Mgogoro wa Kiuongozi.Hata hivyo pampja na hali hiyo kuwepo,tunaimani kwamba,sintofahamu hii ya Kiuongozi tutaumaliza wana CUF wenyewe.

  Mara nyingi huwa siyo kawaida yangu kusimama hadharani kuzungumzia hali ya chama kupitia Vyombo vyenu vya habari,lakini kwa hali ilivyo nimewajibika kutokeza hadharani kuzungumza nanyi.

  Kwa mujibu wa Katiba ya CUF Ibara ya 88 (2) Nanukuu.Katibu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama atakuwa na wajibu Ufuatao,Mwisho wa kunukuu.Ibara ya 88 (2) (a) Atakuwa Mtendaji Mkuu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Chama Ibara ya 87 (1)Wajibu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Taifa ni kuhakikisha Usalama wa Chama Nchini kote

  Nimeona ninukuu vifungu hivi vya Katiba ya CUF ili kuweka sawa uhalali wangu katika kutoa Taarifa hii kwenu ninyi Waandishi wa Habari.Tunazo Taarifa kwamba,Katibu Mkuu wetu anafanya Vikao mbalimbali na Viongozi wa Chadema vyenye muelekeo wa kuhujumu harakati za chama chetu pamoja na baadhi ya Viongozi wa CUF upande wa Tanzania Bara.

  Napenda kuchukua fursa hii kumsihi Katibu Mkuu wa Chama changu,Mhe,Maalim Seif,kwamba aache kufanya hivyo kwani vikao hivyo havina tija kwake ziadi ya kujenga Uhasama dhidi ya Wanachama na Viongozi wa CUF wa Bara na Zanzibar.

  Nimshauri Katibu Mkuu wangu kwamba,Viongozi wa Chadema anaowatumainia kama ndiyo wataweza kumsaidia katika dhamira zake,atakuwa anapoteza muda wake bure.Tunazo Taarifa kwamba kuna Vijana wanaandaliwa kuja kuvamia Ofisi Kuu za CUF Buguruni kwa ajili ya kufanya Uharibifu wa Mali za Chama.

  Nichukue fursa hii pia kutoa ONYO KALI kwamba Vijana hao wasithubutu wala kujaribu kufanya kitu kama hicho kwani Ulinzi wa Chama umejipanga vyema kukabiliana vikali na Kikundi chochote ambacho kina dhamira ya kufanya hujuma yeyote dhidi ya chama chetu cha CUF.

  Kuhusu kuwafanyia hujuma baadhi ya Viongozi wa Chama chetu,tunawaambia kwamba,wote wanaotaka kufanya Vitendo hivyo tunawajua mmoja mmoja na anapoishi,ila kwa sababu maalum,sitoweza kuwataja kwa sasa,lakini kwa kuwa,chama chetu kinafanya kazi kwa mujibu wa sheria za Nchi,Tayari tumevitaarifu Vyombo vya Ulinzi na Usalama vya Serikali juu ya Vitisho ya vitendo dhalimu vinavyokusudiwa kufanywa na Wasaliti wa Chama chetu dhidi ya Viongozi wetu wa Chama upande wa Tanzania Bara.

  Lakini pia napenda kuchukua fursa hii kutoa Onyo pia kwa wale wanaojiita ni Viongozi wa CUF halafu wanazungumzia Uchochoroni na kuwatukana Viongozi halali wa Chama cha CUF,kwamba waache mara moja,tumewavumilia sana kiasi cha kutosha sasa dawa yao iko jikoni mmoja mmoja baada ya mwingine tutawajibika nao.

  Waheshimiwa Wanahabari nawashukuru,asanteni sana kwa kunisikiliza.

  HAKI SAWA KWA WOTE

  Masoud Omar Mhina

  MKURUGENZI WA ULINZI NA USALAMA CUF TAIFA.
  Mkurugenzi wa Usalama wa Chama cha Wananchi (CUF), Masoud Mhina, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana, kuhusu madai ya hujuma zinazopangwa kufanywa dhidi ya chama hicho. Kushoto ni Ofisa Dawati wa CUF, Awadhi Mdoe.
  Ofisa Dawati wa CUF, Awadhi Mdoe, akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kulia ni Naibu Kamanda wa Blue Gurd, Wilaya ya Kinondoni, Mohamed Kiotola, Mkurugenzi wa Haki za Binadamu, Zainabu Mdolwa, Mkurugenzi wa Usalama wa Chama cha Wananchi (CUF), Masoud Mhina na Mkurugenzi wa Blue Gurd wa Wilaya ya Temeke, Saidi Mtumbwe.
  Wafuasi wa chama hicho wakiwa kwenye mkutano huo.

  0 0

   
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimsikiliza mwananchi, Bi. Sobha Mohamed, aliyejitokeza kueleza kero ya masuala ya mirathi  anazozipata katika mahakama mbele yake wakati wa sherehe za uzinduzi Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama Mtaa wa Chimala Ocean road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017.

    Jaji Kiongozi Mhe Ferdinand Wambali akichukua melezo ya mwananchi, Bi. Sobha Mohamed, aliyejitokeza kueleza kero ya masuala ya mirathi  anazozipata katika mahakama mbele yake wakati wa sherehe za Kuzinduzi Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama Mtaa wa Chimala Ocean road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017.PICHA NA IKULU


  0 0


   Waya wa umeme uliokatika ukiwa unaanza kutoa moshi baada ya kukatika mtaa wa Mchikichi na Msimbazi.


    Gari la Zimamoto likiwa eneo la tukio mtaa wa Mchikichi na Msimbazi baada ya waya wa umeme kukatika na kuanza kutoa moshi na hatimaye moto.

   Askari wa zimamoto wakiwa wanajaribu kuuzima moto huo kabla ya shirika la umeme la Tanesco hawajafika.
   Gari la Shirika la umeme Tanesco likiwasili eneo la tukio mtaa wa Mchikichi na Msimbazi baada ya waya wa umeme kukatika na kuanza kutoa moshi na hatimaye moto.

  Wafanyakazi wa Shirika la Umeme la Tanesco wakiwa wanajadiliana na askari wa zimazoto baada ya kufika eneo la tukio na kuzima umeme.
  Picha zote na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya akizungumza na Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji nchini kabla ya Balozi huyo kuzindua Mkataba wa Huduma kwa Mteja ulioandaliwa na Idara hiyo ambao unalenga kuboresha zaidi huduma zitolewazo na Uhamiaji ambapo kuanzia sasa Pasipoti zitapatikana kwa siku tano za kazi mara baada ya mteja kuiomba Makao Makuu Dar es Salaam na Zanzibar, pia Wateja wa mikoani watapata Pasipoti hizo kwa siku zisizozidi kumi. Uzinduzi huo umefanyika Makao Makuu ya Idara hiyo, Kurasini jijini Dar es Salaam. Watatu kushoto (upande wa pili) ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Idara hiyo, Victoria Lembeli.

  Na Humphrey Shao, Globu ya jamii.

  Idara ya uhamiaji imezindua mkataba wa huduma kwa wateja ambao utawawezesha kutoa hati ya kusafiria ndani ya siku tano bila kuchelewa.

  Akizungumza na wahabari katika makao makuu ya idara ya uhamiaji jijini Dar es Salaam,Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya amesema kuwa kama watumishi wa idara hiyo watashindwa kukidhi vigezo hivyo walivyojiwekea wananchi wana haki ya kulalamika na kutoa taarifa katika ngazi za juu.

  “Tumejiwekea viwango kuwa wakati wote mtu kama ataomba pasipoti apewe ndani ya sikutano mkataba huo umeonyesha wajibu wa mtoaji huduma  kumuhudumia mteja vile inavyotakikana” amesema Balozi Yahya.

  Ameongeza kuwa kuanzia sasa mteja ni mfalme pindi anapofika katika idara hiyo kuhitaji hati ya kusafiria na sasa ana fursa ya kulalamika pindi huduma atakayopata kuwa aitakuwa na radha.Amemaliza kusema kuwa kuwa kuanzia sasa watu wote watapewa huduma kwa heshima na taadhima kutoka idara ya uhamiaji.
  Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Mkataba wa Huduma kwa Mteja wa Idara ya Uhamiaji. Mkataba huo ambao unalenga kuimarisha huduma mbalimbali za Idara hiyo pia umeelekeza kuanzia sasa Hati za Kusafiria (Pasipoti) zitatolewa kwa siku tano za kazi kwa watakaoomba Makao Makuu Dar es Salaam na Zanzibar, pia Wateja wa mikoani watapata Pasipoti hizo kwa siku zisizozidi kumi. Wapili kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Idara hiyo, Victoria Lembeli. Uzinduzi huo umefanyika Makao Makuu ya Idara hiyo, Kurasini jijini Dar es Salaam
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya akionesha machapisho ya mkataba wa huduma kwa wateja kati ya Idara ya Uhamiaji na wananchi.
  Baadhi ya wananchi waliofika katika halfa ya uzinduzi wa mkataba huo.
  . Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya katikati akiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa idara ya uhamiaji.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya akisalimiana na watendaji wa uhamiaji.

  0 0

  Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Rogers Kibula akimuelezea maendeleo ya wagonjwa wa Moyo waliolazwa katika wodi namba tatu Mohammed Barhoumi ambaye ni Makamu Rais wa Kampuni ya Medtronic kutoka nchini Lebanon ambao ni watengenezaji wa vifaa tiba vya magonjwa ya Moyo alipotembea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuangalia huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. Mohamed Janabi.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiongea jambo na Mohammed Barhoumi ambaye ni Makamu Rais wa Kampuni ya Medtronic kutoka nchini Lebanon ambao ni watengenezaji wa vifaa tiba vya magonjwa ya Moyo alipotembea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuangalia huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimuonyesha jengo la Maabara Kuu ya Taifa (halipo pichani) Mohammed Barhoumi ambaye ni Makamu Rais wa Kampuni ya Medtronic kutoka nchini Lebanon ambao ni watengenezaji wa vifaa tiba vya magonjwa ya moyo. Kushoto ni Divin Akaba na kulia ni Stranix William wote kutoka Medtronic.
  Daktari Bingwa ya upasuaji wa magonjwa ya Moyo kwa watoto Godwin Sharau akimueleza jinsi wanavyofanya upasuaji wa moyo kwa watoto Mohammed Barhoumi ambaye ni Makamu Rais wa Kampuni ya Medtronic kutoka nchini Lebanon ambao ni watengenezaji wa vifaa tiba vya magonjwa ya moyo. Kulia ni Daktari wa Upasuaji wa Mgonjwa ya Moyo Hussein Hassanali.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiagana na Mohammed Barhoumi ambaye ni Makamu Rais wa Kampuni ya Medtronic kutoka nchini Lebanon ambao ni watengenezaji wa vifaa tiba vya magonjwa ya moyo mara baada ya kumaliza kutembelea Taasisi hiyo leo na kujionea kazi mbalimbali wanazozifanya. 


  Picha na Anna Nkinda – JKCI

  0 0

  Serikali imezindua mwongozo wa mpango na usanifu wa ujenzi wa barabara zinazopitisha magari machache kwa lengo la kutoa maelekezo na kuwawezesha wahandisi wanaofanya usanifu wa barabara hizo kutumia gharama nafuu za ujenzi.

  Akizungumza katika uzinduzi huo leo jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga amesema kuwa mwongozo huu utakuwa tiba na kuwezesha Serikali kujenga barabara nyingi na gharama nafuu.

  “Ujenzi na ukarabati ya barabara zinazopitisha magari chini ya 300 kwa siku utakuwa wa gharama nafuu, kama tutatumia mwongozo huu kwani utasaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazokabili barabara nyingi hususan za vijijini”, amesema Katibu Mkuu.

  Amewataka wahandisi na Mafundi ujenzi kutumia mwongozo huo katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuweza kusaidia kazi na miradi mbalimbali ya barabara kuweza kufanyika kwa viwango vilivyo bora na gharama nafuu.“Hakikisheni wahandisi na Mafundi ujenzi mnafuata mwongozo huu ipasavyo na kuanzia sasa uwe dira kwenu katika kazi zenu za kila siku”, amesisitiza Eng. Nyamhanga.

  Ameongeza kuwa kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanywa Serikali imegundua uhitaji mkubwa katika mtandao wa barabara nchini ili kusaidia maendeleo ya kila mwananchi mijini na vijijini.Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Barabara katika Wizara hiyo Eng. Ven Ndyamukama amesema kuwa mwongozo huo unafananua namna ujenzi wa barabara hizo unavyokuwa ikiwemo kujenga kulingana na idadi ya magari yanayopita.

  Ameongeza kuwa Mwongozo huo unaelekeza kutumia rasilimali chache zilizopo na kuhakikisha masuala ya mazingira katika maeneo yanayojengwa barabara hizo yatazingatiwa.
  Mkurugenzi wa Barabara, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Ven Ndyamukama, akitoa hotuba ya utangulizi katika uzinduzi wa Mwongozo wa ujenzi wa Barabara zinazotumiwa na magari machache, uliozinduliwa leo jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamuhanga, akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa Mwongozo wa ujenzi wa Barabara zinazotumiwa na magari machache, uliozinduliwa leo jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamuhanga (kushoto), akikata utepe kwenye kitabu cha Mwongozo wa ujenzi wa Barabara zinazotumiwa na magari machache, mara baada ya kuuzindua leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meneja wa AFCAP Kanda ya Mashariki na Kati mwa Afrika, Eng. Nkulule Kaleta.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamuhanga (kushoto), akimkabidhi nakala ya kitabu cha Mwongozo wa Ujenzi wa Barabara zinazotumiwa na magari machache, mmoja wa wadau waliohudhuria uzinduzi huo, leo jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamuhanga (wa nne kutoka kulia waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe waliohudhuria uzinduzi wa Mwongozo wa ujenzi wa Barabara zinazotumiwa na magari machache hapa nchini.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

  0 0

  Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma

  Nchi za Afrika Mashariki zimekubaliana kuwa Makao Makuu ya Lugha ya Kiswahili kuwa Tanzania ambayo yatakuwepo Zanzibar.

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Nnauye ameyasema hayo leo Bungeni, Mjini Dodoma alipokuwa akitoa ufafanuzi juu ya jitihada mbalimbali ambazo Tanzania inazichukua katika kukuza Lugha ya Kiswahili katika ngazi ya Kimataifa.

  Nape amesema kuwa maamuzi hayo ya kuifanya Tanzania kuwa Makao Makuu ya Lugha ya Kiswahili yametokana na Tanzania kuzalisha walimu wengi wa Kiswahili ambao wanatumika katika ngazi mbalimbali za elimu ndani na nje ya nchi.

  Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Anastazia Wambura amesema kuwa Wizara hiyo kwa sasa inachukua hatua mbalimbali kuhakikisha kuwa vyombo vya habari vinakuwa mawakala wa kulinda Lugha ya Kiswahili ambapo Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) kwa kushirikiana na wadau wa Kiswahili limeendelea kuendesha semina, warsha, makongamano na kutoa elimu inayohusu matumizi fasaha ya Lugha ya Kiswahili.

  Aidha, aliendelea kwa kusema kuwa Waandishi wa Habari wanalo jukumu kubwa la kuhakikisha Lugha hiyo inaendelezwa ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuzingatia matumizi sahihi ya Lugha hiyo katika majukumu yao ya kila siku.

  “Kutumia zana kama vile Kamusi na vitabu vya miongozo ya uandishi pamoja na kuhudhuria makongamano ya Kitaifa na ya Kimataifa ya Lugha ya Kiswahili inasaidia kuongeza ujuzi na uweledi wa Lugha ya Kiswahili, kujua istilahi za kisayansi na kiteknolojia na hivyo kuandika na kutangaza kazi bora na zenye maudhui lengwa kwa jamii na kuepuka upotoshaji wa maneno ya Kiswahili usio wa lazima,” alifafanua Anastazia Wambura.

  Hata hivyo Wizara hiyo iko katika maandalizi ya Sera ya Lugha ambayo itabainisha majukumu ya Vyombo vya Habari katika matumizi na uendelezaji wa Lugha ya Kiswahili.

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiongea katika uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa dhamana ya Hifadhi ya Mazingira. Bodi hiyo iko chini ya Uenyekiti wa Bw Ali A. Mafuruki. Uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiwakaribisha wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa dhamana ya Hifadhi ya Mazingira (hawapo pichani), kulia ni Bw. Ali Mufuruki Mwenyekiti wa Bodi.
  Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Ngosi Mwihava (kushoto) akiwa na Bw. Ali Mufuruki Mwenyekiti wa Bodi, wakati wa halfa ya uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa dhamana ya Hifadhi ya Maizngira jiini Dar es Salaam.
  Sehemu ya Wajumbe wa Bodi (mstari wa mbele) wakifuatilia maelezo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba katika hafla ya uzinduzi wa Bodi na Mfuko wa Dhamana ya Mazingira.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa dhamana ya Hifadhi ya Mazingira, mara baada ya kuizindua hii leo, Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Mheshimiwa Rais, Dkt. John Magufuli hajawahi kutangaza ama kutoa kauli ya kufutwa kwa vyama vya siasa nchini.

  Ametoa kauli hiyo leo (Februari, 2, 2017) Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Freeman Mbowe  katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu.

  Katika swali lake Mheshimiwa Mbowe alisema Rais Dkt.  Magufuli alinukuliwa akisema atahakikisha anafuta vyama vyama vya upinzani na ifikapo mwaka 2020 hakuna upinzani nchini.

  Pia Mheshimiwa Mbowe alitaka kujua nini kauli ya Serikali kuhusu kunyimwa dhamana kwa Mbunge wa Arusha Mjini, Mheshimiwa Godbless Lema ambaye anashikiliwa kwa muda miezi mitatu.

  Mbali na Mheshimiwa Lema, pia kiongozi huyo alitaka kujua kuhusiana na kufungwa kwa Mbunge wa Kilombelo, Mheshimiwa Peter Lijualikali pamoja na madiwani sita wa chama hicho ambao wamefungwa na viongozi wengine 215 wanakabiliwa na kesi mbalimbali.

  “Kwanza nataka nikanushe kwamba Mheshimiwa Rais hajawahi kutangaza kuvifuta vyama vya upinzani. Pia Watanzania wote wanajua nchi hii inaongozwa kwa sheria, kanuni na taratibu i,” amesema Waziri Mkuu.

  Waziri Mkuu ameongeza kuwa “tunajua katika kuendesha nchi tunaendesha kwa mihimili mitatu ipo Serikali, Mahakama na Bunge na hakuna mhimili unaoweza kuuingilia mhimili mwingine,”.

  “Pia Watanzania wote wanajua kwamba jambo lolote ambalo lipo Mahakamani haliwezi kuzungumzwa mahali pengine popote, hivyo siwezi kutumia nafasi hii kuzungumzia mambo yote yanayoendelea chini ya sheria na yaliyo mahakamani,” amesema.
  Wakati huo huo; Waziri Mkuu amewahakikishia Watanzania kwamba suala la upungufu wa sukari halitatokea nchini kwa sababu viwanda vya ndani vinaendelea kuzalisha na hadi mwishoni mwa Januari vilifikia asilimia 86 ya uzalishaji.

  “Hadi kufikia mwishoni mwa msimu wa uzalishaji ambao ni mwezi Machi, tunaweza kuwa tumefikia malengo na kama itajitokeza upungufu Serikali itatafuta namna nzuri ya kupata sukari kwa kushirikiana na wenye viwanda nchini,” amesema.

  Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Mbunge wa Mvomero, Mheshimiwa Suleiman Sadiq aliyetaka kujua hali ya sukari ilivyo nchini kwa sasa na hatua gani zinazochukuliwa na Serikali ili kunusuru hali ya uhaba wa sukari isijitokeze.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  S. L. P. 980,
  DODOMA.
  ALHAMIS, FEBRUARI 02, 2017

  0 0

  JANET
  Na. Immaculate Makilika- MAELEZO
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda  Bi. Janeth Mayanja amemvua madaraka  Mwalimu Mkuu  wa Shule ya Msingi Bunda B, Bw. Laurent Agustino kwa tuhuma za kushiriki kusaidia mwanafunzi mmoja kufanya udanganyifu  katika mtihani wa darasa la nne.
  Mwalimu huyo anatuhumiwa kumruhusu  mwanafunzi wa darasa la tano kufanyia mtihani wa mwanafunzi wa darasa nne kwa lengo la kumsaidia  mwanafunzi huyo  ambaye hajui kusoma wala kuandika ili aweze kufaulu.
  Mkurugenzi huyo ametoa kauli hiyo leo wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari hizi.
  Kufuatia tukio hilo Bi. Janeth  ametoa onyo kwa walimu wote wa shule zilizofanya vibaya  na kuwataka kufanya vizuri katika matokeo ya mitihani kwa mwaka 2017 na kuahidi kuwavua madaraka walimu wa shule zitakazofanya vibaya.
  Aidha, Mkurugenzi huyo wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda amewataka walimu wakuu, waratibu  na walimu wote kutekeleza kutekeleza majukumu yao kulingana na sheria na kanun9 a utumishi wa Umma.
  Mkurugenzi huyo amezizawadia   shule kumi  za Msingi  zilizofanya vizuri katika mtihani wa kumaliza Darasa la saba kwa mwaka 2016 kwa ajili ya kuboresha kiwango cha elimu katika eneo hilo.
  Utaratibu huo ulenga kutoa  hamasa kwa wanafunzi na walimu wilayani humo na kuongeza juhudi katika kufundisha na kujifunza kwa ajili ya kuongeza kiwango cha ufaulu katika Halmashauri hiyo.
  Amezitaja shule  zilizoingia kumi bora ni pamoja na Olympus, Daystar, St. Paul, Mzuma, Kabarimu B, Bigutu, Bukore, Kung’ombe, Kabarimu A na Bitaraguru ambazo zote zimetunukiwa vyeti vya kutambua mchango na juhudi wanazofanya.
  Mayanja alisema kuwa kati ya shule hizo  nne ni shule  binafsi  na sita za Serikali ambazo  ambapo pamoja na zimekabidhiwa  hundi za fedha.

  0 0
older | 1 | .... | 1125 | 1126 | (Page 1127) | 1128 | 1129 | .... | 1898 | newer