Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1119 | 1120 | (Page 1121) | 1122 | 1123 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo amefanya ziara katika chuo kikuu cha Arusha. Katika ziara hiyo Mkuu wa mkoa amezungumza na uongozi wa chuo,watumishi pamoja na wanafunzi.
  Pia alipata fursa ya kutembelea miundo mbinu mbali mbali ya chuo hicho ambacho kinamilikiwa na kanisa la Waadventista Wasabato.

  Alipata muda wa kuzungumza na wanafunzi na kusikiliza kero zao na changamoto zinazowakabili ikiwemo kutokuridhishwa na huduma zinazotolewa na mfuko wa Bima ya Afya katika utoaji wa kadi za Bima ya Afya hivyo kusababisha usumbufu mkubwa wakati wa utoaji wa huduma hiyo chuoni hapo.

  Masuala mengine ni kama tatizo la kukatika umeme mara kwa mara, tatizo la maji, ulinzi na usalama chuoni hapo, sehemu kubwa ya wenye sifa ya kukopeshwa na bodi ya mikopo kutokuipata mikopo hiyo, pia wamemweleza hofu yao ya kumaliza masomo na kukosa ajira.

  Katika kujibu changamoto hizo mkuu wa mkoa ameuagiza uongozi wa NHIF (bima ya Afya) mkoa wa Arusha kufika chuoni hapo mara moja ili kuweza kulitatua tatizo hilo ndani ya wiki moja toka leo.

  Mkuu wa mkoa ametoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru, mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndg. Alexander Mnyeti na Mhandisi wa maji wilaya ya Arumeru kufika chuoni hapo siku ya Jumatano tarehe 01/02/2017 na kukaa na uongozi wa chuo kuona namna wanaitatua kero hiyo ya maji ya muda mrefu.

  Kuhusiana na suala la ulinzi chuoni hapo na maeneo ya jirani Mh. Mkuu wa mkoa ameihamasisha jamii nzima ya Arumeru bila kuwasahau wanachuo wenyewe kuona namna gani wanaweza kujenga kituo cha polisi ili kuimarisha usalama chuoni hapo na maeneo ya jirani, kwa kuanzia Mh. Gambo ametoa mabati 100 ili kuamsha ari ya wananchi na jamii nzima ya Arusha University kuanza ujenzi huo mara moja.

  Mh. Gambo ameichukua hoja ya wanafunzi walio na sifa za kukosa mkopo na kuagiza uongozi wa chuo kumpa majina ya wanafunzi husika na ofisi yake kuyawasilisha bodi ya mikopo ili yashughulikiwe, pia ametoa changamoto kwa vyuo kutoa kozi kulingana na mahitaji ya serikali kwa wakati husika ili kuepusha mgogoro wa kuwa na wahitimu wengi wasio na ajira.

  Vile vile katika kujibu baadhi ya changamoto Mh Gambo aliwapongeza wanafunzi kwa ujasiri wa kutoa kero zao bila woga na ameahidi ataweka utaratibu wa kutembelea vyuo vikuu vilivyopo mkoani Arusha ili kujua mazingira halisi na matatizo yanayokabili vyuo husika.

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Kitengo cha Sanaa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bibi. Leah Kihimbi ambaye alimwakilisha Mhe. Waziri Nape Nnauye akitoa maoni yake kuhusiana na igizo la Tamasha la "MajiMaji Flava" ambalo lilionyesha baadhi ya matukio ya ukatili yaliyofanywa na Wajerumani enzi za ukoloni dhidi ya watu weusi. Tamasha hilo lilifanyika jana 27/01/2017 Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es Salaam.
  Waigizaji wa Tamasha la "MajiMaji Flava" wakielimisha jamii kwa vitendo juu ya baadhi ya matukio yaliyowahi kutokea wakati wa kipindi cha ukoloni wa Wajerumani nchini Tanzania 27/01/2017 katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wageni waalikwa toka mataifa mbalimbali wakishuhudia maigizo mbalimbali wakati wa Tamasha la "MajiMaji Flava" ambalo lilionyesha baadhi ya matukio ya ukatili yaliyofanywa na Wajerumani enzi za ukoloni dhidi ya watu weusi. Tamasha hilo lilifanyika jana 27/01/2017 Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es Salaam.
  Waigizaji kutoka Ujerumani na Tanzania wakiigiza namna baadhi ya matukio wakiyoyafanya Viongozi mbele ya Wananchi kipindi cha ukoloni kilichopelekea watu wengi kupoteza maisha wakati wa vita vya maji maji.
  Waigizaji kutoka Ujerumani na Tanzania wakitoa burudani ya muziki wakati wa "Tamasha la MajiMaji Flava"lililofanyika jana 27/01/2017 Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es Salaam.
  (Picha zote na Benedict Liwenga-WHUSM)

  0 0

   Naibu waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Anastazia Wambura, akitoa hotuba ya ufunguzi wa chilumbo, (kongamano) la Kiswahili, lililofadhiliwa na benki ya MCB, na kufanyika chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Kigamboni jijini Dar es Salaam, Januari 27, 2017.

  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
  BENKI ya Mwalimu, (MCB), imetoa semina kwa walimu na washiriki wa Chilumbo, (Kongamano), la Kiswahili lililofanyika Chuo Cha Mwalimu Nyerere Kigamboni jijini Dar es Salaam, Januari 27, 2017.
  Katika semina hiyo, maafisa wa MCB walielezea huduma mbalimbali zitolewazo na benki hiyo mpya inayomilikiwa na chama cha walimu nchini, (TTU), ambapo Meneja Mahusiano ya wateja wa benki hiyo, Bw.Charles Shadrack, (pichani juu), alisema, benki hiyo inatoa huduma za kibenki ikiwa ni pamoja na kutoa mikopo yenye riba nafuu.
  “Kwa mfanyakazi wa serikali, anachotakiwa kuja nacho baada ya kufungua akaunti kwenye benki yetu ni Salary sleep ambapo tunatoa mkopo wa hadi shilingi milioni 30.” Alisema.
  Alisema, benki hiyo pia imo kwenye kundi la mabenki yanayotumia ATM za umoja hivyo mteja anayo fursa ya kupata huduma za kibenki mahala popote nchini.
  Akifungua chilumbo hilo, Naibu waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Anastazuia Wambura, amewataka washiriki kukienzi Kiswahili kwani ni lugha inayokua kwa kasi duniani.
  “Rais wetu ameonyesha njia, niwape changamoto magwiji wa Kiswahili, jifunzeni kwa bidii ili mkitumie kama ajira kwani soko la walimu wa Kiswahili linapanuka siku hadi siku.” Aisema.


   Wasiriki wakifurahia mada zilizokuwa zikitolewa
   Washiriki wakiwa kwenye ukumbi wa Utamaduni palikofanyika chilumbo
   Naibu waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Anastazia Wambura, (kushoto), akipena mikono na Meneja Masoko na Uhusiano wa MCB, Bi. Rahma Ngassa, mara baada ya kutoa hotuba yake
   Meneja Masoko na Uhusiano wa MCB, Rahma Ngassa, Meneja wa Huduma kwa wateja wa benki hiyo, Bi.Flora Mbogo na Meneja Uhusiano wa wateja, Bw.Charles Shadrack, wakiwasikiliza washiriki mbalimbali waliohudhuria chilumbo (kongamano), hilo na wakataka kujua huduma zitolewazo na MCB
   Meneja Uhusiano wa wateja, Bw.Charles Shadrack,(kushoto), akifafanua jambo kwa washiriki hawa waliokuwa na kiu ya kujua huduma zitolewazo na benki hiyo mpya kabisa hapa nchini
   Meneja wa MCB, tawi la Samora katikati ya jiji, Bw.Cassian Clovis, (kushoto), akijadiliana jambo na Meneja Uhusiano wa wateja, Bw.Charles Shadrack, na Afisa Mikopo wa benki hiyo, Bw.Isaya Hagamu, huku chilumbo kikiendelea
   Wimbo wa taifa ukiimbwa
   Makamu Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, anayeshughulikia masuala ya Mipango, Fedha na Utawala, Dkt.Magreth Shiwa, akitoa hotuba ya kuwakaribisha wageni
  Afisa Mikopo wa benki ya MCB, Bw.Isaya Hagamu, akitoa mada juu ya upatikanaji mikopo kwenye benki hiyo.
   Naibu waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Anastazia Wambura, akitoa hotuba
   Baadhi ya washiriki wakisikiliza kwa makini
   Msanii Muhogo mchungu naye alikuwepo kwenye chilumbo (kongamano) la Kiswahili   Afisa Mikopo wa benki ya MCB, Bw.Isaya Hagamu, (wakwanza kushoto), akitoa maelezo ya shughuli zifanywazo na benki hiyo kwa washiriki hawa waliokuwa na hamu ya kutaka kujua huduma zitolewazo na benki hyo
   Afisa Mikopo wa benki ya MCB, Bw.Isaya Hagamu, akitoa mada juu ya upatikanaji mikopo kwenye benki hiyo.
   Mtunzi maarufu wa vitabu Shafi Adam Shafi naye alikuwepo
   Meneja Masoko na Uhusioano wa MCB, Bi. Rahma Ngassa, (katikati), na Meneja Uhusiano wa wateja, Bw. Charles Shadrack, (kushoto), wakimsikiliza mwenyeji wao Meneja Uhusioano wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Bi. Evelyn Mpasha  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Bw. Christopher Ole Sendeka kuchukua hatua kali kwa wote waliohusika na upotevu zaidi ya sh. bilioni moja za vyama vya ushirika.

  Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo jana jioni (Ijumaa, Januari 27, 2017) alipozungumza na watumishi wa Mkoa wa Njombe wakati wa majumuisho ya ziara yake ya kikazi ya siku saba mkoani hapa.

  Alisema kati ya fedha hizo sh. milioni 532.736 zilipotea katika SACCOS ya Kurugenzi  Njombe pamoja na sh. milioni 900 zilizopotea katika Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo kiitwacho Wafanyabiashara Njombe SACCOS.

  “Maofisa Ushirika nchini mmeendelea kudhoofisha jitihada za Serikali katika kuimarisha ushirika. Katika eneo hili ninahitaji Mkuu wa Mkoa ufuatilie suala hili na kuwachukulia hatua wahusiuka wote,” alisema.

  Waziri Mkuu aliwaagiza Wakuu wote wa Wilaya kuwatumia warajisi wa ushirika kuimarisha ushirika Mkoani Njombe.”Tunataka ushirika ulete tija kwa wananchi na hatutaki ushirika ulioambatana na harakati za kugawa watu. Endeleeni kuwashughulikia wanaushirika wasio waaminifu,”.

  Aidha, Waziri Mkuu aliwasisitiza watumishi wa umma wote nchini kuzingatia uadilifu, uaminifu, kutojihusisha na rushwa na kutumia ipasavyo fedha za umma Serikali itachukulia hatua kali dhidi ya watumishi wote wanaotumia nafasi zao kujinufaisha binafsi.

  Alisema anataarifa za Watendaji wa Wakuu wa Wilaya ya Makete akiwemo Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw. Francis Namsumbo, Mweka Hazina Bw. Edward Mdagachule, Ofisa Utumishi, Bw. Nicodemas Tindwa na Mkaguzi wa Ndani Bw. Michael Shija kuhusika na upotevu wa sh. milioni 71 zikiwemo sh milioni 41 za UNICEF.

  Waziri Mkuu alisema kuwa watumishi hao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya utoaji wa rushwa kwa vyombo mbalimbali ili kuficha ubadhilifu huo. “Mkuu wa Mkoa hakikisha hatua stahiki zinachukuliwa kuhusiana na matukio haya,”.

  Pia alimuagiza Mkuu huyo wa Mkoa kuhakikisha kuwa ……..wa Wanging’ombe Bw. Edwin Kigoda anachukuliwa hatua stahiki kwa ubadhilifu wa sh. milioni 37.9 zilizotolewa kwa ajili ya kuwajengea uwezo Walimu katika stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK).

  Mbali na watumishi hao pia Waziri Mkuu alimtaka Bw. Ole Sendeka kumchunguza na kumchukulia hatua Ofisa Ardhi wa Mji wa Njombe, Bw. Addo Kabange ambaye anatuhumiwa kuuza viwanja mara mbili, kuchukua rushwa na kujipatia viwanja vingi kwa bei nafuu na kuviuza kwa wananchi kwa bei ya juu.

  Wakati huo huo, Waziri Mkuu alisema atawaelekeza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Fedha za Serikali (CAG), Msajili wa Hazina na Mrajisi wa Ushirika kuanza kufuatilia malalamiko kuhusu umiliki wa kiwanda cha chai cha Lupembe pamoja na kufuatilia mwenendo wa mgawanyo wa hisa za kiwanda hicho.

  Alisema alipotembelea kiwanda cha chai cha Lupembe ambapo alifarijika kukuta kiwanda hicho kimeanza kufanya kazi baada ya kusimama kwa takriban miaka nane kutokana na mgogoro uliopo baina ya mwekezaji wa Kiwanda hicho na Umoja wa Wakulima wa Chai Muvyulu.

  Waziri Mkuu alisisitiza kwamba Serikali ya Awamu ya Tano haitavumilia migogoro ya kuzuia ajira kwa wananchi, hivyo aliahidi kushughulikia malalamiko kutoka pande hizo mbili na kutafuta njia ya kutatua mgogoro uliopo.

  Alisema baada ya kusomewa taarifa ya kiwanda na kwa upande mwingine taarifa ya wanaushirika alibaini kuwepo kwa mgogoro unaohitaji kutatuliwa ili kuwezesha shughuli za kiwanda kuendelea kwa amani na usalama.

  Aidha, Waziri Mkuu alielekeza shughuli za ulimaji na uvunaji wa majani ya chai kutoka kwa wakulima na kupeleka katika kiwanda hicho iendelee na kiwanda kisisimamishe kazi ili kulinda soko la wakulima na ajira za watumishi wa kiwanda hicho,” alisema.

  Alisema kwa kuwa kiwanda hicho kinamilikiwa kwa ubia, alimwelekeza Mkurugenzi wa kiwanda hicho kuhakikisha kuwa wanaweka wawakilishi wawili au watatu wa wanaushirika katika Bodi ya Kiwanda hicho.

  Katika hatua nyingine Waziri Mkuu alizungumzia suala la kuchelewa kuanza kwa mradi wa chuma cha Liganga, ambapo alisema ucheleweshaji huo si wa makusudi bali ni mpango wa Serikali wa kujiridhisha na vipengele mbalimbali vya mkataba ili uwe wa manufaa kwa Watanzania.

  Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema baada ya kutembelea eneo ambalo uchimbaji utakapofanyika, na kujionea maendelezo ya wananchi yaliyopo, alipata mashaka na kiasi cha sh. bilioni 13 kilichotengwa na wawekezaji kwa ajili ya fidia kwa wananchi watakaopisha mradi huo.

  Alisema Serikali haina budi kufanya tathmini ya kina na kujiridhisha. “Nataka nimkumbushe Mheshimiwa Mbunge (Deo Ngalawa-Ludewa) na Mwenyekiti wa NDC kujiridhisha na wahusika wanaotarajiwa kupata fidia hiyo,”.

  Akizungumzia kuhusu maslahi ya watumishi, Waziri Mkuu alisema Serikali kupitia Bodi ya Motisha na Mishahara inaendelea kufanya tathmini ya uzito wa kazi ili kupanga upya viwango vya motisha na mshahara kwa watumishi wote.

  Pia aliwasisitiza waajiri wote wakiwemo Wakurugenzi kutenga fedha kwa ajili ya likizo, masomo na uhamisho, kuandaa leave roster na mipango ya mafunzo kwa watumishi.

  (Mwisho)
         
  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMAMOSI, JANUARI 28, 2017.
                                                   

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda (kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Uwekezaji wa Zambia, Bi. Kayula Siame, wakitia saini mmoja wa Mikataba ya kuanzishwa kwa Kituo cha Pamoja cha Mpakani cha Tunduma/Nakonde, ifikapo Februari Mosi, 2017.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda (kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Uwekezaji wa Zambia, Bi. Kayula Siame, wakionesha Mikataba ya kuanzishwa kwa Kituo cha Pamoja cha Mpakani baada ya kusainiwa ili kuruhusu kuanzishwa rasmi kwa kituo cha mpakani cha Tunduma/Nakonde, ifikapo Februari Mosi, 2017.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda (kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Uwekezaji wa Zambia, Bi. Kayula Siame, wakibadilishana Mikataba ya kuanzishwa kwa Kituo cha Pamoja cha Mpakani Tunduma/Nakonde baada ya kusainiwa ili kuruhusu kuanzishwa rasmi kwa kituo hicho ifikapo Februari Mosi, 2017.

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban (kushoto), na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Uwekezaji wa Zambia, Bi. Kayula Siame, wakitia saini moja ya mikataba ya kuanzishwa kwa Kituo Cha Pamoja na Mpakani katika Mpaka wa Tunduma na Nakonde unaotarajiwa kuanza kufanyakazi rasmi Februari mosi, 2017.

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban (kushoto), na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Uwekezaji wa Zambia, Bi. Kayula Siame, wakionesha mikataba waliyosaini ili kuruhusu kuanzishwa rasmi kwa Kituo Cha Pamoja cha Mpakani katika Mpaka wa Tunduma na Nakonde unaotarajiwa kuanza rasmi Februari mosi, 2017.

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban (kushoto), na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Uwekezaji wa Zambia, Bi. Kayula Siame, wakibadilishana Mikataba waliyosaini ili kuruhusu kuanzishwa rasmi kwa Kituo Cha Pamoja na Mpakani katika Mpaka wa Tunduma na Nakonde unaotarajiwa kuanza rasmi Februari mosi, 2017.

  Makatibu Wakuu kutoka Tanzania na Zambia wanaohusika na masuala ya fedha, biashara na viwanda wakiwa katika kikao cha kupitia nyaraka mbalimbali za mikataba ya namna ya kuendesha Kituo cha Pamoja cha Mpakani, Tunduma/Nakonde, uliofanyika Jijini Mbeya. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban, Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Uwekezaji wa Zambia, Bi. Kayula Siame, Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Miundombinu wa Zambia, Mhandisi Charles Mushota, na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais wa Zambia, Bright Nundwe.

  Baadhi ya wataalamu wa sheria na masuala ya kodi kutoka Tanzania wakifuatilia kwa makini majadiliano na maboresho ya mikataba na nyaraka mbalimbali zilizosainiwa kwa ajili ya kuanzishwa rasmi kwa Kituo cha Pamoja cha Mpaka wa Tunduma/Nakonde cha nchi za Tanzania na Zambia, Jijini Mbeya.

  Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda (Kulia), akisisitiza jambo wakati wa kikao kilichowahusisha Makatibu Wakuu wa baadhi ya wizara zinazohusika na masuala ya Fedha, Biashara, viwanda na Uwekezaji kutoka nchi za Tanzania na Zambia, uliofanyika Jijini Mbeya, wakijadili namna bora ya kuanzisha Kituo cha Pamoja katika mpaka wa nchi hizo mbili wa Tunduma na Nakonde

  Baadhi ya wataalamu wa sheria na masuala ya kodi kutoka Tanzania wakifuatilia kwa makini majadiliano na maboresho ya mikataba na nyaraka mbalimbali zilizosainiwa kwa ajili ya kuanzishwa rasmi kwa Kituo cha Pamoja cha Mpaka wa Tunduma/Nakonde cha nchi za Tanzania na Zambia, mkutano uliofanyika katika eneo la Vwawa, mkoa wa Songwe.

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban (kushoto), na Mwenyekiti Mwenza wa Kikao cha kupitia Mikataba na nyaraka mbalimbali za uanzishwaji wa Kituo cha Pamoja na Mpakani (One Stop Border Post) ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Uwekezaji wa Zambia, Bi. Kayula Siame, wakiangalia Mkataba huo kabla ya kusainiwa.

  Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Bw. Jocktan Kyamuhanga (kushoto), Mtaalamu kutoka idara ya Sera Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Zuberi (katikati) na Naibu Kamishna wa TRA Bw. Charles Kichere, wakiangalia kwa makini nyaraka za kuanzishwa kwa Kituo cha Pamoja cha Mpakani kabla ya mikataba hiyo kusainiwa ili kuanzishwa rasmi kwa kituo hicho cha Tunduma/Nakonde, ifikapo Februari Mosi, 2017.

  (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)


  ……………………………………

  Benny Mwaipaja-WFM, Mbeya

  TANZANIA na Zambia, zimetiliana saini Mikataba Minne kwa ajili ya uanzishwaji rasmi wa kituo cha pamoja katika mpaka wa Tunduma na Nakonde, kitakachoanza kufanyakazi rasmi Februari mosi mwaka huu, ili kurahisisha ufanyaji biashara kati ya nchi hizo mbili


  Uamuzi wa kuanzishwa kwa huduma hiyo ijulikanayo kama One Stop Border Post, ni utekelezaji wa maagizo ya Marais wa nchi hizo Mbili, Waheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, na Edger Lungu, waliyoyatoa wakati Rais huyo wa Jamhuri ya Zambia, Edger Lungu alipofanya ziara ya kikazi hapa nchini hivi karibuni.

  Mikataba iliyotiwa saini ni makubaliano ya Mwongozo wa Utendaji wa Kituo cha Pamoja cha Tunduma/Nakonde pamoja na Mfumo wa Urahisishaji Biashara kwa lengo la kukuza biashara kati ya nchi hizo mbili.

  Waliosaini Mikataba hiyo kwaniaba ya Serikali ya Tanzania, Mjini Vwawa, wilaya ya Momba, mkoani Songwe, ni Naibu Katibu Mkuu wa Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Adolf Mkenda, huku Zambia ikiwakilishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Uwekezaji wa nchi hiyo, Bi. Kayula Siame.

  Wakizungumza baada ya kutiwa saini kwa mikataba hiyo Makatibu wakuu hao wamesema kuwa Uanzishwaji wa Kituo cha Pamoja Mpakani Tunduma/Nakonde, utarahisisha ufanyaji wa biashara kati ya Tanzania na Zambia kwa kupunguza ukaguzi kwani ukaguzi utafanyika mara moja katika kituo cha kuingia badala ya kufanyika mara mbili katika nchi zote mbili pamoja na kuongeza makusanyo ya kodi

  “Lengo la kituo hicho pia ni kuifanya biashara kati ya Tanzania na Zambia kuwa huru lakini ikifuata misingi na taratibu za kufanya biashara mpakani. Pia kitarahisisha biashara katika eneo la mpakani na kuvutia wananchi na wafanyabiashara kutoka nchi zote mbili kutumia kituo hiki na kuepuka kutumia njia zisizo rasmi kupitisha mizigo na hivyo kupunguza ufanyaji wa biashara za magendo kama si kukomeshwa kabisa” Alisisitiza Bi. Amina Khamis Shaaban

  Alisema kuwa utaratibu huo unatarajia kuona kuongezeka kwa ushirikiano kati ya taasisi za serikali za nchi hizi kwani shughuli katika kituo zitakuwa zinafanyika kwa uwazi katika eneo moja.

  Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara wa Zambia, Bi. Kayula Siame, amesema kuwa anatarajia kuwa wananchi wa nchi hizo mbili watatumia fursa ya kuwepo kituo hiki kuweza kufanikisha biashara zao na kuepuka kupitisha bidhaa zao kwa njia za magendo ama njia za panya ili kukwepa kukamatwa na vyombo vya dola.

  Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji wa Tanzania, Prof. Adolf Mkenda, alieleza kuwa kuboresha kwa huduma katika Mpaka huo wa Tunduma na Nakonde utaongeza biashara ya kusafirisha mizigo katoka Bandari ya Dar es salaam kwenda Zambia na nchi nyingine jirani.

  Kwa upande wake Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Charles Kichere Amesema kuwa huduma hiyo itaanza Februari mosi mwaka huu kwa kutumia majengo ya forodha yaliyopo katika mpaka huo wa Tunduma na Nakonde nchini Zambia baada ya kufanyiwa ukarabati na kuwekwa mifumo ya teknohama, wakati kazi ya ujenzi wa kituo kipya kwa upande wa Tanzania ukiendelea kujengwa.

  Kituo cha Tunduma/Nakonde kitakuwa kituo cha Tano kufanya kazi baada vituo vinne kukamilika na kufanya kazi katika mipaka ya Tanzania na nchi jirani za Kenya, Rwanda na Burundi.

  Vituo hivyo ni Holili-Taveta katika mpaka wa Tanzania na Kenya, Kituo cha Rusumo katika mpaka wa Tanzania na Rwanda, Mutukula katika mpaka wa Tanzania na Uganda na Kabanga/Kobela katika mpaka wa Tanzania na Burundi.

  Kwa upande wa Zambia, hiki kitakuwa kituo cha Pamoja cha Mpakani cha pili baada ya kituo cha Chilundu kilichopo katika mpaka wa Zambia na Zimbabwe.

  0 0


  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mbarawa (katikati) akiwa ameongozana na Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mhandisi. Profesa Zacharia Mganilwa pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mhandisi. Profesa Blasius Bavomara baada ya kupokelewa na Bendi ya Jeshi la Polisi kuelekea kwenye viwanja vya chuo tayari kwa ajili ya kuanza sherehe ya mahafali ya 32 ya chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) 27/01/2017 jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mbarawa ambaye alikuwa mgeni rasmi akiwahutubia Wahitimu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wakati wa mahafali ya 32 ya chuo hicho yaliyofanyika leo 27/01/2017 chuoni hapo jijini Dar es Salaam.

  Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mhandisi. Profesa Zacharia Mganilwa akiwahutubia Wahitimu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wakati wa mahafali ya 32 ya chuo hicho yaliyofanyika leo 27/01/2017 chuoni hapo jijini Dar es Salaam.  Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mhandisi. Profesa Blasius Bavo Nyichomba akiwahutubia Wahitimu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wakati wa mahafali ya 32 ya chuo hicho yaliyofanyika leo 27/01/2017 chuoni hapo jijini Dar es Salaam.  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mbarawa (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mhandisi. Profesa Zacharia Mganilwa wakati wa mahafali ya 32 ya chuo hicho yaliyofanyika leo 27/01/2017 chuoni hapo jijini Dar es Salaam.  Baadhi ya Wahitimu wa kozi mbalimbali toka chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wakisikiliza hotuba za Viongozi mbalimbali wakati wa mahafali ya 32 ya chuo hicho yaliyofanyika leo 27/01/2017 chuoni hapo jijini Dar es Salaam.

  Baadhi ya Viongozi na Watendaji wa chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi wakati wa mahafali ya 32 ya chuo hicho yaliyofanyika leo 27/01/2017 chuoni hapo jijini Dar es Salaam.

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mbarawa(aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wahitimu wa kozi mbalimbali toka chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) mara baada ya kuwatunuku Stashahada ya Uzamili, Shahada, Stashahada na Astashahada wahitimu hao leo 27/01/2017 jijini Dar es Salaam.

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mbarawa(aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) pamoja na Wafanyakazi wa chuoni hapo mara baada ya mahafali yaliyofanyika leo 27/01/2017 jijini Dar es Salaam.


  Wahitimu pamoja na Viongozi mbaimbali wakiwa katika maandamano kuelekea viwanja vya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kwa ajili ya kumpokea mgeni rasmi na shughuli ya mahafali kuanza chuoni hapo leo 27/01/2017 jijini Dar es Salaam.


  (Picha/Habari na Benedict Liwenga-WHUSM)  SERIKALI iko mbioni kujenga Reli ya Kati kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro yenye kutumia umeme ambayo itakuwa ikisafiri kwa kasi ya Kilomita 160 kwa saa.

  Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mnyaa Mbarawa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 32 ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).

  Mhe. Mbarawa amesema kwamba kwa sasa Serikali iko katika hatua za mwisho za kumpata mzabuni atakayejenga reli hiyo kwa kiwango cha Kisasa (Standard Gauge).

  “Reli hiyo sio Garimoshi, ni reli itayotumia umeme, kwahiyo kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro tutaweza kwenda kwa saa moja na nusu ambapo ndani ya reli hiyo kutakuwa na huduma nzuri na za kisasa ikiwemo huduma ya intaneti na mambo mengine mengi”, alisema Profesa Mbarawa.

  Katika hatua nyingine Mhe. Mbarawa amewapongeza Wahitimu wa kozi mbalimbali kwa bidii zao walizozifanya wakati wa masomo yao kuwataka kutumia hazina kubwa ya elimu waliyoipata chuoni hapo kwa manufaa yao binafsi, ya familia na Taifa kwa ujumla.

  “Tunasherehekea mahafali haya ya 32 huku chuo kikiwa kimebadilika na kupiga hatua za haraka katika miaka 42 ya kuwepo kwake tangu kianzishwe mwaka 1975, maendeleo makubwa yameonekana na sisi sote ni mashahidi, na maendeleo haya yasingeonekana bila juhudi za pamoja kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Ujenzi pamoja na juhudi za Baraza la Uongozi, Uongozi wa Chuo, nyie Wanafunzi, wadau wengine na Watanzania wote kwa ujumla, nachukua fursa hii kuwapongeza sana kwa kazi kubwa mlioifanya”, alisema Profesa Mbarawa.

  Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji, Mhandisi Profesa Zacharia M.D Mganilwa amesema kuwa, anaishukuru Serikali kwa ushirikiano mkubwa inaoutoa katika chuo hicho tangu kuanzishwa kwake takribani miaka 42 iliyopita ambapo ametaja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana ikiwemo ongezeko la Wahitimu toka 688 katika Mahafali ya 31 hadi kufikia wahitimu 1,118 katika mahafali hayo ya 32 ya chuo hicho.

  Ameongeza kuwa, mafaniko mengine yanaonekana katika upande wa elimu ya mafunzo yatolewayo chuoni hapo, kuwa ni chuo pekee kinachotoa mafunzo katika sekta ya usafirishaji na uchukuzi, hivyo kimekuwa kikitoa mafunzo kuanzia ngazi ya watendaji yaani Astashahada na shahada na pia kwa Mameneja.

  Amezitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili chuo hicho kuwa ni upatikanaji wa vifaa vya kufundishia ambavyo huendana na mabadiliko ya kiteknolojia na baadhi ya vifaa hivyo ni aghali, vile vile suala la mahitaji ya Wataalam katika nyanja mbalimbali ambapo miundombinu iliyopo imekuwa haitoshelezi idadi ya wanafunzi wanaosoma chuoni hapo.

  Awali kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi katika mahafali hayo, Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi wa Chuo hicho, Mhandisi. Profesa Blasius Bavo Nyichomba amesema kuwa, chuo hicho kwa sasa kipo katika mkakati wa kuendelea kutafuta fedha za kununua vitendea kazi kupitia mapato ya ndani pamoja na fedha toka kwa wadau mbalimbali wa maendeleo ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia.

  Katika mafahali hayo yaliyofanyika leo 28 Januari, 2017, jumla ya Wahitimu 1,118 wamehitimu katika kozi mbalimbali za Stashahada ya Uzamili, Shahada, Stashahada na Astashahada zitolewazo na Chuo hicho.

  0 0

  Naibu waziri wa Nishati na madini Dr,Merdadi Kalemani akiwasilia katika mgodiwa wa RZ ambako kumetokea tukio la watu 14 kufukiwa na udongo wakati wakiendelea na kazi za uchimbaji.
  Mbunge wa Jimbo la Busanda ,Lorencia Bukwimba akielekea kwenye eneo la shimo ambapo watu wamefunikwa.
  Mbunge wa Jimbo la Busanda ,Lorencia Bukwimba akiwapa pole ndugu na jamaa ambao walikuja kujua kile ambacho kitaendelea kwa undugu zao.
  Wananchi wakiwa nje ya Ngome ya mgodi wakifatilia kile ambacho kinaendelea
  Sehemu ambayo inatumiwa kutolea udongo.
  Ndugu wakiwa katika masikitiko makubwa wakijiuliza ni lini ndugu zao watatoka shimoni.
  Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja jenerali Ezekiel Kyunga akiwa katika eneo la tukio akifatilia kile kinachoendelea
  Mkuu wa wilaya ya Geita,Herman Kapufi akipandisha juu baada ya kutoka shimoni
  Naibu waziri wa nishati na madini,Dr Medadi Kalemani akioneshwa baadhi ya maeneo yaliyopata dosari kwenye mgodi huo

  …………………………………………………………………..
  IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE


  NAIBU waziri wa Nishati na Madini Dk. Medard Kalemani ametembelea Mgodi wa RZ uliofukia Watanzania 13 na raia mmoja wa Nchini China anayetambulika kwa jina la Meng Juping na kusema kuwa serikali itaendelea kuweka nguvu ili kusaidia uokoaji.

  Katika ziara yake hiyo ya dharura Naibu Waziri huyo ametoa pole kwa niaba ya serikali kwa uongozi wa Mkoa, Wananchi pamoja na Mgodi huo kukumbwa na tukio hilo.

  Mara baada ya kupokea taarifa ya maafa hayo, iliyosomwa na kamishina msaidizi wa madini kanda ya ziwa victoria, Dk. Kalemani aliutaka uongozi wa Mkoa pamoja kamati ya uokoaji kujikita zaidi kwenye shughuli ya uokojai na waachane na mambo mengine ambayo yanaweza yakasababisha zoezi hilo liwe gumu.

  ‘’Ndugu zangu mimi kwa niaba ya serikali kuu napenda nitoe pole kwa hiki kilichowakumba Mkoa pamoja na Mgodi lakini napenda kuwaambia kuwa Kamati ya ulinzi na Usalama pamoja natimu ya uokoaji mhakikishe mnasimamia vyema zoezi hili ili tuwaokoe ndugu zetu ambao wamo humo ndani ya shimo,’’alisema Naibu waziri Kaleman.

  ‘’Kingine niagize hapa hakikisheni mnatoboa shimo kwa kutumia drilling ili tupate mwanya wa kuwapatia chakula ndugu zetu ambao wamefukiwa na udongo wakati juhudi za kufukua zikiendelea ,’’aliongeza.

  Akizungumza na Maduka online mapema asubuhi ya leo kamishina msaidizi wa madini kanda ya ziwa victoria Yahaya Samamba alisema kuwa kamati ya uokozi kwa kushirikiana kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Geita, ilibadilisha mfumo wa uokoaji kwa kutumia wachimbaji wadogowadogo baada ya mashine za kisasa kufikia usawa mita 20 ambazo haziwezi kuhimili uzito.

  ‘’Mitambo hii imekomea mita 20 tumeona tutumie wachimbaji wadogo ili twende sambaba na uokoaji uliosalama..kwahiyo usiku wa jana (juzi) saa 5:00 kamili usiku tulisitisha kutumia mashie yaani Magreda kutokana na usawa tuliofikia kuwa laini,’’alisema Samamba.

  Kwa upande wake Mhandisi kutoka kampuni ya uchimbaji ya Busolwa Mine Eng. Nayompa wakati akitoa mtazamo wake namna zoezi hilo linavyokuwa gumu alisema ramani zinazotolewa na wachina ni za kubahatisha na hawana uhakika nazo ndizo sababu zimechelewesha uokoaji na zoezi kuonekana halikamiliki kwa wepesi.

  “Mimi ninachokiona hapa wachina hawa ndugu zetu wachina wameshindwa kutupatia ramani ya uhakika ndiyo maana tunabahatisha bahatisha tu..mwandishi hata wewe jana ulikuwa shuhuda namna gari la kutoboa lilivyoshindwa kulenga kwenye shimo walipo ndugu zetu,’’alisema Eng. Nayompa.

  Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Busandwa ambako tukio hilo limetokea Lolensia Bukwimba alisema haipaswi watu kunyosheana kidole kwa sasa wakati nguvu na jtighada zikiendelea kufanywa.

  Hata hivyo Rais wa shirikisho wa vyama vya wachimbaji wa madini ,John Wambura Bina,amepongeza juhudi ambazo zinafanyika kwa makapuni ya madini kujitolea pamoja na serikali na wanaamini kuwa juhudi za uokoaji zinazoendelea zinaweza kuzaa matunda.

  Viongozi mbalimbali wa serikali na chama jana walitembelea eneo la Mawemeru kuliko mgodi wa RZ ambao unamilikiwa na wawekezaji wa Kichina huku leseni ya madini ikiwa ni ya Mtanzania Ahamed Mbaraka.

  Matumaini kwa siku ya leo yanaonekana kwani hadi kufikia majira ya saa moja kamili watu ambao wapo chini waligonga bomba kwa kuashiria kuwa wapo karibu na sehemu ya kutokea.

  0 0

  Na Benedict Liwenga

  Serikali iko mbioni kujenga Reli ya Kati kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro yenye kutumia umeme ambayo itakuwa ikisafiri kwa kasi ya Kilomita 160 kwa saa.

  Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mnyaa Mbarawa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 32 ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).

  Mhe. Mbarawa amesema kwamba kwa sasa Serikali iko katika hatua za mwisho za kumpata mzabuni atakayejenga reli hiyo kwa kiwango cha Kisasa (Standard Gauge).

  “Reli hiyo sio Garimoshi, ni reli itayotumia umeme, kwahiyo kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro tutaweza kwenda kwa saa moja na nusu ambapo ndani ya reli hiyo kutakuwa na huduma nzuri na za kisasa ikiwemo huduma ya intaneti na mambo mengine mengi”, alisema Profesa Mbarawa.

  Katika hatua nyingine Mhe. Mbarawa amewapongeza Wahitimu wa kozi mbalimbali kwa bidii zao walizozifanya wakati wa masomo yao kuwataka kutumia hazina kubwa ya elimu waliyoipata chuoni hapo kwa manufaa yao binafsi, ya familia na Taifa kwa ujumla.

  “Tunasherehekea mahafali haya ya 32 huku chuo kikiwa kimebadilika na kupiga hatua za haraka katika miaka 42 ya kuwepo kwake tangu kianzishwe mwaka 1975, maendeleo makubwa yameonekana na sisi sote ni mashahidi, na maendeleo haya yasingeonekana bila juhudi za pamoja kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Ujenzi pamoja na juhudi za Baraza la Uongozi, Uongozi wa Chuo, nyie Wanafunzi, wadau wengine na Watanzania wote kwa ujumla, nachukua fursa hii kuwapongeza sana kwa kazi kubwa mlioifanya”, alisema Profesa Mbarawa.

  Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji, Mhandisi Profesa Zacharia M.D Mganilwa amesema kuwa, anaishukuru Serikali kwa ushirikiano mkubwa inaoutoa katika chuo hicho tangu kuanzishwa kwake takribani miaka 42 iliyopita ambapo ametaja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana ikiwemo ongezeko la Wahitimu toka 688 katika Mahafali ya 31 hadi kufikia wahitimu 1,118 katika mahafali hayo ya 32 ya chuo hicho.

  Ameongeza kuwa, mafaniko mengine yanaonekana katika upande wa elimu ya mafunzo yatolewayo chuoni hapo, kuwa ni chuo pekee kinachotoa mafunzo katika sekta ya usafirishaji na uchukuzi, hivyo kimekuwa kikitoa mafunzo kuanzia ngazi ya watendaji yaani Astashahada na shahada na pia kwa Mameneja.

  Amezitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili chuo hicho kuwa ni upatikanaji wa vifaa vya kufundishia ambavyo huendana na mabadiliko ya kiteknolojia na baadhi ya vifaa hivyo ni aghali, vile vile suala la mahitaji ya Wataalam katika nyanja mbalimbali ambapo miundombinu iliyopo imekuwa haitoshelezi idadi ya wanafunzi wanaosoma chuoni hapo.

  Awali kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi katika mahafali hayo, Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi wa Chuo hicho, Mhandisi. Profesa Blasius Bavo Nyichomba amesema kuwa, chuo hicho kwa sasa kipo katika mkakati wa kuendelea kutafuta fedha za kununua vitendea kazi kupitia mapato ya ndani pamoja na fedha toka kwa wadau mbalimbali wa maendeleo ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia.

  Katika mafahali hayo yaliyofanyika leo 28 Januari, 2017, jumla ya Wahitimu 1,118 wamehitimu katika kozi mbalimbali za Stashahada ya Uzamili, Shahada, Stashahada na Astashahada zitolewazo na Chuo hicho.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Makamu wa  Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika  uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Januari 28, 2017 wakati akielekea kupanda ndege kuelekea  Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU).
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa  katika  uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Januari 28, 2017 wakati akielekea kupanda ndege kuelekea  Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU).
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wakuu wa vikosi vya ulinzi na usalama  katika  uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Januari 28, 2017 wakati akielekea kupanda ndege kuelekea  Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU).
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wakuu wa vikosi vya ulinzi na usalama  katika  uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Januari 28, 2017 wakati akielekea kupanda ndege kuelekea  Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU).
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wafanyakazi katika  uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Januari 28, 2017 wakati

  akielekea kupanda ndege kuelekea  Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU).
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Mungano wa Visiwa vya Comoro Mhe. Azali Assoumani walipokutana kwenye ndege katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Jumamosi Januari 28, 2017 tayari kwa safari ya Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU). Rais Assoumani alikuwa akitokea Comoro kupitia Dar es salaam. Picha na IKULU


  0 0


  Na. Lilian Lundo – MAELEZO

  Mratibu Elimu Kata (MEK) ni mmoja kati ya kiungo kikubwa kati ya ofisi ya elimu ya wilaya na shule za Serikali katika ngazi ya kata ambaye ndiye mfuatiliaji mkubwa wa maendeleo ya elimu ndani ya kata.

  Shughuli nyingine zinazofanywa na MEK ni pamoja na kufuatilia maendeleo ya taalamu ya wanafunzi katika kata yake, kukagua ufundishaji wa walimu, kufuatilia mahudhurio ya wanafunzi pamoja na kusimamia vikao mbalimbali vya shule zilizoko katika kata yake.

  Asilimia kubwa ya Waratibu Elimu Kata walikuwa wanashindwa kufikia malengo ya kazi zao kutokana na changamoto ya usafiri, ambapo wengi wao walikuwa wakitumia usafiri wa baiskeli ambao ha ukuwa usafiri rafiki kutokana na kazi yao ya kukagua shule zote katika kata wanazozisimamia.

  Serikali kwa kuliona hilo, kupitia Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (EQUIP-T) ilitoa pikipiki kwa kila MEK katika mikoa ya Dodoma, Kigoma, Lindi, Shinyanga, Simiyu na Mara ili kurahisha ufuatiliaji wa mendeleo ya shule zao kwa urahisi.

  Pikipiki hizo zimeleta mafanikio kwa kupunguza idadi ya wanafunzi watoro, kiwango cha ufaulu kupanda kutokana na ukaguzi wa mara kwa mara wa walimu pamoja na matatizo kutatuliwa kwa haraka kufuatia taarifa za shule kufika ofisi za wilaya kwa wakati.

  Sweetbert Malimi ni Mratibu Elimu Kata wa Sanzawa Wilaya ya Chemba, Mkoani Dodoma anasema kwamba Pikipiki imemuwezesha kushughulikia kwa wakati matatizo yanayotokea katika shule anazozisimamia tofauti na kipindi ambacho hakuwa na pikipiki.

  Anaendelea kusema kuwa, matatizo yalipokuwa yakitokea katika shule anazosimamia yalikuwa yakimsubiri MEK hata kwa mwezi mzima. Lakini sasa hivi hali imekuwa tofauti kutokana na urahisi wa kufikika kuzitembelea kutembelea shule zake hata mara mbili kwa wiki.

  Vilevile, Mratibu Malimi amesema kuwa ameweza kukagua na kufuatilia kwa wakati maendeleo ya taaluma ya wanafunzi pamoja na ufundishaji wa walimu ambapo kabla ya kuwa na pikipiki kulikuwa na baadhi ya walimu walijisahau kutokana na kutokaguliwa mara kwa mara.

  Anaendelea kwa kusema kuwa, ufuatiliaji huo umeletea mafanikio makubwa katika Mkoa wa Dodoma, ambapo ufaulu wa darasa la saba kwa wilaya ya Chemba peke yake ulipanda kutoka asilimia 30 mwaka 2015 mpaka asilimia 46 mwaka 2016. 

  Kwa upande wake Mratibu Elimu Kata wa Songambele iliyoko Wilaya ya Kongwa, Mkoani Dodoma amesema kuwa katika kata yake ana shule Sita za kuzifuatilia ambapo kabla ya kupata pikipiki alikuwa anatumia baiskeli kutembelea shule hizo na aliweza kutembelea shule hizo mara moja kwa wiki.

  Baada ya kupata pikipiki anauwezo wa kutembelea shule hizo mara tatu hadi nne kwa wiki akifuatilia maandalio ya walimu, maazimio ya kazi, utengenezaji wa zana za kujifunzia na kufundishia, mahudhurio ya wanafunzi pamoja na kuhudhuria vikao vya kamati ya shule.

  Aidha, amesema kuwa kutokana na ufuatiliaji huo wa mara kwa mara katika shule hizo kumepelekea umakini mkubwa wa ufundishaji wa walimu kwa kufuata taratibu za ufundishaji kama vile kuwa na maandalio, maazimio ya kazi pamoja na kuwa na zana za ufundishaji.

  Pia amesema kuwa kwa kutumia pikipiki aliyopewa amekuwa akiwatembelea wazazi ambao watoto wao ni watoro, na kuwashauri juu ya umuhimu wa elimu kwa watoto wao na wazazi wenyewe. Juhudi hizo zimepelekea wazazi wengi kubadilika na wamekuwa na mtazamo chanya kwa kushirikiana na walimu katika kufuatilia mahudhurio na maendeleo ya taaluma ya watoto wao.

  Nae, Mratibu Elimu Kata wa Kagera Manispaa ya Kigoma Mkoani Kigoma Jovitus Augustus anasisitiza kuwa kabla ya kupewa pikipiki kata yake ilikuwa na changamoto ya utoro kwa wanafunzi pamoja na ufaulu duni wa wanafunzi wa darasa la saba.

  “Pikipiki niliyopewa kupitia mpango wa EQUIP-T umeniwezesha kutengeneza mipango kazi ya wiki na kuisambaza katika shule zote za kata pamoja na kufuatilia utekelezaji wake,” alifafanua Jovitus.

  Ameendelea kusema kuwa pikipiki hiyo imemuwezesha kukagua utekelezaji na utoaji taaluma kwa kukagua maazimio ya kazi na maandilio ya somo pamoja na kufanya vikao vya mara mara kwa mara na walimu ili kupata maelezo ya walimu walioshindwa kutekeleza wajibu wao.

  Aidha, kupitia juhudi hizo zilizofanyika, ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba shule za msingi za kagera na Mgumile ulipanda pamoja na mahudhurio ya walimu na wanafunzi katika kata hiyo umeongezeka.

  Vilevile, umeanzishwa utaratibu wa mitihani ya kata kwa darasa la saba pamoja na kuweka kambi kwa wanafunzi wanaojiandaa na mitihani wa darasa la Saba.

  Kwa upande wake mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi ya Mazoezi Bunda iliko Halmashauri ya Mji Bunda Mkoa wa Mara, Mwalimu Vicent Ndunguru, aliipongeza Serikali kupitia Mpango wa EQUIP-T kwa kutoa pikipiki kwa Waratibu Elimu Kata ambao kwa kiasi kikubwa umewarahisishia utendaji kazi wao.

  Amesema kuwa mambo mengi yalikuwa hayaendi yalivyotakiwa kuwa kutokana na MEK kutotembea shule mara kwa mara kutokana na ukosefu wa usafiri wa uhakika.

  Kupatiwa pikipiki MEK imekuwa chachu ya kutembelea shule zilizochini ya kata yake mara kwa mara ili kufuatilia maendeleo ya shule na kuwasilisha taarifa zake ofisi za elimu wilaya kwa wilaya kwa wakati.

  Mwalimu Ndunguru ambaye pia ni Msaidizi wa MEK katika kata ya Nyasura amesema kuwa, MEK huyo amekuwa msimamizi bora wa elimu kwa kuitisha vikao vya mara kwa mara kujadili maendeleo ya shule katika kata yake, shule ya Msingi Mazoezi Bunda ndio eneo lilochaguliwa kwa ajili ya kufanyia mikutano hiyo.

  Ndunguru ameendelea kusema kuwa, MEK huyo amekuwa chachu ya maendeleo ya shule zilizoko katika kata hiyo hasa baada ya kuwa na uhakika na usafiri ambao kwa asilimia kubwa umemuwezesha kufanya kazi zake kwa urahisi na hata kufikia malengo aliyowekewa na mwajiri wake na yale aliyojiwekea yeye mwenyewe katika kuhakikisha ubora wa elimu uaongezeka siku hadi siku kutoka ngazi ya kata mpaka Taifa.

  Mwalimu Ndunguru ameishukuru Serikali kwa jitihada ya kujali sekta ya elimu, na kuiomba Serikali kuendeleza utaratibu wa ugawaji wa pikipiki kwa Waratibu Elimu Kata wa mikoa mingine iliyobaki ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi kama ambavyo wenzao waliopewa pikipiki walivyoweza kufanikiwa kupandisha kiwango cha ufaulu na kukomesha tatizo la utoro kwa wanafunzi.

  Serikali kupitia mpango huo pia umetoa vishikwambi kwa Waratibu Elimu Kata hao, ambao wamekuwa wakitumia vifaa hivyo kwa ajili ya kupokea taarifa kutoka kwa walimu wakuu wa shule wanazozisimamia na wao kuzituma taarifa hizo ofisi za elimu za wilaya.

  Mpango wa EQUIP-T tayari umeshatoa jumla ya pikipiki 1,000 kwa Waratibu Elimu Kata wa mikoa ya Dodoma, Kigoma, Lindi, Shinyanga, Simiyu, Shinyanga na Mara ambazo zilitolewa kati ya mwaka 2014 na 2015 na wanawaezesha waratibu hao kupata fedha ya mafuta na utengenezaji wa pikipiki hizo kila mwezi.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na baadhi ya wanawake wa Njombe kabla ya kuondoka kwenye Ikulu ndogo baada ya kuhitimisha ziara yake ya mkoa huo Januari 28, 2017. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Njombe, Luth Msafiri.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mkuu wa wilaya ya Njombe, Luth Msafiri kwenye Ikulu ndogo ya Njombe baada ya kuhitimisha ziara yake ya mkoa huo, Januari 28, 2017. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Shindano la kumsaka mlimbwende wa MISS KIBOSHO 2017 Jijini Mwanza limeanza jana katika viunga vya Kibosho Luxury Bar iliyopo Kiseke Ilemela Jijini Mwanza ambapo wanyange 10 wanawania nafasi hiyo.

  Wanyange hao kama wanavyoonekana pichani ni Caren Nestory, Dorice Ezra, Jullieth Michael, Elizabeth Faustine, Christina Lucas, Nasra Ramadhan, Jacline Moses, Denzry Michael, Kephlin Jacob na Aida Gazar.

  Shindano hilo limeandaliwa na Raj Entertainment kwa udhamini wa Kibosho Luxury Bar, Wema Salon na Ngenda Salon huku likiwa limelenga kukuza sanaa ya ulimbwende kuanzia za mitaa hadi kitaifa.

  Baada ya usiku ya kuamkia leo wanyange hao kuchuana vikali, fainali itafanyika leo kuanzia majira ya saa moja jioni katika viunga hivyo vya Kibosho Luxury Bar Kiseke Jijini Mwanza kwa kiingilio cha shilingi 5,000 tu.
  Binagi Media Group
  Wanyange wa shindano la Miss Kibosho 2017 wakionesha makeke yao jukwaani
  Washereheshaji wakimtambulisha Matron wa Miss Kibosho 2017, Fania Hassan (katikati) ambaye alikuwa Miss Utalii nchini mwaka 2006.
  Kila mlimbwende alionesha makeke ya hali ya juu hadi kuwapa wakati mgumu majaji. Kumbuka majaji ni Leonald Kaduguda (kushoto), Mama Ngenda Lutalo (katikati) na Mwl.Tatu Ngelengela (kulia).
  Umakini katika kufuatilia kinyang'anyiro cha Miss Kibosho 2017
  Majaji wakiahilisha shindano la Miss Kibosho 2017 usiku wa kuamkia leo. Kushoto ni Leonald Kaduguda, Mama Ngenda Lutalo (kulia) na Mwl.Tatu Ngelengela (katikati). Fainali itafanyika leo jioni kuanzia majira ya saa moja kamili.

  0 0

  MADI
  Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi wakiwasili katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro,Maawenzi wakiwa  wamebeba zawadi mbalimbali kwa ajili ya kutoa kwa wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo
  Katibu wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro,Mawenzi ,Boniface Lyimo akizungumza mara baada ya kuwapokea Madiwani hao na kutoa maelekezo ya namna ya kutoa zawadi hizo kwa wagonjwa waliolazwa katika Hospitali hiyo
  Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi,wakielekea katika wodi walimolazwa wagonjwa kwa ajili ya kutoa zawadi.
  Mwenyekiti wa Madiwani wa Chadema na Diwani wa kata ya Kiusa,Stephen Ngasa akikabidhi zawadi ya sabuni ya unga kwa wagonjwa waliolazwa katika Hopstali ya Mawenzi.
  Diwani wa kata ya Mawenzi,Hawa Mushi akitoa zawadi kwa mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika hospitali hiyo.
  Diwani wa kata Pasua ,Charles Mkalakala akikabidhi zawadi kwa mmoja wa wagonjwa katika Hospitali hiyo.
  Madiwani wakiongojea kuingia katika wodi nyingine kwa ajili ya kutoa zawadi kwa wagonjwa katika hospitali hiyo.
  Madiwani wakitoa zawadi katika wodi ya wanawake Hospitali ya Mawenzi
  Mwenyekiti wa Madiwani wa Chadema,Stephen Ngasa akizungumza na baadhi ya viongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro,awenzi mara baada ya kuhitimisha zoezi la kutoa zawadi kwa wagonjwa pamoja na kusafisha mazingira katika Hospitali hiyo.
  Mwenyekiti wa Madiwani wa Chadema,Stephen Ngasa akiagana na katibu wa Hosptali ya Mawenzi ,Boniface Lyimo mara baada ya kuhitimisha zoezi la kutoa zawadi na kusafisha mazingira ya hosptali hiyo.Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

  0 0


  Diwani wa Kata ya Pongwe (CCM) Mbaraka Sadi akiangalia namna wanavyoandika wanafunzi wanaosoma shule ya Msingi ya Mchanganyika Kata ya Pongwe Jijini Tanga wakati wa ziara yake
  Diwani wa Kata ya Pongwe (CCM) Mbaraka Sadi wa kwanza kushoto akisikiliza kero za wanafunzi hao.
  Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule ya Msingi Mchanganyiko ya Pongwe ya wanafuzi wasiosikia na wenye matatizo ya ngozi (Albino),Waziri Mfaume kulia akimuonyesha diwani wa Kata ya Pongwe (CCM) Mbaraka Sadi maeneo yenye mapori yaliyozunguka shule hiyo ambayo ni hatari kwa usalama wa wanafunzi hao wakati wa ziara ya diwani huyo

  WATOTO wenye ulemavu wa ngozi na wasioona wanaosoma shule ya msingi ya mchanganyiko ya Pongwe iliyopo Jijini Tanga wapo hatarini kuvamiwa na watu waovu na kuwafanyia vitendo vya kikatili kutokana kukosa uzio na sehemu kubwa kuzungukwa na pori ambalo ni hatari kwa usalama wao.

  Shule hiyo ambayo inapokea watoto wenye matatizo hayo kutokana mikoa mbalimbali Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa ya kukosekana uzio huku sehemu kubwa ikipakana na pori jambo ambalo linaweza kusababisha hatari kwa ustawi wao kielimu.

  Hayo yalibainishwa na Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule hiyo, Waziri Mfaume wakati wa ziara ya Diwani wa Kata ya Pongwe (CCM) Mbaraka Sadi aliyoifanya kuangalia changamoto ambazo zinaikabili na kuona namna ya kuzipatia ufumbuzi.

  Waziri alisema licha ya kufanya jitihada kubwa za kuanza ujenzi wa
  uzio huo eneo la mbele ya shule hiyo lakini mpaka sasa hakuna msaada wowote ambao wamekuwa wakiupata ili kukabiliana na tatizo hilo ambalo linatishia usalama wa watoto hao.

  Alisema awali changamoto hiyo ilikuwa eneo la mbele ya shule hiyo na kuona namna ya kulipatia ufumbuzi haraka ikiwa ni mkakati wa kuendelea kuwavutia wadau kuweza kusaidia lakini suala hilo mpaka sasa limeshindwa kupatiwa tiba.

  “Awali tuliona tuanze kujenga ujenzi wa fensi mbele ya shule hii
  lengo likiwa kuwavuta wadau wengine ili kutusaidia lakini tukashindwa kujenga eneo ambalo ni pori kubwa na hivyo ni hatari kwa usalama wa wanafunzi “Alisema.

  Aidha alisema licha ya jambo hilo lakini lingine ambalo limekuwa
  kikwazo kwao kwenye suala la usalama ni walinzi ambao wanalinda shule hiyo ambao ni mgambo wanaotumia virungu na mapango ambazo ni silaha ndogo kuweza kuwakabili wahalifu.

  “Ukiangalia kwenye shule hii tuna wanafunzi 87 ikiwa ni mchanganyiko wa walemavu wenye ualibinisimu,wasiosikia na wengine hawaoni hivyo ni hatari sana iwapo kutakuwa hakuna uzio na hawa wanatoka mikoa mbalimbali hapa”Alisema .

  Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo, Diwani wa Kata ya Pongwe (CCM) Mbaraka Sadi alisema shule hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa ya uzio kwa sababu ipo kwenye mazingira magumu kwani imezungukwa na pori ambalo ni hatari kwao.

  “Hii changamoto ni kubwa sana na hatari kwa usalama wa wanafunzi wanaosoma kwenye shule hiyo hivyo niwaombe wadau wa elimu,viongozi na serikali kuona namna ya kusaidia jambo hilo kwa maendeleo ya taalumu za watoto hao “Alisema.

  Hata hivyo alisema pia suala la uhaba wa madarasa kwenye shule hiyo atalichukua na kulifikisha kwenye kikao cha baraza la madiwani ili waweze kuona namna ya kuyashughulikia.

  Naye kwa upande wake,Mwenyekiti wa Mtaa wa Pongwe,Hemed Kileo alisema kukosekana kwa uzito kwenye shule hiyo ni jambo la hatari hivyo kuziomba mamlaka husika kuona namna ya kulishughulikia.

  Alisema shule hiyo ambayo ilianzishwa mwaka 1948 ikiwa na darasa la kwanza mpaka la sita ambayo walikuwa wakisoma wakoloni kabla ya mwaka 1957 kubadilishwa matumizi na kuwa shule ya bweni na baadae ikiwa ni ya mchanganyiko .


  Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

  0 0


  NA CHRISTINA MWAGALA,Dar es Salaam

  MEYA wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amewataka Madaktari ,wauguzi pamoja na watoa huduma za afya katika Hospitali Vijibweni kutumia taaluma yao vizuri ili kuwawezesha wananchi wa eneo hilo kupata huduma nzuri.

  Meya Isaya ametoa ushauri huo jijini Dar es Salaam jana katika hafla iliyoandaliwa na wauguzi wa Hospitali hiyo iliyopo Wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam wakati walipokuwa wakiuwaga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka 2017.

  Katika hafla hiyo pamoja na mambo mengine Meya Isaya alisisitiza kwamba kila mmoja anapaswa kufanya kazi kwa upendo kwani kazi yao ni yawito kuliko sekta nyingine.

  Alisema wananchi wanapopata huduma nzuri hupata faraja lakini wanapokumbwa na misukosuko kwa watoa huduma sio jambo zuri kwani unaweza kumuongezea mgonjwa maradhi mengine na hivyo akawasihi wafanye kazi zao kwa upendo.

  “ Niko pamoja na nyinyi, najua kazi yenu hii ni yawito, lakini mnaposhindwa kufanya kama ambavyo imekusudiwa hili ni tatizo, kwanini mpate sifa mbaya katika huduma yenu?” aliuliza Meya Isaya.

  Awali akisoma risala Dokta wa hospitali hiyo, alisema kwamba Hospitali hiyo inatoa huduma za rufaa kwa Kata za vijibweni ,Mjimwema, Kigamboni, Tungi, Somangila, Kibada na maeneo yote ya manispaa ya Kigamboni ambapo kwa sasa hospitali hiyo ndio inayofanya kazi za hospitali ya Wilaya katika manispaa ya Kigamboni.

  Alieleza kwamba Hospitali hiyo inatoa huduma za wagonjwa wa nje (OPD) na ndani (IPD) pamoja na vipimo mbalimbali vya maabara na Ultrasound, Huduma za meno, Macho, Kisukari, huduma za maabara, baba na mtoto, magonjwa ya akili ,wagonjwa walio na maambukizi ya Ukimwi pamoja na mazoezi ya viungo.

  Alieleza kwamba hospitali hiyo kwa sasa imepata mafanikio mbalimbali ikiwemo kununua mashine ya kisasa ya Ultrasound kwa mkopo wa bima ya afya, kufungua chumba cha matibabu kwa ajili ya wagonjwa wabima.

  Aidha alisema kwamba kununua mashine ya kufulia kwa ajili ya kuendesha shuguli za ufuaji wa mashuka ya wagonjwa na nguo nyingine kwa ajili ya matumizi ya wagonjwa.

  Mafanikio mengine waliyataja kuwa ni kuendesha malipo ya huduma za afya kwa njia ya Kielekronikia, kuongezeka kwa mapato kutoka milioni 10 kwa mwezi hadi kufikia milioni 18, nazaidi kwa mwezi sambamba na mapato yatokanayo na bima toka milioni 6 hadi milioni 10.Akizungumzia changamoto alisema kwamba wanaupungufu wa wafanyakazi 117 wa kanda mbalimbali ,kujaa mara kwa mara kwa matanki ya kuhifadhia maji taka na hivyo kusababisha gharama kubwa ya unyonyaji wa maji taka.

  0 0  0 0


  Jumamosi Januari 28,2017- Chama cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga Mjini katika mkoa wa Shinyanga kimefanya Kongamano ikiwa ni uzinduzi wa wiki ya Maadhimisho ya miaka 40 tangu kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi CCM tarehe 05.02.1977.
  Kongamano hilo limefanyika leo Katika Ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Shinyanga mjini na mkoa wa Shinyanga,makada wa CCM na vyama vya upinzani na watu mbalimbali wenye mapenzi mema wakiwemo wanafunzi wa Shule ya sekondari Buluba na Kom sekondari.
  Mada mbalimbali zilitolewa wakati wa kongamano hilo ikiwemo historia ya CCM na mafanikio ya chama hicho tangu kuanzishwa kwake mwaka 1977.
  Katika kuadhimisha wiki ya maadhimisho ya miaka 40 ya CCM,Chama cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga kitashiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo katika ngazi ya matawi ikiwemo,kupanda miti,kusalimia wagonjwa,watoto yatima,walemavu,kutembelea shule,michezo na kufanya mikutano ya ndani badala ya mikutano ya hadhara.
  Vyama asili vilivyozaa CCM ni Tanganyika African National Union (TANU) cha Tanganyika  na Afro Shiraz Party (ASP) cha Zanzibar vyote vikiwa ni vyama vya ukombozi.Kauli mbiu ya maadhimisho ya miaka 40 ya CCM ni "CCM Mpya,Tanzania Mpya".
  Viongozi mbalimbali wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini na mkoa wa Shinyanga wakiwa meza kuu.Wa kwanza kushoto ni Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Charles Sangura,akifuatiwa na naibu meya wa manispaa ya Shinyanga Agnes Machiya,Katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga Alhaj Saad Kusilawe,mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Kanali mstaafu Tajiri Maulid na meya mstaafu wa manispaa ya Shinyanga ambaye sasa ni diwani wa Kata ya Kambarage Hassan Mwendapole
  Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Charles Sangura akizungumza wakati wa kongamano hilo ambapo alisema katika kusherehekea miaka 40 ya CCM watashiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo sambamba na kufanya mikutano ya ndani badala ya mikutano ya hadhara
  Makada wa CCM na wazee wa CCM wakiwa ukumbini
  Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Charles Sangura alisema lengo la maadhimisho miaka 40 ya CCM ni kujimbusha walipotoka,walipo na wanapoelekea.Kushoto ni Katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Rajab Makuburi
  Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Charles Sangura akizungumza ukumbini
  Wanachama wa CCM wakiwa ukumbini
  Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Kanali mstaafu Tajiri Maulid akifungua kongamano hilo ambapo aliwataka wanaCCM kujivunia mafanikio ambayo yamepatikana tangu chama hicho kianzishwe mwaka 1977
  Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Kanali mstaafu Tajiri Maulid akisitiza jambo ukumbini
  Wanachama wa CCM wakiwa ukumbini
  Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Kanali mstaafu Tajiri Maulid akizungumza wakati wa kongamano hilo ambapo aliwasisitiza wanachama wa chama hicho pamoja na watanzania kwa ujumla kuendeleza mshikamano uliopo nchini
  Wanafunzi wa shule ya sekondari KOM wakiwa na mwalimu wao ukumbini wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini
  Viongozi mbalimbali wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini wakiwa ukumbini
  Wafuasi wa CCM wakiwa ukumbini
  Tunafuatilia kinachoendelea ukumbini
  Mwalimu Patrick Kija alitoa mada kuhusu historia ya Chama Cha Mapinduzi na kuelezea harakati za ukombozi kutoka enzi za ukoloni
  Mwalimu Patrick Kija akitoa historia ya CCM
  Tunamfuatilia mtoa mada...
  Aliyekuwa katibu tawala wa CCM mkoa wa Shinyanga Abdul Dachi akichangia mada kuhusu historia ya Chama Cha Mapinduzi
  Katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga Alhaj Saad Kusilawe akitoa mada kuhusu mafanikio ya CCM tangu kianzishwe mpaka sasa.Alisema hata Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umeimarika zaidi
  Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Kanali mstaafu Tajiri Maulid,mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Erasto Kwilasa na diwani wa kata ya Kambarage Hassan Mwendapole wakifuatilia kwa umakini kilichokuwa kinaendelea ukumbini
  Katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga Alhaj Saad Kusilawe alisema chama hicho kimeleta mabadiliko makubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu,afya ,uchumi n.k
  Tunafuatilia kinachoendelea
  Meya mstaafu wa manispaa ya Shinyanga ambaye sasa ni diwani wa Kata ya Kambarage Hassan Mwendapole akionesha ilani ya uchaguzi ya 2015 ya CCM wakati akitoa mada kuhusu mafanikio ya CCM katika awamu ya tano inayoongozwa na rais John Pombe Magufuli.
  Mwendapole aliwataka wananchi kuwapuuza baadhi ya watu wanaobeza mafanikio yaliyofikiwa na CCM 
  Wanachama wa CCM wakiwa ukumbini
  Makada wa CCM na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wakiwa ukumbini
  Tunafuatilia kinachoendelea....
  Mwanachama wa CCM Joseph Maige akichangia hoja ukumbini
  Viongozi wa CCM wakifuatilia michango ya washiriki wa kongamano hilo
  Kada wa CCM Charles Gishuli akichangia mada ukumbini
  Mkuu wa wilaya mstaafu Zipporah Pangani akichangia hoja wakati wa kongamano hilo ambapo aliomba Chama Cha Mapinduzi kijikite katika kutoa elimu juu ya ilani ya uchaguzi ya chama hicho sambamba na kuimarisha chama katika ngazi ya matawi
  Mwanafunzi Mariam Mrisho anayesoma kidato cha tano katika shule ya sekondari Buluba iliyopo mjini Shinyanga akichangia hoja katika kongamano hilo
  Kada wa CCM Mussa Jonas akichangia hoja ambapo alisisitiza umuhimu wa Chama Kujulikana kwanza badala ya mtu kujulikana zaidi
  Mwanafunzi Stephen William kutoka Kom sekondari akizungumza ukumbini
  Vijana wa CCM wakipiga makofi baada ya kufurahia jambo ukumbini
  Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Kanali Mstaafu Tajiri Maulid akizungumza wakati wa kongamano hilo ambapo alisema katika kusherehea miaka 40 ya CCM wamejipanga kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo
  Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini akizungumza ukumbini
  Mwenyekiti wa CCM mko wa Shinyanga Erasto Kwilasa akifunga kongamano hilo ambapo aliwasititiza wanachama wa CCM kutoendekeza makundi ndani ya chama
  Kwilasa alisema pia alitumia fursa hiyo kuipongeza serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais John Pombe Magufuli kwa kujali wanyonge na kuahidi kuwa chama hicho kitaendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na rais Maguful katika kurudisha heshima ya nchi
  Vijana wa CCM wakiondoka ukumbini
  Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

  0 0

  Ni simulizi ya kweli inayo lenga kuelimisha jamii kuhusiana na suala la ndoa katika karne ya sasa. Kumekuwa na sababu za hapa na pale zinazo pelekea vijana wengi kuchelewa au kushindwa kabisa kuoa na kuolewa.


  Kuoa na kuolewa ni moja kati ya sehemu ya maisha ya mwanadam na inafika wakati mtu anakuwa na shauku ya kuoa au kuolewa, lakini kutokana na baadhi ya vikwazo vinavyo jitokeza imekuwa ni changamoto kubwa.


  Baada ya kuliona hilo kwa jicho pevu “WAELIMISHAJI CREW”  Zaydar ,Moses, Aisha, Happy & Kilaka wamekuletea ujumbe mzito kwa njia ya video  kupitia Short Films zinazo andaliwa na Vinec Production Tanzania - Dar es salaam.

  Tunaomba ushirikiano wako wa kusambaza hii video iliyobeba ujumbe mzito wenye kuelimisha Jamii. Kwa msaada na maswali kuhusiana na video hii pamoja na wasanii walio shiriki humo wasiliana nasi kwenye 0658161950 asante.

  0 0

  Mwanadiplomasia mahiri wa Tanzania aliyepata pia kuwa Katibu Kiongozi-Ikulu, Balozi Ombeni Sefue ameteuliwa kuwa Mtanzania wa kwanza kuingia katika Jopo la Watu Mashuhuri katika Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM).

  Kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa APRM tawi la Tanzania, Rehema Twalib anayehudhuria mikutano ya Umoja wa Afrika na APRM mjini Addis Ababa, Ethiopia, Balozi Sefue ameidhinishwa kwenye kikao cha juu ya Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika ambao ni wanachama wa APRM kilichofanyika juzi Jumamosi mchana.

  “Haikuwa kazi rahisi kupata nafasi hii. Nchi nyingi za Afrika zilileta majina ya watu wao mashuhuri ili kuingia katika jopo hili muhimu. Balozi Sefue licha ya kuwa na utumishi uliotukuka kama mwanadiplomasia mkongwe pia aliungwa mkono kwa nguvu zote na Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania,” alisema Katibu Mtendaji huyo.

  APRM ni Mpango wa Afrika uliobuniwa na Wakuu wa Umoja wa Afrika kwa lengo la kuwa na chombo kitakachosaidia kuhimiza nchi wanachama kuenzi utawala bora na utoaji wa huduma bora za kiuchumi, biashara na za kujamii kwa wananchi wao kupitia mfumo wa kujitathmini zenyewe na kukosoana.

  Kwa mujibu wa tovuti ya APRM, Jopo la Watu Mashuhuri ni chombo cha juu cha kuwashauri Wakuu wa Nchi Wanachama wa APRM katika uendeshaji wa Mpango huo na husimamia mchakato mzima wa kujitathmini.

  Wajumbe wa jopo hilo ambao hudumu hadi miaka minne hupendekezwa na nchi zao na baada ya mchakato mrefu wenye ushindani majina ya waliokidhi vigezo huwasilishwa na kuidhinishwa na na kikao cha juu katika APRM-Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali.

  Tanzania ni miongoni mwa wanachama 35 kati ya nchi 54 wa Nchi za AU zilizojiunga na APRM na ilijiunga rasmi na Mpango huo tangu mwaka 2004.Tayari Tanzania ilishafanyiwa tathmini ya kwanza ya utawala bora na inaendelea kutekeleza mapendekezo yaliyotolewa.

  Katika mkutano huo Mwenyekiti wa Wakuu wa Nchi za APRM Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya aliwapongeza wajumbe wa jopo hilo na kuwata kushiriki vyema katika kuihuisha APRM na kuwa chombo chenye thamani kubwa kwa Afrika kama walivyotarajia waasisi wake akina Thabo Mbeki, Olusegun Obasanjo, Benjamin Mkapa na wengine.

  Balozi Sefue ataungana na wajumbe wengine wapya ambao ni pamoja na Prof. Ibrahim Agboola Gambari (Nigeria), Balozi Mona Omar Attia (Misri) Bi. Fatma Zohra Karadia (Algeria), Askofu Don Dinis Salomão Sengulane (Msumbiji) na Prof. Augustin Loada (Burkina Faso). Wajumbe wa zamani wanaoendelea ni pamoja na  Prof. Youssouf Khayal (Chad) ambaye kwa sasa atakuwa Mwenyekiti wa Jopo hilo na Brigitte Mabandla (Afrika Kusini) ambaye atakuwa Makamu Mwenyekiti.

  Mkutano huo pia ulijadili Ripoti za tathmini za nchi katika maeneo anuai ya utawala bora kwa nchi za Kenya (ikiwa ni ripoti ya pili kuwasilishwa), Sudan, Chad, Senegal, Djibouti pamoja na ripoti ya utekelezaji ya Zambia.


  0 0

  Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi,Nsato Marijani akiwasili katika eneo lilipo jengo la ghorofa ambalo ni makazi ya sakari lililoungua moto huku akiongozana na Mwenyeji wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa.
  Jengo la ghorof mbili ,makazi ya askari Polisi wa vikosi mbalimbali mjii Moshi liliungua moto sehemu ya juu na kueteketeza vyumba tisa pamoja na mali za asakri waliokuwa wakiishi katika vyumba hivyo..
  Kamishna Marijani akiangalia athari iliyotokana na moto katika jengo hilo ulioteketeza vyumba tisa zikiwmo samani za ndani na nguo za familia za askari hao.
  Kamishna Marijani akizungumza na CPL Erick Mwantingo mmoja wa askari waliopoteza vitu vyote vya ndani katika tukio hilo la moto.
  Kamishna Marijani akita pole kwa PC  Maswi ambaye pia amepoteza vitu vyote vya ndani zikiwemo nguo katika tukio la moto lililoteketeza sehemu ya juu ya jengo hilo.
  Kamishna Marijani akimfariji  CPL,Simba baada ya kutembelea jengo hilo kujionea athari iliyotokana na moto huo.
  Kamishna Marinaji akimpa pole SGT Hashim baada ya kupoteza vitu vyote vya ndani pamoja na mavazi kufuatia moto ulioteketeza seheumu ya juu ya jengo hilo.
  Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa akimuongoza Kamishna Marijani kukagua maeneo mengine  ya jengo hilo ambalo linakumbwa na tukio la moto kwa mara ya pili sasa.
  Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi ,Nsato Marijani akisalimiana na baadhi ya viongozi pamoja na wageni waliofika kwa ajili ya kutoa pole kwa asakri waliounguliwa vitu katika jengo hilo.
  Waliovalia kiraia ni askari Polisi waliofikwa na janga la kuunguliwa moto vitu vya ndani pamoja na mavazi wakionekana wenye huzuni.
  Afisa Mnadhimu daraja la kwanza wa jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Koka Moita akizungumza wakati wa ukaribisho wa Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi,Nsato Marijani alipotembelea kambi ya polisi mjini Moshi.
  Kamnada wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi Mwandamizi,Wilbroad Mutafungwa akitoa taarifa juu ya tukio la moto katika jengo la makazi ya askari Polisi.
  Baadhi ya wanandugu wa familia zilizounguliwa moto wakionekaa wenye huzuni.
  Mkuu wa Shule ya Polisi,Kamandanti Matanga Mbushi akizungumza wakati wa kuzifariji familia za askari waliopoteza vitu vyao katika tukio la moto.
  Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi,Nsato Marijani akitoa salamu za pole kwa niaba ya Mkuu wa jeshi la Polisni nchini ,IGP Ernest Mangu kwa askari waliopoteza vitu vyao wakati wa tukio la moto lililoteketeza vyumba tisa katika makazi ya askari Polisi mjini Moshi.
  Mmoja wa wageni waalikwa akizungumza wakati akitoa salamu za pole kwa jeshi la polisi. 

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.

  JESHI la Polisi nchini limetangaza kuwahamisha askari tisa wa vikosi mbalimbali vya jeshi hilo waliopoteza mali zao wakati wa tukio la moto lililoteketeza vyumba tisa vya jengo la ghorofa mbili ambalo ni makazi ya askari.

  Mbali na hatua hiyo jeshi hilo pia limetoa kiasi cha Sh Milioni tisa kwa familia za askari hao kwa ajili ya kuanza kununua vitu vidogo yakiwemo mavazi baada ya kutoambulia chochote wakati wa tukio hilo zikiwemo sare za jeshi hilo.

  Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi,Nsato Marijani ametoa kauli hiyo jana kwa niaba ya Mkuu wa jeshi la Polisi ,Inspekta Jenerali,Ernest Mangu wakati akizifariji familia za askari hao pamoja na kutembelea jengo lililoteketea kujionea athari za moto huo uliotokea usiku wa kuamkia juzi.

  Akiwasilisha salamu za Pole kwa niaba ya IGP Mangu,Kamishna Marijani alisema jeshi la Polisi litaendelea kutoa msaada kwa askari hao hadi pale maisha yao yatakaporejea huku akivishukuru vikosi vya jeshi la zima moto vya uwanja wa ndege wa KIA,kiwanda cha sukari cha TPC na Halmashauri kwa kazi waliyofanya.

  Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi,Wilbroad Mutafungwa amemwelea kamishna Nsato kuwa thamani ya mali za askari zilizoteketea kwa moto imefikia sh Mil 93.9 huku akiomba wadau kujitokeza kusaidia familia hizo.

  Tukio la moto katika jengo hilo lililopo jirani na ofisi za kikosi cha kutuliza ghasia lilitokea usiku wa kuamkia jana majira ya saa 2:30 usiku ,ukianzia katika chumba kimojawapo cha ghorofa ya pili na kuenea katika vyumba vingine nane wakati huo umeme ukiwa umekatika.

  Kufuatia moto huo familia tisa za askari hao zenye jumla ya watu 40, ambao 23 ni watu wazima na 17 ni watoto tayari zimepatiwa malazi ya muda katika chuo cha Polisi Moshi wakati taratibu nyingine za kuwasaidia zikiendelea.

  Tayari jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro limeunda timu ya wataalamu kutoka katika jeshi hilo wakisaidiana na wale wa kikosi cha zimamoto pamoja na shirika la umeme (TANESCO) kufanya uchunguzi wa matukio ya moto katika jengo hilo.

  Mwisho.

older | 1 | .... | 1119 | 1120 | (Page 1121) | 1122 | 1123 | .... | 1898 | newer