Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 110 | 111 | (Page 112) | 113 | 114 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Washiriki wa Mashindano ya Miss Inter University Dar es Salaam, wakiwa katika mazoezi ya katika Ukumbi wa Sansiro Dar es Salaam jana kujiwinda na Onyesho litakalofanyika kesho (Leo) katika Ukumbi huo wa Sansiro, washindi wataungana na washindi wa kanda zingine kuunda kikosi cha Tanzania katika mashindano ya Vyuo Vikuu Tanzania(Tanzania ambassador of Democracy 2013).
  Washiriki wa Mashindano ya Miss Inter University Dar es Salaam, wakiwa katika Pozi  wakati wa mazoezi katika Ukumbi wa Sansiro Dar es Salaam leo kujiwinda na Onyesho litakalofanyika june 29 katika Ukumbi huo wa Sansiro, washindi wataungana na washindi wa kanda zingine kuunda kikosi cha Tanzania katika mashindano ya Vyuo Vikuu Tanzania(Tanzania ambassador of Democracy 2013).(Picha na Shaaban Mpalule).

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi mbalimbali pamoja na vijana wa umri wa CPTM 29ers waliohudhuria mkutano wa Smart Partneship Dialogue 2013 wakati wa ufunguzi rasmi wa mkuatno huo unaoshirikisha watu zaidi ya 800 katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Convention Centre jijini Dar es salaam Ijumaa Juni 28, 2013
  Rais Kikwete na viongozi mbalimbali wa nchi za Afrika wakishiriki katika mijadala na vijana wa CPTM 29ers 
  Viongozi mbalimbali wa nchi za Afrika wakishiriki katika mijadala na vijana wa CPTM 29ers 
  Mjadala ukiendelea
  Rais wa Sri Lanka akishiriki mjadala na vijana wa CPTM 29ers
  Rais Omar Bongo katika mjadala huo
  Kijana akichangia
  Vijana wakichangia mjadala

  Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Rais Mstaafu wa Msumbiji Joachim Chissano katika mjadala

  Kijana akichangia katika mjadala
  Rais wa Sri Lanka na Dkt Mihaela Smith wakifuatilia mjadala  Rais Kikwete akipiga ngoma kuashiria mwisho wa mjadala wa viongozi na vijana
  Rais Kikwete akipiga ngoma kuashiria mwisho wa mjadala wa viongozi na vijana
  Rais Kikwete akisalimiana na vijana hao
  Wanahabari wa ndani na nje ya nchi wakirekodi tukio hilo la kihistoria
  Wageni mbalimbali katika mkutano huo
  Ujumbe wa Swaziland
  Ujumbe wa Tanzania
  Meza kuu
  Meza kuu
  Vijana nwa THT wakitumbuiza


  Viongozi mbalimbali
  THT wakitumbuiza
  Meza kuu wakifurahia onesho la THT
  Wanafunzi wakiimba kwa furaha

  Meza kuu wakishangilia
  Sehemu ya wageni

  0 0

  BENDI ya African Stars “Wana Twanga Pepeta”  kesho Jumapili itazindua albamu yake 10 ijulikanyo kwa jina la Nyumbani Ni Nyumbani kwenye viwanja vya Leaders Club huku ikisherehekea miaka 15 tokea kuanzishwa kwake.
  Uzinduzi huo utapambwa  na michezo mbali mbali kuanzia saa 3.00 asubuhi ambapo timu nane za mpira wa miguu zitawania zawadi mbali mbali katikamichuano ijulikanalo kwa jina la ASET Bonanza. Timu hizo zitaongozwa na ile ya waandishi wa habari za michezo, Taswa FC na nyingine kama Brake Point, Mango, Namanga, Kivukoni, Camp Combine, Wagadau na Kunduchi.
  Mbali a burudani kutoka kwa Twanga Pepeta, siku hiyo pia kutakuwa na burudani kutoka kwa wanamuziki wa kizazi kipya, Linex, Barnaba, bila kusahau, wakongwe wa muziki wa dansi nchini, bendi ya Mlimani Park maarufu kwa mtindo wa Sikinde Ngoma ya Ukae.
  Mkurugenzi wa kampuni ya ASET inayomili bendi hiyo, Asha Baraka alisema kuwa bendi inayoundwa na wanamuziki chipukizi au Yosso, Aset Academia nayo itatoa burudani ya utangulizi katika uzinduzi huo uliodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro, Clouds Media Group, Radio One na CXC Africa.
  Asha alisema kuwa wamejipanga kukoga nyoyo za mashabiki siku hiyo kwani wameandaa shoo mbali mbali zijulikanazo kwa jina la Twanga 2013 na nyimbo zao mpya zilizomo kwenye albamu hiyo ambazo ni Nyumbani ni Nyumbani uliyotungwa na Kalala Junior, Ngumu Kumeza (Ibrahim Mpoyo), Mwenda Pole (Badi Bakule), Kila Nifanyalo (Jumanne Saidi), Shamba la Twanga (Greyson Semsekwa na Twanga 2013 ambao ni utunzi wa wanamuziki wote wa bendi hiyo.
  Albamu nyingine za bendi hiyo ni Kisa Cha Mpemba iliyozinduliwa mwaka 1999, Jirani (2000), Fainali Uzeeni (2001),  Chuki  Binafsi (2002), Ukubwa Jiwe (2003), Mtu Pesa (2004), Safari (2005),Password (2006),  Mtaa wa Kwanza (2007),  Mwana Dar es Salaam (2009) na Dunia Daraja iliyozinduliwa mwaka 2011.
  Asha alisema kuwa wameamua kufanya hivyo ili kuwakumbusha mashabiki wao wapi walipoanzia (tokea) na wapi wanapokwenda katika muziki wa dansi. Alisema kuwa kimuziki wamepata mafanikio makubwa sana kutokana na kupata mialiko ya kimataifa kama nchi za Ulaya mama Uingereza, Ujerumani, Uholanzi, Finland, Norway na nyingine nyingi.


  0 0

   Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Mfalme wa Swaziland, King Mswati katika hafla ya chakula cha usiku alichokiandaa kwenye viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam jana usiku, kwa waliohudhuria Mdahalo wa Kimataifa wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia kwa Manufaa ya Wote (Global Smart Partinership Dialogue). TBL ni moja kati kampuni zilizofadhli hafla hiyo.
   Mahali palipoandaliwa kwa dina kwenye viwanja vya Gymkhana
   Rais wa zamani wa Msumbiji, Joachim Chisano (kushoto) akikaribishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernald Membe katika hafla ya chakula cha usiku.
   JK akiwa na Museveni wa Uganda (kushoto), Kingi Mswati wa Swaziland na Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi
   Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Alnold Kilewo (kushoto), akiwa na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Chibuku cha Dar Brew, Kilowi Suma (wa pili kushoto), katika hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na Rais Jakaya Kikwete  kwa marais na viongozi mbalimbali waliohudhuria Mdahalo wa Kimataifa wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia kwa Manufaa ya Wote (Global Smart Partinership Dialogue). Kutoka kulia ni Kiongozi wa mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, Halfan Mpango na Mkurugenzi wa Mfuko wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Esther Mkwizu. Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ni kati ya kampuni zilizofadhili hafla ya chakula hicho.
   Rais wa Uganda, Yoweri Museveni akihutubia katika hafla hiyo.
   Rais Jakaya Kikwete akiwaongoza baadhi ya marais na viongozi wengine kucheza muziki uliokuwa ukiporomoshwa na kikundi cha sanaa cha Tanzania House of Talent (THT), wakati wa hafla ya chakula cha usiku
   Rais Jakaya Kikwete akiwaongoza baadhi ya marais na viongozi wengine kucheza muziki uliokuwa ukiporomoshwa na kikundi cha sanaa cha Tanzania House of Talent (THT), wakati wa hafla ya chakula cha usiku alichokiandaa viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam jana usiku, kwa marais na viongozi waliohudhuria Mdahalo wa Kimataifa wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia kwa Manufa ya Wote (Global Smart Partinership Dialogue). Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ilikuwa kati ya kampuni zilizofadhili hafla ya chakula hicho.
   Bendi ya THT ikitumbuiza katika hafla hiyo
   Msanii Mwasiti akipongezwa na Mbunge wa Afrika Mashariki, Adam Kimbisa. Kulia ni Mbunge wa bunge hilo, Shy Rose Bhanji na Abdul Mwinyi ambaye pia ni Mbunge wa Bunge hilo.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
                                                Kimbisa akiwa na Mwinyi, Bhanji na Richard Kasesera

  0 0

  Mwanamuziki wa Reggae nchini Jhikoman afungua mtandao wake www.jhikoman.com mtandao ambao unaweza kusikiliza nyimbo na kusoma mambo mbali mbali ya Jhikoman and Afrikabisa band. Wadau msikose kumpa shavu mtoto wenu Jhikoman Manyika at www.jhikoman.com 

  0 0

  a cross section of dawoodi Bohra members who had come to receive Ali Qadar Wamolai syedi Mufaddal Bhaisaheb Saifuddin in Dar es Salaam today 29 June 2013 at the Annadil Burhani grounds.
  Ali Qadaar Syedi Mufadal bhaisaheb Saifuddin and his Worship mayor Jerry Silaa planting a palm tree.
  Ali Qadaar Syedi Mufadal bhaisaheb Saifuddin Handing over to his Worshipl mayor Jerry Silaa 1,252 palm trees for tree planting exercise to be carried out by Burhani Foundation in Tanzania.
  Ali Qadaar Syedi Mufadal bhaisaheb Saifuddin leading the way with his Worship mayor Jerry Silaa for the ceremonial tree planting.
  Ali Qadaar Syedi Mufadal bhaisaheb Saifuddin watering tree seedlings upon his arrival in dar es salaam, overlooking is His worship mayor Jerry Silaa.
  Ali Qadaar Syedi Mufadal bhaisaheb Saifuddin with his Worship Ilala Municipal Council mayor Hon. Jerry Silaa.
  ======  ===== = ====
  The heir apparent to His Holiness Dr Syedna Mohammed Burhanuddin, the Spiritual Leader of to the one million plus strong worldwide Dawoodi Bohra community, Ali Qadar wamolai syedi Mufaddal Bhaisaheb Seifuddin arrived in Dar es Salaam, Tanzania on Saturday 29 June and was received by His Worship Jerry Silaa, Mayor of Ilala Municipal Council at the Julius Nyerere International Airport VIP Lounge.

  The entourage proceeded to annadil Burhani where by the Ali Qadar Syedi Mufaddal Bhaisaheb Seifuddin handed over on behalf of the Burhani Foundation in Tanzania ,to His Worship Mayor Jerry Silaa, 1,252 Palm trees that would be planted along the 13km Nyerere Road.

  Syedi Mufadal bhaisaheb urged the mayor and his council to keep on keeping the environment clean and green at par with Mayor Jerry Silaa Campaign.

  The global tree planting drive by the Burhani Foundation is part of the golden jubilee celebration of the 50 years leadership of Syedna Mohammed Burhanuddin Saheb (TUS)

  0 0

  LICHA ya kuwepo kwa shule za msingi na sekondari kwa Mkoa wa Kilimanjaro ambazo kwa kiasi fulani zinakidhi mahitaji, bado kuna changamoto kadha wa kadha ambazo zinaathiri maendeleo ya kitaaluma kwa baadhi ya maeneo. Wilaya ya Rombo ambayo ni moja ya wilaya za Mkoa wa Kilimanjaro ni miongoni mwa maeneo yanayokabiliwa na changamoto za kipekee kitaaluma hasa elimu ya sekondari.

  Wilaya hii imefanikiwa kuwa na shule nyingi za sekondari hasa zile za Serikali licha ya kukabiliwa na changamoto kadhaa katika uendeshaji wa shule hizi. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wadau wa elimu wilayani Rombo, kuna jumla ya shule za Sekondari 48; yaani shule zinazomilikiwa na Serikali 41 huku zile za binafsi zikiwa saba tu.

  Tofauti na maeneo mengine ya Tanzania idadi kubwa ya wazazi wilayani Rombo wana mwamko wa kuwapeleka watoto wao shule kupata elimu ya sekondari mara baada ya elimu ya msingi. Hatua hii pekee ya kumpeleka sekondari mtoto ni kutambua umuhimu wa elimu kiasi fulani kwa mtoto. Wapo pia wanaojitahidi na hata kulipa michango na mahitaji kwa wakati japo si wote.

  Lakini kumpeleka mtoto shule na kutomfuatilia anafanya nini wakati gani na hata anaporudi nyumbani baada ya shule haitoshi. Uchunguzi mdogo uliofanyika katika baadhi ya maeneo ya mpakani mwa Tanzania na Kenya katika ndani ya Wilaya ya Rombo, yakiwemo maeneo ya Holili, Tarakea na Rongai imebaini licha ya baadhi ya wazazi kuwa na mwamko wa kuwapeleka sekondari watoto wao hawafuatilii maendeleo yao kabisa.

  Hali hii imesababisha wanafunzi hao kujihusisha na shughuli nyingine zaidi ya elimu za kutafuta fedha (biashara). Maeneo haya yapo mpakani sehemu ambazo zinashughuli nyingi za kibiashara na kazi ndogo ndogo za kufanya. Uchunguzi umebaini wapo wanafunzi ambao hufanyabiashara na kazi za vibarua ndogo ndogo huku wakiendelea na shule jambo ambalo linaathiri maendeleo yao kitaaluma na eneo zima.

  Wapo wanafunzi wa sekondari ambao hufanya kazi za kuendesha pikipiki za abiria maarufu kama bodaboda mpakani na huku wakiendelea na shule, wapo pia ambao hufanya vibarua vya kubeba mizigo na hata kulimishwa kwenye mashamba hasa eneo la Kenya na kulipwa ujira wa siku. Shughuli hizi za utafutaji kipato zinapowanogea wengine huacha kabisa shule na kuendelea za shughuli za utafutaji kipato.

  Wasichana wao hukimbilia kufanya kazi za ndani hasa kwa wenyeji wa Kenya na pia kufanya kazi za uuzaji vinywaji baa. Mji wa Loitokitoki uliopo mpakani kabla ya kuingia nchini Kenya ndio wenye idadi kubwa ya biashara na shughuli kama hizi ambazo hufanywa na wasichana wengine wakiwa wamekimbia shuleni ama baada ya darasa la saba bila kujali kama amechanguliwa kuendelea au kuishia mnjiani kutokana na uangalizi mdogo ki-malezi.

  Ramadhan Ally ni mmoja wa wakazi wa Tarakea wilayani Rombo, anasema baadhi ya wanafunzi huamua kujiingiza kwenye shughuli za utafutaji kipato kutokana na usimamizi mdogo wa wazazi/walezi wao. "Wapo wazazi ambao wamewaacha watoto wao chini ya uangalizi wa bibi au babu wao wapo 'busy' kibiashara nchini Kenya, wapo wazazi wengine huwashirikisha watoto wao kufanya vibarua vya mpakani ili kukuza kipato cha familia...sasa hali kama hii inamfanya mtoto asione umuhimu wa shule na wakati mwingine baadae uamua kuacha kabisa shule," anasema Ally.

  Anaongeza kuwa wapo baadhi ya wazazi hawawatimizii mahitaji ya shule watoto wao hivyo watoto kuamua kutafuta chochote wenyewe. Hili huwenda likawa na ukweli, uchunguzi uliofanyika katika sekondari za Tanya, Nduweni, Ngaleko, Urauri na Mbomai umebaini muitikio wa ulipaji wa ada na michango mingine kwa wazazi/walezi ni mdogo sana kwa wazazi. Kiujumla madeni ni mengi dhidi ya wanafunzi.

  Venance Mramba ni Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Sekondari ya Nduweni, katika mazungumzo na mwandishi wa makala haya anakiri mwamko mdogo wa waza/walezi kwa ulipaji ada na michango mingine shuleni hapo. "...Ukweli hapa madeni ya wanafunzi ni mengi ikiwemo ada na michango mingine...," anasema Mramba.

  Victus Kiwango ni Mkuu wa Sekondari ya Tanya iliyopo wilayani Rombo maeneo ya mpakani, anakiri pia mwamko mdogo wa wazazi kuchangia ada na michango mingine katika shule yake, anaongeza kuwa wapo wanaodiriki kusema kuwa uwezo wao kiuchumi ni mdogo wa ulipaji ada na michango mingine.  

  Hata hivyo kwa upande wake Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Sekondari ya Holili, Benson Samizi iliyopo eneo la Wilaya ya Rombo mpakani anabainisha kuwa mwitikio wa wazazi kufuatilia maendeleo ya watoto wao shuleni hapo ni mdogo kabisa. Anasema hata wanapo itisha mkutano wa wazazi shuleni hapo mwitikio huwa ni mdogo pia, wazazi wengi huagiza wawakilishi baada ya kuja wao wenyewe.

  "...Changamoto nyingine shuleni kwetu ni u-'busy' wa wazazi na biashara zao. Naamini wazazi wengi hapa hawafuatilii maendeleo ya watoto wao shuleni, mzazi utakuta unamuita kumshirikisha jambo kwa maendeleo ya manae lakini anatuma mwakilishi, majukumu yao kiusimamizi kwa mtoto anayatupa kwa mwalimu...sasa mwalimu hawezi kufanya kila kitu bila ushirikiano na mzazi," anasema Samizi.

  "Binafsi nilijaribu kufanya utafiti mdogo shuleni kwetu wa kuangalia ni kwa kiasi gani wazazi wanafuatilia maendeleo ya mtoto shuleni...lakini huwezi amini kwa mwaka mzima walikuja wazazi wawili tu wenyewe kuulizia maendeleo ya watoto wao, hapa unaweza kuangalia ni namna gani watu hawa wapo 'busy' na shughuli zao zaidi ya maendeleo ya mtoto shuleni. Hata ukiitisha kikao cha wazazi hawafiki robo tatu ya wanafunzi wanaokuja shuleni," anasema mwalimu Samizi.

  Aidha anakiri uwepo wa wanafunzi ambao hurubuniwa na kujiingiza katika shughuli nyingine nje ya masomo na wengine kuacha shule. Anasema kuwa kwa mwaka 2013 shule hiyo ilipewa jumla ya wanafunzi wa kidato cha kwanza 140 lakini walioripoti ni wanafunzi 85 tu, huku wengine 30 kupelekwa katika shule za binafsi. idadi iliyosalia hawajulikani walipo hadi sasa. Anaongeza kuwa kuanzia mwaka 2011 hadi Mai 2013 jumla ya wanafunzi 7 walitiwa mimba na kesi zao kushughulikiwa katika hatua anuai.

  Sim Msami Silayo ni Mwalimu Mkuu wa Sekondari ya Urauri iliyopo maeneo ya mpakani Wilaya ya Rombo, anasema tangu nyakati za ukoloni kulikuwa na kasumba ya wanafunzi kwenda kufanya vibarua maeneo ya mpakani anasema hali hii imeendelea mpaka leo. Anasema zipo baadhi ya familia zinautaratibu wa kwenda kufanya vibarua kwa makundi hivyo kuwaathiri baadhi ya wanafunzi.

  Anasema kwa taarifa ambazo wanazo wapo baadhi ya mabinti hukimbia shule na kwenda kufanya kazi za uuzaji vinywaji baa na wengine kazi za majumbani hali ambayo uongozi wa shule umekuwa ukiendelea kupambana kukabiliana na changamoto hiyo.

  Wakati hali iko hivyo wanafunzi kama Thabit Kayanda (si jina lake halisi) japokuwa ni mmoja wa wanafunzi wilayani Rombo wanamtazamo tofauti. "...Unapoona mzazi yupo 'busy' na biashara zake kiasi hata cha kutokutimizia mahitaji yako ya shule lazima uanze kujitengenezea maisha yako mwenyewe hivyo mtu unajikuta unaingia katika biashara au shughuli zingine kujipatia fedha. Na kama unafanya na kufanikiwa (kupata fedha) unajikuta unaona hakuna haja ya kuendelea na shule...kumbuka kila mmoja anasoma ili aje kupata fedha za kuendesha maisha yake, kama unaanza kufanikiwa chochote hakuna haja ya kuendelea na shule," ni maneno ya Kayanda na mtazamo tofauti.   

  Hata hivyo mtazamo wa wanafunzi kama Kayanda na changamoto nyingine zilizopo wilayani Rombo haziondoi umuhimu wa elimu kwa kila mtoto. Hivyo kila mmoja na kila upande unakila sababu ya kuhakikisha unatimiza wajibu wake na elimu kupewa kipaumbele maeneo yote bila kujali changamoto zilizopo.
  *Imeandaliwa na www.thehabari.com 


  0 0  0 0


  Wizara ya Maliasili na Utalii inashiriki kwenye maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya SABASABA mwaka huu yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius.K.Nyerere, Saba Saba, Barabara ya Kilwa.  Wizara inawakaribisha wananchi wote wenye kiu ya kuona na kuelimika kuhusu shughuli za Utalii, Ufugaji Nyuki, Uhifadhi wa Misitu, Malikale na Wanyamapori. Ikumbukwe kuwa Banda la Maonesho la Wizara miaka yote huwavutia watu wengi wanaoshiriki katika maonesho ya Viwanda na Biashara  hali ilinayowapelekea watu wengi kushindwa kuingia ndani kuona wanyama kutokana na umati mkubwa wa watu wanaofurika hasa inapokaribia kilele cha maonyesho.

  Wizara inapenda kuwajulisha wananchi wanaopenda kujielimisha na kuona shughuli mbalimbali za Wizara kutembelea banda kuanzia Mwanza wa maonyesho badala ya kusubiri siku ya ufunguzi Julai 4 mwaka huu ambapo watu hufulika kiasi cha wengi kushindwa kutii kiu zao wafikapo bandani.

  Aidha, katika kuimalisha utalii wa ndani Wizara imeandaa safari za kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi kwa gharama nafuu ambapo  mtu mzima atalazimika kulipa Tsh 15,000/-  na mtoto Tsh 5,000/- ikiwa ni gharama za usafiri kutoka viwanya vya Sabasaba hadi hifadhini na kurejea siku hiyo hiyo jijini Dar es Salaam.

  Sambamba na hilo Wizara imetoa ufadhili kwa vikundi vya asali kutoka wilaya zote nchini zenye wafugaji nyuki ili kutoa fursa kwa wananchi kujifunza juu ya umuhimu wa asali mwilini. Vikundi hivi vinapatikana katika Banda la Asali litakalokuwa na maonyesho ya asali na bidhaa zitokanazo na nyuki.

  Wizara haijawasahau wananchi wanaopenda kutunza mazingira kwa kupanda miti ya matunda, kivuli pamoja na mapambo kwa kuhakikisha inawaletea miche mbalimbali bandani inayouzwa kwa bei nafuu.

  Ndani ya banda wananchi watapata fursa ya kukutana na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii, wanyamapori na mambo ya kale watakaokuwa wanatoa elimu juu ya jambo lolote litakalokuwa linamtatiza mwananchi aliyefika bandani hapo.

  Miongoni mwa wanyamapori hai watakaokuwepo ni kama vile Chui, Nyoka, Ndege wa aina mbalimbali pamoja na mfalme wa pori SIMBA.

  0 0

  The Host patron and adviser to the Global 2013 Smart Partners Dr.Jakaya Mrisho Kikwete presents Commonwealth Partnership for Technology and Management(CPTM) Companion award to Sir Martin Laing (Malta) during a dinner he hosted for Smart partner participants held at Mwalim Nyerere International Conference Centre in Dar es Salaam yesterday evening.
  President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete presents CPTM Award to Sir.Charles Masefield UK yesterday evening during the Smart partnership Dinner hosted for participants in Dar es Salaam yesterday evening.
  President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete pose for a photograph with the recipients of Commonwealth Partnership for Technology and management(CPTM) awards.On the lest is Sir.Martin Laing of Malta and on the right is Sir.Charles Masefield United Kingdom.
  President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete and his guest King Mswati III of Swaziland admire a lion trophy on display at Mwalimu Nyerere conference Centre yesterday during a dinner hosted for participants to Smart Partnership International Dialogue held at Mwalimu Nyerere International Conference Centre in Dar es Salaam yesterday evening.
  President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete gives description of a lion trophy to Malaysian Prime Minister Najib Razak (second left) and King Mswati III of Swaziland at Mwalimu Nyerere Conference Centre during a dinner he hosted to the participants of of Smart Partnership International Dialogue yesterday evening.(photos by Freddy Maro).

  0 0

   Mshindi wa droo kubwa ya Promosheni ya Cheka Nao Bw.Mkude Iddi, mkazi wa Morogoro, (kushoto) akioneshwa ujumbe wa M-Pesa wenye  Tsh milioni 2 na Meneja Mauzo wa Vodacom Kanda ya Morogoro, Kamanda Kasapila, alizotumiwa kwa kushinda katika promosheni hiyo inayoendeshwa na Vodacom Tanzania. Mshindi huyo ni kati ya washindi 5 waliojishindia shilingi Milioni 2 kila mmoja kwenye Promosheni hiyo  inayowawezesha  wateja kuongea na mitandao yote kwa bei nafuu. Ili kujiunga wateja wanatakiwa kupiga *149*01#.
  Meneje Mauzo wa Vodacom Tanzania Kanda ya Morogoro, Bw. Kamanda Kasapila (kushoto) akimshuhudia mshindi wa droo kubwa ya Promosheni ya Cheka Nao, Bw.Mkude Iddi, akisaini baada ya kutoa fedha zake kwa njia ya M-Pesa alizotumiwa baada ya kushinda katika promosheni hiyo. Mshindi huyo ni kati ya washindi 5 waliojishindia shilingi Milioni 2 kila mmoja kwenye Promosheni hiyo  inayowawezesha wateja kuongea na mitandao yote kwa bei nafuu. Ili kujiunga wateja wanatakiwa kupiga *149*01#.
   Mshindi wa droo kubwa ya Promosheni ya Cheka Nao Bw.Mkude Iddi, mkazi wa Morogoro (kulia) akihesabu fedha zake baada ya kukabidhiwa na Mejena Mauzo wa Vodacom Tanzania Kanda ya Morogoro, Bw. Kamanda Kasapila. Mshindi huyo ni kati ya washindi 5 waliojishindia shilingi Milioni 2 kila mmoja kwenye Promosheni hiyo  inayowawezesha  wateja kuongea na mitandao yote kwa bei nafuu. Ili kujiunga wateja wanatakiwa kupiga *149*01#.


  Baadhi ya waandishi wa habari wakimfanyia mahojiano mshindi wa droo kubwa ya promosheni ya Cheka Nao Bw.Mkude Iddi, mkazi wa Morogoro (kulia) baada ya kukabodhiwa shilingi milioni mbili alizojishindia kupitia promosheni ya Cheka Nao hiyo  inayowawezesha  wateja kuongea na mitandao yote kwa bei nafuu. Ili kujiunga wateja wanatakiwa kupiga *149*01#.


  0 0

   
   Katika picha ya pamoja Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Steve Gannon akiwa na kikosi cha timu ya Chang`ombe B kabla ya kuanza mechi ya kujenga ujirani mwema kati ya SBL na timu ya Chang`ombe B jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Steve Gannon akikabidhi jezi kwa nahodha wa timu ya Chang`ombe B kabla ya kuanza mechi ya ujirani mwema kati ya timu ya Kmpuni ya Serengeti na vijana kutoka Chang`ombe B mwishoni mwa wiki katika viwanja vya DUCE jijini Dra es Salaam
   Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Steve Gannon (kushoto) akisalimiana na moja ya wachezaji wa timu ya kampuni hiyo  Erick Salvatory(kulia)wakati wa ukaguzi kabla ya kuanza kwa mechi ya ujirani mwema kati ya SBL na vijana kutoka Chang`ombe B iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya DUCE jijini Dar es Salaam.  
   Mwenyekiti wa mtaa wa Chang`ombe B Ahmed Khalid akiongea na vyombo vya habari wakati wa mechi ya ujirani mwema kati ya timu ya Chang`ombe B na Kampuni ya Bia ya Serengeti mwishoni mwa wiki katika viwanja vya DUCE  jijini Dar es Salaaam. 
   Mkurugenzi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Steve Gannon akiongea na vyombo vya habari wakati wa mechi ya ujirani mwema kati ya timu ya Chang`ombe B na Kampuni ya Bia ya Serengeti iliyoandaliwa na kampuni hiyo mwishoni mwa wiki katika viwanja vya DUCE  jijini Dar es Salaaam. 
   Wadau wakifuatilia mchezo huo kwa makini. 
    Erick Salvatory mwenye namba 10 mgongoni akimtoka adui wake kutoka timu ya Chang`ombe wakati wa mechi ya ujirani mwema kati ya Kampuni ya Bia ya Serengeti na Chang`ombe B  iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya DUCE jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Steve Gannon akikabidhi jezi kwa nahodha wa timu ya Chang`ombe B kabla ya kuanza mechi ya ujirani mwema kati ya timu ya Kmpuni ya Serengeti na vijana kutoka Chang`ombe B mwishoni mwa wiki katika viwanja vya DUCE jijini Dra es Salaam.

  0 0


  0 0


  Na Edwin Moshi, Makete.
  .
  Mahakama ya mwanzo Makete mjini wilayani Makete mkoani Njombe imemuhukumu katibu wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wilaya hiyo Bw Godfrey Mahenge (63) kwenda jela miezi 9 kwa kosa la kutotii amri halali ya jeshi la polisi Makete

  Akitoa hukumu hiyo hakimu wa mahakama ya mwanzo Makete mjini Mh. John Mpitanjia amesema mtuhumiwa huyo alitumia lugha ya matusi kwa askari polisi na kuwaita kuwa ni wauaji na kudai kuwa wametumwa na chama cha mapinduzi (CCM)

  Amesema baada ya mahakama yake kuridhishwa na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashataka, mshtakiwa alitakiwa kutumikia kifungo cha miaka miwili gerezani lakini kutokana na kutenda kosa hilo kwa mara ya kwanza mahakama imeamua kumfunga miezi 9 gerezani ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo

  Mshtakiwa huyo hakuwa na lolote la kijitetea na hakimu kumpatia adhabu hiyo na kusema kuwa rufaa kwa mshtakiwa ipo wazi endapo anahisi ameonewa.  
                                                   

  0 0

  Na Edwin Moshi, Makete

  Ofisi ya afya wilaya ya Makete mkoani Njombe imekusudia kununua kamera kwa ajili ya kupigia picha za baadhi ya watu wanaojisaidia ovyo mitaani kwa lengo la kuwadhibiti na kuwachukulia sheria watu wa namna hiyo ikiwemo kuwafikisha mahakamani

  Kauli hiyo imetolewa leo katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Makete na Afisa afya wilaya hiyo Bw. Boniphace Sanga katika kikao kilichowahusisha mkuu wa polisi Makete, Afisa biashara, afisa afya pamoja na wamiliki na wahudumu wa baa na vilabu vya pombe za kienyeji

  Bw. Sanga amesema ofisi yake imefikia hatua hiyo baada ya kuona vitendo vya kujisaidia hovyo hasa maeneo ya baa na vilabu yanakithiri licha ya adhabu mbalimbali kuchukuliwa dhidi yao, na wengine kudai kuwa wanaonewa na ofisi yake, hivyo wameamua kununua kamera ambazo wakiwapiga picha watu hao picha moja wanawapelekea wenyewe na nyingine wanaihifadhi na kuitumia kama ushahidi mahakamani

  Amesisitiza wamiliki na wahudumu hao kuhakikisha wanatunza usafi wa maeneo yao ya biashara kwa kuweka vyombo vya kuhifadhi taka na kuhakikisha wanapokwenda kuzitupa dampo vyombo hivyo wanarudi navyo, na kuwepo kwa maji moto ya kuoshea glasi ama vikombe vya kupimia pombe za kienyeji

  Ameongeza vitu vingine wanavyotakiwa kuvifanya kuwa ni kuvaa sare sketi nyeusi, blauzi nyeupe na kofia ama kilemba na wanaume suruali nyeusi, shati nyeupe na kofia pamoja na kufunga taa za mwanga mkubwa kwenye maeneo ya giza ya nyumba zote za biashara za vileo kwani wateja wakishakunywa pombe hupenda kwenda jirani kwenye maeneo yenye giza na kujisaidia hapo

  “Hayo ni maagizo tafadhali yazingatiwe la sivyo tutawanyang’anya leseni za kufanyia biashara, mteja akiona kagiza kadogo tuu hapo hapo anajisaidia na matokeo yake athari za mikojo ama vinyesi vinawaathiri watu wote” alisema Sanga

  Kwa upande wake mkuu wa polisi wilaya ya Makete (OCD) SP Peter Kaiza amewataka wahudumu hao kuzingatia muda wa kufunga na kufungua nyumba za kuuzia vileo na kusisitiza kuwa hakuna mtu yeyoteakiwemo yeye ambaye upo juu ya sheria.Amesema kumekuwa na utaratibu ambao unafanywa na baadhi ya maafisa wakubwa wa serikali ambao kwa wadhifa wao ama vyeo vyao huwafuata wahudumu wa vilabu ama baa na kuwataka kufungua kabla ya muda halali kwa kisingizio kwamba hakuna atakayekuuliza, hivyo kuwataka wakatae na kuwataka wawaambie waje muda wa kufungua ukifika

  SP Kaiza amesema hali hiyo kwa hivi sasa haitafumbiwa macho na wao kama jeshi la polisi wataanza kuwakamata wote wanaokiuka masharti ya leseni zao na kuwafikisha mahakamani ili waadhibiwe kwa mujibu wa sheria

  “Hakuna hata mmoja aliyepo juu ya sheria, na endapo tutakukamata umewahi kufungua ama umechelewa kufunga kwa kisingizio cha kuwahofia wateja wako kuwa ni watu wakubwa hapa, tutakumata na kukufikisha mahakamani, na kumbuka hakuna atakayekutetea na waliokudanganya watakuacha utaabike peke yako” alisema Kaiza

  Naye Afisa biashara Bw. Edonia Mahenge amesema ni marufuku kuchangaya pombe za kienyeji na za viwandani na kuziuza katika chumba kimoja na kama mtu anataka kufanya hivyo anatakiwa kutenga mabanda mawili kwa kuwa hizo ni biashara nyingi tofauti

  Amesema hayo kufuatia ombi lililotolewa na mmoja ya mmiliki wa kilabu cha pombe za kienyeji katika kitongoji cha Dombwela Bw. Harun ambaye amesema wanaomba kuruhisiwa kuuza vileo vyote kwa pamoja kwa kuwa hawana mitaji ya kutosha kupanga mabanda mawili, hali iliyopingwa na SP Kaiza na kusisitizwa na afisa biashara kuwa hiyo haiwezekani

  Afisa biashara huyo amesema maagizo hayo yaliyotolewa katika kikao hicho yatatumika wilaya nzima hivyo wafanyabiashara hao wanatakiwa kuyazingatia na kutekeleza maagizo hayo

  0 0

   Msanii wa Muziki wa Hip Hop,Roma Mkatoliki akipanga na kupangua vina vyake wakati wa Onyesho Kabambe la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013,lililofanyika usiku wa Kuamkia leo kwenye Uwanja wa Mkwakwani,jijini Tanga.
   Mkali wa Hip Hop,Prof. Jay a.k.a a.ka The Heavy Weight  MC akikamua vilivyo mbele ya Wakazi lukuki waliofika kwenye viwanja vya Mkwakwani kuona Onyesho la Muziki linaloongozwa na Kampuni ya Bia Tanzania kupitia Bia yake ya Kilimanjaro maarufu kama Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013.
  Mwana FA a.k.a Binamu akiimba wimbo wake wa Yalaiti na Mwanadada aliepanda jukwaani kuimba badala ya Msanii alieimba nae wimbo huo.
  Binamu akikamua huku shangwe zikitawala.
  Msanii wa Muziki wa Taratibu,Maarufu kwa jina la Recho akiimba nyimbo zake mbali mbali wakati wa Onyesho la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013,lililofanyika usiku wa Kuamkia leo kwenye Uwanja wa Mkwakwani,jijini Tanga.
  Mamaa wa Majanga aitwae Snura akiwapagawisha wakazi wa Tanga na goma lake lililoshika hatamu sana hapa nchini (MAJANGA).
  Ali Kiba na madansa wake wakitoa Burudani kwenye Onyesho hilo.
  Mkali wa Hip Hop hapa nchini kwa Mwaka 2012/13,Kala Jeremier akifanya mambo yake mbele ya Mashabiki wake Lukuki waliofika ndani ya Uwanja wa Mkwakwani,Jijini Tanga usiku wa kuamkia leo.
  Tanga ilizizima kwa shangwe wa Onyesho Kabambe la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013,lililofanyika usiku wa Kuamkia leo kwenye Uwanja wa Mkwakwani.  0 0

   
   Askari Jamii wakiwa kwenye mandamo wakipita mbele ya mgeni rasmin hayupo pichani, katika kilele cha Madhimisho ya wiki ya Safiri Salama, huko katika kiwanja cha Polisi Mahonda.
   Kamishna wa Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa akiwahutubia wananchi katika madhimisho ya wiki ya Safiri Salama, kulia Meneja kitengo cha maradhi yasiyoambukiza Wizara ya Afya Zanzibar Omar Mwalim na kushoto Mkuu wa Wilaya Mkoa wa Kaskazini (B) Khamia Jabir, huko katika kiwanja cha Polisi Mahonda Mkoa wa Kaskazini (B). Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
  Meneja kitengo cha maradhi yasiyoambukiza Wizara ya Afya Zanzibar Omar Mwalim Omar akitoa nasaha kwa madereva kupunguza ajali za makusudi, huko Mahonda katika Madhimisho ya wiki ya Safiri Salama yaliodhaminiwa na Wizara ya Afya na Jeshi la Polisi Zanzibar.

  =========  ======  ======  =======
  Na Salum Vuai, Maelezo.

  WATU 52 wamepoteza maisha na wengine 332 wamejeruhiwa kutokana na ajali 175 za barabarani zilizotokea katika Mkoa wa Kaskazini Unguja kati ya Januari mwaka 2011 hadi katikati ya mwaka 2013.

  Takwimu hizo zimetolewa jana na Mkuu wa Usalama Barabarani wa jeshi la Polisi mkoani humo Ali Muhsin, wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya ‘Safiri Salama’, yaliyofanyika katika viwanja vya Mahonda, Wilaya ya Kaskazini B.

  Mkuu huyo alisema, ajali za barabarani ni tishio kubwa kwa watumiaji  wote wa barabara, wakiwemo madereva, abiria na watembeao kwa miguu, na kwamba tahadhari kubwa inahitaji kuchukuliwa kuziepuka.

  Alieleza kuwa, endapo watumiaji wa barabara hawatakuwa waangalifu, majanga ya maafa, ulemavu wa kudumu, majeraha, hasara kwa mali na uharibifu wa miundombinu, vitaendelea kuliandama taifa.

  Alitaja sababu mbalimbali zinazochangia ajali hizo, kuwa ni uhaba wa miundombinu imara, ubovu wa vyombo vya moto, mabadiliko ya hali ya hewa, utendaji mbaya wa wasimamizi wa sheria za usalama barabarani na kasoro za kibinadamu.

  Ili kumaliza au kupunguza ajali za barabarani, Muhsin alisema hatua kadhaa zinapaswa kuchukuliwa, ikiwemo kutoruhusu magari na vyombo vyengine visiingizwe barabarani hadi vithibitishe kuwa na sifa kwa mujibu wa sheria.

  Aidha alishauri vyombo vyenye majukumu ya kutoa huduma kwa umma na kusimamia sheria kama vile polisi, mahakama, Idara ya Usafiri na Leseni, Bodi ya Mapato Zanzibar na vyengine, vitekeleze majukumu yao kwa uadilifu na uaminifu.   

  Kwa upande wake, mgeni rasmi katika sherehe hizo Kamishna wa Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa, alisema ajali za barabarani ndizo zinazoongoza kwa kuua watu wengi, kuliko vifo vitokanavyo na sababu nyengine.

  Alieleza, takwimu zinaonesha kuwa, takriban watu milioni moja na laki mbili hufariki kwa ajali hizo kila mwaka duniani kote. Kwa Zanzibar, alisema ajali 3869, zimeripotiwa kutokea kati ya mwaka 2009 hadi 2012, ambapo kati ya hizo, watu 450 walipoteza maisha, na 3855 walipata majeraha mbalimbali.

  Kamishna huyo aliongeza kuwa, kwa kipindi cha Januari hadi Machi mwaka 2013, jumla ya ajali 196 zimeripotiwa, ambazo zimesababisha vifo vya watu 24 na majeruhi 258.

  Aidha alisema, ukiondoa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkoa wa Kaskazini Unguja ndio unaoongoza kwa ajali nyingi za barabarani, kulinganisha na mikoa mingine minne Unguja na Pemba.    

  Alifahamisha kuwa, kwa kutambua uzito wa jambo hilo, Jeshi la Polisi kamisheni ya Zanzibar, limekuwa likifanya jitihada mbalimbali kwa kushirikiana na wadau wote wa matumizi ya barabara ili kuimarisha usalama wa watumiaji.

  Aliwataja wadau hao kuwa, ni jamii yote ya Zanzibar, taasisi za serikali na binafsi, ikiwemo Bodi ya Mapato Zanzibar na Wizara ya Afya, ambayo imeshirikiana kikamilifu na jeshi hilo kufanikisha wiki hiyo ya ‘Safiri Salama’.

  Hata hivyo, alikumbusha kuwa, jukumu la kuhakikisha usalama wa barabarani la jeshi la polisi pekee, bali ni la kila mmoja kwa nafasi yake, huku akisisitiza matumizi mazuri ya barabara ikiweemo kuzitunza badala ya kuziharibu kwa visingizio mbalimbali, pamoja na kung’oa vyuma vya alama za barabarani.

  Naye Meneja wa kitengo cha maradhi yasiyoambukiza kutoka Wizara ya Afya Omar Mwalimu, alisema hospitali kuu ya Mnazimmoja, imekuwa ikipokea majeruhi na maiti wengi kutokana na athari za ajali za barabarani, na kusema zinailazimu serikali kutumia fedha nyingi nje ya bajeti yake, kuwatibu watu wanaopatwa na ajali.

  Wiki ya ‘Safiri Salama’ ilianza tarehe 24 Juni mwaka huu, kwa mikutano ya kutoa elimu kwa watumiaji wa barabara, kama vile madereva na makondakta, wanafunzi, mabagwani na wananchi wengine wa Mkoa wa Kaskazini.   

  Sherehe hizo zilizopambwa kwa burudani mbalimbali zilizobeba ujumbe wa usalama barabarani kutoka kwa kikundi cha Black Roots chini ya msanii Makombora na utenzi, zilihudhuriwa pia na Wakuu wa Wilaya za Kaskazini B, Khamis Jabir Makame na Riziki Juma Simai wa Kaskazini A, pamoja na makamada wa Polisi wa mikoa mitatu ya Unguja.

  0 0


  Mmoja wa wapita njia akisoma moja ya bango lenye tangazo la tamasha la Filamu litakaloanza kufanyika jijini Mwanza leo katika uwanja wa Nyamagana.
  ================    ========= ========  

  JIJI la Mwanza kutwa nzima ya jana ilishuhudia hekaheka kubwa ya maandalizi ya uzinduzi wa Tamasha la Wazi la Filamu Tanzania, maarufu kama ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’ ambalo litafanyika katika Uwanja wa Nyamagana, leo.

  Wakazi wa Mwanza wanatarajia kuanza kushuhudia kitu kingine ambacho hakijawahi kuonekana, wakati wa uzinduzi huo ambao unatarajiwa kufanyika mchana wa leo. Mratibu wa Tamasha hilo aliye pia Mkurugenzi wa Sophia Records, Musa Kissoky, alisema wakazi wa Mwanza na maeneo ya jirani wasubiri kuona vitu vya aina yake wakati wote wa tamasha hilo linalotarajiwa kumalizika mwishoni mwa wiki.


  Kissoky alisema, tamasha hilo ambalo litakuwa la bure kwa watu wote na kushirikisha mastaa wa filamu hapa nchini, litakuwa la aina yake na kuwataka wakazi wa Mwanza wajitokeze kwa wingi kushuhudia mambo yanayoendelea.   Kila kitu kimekamilika, yaani tunaleta kitu tofauti ambacho watu watashangaa, ndio maana mpaka sasa wengi wanapigwa na bumbuwazi kuhusu kile tutakachofanya siku hiyo,” alisema.

  Naye Meneja wa kinywaji cha Grand Malt walio wadhamini wakuu wa tamasha hilo, Consolata Adam, alisema wameamua kufanya kweli zaidi kwani wanataka kuona Watanzania wanapata kitu chenye uhakika. Tumejipanga katika hili na wala hatutanii. Tunawakaribisha watu wote wenye mapenzi na filamu zetu za Tanzania kufika na kushuhudia tamasha hili ambalo mwaka huu limeboreshwa zaidi,” alisema Consolata.

  Naye Meneja Habari na Mawasiliano wa TBL, Edith Mushi, alisema, kutokana na ubora wa kinywaji cha Grand Malt hata tamasha hilo litakuwa la aina yake na litakaloiteka mikoa yote ya Kanda ya Ziwa.  “Tumeona jinsi wananchi wanavyozipenda filamu za Tanzania, maarufu kama ‘Bongo Movies’ na jinsi walivyo na kiu ya kuwaona wasanii wa filamu ana kwa ana, sasa kazi kwao kuwashuhudia na kuona tamasha bora zaidi,” alisema.

  Wasanii wakali wa Bongo Muvi wakiwemo Aunty Ezekiel, Vicent Kigosi ‘Ray’, Jacqueline Wolper, Irene Uwoya, Jacob Steven ‘JB’, Mahsein Awadh ‘Dk Cheni’na  Issa Mussa ‘Cloud’ ni baadhi ya wasanii walioahidi kufanya kweli pia katika tamasha hilo, huku bendi ya Extra Bongo chini ya Alli Choki ikitumbuiza.

  Tamasha hilo la filamu limedhaminiwa na kinywaji cha Grand Malt kisicho na kilevi ambacho kinazalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

  0 0  0 0

  Taswira mbalimbali zinazoonesha maandalizi ya mapokezi makubwa ya Rais wa Marekani Barack Obama atapowasili Ikulu jijini Dar es salaam mchana huu. Rais Jakaya Mrisho Kikwete kama ilivyo kawaida yake amepita kila mahali kuangalia kwamba mambo yanaenda mswano, ikiwa ni pamoja na kusaliamiana na makundi ya wananchi wa Dar es salaam walioko katika lango kuu la Mashariki.
  PICHA NA IKULU


older | 1 | .... | 110 | 111 | (Page 112) | 113 | 114 | .... | 1898 | newer