Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live

BAADHI YA WAKAZI WA MWENGE MSHINDO WA MSHITAKI MBUNGE WAO KWA NAIBU WAZIRI DKT. ANGELLINA MABULA

0
0

Baadhi ya wakazi wa mwenge mshindo manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wamemshitaki Mbunge wao Leonidas Gama kwa Naibu Waziri wa ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angellina Mabula kwa kuwazulumu maeneo yao.


TUZO ZA UMAHIRI WA UANDISHI WA HABARI TANZANIA

0
0

WAZIRI MKUU AZINDUA SAFARI ZA ATCL DAR/DODOMA

0
0
Mapema asubuhi Leo; Baadhi ya wabunge wakisafiri kwa ndege ya Air Tanzania kuelekea Dodoma.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua safari za ndege za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kutoka jijini Dar es Salaam kwenda Makao Makuu ya Nchi, Dodoma.

Akizindua safari hizo leo (Jumatatu, Januari 16, 2017) amesema safari hizo zitawezesha wafanyabiashara na wananchi wengine kutoka Dodoma na kwenda katika maeneo mengine kwa urahisi. Amesema kuanzishwa kwa safari hizo ni moja ya utekelezaji wa ahadi za Mheshimiwa Rais, Dkt. John Magufuli za kufufua ATCL na kuboresha usafiri wa anga nchini.

Aidha, Waziri Mkuu ametoa wito kwa watumishi wa umma, wafanyabiashara na wananchi wa Dodoma kutumia ndege hizo kwa safari za kwenda katika maeneo mbalimbali kwani ni za uhakika na gharama zake ni nafuu. “Tuna ndege nzuri. Tuzitumie kwenda katika maeneo mengine kwani gharama zake ni nafuu. Kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam ni sh. 165,000, kwenda na kurudi ni sh. 299,000,” amesema.

Amesema ndege nyingine kama hiyo inatarajia kuwasili nchini Juni mwaka huu jambo ambalo litaongeza idadi ya safari za ndege hizo nchini na maeneo mengine ya nchi jirani. Naye Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai ametoa wito kwa wakazi wa Dodoma kutumia vizuri fursa hiyo ya safari za ndege za ATCL kwa kuwa utawawezesha kusafiri kwa muda mfupi tofauti na vyombo vingine vya usafiri.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bw. Jordan Rugimbana ameshukuru kwa uanzishwaji wa safari hizo kwa kuwa zitarahisisha kutoka katika Makao Makuu ya nchi na kwenda katika mikoa mingine nchini.

Naye Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Malecela ameupongeza uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli kwa namna anavyofanya kazi. Amefurahishwa na uanzishwaji wa safari hizo.

Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa ATCL. Kapten Richard Shaidi ametumia fursa hiyo kuipongeza Serikali kwa ujio wa ndege hizo na kwamba hiyo ni moja ya mikakati ya Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli ya kufufua ATCL.

“Hivi karibuni tunaanza kwenda nchi jirani. Mwakani tutapata ndege nyingine kubwa itakjayokuwa inafanya safari za masafa ya kati na ya mbali. Naipongeza Serikali kwa kutoa ahadi na kuitekeleza kwani kutoa ahadi ni jambo rahisi ila utekelezaji wake ndiyo kazi. Lakini Serikali imeweza,” amesema.

Aidha, Mwenyekiti wa Bodi ya ATCL, Bw. Emmanuel Korosso amesema hivi karibuni shirika hilo linatarajia kuanza safari za kwenda katika miji ya Tabora, Songea, Mtwara, Mpanda, Mafia na Jiji la Tanga.

Akizungumzia kuhusu safari za Dodoma amesema zitafanyika mara mbili kwa wiki, siku ya Ijumaa na Jumatatu. Hata hivyo wanatarajia kuongeza safari hapo baadae.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
JUMATATU, JANUARY 16, 2017.

Wachezaji wawasili kwenye kliniki Airtel Rising Stars

0
0
Wachezaji bora walioibuka kutoka katika mashindano ya Airtel Rising Stars msimu wa sita wamewasili rasmi leo kambini ili kuhudhuria mafunzo ya soka yaliyoandaliwa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF)

Mafunzo hayo yatakayodumu kwa muda wa wiki moja yanayotegemea kuanza kesho chini ya makocha wa timu za taifa za vijana yatashirikisha wachezaji nyota 65 kutoka katika mikoa mbalimbali iliyoshiriki michuano ya Airtel Rising Stars mwaka jana.

Akiongea na waandishi wa habari wakati kikosi hicho kilipowasili , Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF , Salim Madadi alisema” Tumejipanga vyema kupokea wachezaji hawa na kuwanoa ili kuendelea kutafuta vipaji kwa ajili ya timu zetu za vijana za taifa, ni matumaini yangu kuwa mafunzo haya ya muda mfupi yatawasaidia vijana hawa kupata mbinu za mpira lakini pia kuziwezesha timu zetu kupata wachezaji bora kwaajili ya vikosi vyao.”

Mmoja kati ya wachezaji walioingia kambini hapo Amrani Rajabu Kutoka Mogogoro Alisema” ninafurahi kuona kambi hii inafanyika kama tulivyoahidiwa na kwakweli najisikia furaha kuwa mmoja kati ya wachezaji waliofanya vizuri katika mashindano ya Airtel Rising Stars mwaka jana. Nimejipanga kutumia fursa vyema kwani naamini huu ndio mwanzo mzuri wa safari yangu ya kuwa mchezaji nyota duniani. nawashukuru sana Airtel kwa kuanzia mpango huu na kutupatia nafasi ya kuonyesha vipaji vyetu.”

Wachezaji waliowasili kambini ni pamoja na Anthony Alfred (Mbeya), Amrani Rajabu (Morogoro), Yassin Ally (Temeke), Adam Almasi (Temeke), Mustafa Mhando (Kinondoni), Nickson Dimoso (Morogoro), Salum Mgonza (Kinondoni), Abdul Hassan (Morogoro), Benjamin Kawambwa (Mbeya), Yusuf Abdul (Temeke), Ibrahim Ngoitame (Morogoro), Mathias Juan (Ilala), Kambi Ramadhan (Kinondoni), Daniel Ndalo (Mwanza), Salum Yohana (Kinondoni), Esmail Kovu (Temeke), Munir Mzee (Ilala), Idrissa Omar (Ilala), Patrick Reuben (Morogoro), Ramadhan Gido (Mwanza), Said Maulid (Temeke), Ally Hamisi (Kinondoni), Nyamawi Athumani (Morogoro), Jabir Masumbuko (Morogoro), Tepsi Evance (Morogoro), Ernes Kamage (Mbeya), Gustafa Simon (Ilala), Ramadhan Chundo (Temeke), Hassan Kapera (Kinondoni), Juma Abdul (Ilala), Lameck Juma (Mbeya), Shabani Mangula (Kinondoni), Michael Joseph (Mwanza), Boniface Makala (Morogoro), Abdillah Kihulo (Temeke), Albinius Haule (Mbeya) kwa wanavulana na wasichana ni pamoja na Agatha Joel (Temeke), Fadhila Esmail (Arusha), Zubeda Mohammed (Kinondoni), Faraja Hamadi (ilala), Eva Jackson (Temeke), Violet Thadeo (Temeke), Zainabu Mrisho (Kinondoni), Fumu Mohammed (Ilala), Asphat Kasindo (Temeke), Elizabeth Julius (Temeke), Stella Wilbert (Kinondoni), Hawa Ally (Zanzibar), Christina Samuel (Temeke), Anna Anrea (Kinondoni), Grace Yusuf (Ilala), Shamimu Hamisi (Temeke), Mwantumu Ramadhani (Kinondoni), Hadlfa Mussa (Lindi), Zainabu Mrisho (Ilala), Fatuma Yusuf (Ilala), Eva Michael (Arusha), Oppa Msolidi (Temeke), Yustina Mboje (Temeke) na Zainabu Mohammed (Ilala).
wachezaji nyota wavulana wa Airtel Rising Stars wakiwa na Mkurugenzi wa ufundi wa soka la vijana TFF na kocha wa zamani wa timu ya taifa , Kim Paulsen mara baada ya kuwasilia kambini kwaajili ya mafunzo ya muda wa wiki moja .
 

Homa ya Ndege yagunduliwa Uganda

0
0
 Serikali ya Uganda, imethibitisha kuwepo kwa ugonjwa wa homa ya ndege katika maeneo karibu na fuo za Ziwa Victoria.
Virusi hivyo vimethibitishwa kwa ndege wanaohama, bata wanaofugwa na kuku.
Wakuu sasa wametoa tahadhari kwa jamii za maeneo hayo kuhakikisha kuwa ugonjwa huo hausambai na kuwaambukiza watu. Mwaandishi wa BBC nchini Uganda, Catherine Byaruhanga. Anasema kuwa ripoti za awali za ndege waliokufa zilianza kutolewa mwanzo tu wa mwaka huu.
Jamii za maeneo hayo, wamesema kuwa, walizipata mizoga ya ndege wengi waliokuwa wakihamia Uganda wakati wa majira ya baridi katika maeneo ya kaskazini mwa dunia.
Majaribio kadhaa yaliyofanywa na wataalamu, yalithibitisha kuwa, ndege hao walifariki kutokana na maradhi ya Highly Pathogenic Avian Influenza au bird flu, yaani homa kali ya ndege kama inavyofahamika.
Chembechembe zilizokusanywa kutoka kwa mizoga ya bata wa kufugwa na kuku, katika Wilaya moja ya eneo hilo karibu na Ziwa Victoria upande wa Uganda, zilithibitisha hilo.
Hakuna taarifa zozote za ugonjwa huo kuambukiza binadamu, na serikali ya Uganda imesema kuwa, inawashauri jamii za maeneo hayo kuhusu namna ya kujikinga kupatwa na ugonjwa huo na mbinu za kuzua kuzambaa zaidi.
Vikosi vya majanga ya dharura vimetumwa huko ili kukusanya mizoga ya ndege hao waliokufa.
Hii ni mara ya kwanza kwa mlipuko wa ugonjwa huo kutokea nchini Uganda, lakini mamlaka kuu ya nchi hiyo, imefumbua mbinu mpya ya kukabiliana kwa haraka namna ya kushughulikia majanga ya dharura ya kiafya, hasa kufuatia visa vya ugonjwa hatari wa Ebola.
CHANZO:bbcswahili

DC WA KAKONKO,KANALI NDAGARA AKUTANA NA BARAZA LA MADIWANI KUJADILI MIKAKATI MIPYA YA KUONGEZA MAPATO

0
0
 Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagara ameliomba baraza la madiwani la halmashauri ya Wilaya ya Kakonko na Mkurugenzi kubuni vyanzo ambavyo havita waumiza wananchi katika uchangiaji na kuwashirikisha Wananchi katika Shughuli za maendeleo ili kuhakikisha bajeti iliyo pangwa ya mwaka 2017-2018 inafanikiwa kwa asilimia 88% ya bajeti iliyopangwa kwa ukusanyaji mapato ipasavyo.

Pia aliwaomba Madiwani wa upinzani kuacha tabia ya kupinga rasimu ya pendekezo la bajeti iliyopendekezwa ya mwaka 2017-2018 pasipokuwa na hoja ya msingi ikiwa ni pamoja na kupinga kodi ya majengo ya kila mwananchi kuchangia kiasi cha shilingi 5000 kwa mwaka hali inayopelekea halmashauri hiyo kushindwa kuwa na vyanzo vingi vya mapato.

Rai hiyo aliitoa Jana (Leo) katika kikao cha baraza la madiwani cha kuipitia na kupitisha rasimu ya bajeti inayo pendekezwa na balaza hill ambapo Ndagara aliwaomba madiwani kuwashawishi Wananchi kuchangiq shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kuchangia Ujenzi wa vyumba vya madarasa na kuchangia michango mingine iliyopendekezwa kwenye rasimu ilikufikia lengo la kukusanya mapato kwa asilimia 80%.

Aidha Ndagara aliwaomba madiwani kwa kushirikiana na Mkurugenzi kubuni vyanzo vipya vya mapato ya ndani ilikuepuka viporo vilivyo baki kwa bajeti ya mwaka uliopitq ambapo halmashauri hiyo ilishindwa kufikia lengo na kukusanya mapato kwa asilimia 28% kutokana na kukosekana kwa vyanzo vipya vya mapato katika Wilaya.

"Ushauri wangu katika baraza hili kwenye hii bajeti mlio ipitisha nilazima kuwa na vipaumbele ilikuepuka hivi vipolo vilivyo baki niungane na Afisa mipango, tuwqshirikishe Wananchi kwa nguvu kubwa na tuache kuitegemea serikali siku zote lazima tukusanye kodi ilikuweza kuipatia halmashauri mapato kuacha kuweka vipingamizi visivyo kuwa na msingi ", alisema Kanali Ndagara.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Kakonko Lusubiro Mwakabibi aliwaomba madiWani kuikataa bajeti kwa hoja ya msingi, kupinga suala la kila mwananchi kuchangia shilingi 5000 kwa mwaka ni kupinga maendeleo hakuna mwananchi anaeweza kukosa kiasi hicho cha hela kwa mwaka suala la msingi tuongeze vyanzo vya ukusanyaji wa mapato.

Mwakabibi alisema Madiwani wanatakiwa kuwaelimisha Wananchi juu ya ulipaji modi na kuchangia mapato ya serikali, halmashauri ya kakonko ni halmashauri ya mwisho katika ukusanyaji wa mapato nchini kutokana na vyanzo vidogo vya ukusanyaji mapato halmashauri baada ya kuliona hill imeandaa vyanzo vipya vya mapato ilikuhakikisha mapato yanaongwezeka.

Nae Mwenyekiti wa halmashauri ya Kakonko Juma Maganga alisema halmashauri imeandaa bajeti ya shilingi bilioni 29.7 iliyopitishwa na madiwani ya mwaka wa fedha 2017 -2018 itakayo husisha makusanyo ya mapato ya ndani na fedha kutoka Serikali kuu itakayo saidia kukamilisha shuguli za maendeleo ya halmashauri hiyo.
MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagara akizungumza kwenye baraza la madiwani la halmashauri ya Wilaya ya Kakonko,katika suala zima la kupanga mkakati mpya wa kubuni vyanzo vya mapato ambavyo havita waumiza wananchi katika uchangiaji na kuwashirikisha Wananchi katika Shughuli za maendeleo ili kuhakikisha bajeti iliyo pangwa ya mwaka 2017-2018 inafanikiwa kwa asilimia 88% ya bajeti iliyopangwa.
 Baadhi ya Madiwani wakiwa kwenye baraza la madiwani la halmashauri ya Wilaya ya Kakonko,wakimsikiliza  Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagara alipokuwa akizungumza nao mapema jana katika suala zima la mkakati mpya wa kubuni vyanzo vipya vya mapato ambavyo havita waumiza wananchi katika uchangiaji na kuwashirikisha Wananchi katika Shughuli za maendeleo ili kuhakikisha bajeti iliyo pangwa ya mwaka 2017-2018 inafanikiwa kwa asilimia 88% ya bajeti iliyopangwa.  

ZANZIBAR INAZIDI KUKUA KWA KASI YA KIMAENDELEO-BALOZI WA KOREA KUSINI NCHINI

0
0

Balozi Song Kati kati akielezea faraja yake kwa Balozi Seif kutokana na Makampuni na Taasisi za nchi yake kuonyesha azma ya kutaka kusadia maendeleo ya Wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
Balozi Seif Kushoto akisisitiza malengo ya SMZ katika kuimarisha miundombinu ya sekta mbali mbali nchini ili kuwajengea maisha bora wananchi wake.
Balozi Seif Kushoto akimpatia zawadi ya vyakula vya viungo Balozi wa Korea Kusini Bwana Song mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Oisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.Picha na – OPMR – ZNZ.
Balozi wa Korea Nchini Tanzania Bwana Song Geum Yong akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Vuga Mjini Zanzibar walipokutana kwa kubadilishana mawazo.

Balozi wa Korea Kusini Nchini Tanzania Bwana Song Geum Yong amesema Zanzibar inazidi kubadilika Kimaendeleo kutokana na kasi kubwa ya miundombinu inayoendelea kuwekwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikiungwa mkono na Mataifa na Taasisi washirika wa Maendeleo.

Amesema Taasisi na Makampuni ya Korea yanafurahia mabadiliko hayo na kuamua kusaidia ujenzi wa Miradi ya Kielimu akiutolea mfano ule wa Skuli ya Sekondari ya Kwarara uliomalizika hivi karibuni ili kuipa nguvu zaidi Sekta ya Elimu Zanzibar ambayo ndio kichwa cha maendeleo hayo.

Balozi Song Geum Yong alieleza hayo wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar aliyekuwepo Visiwani Zanzibar katika uzinduzi wa Skuli hiyo pamoja na kuhudhuria maadhimisho ya sherehe za kutimia miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Alisema anapata faraja kuona kuwa ujenzi wa Skuli hiyo uliopata msaada kutoka Shirika la Maendeleo ya Korea { KOICA }, Good Neighbors, Shirika la Utangazaji la Korea { SBS } na Taasisi ya Wasanifu Majengo ya Korea umekwenda sambamba na ujenzi wa Kituo cha Habari cha Kimataifa cha Tumaini.

Balozi Song alieleza kwamba Kituo hicho cha kurekodia Matangazo ya Redio na Televisheni cha Tumaini kilichoanzishwa kwenye Skuli hiyo ya Sekondari Kwarara kwa kiasi kikubwa kitasaidia kutoa Taaluma kwa Wanafunzi pamoja na Wananchi wa sehemu mbali mbali hapa Zanzibar.

Akitoa shukrani zake kwa misaada mbali mbali inayotolewa na Korea kwa Tanzania na Zanzibar kwa jumla Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema Serikali inakusudia kujenga Bara bara ya lami inayoingia kutoka bara bara Kuu hadi kwenye Skuli hiyo ili kuwaondoshea usumbufu wa Mawasiliano Wananchi na Wanafunzi wa eneo hilo.

Balozi Seif alisema Korea ya Kusini inastahiki kupongezwa kwa jitihada zake za kuunga mkono maendeleo ya Zanzibar, lakini hata hivyo alimshauri Balozi Song kutumia maarifa yake katika kuzishawishi Taasisi na Makampuni ya nchi yake kuendelea kuelekeza nguvu zao katika uwekezaji wa sekta tofauti ikiwemo ile ya usafiri wa Baharini.

Alisema sekta ya Kilimo Zanzibar hasa katika upande wa umwagiliaji pia inastahiki kuungwa mkono zaidi ili kuwaongezea nguvu za uzalishaji Wakulima kwa vile zaidi ya asilima 80 ya Wananchi wa Visiwa vya Zanzibar wanaendesha maisha yao kwa kutegemea sekta hiyo.


Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

WAZIRI MKUU AZINDUA SAFARI ZA ATCL DAR/DODOMA

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea mfano wa Boarding Pass kutoka kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mahandisi Edwin Ngonyani kabla ya kusafiri kwa ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kutoka uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere, Dar es salaam kwenda Dodoma Januari 16, 2017. Alikuwa akizindua safari za ndege za shirika hilo kati ya viwanja viwili hivyo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kabla ya kupanda ndege ya Shirika hilo kwenye uwanja wa Ngege wa Julius Kambarage Nyerere kwenda Dodoma ikiwa ni uzinduzi wa safari za ndege za ATCL kati ya viwanja viwili hivyo, Januari 16, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisafiri kwa ndege ya Bombardier Q400 ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kutoka uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere kwenda Dodoma Januari 16, 2017. Alikuwa akizindua safari za ndege za ATCL katika viwanja viwili hivyo. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Leonard Chamuriho.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia viongozi na wananchi wa Dodoma baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Januari 16, 2017 ikiwa ni uzinduzi wa Safari za ndege za Shirika hilo kati ya viwanja viwili hivi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam ikiwa ni uzinduzi wa safari za ndege za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) Januari 16, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana ​ baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam ikiwa ni uzinduzi wa safari za ndege za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kati ya viwanja viwili hivyo, Januari 16, 2016. Wapili kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijan, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), Kapteni Richard Shaidi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam ikiwa ni uzinduzi wa safari za ATCL kati ya viwanja viwili hivyo, Januari 16, 2017. Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Leonard Chamuriho. Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Anthony Mavunde na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Christina Mndeme.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wafanyakazi wa Shirika la Ngege ya Tanzania (ATCL) baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ikiwa ni uzinduzi wa safari za ndege za ATCL kati aya viwanja viwili hivyo, Januari 16, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ikiwa ni uzinduzi wa safari za ndege za ATCL kati aya viwanja viwili hivyo, Januari 16, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Spika wa Bunge, Job Ndugai baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma akitoka uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ikiwa ni uzinduzi wa safari za ndege za ATCL kati aya viwanja viwili hivyo, Januari 16, 2017.
Mtendaji Mkuu wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), Kapteni Richard Shaidi akizungumza katika uzinduzi wa safari za ndege za ATCL kati ya Uwnja wa Julius Kambarage Nyerere na Dodoma,mjini Dodoma Januari 16, 2017. Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana akizungumza katika uzinduzi wa safari za ndege za ATCL kati ya Uwnja wa Julius Kambarage Nyerere na Dodoma,mjini Dodoma Januari 16, 2017. Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma .

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, akizungumza katika uzinduzi wa safari za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kati ya uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere na Dodoma Januari 16, 2017.
Waziri Mkuu, Mstaafu John Malecela akizungumza katika uzinduzi wa safari za ndege za ATCL kati ya Uwnja wa Julius Kambarage Nyerere na Dodoma,mjini Dodoma Januari 16, 2017. Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua safari za ndege za Shirika la Ndege la Tanzania kati ya uwanja wa Julius Kambarage Nyerere na Dodoma katika hafla iliyofanyika kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Januari 16, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Muhimbili Yatoa Msaada wa Vitanda 20 16-01-2017

0
0

Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Bi. Agness Mtawa akikabidhi vitanda vitano kwa Mganga Fawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Mafia, Abdallah Bhai. Vitanda hivyo vimetatumika kwa kina mama wakati wa kujifungua.
Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga wa hospitali hiyo, Bi. Agness Mtawa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi vitanda hivyo.
Mganga Fawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Mafia, Abdallah Bhai akizungumza na waandishi wa habari leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Mumbili (MNH) .
 
 
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imetoa msaada wa vitanda 20 vinavyotumika wakati kina mama wanapojifungua kwa Hospitali ya Wilaya ya Mafya , Hospitali ya Sinza-Palestina pamoja na Hospitali ya Temeke.

Kati ya vitanda hivyo , Hospitali ya Temeke watapatiwa vitanda vinane, Hospitali ya Sinza -Palestina vitanda saba wakati Hospitali ya Wilaya ya Mafya wamekabidhiwa vitanda vitano leo.

Akikabidhi msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili , Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga, Agnes Mtawa amesema lengo ni kuboresha huduma za afya na kumuwezesha mama kujifungua katika mazingira salama.

"Tulipata taarifa kwamba wenzetu wanahuitaji mkubwa wa vitanda vya kujifungulia hivyo tukaona tuwasaidie na hatutaishia hapa tutaendelea kushirikiana kadiri inavyowezekana," amesema Sister Mtawa.

Akipokea msaada huo, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Mafya, Abdalah Bhai amesema msaada huo umekuja wakati muafaka na kwamba vitanda hivyo vitakidhi mahitaji.

“ Hospitali ya Wilaya ya Mafya ilikua inahitaji vitanda vitano vya kujifungulia na leo wenzetu Muhimbili wametupatia vitanda hivyo, hivyo kulingana na mahitaji yetu tunawashukuru sana, tunawaomba wadau wengine wajitokeze kusaidia vitendea kazi vingine," amesema Mganga Mfawidhi Bhai.

Kwa mujibu wa Mganga huyo Mfawidhi awali hospitali hiyo ilikuwa na vitanda vya kujifungulia vitatu ambavyo vipo chini ya kiwango.

ZOEZI LA KUHAKIKI WATUMISHI WASTAAFU LAANZA MKONI KIGOMA.

0
0
Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kigoma

WATUMISHI wastaafu wa serikali wanaolipwa na serikali kupitia wizara ya fedha na mipango wameitaka serikali kurekebisha viwango vya malipo ya pensheni wanayolipwa sasa kufuatia kupanda kwa gharama za maisha ambako hakuendani na hali halisi ya malipo wanayolipwa.

Wakizungumza katika zoezi la uhakiki wa wastaafu wanaolipwa na wizara ya fedha na Mipango linaloendelea mkoani Kigoma, Wastaafu hao wamesema kuwa kwa sasa kiwango wanacholipwa wastaafu waliostaafu utumishi wao muda mrefu hakiendani na malipo yanayotolewa kwa wastaafu waliostaafu hivi karibuni.

Shaban Funenge mstaafu wa jeshi la wananchi wa Tanzania alisema kuwa wastaafu wengi ambao wamestaafu kwa zaidi ya miaka 10 wamekuwa na manung’uniko sana na kwamba serikali haina budi kufanya maboresho kwa wastaafu hao na kuondoa tofauti zao.Akizungumzia zoezi la Uhakiki linaloendelea Patrick Maganga alisema kuwa zoezi limekuja wakati muafaka ambao malalamiko ya wastaafu yamekuwa mengi na kwamba ametaka zoezi hilo liende sambamba na maboresho ya malipo kwa wastaafu hao.

Kwa Upande wake Emilia Maibori ambaye ni Mwalimu Mstaafu alisema kuwa mafao ya wastaafu yanapaswa kutolewa kwa wakati muafaka badala ya wastaafu kulalamika kufuatia kucheleweshwa kwa malipo hayo akieleza kuanza kupata malipo hayo mwaka 2015 kuafuatia kushindwa kupata malipo hayo tangu mwaka 2005 alipostaafu ambapo ameeleza kuridhishwa na zoezi la uhakiki linaloendelea.

Akieleza kufanyika kwa uhakiki huo Mkaguzi Mkuu Msaidizi wa ndani wa serikali,Stanslaus Mpembe alisema kuwa kwa zaidi ya mikoa 21 ambayo uhakiki huo umefanyika mafanikio yamekuwa makubwa na idadi kubwa ya wstaafu wamekuwa wakijitokeza.Mpembe alisema kuwa licha ya wastaafu wanaojitokeza pia serikali imetoa fursa kwa wastaafu ambao wamelazwa kwenye hospitali mbalimbali kufikiwa na watumishi wanaoendesha zoezi hilo na kwamba ndugu wa wastaafu hao wametakiwa kujitokeza kutoa taarifa za wastaafu hao ili waweze kufuatwa maeneo walikolazwa.

Wakati zoezi likiendelea mikoa mbalimbali nchini Mkaguzi huyo alisema kuwa baada ya zoezi kupita kwenye mkoa husika wastaafu ambao hawajahakikiwa wanatakiwa kujiorodhesha kwenye ofisi za hazina ndogo za mikoa waliyopo kabla ya muda wa zoezi hilo haujamalizika.

Naye ofisa habari wa Wizara ya Fedha na Mipango Ben Mwaipaja amewataka watumishi waastafu kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo la uhakiki kwenye mikoa yote watakayo pita.

"Mpaka sasa tumeshapita jumla ya Mikoa 21 bado mikoa ya lindi,Mtwara na Zanzibar ambapo napo zoezi litaendelea ninawaomba wastaafu wajitokeze ili wasije poteza haki zao"alisema Mwaipaja.

WATUMISHI wastaafu wa serikali wanaolipwa na serikali kupitia wizara ya fedha wakifanyiwa uhakiki mkoani Kigoma. WATUMISHI wastaafu wa serikali wanaolipwa na serikali kupitia wizara ya fedha wakifanyiwa uhakiki mkoani Kigoma

NCHI HAIJAKUMBWA NA BAA LA NJAA-MAJALIWA

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema nchi haijakumbwa na baa la njaa na amewataka Watanzania utosikiliza kampeni za upotoshwaji zinazofanywa na baadhi ya wafanyabiasha kuhusu hali ya chakula kwani si za kweli bali ni za uzushi zenye lengo la  kupandisha bei za vyakula.

Amesema Serikali ndio yenye jukumu la kutoa taarifa za kuwepo kwa njaa ama kutokuwepo na kwamba taarifa zinazosambazwa za kuwepo kwa baa la njaa nchini hazina ukweli wowote na Serikali inawahakikishia wananchi kuwepo kwa usalama wa chakula.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo
(Jumatatu, Januari 16, 2017) wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa mara baada ya kuzindua safari za ndege za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma, ambapo amesisitiza kwamba hali ya upatikanaji chakula nchini ni tofauti na inavyoelezwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo baada ya kutolewa kwa taarifa katika vyombo mbalimbali vya habari kuhusu kuwepo kwa baa la njaa nchini jambo ambalo si la kweli. Amewataka wananchi kuwa watulivu na jambo hilo likitokea Serikali itatoa taarifa.

“Mwaka jana nchi ilikuwa na akiba ya chakula cha zaidi ya tani milioni tatu hali iliyopelekea baadhi ya Wabunge na wafanyabiashara kuomba kibali cha kuuza nafaka nje ya nchi, ambapo Serikali ilitoa kibali hicho baada ya kujiridhisha kuwepo kwa akiba ya kutosha ya chakula,” amesema.

Amesema baada ya kutolewa kwa kibali hicho tani milioni 1.5 ziliuzwa nje ya nchi na
Kiasi cha tani milioni 1.5 zilizobaki zilihifadhiwa kama akiba ambapo tayari wameruhusu ziuzwe hapa nchini ili kupunguza kupanda kwa bei za vyakula nchini.

“Naomba wananchi msiwe na wasiwasi juu ya hali ya chakula nchini. Msisikilize kelele zinazopigwa na watu mbalimbali pamoja kwenye baadhi ya vyombo vya habari yakiwemo magazeti kwani taarifa hizo si za kweli. Chakula kipo cha kutosha licha ya mvua kusuasua katika baadhi ya maeneo nchini,” amesema.

Hata hivyo Waziri Mkuu amesema kuwa kwa sasa mvua zimeanza kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini, hivyo amewaomba wananchi kuzitumia kwa kulima mazao ya muda mfupi yanayostahimili ukame.

Waziri Mkuu amesema kwamba endapo kutatokea uhaba wa chakula nchini, Serikali itatoa utaratibu wa namna ya upatikanaji wa chakula kwa wananchi wake. Kuhusu kupanda wa bei ya vyakula katika baadhi ya masoko amesema inatokana na kuwepo kwa uhaba wa chakula katika nchi jirani.

Aidha, Waziri Mkuu amesema kwamba Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, itatoa taarifa kuhusiana na hali halisi ya chakula nchini kwa sasa na pia itatoa taarifa kuhusu hali ya mvua ili Watanzania waweze kupata ukweli wa hali ilivyo.


 IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.     
JUMATATU, JANUARI 16, 2017.

NEWZ ALERT:RAIS DKT MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA WABUNGE WAWILI NA BALOZI MMOJA.

0
0

MBUNGE WA TANGA AWAOKOA ASKARI WA JIJI LA TANGA NA KIPIGO KUTOKA KWA WASAFIRISHAJI

0
0

 Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Mhina Mustapha Selebosi mwenye miwani na tisheti akizungumza na wasafirishaji wanaofanya shughuli zao kati ya Mombasa nchini Kenya kuhusu kuwataka kuhamia eneo la stendi mpya ya kange kwa ajili ya kutoa huduma zao kulia mwenye kofia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaj Mussa Mbaruku.
 Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Mhina Mustapha Selebosi mwenye miwani na tisheti akizungumza na wasafirishaji wanaofanya shughuli zao kati ya Mombasa nchini Kenya kuhusu kuwataka kuhamia eneo la stendi mpya ya kange kwa ajili ya kutoa huduma zao katikati mwenye kofia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga,Alhaj Mussa Mbaruku
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj Mhina Mustapha Selebosiakisisitiza jambo kwa wasafirishaji hao kulia kwenye kofia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku
MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CUF) alhaj Mussa Mbaruku jana amelazimikakuingilia kati na kuwaokoa askari wa Jiji la Tanga waliotaka kupigwana wafanyabiashara wa magari yaendayo Mombasa nchini Kenya kwa madaiya kukamata magari yanayotakiwa kuhamia stendi ya kange na kuwatoza
faini bila ya kuwa na mashine za EFDs.

Askari wa Jiji la Tanga ambao walinusurika kipigo hicho na kumlazimuMbunge huyo kuwaingilia kati na kuwaondoa eneo hilo ni Timime Makasina Emanuel Lyimo ambao walikuwa tayari wamezingizwa na wafanyabiasharahao wakijiandaa kuwatembezea mkongoto.

Magari hayo yalikuwa yamepakiwa kwenye eneo la barabara 10 karibu naAssad Hotel ambapo kumekuwa kukipakiwa magari yanayoelekea Mombasanchini Kenya ambapo askari hao walidaiwa kukamata moja ya garilinaloelekea mjini Mombasa na kulitaka kulitoza faini.

Baada ya kuwepo na kadhia hiyo ilimlazimu Mbunge huyo ambaye yupomkoani Tanga mapumziko ya mwishoni mwa wiki kabla ya kwenda mkoaniDodoma kuendelea na vikao vya kamati aliamua kufika eneo la tukio nakuwachukua askari hao kwa gari lake na kuwapeleka mpaka kwenye ofisizao zilizopo Kata ya Nguvumali Jijini Tanga.

Akizungumza  na wasafirishaji hao,Mbunge huyo aliwataka kuwawatulivu kwani suala hilo linajadilika na huenda likapatiwa ufumbuzikutokana na vikao vya baraza la madiwani ambavyo vinatarajiwa kuketihivi karibuni mjini hapa.

  Aidha pia Mbunge huyo alishtusha na kitendo cha askari hao kuchukuaushuru bila ya kutumia mfumo wa kieletroniki jambo ambalo ni kunyumena utaratibu wa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli.

Hata hivyo askari, Timime Makasi ambaye ni askari wa Jiji ambayealisema wao wanafanya kazi chini ya Halmashauri ya Jiji hilo nawanatekeleza agizo hilo kama walivyoelekezwa ya kukamata gari zoteambazo zinatakiwa kupaki kwenye stendi kuu ya Kange.

Alisema kufuatia agizo hilo la halmashauri la kuzikamata gari hizo naatakae kwenda kinyume atatakiwa kutozwa faini ya shilingi 50,000 jambolililozua utata baada ya askari hao kuonekana kutokuwa na mashine zakielektroniki.

Aidha pia mmoja wa wamiliki wa magari yanayofanya safari zake za TangaMombasa Mohammed Nassor alisema kuwa swala liliwashitua zaidi nikutokuwepo na mashine hizo za risiti kama Serikali ilivyoelekeza jamboambalo lilitaka kuzua mzozo baina ya wafanyabiashara na askari hao.

Akizungumzia sakata hilo,Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj MustaphaSelebosi alisema halmashauri ina uhaba wa mashine za EFDs nahawaruhusu askari hao wa Jiji kuchukua ushuru bila kuwepo kwa mashinehizo.

Alisema wanachotakiwa kukifanya askari hao ni kulikamata gari nakulipeleka depo ya Halmashauri ambao ndio kunafanyika taratibu zakutozwa faini kwa mfumo wa mashine za EFDs.

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

MWILI WA MWANDISHI WA HABARI KAMPUNI YA UHURU PUPLICATIONS,AMINA ATHUMAN WAAGWA JIJINI DAR NA KUSAFIRISHWA KIJIJINI KWAKO LUSHOTO MKOANI TANGA

0
0

Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam wakiusalia mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari wa Kampuni ya Uhuru Publications, marehemu Amina Athumani nyumbani kwao Kipunguni A jijini Dar es Salaam jana, kabla ya kusafirishwa mkoani Tanga kwa mazishi yanayofanyika leo. (Picha na Francis Dande).
Baadhi ya waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari wa Kampuni ya Uhuru Publications kabala ya kusafiriswa mkoani Tanga kwa mazishi.
Meneja wa rasilimali Watu wa Kampuni ya Uhuru Publications akisoma salama za rambiorambi za kampuni hiyo.
Mkwe wa marehemu.
Baadhi ya waombolezaji.
Waombolezaji wakiwa msibani.
Mwili wa marehemu ukitolewa nyumbani kwao Kipunguni A.











NAIBU ANASTAZIA WAMBURA APOKEA BENDERA YA TAIFA TOKA KWA MISS TEEN HERITAGE 2016 NA KUZINDUA KITABU CHA "UTAMU WA CHUNGWA SI RANGIYE"

0
0
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Anastazia J. Wambura (katikati) akiongea na Waandishi wa habari huku akiwasisitiza Vijana kuiga mfano bora aliofanya Mrembo aliyeshika nafasi ya pili katika Tuzo za Urithi wa Asili wa Mabinti wenye Umri chini ya Miaka 20 wa mwaka 2016 Cecilia Godfrey (kulia) leo 16 Januari, 2017 Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa katika Wizara hiyo Bibi. Leah Kihimbi.
Mrembo wa aliyeshika nafasi ya pili katika Tuzo za Urithi wa Asili wa Mabinti wenye Umri chini ya Miaka 20 wa mwaka 2016 Cecilia Godfrey (kulia) akiwaeleza Waandishi wa Habari (hawapo pichani) baadhi ya changamoto alizopitia wakati wa mashindano hayo yaliyofanyika nchini Srilanka. Aliyekaa katikati ni Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Anastazia J. Wambura na Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa katika Wizara hiyo Bibi. Leah Kihimbi, 16 Januari, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Mrembo wa aliyeshika nafasi ya pili katika Tuzo za Urithi wa Asili wa Mabinti wenye Umri chini ya Miaka 20 wa mwaka 2016 Cecilia Godfrey (kulia) akiwaonyesha Waandishi wa Habari (hawapo pichani) baadhi ya zawadi mbalimbali alizopata wakati wa mashindano hayo yaliyofanyika nchini Srilanka. Aliyekaa katikati ni Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Anastazia J. Wambura na Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa katika Wizara hiyo Bibi. Leah Kihimbi, 16 Januari, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Anastazia J. Wambura (kushoto) akipokea Bendera ya Taifa toka kwa Mrembo aliyeshika nafasi ya pili katika Tuzo za Urithi wa Asili wa Mabinti wenye Umri chini ya Miaka 20 wa mwaka 2016 Cecilia Godfrey (kulia) 16 Januari, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Anastazia J. Wambura (kushoto) akimpongeza Mrembo aliyeshika nafasi ya pili katika Tuzo za Urithi wa Asili wa Mabinti wenye Umri chini ya Miaka 20 wa mwaka 2016 Cecilia Godfrey baada ya kupokea bendera ya Taifa toka kwake leo 16 Januari, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Anastazia J. Wambura (wa tatu kushoto)akiwa katika picha ya pamoja Mrimbwende aliyeshika nafasi ya pili katika Tuzo za Urithi wa Asili wa Mabinti wenye Umri chini ya Miaka 20 wa mwaka 2016 Cecilia Godfrey(katikati) baada ya kupokea bendera ya Taifa toka kwake leo 16 Januari, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Anastazia J. Wambura (kushoto) akiongea na Waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa jamii kusoma vitabu vinavyoandikwa na waandishi mbalimbali hususan rika la Vijana ili wapate kuelimika. Kulia ni Mwandishi Chipukizi wa Vitabu Bi. Rachel Maleza.
Mwandishi Chipukizi wa Vitabu Bi. Rachel Maleza (kulia) akiongea na Waandishi wa habari kuhusu dhamira yake ya kuandika kitabu kwa ajili ya lengo la kuelimisha jamii hasa Vijana. Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Anastazia J. Wambura.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Anastazia J. Wambura (wa pili kushoto) akizindua Kitabu cha “Utamu wa Chungwa Sio Rangiye” kilichotungwa na kuandikwa na Mwandishi Chipukizi wa Vitabu Bi. Rachel Maleza (wa pili kulia). Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa katika Wizara hiyo Bibi. Leah Kihimbi na Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Lugha Bibi. Shani Kitogo. 
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe. Anastazia J. Wambura (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mwandishi Chipukizi wa Vitabu Bi. Rachel Maleza (wa pili kulia) mara baada ya kuzindua kitabu cha "Utamu wa Chungwa si rangiye" leo 16 Januari, 2017.

(Picha zote na Benedict Liwenga-WHUSM)

WAZIRI NAPE ATEMBELEA TBC,AWATAKA WAFANYAKAZI KUFANYA KAZI KWA ARI ILI KUWA MFANO BARANI AFRIKA

0
0

Na Shamimu Nyaki-WHUSM

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye amewataka wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kufanya kazi kwa ari ili kuhakikisha linakuwa mfano Barani Afrika katika kuhabarisha umma.

Waziri Nape ameyasema hayo leo alipofanya ziara katika Shirika hilo ili kuona utendaji kazi pamoja na kuona changamoto mbalimbali zinazolikabili Shirika hilo.

“Fanyeni kazi kwa bidii na uadilifu kwa kutoa taarifa za ukweli na zenye uhakika kwa watazamaji puuzeni propaganda zinazoenezwa mtaani kuwa Shirika hili limepoteza Watazamaji na wasikilizaji kwa manufaa ya Taifa letu”.Alisema Waziri Nape.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Dkt.Ayoub Ryoba ameeleza kuwa Shirika linaendelea kuongeza wasikilizaji na watazamaji ambapo kuanzia mwaka 2012 hadi 2016 limeongeza mitambo kutoka kumi na mbili hadi hadi kumi na tisa iliyofungwa Mtwara,Rombo,Mbambabei na Tarime.

Aidha, Dkt Ryoba ameongeza kuwa Shirika hilo bado linaendelea kuwa katika historia ya Kuwa Shirika lililohabarisha umma juu ya Jitihada za Serikali ya Tanzania katika Ukombozi wa Bara la Afrika pamoja na kuendelea kukuza lugha ya Kiswahili kupitia kipindi cha malenga wapya.

“Shirika letu linaendelea kutoa habari, elimu na burudani zinazozingatia muktadha wa Utamaduni wa Nchi yetu ambapo kwa kipindi cha mwaka jana tumekuwa tukirusha matukio mubashara kupitia mitandao ambayo yana wafuatiliaji zaidi ya million tano.” Alisema Dkt.Ryoba.

Shirika hilo linaendelea kuwafikia watazamaji na wasikilizaji wengi zaidi ndani na nje ya nchi kwa kuendelea kuweka mikakati ya kuongeza vituo vingi zaidi.
 Makamu Mwenyekiti Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Bw. William Kalaghe Akimueleza jambo Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye alipofanya ziara na kuongea na watumishi wa Shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Taifa (TBC) Dkt. Ayoub Rhioba akimueleza jambo Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye wakati alipokutana na uongozi wa Shirika hilo wakati wa ziara na kuongea na watumishi wa Shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye akiongea na uongozi wa Shirika la Utangazaji Taifa (TBC) alipofanya ziara ya  kuongea na watumishi wa Shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye akitembelea maeneo mbalimbali ya studio za Shirika la Utangazaji Taifa (TBC) wakati wa ziara katika shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye akisaini kitabu cha wageni wakati wa Ziara katika shirika wa Shirika la Utangazaji Taifa (TBC) leo Jijini Dar es Salaam.


 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Taifa (TBC) Dkt. Ayoub Rhioba akitoa taarifa ya utekelezaji wa shirika hilo kwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye ambapo alimueleza mipango ya shirika hilo katika kuhakikisha linakuwa mfano barani Afrika.
  Makamu Mwenyekiti Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Bw. William Kalaghe akimkaribisha Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye kuongea na wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Taifa (TBC) alipofanya ziara katika shirika hilo.
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye akiongea na wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Taifa (TBC).
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Taifa (TBC) wakimueleza Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye changamoto za kiutendaji zinazolikabili shirika hilo wakati wa ziara katika shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Taifa (TBC) wakimsikiliza Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye.
 
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa TBC na wafanyakazi wa Shirika hilo.
(PICHA NA IDARA YA HABARI/WHUSM)

SERIKALI YAWAONDOA HOFU WANANCHI JUU YA HALI YA UPATIKANAJI WA CHAKULA NCHINI.

0
0
 Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya upatikanaji wa chakula nchini leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Mathew Mtigumwe.
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi akitoa maelekezo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Charles Tizeba9hayupo pichani) na waandishi hao kuhusu hali ya upatikanaji wa chakula nchini leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano baina yao na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba (hayupo pichani) kuhusu hali ya upatikanaji wa chakula nchini, mkutano umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo leo jijini Dar es Salaam. Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO.

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
SERIKALI imesema kuwa hali ya upatikanaji wa chakula nchini ni ya kuridhisha na kuwataka wananchi kupuuza taarifa zinazodai kuwa hali ya chakula ni mbaya.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya upatikanaji na chakula nchini.

“Ndugu waandishi ukweli ni kwamba hali ya upatikanaji wa chakula nchini ni ya kuridhisha sana katika maeneo mengi, hivyo siyo kweli kwamba kuna tatizo la njaa kama baadhi ya watu wanavyojaribu kupotosha,” alisisitiza Dkt. Tizeba.

Aidha Dkt. Tizeba aliongeza kuwa pamoja na kuwepo kwa hali nzuri ya chakula, Serikali kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) imeendelea kuweka akiba ya chakula kwa kununua jumla ya tani 62,087.997 za mahindi ili kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na chakula cha kutosha,
Dkt. Tizeba amesema kuwa kwa mwaka wa fedha 2016/2017 Serikali  imejipanga kununua jumla ya tani 100,000 za chakula ambapo hadi  kufikia Januari 8 mwaka 2017 imenunua jumla ya tani 62,087.997 za mahindi sawa na asilimia 62 ya lengo ililojiwekea.

“Kati ya kiasi kilichonunuliwa, tani 38,162.280 zimenunuliwa kupitia vituo vya ununuzi na tani 23,925.717 kupitia vikundi vya wakulima hivyo hadi kufikia tarehe 12 Januari, 2017 Wakala wana akiba ya tani 88,152.443 za mahindi,” alisema Dkt. Tizeba.

Waziri Tizeba ameongeza kuwa hadi kufikia katikati ya mwezi Januari, 2017 hali ya chakula na upatikanaji wake hapa nchini bado ni ya kuridhisha na hasa upatikanaji wa vyakula kama mchele na maharage ikilinganishwa na zao la mahindi.

Aidha, Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, FAO, TFNC pamoja na wadau wengine wanaendelea kufanya tathmini ya kina ya hali ya chakula na lishe nchini ambayo inatarajiwa kukamilika Januari 28 mwaka 2017 na itazihusisha Halmashauri 55, tathmini hiyo itaiwezesha Serikali kupata taarifa za uhakika zaidi kuhusu hali ya chakula na lishe nchini.

Amefafanua kuwa kutokana na hali ya mwenendo wa unyeshaji wa mvua za vuli na msimu kutokuridhisha katika maeneo mengi ya nchi, Serikali imewashauri wakulima kutumia mbegu zitakazokomaa mapema na kupanda mazao yanayostahimili ukame pamoja na kutumia kwa uangalifu na kuhifadhi akiba ya chakula cha kutosha kwa matumizi katika kaya.
Aidha, Sekta binafsi zimehamasishwa kuendelea kushiriki katika kutoa masoko ya kununua na kuuza mazao katika maeneo yenye ziada na kuyauza katika maeneo yenye uhaba.
Ufafanuzi huo umetolewa kufuatia kuwepo kwa taarifa za upotoshwaji juu ya hali ya upatikanaji wa chakula hapa nchini ambapo Dkt. Tizeba amesema huo ni upotoshaji wenye lengo la kuwatia hofu wananchi.

KAMATI YA BUNGE YA BAJETI YATEMBELEA BANDARI

0
0
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Injinia Edwin Ngonyani (Mb) (wa kwanza kulia) akisisitiza jambo mbele ya Kamati ya Bunge ya Bajeti wakati Kamati hiyo ilipotembelea Bandari ya Dar es Salaam mapema leo. Katikati ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Hawa Ghasia(Mb). Kamati za Kudumu za Bunge zimeanza shughuli zake hii leo ambapo katika wiki hii takribani Kamati za Kisekta 12 zitakuwa zikifanya ziara za kukagua miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali nchini kabla ya kurejea Mjini Dodoma kwa ajili kuendelea na vikao vyake.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti Mhe. Hawa Ghasia (Mb) akizungumza wakati Kamati hiyo ilipotembelea Bandari ya Dar es Salaam.
Wajumbe wa Kamati ya Bajeti wakiendelea na Kikao.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti Mhe. Hawa Ghasia (Mb) akimueleza jambo Kaimu Meneja wa Bandari wa Dar es Salaam Bw. Nelson Mlali wakati wa ziara hiyo.
Kaimu Meneja wa Bandari wa Dar es Salaam Bw. Nelson Mlali akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakati wa ziara hiyo.

(Picha na Ofisi ya Bunge)

MAC AUTO ACCESSORIES YAJA NA KIFAA KIPYA CHA ULINZI WA MAGARI

0
0

TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE (JKCI) KWA KUSHIRIKIANA NA HOSPITALI YA APOLO, BANGALOLE YA NCHINI INDIA WAWAFANYIA WAGONJWA UPASUAJI WA MOYO

0
0
 Madaktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na Madaktari  wa Hospitali ya Apolo, Bangalole ya nchini India wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kumuwekea  milango miwili ya moyo ya chuma (Aortic na Mitral Valuves) ambayo itamsaidia kupitisha damu vizuri katika moyo. Kutoka kulia ni Dkt. Sathyaki Nambala, akifuatiwa na Dkt. Bashir Nyangasa  na kushoto ni Dkt. Lebighe Khan.
Madaktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na Madaktari  wa Hospitali ya Apolo, Bangalole ya nchini India wakiendelea na kazi ya kumfanyia  mgonjwa upasuaji wa kumuwekea  milango miwili ya moyo ya chuma (Aortic na Mitral Val uves) ambayo itamsaidia kupitisha damu vizuri katika moyo. Mgonjwa huyo milango yake miwili ya moyo haikuwa inafanya   kazi vizuri ya kupitisha damu.

Picha na Anna Nkinda - JKCI
Viewing all 46206 articles
Browse latest View live




Latest Images