Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1122 | 1123 | (Page 1124) | 1125 | 1126 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto amewataka wasanii kuondoa makundi yaliyopo kwenye muziki na kuanza kushirikiana kwa pamoja ili kuleta mafanikio kwa wengi.

  Akiongea na mwandishi wetu Jumatatu hii muimbaji huyo amedai kila msanii nchini anafanya kazi kivyake hali ambayo inawanyima zaidi wasanii fursa za kibiashara.

  “Kwa muda mrefu sasa wasanii wa Tanzania wamekua wakifanya kazi nzuri ndani na nje ya nchi, lakini kila mtu anacheza karata yake kivyake kutokana na network na nguvu yake,” alisema Mpoto. “Nadhani sasa wakati umefika kuondoa tofauti zetu, makundi, tukawa team moja tukae tuone tunawezaje kusaidiana kwenye nyanja za kibiashara,”

  Aliongeza, “Kuwa kama wasanii wa Taifa la Tanzania wenye muelekeo mmoja bila kuingilia fani ya mtu wala maisha binafsi, Wazo langu tusitawanyike ikawa kila mtu anaenda kivyake, ukiotea hit basi ndiyo unapata hela, najaribu tu kuwaza kwa sauti kama wazo lina mashiko, #teamtanzania,”

  Muimbaji huyo ni mmoja kati ya wasanii ambao wanapiga deal nyingi nje ya muziki ukiachia mbali deal za ubalozi za makumpuni mbalimbali alizopewa

  0 0

  Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amewataka Vijana kuwa na tabia ya kufanya mazoezi mara kwa mara, kwani kufanya hivyo kunapelekea Afya zao kuwa imara na kuepuka magonjwa yanayoweza sababisha vifo vya mapema.

  Akizungumza Jijini Dar es Salaam wakati akizindua Bonanza la Michezo maeneo ya Tabata lililoandaliwa na Windhoek beer DAS Mpogolo amesema kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) vijana wengi wanapoteza maisha kwa kutotunza Afya zao na kueleza kuwa vifo takribani 3000 vimeripotiwa vinavyotokana na shinikizo la damu huku Tanzania ikiwa nchi ya 85, huku kwa ugonjwa wa kisukari watu takribani 9257 wamepoteza maisha na Tanzania ikishika nafasi ya 35 kidunia na Kiharusi zaidi ya 5000 wamepoteza maisha na Tanzania ikishika nafasi ya 102 kidunia.

  Kutokana na Takwimu hizo DAS Mpogolo amesisitiza mazoezi kwa vijana kwa kufanya michezo ambayo inawakutanisha na kuanzisha mahusiano na kuleta undugu, huku akiwasisitiza waandaaji waandae mabonanza kama hayo yakishirikisha michezo ya aina tofauti siyo mpira wa miguu pekee.

  Bonanza hilo lilikuwa kivutio baada ya Timu mbili za Kwetu Pazuri wakiwa wenyeji na Bongo Fleva, huku timu ya Kwetu Pazuri ikiwa na wachezaji ambao ni wasanii wa familia moja Ali Kiba na Abdul Kiba na mchekeshaji maarufu kama Kupe ambaye aliipatia ushindi Kwetu Pazuri kwa kushinda goli mbili kwa nunge, na kwa upande wa Bongo Fleva timu yao ilipambwa na mastaa wakongwe akiwemo KR, Mchizi Mox, Soggy Doggy, Suma G, M2THE P, na Juma Nature.
   


  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Palestina nchini Mhe. Hazem M.Shabat, Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia kitabu alichokabidhiwa na Balozi wa Palestina nchini Mhe. Hazem M.Shabat, Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Palestina nchini Mhe. Hazem M.Shabat (kushoto) mara baada ya kumaliza mazungumzo, Ikulu jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto), akiongozwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Saleh Mhando wakati akiwasili ofisi ya mkoa huo kwa ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kuona changamoto za masuala ya ulinzi na usalama na kuyatafutia ufumbuzi.Wengine ni viongozi wa serikali mkoani hapo.
  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Saleh Mhando (kushoto), akitoa taarifa ya Mkoa kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo mkoani hapo ikiwa na lengo la kuona changamoto za masuala ya ulinzi na usalama na kuyatafutia ufumbuzi.
  Katibu Tawala Mkoa wa Katavi, Paul Chagonja akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo mkoani hapo yenye lengo la kuona changamoto za masuala ya ulinzi na usalama na kuyatafutia ufumbuzi.Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Matinga.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(wakwanza kulia), akimsikiliza Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Saleh Mhando, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo mkoani hapo kwa lengo la kuona changamoto za masuala ya ulinzi na usalama na kuyatafutia ufumbuzi.Wengine ni viongozi wa mkoa huo kutoka kada mbalimbali.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (watatu kulia),akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Saleh Mhando,(wapili kulia). Naibu Waziri alifika mkoani hapo kwa ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kuona changamoto za masuala ya ulinzi na usalama na kuyatafutia ufumbuzi. Wengine ni viongozi wa mkoa huo kutoka kada mbalimbali (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

  0 0

  Leo tumeangazia habari za michezo zikiwemo za hapa Tanzania na nje ya Tanzania ,Ni habari tano za juu kwa undani wa habari hizo hii hapa video yake.

  Attachments area Preview YouTube video HABARI TANO ZA MICHEZO NA RUVUMA TV

  0 0

  Golikipa wa timu ya NSSF, Mfaume Mzee  akisalimiana na wachezaji wa timu ya Tanesco wakati wa mchezo wa Nusu Fainali ya michuano ya Ligi ya Mashirika ya Umma uliofanyika kwenye uwanja wa TPDC Mikocheni jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Tanesco ilishinda 4-1. (Picha na Francis Dande).
  Wachezaji wa NSSF wakiwa katika mazoezi kabla ya mchezo wao na Tanesco.
  Wachezaji wa NSSF wakijadiliana jambo muda mfupi kabla ya mchezo.
  Viongozi wa NSSF pamoja na wachezaji wakiwa katika picha ya pamoja.
  Timu za NSSF na Tanesco zikikaguliwa.
  Golikipa wa timu ya NSSF, Mfaume Mzee akijaribu kuokoa  moja ya hatari langoni mwake.
  Nahodha wa NSSF, Baome Kiwamba akimiliki mpira.
  Mshambuliaji wa timu ya NSSF, Shaban Enzi akichuana na beki wa Tanesco, Nicholous Peter katika mchezo wa nusu fainali ya mashindano ya timu zaMashirika ya Umma.
  Kiungo wa NSSF, Salum Swedi akichuana na Fortunatus Mgumba.
  Mshambuliaji wa NSSF, Baome Kiwamba akichuana na beki wa Tanesco, Stanley Uhagile.
  Kocha Msaidizi wa timu ya NSSF, Ali Chuo akitoa maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa mapumziko. 
  Mashabiki wa timu ya NSSF wakifuatilia mchezo huo.
  Mashabiki wa timu ya NSSF.

  0 0

  DC  Kilolo  Asaia Abdalaha  akifafanua  jambo
  Mwenyekiti  wa Halmashauari ya  Kilolo  akifugua  kikao  kushoto  ni mkurugenzi  mtendaji wa Halmashauri ya  Kilolo

  Baraza la madiwani  Kilolo

  Na MatukiodaimaBlog 

  BAADA ya  mradi  wa maji Ipalamwa  kujengwa chini ya  kiwango kwa bomba kupasuka ovyo kabla ya mradi  kukabidhiwa ,baraza   la madiwani  la Halmashauri ya  wilaya ya  Kilolo  mkoani  Iringa  limempa muda  wa  wiki  mbili mkandarasi  wa kampuni ya Norcom Ltd kukamilisha mradi  wa maji wa Ipalamwa  kwa  ubora unaotakiwa zinginevyo mkataba  wake  utavunjwa.

  Huku  mkuu  wa  wilaya  ya  Kilolo  Asia  Abdalaha akiagiza Halmashauri hiyo  kutomlipa fedha  yeyote  mkandarasi   huyo hadi  hapo atakapokamilisha mradi  kwa  kiwango  kinachotakiwa  vinginevyo kama  kuna pesa  alilipwa awali basi  pindi  mkataba  wake utakapovunjwa atapaswa  kuzirudisha  fedha  hizo.

  Wakitoa  maadhimio  hayo katika  kikao  cha  baraza  la  madiwani   kilichofanyika  juzi  katika  ukumbi  wa Halmashauri  ya  Kilolo  na  kuhudhuriwa na mkuu  wa  wilaya  ya  Kilolo ,madiwani  hao  walisema  kuwa wamechoshwa na mkandarasi  huyo  kuendelea kuchelewesha  mradi  huo  wa  maji na  kuwa sasa  wanaona  suala   hilo la kero ya  maji kijiji  cha Ipalamwa  lifike  mwisho  kwa  kumpa  muda  wa  mwisho  kwa ajili ya  kukamilisha mradi   huo .

  Mhandisi   wa  maji  wa  wilaya ya  Kilolo Enock Basyagile   akijibu  hoja  za  baraza  la madiwani  juu ya  ucheleweshwaji  wa  mradi  huo   alisema  kuwa sababu ya  kuchelewa kwa  kazi hiyo ni  kutokana na  kukosekana  kwa   fedha kati ya Halmashauri na mkandarasi   ila  kwa   sasa  fedha  zimeingia na mchakato  wa  kufanya  kazi   hiyo  kwa  kununua  vifaa  vya mradi  huo  ikiwa ni  pamoja na mchakato  wa malipo kwa mkandarasi   huyo.

  Mkuu wa  wilaya  ya  Kilolo Asia  Abdalah  alisema  hakubaliani  na  uamuzi  wa mhandisi    wa maji  wilaya  kutenga   fedha  ama  kufanya mchakato  wa malipo  ya Tsh  milioni 19 kwa  mkandarasi  huyo  aliyejenga  mradi  huo  chini ya  kiwango ila alitegemea  kuona mkandarasi  huyo anachukuliwa hatua kwa kufanya  kazi  chini ya  kiwango.

  " Sikubaliani  hata  kidogo  na uamuzi  wa kumlipa fedha  mkandarasi  huyo ama  Halmashauri  kununua mabomba kwa ajili ya kukarabati  mradi ambao haujakabidhiwa  kwa  wananchi .....naagiza mkandarasi  huyo afanye  kazi hiyo  kwa gharama  zake na  asilipwe  pesa  yoyote  hadi mradi  utakapokabidhiwa "

   Mwenyekiti  wa Halmashauri  ya  Kilolo Bw Vellance Kihwaga  alisema  sababu  kubwa ya  mradi   huo  kuendelea  kusumbua kwa mabomba  kupasuka  ni  baada ya  mkandarasi huyo  kwenda  kinyume na mkataba  wa kazi  hiyo kwa kuweza mabomba membamba  zaidi    kuliko  nguvu  ya maji   hivyo pindi  maji  yakifunguliwa mabomba  hayo   hupasuka .

  Alisema  kutokana na ubovu   huo  wa mabomba  kamati ya  fedha  ilifanya  ziara ya  ukaguzi  wa  mradi  huo  toka  mwaka jana  na  kumwagiza mkandarasi  huyo kufanya marekebisho  kwa  kutoka mabomba   yote  yasiyo  na ubora na  kufunga mabomba  yenye ubora  na alikubali  kuifanya kazi   hiyo  ndani ya wiki mmoja na kamati  ilimpa  mwezi  mmoja  ila hadi  sasa ni  zaidi ya miezi 4 kazi   hiyo   haijafanyika .

   Mkurugenzi  mtendaji wa  Halmashauri ya  Kilolo Bw Aloyce Kwezi alisema  kuwa mkanadarasi  huyo bado  hajalipwa  fedha   yoyote  na  kuwa Halmashauri  haitamlipa fedha  hadi  hapo mradi  utakapokamilika na anapaswa  kufanya kazi  hiyo  kwa  gharama  zake na iwapo atashindwa  kwa muda  uliotolewa basi  halmashauri  itavunja mkataba  huo.
  Wakati  huo  huo serikali  ya  wilaya ya  Kilolo imepiga  marufuku  wageni  kuingia katika  vijiji ama kata na  kuendesha  miradi  mbali mbali pasipo kushiriisha viongozi wa  ngazi  zote  za vijiji ama Halmashauri .
  MWISHO

  0 0
  0 0

  Makampuni nguli Exim Bank ya nchini Tanzania na shirika la ndege la Oman yaungana kutoka punguzo la aina yake kwa wateja wa benki hiyo. Kwa mwaka mzima, wateja wa huduma ya Preferred Banking ya Exim watapata punguzo la asilimia 15% kwa safari zote za kutoka nchini zinazofanywa na shirika la Oman Air.


  Akizungumza ofisini kwake, Meneja masoko wa Exim Bank Bi Mariam Mwapinga alisema ‘Punguzo hilo litadumu kwa miezi 12 kwa wateja watakaokata tiketi za ndege kati ya mwezi Septemba 2016 na Septemba 2017, na kusafiri kabla ya mwezi Desemba 2017.

  Kuhusu kiwango hasa cha punguzo hilo, Bi Mwapinga alisema ‘Punguzo ni asilimia kumi na tano, kwa mfano kama gharama ya tiketi ni shilingi milioni moja, basi utapunguziwa laki moja na nusu’.


  Alipoulizwa juu ya wateja wapya, kama nao wanaweza kupata punguzo hili, Bi Mwapinga alisema ‘Ndio wanaweza, wanachotakiwa ni kufuata hatua chache tu kuweza kujiunga na familia yetu. Kwanza watatakiwa kutembelea tawi lolote la Exim Bank na kufungua akaunti chini ya huduma ya Preferred Banking.’


  Aliendelea kutoa maelezo, ‘Huduma ya Preferred Banking ni huduma ya kipekee, yaani unaweza kupata huduma zote za kibenki kwa kujinafasi. Ukiwa na akaunti hii utapata meneja uhusiano, maalumu kwa ajili yako pekee, viwango vyenye upendeleo wakati ukibadili fedha za kigeni, punguzo maalumu kwa makampuni washirika kama vile kama Ramada Hotels na maduka ya Shoppers. Pia utapata punguzo la asilimia 15 unaposafiri na ndege za Oman Air kuelekea safari zaidi ya 50 duniani.’

  Kwa maelezo zaidi ya jinsi ya kujiunga na Exim Preferred Banking na kupata punguzo hii, fika katika tawi lililo karibu nawe au piga simu namba +255 784 107 600. Pia unaweza kutuma barua pepe kwenda customerservice@eximbank-tz.com au tembelea kurasa zao za Facebook na Twitter @eximbanktz na @Exim_BankTz. Safari njema, wasalimie uendako.

  0 0


  Waziri Mkuu, Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa, MB. anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye harambee iliyoitishwa na Shirika lisilo la kiserikali la Land O’Lakes ikilenga kukusanya fedha kwa ajili ya uwezeshaji wa wanawake katika kilimo hasa kilimo biashara nchini kupitia taasisi iliyojikita kwenye kuendeleza wanawake katika kilimo Tanzania (CAWAT).

  Akizungumza na waandiishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Mradi wa Ubunifu  Katika Maswala ya Kijinsia na Kuimarisha Uhakika wa Chakula Katika Ngazi ya Kaya, unaoendeshwa na Land O Lakes, na kufadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Watu wa Merekani (USAID),  Dk Rose Kingamkono, alisema katika harambee hiyo Waziri Mkuu Majaliwa,ataungana na wageni waalikwa wengine zaidi ya 200 na kwamba zaidi ya sh milioni 150 zinatarajiwa kukusanywa.

  Alisema lengo la harambee hiyo inayotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam Februari 17 mwaka huu ikiwa na kauli mbiu “WEZESHA KILIMO BIASHARA ILI KUKUZA  AJIRA, JAMII NA VIWANDA ENDELEVU” ni kukusanya kiasi hicho cha pesa kitakachosaidia kuijengea uwezo wa kiutendaji taasisi hiyo mpya ya CAWAT iliyoanzishwa mahususi kusimamia programu endelevu katika kumnyanyua mwanamke kupitia kilimo chenye tija na ufanisi.

  “Mwanamke akijengewa uwezo  wa kufanya shughuli za uzalishaji mali kwa ufanisi atakuwa na mchango mkubwa katika kuboresha  ustawi wa familia na jamii kwa ujumla, huku pia akiondoa kabisa tatizo la upungufu wa chakula na lishe duni katika kaya zetu na hayo ndio malengo ya kuanzishwa kwa CAWAT tunayoipigania sasa.

  “Tafiti zimeonyesha kwamba uchumi ulioshikiliwa mikononi mwa mwanamke huelekeza matumizi yake kwa ajili ya ustawi wa familia zaidi kuliko ilivyo kwa uchumi ulioshikiwa mikononi mwa mwanaume’’ alisema.

  Alisema taasisi hiyo ya CAWAT kwa sasa ipo kwenye mchakato wa awali wa kuanza kujitegemea yenyewe kiuendashaji bila kutegemea msaada iliyokuwa ikiupata kutoka kwenye mradi  unaohusu ‘Ubunifu katika masuala ya kijinsia na kuimarisha uhakikaka wa chakula katika ngazi ya kaya (Innovations in Gender Equality (IGE), to Promote Household Food Security  unaotarajiwa kuisha Machi  mwaka huu.

  “Kuelekea katika kujiendesha yenyewe bila kutegemea msaada inayoupata kutoka mradi wa IGE, taasisi hii ya CAWAT bado ina safari ndefu inayohitaji msaada kutoka kwa wadau mbalimbali wa maendeleo ili iweze kutimiza wajibu wake wa kuwasaidia wakina mama walio kwenye sekta hii muhimu ya uzalishaji. Tunawaomba sana  watanzania mmoja mmoja, taasisi, mashirika, balozi mbalimbali waguswe katika kusaidia hili.’’ Alisema.

  Akizungumzia umuhimu kuwasaidia na kuwawezesha wanawake waliopo kwenye sekta ya kilimo, jukumu ambalo ndio linatekelezwa na taasisi ya CAWAT, Dk Kingamkono alisema pamoja na wanawake kuwa wahusika wakuu na wanatumia muda mwingi kwenye shughuli za awali za kilimo, mara nyingi wamekuwa hawafaidiki na jasho la kazi zao.

  “Hali hii ni kwa kuwa wanaume wamekuwa wakihodhi masuala yote yanayohusiana na faida zitokanazo na kilimo kwa kuhusika zaidi mwisho wa mnyororo wa kilimo kwa mfano maamuzi ya matumizi ya mapato yatokanayo na kilimo ambayo ni pmoja na masoko (kiasi gani kiuzwe na matumizi ya mapato yatokanayo na mauzo), na hata rasilimali zalishi za kilimo ikiwemo ardhi, upatikanaji wa pembejeo, mitaji, na huduma za ugani,’’

  “Hii ni kutokana na sababu kadhaa ikiwemo zile za tamaduni na mila zisizozingatia jinsia na baadhi ya sheria ambazo sio rafiki kwa mwanamke,’’ alibainisha.

   “Zaidi, tafiti zinaonesha kwamba wanawake wamekuwa na mzigo mzito katika sekta hii, hasa kwa shughuli za awali kwenye mnyororo wa thamani wa shughuli za kilimo ambazo ni uandaaji wa shamba, upandaji wa mazao, upaliliaji wa shamba, utunzaji, uvunaji, uhifadhi na usindikaji.,’’ alitaja.

  Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2014 zinaonesha kuwa, kilimo nchini ndio nguzo kuu ya uchumi ikichangia takribani asilimia 30 ya pato la taifa na asilimia 67 ya ajira, huku wanawake wakiwa ndio nguvu kazi kubwa ukilinganisha na wanaume na hutumia nyenzo duni zinazosababisha wao kutumia nguvu nyingi sana na muda mrefu, hali ambayo huchangia kudhorotoshe afya zao na watoto wanaokuwa tumboni mwao wakati wa ujauzito.
   Mkurugenzi wa Mradi wa Ubunifu  Katika Maswala ya Kijinsia na Kuimarisha Uhakika wa Chakula Katika Ngazi ya Kaya, unaoendeshwa na taaisisi ya Land O Lakes, na kufadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Watu wa Merekani (USAID),  Dk Rose Kingamkono (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na harambee iliyoitishwa na taasisi hiyo ikilenga kukusanya fedha kwa ajili ya uwezeshaji wa wanawake katika kilimo biashara  kupitia taasisi iliyojikita kwenye kuendeleza wanawake katika kilimo Tanzania (CAWAT). Wengine ni maofisa wa taasisi hiyo.

  0 0

  Picha ya pamoja ya wakuu wa nchi za umoja wa Afrika katika mkutano wao wa 28 jijini Addis Ababa, Ethiopia. Rais Dkt John Pombe Magufuli ni wa pili mstari wa pili kulia.

  0 0

  Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

  BOTI ya mizigo iliyokuwa ikitokea Kigoma kuelekea Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo ya Kalemi, imepotea katika ziwa Tanganyika ikiwa na Watu sita pamoja na Shehena ya vitungu gunia 110, ngano mifuko180 ,Mafuta ya taa dumu 20 na kreti za soda 70  ambayo mpaka sasa haijulikani ilipo.

  Akizungumza na Wanahabari Mkoani humo kamanda wa polisi  Mkoa wa Kigoma Fredinandi Mtui alisema Mnamo tarehe 23 januari majira ya saa 16:30 jioni boti iliyotengenezwa  kwa mbao MV.Ngendo ya Buchuma, boti ya mizigo inayo milikiwa na  Mussa Hamisi Mkazi wa ujiji Kigoma Manispaa ,iliondoka  Katika Bandari ya Kibirizi ikiwa na shehena ya vitunguu, Ngano na watu sita kuelekea Congo ambayo mpaka sasa haijafika Congo na haijulikani ilipo.

  Mtui alisema mpaka sasa boti hiyo haijulikani ilipo na hakuna chochote kilicho onekana kati ya mizigo wala abiria Waliokuwa wamepanda katika boti hilo, Askali wanamaji wakishirikiana na Chama cha Wamiliki wa maboti Wanaendelea na taratibu za kuitafuta boti hiyo inasemekana imepotelea maji ya Kongo.

  Alisema kumekuwa na taarifa zilizo kuwa zikizungumzwa mitaani kwamba  kunamiili imeonekana, taarifa hizo sio za kweli hadi sasa hawajajua kama watu hao watakuwa hai au wamekufa maji, tumewasiliana na Watu waliopembezoni mwa ziwa Tanganyika hawajaona kitu chochote hadi sasa , aliwataka Wananchi kuwa na subira kuweza kutambua kama watakuwa salama au wamekufa.

  "baada ya kupata taarifa kuhusu  Boti hiyo iliyokuwa ikielekea Congo kwamba haijafika kwa Muda ulio takiwa,Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Wamiliki wa Maboti walianza jitihada za kuitafuta boti hiyo maeneo ya mwambao mwa ziwa Tanganyika, na hatujapata taarifa yoyote ambapo ingekuwa imezama mizigo iliyo kuwemo katika boti hiyo ingekuwa imeanza kuelea, tumewasiliana na  Mikoa baadhi ambayo ziwa Tanganyika limepita pamoja na Nchi za Burundi na Congo kupitia ubalozi mdogo waweze kutujulisha endapo wataiona boti hiyo",alisema Mtui.

  Nao Baadhi ya ndugu wa Wasafiri walio kuwemo katika Boti hiyo wameanza kutandika msiba kuwaombolezea Ndugu zao waliopotea katika Boti hiyo , Hamis Kakolwa ni mmoja kati ya abiria waliokuwa wakisafiri kuelekea Kalemii Congo.

  Mgeni Kakolwa ni Mdogo Wa Hamis Kakolwa alisema Ndugu yao aliondoka siku ya tarehe 21 akielekea Kalemi kupeleka biashara zake, baada ya siku mbili kupita walifanya mawasiliano na watu wa Congo kujua kama boti waliokuwa wakisafiria ndugu yao imefika wakaambiwa haijafika ndipo walipoa anza kuwasiliana na Mmiliki wa boti hilo na kubaini kuwa boti hilo lilipotelea ziwani.

  Kakolwa alisema baada ya familia yao kuona hakuna mafanikio ya kuipata boti hiyo kwa siku 7 kupita waliamua kuandaa msiba wa kjmuombolezea ndugu yao kwasababu hawana uhakika kama atapona au amekufa.

  0 0

   Mwenyekiti wa Taifa wa Tanzania Girl Guide Association (TGGA), Profesa Martha Qorro (kushoto), akimvisha beji Mjumbe wa Bodi ya Udhamini wa TGGA,  Zakhia Meghji wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo, Mikocheni Dar es Salaam juzi. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
   Kamishna Mkuu wa TGGA,  Symphorosa Hangi, akimpongeza Anna Abdalah 

  Na Richard Mwaikenda.

  MJUMBE wa Bodi mpya ya Tanzania Girl Guides Association (TGGA), Anna Abdalah, amewataka viongozi Wanawake kukutana na Wasichana kuwapiga msasa wa kuwaaandaa kuwa viongozi bora wa baadaye.

  Anna Abdalah ambaye amekuwa kiongozi wa muda mrefu nchini, aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya TGGA, Mikocheni Dar es Salaam juzi.

  Alisema ana mpango wa kuwaalika viongozi mbalimbali Wanawake akiwemo Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akutane na Wasichana wanachama wa TGGA wawafundishe maadili ya uongozi kwa lengo la kuwaandaa kuwa viongozi bora wa baadaye.

  Anna Abdalla alisema kuwa  hata yeye na Zakia Meghji pamoja na baadhi ya viongozi wengine wanawake walioshika nyadhifa mbalimbali nchini, enzi za usichana wao walipitia kwenye chama hicho na kulelewa vizuri. 

  Pia katika kikao kijacho cha Bunge, anatarajia kukutana na Wabunge Wanawake na kuwaeleza umuhimu wamara kwa mara  kukutana na wasichana  kuwafundisha kwa kuwapa hamasa uongozi ili nao wawe kuwa wabunge na hata miongoni mwao kuwa Spika na mawaziri.

  "Nataka siku za usoni,tuwaalike viongozi mbalimbali akiwemo, Samia Suluhu Hassan, Naibu Spika wa Bunge, Wabunge na Mawaziri Wanawake ili mje mjumuike nao pamoja, mjifunze mambo mbalimbali ya uongozi na mhamasike, ili siku moja nanyi mje kuwa kama, Samia, Kamishna, Spika wa Bunge, Wabunge na hata uwaziri pia" alisema Anna Abdalah, huku akipigia makofi na waalikwa katika hafla hiyo.

  Katika hafla hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa Jaji mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Engera Kileo, ilihudhuriwa na wanachama wa chama hicho, wakiwemo pia wasichana watatu waliotoka Rwanda, Uganda na Madagasca waliokuwepo 

  nchini katika mafunzo ya uongozi, maadili na utamaduni. Wasichana hao ni; Michelline Uwiringiyimana (Rwanda), Recheal Baganyire (Uganda) na Andriambolamanana Vahatrimama. 

  Kamishna Mkuu wa TGGA,  Symphorosa Hangi, aliwataja Wajumbe wa Bodi hiyo kuwa ni; Zakia Meghji, Anna Abdalah, Grace Makenya, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia  Mjema na Mke wa Waziri Mkuu mstaafu, Tunu Pinda. Mwenyekiti wa Bodi hiyo  atateuliwa miongoni mwao.
    Mwenyekiti wa Taifa wa Tanzania Girl Guides Association (TGGA), Profesa Martha Qorro (kushoto), akimpongeza Mjumbe wa Bodi ya Udhamini wa TGGA,  Anna Abdalah wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo, Mikocheni Dar es Salaam juzi. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
   Mkuu wa Wilaya ya Ilala, ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya TGGA, Sophia Mjema (aliyekaa kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa TGGA wakati wa hafla hiyo. Aliyekaa kushoto ni Mariamu Kimbisa  ambaye ni Kamishna wa Kimataifa wa TGGA. Wa tatu kulia waliosimama ni Kamishna Mkuu wa TGGA, Hangi.
   Wasichana Michelline Uwiringiyimana (Rwanda), kulia, Recheal Baganyire (Uganda), katikati, na Andriambolamanana Vahatrimama wa Madagascar ambao wapo nchini kaitika programu ya mafunzo ya kubadilishana uzoefu katika masuala ya utamaduni, uongozi na maadili.wakiwa katika hafla hiyo.
   Wakipiga makofu baada ya kufurahishwa na hotuba ya Anna Abdalah

   Anna Abdalah akihutubia katika hafla hiyo
   Mmoja wa wabia wa moja kati ya majengo ya TGGA, akisalimiana na Anna Abdalah
   Katibu wa Taifa wa TGGA, Grace Shebe akitoa shukrani kwa wajumbe wapya wa bodi na wageni waalikwa kwa kuhudhuria uzinduzi huo.
   Wajumbe wa Bodi wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa TGGA pamoja na wanachama wa chama hicho.
   Sasa ni wakati wa msosi
   Wajumbe wa Bodi wakijadiliana jambo na watendaji wa TGGA
   Profesa Qooro akimuaga Zakia Meghji. Katikati ni Kamishna Mkuu wa TGGA, Hangi.
   Qooro akigana na Anna Abdalah. Kushoto ni Hangi
  Mjumbe wa Bodi Grace Makenya akiaga

  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Malika Berak (kushoto), ofisini kwake, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza kwa makini Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Malika Berak wakati wa mazungumzo yao yaliofanyika ofisini kwake, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Malika Berak (kushoto) mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwake, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

  ...............................................................

  Serikali ya Ufaransa kupitia Benki ya Maendeleo ya Nchi hiyo (AFD) imeahidi kuwa inampango wa kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu kutoka wastani wa euro milioni 50 hadi euro milioni 100 kwa mwaka katika miaka ijayo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.

  Balozi wa Ufaransa hapa Nchini Malika Berak ametoa kauli hiyo Ikulu Jijini Dar es Salaam alipokutana na Kufanya mazunguzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuhusu hatua zilizofikiwa katika uandaaji wa kongamano la uwekezaji litakalofanyika Jijini Dar es Salaam kuanzia mwanzoni mwa mwezi Aprili mwaka huu.

  Balozi huyo amesema mkopo huo itaiweza na kuisaidia Tanzania kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi hasa katika sekta za maji na usafi wa mazingira na miradi ya umeme. Kuhusu uandaaji wa kongamano la uwekezaji nchini, Balozi Malika Berak amemweleza Makamu wa Rais kuwa maandalizi ya kongamano hilo kubwa la Kibiashara linalolenga kujenga na Kuimarisha ushirikiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Ufaransa yanakwenda vizuri.

  Balozi huyo amesema kuwa kongamano hilo ambalo litakuwa la Kikanda litajadili kwa kina fursa za uwekezaji hapa nchini hasa kwenye maeneo ya nishati, usafirishaji, teknolojia ya habari na Mawasiliano na miradi ya maendeleo.

  Balozi Malika Berak amemhakikishia Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan kuwa kongamano hilo la kibiashara litawakutanisha pamoja wafanyabiashara Watanzania na wenzao wa Ufaransa katika kujadili na kubadilisha uzoefu katika masuala mbalimbali yakiwemo ya kibiashara kama hatua ya kuimarisha shughuli zao za kiuchumi.

  Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameipongeza Serikali ya Ufaransa kupitia kwa balozi wake hapa nchi kwa ufadhili wa miradi mbalimbali ya maendeleo hasa katika sekta ya maji na usafi wa mazingira, nishati na mapambano dhidi ya umaskini nchini.

  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amemhakikishia Balozi wa Ufaransa hapa nchini Malika Berat kuwa Tanzania itaendelea kudumisha na kuendeleza mahusiano yaliyopo kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa pande Mbili yaani Tanzania na Ufaransa.

  Makamu wa Rais pia amepongeza jitihada za Serikali kupitia Ubalozi wake hapa nchini za kuona umuhimu wa kuandaa Kongamano la kibiashara hapa nchini ambalo litatoa fursa kubwa kwa watalaamu wa sekta mbalimbali nchini kukutana na kujadiliana mambo kadhaa ikiwemo fursa za uwekezaji nchini.

  Amesisitiza kuwa Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakt John Magufuli inaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini kwa kupambana na vitendo vya rushwa kama hatua ya kuhamasisha wawekezaji wengi kuja kuwekeza hapa nchini.

  Makamu wa Rais amemweleza Balozi wa Ufarana hapa nchini kuwa milango ya ofisi yake ipo wazi muda wote hivyo kama watakwama sehemu yeyote katika kuandaa kongamano hilo amfahamishe haraka ili aweze kuchukua hatua haraka kusaidia mchakato huo kutokana na muhimu wa kongamano hilo hasa wakati huu ambapo Tanzania inataka kujenga uchumi wa viwanda nchini.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akikata utepe kuzindua rasmi Makao Makuu ya Wizara yaliyopo katika jengo la Masomo ya Biashara na Sheria katika Chuo Kikuu cha Dodoma ambako Wizara imehamia rasmi makao maku ya Serikali mkoani Dodoma

  Katibu Mkuu Prof sifuni Mchome akitoa maelezo mafupi kwa Mhe. Waziri Dkt Mwakyembe mara baada ya kukata utepe na kuzindua rasmi ofisi za wizara mjini Dodoma
  Katibu Mkuu Prof sifuni Mchome akitoa maelezo mafupi kwa Mhe. Waziri Dkt Mwakyembe mara baada ya kukata utepe na kuzindua rasmi ofisi za wizara mjini Dodoma
  Mhe. Waziri Dkt Mwakyembe akitia saini kitabu cha wageni mara baada ya kukata utepe na kuingia ndani ya jengo la Wizara ambako alizindua rasmi ofisi za wizara mjini Dodoma
  Mhe. Waziri Dkt Mwakyembe katika picha ya pamoja na watumishi na wageni wake mara baada ya kuzindua rasmi ofisi za wizara mjini Dodoma ambako wizara imehamia rasmi mkoani Dodoma
  Mhe. Waziri Dkt Mwakyembe aksalimiana na viongozi mbalimbali kabla ya kukata utepe na kuingia ndani ya jengo la Wizara ambako alizindua rasmi ofisi za wizara mjini Dodoma  ……………………………………………………………………..

  Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe amezindua rasmi Ofisi za wizara yake mkoani Dodoma na kuwataka Watumishi wa wizara waliohamia Makao Makuu ya Serikali, Dodoma kutekeleza majukumu yao kama inavyotakiwa.

  Dkt Mwakyembe amezindua rasmi makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria yaliopo mkoani Dodoma katika viunga vya Chuo Kikuu cha Dodoma baada ya wizara hiyo na watumishi wake 31 kuhamia rasmi makao makuu ya Serikali mkoani Dodoma.

  Baada ya uzinduzi huo Mhe. Mwakyembe alisema kitendo cha kuhamia mkoani DODOMA ni utekelezaji wa agizo la kuhamia makao makuu ya Serikali ambalo lilitolewa mwezi Julai mwaka 2016 na hivyo watumishi wanapaswa kutekeleza majukumu yao na kuwahudumia wananchi kama walivyokuwa Dar es salaam.

  Uzinduzi huo ulihudhuriwa na Jaji Mfawidhi Kanda ya Dodoma, Mkuu wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kanda ya Dodoma, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Dodoma, Prof Kikula na watumishi 31 wa wizara ambao wamehamia Dodoma katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa agizo hilo la Serikali.

  Awamu ya Kwanza yenye watumishi 31 wa wizara wakiongozwa na Waziri Dkt Dkt. Harrison Mwakyembe, Katibu Mkuu Prof. Sifuni Mchome na Naibu Katibu Mkuu Bw. Amon Mpanju imehamia rasmi mkoani Dodoma. Awamu ya pili na ya tatu zitafuata utaratibu ambao umewekwa na zoezi hilo linatarajiwa kukamilika mapema mwaka 2018.

  Kufuatia kuhama rasmi kwa ofisi za wizara sasa mawasiliano yote yatafanywa kupitia anuani ya Katibu Mkuu Sanduku la Posta 315 Dodoma, namba ya simu ni 026 2321680, nukushi ni 026 2321679 na baru pepe ni ile ile ya km@sheria.go.tz

  0 0

   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa(MB) akimsikiliza Mbunge wa Iramba Mashariki Mheshimiwa Allan Kiula wakati walipo kutana katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma Waziri Mkuu yupo Mkoani Dodoma katika kushiriki Mkutano wa Sita wa Bunge la Kumi na moja amabao umeanza leo Tarehe 31 January 2017

  Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

  0 0


  Mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo akiingia ukumbini tayari kwa kuanza rasmi kwa kongamano na waandishi wa habari na wadau mbalimbali wa maendeleo katika mkoa wa Arusha.
  Mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Gabriel Daqqaro akizungumza na waandishi wa habari na wadau wa maendeleo katika komgamano hilo.

  Mkurugenzi wa Kituo cha mikutano cha kimataifa AICC Elishilia Kaaya akizungumza na wadau mbalimbali waliohudhuria katika kongamano hilo na yeye kama mwenyeji wa eneo hilo akiwakaribisha katika kituo hicho.

  Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo akizungumza na waandishi wa habari katika kongamano ambalo aliwaahidi waandishi kuwa ataliiitisha kwaajili ya kujadili na kupata taarifa ya maendeleo katika mkoa wa Arusha pamoja na wadaumbalimbali.

  Mwenyekiti wa Arusha press club (APC) Akizungumza na katika kongamano hilo.
  Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega akizungumza katika kongamano hilo .
  Wa kwanza kushoto ni Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Charles Mkumbo ,akiwa kwenye kongamano katika kituo uliofanyika katika kituo cha kimataifa cha mikutano AICC katika ukumbi wa Mbayuwayu.
  Wadau wa Utalii kutoka TANAPA wakiwa katika kongamano la wadau wa habari mkoa wa Arusha .
  Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika kongamano hilo lililoitishwa na mkuu wa mkoa wa Arusha ili kuangalia na kujadili maendeleo ya mkoa kwa ujumla.
  Wa kwanza kushoto ni mwandishi wa habari wa gazeti la mwananchi Mussa Juma ,akifuatiwa na Omary Moyo wakiwa katika kongamano hilo.
  Mgeni rasmi mkuu wa mkoa pamoja na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari waliohudhuria kongamano hilo.Picha na Vero Ignatus Blog
  Mwandishi wa habari wa kituo cha luninga cha chanel ten Jamillah Omary akiwa na mkurugenzi mwenza wa Me Production ambaye pia ni mpiga picha wa kituo cha luninga cha ITV Anold Rweyemamu.Picha na Vero Ignatus Blog
  Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa jiji la Arusha Athuman Kihamia,aliyeko kushoto kwake ni mwenyekiti wa ccm mkoa ndugu Laizer


  Na.Vero Ignatus, Arusha.


  Mkuu wa mkoa wa Arusha Mashaka Mrisho Gambo amefungua Kongamana kutoa taarifa ya maendeleo katika mkoa wa Arusha ambapo kongamano hilo limewashirikisha wadau wa habari katika kuangalia na kutafakari na kupitia pamoja na kuangalia mpango mkakati wa maendeleo katika mkoa.

  Gambo amesema kuwa kongamano hilo lina lengo la kutoa mrejesho kwa Watanzania kupitia waandishi kwa kipindi cha miezi sita ,na kuangalia mambo gani serikali ikiyapa kipaumbele itaondoa changamoto mbalimbali katika jamii kwa ujumla.

  Aidha amesema kuwa utekelezaji wa shughuli za kiserikali katika mkoa wa Arusha kwa kipindi cha miezi sita hadi kufikia desemba 2016 umekuwa na mafanikio makubwa ,ambapo amesema kuwa hii ni kutokana na utamaduni wa kufanya na kutekeleza majukumu ya kazi kwa vitendo.

  Amesema utekelezaji huo umechangia katika kuboreka kwa maeneo mbalimbali ya sekta muhimu katika kukuza uchumi katika mkoa hasa pato la mkoa na wananchi moja kwa moja.

  “Katika kipindi hiki,miradi mingi ya maendeleo imetekelezwa na kupewa kipaumbele cha kutosha hivyo kwa namna moja kutekeleza mkakati wa Taifa wa kukuza uchumi na kuondoa umaskini (MKUKUTA II)katika mkoa na taifa kwa ujumla”alisema Gambo.

  Amesema kuwa Mkoa umesimamia utekelezwaji wa shughuli za serikali na kushuhudia mafanikio katika sekta za kilimo,afya,maji,barabara,mofugo,maliasili na nyinginezo kama takwimu zilivyowasilishwa .

  Amesema kuwa serikali imejipanga kuhangaika na wale wote ambao wanachochea migogoro kwa wananchi na kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi hatutawafumbia macho.

  Kwa upande wamafanikio utekelezaji wa mkoa kuanzia mwaka 2005 mkoa ulikuwa na shilingi 723,809 milioni kwa mwaka huo mkoa ulikuwa wa (9) katika kuchangia patao la Taifa,ambapo pato la mkazi lilikadiriwa kuwa shilingi 506,902 kwa mwaka sawa na shilingi 1,389 kwa siku.

  Kwa mwaka 2010 pato la mkoa wa Arusha lilikuwa shilingi 2,136,514milioni kwa kuchangia pato la taifa Arusha ilikuwa ya 7.mwaka huo pato la mkazi wa Arusha lilikuwa shilingi 1,283,361 kwa mwaka sawa na shilingi 3,516 kwa siku.

  Hadi mwaka 2015 pato la mkoa linakadiriwa kuwa shilingi 4,271,447milioni.
  kwa takwimu hizo pato la mkazi wa Arusha lilikuwashilingi 2,322,031 milioni kwa mwaka ni sawa na shilingi 6,361 kwa siku.

  0 0


  Meneja Mifumo ya Forodha toka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  Bw. Tinkasimile Felix (kushoto) akipokea tuzo ya ubunifu wa mradi TANCIS, ambao umeunganisha mifumo midogomidogo ya Forodha toka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga.  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah Kibonde, akilifurahia kombe hilo la ushindi wa jumla.
  Maofisa wa SSRA, David Nghambi (kushoto) na Ally Masaninga, wakiwa wamelishikilia kombe hilo.
  Ofisa Habari wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Freddy Maro, akizungumza wakati akimkaribisha Msemaji wa Serikali kutoka Kitengo cha Mawasiliano cha wizara hiyo, Mindi Kasiga.
  Msemaji wa Serikali kutoka Kitengo cha Mawasiliano cha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mindi Kasiga, akifurahia jambo pamoja na Ofisa Habari wa wizara hiyo, Freddy Maro, wakati wa hafla ya kukabidhi Tuzo kwa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) na TRA jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
  Baadhi ya Maofisa wa SSRA na TRA, wakiwa katika hafla ya kikabidhi tuzo hizo za Umoja wa Afrika (AU) kwa taasisi hizo.
  Msemaji wa Serikali kutoka Kitengo cha Mawasiliano cha wizara hiyo, Mindi Kasiga, akizungumza wakati wa kukabidhi tuzo za Umoja wa Afrika (AU) katika kipengele cha Ubunifu wa mradi wa kazidata ya Taifa ya Sekta ya Hifadhi ya Jamii na ushindi wa Jumla kwa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) jijini hivi karibuni.
  Baadhi ya waandishi wa habari, wakiwa katika hafla hiyo ya kukabidhi tuzo hizo.

  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah Kibonde, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Taasisi yake ilivyofanikiwa kupata tuzo ya Ubunifu wa mradi wa kazidata ya Taifa ya Sekta ya Hifadhi ya Jamii, iliyotolewa na Umoja wa Nchi za Afrika (AU).
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii, Bi. Sarah Kibonde, akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa tuzo hizo.
  Meneja Huduma za Mlipa Kodi toka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo akielezea namna Mamlaka ya Mapato ilivyofanikiwa kupata tuzo katika kipengele cha Ubunifu wa mradi TANCIS, ambao umeunganisha mifumo midogomidogo ya Forodha na kupelekea kurahisisha utoaji wa huduma na kuongeza ukusanyaji wa mapato, tuzo iliyotolewa na Umoja wa Nchi za Afrika (AU).
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah Kibonde (kulia) akiwa na Meneja Huduma za Mlipa Kodi toka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo.
  Msemaji wa Serikali kutoka Kitengo cha Mawasiliano cha wizara hiyo, Mindi Kasiga, akifafanua mambo mbalimbali wakati wa kukabidhi tuzo hizo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah Kibonde na katikati ni Meneja Huduma za Mlipa Kodi toka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Richard Kayombo.


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akiangalia ubora wa nondo zinazozalishwa kwenye kiwanda cha kuzalishia chuma cha Uniqeu Steel Meel wakati waa  ziara yake ya kukaagua maendeleo ya viwanda mbalimbali jijini hapa ili kuona namna ya ufanisi wake na changamoto zinazowakabili.
  Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella wa pili kutoka kushoto akimuonyesha kitu mmoja wa viongozi wa kiwanda cha kuzalishia chuma cha Uniqeu Steel Meel wakati waa  ziara yake ya kukaagua maendeleo ya viwanda mbalimbali jijini hapa ili kuona namna ya ufanisi wake na changamoto zinazowakabili(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

  Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye kiwanda cha kuzalishia chuma cha Mjini Tanga cha (Uniqeu Steel Meel) wakati wa ziara yake ya kukaagua maendeleo ya viwanda mbalimbali jijini hapa ili kuona namna ya ufanisi wake na changamoto zinazowakabili.
  Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella wa pili kutoka kushoto akiteta jambo na mmoja kati ya wamiliki wa kiwanda cha kuzalisha chuma cha (Uniqeu Steel Meel) wakati wa ziara yake ya kukaagua maendeleo ya viwanda mbalimbali jijini hapa ili kuona namna ya ufanisi wake na changamoto zinazowakabili kulia ni Mhasibu wa kiwanda hicho,Sikander Husein Omari na Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa.
  Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella katikati akimsikiliza kwa umakini Mhasibu wa kiwanda cha chuma cha (Uniqeu Steel Meel),Sikander Hussein Omari  wakati wa ziara yake ya kukaagua maendeleo ya viwanda mbalimbali jijini hapa ili kuona namna ya ufanisi wake na changamoto zinazowakabili.
  Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella  katikati akionyeshwa namna chuma zinavyozalishwa kwenye kiwanda cha Uniqeu Steel Meel) wakati wa ziara yake ya kukaagua maendeleo ya viwanda mbalimbali jijini hapa ili kuona namna ya ufanisi wake na changamoto zinazowakabili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa.
  Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella  katikati akitazama namna chuma zinazozalishwa kwenye kiwanda cha chuma cha Uniqeu Steel Meel) wakati waa  ziara yake ya kukaagua maendeleo ya viwanda mbalimbali jijini hapa ili kuona namna ya ufanisi wake na changamoto zinazowakabili.

  Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella  akitazama namna chuma akiwa amepanda kwenye chuma hizo kuona ubora wake  wakati waa  ziara yake ya kukaagua maendeleo ya viwanda mbalimbali jijini hapa ili kuona namna ya ufanisi wake na changamoto zinazowakabili.
  Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akiangalia ubora wa nondo zinazozalishwa kwenye kiwanda cha kuzalishia chuma cha Uniqeu Steel Meel wakati waa  ziara yake ya kukaagua maendeleo ya viwanda mbalimbali jijini hapa ili kuona namna ya ufanisi wake na changamoto zinazowakabili.


  0 0
  Dodoma, Jumanne, Januari 31, 2017:  

  Serikali leo imeainisha utekelezaji na kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi katika sekta mbalimbali katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa Sita wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Majibu ya Serikali kwa baadhi ya hoja ni kama ifuatavyo:

                            Ujenzi Nyumba za Walimu.

  Akijibu hoja kuhusu ujenzi wa nyumba za walimu, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo, ameliambia Bunge kuwa Serikali ilitenga kiasi cha Sh. Bilioni 13.9 katika Bajeti ya mwaka huu kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu wa Sekondari, na Shilingi bilioni 11.4 kwa nyumba za walimu wa Shule za Msingi.

  Aidha, Waziri Jafo ameeleza kuwa tayari nyumba 146 za walimu zimeshajengwa nchini kupitia Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari. Pia amezungumzia Serikali kuanza kulipa madeni ya walimu.

                               Ujenzi wa Viwanda Nchini

  Akijibu swali kuhusu uwekezaji wa viwanda nchini hususani mkoani Tabora ambako kuna kilimo cha Tumbaku na maeneo mengine yenye malighafi, Mhandisi Edwin Ngonyani kwa niaba ya Waziri wa Viwanda ameliambia Bunge kuwa tayari Serikali imeshafanya mazungumzo na wawekezaji kutoka Vietnam na kuzitaka Halmashauri zote nchini kuendelea kuitikia wito wa kutenga maeneo ya uwekezaji.

  “Kituo cha uwekezaji Nchini (TIC) kimepewa maelekezo maalum kunadi fursa hii kwa wawekezaji katika sekta ya tumbaku na sigara hapa nchini,” alisema Mhandisi Ngonyani ambaye pia ni Naibu Waziri, Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

                     Tupende Bidhaa Zetu.

  Akijibu hoja kuhusu bidhaa nyingi za Kenya kuingia nchini, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Suzan Kolimba amesema moja ya changamoto inazozikumba bidhaa za Tanzania ni wananchi wake kupenda vya nje.

  “Katika kukabiliana na changamoto hiyo, Serikali iliunda Kamati ya Kitaifa ya Kudhibiti na Kusimamia Uondoaji wa wa Vikwazo visivyo vya Kiforodha na kuhamasisha wafanyabiashara nchini kuzalisha bidhaa zenye ubora,” alisema.

                               Serikali yagharamia 100% umeme vijijini  

  Serikali imesisitiza kuwa inagharamia ujenzi wa umeme vijijini kupitia Wakala wa Kusambaza Umeme Vijijini (REA) kwa asilimia 100. Akijibu maswali ya wabunge, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, alisema wananchi wanalazimika kuchangia Sh. 27,000 tu ambazo ni gharama za kodi ili waunganishiwe huduma hiyo wakati mradi ukiwa unaendelea.

  “Lengo ni kuhamasisha na kuwawezesha wananchi wa vijijini wenye vipato vidogo kuweza kupata huduma za umeme kwa gharama nafuu,” alisema akisisitiza kuwa wale ambao huomba huduma hiyo baada ya wataalam wa REA kumaliza kazi yao ndio hulazimika kulipia umeme huo kwa Sh. 177,000 tu badala ya Sh. 320,960/- wanazotozwa wakazi wa mijini kwa umbali usiohitaji nguzo.  

                                   Bei ya maji kupungua

  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge amesema Serikali itaendelea kupunguza gharama za maji nchini hasa vijijini kadiri gharama za umeme zitakavyoendelea kupungua hasa wakati huu nchi inapoingia katika uchumi wa gesi.

  Aliongeza kuwa kwa upande wa vijijini miradi ya umeme wa jua na nishati nyingine za bei nafuu pia itasaidia kupunguza gharama za umeme na kusaidia wananchi kupata maji katika miradi mingi inayondelea sasa nchini.

                                     Madai ya Unyanyasaji Zanzibar

  Serikali imewataka wananchi wote wanaodai kufanyiwa unyanyasaji na vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kutoa taarifa za matukio hayo polisi ili hatua stahiki zichukuliwe.

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba alisema kwa kuwa hakuna  tarifa za kuripotiwa kwa matukio hayo katika kituo chochote cha Polisi, atachukua pia hatua za kutuma maafisa wake kufanya uchunguzi zaidi.

   


  Dkt. Hassan Abbasi,
  Mkurugenzi Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali

older | 1 | .... | 1122 | 1123 | (Page 1124) | 1125 | 1126 | .... | 1897 | newer