Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

Taarifa ya ujio wa ziara ya Rais wa Uturuki nchini

0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI



 

 



Taarifa kuhusu ziara ya Rais wa Uturuki nchini.

Rais wa Jamhuri ya Uturuki, Mheshimiwa Recep Tayyip Erdogan anatarajiwa kufanya ziara ya kitaifa ya siku mbili nchini tarehe 22 na 23 Januari 2017 kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. 

Mhe. Rais Erdogan ambaye ataambatana na Mkewe, na kuongoza ujumbe wa watu 150 wakiwemo Mawaziri, Wabunge, Maafisa kutoka Serikalini na Wafanyabiashara anatarajiwa kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere tarehe 22 Januari, 2017 jioni  na atapokelewa na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Madhumuni ya ziara hiyo ni kukuza mahusiano mazuri yaliyopo baina ya Uturuki na Tanzania pamoja ‎na kupanua fursa za uwekezaji hususan katika maeneo ya biashara  na uwekezaji.

Wakati wa ziara hiyo, Mhe. Erdogan  atakutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa mazungumzo ya faragha yatakayofuatiwa  na mazungumzo rasmi yatakayowahusisha wajumbe wa pande mbili na baadaye Marais hao watashuhudia uwekwaji saini wa mikataba ya ushirikiano kwenye maeneo mbalimbali. 

Siku hiyo ya tarehe 23 Januari, 2017, kutakuwa na Kongamano la Biashara kati ya Uturuki na Tanzania litakalowakutanisha Wafanyabiashara kutoka nchi hizi mbili. Kongamano hilolitahutubiwa na viongozi wa Tanzania na Uturuki.
Mhe. Rais Erdogan na ujumbe wake watashiriki Dhifa ya Chakula cha jioni kilichoandaliwa Ikulu kwa heshima yake na Mhe. Rais Magufuli.
Mahusiano ya Uturuki na Tanzania
Mahusiano ya Tanzania na Uturuki ni mazuri. Ikumbukwe kuwa, kufunguliwa kwa mara nyingine kwa Ubalozi wa Uturuki hapa nchini mnamo Mei 2009 kuliongeza kasi ya mahusiano baina ya nchi hizi mbili.  Tangu kipindi hicho kumekuwa na ziara za viongozi wa kitaifa wa nchi hizi mbili ili kukuza na kudumisha mahusiano. Katika hatua nyingine Tanzania imetangaza kufungua Ubalozi wake nchini Uturuki na hivi leo Mhe. Rais atamwapisha Balozi Mteule, Prof. Elizabeth Kiondo atakayetuwakilisha Uturuki.
Pia kumekuwa na ziara za viongozi wakuu wa kitaifa wa nchi hizi mbili ikiwemo ziara ya Rais mstaafu wa Uturuki, Mhe. Abdullah Gul  nchini mwaka 2009 ; ziara ya Rais wa Awamu ya Nne wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete nchini Uturuki mwaka 2010 na ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein mwaka 2011.
Tume ya Pamoja ya Biashara
Tanzania na Uturuki zinashirikiana pia kupitia Tume ya Pamoja ya Biashara ambayo ilianzishwa baada ya kusainiwa kwa Mkataba wa Ushirikiano kwenye masuala ya Biashara mwaka 2010. Kikao cha kwanza cha Tume hiyo kilifanyika Jijini Dar es Salaam mwezi Novemba 2012. Katika kikao hicho pande zote zilikubaliana kushirikiana kwenye maeneo mbalimbali hususan biashara na uwekezaji, elimu, Kilimo, Nishati na Madini, Maendeleo ya viwanda na mawasiliano ya simu.

Kikao cha Pili cha Tume ya Pamoja ya Biashara kati ya Tanzania na Uturuki kilifanyika tarehe 11 – 12 Januari 2017, Uturuki kwa lengo la kujadili utekelezaji wa Makubaliano ya Kikao cha Kwanza na kuibua maeneo mapya ya ushirikiano kati ya pande hizi mbili. Aidha, Mkutano huu pia ulikuwa na umuhimu wa kipekee kwa kuwa ulifanyika ikiwa ni maandalizi ya ziara ya Kiserikali ya Mheshimiwa Recep Tayyip Erdoğan, Rais wa Jamhuri ya Uturuki inayotarajiwa kufanyika tarehe 23 Januari, 2017.

Pande zote mbili zimekubaliana kuongeza nguvu katika kuhamasisha uwekezaji kwenye nchi zetu. Katika kutekeleza hili, Uturuki imepanga kuandaa Mkutano wa Uwekezaji kati ya Tanzania na Uturuki ndani ya robo ya pili ya mwaka huu jijini Istanbul. Vile vile, nchi zote mbili zimekubaliana kubadilishana taarifa za fursa za uwekezaji kupitia Balozi zetu na Baraza la Biashara la Tanzania na Uturuki. Aidha, Taasisi zetu za Uwekezaji zimeelekezwa kuanza majadiliano ya kuingia Mkataba wa Ushirikiano ili kuhamasisha uwekezaji nchini. Hali kadhalika, Uturuki imemchagua Mwambata wa Biashara katika Ubalozi wao wa Dar es Salaam na Tanzania imeahidi kuteua Afisa Maalum ndani ya mwezi mmoja kushughulikia uhamasishaji wa uwekezaji na biashara kati ya nchi hizi mbili.

Mafanikio yaliyopatikana kutokana na ushirikiano kati ya Tanzania na Uturuki.

Tangu kuanzishwa kwa Tume ya pamoja ya ushirikiano ya kiuchumi mafanikio ya ushirikiano baina ya nchi hizi mbili yameonekana ikiwemo:- Kuimarishwa kwa ushirikiano katika masuala ya Usafiri wa Anga ambapo Shirika la Ndege la Uturuki lilianzisha safari tatu  za moja kwa moja kutoka Istanbul hadi Dar es Salaam, Kilimanjaro na hivi karibuni Zanzibar. Kuanzishwa kwa safari hizi kumekuza biashara kati ya Uturuki na Tanzania  ambapo mwaka 2009  ukubwa wa biashara ulikuwa Dola za Marekani milioni 66 sawa na shilingi bilioni 145.2 lakini hadi kufikia Februari 2016 biashara kati  ya nchi hizi mbili iliongezeka kwa Dola za Kimarekani milioni 160 sawa na shilingi bilioni 352. 

Aidha, kuzinduliwa kwa Baraza la Biashara kati ya Tanzania na Uturuki mwaka 2013 ambalo kumewezesha kuimarisha ushirikiano wa sekta binafsi za nchi hizi mbili na  Kuongezeka kwa Makampuni ya Uturuki yaliyowekeza nchini ambapo hadi sasa ni Kampuni 30 zimefanya uwekezaji wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 305.08 na zinatarajiwa kutengeneza ajira 2,959.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dar es Salaam
20 Januari, 2017


ELIMU BURE YAONGEZA UDAHILI WA WANAFUNZI SHULE ZA MSINGI

0
0
Na: Frank Shija - MAELEZO

ELIMU bure yaongeza idadi ya udahili wa wanafunzi wa shule za msingi nchini waongezeka kutoka 1,282,000 mwaka 2015 hadi kufikia 1,896,000 mwaka 2016 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 84.5.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais –Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Mussa Iyombe alipokuwa anaongea katika kipindi cha tunatekeleza kinachoratibiwa na Idara ya Habari – MAELEZO na kurushwa na Televisheni ya Taifa (TBC1) jana jijini Dar es Salaam.

Mhandisi Mussa Iyombe amesema kuwa dhamira ya Serikali nikuhakikisha inatoa huduma bora za kijamii ikiwemo elimu, afya, miundombinu na maji safi.“Dhamira ya Serikali ni kutoa huduma bora za afya,elimu,maji na miundombinu ndiyo maana Serikali ya Awamu ya Tano ikaja na Sera ya Elimu bure ili kutoa fursa kwa wananchi wake kupata elimu,"alisema Mhandisi Iyombe.

Aidha Muhandisi Iyombe amebainisha kuwa kazi kubwa ya TAMISEMI ni kuratibu na kusimamia Mikoa, Wilaya na Halmashauri katika utoaji wa huduma bora za maendeleo kwa wananchi.

Aliongeza kuwa ili Serikali iweze kutimiza azma yake ya kuwapatia huduma za maendeleo wananchi wake imeweka mfumo dhatibiti wa ukusanyaji wa mapato katika halmashauri nchini ili kuhakikisha fedha inapatika kiwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.

Mhandisi Iyombe amesema kuwa mapato yanayokusanywa na halmashauri nchini ni kwa ajili ya kutoa huduma za kimaendeleo ili wananchi wanufaike.

SERIKALI KUANGALIA UPYA KANUNI ZA TAFITI ILI ZIWEZE KUFANYA KAZI KWA WAKATI

0
0
 Mshauri wa mradi wa Wema, Dk. Alois Kullaya (kushoto), akimuelekeza jambo Waziri Tizeba.
 Taswira ya shamba hilo la jaribio la mbegu za mahindi lililopo Makutupora mkoani Dodoma.
 Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi,  Charles Tizeba (kushoto), akizungumza na watafiti wa kilimo na wanahabari (hawapo pichani), wakati alipotembelea shamba la jaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma leo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk.Hassan Mshinda.
 Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Hussein Mansour akizungumza katika mkutano huo kabla ya kumkaribisha Waziri Tizeba.
 Mkutano ukiendelea.
 Mshauri wa masuala ya Bioteknolojia Dk.Nicholaus Nyange (kulia), akitoa mada kuhusu, Bioteknolojia ya kisasa katika sekta 
ya kilimo nchini.
 Mshauri wa mradi wa Wema, Dk. Alois Kullaya (kulia), akitoa mada kuhusu utafiti wa mahindi yanayohimili ukame.
 Taarifa ikitolewa mbele ya Waziri Tizeba (kushoto)
 Safari ya kuelekea shamba la jaribio la mbegu za mahindi ikiendelea. Katikati ni Waziri Tizeba.
 Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo Kanda ya Kati Makutupora, Leon Mroso (katikati), akitoa ufafanuzi kuhusu shamba hilo la jaribio hilo.
 Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi,  Charles Tizeba (kulia), akizungumza na watafiti wa kilimo wakati alipotembelea jaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma leo. Kushoto ni Mshauri wa mradi wa Wema, Dk. Alois Kullaya na Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo Kanda ya Kati Makutupora, Leon Mroso.
Waziri Tizeba  (wa sita kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na watafiti wa kilimo baada ya kutembelea shamba hilo.

Dotto Mwaibale, Dodoma

SERIKALI imesema itaangalia upya taratibu na kanuni zilizopo ili kuharakisha tafiti za kilimo zinazofanyika nchini zianzekufanya kazi kwa wakati.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi,  Charles Tizeba wakati alipotembelea jaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma leo asubuhi.

"Binafsi nisema katika teknolojia hii ya uhandisi jeni kwa hapa nchini tumechelewa kutokana na taratibu na kanuni zetu kutuchelewesha kwani maarifa ya watafiti wetu hayawafii walengwa kutokana na kanunu hizo" alisema Tizeba.

Alisema ni lazima serikali kuangalia jambo hilo ili kufupisha matokeo ya utafiti wa wataalamu wetu kuendelea kufanya hivyo ni kucheleweshana.

Alisema mbegu hii ambayo inafanyiwa utafiti kwa wenzetu wa Afrika Kusini wameanza kuitumia wakulima wao lakini kwa sisi kwa utaratibu wetu mbegu hiyo tutaanza kuitumia mwaka 2021 ni miaka minne zaidi.

"Tusisubiri taratibu hizi tutazungumza na wenzetu wa Ofisi ya Mkamu wa Rais  Mazingira na Tume ya Taifa Sayansi na Teknlojia (Costech) ili kuona namna ya kupunguza taratibu na kanuni hizo ambazo hazina tija kwa mkulima.

Alisema kama utafiti umefanyika na ukatoa matokeo mazuri hakuna sababu ya kusubiri na kupoteza muda wa matumizi ya teknolojia hiyo.

Alisema leo tabia nchi imeendelea kukua na ukame lakini sisi tunajifunga katika jambo ili ni lazima tujipange na kutumia teknolojia hii muhimu.

Akizugumzia kuhusu mtazamo hasi wa baadhi ya wananchi kuhusu matumizi ya  vyakula vya GMO alisema mitazamo hiyo inachochewa na wanaharakati kwa faida zao binafsi na kama wanaushahidi wa jambo hilo ni vizuri wakatoa ushahidi huo hadharani badala ya kupotosha umma.

"Kama mtu anaushahidi huo namuomba aniletee badala ya kuzungumza mitaani kwani wenzetu wa nchi zingine wanatumia vyakula hivyo na kama vingekuwa si sahihi wangewezaji kuvitumia" alihoji Tizeba.

Mkurugenzi Mkuu wa Costech Dk.Hassan Mshinda alisema kazi kubwa ya Costech ni kufadhili tafiti mbalimbali na kuhakikisha zinawafikia walengwa na akaishukuru serikali kwa hatua iliyofikia ya kuona taratibu na kanuni zilizopo jinsi zinavyorudisha nyuma maendeleo ya tafiti hizo za uzalishaji wa mbegu ambazo zikipatikana kwa wingi bei yake itakuwa ndogo tofauti na sasa na kumkomboa mkulima.

SERIKALI KUPITIA UPYA KANUNI ZA UTANGAZAJI

0
0
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO.

Serikali imejipanga kupitia upya kanuni za utangazaji za Sheria ya Utangazaji ya mwaka 2003 ili kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye wakati wa ziara yake kwa vyombo vya habari vya Channel, na Tumain Media iliyolenga kuimarisha mahusiano yaliyopo kati ya Serikali na vyombo vya habari nchini.

Waziri Nape amesema kuwa lengo la mapitio ya kanuni hizo ni uboreshwaji wa kanuni hizo ili kuisaidia kukuza sekta ya utangazaji.

“Kuna baadhi ya wadau wamekuwa wakilalamika kuhusu kupitwa kwa wakati kwa kanuni hizo, hivyo tumeona ni vyema kuungana nao ili kuzipitia upya na kuona palipo na mapungufu” alisema Waziri Nape.

Aidha, Waziri Nape aliongeza kuwa baadhi ya maeneo katika kanuni hizo yanayohitaji kupitiwa upya ni aina za leseni zilizopo, kubadilika kwa jamii inayotuzunguka pamoja na mabadiliko ya teknolojia yanayokuwa kwa kasi.

Mbali na hayo Waziri Nape amesema kuwa Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) ipo katika hatua za mwisho za kuandaa kanuni za kudhibiti masuala ya matumizi ya mitandao ya kijamii nchini.

Katika hatua hiyo Waziri Nape amewataka wadau mbalimbali kutoa maoni ili kusaidia kuboresha kanuni za mitandao ya kijamii kwa lengo ili kukuza tasnia ya habari.

Hata hivyo, Waziri Nape ameahidi kuendelea kushirikiana na vyombo vya habari nchini katika kutoa habari kwa ajili ya kuhabarisha umma kuhusiana na mambo mbalimbali yahusuyo Serikali katika kutekeleza majukumu yake.

“Kwa yeyote atakayepata changamoto ya aina yeyote kutoka kwa watumishi wa Serikali ikiwemo ya upatikanaji wa habari milango ipo wazi katika kurepoti changamoto hiyo” alisisitiza Waziri Nape.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye yupo katika ziara ya kutembelea vituo vya Televisheni kujionea utendaji kazi wa vituo hivyo ikiwa pamoja na changamoto zilizopo ili kupata namna bora ya kuiendeleza sekta ya habari kwa manufaa ya taifa, mpaka sasa ameshatembelea Kampuni nane za vyombo vya habari.

WANANCHI WATAKIWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUPIGA KURA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI NA UBUNGE

0
0


Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage (Katikati) akitoa Risala kuhusu upigaji wa Kura katika uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Dimani Zanzibar na Kata 19 za Tanzania Bara leo mjini Zanzibar. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar, Mhe. Hamid M. Hamid na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa NEC, Bw. Emmanuel Kawishe (Kulia).




Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa NEC, Bw. Emmanuel Kawishe (Kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu masuala ya Kisheria ya kuzingatiwa na wapiga Kura, Mawakala wa Vyama vya Siasa wakati wa Uchaguzi mdogo wa Ubunge na Udiwani utakaofanyika kesho, Januari 22, 2017. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa NEC, Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage.

Waandishi wa Habari wakiuliza maswali mbalimbali wakati wa Mkutano huo. 


Na. Aron Msigwa –NEC, Zanzibar.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewataka wananchi wanaoishi katika kata 19 zitakazofanya Uchaguzi mdogo wa Madiwani kwa upande Tanzania Bara na Ubunge katika jimbo la Dimani Zanzibar, Januari 22, 2017 wajitokeze kwa wingi kupiga kura kuwachagua viongozi wanaowataka watakaowaongoza kwa kipindi cha miaka 3.

Akizungumza na vyombo vya Habari leo mjini Zanzibar, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Rufaa, Mhe. Semistocles kaijage amesema kuwa maadalizi ya Uchaguzi huo yamekamilika na wananchi wote wenye sifa za kupiga kura katika uchaguzi wajitokeze wingi kutimiza wajibu wao wa Kikatiba.

Mhe. Kaijage amewapongeza wananchi wanaoishi katika Jimbo la Dimani, Zanzibar na wale wa Kata 19 za Tanzania Bara watakaofanya uchaguzi mdogo hapo kesho (Januari 22, 2017) kwa utulivu waliouonyesha katika kipindi chote cha Kampeni za wagombea wa vyama mbalimbali vya Siasa.

Amesema licha ya kuwepo kwa dosari za hapa na pale zilizojitokeza zikiwemo za ukiukwaji wa Maadili ya Uchaguzi kwa baadhi ya Vyama na wagombea wao, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilichukua hatua za kukemea vitendo hivyo ili kuwezesha Kampeni za Uchaguzi kufanyika kwa Usalama na Amani.

“Licha ya kwamba kutakuwa na ulinzi wa kutosha katika vituo vya kupigia kura, Ni matumaini ya Tume kuwa hali ya Amani na Utulivu ambayo imekuwepo hadi sasa na kama ilivyokuwa katika Chaguzi zilizopita itaendelea kudumishwa ili kuhakikisha uchaguzi huu unafanyika kwa Utulivu, Amani na Ustawi wa Taifa letu” Amesema Jaji Kaijage.

Ameeleza kuwa katika uchaguzi huo jumla ya Wapiga Kura 9,280 wa Jimbo la Dimani Zanzibar wanatarajiwa kupiga kura ili kumchagua Mbunge atakayewaongoza kwa kipindi cha miaka 3 kupitia vituo 29 vya Kupigia Kura katika Jimbo hilo. 

Kwa upande wa Uchaguzi Mdogo wa Madiwani katika Kata 19 za Tanzania Bara Wapiga Kura 134,705 walioandikishwa wanatarajia kupiga kura katika vituo 359 ambavyo vilitumika katika Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. 

“Naomba nitumie fursa hii kutoa rai kwa wananchi waliojiandikisha wajitokeze kwenye vituo vilivyotumika wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ili waweze kupiga kura kuwachagua viongozi mnaowataka bila hofu, woga, wasiwasi au ushawishi” Amesisitiza.

Kuhusu mchakato mzima upigaji wa kura ikiwemo taratibu za kuzingatiwa na wananchi kwenye vituo vya kupigia Kura, uhesabuji wa Kura, ujumlishaji wa Kura na Utangazaji wa matokeo amesema kuwa hatua zote zitafanywa na Wasimamizi wa Uchaguzi kwa kuzingatia Sheria.

Amesema kuwa siku ya uchaguzi Januari 22, 2017 vituo vyote vitafunguliwa saa 1:00 asubuhi na kufungwa saa 10:00 jioni na kufafanua kuwa iwapo wakati wa kufunga Kituo watakuwepo Wapiga Kura katika mstari ambao wamefika kabla ya saa kumi jioni na hawajapiga wataruhusiwa Kupiga Kura. 

Jaji Semistocles amesisitiza kwamba mtu yeyote hataruhusiwa kujiunga katika mstari wa Wapiga Kura baada ya saa kumi (10:00) jioni muda ulioainishwa kisheria.

Ameeleza kuwa kwa kila mpiga kura katika jimbo hilo akumbuke kubeba Kadi yake ya Mpiga Kura kwa kuwa Sheria ya Uchaguzi inaelekeza kuwa ili Mpiga Kura aruhusiwe kupiga kura ni lazima awe na kadi ya Mpiga Kura. 

“ Naomba ieleweke wazi kuwa Fomu Na. 17 sio mbadala wa Kadi ya Mpiga Kura, Wapiga Kura ambao wana Kadi ya Mpiga Kura lakini taarifa zao hazimo katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Kituoni, hawataruhusiwa kupiga kura” Amesisitiza Jaji Kaijage.

Amesema kuwa ni marufuku na ni kosa la jinai kumkataza mtu kwenda Kupiga Kura akisisitiza kwamba siku hiyo ya kupiga kura kipaumbele kitatolewa kwa wagonjwa, watu wenye ulemavu, wanawake wajawazito au wenye watoto wachanga na wazee ambao hawatatakiwa kupanga mstari. 

Jaji Semistocles amefafanua kuwa wakati wote wa Kupiga Kura na Kuhesabu Kura, Mawakala wa Vyama vya Siasa watakuwepo kwenye vituo kwa kuwa wajibu wao ni kulinda maslahi ya Vyama vyao vya Siasa na Wagombea wao.Hata hivyo amesema hawatakiwi kuingilia masuala ya utendaji ambayo yamekabidhiwa kwa Msimamizi wa Kituo.

Amesema Mawakala hao wataruhusiwa kuwepo Vituoni kwa mujibu wa Sheria na Kanuni na kusisitiza kwamba Wakala asiyekuwa na barua ya utambulisho kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi na ambaye hatakula kiapo cha kutunza siri hataruhusiwa kuingia katika Kituo cha Kupigia, Kuhesabia na Kujumlishia Kura.

Katika hatua nyingine Jaji Kaijage amebainisha kuwa Kura zilizopigwa zitahesabiwa katika Kituo cha Kupigia Kura mara tu Upigaji Kura utakapokamilika na matokeo husika ya Kituo kujazwa kwenye Fomu za Matokeo Na. 21B kwa upande wa Ubunge na Fomu Na. 21C kwa upande wa Udiwani kisha fomu hizo kutiwa saini na Msimamizi wa Kituo/Msimamizi Msaidizi wa Kituo, Mawakala wa Vyama au Mgombea aliye Kituoni. 

Amesema nakala moja watapewa Mawakala/Mgombea na nakala nyingine itabandikwa nje ya Kituo cha Kuhesabia kura ambapo Wakala wa kila Chama cha Siasa na mlinzi wa Kituo watakaokuwa Kituoni wataruhusiwa kusindikiza msafara wa kupeleka matokeo ya Uchaguzi kwenda kwa Msimamizi wa Uchaguzi/Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Kata kwa upande wa Tanzania Bara na kwa Msimamizi wa Uchaguzi/Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Dimani kwa upande wa Zanzibar. 

Amefafanua kuwa matokeo yote yakishapokelewa na Msimamizi wa Uchaguzi kwa upande wa Uchaguzi wa Ubunge na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi kwa upande wa Uchaguzi wa Udiwani, yatajumlishwa mbele ya Mawakala na wote wanaoruhusiwa kuingia kwenye vituo vya Kujumlishia Kura.

“ Kama ilivyokuwa wakati wa Kuhesabu Kura, baada ya Ujumlishaji kukamilika matokeo ya Ubunge ngazi ya Jimbo yatajazwa katika Fomu Na. 24B na yale ya Diwani katika Kata yatajazwa katika Fomu Na. 24C, Fomu za Matokeo hayo zitatiwa saini na Msimamizi wa Uchaguzi na Mawakala watakaokuwepo watapewa nakala za Fomu za Matokeo na Nakala moja itawekwa mahali pa wazi nje ya Kituo cha Kujumlisha Kura” 

Akitoa ufafanuzi kuhusu kampeni za uchaguzi huo amesema zitamalizika leo (Januari 21) saa 12 jioni na Vyama, Wagombea na mashabiki hawataruhusiwa kufanya kampeni za aina yoyote ikiwa ni pamoja na kutumia alama zozote zinazoashiria Kampeni kama vile bendera na mavazi ya vyama vyao.

Kuhusu uwazi katika uendeshaji wa uchaguzi huo amefafanua kuwa vyama vyote vya Siasa vinavyoshiriki katika Uchaguzi vinatakiwa kuhakikisha kwamba vinaweka Mawakala katika vituo vyote vya Kupigia Kura na Kujumlishia Kura ambao watatimiza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa. 

Jaji Kaijage amesisitiza kuwa kwa kuzingatia Maadili ya Uchaguzi ya mwaka 2015 yaliyokubaliwa na Vyama vyote vya Siasa, Wapiga Kura wanatakiwa kuondoka Vituoni mara baada ya kupiga kura ili kuendelea na shughuli zao kwa kuwa Vyama vya Siasa vyenye wagombea vitakuwa na Mawakala vituoni ambao watalinda maslahi ya Vyama na Wagombea wao huku watu waliotajwa kwenye Sheria ya Uchaguzi wakiwemo Wagombea, Mawakala, Afisa wa Tume, Msimamizi wa Uchaguzi na Afisa Usalama ndiyo watakaoruhusiwa kuingia kwenye Vituo vya Kupigia, Kuhesabia na Kujumlishia Kura.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria wa NEC, Bw. Emmanuel Kawishe amewaaeleza waandishi wa Habari kuwa kwa mujibu wa sheria mwenye mamlaka ya kumtangaza Mshindi ngazi ya Ubunge ni Msimamizi wa Uchaguzi na kwa ngazi ya Udiwani mwenye mamlaka ya kufanya hivyo ni Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi.

Amesema kuwa zoezi la Kupiga Kura, Kuhesabu kura ,Kujumlisha Matokeo na Kutangaza matokeo litafanywa kwa uwazi na kwa kuzingatia Sheria na kutoa wito kwa wananchi wajitokeze kwa wingi kuwachagua viongozi wao.

Amesema kuwa wananchi watakaoruhusiwa kupiga kura ni wale wenye sifa ambao watakuwa na kadi za kupigia kura na ambao majina yao yameonekana kwenye Daftari la kudumu la kupigia Kura na kusisitiza kwamba mwananchi ambaye jina lake halitakuwa kwenye Daftari la Kudumu la kupigia kura hataruhusiwa kupiga kura.

“Utaratibu wa kupiga kura umeelezwa katika Sheria, Ukisoma kifungu cha 63 kifungu kidogo cha 3 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi A, kinaeleza wazi mwananchi anapofika kituoni alipopangiwa na Tume anaonyesha kadi yake ya kupigia kura na kisha jina lake linaitwa kwa sauti na ikiwa amekidhi sifa anaruhusiwa kupiga kura asipokidhi sifa Msimamizi wa Uchaguzi anayo Mamlaka ya kumzuia asipige Kura” Amesema.

UHUSIANO WA TANZANIA NA CHINA UNACHOCHEA UCHUMI – MAMA SAMIA.

0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni 70 na laki nne kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi Chato kutoka kwa Balozi wa China nchini Dkt. Lu Youqing wakati wa hafla ya uzinduzi wa sherehe za maadhimisho ya Mwaka Mpya wa China leo jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam leo wakati hafla ya kufungua sherehe za maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Jamhuri ya watu wa China.China inasherehekea Mwaka Mpya ambapo mwaka huu umepewa jina la Jogoo (Rooster).
Balozi wa China nchini Tanzania Balozi Dkt. Lu Youqing akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa sherehe za maadhimisho ya Mwaka Mpya wa China leo jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan (wapili kutoka kulia) akiwaongoza viongozi na wananchi kuimba wimbo wa Taifa wakati wa hafla ya uzinduzi wa sherehe za maadhimisho yam waka mpya wa China leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye, Balozi wa China nchini Dkt. Lu Youqing na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akimsikiliza kwa makini Balozi wa China nchini Dkt. Lu Youqing wakati wa hafla ya uzinduzi wa sherehe za maadhimisho ya Mwaka Mpya wa China leo jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye mara baada ya kuwasili katika viwanja vya mnazi mmoja kwa ajili ya kufungua sherehe za maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Jamhuri ya watu wa China leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga.
 

Baadhi ya vikundi mbalimbali vya burudani kupitia Sanaa wakionyesha umahiri wao wakati wa hafla ya uzinduzi wa sherehe za maadhimisho ya Mwaka Mpya wa China leo jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni 70 na laki nne kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi Chato kutoka kwa Balozi wa China nchini Dkt. Lu Youqing wakati wa hafla ya uzinduzi wa sherehe za maadhimisho ya Mwaka Mpya wa China leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa maadhimisho hayo wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea katika hafla ya kuadhimisha mwaka mpya wa China leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa maadhimisho hayo wakitembelea baadhi ya mabanda yaliyopo katika viwanja vya Mnazi Mmoja ikiwa ni sehemu ya maadhimisho yam waka mpya wa China leo jijini Dar es Salaam. China wanasherehekea mwaka mpya leo na kesho katika viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 11 jioni.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali ya Tanzania na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing baada ya kumalizika kwa hafla ya uzinduzi wa sherehe za maadhimisho ya Mwaka Mpya wa China leo jijini Dar es Salaam.Maadhimisho hayo yanafanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia saa 4;00 asubuhi hadi saa 11 jioni na yanatarajiwa kumalizika kesho tarehe 22 Januari 2017.



Picha zote na: Frank shija & Shamimu Nyaki

TANZANIA KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI KUHARAKISHA MAENDELEO YA NCHI

0
0
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kushoto), akiwa katika mazungumzo na mgeni wake ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, walipokutana Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (katikati) pamoja na maafisa waandamizi wa Wizara hiyo wakiwa katika mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es salaam.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, (kulia) akisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (hayupo pichani) wakati wa mazungumzo kati yao yaliyofanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dares salaam ambapo IMF imeipongeza Tanzania kwa kusimamia vizuri ukuaji wake wa uchumi.
Ujumbe wa Tanzania na Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF wakiwa katika mazungumzo Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam, ambapo Shirika hilo limeahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania ili kufikia maendeleo inayoyatarajia kwa manufaa ya Taifa na wananchi wake kiuchumi na kijamii.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, (kulia) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (hayupo pichani), Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dares salaam ambapo IMF imeipongeza Tanzania kwa kusimamia kikamilifu ukuaji wake wa uchumi.
Mkurugenzi wa Idara ya Sera wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Ollal, akisisitiza jambo wakati wa mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, walipokutana Makao Makuu ya Wizara hiyo, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akizungumza jambo na mgeni wake ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, (hayupo pichani), Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akizungumza jambo na mgeni wake ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, (hayupo pichani), Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kushoto), akiagana na mgeni wake ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati yao yaliyofanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es salaam, ambapo IMF, imesifu jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano, katika kusimamia na kukuza uchumi wa Taifa.
……………..

Benny Mwaipaja,WFM-Dar es salaam



SERIKALI imesema kuwa inatambua mchango mkubwa wa sekta binafsi katika kukuza uchumi wa nchi na kuahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano na sekta hiyo ili kuharakisha maendeleo ya wananchi kupitia sekta ya viwanda na biashara.

Hayo yamesema na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, alipokutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es salaam.

Amesema kuwa uchumi wa nchi unategemea sana sekta binafsi yenye nguvu na yenye utulivu ambayo itachangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya nchi kwa njia ya uwekezaji na ulipaji kodi.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, amesema kuwa Shirika lake limeridhika na kiwango kikubwa cha ukuaji wa uchumi wa Tanzania miongoni mwa nchi za Afrika na kwamba wanatarajia kuona uchumi huo ukiendelea kukua zaidi kwa ushirikiano na sekta binafsi.

Ametaja sifa za ukuaji huo kuwa ni pamoja na kuimarishwa kwa ukusanyaji wa kodi, udhibiti wa mfumuko wa bei na thamani ya shilingi, uwajibikaji na pamambano dhidi ya rushwa, ufisadi, na utekelezaji mzuri wa Bajeti ya serikali.

Hivi karibuni Bodi ya Wakurugenzi ya IMF ilitoa taarifa yake ya mapitio ya mwenendo wa uchumi wa Tanzania na kueleza kuridhika kwake na uimara wa uchumi huo baada ya kutoyumba katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016 na kueleza kuwa utaendelea kukua kwa wastani wa asilimia 7 kama ilivyopangwa.

Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani ni chombo cha kimataifa kinachosaidia ukuaji wa uchumi wa nchi wanachama wake kwa kuweka mikakati na kuzikopesha fedha kwaajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo ya kiuchmi na kijamii ikiwemo, elimu, afya, miundombinu, nishati na miradi mingine kadha wa kadha.

KINANA AMNADI MGOMBEA UDIWANI NGARENANYIUKI LEO

0
0
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimnadi mgombea Udiwani katika kata ya Ngarenanyuki, Arumeru mkoani Arusha, Mwalimu Zakaria Nnko, wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata hiyo, uliofanyika katika uwanja wa shule ya Ngarenanyuki, leo Januari 21, 2017. (Picha na Bashir Nkoromo)

KINANA: CHAGUENI VIONGOZI WATAKAOWASAIDIA SIYO WATAKAOSHUGHULIKA NA SHIDA ZA MATUMBO YAO

0
0
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimnadi mgombea Udiwani kata ya Ngarenanyuki, Arumeru mkoani Arusha, Mwalimu Zakaria Nnko, wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata hiyo, uliofanyika kwenye Viwanja vya Mpira vya Shule ya Ngarenanyuki, leo Januari 21, 2017.

Akimnadi Mgombea huyo, Kinana amewataka Watanzania kujenga tabia ya kuchagua  viongozi watakaowasaidia na kuacha kuchagua ambao wakishapata madaraka wanashughulikia shidao za matumbo yao badala ya shida za wananchi waliowachagua.

Alisema, baadhi ya wa wananchi wamekuwa hawatazami sifa na uwezo wa mgombea atakayewatumikia, badala yake kuchagua kwa kukurupuka kuchagua viongozi ambao baadaye hawawasaidii kutatua kero zao, na hivyo kubaki wanalalamikia serikali kuwa haiwahudumii.

Kinana aliwataka wananchi wa Kata ya Ngarenanyuki kumchagua Mwalimu Nnko, akimwelezea kuwa anamtambua vyema kuwa ni mchapakazi na ni mtu ambaye ameridhika na maisha hivyo anagombea ili kuwasidia wanannchi na siyo kujisaidia yeye kuneemesha tumbo lake.

Uchaguzi mdogo unafanyika katika maeneo mbalimbali nchini, kujaza nafasi zilizobaki wazi kuokana na sababu mbalimbali zilizofanya madiwani na wabunge wlioshinda kutokuwepo. Uchaguzi huo unafanyika chini ya usimamizi wa tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipokea saluti ya Kijana wa CCM, aliyempa saluti hiyo ya heshima baada ya kumvalisha skafu alipowasili kwenye Viwanja vya Mpira ya Shule ya Msingi Ngarenanyuki, kufunga kampeni hizo leo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasalimia ananchi baada ya kumvalisha skafu alipowasili kwenye Viwanja vya Mpira ya Shule ya Msingi Ngarenanyuki, kufunga kampeni hizo leo
Wananchi wakiwa na ujumbe kwnye mabango ambapo alisema wakimchagua mgombea wa CCM, CCM itamsukuma mgombea huyo kuhakikisha wanakopehwa bodaboda
Wananchi wakimshangilia Kinana kwenye mkutano huo
Baadhi ya watu mbalimbali waliohudhuria mkutanohuo
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akisalimia wananchi kwenye mkutano huo
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Lekule Laizer akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kumnadi Mgombea na kisha kufunga kampeni hizo
Vijana wakiwa kwenye mtiilikufaidi vizuri mkutano huo
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akihutubia mkutanohuo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimnadi mgombea Udiwani katika kata ya Ngarenanyuki, Arumeru mkoani Arusha, Mwalimu Zakaria Nnko, wakati wa mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata hiyo, uliofanyika kwenye Viwanja vya  Mpira vya shule ya Ngarenanyuki, leo Januari 21, 2017. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

WACHINA WASHEHEREKEA MWAKA MPYA WAO KATIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia  wakati wa maadhimisho ya sherehe za mwaka mpya wa Jamhuri ya Watu wa China zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja  jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea hundi ya shilingi milioni 70 kutoka kwa  Balozi wa China nchini Mhe. Dk. Lu Youqing iliyotolewa na Taasisi pamoja na Jumuiya ya Wachina wanaoishi Tanzania kuchangia shule ya msingi ya Chato iliyopo mkoani Geita wakati wa maadhimisho ya sherehe za mwaka mpya wa kichina zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja  jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na wageni wengine waalikwa pamoja na wasanii waliotumbuiza wakati wa maadhimisho ya sherehe za mwaka mpya wa kichina zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja  jijini Dar es Salaam.
 Sehemuya watu waliohudhuria sherehe za mwaka mpya wa Kichina zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa China nchini Mhe. Dk. Lu Youqing wakati wa maadhimisho ya sherehe za mwaka mpya wa Kichina zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja  jijini Dar es Salaam
                                  ......................................................................................... 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Tanzania itaendelea kudumisha,kuimarisha na  kuendeleza mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na China kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa pande hizo MBILI.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam katika sherehe ya maadhimisho ya mwaka mpya wa Kichina hapa nchini sherehe ambazo zimehudhuriwa na mamia ya raia wa China na Tanzania.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa China imekuwa mshirika na mdau mkubwa wa maendeleo hapa nchini na hali hiyo inatokana na mahusiano mema na mazuri yaliyopo kati ya nchi hizi Mbili.


Makamu wa Rais amemhakikishia Balozi wa China hapa nchini Dkt Lu Youqing kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli itakuwa bega kwa bega na serikali ya China hasa katika uimarishaji wa sekta za biashara, utamaduni, elimu, afya  na masuala ya kijeshi kwa ajili ya maslahi na ustawi wa wananchi wa Tanzania na China.
Makamu wa Rais amesisitiza kuwa Tanzania itaendelea kujifunza mambo mengi kutoka China ili kuharakisha shughuli za maendeleo za wananchi kutokana na Taifa la China kupiga hatua kubwa ya kimaendeleo.


Amehimiza ubadilishanaji wa wataalamu kati ya Tanzania na China katika sekta mbalimbali kama hatua ya kuongeza kasi ya maendeleo kwa wananchi nchini.

Kwa Upande wake, Balozi wa China hapa nchini Dkt Lu Youqing amepongeza hatua zinachukuliwa na serikali ya Tanzania katika kupambana na rushwa na ufisadi.

Dkt  Lu Youqing amesema serikali ya China na raia wake wanafurahishwa na hatua hizo kwa sababu zinalenga kuondoa na kukomesha rushwa na ufisadi kwani tabia hizo zikiachwa ziendelee zinachangia kwa kiasi kikubwa kuzorotesha utoaji wa huduma bora na za msingi kwa wananchi.


 
 

Balozi huyo wa Tanzania hapa nchini Dkt  Lu Youqing pia amewashukuru wananchi wa Tanzania kwa kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Mnazi Moja katika kusheherekea sikukuu ya Mwaka mpya wa Kichina sherehe ambazo inapambwa na michezo mbalimbali ikiwemo sarakasi na vikundi vya ngoma asili kutoka China na maonyesho.
Katika Maadhimisho hayo, Balozi wa China nchini Tanzania Dkt  Lu Youqing amemkabidhi Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mfano wa hundi ya shilingi milioni 70 fedha ambazo zitatumika katika ujenzi kwenye shule ya msingi Chato iliyopo mkoani Geita.

WANANCHI WATAKIWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUPIGA KURA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI NA UBUNGE

0
0
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage (Katikati) akitoa Risala kuhusu upigaji wa Kura katika uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Dimani Zanzibar na Kata 19 za Tanzania Bara  leo mjini Zanzibar. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar, Mhe. Hamid M. Hamid na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa NEC, Bw. Emmanuel Kawishe (Kulia).


 Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa NEC, Bw. Emmanuel Kawishe (Kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu masuala ya Kisheria ya kuzingatiwa na wapiga Kura, Mawakala wa Vyama vya Siasa wakati wa Uchaguzi mdogo wa Ubunge na Udiwani utakaofanyika kesho, Januari 22, 2017. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa NEC, Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage.

 Waandishi wa Habari wakiuliza maswali mbalimbali wakati wa Mkutano huo.


Na. Aron Msigwa –NEC, Zanzibar.


Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewataka wananchi wanaoishi katika kata 19 zitakazofanya Uchaguzi mdogo wa Madiwani  kwa upande  Tanzania Bara na Ubunge katika jimbo la Dimani Zanzibar, Januari 22, 2017 wajitokeze kwa wingi kupiga kura kuwachagua viongozi wanaowataka watakaowaongoza kwa kipindi cha miaka 3.


Akizungumza na vyombo vya Habari leo mjini Zanzibar, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Rufaa, Mhe. Semistocles kaijage amesema kuwa maadalizi ya Uchaguzi huo yamekamilika na wananchi wote wenye sifa za kupiga kura katika uchaguzi  wajitokeze wingi kutimiza wajibu wao wa Kikatiba.


Mhe. Kaijage amewapongeza wananchi wanaoishi katika Jimbo la Dimani,  Zanzibar na wale wa Kata 19 za Tanzania Bara watakaofanya uchaguzi mdogo hapo kesho (Januari 22, 2017) kwa utulivu waliouonyesha katika kipindi chote cha Kampeni za wagombea wa vyama mbalimbali vya Siasa.


 Amesema licha ya kuwepo kwa dosari za hapa na pale zilizojitokeza zikiwemo za ukiukwaji wa Maadili ya Uchaguzi kwa baadhi ya Vyama na wagombea wao, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilichukua hatua za kukemea vitendo hivyo ili kuwezesha Kampeni za Uchaguzi kufanyika kwa Usalama na Amani.


“Licha ya kwamba kutakuwa na ulinzi wa kutosha katika vituo vya kupigia kura, Ni matumaini ya Tume kuwa hali ya Amani na Utulivu ambayo imekuwepo hadi sasa na kama ilivyokuwa katika Chaguzi zilizopita itaendelea kudumishwa ili kuhakikisha uchaguzi huu unafanyika kwa Utulivu, Amani na Ustawi wa Taifa letu” Amesema Jaji Kaijage.


Ameeleza kuwa katika uchaguzi huo  jumla ya Wapiga Kura 9,280 wa Jimbo la Dimani Zanzibar wanatarajiwa kupiga kura ili kumchagua Mbunge atakayewaongoza kwa kipindi cha miaka 3 kupitia vituo 29 vya Kupigia Kura katika Jimbo hilo.


Kwa upande wa Uchaguzi Mdogo wa Madiwani katika Kata 19 za Tanzania Bara Wapiga Kura 134,705 walioandikishwa wanatarajia kupiga kura  katika vituo 359 ambavyo vilitumika katika Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.


“Naomba nitumie fursa hii kutoa rai kwa wananchi waliojiandikisha wajitokeze kwenye vituo vilivyotumika wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ili waweze kupiga kura kuwachagua viongozi mnaowataka bila hofu, woga, wasiwasi au ushawishi” Amesisitiza.


Kuhusu mchakato mzima upigaji wa kura ikiwemo taratibu za kuzingatiwa na wananchi kwenye vituo vya kupigia Kura, uhesabuji wa Kura, ujumlishaji wa Kura na Utangazaji wa matokeo amesema kuwa hatua zote zitafanywa na Wasimamizi wa Uchaguzi kwa kuzingatia Sheria.


Amesema kuwa siku ya uchaguzi Januari 22, 2017 vituo vyote  vitafunguliwa saa 1:00 asubuhi na kufungwa saa 10:00 jioni na kufafanua kuwa iwapo wakati wa kufunga Kituo watakuwepo Wapiga Kura katika mstari ambao wamefika kabla ya saa kumi jioni na hawajapiga wataruhusiwa Kupiga Kura.


Jaji Semistocles amesisitiza kwamba mtu yeyote hataruhusiwa kujiunga katika mstari wa Wapiga Kura baada ya saa kumi (10:00) jioni  muda ulioainishwa kisheria.

Ameeleza kuwa kwa kila mpiga kura katika jimbo hilo akumbuke kubeba Kadi yake ya Mpiga Kura kwa kuwa Sheria ya Uchaguzi inaelekeza kuwa ili Mpiga Kura aruhusiwe kupiga kura ni lazima awe na kadi ya Mpiga Kura.


“ Naomba ieleweke wazi kuwa Fomu Na. 17 sio mbadala wa Kadi ya Mpiga Kura, Wapiga Kura ambao wana Kadi ya Mpiga Kura lakini taarifa zao hazimo katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Kituoni, hawataruhusiwa kupiga kura” Amesisitiza Jaji Kaijage.

Amesema kuwa ni  marufuku na ni kosa la jinai kumkataza mtu kwenda Kupiga Kura akisisitiza kwamba siku hiyo ya kupiga kura kipaumbele kitatolewa kwa wagonjwa, watu wenye ulemavu, wanawake wajawazito au wenye watoto wachanga na wazee ambao hawatatakiwa kupanga mstari.


Jaji Semistocles amefafanua kuwa wakati wote wa Kupiga Kura na Kuhesabu Kura, Mawakala wa Vyama vya Siasa watakuwepo kwenye vituo kwa kuwa wajibu wao ni kulinda maslahi ya Vyama vyao vya Siasa na Wagombea wao.

 Hata hivyo amesema hawatakiwi kuingilia masuala ya utendaji ambayo yamekabidhiwa kwa Msimamizi wa Kituo.


Amesema Mawakala hao wataruhusiwa kuwepo Vituoni kwa mujibu wa Sheria na Kanuni na kusisitiza kwamba Wakala asiyekuwa na barua ya utambulisho kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi na ambaye hatakula kiapo cha kutunza siri hataruhusiwa kuingia katika Kituo cha Kupigia, Kuhesabia na Kujumlishia Kura.


Katika hatua nyingine Jaji Kaijage amebainisha kuwa Kura zilizopigwa  zitahesabiwa katika Kituo cha Kupigia Kura mara tu Upigaji Kura utakapokamilika  na matokeo husika ya  Kituo kujazwa kwenye Fomu za Matokeo Na. 21B kwa upande wa  Ubunge na Fomu Na. 21C kwa upande wa  Udiwani kisha fomu hizo kutiwa saini na Msimamizi wa Kituo/Msimamizi Msaidizi wa Kituo, Mawakala wa Vyama au Mgombea aliye Kituoni. 


Amesema nakala moja watapewa Mawakala/Mgombea na nakala nyingine itabandikwa nje ya Kituo cha Kuhesabia kura ambapo Wakala wa kila Chama cha Siasa na mlinzi wa Kituo watakaokuwa Kituoni wataruhusiwa kusindikiza msafara wa kupeleka matokeo ya Uchaguzi kwenda kwa Msimamizi wa Uchaguzi/Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Kata kwa upande wa Tanzania Bara na kwa Msimamizi wa Uchaguzi/Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Dimani kwa upande wa Zanzibar.


Amefafanua kuwa matokeo yote yakishapokelewa na Msimamizi wa Uchaguzi kwa upande wa Uchaguzi wa Ubunge na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi kwa upande wa Uchaguzi wa Udiwani, yatajumlishwa mbele ya Mawakala na wote wanaoruhusiwa kuingia kwenye vituo vya Kujumlishia Kura.


“ Kama ilivyokuwa wakati wa Kuhesabu Kura, baada ya Ujumlishaji kukamilika matokeo ya Ubunge ngazi ya Jimbo yatajazwa katika Fomu Na. 24B na yale ya Diwani katika Kata yatajazwa katika Fomu Na. 24C, Fomu za Matokeo hayo zitatiwa saini na Msimamizi wa Uchaguzi na Mawakala watakaokuwepo watapewa nakala za Fomu za Matokeo na Nakala moja itawekwa mahali pa wazi nje ya Kituo cha Kujumlisha Kura”   


Akitoa ufafanuzi kuhusu kampeni za uchaguzi huo amesema zitamalizika leo (Januari 21)  saa 12 jioni na Vyama, Wagombea na mashabiki hawataruhusiwa kufanya kampeni za aina yoyote ikiwa ni pamoja na kutumia alama zozote zinazoashiria Kampeni kama vile bendera na mavazi ya vyama vyao.


Kuhusu uwazi katika uendeshaji wa uchaguzi huo amefafanua kuwa vyama vyote vya Siasa vinavyoshiriki katika Uchaguzi   vinatakiwa kuhakikisha kwamba vinaweka Mawakala katika vituo vyote vya Kupigia Kura na Kujumlishia Kura ambao watatimiza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa.


Jaji Kaijage amesisitiza kuwa kwa kuzingatia Maadili ya Uchaguzi ya mwaka 2015 yaliyokubaliwa na Vyama vyote vya Siasa, Wapiga Kura wanatakiwa kuondoka Vituoni mara baada ya kupiga kura ili kuendelea na shughuli zao kwa kuwa  Vyama vya Siasa vyenye wagombea vitakuwa na Mawakala vituoni ambao watalinda maslahi ya Vyama na Wagombea wao huku watu waliotajwa kwenye Sheria ya Uchaguzi wakiwemo Wagombea, Mawakala, Afisa wa Tume, Msimamizi wa Uchaguzi na Afisa Usalama ndiyo watakaoruhusiwa kuingia kwenye Vituo vya Kupigia, Kuhesabia na Kujumlishia Kura.


Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria wa NEC, Bw. Emmanuel Kawishe amewaaeleza waandishi wa Habari kuwa kwa mujibu wa sheria mwenye mamlaka ya kumtangaza Mshindi ngazi ya Ubunge ni Msimamizi wa Uchaguzi na kwa ngazi ya Udiwani mwenye mamlaka ya kufanya hivyo ni Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi.


Amesema kuwa zoezi la Kupiga Kura, Kuhesabu kura ,Kujumlisha Matokeo na Kutangaza matokeo litafanywa kwa uwazi na kwa kuzingatia Sheria na kutoa wito kwa wananchi wajitokeze kwa wingi kuwachagua viongozi wao.


Amesema kuwa wananchi watakaoruhusiwa kupiga kura ni wale wenye sifa ambao watakuwa na kadi za kupigia kura na ambao majina yao yameonekana kwenye Daftari la kudumu la kupigia Kura na kusisitiza kwamba mwananchi ambaye jina lake halitakuwa kwenye Daftari la Kudumu la kupigia kura hataruhusiwa kupiga kura.


“Utaratibu wa kupiga kura umeelezwa katika Sheria, Ukisoma kifungu cha 63 kifungu kidogo cha 3 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi A, kinaeleza wazi mwananchi anapofika kituoni alipopangiwa na Tume anaonyesha kadi yake ya kupigia kura na kisha jina lake linaitwa kwa sauti na ikiwa amekidhi sifa anaruhusiwa kupiga kura asipokidhi sifa Msimamizi wa Uchaguzi anayo Mamlaka ya kumzuia asipige Kura” Amesema.

NAIBU WAZIRI WAMBURA AONGOZA MAZOEZI UWANJA WA SAMORA IRINGA ASUBUHI YA LEO

0
0
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura (wa  tatu kutka  kushoto mwenye kikoi shingoni ) akizindua rasmi mazoezi  ya  viungo kwa  mkoa wa Iringa kama agizo la  serikali kila jumamosi ya pili ya  ya mwezi wananchi  wote kushiriki mazoezi ,kushoto kwake ni mbunge wa Kilolo Venance  Mwamoto  na kulia ni mbunge wa  viti maalum mkoa  wa Iringa Ritta Kabati (CCM) akifuatiwa na mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza (PICHA ZOTE NA MATUKIODAIMABLOG
 Katibu tawala wa  mkoa wa Iringa Wamoja  Ayub kulia  akifurahia mazoezi kulia kwake ni mbunge Mwamoto  na mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Amina Masenza


 Afisa habari  Manispaa ya  Iringa  Sima Bingieki wa  kwanza  kushoto   akishiriki mazoezi  leo uwanja  wa  samora
 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura wa  pili  kulia  akifurahia  mazoezi na mkuu wa  mkoa wa Iringa Amina Maasenza  wa kwanza  kulia
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura wa tatu kushoto na  viongozi mbali mbali wakiongozwa  kufanya mazoezi na Dc Iringa  Richard Kasesela
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura kulia akifanya mazoezi ya  viungo na mbunge  wa  viti maalum mkoa wa Iringa  Ritta Kabati  katika  uwanja  wa  samora  Iringa  leo
Watumishi  ofisi ya  mkuu wa Mkoa na  RPC Iringa  wakiwa katika mazoezi
Baadhi  ya  wananchi  wa mji  wa  Iringa  wakiwa  katika mazoezi  leo kutoka  uwanja  wa  samora  kuelekea  ofisi ya RC Iringa
Hivi ndivyo  wananchi  walivyoshiriki mazoezi  Iringa
Wananchi  walioshiriki mazoezi  wakiwasili  ofisi ya RC Iringa  wakitokea  Samora
Wananchi na  viongozi  walioshiriki mazoezi wakiingia  viwanja  vya RC Iringa
Kila  mmoja  afurahia mazoezi
Mazoezi  kwa  afya 
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura wa tatu kushoto na  viongozi mbali mbali wakiongozwa  kufanya mazoezi na Dc Iringa  Richard Kasesela,wa  kwanza  kushoto  ni mkuu  wa mkoa Iringa Amina Masenza ,mbunge wa viti wa  maalum mkoa  wa Iringa  Ritta Kabati ,mbunge  wa Kilolo Venance  Mwamoto na katibu tawala  mkoa  wa Iringa  wamoja  Ayub
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura akipongeza  wananchi  kwa  kuitikia mazoezi ,katikati ni mkuu wa  mkoa  wa Iringa Amina Masenza na mkuu wa  wilaya  Iringa Richard Kasesela
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia James Wambura mwenye kikoi shingoni akiongoza mazoezi  Iringa  leo
Mazoezi  ya  viungo  kwa afya  yakiendelea
Ni  Full mazoezi  Iringa
Diwani  mstaafu  wa Mtwivila Vitus Mushi katikati  akishiri mazoezi
Mpiga  picha maarufu  Iringa  Said Mnyalugendo  kushoto  akiwa katika mazoezi
Kamanda  wa  polisi  wa mkoa wa Iringa Julius Mjengi  kushoto akiwa na kamanda wa kikosi cha  zimamoto na uokoaji Bw  Komba wakishiriki mazoezi  leo
Mazoezi  kila mmoja kwa afya
Askari  wa FFU  wakishiriki mazoezi
Wananchi  walioshiriki mazoezi  wakimsikiliza naibu  waziri
Walioshiriki mazoezi  wakitoka  uwanja  wa Samora kwa mazoezi kurudi  ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa
Kamanda wa  polisi mkoa  wa  Iringa Julius Mjengi kulia akifurahia mazoezi na kamanda  wa kikosi cha zimamoto na uokoaji mkoa wa Iringa Bw Komba
Tupo  safi  askari  polisi  wakiwa katika mazoezi
mazoezi  kutoka  uwanja  wa  Samora  Iringa  kuelekea ofisi ya  mkuu wa mkoa wa Iringa
Mazoezi  kwa  afya  yanaweza  saidia  kupunguza magonjwa mbali mbali kama  Kisukari
Shughuli  nyingine  zasimama kupisha mazoezi ya  viugo Iringa
DC  Kasesela  akiongoza mazezi
Mazoezi  safi
Askari  polisi wakiwajibika kisawa sawa
 watumishi ofisi ya RC  Iringa Bw Shimwela  akiwajibika na  wenzake
Mbunge  Mwamoto  na  mkuu wa  mkoa  Masenza  wakifanya mazoezi
Mkuu  wa mkoa wa Iringa Amina Masenza na mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto  wakifurahia mazoezi
Mwenyekiti  wa UWT  Iringa  vijijini Shakra  Kiwanda na afisa  ushiriki  mkoa wa Iringa John Kiteve  wakiwa katika mazoezi
Mkuu  wa  wilaya ya  Iringa  Bw Kasesela  akiwatazama  viongozi  wenzake wakiendelea na mazoezi uwanja wa Samora leo

WAZIRI NAPE NNAUYE AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA ITALIA NCHINI.

0
0


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kulia) akisalimiana na Balozi wa Italia nchini Tanzania, Mhe. Roberto Mengoni wakati alipotembelewa ofisini kwake leo 21 Januari, 2017 Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kulia) akifanya mazungumzo na mgeni wake ambaye ni Balozi wa Italia nchini Tanzania, Mhe. Roberto Mengoni kuhusu mausuala mbalimbali ya habari ofisini kwake 21 Januari, 2017 Jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kulia) akifafanua baadhi ya masuala mbalimbali yanayohusiana na habari wakati alipofanya mazungumzo na Balozi wa Italia nchini Tanzania, Mhe. Roberto Mengoni ofisini kwake 21 Januari, 2017 Jijini Dar es Salaam.


Balozi wa Italia nchini Tanzania, Mhe. Roberto Mengoni (kushoto) akieleza masuala mbalimbali yanayohusiana na habari na utamaduni wa Italia wakati alipomtembelea Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye leo 21 Januari, 2017 Jijini Dar es Salaam.


Balozi wa Italia nchini Tanzania, Mhe. Roberto Mengoni (kushoto) akimpatia Kadi ya Mawasiliano Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye wakati alipomtembelea ofisini kwake leo 21 Januari, 2017 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA)

NAIBU MEYA ILALA AWATAKA WENYE VIWANDA KULINDA MASLAHI YA WAFANYAKAZI

0
0


Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala , Omary  Kumbilamoto akizungumza na wadau wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha dawa cha ZENUFA.



Mkurugenzi wa kiwanda cha Zenufa Laboratories Ltd,Hitesh Upret akizungumza na wadau wa wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho na muonekano wa alama mpya.



Afisa Tarafa Ilala , Edita Samson akizungumza kwa niaba ya mkuu wa Wilaya ya Ilala wakati wa uzinduzi wa nembo mpya ya dawa ya Zenufa.


Mkurugenzi mtendaji wa bohari ya Dawa nchini(MSD), Laurean Rugambwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa nembo mpya ya dawa ya Zenufa.


Na Humphrey Shao, Globu ya jamii

NAIBU Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti, Omary Kumbilamoto amewataka wenye viwanda kulinda maslahi ya wafanyakazi kabla ya serikali kuingilia kati.
Kumbilamoto amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa nembo mpya ya kiwanda cha dawa cha ZENUFA kilichopo kata ya Kipawa.

“tunashukuru kwa ujenzi wa kiwandahiki na kuweza kuongeza ajira kwa vijana wetu kama ilivyo sera ya serikali kuwa nchi ya viwanda lakini kikubwa ninacho waomba muweze kuangalia maslahi ya wafanyakazi kuliko kusubiri msumbuliwe na serikali”amesema Kumbilamoto.

Ametaja kuwa itakuwa jambo la aibu kuona mkuu wa mkoa au Meya ama Naibu Meya anakuja tena kiwandani hapa kwa ajili ya kuja kusuluhisha mgogoro wa kiwanda na wafanyakazi.

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa boahari ya dawa nchini, Raurean Rugambwa amesema kuwa serikali imejipanga kuakikisha inasaidina na wawekezaji wa viwanda vya dawa kwa kuwa hakikishia uakika wa soko.

Ametajakuwa kwa sasa serikali yako imekuwa ikiagiza dawa kwa asilimia 90% kutoka nje ya nchi kutokana na upungufu wa viwanda vya dawa hapa nchini.

Hivyo amewataka wawekezaji kujitokeza katika uwekezaji mpya wa viwanda vya dawa katika mpangomaalumu wa mashirikiano na serikali(PP).


wananchi na wadau waliofika katika uzinduzi huo wakifatilia kwa makini matukio yanayoendelea

Mkurugenzi wa kiwanda cha Zenufa Laboratories Ltd,Hitesh Upret akiwaonyesha wageni waliofika kiwandani hapo sehemu ya kiwanda hicho ambacho kinazalisha dawa aina ya Zenufa.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Dar es Salaam,Ramadhani Madabida akizungumza jambo na mmoja wa watumsihi kutoka MSD waliofika katika uzinduzi wa kiwanda hicho.

NHIF TANGA YATOA MIKOPO YA VIFAA TIBA NA UKARABATI KWENYE HOSPITALI NA VITUO VYA AFYA WENYE THAMANI YA MILIONI 559.2

0
0

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa Tanga (NHIF) umefanikiwa kutoamikopo ya vifaa tiba na ukarabati katika vituo vya afya na hospitalivyenye thamani ya Milioni 559.2.

Vituo ambavyo vilikopeshwa ni Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo,Hospitali za wilaya ya Korogwe, Lushoto, Handeni ikiwemo vituo vyaAfya Makorora, Kituo cha Afya Pongwe, Mikanjuni na Ngamiani.

Hayo yalisemwa hivi karibuni na Meneja wa Mfuko huo mkoani hapa, AllyMwakababu (Pichani Juu)wakati akielezea taarifa ya utendaji kwa waandishi wa habarimjini hapa

Alisema baadhi ya vituo vya afya  vilivyokopeshwa na mfuko huo katiyao vinne vimemaliza kurejesha mikopo yao ambavyo ni Hospitali yawilaya ya Pangani,Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo (mkopo waawali) na kituo cha Afya cha Besha na Makorora ambapo ni mkopo wa
awali.

Meneja huyo alisema licha ya kuwepo kwa uhamasishaji mkubwa
wanaoufanya lakini vituo vingi havijachangamkia fursa hiyo ya mikopoya vifaa tiba, ukarabati wa majengo na dawa.

“Hivyo nivisihi vituo kujitokeza kuchangamkia fursa hii ya mikopo yavifaa tiba, ukarabati wa majengo na dawa kwenye maeneo yao “AlisemaMeneja huyo.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

DKT SHEIN AFUNGA KAMPENI ZA CCM LEO

0
0
Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohameed Shein, akimtambulisha Mgombea wa Ubunge Jimbo la Dimani CCM Zanzibar,Juma Ali Juma wakati wa ufungaji wa kampeni za Uchaguzi mdogo wa Ubunge wa jimbo hilo uliofanyika leo katika viwanja vya mpira Fuoni.(Picha na Othman Maulid).
KUU CC 2
Baadhi ya Wanachama cha Mapinduzi CCM Jimbo la Dimani wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar alipokuwa akizungumza katika ufungaji wa Kampeni za CCM za Uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo Dimani  leo katika uwanja wa Mpira Fuoni  Mkoa wa Mjini Magharibi .
KUU CC 3
 
Maelfu ya  Wanachama cha Mapinduzi CCM Jimbo la Dimani wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar alipokuwa akizungumza nao leo katika ufungaji wa Kampeni za CCM za Uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo Dimani katika uwanja wa Mpira Fuoni  Mkoa wa Mjini Magharibi.
KUU CC 4
 Wanachama wa Chama cha  Mapinduzi CCM Jimbo la Dimani wakinyanyua mikono juu kuunga mkono Hotuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar alipokuwa akizungumza katika ufungaji wa Kampeni za CCM za Uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo Dimani  leo katika uwanja wa Mpira Fuoni  Mkoa wa Mjini Magharibi.
KUU CC 5
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar alipokuwa akizungumza na Wanachama wa Chama cha  Mapinduzi CCM  katika ufungaji wa Kampeni za CCM uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo Dimani  leo katika uwanja wa Mpira Fuoni  Mkoa wa Mjini Magharibi ,.

KUU CC
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar akisalimiana na Mgombea Ubunge Jimbo la Dimani Juma Ali Juma wakati alipowasili katika Viwanja vya Mpira Fuoni Mjini Magharibi katika Ufungaji wa Kampeni za CCM za Uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo hilo leo.
KUU CC 1
 Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akisalimiana na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid wakati alipowasili katika Viwanja vya Mpira Fuoni Mjini Magharibi katika Ufungaji wa Kampeni za CCM za Uchaguzi mdogo wa Ubunge Jimbo la Dimani zilizofanyika leo.

NAIBU WAZIRI MASAUNI ATEMBELEA MAKAO MAKUU YA JESHI LA POLISI JIJINI MBEYA

0
0
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(wapili kulia), akifurahia jambo wakati alipotembelea makazi ya mbwa wanaotumika na Jeshi la Polisi katika masuala ya ulinzi na usalama.Baada ya Naibu Waziri ni Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya,Emmanuel Lukula.

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akipanda mti katika makazi ya mbwa wanaotumika katika masuala ya ulinzi na usalama na Jeshi la Polisi.Naibu Waziri yupo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na maafisa wa Jeshi la Polisi alipowasili Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kubaini mafanikio na changamoto za jeshi hilo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisikiliza maelezo juu ya gari lililokamatwa likisafirisha wahamiaji haramu kutoka kwa Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Benjamini Kaizaga(aliyenyoosha mkono).Naibu Waziri yupo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(watatu kushoto), akisikiliza maelezo kutoka kwa Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Benjamini Kaizaga, juu ya gari lililokamatwa likisafirisha madawa ya kulevya.Wengine mstari wa mbele ni Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Mbeya Emmanuel Lukula(wapili kulia) na Naibu Kamishna wa Uhamiaji,Asumsio Achachaa .Naibu Waziri yupo jijini Mbeya kwa ziara ya kikazi.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

BARABARA YA NJOMBE-MAKETE KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI-MAJALIWA

0
0
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Iwawa wilayani  Makete wakimwimbia Waziri mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipokwenda shuleni hapo kufungua madarasa   yao Januari 21, 2017.
OG
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Iwawa iliyopo Makete kabla ya kufungua madarasa  ya shule hiyo Januari 20,1, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
OG 5
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Iwawa ya Makete,  Novatus Msivala  kwenda kufungua madarasa  ya shule hiyo Januari 21, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
1OG 3
Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa  akifungua madarasa  ya shule ya Sekondari ya Iwawa  iliyopo Makete Januari 21, 2017.. (Picha na Ofisiya Waziri Mkuu)
NJO 1
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka wakiwa wameketi kwenye madawati ya moja kati ya madarasa mawili mapya yaliyofunguliwa na Waziri Mkuu katika shule ya sekondari ya Iwawa iliyopo Makete Januari 21, 2017.  Katikati ni Mbunge wa Makete, Norman Sigala., (Picha na Ofisi ya  Waziri Mkuu)
OG 2
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole  Sendeka (kulia kwake ) na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Njombe, Deo Sanga kukagua maeneo ya shule ya sekondari ya Iwawa wilayani Makete  baada ya kufungua madarasa ya shule hiyo Januari 21, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
OG 1
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na walimu wa shule ya sekondari ya Iwawa iliyopo Makete baada ya kufungua madarasa  ya shule hiyo Januari 21, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
OG
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa  Njombe wakati alipokagua ujenzi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Njombe katika eneo la Wikichi katika  Wilaya  ya Njombe Januari 21, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
NJO
 Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Iwawa wilayani  Makete wakimwimbia Waziri mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipokwenda shuleni hapo kufungua madarasa   yao Januari 21, 2017. (Picha na ofisi  ya Waziri Mkuu
NJO 1 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka wakiwa wameketi kwenye madawati ya moja kati ya madarasa mawili mapya yaliyofunguliwa na Waziri Mkuu katika shule ya sekondari ya Iwawa iliyopo Makete Januari 21, 2017.  Katikati ni Mbunge wa Makete, Norman Sigala., (Picha na Ofisi ya  Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema katika mwaka huu wa fedha Serikali imetenga sh. bilioni 19 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Njombe-Makete yenye urefu wa kilomita 109.4 kwa kiwango cha lami.
Ametoa kauli hiyo jana  (Ijumaa, Januari 20, 2017) wakati akizungumza na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete alipowasili katika kata ya Mtamba wilayani hapa akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Njombe.
Waziri Mkuu amesema usanifu wa kina wa barabara ya Njombe-Makete kwa ujenzi wa kiwango cha lami umekamilika hivyo amewataka wananchi waendelee kuwa na subira.
Amesema barabara nyingine inayotarajiwa kujengwa ni ya kutoka Makete hadi Mbeya kupitia Isyonji yenye urefu wa kilomita 96 ambayo imetengewa sh. milioni 50 kwa ajili ya kufanyiwa usanifu.
Waziri Mkuu amesema wananchi waendelee kushirikiana na Serikali kwani imedhamiria kuwatumikia kwa kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili katika maeneo yao.
Aidha, Waziri Mkuu amewataka wahandisi wa wilaya hiyo kuhakikisha wanawasimamia vizuri wakandarasi wanaojenga miradi mbalimbali katika halmashauri zao kuhakikisha kama viwango vinalingana na thamani halisi ya fedha zinazotolewa.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliwataka wakuu wa Idara katika halmashauri kupambana na vitendo vya rushwa na wahakikishe watumishi hawatowi huduma kwa kuomba rushwa.
“Kwanza watumishi watambue kwamba rushwa ni dhambi. Pia kiutumishi ni makosa makubwa hivyo wajiepushe na vitemdo hivyo,” amesema.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Makete Bi. Veronica Kessy amesema kujengwa kwa barabara hizo kwa kiwango cha lami kutaimarisha ukuaji wa uchumi wa wilaya hiyo na Mkoa wa Njombe kiujumla hivyo wananchi kupata tija.
“Mfano barabara ya kutoka Makete hadi Mbeya kupitia Bulongwa, Iniho, Kikondo na Isyonje itasaidia wilaya kufunguka hivyo kurahisisha usafirishaji wa mazao ya misitu kama mbao,” amesema.
Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya amesema barabara hii pia itaunganisha Wilaya hiyo na kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Songwe hivyo watapata fursa ya kuanzisha kilimo cha maua. Awali walishindwa kulima maua kwa sababu hakukuwa na usafiri wa uhakika.
Awali Waziri Mkuu alitembelea shamba la mifugo la Kitulo linalomilikiwa na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi lenye jumla ya Ng’ombe 750 wakiwemo ndama 61, majike 212, mitamba 273, madume 21, na madume wadogo 183.
Shamba hilo linazalisha wastani wa lita 450,000 za maziwa kwa mwaka kutokana na ng’ombe 123 wanaokamuliwa. 
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI, JANUARI 21, 2017.

Newz alert:Rais Dkt.Magufuli amteua Anne Kilango Malecela kuwa Mbunge

0
0


WATUMISHI MKOANI SINGIDA WAAGIZWA KULIMA MAZAO YANAYOTUMIA MAJI KWA UFANISI

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi akipanda mbegu bora ya mbaazi inayozalishwa katika shamba la Mpambaa halmashauri ya Singida, anayefuata ni Mwenyekiti wa halmashauri ya Singida Eliya Digha.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi akionyesha mbegu bora ya muhogo aina ya Momba inayozalishwa katika shamba la Mpambaa halmashauri ya Singida, katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo na anayefuata ni Afisa Kilimo halmashauri ya Singida Abel Mungale.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi akiandaa mashimo ya kupanda mbegu bora ya mbaazi inayozalishwa katika shamba la Mpambaa halmashauri ya Singida.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi akiwaonyesha watumishi wa halmashauri namna ya kupanda mbegu bora ya mbaazi katika shamba la Mpambaa halmashauri ya Singida.

Watumishi wa halmashauri ya Singida wakizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi (hayupo pichani).
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi akipanda mti wa mwembe katika eneo la sekondari ya Ilongero Wilayani Iramba.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi akipanda viazi lishe na mihogo katika shamba la mkulima bora wa eneo la Old Kiomboi Wilayani Iramba.


……………….

Watumishi wa halmashauri zote saba za Mkoa wa Singida wameagizwa kulima nusu ekari ya mazao yanayotumia maji kwa ufanisi hasa zao la muhogo, viazi au mtama ili kuwa na uhakika wa chakula cha kutosha msimu ujao huku shule zote zikiagizwa kulima ekari moja ya mihogo au mtama ili wanafunzi wapate chakula shuleni.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimi ametoa agizo hilo alipotembelea na kuzindua shamba la mbegu bora ya mihogo la ekari kumi lililopo kijiji cha Mpambaa, Halmashauri ya Singida ambalo litazalisha mbegu kwa ajili ya wakulima wa Mkoa wa Singida.

Dokta Nchimbi ametumia kauli mbiu ya kuongoza ni kuonyesha njia kwa kulima mihogo shamba lake mwenyewe lenye ukubwa wa ekari tatuna hivyo kuwaagiza watumishi na viongozi wote kuonyesha mfano kwa kulima mazao hayo kwa msimu huu.

Pamoja na upandaji wa mbegu za Muhogo, Dokta Nchimbi pia amezindua shamba la mbegu bora za mbaazi kwa kupanda mbegu hizo pamoja na kupalilia shamba la mbegu bora za mtama ambapo aina 25 za mtama zinafanyiwa majaribio ili kupata mbegu itakayofaa kwa mkoa wa Singida.

Aidha ametembelea mashamba ya wakulima wa mtama wa halmashauri ya Wilaya ya Ikungi pamoja na kushiriki upandaji wa mtama wa shamba la shule ya Msingi Mampanta wilayani Iramba na kupanda viazi na mihogo katika shamba la Mkulima wa Old Kiomboi wilayani Iramba.

Amesema wakulima wakielimishwa juu ya mazao yanayotumia maji kwa ufanisi watapanda mazao hayo ambayo ni mtama, viazi, muhogo na mbaazi ambapo wakulima watakuwa na uhakika wa chakula pamoja na kujipatia fedha kwa kuuza mazao hayo.

Dokta Nchimbi ametoa hamasa kwa wakulima wote kulima mazao hayo yanayotumia maji kwa ufanisi na wajitume kwa bidii kuliko kulalamikia serikali bila kufanya kazi kwakuwa awamu ya sasa ya uongozi ni ya kuchapa kazi kwa bidii.

Wakati huo huo Dokta Nchimbi amefanya vikao na watumishi wa halmashauri za Singida, Ikungi na Iramba mara baada ya kutembelea mashamba ya wakulima na kushiriki nao katika kupanda mtama, kupalilia baadhi ya mashamba, kupandqa mihogo na viazi.

Dokta Nchimbi amewaasa watumishi wote Mkoani Singida kuwa waadilifu, wachape kazi na hasa kulima mazao yanayotumia maji kwa ufanisi pamoja na kufanya shughuli nyingine za kuwaingizia kipato kama vile kufuga kuku na kuwa na mizinga ya nyuki ili wawe na kipato kingine nje ya mshahara.

Amesema watumishi wengine hujiingiza kwenye wizi kutokana na tamaa tu ila endapo watakuwa na vyanzo vingine vya fedha nje ya mshahara itapunguza kutokuwa waaminifu pamoja na kutokulalamika mara kwa mara.

Baadhi ya watumishi waliohudhuria vikao hivyo wamempongeza Mkuu wa Mkoa Dokta Nchimbi kwa nasaha alizowapa huku wakiahidi kuchapa kazi kwa bidii na uadilifu pamoja wakijishughulisha na kilimo ili wawe na kipato cha ziada.
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images