Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 109 | 110 | (Page 111) | 112 | 113 | .... | 1898 | newer

  0 0  0 0

  Na Edwin Moshi, Njombe.

  Jeshi la polisi wilayani Makete mkoani Njombe limewataka wamiliki wa nyumba za kulala wageni wilayani hapo kuhakikisha wanaandikisha taarifa za wageni wanaofika kulala kwenye nyumba hizo, kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kuwaweka salama pindi kunapotokea tatizo

  Hayo yamesemwa na mkuu wa polisi wilaya ya Makete SP Peter Kaiza wakati akizungumza katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya hiyo kuhusiana na tabia ya baadhi ya wahudumu wa nyumba za kulala wageni kudharau kuandikisha taarifa zinazowahusu wageni kwa kinachodhaniwa kuwa ni kuwaibia wamiliki kwani suala hilo ni hatari kwao na kwa jeshi la polisi pia

  “Akuja mgeni kulala kwenye nyumba unayofanyia kazi, wewe hujampa daftari akandika jina na taarifa zingine, usiku linatokea la kutokea mtu ananyooka(anakufa) sasa utajibu nini kwa bosi wakao na kuja kutoa taarifa polisi utaanza anza je” alisema Kaiza

  Katika hatua nyingine kaiza amezungumzia dhana iliyojengeka kwa wahudumu hao kuwa wateja wengi huandika taarifa za uongo hivyo kuona hakuna haja ya kuandika taarifa zao akisema si kweli kuwa kila taarifa itakuwa ya uongo na kusisitiza kuwa wawaandikishe kwa kuwa zitasaidia pindi likitokea tatizo

  Kwa upande wake afisa biashara wilaya ya Makete Bw. Adonia Mahenge(PICHANI) amesema ni vyema wahudumu wa afya wakatambua umuhimu wa kutunza taarifa hizo kwani ni suala la kisheria ambalo linatakiwa kufuatwa na kila mhudumu wa nyumba ya kulala wageni

  Amesema katika kusisitiza hilo watafanya ukaguzi muda wowote kuona kama hatua hizo zinafuatw na ambaye atakuwa amekiuka utaratibu atachukuliwa hatua kali za kisheria, waweke mabango yanayoonesha utaratibu na kanuni na masharti ya kulala kwenye nyumba ya wageni, kuboresha nyumba hizo ikiwemo usafi na ubora wa huduma

  Amesema maazimio hayo yanatakiwa kutumika ndani ya wilaya nzima ya Makete ikiwemo Makete mjini, Ikonda, Bulongwa, Matamba na maeneo mengine ambayo nyumba hizo zipo

  0 0

  Wasanii wa kikundi cha Bombeso Cruw wakitoa burudani wakati wa promosheni ya ya Relstar Oil inanayotengenezwa na Kampuni ya Gapco Eneo la mwembe yanga Dar es salaam kutoka kushoto ni Omar Salimu Halima Masoud na Jafari Halawi.
  Mkuu wa Mafuta ya Gapco Bw. Suraj Vikash akizungumzia promosheni hiyo

  Wasanii wa kikundi cha Bombeso Cruw wakitoa burudani wakati wa promosheni ya ya Relstar Oil yanayotengenezwa na Kampuni ya Gapco Eneo la mwembe yanga Dar es salaam kutoka kushoto ni Omar Salimu Halima Masoud na Jafari Halawi picha na www.burudan.blogspot.com

  Wasanii wa kikundi cha Bombeso Cruw wakitoa burudani wakati w

  0 0

    Waziri wa Afya  Juma  Nuni  Haji akipokea mandamano  yaliongozwa  na vijana wa Chipkizi, katika madhimisho ya siku ya upigaji vita matumizi na biashara haramu ya madawa ya kulevya Duniani huko  Meya , nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. 
    Waziri wa Afya  Juma  Nuni  Haji akiwa na viongozi mbalimbali, Makanda wa Polisi katika picha ya pamoja na walioacha kutumia madawa ya kulevya huko Meya katika madhimisho ya siku ya upigaji vita matumizi na biashara haramu ya madawa ya kulevya Duniani Jun 26.
   Waziri wa Afya  Juma  Nuni  Haji, akiwahutubia wananchi na waliocha kutumia madawa ya kulevya katika madhimisho ya siku ya upigaji vita matumizi na biashara haramu ya madawa ya kulevya Duniani, kuli Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Tume ya Dawa za kulevya Muhmoud Mussa,kushoto Naibu Kadhi Mkuu Zanzibar Hassan Othman.
   Addy Amer alieacha kutumia madawa ya kulevya akitoa ushuhuda wa madawa ya kulevya, na kuwataka vijana wasijaribi kuyatumia kwani yanahatarisha maisha kwa ujumla. 
  Walioacha kutumia madawa ya kulevya wakipita kwa mandamano mbele ya mgeni rasmin  Waziri wa Afya  Juma  Nuni  hayupo pichani, katika madhimisho ya siku ya upigaji vita matumizi na biashara haramu ya madawa ya kulevya Duniani.Picha na Makame Mshenga- Maelezo Zanzibar.


  0 0  0 0

  TAMASHA la Mastaa Chipukizi lililokuwa lifanyike Jumamosi Juni 29 kijiji cha wasanii Mwanzega Mkuranga limeahirishwa ili kutoa nafasi kwa  wasanii na viongozi mbalimbali kushiriki kikamilifu katika maandalizi na mapokezi ya  Rais wa Marekani, Baraka Obama.
   
  Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA), Caaasim Taalib alisema jana kuwa wanachama wengi waliokuwa washiriki tamasha hilo watakuwa katika maandalizi ya ujio wa Rais Obama hivyo litafanyika mwezi Agosti baada ya sikukuu ya Idd el Fitri.
   
  Taalib alisema anawaomba radhi wananchi wa Mkuranga, viongozi mbalimbali na wasanii washiriki wa tamasha hilo waliokuwa wamejiandaa kuonesha vipaji vyao katika tamasha hilo.
   
  ‘Tumeamua kutoa nafasi hii kwa wanachama wa SHIWATA ili washiriki kikamilifu kudumisha amani katika wakati huu ambao tunatembelewa na Rais Obama na wasanii washiriki kikamilifu, tunaomba tutoe taarifa katika vyombo vya dola mara tunapoona kuna unjifu wa amani’ alisema Taalib.
   
  Mwenyekiti huyo alisema mgeni rasmi aliyekuwa ameandaliwa, Naibu Waziri wa Kilimo, Adam Malima amepelekewa ujumbe huo pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida na wabunge wa Dar es Salaam nao wamearifiwa kuhusu kusogezwa mbele tamasha hilo.
   
  Alisema sambamba na tamasha hilo, SHIWATA ilikuwa ikabidhi nyumba kwa mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania‘Taifa Stars’, Jellah Mtagwa na wasanii wengine 14 ambao wamekamilisha michango ya ujenzi  wa nyumba zao katika kijiji chao cha Mwanzega Kimbili, Mkuranga.
   
  Wengine watakaokabidhiwa nyumba zao ni msanii maarufu nchini, Lumole Matovola ‘Big’ wa Bongo movie ambaye ni wanachama wa SHIWATA wangine ni Mwandishi wa Habari, Josephine Moshi, Farida Ndimbo wa Jeshi la Magereza, Flora Kafwembe wa JKT Mgulani na Nyanza Kisadugwa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).  
   
   Mpaka sasa SHIWATA imejenga nyumba 24 kwa ajili ya wasanii katika eneo la hekari 300 na wanajiandaa kulima shamba la hekari 500 walizonazo ili kujikwamua kimaisha.

  0 0


  Afisa uhusiano na matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki, akikagua timu wakati wa uzinduzi wa michuano ya Airtel Rising Stars katika mkoa wa kisoka wa Temeke ambapo Faru Boys football ilichuana na timu ya Mapambano katika mechi ya ufunguzi.
  Beki wa timu ya Faru Boys Nassoro Dibagula (kushoto) akitoa mpira katika eneo la hatari mbele ya Abdalah Juma wa Mapambano katika mechi ya ufunguzi wa michuanoa ya vijana wenye umri chini ya miaka17 ya Airtel Rising Star,. Mkoa wa Temeke, uliofanyika kwenye uwanja wa Twalipo jijini Dar es Salaam Juni 25, 2013. Faru Boys ilishinda 1-0.

  Timu ya Mbaspo Academy ilifanya mauaji juzi Jumanne kwa kubamiza bila huruma timu ya Mbeya Sekondari 6-0 katika mashindano yanayoendelea ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars ngazi ya mkoa. Mechi hiyo ilichezwa kwenye kiwanja cha Magereza mkoani Mbeya.

  Washindi walifungua kitabu chao cha magoli katika dakika ya sita kupitia kwa mshambuliaji wao mahili Jackson Mwaibale aliyefunga magoli manne peke yake. Mshambuliaji huyo kinda aliifungikia tena timu yake magoli matatu katika dakika za 16, 20 na 74. Wanafunzi wa shule ya sekondari Mbeya waliokuja kushangilia timu yao walijikuta kwenye hali ya kukata tamaa baada ya timu yao kuwanyong’onyesha na wapinzani wao Mbaspo.

  Peter Noah, mshambuliaji mwingine hatari wa timu ya Mbaspo, aliifungia tena timu yake katika dakika ya 30. Alikua ni yeye tena katika dakika ya 68 alipoitimisha kalamu ya magoli baada ya kuwapita walinzi wa Mbeya Sekondari na kumuacha golikipa akiduwaa baada mpira kutinga wavuni.

  Kwa upande mwingine timu ya Faru Boys football walipata ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya wapinzania wao Mapambano katika mechi ya ufunguzi ya ARS, katika mkoa wa Temeke uliofanyika katika uwanja wa Twalipo jumanne jioni jijini Dar es Salaam.

  Timu zote zilianza mchezo kwa kasi na babada ya kosa kosa za hapa na pale hatimaye Yohana Joseph ilifanikiwa kuitoa kimasomaso timu yake alipounganisha krosi kutoka upande wa kushoto ambayo iliingia moja kwa moja wavuni. Goli hili lilipokelewa kwa furaha na washabiki wa Faru.

  Mchezo mwingine wa Another Airtel Rising Stars, mkoa wa Ilala, ilichezwa kwenye kiwanja cha soka cha shule ya sekondari ya Benjamin William Mkapa ambapo timu ya Amana Shooting ilishinda 2-0 dhidi ya Msimamo Youth Academy. Magoli hayo yalipatikana kupitia kwa Isiaka Mohamed dakika ya 22 na Ally Shaban dakika ya 68.

  Mkoa wa Mwanza ulitarajia kuzindua mechi zake za ARS ngazi ya mkoa leo, Juni 26 wakati Morogoro na Mbeya walitarajiwa kuendeleza na mechi za mashindano hayo leo, Juni 26, 2013.

  Wakati huo huo, mkoa wa kisoka wa Kinondoni umetangaza kombaini yao ya wachezaji 15 watakaowakilisha mkoa huo kwenye mashindano ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa yatakayofanyika wenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 2 hadi 7.

  Wachezaji hao ni Hamza Mohamed, Hamza Abdallah, Twalib Athuman, Fred Bakari, Hazzad Jumanne, Salim James, Abubakary Mohamed, Willy Kalolo, Didas Proches, Mustafa Yusuf, Rashid Khalifan, James Msuva, Isiaka Lukana, Ally Amin na Shabani Idd.

  0 0

  Mtoto Faith Warioba anayesoma katika shule ya awali ya Montessori jijini Dar es Salaam akimlaki kwa maua Rais Mahinda Rajapaksa wa Srilanka muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ziara ya kikazi nchini huku Rais Dkt.Jakaya Kikwete akishuhudia.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mgeni wake Rais Mahinda Rajapaksa wa Srilanka muda mfupi baada ya kuweasili nchini kwa ziara ya kikazi leo asubuhi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.Kushoto ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik.
  Rais wa Srilanka Mhe.Mahinda Rajapaksa akisalimia na Msaidizi wa Rais Masuala ya Kidiplomasia,Balozi Liberata Mulamula wakati Rais Kikwete alipokuwa akiwatambulisha baadhi ya viongozi na wasaidizi wake kwa mgeni wake muda mfupi baada ya kuwasili nchini kwa ziara ya kikazi leo asubuhi.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais wa Srilanka Mhe.Mahinda Rajapaksa wakipokea heshima za urais muda mfupi baada ya mgeni huyo kuwasili katika uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
  Rais Wa Sri Lanka Me.Mahinda Rajapaksa akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa na Jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo asubuhi kwa ziara ya kikazi nchini.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Mahinda Rajapaksa wa Sri Lanka wakiangalia vikundi mbalimbali vya ngoma za utamaduni vilivyokuwa vikitumbuiza katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakati wa shamrashamra za kumpokea mgeni huyo wakati alipowasili leo asubuhi kwa ziara ya kikazi nchini.(picha na Freddy Maro).

  0 0

  TAARIFA KWA MADAKTARI ,WAFAMASIA , MAAFISA AFYA MAZINGIRA NA MAAFISA WATEKNOLOJIA MAABARA WALIOPANGIWA VITUO VYA KAZI WAKIWA BADO WAKO KWENYE MAFUNZO KWA VITENDO (INTERNSHIP).

  Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii anapenda kuwataarifu waajiri wote kwamba, katika zoezi la upangaji wa vituo vya kazi imebainika kwamba kwa bahati mbaya wamepangwa madaktari ,wafamasia , maafisa afya mazingira na maafisa wateknolojia maabara ambao bado wako kwenye mafunzo kwa vitendo (internship).

  Madaktari ,wafamasia , maafisa afya mazingira na maafisa wateknolojia maabara hawa, hawajasajiliwa kwenye mabaraza yao ya kitaaluma ikiwa ni moja ya masharti wanayotakiwa kutimiza kabla ya kuajiriwa Serikalini kwa mujibu wa Waraka wa Utumishi Na.1 wa mwaka 2009, kuhusu miundo ya kada zilizo chini ya Wizara ya Afya na ustawi wa Jamii. Kwa taarifa hii, wahusika wameondolewa kwenye orodha ya waliopangiwa kazi na nafasi zao zitajazwa na wataalam wengine wenye sifa kwa mujibu wa Muundo.

  Aidha, kwa tangazo hili, tunapenda kusisitiza kwamba kwa wale wote waliopangiwa vituo vya kazi wakaripoti moja kwa moja kwa mamlaka ya ajira zao wakiwa na vyeti vya kumaliza mafunzo kwa vitendo (Internship),usajili wa muda(MD), usajili wa kudumu(DDS) na wafamasia.Hakutakuwepo barua maalum za kuwatambulisha kama ilivyokuwa miaka ya nyuma, hivyo waajiri wote wanatakiwa kuwapokea na kuwapangia kazi.

  Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza na utakaojitokeza kwa waajiri pamoja na wataalam waliopangiwa vituo kwa makosa.

  Orodha ya wataalam waliopangiwa vituo vya kazi kwa makosa ni kama ifuatavyo:

           MADAKTARI WALIO KWENYE MAFUNZO KWA VITENDO NA AMBAO HAWAJASALIWA
          JINA    JINSI   ANUANI  KITUO CHA KAZI
  1       DR. ADROSTER METHOD KYAKABANJA  KE      C/O SEKOU TOURE REG. HOSP. S.L.P. 132, MWANZA   MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA KYERWA
  2       DR. CASTORY J. MWANGA   ME      S.L.P. 1470 MOSHI       KATIBU TAWALA MKOA WA  MTWARA
  3       DR. CHRISTIAN MICHAEL   ME      SLP 65007, DSM. MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA MAKAMBAKO
  4       DR. DANSTAN NGENZI      ME      S.L.P. 8, IRINGA        MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA MULEBA
  5       DR. DAVID MWASOTA       ME      S.L.P. 1483, MBEYA      KATIBU TAWALA MKOA WA  SINGIDA
  6       DR. ENOCK F. MOYO       ME      SLP 82, SONGEA. MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA SIMANJIRO
  7       DR. ESTHER TIMOTH       KE      SLP 9083 DSM    KATIBU TAWALA MKOA WA ARUSHA
  8       DR. FAUSTINA E. MBUYA   KE      SLP 2946, DSM.  KATIBU TAWALA MKOA WA  LINDI
  9       DR. FEISAL  A. SAID     KE      10773 DSM       MKURUGENZI WA JIJI TANGA
  10      DR. FELICIAN KACHINDE   ME      S.L.P. 2289, DSM        MKURUGENZI WA MANISPAA YA KIGOMA
  11      DR. FRIDA PASCAL NJAU   KE      SLP 11535, ARUSHA.      MKURUGENZI WA MANISPAA YA ARUSHA
  12      DR. FURAHA MWAKAFWILA   ME      SLP 29, TUNDUMA.        MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA KILOLO
  13      DR. GABRIEL CHAMBALO    ME      C/O JUMA M. MAKUNGUS.L.P. 25, MEATU     MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA MEATU
  14      DR. GENDAGENDA MKOMBOZI ME      SLP 65014, DSM. MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA SERENGETI
  15      DR. GORDIAN J. KIKOMPOLISI      ME      S.L.P. 65007, DSM       MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA MISENYI
  16      DR. HALID GONGORO       ME              MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA BAGAMOYO
  17      DR. HAMIDU ADINANI      ME      S.L.P. 1438, MOSHI      KATIBU TAWALA MKOA WA  SIMIYU
  18      DR. HENRICK B. MAHENGE  ME      S.L.P 1446 IRINGA       KATIBU TAWALA MKOA WA  KILIMANJARO
  19      DR. HENRY CHINYUKA      ME      C/O GOOD SAMARTAN OF TZ S.L.P. 3010 MOSHI       MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA ULANGA
  20      DR. HENRY JACKSON       ME              KATIBU TAWALA MKOA WA  SINGIDA
  21      DR. HONSIA ELISA MOSHI  ME      S.L.P. 419, MBEYA       MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA SIKONGE
  22      DR. IMMACULATE HENRY KALUNGI    KE      SLP 65471, DSM. KATIBU TAWALA MKOA WA  RUKWA
  23      DR. JAIROS N. HILIZA    ME      C/O MULERA PARISH, SLP 71, KASULU.      MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA UVINZA
  24      DR. JANE KAGOLI MAGANGA KE      SLP 10255, MWANZA.      KATIBU TAWALA MKOA WA  KAGERA
  25      DR. JOHN LUHAGA ME      S L P 1464, BUGANDO     MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA MISUNGWI
  26      DR. LEE M. MWAKALINGA   ME      S.L.P. 3888, MBEYA      MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA RUNGWE
  27      DR. MAJA LUKANYA SOSOMA ME      S.L.P. 361, BARIADI - SIMIYU    MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA BUKOMBE
  28      DR. MAJALIWA GERALD MARWA       ME              KATIBU TAWALA MKOA WA  KILIMANJARO
  29      DR. MANYANZA SYLVESTER MPONEJA  ME      S.L.P. 31891, DSM       KATIBU TAWALA MKOA WA  NJOMBE
  30      DR. MARIA E. KAPINGA    KE      SLP 5628 DSM    MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA UVINZA
  31      DR. MHANDO JOHN ME      S.L.P. 904, DODOMA      KATIBU TAWALA MKOA WA  MOROGORO
  32      DR. MUSSA GABRIEL       ME      SLP 419 MBEYA   KATIBU TAWALA MKOA WA  NJOMBE
  33      DR. NASSIB DAUD MSUYA   ME      SLP 419, MBEYA. MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA NZEGA
  34      DR. NIKUNDIWE KAJIRU    ME      S.L.P. 419, MBEYA       MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA KYELA
  35      DR. NTUGWA NYOROBI      ME      S.L.P. 1, MASWA SIMIYU  KATIBU TAWALA MKOA WA  SIMIYU
  36      DR. NURU NDOMONDO       KE              KATIBU TAWALA MKOA WA  KAGERA
  37      DR. RAJABU A. MRAMBA    ME      SLP 11501, DSM. KATIBU MKUU WAIZARA YA FYA NA USTAWI JAMII (MBEYA RUFAA)
  38      DR. SAMWEL C. MKUMBE    ME      SLP 2923, MBEYA.        MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA HANDENI
  39      DR. SHEEL AHMED SALEEM  ME      S.L.P. 40552, DSM       MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA LINDI
  40      DR. SOPHIA VALERIAN MOSHA       KE      SLP 132, MWANZA.        KATIBU TAWALA MKOA WA  KAGERA
  41      DR. SUKE  KUBITA MAGEMBE        ME      SLP 132, MWANZA.        MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA KWIMBA
  42      DR. WBESTER CHAMI       ME      S.L.P 152 S'WANGA       KATIBU MKUU WAIZARA YA FYA NA USTAWI JAMII (SUMBAWANGA CATC)
  43      DR. WILLIAM BENEDICT KAIJAGE    ME      SLP 33, KALIUA. KATIBU TAWALA MKOA WA  TABORA
  44      DR. ZAWADI BWANALI      ME      S.L.P. 634, MASASI      KATIBU TAWALA MKOA WA MTWARA
  45      DR. ZENA A. SULEIMAN    KE      S.L.P 72735 DSM KATIBU TAWALA MKOA WA  SIMIYU


  WAFAMASIA WALIO KWENYE MAFUNZO KWA VITENDO (INTERNSHIP)
          JINA    JINSI   ANUANI  KITUO CHA KAZI/MWAJIRI
  1       ANOLD KATIKIRO  ME      S.L.P 419 MBEYA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA MASWA
  2       APOLINARY MWAKABANA     ME      S.L.P 170 IPINDA - KYELA        MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA MOMBA
  3       ERIC MUHIKAMBELE        ME      S.L.P 5472 MOROGORO     KATIBU TAWALA MKOA WA TANGA
  4       EULAMBIUS MATHIAS       ME      S.L.P.267, LUSHOTO      MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA LUSHOTO
  5       KALENDOLO J. MASATU     ME              MKURUGENZI WA MANISPAA YA TEMEKE
  6       MAGEMBE K. NGASSA       ME      S.L.P.100, SAME KATIBU MKUU WIZRA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
  7       MARTIN JACKSON  ME      S L P 87, ARUSHA        KATIBU TAWALA MKOA WA MARA
  8       MOHAMED S. ULOMBE       ME      S.L.P 31791 DSM MKURUGENZI WA MANISPAA YA MTWARA
  9       MUSTAPHA LUTAVI ME      S L P24258, DAR ES SALAAM       MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA HANDENI
  10      OSWALD MWIHAVA  ME      S.L.P 19374 DSM KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI
  11      SYLIVIA S. SWAI KE      S LP 860, BUKOBA        MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA BUKOBA
  12      THERESIA  E. SHEMSIKA   KE      S.L.P.3054, MOSHI       KATIBU MKUU WIZRA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
  13      TIMOTHEO SAMWEL ME      S.L.P 419 MBEYA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA MLELE
  14      CHIMPAYE JULIUS ME      S.L.P 12654 DSM MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA RORYA
  15      KENETH JOHN     ME      S.L.P 154  MANYONI SINGIDA      MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA BUKOMBE
  16      MASUDI LUGANDYA ME      S.L.P 1370 MWANZA       MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI MASASI
  17      RENATUS FRANCIS ME      S.L.P 44 MWANZA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA NAMTUMBO

          MAAFISA AFYA MAZINGIRA DARAJA LA II  WALIO KWENYE MAFUNZO KWA VITENDO
  NA      JINA KAMILI     JINSIA  ANUANI  KITUO CHA KAZI
  1       WINFRIDA TIBAKYA        F       S.L.P104467 DSM MKURUGENZI WA MANISPAA YA MOSHI

          MAAFISA WATEKENOLOJIA MAABARA   WALIO KWENYE MAFUNZO KWA VITENDO
  NA      JINA KAMILI     JINSIA  ANUANI  KITUO CHA KAZI
  1       JACKSON E MACHA ME      S L P 317, OLD MOSHI    MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA KOROGWE
  2       TEDDY F. MSAKI  KE      S.L.P 480 MOSHI MKURUGENZI WA MANISPAA YA MOSHI
  3       JONATHAN J MUFUMYA      ME      S L P 79601, DAR ES SALAAM      MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA MAKAMBAKO


  KAIMU KATIBU MKUU
  27/6/2013

  0 0

   Meneja Chapa wa Tigo Tanzania Bw. William Mpinga akiongea na waandishi wa habari kuhusu tamasha kubwa la Tigo Mini Kabaang litakalofanyika siku ya jumapili hii bure kabisa katika viwanja vya  CCM Kirumba jijini Mwanza, kushoto msanii Diamond Platnumz na kulia msanii Madee ambao watatoa shoo siku hiyo na wasanii wengine. 
   Msanii wa bongo flava Diamond Platnumz akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu tamasha kubwa la Tigo Mini Kabaang litalofanyika mjini Mwanza siku ya jumapili pembeni yake Meneja Chapa wa Tigo Tanzania Bw. William Mpinga. 
   Msanii Madee akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu tamasha kubwa la Tigo Mini Kabaang litalofanyika mjini Mwanza siku ya jumapili pembeni yake ni Meneja Chapa wa Tigo Tanzania Bw. William Mpinga na Diamond Platnumz . 
   Msanii Richie Mavoko akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu tamasha kubwa la Tigo Mini Kabaang litalofanyika mjini Mwanza siku ya jumapili kulia kwake ni Msanii Madee, meneja wa Tigo Bw. William Mpinga na Diamond Platnumz.

  0 0  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Kiongozi wa Shirika la UNDP(UNDP Administrator) Bi. Helen Clark ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha na kufanya mazungumzo na Kiongozi wa Shirika la UNDP(UNDP Administrator) Bi. Helen Clark ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Spika wa bunge la Oman Mhe. Sheikh Khalid Bin Hilal Al Mawaali ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wajumbe waliofuatana na Spika wa Bunge la Oman ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Spika wa Bunge la Oman Mhe.Sheikh Khalid Bin Hilal Al Mawaali ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Oman Mhe.Sheikh Khalid Bin Hilal Al Mawaali na ujumbe wake ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.kulia ni Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai.
  (picha na Freddy Maro).

  0 0


  WADAU WA MTANDAO WETU WA FULLSHANGWE TUNAWAOMBA RADHI KWA USUMBUFU ULIOJITOKEZA KUANZIA LEO KUTOKANA NA MTANDAO WETU KUTOKUWA HEWANI KUTOKANA NA SABABU ZILIZO NJE YA UWEZO WETU HATA HIVYO WATAAAMU WETU WANAFANYA KILA LIWEZEKANALO ILI TUWEZE KUREJEA WAKATI WOWOTE 

  TUNATUMIA NAFASI HII PIA KUWAOMBA RADHI WADHAMINI WETU NMB, NBC SBL, NHIF NA WILNA INTERNATIONAL TUNAOMBA MTUVUMILIE WAKATI TUNASHUGHULIKIA TATIZO HILO.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal akikagua Gwaride Maalum lililoandaliwa na Wahitimu wa kozi ya Uofisa na Ukaguzi wa Jeshi la Polisi leo katika Chuo cha Taaluma ya Polisi, Kurasini, Jijini Dar Es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal akimvisha Cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Mhitimu wa Kozi ya Ukaguzi wa Polisi INSP. Leah Cheyeki kwa niaba ya Wahitimu wenzake kutokana na kufanya vizuri katika Mafunzo hayo. Sherehe za kuhitimisha Mafunzo hayo zimefanyika katika Chuo cha Taaluma ya Polisi leo Kurasini, Jijini Dar es Salaam.
  Wahitimu wa kozi ya Uofisa na Ukaguzi wa Polisi wakipita mbele ya Mgeni Rasmi kwa mwendo wa haraka Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayupo pichani. Sherehe za kuhitimisha Mafunzo hayo zimefanyika leo katika Chuo cha Taaluma ya Polisi, Kurasini, Jijini Dar es Salaam.
  Kikosi cha Judo kikionesha Onesho Maalum la namna ya kupambana na Mhalifu ambaye hataki kutii amri halali ya Polisi. Sherehe za kufunga Mafunzo ya Kozi ya Uofisa na Ukaguzi wa Polisi zimefanyika Chuo cha Taaluma ya Polisi, Kurasini, Jijini Dar es Salaam.

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Dkt. Emmanuel John Nchimbi(wa pili kutoka kushoto mwenye suit nyeusi)akiwa na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama ambao wamehudhuria Sherehe hizo za ufungaji Mafunzo ya Kozi ya Uofisa na Ukaguzi wa Polisi(katikati) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja.
  Baadhi ya Wananchi waliohudhuria Sherehe za Ufungaji Mafunzo ya Kozi ya Uofisa na Ukaguzi wa Polisi katika Chuo cha Taaluma ya Polisi, Kurasini Jijini Dar es Salaam(Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

  0 0
 • 06/27/13--21:44: Chezea Obama weyeee
 • Akina mama wakifanya usafi barabarani asubuhi hii maeneo ya chang'ombe jijini Dar


  0 0
 • 06/29/13--00:21: MTEMVU ALIVYOUNGURUMA TEMEKE
 •  Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (aliyevaa miwani katikati), akifuatwa na wananchi baada ya kumaliza mkutano wa kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Kata ya Temeke, Dar es Salaam hivi karibuni.
   Mbunge wa Jimbo la Temeke, Dar es Salaam, Abbas Mtemvu akihutubia katika mkutano wa hadhara wa kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Kata ya Temeke, Dar es Salaam hivi karibuni. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
   Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu akimsikiliza Mweka Hazina wa Kikundi cha Kuweka na Kukopa (VICOBA), Anjela Ndigula ambaye alipokea sh. 50,000 alizotoa msaada kwa Muya Thabit ili ajiunge na kikundi hicho, baada ya kuambiwa hana haki hivyo anashindwa kulipia pango. Msaada huo aliutoa katika mkutano wa hadhara wa kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Kata ya Temeke, Dar es Salaam hivi karibuni.
   Muya Thabit akicheza kwa furaha baada Mbunge Mtemvu kumsaidia fedha za kujiunga na vicoba
   Diwani wa Kata ya Temeke, Khamis Nsombo, akiwazawadia fedha wasanii wa kikundi cha Msimamo

  Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu akikizawadia fedha kikundi cha sanaa cha Msimamo kilichokuwa kinatumbuiza katika mkutano wa hadhara wa kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Kata ya Temeke, Dar es Salaam hivi karibuni. Pia aliahidi kukipatia kikundi hicho sh. 500,000 za kununulia vifaa zikiwemo ngoma.


   Mtemvu akiangalia wakati msanii wa Msimamo akicheza ngoma
                               Wasanii wakicheza ngoma ya Lizombe ya asili ya Mkoa wa Ruvuma
                                               Msanii akichangamsha mkutano huo
                           Mtemvu akiteta jambo na Diwani wa Kata ya Temeke, Khamis Nsombo
                                                Nsombo akiteremka kutoka jukwaani baada ya kuhutubia
                                                         Mtemvu akiwasalimia wananchi
                             Muya Thabit akiomba fedha kwa Mbunge Mtemvu ili alipe pango
                                      Wananchi wakiuliza maswali kwa Mbunge wao Mtemvu

  0 0

   Washiriki katika mafunzo ya uongozi na biashara yananofanyika kwenye Ukumbi wa Nafasi Jijini Dar es Salaam wakifuatilia mafunzo hayo, washiriki hao wametoka katika taasisi mbalimbali zinazojishughulisha na sanaa na sanaa za maonesho.  Mafunzo haya yanatolewa na Britishi Council, na mwezeshaji ni Faisal Kiwewa kutoka shirika la Bayimba la nchini Uganda.

  0 0


  Bendi ya Mashauzi Classic chini ya I sha Mashauzi imeandaa Uzinduzi Rasmi wa Ukumbi wa Nawina Resort Mbagala kuu baada ya Matengenezo kutokana na ajali ya moto iliyotokea mwanzoni mwa mwaka huu.

  akizungumzia Uzinduzi huo mkurugenzi wa Nawina Resort Marry Komba, amesema kwamba Matayarisho yamekamilika na Tayari Isha Mashauzi na Kundi lake wamekamilisha taratibu zote kuhusiana na Onyesho hilo la Uzinduzi siku ya jumamosi tarehe 29 mwezi huu.

  "Kikubwa ninamshukuru Mungu kwa kuwezesha kukamilika kwa Ukumbi huu wa Nawina Resort, kama unavyojulikana ukumbi huu na wakazi wengi wa Mbagala Kuu, ndiyo pekee uliokuwa ukiwapatia burudani mbalimbali wakazi wa maeneo haya a Vitongoji vyake vyote, kwa hiyo nawaomba wakazi wa mbagala Kuu waendelee kuunga mkono juhudi hizi ambazo ni kiburudisho kwao, nachukua fulsa hii kuwakaribisha sana siku ya Ufunguzi ili waweze kufika kushuhudia Nawina Mpya chini ya Mashauzi Classic" alisema Marry Komba

  Awali kabla ukumbi wa Nawina Resort aujaungua Moto, ulikuwa ni kati ya Miimili ya Burudani iliyokuwa ikiwapa raha wakazi mbalimbali wa Mbagala, ikiwa ni pamoja na Miziki ya Kizazi kipya, Miziki ya Bendi, Taarabu na hata vikundi vya Sanaa kutoka kwa wasanii mbalimbali hapa nchini.

  kwa Upande wake Isha Ramadhani maaufu kama Isha Mashauzi amesema kwamba wamejipanga kufanya Onyesho kali na la kusisimua ambapo wakazi wa Mbagala Kuu na Vitongoji vyake wafike ili waweze kufurahia Burudani kutoka katika kundi lake," Nimejipanga vizuri kuhakikisha wakazi na wapenzi wangu tunafanya kitu kipya na siku hiyo nitawapa pia vitu vipya kwa kuwa ni siku ya Ufunguzi wa Ukumbi Mpya, maana hivi sasa Nawina ni mpya kwa hiyo tutaingia na nyimbo zingine mpya ambazo ni burudani ya kupendeza" alisema Isha Mashauzi

  katika onyesho hilo ambalo linatarajia kuanza majira ya saa mbili za Usiku , kiingilia  kimewekwa cha kuridhisha ili kuwafanya wakazi wote wa mbagala kufika ili kupata burudani wakiwa nafamilia zao kwa shilingi 5000 tu.

  Kuhusiana na Ulnzi wa mali za wote watakaofika, Usalama wa vyombo vya Usafiri , mkurugenzi wa Nawina Resort  Marr Komba alisema kuwa ulinzi ni wa kutosha kwa wote watakaofika siku hiyo.

  0 0

  Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani DCP Mohammed Mpinga akipokea funguo kutoka kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe. Pereira Silima baada ya Pikipiki hizo kukabidhiwa na SUMATRA Mjini Morogoro junni 2013.
  Wajumbe wakisikiliza utekelezaji wa Maazimio kutoka kwa Insp. Sokoni wakati wa Mkutano wa watendaji wa SUMATRA na Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mjini Morogoro katika Hotel ya Glonency 88 .
  Kaimu Mkurugenzi wa SUMATRA Ahmed Kilima akimkabidhi Pikipiki 5 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Pereira Silima ambaye alikuwa Mgeni Rasmi wakati wa ufungaji wa Mkutano wa watendaji wa Jeshi la Polisi na SUMATRA mjini Morogoro.

  0 0

  Washiriki wakijaribu kutumia kipimo kupima kipenyo cha mti katika mafunzo hayo Picha zote na Asteria Muhozya, Afisa Habari  Wizara ya  Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto.
  Baadhi ya Maafisa Habari katika mafunzo ya vitendo kuhusu namna ya  kupima urefu wa mti ili kuweza kujua kiwango cha kaboni iliyomo katika miti. Zoezi hili limefanyika katika msitu wa kupandwa Morogoro.
  Dr. Zahabu akitoa maelekezo ya namna ya zoezi zima la kupima upana wa misitu linavyofanyika.

  Mafunzo ya kuwajengea Uelewa Maafisa Habari kutoka katika Wizara zinazohusika moja kwa moja na masuala ya mazingira kuhusu Namna ya Kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi . Vilevile Mpango wa Kupunguza Uzalishaji wa Hewa ya Ukaa kutokana na Ukataji Miti ovyo na Uharibifu wa Mazingira. Mafunzo haya yametolewa na Regalia Media kwa ufadhili wa REDD 

older | 1 | .... | 109 | 110 | (Page 111) | 112 | 113 | .... | 1898 | newer