Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1111 | 1112 | (Page 1113) | 1114 | 1115 | .... | 1898 | newer

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema katika mwaka huu wa fedha Serikali imetenga sh. bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Njombe-Makete yenye urefu wa kilomita 109.4 kwa kiwango cha lami.

  Ametoa kauli hiyo jana  (Ijumaa, Januari 20, 2017) wakati akizungumza na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete alipowasili katika kata ya Mtamba wilayani hapa akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Njombe.

  Waziri Mkuu amesema usanifu wa kina wa barabara ya Njombe-Makete kwa ujenzi wa kiwango cha lami umekamilika hivyo amewataka wananchi waendelee kuwa na subira.

  Amesema barabara nyingine inayotarajiwa kujengwa ni ya kutoka Makete hadi Mbeya kupitia Isyonji yenye urefu wa kilomita 96 ambayo imetengewa sh. milioni 50 kwa ajili ya kufanyiwa usanifu.

  Waziri Mkuu amesema wananchi waendelee kushirikiana na Serikali kwani imedhamiria kuwatumikia kwa kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili katika maeneo yao.

  Aidha, Waziri Mkuu amewataka wahandisi wa wilaya hiyo kuhakikisha wanawasimamia vizuri wakandarasi wanaojenga miradi mbalimbali katika halmashauri zao kuhakikisha kama viwango vinalingana na thamani halisi ya fedha zinazotolewa.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliwataka wakuu wa Idara katika halmashauri kupambana na vitendo vya rushwa na wahakikishe watumishi hawatowi huduma kwa kuomba rushwa.

  “Kwanza watumishi watambue kwamba rushwa ni dhambi. Pia kiutumishi ni makosa makubwa hivyo wajiepushe na vitemdo hivyo,” amesema.

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Makete Bi. Veronica Kessy amesema kujengwa kwa barabara hizo kwa kiwango cha lami kutaimarisha ukuaji wa uchumi wa wilaya hiyo na Mkoa wa Njombe kiujumla hivyo wananchi kupata tija.

  “Mfano barabara ya kutoka Makete hadi Mbeya kupitia Bulongwa, Iniho, Kikondo na Isyonje itasaidia wilaya kufunguka hivyo kurahisisha usafirishaji wa mazao ya misitu kama mbao,” amesema.

  Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya amesema barabara hii pia itaunganisha Wilaya hiyo na kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Songwe hivyo watapata fursa ya kuanzisha kilimo cha maua. Awali walishindwa kulima maua kwa sababu hakukuwa na usafiri wa uhakika.

  Awali Waziri Mkuu alitembelea shamba la mifugo la Kitulo linalomilikiwa na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi lenye jumla ya Ng’ombe 750 wakiwemo ndama 61, majike 212, mitamba 273, madume 21, na madume wadogo 183.

  Shamba hilo linazalisha wastani wa lita 450,000 za maziwa kwa mwaka kutokana na ng’ombe 123 wanaokamuliwa. 

  (Mwisho)

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMAMOSI, JANUARI 21, 2017.


  0 0

  NA HASSAN SILAYO-MAELEZO.

  Mkoa wa Mara ni Moja ya Mikoa ambayo kwa kiasi kikubwa imekuwa ikiendelea na utamaduni wa kukeketa watoto wa kike jambo ambalo ni kinyume na haki za mtoto na sheria mbalimbali duniani.

  Kila mwaka takribani watoto milioni mbili wako katika hatari ya kukeketwa ambako kwasasa Tanzania ina asilimia 32 ya hali ya ukeketaji suala ambalo Serikali hairidhiki nalo.

  Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga alifanya ziara ya siku 2 Mkoani Mara katika Wilaya za Tarime na Musoma.

  Katika ziara hiyo Bi. Sihaba ambayo alimuwakilisha Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katika mahafali ya 9 ya Kituo cha kulea watoto waliokimbia ukeketaji cha Masanga (ATFGM) katika kata ya Masanga Tarime Vijijini.

  Katika hotuba yake Katibu Mkuu Bi. Sihaba alionesha kushangazwa na vitendo vya ukeketaji vinavyofanywa na wenyeji wa Mkoa wa Mara na kuviita ni vitendo vya kikatili dhidi ya watoto wa kike, kwani inakatisha ndoto na matarajio ya watoto hao.

  Akitoa kauli ya Serikali Bi. Sihaba alisema kuwa Serikali itawachukulia hatua kali za kisheria watakaogundulika kuendeleza vitendo vya ukeketaji kwani ni kinyume na Sheria ya Nchi na nikinyume na mikataba mbalimbali ya Kimataifa iliyojielekeza katika kulinda haki mbalimbali za mtoto.

  Akionesha kudhamiria kukabiliana na tatizo la ukeketaji katika mkoa wa Mara Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga alikutana na Wazee wa kimila kutoka Koo tano za Bukenye, Nyabasi, Bukira, Butimbaru, Buhunyaga.

  Katika mazungumzo hayo yaliyolenga kuweka mikakati ya kukomesha tamaduni ya ukeketaji mkoani Mara, Mzee wa kimila kutoka Koo ya Bukenye Mzee Elias Maganya alisema kuwa walishapata elimu kutoka kwenye Jukwaa la Kulinda Utu wa watoto(CDF) na changamoto ni jinsi ya kuzifikia koo nyingine Mkoani huko ili kuwezesha kuondoa kabisa mila hiyo.

  Mzee Elias alisema kuwa sasa ni jukumu la Serikali kuona umuhimu wa kuwawezesha kutembea Koo hadi Koo kwa ajili ya kuelimisha jamii kuhusu madhara ya ukeketaji.

  Naye Mzee wa Kimila kutoka Koo ya Bukira Mzee Sinda Nyangore ameishauri Serikali na mashirika mengine kutoa elimu katika vipindi vyote vya mwaka na kuacha utaratibu wa kutoa elimu katika msimu wa ukeketaji kwenye koo mbalimbali.

  Aidha,Mzee kutoka koo ya Butimbaru Mwita Nyasibora alishauri mpango wa kutoa elimu kwa jamii kuhusu madhara ya ukeketaji yafanyika kwa wakati wote badala ya kusubiri kipindi cha ukeketaji ndipo serikali na asasi nyingine za kiraia kujitokeza kutoa elimu.

  Akijibu hoja hizo Bi. Sihaba Nkinga amesema kuwa, kweli upo umuhimu wa kutekeleza suala hilo la kupeleka elimu juu ya madhara ya ukeketaji ili kuweza kuwasaidia watoto wakike katika koo hadi koo kwani tofauti na hapo lengo kusudiwa haliwezi kufikiwa na itakuwa ni tofauti na malengo ya serikali katika kupambana na tamaduni ya ukeketaji.

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tarime Bw. Glorius Luoga katika hotuba yake aliyoitoa katika mahafali hayo, aliyataja majina ya mangariba maarufu ambao wanatafutwa na vyombo vya dola kwa vitendo vya ukeketaji katika maeneo mbalimbali wilayani Tarime.

  Mkuu wa Wilaya huyo pia, alisema ofisi yake imeshawapeleka katika vyombo vya Sheria baadhi ya watu wanaojihusisha na vitendo vya ukeketaji na kuahidi kuendelea kuwachukulia hatua kali za Kisheria wale watakaoendelea na vitendo hivyo vya ukeketaji.

  Aidha, Bw. Luoga alioneshwa kuchukizwa na aina ya wazazi na walezi wanaolazimisha kuwatahiri watoto wa kiume kwa mara ya pili baada ya tohara salama kwani kitendo hicho ni sawa na kumjeruhi mtoto.

  Akiongea na wahitimu, wazazi, walezi na mangariba wastaafu, Mkuu wa Wilaya ya Bunda Bi. Lydia Bupilipili alisema, wazazi na walezi wanapaswa kuona umuhimu wa kuwapeleka watoto wa kike shuleni ili waweze kutimiza ndoto walizojiwekea katika maisha yao.

  Akiongea mbele ya Mkurugenzi wa Kituo cha Kulea Watoto waliokimbia Kukeketwa cha (ATFGM-Massanga) Sister Stella Mgaya aliishukuru Serikali ya Wilaya na Wizara ya Afya kupitia Maafisa Maendeleo ya Jamii kwa ushirikiano wanaoupata pale wanapohitaji.

  Aidha, Sister Stella Mgaya alisema kuwa kituo hicho kimekuwa kikikumbwa na changamoto nyingi ikiwemo kuwa na idadi kubwa ya watoto kituoni hapo baada wanaokataliwa na wazazi/walezi pindi wanapotoka kituoni hapo hivyo kuongeza gharama ya kuwapeleka shuleni, Sister Mgaya

  Wakisoma risala kwa mgeni rasmi wahitimu wa kituo cha kulea watoto cha masanga walitoa maombi yafuatayo kwa Katibu Mkuu Bi. Sihaba Nkinga waliomba kuendelezwa kielimu pindi wanapomaliza kituoni hapo wakati mwingine wanakataliwa na kutengwa na wazazi/walezi wao.

  Aidha, Watoto hao waliiomba pia serikali kukamata wazazi/walezi wanaowalazimisha kukeketwa pindi wanapotoka kituoni hapo na kuendelea na kuutilia mkazo utaratibu wa kuchukuliwa hatua kali za kisheria kwa wazazi,walezi na mangariba wanaojihusisha na kazi ya ukeketaji ikiwemo kifungo cha miaka 5-10 jela.

  Rai yangu kwa watanzania na hasa makabila yanayoendeleza mila ya ukeketaji wa watoto wa kike ni kuacha tamaduni hii ambayo ni kinyume na sheria za nchi na hata mikataba mbalimbali ya kimataifa inayolenga kumlinda mtoto wa kike. Pia ni muda wa kujikita katika kumuendeleza mtoto wa kike kielimu ili waweze kutimiza malengo na ndoto walizojiwekea kwani “Tanzania Bila ukeketaji inawezekana”
  MWISHO.

  0 0  0 0  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Laptop Mwandishi Chipukizi wa Vitabu vya Taaluma, Ali Salum Alujai ukiwa ni msaada aliompatia ili aweze kufanya vizuri zaidi katika uandishi wake. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Ikulu ndogo ya Njombe.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


  MAJALIWA:SERIKALI IMEANZA KULIPA MADENI YA WATUMISHI
  *Jumla ya sh. bilioni 29 zililipwa mwaka jana

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imelipa jumla ya sh. bilioni 29 kwa watumishi mbalimbali wa umma wakiwemo walimu ikiwa ni sehemu ya madeni yao.

  Alitoa kauli hiyo jana (Jumamosi, Januari 21, 2017) wakati akizindua vyumba vitatu vya kisasa vya madarasa katika shule ya sekondari Iwawa iliyoko wilayani Makete.

  Waziri Mkuu alisema Serikali imedhamiria kumaliza madeni ya watumishi hao, ambapo hadi kufikia Novemba mwaka jana jumla sh. bilioni 29 zililipwa kwa watumishi 31,000.

  Alisema kwa sasa Serikali imejipanga kuhakikisha hakuna madeni mapya yanayozalishwa hivyo amewataka watumishi wa umma na wananchi kuendelea kuiunga mkono Serikali.

  Hata hivyo alisema Serikali inaendelea na mikakati ya kuboresha sekta ya elimu kwa kujenga mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia.

  “Tumeanza mradi wa ujenzi wa nyumba za walimu katika halmashauri nchini. Hapa Makete tumeleta sh. milioni 557 kwa ajili ya ujenzi huo,” alisema.

  Alisema nyumba hizo za walimu zinazojengwa katika maeneo mbalimbali hususan ya vijijini ni za kisasa ambazo zinalenga kuwaondolea changamoto ya makazi.

  Waziri Mkuu alisema Serikali inafanya jitihada za dhati za kuhakikisha kila Mtanzania anapata elimu kwa kuwa elimu ni kichocheo cha maendeleo ya jamii.

  “Tumedhamiria kumpatia elimu kila Mtanzania, hivyo halmashauri zihakikishe kila kijiji kinakuwa na shule ya msingi na lazima ziwe na darasa la awali,” alisema.

  Naye Mkuu wa Shule hiyo, Mwalimu Novatus Msivala aliishukuru Serikali kwa kugharamia ujenzi wa vyumba hivyo vitatu vya madarasa na matundu 10 ya vyoo pamoja na uingizaji wa maji kwenye vyoo na utengenezaji wa madawati 46.

  Alisema ujenzi huo umegharimu sh. milioni 95 ambao utasaidia kupunguza msongamano kwa wanafunzi. Kwa sasa Serikali na wananchi wanaendelea kukamilisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi ya walimu.
                          
  Katika hatua nyingine jana Waziri Mkuu alitimiza ahadi yake ya kumpatia laptop mwanafunzi Ally Alijai wa Chuo kikuu cha SAUT tawi la Songea mkoani Ruvuma.

  Ahadi hiyo aliitoa mwanzoni mwa mwezi huu alipokuwa katika ziara yake kikazi mkoani Ruvuma, lengo likiwa ni kuendeleza kipaji cha utunzi wa vitabu kwa mwanafunzi huyo.

  Alisema mwanafunzi huyo alionyesha umahiri mkubwa katika utungaji wa kitabu ambacho kinaweza kutumika kufundishia katika shule za sekondari.

  Hata hivyo Waziri Mkuu alisema tayari kitabu hicho kimeshawasilishwa Taasisi ya Elimu Tanzania (TEA) kuona kama kinaweza kuanza kutumika kwa kufundishia. Mwanafunzi huyo alishukuru kwa zawadi hiyo na kuahidi kutunga vitabu vizuri zaidi.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMAPILI, JANUARI 22, 2017.


  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua jengo la Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe katika eneo la Igwachanya Januari 17, 2017. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe baada ya kuweka jiwe la msingi la jengo hilo katika eneo la Igwachanya , Januari 17, 2017.
   
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha chai cha Kibena wilayani Njombe Januari 21, 2017.
  Waziri Mkuu, Kasisim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa eneo la Igwachanya wilayani Wanging’ombe baada ya kuweka jiwe la msingi la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo Januari 21, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Ilembula wilayani Wanging’ombe Januari 21, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Makamu Mwenyeiti wa CCM (Bara) Philip Mangula baada ya kuwasili kwenye jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe kufungua jengo hilo Januri 21, 2017. Mangula ni mkazi wa eneo hilo.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi na wafanyakazi wa Kiwanda cha Chai cha Kibena wilayani Njombe baada ya kukitembelea Januari 21, 2017.

   
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama ngoma ya wasanii wa eneo la Wikichi wilayani Njombe wakati alipowasili kwenye eneo la Mradi wa Ujenzi wa Hospitali Mpya ya Rufaa ya Mkoa huo, Januari 21, 2017.Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher `Ole Sendeka.  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema jumla ya vijiji 53 vya mkoa wa Njombe vitapatiwa huduma ya maji safi na salama katika mwaka huu wa fedha.

  Alitoa kauli hiyo jana (Jumamosi, Januari 21, 2017) wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya Wanging’ombe katika mkutano wa hadhara katika kata ya Ilembula.

  Waziri Mkuu alisema zaidi ya sh. bilioni 2.4 zimetengwa kwa ajili ya kugharamia mradi huo wa maji katika miji ya Makambako, Njombe na wilaya ya Wanging’ombe.Alisema kati ya vijiji hivyo vitakavyopatiwa maji, vijiji 22 ni vya wilaya ya Wanging’ombe, hivyo aliwaomba wananchi hao kuwa na subira.

  Kwa mujibu wa Waziri Mkuu tayari zabuni ya mradi huo imeshatangazwa, hivyo amewaagiza viongozi wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji watafute mkandarasi mzuri.Alisema lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma ya maji katika umbali usiozidi mita 400 kutoka mahali anapoishi.

  Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo baada ya Mbunge wa Wanging’ombe, Mheshimiwa Mhandisi Gerson Lwenge kumuomba awasaidie katika kutatua kero ya maji.Mbunge huyo ambaye pia ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji alisema “Mheshimiwa Waziri Mkuu sisi tunakabiliwa na changamoto ya maji, leo tunaomba ututatulie kero hii”.

  Changamoto nyingine aliyoitaja Mheshimiwa Lwenge ni pamoja na ukosefu wa hospitali ya wilaya, ambapo Waziri Mkuu aliigiza halmashauri hiyo kuanza ujenzi.Alisema Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 inaelekeza kuwa na hospitali katika kila wilaya, kituo cha afya kwa kila kata na zahanati kwa kila kijiji.

  Katika hatua nyingine Waziri Mkuu alimuagiza Mkuu wa Wilaya hiyo Bw. Ally Kasinge kukutana na viongozi wa kata na vijiji vinavyozunguka hifadhi ya Mapanga Kipengele ili kutatua kero ya mpaka.
                     

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMAPILI, JANUARI 22, 2017.
                                        

  0 0


  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (Kushoto), akiwa na Mbunge Mteule, Profesa Palamagamba Kabudi na Waziri wa zamani, Omari Nundu, walipokutana jana, Januari 21, 2017, kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA). (Picha na Bashir Nkoromo).


  0 0

   Watafiti wakiwa lango kuu la kuingia katika  shamba la jaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni (GMO), chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma. Watafiti hao walikuwa wameongoza na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Charles Tizeba kutembelea shamba hilo.
   Mshauri wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAM), Dk. Nicholaus Nyange (kulia), akitoa mada ya matumizi ya Bioteknolojia ya kisasa katika sekta ya kilimo mbele ya Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Charles Tizeba mjini Dodoma.
   Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk.Hassan Mshinda (kulia), akitoa maelezo mbele ya Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Charles Tizeba (wa pili kushoto), alipotembelea shamba la jaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni (GMO) lililo chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma juzi. 
   Msafara ukielekea kwenye shamba hilo la majaribio.
   Waziri Tizeba (wa sita kutoka kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na watafiti wa kilimo mbele ya shamba hilo la majaribio ya mbegu za mahindi katika kituo cha kilimo cha Makutupora mkoani Dodoma.
  Watafiti na Waziri Tizeba wakijadiliana mbele ya shamba hilo.

  Na Dotto Mwaibale, Dodoma

  MATUMIZI ya Bioteknolojia ya Kisasa katika Sekta ya Kilimo nchini yataleta mafanikio makubwa kwa wakulima na taifa kwa ujumla.

  Hayo yalielezwa na Mshauri wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAM), Dk. Nicholaus Nyange wakati akitoa taarifa kwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Charles Tizeba alipotembelea shamba la jaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma. 

  "Matumizi ya Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo Tanzania ni muhimu hasa katika kipindi hiki ambacho maeneo mengi ya nchi yanakabiliwa na ukame kutokana na tabia nchi" alisema Dk.Nyange.

  Alisema taaluma ya uhandisi jeni inawezesha kuhamisha jeni kutoka kwa kiumbe hai kimoja na kuingiza katika kiumbe hai kingine ili kupata sifa lengwa na kutengeneza bidhaa kwa matumizi mbalimbali.

  Akizungumzia kuhusu usalama wa matumizi ya Bioteknolojia hapa nchini alisema ni vema kuanza mchakato wa kuendeleza mazao yaliyofanyiwa mabadiliko ya kijenetiki (GMO) ambayo yameleta mafanikio makubwa katika nchi nyingine kwa mfano mahindi yanayostahimili ukame na bungua muhogo unaostahimili ugonjwa wa batobato na michirizi kahawia, migomba yenye ukinzani dhidi ya ugonjwa wa mnyauko na pamba yenye ukinzani kwa wadudu waharibifu.

  Dk. Nyange alisema Changamoto kubwa iliyopo katika matumizi ya teknolojia hiyo ni kuongezeka kwa upotoshaji kutoka kwa wanaharakati na wapinzani kutokana na ufahamu na uelewa wa watafiti, viongozi, wanasiasa na umma kwa jumla kuhusu masuala ya taaluma hiyo kuwa  bado ni mdogo ukiwemo uwekezaji mdogo katika utafiti na maendeleo.

  0 0

  Waimbaji wa Kwaya ya Kanisa la EAGT Kaangaye kutoka Nyakato Jijini Mwanza, leo wamefanyika Baraka kubwa baada ya kuhudumu vyema katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu la Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza.

  Waumini wengi wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya wamefurahishwa na huduma ya kwaya hiyo. Pongezi kubwa ziwaendee Mwenyekiti wa kwanya hiyo, Abednego Magesa na Mchungaji Samson Mniko kwa malezi mema yaliyofanikisha wanakwaya hao kumtumikia Mungu kwa bidii kubwa.
  Na Binagi Media Group
  Waimbaji wa Kwaya ya Kanisa la EAGT Kaangaye lililopo Nyakato Jijini Mwanza, wakihudumu kwa bashasha kubwa kwenye ibada za hii leo jumapili katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza
  Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, Dkt.Daniel Moses Kulola, akisisitiza jambo kwenye ibada za hii leo jumapili. Ibada ya kwanza kila jumapili huanza saa 12:00 asubuhi, ibada ya pili saa 01:00 asubuhi na ibada ya tatu saa 04:30 asubuhi.
  Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza, wakimsikiliza Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo, Dkt.Daniel Moses Kulola
  Waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza, wakifuatilia ibada za leo jumapli
  Mahubiri na Mafundisho ya neno la Mungu kutoka Kanisa la EAGT Lumala Mpya pia yanarushwa kupitia runinga ya Star Religion inayopatikana kwenye kisimbuzi cha Continental ambapo visimbuzi hivyo vinapatikana kanisani hapo kwa punguzo kubwa.
  Picha na Craty Cleophace @EAGT Lumala Mya

  0 0

  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiongozana na Mkuu wa Jeshi la Magereza jijini Mbeya Kamishna Msaidizi Paul Kajida (kulia) wakati alipowasili kukagua shughuli za uzalishaji thamani za ndani na sabuni katika gereza la Ruanda .Naibu Waziri yupo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.
  Mkuu wa Kiwanda cha Gereza la Ruanda ASP Michael Kuga, akisoma taarifa ya hali ya uzalishaji wa sabuni na thamani za ndani mbele ya Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa ziara ya kikazi ya ukaguzi wa shughuli za maendeleo zinazofanyika katika magereza yaliyopo jijini Mbeya.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(wapili kushoto) akipata maelezo juu ya utengenezwaji wa kiti kinachotengenezwa na wafungwa wa gereza la Ruanda wakishirikiana na wataalamu wa Jeshi la Magereza.Naibu Waziri yupo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wakwanza kulia waliokaa), akiangalia picha za thamani za ndani zinazotengenezwa na wafungwa wa Gereza la Ruanda wakishirikiana na wataalamu wa Jeshi la Magereza.Wengine waliokaa baada ya Naibu Waziri ni Mkuu wa Kiwanda hicho,ASP Michael Kuga ,Kamanda wa Jeshi la Zimamoto Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Jesuald Ikonko na Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya Emmanuel Lukula.Naibu Waziri yupo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza alipotembelea Kiwanda cha sabuni zinazotengenezwa na wafungwa wa gereza la Ruanda wakishirikiana na wataalamu wa Jeshi la Magereza.Wanaomsikiliza ni Mkuu wa Kiwanda() na Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Paul Kajida. 
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akiangalia moja ya sabuni zinazozalishwa na wafungwa wa Gereza la Luanda wakishirikiana na wataalamu wa Jeshi la Magereza.Kulia ni Mkuu wa Kiwanda hicho.Naibu Waziri yupo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

  IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

  0 0

   Vifaranga vya mbegu ya kuku wa kienyeji vinavyofugwa kisasa.
   Wakiwa na furaha ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Abuu Mjaka akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Namaingo Business Agency Limited, Ubwa Ibrahim baada ya kuzindua Mradi wa Ufugaji  Kuku kwa wanachama 3000 wa kampuni hiyo kutoka mikoa ya Lindi Mtwara na Ruvuma katika hafla iliyofanyika Kijiji cha Miteja, wilayani humo juzi. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
   Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Abuu Mjaka akifungua mlango katika banda la vifaranga vya mbegu vya mradi huo.
   Mpiga Picha wa Gazeti la Tanzania Daima,  Said Powa ambaye aliliwakilisha kundi la Wananchama Wanahabari la Kwanza One akipokea cheti cha usajili kutoka kwa  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Mjaka wakati wa hafla hiyo
   Kundi la Wanahabari la Kwanza One likishangilia kwa furaha baada ya kukabidhiwa cheti cha kuwa miongoni mwa wanachama watakaoshiriki kwenye mradi huo
   Mbegu za mazao zilizooteshwa kwa ajili ya kulisha kuku

   Mkurugenzi wa Kampuni ya Ufugaji Kuu ya Shitindi Poutry Farm, Shitindi (katikati) akizungumza wakati wa uzinduzi, ambapo aliahidi kununua mayai ya wanachama wa ufugaji wa kuku wa Namaingo.


   Ni burudani kwa kwenda mbele
   Mtalaamu wa ufugaji kuku wa kienyeji akielezea jinsi mfugaji anavyoweza kuzalisha majani ya malisho kwa kutumia mazao mblimbali

   Mkurugenzi Mtendaji wa Namaingo, Ubwa Ibrahim akizungumza wakati wa hafla hiyo
   Sehemu ya umati uliohudhuria hafla hiyo
   Mjaka akihutubia wakati wa hafla hiyo
   Baadhi ya Wananchi wakisikiliza kwa makini hotuba
   Moja ya mabanda ya kuku yaliyoandaliwa kwa ajili ya
  Wanachama wakifurahia baada ya kukabidhiwa cheti cha usajiri wa Biashara cha Brela


  Mwenyekiti wa Namaingo Mkoa wa Ruvuma akipokea cheti cha Brela
  Dk. Hassan Kijaki Mtaalalamu wa Mifugo wa Mkoa wa Lindi akielezea kufurahishwa na kitendo cha Namaingo kuwekeza mradi wa kuku mkoani humo.
  Mchumi wa Mkoa wa John Mwalongo akihutubia wakati wa hafla hiyo
  Bi Ubwa na Mjaka wakikagua bidhaa mbalimbali za wAJASIRIAMALI ZILIZOFUNGWA KWA NJIA YA KISASA  0 0

  Mwenyekti wa Klabu ya Golf ya Jeshi ya Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo Brigedia Jenerali Michael Luwongo akizungumza na Wachezaji wa Klabu hiyo Jijini Dar es Salaam,wachezaji hao wanataraji Kuwakilisha katika mashindano ya Miaka 10 ya Klabu yanayotarajiwa kufanyika Mwezi February mwaka huu.(Picha na Luteni Selemani Semunyu).
  Mwenyekiti wa Klabu ya Golf ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo Brigedia jenerali Michael Luwongo akisisitiza jambo wakati akizungumza na Baadhi ya Watendaji wa klabu hiyo hawapo pichani kuhusu maandalizi ya Miaka 10 ya Klabu hiyo Jijini Dar es Salaam. (Picha na Luteni Selemani Semunyu) .
  Baadhi ya Wachezaji wa kulipwa na wale wa Ridhaa wa Klabu ya Golf ya Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania ya Lugalo wakiwa katika mazoezi kwa Ajili ya Maandalizi ya mashindano ya Maadhimisho ya Miaka 10 ya Klabu hiyo yanayotarajiwa kufanyika Mwezi February Mwaka huu 2017 Jijini Dar es Salaam. (Picha na Luteni Selemani Semunyu) .
  Baadhi ya Wachezaji wa kulipwa na wale wa Ridhaa wa Klabu ya Golf ya Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania ya Lugalo wakijadiliana wakati wa mazoezi kwa ajili ya mashindano ya Maadhimisho ya Miaka 10 ya Klabu hiyo yanayotarajiwa kufanyika Mwezi February Mwaka huu 2017 Jijini Dar es Salaam. (Picha na Luteni Selemani Semunyu) .

  ………………
  Na Luteni Selemani Semunyu JWTZ.
  Klabu ya Golf ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo iko katika maandalizi ya viwanja kwa ajili ya mashindano ya kuadhimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwa klabu hiyo mwaka 2006.

  Akizungumza na waandishi wa Habari msimamizi wa viwanja ambaye pia ni mchezaji wa kulipwa wa klabu ya Lugalo David Helela alisema kila kitu kinaenda sawa na wanaangalia sehemu ngumu kuchezeka kuondoa vikwazo visivyo na sababu.

  “kuna vikwazo vinavyopaswa kuwepo katika Uwanja wa golf lakini kuna vikwazo vingine vinakuwepo lakini havina sababu wala havina mchango katika kuonyesha umahiri wa mchezaji hivyo tunaviondoa”, Alisema Helela.
  Aliongeza kuwa mbali na kuviondoa bado viwanja kama namba 12 vitaendel;ea kuwa moja ya kiwanja kigumu kwa mchezaji atakayecheza katika uwanja huo kutoka na jinsi ulivyowekwa kwa lengo tu la kukamilisha sifa za uwanja wa Golf.

  Helela Alisema katika kuelekea kuadhimiasha Miaka 10 klabu ya lugalo itabaki kuwa ndio klabu pekee inayothamini kwa kiwango kikubwa mchango wa wachezaji wa kulipwa ambao mbali na kuwatumia katika kufundisha vijana na kusimamia sheria za mchezo lakini wamekuwa wakishirikishwa katika mashindano ya wachezaji wa kulipwa .

  Kwa Upande wake Afisa Tawala wa Klabu hiyo Kapteni Amanzi Mandengule alisema amefanya ukaguzi wa Awali kazi zinaenda vizuri na kutoa wito kwa wadhamini kuongeza nguvu ili kuwa na mashindano Bora.

  “ Kuna wadhamini tuliofanikia na wako tayari na wameanza maandalizi lakini Milango iko wazi kwa wadhamini wengine kujitokeza kwani Mashindano ya Miaka 10 ya Klabu yanatarajiwa kuwa ya Aina yake ukilinganisha na mashindano yaliyowahi kuandaliwa”Alisema kapteni Mandengule.

  Aliongeza kuwa taarifa rasmi ya mashindano na Mgeni rasmi inatarajiwa kutolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa Klabu Brigedia Jenerali Michael Luwongo ili kuelezea kwa kina mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika katikati ya Mwezi wa Pili.

  Katika mashindano hayo yanayotarajiwa kuwa ya siku tatu Vilabu vyote vimealikwa na makundi yote ya mashindano yatashirikishwa katika mashindano hayo ambayo yatakuwa ni mashindano ya Kwanza makubwa nchini kwa mwaka 2017 .

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo LAND O’ LAKES Dkt. Rose Kingamkono akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mradi wa uhamasishaji usawa wa kijinsia katika kilimo, uhakika wa chakula na lishe leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mtafiti kutoka Taasisi ya Taaluma ya Maendeleo UDSM Profesa Bertha Omari Koda.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo LAND O’ LAKES Dkt. Rose Kingamkono akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) kitabu kinachotumika kutoa elimu juu ya usawa wa kijinsia katika sekta ya kilimo, sheria za kimila leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mhadhiri wa Shule Kuunya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC) Bw. Dotto Kuhenga, Mtafiti kutoka Taasisi ya Taaluma ya Maendeleo UDSM Profesa Bertha Omari Koda na Mtaalamu Mwelekezi wa masuala ya Jinsia,Utawala Bora na Maendeleo kutoka LAND O’ LAKES Bibi. Margreth Henjewele.
  Mtafiti kutoka Taasisi ya Taaluma ya Maendeleo UDSM Profesa Bertha Omari Koda akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano wao na waandishi hao(hawapo pichani) kuhusu mradi wa uhamasishaji usawa wa kijinsia katika kilimo, uhakika wa chakula na lishe leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo LAND O’ LAKES Dkt. Rose Kingamkono na Mtaalamu Mwelekezi wa masuala ya Jinsia,Utawala Bora na Maendeleo kutoka LAND O’ LAKES Bibi. Margreth Henjewele.
  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Sehemu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya umma –SJMC) Bw, Dotto Kuhenga akionyesha waandishi wa habari kitabu cha mwongozo wa waandishi wa habari katika utekelezaji wa mradi wa uhamasishaji usawa wa kijinsia katika kilimo, uhakika wa chakula na lishe leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo LAND O’ LAKES Dkt. Rose Kingamkono na Mtafiti kutoka Taasisi ya Taaluma ya Maendeleo UDSM Profesa Bertha Omari Koda (kulia).
  Mtaalamu Mwelekezi wa masuala ya Jinsia,Utawala Bora na Maendeleo kutoka LAND O’ LAKES Bibi. Margreth Henjewele akitoa ufafanuzi kuhusu mradi wa uhamasishaji usawa wa kijinsia katika kilimo, uhakika wa chakula na lishe leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo LAND O’ LAKES Dkt. Rose Kingamkono.


  Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO.

  0 0

   Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage (Katikati) akizungumza na Msimamizi kituo cha Dimani Bi. Abdu Simai Haji leo wakati zoezi la upigaji kura likiendelea katika jimbo la Dimani.
   Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage (Katikati) akizungumza na waandishi wa Habari wa Zanzibar kutoa tathmini ya hali ya Uchaguzi mara baada ya kuetembelea vituo mbalimbali vya kupigia kura katika jimbo la Dimani leo.

   Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage (wa pili ) akiwa ameambatana na Baadhi ya Watendaji wa NEC na  Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Bi. Idaya Selemani Hamza (wa Kwanza) akiwasili katika kituo cha Kupigia Kura cha Kombeni katika jimbo la Dimani kuangalia maendeleo ya  Upigaji wa Kura leo.
   Mmoja wa Wananchi katika jimbo la Dimani akipiga Kura yake kumchagua Mbunge katika jimbo la Dimani leo.
   Baadhi ya Wangalizi wa Uchaguzi katika jimbo la Dimani wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa Uchaguzi mdogo wa Ubunge katika jimbo la Dimani leo.

   Mmoja wa Wananchi katika jimbo la Dimani akipiga Kura yake kumchagua Mbunge katika jimbo la Dimani leo.
  Wananchi wakiangalia majina yao kabla ya kupiga kura katika kituo cha Bweleo katika jimbo la Dimani leo.

  Picha na Aron Msigwa –NEC.

   Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage (Kushoto) akizungumza na Mawakala wa Vyama vya Siasa waliokuwepo ndani ya kituo cha kupigia Kura cha Kombeni katika jimbo la Dimani leo. Wengine wanaochukua taarifa ni Watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).


  Na. Aron Msigwa – NEC, Zanzibar.
  22/1/2017.

  Hatimaye wananchi wa Jimbo la Dimani visiwani Zanzibar waliojiandikisha katika Daftari la Kudumu la Mpiga leo wamejitokeza kwa wingi katika vituo mbalimbali kupiga kura kumchagua Mbunge atakayewawakilisha kwa kipindi cha miaka miaka 4.

  Zoezi la upigaji wa Kura katika vituo mbalimbali lilianza majira ya saa 1 asubuhi  likifanyika kwa hali ya Amani na Utulivu huku baadhi ya wananchi waliojitokeza kupiga kura wakipongeza maandalizi mazuri yaliyofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzine (NEC)  kufanikisha Uchaguzi huo.

  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Rufaa, Mhe. Semistocles Kaijage akizungumza kuhusu mwenendo wa Uchaguzi huo mara baada ya kutembelea vituo  vya kupigia kura katika jimbo hilo na  kuzungumza  na Mawakala wa Vyama vya Siasa waliokuwepo vituoni, Waangalizi wa Uchaguzi na Wasimamizi wa Uchaguzi  huo amesema Tume imeridhishwa na kazi nzuri  iliyokuwa ikiendelea katika vituo mbalimbali vya kupigia Kura.

  Viongozi wa Tume tumetembelea vituo mbalimbali vya kupigia Kura katika jimbo la Dimani; tumeona wenyewe upigaji wa Kura unaendelea vizuri, tumewauliza Mawakala, Watazamaji na Wasimamizi wa Vituo vya Uchaguzi  kila mmoja amesema Uchaguzi unakwenda vizuri, nachoweza kuwaambia watanzania Uchaguzi Dimani unakwenda Vizuri” Amesema Jaji Kaijage.

  Amesema Wasimamizi wa Uchaguzi katika Jimbo hilo wanaendelea kufanya kazi zao kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Maadili pia kushughulikia kwa haraka changamoto zilizokuwa zikijitokeza katika  baadhi ya vituo vya kupigia Kura.

  Ameeleza kuwa zoezi zima la upigaji wa Kura linaendeshwa kwa uwazi mkubwa, Utulivu na Amani na kuwawezesha wananchi kupiga kura bila vikwazo vyovyote.

  Aidha, Mhe. Kaijage amebainisha kwamba endapo yatajitokeza malalamiko yoyote wakati zoezi la upigaji wa Kura likiendelea katika vituo mbalimbali , Mawakala wa Vyama vya Siasa ambao ni wasimamizi wa Maslahi ya Wagombea na Vyama vyao Vituoni watajaza fomu  ya malalamiko  Na. 14 kwa mujibu wa Sheria ambayo inatoa fursa ya kushughulikiwa kwa malalamiko hayo.

  Aidha, amebainisha kuwa mara baada ya zoezi la upigaji wa kura kumalizika leo saa 10 jioni kazi ya kuhesabu Kura itafuata ili hatimaye wamnanchi wa Jimbo la Dimani waweze kupatiwa matokeo ya maamuzi waliyoyafanya kupitia Kura zao.

  Mhe. Kaijage amesisitiza kuwa Wasimamizi wote wa Uchaguzi huo wamepewa mafunzo ya kuzingatia ili kuhakikisha wanaendesha zoezi hilo kwa ufanisi mkubwa na kuwezesha matokeo kutangazwa kwa wakati ili kuwawezesha wananchi kumjua mshindi wa Uchaguzi huo.

  “ Endapo taratibu zote za Uchaguzi zitakuwa zimekamilika kwa mujibu wa Sheria, hakutakuwa na sababu yoyote ya kuchelewesha matokeo,mpaka sasa Tume ya Taifa ya Uchaguzi tumeridhishwa na mwenendo mzima wa zoezi la upigaji wa Kura na matokeo yatatolewa kwa wakati” Amesisitiza.

  Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe akizungumzia zoezi la Upigaji wa Kura amesema kuwa Wapiga Kura wanaoruhusiwa kupiga kura ni wale waliokidhi Sifa na Vigezo vilivyoainishwa kisheria kuwawezesha kupiga Kura.

  Amesema  kwa mujibu wa Sheria Msimamizi wa Kituo ndiye mwenye mamlaka ya maamuzi katika kituo cha kupigia Kura ikiwa ni pamoja na kuamuru kuondolewa kwa mtu yeyote atakayeonekana kufanya fujo au kuzuia zoezi la uchaguzi kuendelea kituoni.

  Katika Uchaguzi Uchaguzi huo mdogo wa Ubunge wa jimbo la Dimani jumla ya Wapiga Kura 9,280 wanatarajiwa Kupiga kura katika Vituo 29 huku vyama vya Siasa vyenye wagombea vinavyoshiriki Uchaguzi huo ni 11 huku Waangalizi wa Uchaguzi waliojitokeza kushiriki katika Uchaguzi huo ni zaidi ya 300.

  0 0

  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akizungumza katika kikao cha wadau kutoka taasisi mbalimbali waliokutana na kamati ya marekebisho ya wepesi wa kufanya shughuli nchini, kushoto kwa waziri ni Katibu Mkuu biashara na uwekezaji Mhe. Prof. Adolf Mkenda, Mwenyekiti wa kamati ya kuboresha mazingira ya biashara Dkt. John Mduma, kulia kwa waziri ni Katibu tawala Kibaha Ndg. Anatory Mhango.

  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akizungumza katika kikao cha wadau kutoka taasisi mbalimbali waliokutana na kamati ya kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini katika ukumbi wa kituo cha utafiti wa miwa na muhogo mjini Kibaha.
  Katibu Mkuu Biashara na Uwekezaji, Mhe. Prof. Adolf Mkenda akizungumza katika kikao cha wadau kutoka taasisi mbalimbali waliokutana na kamati ya kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini katika ukumbi wa kituo cha utafiti wa miwa na muhogo mjini Kibaha.
  Wadau kutoka taasisi mbalimbali za serikali waliokutana na kamati ya kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini katika ukumbi wa kituo cha utafiti wa miwa na muhogo mjini Kibaha.
  Wadau kutoka taasisi mbalimbali waliokutana na kamati ya kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini katika ukumbi wa kituo cha utafiti wa miwa na muhogo mjini Kibaha.
  Wadau kutoka taasisi mbalimbali waliokutana na kamati ya kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini katika ukumbi wa kituo cha utafiti wa miwa na muhogo mjini Kibaha.

  ………………

  Waziri wa viwanda, Biashara na uwekezaji akutana na kamati ya kuboresha ya mazingira ya biashara ambayo inahusisha wataalamu kutoka sekta mbalimbali katika wizara zote, TBS, EWURA, SUMATRA, TRA, OSHA, WMA, NCC, n.k na kujadili changamoto mbalimbali ambazo ni vikwazo katika wepesi wa kufanya shughuli.

  Waziri amehimiza wataalamu hawa kujadili changamoto na kutoa mapendekezo ya namna ya kuondoa kero hizo ili kuboresha urahisi wa kufanya shughuli nchini Tanzania na kuvutia wawekezaji.

  Waziri amehimiza ulipaji wa kodi ili kuleta maendeleo ya watu, kwani kwa takwimu Tanzania ni ya 154 kati ya nchi 190 hivyo kuhimiza wafanyabiashara wote kuwa na Tin namba na pia kulipa kodi.

  Mkutano huu umefanyika jumamosi tarehe 21/1/2017 ukumbi wa kituo cha utafiti wa miwa na muhogo mjini Kibaha.

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh. Athnony Mtaka akizungumza katika kikao naKatibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi NEEC, Bi Beng’i na watendaji wengine.
  Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh. Athnony Mtaka akiwa katika picha ya pamoja naKatibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi NEEC, Bi Beng’i na watendaji wengine mara baada ya kikoa hicho.


  *Waziri Mkuu Kuzindua Feb; Mtaka Ataka Viwanda

  *Dk Jingu Asisitiza ubia kwenye ranchi
  ……………………………………………………………
  RAS Sagini: nusu ya wakazi wa Itilima ni waganga; Ataka uzalishaji

  KUTOKANA na riba kubwa na masharti magumu ya ukopaji katika mabenki ya biashara, wafanyabiashara wadogo wadogo wa Simiyu, wataunganishwa na wafanyabiashara wakubwa duniani ili kupata mitaji na masoko nje ya nchi.

  Akitoa taarifa ya Baraza kwa Kamati, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Beng’I Mazana Issa, alisema Baraza lake tayari limeshaanza kutekeleza mikakati ya kuunganisha mkoa wa Simiyu na wawekezaji ili kuhakikisha wananchi wa mkoa huo wanashiriki katika shughuli za uwekezaji (local content).

  Alisema Baraza lake pamoja na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) chini ya mradi wa ‘Tanzania Venture Capital & Private Sector Equity’, watanzindua program ya kuwaunganisha wafanyabiashara wadogo, wawekezaji wa ndani na wafanyabiashara wenye mitaji mikubwa duniani.

  “Wafanyabiashara wadogo wa Simiyu pamoja na wengine kutoka mikoa yote ya Tanzania, wataingia ubia na wafanyabiashara wenye mitaji mikubwa duniani kupitia utaratibu wa venture capital,” alisema Ms Issa.

  Katibu Mtendaji huyo alisema katika utaratibu huo, badala ya wafanyabiashara wadogo kutoka Simiyu na wale wa mikoa mingine kutafuta mikopo yenye riba kubwa na masharti magumu kwenye mabenki “wataingine mikataba na makampuni yenye mitaji na ujuzi kwa makubaliano ambayo pande zote zitanufaika,” alisema mtaalamu huyo wa mambo ya fedha, mitaji na uwekezaji.

  Alisema program hiyo inatarajiwa kuzinduliwa mapema mwezi ujao (4/2/2017) mjini Dodoma na kuongeza kuwa uzinduzi huo utafanywa na Waziri Mkuu, Mh Majaliwa Kassim Majaliwa.

  DR JINGU ASHAURI KUHUSU RANCHI

  Wakati huo huo mkoa wa simiyu umeshauriwa kuangalia uwezekano wa kuanzisha ranchi binafsi ambazo zitafanya kazi kwa ubia na ranchi za Srikali zilizopo ili kuweka msukumo katika maendeleo ya mifugo nchini.

  Akiongea na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Simiyu mwishoni mwa wiki, Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Dk John Jingu, alisema watu binafsi na hata Halmashauri wanaweza wakaanzisha ranchi ambazo zitaingia ubia na ranchi za serikali.

  Tanzania ina ranchi kadhaa za Serikali na zingine za binafsi ikiwa ni pamoja na Ruvu, Mkata, Manyara, Mkwaja, Ndarakwai. Ranchi za Serikali zinamilikiwa na Kampuni ya Ranchi ya Taifa, NARCO.

  Dk Jingu aliupongea mkoa wa Simiyu kwa kuwa mfano hai kupigiwa katika shughuli za kuhamasisha uwezesha kiuchumi kwa vile maendeleo ya viwanda ambayo yameanza kukita mizizi katika mkoa huo mpya ni mfano hai unaoonesha kuwa kila kitu kinawezekana tukiamua.

  “Kinachotakiwa ni mtaji, masoko na teknolojia ili tuweze kujenga uchumi wa wananchi wetu na hatimaye uchumi wa Taifa zima, Simiyu mmeonesha mfano mzuri wa kuigwa,” alisema.

  Alitoa wito kwa viwanda vinavyoanzishwa na kwa wafanyabiashara wote wa Tanzania kuzingatia ubora wa bidhaa akikumbushia mchele wa Tanzania ambao haukununuliwa Dubai tofauti na ule wa Pakistani na India kwa kuwa na mchanganyiko maalum.”

  Dk Jingu alihimiza ubora na ‘grading’ ya bidhaa ikiwa ni pamoja na kujua historia ya bidhaa zetu kwa kila tunachozilisha hadi zinapelekwa sokoni ili mteja apate maelezo yote husika huku viwango vya ubora wa kimataifa ukizingatiwa.

  0 0

   RAIS wa Uturuki Mheshimiwa Recep Erdogan amewasili nchini leo jioni (Jumapili, Januari 22, 2017) kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na kupokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kupokelewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na niaba ya Mheshimiwa Rais. Dkt. John Magufuli.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiteta jambo na mgeni wake
   RAIS wa Uturuki Mheshimiwa Recep Erdogan mara baada ya kuwasili nchini leo jioni (Jumapili, Januari 22, 2017) kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na kupokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,kulia ni mke wa Rais wa Uturuki,Mama Emine Erdogan

  RAIS wa Uturuki Mheshimiwa Recep Erdogan amewasili nchini leo jioni (Jumapili, Januari 22, 2017) kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na kupokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kupokelewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na niaba ya Mheshimiwa Rais. Dkt. John Magufuli.

  Rais huyo ameambatana na mkewe Mama Emine Erdogan pamoja na Mawaziri watatu ambao ni Waziri wa Mambo ya Nje Mheshimiwa Mevlüt Çavuşoğlu,Waziri wa Uchumi Mheshimiwa Nihat  Zeybekekci na Waziri wa Nishati na Maliasili Mheshimiwa Berat Albayrak
  .
  Pia Rais huyo ameambatana na wafanyabiashara wapatao 85 wa nchi hiyo.

                              
  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S. L. P. 3021,
  11410 - DAR ES SALAAM
  JUMAPILI, JANUARI 22, 2016.

  0 0

  0 0

  Mkurugenzi wa Taasisi ya Agri-Busness Media Innitiative In Tanzania (AMI-TZ) ya Jijini Mwanza, Deborah Mallaba, akikagua shamba la hekari mbili la taasisi hiyo ambalo lina mkusanyiko wa matunda na mbogamboga za aina mbalimbali, lililopo Igombe Ziwani, Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza.

  Na Binagi Media Group
  Taasisi ya AMI-TZ inajihusika na kilimo cha matunda na mbogamboga kama vile matikiti maji, nyanya, bamia, nyanya, pilipili mbuzi na aina nyinginezo nyingi.

  Baada ya mavuno, taasisi hiyo hufanya usindikaji wa mazao kwa ajili ya kuwafikishia wateja wake majumbani, maofisini na mengine huuzwa moja kwa moja shambani.

  "Baadhi ya vijana ukiwaeleza suala la kilimo wanakuona kama vile umepitwa na wakati lakini wale wanaojitambua wameingia kwenye kilimo na kinawalipa. Hivyo niwahamasishe watumie muda wao vizuri kwa kujishughulisha kwenye kilimo hivyo wasisubiri tu kazi za maofisini". Anasisitiza Deborah Mallaba, Mwanahabari na Mkurugenzi wa Taasisi ya AMI-TZ.

  Mallaba anawasisitiza viongozi wa serikali kuanzia ngazi ya Kata hadi Wilaya, kuongeza jitihasa za kuwakusanya vijana pamoja na kuwapatia mitaji ikiwemo pembejeo ili wajikite kwenye kilimo maana kilimo ni biashara na kinalipa ambapo pia hatua hio itasaidia kupunguza vijana mitaani.

  "Napenda kuwaambia akina dada waamuke maana si vyema kuzurura tu wakisema hakuna ajira. Mfano mimi nimeanza kujiwekea kipato changu kupitia kilimo na nataka kuwa mafano bora kwa vijana wengine". Anasisitiza Aneth Shosha ambaye ni Afisa Masoko wa taasisi ya AMI-TZ huku akiwakaribisha vijana wengine kwenye taasisi hiyo ili wajifunze zaidi kuhusu kilimo.
  Aneth Shosha ambaye ni Mratibu/ Afisa Masoko wa Taasisi ya Agri-Busness Media Innitiative In Tanzania (AMI-TZ), akimwagilia maji kwenye shamba la bamia
  Wachapa kazi wakichakarika
  Kilimo cha nyanya
  Mfumo wa umwagiliaji kwa kutumia mashine kutoka Ziwa Victoria ndio hutumika kwenye shamba hili. 
  Kwa msaada na ushauri, piga simu nambari 0754 99 66 13

  0 0

  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla leo 22 Januari 2017, ameshiriki Maulid ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW), iliyoandaliwa na kampuni ya Nida Textile Mills Ltd, ambapo pia hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa Rais Mstaafu wa awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi pamoja na viongozi wengine mbalimbali wa kiserikali akiwemo Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na viongozi wa Dini nchini. 

  Katika hafla hiyo, Al-Haji Ali Hassan Mwinyi amewataka watanzania kuwa na tabia ya kuyafanyia muendelezo yale mema wanayoyafanya, kama walivyofanya kampuni hiyo ya Nida na kuwakutanisha pamoja waislamu na kumsifu katika kumbukumbu hizo za kiongozi wa waislamu Mtume Muhammad (S.A.W).
  Tazama MO tv kuona tukio hilo hapa:
  Mbali na Dk. Kigwangalla, wageni wengine ni pamoja na Naibu Waziri Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo, Waziri wa zamani wa Ulinzi Profesa Juma Kapuya, Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahimu Lipumba, Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega huku kwa viongozi wa dini walikuwepo Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum na Kadhi Mkuu wa Tanzania Abdallah Mnyaa ambapo wote kwa pamoja walipewa zawadi maalum na kampuni hiyo.
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wageni mbalimbali wakati akiwasili kwenye hafla hiyo ya maulidi ya Mtume
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wageni mbalimbali katika tukio hilo
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla akijadiliana jambo na wageni waalikwa wengine katika tukio hilo akiwemo Prof. Ibrahim Lipumba
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wageni katika hafla hiyo ya maulidi ya Mtume
  Baadhi ya vijana wa Madrasa mbalimbali kutoka Dar es Salaam na baadhi ya mikoa wakifuatiliatukio hilo
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Naibu waziri wa Tamisemi, Mh. Suleiman Jafo wakati akiwasili kwenye hafla hiyo ya maulidi ya Mtume
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla akijadiliana jambo na Naibu waziri wa Tamisemi wakati wakiwasubiria wageni waalikwa akiwemo Rais Mstaafu wa awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi pamoja na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal wakati wa kumpokea alipowasili kwenye hafla hiyo.
  dua zikiendelea
  Dua zikiendelea
  Rais Mstaafu wa awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi ambaye alikuwa mgeni rasmi, akizungumza katika tukio hilo
  Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akipokea zawadi kwenye hafla hiyo.
  Dk. Kigwangalla akipokea zawadi katika hafla hiyo
  Wageni mbalimbali wakifuatilia hafla hiyo ya Maulidi


  0 0

   Baadhi ya wakazi wa Njombe Mjini wamiwa wanamsikiliza waziri Mkuu Kassm Majaliwa katika maeneo ya Wikichi Mjini Njombe
   Waziri mkuu Majaliwa akizungumza na wakazi wa njombe Maeneo ya Hospitali ya Mkoa wa njombe Mtaa wa Wikichi Njombe Mjini.
  Wziriri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa wakitembelea maeneo mbalimbali ya kiwanda cha chai cha Kibena 
  WAZIRI  Mkuu wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa ameahirisha ziara yake mkoani Njombe ambapo ameelekea jijini Dar es salaam ambako anatarajia kumpokea Rais wa Uturuki ambaye anakuja hapa nchini kwa ziara ya kikazi Ziara yake inatarajiwa kuendelea januari 25 kwa siku tatu.
  Waziri mkuu amekuwa mkoani Njombe kwa siku tatu ambapo amepita katika halmashauri tatu za mkoa huo kabla ya kuahirisha ziara hiyo na kurejea jijini Dar es Salaam kwa majukumu mengine ya kiutendaji ziara yake mkoani Njombe ilikuwa ya siku sita na kuzitembelea halmashauri zote za mkoa huo.
  Waziri mkuu Juzi aliwaaga viongozi wa mkoa wa Njombe na kuelekea jijini Dar Es Salaam katika viwanja vya ndege mkoani Iringa huku akitarajia kulejea tena mkoani humo Januari 25 na kumaliza ziara yake baada ya siku tatu.

  Akirejea Njombe atatembelea halmashauri ya wilaya ya Njombe na kutembelea kiwanda cha chai na kuzungumza na wakulimqa wa zao hilo, kasha kuzungumza na wakazi wa Mji wa Njombe baadaye kwenda wilayani Ludewa ambako pia atakutaa na wakazi wa Mundini na Liganga kutako tarajiwa kuwa na migodo ya makaa yam awe na Chuma.
  Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka akizungumza na Nipashe kuhusiana na kuahirishwa kwa ziara hiyo alisema kuwa waziri mkuu alikuwa mkoani humo kwa siku tatu ambapo ameahilisha kuendelea na ziara na kasha kulejea tena Januari 25.

  Alisema kuwa waziri mkuu anaelekea jijini Dar es Salaam kwa kuwa nchi itakuwa ikipokea ugeni wa Rais wa Uturuki ambaye anafanya ziara yake hapa nchini ambapo baada ya ziara ya Rais Huyo Waziri mkuu watalejea Mkoani Njombe.
  Mwishoni mwa wiki jana Waziri mkuu alikuwa mkoani Njombe na kuzungumza na wakazi wa maeneo mbalimbali ya halmashauri za wilaya Makete, Wangingombe, na mji wa Makambako ambako ndio alianzia ziara yake.

  Akiwa Wangingombe alifungua jingo la Halimashauri ya Wangingombe na kuzungumza na wananchi wa Mjia huo kasha kuwataka watumishi wa halmashauri na wilaya kuhamia halmashauri hiyo ifikapo mwezi februari.

  Waziri hakusika kuwaeleza wananchi adhima ya serikali kuwaletea maendeleo ikiwa ni pamoja na kumaliza matatizo ya maji na kufanya wafanye shughuli za kimaendeleo bila Bughuza.

older | 1 | .... | 1111 | 1112 | (Page 1113) | 1114 | 1115 | .... | 1898 | newer