Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

MTANDAO WA WADAU WA ASASI ZA KIRAIA UNAOTETEA MAREKEBISHO YA SHERIA NA SERA IHUSUYO USALAMA BARABARANI WAKUTANA NA WABUNGE

$
0
0
Mtandao wa wadau kutoka asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya sheria na sera ihusuyo usalama barabarani Tanzania siku ya tarehe 26 na 27 Januari, 2017 wamefanikiwa kukaa na baadhi ya wabunge kutoka kamati ya mambo ya nje, Ulinzi na usalama, Katiba na sheria pamoja na miundo mbinu katika kikao kilichoongozwa chini ya mwenyekiti wake Mbunge wa Muheza Mheshimiwa Balozi Adadi Rajabu, pamoja walionyesha ushirikiano wao katika kuboresha usalama bararani kwa maendeleo ya Taifa letu.

Wajumbe wa kikao husika walipata nafasi ya kusikiliza mada mbalimbali kuhusiana na masuala ya usalama barabarani na hali ilivyo sasa, ambapo ilielezwa kuwa hali ilivyo kulingana na takwimu zinaonyesha kuwa takribani watu milioni 1.25 hufariki dunia kila mwaka kutokana na ajali za barabarani, aidha, watu milioni 20 hadi 50 hujeruhiwa na wengine hupata ulemavu wa kudumu wengi wao wakiwa ni vijana wenye nguvu kazi ya Taifa. Hii ni kutokana na takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) 2015.
Kwa upande waTanzania Bara, taarifa kutoka jeshi la polisi Kikosi cha Usalama Barabarani inaonyesha kwamba, kwa mwaka 2016 jumla ya watu 3,256 walipoteza maisha kutokana na ajali za barabarani. Katika vifo hivyo wanaume ni 2,580 na wanawake ni 676. Aidha kumekuwa na majeruhi 8,958 kati yao wanaume ni 6,470 na wanawake 2,488. Wakati vyombo vya moto vilivyoongoza katika ajali ni magari binafsi ambayo idadi yake 3,649 ikifuatiwa na pikipiki kwa idadi ya 2,544.

Kutokana na idadi kubwa ya vifo vinavyotokana na ajali za barabarani nchini, Mtandao wa wadau kutoka asasi za kiraia unaotetea marekebisho ya sheria na sera zinazohusu usalama barabarani Tanzania umeona umuhimu na kuchukulia jambo hili kulifanyia kazi kwa kina. Tafiti zinaonyesha kwamba asilimia 76 ya ajali zote zinatokana na vyanzo vya kibinadamu kama vile Ulevi, Mwendokasi, Uzembe, Uchovu, kupuuzia au kutokuwa makini uwapo barabarani na kutokutii sheria za Usalama Barabarani. Tuna amini matendo haya ya kibinaadamu yana dhibitika kisheria, hivyo basi tunaisihi serikali kuboresha sheria.
Kama wadau wa Usalama Barabarani, tunadhani kuna umuhimu wa sheria sasa kuboreshwa, na hivyo utashi wa kisiasa unatakiwa. Ndiyo maana tukaitisha majadiliano ya pamoja na Wabunge pamoja na wadau mbalimbali wa Usalama Barabarani ili kuona ni kwa namna gani tunaweza kuleta mabadiliko ya sheria kwa ufanisi na kwa haraka.

Wabunge waliohudhuri kikao hiki kwa ujumla wao, waliona umuhimu wa kuwa na mikakati ya kitaifa ya kupunguza ajali na walikiri kwa nia moja na kukubali kuunda Mtandao wa Wabunge wanaotetea usalama barabarani.

Maeneo ambayo tunayapa kipaumbele katika maboresho ya sheria ni kama haya yafuatayo: a) Matumizi ya mikanda; Sheria ya sasa ya Usalama barabarani inasema ni kosa kisheria kwa dereva na abiria anayekaa kiti cha mbele kutokufunga mkanda wakati wa safari lakini sheria hiyo hiyo haisemi chochote kwa abiria wanaokaa kiti cha nyuma.
Utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) unasema kuwa iwapo ajali ikitokea madhara/athari kwa abiria wa kiti cha mbele itapungua kwa 50% na kwa abiria wa nyuma madhara yatapungua kwa 70%. Kanuni zilizotungwa na SUMATRA zinataka abiria wote wafunge mkanda ila kwa vile sheria mama (Road Traffic Act of 1973) ipo kimya katika eneo hili utekelezaji wa kanuni unakuwa mgumu.

Hivyo basi ni rai yetu sheria hiyo ibadilishwe na kuwataka abiria wote wanaokuwa katika chombo cha usafiri wa kibiashara au binafsi kufunga mkanda wakati wote wa safari. b) Matumizi sahihi ya kofia ngumu; Sheria ya sasa ya usalama barabarani inasema kuwa ni kosa kwa muendesha pikipiki kutokuvaa kofia ngumu wakati wa kuendesha chombo hicho. Lakini sheria hiyohiyo haisemi chochote kwa abiria anayepanda katika chombo hicho.

Vilevile pamoja na kuanisha kosa kwa dereva wa pikipiki kutokuvaa kofia ngumu lakini pia sheria haielezi ni jinsi gani kofia inatakiwa kuvaliwa na aina maalum ya kofia inayotakiwa kuvaliwa. Kwa mujibu wa Utafiti wa Shirika la Afya Duniani (WHO) unaonyesha kuwa iwapo ajali itatokea madhara yanayotokea kwa kutovaa kofia maalum na kwa usahihi ni makubwa sana ukilinganisha na kofia hiyo ikivaliwa kwa usahihi. Hivyo basi ukizingatia kuwa sasa hivi usafiri wa pikipiki umekuwa unatumika kwa kiasi kikubwa (public transport) hivyo ni rai yetu sheria hiyo ifanyiwe maboresho na kuweka kuwa ni sheria kwa mtu yoyote anayepanda pikipiki kuvaa kofia ngumu na kwa usahihi.

c) Ulevi: Sheria ya sasa ya usalama barabarani inasema kuwa itakuwa kosa kwa mtu yoyote kuendesha chombo cha moto akiwa na kiwango cha kilevi katika damu yake kinachozidi asilimia 0.08% katika mfumo wa mwili. Kiwango hiki ni kikubwa sana kikilinganishwa na tafiti zilizofanywa na Shirika la Afya Duniani na kupendekeza kiwango cha asilimia 0.05% kwa dereva aliyebobea (experienced driver) na asilimia 0.02% kwa dereva mchanga (young driver). Hivyo basi ni rai yetu kuwa sheria ifanyiwe marekebisho ili iendane na kiwango cha sasa cha kimataifa kilichofanyiwa utafiti.

d) Mwendo kasi (Speeding): Mwendokasi umeendelea kuwa sababu kubwa ya ajali zinazogharimu uhai wa watu wengi. Sheria yetu inayo mapungufu kadhaa pamoja na juhudi nyingi za Jeshi la Polisi na wadau wengine kutaka kudhibiti jambo hili limeendelea kuwa tatizo. Adhabu zisizokidhi wala kuleta hofu kwa maderava wasiotaka kutii zimeendelea kufifisha juhudi za kudhibiti tatizo hili.

Tunatoa wito kwa watunga sera kushirikiana zaidi na wadau kuuelimisha umma katika eneo la uhusiano wa adhabu zitokanazo na makosa ya usalama barabarani na ongezeko la ajali. Pia sheria kufanyiwa maboresho na kuangalia kwa upya mianya iliyopo.

TAMKO HILI LIMETOLEWA LEO NA MTANDAO WA WADAU KUTOKA ASASI ZA KIRAIA:
1. TAWLA
2. TAMWA
3. WLAC
4. TCRF
5. TLS
6. TMF
7. RSA
8. AMEND TANZANIA
9. SHIVYAWATA
10. TABOA &
11. SAFE SPEED FOUNDATION

MAJALIWA ATEMBELEAWA NYUMBANI KWAKE NA MFANYABIASHARA SABODO

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na Mfanyabiashara Maarufu nchini, Mustafa Sabodo ambaye leo Januari 29, 2017  alikwenda kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam kumtembela.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na mkewe Mary wakizungumza na Mfanyabaishara Maarufu nchini, Mustafa Sabodo ambaye  leo Januari 29, 2017 alikwenda kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salam kumtembelea 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na  Mfanyabiashara Maarufu nchini, Mustafa Sabodo ambaye Januari 29, 2017 alikwenda kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam kumtembelea. 

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na  Mfanyabiashara Maarufu nchini, Mustafa Sabodo ambaye Januari 29, 2017 alikwenda kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam kumtembelea.

Mkurugenzi wa Uchaguzi, Kailima afanya mahojiano na TBC

$
0
0
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani (kulia) akionesha moja ya fomu zinazotumika katika Uchaguzi wakati akifanya mahojiano na Mtangazaji Mwandamizi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Shaban Kissu.
Mtangazaji Mwandamizi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Shaban Kissu (kushoto) akifanya mahojiano na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani (kulia) akifafanua jambo.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mtangazaji Mwandamizi wa TBC, sHaban Kissu.Picha na Hussein Makame, NEC

KUKANUSHA TAARIFA ILIYOANDIKWA NA GAZETI LA RAIA MWEMA KUHUSU KUONGEZWA MUDA WA LESENI ZA VITALU VYA UWINDAJI BILA KUFUATA TARATIBU

$
0
0
 Wizara ya Maliasili na Utalii inakanusha taarifa iliyoandikwa na gazeti la Raia Mwema Toleo Na. 494 (ISSN 1821-6250) la Jumatano tarehe 25-31 Januari, 2017 ikiwa na kichwa cha habari “Waziri Maghembe Matatani”. Habari hiyo imeeleza kuwa, Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe anadaiwa kuongeza muda wa leseni za vitalu vya uwindaji kwa kampuni za uwindaji wa kitalii kinyume na taratibu.
Aidha, habari hiyo imeeleza kuwa waziri hakufuata utaratibu uliowekwa katika kifungu cha 38 (6) cha Sheria ya Uhifadhi Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009 ambayo inaweka utaratibu wa kufuatwa kabla waziri hajatoa leseni upya. Pa, habari hiyo imeeleza kuwa sheria hiyo inataka itangazwe kwenye magazeti utaratibu wa kuomba vitalu kwa waombaji pamoja na kufanyiwa tathmini.
Vilevile, habari hiyo imeeleza kuwa waziri anatakiwa kushauriwa na chombo ambacho ndicho hufanyia tathmini kampuni hizo. Taarifa hiyo imeripoti kuwa hapo awali kulikuwa na kamati ya kumshauri waziri ambayo ilivunjwa mwaka 2012 na aliyekuwa waziri wa Wizara hiyo, Khamis Kagasheki na hivyo kuhoji uhalali wa kufanya maamuzi bila kushauriwa na chombo hicho.
Habari hiyo siyo ya kweli, kwani Waziri hakutoa leseni za umiliki wa vitalu vipya bali ameongeza muda wa umiliki wa vitalu kwa mujibu wa kifungu cha 38 (8) cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009 sambamba na kanuni ya 16 ya Kanuni za Uwindaji wa Kitalii za mwaka 2015. Sheria na Kanuni hiyo inaelezea utaratibu wa kuongeza muda wa umiliki wa vitalu kwa wale walioomba kuendelea na umiliki wa vitalu vya awali (renewal of hunting block).
Waziri kabla ya kuongeza muda wa umiliki wa vitalu (renewal) alikaribisha maombi kwa wale wanaotaka kuongezewa muda wa umiliki wa vitalu wanavyovimiliki kwa mujibu wa Sheria tajwa hapo juu kwa barua yenye Kumb. Na. CHA.79/519/47 ya terehe 22 Aprili, 2016. Aidha maombi hayo yalipitiwa na Kamati ya Ushauri ya Ugawaji wa Vitalu vya Uwindaji ambayo ipo kisheria na iliteuliwa Septemba 2013, kinyume na madai ya mwandishi kuwa Kamati hiyo haipo. Baada ya tathmini ya maombi hayo, Kamati hiyo ilimshauri Waziri kwa mujibu wa sheria.
Kwa kufuata utaratibu ulioanishwa katika Kifungu cha 38 (8) na (9) cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori, kifungu hiki kinampa Mamlaka Waziri kuongeza muda wa umiliki wa vitalu (Renew of hunting blocks). Kanuni ya 16 kanuni ndogo ya (1), (2), (3), (4), (5), (7), (8), (9) na (10) ya Kanuni za Uwindaji wa Kitalii  zinatoa utaratibu wa kufuatwa wakati wa kuongeza muda wa umiliki wa vitalu kwa muhula mwingine wa uwindaji na utaratibu huo umefuatwa.
Kwa kuzingatia utaratibu huo, wamiliki wa sasa wa vitalu kama Kanuni zinavyoelekeza, waliwasilisha maombi yao Wizarani. Idara ya Wanyamapori ilipitia maombi hayo na kuwasilisha kwenye Kamati ya Ushauri ya Ugawaji wa Vitalu vya Uwindaji. Kamati hiyo ilipitia maombi hayo tarehe 26 hadi 27 Julai 2016 na tarehe 13 Januari 2017. Hivyo, baada ya Kamati kukamilisha taratibu zote na kujiridhisha iliwasilisha ushauri wake kwa Mhe. Waziri.
Kifungu cha 38 (6) cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori alichokitaja mwandishi wa gazeti hilo, kinaeleza utaratibu wa ugawaji wa vitalu kwa waombaji wapya na siyo kwa wale wanaoomba kuendelea na umiliki wa vitalu kwa msimu mwingine (renewal).
Uongezaji wa muda wa umiliki wa vitalu vya uwindaji ulifuata Sheria, Kanuni na Taratibu, Hivyo tunawoamba wananchi wapuuze habari hiyo kwani mwandishi alikusudia kuupotosha umma kwa kunukuu na kutafsiri vifungu vya Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori isivyo sahihi.
Imetolewa na,
KATIBU MKUU
29 Januari, 2017

WACHEZAJI WANAWAKE WAJIPANGA MIAKA 10 YA LUGALO GOLF CLUB

$
0
0
NAHODHA WA ZAMANI WA TIMU YA TAIFA YA WANAWAKE HAWA WANYENCHE AKIWA KATIKA MAZOEZI KUJIANDAA NA MASHINDANO YA MAADHIMISHO YA MIAKA 10 YA KLABU YA GOLF YA JWTZ YA LUGALO FEBRUARI MWAKA HUU JIJINI DAR ES SALAAM(PICHA NA LUTENI SELEMANI SEMUNYU)

MCHEZAJI WA KLABU YA LUGALO VICKY ELIAS ( WAKWANZA KUSHOTO) AKIPIGA MPIRA WAKATI WA MAZOEZI KUJIANDAA NA MAADHIMISHO YA MIAKA 10 YA KLABU HIYO JIJINI DAR ES SALAAM WANAOMTAZAMA NA HAWA WANYENCHE (KATIKATI) NA SALIM MWENYENZA(KULIA).(PICHA NA LUTENI SELEMANI SEMUNYU).

MCHEZAJI HABIBA LIKULI WA KLABU YA LUGALO AKIWA KATIKA MAZOEZI KUJIANDAA NA MASHINDANO YA MAADHIMISHO YA MIAKA 10 YA KLABU YA GOFU YA JWTZ YANAYOTARAJIWA KUFANYIKA FEBRUARI JIJINI DAR ES SALAAM.(PICHA NA LUTENI SELEMANI SEMUNYU).
MCHEZAJI NICHOLOUS CHITANDA( KATIKATI)WA KLABU YA LUGALO AKIWA KATIKA MAZOEZI KUJIANDAA NA MASHINDANO YA MAADHIMISHO YA MIAKA 10 YA KLABU YA GOFU YA JWTZ YANAYOTARAJIWA KUFANYIKA FEBRUARI JIJINI DAR ES SALAAM.(PICHA NA LUTENI SELEMANI SEMUNYU).

……………………………………………………………………………
Na Luteni Selemani Semunyu JWTZ

IDADI ya Wanawake wanaojiandaa na mashindano ya miaka 10 ya klabu ya golf ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania imeongezeka na kuongeza joto la maadhimisho ya klabu hiyo yanayotarajiwa kufanyika mwezi Februari Jijini Dar es salaam.

Mmoja wa wachezaji hao ni aliyekuwa nahodha wa timu ya Taifa ya Wanawake Hawa Wanyenche ambaye kwa muda mrefu hakuwa akionekana viwanjani kucheza lakini sasa ameibukia katika klabu ya Lugalo.

Akizungumza wakati wa mazoezi yake katika klabu ya lugalo Hawa alisema anaona kiwango chake kinaanza kurejea kutokana na kutokuwa uwanjani muda mrefu na anaamini kuibuka na ushindi katika mashindano hayo na yeyote yajayo ili kurejesha heshima yake.

“ Unajua ni muda mrefu sijaingia uwanjani na falsafa yangu ni kuishinda sio kushindwa na siri ya kushinda ni mazoezi ndio maana nimeanza mapema hivyo wanawake wengine wanajua wako vizuri katika golf waje tupambane”. Alisema Hawa.

Aliongeza kuwa ni wakati muafaka kwa Wachezaji wengine wa Vilabu vingine nao kujipanga na kuhakikisha wanashiriki ili kufanikisha mashindano lakini pia kuzihirisha uwezo wao.

Naye Mchezaji Vicky Elias alisema muda umekwisha na ukizingatia kuna uwezekano wa wachezaji kutoka katika nchi mbalimbali kuja kushiriki michuano hiyo hivyo mazoezi pekee ndio yatakayowafanya kuibuka na Ushindi.

“ Wachezaji wengi wamekamia mashindano haya lakin I nitashinda ingawa nikishindwa nitakubaliana kwa kuwa ni moja ya matokeo katika Golf kwani mchezo huo hautabiriki” Alisema Vicky.

Kwa Upande wake mchezaji Chipukizi Habiba Likuli alisema kikubwa ni kukabiliana na ushindani na kuibuka na ushindi na kulibakiza kombe la historia kwa klabu.

“ Mashindano yaliyopita nilicheza katika kundi la Watoto Junior lakini kutokana naKiwango changu ninaimani nitakuwa na uwezo wa kuchezea kundi la Wanawake Ladies katika mashindano hayo kama kanuni zitaruhusu” Alisema Habiba.

Kwa upande wake Kapteni wa Klabu ya golf ya Lugalo Kapteni Japhet Masai alisema katika kuyapa uzito mashindano hayo wamepeleka mialiko katika nchi za Zambia,Kenya,Malawi ,Zimbambwe , Rwanda na Uganda.

Aliongeza kuwa tarehe na mgeni Rasmi katika Mashindano hayo anatarajiwa kutangazwa na mwenyekiti wa Klabu hiyo Brigedia Jenerali Michael Luwongo Jumanne saa nne katika Klabu hiyo.

Wachimbaji 15 waliokuwa wamefukiwa na kifusi katika mgodi wa RZ Nyarugusu, Mkoani Geita waokolewa

$
0
0
Wachimbaji 15 waliokuwa wamefukiwa na kifusi katika mgodi wa RZ uliopo Nyarugusu, Mkoani Geita wameokolewa wote wakiwa asubuhi ya leo. Wachimbaji hao walikumbwa na kadhia hiyo, siku mbili zilizopita baada ya udongo kufunika sehemu ya kutokea. ila kwa juhudi mbalimbali walizokuwa wakizifanya, waliweza kuwasiliana na waliokuwa nje ya mgodi na hatimae kufanikiwa kuokolewa leo asubuhi.
Sehemu ya Askari Polisi na wa Kikosi cha uokoaji wakiendelea na zoezi la uokozi kwa waathirika wa tukio hilo, asubuhi ya leo.
Zoezi la uokoaji kwa ndugu zetu hao lilizovyofanikiwa kwa jitihada za vikosi vya usalama na uokoaji wakisaidiana na wananchi.
Baadhi ya Raia wa kigeni wenye asili ya China wakimjulia hali mwenzao ambaye alikuwa ni mmoja wa walikumbwa na dhoruba hilo la kufukiwa na kifusi katika Mgodi wa RZ Nyarugusu, Mkoani Geita.
 Zoezi la uokoaji kwa ndugu zetu hao lilizovyofanikiwa kwa jitihada za vikosi vya usalama na uokoaji wakisaidiana na wananchi.

ZIARA YA KIKAZI YA NAIBU WAZIRI MASAUNI WILAYANI NKASI KUTEMBELEA IDARA ZA WIZARA

$
0
0
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na maafisa wa Jeshi la Polisi baada ya kuwasili wilayani Nkasi kwa ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kupitia shughuli zinazofanywa na idara zilizopo ndani ya wizara yake na kubaini changamoto wanazokutana nazo na kuzitafutia ufumbuzi.Kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Said Mtanda. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Afisa Uhamiaji Wilaya ya Nkasi, Juma Khamis Ali (kushoto), akikabidhi taarifa ya Idara yake kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo wilayani humo ikiwa na lengo la kupitia shughuli zinazofanywa na idara hizo na kubaini changamoto wanazokutana nazo na kuzitafutia ufumbuzi.Wengine pichani ni wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wilayani humo. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wafanyakazi wa idara zilizopo ndani ya wizara yake(hawapo pichani), wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya wilayani Nkasi ikiwa na lengo la kupitia shughuli zinazofanywa na idara hizo na kubaini changamoto wanazokutana nazo na kuzitafutia ufumbuzi. Wengine pichani ni wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wilayani humo (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Said Mtanda(kulia) akizungumza na wafanyakazi wa idara zilizopo ndani ya wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (hawapo pichani),wakati akimkaribisha Naibu Waziri wa Wizara hiyo ,Mhandisi Hamad Masauni(wapili kulia) wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya Naibu Waziri huyo wilayani humo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(wakwanza kulia), akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kikao cha ndani na watumishi wa idara zilizopo chini ya wizara yake wilayani Nkasi.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

JUMUIA YA WAZAZI WILAYA YA KINONDONI YAADHIMISHA MIAKA 40 YA CCM KWA KUFANYA USAFI NA KUTOA VFAA KWENYE ZAHANATI YA KIBAMBA, DAR ES SALAAM

$
0
0
Jumuia ya Wazazi wilaya ya Kinondoni, jana, Januari 28, 2017, imeadhimisha miaka 40 ya kuzaliwa kwa CCM, kwa kufanya usafi na kutoa vifaa mbalimbali kweye zahanati ya Kibamba, Ubugo jijini Dar es Saaam. Pichani, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi ya CCM, wilaya hiyo, Lucas Mgonja (wapili kulia), akikabidhi ufagio kwa Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo, Mwahawa Kiroboto. Kushoto ni Muuguzi Mfawishi wa Zahanati hiyo, Jesca Mpolanigwa.
Lucas Mgonja akikabidhi sabuni
Lucas Mgonja akikabidhi kifaa cha kupima homa 
Lucas akikabidhi ndoo
Mgonja akikabidhi sabuni ya kufanyia usafi
Mganga Mfawidhi akitoa neno la shukurani baada ya kukabidhiwa vifaa na Mgonja
Mgonja akizungumza na Mwandishi wa habari wa Clouds Tv, Salum Mwinyimkuu, baada ya kukabidhi vifaa
Mgonja (Wapili kushoto) akiongoza badhi ya viongozi wa Jumuia ya wazazi wilaya ya Kinondoni kukata miti na kufyeka nyasi kwenye Zahanati hiyo
Badhi ya viongozi wa Jumuia ya wazazi wilaya ya Kinondoni wakishiriki kufanya usafi kwenye Zahanati hiyo
Mwanahawa na Mpolanigwa wakifanya usafi kwenye Zahanati hiyo
Baadhi ya viongozi wa Jumuia ya wazazi Kinondoni wakifanya usafi kwenye Zahanati hiyo
Mgonja akizungumza kabla ya yeye na ujumbe wake kuondoka kwenye Zahanati hiyo
Baadhi ya viongozi na wanachama wa CCM kutoka Jumuia ya Wazazi wilaya ya Kinodoni wakimsikiliza Mgonja kwenye Zahanati hiyo kabla ya kuondoka
Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Stanley Mkandawile akimpongeza Mwenyekiti wa Jumuia ya wazazi Jimbo la Ubungo, Justine Sangu, baada ya kufanya usafi na kutoa vifaa kwenye zahanati hiyo
Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Stanley Mkandawile akimpongeza Mwenyekiti wa Jumuia ya wazazi Wilaya ya Kinondoni, Lucas Mgonja, baada ya kufanya usafi na kutoa vifaa kwenye zahanati hiyo. Picha zote na Bashir Nkoromo).

RAIS DKT. MAGUFULI AHUDHURIA KIKAO CHA UMOJA WA AFRIKA (AU) MJINI ADDIS ABABA ETHIOPIA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati alipokuwa kwenye mojawapo ya vikao vya Umoja wa Afrika (AU) vinavyofanyika katika Makao makuu yake mjini Addis Ababa nchini Ethipia. PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Manuel Olveira Guterres wakati alipokuwa kwenye mojawapo ya vikao vya Umoja wa Afrika (AU) vinavyofanyika katika Makao makuu yake mjini Addis Ababa nchini Ethipia. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga.

MLIMBWENDE WA SHINDANO LA MISS KIBOSHO 2017 JIJINI MWANZA APATIKANA.

$
0
0
Baada ya mtifuano mkali wa kumtafuta mlimbwende wa shindano la MISS KIBOSHO 2017 kufanyika kwa mara ya kwanza usiku wa ijumaa Januari 27,2017 na jana jumamosi Januari 28,2017 katika Ukumbi wa Kibosho Luxury Bar Kiseke Ilemela Jijini Mwanza, hatimaye mshindi amejulikana.

Mshindi wa shindano hilo lililofana vyema alikuwa ni Kephlin Jacob (katikati), nafasi ya pili ni Aida Gazar (kulia) na nafasi ya tatu ni Caren Nestory (kushoto), ambapo wanyange hao walifanikiwa kupenya na kuibuka na ushini huo miongoni mwa wanyange 10 walioshiriki shinano hilo.

Miss Kibosho 2017 iliandaliwa na Raju Entertainment kwa ushirikiano wa karibu na Kibosho Luxury Bar and Guest House Kiseke, Wema Salon, Mama Ngenda Sakon, Top Model na Hangano Cultural Group lengo lake ikiwa ni kukuza vipaji vya urembo kitaifa na kimataifa.
Na Binagi Media Group
Miss Kibosho 2017 Kephlin Jacob (katikati), Miss Kibosho 2017 nambari mbili, Aida Gazar (kulia) na Miss Kibosho nambari tatu ni Caren Nestory (kushoto).
Awali hatua ya tatu bora ilikwena kwa washiriki, Caren Nestory (kushoto), Kephlin Jacob (katikati) na Aida Gazar (kulia)
Awali washiriki waliotinga nafasi tabo bora ni Caren Nestory, Jackline Moses, Denzry Michael, Kelphine Jacob na Aida Gazar.
Washiriki wote 10 wa Miss Kibosho 2017 ambao ni Caren Nestory, Dorice Ezra, Jullieth Michael, Elizabeth Faustine, Christina Lucas, Nasra Ramadhan, Jacline Moses, Denzry Michael, Kephlin Jacob na Aida Gazar.

MTUMISHI WA UMMA ATAKAYESHINDWA KUWASILISHA SIFA ZAKE ZA ELIMU, KUJIFUKUZISHA KAZI IFIKAPO MACHI 1 / 2017.

$
0
0
Mtumishi wa Umma atakayeshindwa kuwasilisha cheti cha elimu na taaluma au “Index number” ya mtihani ili zihakikiwe na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), itakapofika tarehe 1 Machi, 2017 atakua kajiondoa kazini mwenyewe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) alibainisha hayo mwishoni mwa wiki wakati akifungua mkutano wa Watendaji Wakuu wa Wakala za Serikali jijini Dar es salaam.
“Watendaji Wakuu ninawaomba msimamie uhakiki wa vyeti ili watumishi wenu wafanye kazi kwa sifa stahiki” Waziri Kairuki alisisitiza.
Aliongeza Serikali ilisitisha ajira mpya ili kupisha zoezi la kuondoa Watumishi hewa, zoezi ambalo limefika ukingoni na siku za karibuni ajira zitarudishwa.
Waziri Kairuki aliwataka Watendaji Wakuu kuweka mikakati ya kuepuka watumishi hewa na kusimamia kwa dhati kwasababu jambo hilo limeumiza na kupoteza rasilimalifedha nyingi za Serikali.
Alisema anatambua kuna Wakala zenye upungufu wa Watumishi hivyo zinaingia gharama kubwa za kuajiri wafanyakazi wa mikataba, hata hivyo alielekeza kila Mtendaji Mkuu ajiridhishe kwa kuandaa taarifa ya mahitaji halisi ya Watumishi.
Waziri Kairuki, pamoja na hilo alielekeza Wakala zenye Watumishi wa mikataba zifanye tathmini na kuhakiki kama kweli watumishi hao wanahitajika kwa kuwa eneo hilo ni moja ya maeneo yenye ajira za mashaka kwa baadhi ya Taasisi.
Waziri Kairuki aliongeza kuwa yapo malalamiko kuhusu suala la maadili na uwajibikaji yanayozigusa Wakala za Serikali. Aliainisha masuala hayo ni pamoja na Watumishi hewa, taarifa chafu za Watumishi, matumizi mabaya ya madaraka na rasilimali za Umma, kutosimamia ipasavyo utekelezaji wa mifumo ya utendaji kazi na wakati mwingine kutotekeleza majukumu ya msingi ya wakala.
Alifafanua kuwa amegundua kupitia taarifa mbalimbali kuwepo kwa  changamoto ya mawasiliano hafifu kati ya Wizara mama na Wakala zilizo chini yao ambapo taarifa kutoka katika Wakala hazichambuliwi inavyostahili na hata zinapochambuliwa na wizara mama, hazitoa mrejesho kwenda katika Wakala.
Awali, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Dkt. Laurean Ndumbaro alizitaka Wakala za Serikali kuimarisha eneo la ufuatiliaji na tathmini ili kuimarisha utendaji kazi na kuleta mabadiliko yanayotarajiwa na Watanzania.
 Alisema matarajio ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha Wakala za Serikali zinapunguza utegemezi kwa Serikali kwa kujitegemea kimapato kutokana na vyanzo vyake vya ndani hasa kwa Wakala zinazoingiza mapato makubwa kutokana na huduma zinazotoa.
Serikali ilianzisha Wakala kwa lengo la kuzifanya vyombo vya kutekeleza majukumu kwa niaba ya Serikali kwa tija na ufanisi zaidi, pia kupunguza urasimu na hivyo kutoa huduma bora kwa wakati kwa wananchi.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

RAIS MSTAAFU MWINYI AZINDUA WIKI YA SHERIA NCHINI

$
0
0
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi akiongoza Matembezi ya Uzinduzi wa Wiki ya Sheria nchini leo.Kushoto ni Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma na kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof.Sifuni Mchome.
Jaji Mfawidhi wa MahakamaKuu Divisheni ya Kazi Mhe. Aisha Nyerere akionesha bango kabla ya kanza kwamatembezi ya Uzinduzi wa wiki ya Sheria Nchini leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma akiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali kabla ya kuanza kwa matembezi ya zinduzi wa wiki ya Sheria leo jijini dar es salaam.
Baadhi ya Watumishi wa Mahakamawakiwakwenye Matembezi hayo.
Baadhi ya Watumishi wa Mahakamawakiwakwenye Matembezi hayo.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi akizungmza wakati wa Uzinduzi wa Wiki ya Sheria nchini leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam .


PICHA ZOTE NA LYDIA CHURI-MAHAKAMA

MAKAMU WA RAIS AMTUMIA SALAMU ZA POLE NA PONGEZI RC WA GEITA MEJA JENERALI MSTAAFU EZEKIEL KYUNGU KWA KAZI NZURI YA UOKOAJI WALIOFUKIWA MGODINI MKOANI GEITA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amemtumia salamu za pole na pongezi Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga kwa kazi nzuri na kubwa waliyoifanya ya kuwaokoa wachimbaji wadogo 15 waliofukiwa na maporomoko ya udongo kwenye Mgodi wa Dhahabu wa RZU uliopo katika Kijiji cha Nyarugusu, wilaya ya Geita katika mkoa wa Geita.

Tukio hilo la kufukiwa wachimbaji hao wadogo 15 wakiwemo Watanzania 14 na Raia Mmoja wa China lilitokea usiku wa Tarehe 26 Januari mwaka 2017.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesema amepokea kwa furaha taarifa za kuokolewa kwa wachimbaji hao wadogo na amesifu na kupongeza jitihada za kuwaokoa wachimbaji hao  zilizofanywa na Serikali ya Mkoa wa Geita, Jumuiya ya Wachimbaji Wadogo wa mkoa wa Geita, Wamiliki wa Migodi ya Dhahabu na wananchi kwa ujumla kwa kutoa vifaa mbalimbali vya uokoaji jitihada ambazo zimepelekea kuokolewa kwa wachimbaji hao wakiwa hai.

Makamu wa Rais amesisitiza kuwa “jitihada ,Umoja na Mshikamano ulioonyeshwa na makundi mbalimbali katika kuwaokoa ndugu zetu waliofukiwa na maporomoko ya Udongo wakiwa kazini huko Geita ni mfano mzuri na wakuigwa na wananchi na taasisi nyingine nchini katika kujitolea kwa hali na mali hasa vifaa vya uokoaji kwa ajili ya kusaidia watu wanaopatwa na majanga ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea kama walivyofanya ndugu zetu wa mkoa wa Geita nawapongeza Sana”.

 Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewataka wamiliki wa migodi kote nchini wahakikishe wanafanya kazi zao zauchimbaji wa madini kwa kuzingatia kanuni,taratibu na sheria kama hatua ya kuepuka madhara yanayoweza kutokea wakiwa wanafanya shughuli zao za uchimbaji wa madini.

Kupitia kwako Mkuu wa mkoa wa Geita napenda kutuma salamu za pole kwa ndugu, jamaa na marafiki kufuatia kutokea kwa tukio hilo na nawaombea kwa Mwenyezi Mungu wachimbaji hao ambao kwa sasa wanapatiwa matibabu Katika Hospitali ya Serikali ya mkoa wa GEITA matibabu mema ili waweze kupona haraka na kurejea kwenye kazi zao za kujitafutia riziki.

Wakati huo huo, Makamu wa Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu, Kitengo cha Kudhibiti Maafa nchini, Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Wizara ya Mambo ya Ndani kwa ushirikiano mkubwa walioutoa kwa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Geita na kupekelea kuchukuliwa hatua za haraka katika kushughulikia ajali hiyo.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Dar es Salaam            
29-Jan-2017


KAIMU KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA DR. JUMA MALEWA AHITIMISHA ZIARA MAGEREZA MKOANI MOROGORO NA PWANI

$
0
0
Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa (wa kwanza kulia) akitembelea jengo la Karakana ya Ufundi ya Gereza Wami Vijana. Jengo hilo pamoja na kuendelea kutumika lakini bado linahitaji kukamilishwa kujengwa na kuwekewa miundombinu ili liweze kutoa huduma kama ilivyokusudiwa.
Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa (katikati) akipata maelezo mafupi ya kiutendaji kutoka kwa Mkuu wa Gereza la Mahabusu Mrakibu wa Magereza (SP) Zephania Neligwa (aliyesimama) ofisini kwake wakati wa ziara ya Kaimu Kamishna Jenerali Mkoani Morogoro aliyoifanya mwishoni mwa juma.
Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa (wa kwanza kushoto) akitolea ufafanuzi hoja mbalimbali zilizotolewa na baadhi ya Maafisa na Askari katika kikao kilichojumuisha askari wa Ofisi ya Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro na Gereza Mahabusu. 
Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa (katikati)akisisitiza jambo wakati wa kikao kikao chake kilichojumuisha askari wa Ofisi ya Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro na Gereza Mahabusu. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Mzee R.Nyamka. Na kulia Mkuu wa Shirika la Magereza (Corporation Sole) Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Joel Bukuku na nawa mwisho ni Mkuu wa Kitengo cha Uwekezaji na Ujasiliamari wa Jeshi la Magereza Mrakibu Mwandamizi wa Magereza (SSP) Uswege Mwakahesya.
Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkuu wa Gereza Kihonda mara alipowasili kituoni hapo kujionea shughuli mbalimbali kituoni hapo sanjari na kuongea na maafisa na askari wa kituo hicho mwishoni mwa Juma hili.
Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa (wa kwanza kushoto) akikagua maendeleo ya jengo jipya la ofisi ya Mkuu wa Gereza Kihonda. Jengo hilo linashengwa kwa jitihada za Mkuu wa Gereza hilo kwa kushirikiana na maafisa na askari wa kituo hicho. Viongozi wengine hapo ni Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Mzee Nyamka, Mkuu wa Shirika la Magereza (Corporation Sole) Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Joel Bukuku na Mkuu wa Gereza Kihonda Kamishna Msaidizi wa Magereza Ben Mwansasu.
Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa akiendelea kusikiliza hoja mbalimbali za maafisa na askari wa Gereza Kihonda wakati wa ziara ya kikazi kituoni hapo. Aliyesimama ni Mkaguzi Msaidizi wa Magereza (A/Insp) Amani Moses akichangia jambo wakati wa kikao hicho.
Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa akisalimiana na baadhi ya maafisa wa gereza Kihonda mara alipowasili akiwa tayari kufanya kikao na watendaji wa gereza hilo.
Mmoja wa askari wa gereza Kihonda akiwa na sura ya bashasha baada ya kupata fursa ya kusalimiana na Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza mara baada ya kikao wakati wa ziara ya Kaimu Kamishna Jenerali katika baadhi ya vituo mkoani Morogoro ikiwemo gereza Kihonda, mwishoni wa juma hili.
Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa akikagua maendeleo ya moja ya nyumba za zinazojengwa kwa mtindo wa kujitolea katika gereza la Wanawake Kingolwira mkoani Morogoro ikiwa ni jitihada za kukabiliana na tatizo la uhaba wa nyumba kituoni hapo. Aliyefuatana naye ni Mkuu wa Gereza la Wanawake Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Loyce Luhembe
imu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa (katikati) akitolea ufafanuzi wa jambo katika kikao chake na watumishi wa gereza Kihonda alipofanya ziara ya kiutendaji katika baadhi ya Magereza ya mkoa wa Morogoro. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Magereza mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Mzee Nyamka na kulia Mkuu wa Gereza la Kihonda, Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Ben Mwansasu.
Baadhi ya Maafisa na askari wa Kingolwira Complex inayojumuisha Chuo cha Uhunzi na Udereva, Gereza Mtego wa Simba, Gereza Mkono wa Mara na Gereza la Wanawake Kingolwira katika kikao cha pamoja na Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa alipofanya ziara katika vituo hivyo kujionea shughuli mbalimbali za kila siku.
.Sehemu ya Maafisa na askari wa vituo vya Bwawani Sekondari (inayomilikiwa na Jeshi la Magereza) na Gereza Ubena mkoani Pwani wakiwa katika kikao cha pamoja na Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa (hayupo pichani) alipofanya ziara vituoni hapo ili kujionea shughuli za vitu hivyo lakini pia kusiliza shida na maoni ya watumishi katika vituo hivyo jana tarehe 28.01. 2017.
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Pwani (RPO), Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Boyd Mwambingu akitolea ufafanuzi moja ya hoja zilizoibuka katika kikao cha Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa na wafanyakazi wa vituo hivyo alichofanya mwishoni mwa juma.
Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maafisa na askari wa gereza Wami Kuu na Vijana alipifanya ziara ya kikazi vituoni hapo.
Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maafisa na askari wa Gereza la Mahabusu Morogoro alipofanya ziara mkoani humo mwishoni mwa juma.
Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maafisa na askari wa gereza Kihonda alipofanya ziara ya kikazi kituoni hapo Ijumaa, 27.01.2017.
Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maafisa na askari wa Kingolwira Complex mara baada ya kikao kilicholenga kusikiliza kero na hoja mbalimbali za watumishi hao, tarehe 28.01.2017.

Picha zote na ASP Deodatus Kazinja, PHQ



Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa katika hali ya kuamsha hari na morali ya kufanya kazi kwa watendaji wa Jeshi la Magereza amefanya ziara ya kikazi katika baadhi ya Magereza ya Mkoa wa Morogoro na Pwani mwishoni juma hili.

Ziara hiyo imejumuisha Magereza ya Mbigiri, Wami Kuu, Wami Vijna, Mahabusu, Kihonda, Kingolwira Complex yote ya mkoa wa Morogoro na Shule ya Sekondari Bwawani na gereza Ubena vya mkoani Pwani.

Kutoka kwa Kaimu Jenerali maafisa na askari aliwapata taarifa fupi ya Uwekezaji wa Ubia katika kiwanda cha sukari cha gereza Mbigiri Mkoani Morogoro kati ya Jeshi la Magereza na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya PPF na NSSF. Alisema uwekezaji huu ni kwa faida ya Jeshi kama Taasisi hivyo ni vizuri kila askari akalifahamu hilo.

Katika ziara hiyo pia alipata wasaa wa kufanya vikao na watendaji ambapo maafsa, askari na watumishi raia walipata fursa ya kuuliza maswali moja kwa moja kutoka kwa Mtendaji mkuu wa Jeshi la Magereza ambapo baadhi ya mambo yalipatiwa majibu ya papo hapo na mengine kupewa ahadi ya kutatuliwa katika siku za usoni hasa yenye uhusiano na masuala ya kibajeti.

Miongoni mwa masuala yaliyoonekana kuwa ni tatizo sugu ni pamoja na huduma za maji, usafiri, matibabu kwa wafungwa na mahabusu, sare za askari, posho mbalimbali kulingana na stahiki ya kila askari na mambo mengine madogo madogo ambayo yote kimsingi yanagusia suala la fedha.

Katika vikao hivyo Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa alitolea maelekezo baadhi ya mambo yaliyohitaji kauli ya Makao Makuu ya Jeshi lakini pia aliwahakikishia kuwa ofisi yake itaendelea kushughulikia kero zote na kusaidia kwa haraka pale inapohitaji kwa kutegemeana na hali ya fedha kwa wakati huo.

Kaimu Kamishna Jenerali aliwaasa maafisa askari kuwa waangalifu wanapotumia mitandao ya kijamii hasa kwa kuzingatia viapo vya utumishi wao.“Ninyi ni askari wenye viapo vya utii wa mamlaka zilizopo, jiepusheni na mijadala ya mitandaoni kwani mingine iko kinyume na maadili ya kazi zetu. Ukipokea ujumbe usiofaa futa kabisa badala ya kuusambaza” alisisitiza Dr. Malewa

Aidha Dr. Malewa aliwataarifu watumishi hao adhma yake kuu ya kuona Jeshi linakuwa na hospitali kubwa nayakisasa ili kuondoa kero na aibu inayowapata askari na familia zao wanapokuja kutibiwa Jijini Dar es salaam.

Ni dhamira yangu kuona tunaanzisha ujenzi wa hospitali hivi karibuni ili kuondoka na adha ambayo wote mnaifahamu, na hospitali hii tutaijenga kwa kutumia vyanzo mbali mbali ikiwemo na sisi kama askari kujitolea. Naomba mtuunge mkono mara wazo hili litakapoletwa kwenu” alisisitiza Kaimu Jenerali.

Mwisho aliwataka maafisa na askari kudumisha nidhamu kazini ikiwa ndiyo msingi mkuu wa mafanikio hasa katika kazi za majeshi.
Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP)Mzee Nyamka akitoa taarifa ya utendaji katika mkoa wake kwa Kaimu Kamishna Magereza Dr. Juma Malewa (hayupo pichani) mwishoni mwa juma hili alipofanya ziara ya kiutendaji katika baadhi ya Magereza mkoani humo.
Baadhi ya Maafisa na askari wa Gereza Mbigiri Mkoani Morogoro wakifuatilia ufafanuzi wa hoja mbalimbali walizozitoa mbele ya Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa (hayupo pichani) alipofanya ziara kituoni hapo na kufanya Baraza la watumishi hao ili kusikiliza kero, hoja na mapendekezo yote ikiwa ni kuboresha utendaji kazi wa siku kwa siku.
Baadhi ya Maafisa na askari wa Gereza Wami Kuu pamoja na Wami Vijana Mkoani Morogoro kwa pamoja kwa makini wakifuatilia ufafanuzi wa hoja mbalimbali walizozitoa kwa Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza Dr. Juma Malewa (hayupo pichani) katika Baraza la pamoja alipowatembelea hivi karibuni kuona utendaji kazi katika vituo vyao lakini pia kuwapa hamasa ya utendaji kazi.
 

Kompyuta za Bayport mkoani Mara kuelekezwa shule za Kata

$
0
0
Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa, akimkabidhi kompyuta sita Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara, Mheshimiwa Ado Mapunda kwa ajili ya kuongeza ufanisi katika ofisi za umma mkoani Mara. Wengine kwenye tukio hilo ni watumishi wa Bayport, akiwamo Meneja wa Kanda ya Ziwa wa Bayport, Lugano Kasambala wa kwanza kushoto. Picha na Mpiga Picha Wetu Mara.


Na Mwandishi Wetu, Mara.

SERIKALI ya Mkoa Mara kwa kupitia Katibu Tawala wake, Mheshimiwa Ado Mapunda, imewaagiza watendaji wa serikali mkoani humo kuhakikisha kompyuta walizopewa na Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, zinaelekezwa kwenye shule za kata ili kuchangia ukuzaji wa kiwango cha elimu.


Mheshimiwa Mapunda aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati anapokea kompyuta sita kutoka Bayport zilizoelekezwa katika Halmashauri ya Tarime, Rorya na Manispaa ya Musoma, huku kila ofisi ikipata kompyuta mbili ikiwa ni mwendelezo wa ugawaji wa vitendea kazi kutoka kwenye taasisi hiyo inayojihusisha na mikopo ya fedha taslimu kwa watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni zilizoidhinishwa.


Akizungumza katika makabidhiano hayo, Katibu Tawala huyo alisema lengo la Mkoa wao ni kuona kiwango cha elimu kinapiga hatua kubwa, hivyo wameona msaada huo uelekezwe zaidi katika shule za kata kwa ajili ya kuhifadhi kumbukumbu muhimu za wanafunzi wao.


Alisema kufanya hivyo kutaongeza ukuzaji wa elimu ya wanafunzi wa mkoani Mara, ili iwe njia ya kuandaa wataalamu wazuri kwa kutumia vema teknolojia ya kompyuta inayoboresha utendaji wa kazi.


“Tunashukuru wenzetu wa Bayport wa Kanda ya Ziwa pamoja na Makao Makuu kwa kutuletea msaada huu mkubwa kwetu ambao kwa hakika tutautumia vizuri katika Mkoa huu wa Mara ili ulete tija kama mlivyokusudia wakati mnafikiria kusambaza.


“Ofisi yetu imeagiza kompyuta hizi zisambazwe katika baadhi ya shule za kata kwa kuzitumia kwa namna moja ama nyingine ili wanafunzi wetu wasonge mbele zaidi kwa kuanzia kurekodi vizuri takwimu zao kama njia ya kugundua tunafanya juhudi za kutuvusha hatua ya juu zaidi,” Alisema Mapunda.


Naye Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa, alisema ndoto zao zinaelekea kukamilika kuhakikisha kwamba msaada wa kompyuta zao unafika kwa haraka kama walivyokusudia na kuuzindua mwaka jana jijini Dar es Salaam.


“Kompyuta tulizotoa Mara na Kanda ya Ziwa ni mwendelezo wetu wa kutoka kwenye kompyuta 125 tulizomkabidhi Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, huku 80 zikielekezwa mikoani na kuufanya mzigo wote ufikie 205 wenye thamani ya Sh Milioni 500,” Alisema Mercy.



Mbali na Mara, Bayport pia walikabidhi kompyuta mbili kwa Halmashauri ya Wilaya Misungwi, mkoani Mwanza na kuifanya Kanda ya Ziwa kuvuna kompyuta nane za taasisi hiyo ambapo pia ilitangaza kuwa utaratibu huo wa kufikisha kompyuta utaendelea katika wilaya na mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara wakiamini utasaidia kuongeza ufanisi katika ofisi za umma.


MAWAKALA MPAKA WA TUNDUMA/NAKONDE WAONYWA KUKWAMISHA BIASHARA

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Songwe.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda, amewaonya mawakala wa forodha katika mpaka wa Tanzania na Zambia wa Tunduma/Nakonde kuacha Mara moja tabia ya kuwachelewesha madereva wa malori yaendayo masafa marefu kwa makusudi ili wapewe rushwa.

Prof. Mkenda ametoa onyo hilo katika mpaka huo wa Tunduma na Nakonde, baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya madereva wa malori waliodai wamekuwa wakicheleweshwa kuvuka mpaka huo kwa zaidi ya siku tatu hadi tano.

Wadereva hao wameeleza kuwa mawakala wa forodha wamekuwa wakiwaambia kuwa nyaraka zao zinazohusika na mizigo wanayosafirisha zimekuwa zilicheleshwa na kituo cha Forodha upande wa Zambia.

Hata hivyo Meneja wa Mamlaka ya Mapato Zambia (ZRA), Kituo cha Nakonde, Bw. Nase Lungu, amekana kuhusika na ucheleweshaji huo na baada ya ukaguzi wa moja ya nyaraka hizo ilibainika kuwa upande wa Zambia unatoa nyaraka hizo kwa wakati lakini zimekuwa zikifichwa na Mawakala wa Forodha upande wa Tanzania.

Wakitoa ufafanuzi wa tuhuma hizo, madereva hao wamesema kuwa mawakala wa forodha kwa muda mrefu wamekuwa wakiwaeleza kuwa mtandao wa intaneti wa Upande wa Zambia unaotumika kuchakata nyaraka zao uko chini, hivyo walitakiwa kutoa shilingi 10,000 kwa kila nyaraka ili “kurahisisha” kazi hiyo kwa kuwapa kitu kidogo maafisa wa forodha wa Zambia.

“Mawakala wengine wa forodha wana nyumba zao za kulala wageni hapa Tunduma kumbe wanatulazimisha kukaa hapa ili tulale kwenye nyumba hizo hali inayotutia hasara na wanatumia kutokujua kwetu kutudanganya kwamba mtandao uko chini wakijua hatuna uwezo wa kufuatilia huko Zambia” alieleza kwa masikitiko dereva mmoja 

Baada ya kubaini uwepo wa vitendo hivyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda, ameagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA upande wa Tunduma kuandika kibao chenye namba za simu za Mkuu wa TRA mpakani hapo zitakazotumiwa na madereva wanaocheleweshwa kwa makusudi kutoa malalamiko yao.

“Tunataka madereva mtumie siku moja tu kukamilisha nyaraka zenu ili muendelee na safari yenu vinginevyo tutadumaza biashara kati ya Zambia na Tanzania na pia tutaifanya Bandari yetu ya Dar es salaam kushindwa kuleta tija” aliongeza Prof. Mkenda 

Alisema kuwa wakala wa forodha atakayebainika kufanya mchezo huo mchafu wa kuwarubuni madereva na kuwachelewesha kupeleka mizigo nchini Zambia, watanyang’anywa leseni zao za biashara.

Meneja Msaidizi wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, mikoa ya Songwe na Mbeya, Bw. Jomimassa Nsindo, amesema kuwa ofisi yake itashirikiana na madereva kukomesha vitendo hivyo ambavyo amesema vinaharibu uchumi na biashara mpakani hapo.

Naye Mkuu wa wilaya ya Momba, mkoani Songwe, Bw. Juma Irando, alisema kuwa ataitisha kikao cha Madereva, Mawakala wa Forodha na Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA katika Mpaka huo wa Tunduma/Nakonde mapema, ili kuweka msimamo wa serikali na kuwaeleza wahusika wanaokiuka taratibu hatua watakazochukuliwa.

Prof. Mkenda na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban, walikwenda katika mpaka huo wa Tunduma na Nakonde, kuangalia maandalizi ya uanzishwaji wa Kituo cha Pamoja cha Mpakani kati ya Tanzania na Zambia, unaotarajiwa kuanza Februari mosi, 2017, baada ya kusainiwa kwa mikataba kati ya nchi hizo mbili, juzi.

KAMPENI YA KUCHEZA OLIMPIKI 2020 KUZINDULIWA KESHO UWANJA WA KARUME

$
0
0
Mkurugenzi wa Michezo, Yusuph Omari; Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kwa kushirikiana na Makamu Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Henry Tandau kesho Jumatatu Januari 30, kwa pamoja watazindua kampeni maalumu za kuifanikisha Tanzania kushiriki michuano ijayo ya Olimpiki itakayofanyika Tokyo, Japan.

Uzinduzi wa kampeni hizo unaopewa jina la ‘The Road to Tokyo 2020’ utafanyika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam saa 5.00 asubuhi ambako wadau na wafamilia wa mpira wa miguu wanakaribishwa.

Tayari timu ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 23 ‘Kilimanjaro Warriors’ imeingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya awali ya kucheza mechi za kufuzu fainali hizo za za Olimipiki.

Kambi hiyo imepigwa kwenye Hosteli za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ambako pia kuna Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazoezi kulingana na program za walimu.

Tanzania haijapata kushiriki Michuano ya Olimpiki kwa upande wa mpira wa miguu jambo ambalo limeisukuma TFF kuona kuwa ni fursa ya mpira wa miguu kuchezwa hivyo inashirikiana na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), kufanikisha mipango na taratibu.


IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

SHIBUDA ATAKA RAIS MAGUFULI AUNGWE MKONO

MAKATIBU WAKUU WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO NA WIZARA YA VIWANDA,BIASHARA NA UWEKEZAJI WATEMBELEA MPAKA WA TUNDUMA/NAKONDE

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda (kushoto), akiwa pamoja na Mkuu wa wilaya ya Momba mkoani Songwe, Bw. Juma Irando (katikati), na maafisa kadhaa wa Wizara ya Fedha na Mipango na Wizara ya Viwanda, Biashara naUwekezaji, wakitoka katika Ofisi za Mkurugenzi wa Mji wa Tunduma kuelekea mpakani mwa Tanzania na Zambia eneo la Tunduma na Nakonde
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban (aliyeshika mkoba), Mkuu wa Wilaya ya Momba mkoani Songwe, Bw. Juma Irando (aliyeshika mikono yake), Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda (Aliyesimama nyuma ya Mkuu wa wilaya), wakisikiliza maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Afisa Mfawidhi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-Tunduma, Bw. Magori Cosmas (wa pili kulia), kuhusu maandalizi ya kuanzisha rasmi Kituo cha Pamoja cha Mpakani Tunduma/Nakonde katika nchi za Tanzania na Zambia
Afisa Mifumo ya Kompyuta wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Bw. Yasin Kilima (aliyeshika simu katikati), akitoa ufafanuzi wa namna TRA ilivyojiandaa kuweka mifumo itakayo saidia kurahisisha kazi ya utoaji huduma wa pamoja na wenzao wa Zambia, mbele ya Ujumbe ulioongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban (wa pili kulia laiyevaa miwani), wakati walipotembelea mpaka wa Tanzania na Zambia kujionea maandalizi ya kuanzishwa rasmi kwa Kituo cha Pamoja cha Mpakani unaotarajiwa kuanza Februari mosi, 2017.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda (kushoto), akisisitiza jambo wakati timu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na wizara yake walipotembelea na kukagua miundombinu ya Ofisi ya Uhamiaji Kituo cha Mpakani cha Tunduma.
Mkuu wa Wilaya ya Momba, mkoani Songwe, Bw. Juma Irando, akiongea jambo wakati timu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, ilipofanya ziara katika Kituo cha mpakani cha Tunduma/Nakonde kuangalia maandalizi ya uanzishwaji wa Kituo cha Pamoja na Mpakani baada ya kusainiwa kwa mikataba kati ya Tanzania na Zambia, na kutakiwa kuanza rasmi mwanzoni mwa Februari, 2017
Kaimu Afisa Uhamiaji Mfawidhi wa Kituo cha mpakani Tunduma/Nakonde, Bw. Tabaran Mzee (kulia), akiueleza ujumbe kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji namna idara yake ilivyojiandaa kuanza kutoa huduma ya pamoja mpakani kati ya maofisa kutoka Zambia na Tanzania ambao watakuwa wakitumia ofisi moja kuwahudumia watu wanaotumia mpaka huo kuvuka kwenda kila upande wa nchi (Tanzania na Zambia)
Makatibu Wakuu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, wakiwa pamoja na maofisa wa mamlaka ya Mapato kutoka Zambia wakiangalia hali ya biashara na uwekezaji katika Mpaka wa Tunduma na Nakonde ikiwa ni maandalizi ya kuanza rasmi kwa utoaji wa huduma wa pamoja kati ya nchi hizo mbili ili kuboresha mazingira ya biashara baada ya kusainiwa kwa mikataba ya kuanzishwa kwa huduma hiyo katika mpaka huo
Makatibu Wakuu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, wakiwa pamoja na maofisa wa Mamlaka ya Mapato kutoka Zambia (ZRA) walipotembelea upande wa pili wa mpaka huo-Nakonde ili kujionea maandalizi ya kuanza rasmi kwa Kituo cha Pamoja cha Mpakani kati ya Tanzania na Zambia baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya kuanzishwa kwa huduma hiyo Februari mosi, 2017
Kituo cha Forodha cha Nakonde Upande wa Zambia
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Zambia-Nakonde, Bw. Nase Lungu, (aliyenyoosha mkono), akitoa maelezo namna ofisi yake ilivyojipanga kuhudumia wateja wao kupitia utaratibu mpya wa kushirikiana kwenye jengo moja kati ya maafisa wa Forodha wa Tanzania na Zambia, wakati Ujumbe kutoka nchi hizo mbili walipotembelea mpaka huo kujionea maandalizi yalipofikia kabla ya kuanza rasmi kwa utaratibu huo Februari Mosi, 2017
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda (katikati), akisalimiana na mmoja wa madereva wanaoendesha malori kwenda Zambia, kabla ya kusikiliza kero zao mbalimbali, ambapo malalamiko makubwa yalikuwa ni kutumia muda mrefu mpakani mwa Tunduma/Nakonde kunakowatia hasara na kuchelewesha biashara
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda (wa pili kulia), akitoa maelekezo namna ambavyo maofisa wa TRA Tanzania na Zambia wanavyopaswa kushughulikia kero za madereva na wananchi wanaotumia mpaka wa Tanzania na Zambia (Tunduma na Nakonde) ili kuboresha biashara mpakani hapo
Ujumbe wa Tanzania na maafisa wa Zambia walipotembelea na kukagua miundombinu ya utoaji huduma pamoja baada ya kutiwa saini kwa mikataba ya kuanza kwa Kituo cha Pamoja cha Mpakani, (Tunduma/Nakonde), huduma inayotarajiwa kuanza rasmi Februari Mosi, 2017
Ujenzi wa Kituo cha Pamoja Mpakani upande wa Tanzania-Tunduma, ukiendelea kwa kasi na una tarajiwa kukamilika baada ya miezi 16 ijayo

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)

………….

Na Benny Mwaipaja, WFM, Songwe 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda, amewaonya mawakala wa forodha katika mpaka wa Tanzania na Zambia wa Tunduma/Nakonde kuacha Mara moja tabia ya kuwachelewesha madereva wa malori yaendayo masafa marefu kwa makusudi ili wapewe rushwa.

Prof. Mkenda ametoa onyo hilo katika mpaka huo wa Tunduma na Nakonde, baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya madereva wa malori waliodai wamekuwa wakicheleweshwa kuvuka mpaka huo kwa zaidi ya siku tatu hadi tano.

Wadereva hao wameeleza kuwa mawakala wa forodha wamekuwa wakiwaambia kuwa nyaraka zao zinazohusika na mizigo wanayosafirisha zimekuwa zilicheleshwa na kituo cha Forodha upande wa Zambia.

Hata hivyo Meneja wa Mamlaka ya Mapato Zambia (ZRA), Kituo cha Nakonde, Bw. Nase Lungu, amekana kuhusika na ucheleweshaji huo na baada ya ukaguzi wa moja ya nyaraka hizo ilibainika kuwa upande wa Zambia unatoa nyaraka hizo kwa wakati lakini zimekuwa zikifichwa na Mawakala wa Forodha upande wa Tanzania.

Wakitoa ufafanuzi wa tuhuma hizo, madereva hao wamesema kuwa mawakala wa forodha kwa muda mrefu wamekuwa wakiwaeleza kuwa mtandao wa intaneti wa Upande wa Zambia unaotumika kuchakata nyaraka zao uko chini, hivyo walitakiwa kutoa shilingi 10,000 kwa kila nyaraka ili “kurahisisha” kazi hiyo kwa kuwapa kitu kidogo maafisa wa forodha wa Zambia.

“Mawakala wengine wa forodha wana nyumba zao za kulala wageni hapa Tunduma kumbe wanatulazimisha kukaa hapa ili tulale kwenye nyumba hizo hali inayotutia hasara na wanatumia kutokujua kwetu kutudanganya kwamba mtandao uko chini wakijua hatuna uwezo wa kufuatilia huko Zambia” alieleza kwa masikitiko dereva mmoja 

Baada ya kubaini uwepo wa vitendo hivyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda, ameagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA upande wa Tunduma kuandika kibao chenye namba za simu za Mkuu wa TRA mpakani hapo zitakazotumiwa na madereva wanaocheleweshwa kwa makusudi kutoa malalamiko yao.

“Tunataka madereva mtumie siku moja tu kukamilisha nyaraka zenu ili muendelee na safari yenu vinginevyo tutadumaza biashara kati ya Zambia na Tanzania na pia tutaifanya Bandari yetu ya Dar es salaam kushindwa kuleta tija” aliongeza Prof. Mkenda 

Alisema kuwa wakala wa forodha atakayebainika kufanya mchezo huo mchafu wa kuwarubuni madereva na kuwachelewesha kupeleka mizigo nchini Zambia, watanyang’anywa leseni zao za biashara.

Meneja Msaidizi wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, mikoa ya Songwe na Mbeya, Bw. Jomimassa Nsindo, amesema kuwa ofisi yake itashirikiana na madereva kukomesha vitendo hivyo ambavyo amesema vinaharibu uchumi na biashara mpakani hapo.

Naye Mkuu wa wilaya ya Momba, mkoani Songwe, Bw. Juma Irando, alisema kuwa ataitisha kikao cha Madereva, Mawakala wa Forodha na Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA katika Mpaka huo wa Tunduma/Nakonde mapema, ili kuweka msimamo wa serikali na kuwaeleza wahusika wanaokiuka taratibu hatua watakazochukuliwa.

Prof. Mkenda na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban, walikwenda katika mpaka huo wa Tunduma na Nakonde, kuangalia maandalizi ya uanzishwaji wa Kituo cha Pamoja cha Mpakani kati ya Tanzania na Zambia, unaotarajiwa kuanza Februari mosi, 2017, baada ya kusainiwa kwa mikataba kati ya nchi hizo mbili, juzi.
Mwish

TAARIFA YA UOKOZI WACHIMBAJI MADINI WALIOFUKIWA NA KIFUSI- GEITA

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA NISHATI NA MADINI



  
ZOEZI LA UOKOAJI WACHIMBAJI 15 WALIOFUKIWA NA KIFUSI KATIKA MGODI WA DHAHABU GEITA   LAKAMILIKA KWA MAFANIKIO

Wizara ya Nishati na Madini inapenda kuufahamisha  umma kuwa, Zoezi la kuwaokoa wachimbaji 15 waliofukiwa na kifusi  tarehe 26/01/2017 kwenye mgodi wa dhahabu eneo la kijiji cha Mawemeru, Nyarugusu Wilayani Geita limekamilika kwa mafanikio.

Ajali ya kufukiwa wachimbaji hao iliyohusisha Watanzania 14 na raia 1 wa China ilitokea kwenye leseni ya uchimbaji wa Kati wa madini ya dhahabu yenye Namba ML 492/2013 inayomilikiwa na Bw. Ahmed Mubarak Adam.

Chanzo cha ajali hiyo ilikuwa ni kuanguka kwa shaft ya mgodi huo na kufukiwa na kifusi wakati wachimbaji hao wakifanya kazi mgodini chini ya ardhi.

Tukio la uokoaji limefanikiwa leo tarehe 29/01/2017 ambapo wahanga hao walianza kutolewa shimoni kuanzia saa 5 hadi saa 5:30 asubuhi wote 15 wakiwa hai ingawa walikuwa wamedhoofika kiafya.  Aidha, wachimbaji hao wamepewa huduma ya kwanza katika eneo la ajali na kisha kukimbizwa Hospitali Teule ya Rufaa ya Geita. Hadi sasa wachimbaji hao wapo Hospitali wakiendelea na matibabu kwa uchunguzi zaidi wa afya zao.

Juhudi za kuokoa wachimbaji hao  ambazo zilifanyika kwa kufukua kifusi katika eneo la ajali zilianza mara baada ya tukio hilo kutokea. Uongozi wa Mkoa wa Geita ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa Meja. Jen.(Mst) Ezekiel E. Kyunga ulishirikiana na Wataalam wa Wizara ya Nishati na Madini na Kampuni za Madini mbalimbali mkoani Geita katika zoezi la ufukuaji kifusi ili kuokoa maisha ya wchimbaji hao

 Kampuni zilizoshiriki kwa kutoa mitambo na vifaa mbalimbali ni Kampuni ya Busolwa Mining Ltd; Kampuni ya Geita Gold Mine (GGM); Kampuni ya Nyarugusu Mining Ltd; Nsangano Mining Project; Metchell Tanzania Drilling; WAJA Hospital pamoja na wachimbaji wadogo wa Mkoa wa Geita wakiongozwa na Viongozi wa wachimbaji madini Wilaya, Mkoa na Taifa.

Akizungumza mara baada ya kuokolewa wachimbaji hao, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard amewashukuru wadau wote walioshiriki kwa hali na mali kufukua kifusi na hatimaye kufanikiwa kuwatoa wachimbaji chini ya ardhi wakiwa hai.

Dkt. Kalemani amewaomba Watanzania kuendelea na moyo huo pale majanga kama haya yanapotokea. Aidha, Dkt. Kalemani ameagiza shughuli zifungwe kwa muda wa siku tano kwenye mgodi uliopata ajali kuanzia tarehe 29/01/2017 ili kutoa nafasi kwa Kamishna wa Madini kufanya tathmini ya hali ya usalama wa mgodi na kutoa maelekezo kabla ya shughuli kuanza.

Vilevile, amewataka wachimbaji wawe watulivu katika kipindi ambacho tathmini ya hali ya usalama wa mgodi inafanyika na kuagiza Uongozi wa Mkoa kuhakikisha kuwa ulinzi unaimarishwa eneo la mgodi ili watu wasiweze kuingia na kuhatarisha maisha yao. 

Pia, ameagiza ukaguzi wa kina ufanyike kwenye migodi mingine ya wachimbaji wadogo na ya kati eneo la Nyarugusu na kwingineko nchini ili kuhakikisha kuwa migodi inakuwa salama kwa wachimbaji wa migodi husika.

Imetolewa na;
KATIBU MKUU
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
29/1/2017

Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>