Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live

BENKI KUU YA TANZANIA (BOT) YAWAJENGEA UWEZO WAJUMBE WA KAMATI YA HESABU ZA SERIKALI (PAC)

0
0
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Prof. Benno Ndulu (katikati) akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) (hawapo pichani) kuhusu majukumu mbalimbali ya Benki hiyo wakati wa Kikao cha siku mbili cha Kuwajengea Uwezo Wajumbe wa Kamati hiyo kuhusu majukumu ya benki hiyo kilichofanyika jijini Dar es Salaam 13-14 Januari, 2017.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Prof. Benno Ndulu (kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Mhe. Naghenjwa Livingstone Kaboyoka (Mb) wakiteta jambo wakati wa Kikao cha siku mbili cha Kuwajengea Uwezo Wajumbe wa Kamati hiyo kuhusu majukumu ya benki hiyo kilichofanyika jijini Dar es Salaam 13-14 Januari, 2017.
Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Mhe. Naghenjwa Livingstone Kaboyoka (Mb) (wa pili kulia) akiwaeleza jambo Wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) pamoja Watendaji wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) wakati wa Kikao cha siku mbili cha Kuwajengea Uwezo Wajumbe wa Kamati hiyo kuhusu majukumu ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kilichofanyika jijini Dar es Salaam 13-14 Januari, 2017.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Prof. Benno Ndulu (wa pili kushoto), Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Mhe. Naghenjwa Livingstone Kaboyoka (Mb) (wa pili kulia) pamoja na Viongozi mbalimbali wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) wakifurahia jambo wakati wa Kikao cha siku mbili cha Kuwajengea Uwezo Wajumbe wa Kamati hiyo kuhusu majukumu ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kilichofanyika jijini Dar es Salaam 13-14 Januari, 2017.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA BUNGE-DAR ES SALAAM)

MEJA.GEN MILANZI: ACHENI KUINGIZA MIFUGO KATIKA HIFADHI ZA TAIFA.

0
0
Na Daudi Manongi-MAELEZO.
   Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja.Gen Gaudence Milanzi amewaasa wafugaji kuacha kuingiza mifugo katika hifadhi za taifa ili kuzitunza hifadhi hizo.
Katibu Mkuu uyo aitoa wito huo wakati akizungumza baada ya kufanya matembezi ya kupinga ujangili unaofanywa dhidi ya Tembo  ya kilometa 5 kutoka Ubalozi wa China mpaka Hoteli ya Sea Cliff  ambapo wageni mashughuli kama Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe.Benjamini William Mkapa alishiriki.
“Hifadhi za taifa hapa nchini hazina budi kulindwa na kutunzwa ili vizazi vijavyo viweze kuzifaidi kwani maeneo hayo yametengwa kwa ajili ya wanyama pori pekee na siyo kwa mifugo na hivyo kila mwananchi analo jukumu la kuyalinda mazingira haya,”Aliongeza Mej.Gen Milanzi.
Awali akizungumza katibu mkuu huyo alisema kuwa Serikali ina mkakati mkubwa wa kuhakikisha inashirikiana na nchi zingine katika kutokomeza kabisa Ujangili wa pembe za ndovu nchini.
Aidha aliishukuru Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kwa kuwa mstari wa mbele katika kupambana na ujangili wa pembe za ndovu ikiwemo upigaji  marufuku biashara ya pembe za ndovu na viwanda vya kuchonga pembe hizo ifikapo mwezi machi Mwaka huu.
Mbali na hayo katibu Mkuu uyo amewaasa watanzania kuwafichua wale wote wanaojihusisha na biashara hiyo na kuonya kuwa kwa kushiriki katika biashara hii tutawafanya tembo wetu kuwa historia kwani hawatakuwepo tena.
Naye Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe.Benjamini William Mkapa amewataka watanzania kulinda na kutunza mbuga zetu kwani ni urithi wa kila mtanzania na kuzitaka nchi mbalimbali kusaidia katika kulinda urithi huu wa wanyama na kuvitaka vyombo vya habari kushiriki vyema katika kutangaza mbuga zetu na pia kutangaza jitihada zinazofanywa na serikali katika kutokomeza ujangili wa pembe za ndovu.

MAPAMBANO DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA YAZIDI KUSHIKA KASI

0
0
Askari Polisi wakiwa wananyofoa mimea ya bhangi ambayo ilikuwa imepandwa kwenye moja ya shamba lililopo katika kijiji cha Kismiri Juu kata ya Uwiro tarafa ya King’ori wilayani Arumeru. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha).
MKU3
Askari wa Jeshi la Polisi wakiteketeza magunia ya bhangi kwa kuchoma moto mara baada ya kuyakusanya kutoka kwenye moja ya nyumba ya mkulima wa zao hilo haramu eneo la kismiri Juu wilayani Arumeru. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha).
MKU4
Askari wa Jeshi la Polisi wakitoa magunia ya bhangi katika moja ya nyumba iliyopo katika kijiji cha Engalaon kata ya Mwandeti tarafa ya Muklati wilayani Arumeru mara baada ya wenyeji kukimbia na kuacha mlango. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
 
……………………………………………………………
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Pamoja na Jeshi la Polisi mkoani hapa kufanikiwa kuongeza takwimu za ukamataji wa madawa ya kulevya kwa makosa 75 zaidi kwa mwaka 2016 kulinganisha na mwaka 2015,imeonekana kwamba mwaka huu  2017 kwa kushirikiana  na vyombo vingine vya Usalama pamoja na Tume ya Kuratibu na Kudhibiti dawa za kulevya nchini, kasi hiyo ya kuthibiti kilimo cha madawa ya kulevya aina ya bhangi ambacho kinalimwa baadhi ya maeneo ya wilaya ya Arumeru imeanza mapema.
 
Akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake mara baada ya operesheni ya kutokomeza madawa hayo kufanyika kwa siku mbili, Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo alisema kwamba  Jeshi hilo pamoja na vyombo vingine limeamua kuanza kuharibu mimea iliyopo mashambani mapema hasa kipindi hiki cha masika ambapo uoteshaji ufanyika ili kazi ya kudhibiti madawa hayo huko mbeleni iwe rahisi.
 
Kamanda Mkumbo alisema katika operesheni hiyo jumla ya hekari 31 za mimea ya bhangi ziliharibiwa huku gunia 58 na kilogramu 210 ziliteketezwa kwa moto katika maeneo ya kijiji cha Kismiri Juu kata ya Uwiro tarafa ya King’ori na katika kijiji cha Engalaon kata ya Mwandeti tarafa ya Muklati wilayani Arumeru.
 
“Siku ya kwanza Jumanne tarehe 10.01.2017 Operesheni hiyo ilifanyika katika kijiji cha Kismiri Juu kata ya Uwiro tarafa ya King’ori na kupata jumla ya magunia 31 ya bhangi na kilogramu 210 za mbegu zilipatikana huku hekari 19 za mimea hiyo ziliharibiwa”.
 
“Siku ya tarehe 12.01.2017 Alhamisi operesheni hiyo iliendelea tena katika maeneo ya kijiji cha Engalaon kata ya Mwandeti tarafa ya Muklati na kufanikiwa kupatikana kwa magunia 27 na kuharibu hekari 12 za mimea ya bhangi hivyo kufanya jumla ya magunia 58 kupatikana, mbegu kilogramu 210 kupatikana na hekari 31 za mimea huo kuharibiwa”. Alifafanua Kamanda Mkumbo.
 
Kamanda Mkumbo alitoa onyo kali kwa viongozi wanaoishi au kufanyia kazi maeneo hayo, kuacha mara moja kuwaunga mkono wakulima wa bhangi.
 
Jeshi la Polisi mkoani hapa linawaonya viongozi wa maeneo ambayo zao hilo linalimwa kuacha mara moja kuwaunga mkono wakulima hao, naamini ulimaji mpaka uuzaji wa bhangi unafanywa kwa uwazi katika maeneo hayo bila wao kuchukua hatua”.
 
“Watambue kwamba wao ni walinzi wa amani katika maeneo yao na washirikiane na Jeshi la Polisi katika kutokomeza kabisa kilimo hicho cha bhangi ambayo inaleta madhara makubwa kwa jamii hasa kundi la vijana”. Alisisitiza Kamanda Mkumbo.
 
Naye mkuu wa kitengo wa kuthibiti dawa za kulevya nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi(SACP) Mihayo Msikhela alisema Jeshi la Polisi nchini limejipanga hasa kwenye kuzuia kuliko kutibu ndio maana wameamua kuharibu mapema mimea ya zao hilo haramu kabla ya kukomaa na kusambaa.
 
Alisema kwamba kiwango cha uteketezaji wa dawa za kulevya hapa nchini kwa mwaka 2016 kiliongezeka ikilinganishwa na mwaka juzi 2015.
 
Kwa upande wake Afisa sheria mkuu toka Tume ya Kuratibu na Kuthibiti dawa za kulevya Bi. Christina Gervas alisema kwamba kadri bajeti itakaporuhusu watazidi kushirikiana na vyombo vya Usalama kufanya operesheni mara kwa mara katika maeneo ambayo bhangi inalimwa na pia kuahidi kutoa elimu kwa wakulima na viongozi wa maeneo hayo ili waweze kuachana na zao hilo haramu na kujikita kwenye mazao halali ya chakula na biashara.

Kivutio cha Kitalii cha Zanzibar: Ernie Els Design yasaini mkataba na Zanzibar Amber Resort kujenga uwanja wa Gofu wa kimataifa Zanzibar.

0
0
 Mkurugenzi wa Zanzibar Amber Resort, Saleh Mohammed Said akitia saini mkataba wa makubaliano na mcheza Gofu duniani Ernie Els ambae ana kampuni ya Ernie Els Design huko Afrika Kusni leo 
 Mkurugenzi wa Zanzibar Amber Resort, Saleh Mohammed Said akiwa pamoja  na mcheza Gofu maarufu duniani Ernie Els ambae ana kampuni ya Ernie Els Design huko Afrika Kusni leo wakati wa utiaji saini makubaliano ya kujenga kiwanja kikubwa cha Gofu Zanzibar
 Mkurugenzi wa Zanzibar Amber Resort, Saleh Mohammed Said akisalimiana  na mcheza Gofu maarufu duniani Ernie Els ambae ana kampuni ya Ernie Els Design huko Afrika Kusni leo wakati wa utiaji saini makubaliano ya kujenga kiwanja kikubwa cha Gofu Zanzibar

‘Kivutio hicho cha utalii kitakua cha kwanza cha aina yake Afrika ya Mashariki’ 

Zanzibar, Tanzania, Afrika ya Mashariki Januari 13, 2017 

Ernie Els Design inafuraha kutangaza imekamilisha makubaliano na Zanzibar Amber Resort na sasa ipo katika hatua ya kwanza ya ujenzi wa kiwanja hicho chenye hadhi ya kimataifa ambacho ni cha kwanza cha aina yake Afrika ya Mashariki.

 Ujenzi unakusudiwa kuanza mwaka 2017. Kiwanja hiki kitakuwa Kaskazini-Mashariki mwa kisiwa cha Zanzibar. Ernie Els anasema, “Kama mbunifu wa viwanja vya gofu, ninajisikia mwenye bahati kubwa kufanya kazi na Zanzibar Amber Resort. Na kutunukiwa baadhi ya mandhari nzuri za Bahari ya Hindi kwa kweli ni fursa kubwa kwetu. 

Wateja wetu na mimi tuna mtazamo unaofanana na ninao uhakika kuwa kazi yetu hapa itaandaa viwango vipya, ikiacha urithi kwa Zanzibar na wachezaji wa gofu kwa ujumla”.

 Kiwanja hichi kitakua mojawapo ya vivutio vingi vitakavyo jengwa kwenye eneo lenye ukubwa wa ekari 638, na kupakana na kilomita 4 za fukwe ya Bahari ya Hindi. Zanzibar Amber Resort itakua na mahoteli matano za kimataifa na nyumba za aina mbali mbali za kifahari. 

Haki miliki za nyumba zitatolewa kwa kipindi cha miaka tisini na tisa (99), na fursa ya nyongeza ya miaka arobaini na tisa (49) kwa wazawa na wageni. 

Zanzibar Amber Resort iko karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa ya Zanzibar ambalo linahudumiwa na mashirika ya ndege za Qatar, Uturuki, Condor, Kenya na Ethiopia.

 Brian Thomson & Saleh Said, Wakurugenzi wa Zanzibar Amber Resort waliongezea, “Tulivyoanza mijadala na Ernie, tulibaini kuwa tuna mtazamo unaofanana, wakujenga kujenga kiwanja cha kimataifa cha kipekee ambayo itachochea zaidi uzoefu wa mchezo huu kwa wachezaji wote.

 Uwepo wa kiwanja cha gofu kilicho tengenezwa na Ernie Els Design na hoteli za kimataifa kama vile Anantara na nyinginezo, itachochea utalii wa kifahari wa kipekee kisiwani hapo.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JANUARI 15, 2017

0
0

MWANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO GAZETI LA UHURU AMINA ATHUMAN AFARIKI DUNIA

0
0
 Mwandishi wa habari za Michezo wa Gazeti la Uhuru, Amina Athuman (pichani enzi za uhai wake) amefariki Dunia leo asubuhi katika Hosptali ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar alikokuwa amelazwa.
Pichani Kushoto ni aliyekuwa mwandishi wa habari za Michezo wa gazeti la Uhuru Publications, Amina Athuman ambaye amefariki asubuhi ya leo Visiwani Zanzibar,akiwa na Mwandishi Mwenzake Zainabu Nyamka kutoka Michuzi Media Group,wakiwa wote uwanjani kuripoti habari za mashindano ya kombe la Mapinduzi hivi karibuni.


Amina alilazwa Hospitalini hapo baada ya kuzidiwa (kushikwa na uchungu) kutokana na ujauzito na kukimbizwa kupata huduma katika hospitali hiyo ambapo alijifungua mtoto wa Kiume (Bahati mbaya) na yeye akaendelea kupatiwa matibabu hadi umauti ulipomkuta asubuhi ya leo.

Amina alikua mjini Zanzibar kikazi alipokwenda kuripoti mashindano ya Kombe la Mapinduzi, ambapo alikuwa arejee jijini Dar es Salaam jana.

Mungu ilaze roho ya Marehemu,
 mahala pema peponi, Amina

MASHINDANO YA NAGE MAPINDUZI CUP YAFIKIA TAMATI, NAIBU WAZIRI NGONYANI, MASAUNI WAMWAGA ZAWADI KWA WASHINDI

0
0
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani akiwasalimia wachezaji wa Karakana City wakati akikagua timu za mchezo wa Nage zilizoingia Fainali ya Mashindano ya Nage Mapinduzi CUP 2016-2017. Aliyevaa kofia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, ambaye ndiyo mwandaaji wa Mashindano hayo. Ngonyani aliyafunga Mashindano hayo yaliyofanyika katika Uwanja wa Amani, mjini Unguja, Zanzibar.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani akizungumza na mamia ya wananchi waliouhudhuria katika Fainali ya Mashindano ya Nage Mapinduzi CUP katika Uwanja wa Amani, mjini Unguja, Zanzibar. Katikati ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, ambaye ndiyo mwandaaji wa Mashindano hayo. Ngonyani aliyafunga Mashindano hayo yaliyofanyika katika Uwanja wa Amani, mjini Unguja, Zanzibar. Kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangala. Katika mashindano hayo, timu ya Six Centre iliibuka mshindi dhidi ya timu ya Karakana City zote za mjini Unguja. Picha na Felix Mwagara.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani (wapili kulia) kuja kufunga Fainali ya Mashindano ya Nage Mapinduzi CUP 2016-2017 katika Uwanja wa Amani, mjini Unguja, Zanzibar. Katika hotuba yake Masauni ambaye ndiyo aliyeandaa msahindano hayo alisema, mchezo huo utazidi kuthaminiwa ili kuwaweka vijana pamoja. Picha na Felix Mwagara.
Mchezaji wa timu ya Six Centre ya Mwera ambayo imepata ushindi, akikwepa mpira katika mchezo wa Fainali ya Mashindano ya Nage Mapinduzi CUP 2016-2017, kati ya timu hiyo na Karakana City ya Chumbuni, katika viwanja vya Amani, mjini Unguja, Zanzibar. Picha na Felix Mwagara.
Msanii wa kizazi kipya, Kheri Sameer Rajab (Mr. Blue), akitoa burudani huku akishangiliwa na Waheshimiwa Wabunge pamoja na Wawakilishi wakati wa Fainali za Mashindano ya Nage Mapinduzi CUP 2016-2017 yaliyofanyika katika Uwanja wa Amani, mjini Unguja, Zanzibar. , Watatu kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akifuatiwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangala. Picha na Felix Mwagara.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akiwa katika picha ya pozi na Msanii wa nyimbo za Singeli, Manfongo kabla ya msanii huyo kupanda jukwaa kutoa burudani katika
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, (watatu kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na wasanii maarufu wa kizazi kipya kutoka Tanzania Bara na Visiwani kabla ya Wasanii hao kupanda jukwaani kutoa burudani katika Fainali ya Mashindano ya Nage Mapinduzi CUP 2016-2017 yaliyofanyika katika Uwanja wa Amani, mjini Unguja, Zanzibar. Mashindano hayo yaliandaliwa na Mhandisi Masauni ili kukuza vipaji vya vijana. Picha zote na Felix Mwagara.

ZIARA YA KAMISHNA MSAIDIZI NISHATI, KWENYE MRADI WA UMEME JUA UKEREWE

0
0
Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Styden Rwebangila (wa kwanza kulia) pamoja na wataalam kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini wakiwa katika kivuko cha kuelekea katika Wilaya ya Ukerewe, Mwanza kwa ajili ya kukagua miradi ya umeme jua inayotekelezwa na kampuni ya Rex Energy.
Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Styden Rwebangila (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji kutoka kampuni ya Rex Energy, Francis Kibhisa (kulia) katika ziara hiyo.
Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Styden Rwebangila (kulia) akibadilishana mawazo na Afisa Sheria kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe, Peter Malendecha (kushoto) mara baada ya kuwasili katika wilaya hiyo.
Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Styden Rwebangila (kulia nyuma) pamoja na wajumbe wengine wakielekea katika kisiwa kidogo cha Ghana/Siza kwa ajili ya kukagua miradi ya umeme jua inayotekelezwa na kampuni ya Rex Energy.
Mkurugenzi Mtendaji kutoka kampuni ya Rex Energy, Francis Kibhisa (kulia) akielezea hatua ya utekelezaji ya miradi ya kusambaza umeme katika kisiwa cha Ghana/Siza wilayani Ukerewe kwa Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Styden Rwebangila (kushoto)
Sehemu ya miundombinu ya umeme iliyokamilika katika kisiwa cha Ghana/Siza
Katibu wa Kitongoji cha Ghana/Siza wilayani Ukerewe, Frank Matondane akielezea mahitaji ya umeme katika kitongoji hicho mbele ya Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Styden Rwebangila pamoja na wataalam kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini (hawapo pichani)
Mkurugenzi Mtendaji kutoka kampuni ya Rex Energy, Francis Kibhisa (kushoto) akionesha eneo litakalowekwa mitambo ya umeme katika kitongoji cha Ghana/Siza wilayani Ukerewe kwa Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Styden Rwebangila (kulia).

NAIBU WAZIRI KIGWANGALA AWAKABIDHI WAZEE 200 KADI ZA BIMA ZA AFYA JIMBO LA MASAUNI, UNGUJA ZANZIBAR

0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangala, akimkabidhi Bi. Salma Salum kadi ya bima ya Afya katika viwanja vya Mnarani, Mwembe Kisonge, Mjini Unguja, Zanzibar. Kadi zaidi ya 200 walikabidhiwa wazee wa Jimbo la Kikwajuni ambapo anatoka Mbunge wa Jimbo hilo ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto). Picha zote na Felix Mwagara
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimkaribisha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangala, katika Sherehe za Kukabidhi Bima ya Afya kwa Wazee wa Jimbo la Kikwajuni, iliyofanyika katika Viwanja vya Mnarani, Mwembe Kisonge, Mjini Unguja, Zanzibar. Picha na Felix Mwagara.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangala akizungumza na wananchi wa Jimbo la Kikwajuni (hawapo pichani), kabla ya kukabidhi kadi za Bima ya Afya kwa wazee zaidi ya 200 wa jimbo hilo ambalo anatoka Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto). Kulia ni Mwakilishi wa Jimbo hilo, Nassor Salim Jazeera. Tukio hilo lilifanyika katika Viwanja vya Mnarani, Mwembe Kisonge, Mjini Unguja, Zanzibar. Picha na Felix Mwagara.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akuzungumza na wananchi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangala (wapili kulia), kukabidhi kadi za Bima ya Afya kwa Wazee zaidi ya 200 wa Jimbo la Kikwajuni. Kulia ni Mwakilishi wa Jimbo hilo, Nassor Salum Jazeera. Tukio hilo lilifanyika katika Viwanja vya Mnarani, Mwembe Kisonge, Mjini Unguja, Zanzibar. Picha na Felix Mwagara.
Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapindiuzi, Zanzibar, Bi Harusi Said akizungumza na wananchi katika Sherehe za kukabidhi Bima ya Afya kwa Wazee zaidi ya 200 wa Jimbo la Kikwajuni ambapo anatoka Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) ambaye ni Mbunge wa Jimbo hilo. Tukio hilo lilifanyika katika viwanja vya Mnarani, Mwembe Kisonge, Mjini Unguja, Zanzibar. Picha na Felix Mwagara.

MAMA SAMIA ATOA DARASA KUBWA LA SIASA KWA WANA CCM KASKAZINI B UNGUJA

0
0

Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kaskazini na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa mkoa wa Kaskazini B, Unguja wakati wa Kufungua Mafunzo maalum ya Viongozi na watendaji wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake wa ngazi ya Matawi, Wadi na Majimbo

Wana CCM wa Kaskazini B wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye mafunzo ya Uongozi yaliofunguliwa na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kaskazini na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kaskazini na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifundisha kwa vitendo masuala ya Uongozi kwa wakazi wa mkoa wa Kaskazini B, Unguja wakati wa Kufungua Mafunzo maalum ya Viongozi na watendaji wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake wa ngazi ya Matawi, Wadi na Majimbo.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kaskazini ,Unguja, Ndugu Juma Haji akihutubia kabla ya kumkaribisha Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kaskazini na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kufungua mafunzo maalum ya Uongozi yaliofanyika Mkokotoni Kaskazini B,Unguja kwenye Chuo cha Amali.





Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimjulia hali Waziri wa Mambo ya Ndani wa zamani Mzee Ali Ameir nyumbani kwake Donge Kichavyani, Zanzibar

Msiba wa Marehemu Amina Athumani Mwandishi wa Habari za Michezo Gazeti la Uhuru na Mzalendo Kisiwani Zanzibar.

0
0
Katibu wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi na Makamo Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar Ndg Khamis Said akimfariji Mume wa Marehemu Amina Athumani Ndg Toufik Majaliwa alipofika nyumbani kwa jamaa wa marehemu katika mtaa wa kariakoo unguja leo. kutowa mkono wa pole akiwa na waandishi wa habari za michezo Zanzibar ZASWA.

Kwa taarifa za msemaji wa familia Ndg Nurdin Ramadhani amesema mwili wa marehemu tasafirishwa kesho asubuhi na Boti ya Kampuni ya Azam Marine saa moja asubuhi kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika Kijiji kwao Lushoto siku ya Jumanne mchana. 

Mwili wa marehemu utawasili jijini Dar es Salaam saa tatu asubuhi ukitokea Zanzibar baada ya kuwasili katika bandari ya Dar es Salaam utasafirishwa kuelekea kijiji kwao Wilaya ya Lushoto Mkoano Tanga kwa ajili ya mazishi.
 Katibu wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi Ndg Khamis Said akimfariji kaka wa marehemu Ndg Nurdin Ramadhani alipofika katika msiba kutowa pole leo asubuhi.
Katibu wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi Zanzibar Ndg Khamis Said akimfariji Mume wa Marehemu Amina Athuman Ndg Toufik Majaliwa alipofika nyumbani kwa ndugu wa marehemu katika mtaa wa kariakoo zanzibar leo asubuhi kutowa mkono wa pole kwa wafiwa.


Katibu wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi Zanzibar Ndg Khamis Said akizungumza na waandishi wa habari za michezo Zanzibar Zaswa alipofika nyumbani kwa ndugu wa marehemu katika mtaa wa kariakoo zanzibar.
Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa  Habari za Michezo Zanzibar Ndg Mwinyimvua Mnzuki akizungumza na waandishi wa habari kwa kupokea kwa masikitiko kifo cha mwandishi mwezao mrehemu amani athuman kilichotokea leo asubuhi katika hopspitali ya mnazi mmoja.
Ndugu wa marehemu wakiwa msibari wakisubiri taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu kuelekea Wilayani Lushoto Mkoani Tanga.

Wanafamilia wa marehemu Amina Athumani wakiwa katika msiba huo katika mtaa wa kariakoo Zanzibar.
Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot 
Zanzinews.com.
0777424152 Or 0715424152., 

MO Dewji akanusha kuzungumza kuhusu pesa za tetemeko la ardhi Kagera

0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji amekanusha taarifa ambazo zimesambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa amefanya mahojiano na kituo cha Redio cha Times FM kuhusu pesa zilizochangishwa katika Tetemeko la Ardhi la Kagera lililotokea mwezi Septemba, 2016.

Dewji amesema hajafanya mahojiano na kituo chochote cha habari kuhusu tetemeko la Kagera na habari hiyo haina ukweli wowote zaidi ni mbinu ambayo imetumiwa na baadhi ya watu kwa ajili ya kuchafua jina lake na kampuni yake ya MeTL Group ambayo mpaka sasa ina wafanyakazi zaidi ya watu 28,000.

Aidha Dewji amesema ana imani na Serikali ya awamu ya tano na kuwatoa hofu Watanzania kuwa ataendelea kushirikiana na Serikali kusaidia jamii yenye uhitaji ikiwa ni sehemu ya ahadi yake ya kutumia nusu ya utajiri wake kusaidia watu wenye uhitaji.

“Nitumie nafasi hii kuwajulisha Watanzania wenzangu kuwa hii habari ambayo inasambazwa na watu katika mitandao ni ya uongo na haina ukweli wowote, sijafanya mazungumzo na media yoyote na mimi nilichangia pesa kwa nia nzuri, nina imani na Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli kuwa inafanya kazi kwa faida ya watu wote bila kufanya ubaguzi,” amesema Dewji.

Katika ujumbe ambao unaonekana kusambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwepo Facebook, Instagram na WhatsApp imeandikwa kuwa MO Dewji amefanya mahojiano na Redio Times FM na kusema kama angejua mapema kuwa wahanga hawatopatiwa pesa hizo asingechangia

Wakulima viazi Njombe waishukuru SAGCOT kuwawezesha

0
0
Mtaalam na Mratibu wa Mradi wa kuzalisha na kusambaza mbegu bora za viazi mviringo kwa wakulima – Njombe toka SAGCOT, Bw.Owekisha Kwigizile akitoa mafunzo kwa wanakikundi cha Matunda group katika kata ya Mhaji, halmashauri ya Wilaya ya wanging’ombe Mkoani Njombe hivi karibu alipowatembelea na kuwaelimisha juu y Mradi wa kuzalisha na kusambaza mbegu bora za viazi mviringo unaoratibiwa na Mpango wa kuendeleza kilimo ukanda wa kusini mwa Tanzania (SAGCOT). Chini ya unafadhiliwa na Serikali ya watu wa Marekani(USAID) kupitia Shirika la Kimataifa la kusimamia mapinduzi ya kijani barani Afrika(AGRA).
Mkulima Bi Sara Martin akimwonesha kitu Mtaalam na Mratibu wa Mradi wa kuzalisha na kusambaza mbegu bora za viazi mviringo kwa wakulima – Njombe toka SAGCOT, Bw.Owekisha Kwigizile alimpomtembelea shambani kwake katika kijiji cha Maduma kata ya Kichiwa ,Halmashauri ya wilaya ya Njombe na kuona maendeleo ya kilimo cha zao hilo. Mradi huo unafadhiliwa na Serikali ya watu wa Marekani(USAID) kupitia Shirika la Kimataifa la kusimamia mapinduzi ya kijani barani Afrika(AGRA)na kuratibiwa na Mpango wa kuendeleza kilimo ukanda wa kusini mwa Tanzania(SAGCOT).
Mkulima Bi. Agusta Madembwe wa kijiji cha Nyanga, kata ya Ikuna, Halmashauri ya wilaya ya Njombe akikagua shamba lake alilipanda mbegu mpya za viazi mviringo alizozipata kupitia Mradi wa kuzalisha na kusambaza mbegu bora za viazi mviringo kwa wakulima – Njombe unaoratibiwa na Mpango wa kuendeleza kilimo ukanda wa kusini mwa Tanzania (SAGCOT). Akiwa na matumaini makubwa ya uzalishaji kwani amelima kwa njia ya kisasa.

Na Mwandishi Wetu, Njombe

WAKULIMA wa viazi Mkoani Njombe wameushukuru Mpango wa kuendeleza Kilimo Ukanda wa kusini mwa Tanzania (SAGCOT) kwa kuwaletea mradi wa uzalishaji na usambazaji mbegu bora za viazi pamoja elimu juu ya zao hilo ambapo sasa uzalishaji wake umeongezeka.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wakulima wa viazi mkoani hapa wamewaambia waandishi habari jana kuwa kuwepo kwa mradi huu toka SAGCOT umetusaidia kutoka katika kilimo cha mazoea na kuingia kwenye kilimo biashara.

Mchungaji Michael Nyagawa toka kijiji cha Lunguya, kata ya Mtwango Halmashauri ya Wilaya ya Njombe ni mmoja wa wakulima waliofaidika na mradi wa uzalishaji na usambazaji wa mbegu bora za viazi toka SAGCOT alisema wakulima wa viazi walikuwa na mazingira magumu katika uzalishaji.

“Tulifika kipindi hekali moja ya viazi unavuna gunia 20 tu, lakini sasa tunapata gunia 60 mpaka 80 kwa hekali,” alisema MchungajiNyagawa na kufafanua kuwa kupitia mafunzo na mbegu mpya toka SAGCOT uzalishaji wa viazi umeongezeka na kuinua vipato kwa wakulima,” alisema.

Mchungaji huyo hakusita kusema kuwa kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu zao hilo vilichangia uzalishaji kuwa mdogo kama vile uandaaji wa shamba, namna ya kupanda mbegu, uhifadhi wa mbegu katika maghala na pia mbegu ilikuwa ya zamani sana.

“SAGCOT imetupatia mbegu za aina nne ambazo ni Tengeru,Sherekea,Asante na Meru ambazo zimetolewa bure kwa sisi wakulima” alisema Mchungaji Nyagawa na kuongezea kuwa hata pale tunapovuna mazao yote yanakuwa mali yetu.

Alisema SAGCOT imembadilisha na sasa amekuwa akizalisha mbegu na kusambaza kwa wakulima wengine ili kuisaidia SAGCOT katika usambazaji wa mbegu bora na elimu juu ya uzalishaji wa viazi.

“ Elimu waliyonipatia nami nitaitoa kwa wakulima wengine ili kukuza uzalishaji na kujikwamua kiuchumi,” alisema Mchungaji huyo na kuishukuru SAGCOT.

Naye, Bi.Sara Martin kutoka kijiji cha Maduma, Kata ya Kichiwa Halmashauri ya wilaya ya Njombe alieleza jinsi alivyoupokea mradi huo toka SAGCOT na jinsi ulivyomsadia katika kujikwamua kiuchumi.

“Ilikuwa vigumu kuachana na mbegu tuliyoizoea lakini baada ya mafunzo na kupanda mbegu mpya nikaona mafanikio makubwa katika mbegu hizi mpya,” alisema Bi.Nyagawa na kuongezea kuwa uzalishaji ulikuwa mara mbili ya tulivyokuwa tukizalisha kabla ya mradi huu.

Alisema baada ya kulima kwa majaribio msimu wa pili aliweza kulima heka kumi zilizompekelea kupata zaidi ya magunia 300 na kwa sasa amekuwa mzalishaji na muuzaji wa mbegu kwa wakulima wengine na pia amekuwa akitoa elimu kwa wakulima wengine wajiunge katika kutumia mbegu mpya.

“Nimeweza kumlipia ada ya chuo kikuu mtoto wangu na nimefanikiwa kununua Ng’ombe wa maziwa na maisha kwa ujumla yamebadilika,” alisema Bi.Sara.

“Hali yangu ya maisha ni nzuri kwani kipato changu kimeongezeka lakini kabla mradi huu maisha yalikuwa magumu na nisingeweza hata kulipia ada lakini kwa uwepo wa SAGCOT umenifanya niwe na mafanikio na furaha katika maisha.

Kwa upande wake, Mtaalam toka SAGCOT na Mratibu wa mradi wa uzalishaji na usambazaji mbegu bora za viazi kwa mkoa wa Njombe, Bw.Owekisha Kwigizile alisema mwitiko wa wakulima katika mradi huu umekuwa mkubwa na hata uhamasishaji wa wao kwa wao umekuwa mkubwa.

“Nafarijika kwa mafanikio yanayopatikana kwa wakulima walioupokea mradi huu kwani mafanikio yao ndio hamasa kwetu katika kuendeleza mafunzo zaidi kwa wakulima,” alisema Bw.Kwigizile

Alisema ili kufanya uzalishaji wa viazi kuongezeka wakulima walionufaika na mradi hawanabudi kuwahamasisha na wengine kwa kuwapa mafunzo na mbegu bora ambazo wao sasa wanazalisha ili kuongeza uzalishaji na kuachana na kutumia mbegu ya zamani ambayo haina tija.

Kwa mkoa wa Njombe SAGCOT imejikita katika kutoa mafunzo na kusambaza mbegu za zao la viazi ambalo hapo awali lilionekana kuwa na changamoto katika uzalishaji wake.

Mradi huo unafadhiliwa na Serikali ya watu wa Marekani (USAID) kupitia Shirika la kusimia mapinduzi ya kijani barani Afrika (AGRA) .



Mwisho.

KIASI CHA DOLA ZA MAREKANI BILIONI MOJA ZATENGWA KUIMARISHA ZAO LA MUHOGO NCHINI

0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji anayeshughulikia viwanda Dk. Adelhelm Meru (kushoto), akiwa na Mwenyekiti wa TAEPZ, Dior Feng wakati wa kutia saini makubaliano ya mradi wa zao la muhogo nchini utakaogharimu Dola za Marekani bilioni 1. Waliosimama kutoka kushoto ni balozi wa China nchini, Dk. Lu Youqing na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TPSF), Godfrey Simbeye. Mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji anayeshughulikia viwanda Dk. Adelhelm Meru (kushoto), akibadilishana nyaraka na Mwenyekiti wa TAEPZ, Dior Feng baada ya kusaini mradi wa zao la muhogo nchini utakaogharimu Dola za Marekani bilioni 1. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni balozi wa China nchini, Dk. Lu Youqing na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TPSF), Godfrey Simbeye. Mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji anayeshughulikia viwanda Dk. Adelhelm Meru, akizungumza katika hafla ya utiaji saini makubaliano ya mradi wa kusindika muhogo nchini utakaogharimu Dola za Marekani bilioni 1, wengine katika picha ni Mwenyekiti wa TAEPZ, Dior Feng na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TPSF), Godfrey Simbeye. Mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

KIASI cha Dola za Marekani bilioni moja kimetengwa kwa ajili ya kuimarisha zao la muhogo nchini kupitia mkataba wa kibiashara baina ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya Tanzania Agricultural Export Processing Zone Limited and Epoch Agriculture (TAEPZ) kutoka China.

Akizungumza wakati wa utiaji saini makubaliano hayo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji anayeshughulikia viwanda Dk. Adelhelm Meru, alisema huu ni wakati wa wakulima kunufaika na Kilimo cha muhogo baada ya kulima kimazoea.

Alisema, kwa muda mrefu Watanzania wamekua wakilima muhogo kwa ajili ya chakula tu huku wakisafirisha muhogo ghafi hali inayokosesha serikali mapato na kunufaisha mataifa ya nje kupitia zao hilo lenye manufaa mengi.

“Lengo la serikali kuwa na uchumi wa viwanda linaanza kutimia, huu ni uwekezaji mkubwa katika sekta ya kilimo cha biashara. Kutakuwa na shamba kubwa la mihogo, kutajengwa viwanda mbalimbali vya kuzalisha unga wa mihogo, makopa, chakula cha mifugo, sukari ya viwandani na mbolea.

“Hii fursa tusiiache, kama mlikua mkilima mihogo kwa kiwango kidogo ongezeni mashamba kwa sababu soko la uhakika lipo, pia tunashauri mnunue hisa katika kampuni hii ili ikiwezekana tuimiliki kwa kiwango kikubwa,” alisema Dk. Meru.

Vilevile alipongeza urafiki wa kibiashara baina ya Tanzania na China na kumshukuru balozi wa China nchini, Balozi Lu Youqing kutokana na juhudi za kuhakikisha Tanzania inakuwa na uchumi wa kati kwa kuleta wawekezaji wengi kila mwaka.

Aliongeza kuwa mradi huu utasaidia wakulima wa mihogo kuongeza ufanisi na kuhakikisha wanapata mbegu bora ili kufikia kiwango kinachotakiwa katika kipindi cha miaka mitano ya majaribio, pia kutakuwepo na mafunzo juu ya ulimaji bora wa zao hili pamoja na namna ya kusindika.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TPSF), Godfrey Simbeye amewataka wakulima kugeukia Kilimo cha muhogo kwa sababu wawekezaji hawa wanahitaji tani milioni tano kwa mwaka.

“Takwimu zinaonyesha Tanzania tunazalisha tani milioni tano za mihogo mibichi kwa mwaka, Kampuni ya TAEPZ inahitaji tani milioni 2.5 za muhogo mkavu (makopa), maana yake ikiwa mibichi kutoka shambani inakua na uzito mara mbili.

“Tumeamua kuwaita wawekezaji kwa sababu tuliwahi kupewa fursa ya kusafirisha tumbaku na nyama kwenda China, lakini tulishindwa kutimiza vigezo kutokana na kila mmoja kusafirisha kwa namna yake bila kuzingatia ubora , naamini katika hili tutafanikiwa kutimiza malengo tuliyojiwekea,” alisema Simbeye.

Balozi wa China nchini Dk. Lu Youqing, akizungumza katika mkutano huo alisema, “naamini mkataba huu utaleta tija kwa Watanzania, kwa sababu muhogo ni zao muhimu wa raia wa China na lina faida kubwa. Rais Dk. John Magufuli wakati wa kampeni za urais pia aliwahi kugusia ushurikiano katika mazao ya chakula.

“Hata Waziri wa Mambo ya Nje Jamhuri ya Watu wa China, WANG Yi alipokuja nchini mapema mwezi huu alitilia mkazo kuhusiana na kusafirisha mazao ya biashara China. Kwa hiyo ili kuboresha uhusiano wetu ulioasisiwa na Mwenyekiti Mao Tse Tung na Mwalimu Julius Nyerere, serikali yetu itawekeza zaidi ili kukuza uchumi wa Tanzania.”

Alibainisha kuwa kwa sasa Tanzania ndiyo nchi inayoongoza Afrika kuwa na uwekezaji mkubwa kutoka China ambapo kiasi cha Dola za Marekani Bil 6.62 kimewekezwa nchini katika miradi mbalimbali. Hivyo, hata katika usafirishaji mihogo China watahakikisha Tanzania inazipita Nigeria na Ghana ambazo ndizo zinazoongoza kwa kusafirisha zao hilo kwa sasa.

Akitoa sababu za kuichagua Tanzania katika mradi huo, mwenyekiti wa TAEPZ, Dior Feng alisema ni kutokana na ardhi yenye rutuba na wananchi wengi kujishughulisha na Kilimo cha mihogo lakini hawana soko la uhakika, hivyo wakipewa maelekezo wanaweza kufikia kiwango kinachohitajika.

“Tanzania kuna fursa nyingi za Kilimo, katika awamu ya kwanza ya mradi huu tutaanzisha kiwanda za kusindika mihongo katika mikoa mitatu ambayo ni Lindi, Pwani na Mtwara, ingawa baadaye tutaongeza mikoa mingine mradi utakapoonyesha mafanikio.

“Tuna imani na kasi ya awamu hii na ndiyo maana tumekubali kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha kwa sababu serikali itatusaidia kuhakikisha mradi unafanikiwa kwa kiwango kikubwa,” alisema Feng.

Kwa muda mrefu sasa Tanzania imekuwa na urafiki mzuri na China katika sekta mbalimbali ikiwemo miundombinu, nishati na uchumi, hivyo hii ni fursa ya kipekee kwa wakulima kunufaika na zao la muhogo.

MWILI WA MAREHEMU AMINA ATHUMAN KUWASILI JIJINI DAR ASUBUHI HII NA BAADAE KUSAFIRISHWA KIJIJINI KWAO LUSHOTO KWA MAZISHI

0
0
  Mwili wa mwandishi wa habari za michezo wa gazeti la uhuru na mzalendo Amina Athuman ukisafirishwa asubuhi hii na boti ya kilimanjaro kuelekea Dar es Salaam na kusafirishwa hadi kijijini kwao Lushoto kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika siku ya jumanne mchana. Marehemu alikuwa Zanzibar kikazi akiripoti habari za michezo kombe la Mapinduzi na kumkuta mauti hayo baada ya kujifungua mtoto wa kiume, kwa bahati mbaya mtoto akafariki baada ya kuzaliwa na yeye kupata kifafa cha uzazi na kufariki jana asubuhi. Mwenyenzi mungu ampe kauli thabiti na amsamehe madhambi yake-Ameen

MAGAZETI YA LEO JUMATATU JANUARI 16, 2017

0
0


Zoezi la kuchagua mshindi wa tuzo ya ALM 2016 lafungwa, MO Dewji aongoza kwa asilimia 60.8

0
0
Jarida la African Leadership limefunga zoezi la kupiga kura kuchagua mshindi wa tuzo ya African Leadership Magazine Person Of The Year 2016, tuzo ambazo Mtanzania Mohammed Dewji alikuwa mmoja kati ya watu nane ambao walikuwa wakiwania.
Baada ya kufungwa kwa zoezi hilo, Mohammed Dewji ambaye pia ni Mkurugenzi wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group) ameibuka mshindi baada ya kuongoza kwa asilimia 60.8.
MO Dewji ameongoza kwa kupata kura nyingi na akifuatiwa na Rais Mstaafu wa Ghana, John Mahama ambaye amepata apata asilimia 38.3.
Kwasasa bado Jarida la African Leadership bado hawajatoa taarifa ni lini watakabidhi tuzo kwa mshindi wa wa tuzo ya African Leadership Magazine Person Of The Year 2016.
KAWAIDA: Zoezi la kuchagua mshindi wa tuzo ya ALM 2016 lafungwa, MO Dewji aongoza kwa asilimia 60.8 Jarida la African Leadership limefunga zoezi la kupiga kura kuchagua mshindi wa tuzo ya African Leadership Magazine Person Of The Year 2016, tuzo ambazo Mtanzania Mohammed Dewji alikuwa mmoja kati ya watu nane ambao walikuwa wakiwania. 

 Baada ya kufungwa kwa zoezi hilo, Mohammed Dewji ambaye pia ni Mkurugenzi wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group) ameibuka mshindi baada ya kuongoza kwa asilimia 60.8. MO Dewji ameongoza kwa kupata kura nyingi na akifuatiwa na Rais Mstaafu wa Ghana, John Mahama ambaye amepata apata asilimia 38.3. Kwasasa bado Jarida la African Leadership bado hawajatoa taarifa ni lini watakabidhi tuzo kwa mshindi wa wa tuzo ya African Leadership Magazine Person Of The Year 2016.

DC HAI ,GELASIUS BYAKANWA AMUACHIA MKURUGENZI WA HALMASHAURI HIYO HATMA YA WATUMISHI WABADHILIFU

0
0
Mkuu wa wilaya ya Hai ,Gelasius Byakanwa akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai kuhusu ubadhilifu uliofanyika wakati wa zoezi la utengenezaji wa madawati.Kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Yahana Sintoo.
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai wakiwa katika kikao hicho.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akionesha sehemu ya nyaraka ambazo zinaonesha namna baadhi ya watumishi walivyoshiriki kufanya ubadhilifu wa fedha za madawati.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanawa (katikati) akiwa na katibu tawala wa wilaya hiyo,Upendo Wela (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Halamshauri ya wilaya hiyo Yohana Sintoo (kushoto).
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yohana Sintoo akizungungunza wakati wa kikao hicho . 
 
Na Dixon Busagaga,Hai.
 
 MKUU wa wilaya ya Hai, Gelasius Byakanwa ametoa jukumu kwa mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo,Yohana Sintoo la kuamua hatma ya watumishi wake watano wanaotajwa katika tuhuma za ubadhilifu wa fedha wakati wa zoezi la utengenezaji wa madawati.
 
 Akiwa ndio mamlaka ya nidhamu kwa watumishi wa halmashauri hiyo,Mkurugenzi Sintoo ndiye mwenye maamuzi ya kuwasimamisha kazi watumishi hao baada ya tume iliyoundwa na mkuu wa wilaya hiyo, Byakanwa kumaliza kazi yake ya uchunguzi dhidi ya watumishi hao na kubaini mapungufu kadhaa.

 Akihitimisha taarifa yake wakati wa kikao na watumishi wa halmashauri hiyo,Byakanwa aliagiza taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) kuchunguza na kuchukua hatua dhidi ya watumishi hao akiwemo aliyekuwa kaimu Mkurugenzi ,Mhandisi Kweka.

 “Mamlaka ya nidhamu ya watumishi wa  Halmashauri ni mkurugenzi pamoja na baraza la madiwani ,lakini mwajiri ni ofisi ya katibu tawala mkoa ,Ofisi hizi mbili ndizo zinazoweza kukaa na kuchukua hatua za kuzuia matukio au vitendo kama hivyo.”alisema Byakanwa.

 “Niishauri ofisi ya Katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro pamoja na ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai  ambayo ndio mamlaka ya nidhamu kwa watumishi hao kupima kuhusu hatua za kuchukua dhidi ya watumishi hawa”aliongeza Byakanwa.

 Mkuu huyo wa wilaya alisema tuhuma zinazowakabili watumishi hao ,majina yao tumeyahifadhi kwa sasa ni pamoja na kupitisha barua ya malipo bila kujiridhisha kama kuna mkataba wa kutengeneza madawati na kufanya malipo ya fremu za madawati badala ya madawati.

 Tuhuma nyingine inaihusu timu ya ukaguzi  iliyokiri kukamilika kwa kazi bila ya kuonesha kama walipokea madawati au walienda kukagua kazi ya mzabuni  licha ya mzabuni kuomba malipo ya fremu za madawati badala ya  Madawati kamili.

 Ofisi ya elimu msingi,ofisi ya mkurugenzi,ofisi ya Mhasibu wa Halamshauri na kitengo cha manunuzi pia zinatuhumiwa kushindwa kubaini nyaraka zilizowasilishwa na mzabuni endapo zilikuwa ni kwa ajili ya fremu za Madawati badala ya  Madawati kamili.

Katika kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo Byakanwa alisema kampuni iliyopewa zabuni ya kutengeneza madawati ni ya Ujenzi na haijawahi kufanya kazi ya kutengeneza madawati, kuwa na karakana wala  vifaa vya uselemala .

Byakanwa alisema kwa malipo yaliyofanyika Halmashauri ilipoteza zaidi ya sh Mil 12 huku akishangazwa na hatua ya mmoja wa watumishi wanaotuhumiwa kuomba malipo badala ya mzabuni.

Akionyesha namna watumishi hao walivyokiuka taratibu Byakanwa alisema taarifa ya uchunguzi inaonyesha Halmashauri iliunda timu ya ukaguzi ambayo katika cheti cha ukaguzi na mapokezi ya bidhaa kinaonyesha bidhaa au madawati yalipelekwa ,Julai 16, 2016 ,siku 12 tangu siku ya mkataba na mzabuni.

“Mmoja w wajumbe wa kamati hiyo ya ukaguzi alikuwa ni mjumbe wa kamati ya kuratibu zoezi la Madawati ,alikuwa na jukumu la kusambaza mbao kwa wazabuni na alikuwa anajua kuwa hajapeleka mbao za kutosha kwa mzabuni ,katika maelezo yake mbele ya tume anakiri kuwa mzabuni hajamaliza kazi kwa sababu Halmashauri haijampa mbao.”alisema Byakanwa.

Alisema mzabuni aliieleza tume kuwa anadaiwa madawati 246 na halmashauri na kuwa amekamilisha kutegeneza madawati 154 na ueleza kua alishindwa kukamilisha kutokana na kukosa mbao kutoka halmashauri.

“June 9,2016 malipo ya Sh Mil 19.2 yakalipwa kwa ajili ya fremu za madawati siyo Madawati.Vocha ya malipo ikasainiwa na DT na kuandaliwa na mtumishi mwingine (jina tunalo)  ikakamilisha mchezo.”alisema Byakanwa.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kufanya hivyo ilikuwa ni kinyume cha taratibu za malipo kwa kuwa wahusika walipaswa kujiridhisha na nyaraka walizokuwa wakitumia ,kwa nini mzabuni aliamua kudanganya Halmashauri.

Byakanwa aliishauri ofisi ya Katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro pamoja na ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai  ambayo ndio mamlaka ya nidhamu kwa watumishi hao kupima kuhusu hatua za kuchukua dhidi ya watumishi hao.

Kwa upande wake mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai,Yahana Sintoo alisema licha ya kwamba amefika wakati zoezi la uchunguzi lina kamilika bado atafanyia kazi taarifa hizo kwa umakini mkubwa ili kujiridhisha na utendajji kazi wa watumishi wa halmashauri hiyo.

Mwisho.

Mwenyekiti wa NEC Jaji Kaijage aridhishwa maandalizi Uchaguzi Mdogo Kata ya Ngh'ambi

0
0
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mpwapwa Bw. Mohamed Maje (aliyesimama) akitoa maelezo ya kumkaribisha Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (kulia kwake) baada ya kuwasili kwenye Kata ya Ngh’ambi kufuatilia mwenendo wa uchaguzi mdogo wa diwani wa kata hiyo unaotarajiwa kufanyika Januari 22 mwaka huu.
Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Ngh’ambi James Mkinga (wa pili kulia) akimueleza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (R) Semistocles Kaijage (wa pili kushoto aliyekaa) kuhusu mwenendo wa Uchaguzi Mdogo wa Kata hiyo unaotarajiwa kufanyika tarehe 22 Januari mwaka huu.Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa NEC Bw. Emmanuel Kawishe, Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mpwapwa Bw. Mohamed Maje (katikati) na kulia ni Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Kata hiyo Clemence Fugusa.
Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Ngh’ambi James Mkinga (aliyesimama) akitoa taarifa ya mwenendo wa Uchaguzi Mdogo wa kata hiyo.
Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe (kushoto) akifafanua jambo kwenye kikao cha kupokea taarifa ya mwenendo wa Uchaguzi Mdogo wa Kata ya Ngh’ambi unaotarajiwa kufanyika Januari 22 mwaka huu.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mpwapwa Bw. Mohamed Maje (kulia) akimueleza jambo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (katikati) na Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe baada ya kikao cha kupokea taarifa ya mwenendo wa Uchaguzi Mdogo wa Kata ya Ngh’ambi.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (kushoto) akikagua daftari la kudumu la wapiga kura kwenye kituo cha kupigia kura cha Kata ya Ngh’ambi kilichopo kwenye Zahanati ya Ngh’ambi. Kushoto kwake aliyevaa miwani ni Afisa Uchaguzi halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa Bi. Martina Batholomeu.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (aliyevaa kofia nyeusi) akipokea maelezo kuhusu mabango ya Uchaguzi kutoka kwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Ngh’ambi James Mkinga (wa tatu kushoto) wakati alipokuwa akikagua mabango hayo nje ya kituo cha kupigia kura cha Kata ya Ngh’ambi kilichopo kwenye Zahanati ya Ngh’ambi.Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (R) Semistocles Kaijage (kulia) akieleza jambo baada ya kukagua mabango ya Uchaguzi kwenye kituo cha kupigia kura cha kata ya Ngh’ambi.Katikati ni Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa NEC Bw. Emmanuel Kawishe na kushoto ni Afisa Uchaguzi halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa Bi. Martina Batholomeu.


Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (kushoto) akisalimiana na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mpwapwa Bw. Mohamed Maje baada ya kuwasili wilayani Mpwapwa kutembelea kata ya Ngh’ambi inayotarajia kufanya uchaguzi mdogo Januari 22 mwaka huu.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Polisi wilaya ya Mpwapwa OCD Hussein Mdoe baada ya kuwasili wilayani Mpwapwa kutembelea kata ya Ngh’ambi inayotarajia kufanya uchaguzi mdogo Januari 22 mwaka huu.Katikati ni Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mpwapwa Bw. Mohamed Maje.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji (R) Semistocles Kaijage (katikati) akiongoza kikao cha kupokea taarifa kuhusu mwenendo wa uchaguzi mdogo wa Kata ya Ngh’ambi unaotarajiwa kufanyika Januari 22 mwaka huu.Kulia kwake ni Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mpwapwa Bw. Mohamed Maje, Mkuu wa Polisi wilaya ya Mpwapwa OCD Hussein Mdoe na kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa NEC Bw. Emmanuel Kawishe, Mkuu wa Kanda ya Kati ya Uchaguzi Bi. Saada Kangeta na Afisa Utumishi wa Tume Athumani Masesa.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (katikati) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri wakati alipomtembelea ofisini kwake kabla ya kutembelea Kata ya Ngh’ambi.Kulia ni Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mpwapwa Bw. Mohamed Maje.
Picha na Hussein Makame, NEC.

…………..

Hussein Makame, NEC-Mpwapwa

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji (R) Semistocles Kaijage amesema kila kitu kiko sawa tayari kwa uchaguzi mdogo wa kumpata diwani wa kata ya Ngh’ambi iliyoko katika halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.

Mhe. Jaji (R) Kaijage ameyasema hayo kutokana na kuridhishwa na maandalizi ya uchaguzi mdogo wa kata ya Ngah’ambi baada ya kutembelea na kufuatilia mwenendo wa uchaguzi wa kata hiyo unaotarajiwa kufanyika tarehe 22 Januari mwaka huu.

Akitoa taarifa fupi ya mwenendo wa uchaguzi mdogo wa kata hiyo, Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mpwapwa Bw. Mohamed Maje alisema karibu vifaa vyote kwa ajili ya uchaguzi huo vimepokelewa na kampeni za uchaguzi huo zinaendelea kwa amani na utulivu.

Alisema baada ya uteuzi wa wagombea kufanyika Desemba 22 mwaka 2016 wagombea wanne kutoka vyama vya ADC, CCM, CHADEMA na CUF waliteuliwa ambao ni David Mazengo, Richard Kaleme, Leornard Majenda na Hassan Kiuka, mtawalia.

Kwa upande wa pingamizi kwa wagombea, Bw. Maje alisema walipokea pingamizi kutoka vyama vya CHADEMA na CCM ambapo mgombea wa CHADEMA alipinga uteuzi wa mgombea wa CCM kwa madai kuwa si mkazi wa halmashauri husika.

“Pingamizi hili lilitolewa uamuzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata kwa kutupilia mbali madai hayo baada ya uthibitisho kuwa mgombea wa CCM ni mkazi halali wa halmashauri husika.Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo pia alikubaliana na uamuzi wa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata.” alisema Bw. Maje na kuongeza kuwa:

“Mgombea wa chama cha CCM alipinga uteuzi wa mgombea wa chama cha CHADEMA kuwa fomu ya uteuzi namba 8 C sehemu C na D imesainiwa na mtu ambaye si Katibu wa chama husika wa mkoa au Wilaya”

“Pingamizi hili pia lilitolewa uamuzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata kwa kutupilia mbali madai hayo baada ya uthibitisho wa maandishi kuwa aliyesaini ndiye Katibu wa chama husika wilaya ya Mpwapwa.Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo alikubaliana na uamuzi huo”

Aliongeza kuwa kamati za maadili kwa ngazi ya jimbo na kata zinafanya kazi na kwamba hadi kufukia Januria 13 kamati hazikupokea malalamiko yoyote kutoka kwenye vyama vinavyoshiriki uchaguzi mdogo kata hiyo.

Alisema wanatarajia kutoa mafunzo kwa makarani waongozaji na wasimamizi wa vituo vya kupigia kura tarehe 18 na 19 Januari na wameshaandaa vituo 12 vya kupigia kura vyenye wapiga kura 4123.

Kwa upande wa Mkuu wa Jeshi la Polisi wilaya ya Mpwapwa OCD Hussein Mdoe alisema hadi sasa kampeni zinafanyika kwa kuzingatia taratibu za nchi na taratibu za uchaguzi na hakuna vurugu zozote zilizojitokeza.

Hata hivyo aliwakumbusha wananchi kuwa jukumu la ulinzi na usalama ni la kila mwananchi na anaamini wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi wa kata na kamati za maadili zitawakumbusha wananchi jukumu hilo.

Kwa upande wa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Ngh’ambi Bw. James Mkinga alisema maandalizi yote ya uchaguzi yamekamilika na wameshabandika daftari la kudumu la wapiga kura kwenye vituo vya kupigia kura.

Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe aliwakumbusha wasimamizi wasaidizi kuhakikisha Sheria, kanuni na taratibu zote za Uchaguzi zinazingatiwa.

Aliwataka wawakumbushe wananchi kufika kwenye vituo vya kupigia kura kwa wakati ili kuepuka kukosa haki ya kupiga kura kwa sababu ya kuchelewa kufika kituoni.

“Hakikisha mnavikumbusha vyama vyote kuondoa mabango ya kampeni yaliyopo kituoni siku ya kupiga kura na kama hawawezi kuyaondoa uwafahamishe kwamba utayaondoa kwa sababu sheria inakataza” alisema Bw. Kawishe na kuongeza kuwa:

“Wakumbusheni wasimamizi wa vituo kufuata Sheria, kanuni na taratibu na yeyote atakayekiuka Sheria Tume ya Taifa ya Uchaguzi haitasita kumchukulia hatua za Kisheria”

Aliwakumbusha kuhakikisha kuwa mawakala wa vyama wanafuata taratibu zote inapotokea chama kinataka kumbadilisha wakala kwenye kituo cha kupigia kura.

Naye Mkuu wa Kanda ya Kati ya Uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Saada Kangeta aliwakumbusha wasimamizi wasaidizi kuwa iwapo litajitokeza jambo linaloweza kuchelewesha matokeo kama kufanya uamuzi ya kura za mgogoro wawafahamishe wananchi ili kuepuka vurugu.

Mkoa wa Mbeya wafikiwa na kompyuta za Bayport

0
0
Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa, wa pili kutoka kushoto, akimkabidhi kompyuta nane Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Nyasenga Enock kwa ajili ya kuzigawa kwa Halmashauri nne za Mkoa huo wa Mbeya. Wa kwanza kushoto ni Meneja wa Kanda ya Kusini wa Bayport Financial Services, Emmanuel Nzuttu. Wa pili kutoka kulia ni Meneja wa Bayport Mbeya, Mohamed Kisoki akifuatiwa na wakala wake Kurwa Lighton. Picha na Mpiga Picha wetu Mbeya.

Mbeya wataka kompyuta za Bayport ziongeze ufanisi wa kazi

Na Mwandishi Wetu,Mbeya

SERIKALI ya Mkoa wa Mbeya, zimewataka watumishi wa umma katika mkoa wao,hususan kupitia ofisi zitakazonufaika na msaada wa kompyuta nane kutoka kwenye taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services, kuongeza ufanisi wa kazi kwa kupitia vitendea kazi hivyo vilivyotolewa.

Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa Mbeya, Nyasenga Enock, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mheshimiwa Amos Makalla, kwenye makabidhiano ya kompyuta zilizotolewa na Bayport kwa ajili ya ofisi ya Halmashauri ya Tunduma, Ileje, Mbeya na Rungwe, huku kila ofisi ikipokea kompyuta mbili.
Majadiliano yakiendelea katika makabidhiano hayo ya kompyuta kutoka Bayport Financial Services mwishoni mwa wiki, mkoani Mbeya.

Akizungumzia hilo, Enock alisema kwamba haitakuwa na maana kama msaada wa kompyuta za Bayport hautaongeza ufanisi kazini na kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kutumia vyema vitendea kazi hivyo vipya vinavyoweza kuleta tija kama kila mtumishi atafanya kazi kwa nguvu zote ili kuwatumikia wananchi.

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Nyasenga Enock akigawa kompyuta hizo kwa wahusika baada ya kukabidhiwa na Bayport Financial Services.
Ugawaji wa kompyuta ukiendelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mbeya.
“Huu ni msaada mkubwa kwa mkoa wetu, hususan wale ambao kwa namna moja ama nyingine watazipokea kompyuta hizi kama ilivyoelekezwa na Ofisi ya Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, ukizingatia kwamba mpango huu ulizinduliwa kwao tangu mwaka jana.


“Nawaomba wale ambao watapokea kompyuta hizi wakafanye kazi kwa nguvu zote tukiamini kuwa wenzetu wa Bayport watakapoamua kufanya utafiti wa vifaa vyao jinsi vilivyotumika, basi kuwe na tija ili waendelee kushirikiana na sisi kwa mambo mengine,” Alisema Enock.


Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa, alisema ni furaha yao kuzifikisha kompyuta hizo kwa mkoa Mbeya, ikiwa ni siku chache baada ya kuingia mwaka mpya wa 2017.


“Tunaamini kwa kiasi kikubwa kuwa wenzetu wa Mbeya watazitumia kompyuta tulizo wapa kama sehemu ya kupanua wigo wa kuwatumikia wananchi kwa ajili ya kukuza uchumi wao na Watanzania kwa ujumla kwa namna moja ama nyingine.


“Baada ya kuingia mwaka mpya wa 2017, Mkoa wa Mbea wamekuwa wa kwanza kupokea kompyuta zetu na tunaamini utaratibu huu utaendelea kwa mikoa nyingine kama tulivyojipanga kuhakikisha kwamba tunapunguza changamoto za ukosefu wa kompyuta kwa ofisi za serikali kwa sababu ni jambo la msingi na serikali haiwezi kufanya kila kitu,” alisema Mercy.


Taasisi hiyo inayojihusisha na mikopo kwa watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni binafsi zilizoidhinishwa, imeamua kusambaza kompyuta 80 kwa ofisi za serikalini mikoani, huku Wizara ya Utumishi Makao Makuu tukiacha kompyuta 125, huku kompyuta zote hizo zikiwa na thamani ya Sh Milioni 500.
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live




Latest Images