Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1124 | 1125 | (Page 1126) | 1127 | 1128 | .... | 1897 | newer

  0 0  TAARIFA KWA UMMA

  MAADHIMISHO YA SIKU YA ARDHIOEVU DUNIANI TAREHE 2 FEBRUARI 2017

  Kesho tarehe 2 Februari, 2017 ni maadhimisho ya siku ya Ardhioevu Duniani. Siku hii inaadhimishwa duniani kote kwa kutoa elimu na kuwakumbusha watu wote kuhusu uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali za ardhioevu.
  Ardhioevu ni maeneo ya ardhi yaliyopo kandokando na ndani ya Chemchem, Mito, Maziwa na mwambao wa bahari wenye kina cha maji yasiyozidi mita sita wakati wa kupwa. Ardhioevu pia hujumuisha Madimbwi, Mabwawa, Tingatinga na sehemu zote yanapokusanyika maji kipindi kirefu cha mwaka.
  Tanzania hujumuika na nchi nyingine wanachama wa Mkataba wa “Ramsar” kuadhimisha siku ya ardhioevu duniani Februari 2 kila mwaka. Ujumbe wa mwaka huu wa Siku ya Ardioevu ni: "Ardhioevu Hupunguza Athari za Majanga” (Wetlands for Disaster Risk Reduction)". 
  Tafsiri ya kauli mbiu hii ni kwamba, Ardhioevu huzuia majanga ya mafuriko yanayoweza kutokea katika pwani za bahari, hupunguza athari za kiafya zinazoweza kujitokeza kutokana na madini hatarishi kama Zebaki, hupunguza uwezekano wa kutokea kwa baa la njaa kwa kuwa maeneo okozi wakati wa kiangazi kama vyanzo vya maji na chakula kwa binadamu na wanyama. 
  Ardhioevu pia ni maeneo yenye uzalishaji mkubwa wa chakula kama vile mpunga na mbogamboga na chanzo cha maji yanayotumika kwenye kilimo cha umwagiliaji nchini. Arhioevu pia ni sekta endeshi ya uchumi wa nchi kwa kuwa ni chanzo cha maji yanayotumika kwenye kilimo, viwandani pamoja na uzalishaji wa umeme wa maji kwa gharama ndogo.

  Inakadiriwa kuwa asilimia 10 ya ardhi ya Tanzania ni ardhioevu ambayo ni muhimu kwa bioanwai, uchumi, shughuli za kijamii na kiikolojia. Maeneo haya ni makazi muhimu ya aina mbalimbali za viumbe hai wakiwemo samaki, viboko, mamba, ndege na viumbe wengine wasio na uti wa mgongo. Katika ikolojia ya ardhioevu tunapata bioanwai kubwa kuliko eneo lingine lolote duniani. Maeneo haya ni vyanzo vya maji kwa kipindi chote cha mwaka, huhifadhi maji na kupunguza mafuriko kwa maeneo ambayo ni hatarishi.
  Maeneo haya ni muhimu kwa kuchuja kemikali zilizopo kwenye maji yaliyochafuka hususani kutoka kwenye kilimo, viwanda na matumizi ya nyumbani. Madini yanayochujwa kwa wingi  na ardhioevu ni pamoja na madini ya Nitrojen, Phosphorus na madini ya Aluminium na Chuma. Madini ya Nitrojen na Phosphorus husababisha kupungua kwa hewa muhimu ya oxygen kwa viumbe wa majini.
  Hii hutokana na kumea kwa wingi kwa mimea aina ya mwani (Algae) ambayo ikiota kwa wingi kwenye uso wa maji husababisha ukijani unaozuia mwanga wa jua kufika kwenye kina cha maji na kuzuia “photosynthesis” kutokea. Hewa ya “oxygen” itapungua majini  na viumbe maji kama samaki hufa kwa wingi.
   Ardhioevu pia huzuia mmomonyoko wa udongo kwenye fukwe/kingo za mito na mifereji unaoweza kusababishwa na mawimbi ya bahari. Ardhioevu pia ni vyanzo vya umeme, na huchangia huduma ya usafirishaji na ni maeneo mazuri kwa ajili ya kubarizi.
   Maeneo ya ardhioevu yanasimamiwa na mkataba wa “Ramsar” ambayo Tanzania imeweka saini, Sheria ya Usimamizi wa Wanyamapori na Mazingira yake, na ndio msingi wa usimamizi na matumizi endelevu ya ardhioevu duniani. Mkataba huu ulisainiwa na nchi wanachama kwa mara ya kwanza katika mji wa Ramsar nchini Iran mwaka 1972. 
  Lengo la kuanzishwa kwa  mkataba huu ni kuhifadhi Ndege maji kwa mfano Korongo Taji, Korongo Nyangumi Bungunusu, Herroe Mkubwa, Heroe Mdogo. Ndege hawa ni muhimu kwa utalii na uhifadhi wa mazingira na mwingiliano wa bianuwai. Pia ni dalili ya afya ya mazingira. Tanzania iliweka saini makubaliano haya mwaka 2000.
   Tanzania kuna maeneo ya Ardhioevu  manne ambayo ni; Ziwa Natron yenye umuhimu wa kuhifadhi ndege aina ya Heroe Wadogo-(Lesser flamingo), Malagarasi Muyovosi  ina umuhimu wa kuhifadhi ndegemaji aina ya  Korongo Domkiatu (Shoebill Stork), Bonde la Mto Kilombero yenye umuhimu wa uhifadhi wa Puku na Rufiji mafia Kilwa uhifadhi wa Mikoko na Mazao ya Baharini.
  Serikali imeendelea kuimarisha usimamizi wa ardhioevu nchini. Hata hivyo, ardhioevu nyingi nchini zinaharibika na zingine kutoweka kutokana na ongezeko la shughuli za kimaendeleo zisizo endelevu kama vile ujenzi kwenye vyanzo vya maji, ufugaji holela, kilimo kisichozingatia kanuni za kilimo cha kisasa na kukata miti ovyo. 

  Athari zingine zinazotokana na matumizi mabaya ya ardhioevu ni pamoja na vifo vya mimea maji na wanyama wanaotegemea maji kuishi na kunywa kutokana na matumizi yasiyoendelevu, ukosefu wa mapato kwa jamii kutokana na kuathiriwa kwa sekta za uvuvi, utalii, kilimo cha umwagiliaji na ufugaji. Binadamu, mimea na wanyama wakiwemo samaki pia huathirika kwa kukosa maji.

  Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania inawakumbusha wananchi kuwa maeneo ya ardhioevu ndio vyanzo vya maji ambayo binadamu wanatumia kila siku. Mimea na Wanyama pia hutegemea maji kutoka kwenye ardhioevu. Mamlaka inatoa wito kwa wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya Ardhioevu, kushirikiana na Serikali na Taasisi zake pamoja na Taasisi zisizo za Kiserikali katika kuyatunza maeneo haya. 
  Mamlaka inatoa wito kwa  wananchi kutekeleza sheria mbalimbali za uhifadhi ikiwemo Sheria ya Uhifadhi Wanyamapori Namba 5 ya mwaka 2009, Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 na Sheria nyingine za kisekta kama ya Maji na Uvuvi na kuwahimiza wale wote wanaoishi kwenye maeneo ya ardhioevu na hifadhi kuhama bila shuruti.


           Martin T. Loibooki
  KAIMU MKURUGENZI MKUU-TAWA
  1 Februari 2017  0 0

  Mkuu wa wilaya Kahama Fadhili Nkurlu akipanda mti kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya upandaji miti milioni moja na laki sita itakayopandwa katika maeneneo mbalimbali wilayani kahama kwa lengo la kutunza mazingira pamoja na kuufanya mji wa Kahama upendeze.
  Mkuu wa wilaya kahama Fadhili Nkurlu akimwagia maji mti alioupanda wakati alipozindua kampeni ya upandaji miti
  Mkuu wa polisi wilaya ya Kahama Mussa Mchenya akishiriki pia upandaji miti.
  Afisa Usalama wa Wilaya ya Kahama Aretus Lyimo akishiriki upandaji miti wakati wa zoezi la uzindunzi wa upandaji miti milioni moja na laki sita.
  Katibu Tawala wa Wilaya Kahama Timothy Ndanya akishiriki pia kupanda miti.
  Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo akifurahia wakati alipokuwa akipanda mti katika eneo la mgodi wa Buzwagi.
  Meneja raslimali watu wa Mgodi wa Buzwagi Solomon Rwangabwoba akifurahia kupanda mti wakati wa uzindunzi wa kampeni ya upandaji miti milioni moja na laki sita itakayoendeshwa na mgodi wa Buzwagi.
  ******************************************************
  PICHA ZA MAAFISA WAKUU WA KAMPUNI YA ACACIA MINING PLC WAKIPANDA MITI WAKATI WALIPOFANYA ZIARA KATIKA MGODI WA BUZWAGI.
  Afisa Mkuu Mwendeshaji wa Kampuni ya Acacia Mark Marcombe akishiriki zoezi la upandaji miti milioni moja na laki sita miti ambayo inatajwa kuwa itasaidia katika kuipendezesha wilaya ya Kahama.
  Afisa Mkuu wa Idara ya Raslimali watu wa Kampuni ya Acacia Peter Gereta akishiriki zoezi la upandaji miti.
  Makamu wa Rais wa Kampuni ya Acacia anaeshughulikia Masuala ya Kampuni (Corporate Affairs) Deo Mwanyika akishiriki pia kupata mti.
  Mh. Salome Makamba MB-(Viti Maalumu) akishiriki pia upandaji miti baada ya kupita karibu na eneo ambapo zoezi la upandaji miti lilikuwa likifanyika na akaona ni vyema na yeye akashiri katika kuunga mkono jitihada za Mgodi wa Buzwagi katika kupanda miti itakayosaidia katika utunzaji wa mazingira wa wilaya ya Kahama na Taifa kwa ujumla.
  Afisa Mkuu wa Idara ya Utafiti wa madini (Exploration) Peter Spora akifurahia wakati alipokuwa akipanda mti katika eneo la Mgodi wa Buzwagi.
  Taarifa kwa vyombo vya Habari:
  Wakia Moja Mti Mmoja - Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi wajipanga kupanda miti milioni 1.6
  Kahama: 31/01/2017. Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi leo umezindua kampeni ya upandaji miti katika Wilaya ya Kahama ikiwa na lengo la kupanda mti kwa kila wakia ya dhahabu ambayo imechimbwa kwenye mgodi wa Buzwagi, ambapo miti zaidi ya milioni moja na laki sita inatarajiwa kupandwa katika kipindi cha miaka miwili.
  Akizindua kampeni hiyo Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu ameupongeza uongozi wa Mgodi wa Buzwagi kwa hatua hiyo na kusema ni ya kizalendo kwa kuwa itasaidia katika kuboresha hali ya mazingira ya wilaya ya Kahama.
  “Jukumu la upandaji miti na kuhakikisha mazingira yetu yanatunzwa ni letu sote, Wenzetu wa Buzwagi wameanza kuonyesha jitihada kwa kupanda miti milioni moja na laki sita, hivyo sote kama Jamii hatuna budi kuwaunga mkono kwa kuhakikisha kila mmoja wetu katika eneo lake anapanda miti na kuifanya wilaya yetu ya Kahama izidi kupendeza”Alisema Nkurlu.
  Akizungumzia Malengo ya Kampeni hiyo Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo amesema kama wadau muhimu wa mazingira wanalojukumu la moja kwa moja kuhakikisha shughuli za utunzaji wa mazingira zinakuwa ni sehemu ya maisha ya kila siku.
  Na kupitia mipango ya muda mrefu uongozi umejiwekea lengo la kupanda mti mmoja kwa kila wakia moja ya dhahabu itakayokuwa ikizalishwa katika kipindi chote cha uhai wa Mgodi wa Buzwagi ambapo inakisiwa mpaka shughuli za uzalishaji zitakapositishwa takribani wakia milioni moja na laki sita zitakuwa zimezalishwa.
  “Leo tunazindua awamu ya kwanza ya kampeni hii ambayo itahusisha upandaji wa miti laki tano, ambapo mpaka sasa miti elfu ishirini imekwisha pandwa na tunatarajia mpaka mwisho wa mwaka huu awamu ya kwanza ya miti laki tano itakuwa imepandwa” Alisema Mwaipopo. “
  “Kwa kupanda miti hii, tunakusudia kuwa sehemu muhimu ya wadau wa mazingira wenye lengo la kuipendezesha wilaya yetu ya Kahama, pia kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na kuonyesha utayari wetu kama Kampuni katika kurejesha katika hali ya awali ya mazingira ya eneo la Mgodi itakapofikia wakati wa kuufunga. Aliongeza Mwaipopo.
  Miti aina mbalimbali inatarajiwa kupandwa katika zoezi hili huku mti maarufu wa “Acacia” unaobeba jina la Kampuni mama ya Acacia Mining Plc inayomiliki Mgodi wa Buzwagi ikiwa ni sehemu ya miti itakayopandwa,
  Huku zaidi ya shilingi milioni mia sita na arobaini na tano zikitarajiwa kutumika katika awamu ya kwanza ya upandaji miti laki tano.
  Katika hatua nyingine maafisa wakuu wa Kampuni ya Acacia kutoka ofisi za Acacia Mining Plc London pamoja na Dar es salaam walishiriki pia katika zoezi la upandaji miti katika eneo la Mgodi wa Buzwagi wakati walipofanya ziara ya kikazi mgodini hapo.
  “Wakia Moja Mti Mmoja”
  Imetolewa na Idara ya Mawasiliano Mgodi wa Buzwagi
  Simu  +255 22 2164 200

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali wakati alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa zamani wa baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja leo katika semina ya Siku moja kuhusu Umuhimu wa Takwimu na matumizi yake.
  Baadhi ya washiriki wa Semina ya Siku moja kuhusu Umuhimu wa Takwimu na matumizi yake akimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipoifungua semina hiyo leo iliyofanyika katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja.
  Viongozi wa serikali walioshiriki katika Semina ya Siku moja kuhusu Umuhimu wa Takwimu na matumizi yake akimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipoifungua semina hiyo leo iliyofanyika katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akifungua semina ya siku moja kuhusu Umuhimu wa Takwimu na Utekelezaji wake kwa Viongozi mbali mbali katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja leo,(kushoto) Makamo wa Rais Balozi Seif Ali Iddi na katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Kiongozi Dkt.Abduhamid yahya Mzee (kulia).
  Mtakwimu Mkuu wa Serikali Bibi Mayasa Mahfoudh Mwinyi alipokuwa akitoa Muhtasari wa Majukumu ya Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali katika Upatikanaji wa Takwimu na Utekelezaji wake katika semina ya viongozi iliyofanyika leo katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mjini Unguja.
  Viongozi wa serikali walioshiriki katika Semina ya Siku moja kuhusu Umuhimu wa Takwimu na matumizi yake akimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipoifungua semina hiyo leo iliyofanyika katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja.
  waziri wa Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi Mhe,Hamad Rashid Mohamed alipokuwa akitoa mchango wake katika semina ya siku moja kuhusu Umuhimu wa Takwimu na Utekelezaji wake kwa Viongozi mbali mbali wa Serikali iliyofanyika leo katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi Mmoja. Picha na Ikulu, Zanzibar.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan va viongozi wengine mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Addis Ababa, Ethiopia, alikohudhuria Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika leo February 1, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akishuka kwenye ndege katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Addis Ababa, Ethiopia, alikohudhuria Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika leo February 1, 2017. Mbele yake ni Mkuu wa Itifaki Balozi Grace Martin.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilsalimiana na baadhi ya wafayanyazi katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam alipowasili akitokea Addis Ababa, Ethiopia, alikohudhuria Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika leo February 1, 2017.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipungia wananchi mikono alipowasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Addis Ababa, Ethiopia, alikohudhuria Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika leo February 1, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Inspecta Jenerali wa Polisi IGP Ernest Mangu baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Addis Ababa, Ethiopia, alikohudhuria Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika leo February 1, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt Juma Malewa baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitokea Addis Ababa, Ethiopia, alikohudhuria Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika leo February 1, 2017. PICHA NA IKULU.


  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma jFebruari 1, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0  0 0  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akifungua mafunzo ya siku tatu ya kanuni na sheria za manunuzi kwa wafanyakazi wa Taasisi hiyo yanayotolewa na wataalamu kutoka Bodi ya Ununuzi na Ugavi (PSPTB). Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo na kuzifahamu sheria za manunuzi .

  Hasa utaratibu katika ununuzi wa Umma kwa kutumia sheria ya ununuzi wa Umma na kanuni zake ikiwa ni pamoja na mabadiliko mbalimbali ya sheria ya mwaka 2016
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akifafanua jambo wakati akifungua mafunzo ya siku tatu ya kanuni na sheria za manunuzi kwa wafanyakazi wa Taasisi hiyo yanayotolewa na wataalamu kutoka Bodi ya Ununuzi na Ugavi (PSPTB).
  Washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya kanuni na sheria za manunuzi kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifuatilia mafuzo yaliyokuwa yanatolewa na wataalamu kutoka Bodi ya Usimamizi na Ugavi (PSPTB). Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo na kuzifahamu sheria za manunuzi .
  Washiriki wa mafunzo ya siku tatu ya kanuni na sheria za manunuzi kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifuatilia mafuzo yaliyokuwa yanatolewa na wataalamu kutoka Bodi ya Usimamizi na Ugavi (PSPTB). Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo na kuzifahamu sheria za manunuzi .
  Amosi Kasinza Afisa Mkuu wa Utafiti na Ushauri PSPTB akitoa mada katika mafunzo hayo yaliyofanyika leo katika Taasisi ya Jakaya Kikwete jijini Dar es salaam.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi ( wa kwanza kulia) akikagua gwaride wakati wa kufunga mafunzo ya jeshi Usu kwa wahifadhi wa wanyamapori 103 kutoka TANAPA, TAWA na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro yaliyofanyika jana katika kituo cha mafunzo cha Mlele mkoani Katavi. Wengine ni Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa, Rachel Kasanda ( wa pili kushoto) pamoja na viongozi wa taasisi.

  Paredi ikipita mbele ya mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi ( hayupo pichani) wakati wa kufunga mafunzo ya jeshi Usu kwa wahifadhi wa wanyamapori 103 kutoka TANAPA, TAWA na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro yaliyofanyika jana katika kituo cha mafunzo cha Mlele mkoani Katavi.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi ( wa katikati) akiwa amesimama kiukakamu wakati Paredi ikipita mbele yake( haipo pichani ) kabla kufunga mafunzo ya jeshi Usu kwa wahifadhi wa wanyamapori 103 kutoka TANAPA, TAWA na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro yaliyofanyika jana katika kituo cha mafunzo cha Mlele mkoani Katavi.

  Baadhi ya wahitimu wa mafunzo wakiwa wamesimama kikakamavu wakati wakila viapo vya utii na nidhamu katika utendaji wa kazi.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi akizungumza kwenye mkutano uliofanyika jana mjini Morogoro ulioandaliwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) walipokutana na Wahifadhi Wakuu wa Mapori ya Akiba nchini kwa lengo la kuweka mikakati ya kukabiliana na tatizo la ujangili.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi akizungumza wahifadhi wa wanyamapori 103 kutoka TANAPA, TAWA na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kabla ya kufunga mafunzo ya jeshi Usu yaliyofanyika jana katika kituo cha mafunzo cha Mlele mkoani Katavi

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi ( wa kwanza kulia) akiangalia sehemu ambapo wahitimu wa mafunzo walilenga shabaha kwa kutumia risasi ya moto kwenye picha inayoonekana wakati wa kufunga mafunzo ya wahifadhi wa wanyamapori 103 kutoka TANAPA, TAWA na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro yaliyofanyika jana katika kituo cha mafunzo cha Mlele mkoani Katavi.
  Wengine ni Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa, Rachel Kasanda ( wa pili kushoto) pamoja
  na viongozi wa taasisi.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi ( wa kwanza kushoto) mara baada kufunga mafunzo ya jeshi Usu kwa wahifadhi wa wanyamapori 103 kutoka TANAPA, TAWA na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro yaliyofanyika jana katika kituo cha mafunzo cha Mlele mkoani Katavi. Wengine ni Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa, Rachel Kasanda ( wa pili kushoto) Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu TANAPA, Mtango Mtaiko ( wa tatu kushoto) pamoja na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TAWA, David Kanyatta ( wa pili kulia) pamoja na Naibu Mhifadhi Mkuu Ngorongoro, Dkt. Maulusi Msuha ( wa kwanza kulia).
   
  =======  =======  =========

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi, amesema hatamvumilia mtumishi yeyote atayejihusisha na vitendo vya rushwa kuwa ni lazima ataondolewa mara moja ili asiendelee kuchafua taswira ya Wizara.

  Alitoa rai hiyo jana wakati akifunga mafunzo ya jeshi Usu kwa wahifadhi wa wanyamapori 103 kutoka Mamlaka ya Hifadhi Tanzania (TANAPA), Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori ( TAWA) na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ( NCAA).

  Alisema Wizara kwa sasa inabadili mfumo wa kiraia na kuendesha kwa mfumo wa kijeshi hivyo mtumishi yeyote asiyejihusisha na vitendo viovu vya namna yeyote Yule hatasalimika.

  Wakati huo huo , Maj. Gen. Gaudence Milanzi alifungua mafunzo ya ukakamavu kwa maafisa wanyamapori wa daraja la pili kutoka TAWA yatakayochukua muda wa wiki tano lengo likiwa ni kuwandaa watumishi wa taasisi hiyo katika kuboresha mbinu za kupambana na majangili.

  Akizungumza jana na wahitimu hao kabla ya kufunga mafunzo hayo katika kituo cha Mafunzo cha Mlele mkoani Katavi ,Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Milanzi aliwataka wahifadhi hao wakaoneshe kile walichojifunza kwa kwa kujenga mahusiano mazuri na wanavijiji wanaozunguka hifadhi nchini baadala ya kujenga uadui.

  Aliwasihi wahitimu hao kutumia silaha kwa weledi pale inapobidi hasa inapohitajika kunusuru maisha ya watu na sio kuua.

  Aidha, Milanzi aliwaagiza wakuu na viongozi wa taasisi zote zilizo chini ya Wizara wahakikishe wanashiriki katika mafunzo hayo kwa kuwa Wizara inatoka kwenye mfumo wa kiraia na kuelekea kwenye mfumo wa kijeshi katika utendaji wa shughuli za uhifadhi nchini.

  Akitoa maelezo ya awali kabla ya hotuba ya Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TAWA, David Kanyatta aliwataka wahifadhi waliopewa mafunzo hayo wakajitume kwa kufanya kazi kwa bidii katika vituo vyao vya kazi ili kuonesha tija kwa taifa katika uhifadhi.

  Kabla ya kuwahutubia wahitimu hao, Katibu Mkuu Milanzia alioneshwa mbinu mbalimbali kwa vitendo walizojifunza katika kupambana majangili ambao wamekuwa wakitumia silaha nzito wakati wakifanya ujangili.


  0 0

   
  Mwenyekiti wa Kundi la Wabunge wa Uzazi Salama Mh. Jenista Mhagama (katikati) akifungua mkutano kati ya Muungano wa Utepe Mweupe (WRATZ) na Wabunge wa uzazi salamaMeneja Mradi wa Muungano wa Utepe Mweupe (WRATZ), Bi. Sizarina Hamisi (mbele) akiwasilisha mada katika mkutano kati ya WRATZ na kundi la Wabunge wa uzazi salama mjini Dodoma. Meneja Mradi wa Muungano wa Utepe Mweupe (WRATZ), Bi. Sizarina Hamisi (mbele) akiwasilisha mada katika mkutano kati ya WRATZ na kundi la Wabunge wa uzazi salama mjini DodomaMkutano kati ya Muungano wa Utepe Mweupe (WRATZ) na Wabunge wa uzazi salama ukiendelea. Mkutano kati ya Muungano wa Utepe Mweupe (WRATZ) na Wabunge wa uzazi salama ukiendelea.

  WABUNGE wa kundi la uzazi salama wametakiwa kuhamasisha na kutetea Bajeti ya Afya ya Uzazi na Mtoto ili ipewe kipaumbele katika mipango ya Halmashauri kwa mwaka 2017/2018. 

  Hamasa hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kundi la Wabunge wa Uzazi Salama, Mh. Jenista Mhagama wakati akifungua mkutano uliowakutanisha wabunge wa kundi hilo wapatao 30 pamoja na Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama (WRATZ) mjini Dodoma kujadili kuhusu mchango wa wabunge katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi. 

  Akiwasilisha mada katika mkutano huo Meneja mradi wa Muungano wa Utepe mweupe (WRATZ) Bi Sizarina Hamisi alisema kwa mujibu wa takwimu ya Idadi ya Watu na Afya Tanzania ya mwaka 2015-2016 zinaonyesha kuwa kwa sasa wakina mama 30 na watoto wachanga 180 wanapoteza maisha kila siku kutokana na matatizo yatokanayo na uzazi. 

  Kwa upande wao baadhi ya wabunge wamekiri kuwa pamoja na jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali bado vifo vya mama na mtoto vitokanavyo na uzazi ni changamoto hivyo kuna haja yakuongeza jitihada ili kutatua tatizo hilo ikiwemo bajeti ya afya ya mama na mtoto hasa huduma za muhimu na dharura kupewa kipaumbele kuanzia ngazi za halmashauri mpaka serikali kuu.

  0 0


  Mratibu wa Mafunzo ya Mabingwa wa Tiba ya Mifupa nchini (SICOT , Société Internationale de Chirurgie Orthopédique et de Traumatologie) Dk. Robert Mhina (kulia) kutoka Taasisi ya Mifupa Tanzania (MOI) , akishiriki mafunzo ya utoaji huduma kwa majeruhiwa wa ajali kwa njia ya video yaliyoratibiwa na kufanyika kwa njia ya video kwenye kumbi za Wakala ya Mafunzoa kwa Njia ya Mtandao, yakijumuisha nchi. Kushoto ni Dk.Lukwinyo na Dk.Mbaruku Mlinga.


   Madaktari mbalimbali wakifuatilia mafunzo hayo kwa makini.

  Madaktari wa Tiba ya Mifupa wakishiriki mafunzo hayo. Kutoka kushoto ni Dk.Hamid Masoud, Dk.Valentine Restus na Dk. Joseph Msemwa.  Na Dotto Mwaibale

  UMOJA wa Madaktari Bingwa wa Mifupa Duniani (SICOT) ikishirikiana na Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), umetoa elimu ya  kutoa huduma kwa majeruhi wa ajali kwa njia ya mtandao wa mafunzo kwa njia ya video.

  Umoja huo ulitoa elimu hiyo kwa kushirikiana na Madaktari Bingwa na wataalamu wa Mifupa kutoka nchi za Tanzania, Marekani, Pakistani na Brazil.

  Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo akiwa TaGLA, Dar es Salaam, Mratibu wa Umoja huo hapa nchini, Dk. Robert Mhina alisema kupitia mafunzo haya wameweza kujadili mambo mbalimbali yahusuyo ajali za barabarani.

  “Huwa tunajadili mada mbalimbali kama ajali za barabarani kwa kubadilishana uzoefu na Madaktari wa nchi nyingine kwa kutumia mtandao wa mafunzo kwa njia ya video, na wakati wote huwa tunazungumza na nchi kutoka mabara mengine ili kubadilishana uzoefu,”alisema.

  Alisema madaktari hao huwa wanakubaliana katika kujadili mada na kujadili kuhusu mambo muhimu yanayohusu tiba ya mifupa huku wakipeana majukumu.

  “Kupitia vikao hivi hutusaidia sana hata kwa wale wanafunzi wanaojifunza Ubingwa kuona kitu gani kinaendelea duniani, bila gharama za kusafiri nje ya nchi” alisema Dk Mhina.

  Alisema tayari Umoja huu inaangalia uwezekano wa kutoa nafasi kwa wanafunzi kutembela vituo kingine katika nchi hizo ili kuona na kuongeza uzoefu zaidi.

  “Mwaka huu kuna vikao kama sita hivi, kikao hiki ni mwazo tu,”alisema na kuongeza kuwa kupitia mkutano huo itawasaidia wananchi kwa kuboreshewa ufanyaji wa tiba sahihi za mifupa hivyo kupata huduma za matibabu zilizoboreshwa kutokana na ajali za barabarani.

  Watoa mada katika mkutano huo uliofanyika kwa njia ya video walikuwa ni pamoja na Dk. Syed M. Avais wa King Edward Medical University, Dk. Robert D. Zura wa Louisiana State University Health Science Center na Dk. Robert I. Mhina, wa  Taasisi ya Mifupa Tanzania (MOI) kutoka nchini Tanzania.

  0 0
 • 02/01/17--06:59: Ulega cup Mkuranga
 •   Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) Cassim Taalib katikati akiwa ameshika la timu yake ya SHIWATA walilochukua hivi karibuni.


  TIMU ya Kombaini ya Kata ya Mbezi juzi iliibuka kidedea baada ya kulipiza kisasi kwa kushinda nao 1-0 dhidi ya mahasimu wao wakubwa Shungubweni.

  Katika mchezo huo wa kugombea ubingwa wa Kombe la Mbunge wa Mkuranga,Ulega cup uliofanyika uwanja wa Mawasiliano wa Kata ya Mbezi,washindi wa mchezo huo wanaindwa na wachezaji wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) was ushindi huo inasonga mbele katika mashindano hayo.

  Bao lililoipa ushindi Kata ya Mbezi lilipatikana dakika ya 36 kupitia kwa Maulid Mtungata kwa shuti kali la mbali baada ya kutokea piga nikupige katika lango la Shungubweni.

  Katika mashindano hayo yanayoshirikisha timu kutoka Tarafa nne zenye jumla ya timu 25 kutoka Kata 25 za wilaya ya Mkuranga kila tarafa itatoka timu mbili.

  Tarafa ya Shungubweni timu mbili zilishiriku za Mbezi na Shungubweni yenyewe ambazo zote zimefanikiwa kuingia hatua ya pili baada ya mchezo wa kwanza Shungubweni kuishinda Mbeki kwa mabao 4-0.
  Mwisho

  0 0

  HABARI ZA LEO WADAU KUNA FURSA AMBAYO IPO WAZI, WAPO WAWEKEZAJI WANAOTAKA KUKODISHA MASHAMBA YA KAHAWA(COFFEE ESTATE) KWA MIKATABA YA MUDA MREFU ENDAPO UNALO AU UNAJUA ANAYEKODISHA MKOA WOWOTE NAOMBA TUWASILIANE KWA NAMBAHAPO CHINI
  MR. AMAN 0788503209

  0 0

  geni rasmi wa ufunguzi wa Mkutano wa uhamasishaji wa Afya na lishe kwa vijana (hasa kwa wasichana),Mkurugenzi wa Kinga,Wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na watoto Dkt.Neema Rusibamayila akisoma hotuba wakati wa mkuitano huo ambao wa siku tatu unaofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere
  Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) Dkt.Joyce Kaganda akizungumza kwenye mkutano huo
  Baadhi wa washiriki wa mkutano huo wakifuatilia uwasilishaji wa mada.Mkutano huo wa Kimataifa unawashirikisha viongozi wa juu wa serikali, mashirika na taasisi binafsi pamoja na wadau wa maendeleo nchini na nje ya nchi
  Picha ya pamoja ya washiriki wa Mkutano huo ambao unalengo la kutunza afya ya vijana hususani wasichana kwani ni wazazi wa baadae kutoka wanapozaliwa hadi makuzi yao .Nchi zinazoshiriki mkutano huo ni pamoja na Tanzania,Ethiopia,Senegal na Kenya(Picha zote na Rayson Mwaisemba-Wizara ya Afya)

  0 0


   

   Na: Lilian Lundo – MAELEZO - Dodoma

  Vyuo Vikuu hapa Nchini vimeagizwa kuacha mara moja kutoza ada kwa fedha za kigeni kwa wanafunzi ambao ni watanzania.

  Agizo hilo limetolewa leo Bungeni, Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge Jaku Hashimu Ayoub kwamba kumekuwa na malalamiko ya wanafunzi wa Elimu ya Juu Tanzania ambao ni wazawa kulipishwa ada ya masomo yao kwa fedha za kigeni badala ya fedha za Kitanzania.

  “Sarafu inayotakiwa kutumika Tanzania ni shilingi ya Kitanzania kwa mujibu wa kifungu cha 25 na 26 cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ya mwaka 2006. Aidha, kwa Tanzania malipo ya kitu au huduma yoyote inapaswa kulipwa kwa shilingi ya Kitanzania kama ilivyoainishwa kwenye kifungu cha 28 cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania, 2006,” alifafanua Mhandisi Manyanya.

  Aliendelea kwa kusema kuwa japo Wizara haijapokea malalamiko yoyote ya kutozwa fedha za kigeni kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu tangu itoe agizo kama hilo kwa wamiliki wa vyuo Septemba 07, 2016.

  Hivyo basi kwa mara nyingine Mhandisi Manyanya ameviagiza vyuo ambavyo bado vinatoza wanafunzi Watanzania fedha za kigeni kuacha mara moja kwani vyuo hivyo vimeelekezwa kutoza wananchi wa Kitanzania kwa pesa ya Kitanzania.

  Aidha Mhandisi Manyanya amewataka watanzania kutoa taarifa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ikiwa kuna Chuo chochote kinachotoza ada kwa Watanzania kwa fedha za Kigeni ili hatua stahiki za kisheria zichukuliwe dhidi ya wahusika.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Ghana Mhe. Nana Addo Dankwa Akufo katika Uwanja wa Kimataifa wa Bole Mjini Addis Ababa Ethiopia muda mfupi kabla ya kuondoka nchini humo alikokuwa akihudhuri Mkutano wa 28 wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) uliomalizika jana.  Mhe. Rais Nana Addo ameahidi kuendeleza na kuimarisha zaidi ushirikiano na uhusiano kati ya nchi yake na Tanzania na amekubali mwaliko wa Mhe. Rais Magufuli wa kuitembelea Tanzania.


  0 0

  Na. Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma

  Serikali itaendelea kutoruhusu uvuvi kufanyika ndani ya Pori la Akiba la Selous kutokana na ukiukwaji wa taratibu zilizokuwa zimewekwa wa kuingia ndani ya hifadhi hiyo.

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhandisi Ramo Makani ameyasema hayo leo Bungeni, Mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Rufiji Mohamed Mchengerwa juu ya hatua ambazo Serikali inazichukua kutoa ridhaa kwa wananchi waishio maeneo ya hifadhi kupata ruhusa kisheria kuweza kuvua samaki.

  “Mwaka 1994, wananchi wa Kata ya Mwaseni, Mloka, Ngoroka na Kipungila Wilaya ya Rufiji waliruhusiwa kuingia ndani ya Pori la Akiba Selous na kuvua Samaki. Hata hivyo, baadhi ya wanavijiji walikiuka taratibu zilizokuwa zimewekwa kwa kuingia ndani ya hifadhi bila kujiandikisha na kuvua samaki kinyume cha sheria,” alifafanua Mhandisi Makani.

  Aliendelea kwa kusema kuwa baadhi ya wavuvi walibainika kujihusisha na vitendo vya ujangili wa wanyamapori, uvuvi haramu wa kutumia sumu, ukataji miti ovyo kwa ajili ya kukausha samaki na kutengeneza mitumbwi pamoja na uharibifu wa mazingira uliotokana na uchomaji wa moto ovyo kinyume cha sheria.

  Mhandisi Makani amesema kuwa kwa kuzingatia hali ya usalama katika maeneo ya uhifadhi wa wanyamapori, Wizara ya Maliasili na Utalii itaendelea kutoruhusu uvuvi kufanyika ndani ya Pori la Akiba Selous.

  Aidha Wizara inawashauri wananchi wa Kata za Mwaseni, Mloka na nyinginezo zilizo jirani kutumia mabwawa mengine yaliyoko nje ya Pori hilo yenye fursa kubwa kwa kufanya shughuli za uvuvi.

  Mabwawa ambayo wananchi wameshauriwa kuyatumia ni Bwawa la Zumbi lililoko vijiji vya Nyaminywili, Kipugira na Kipo, Bwawa la Ruwe lililopo Mkongo, Lugongo lililopo kijiji cha Mtanza na Bwawa la Zimbwini lililopo Mji wa Kibiti.

  Mabwawa hayo ya Mto Rufiji yatatoa fursa ya shughuli za uvuvi hivyo kusaidia kuinua kipato cha wananchi.

  Vile vile Mhandisi Makani amesema kuwa, Wizara hiyo kwa kutambua mahitaji ya wananchi katika maeneo hayo ya kufanyia kazi na kujiletea maendeleo kiuchumi na kijamii. Wizara hiyo inaendelea kushauriana na Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji kuhusu namna ya kutekeleza mpango wa kuwajengea mabwawa ya samaki ili pamoja na mabwawa ya asili yaliyopo yawawezeshe kufanya shughuli za uvuvi endelevu.


  0 0


  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Seleman S.Jafo akizungumza na walimu, wanafunzi na Kamati ya shule ya msingi Chang’ombe A Manispaa ya Dodoma alipofanya ziara kujionea maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ambao umekamilka kwa asilimia mia moja. Kulia kwake ni Kaimu Afisa Elimu Mkoa Dodoma Bw. Tumsifu Mwasamale na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bi. Nelly kinyaga kushoto kwake ni Diwani Kata ya Chang’ombe Mhe.Bakari Samweli Fundikira
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Seleman S.Jafo akifungua mlango ili kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa ambao umekamilika kwa asilimia mia mojaNaibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Seleman S. Jafo akitoa agizo kwa halmashauri, kamati za shule na mikoa nchini kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake kutumia juhudi na maarifa ili kuwaletea wananchi maendeleo kwa haraka. Ameridhishwa na ubora na kasi waliyoitumia kujenga majengo hayo.

  Mojawapo ya madarasa yaliyokamilika katika shule ya msingi Chang’ombe A Manispaa ya Dodoma. Jumla ya vyumba vya madarasa sita vimejengwa ili kukabiliana na changamoto ya vyumba vya madarasa katika shule hiyo inayotokana na wingi wa wanafunzi, shule hiyo ina zaidi ya wanafunzi 2000

  NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Seleman Jafo amewataka wanafunzi na walimu wa shule ya msingi ya Chang’ombe kutunza na kuitumia miundombinu iliyojengwa ili kuongeza ufaulu katika shule hiyo.

  Jafo ametoa kauli hiyo leo alipotembelea shule hiyo ili kukagua utekelezaji wa agizo alilolitoa juu ya kukamilisha ukarabati wa miundombinu katika shule hiyo ifikapo 10 januari, mwaka huu.

  Novemba 3, mwaka jana Jafo alitoa agizo kwa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kuhakikisha inakamilisha ujenzi wa matundu 20 ya vyoo na vyumba vya madarasa 8 pamoja na ukarabati wa vyumba vya madarasa 2 katika shule ya Chan’gombe A ifikapo januari, 10 mwaka huu kabla ya msimu wa masomo kuanza.

  Katika ziara hiyo, Jafo amesema ameridhishwa kwa hatua nzuri ya ukarabati huo na kupongeza uongozi wa Halmashauri ya Manispaa , kamati ya shule ya Chang’ombe ,walimu na Diwani wa Kata ya Chang’ombe kwa utekelezaji huo.

  Amesema shule hiyo inapaswa kuongeza ufaulu wake ili iwe mfano mzuri wa kuigwa kwa shule nyingine .Amesema awali alitoa agizo hilo baada ya kubaini changamoto mbalimbali katika shule ya msingi ya Chang’ombe A .

  ‘’Maagizo niliyoyatoa yalikuwa magumu sana lakini nia yangu ilikuwa kuwatengenezea mazingira rafiki wanafunzi na walimu , nimefarijika na utekelezaji wake, hali haikua nzuri hapo mwanzo lakini nimefarijika kwa kazi nzuri, muonekano wa madarasa unaridhisha nawapongeza sana’’ amesema Naibu Waziri huyo

  Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Nelly Kinyaga ameishukuru serikali kwa kuboresha miundombinu ya shule hiyo ambapo awali mazingira ya shule hiyo yalikuwa sio rafiki kwa wanafunzi na walimu kutokana na upungufu wa matundu 20 ya vyoo na vyumba vya madarasa 8.

  ‘’Kwakweli kulikuwa na changamoto sana wanafunzi walikua wengi na madarasa machache lakini kwasasa hatuna watoto wanaokaa chini na msongamano wa wanafunzi darasani umepungua kwa kiasi kikubwa ,naishukuru serikali na Jafo kwa kutilia mkazo ukarabati wa miundombinu ya shule yetu’’ amesema

  Mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo, Ally Mohamed Swalehe ameishukuru serikali kwa kuboresha miundombinu ya shule hiyo rafiki kwa kuwa itaongeza ufaulu katika mitihani na kuepusha magonjwa ya milipuko shuleni hapo.

  0 0
 • 02/01/17--07:42: JARIDA LA NCHI YETU

 • 0 0

  Serikali imetoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa mikopo kwa vijana na malipo ya ada kwa fedha za kigeni. Ufafanuzi huo umetolewa mjini hapa leo wakati wa kikao cha pili katika Mkutano wa Sita wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Kuwainua Vijana Kiuchumi

  Akijibu hoja kuhusu namna vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini wanavyoweza kufaidika kiuchumi, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira), Anthony Mavunde, amesema Serikali imetenga fedha za kutosha kupitia mifuko mbalimbali kuwawezesha vijana kwa mitaji na mafunzo ya ujasiriamali ili kuwainua kiuchumi.

  Ameongeza kuwa vijana wenyewe ndio wanaopaswa kuchangamkia fursa hizo na pale wanapojiunga katika vikundi mbalimbali wamekuwa wakipewa mikopo kwa ajili ya mitaji. Alitoa mfano wa jinsi Serikali ilivyowawezesha vijana waliojiunga na kuwekeza katika viwanda vidogo vya maziwa na chaki mkoani Simiyu.

  Amewataka pia Wabunge na Halmashauri zote nchini kuendelea kupigania kutengwa maeneo maalum katika sekta mbalimbali kwa ajili ya kuwapatia vijana na kutengwa kwa asilimia 5 ya mapato ya Halmashauri kwa maendeleo ya vijana

  Ada kwa Fedha za Kigeni

  Serikali imesema, ingawa haijapokea malalamiko yoyote kuhusu wananchi wasioridhihwa na mtindo wa kutakiwa kulipa malipo ya ada kwa fedha za kigeni katika baadhi ya shule na vyuo, lakini imesisitiza kuwa wale wanaotoza ada kwa fedha za kigeni wanakiuka Sheria.

  Akitoa ufafanuzi huo, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Stella Manyanya amesema kwa mujibu wa kifungu cha 28 cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT), 2006, fedha inayopaswa kutumika kwa malipo ya huduma nchini ni Shilingi ya Tanzania. Ameviagiza vyuo na shule nchini kuacha kutoza ada kwa fedha za kigeni na kuhimiza wananchi watakaobainika kufanya hivyo kutoa taarifa Serikalini.

  Si Tatizo Kutumia Majengo UDOM

  Serikali imesisitiza kuwa baadhi ya Wizara zilizoanza kutekeleza agizo la kuhamia Dodoma kutumia baadhi ya majengo kwa muda kwenye Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) hakutaathiri shughuli za chuo.

  Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama. Waziri Jenista amesisitiza kuwa baadhi ya Wizara zitatumia majengo ya UDOM kwa sababu mengi ya majengo hayo yalikuwa hayatumiki kwa sasa kwa shughuli za chuo hicho na hakutakuwa na muingiliano na shughuli za chuo.

  Mradi wa Mabilioni Maji Dar

  Serikali kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji Dar es Salaam imeanza kutekeleza mradi wa usambazaji wa maji utakaogharimu Dola za Marekani milioni 32.772 ambazo ni mkopo kutoka Benki ya Exim ya China. Mradi huo utahusisha sehemu yote ya jimbo la Kawe, Dar es Salaam. Mradi huo utachukua miezi 15.

  Imetolewa na:

  Idara ya Habari-MAELEZO.


older | 1 | .... | 1124 | 1125 | (Page 1126) | 1127 | 1128 | .... | 1897 | newer