Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46314 articles
Browse latest View live

MECHI YA YANGA NA SIMBA YAPIGWA KALENDA HADI FEBRUARI 25

$
0
0


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baina ya mahasimu, Simba na Yanga umesogezwa mbele hadi Februari 25, kutoka na Yanga kuwa na mashindano ya kimataifa ambapo itawawia vigumu kucheza siku hiyo.

Mchezo huo uliotakiwa kufanyika Februari 18, mwaka huu umesogezwa mbele kuwapisha Mabingwa hao wa ligi kuu 2015/2016 kumaliza mechi zao dhidi ya Ngaye De Mba ambao utachezwa Februari 10 nchini Comoro na kurudiana Februari 17 katika Uwanja wa Taifa.

Habari kutoka ndani ya Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema kwamba sababu ya kusogezwa mbele kwa mchezo huo ni muingiliano na Ratiba ya michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika.Februari 10, mwaka huu, 

Kwa sababu hiyo, mchezo wa Simba na Yanga usingeweza kufanyika tena Februari 18 na busara za TFF zimeupeleka hadi Februari 25.

SHIRIKA LA WAKIMBIZI DUNIANI (UNHCR) LAKABIDHI PIKI PIKI NNE NA KOMPYUTA MOJA WILAYA YA KAKONKO MKOANI KIGOMA

$
0
0
                      Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

SHIRIKA la kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR)  kupitia shirika linalosimamia Shughuli za mazingira kambi za Nduta na Mtendeli na Vijiji vinavyo zunguka kambi (REDESO) limekabidhi Pikipiki nne, Kompyuta moja  pamoja na mafunzo kwa Madiwani vyenye thamani ya shilingi milioni 16.8 kwa halmashauri ya Wilaya ya Kakonko lengo ikiwa ni Kuwawezesha maafisa Wa Maliasili kupita katika maeneo ya misitu iliyo haribiwa na Kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira kwa Wanawake na Vijana.

Akikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya Kiongozi wa UNHCR Mratibu wa Mazingira idara ya Wakimbizi Mkoa wa Kigoma Thobias Sijabaje, 
Mkuu wa Wilaya ya Kakonko , Kanali Hosea Ndagala katika Kikao cha baraza la madiwani kilicho andaliwa na REDESO kwa ajili ya kutoa tathimini , kukabidhi fedha na vifaa vya ofisi kwa maafisa wa Maliasili na madiwani kuelimishwa jinsi ya kutoa elimu kwa Wanawake na vijana juu ya utunzaji wa mazingira. 

Alisema  shirika la UNHCR kwa kupitia REDESO limeamua kutoa Vifaa hivyo na mafunzo kwa madiwani kutokana na hali ya uharibifu wa mazingira  ilivyo katika maeneo yanayo zunguka kambi za wakimbizi kutokana na ujio wa wakimbizi uliopelekea athari kubwa iliyopelekea misitu mingi kuharibiwa lengo ikiwa ni kutafuta ufumbuzi juu ya Suala hilo.

"Kwa kuzingatia hilo tumeandaa mpango wa zaidi ya bilioni moja ya uhifadhi wa mazingira ilikuweza kushirikiana na halmashauri katika kutunza misitu , kwakuanzia tumeanza na vifaa ambavyo tumtetoa kwa wataalamu kuweza kufuatilia maeneo yaliyo haribiwa kwa kiasi kikubwa ilikuweza kupanda miti na kutoa elimu ya uhifadh wa mazingira kwa Wananchi",alisema Sijabeje.

Alisema tatizo la mazingira katika kambi za wakimbizi huwa halikwepeki katika vijiji vinavyo zunguka kambi uharibifu Mkubwa umefanyika.Baada ya kuliona tatizo hilo linalo pelekea uharibifu wa  na uongozi wa  UNHCR kuweza kuangalia jinsi gani ya kutatua tatizo hilo,  na kuamua badala ya kutumia kuni na kujenga Nyumba kwa kutumia miti waliamua kubuni njia ya ufyatuaji wa tofari zinazo tumia udongo,chokaa na Simenti pamoja na kutengeneza majiko yenye uwezo wa o tumia kuni kidogo ilikuepukana na athari zitokanazo na uharibifu wa mazingira. ya

Athari zilizo sababishwa na ujio wa wakimbizi ni pamoja na uharibifu wa mazingira katika maeneo ya kambi zao na maeneo yaliyo jirani na kambi hiyo, kutokana na ukataji wa miti, uharibifu wa vyanzo vya maji na  kwaajili ya matumizi ya kujengea Nyumba za wakimbizi za kudumu na matumizi ya kuni kwaajili ya kupikia.

Aidha  Mtaalamu wa Mazingira Taifa Dkt Braiton Gwamagobe alisema kumekuwa na tabia ya vijana wengi kuingia misituni na kukata misitu bila kujali madhala yanayo weza kujitokeza hali inayopelekea ukame na uharibifu wa tabaka la ozoni unaosababishwa na hewa chafu kutokana na kutokuwa na miti ya kutosha.

Gwamagobe alisema  wakitaka elimu ya utunzaji wa misitu na mazingira ifanikiwe ni pamoja na kutoa elimu hiyo kwa Vijana na wanawake ambao ndio watumiaji wakubwa wa maliasili za misitu kutokana na nguvu kazi waliyo nayo  inayopelekea uharibifu wa  miti kwa kuchoma mkaa, ukataji wa mbao na kulima maeneo ya vyanzo vya maji.

Alisema katika utafiti walio ufanya katika Wilaya ya kakonko wamebaini uharibifu Mkubwa umefanyika hasa katika maeneo ya Kambi za wakimbizi na vijiji vinavyo zungika kambi hizo, na baada ya kufanya tathimini walibaini wanao jihusisha na shughuli hizo wengi wao ni vijana ambao wakipatiwa elimu watasaidia kupambana na athari hizo.

Akitoa Shukrani zake wakati akipokea vifaa hivyo Mkuu wa Wilaya ya Kakonko , Kanali Hosea Ndagala aliwashukuru UNHCR kwa kuthamini umuhimu wa kutunza mazingira kwa kuwawezesha maafisa wa maliasili kufanya shughuli za utunzaji wa mazingira na kutoa wito  kwa maafisa hao kuvitumia vifaa hivyo kwa kazi ya utunzaji wa mazingira na si kwa kazi nyingine.

Alisema Vifaa hivyo vitumike kuwapatia elimu Wananchi wa Vijiijini jinsi ya kutunza mazingira ,kuzungukia maeneo ya liyo halibiwa kwa ukataji miti na sio vifaa vya kufanyia Shughuli zao binafsi ilikufikia lengo la uboreshaji wa mazingira kama mkakati wa UNHCR unavyo eleza
 
 Kiongozi wa UNHCR Mratibu wa Mazingira idara ya Wakimbizi Mkoa wa Kigoma Thobias Sijabaje,akikabidhi funguo za Piki piki  kwa Mkuu wa Wilaya ya Kakonko katika Kikao cha baraza la madiwani kilicho andaliwa na REDESO kwa ajili ya kutoa tathimini , kukabidhi fedha na vifaa vya ofisi kwa maafisa wa Maliasili na madiwani kuelimishwa jinsi ya kutoa elimu kwa Wanawake na vijana juu ya utunzaji wa mazingira.
Mkuu wa Wilaya ya Kakonko , Kanali Hosea Ndagala akipokea  Kompyuta moja  pamoja na mafunzo kwa Madiwani vyenye thamani ya shilingi milioni 16.8 kwa halmashauri ya Wilaya ya Kakonko lengo ikiwa ni Kuwawezesha maafisa Wa Maliasili kupita katika maeneo ya misitu iliyo haribiwa na Kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira kwa Wanawake na Vijana.

Wachezaji Airtel Rising Stars wachanguliwa kujiunga na timu za Taifa

$
0
0
Baada ya kumalizika kwa kliniki ya wiki moja ya Airtel Rising Stars mwishoni mwa wiki jana, wavulana 16 wamechanguliwa kujiunga na timu ya taifa ya Serengeti Boys huku wasichana watatu wakichanguliwa kujiunga na timu ya taifa ya wanawake - Twiga Stars na wengine 17 kuchagulia kuingia timu ya wasichana chini ya miaka 17 ya Kilimanjaro Queens.

Akiongea na waandishi wa habari leo kutangaza majina ya wachezaji hao, Mkurugenzi wa Ufundi TFF Salum Madadi alisema makocha walikuwa na kibarua kigumu kuchangua wachezaji kwani wachezaji wote walionyesha vipaji vya hali ya juu sana. Madadi alisema kwa hali hiyo, ni dhahiri kuwa michuano ya Airtel Rising Stars ambayo ilianzia kwenye ngazi ya wilaya, uchanguzi dhidi ya wachezaji ulikuwa wakuridhisha.

Tulikuwa na jumla ya wachezaji 65 kwenye kliniki ya Airtel Rising Stars, wavulana 40 na wasichana 25. Ni kweli kuwa wachezaji wote hawawezi kuchanguliwa kuchezea timu ya taifa, lakini wachezaji ambao wamebaki tutaendelea kuwatumia kwenye michuano mbali mbali ya vijana. Pia wengine watachanguliwa na klabu zetu kuchezea timu zao za vijana. Natoa wito kwa uongozi kuwatumia vizuri vijana hao kwani vipaji wanavyo wanahitaji uzoefu tu, alisema Madadi.
Meneja Uhusian wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando akizungumza wakati wa kutangaza wachezaji waliochanguliwa kutokana na michuano ya Airtel Rising Stars na kujiunga na timu za taifa za vijana ikiwemo Serengeti Boys.

Mimi kama Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, nitahakikisha Shirikisho inaengemea kwenye upande wa kukuza timu na mashindano ya vijana ili kujenga timu bora ya Taifa. Natoa shukrani kwa Airtel katika mchango wake wa kukuza soka la vijana hapa nchini. Nina uhakika Airtel itaendelea na mashindano haya ya Airtel Rising Stars ili kuendelea kuibua vipaji vya vijana wetu, alisema Madadi.

Tuko kwenye harakati za kuhakikisha tunakuwa na timu za kudumu za umri wa chini ya miaka ya 14, 17 na 19. Tukifanya hivyo tutaweza kujenga timu ambayo itafanya vizuri kwenye fainali za michuano ya AFCON ambayo itafanyika hapa Tanzania kwa mara ya kwanza mwaka 2019, aliongeza Madadi.

Akiongea juu ya kuchangua wachezaji, kocha mkuu wa timu ya Serengeti Boys Bakari Shime ambaye alisimamia kliniki hiyo alisema makocha walichangua wachezaji kulingana na mahitaji ya sasa ya timu ya Serengeti Boys. Tuliengemea kwenye wachezaji ambao wanaweza kuelewa na kuendana na mfumo wa mpira wa mashidano na wachezaji wenye uelewa wa haraka. Kama mnavyojua, timu yetu ya Serengeti imecheza mechi nyingi za kimataifa kwenye miaka miwili iliyopita na hivyo kupata uzoefu wa kimataifa.
Mkurugenzi wa ufundi wa soka la vijana Tanzania chini ya TFF, Kim Paulsen akizungumza wakati wa kutangaza wachezaji waliochanguliwa kutokana na michuano ya Airtel Rising Stars na kujiunga na timu za taifa za vijana ikiwemo Serengeti Boys.

Nia yetu ilikuwa kupata wachezaji wa kuendana na mfumo huo, alisema Shime. Kwa upande wake, Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando aliwapongeza wachezaji waliochanguliwa kujiunga na timu za taifa.

Wachezaji hawa walianza kucheza michuano ya Airtel Rising Stars tangu ngazi ya wilaya. “ Airtel tunayo furaha kuweza kuwafanya wachezaji hawa kutimiza ndoto zao za kucheza mpira wa kulipwa. Kama mnavyojua mpira kwa sasa sio burudani pekee, bali pia ni ajira kwa wachezaji wengi duniani. Ni hamasa kubwa kuona vijana wakianza kujipatia riziki zao kutokana na vipaji vyao vya kucheza mpira wa miguu” alisema Mmbando.

MASAUNI AZINDUA UJENZI WA OFISI ZA POLISI KATIKA KIJIJI CHA UTENGULE WILAYANI MBEYA

$
0
0
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizindua Ujenzi wa Jengo litakalotumika kwa ajili ya ofisi za Jeshi la Polisi katika kijiji cha Utengule.Wanaoshuhudia ni baadhi ya mafundi wakiongozwa na Mhandisi wa Wilaya ya Mbeya, Jesse Shengena (kulia), eneo la ujenzi wa ofisi hizo limetolewa na wananchi ili kuweza kuimarisha ulinzi katika kijiji cha Utengule wilayani Mbeya.
Mhandisi wa Wilaya ya Mbeya, Jesse Shengena (kushoto), akimuelekeza Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(katikati) ramani ya Ujenzi wa Jengo litakalotumika kwa ajili ya ofisi za Jeshi la Polisi katika kijiji cha Utengule wilayani Mbeya. Kulia ni Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Emmanuel Lukula.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Emmanuel Lukula, akitoa maelezo juu ya Ujenzi wa Jengo litakalotumika kwa ajili ya ofisi za Jeshi la Polisi kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), eneo la ujenzi wa ofisi hizo limetolewa na wananchi ili kuweza kuimarisha ulinzi katika kijiji hicho cha Utengule wilayani Mbeya.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Utengule baada ya kuzindua Ujenzi wa Jengo litakalotumika kwa ajili ya ofisi za Jeshi la Polisi katika kijiji cha Utengule wilayani Mbeya.Naibu Waziri aliwashukuru wananchi hao kwa kujitolea eneo la kujengwa ofisi za watumishi na askari wa jeshi ikiwa ni juhudi zao katika kupambana na matukio ya uhalifu katika kijiji chao.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia), akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Utengule, alipowasili kuzindua ujenzi wa jengo litakalotumika kwa ajili ya ofisi za Jeshi la Polisi huku eneo hilo likitolewa na wananchi wa kijiji hicho.Kulia ni Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Emmanuel Lukula.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

MSIMU WA PILI WA MRADI WA KUWAWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI KUPITIA TAASISI YA "MANJANO FOUNDATION"

$
0
0
Mradi wa Kuwawezesha wanawake Kiuchumi Kupitia Tasnia ya urembo ujulikanao kama Manjano Dream-Makers ulioasisiwa na Taasisi ya Manjano Foundation utaendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa Mikoa ya Dar es salaam, Mbeya, Mtwara, Tabora na Kigoma kwa mwaka 2017. 

Mafunzo hayo yatatolewa kwa Wanawake watakaotuma maombi na watakaochaguliwa katika Mikoa hiyo husika. Baada ya mafunzo hayo wanaweke hao watakuwa chini ya uangalizi wa Taasisi hiyo kwa mwaka mmoja kwa lengo la kuhakikisha wanafikia malengo yao waliojiwekea. 

Wanawake wakazi wa mikoa ya Dar es salaam, Mbeya, Mtwara, Tabora na Kigoma wanaopenda kunufaika na mradi huo wanaombwa kutuma maombi na kujisajili kupitia Tovuti ya http://www.manjanofoundation.org/
Mafunzo hayo yana lengo la kumsaidia mjasiriamali Mwanamke kujikwamua na kujiongezea kipato kupitia Tasnia ya Vipodozi.

 Awamu ya kwanza ni kumfundisha maswala ya biashara namna ya kuibua na kubuni miradi mbalimbali namna ya kuandika mpangilio wa biashara ikiwemo matumizi sahihi ya rasilimali muda, kutokufuja fedha, muda na pia namna ya kujitunzia akiba itokanayo na biashara yake. 
Awamu ya pili ya mafunzo hayo itahusu kuwafundisha jinsi ya kupamba ma harusi na matumizi sahihi ya vipodozi vya LuvTouch Manjano na elimu ya ngozi.

Biashara 5 unazoweza kuzifanya jijini Dar es Salaam na kukuingizia kipato

$
0
0

Na Jumia Travel Tanzania

Kuishi katika jiji kubwa kama vile Dar es Salaam kuna changamoto nyingi endapo hauna shughuli maalum ya kukuingizia kipato cha kila siku. Na ili kufanikiwa katika hilo basi huna budi kuwa mwerevu wa kugundua ni biashara ipi ukiifanya itakuwa inakuingizia kipato cha haraka.

Kama unaishi au ulikuwa na mpango wa kuja kutafuta maisha jijini Dar es Salaam, Jumia Travel inakushauri kujaribu kufanya shughuli zifuatazo ili kukuingizia kipato:

Kuuza vinywaji baridi (maji, soda, juisi, n.k.)
Kwa kipindi kirefu hali ya hewa ya jiji la Dar es Salaam huwa ni joto na jua kali, hivyo kupelekea uhitaji na utumiaji mkubwa wa vinywaji baridi. Hii ni fursa kubwa kwa wafanyabiashara kwani watu hawawezi kuvumilia jua kali bila ya kutumia vinywaji kama vile maji, soda au juisi. Mtaji wa biashara hii sio mkubwa sana na haihitaji ofisi, kitu ambacho kinamuwezesha mtu yeyote kufanya biashara hii.  

Kuuza matunda
Wakazi wa jiji hili hupendelea matunda katika milo yao tofauti iwe ni asubuhi, mchana au usiku. Biashara hii ni nzuri kwa kigezo kikubwa kwamba watu hawana mashamba, matunda mengi huingizwa kutoka mikoa mingine. Mtaji wa biashara hii ni mdogo na sehemu nzuri za kupatia wateja ni kwenye vituo vya mabasi, pembezoni mwa barabara, karibu na migahawa au karibu na ofisi.

Kuuza magazeti
Magazeti ni nyenzo mojawapo ya kupatia habari ambayo wakazi wengi wa Dar es Salaam huitumia. Kutokana na kutingwa na shughuli nyingi, wengi wao huwa hawana muda wa kupitia kwenye sehemu maalum zinazouza magazeti. Njia pekee ya kuwafikia ni kwenye foleni za magari asubuhi wanapokwenda na jioni wanaporudi kwenye shughuli zao.

Uchuuzi wa vyakula vya baharini (Pweza, ngisi, dagaa kamba, n.k.)
Kijiografia Dar es Salaam imepakana na bahari ya Hindi kwa sehemu kubwa na kupelekea upatikanaji wa vyakula vya baharini kuwa rahisi. Vyakula kama vile samaki wa aina tofauti, pweza, ngisi, dagaa kamba na kadhalika ni baadhi ya vinavyopendwa na wakazi wengi. Biashara hii ni rahisi kuifanya kwani haihitaji mtaji mkubwa wala ofisi na pia hivyo vyakula huuzwa kwa gharama ndogo ambayo kila mtu anaweza kuimudu. Hufanyika muda wa jioni kandokando ya barabara na kwenye vituo vya mabasi ambapo watembea kwa miguu na abiria wengi hupita wakirejea makwao.   

Kuuza vocha za muda wa maongezi wa kwenye simu
Faida ya kuishi kwenye jiji hili ni kwamba makampuni na taasisi zote kubwa ofisi zake zinapatikana hapa. Hali hiyo hutoa fursa kwa wafanyabiashara kuwa mawakala ili kuwafikia wateja wa kawaida. Mojawapo ya huduma muhimu inayotumika muda wote ni huduma za simu za mkononi kwa ajili ya mawasiliano ambapo si chini ya makampuni matano yanaendesha shughuli zake. Hii hupelekea wanaouza vocha za muda wa maongezi kuwa na uhakika na biashara zao.

Hizo ni baadhi tu ya biashara ndogondogo ambazo zitakufanya uishi vizuri katika jiji la Dar es Salaam ambalo bila ya shughuli maalum ya kufanya si rahisi kulistahimili. Jumia Travel inaamini dondoo hizi zitakuamsha wewe mkazi au mwenyeji ambaye ulikuwa unajiuliza nini cha kufanya ili ujiingizie kipato kwa urahisi.

WAKINAMAMA WA KIKUNDI CHA 2SEEDS WAJIKWAMUA KIMAENDELEO CHINI YA VODACOM TANZANIA FOUNDATION

$
0
0
 Wakinamama wa kikundi cha 2Seeds, wa  kijiji cha  Tabora Wilaya ya Korogwe Tanga, wakishirikiana na Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa  Vodacom  Tanzania Foundation, Sandra Oswald (wapili kulia) kumenya viazi  wakati alipotembelea kikundi hicho hivi karibuni kujionea maendeleo ya miradi  mbalimbali ya ujasiliamali, ufugaji, Kilimo, inayofanywa na kikundi hicho na kufadhiliwa na  mfuko wa kusaidia jamii "Vodacom Tanzania Foundation" kwa  kushirikiana na shirika lisilo la Kiserikali la 2Seeds Network  la nchini Marekani. 
 Mwenyekiti wa kikundi cha 2Seeds cha kijiji cha Tabora Korogwe Tanga,Asha Rajab(wapili kushoto) akimuonyesha Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom  Tanzania Foundation, Sandra Oswald ( kushoto) moja ya mifuko yenye embe zilizotengenezwa kitalaam na kuhifadhiwa kwenye mifuko maalumu tayari kwa kuuzwa sokoni,wakati alipotembelea Kikundi hicho hicho hivi karibuni kujionea maendeleo ya miradi mbalimbali ya  ujasiriamali ,ufugaji,kilimo, inayofanywa na kikundi hichokilichofadhiliwa na  mfuko wa kusaidia jamii”Vodacom Tanzania Foundation” kwa  kushirikiana na shirika lisilo la Kiserikali la 2Seeds Network  la nchini Marekani. 
 Bibi  Masoko wa kikundi cha 2 Seeds  cha kijiji cha  Tabora Wilaya ya Korogwe Tanga ,Mariam Jecha (wapili kulia) akimfafanulia jambo hivi karibuni,Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom  Tanzania Foundation, Sandra Oswald (Kushoto) kuhusiana na jiko la kisasa la kukaangia chips za viazi na mihogo zinazozalishwa na kikundi hicho  baada ya kupata mafunzo  ya ujasiliamali kutoka kwenye taasisi isiyo ya kiserikali ya 2Seeds  ya nchini Marekani  yenye makazi yake makuu Wilayani humo, Mradi huo umefadhiliwa na na mfuko wa kusaidia jamii”Vodacom Tanzania Foundation”
 Moshi Abdallah na Monica Ayubu wa kikundi cha 2Seeds  cha kijiji cha  Tabora Wilaya ya Korogwe Tanga,wakimshuhudia  Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom  Tanzania Foundation, Sandra Oswald,(kulia) akiangalia ubora wa vyakula vinavyosindikwa na kikundi hicho, wakati alipotembelea hivi karibuni kujionea maendeleo ya miradi mbalimbali ya  ujasiriamali ,ufugaji,kilimo, inayofanywa na kikundi hicho kilichofadhiliwa na  mfuko wa kusaidia jamii”Vodacom Tanzania Foundation” kwa  kushirikiana na shirika lisilo la Kiserikali la 2Seeds Network  la nchini Marekani. 
Mratibu wa kikundi cha 2Seeds  cha kijiji cha  Tabora Wilaya ya Korogwe Tanga, Moshi Abdallah(kushoto)  akimuonyesha mradi wa kilimo cha mboga Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom  Tanzania Foundation, Sandra Oswald, wakati alipotembelea hivi karibuni kujionea maendeleo ya miradi mbalimbali ya  ujasiriamali ,ufugaji,kilimo, inayofanywa na kikundi hicho kilichofadhiliwa na  mfuko wa kusaidia jamii”Vodacom Tanzania Foundation” kwa  kushirikiana na shirika lisilo la Kiserikali la 2Seeds Network  la nchini Marekani.

Balozi Mgaza apigia chapuo ‘Hapa Kazi Tu’ Saudi Arabia

$
0
0
Na Mwandishi Maalum, Saudi Arabia.

WATANZANIA waishio nchini Saudi Arabia, wametakiwa kufanya juhudi za kuitangaza nchi yao pamoja na kuangalia namna ya kutekeleza kiu ya nchi ya viwanda kama ilivyoasisiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dr John Pombe Magufuli.
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemedi Mgaza, mwenye suti nyeusi, akifurahia jambo ofisini kwa Waziri anayeshughulikia Masuala ya Hijja na Umrah wa Serikali ya Saudi Arabia, Mhe. Dr. Mohammed Saleh Bin Taher Benten, alipofika ofisini kwake kujadiliana mambo mbalimbali ikiwamo hija ya mwaka huu wa 2017.
Baadhi ya Watanzania wanaoishi nchini Saudi Arabia, wakimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemedi Mgaza, hayupo pichani walipokutana katika kikao cha pamoja kwa ajili ya kuangalia fursa za kimaendeleo nchini Tanzania.

Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki mjini Jeddah, Saudi Arabia na Balozi wa Tanzania nchini hapa, H.E Hemedi Mgaza, alipofanya kikao na Watanzania waishio nchini hapa kama njia za kushirikiana na wadau hao kwa ajili ya kupeleka maendeleo ya uhakika nchini Tanzania na kuisimamia kwa vitendo kauli mbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’.

Akizungumzia juu ya fursa ya uwekezaji nchini Tanzania, Balozi Mgaza alisema ni wajibu wa kila mmoja kufanya kazi kwa nafasi yake kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi yao. Alisema mbali na Watanzania hao kuwekeza kwao kama uwezo wanao, pia wanaweza kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii kwa ajili ya kuchangia fursa hiyo ya watalii inayolipa duniani kote.
Kikao kinaendelea.
Kikao kinaendelea.

“Tukitoka hapa kila mmoja awe balozi shupavu wa kuitangaza nchi yetu ya Tanzania ili pamoja na mambo mengine, tuwe tumechangia ukuzaji wa uchumi wetu kulingana na uwezo wetu kwa kupitia sekta nyeti ya utalii, ambapo pia kama sehemu ya serikali nilisikiliza maoni na ushauri wao ili tusonge mbele..

“Tuonyeshe mazuri ya nchi yetu pamoja na sisi wenyewe kushiriki katika fursa za kiuchumi kuliko kusubiri wengine wafanye wakati tunajua fika kuwa kila mmoja ana wajibu wa kuiletea maendeleo nchi yetu,” alisema Balozi Mgaza.

Kabla ya kikao hicho na Watanzania, Balozi Mgaza pia alifanya mazungumzo na Waziri anayeshughulikia Masuala ya Hijja na Umrah wa Serikali ya Saudi Arabia, Mhe. Dr. Mohammed Saleh Bin Taher Benten.

Katika kikao hicho kilichofanyika ofisini kwa waziri huyo, H.E Mgaza alijadiliana na Dr. Benten masuala mbalimbali yanayohusu maandalizi ya ibada ya Hijja ya mwaka 2017 na fursa kwa mahujaji wa Tanzania.

POLEPOLE AKUTANA NA MAOFISA WAANDAMIZI WA UBALOZI WA MAREKANI, LEO

$
0
0
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole akizungumza na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uchumi na Siasa katika Ubalozi wa Marekani hapa nchini, Marilyn Gayton (kushoto), Katika Ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo Janauari 24, 2017. Wapili kulia ni Ofisa Habari wa Ubalozi huo, Lauren Ladenson. Wanaotazama Kamera ni Maofisa Waandamizi kutoka Idara za Siasa na Ushirikiano wa Kimataifa na Idara ya Itikadi na Uenezi
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole akifafanua jambo wakati akizungumza na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uchumi na Siasa katika Ubalozi wa Marekani hapa nchini, Marilyn Gayton (kulia), Katika Ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Wapili kulia) ni Ofisa Habari wa Ubalozi huo, Lauren Ladenson.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole akifafanua jambo wakati akizungumza na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uchumi na Siasa katika Ubalozi wa Marekani hapa nchini, Marilyn Gayton, Katika Ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. 
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole akifafanua jambo wakati wa mazungumzo hayo. 
 Mazungumzo yakiendelea.

MCHEKESHAJI CHAKU MASTER ATOA USHAURI KWA TIMU ZINAZOSHIRIKI KOMBE LA AZAM SPORT FEDERATION (FA CUP).

$
0
0

Mchekaji wa Mjini Songea mkoani Ruvuma Chaku Master, amezitaka timu ambazo zinashiriki kombe la Azam Sport Federation (FA CUP ) hasa zile ambazo hazipo ligi kuu Tanzania bara, kukaza katika michezo hiyo ili ziweze kutwa ubinga wa FA CUP na sio kuwa wasindikizaji ama kukaa na kusema kombe hilo ni la timu kubwa tu, huku akitolea mfano wa mchezo wa mwaka jana kati ya Yanga na JKT Mlale ambayo yanga ilipata ushindi kwa tabu zaidi. Hii hapa video yake.

WANAHABARI WATEMBELEA SHAMBA LA ZABIBU KITUO CHA UTAFITI WA KILIMO MAKUTUPORA DODOMA

$
0
0
 Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo na Maendeleo Kanda ya Kati, Leon Mroso (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari wakati walipotembelea shamba la utafiti wa zabibu katika Kituo cha Utafiti  wa Kilimo Makutupora mkoani Dodoma leo.
 safari kuelekea shamba la zabibu ikiendelea.
 Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo na Maendeleo Kanda ya Kati, Leon Mroso (katikati), akitoa ufafanuzi wa kilimo cha zabibu kwa wanahabari. Kushoto Mtafiti Msaidizi wa kituo hicho, Richard Malle na kulia ni Mtafiti Andekelile Mwamahonje.
 Wanahabari wakiwa katika shamba hilo.
 Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo na Maendeleo Kanda ya Kati, Leon Mroso (kushoto), akionesha mche wa zabibu uliostawi vizuri.
 Wanahabari wakiangalia shamba hilo.
Mtafiti Msaidizi wa kituo hicho, Richard Malle akitoa ufafanuzi wa kilimo cha zao la zabibu kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)
Na Dotto Mwaibale, Dodoma

VIJANA wametakiwa wajiunge kwenye vikundi na kuanzisha mashamba ya kilimo cha zabibu ili wajipatie kipato badala ya kukaa vijiweni.

Mwito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo na Maendeleo Kanda ya Kati Dodoma, Leon Mroso wakati akizungumza na wanahabari waliotembelea shamba la zabibu katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mkoani Dodoma leo.

"Mwito wangu kwa vijana waanzishe vikundi vitakavyoweza kuwasaidia kuanzisha mashamba ya zabibu ili wajiongezee kipato mikopo ya kuwezeshwa ipo" alisema Mroso.

Alisema mtaji wa kuanzisha shamba la zabibu ni kuanzia sh. milioni tatu hadi nne ambapo baada ya miaka mitatu au minne mkulima anaanza kunufaika na kilimo hicho.

Alisema katika kuinua pato la taifa na la mtu mmoja mmoja serikali imeaanzisha mashamba ya zabibu maeneo mbalimbali mkoani humo ambapo katika Halmshauri ya Wilaya ya Chamwino kuna shamba la ekari 296, katika Kijiji cha Kamaiti wilayani Bahi kuna shamba la ekari 170 na Manispaa ya Dodoma katika Kijiji cha Gawaye kuna ekari 100 ambapo kila mwananchi hasa vijana wamepatiwa ekari moja kuziendeleza.

Alitaja aina za zabibu zinazolimwa katika maeneo hayo kuwa ni za mezani, mvinyo na kukausha ambazo soko lake linapatikana wakati wote.

SAUTI ZA BUSARA KUANZA KURINDIMA FEBRUARI 912 MJI MKONGWE ZANZIBAR

$
0
0
Mwenyekiti wa Bodi wa Sauti za Busara,Simai Said akitoa ufafanuzi na namna tamasha hilo litakavyokuwa siku hiyo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani),ambapo ameeleza kuwa tamasha hilo ambalo limekuwa likiwajumuisha makundi,washabiki na wapenzi mbalimbali litabeba kauli mbiu itakayojulikana #AfricaUnited.Kulia ni ni Balozi Balozi wa Norway nchini Tanzania, Hanne – Marie Kaarstad .

Balozi wa Norway nchini Tanzania, Hanne – Marie Kaarstad (pichani kulia) akizungumza mbele ya Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar,kuhusiana na udhamini wao katika tamasha la Sauti za Busara linalotarajiwa kuanza kurindima Februari 9-12 mjini Ngome Kongwe,Zanzibar,Balozi huyo pia amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza kulidhamini tamasha hilo ambalo limekua likiibua vipaji mbalimbali na kivitangaza nchini na ulimwengu kwa ujumla,Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi wa Sauti za Busara,Simai Said,Mkurugenzi wa tamasha hilo Yusuph Mahmoud pamoja na Meneja wa tamasha hilo,Journey Ramadhan.
Mkurugenzi wa tamasha la Sauti za Busara,Yusuph Mahmoud akielezea mambo mbalimbali yatakayojiri ndani ya tamasha hilo,Simai alieleza kuwa tamasha hilo Wasanii watatumbuiza LIVE kwa asilimia 100.
Viongozi wa tamasha la Sauti za Busara wakizungumza na Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar. 

Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii.

VIKUNDI 40 vyenye wasanii 400 vinatarajiwa kutumbuiza Tamasha la Sauti za Busara linalotarajia kuanza kuridima Februari 9 -12 katika Ukumbi wa Mji Mkongwe Mjini Zanzibar .

Akizungmza na waandshi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Sauti za Busara, Simai Said amesema kuwa tamasha limekuwa likitangaza Tanzania pamoja na kuwaweka Waafrika sehemu moja.

Simai ameiomba Serikali kuunga mkono Sauti za Busara kutokana na kazi kubwa inayofanyika katika kuongezea uchumi wa nchi pamoja na kupata watalii wengi wakati tamasha hilo linapofanyika. Amesema kutokana na Tamasha hilo kuwa na vitu vingi vya kiubunifu imesaidia kuongeza ajira kwa vijana katika pande zote kutokana na kuutumia utamaduni wa Tanzania.

“Sauti za Busara limebakiza siku chache kufanyika pale Mji Mkongwe, Zanzibar 9-12/Februari kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa tamasha la Sauti za Busara lenye kauli mbiu ya ‘AfricaUnited’ mwaka huu tamasha litakua na majukwaa matatu yatakayotumiwa na wasanii wote kimataifa/nyumbani”amesema Simai.

Amesema Watu mbalimbali wenye rangi tofauti, umri tofauti kwa mara nyingine tena wataunganishwa na tamasha kusheherekea muziki wa Ki-Afrika kwa kuwa na matarajio ya mahudhurio ni makubwa kutoka Tanzania na nje ya Nchi kufatia kujaa kwa sehemu za malazi Mji Mkongwe kwa wiki ya tamasha. Wasanii wote watatumbuiza ‘live’ muziki wa Ki-Afrika kila siku kuanzia saa 10:30 jioni mpaka saa 7:00 usiku.Simai amesema tamasha ni kuhakikisha kila mmoja anamudu kiingilio hivyo kwa watanznaia ni Sh 6,000 kwa siku na Sh 20,000 kwa siku nne za tamasha.

Tamasha litakutanisha wanamuziki kutoka sehemu mbali mbali ambapo wanamuziki wa Tanzania watashirikiana na wa Morcco, kutakua na mwanya wa kufahamiana zaidi kupitia vikao vya Movers and Shakers, na hafla itakayofanyika usiku wa wapendanao baada ya tamasha.

Nae Mkurugenzi wa Tamasha hilo, Yusuf Mahmoud amesema tamasha hili ambalo kwa asilimia 100 huwa live kitu ambacho kinalifanya tamasha hili liwe la kipekee huwapakipaumbele wanamuziki chipukizi kutambulisha kazi zao zenye kutambulisha uhalisia wa utamaduni.

Amesema Tamasha la Sauti za Busara hukutanisha wataalamu wa muziki wa kimataifa na kutoa nafasi kw amuziki wa Afrika Mashariki kufwakifikia watu mbalimbali dunia nzima kupitia jukwaa la Sauti za wanamuziki wa nyumbani amabao hutumbuiza tamashani hupata mialiko kushiriki matamasha mbali mbali Barani Ulaya na Afrika.

Amesma kati ya makundi 40 nusu yanatoka Tanzania. Makundi hayo ni Afrijam Band, CAC Fusion, Chibite Zawose Family, Cocodo African Music Band, Jagwa Music, Matona's G Clef Band, Mswanu Gogo Vibes, Rajab Suleiman & Kithara, Tausi Women's Taarab, Usambara Sanaa Group, Wahapahapa Band, Ze Spirits Band. Tuna hakika makundi kama haya yatawakilisha vema matamasha ya nje endapo yatapata nafasi.

Makundi mengine ni Batimbo Percussion Magique (Burundi), Bob Maghrib (Morocco), Buganda Music Ensemble (Uganda), Grace Barbe (Seychelles), H_art the Band (Kenya), Imena Cultural Troupe (Rwanda), Isau Meneses (Mozambique), Karyna Gomes (Guine Bissau), Kyekyeku (Ghana), Loryzine (Reunion), Madalitso Band (Malawi), Pat Thomas & Kwashibu Area Band (Ghana), Rocky Dawuni (Ghana), Roland Tchakounté (Cameroon), Sahra Halgan Trio (Somaliland), Sami Dan and Zewd Band (Ethiopia), Sarabi (Kenya), Simba & Milton Gulli (Mozambique).

Wadhamini wa Tamasha hilo ni Hotel ya Golden Tulip, Africalia, Chuchu FM Radio, Zanlink and Coastal Aviation Embassy of Germany, Ethiopian Airlines, Ikala Zanzibar Stone Town Lodge, Memories of Zanzibar, Mozeti, Music In Africa, Norwegian Embassy, Pro Helvetia, Swiss Agency for Development & Cooperation (SDC), Tifu TV, na wengine wengi.

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MKURUGENZI WA UNEP

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa UNEP Bw. Erik Solheim ambaye yupo nchini kwa ziara ya siku 2.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa UNEP Bw. Erik Solheim ambaye ameongozana na ujumbe wake kwa ziara ya siku 2 wengine waliohudhuria ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Januari Makamba (kulia) na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Faustine Kamuzora.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. Januari Makamba akifafanua jambo wakati wa mkutano wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mkurugenzi Mkuu wa UNEP Bw. Erik Solheim na ujumbe wake .
Picha ya pamoja

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameliomba Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) kuisaidia Tanzania kukabiliana na tatizo kubwa la uharibifu wa mazingira katika maeneo mbalimbali nchini ambao umepelekea mamia ya ekari za misitu kutoweka kutokana na ukataji wa miti kwa ajili ya kutengeneza mkaa.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema pamoja na Serikali kufanya jitihada kubwa za kukabiliana na tatizo la uharibifu wa mazingira ikiwemo mpango wa upandaji wa miti kote nchini lakini bado msaada na nguvu zaidi inahitajika kutoka shirika la Mazingira la UNEP ili kuongeza kasi ya kukabiliana na tatizo hilo nchini.

Amesema Tanzania ina mahusiano mazuri na ya muda mrefu na Shirika la UNEP ambapo shirika hilo limeweza kuisaidia nchi katika miradi mbalimbali ya kuhifadhi mazingira hivyo mahusiano hayo mazuri ni muhimu yakaja na mbinu bora na nzuri za kuhifadhi mazingira ili kuokoa Taifa lisigeuke jangwa kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira unaoendelea nchini.

Makamu wa Rais pia amehimiza wataalamu wa mazingira wajikite zaidi katika kutoa elimu kwa wananchi watumie nishati mbadala kama gesi na makaa ya mawe ili kudhibiti tatizo kubwa la uharibifu wa mazingira ikiwemo ukataji wa miti kwa ajili ya kutengeneza mkaa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa ERIC SOLHEIM amepongeza jitihada zinazofanywa na Serikali ya kukabiliana na uharibifu wa mazingira na kusisitiza kuwa Shirika hilo litaendelea kushirikiana na Serikali Tanzania katika Uhifadhi wa mazingira nchini.

Mkurugenzi huyo amesema suala la kukabiliana na tatizo la uharibifu wa mazingira sio la Serikali pekee hivyo ni muhimu kwa Serikali kushirikiana ipasavyo na mashirika yasiyo ya kiserikali katika kupambana na tatizo ili kupata suluhu ya kudumu.

Naye, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira January Makamba amesema ujio wa Mkurugenzi Mkuu wa UNEP hapa nchini ni fursa ya kipekee ya kufungua na kuimarisha ukurasa mpya wa mahusiano kati ya Tanzania na UNEP.

Makamba amesema kuwa Serikali imetengeneza programu mpya Tano za mazingira ikiwemo kupunguza matumizi ya mkaa ili kuhifadhi misitu,vyanzo vya maji,kushughulikia taka na kujenga uwezo kama hatua mpya kabisa ya kukabiliana na uharibifu wa mazingira nchini.

YANGA WAIANGUKIA SERIKALI WAOMBA KUUTUMIA UWANJA WA TAIFA

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Uongozi wa klabu ya Yanga  imeandika barua Wizara ya Habari Sanaa na Utamaduni na Michezo kuomba iruhusiwe kuanzia wikiendi hii kutumia Uwanja wa Taifa, badala ya Uhuru mjini Dar es Salaam kwa mechi zake za mashindano ya nyumbani.

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit amesema kuwa wameandika maombi hayo kwa lengo la kuanza kuutumia Uwanja wa Taifa kwa michezo yao ya ligi kuu ili wachezaji waanze kuuzoea kelekea mtanange wao wa  michuano ya Afrika, ambayo watatumia Uwanja wa Taifa.

Kwa sababu hiyo, Baraka alisema wanataka waruhusiwe kuanza kuutumia Uwanja wa Taifa, ili wauzoeee mapema hata mechi zao za michuano ya Afrka itakapoanza wawe tayari.

“Kama unavyojua kwa muda mrefu hatujautumia Uwanja wa wetu huu kipenzi wa Taifa baada ya kuzuiwa na Serikali kufuatia vurugu za kwenye mechi yetu na Simba baada ya mashabiki wa wenzetu kufanya fujo na kuvunja viti,”.

“Lakini tutambue kuwa tuliingia mkataba maalum na Serikali wa kuutumia Uwanja huu kwa mechi za mashindano ya Afrika na ule wa Uhuru kwa Ligi Kuu pekee na  kwa kuwa tunakaribia kuanza mechi za Klabu Bingwa  Afrika tunaiomba Serikali ituruhusu kuhamishia mechi zetu za mashindano ya nyumbani Uwanja wa Taifa, ili iwe sehemu ya maandalizi yetu ya michuano hiyo ya Afrika,”amesema Baraka.

Yanga watashuka dimbani dhidi ya Mwadui  mechi itakayochezwa Januari 29 Jumapili Jijini  Dar es Salaam na Februari 05 wataikaribisha Stand United Februari 5 na kisha kuanza maandalizi kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Ngaya De Mbe.

Februari 10, mwaka huu, Yanga watakuwa wageni wa Ngaya De Mbe kutoka visiwa vya Comoro katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Mde mjini Mde nchini Comoro, kabla ya kurudiana Februari 17, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 Picha ya Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit akikabidhiana mkataba Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel  kwa makubaliano ya kutumia Uwanja wa Taifa kwa ajili ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika.
Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Baraka Deusdedit

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA WAJUMBE WA BARAZA LA TAIFA LA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI

$
0
0
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar es salaam Januari 24, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng'i Issa akitoa taarifa ya Baraza hilo katika kikao kati ya Baraza na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kilichofanyika kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam Januari 24, 2017 
 Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, John Jingu  akitoa maelezo kuhusu Baraza hilo katika kikao kati ya Baraza na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kilichofanyika kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam Januari 24, 2017.
  Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na watumishi wa Baraza hilo wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipozungumza nao kwenye makazi yake , Oysterbay jijini Dar es salaam Januari 24, 2017
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi baada ya kuzungumza nao kwenye makazi yake, Oysterbay  jijini Dar es salaam Januari 24, 2017.

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI)

Kijiji cha Mwanzega kupata umeme wa REA

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, Mkuranga
KIJIJI cha Wasanii cha Mwanzega kimechaguliwa kuwemo kwenye orodha ya vijiji saba ambavyo vimepangiwa kupata umeme wa Serikali wa Mamlaka ya Umeme Vijijini (REA).

Mtendaji wa kijiji cha Mwanzega, Kitwana Kambangwa aliwaomba wanakijiji wasipuuzie fursa hiyo kwa vile serikali imeona umuhimu wa kijiji hicho kupata umeme ili kurahisisha maendeleo.

Akiwasomea wananchi taarifa ya Mratibu wa Vijiji na Kata wa Utawala bora na maboresho wa wilaya ya Mkuranga kuhusu mradi huo, Mtendaji wa kijiji, Kambangwa alisema wananchi wewe tayari kutoa miti yao ya mazao na mimea bila fidia ili kupisha kazi ya kupitisha nguzo za umeme wa REA.

'Ndugu zangu Serikali ya Rais John Magufuli imetusikia kilio chetu sisi watu wa vijijini, tunaletewa umeme ili tuwe na maendeleo kama wenzetu wa mjini, tusiipuzie nafasi hii kubalini kupisha nguzo zipite bila kulalamikia fidia' alisema Mtendaji Kambangwa.

Alisema sambamba na kijiji cha Mwanzega, vijiji vingine vitakavyonufaika na mradi wa REA ni Mbezi, Msorwa, Shungubweni, Boza, Kuruti na Mbonga ambavyo mradi huo utapelekwa moja kwa moja kwenye shule za Msingi, Zahanati, Viwanda na Shule za Sekondari.

Awali wakichangia kuhusu mradi huo Dkt.Frederick Mwakibinga alisema umeme ukishaingia kijijini baada ya muda mfupi kutakuwa na maendeleo ambayo yatawanufaisha wananchi wote na kaongeza ajira kwa vijana.
Mwanakijiji mwingine Ramadhani Mwanehekwa alisema wao wako tayari kuruhusu mazao yao kukatwa bila kudai fidia lakini Serikali nayo iwakumbuke katika kuwaletea wananchi huduma za jamii, kama zahanati, barabara, maji na elimu.

Mkutano huo uliohudhuriwa na wanakijiji wengi waume, wanawake na vijana, Ali Ndambwe aliwashauri wanakijiji wenzake wasifikirie kulipwa  fidia kwa ajili ya mazao zitakapopita nguzo waangalie faida watakayoipata vijana wao na majukuu baada ya kuingia umeme na kujengewa viwanda.

Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA), Cassim Taalib aliwapongeza wanakijiji wenzake kukubali kutoa mazao na mimea yao bure kwa wale ambao mradi wa umeme utawapitia.

Katika mkutano huo Mwenyekiti wa kijiji, Abdallah Mwangira aliwataarifu wananchi hao kuwa serikali imewaandalia wananchi wa vijiji hivyo mambo makubwa ya maendeleo ambayo aliahidi kuyasema kikao kijacho.
Kijiji cha Mwanzega ndipo kilipo kijiji cha wasanii ambacho mpaka sasa zimejengwa nyumba 250 za kisasa as wasanii ambazo zitaingia kwenye mradi wa REA.

Mkazi wa Mwanzega Dkt. Frederick Mwakibinga akichangia mada kwa wanakijiji watakaonufaika na mradi huo baada ya kuukubali.
Wanakijiji wa kijiji cha Wasanii Mwanzega Mkuranga wakiwa kwenye mkutano wa kuidhinisha mradi wa Ilene wa REA kupita kijijini hali jana.

TAASISI YA MOYO YAFANYA UPASUAJI WA KUZIBUA MISHIPA YA MOYO ILIYOZIBA KWA ASILIMIA 100 NA KUSHINDWA KUPITISHA DAMU

$
0
0
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Madaktari  Afrika kutoka nchini Marekani kwa mara ya kwanza wamefanya upasuaji wa bila kufungua kifua (Catheterization Procedure) kwa mgonjwa na kuzibua mshipa wa Moyo uliokuwa  imeziba kwa zaidi ya miezi mitatu (kwa lugha ya kitaalamu Chronic Total Occlusion).

Upasuaji huo ambao unatumia mishipa ya damu ulichukuwa muda wa saa moja kwa  kuzibua mshipa mmoja wa damu ambao ulikuwa umeziba kwa asilimia 100 na   kushindwa kupeleka  damu upande wa kushoto wa moyo.

Kambi ya Madakari wa Afrika imeanza tarehe 23/1/2017 na inatarajiwa kumalizika tarehe 29/1/2017. Hadi sasa jumla ya  wagonjwa sita wameshapatiwa huduma za matibabu ya moyo ambayo ni kuzibua mishipa ya moyo iliyokuwa imeziba. Hali za wagonjwa zinaendelea vizuri na wanatarajiwa kuruhusiwa siku yoyote kuanzia kesho.

Tangu kuanza kwa mwaka huu wagonjwa 29  wameshafanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua kati ya wagonjwa hao 23 wamefanyiwa upasuaji katika kambi za ndani na wagonjwa sita wamefanyiwa upasuaji katika kambi ya Madaktari Afrika.

Taasisi inaendelea kuwaomba  Madaktari wote nchini wenye wagonjwa wao wa matatizo ya  moyo wawatume wagonjwa hao katika Taasisi ya Moyo  ili waweze kupatiwa matibabu. Kwa mawasiliano zaidi wawasiliane na Dkt. Peter Kisenge kwa namba 0713 236 502 na  022-2151379 ambaye atawaelekeza utaratibu wa kuwatuma  wagonjwa hao.

Imetolewa na:


Kitengo cha Uhusiano na Masoko
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
24/01/2017

CCM YAWEKA HADHARANI SIRI YA USHINDI WA CHAGUZI ZAKE ZA MADIWANI TANZANIA BARA NA UBUNGE ZANZIBAR

$
0
0
Katibu wa Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole akifafanua mambo mbalimbali mapema leo kwenye Ofisi ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam,kuhusiana na ushindi wa chama cha Mapinduzi (CCM) katika chaguzi mbalimbali zilizofanyika hivi karibuni,za Madiwani na nafasi ya Ubunge huko Zanzibar.

Katika mkutano huo na Waandishi wa Habari, alielezea siri tatu muhimu zilizokiwezesha Chama hicho kupata ushindi, Polepole alizitaja siri ya kwanza ni namna ya mageuzi mapya ya kimuundo na mfumo yaliyolenga kukiwezesha CCM kurudi kwenye mikono ya wananchi kwa serikali yake kujikita zaidi kushughulikia kero zinazowakabili Watanzania na kufanikiwa.

Pole Pole alisema kuwa mabadiliko hayo yamelenga kukirejesha chama wenye misingi uliokifanya kuanzishwa kwake,akabainisha siri ya pili kuwa ushindi huo ni matokeo ya mafanikio ya serikali katika kuweka mikakati ya kubana mianya ya wakwepa kodi pamoja na vita dhidi ya ufisadi.

“Adui yetu mkubwa ni rushwa na vitendo vya ufisadi nchini, Watanzania ni mashahidi kwani muelekeo wa serikali umekuwa thabiti na tumeona watuhumiwa wa vitendo hivyo wakichukuliwa hatua,” alisema.Alisema kuwa siri ya tatu imetokana na kazi nzuri ya utendajikazi wa serikali kwenye utekelezaji wa ahadi zilizotolewa na Chama.
Baadhi ya Wanahabari wakimsikiliza Ndugu Pole Pole alipozungumza nao mapema leo jijini Dar.Picha na Michuzi Jr.

Katika hatua nyingine,Pole Pole alisema kuwa ahadi ya kutoa elimu bure kwa wanafunzi kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha nne, imekuwa na uhalisia mkubwa.“Na zaidi ya yote ni huduma za kiuchumi ambazo zimeendelea kutekelezwa ambapo Chama tunaipongeza serikali na kuikumbusha katika maeneo mengine tuliyowaahidi wananchi, ikiwemo kuendelea kutenga asimilia 10 ya mapato ya Halmashauri kwa ajili ya vijana na wanawake.

“Hii itatoa nafasi kwa vijana na wanawake kupata fursa za mitaji na mikopo yenye masharti nafuu, hivyo suala hilo linapaswa kuwekewa msisitizo zaidi,” aliongeza.Alisema serikali inaendelea na mipango ya ujenzi wa viwanda, vinu vya usagaji mkoani Iringa na Mwanza pamoja na kiwanda cha mafuta ya Alizeti, mambo ambayo tayari Chama kimetoa maelekezo kwa serikali.

Akaongeza kuwa , ununuzi wa ndege kwa ajili ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) umesaidia kuwawezesha wananchi kusafiri kwenye maeneo mbalimbali katika kufanya shughuli muhimu za kiuchumi.

Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeibuka na ushindi mnene katika uchaguzi mdogo wa marudio ya ubunge Jimbo la Diwani na udiwani kwenye kata 20 za Tanzania Bara, Katika uchaguzi huo, kwenye jimbo la Dimani, mgombea wa CCM, Juma Ally Juma, alipata ushindi wa kura 4,860 sawa na asilimia 78.74 dhidi ya mpinzani wake, Abdulrazak Khatib Ramadhan wa CUF, aliyepata kura 1,234.

Ushindi huo umedhihirisha anguko kubwa la CUF, visiwani Zanzibar kwani uchaguzi wa mwaka 2015 licha ya kushika nafasi ya pili, kilipata wastani wa kura 2,300 lakini kwenye uchaguzi wa marudio kura zake zimeshuka kwa zaidi ya asilimia 50.Hivyo ili kujinusuru na hali hiyo, CUF kimetakiwa kumtafuta mchawi aliyepo ndani ya chama hicho visiwani Zanzibar na si kulalamika. 

Aidha CCM imejizolea viti 19 vya udiwani kati ya 20 huku Chadema ikipata kiti kimoja na kufanya Chama kudhihirisha kuwa, bado kinakubalika kwa wananchi.Kufuatia ushindi huo, Chama kimewataka wanachama kurudisha fadhira za ushindi huo kwa wananchi kwa kuwachagulia viongozi wenye mioyo za kizalendo, wachapakazi waliokuwa tayari kuwasikiliza wananchi, katika uchaguzi wa ndani unaofanyika mwaka huu.

CHAKUA YAIOMBA SERIKALI KUKAZIA MATUMIZI YA MFUMO WA ELECTRONICS SEKTA YA USAFIRISHAJI

$
0
0
Na: Lilian Lundo – MAELEZO

Chama cha Kutetea Abiria Tanzania (CHAKUA) kimeiomba Serikali kuongeza nguvu na kuhakikisha matumizi ya tiketi za elekroniki katika sekta ya usafirishaji nchini yanakuwa ya lazima.

Hayo yamesemwa na Afisa Msimamizi wa Chama hicho ambaye anasimamia Mkoa wa Dar es Salaam Mark Serra, alipokuwa akisoma taarifa ya chama hicho kwa waandishi wa habari leo, Jijini Dar es Salaam.

“Chakua imekuwa ikifuatilia kwa karibu mfumo huu na kubaini una manufaa makubwa sana kwa abiria ambapo watatozwa nauli halali iliyoidhinishwa na Sumatra ambazo ndizo bei elekezi kwa mujibu wa sheria,” alifafanua Serra.

Aliendele kusema kuwa kwa kutumia tiketi za Kielekroniki itawalazimu wamiliki wa vyombo vya usafiri kutokupandisha nauli katika kipindi cha mvua au jua kali, kipindi cha wanafunzi wapotoka vyuoni au mashuleni pamoja na kipindi cha sikukuu au mwanzoni mwa mwaka, ambapo mabasi mengi huita vipindi hivyo ni vya kuvuna abiria.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama hicho Hassan Mchanjama amesema kuwa mfumo huo utamnufaisha abiria na kuokoa muda wa kwenda kwenye vituo vya mabasi kwa ajili ya kukata tiketi badala yake mfumo huu utamuwezesha abiria kukata tiketi akiwa nyumbani, ofisini au sehemu yoyote aliyopo kwa kutumia simu yake ya mkononi.

Aliongeza kuwa mfumo huo utarahisisha upatikanaji wa taarifa muhimu za abiria pindi inapotokea ajali kujua abiria wangapi wamepoteza maisha, waliopata ulemavu pamoja na waliopoteza mali zao, ambapo kwa mfumo unaotumika sasa hivi ni vigumu kupata takwimu na taarifa sahihi za abiria.

Hivyo basi kupitia mfumo huo wa kielekroniki CHAKUA itakuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kutekeleza jukumu lake la kumtetea abiria pindi anapopata tatizo kwa kuwa itakuwa na taarifa sahihi za abiria.
Viewing all 46314 articles
Browse latest View live




Latest Images