Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

NEC YARIDHISHWA NA MAANDALIZI YA UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE KATIKA JIMBO LA DIMANI ZANZIBAR

$
0
0
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage (kulia) akiangalia Orodha ya majina ya wapiga kura 603 iliyobandikwa katika kituo cha kupigia Kura cha Skuli ya Maandalizi ya Nyamanzi katika jimbo la Dimani Zanzibar leo. Kulia ni Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Dimani Bi. Idaya Seleman Hamza.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mst. Zanzibar, Mhe. Hamid M. Hamid (katikati) akifafanua jambo kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (R) Mhe. Semistocles Kaijage (kushoto) na Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa NEC, Bw. Emmanuel Kawishe mara baada ya kutembelea kituo cha kupigia kura cha Dimani leo visiwani Zanzibar.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Semistocles Kaijage akizungumza na Watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi leo mara baada ya kutembelea vituo vya kupigia kura katika jimbo la Dimani. Kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji Mstaafu wa Zanzibar, Hamid M.Hamid (wa pili ), Msimamizi Msaidizi wa jimbo la Dimani Bi. Idaya Selemani Hamza (katikati), Mkurugenzi wa huduma za kisheria, Bw. Emmanuel Kawishe (Kulia).
Orodha ya Majina ya Wapiga kura iliyobandikwa Siku nane kabla ya Uchaguzi mdogo wa Ubunge katika kituo cha kupigia kura cha Nyamanzi chenye wapiga Kura 603 katika jimbo la Dimani leo. 
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi , Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Semistocles Kaijage (Kulia) akimweleza jambo Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Emanuel Kawishe (kushoto) mara baada ya kukagua mabango ya Matangazo ya Tume kuhusu upigaji wa kura, Orodha ya Majina ya Wapiga kura na wagombea katika kituo cha kupigia kura cha Skuli ya Maandalizi Kisakasaka, Dimani Zanzibar leo.
Moja ya Tangazo la Elimu ya Mpiga Kura linaloonyesha utaratibu wa kufuata wakati wa kupiga Kura lililobandikwa katika kituo cha kupigia Kura cha Kisakasaka katika jimbo la Dimani.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage (wa tatu kutoka kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji Mst. Zanzibar, Hamid M. Hamid (wa tatu kutoka kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa NEC walipotembelea vituo vya kupigia kura katika Jimbo la Dimani kuangalia maandalizi ya Uchaguzi mdogo wa Ubunge utakaofanyika Jumapili, Januari 22, 2017.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage (kushoto) akiwa ameongozana na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa NEC, Bw. Emmanuel Kawishe akiwasili katika kituo cha kupigia kura cha Skuli ya Maandalizi na Msingi Dimani, Zanzibar kukagua kukamilika maandalizi ya Uchaguzi wa Ubunge katika jimbo hilo leo. Kulia ni Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Dimani bi. Idaya Seleman Hamza.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage (kulia) akiangalia Orodha ya majina ya wapiga kura 603 iliyobandikwa katika kituo cha kupigia Kura cha Skuli ya Maandalizi ya Nyamanzi katika jimbo la Dimani Zanzibar leo. Wengine ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa NEC, Bw. Emmanuel Kawishe (katikati) na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Dimani Bi. Idaya Seleman Hamza.
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa NEC, Bw. Emmanuel Kawishe (katikati) akimweleza jambo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (R) Mhe. Semistocles Kaijage (kushoto) alipotembelea kituo cha kupigia kura cha Skuli ya Maandalizi ya Nyamanzi katika jimbo la Dimani leo. Kulia Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Dimani Bi. Idaya Seleman Hamza.
 

FUATILIA SHUGHULI MBALIMBALI ZA KUAPISHWA KWA RAIS MTEULE WA MAREKANI-DONALD TRUMP

Serikali yafanya ukaguzi miradi ya miundombinu

$
0
0
Kaimu Mkuu wa Idara ya Miradi ya Ujenzi kutoka Baraza la Taifa la Ujenzi Injinia Wambura M. Wambura akiongea na wanahabari (hawapo pichani)kuhusu jukumu la ukaguzi wa kiufundi au kitaalam wa miradi ya ujenzi nchini jijini Dar es Salaam leo (jana).
Kaimu Mkuuwa Idara ya Miradi ya Ujenzi Injinia Wambura akiongea na wanahabari (hawapopichani) kuhusujukumu la ukaguziwakiufundi au kitaalamwamiradiyaujenzinchinijijini Dar es Salaam leo (jana).
KaimuMkuuwaIdarayaMajengokutokaBaraza la Taifa la Ujenzi Injinia Kissamo Fredrick akiongea na wanahabari kuhusu mafanikio ya Baraza hilo katika utekelezaji wa jukumu la kufanya ukaguzi wa kiufundi jijini Dar es Salaam jana (leo). (Pichana Benjamin Sawe- Maelezo).

……………..


Frank Mvungi-Maelezo




SERIKALI kupita Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) imefanya ukaguzi wa miradi mikubwa 163 yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 2 ikijumuisha Barabara, majengo, maji na viwanja vya ndege.


Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Kaimu wa Idara ya Uhandisi wa Baraza hilo Mhandisi Wambura M. Wambura alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya ukaguzi huo.Mhandisi Wambura amesema kuwa miradi yote iliyofanyiwa ukaguzi inatekelezwa chini ya ufadhili wa Serikali.

“Shughuli za kiukaguzi zilizofanyika ni pamoja na kufanya mapitio na tathmini ya michakato ya manunuzi, utekelezaji wa mikataba, utekelezaji wa miradi,ongezeko la gharama za miradi, pamoja na ubora wa kazi zilizofanyika,” alisisitiza Mhandisi Wambura.

Aliongeza kuwa lengo la kaguzi hizo ni kuhakikisha kuwa thamani ya fedha inalingana na ubora wa miundombinu iliyojengwa katika eneo husika.Aidha, Mhandisi Wambura amesema kuwa katika kipindi cha 2015/2016 baraza lilifanya ukaguzi wa kiufundi wa miradi ya matengenezo ya barabara kwa halmashauri zote za Wilaya pamoja na TANROADS kwa Mikoa ya Mbeya,Songwe,Rukwa,Katavi,Kigoma, na Shinyanga ambapo miradi hiyo iliyotekelezwa kwa fedha za mfuko wa Barabara.

Miradi mingine iliyofanyiwa ukaguzi wa kiufundi mwaka 2011 ni 14 iliyohusu ujenzi wa vituo vya afya na 36 ya ujenzi wa zahanati 50 iliyotekelezwa kwenye Halmashauri za Wilaya 20.Akizungumzia changamoto zilizobainika katika ukaguzi unaofanywa na Baraza hilo Wambura alibainisha kuwa ni kutozingatiwa kwa taratibu za kusimamia ubora wa kazi na maandalizi hafifu ya miradi katika hatua za mwanzo katika utengaji bajeti yakutosha,usanifu na ukadiriaji gharama za ujenzi.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Idara ya majengo Bw. Kissamo Elias alitoa wito kwa wadau wa sekta hiyo kulitumia Baraza hilo kufanya kaguzi katika miradi wanayotekeleza ili kuongeza tija hali itakayochochea ukuaji wa sekta hiyo.Baraza la Taifa la Ujenzi ni kitovu cha uratibu wa sekta ya ujenzi kwa taasisi zote zinazoshughulika na shughuli za ujenzi pamoja na wadau ili kuleta umoja,uwiano, na ushirikiano katika utendaji ndani ya sekta ya ujenzi,Baraza linaendelea kusimamia na kuongoza juhudi za kukuza na kuendeleza sekta ya ujenzi nchini.

Baraza la Taifa la Ujenzi ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria ya Bunge namba 20 ya mwaka 1979 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2008,baraza lipo chini ya Wizara ya ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano

NAIBU WAZIRI MASAUNI AIONGOZA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA KUTEMBELEA GEREZA LA KILIMO SONGWE

$
0
0
Naibu Waziri  wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akijibu maswali yaliyoulizwa na waandishi wa habari baada ya kumaliza ziara ya kutembelea shamba la Mahindi linalomilikiwa na Gereza la Kilimo Songwe, lililopo wilayani Mbalizi, jijini  Mbeya.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Kanali Mstaafu Masoud Ally, akiwaongoza wajumbe wengine wa kamati hiyo kusalimiana na Maafisa wa Jeshi la Magereza wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua shughuli zinazofanywa na Gereza la Kilimo Songwe, wilayani Mbalizi, Jijini Mbeya.
 Naibu Waziri  wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia), akiongozana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Kanali Mstaafu Masoud Ally (wakwanza kulia), kuingia ndani ya Gereza la Kilimo la Songwe,lililopo wilayani Mbalizi, jijini Mbeya,  ambapo wajumbe wa kamati walipata fursa ya kusikiliza maoni kupitia  risala iliyoandaliwa na wafungwa wa gereza hilo.Wengine ni viongozi wa gereza hilo.
 Afisa wa Jeshi la Magereza  akijibu maswali yaliyoulizwa na wajumbe wa  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama walipotembelea shamba la mahindi linalomilikiwa na Gereza la Kilimo la Songwe, lililopo wilayani Mbalizi, mkoani Mbeya.Wa kwanza kulia ni Naibu Waziri  wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.

 Naibu Waziri  wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akimpokea Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Kanali Mstaafu Masoud Ally (wapili kushoto), wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua shughuli zinazofanywa na Gereza la Kilimo Songwe, wilayani Mbalizi, mkoani  Mbeya.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

WAWAKILISHI WA UNEP WAKUTANA NA WAZIRI MAKAMBA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akisikiliza kwa makini Wawakilishi kutoka Shirikia La Umoja wa Mataifa linalohusika na Mazingira (UNEP) waliokuja kumtembelea Ofisini kwake mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiwa katika mazungumzo na Wawakilishi wa Shirikia La Umoja wa Mataifa linalohusika na Mazingira (UNEP) pamoja na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Profesa Faustine Kamuzora mapema hii leo.

SACCOS YA POLISI YAJIVUNIA MAFANIKIO YA MIAKA KUMI

$
0
0
 Mwenyekiti wa bodi ya chama cha ushirika cha kuweka akiba na kukopa cha Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD) Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (CGF) Thobias E.M. Andengenye (aliyesimama) akitoa neno mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu wa  nane (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano huo mkoani morogoro jana kulia ni Kaimu Mrajis wa vyama vya Ushirika nchini Bwana Tito Haule, anayefuata ni Makamu Mwenyekiti Kamishna Albert M. Nyamhanga na Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, (ACP) Leonce Rwegasila.
 Wajumbe wa mkutano mkuu wa nane wa chama cha ushirika cha kuweka akiba na kukopa cha Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD), wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi wa mkutano huo Kaimu Mrajis wa vyama vya ushirika nchini Bwana Tito Haule, (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika jana mkoani Morogoro.
Kaimu Mrajis wa vyama vya ushirika nchini Bwana Tito Haule, pamoja na viongozi wa bodi na wajumbe wa chama cha ushirika cha kuweka akiba na kukopa cha Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano mkuu wa nane uliofanyika jana mkoani morogoro. (Picha zote na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi)

Na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi Morogoro
Chama cha ushirika cha kuweka akiba na kukopa cha Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD), kimeendelea kujizolea mafanikio makubwa kwa muda wa miaka kumi toka kuanzishwa kwake huku kikijivunia kukopesha wanachama wake jumla ya fedha taslimu bilioni 113.7

Hayo yamethibitishwa na kaimu Mrajis wa vyama vya ushirika nchini Bwana Tito Haule, wakatia akifungua mkutano mkuu wa nane wa Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD), uliofanyika jana mkoani Morogoro huku ukiwakutanisha wajumbe na wawakilishi 172 kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.

Bwana Haule, alisema kuwa,  mbali na mafanikio makubwa kupatikana pamoja na ongezeko la akiba na amana zenye thamani ya bilioni 23.095  kutokana na ubunifu wa kujenga mtaji wa ndani pia amewaasa viongozi na watendaji kuwa waadilifu na waaminifu ili kufikia malengo makuu yaliyotokana na maadhimio ya vikao vilivyopita.

Aidha, kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Usalama wa Raia Saccos Kamishna Jenerali wa Zimamoto na Uokoaji (CGF) Thobias E.M. Andengenye, alisema kuwa, usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD),  itaendelea kutoa elimu kwa wanachama wake wote na kuendelea kujenga mtaji wa ndani kwa kununua hisa na kuweka akiba pamoja na kurejesha mkopo kwa wakati alisema.

Kamishna Andengenye, ameongeza kuwa, usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD),  itaendelea kuwahudumia wanachama wake wote ili kuwapunguzia makali ya maisha na kuwaepusha na mikopo yenye riba na masharti makubwa ili kukuza ustawi na uchumi wao na kwamba wamejipanga katika kuongeza idadi ya wanachama kupitia fursa walizonazo.

WAZIRI UMMY ATEMBELEA KITUO CHA AFYA BUGURUNI

$
0
0
 Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amembelea kituo cha afya Buguruni akiwa na Waziri wa Maendeleo wa Denmark Mhe. Martin Bille Hermann pamoja na Mkuu wa Wilaya Bi. Sophia Mjema. Lengo la ziara hiyo ni kufuatilia utoaji wa huduma za Afya katika Vituo vinavyomilikiwa na Serikali. Demnark ni mmoja wa Wafadhili wakubwa wa Sekta ya Afya nchini kupitia Mfuko wa Afya wa Pamoja (Health Basket Fund). Picha Kwa Hisani ya Wizara ya Afya

DENMARK KUHAMASISHA WAWEKEZAJI KUJA KUWEKEZA TANZANIA

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (wa kwanza kulia), akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na ujumbe kutoka nchini Denmark, ukiongozwa na Waziri wa nchi anayeshughulikia Sera, Bw. Martin Hermann, walipokutana Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es salaam.
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango na Ujumbe kutoka Serikali ya Denmark ukiongozwa na Waziri wa Nchi-Sera, Bw. Martin Hermann, walipokutana kwa mazungumzo kuhusu ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, Mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi anayehusika na masuala ya Sera, Bw. Martin Hermann (kulia) akiwa na ujumbe wake wakati wa mazungumzo kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (hayupo pichani), Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es salaam, ambapo nchi hizo zimekubaliana kuendeleza ushirikiano utakaojikita katika masuala ya uwekezaji na biashara kwa faida ya pande zote mbili. Kushoto ni Balozi wa Denmark hapa nchini Bw. Einar Jansen.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kushoto), akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na ujumbe kutoka nchini Denmark, ukiongozwa na Waziri wa nchi anayeshughulikia Sera, Bw. Martin Hermann, (hayupo Pichani) walipokutana Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Doto James, wakifuatilia kwa umakini mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango na Waziri wa Nchi anayeshughulika na masuala ya Sera wa Denmark, Bw. Martin Hermann (hawapo pichani), Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi anayehusika na masuala ya Sera kutoka Denmark, Bw. Martin Hermann (kushoto) akimkabidhi Dkt. Mpango, nyaraka za kampuni zinazoonesha nia ya kuwekeza Tanzania katika Sekta ya Gesi na Mafuta wakati akiongoza ujumbe wa nchi hiyo katika mazungumzo kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kulia), Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (katikati) akiangalia nyaraka alizokabidhiwa na Waziri wa Nchi wa Serikali ya Denmark anayehusika na Sera, Bw. Martin Hermann, wakati wa mazungumzo kati yao yaliyojikita katika masuala ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kati ya nchi hizo mbili. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Doto James na kulia kwa Waziri Dkt. Mpango, ni Naibu Katibu Mkuu Dkt. Khatib Kazungu.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (wa pili kushoto) akiwa na wageni wake kutoka Serikali ya Denmark wakiongozwa na Waziri wa Nchi anayehusika na Sera, Bw. Martin Hermann (kushoto), baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati yao ambapo masuala kadhaa yamejadiliwa ikiwemo kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na kijamii hususan katika uwekezaji na biashara, mazungungo yaliyofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kushoto) akipeana mkono wa shukurani na mgeni wake kutoka Serikali ya Denmark, Waziri wa Nchi anayehusika na Sera, Bw. Martin Hermann (kushoto), baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati yao yaliyogusa Nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii hususan katika uwekezaji na biashara, mazungunzo yaliyofanyika makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kushoto) akiwasindikiza wageni wake kutoka nje ya jengo la Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati ya ujumbe wa Serikali ya Denmark na Tanzania uliolenga kuimarisha uhusiano katika masuala ya uwekezaji na biashara.


(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WFM).


……………….



Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es salaam

SERIKALI ya Denmark imeahidi kuwashawishi wawekezaji wakubwa kutoka nchini humo kuja kuwekeza hapa nchini katika sekta za Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Viwanda, Bandari, Gesi na Mafuta.

Ahadi hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam na Waziri wa Nchi wa Serikali ya Denmark anayeshughulikia Sera, Bw. Martin Hermann, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Makao Makuu ya Wizara hiyo.

Bw. Hermann alielezea kufurahishwa kwake na namna Serikali ya Awamu ya Tano ilivyojipanga kuwatumikia wananchi wake kwa kuwaletea maendeleo ya haraka ya kiuchumi pamoja na kuimarisha uwajibikaji, mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi, na kusema kuwa nchi yake inaunga mkono juhudi hizo.

Alisema kuwa nchi yake itasaidia juhudi hizo kwa kuzishawishi kampuni kubwa zenye mitaji na uwezo wa kiteknolojia kutoka sekta binafsi ili zije ziwekeze hapa nchini na hivyo kushiriki katika kukuza uchumi wa nchi.

Amesisitiza pia umuhimu wa serikali kuwekeza juhudi kubwa katika kuendeleza kilimo kwa kuwa sekta hiyo inaweza kuchochea na kutoa mchango mkubwa na wa haraka wa ustawi na maendeleo ya wananchi.

Aidha, Bw. Hermann, ambaye aliambatana na Balozi wa Denmark hapa nchini, Bw. Einar Jensen, amesifu utendaji mzuri wa Rais Mhe. Dkt. John Magufuli katika mapambano dhidi ya vitendo vya ufisadi ikiwemo rushwa na kuishauri Serikali kuweka mfumo wa vita hiyo utakaokuwa endelevu.

Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, alisema Serikali inathamini mchango mkubwa wa Denmark katika kukuza uchumi na maendeleo ya Taifa kwa ujumla kwa kusaidia miradi ya maendeleo na ushauri wa kisera.

“Katika kipindi cha zaidi ya miaka 50 ya uhusiano kati ya nchi hizi mbili tumeshuhudia Serikali ya Denmark ikichangia maendeleo yetu katika nyanja zinazokwenda sambamba na vipaumbele vya maono ya mipango yetu ya maendeleo katika sekta za fedha, miundombinu, kilimo, afya na elimu”alisisitiza Dkt. Mpango.

Dkt. Mpango aliishauri nchi hiyo kwamba mwelekeo wa uhusiano huo sasa uwe katika kushirikiana kiuchumi kwa kuhamasisha uwekezaji na biashara kati ya pande hizo mbili.

Alifafanua kuwa amejaribu kutafuta takwimu za kiwango cha uagizaji na uingizaji wa bidhaa kati ya Tanzania na Denmark lakini cha kusikitisha hakuna biashara hiyo jambo ambalo amesema inabidi lilisisitizwe katika mfumo mpya wa ushirikiano kwa kuwa kuna fursa nyingi zinazoweza kusaidia pande zote mbili kiuchumi.

Alisisitiza kuwa mwelekeo huo ni muhimu utiliwe mkazo sambamba na jitihada za Serikali za kuboresha mazingira ya kufanya biashara na kuwekeza hapa nchini huku akitoa wito kwa kampuni za Denmark zilizopo hapa nchini pia kuvuta kampuni nyingine kutoka nchini mwao kuja kuwekeza Tanzania.

Dkt. Mpango, amewakaribisha wawekezaji hao kuwekeza katika katika sekta za ufugaji wa samaki, ujenzi wa viwanda vya kuchakata samaki, ufugaji wa ng’ombe wa kisasa na viwanda vya kusindika nyama na maziwa, hatua itakayo saidia kukuza mitaji, kuongeza tija katika sekta hizo na ajira kwa kundi kubwa la vijana.

Kuhusu ushauri uliotolewa na Waziri wa nchi wa Denmark anaye shughulikia Sera, Bw. Martin Hermann wa kujenga mfumo endelevu wa kupambana na rushwa na ufisadi, Dkt. Mpango amesema kuwa Serikali imeanzisha mahakama maalumu ya mafisadi ambayo anaamini ni moja ya ujenzi wa mifumo hiyo endelevu ya kupambana na vitendo hivyo.

RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA MABALOZI SITA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akimuapisha Dkt. Emanuel Nchimbi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Brazili, Ikulu jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Januari 20, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. James Msekela  kuwa Balozi wa Tanzania Geneva –Umoja wa Mataifa, Ikulu jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Januari 20, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Mbelwa Kairuki kuwa Balozi wa Tanzania nchini China, Ikulu jijini Dar es salaam leo Ijumaa Januari 20, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. George Madafa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia leo Ijumaa Januari 20, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Elizabeth Kiondo kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uturuki leo Ijumaa Januari 20, 2017.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Fatma Rajab  kuwa balozi wa Tanzania nchini Qatar, Ikulu jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Januari 20, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza machache baada ya kuwaapisha mabalozi hao Ikulu jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Januari 20, 2017. Picha na IKULU

MAZIWA YA ASAS DAIRIES LTD NI MAZIWA BORA - WAZIRI MKUU KASIM MAJALIWA

$
0
0
waziri  mkuu Kasim Majaliwa  akifurahia  ubora  wa  maziwa  ya Asas
Mkurugenzi  wa  kampuni ya  Asas Bw  Salim Abri akiteta  jambo na  waziri  mkuu Kasim Majaliwa
Asas  akimweleza  jambo  waziri  mkuu Kasim Majaliwa
Waziri  Mkuu Kasim Majaliwa akifurahi jambo na Bw Asas
Viongozi  mbali  mbali  wakimsikiliza  waziri mkuu
Waziri  Mkuu  akitoa maelezo kwa  viongozi wa  mkoa  wa Iringa
Familia  ya Asas  wakifuatilia  hotuba ya  waziri mkuu
Mkurugenzi  mtendaji  wa kampuni ya  maziwa  ya  Asas Bw  Fuad Abri akisoma  taarifa ya  kampuni  hiyo  mbele ya waziri mkuu
Wananchi wakifuatilia  hotuba ya  waziri mkuu Kasim Majaliwa
Waziri  wa Nyumba ,ardhi na maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi akizungumza  mbele ya  waziri mkuu
waziri  mkuu Kasim Majaliwa  akifuatilia taarifa ya kampuni ya  Asas ,wengine ni salim Abri na Waziri  wa Nyumba ,ardhi na maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi
Farasi  waliopo shamba  la mifugo  la Asas
Askari  wa  FFU  Iringa  wakitazama ng'ombe shambani kwa  Asas
Nyati  wanaofugwa  shambani kwa Asas Iringa
Kundi  la  Nyati  wanaofugwa  shambani kwa Asas eneo la  Igingilanyi  Iringa

Askari  wa  FFU  Iringa  akipiga  picha na nyati waliopo  shambani kwa Asas
Asakari  wa FFU  Iringa  wakitazama vifaa  vya  kuhamilishia ng'ombe 
Ng'ombe  waliopo  shamba la Asas   la  Nduli
Msafara  wa  waziri  Mkuu  ukiondoka  shambani kwa  Asas
Waziri  mkuu  akishukuru kwa   wenyeji kabla ya  kuondoka
waziri  mkuu Kasim Majaliwa  akiagana na  Salim  Abri
Waziri  mkuu akiagana na  mkurugenzi wa kampuni ya maziwa  ya  Asas  Fuad Abri
Waziri  mkuu  akitembelea  shamba  la mifugo  la Asas
Bw  Feisal  Abri  akimpa  maelezo  waziri  mkuu Kasim Majaliwa
Waziri  mkuu  akiendelea  kutembelea  shamba  la mifugo la Asas
Waziri  mkuu  Kasim Majaliwa  akitazama ng'ombe  ambao  wanasubiri  kupandikizwa mbegu
Zoezi la  kuhamilisha  ng'ombe  likifanyika
Mtaalam  akionyesha  namna ya  kupandikiza mbegu ng'ombe
Waziri  Lukuvi  kulia  akiteta  jambo na waziri  mkuu
Mtambo  wa  maziwa 
Waziri  mkuu  akifurahi majina ya ng'ombe  za  Asas
Zoezi la kukamua  maziwa  likiendelea
Waziri  mkuu Kasim Majaliwa  akisalimiana na Salim Asas  baada ya  kufika  kutembelea  shamba la mifugo  katikati ni mkuu wa  mkoa wa Iringa  Amina Masenza
Waziri mkuu  Kasim  Majaliwa na  viongozi  mbali mbali  wakielekea  kutembelea shamba la mifugo ya  Asas( picha na MatukiodaimaBlog)

Na MatukiodaimaBlog
WAZIRI  mkuu Kasim Majaliwa amepongeza  kampuni ya maziwa ya  Asas  Dairies Limited kwa  uzalishaji wa bidhaa bora  nchini  na  kuwa ni kampuni pekee  ambayo inafanya  vizuri  katika utengenezaji wa bidhaa bora za maziwa na kuwa  imeweza kutekeleza kwa  vitendo kauli  mbiu ya  Rais Dkt  John Magufuli  ya Tanzania  ya  viwanda .

Kuwa  serikali  itaendelea   kuiunga  mkono kampuni  hiyo ya  Asas  ambayo pamoja na  kufanya  vizuri katika ubora  wa  maziwa  bado   ni  kampuni yenye sifa nzuri ya  ulipaji wa  kodi nchini  pia  ni kapuni ya mfano kwa  ufugaji bora  wa ng’ombe
“ Nimefurahishwa na ufugaji  bora  ufungaji  wa  mifugo   unaofanywa na Shamba la kampuni ya Asas ya mkoani mkoani Iringa  ni  mzuri  sana lazima   wafugaji wengine nchini  kufika kujifunza jinsi ya ufugaji .”

Alisema   kuwa bidhaa zinazotengenezwa na kampuni ya Asas Dairies kama  mtindi  unaozalishwa na kampuni hiyo ya  Asas ni mzuri  na hata  ukinywa hauna  hofu ya kuharisha kama mtindi inayotengenezwa na wengine 

Akizungumza leo  wakati wa ziara  yake ya  kutembelea  shamba la Asas lililopo eneo la Igingilanyi  katika  wilaya ya  Iringa ,waziri  mkuu  alisema  kuwa amefurahishwa na ufugaji  unaofanyika katika  eneo hilo na kutaka   watu  wengine  kuanza  kufuga mifugo badala ya  kuwa  wachungaji wa  mifugo .

Kwani  alisema tatizo kubwa ya  migogoro  kati ya  wachungaji na  wakulima inasababishwa  na baadhi ya  watu kuendesha  uchungaji  wa mifugo  badala ya  kufuga  na  hivyo  kupelekea kugombea maeneo ya kuchungia huku  wakulima   wakivamiwa na wachungaji hao .

Alisema  kwa  lengo la  kukomesha  migogoro  kati ya  wachungaji na   wakulima  anawaagiza  maofisa  mifugo  kote nchini  kuanza  kuitambua  mifugo  yote na  kuiweka alama  maalum  itakayosaidia  kutambua eneo  ambalo  mifugo  hiyo inatoka na  itakuwa ni njia ya  kukomesha wachungaji  kuhama hama 

Hivyo  alisema  ni  mhimu  sana  kwa  maofisa  Mifugo  katika Halmashauri  zote nchini  kuanza  kutoa  elimu kwa  wafugaji  ili kuondokana na  kuwa  na  mifugo mingi  isiyo bora  na  badala yake  kuachana na uchungaji  wa  mifugo  na  kujikita na ufugaji .

Alisema  kuwa  kwa  upande  wa Halmashauri  za  wilaya  zote  nchini  zinapaswa  kuwapimia  na kuwapa  hati ya umiliki  wa  ardhi  wawekezaji  wote  wakubwa  waliopo katika maeneo yao  lengo  likiwa ni  kuondokana na migogoro ya  ardhi .

TAZAMA VIDEO HAPA  CHINI 

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA KWENYE UWANJA WA MABEWANI MJINI MAKETE

$
0
0
Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Mabewani mjini Makete, januari 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mku)
WETOWaziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Ujuni wilayani Makete walioziba barabara wakitaka asimame kuwasalimia Januari 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama ndama waliokuwa wakinyweshwa maziwa wakati alipotembelea shamba la ng’ombe la Kitulu wialayani Makete Januari 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KINANA AWAPA SOMO MAWAKALA WA UCHAGUZI MDOGO,AWASHANGAA WAPINZANI KUDAI KUIBIWA KURA KILA UCHAGUZI

$
0
0

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na makada ambao ni mawakala wa CCM katika uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Kijichi, Mbagala, Dar es Salaam, alipokuwa akifunga semina ya mawakala hao, leo Janauari 20, 2017. Uchaguzi mdogo wa Unatarajiwa kufanyika Jumapili hii nchini kote.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisaini kitabu cha wageni alipopita kwenye ofisi ya CCM Kata ya Kijichi akiwa njiani kenda kufunga semina ya makada ambao ni mawakala wa CCM katika uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Kijichi, Mbagala, Dar es Salaam, leo Janauari 20, 2017. Kulia ni Mgombea wa Udiwani kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi huo, Tausi Milanzi.

Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwsili ukumbini kwa ajili ya kufunga semina hiyo. Kulia ni Mgombea Udiwani katika kata ya Kijichi Tausi Milanzi, Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida.

Mawakala wa CCM katika Uchaguzi mdogo wa Udiwani Kata ya Kijichi, Mbagala Dar es Salaam, wakimshangilia, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipowasili ukumbini kufunga semina yao, leo

Meneja wa kampeni za CCM za uchaguzi mdogo wa Udiwani Kata ya Kijichi, Mbagala, Dar es Salaam, akitoa maelezo, kabla ya Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kufunga semina ya mawakala wa CCM katika uchaguzi huo leo

Mgombea wa Udiwani kwa tiketi ya CCM, katika Uchaguzi Mdogo wa Madiwani, Kata ya Kijichi, Mbagala, Dar es Salaam, Tausi Milanzi, akisalimia mawakala wa CCM waliokuwa kwenye semina maalum, kwa ajili ya uchaguzi huo

Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga, akisalimia viongozi na mawakala wa CCM, katika Uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Kijichi .

Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga, akisalimia viongozi na mawakala wa CCM, katika Ucaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Kijichi .

Katibu Mkuu wa CCM, akipokea kadi kutoka kwa aliyekuwa mwanachama wa Chadema Adam Hamis ambaye aliamua kuhamia CCM, wakati wa Semina ya Mawakala wa CCM katika uchaguzi mdogo wa Udiwani Kata ya Kijiji, iliyofanyika leo .

Kisha Katibu Mkuu akampa Kapelo rasmi ya CCM

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Temeke Yahya Sikunjema akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, ili amkaribishe Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kufunga semina hiyo

Mwenyekiti wa CCM mkkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida akifafanua jambo kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kufunga semina hiyo

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na makada ambao ni mawakala wa CCM katika uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Kijichi, Mbagala, Dar es Salaam, alipokuwa akifunga semina ya mawakala hao, leo Janauari 20, 2017. Uchaguzi mdogo wa Unatarajiwa kufanyika Jumapili hii nchini kote.
--------------
 
Na Bashir Nkoromo.

Akifunga semina hiyo, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana aliwashangaa wapinzani kwamba kwa nini kila baada ya uchaguzi huwa wanalalamika kuwa wameibiwa kura.

"Zamani wakati mimi ni Mbunge, wakati wa uchaguzi, kura zilikuwa zinaenda kuhesabiwa wilayani, lakini siku hizi Mawakala wa vyama vyote wapo, walinzi wapo, tena kura zikishapigwa zinahesabiwa hapohapo kisha matokeo yanabandikwa ukutano hapohapo, wizi huo wa kura utatokea wapi?" alisema na kuhoji Kinana.

Kinana aliwaasa mawakala wa CCM katika uchaguzi huo mdogo wa Kijichi, kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake na kusema kwamba, anao uhakika ikiwa mawakala hao watafanya kazi zao vizuri basi CCM itashida.

"Ndugu zanguni, uchaguzi unazo sehemu nyingi, kuna kuteua wagombea, kupiga kampeni, na kupiga kura. sasa katika hatua zote hatua iliyokubwa zaidi ni hii ya kupiga kura, maana hapa ukiharibu umekosa kila kitu", alisema Kinana.

Alisema, japokuwa uchaguzi wa Udiwani katika kata hiyo ya Kijichi ni uchaguzi mdogo, lakini ni lazima kusimama kidete na kuhakikisha CCM nashinda tena kwa kishindo.

"Kweli huu ni uchaguzi mdogo, lakini nachotaka kuwaambia ni kwamba, uchaguzi ni kama kufanyiwa upasuaji, kama unafanyiwa upasuaji wataalam wanaweza kuuita mdogo, lakini wewe unayeenda kupasuliwa usiseme hivyo, ni kama vile kesi inayokukabili mahakamani, unaweza kuidharau ukatahamaki umefungwa, basi tusidharau kamwe uchaguzi huu", alisema, Kinana.

NIT kwa kushirikiana na Wadau watoa zawadi kwa wahitimu waliofanya vizuri.

$
0
0
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT)Prof.Zacharia Mganilwa akimuonesha Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TAZARA Bw. Betram Kiswaga maeneo mbalimbali ya chuo hicho wakati wa kongamano lililowakutanisha wanafunzi waliowahi kusoma katika chuo hicho katika miaka ya nyuma na waliomaliza mwaka ulioisha wa masomo.
Baadhi wa wahitimu na wanafunzi waliowahi kusoma katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wakiwa katika kongamano lililowakutanisha na viongozi wa chuo hicho.

Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Prof.Zacharia Mganilwa akiongea na wahitimu na wanafunzi waliowahi kusoma katika Chuo hicho ambapo alisema dhumuni la kuwakutanisha ni kutoa zawadi kwa wahitimu waliofanya vizuri katika masomo yao ikiwa ni lengo la kuongeza ufaulu na kuwa na wanafunzi bora ambao wanaweza kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa nchi kwa kutumia elimu waliyoipata kutoka chuoni hapo.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TAZARA Bw. Betram Kiswaga akiongea na na wahitimu na wanafunzi waliowahi kusoma katika Chuo hicho ambapo alisema taasisi yake itaendelea kuonesha nia ya kukisaidia chuo hicho ili kiendelee kukua zaidi na kutoa wahitimu bora katika soko la ajira nchini na afrika kwa ujumla.
Baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao wakipewa zawadi kutoka kwa wadau katika sekta ya usafirishaji nchini.
Dkt. John Layaa kutoka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji akitoa mada kuhusu umuhimu wa usafirishaji katika kukuza na kuendeleza uchumi wa nchi wakati wa kongamano la 3 la wanafunzi waliowahi kusoma chuoni hapo, Leo Jijini Dar es Salaam
Mgeni Rasmi Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TAZARA Bw. Betram Kiswaga (Mwenyeshati jeupe)akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wafanyakazi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji(NIT) na wahitimu waliofanya vizuri katika masomo yao

Tutaendelea kuimarisha mahusiano yetu na Bunge la Irani: Ndugai

$
0
0

Na Owen Mwandumbya, Bunge

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai (Mb) amesema Bunge la Tanzania litaendelea kudumisha mahusiano yaliyopo na Bunge Irani ili kubadilishana uzoefu katika maeneo mbalimbali.

Mhe. Ndugai ameyasema hayo Mjini Dodoma leo alipokutana na Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran Nchini Tanzania Mhe. Mohammad Dehghani aliefika Ofisini kwake Dodoma kwa ajili ya kuwasilisha salaam na mualiko rasmi kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislam ya Iran ukimualika Mheshimiwa ndugai kutembelea Bunge la Iran kwa lengo likiwa ni kuimarisha uhusiano wa nchi zetu mbili.

Nashukuru kwa Salaam hizi kutoka kwa Spika wa Bunge la Iran na naahidi kuzifikisha salaam hizi kwa Waheshimiwa Wabunge na pia Ofisi yangu itatolea taarifa juu ya mwaliko huu na kujipanga kutembelea Bunge la Irani kwa kadri muda utakavyoruhusu. Alisema Mhe. Ndugai

Pamoja na mwaliko huo wa Kibunge kutoka kwa Spika wa Bunge la Iran, Balozi huyo Irani pia alitumia fursa hiyo kuwasilisha ombi la Rais wa Iran Mhe. Hassan Rouhani la kumwalika Mhe. Ndugai ili aweze pia kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa kusaidia kutatua mgogoro wa muda mrefu kati ya Palestina na Israel uliopangwa kufanyika tarehe 22 Februari, 2017 Jijini Tehran jambo ambalo pia aliahidi kulitolea majibu hivi karibuni.

Akizungumzia namna ya kuimarisha mahusiano ya Mabunge haya mawili, Mhe. Ndugai alisisitiza umuhimu wa kuanzisha Chama Rafiki cha Kibunge (Parliamentary Friendship Group) baina ya Bunge la Tanzania na Bunge la Iran kwa kuwa kitasaidia sana Wabunge wa Mabunge yote mawili kubadilishana uzoefu na kuimaisha uhusiano uliodumu kwa muda mrefu baina ya Tanzania na Iran.

Kwa upande wa Mhe. Mohammad Dehghani aliipongeza Tanzania kwa kuendelea kuimarisha demokrasia ambayo kwa kiasi kikubwa nchi yake ya Iran imekuwa ikithamini na kuheshimu misingi imara iliyowekwa na Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Nchi yenu imekuwa na historia kubwa sana ya kimahusiano na Iran, pamoja na mambo yote napongeza sana jitihada mnazozichukua kuimarisha demokrasia ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya Wabunge wanawake Bungeni na nimatumaini yetu kuwa mtayafikia malengo mliyojiwekea ya kufikia idadi ya 50 kwa 50. Alisema Bolozi Dehghani

Awali, akimkaribisha mgeni wake, Mhe. Ndugai alimshukuru Mhe. Balozi kwa kutenga muda na kusafiri kutoka Jijini Dar es Salaam kuja Dodoma ambapo pia alitumia nafasi hiyo kumpa pole Mhe. Balozi kwa matukio mawili makubwa yaliyoikumba nchi ya Iran hivi karibuni.

“Mhe. Balozi, kabla ya yote kwa niaba ya Bunge la Tanzania natoa pole kwa msiba mkubwa wa kifo cha Rais wa Nne wa Iran Hayati Akbar Hashemi Rafsanjani kilichotokea taehe 08 Januari, 2017 na pili ni tukio la kuanguka kwa jengo kubwa la kibiashara Jijini Tehran lililosababisha vifo vya watu ishirini (20) na majeruhi zaidi ya 200, tarehe 19 Januari, 2017”. Alisema Mhe. Ndugai

Aidha Mhe. Ndugai alitumia fursa hiyo pia kumshawishi Mhe. Mohammad Dehghani kuanza kufikiria kuhamia Dodoma kwani miundombinu ipo na Ardhi inatosha kabisa kuuwezesha Ubalozi wa Irani kujenga Ofisi na kuendesha shughuli kutokea Dodoma.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai (Mb) akimkaribisha Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran Nchini Tanzania Mhe. Mohammad Dehghani aliefika Ofisini kwake Dodoma kwa ajili ya kuwasilisha salaam na mualiko rasmi kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislam ya Iran ukimualika Mheshimiwa Ndugai kutembelea Bunge la Iran kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa mabunge haya mawili.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai (Mb) akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran Nchini Tanzania Mhe. Mohammad Dehghani aliefika Ofisini kwake Dodoma kwa ajili ya kuwasilisha salaam na mualiko rasmi kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislam ya Iran ukimualika Mheshimiwa Ndugai kutembelea Bunge la Iran kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa mabunge haya mawili.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai (Mb) akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran Nchini Tanzania Mhe. Mohammad Dehghani aliefika Ofisini kwake Dodoma kwa ajili ya kuwasilisha salaam na mualiko rasmi kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislam ya Iran ukimualika Mheshimiwa Ndugai kutembelea Bunge la Iran kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa mabunge haya mawili.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai (Mb) akipokea mwaliko kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislam ya Iran uliowasilishwa na Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran Nchini Tanzania Mhe. Mohammad Dehghani kutembelea Bunge la Iran kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa mabunge haya mawili .Picha na Owen Mwandumbya, Bunge.

Wadau wa Michezo Jitokezeni kudhamini michezo nchini – Waziri Nape

$
0
0

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kushoto) akiangalia tuzo wakati akiipokea kutoka kwa mshindi wa medali ya dhahabu katika mbio za Standard Chartered Mumbai Marathon 2017 Bw. Alphonce Felix Simbu leo wakati wa hafla fupi ya kumpongeza jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati) akimpa mkono wa pongezi mshindi wa medali ya dhahabu katika mbio za Standard Chartered Mumbai Marathon 2017 Bw. Alphonce Felix Simbu baada ya pokea medali hiyo na kumvalisha leo wakati wa hafla fupi ya kumpongeza jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati) pamoja na mshindi wa medali ya dhahabu katika mbio za Standard Chartered Mumbai Marathon 2017 Bw. Alphonce Felix Simbu wakiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) tuzo aliyoipata Bw. Simbu katika mashindano ya Mumbai Marathon yaliyofanyika Januari 15 mwaka huu leo wakati wa hafla fupi ya kumpongeza jijini Dar es Salaam.Picha cha na: Genofeva Matemu – WHUSM.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kushoto) akiteta jambo na Mshindi wa medali ya dhahabu katika mbio za Standard Chartered Mumbai Marathon 2017 Bw. Alphonce Felix Simbu alipompokea na kumpongeza kwa kupeperusha vizuri bendera ya Tanzania katika mashindano hayo leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu kutoka Chama cha Riadha Tanzania Bw. Wilhelm Gidabuday akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumpokea na kumpongeza Mshindi wa medali ya dhahabu katika mbio za Standard Chartered Mumbai Marathon 2017 Bw. Alphonce Felix Simbu leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kumpokea na kumpongeza Mshindi wa medali ya dhahabu katika mbio za Standard Chartered Mumbai Marathon 2017 Bw. Alphonce Felix Simbu leo Jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa medali ya dhahabu katika mbio za Standard Chartered Mumbai Marathon 2017 Bw. Alphonce Felix Simbu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kumpongeza leo jijini Dar es Salaam



Na: Genofeva Matemu – WHUSM

Wadau mbalimbali wa sekta ya michezo nchini wametakiwa kujitokeza kudhamini michezo nchini ili kuweza kurudisha utukufu wa mafanikio katika sekta ya michezo na nchi kwa ujumla.

Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye wakati wa hafla fupi ya kumpokea na kumpongeza mshindi wa medali ya dhahabu katika mbio za standard Chartered Mumbai Marathon 2017 leo Jijini Dar es Salaam.

“Wadau wa michezo jitokezeni tushirikiane kwa pamoja kuboresha michezo nchini na kurudisha utukufu wa mafanikio katika sekta za michezo na nyingine ninazozisimamia kwani ni sekta ambazo zina mvuto ndani ya jamii” amesema Mhe. Nnauye

Aidha Mhe. Nnauye ameipogeza kampuni ya Multi Choice kwa kujitolea na kuwa wazalendo kuwekeza kwa mwanariadha Simbu ambaye amekua na mwanzo mzuri ambao utakua chachu kwa vijana wengi nchini kuthamini na kujituma katika mashindano mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wake mshindi wa medali ya dhahabu katika mbio za Standard Chartered Mumbai Marathon 2017 Bw. Alphonce Felix Simbu amewataka wanariadha wenzake nchini kufanya juhudi katika mazoezi ili kufikia mashindano ya dunia ya riadha Tanzania itoe idadi kubwa ya washiriki katika mashindano hayo.

Naye Katibu Mkuu Chama cha Riadha Tanzania Bw. Wilhelm Gidabuday amempongeza mshindi wa medali ya dhahabu katika mbio za standard Chartered Mumbai Marathon 2017 Bw. Simbu na kumtaka kuendelea kuwa kioo kwa wanariadha wenzake nchini.

WAZIRI UMMY AAGIZA WAKUNGA NA WAUGUZI WASIKAMATWE BILA YA KUFUATA TARATIBU ZILIZOPO

$
0
0
 Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiongea na wadau wa Baraza la Baraza la Wakunga hawapo pichani wakati wa kuzindua mradi wa Mkunga Okoa Maisha kwa kushirikiana na watu wa Canada.
Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katikati akikata utepe kuashiria kuzindua  mradi wa Mkunga Okoa Maisha , wa kwanza kushoto ni Balozi wa Canada  Bi. Susan Steffan na wakawnza kulia ni Katibu Mkuu wa Baraza la Wakunga nchini Dkt. Sebalda Leshabari.


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ametoa agizo kwa viongozi wote nchini kuacha mara moja kuwakamata wauguzi,  wakunga na kuwaweka ndani na badala yake wanapaswa kufuata taratibu zilizopo.
Akizungumza  hayo wakati wa uzinduzi wa mradi wa Mkunga Okoa Maisha Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Ummy Mwalimu  alisema wakunga wanalo baraza ambako ndilo suluhishi la matatizo yao.
"Aidha Mhe. Ummy amesema kuwa pale ambapo muuguzi au mkunga anapokosea  zipo taratibu za kufuata na siyo kumweka ndani kwani kuna Baraza la Wakunga ambalo lina Mamlaka ya kisheria za kuchukua kwa mkunga yoyote ambaye amekwenda kinyume.
"Tunao Wakunga na wauguzi ambao wanafanya kazi zaidi ya masaa, tumeona kilichotokea Sikonge, kiongozi anakuja juu kwanini mtoto amepewa dawa ya Quinn," alisema Ummy.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Baraza la Wakunga nchini Dkt. Sebalda Leshabari amesema kuwa mradi huo unalenga  kupunguza vifo katika Mikoa ya Shinyanga na Simiyu hivyo wauguzi na wakunga ni vema wakashirikiana na Baraza hilo ili kufanikisha malengo yao.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali,( PAC) wakikagua utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini cha Nyigo

$
0
0
 
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali,( PAC) wakikagua utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini cha Nyigo , Mufindi mkoani Iringa, Kamati hiyo inaongozwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani pamoja na Watendaji kutoka Wakala ya Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme nchini ( Tanesco)
Moja ya mashine za kusaga na kukoboa nafaka katika kijiji cha Nyigo, Mufindi mkoani Iringa inayotumia umeme baada ya kuunganishwa na Mradi wa Umeme Vijijini.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali,( PAC) wakimsikiliza Meneja wa Tanesco Mufindi, wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa Mradi wa Umeme Vijijini. Kamati PAC imeambatana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani pamoja na watendaji kutoka Wakala ya Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme nchini ( Tanesco)
Mwenyekiti wa Shirika lisilo la kiserikali linalohusika na utunzaji wa mazingira, Mufindi Environmental Trust,( MUET) Godfrey Mosha,( wa pili kushoto) akiwaonyesha Transfoma ( haipo pichani) Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali,( PAC ) na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani. MUET imeunganishwa na huduma ya umeme, kupitia mradi wa umeme vijijini ili kuendesha kituo cha kupumzikia wasafiri.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI JANUARI 21, 2017

ENG, NYAMHANGA AZINDUA MWONGOZO WA KUWAWEZESHA WAHANDISI WANAWAKE

$
0
0
Imeelezwa kuwa sababu za kihistoria, mila na desturi za jamii ni moja ya changamoto zinazoikabili sekta ya ujenzi kwenye ushirikishaji wa wanawake katika utekelezaji wa miradi ya barabara nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi ),Eng. Joseph Nyamhanga wakati akizindua mwongozo wa kuimarisha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara ambapo Serikali imekuja na mikakati mbalimbali ya kuwashirikisha wanawake katika miradi ya ujenzi wa barabara
"Maandalizi ya mwongozo huu ni sehemu ya mkakati wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano katika utekelezaji wa mikakati mbalimbali iliyojiwekea ili kuinua maisha ya wanawake kiuchumi,'' amesema Eng. Nyamhanga.

Eng. Nyamhanga ameongeza kuwa utekelezwaji wa mwongozo huo ni moja ya kichocheo cha kuwawezesha wanawake kutoa mchango mkubwa zaidi kuchumi nchini ambapo kwa sasa sekta ya ujenzi inachangia asilimia 13.6 kwenye pato la Taifa.

Aidha ametanabaisha kuwa kwa mwaka 2014/15 kumekuwa na ongezeko la ushiriki wa wanawake katika miradi ya barabara wa uwiano wa kila wahandisi 100 wanaume wanawake 6 ambao kwenye usimamizi wa miradi uwiano ukiwa ni asilimia 6.

Kwa upande wake MKurugenzi wa Idara ya Barabara, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Sekta ya Ujenzi, Eng. Ven Ndyamukama amesema ushirikishwaji wa wanawake katika sekta  ya ujenzi ulianza mwaka 1992 kwa kutekelezwa kwenye mikoa ya Mbeya, Tanga, Shinyanga, Mwanza na Mtwara.

"Kama Wizara tuliona umuhimu wa kuanzisha kitengo maalum kwa ajili ya kuhakikisha tunawawezesha wanawake katika kazi za ujenzi na hili limesisitizwa hata kwenye sheria ya Ujenzi ya mwaka 2003 (CIP, 2003) kwa kuhakikisha wanawake wanashirikishwa katika kazi za ujenzi ili kuwainua kiuchumi' amesema Eng. Ndyamukama.

Ameongeza kuwa pamoja na mwongozo huu Wizara imeendelea kuwawezesha wanawake kwenye mafunzo mbalimbali ya ujenzi kupitia vyuo mbalimbali vilivyo chini ya wizara na taasisi binafsi.

Takwimu Kutoka Bodi ya Usajili wa Wahandisi nchini (ERB) na Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB) zinaonesha kwa mwaka 2014, kati ya jumla ya wahandisi 13,148 waliopo nchini wahandisi wanawake ni 926 ambao ni sawa na asilimia 6.5 wakati kati ya Makampuni ya makandarasi 8,071 yaliyosajiliwa ni makampuni 253 yanamilikiwa na wanawake sawa na asilimia 3.
 Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga akitoa maelezo kwa Wadau wa masuala ya Ujenzi katika hafla ya uzinduzi rasmi wa mwongozo wa kuimarisha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara uliofanyika katika ukumbi wa makumbusho ya taifa jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga akitoa maelezo kwa katika Wadau wa masuala ya Ujenzi katika hafla ya uzinduzi rasmi wa mwongozo wa kuimarisha ushirikishwaji wa wananwake katika kazi za barabara uliofanyika katika ukumbi wa makumbusho ya taifa jijini Dar es salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga (kulia) akizindua kitabu cha mwongozo wa kuimarisha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara uliofanyika katika ukumbi wa makumbusho ya taifa jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (kulia) akizindua kitabu cha mwongozo wa kuimarisha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara uliofanyika katika ukumbi wa makumbusho ya taifa jijini Dar es salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga (kulia) akizindua kitabu cha mwongozo wa kuimarisha ushirikihwaji wa wanawake katika kazi za barabara uliofanyika katika ukumbi wa makumbusho jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi wa barabara Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng Ven Ndyamkama akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu mwongozo wa kuimarisha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara,jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga katika picha ya pamoja na wajumbe wa maendeleo ya sekta ya ujenzi mara baada ya kuzindua kitabu cha mwongozo wa kuimarisha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara uliofanyika katika ukumbi wa makumbusho  ya taifa jijini Dar es salaam. Picha na Wizara Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

HIVI NDIVYO DONALD TRUMP ALIVYOAPISHWA WHITE HOUSE KUWA RAIS WA 45,OBAMA AKABIDHI OFISI KIROHO SAFI

Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images