Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1114 | 1115 | (Page 1116) | 1117 | 1118 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Mtoto Braiton Msingwa mwenye umri wa miaka miwili ,Mkazi wa kata ya MATARAWE iliyopo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, amefariki dunia baada ya kutumbukia katika kisima cha maji alipokuwa akijaribu kufuata mapera.Huyu hapa jirani wa familia ya msigwa anaelezea mkasa mzima.


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongella (kulia) pamoja na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri W. Kindamba (kushoto) wakionesha mabango kuashiria uzindizi wa huduma za TTCL 4G LTE katika Jiji la Mwanza akizungumzaMgeni rasmi katika uzinduzi wa Huduma za TTCL 4G LTE katika Jiji la Mwanza, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongella (kulia) wakipongezana na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri W. Kindamba. Mgeni rasmi katika uzinduzi wa Huduma za TTCL 4G LTE katika Jiji la Mwanza, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongella (kulia) wakipongezana na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri W. Kindamba.Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongella (kulia) na mgeni rasmi katika uzinduzi wa Huduma za TTCL 4G LTE katika Jiji la Mwanza akizungumza. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongella (kulia) na mgeni rasmi katika uzinduzi wa Huduma za TTCL 4G LTE katika Jiji la Mwanza akizungumza.Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri W. Kindamba akizungumza katika uzinduzi huo Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri W. Kindamba akizungumza katika uzinduzi huoMgeni rasmi katika uzinduzi wa Huduma za TTCL 4G LTE katika Jiji la Mwanza, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongella akitembelea huduma mbalimbali zinazotolewa na TTCL katika uzinduzi huo. Mgeni rasmi katika uzinduzi wa Huduma za TTCL 4G LTE katika Jiji la Mwanza, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongella akitembelea huduma mbalimbali zinazotolewa na TTCL katika uzinduzi huo.Mgeni rasmi katika uzinduzi wa Huduma za TTCL 4G LTE katika Jiji la Mwanza, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongella akitembelea huduma mbalimbali zinazotolewa na TTCL katika uzinduzi huo. Mgeni rasmi katika uzinduzi wa Huduma za TTCL 4G LTE katika Jiji la Mwanza, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongella akitembelea huduma mbalimbali zinazotolewa na TTCL katika uzinduzi huo.Picha ya pamoja na Mgeni rasmi katika uzinduzi wa Huduma za TTCL 4G LTE katika Jiji la Mwanza, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongella Picha ya pamoja na Mgeni rasmi katika uzinduzi wa Huduma za TTCL 4G LTE katika Jiji la Mwanza, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mh. John MongellaMkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongella (kushoto) akisalimiana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Kamanda, Ahmed Msangi katika uzinduzi huo. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongella (kushoto) akisalimiana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Kamanda, Ahmed Msangi katika uzinduzi huo. 

  KAMPUNI ya Simu Tanzania TTCL, imezindua Huduma za TTCL 4G LTE katika Jiji la Mwanza siku ya Jumatatu, Januari 23, 2017. Mgeni rasmi katika tukio hilo alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe John Mongela alieongozana na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mhe. Mary Tesha Onesmo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Kamanda, Ahmed Msangi. Uzinduzi huo unaifanya Mwanza kuwa miongoni mwa Mikoa ya awali kabisa kupata huduma za 4G LTE ya TTCL yenye kiwango cha juu kabisa cha Ubora, kasi na gharama nafuu kupita kiasi. 

  Mikoa mingine ambayo tayari kampuni hiyo imepeleka huduma za 4G LTE ya TTCL ni pamoja na Dar Es Salaam, Dodoma, Arusha, Mbeya,Morogoro, Pwani na Zanzibar. Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongera alisema TTCL ni kampuni Mama wa Mawasiliano nchini, iliyopewa jukumu la kuwaunganisha Wananchi popote walipo, inabeba jukumu la kufanikisha utendaji wa Sekta nyingine zote zikiwemo shughuli za ulinzi na Usalama wa nchi.

   "Watanzania tunataka kuiona TTCL yetu ikichukua nafasi yake ya kuwa moja ya mashirika muhimu ya Umma yanayochangia Pato la Taifa na ukuaji wa sekta nyingine na hivyo kufanikisha mpango mkakati wa Nchi yetu kuwa Nchi ya Uchumi wa kati, Nchi ya Uchumi wa Viwanda," alisema Mkuu wa Mkoa, Mh. John Mongera. 

  Kwa upande wake Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri W. Kindamba akizungumza katika uzinduzi huo aliwahakikishia Watanzania na wateja wetu wote wa ndani na nje ya Nchi kuwa, kwa juhudi hizi tunazochukua na kwa ushirikiano mkubwa tunaopata kutoka Serikalini na kwa Wadau wetu, TTCL itafanya mapinduzi makubwa na kwa hakika itarejea katika nafasi yake ya kuwa kinara wa utoaji huduma za Mawasiliano nchini Tanzania. "TTCL 4G LTE MWANZA TUMEWAFIKIA"

  0 0

   Mwenyekiti wa Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ameir Haji Khamis akiongea na wajumbe wa baraza hilo katika kikao cha kamati kuu cha tatu cha Baraza la watoto la taifa leo Mjini Morogoro,Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga na Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo Caroline Augustino.
   Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Watoto kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi.Margareth Mussai akiongea na watoto kutoka Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa kikao cha kamati kuu cha tatu cha Baraza la watoto la taifa na kuwapongeza kwa kazi wanazoendelea kuzifanya kwa maslahi ya watoto nchini Leo Mjini Morogoro, Kulia ni Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga akiongea na watoto kutoka Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa kikao cha kamati kuu cha tatu cha Baraza la watoto la taifa ambapo aliwataka katika agenda zao wajadili ukatili dhidi ya ubakaji na ushoga na hatimaye wampelekee taarifa ili kujua nini serikali ikifanye, Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ameir Haji Khamis na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Watoto Bi.Margareth Mussai 
   Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga akimpa laptop Mjumbe wa Baraza la watoto kutoka Mkoa wa Dodoma Helena Charles.Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Watoto Bi.Margareth Mussai
   Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga akimpa Komputa Mjumbe wa Baraza la watoto kutoka Mkoa wa Lindi Juma Adinani. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Watoto Bi.Margareth Mussai
   Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga akimpa laptop Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Watoto kutoka Kinondoni Caroline Augustino. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Watoto Bi.Margareth Mussai
   Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga akimpa laptop Mjumbe wa Baraza la watoto kutoka Temeke Rehema Miraji. . Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Watoto Bi.Margareth Mussai
   Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga akimpa laptop Mwenyekiti wa Baraza la Watoto kutoka Zanzibar Ameir Haji Khamis. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Watoto Bi.Margareth Mussai
   Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga akimpa kompyuta Mjumbe wa Baraza la watoto kutoka Mkoa wa Mwanza Apwiyamwene Nicholaus.Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Watoto Bi.Margareth Mussai.
   Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga akimpa laptop Mjumbe wa Baraza la Watoto kutoka mkoa wa Singida Elibariki Abraham.
   Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kufungua kikao kikao cha kamati kuu cha tatu cha Baraza la watoto la taifa leo Mjini Morogoro.
   Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga akiwa katika picha ya pamoja na walezi wa Baraza la Watoto la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kufungua kikao kikao cha kamati kuu cha tatu cha Baraza la watoto la taifa leo Mjini Morogoro.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga akiwa katika picha ya pamoja na wakurugenzi kutoka Wizara hiyo (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) baada ya kufungua kikao kikao cha kamati kuu cha tatu cha Baraza la watoto la taifa leo Mjini Morogoro. PICHA NA HASSAN SILAYO-IDARA YA HABARI (TIS)

   Na Anthony Ishengoma-MCDGC

  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inakusudia kuanzisha Dawati la Ulinzi la na Usalama katika shule zote  pamoja na Kamati za Ulinzi na Usalama katika ngazi ya Kata na Vijiji Nchini kote ili kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.

  Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Sihaba Nkinga amesema hayo wakati akiongea katika ufunguzi wa Kikao cha Kamati Kuu cha Baraza la Watoto la Taifa kinachofanyika kwa siku mbili Mjini Morogoro.

  Aidha amewataka wajumbe wa Kikao hicho kujadiliana kwa kina juu ya ongezeko la vitendo vya ulawiti na ubakaji dhidi ya watoto na kuwasilisha mapendekezo yao Wizarani  akisema kuwa hivi karibuni vitendo hivyo vimeongezeka kwa wingi sana katika Jamii.

  Aliongeza kuwa kufuatia kuzinduliwa kwa Mpango Mkakati wa Kupambana na Kuzuia Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto wa miaka mitano Serikali itahakikisha vitendo vya ukatili vinapunguzwa kwa asilimia hamsini kupitia mpango kazi huo na kuongeza kuwa vitendo vya ukatili kwasasa vinatofautiana viwango akitaja ukatili huo kuwa ni ubakaji, ulawiti, ukeketeji, mimba na ndoa za utotoni.

  Naye Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Taifa  Caroline Augustino akiongea na vyombo vya Habari baada ya ufunguzi huo kuwa pamoja na kukutana leo jijini Morogoro pia Baraza hilo limefanya ziara mbalimbali mikoani kwa lengo la kuandaa makala maalumu za uelimishaji jamii kwa njia ya radio na runinga ili jamii iweze kufahamu maana  na aina za ukatili dhidi ya watoto.

  Adha Bi. Carolini amewataka wasichana walio katika umri mdogo kuachana na tamaa zinazowapelekea kujiingiza katika matendo mabaya yanayosababisha kukatisha ndoto zao ikiwemo kushindwa kuendelea na masomo pamoja na kujikuta wanapata ndoa za utotoni na kuwataka wazazi na walezi kutambua kuwa mtoto wa kike ana fursa sawa na watoto wakiume hasa kwa jamii za vijiini.

  Bi. Caroline pia amezitaka jamii za wafugaji na badhi zilizoko kanda ya ziwa kuacha tabia ya tohara mbili kwa watoto wa kiume na tohara kwa watoto wa kike akisema tohara kwa wanawake inasababisha vifo na maumivu ambayo huleta hathari mbaya kwa wanawake kwa kipindi kirefu.
  Kakao cha Baraza Kuu la Watoto Taifa pamoja na mambo mengine kinakutana kujadili kuandaa Mkutano Mkuu wa Baraza la Watoto Taifa utakaofanyika Mwezi Aprili Mwaka huu.

  0 0


  Kama inavyojulikana kuwa Mrembo wa Miss Universe Tanzania 2016 Jihan Dimack aliyetwaa taji la Miss Universe Tanzania mapema mwezi wa kumi na moja mwaka 2016 aliondoka nchini tangu tarehe 11 Januari kuelekea Manilla nchini Philipines kwa ajili ya kushiriki Mashindano ya Miss Universe kwa ngazi ya kimataifa .

  Jihan Dimack akiungana na wenzake kutoka nchi mbalimbali Ulimwenguni yupo nchini Phillipines kwa muda wa wiki mbili sasa akiiwakilisha vyema Tanzania katika kuwania taji hilo.

  Mashindano haya ambayo yanazingatia vigezo mbalimbali pia yana utaratibu wa upigaji kura ambao umeshaziduliwa rasmi tangu tarehe 23 Januari 2017 na kura zitapigwa ndani ya siku sita hadi tarehe 30 Januari 2017 ambayo ndo finali za mashindano hayo.

  Utaratibu uliowekwa na uongozi wa Miss Universe mwaka huu ni kwamba kutakua na warembo 12 bora na kati ya hao kumi na mbili mrembo mmoja ataingia kwa kigezo cha kupata kura nyingi kupitia mtandoni.

  Hivyo basi Watanzania wote kwa pamoja tushirikiane katika hili kuhakikisha mrembo wetu kutoka Tanzania Jihan Dimack anapata kura za kutosha kumuwezesha kuingia katika fainali hizo.

  Itakua jambo la faraja sana kufanikisha ushindi kwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa kupiga kura kwa wingi na kila mtu mmoja ana uwezo wa kupiga mpaka kura kumi kwa siku. Ushindi wa mrembo wetu upo mikononi mwetu wenyewe.

  Ili uweze kumpigia kura mrembo wetu Jihan utatakiwa kufanya mambo machache yafuatayo:

  Jinsi ya kumpigia kura Jihan katika mashindano ya Miss Universe kuanzia tarehe 23 January 2017:
  1) VODI: Pakua Vodi app katika Google Store au Apple Store
  2) Kupitia tovuti ya www.missuniverse.com
  3) MISS U APP: Pakua Miss U app 
  4) TWITTER: Tweet kwa kutumia hashtag #MissUniverse alafu utatumia hashtag maalum ya Jihan itakayotolewa muda si mrefu. 

  Tafadhali kumbuka kwa kila mtu ataweza kupiga kura mara 10 kwa siku kwa kila akaunti aliyoisajili.
  ***Kumbuka kuwa website ya missuniverse.com ni mtandao pekee ambapo upigaji kura utaendeshwa.


  0 0

  Na Woinde Shizza,Arusha

  Mfanya biashara maarufu wa madini jijini Arusha, Venance Moshi (30)amefikishwa Mahakamani na kusomewa maelezo ya awali katika kesi inayomkabili ya kushambulia na kumjeruhi mkewe kwa chupa usoni ,wakiwa wanasuluhishwa na baba mkwe, mgogoro wa ndoa yao.

  Mbele ya hakimu , Devota Msofe wa mahakama ya wilaya .Arusha ,mwendesha mashtaka wa serikali ,Agnesi Hyera alieleza mahakama hiyo kuwa mnamo marchi 11 mwaka 2016 katika maeneo ya Moshono kwenye usuluhishi wa mgogoro wa ndoa yao ,mshtakiwa alinyanyua glasi na kumpiga kwenye jicho la kulia mlalamikaji (mkewe) Agnesi Joseph (30)iliomjeruhi vibaya .

  Mwendesha mashitaka aliieleza mahakama hiyo kuwa kuwa hatua hiyo ilimsabishia mlalamikaji atokwe na damu nyingi na baadae kutoa taarifa kituo cha polisi ambapo mtuhumiwa alitiwa mbaroni na baadae kufikishwa mahakamani.

  Baada ya kusomewe maelezo hayo mshitakiwa huyo alikana mashtaka ,na hakimu Msofe alipanga siku ya kuanza kusikilizwa kwa shauri hilo,baada ya upande wa jamhuri kudai kuwa wapotayari kwa usikilizwaji wa kesi hiyo. Katika shauri hilo la jinai namba 438 la mwaka 2016 ,upande wa jamhuri unatarajia kuwasilisha mashahidi watatu na vielelezo kadhaa ikiwemo hati ya polisi(PF3) , hati ya daktari pamoja na picha za jeraha .Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa february 6 ,mwaka huu ,saa tatu asubuhi.

  Aidha katika hatua nyingine ,shahidi namba moja wa kesi hiyo ,Agnes Joseph anatarajia kufungua kesi nyingine ya kudai talaka kwa mumewe huyo waliyefunga naye ndoa mwaka 2012 baada ya ndoa yao kukumbwa na migogoro ya mara kwa mara huku akiambulia kipigo na vitisho. Alisema ameishi na mumewe huyo katika mazingira ya migogoro na wamekuwa wakisuluhishwa mara kadhaa bila mafanikio,

  0 0

   Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akiwa na Mgeni wake ambaye ni Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika Bw. Makhtar Diop, wakiwa katika chumba cha kupumzikia wageni maalumu katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Burundi, Somalia na Malawi Bi. Bella Bird.
   Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika Bw. Makhtar Diop, (wa pili kushoto aliyeshika dafu) alipowasili nchini, akiwa na mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (wa tatu kushoto) ambapo anatarajiwa kushiriki katika uzinduzi wa Mradi wa mabasi yaendayo haraka BRT, Januari 25, 2017, na baadaye kufanya mazungunzo na Waziri huyo alasiri.
   Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika Bw. Makhtar Diop, (kushoto) akinywa maji ya dafu  alipowasili nchini, akiwa na mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kulia) ambapo anatarajiwa kuungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, katika uzinduzi wa Mradi wa mabasi yaendayo haraka BRT, Januari 25, 2017.
  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akiteta jambo na Mkurugenzi Mkazi, baada ya mapokezi ya Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Bw. Makhtar Diop.
  (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)

  0 0


  0 0

  Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. John Ndunguru, amewaasa Wakurugenzi wa Halmashauri wa Mikoa Minne wanaoshiriki Warsha Mkoani hapa, kutumia vema fedha wanazopelekewa ambazo ziko chini ya Mfuko wa LDGD ili Serikali iweze kufikia lengo la kutoa huduma bora kwa wananchi.

  Dkt. Ndunguru ameyasema hayo mwanzoni mwa wiki hii wakati akifungua Warsha ya siku tatu ya utambulisho wa Miongozo Mikuu ya Mfumo utakaotumika katika Kuzipatia Ruzuku ya maendeleo Mamlaka za Serikali za Mitaa hapa nchini.

  Amesema, Wakurugenzi wanapashwa kusimami miongozo hiyo iliyotolewa na ambayo wataelekezwa wakati wa warsha hiyo ili kuhakikisha kuwa malengo ya uanzishwaji wa Mfumo huo yanatekelezwa ambayo ni kutoa huduma bora kwa wananchi.

  Aidha, Dkt. Ndunguru amewataka Wakurugenzi hao kuacha mazoea ya kubaki na fedha nyingi za Mfuko wa LDGD bila kuzitumia kwa wakati, jambo alilosema linawacheleweshea wananchi maendeleo wanayoyahitaji.

  “Usifikiri kuziweka hela kwamba ni utendaji kazi mzuri…na wewe ni jipu. ukitumia fedha hizo vibaya ni jipu, lakini pia ukiziacha bila kuzitumia ni jipu jingine tena jipu baya zaidi kwani unawakosesha wananchi huduma” alisisitiza Dkt. Ndunguru.

  Nae Mshauri Mkuu kwa niaba ya Shirika la Maendeleo la Japan hapa nchini (JICA) Bw. Michiyuki Shimoda, amewataka washiriki wa Warsha hiyo kujifunza kwa umakini miongozo inayohusu “Local Gornvement Development Grant” ambayo itapitiwa katika kikao hicho. Amesema wanatakiwa kuwa makini katika kujifunza miongozo hiyo kwa kuwa wao ndio watumiaji wakubwa nia ikiwa ni kuwaletea wananchi maendeleo.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Serikali za Mitaa Utawala Bora OR – TAMISEMI Dkt. Charles Mhina, amesema lengo la warsha hiyo ni kutoa Elimu ya namna ya kufanya ufuatiliaji wa shughuli zote ambazo zinafadhiliwa chini ya Mfuko wa LDGD.

  Warsha hiyo ya Siku tatu inafanyika katika Ukumbi wa Edem katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro na inashirikisha Wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa Mipango na Uchumi, baadhi ya Makatibu Tawala Wasaidizi wa Sekretarieti za Mikoa, Waweka Hazina na Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka Mikoa minne ya Dodoma, Dar es Salaam, Pwani na Morogoro.
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Dkt.John Ndunguru akiongea na wakurugenzi wa Halmashauri wa mikoa minne walioshiriki Warsha Mkoani hapo.
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Dkt.John Ndunguru wa nne kutoka kulia walio kaa na wa pili kutoka kushoto ni DKT.Charles Mhina akiwa na wakurugenzi wa Halmashauri katika picha ya pamoja.

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), Eric Solheim katika ziara yake mkoani Arusha,Gambo ameiomba UNEP kusaidia fedha mradi wa kulinda chanzo cha maji cha Olgilai kilichopo wilayani Arumeru kinachotumika kusambaza maji jijini Arusha ambacho kimesongwa na shughuli za binadamu kikiwemo kilimo na upandaji miti ambayo sio rafiki na vyanzo vya maji. 
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), Eric Solheim akiwa na ujumbe wake wakifatilia mada iliyowasilishwa na Meneja wa Baraza la Mazingira Kanda ya Kaskazini (NEMC) Novatus Mushi. 
  Mratibu wa kitaifa wa UNEP nchini, Clara Makenya akizungumza jambo kwenye ziara hiyo,kushoto ni Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha, Richard Kwitega na Mkuu wa wilaya ya Arusha, Gabriel Daqarro. 
  Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), Eric Solheim (kushoto kwake) naa maafisa wengine wa UN pamoja na ofisi ya Mkuu wa mkoa. 
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), Eric Solheim (mwenye tai) akiangalia chanzo cha maji cha Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingiri jijini Arusha (AUWSA) eneo la Olgilai Kata ya Kiutu alikofika kuangalia uharibifu wa chanzo hicho.

  0 0

   
   Iringa mjini
  LUKI 1
   Mji wa Iringa ukionekana kwa mbali
  LUKI 2
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (mwenye suti nyeusi) akitatua moja ya mgogoro wa ardhi mkoani Iringa.
  ………………
  Na Hassan Mabuye (Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Ardhi)
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi anaendelea na ziara zake za utatuzi wa Migogoro ya Ardhi nchini, ambapo jumatano hii tarehe 25 Januari 2017 atawapatia wakazi wa kijiji cha Kinywang’anga Iringa vijijini.
  Katika ziara hii Mhe. Lukuvi atakutana na wananchi hao waliopimiwa maeneo yao ya viwanja na mashamba ambao kwasasa hati zao za umiliki wa ardhi hizo zimeishaandaliwa na  ziko tayari kukabidhiwa kwao.
  Ziara hii ni katika utekelezaji wa Programu ya Kitaifa ya kupima na kumilikisha ardhi na kuzuia migogoro ya ardhi wenye lengo la kufanyika kwa nchi nzima. Utekelezaji huo utahusisha kuhakiki mipaka ya Mitaa na Vijiji pamoja na maeneo  mengine yote nchini na kupima kila kipande cha ardhi kwa lengo la kumilikisha ardhi hiyo kwa wananchi, taasisi na Kampuni.
  Sambamba na hilo, Matangazo ya Serikali yanayotambulisha mipaka ya mikoa, Wilaya, Hifadhi za Taifa na vijiji yatafanyiwa marekebisho baada ya mipaka yote nchini kuhakikiwa na kukamilika.
  Aidha mpango huu unalenga kuwaunganisha wadau wa sekta ya ardhi katika kupanga, kupima, na kumilikisha ardhi nchini na kuweka kumbukumbu za vipande vya ardhi ili kuongeza thamani ya ardhi na kuondoa migogoro ya ardhi kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
  Serikali ya awamu ya tano imeweka adhma ya kumaliza migogoro ya ardhi iliyopo sasa na kuzuia kasi ongezeko la migogoro ya ardhi ndani ya miaka mitano kwa kuandaa mpango kabambe wa matumizi na usimamizi wa ardhi kwa kuharakisha na kurahisisha upatikanaji wa hati za umiliki wa viwanja na mashamba.


  0 0

  Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na Bodi ya Mahusiano ya Kigeni kwenye masuala ya Kiuchumi nchini Uturuki (DEIK) wameingia makubaliano kuanzisha Baraza la Kibiashara baina ya nchi mbili,makubaliano hayo yalifikiwa tarehe 23 Januari 2017 jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TPSF),Godfrey Simbeye amesema Baraza hilo litakuwa na majukumu na shughuli mbalimbali kama kusaidia kukuza biashara kati ya nchi hizo mbili,kutoa mchango katika kuanzisha kukuza Viwanda kupitia ushirikiano wa Teknolojia wa mashirika na Taasisi za Kiuchumi za nchini Uturuki.

  Pia amesema kuratibu juhudi za pamoja kukusanya,kuunganisha,
  kuniambia,kutathmini na kieneza taarifa zinazohusu biashara.Amesema Baraza hilo litasaidia kutambua changamoto za kibiashara baina ya nchi hizo mbili na kwenye ushirikiano Kiuchumi.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF),Reginald Mengi amesema kuwa Baraza hilo la Kibiashara baina ya Uturuki na Tanzania litagawa katika kamati za Kitaifa mbili.Kila kundi litakuwa na Wanachama wake na Taasisi  za Kiuchumi au za Kibiashara.

  Amesema kuwa Kamati hizo ndogo za Baraza zinatarajiwa kukutana angalau Mara moja kwa Mwaka,kutazama na kujadili mafanikio ya Baraza kwenye masuala ya Kibiashara,Uwekezaji,
  Teknolojia baina ya nchi hizo mbili.
   Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini,Reginald Mengi akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Uundwaji wa Baraza la Kibiashara baina na Tanzania na Uturuki.
  Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF,Godfrey Simbeye akizungumzia majukumu ya Baraza lilioundwa kati ya nchi mbili za Tanzania na Uturuki.Kushoto ni Mwenyekiti wa TPSF,Reginald Mengi.

  0 0

   Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana maafisa wa Jeshi la Polisi baada ya kuwasili mkoani Songwe kwa ziara ya kikazi na kutembelea idara zilizopo chini ya wizara yake kwa lengo la kufuatilia utendaji kazi wa idara hizo na kuzishauri.( Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
   Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, ACP Mathias Nyange(kulia), akimuongoza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni kutembelea makao makuu ya Jeshi la Polisi mkoani Songwe wakati wa ziara ya naibu waziri yenye lengo la kufuatilia utendaji kazi wa idara za wizara yake  na kuzishauri ili kuweza kudhibiti hali ya uhalifu mkoani hapo.
   Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wakuu wa Idara zilizopo chini ya wizara yake, alipowasili mkoani Songwe kwa ziara ya kikazi ikiwepo kufuatilia utendaji wa idara hizo katika kukabiliana na hali ya usalama kwa mikoa iliyopo mipakani.
   Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia), akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Mkoa wa Songwe, Coletha Peter, alipofanya ziara katika ofisi hizo kwa lengo la kujua zoezi la kuandikisha wafanyakazi wa umma lilipofikia.
   Naibu Waziri wa Wizara ya  Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza  baada ya kupata maelezo ya mradi wa Ujenzi wa ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe unaojengwa kwa ushrikiano wa wadau wa mkoa huo na jeshi la polisi.Wapili kushoto ni Kamanda wa Polisi wa mkoa huo ACP Mathias Nyange.
  Naibu Waziri wa Wizara ya   Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(watano kulia), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa idara zilizopo chini ya wizara yake katika mkoa wa Songwe  mara baada ya kufanya mazungumzo na wafungwa katika gereza la wilaya ya Mbozi ambapo aliwataka kufanya kazi wanazopangiwa ili wawe rasilimali watu katika dhana ya kulipeleka Taifa katika uchumi wa kati.

  IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI –WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI  0 0

  WEK
    Askofu wa Dayosisis ya Mashariki na Pwani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akiweka fedha mara baada ya kuzindua tawi jipya la benki ya Maendeleo la Kariakoo, jijini Dar es Salam, nyuma yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Ibrahim Mwangalaba akifuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Amulike Ngeliama (kulia). 
  WEK 1
  Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Banki Ibrahim Mwangalaba akiteta jambo na baadhi ya wateja wa kwanza waliyohudhuria ufunguzi wa tawi jipya la Kariakoo. 
  WEK 2
  Askofu wa Dayosisis ya Mashariki na Pwani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa  akiweka wakfu na kuzindua tawi jipya la Maendeleo banki, Kariakoo wakati wa hafla hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi, Amulike Ngeliama, na kushoto ni Mkuu wa Jimbo la Kati Mch. Frank KImambo
  WEK 3
  Mkurugenzi mtendaji wa Maendeleo Bank, Ibrahim Mwangalaba akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa tawi la Kariakoo.
  WEK 4
  Baadhi ya Viongozi wa Maendeleo Bank wakiwa katika picha ya pamoja watatu kutoka kushoto ni Meneja wa Tawi Nuru Shadrack katika uzinduzi uliofanyika Kariako na kuzinduliwa na Baba Askofu Dkt Alex Malasusa.
  BAKO
  Meneja wa Tawi la Maendeleo Bank Nuru Shadrack akiwa anaongea na waandishi wa habari hawapo pichani katika uzinduzi wa bank hiyo iliyozinduliwa na Askofu wa Dayosisis ya Mashariki na Pwani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa
  BAK KARI
  Askofu wa Dayosisis ya Mashariki na Pwani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akiwa anazindua Maendeleo bank jiji Dar es salaam akianza kwa Maombi ili bank hiyo iwe na neema kwa watumiaji
  BAK KARI 2
  Baadhi ya Wafanyakazi wa Maendeleo bank wakiwa pamoja na wateja waliojitokeza katika uzinduzi huo jijini Dar es salaam wakiwa tayari kuanza kuweka pesa zao
  BAK KARI 3
  …………….
  Na.Alex Mathias,Dar es salaam.

    Askofu wa Dayosisis ya Mashariki na Pwani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa amezindua Maendeleo Bank Kariakoo jijini Dar es salaam huku akitoa pongezi kwa watumishi wa Kanisa kwa kuweza kuamua kuwasaidia Watanzania katika kuweka pesa zao katika bank hiyo.

  Akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau mbalimbali waliohudhulia uzinduzi huo Askofu Dkt.Alex Malasusa,amesema kuwa ni wakati wa Watanzania kuacha kufisha pesa nyumbani na kuweka kwenye vibubu kwani bank hii itaweza kuwasaidia katika kazi zao pindi wanapokuja kuweka pesa au kuomba mkopa.

  “Hii Maendeleo bank ni ya watu wote haichague dini kwa hiyo mtu yoyote anweza kufungua Account kwa lengo la kutunza pesa zao na pia amewaasa watanzania kuwa na nidhamu ya pesa kwani wataweza kufanya shughuli zao kwa kufuata misingi ya dini pamoja na sheria za nchi”amesema Askofu Dkt.Alex Malasusa

  Kwa Upande wa Mkurugenzi Mtendaji Mr.Ibrahim Mwangaleba amesema kuwa Maendeleo bank ni ya watu wote wa dini zote na inawakaribisha wateja waje kuweka pesa zao katika mahali salama na haitakuwa na ubanguzi wowote japokuwa ni ya Kikristo.

  “Sisi tumeamua kufungua tawi la Maendeleo bank katika eneo la Kariakoo na tunaamini kwa imani kuwa hii itakuwa bank kubwa kuliko tawi lolote hapa jijini Dar es salam na itakuwa bega kwa bega na wateja watakaokuja kuchukua mkopo kwani hapa Fedha zitakuwa na maombi kwa lengo la wateja kwenda kuwa na maendeleo ya hali ya juu”amesema Mwangaleba

  0 0

  Evelyn Mkokoi na Lulu Mussa.

  Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Serikali ya Mapinduzi  Zanzibar (SMZ) ambao pia ni wajumbe wa kamati ya Kusimamia viongozi wakuu wa kitaifa wamekutana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Masuala ya Muungano na Mazingira Mh. January Makamba, Jijini Dar es Salaam wakiwa na lengo la kuzungumzia baadhi ya changamoto za Muungano na kubadilishana mawazo katika maeneo ya Muungano.

  Waziri Makamba aliwapongeza wajumbe wa Kamati hiyo, na  kusema kuwa ujio wao unaonyesha dhamira nzuri ya kuwawakilisha wananchi wa Zanzibar na kuimarisha Muungano uliodumu kwa miaka hamsini na saba (53) sasa.

  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Omary Seif Abeid ambaye pia ni Muwakilishi wa Jimbo la Konde Pemba, alisema kuwa, pande hizi mbili za Muungano hazina Budi kuwakumbuka waasisi wa Muungano huo Hayati Mzee Abeid Amani Karume na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kuunganisha pande mbili hizi na kupatikana kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kusema  kuwa anaeubeza Muungano anajibeza mwenyewe.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba  (katikati) akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi wa Kuu wa Kitaifa. Wajumbe wa Kamati walifanya ziara ya kikazi katika Ofisi ya Makamu wa Rais Mtaa wa Luthuli Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bw. Omary Seif Abeid na Bw. Mihayo Juma N'hunga Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais Zanzibar.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba  (aliyesimama) akiwakaribisha wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi wa Kuu wa Kitaifa mara baada ya kumtembelea Ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora  (aliyesimama) akiongea na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi wa Kuu wa Kitaifa, mara baada ya kufanya ziara ya kikazi. Kushoto ni Mkurugenzi wa Muungano Bw. Baraka Rajab Baraka.
  Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi wa Kuu wa Kitaifa wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba.

  0 0

   United Nations Environment Programme, Executive Director, Erik Solheim (right) speaks to reporters at the news conference held in Dar es Salaam on his official visit to Tanzania on Global environmental agenda, on his right, UN Resident Coordinator, Alvaro Rodriguez.
  United Nations Environment Programme (UNEP), National Coordination Officer, Ms Clara Makenya (right) when she stressed a point to reporters during the press conference held in Dar es Salaam on the official visit to UN Environment Head Erik Solheim to Tanzania. Second left is UNEP, Executive Director, Erik Solheim, far left, UN Resident Coordinator, Alvaro Rodriguez. 
  TANZANIA should adapt recycling waste policy, increasing uses of gas instead of charcoal for cooking as a long term solution on ensuring sustainable environmental protection to tape the pressing challenge of climate change.

  Speaking to reporters in Dar es Salaam on his first visit to the country, UN Environment Programme (UNEP), Executive Director, Erik Solheim said that UNEP is the leading global environment authority that sets the global environment agenda.

  “The discovering of gas reserved in Tanzania should be use as stepping stone to employment, business opportunity and as a tool to alleviate poverty,” he noted.

  He commended that the efforts taken by the government through local municipalities for setting an area in the outskirt of city center Pugu Dampo as a permanently place for cabbage without destructing the environment of the Dar es Salaam city.

  Solheim added that the UN environment works with a wide range of partners, including United Nations entities, international organizations, national governments, non-governmental organizations, the private sector and civil society.

  He added hope that “other leaders will be inspired to pick up the baton and ensure that Africa’s rich natural resources can be conserved, and thus serve as the foundation for a sustainable future and food security for all on the continent.”

  He said that the government should also adding some efforts in banning the uses of plastics bags as the magnitude of it increases the environmental degradation that pose a huge threat to the country’s social and economic development.

  “We also hailed efforts taken by the high commissioners here in Tanzania such as China and former two former Presidents Hon. Mwinyi and Hon. Mkapa for participating in the recently anti-poaching marching,” he stressed.

   On her part, UNEP, National Coordination Officer, Ms Clara Makenya said that the visit of the UNEP boss emphasized much on the reduction of uses of charcoal for cooking as the cultural fuel the cutting of trees across the country.

  “We had an opportunity to meet civil society, NGOs and academicians on the pressing issues of climate change and food security as a scorching agenda in many years to come,” she added.

  UNEP, boss has been following with keen interest and commends the efforts by the President of the United Republic of Tanzania, Dr John Magufuli in the fight of corruption and bring about to an end of poaching and the illegal wildlife trade.

  UN environment views the shift to Dodoma as an opportunity to bring about positive change and development not just to the central part of Tanzania, but also the whole country. The sustainability of this anticipated growth can be reinforced with the integration of environmental consideration.

  In cooperation with partners, UNEP supports cities across the world in addressing environment impacts and integrating the environment into the long term strategic planning. It has been the case with the programs that UN environment has had in the country, such as the poverty and environment initiative.

  Africa Environment Day, marked annually on 3 March, focuses on last year on ‘Combating Desertification in Africa: Enhancing Agriculture and Food Security.’

  The continent has lost 65 per cent of its agricultural land since 1950 due to land degradation, according to figures cited by UNEP. Up to 12 per cent of its agricultural gross domestic product (GDP) is lost due to deteriorating conditions and 135 million people are at risk of having to move from their land by 2020 due to desertification.

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Iringa mjini, Richard Kasesela baada ya kuwali kwenye uwanja wa Nduli  mjini  IringaKulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Amina Masenza. akiwa njiani  kuelekea Njombe kuendelea na ziara ya kazi Januari 25, 2017.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiakaribiwahwa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka baada ya kuwasili Makambako kuendelea na ziara ya mkoa huo, Januari 25, 2017.
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Njombe, Deo Sanga baada ya kuwasili Makambako kuendelea na ziara ya mkoa huo, Januari 25, 2017.  Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0  WITO KWA WALIOKUWA WAFANYAKAZI WA ULIOKUWA MGODI WA DHAHABU BULYANHULU

  UPIMAJI ULIOFANYIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI .

  Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) unawakaribisha walioorodheshwa hapo chini kufika katika ofisi za OSHA zilizopo Kinondoni Manyanya karibu na mahakama kati ya tarehe 26 na 27 Januari ili waweze kupewa majibu yao. Tangazo hili linawahusu waliopimwa Muhimbili tu. Waliopimwa Bugando wanaombwa kusubiri tangazo jingine.  Imetolewa na:
  MTENDAJI MKUU
  WAKALA WA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI (OSHA)
  S.L.P 519, MAHAKAMA ROAD KINONDONI
  DAR ES SALAAM.

  0 0

  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Ramadhan Kailima

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeeleza  kuwa Kura 234 ziliharibika katika Uchaguzi mdogo wa Ubunge katika jimbo la Dimani, Zanzibar Januari 22, 2017.

  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Ramadhan Kailima amesema kuwa Wapiga Kura walioandikishwa katika jimbo la Dimani, Zanzibar ni 9,275.

  Amesema kati ya hao wapiga Kura 6,406 walijitokeza kupiga Kura siku hiyo ambapo Kura halali zilikuwa 6,172 na Kura zilizoharibika zilikuwa 234.

  “Napenda kuwafahamisha wananchi wote kuwa taarifa sahihi za matokeo ya Kura katika Uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Dimani ni kama ifuatavyo; Wapiga Kura walioandikishwa jimbo la Dimani ni 9,275, Waliopiga Kura walikuwa 6,406, Kura halali 6,172 na Kura zilizoharibika ni 234” Amesisitiza.

  Mkurugenzi Kailima ameeleza kuwa katika Uchaguzi huo vyama 11 vilikuwa na wagombea wa Ubunge ambapo Chama cha ACT-Wazalendo kilipata Kura 8, Chama cha ADC Kura 42, Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kura 4860, CHAUMA Kura 10, Chama Cha Wananchi CUF Kura 1234, Chama cha DP Kura 8.

  Vingine ni Chama cha NRA kura 1, SAU Kura 4, TLP kura 2, Chama Cha UMD Kura 2 na Chama Cha UPDP Kura 1 na kufanya jumla ya Kura za Vyama vyote kuwa 6172. 

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop wa kwanza kulia wavivuta kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –TAMISEMI George Simbachawene pamoja na  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –TAMISEMI George Simbachawene na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop wakwanza (kulia) akivuta utepe kuashiria Ufunguzi rasmi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka kadi ya Kieletroniki katika Mashine ya UDART ilikuweza kupita kama ishara ya Ufunguzi rasmi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam. Pembeni yake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –TAMISEMI George Simbachawene akimuelekeza jambo katika mashine hizo.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop pamoja na viongozi wengine wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipita kwenye mashine hizo mara baada ya uzinduzi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kwa wanahabari mara baada ya kuzindua utoaji huo wa huduma ya usafiri.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia mara baada ya kuendesha gari la Mwendo Kasi katika kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo Haraka (BRT) mara baada ya kufungua rasmi Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam.
   ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipungia mkono pamoja na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop mara baada ya kutoka kukagua moja ya basi linalotumika katika utoaji huduma ya Usafiri wa Haraka (BRT)
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo pamoja na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makhtar Diop wakati Msanii Mrisho Mpoto alipokuwa akitumbuiza.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Mhe. Makhtar Diop kwenye sherehe za ufunguzi rasmi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam leo Januari 25, 2017.
  Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Mhe. Makhtar Diop akiongea machache kwenye sherehe za ufunguzi rasmi wa Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji Huduma ya Mabasi yaendayo Haraka katika jiji la Dar es Salaam leo Januari 25, 2017.

  PICHA NA IKULU

  0 0

   
   Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira, Profesa Faustine (kushoto), akizungumza na wakuu wa wilaya za Dodoma na maofisa watendaji na wenyeviti wa serikali za mitaa na wadau wa kilimo  alipotembelea shamba la Jaribio la Mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya Uhandisi Jeni (GMO) chini ya Mradi wa Mahindi Yanayostahimili Ukame (WEMA) katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha  Makutupora mkoani Dodoma leo.
   Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Dodoma wakiwa kwenye mkutano na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira, Profesa Faustine (hayupo pichani), walipotembelea Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mkoani Dodoma leo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deogratius Ndejembi, Bahi, Elizabeth Kitundu, Mpwapwa Jabir Shekimweri na Mshauri wa Kilimo Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Aziza Mumba.
   Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Hussein Mansour akizungumza (kushoto), akiwaelekeza jambo Wakuu wa Wilaya wa Mkoa wa Dodoma walipotembelea shamba la Jaribio la Mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya Uhandisi Jeni (GMO) chini ya Mradi wa Mahindi Yanayostahimili Ukame (WEMA) katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha  Makutupora mkoani Dodoma leo. Kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Elizabeth Kitundu, Kongwa, Deogratius Ndejembi, Mpwapwa, Jabir Shekimweri na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira, Profesa Faustine Kamuzora.
   Wanahabari, watafiti wa kilimo, wenyeviti wa serikali za mitaa na watendaji wakiwa kwenye mkutano kabla ya kutembea shamba hilo la jaribio la mahindi.
    Wanahabari, watafiti wa kilimo, wenyeviti wa serikali za mitaa na watendaji wakiwa nje ya lango kuu la kuingia katika shamba hilo wakisubiri kupewa taratibu za kuingia.
   Mshauri wa Mradi wa Mahindi Yanayostahimili Ukame (Wema), Dk.Alois Kullaya (kulia), akitoa maelezo kabla ya kuingia kwenye shamba hilo la jaribio la mahindi.
  Mtafiti wa Kituo hicho,Ismail Ngolinda (kulia), akitoa maelekezo kuhusu shamba hilo.
  Mshauri wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange (kushoto), akizungumza na viongozi mbalimbali baada ya kutembelea shamba hilo. Kutoka kulia ni  Mshauri wa Mradi wa Mahindi Yanayostahimili Ukame (Wema), Dk.Alois Kullaya, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira, Profesa Faustine, Kaimu Mkurugenzi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira, Richard Muyungi, Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Hussein Mansour na Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo Kanda ya Kati Dodoma, Dk. Leon Mroso.

   Mshauri wa Mradi wa Mahindi Yanayostahimili Ukame (Wema), Dk.Alois Kullaya, akielekeza kuhusu mahindi hayo ya jaribio hilo.
  Picha ya Pamoja.

  Na Dotto Mwaibale, Dodoma
   
  KATIBU Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira, Profesa Faustine Kamuzora amesema utafiti wa kilimo ni muhimu ili kuongeza chakula nchini.
   
  Kamuzora alitoa kauli hiyo alipotembelea shamba la Jaribio la Mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya Uhandisi Jeni (GMO) chini ya Mradi wa Mahindi Yanayostahimili Ukame (WEMA) katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha  Makutupora mkoani Dodoma leo.
   
  Alisema bila ya kuwepo kwa utafiti wa kilimo hatuwezi kufikia ufanisi wa kupata chakula kingi hivyo matokeo mazuri ya utafiti ni muhimu kwa maendeleo ya kilimo.
   
  Alisema majaribio ya kisayansi ni muhimu na ni mkombozi kwa mkulima hasa katika kipindi hiki cha mabadiliko ya tabia nchi na ukame.
   
  Katika hatua nyingine Kamuzora aliwataka wakuu wa wilaya na watendaji na wenyeviti wa serikali za mitaa wa mkoa wa Dodoma waliotembelea shamba hilo kuwa mabalozi kwa wananchi wao kwa kile walichokiona kwenye shamba hilo la majaribio. 
   
  Aliomba kuwepo na subira wakati utafiti huo ukiendelea na kusubiri kuthibitishwa na vyombo vyenye dhamana na kama wataona unafaa basi utatumika.
   
  ” Utafiti haufanywi kwa siku moja na kuanza kutumika una mlolongo mrefu ili kutoa nafasi kwa vyombo husika kuona kama upo salama na kuruhusu kutumika” alisema Kamuzora
  Alisema vyombo vyenye dhamana vikiridhika vitatoa kibali cha kuanza utumiaji wa teknolojia hii mpya licha ya nchi nyingine za wenzetu kuanza kuitumia,” alisema.
   
  Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deogratius Ndejembi alisema ni muhimu sasa kuharakisha matumizi ya teknolojia hiyo badala ya kupoteza muda mwingi ukizingatia kuwa hivi sasa nchi inakabiliwa na ukame hasa katika wilaya yake.
   
  “Kazi inayofanywa na watafiti wetu ni nzuri ila nawashauri wafanye utafiti utakaosaidia katika kipindi hiki cha  mabadiliko ya tabia nchi yaliyopo maeneo mbalimbali.
   
  Mkuu wa Wilaya ya Mpwawa Jabir Shekimweri alisema utafiti huo umeonesha mafanikio makubwa hasa pale unapoyaangalia mahindi yaliyotumia mbegu iliyotokana na teknolojia hiyo kuwa ni bora na makubwa wakati yale yaliyotumia mbegu za kienyeji kuwa dhaifu.
   
  “Nisema kuwa mbegu za utafiti huu zitakapoanza kutumika zitasaidia sana wakulima hasa wa wilaya yangu ambayo inakabiliwa na ukame katika baadhi ya maeneo” alisema Shekimweri.

older | 1 | .... | 1114 | 1115 | (Page 1116) | 1117 | 1118 | .... | 1898 | newer