Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1100 | 1101 | (Page 1102) | 1103 | 1104 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Mhe. Naghenjwa Livingstone Kaboyoka (Mb) (Kulia) akiwaeleza Wajumbe wa Kamati yake kuhusu mada zinazojadiliwa katika Mafunzo ya kuwajengea Uwezo kwa wajumbe hao kuhusu majukumu ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) yaliyowakutanisha wajumbe wa Kamati hiyo leo 13 Januari, 2017 katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) jijini Dar es Salaam.
  Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dkt. Natu Mwamba (mwenye kilemba) akiwafafanulia Wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali kuhusu majukumu ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kabla ya kuanza uwasilishwaji mada wakati wa mafunzo yaliyowakutanisha Wajumbe wa Kamati hiyo leo 13 Januari, 2017 katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) jijini Dar es Salaam.
  Wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) wakifuatilia mada kuhusu majukumu mbalimbali ya Benki ya Tanzania (BOT) zikizowasilishwa na baadhi ya Wajumbe wa Kamati hiyo wakati walipohudhuria mafunzo ya kuwajengea uwezo toka BOT yaliyofanyika leo 13 Januari, 2017 katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya Wajumbe Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) wakiwasilisha mada kuhusu majukumu mbalimbali ya Benki ya Tanzania (BOT) mbele ya Mwenyekiti na naibu Gavana wa BOT leo 13 Januari, 2017 katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) jijini Dar es Salaam.(PICHA ZOTE NA OFISI YA BUNGE-DAR ES SALAAM)

  0 0

   Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akikagua sehemu ya kuhifadhia mizigo ya abiria kilivyoteketea kwa moto  usiku wa kuamkia leo katika Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere ,kulia ni Mkurugenzi wa Uwanja huo Bw. Paul Rwegasha.
   Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere Bw. Paul Rwegasha akimuonesha Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa chumba cha kuhifadhia mizigo ya abiria kilivyoteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo.
   Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere Bw. Paul Rwegasha akimuonesha Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa chumba cha kuhifadhia mizigo ya abiria kilivyoteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo.
   Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere Bw. Paul Rwegasha akimuonesha Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa chumba cha kuhifadhia mizigo ya abiria kilivyoteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo.
  Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) mara baada ya kukagua chumba cha kuhifadhia abiria kilichoteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo (jana),wa kwanza kulia ni Kaimu Katibu Mkuu Sekta ya Uchukuzi Bw. Gabriel Migire. (Picha na Benjamin Sawe-Maelezo).


  Serikali imesema imeunda Tume ya uchunguzi ya watu 12 ili kuweza kuchunguza na kubaini chanzo cha ajali ya moto iliyotokea jana saa Tano usiku katika chumba kidogo cha kuhifadhia mizigo kilichopo kwenye jengo la Pili la abiria (Terminal II) katika uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa  Tume hiyo iliyoundwa inaongozwa  na Joseph Nyahende ambae anatoka katika ofisi za  Makao Makuu ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini.“Ninategemea kupata ripoti ya kitaalamu kutoka kwa Tume hii, ili kutusaidia kubaini kiundani juu ya chanzo haswa kilichopelekea moto huu”, amesema Waziri Mbarawa.

  Aidha, Waziri Mbarawa amefafanua kuwa huduma katika jengo hilo  zinaendelea kama kawaida ambapo awali zilisitishwa na kuhamishiwa katika Jengo la Kwanza la abiria (Terminal I). 

  “Mara baada ya moto kutokea, kitu cha kwanza kilichofanyika ni kuudhibiti moto huu ili usiweze kusambaa katika maeneo ambayo hayajaathirika, kisha tukatafuta njia za kurudisha huduma kwa abairia”, amesisitiza Profesa Mbarawa.


  Katika hatua nyingine, Profesa Mbarawa ameipa miezi miwili  kampuni ya mizigo ya Swissport kurekebisha huduma zinazolalamikiwa na wateja wake na endapo itashindwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa JNIA, Paul Rwegasha ameeleza kuwa tathmini na gharama za mizigo iliyokuwa imehifadhiwa katika chumba hicho bado haijajukana, ambapo ripoti itaeleza gharama hizo pindi itakapokamilisha uchunguzi wake.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.


  0 0

  Katibu Mkuu wa Chama cha Tanzania-China Friendship Promotion Association Bw.Joseph kahama akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya matembezi ya kupinga ujangili wa Tembo (Walk for Elephant 2017) yatakayofanyika kesho asubuhi kuanzia saa 12 asubuhi kuanzia Ubalozi wa China mpaka Hoteli ya Sea Cliff.Kushoto kwake ni Hongxiang Huang kutoa China House.
  Katibu Mkuu wa Chama cha Tanzania-China Friendship Promotion Association Bw.Joseph kahama akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya matembezi ya kupinga ujangili wa Tembo (Walk for Elephant 2017) yatakayofanyika kesho asubuhi kuanzia saa 12 asubuhi kuanzia Ubalozi wa China mpaka Hoteli ya Sea Cliff.
  Katibu Mkuu wa Chama cha Tanzania-China Friendship Promotion Association Bw.Joseph kahama akionyesha tangazo lenye ujumbe wa kuhimiza matembezi ya ku kupinga ujangili wa Tembo (Walk for Elephant 2017) yatakayofanyika kesho asubuhi kuanzia saa 12 asubuhi kuanzia Ubalozi wa China mpaka Hoteli ya Sea Cliff. Kushoto kwake ni Hongxiang Huang kutoa China House.Picha na Daudi Manongi-MAELEZO.


  Na Frank Shija-MAELEZO.

  MKAPA kuongoza matembezi ya hiari ya kilomita tano yanayojulikana kama Walk for Elephant Dar es Salaam 2017yatayofanyika kesho kuanzaia saa 12 asubuhi yaikianzia Ubalozi wa China hadi Sea Cliff Hotel.

  Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Urafiki baina ya Tanzania na China (TCFPA) Joseph Kahama alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na matembezi hayo leo jijini Dar es Salaam.

  Kahama amesema kuwa yana lengo la kuonyesha umoja katika kupinga ujangili unaofanywa dhidi ya Tembo.

  “Tunatarajia kuwa na matembezi ya kwa ajili ya kupinga ujangili dhidi ya Tembo ambapo wageni wetu mashuhuri wanatarajiwa kuwa Marais wastaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi na Mzee Mkapa atakayepokea matembezi hayo katika Hotel ya Sea Cliff,” alisema Kahama.

  Aliongeza kuwa zaidi ya watu 550 wamethibitisha kushiriki katika matembezi hayo wakiwemo baadhi ya watu maarufu kama vile Jokate Mwigelo, Mrisho Mpoto na wasanii wengine.

  Aidha Katibu Mkuu huyo alisema kuwa Chama cha Urafiki baina ya Tanzania na China(TCFPA) imeanzishwa kwa nia ya kudumisha urafiki na uhusiano baina ya raia wa nchini hizo mbili.

  Akijibu swali la mwandishi wa habari aliyetaka kujua ni kwanin china imeamua kusaidia katika vita dhidi ya ujangili ili hali inatajwa kuwa miongoni mwa soko kubwa la bidhaa za meno ya Tembo, Kahama alisema kuwa Serikali ya China haiku tayari kuona nchi yake inatajwa kama soko la meno ya Tembo ndiyo maana Rais Xi Jinping wa China na Barrack Obama wa Marekani wamewahi kutoa tamko la pamoja la kupinga ujangili na ni kosa la jina kwa rai wa China kukamatwa na nyara hizo.

  Chama hicho kimekusudia kuifanya tarehe 14 mwezi wa kwanza kila mwaka kuwa siku ya matembezi ya Walk for Elphant Dar es Salaam 2017 ili kujenga utamaduni endelevu wa kupinga ujangili.

  0 0

   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(Mb) akimvisha nembo ya kijani Mmoja wa askari wahitimu wa Mafunzo Maalum ya Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Kozi Namba 11 kwa niaba ya wahitimu wenzake. Mafunzo hayo Maalum yamefungwa rasmi leo Januari 13, 2017 katika Viwanja vya Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani kilichopo Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(Mb) akitoa hotuba fupi kwa Wahitimu wa Mafunzo Maalum ya Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Kozi Namba 11 kabla ya kuyafunga rasmi leo Januari 13, 2017.
   Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini Dkt. Juma Malewa akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kufunga Mafunzo hayo.
   Askari Wahitimu wa Mafunzo Maalum ya Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Kozi Namba 11 wakiingia uwanjani kwa ajili ya kutoa maonesho mbalimbali ya Ukakamavu na ujasiri.
     Onesho Maalum la Ukakamavu na ujasiri kama inavyoonekana katika picha Askari wa Kikosi Maalum akihimiri kipigo cha nyundo katika mwili wake kwa ujasiri wa hali ya juu.
   Askari Wahitimu wa Mafunzo hayo Maalum wakionesha umahiri wao wa kuvuka vikwazo mbalimbali kwa kutumia kamba kama inavyoonekana katika picha.
  Wahitimu wa Mafunzo Maalum wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Mgeni rasmi kama inavyoonekana katika picha(Picha zote na Jeshi la Magereza).
   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(Mb)  akipokea Salaam ya heshima kutoka Gwaride Maalum la heshima lililoandaliwa na askari wahitimu wa Mafunzo Maalum ya Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Kozi Namba 11. Hafla ya hiyo imefanyika leo Januari 13, 2017 katika Viwanja vya Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani kilichopo Ukonga, Jijini Dar es Salaam(kushoto) ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo Dkt. Juma Malewa .
   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(Mb) akikagua Gwaride Maalum la heshima lililoandaliwa na Askari wahitimu wa Mafunzo Maalum ya Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Kozi Namba 11 kama inavyoonekana katika picha.
   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba(Mb) akimtunuku cheti cha sifa Mmoja wa askari wahitimu wa Mafunzo Maalum ya Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Kozi Namba 11 ambapo Mafunzo hayo yamefungwa rasmi leo Januari 13, 2017 katika Viwanja vya Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani kilichopo Ukonga, Jijini Dar es Salaam.


  0 0


  kamanda wa polisi mkoani Arusha Naibu Kamishna wa polisi Charles Mkumbo akiongea na waandishi wa habari leo juu ya uteketezaji wa magunia ya bangi ,pembeni ni mkuu wa kitengo cha kupambana na kuzuia madawa ya kulevya nchini kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi (SACP) Mihayo Msikhela

  Na Woinde Shizza,Arusha


  Jeshi la polisi mkoani hapa kwa kushirikiana na tume ya kuratibu na kuthibiti dawa za kulevya nchini limeteketeza magunia 58 ya bangi,mbegu za bangi kg 210 huku hekari 19 zilizooteshwa miche ya bangi zikiwa zimeharibiwa .

  Hayo yamebainishwa jana na kamanda wa polisi mkoani Arusha naibu kamishna wa polisi Charles mkumbo wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo alisema kuwa kuteketeza kwa madawa haya ya kulevywa kumefanyika kutokana na operationi ya siku mbili .

  Alisema kuwa operesheni ya kwanza ilofanyika january 10 siku ya jumanne kuanzia muda wa saa 11.00 alfajiri katika eneo la kijiji cha kisimiri juu ndani ya kata ya uwiro tarafa ya kingori na kufanikiwa kupata magunia 31 pamoja na mbegu kilogramu 210 ambazo zote ziliteketezwa na moto ,pamoja na hekari 19 zilizooteshwa miche ya bhangi ambazo ziliaribiwa zote.

  Aliongeza kuwa operationi hiyo iliendelea tena siku ya alhamisi january 12 kuanzia muda wa saa 11.00 alfajiri hadi saa saba mchana katika eneo la kijiji cha Engalaon kata Mwandeti tarafa ya Muklati ambapo walikamata jumla ya magunia 27 ya bangi na kuyateketeza na moto na kuharibu jumla ya hekari 12 zilizooteshwa mmea wa bhangi .

  Mkumbo alisema kuwa jeshi la polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama linaendelea na operationi hii hasa ya kuaribu mimea ya bangi mara kwa mara hasa katika cha mvua hali ambayo itasaidia kuthibiti kilimo hicho.

  Aidha pia jeshi la polisi linawaonya viongozi wa maeneo yanayohusika na kilimo cha bangi kuacha mara moja kuwaunga mkono wakazi wa maeneo hayo kwani matukio hayo yanafanywa kwa uwazi bila wao kuchukua hatua yeyote ,wanapaswa watambue kwamba wao ni walinzi wa maeneo yao ,na kuwasihi viongozi washirikiane kwa pamoja kutokomeza kilimo hicho cha bhangi ambayo inaleta madhara makubwa kwa jamii.

  kwa upande wake mkuu wa kitengo cha kupambana na kuzuia madawa ya kulevya nchini kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi (SACP) Mihayo Msikhela alisema kuwa mikoa ambayo inaongoza na kupatikana kwa zao la bangi ni Tarime ,Morogoro , Arusha pamoja na Kilimanjaro lakini kwa sasa viongozi waliopo katika sehemu hizo wanajitaidi sana kuthibiti ulimwaji wa mazao hayo ya bangi huku akichukuwa muda huo kumpongeza mkuu wa wilaya ya Arumeru kwa kupiga vita ulimwanyi wa bangi pamoja na mkuu wa wilaya ya Tarime jinsi wanavyojitaidi kuthibiti ulimwaji huo wa bangi mpaka kufikia sehemu ya kuwaweza viongozi wa vijiji hivyo ndani kutokana na kusimamia ulimwaji wa zao hilo ambalo limepigwa marufuku hapa nchini

  Aidha alisema kuwa kwakuwa tatizo hili limekuwa kama likijirudia wanampango wa kuboresha sheria za uthibiti ikiwa ni pamoja na kuweka sheria kali zitakazo wabana wale ambao wanatumia ,wanauza pamoja na wanao lima madawa haya ya kulevya hapa nchini .

  0 0  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA NISHATI NA MADINI   

  TAARIFA YA UFAFANUZI KUHUSU KIKAO CHA WAZIRI WA NISHATI NA MADINI MHE. PROF. SOSPETER MUHONGO (MB.) NA UJUMBE WA BENKI YA DUNIA KILICHOFANYIKA TAREHE 28.09.2016

  Wizara ya Nishati na Madini inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu kikao cha Waziri wa Nishati na Madini na Ujumbe wa Benki ya Dunia kilichofanyika tarehe 28.09.2016 kikihusishwa na kupandishwa kwa bei ya umeme kama ilivyoripotiwa na magazeti ya Mwananchi ya tarehe 12.01.2017 lenye kichwa cha habari “Prof. Muhongo alivyoshiriki kupandisha bei ya umeme” na la tarehe 13.01.2017 lenye kichwa cha habari “Prof. Muhongo awekwa mtu kati”.

  Wizara inapenda kuutaarifu Umma kuwa, imekuwa ikifanya vikao na wadau mbalimbali wakiwemo Taasisi za Umma, Binafsi na Washirika wa Maendeleo yakiwemo Mashirika ya Kifedha ya Kimataifa. Lengo la vikao hivyo ni pamoja na kuhamasisha uwekezaji katika Sekta za Nishati na Madini nchini.

  Aidha, tarehe 28/9/2016 Wizara ilifanya kikao na Ujumbe kutoka Benki ya Dunia ikiwa ni mwendelezo wa vikao vya majadiliano kuhusu upatikanaji wa mkopo wa Dola za Marekani Milioni 200 kwa ajili ya kuboresha uendeshaji wa Shirika la Ugavi wa Umeme (TANESCO). Kikao hicho pia kilihudhuriwa na taasisi nyingine zikiwemo Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Shirika la Maendeleo la Petroli Tanzania (TPDC), Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA).

  Katika kikao hicho masuala yaliyojadiliwa yalikuwa ni;

  1.  Upatikanaji wa umeme wa kutosha, uhakika na  bei nafuu kwa ajili ya kuchochea shughuli za maendeleo ya kukuza uchumi wa nchi ikiwemo viwanda, biashara, kilimo na huduma za jamii;
  2.  Kuongeza ufanisi wa utendaji wa Shirika la Umeme (TANESCO); na
  3.  Kupunguza deni la TANESCO.

  Katika kulipunguza deni la TANESCO ambalo linakaribia Shilingi Bilioni 800 (takriban Dola za Marekani Milioni 363) na kuboresha shughuli za utendaji za TANESCO, Benki ya Dunia ilijadiliana na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Nishati na Madini ili kupata mkopo wa Dola za Marekani Milioni 200. Hivyo, katika kikao hicho, hakukuwa na makubaliano ya kupandisha bei ya Umeme kama ilivyoripotiwa na gazeti hilo.

  Vile vile, tunaomba kuutaarifu Umma kwamba Wizara ya Nishati na Madini kwa niaba ya Serikali inafanya majadiliano na Benki ya Maendeleo ya Africa (AfDB), Umoja wa Ulaya (EU), JICA (Japan), na Mashirika mengine ya fedha kwa lengo la kutafuta fedha za kuboresha Sekta ya Nishati.

  Imetolewa na;
    
  WIZARA YA NISHATI NA MADINI
  13.01.2017

  0 0


   


  0 0


  Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza kikao cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kilichofanyika kwenye ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi.
  Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati)akiongoza kikao cha Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kilichofanyika kwenye ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi, kushoto ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa na kulia ni Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
  iWaziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akielezea masuala mbali mbali ambayo yamejadiliwa na Mawaziri wa Tanzania Bara pamoja Visiwani
  Baadhi wa Mawaziri kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia kwa makini kikao hicho ambacho changamoto mabli mbali zinazohusu Muungano.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Annastanzia Wambura, jana akizungumza kwa niaba ya waziri wa wizara hiyo, Mhe.Nape Nnauye, kwenye mchezo wa hisani kati ya timu za UMISETA wilaya za Nyamagana na Ilemela mkoani Mwanza, uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.


  Na Binagi Media Group

  Mhe.Wambura, alisema Serikali haijayafuta mashindano ya UMITASHUMITA na UMISETA na kwamba imejipanga vyema ili kuiendeleza michezo hiyo mwaka huu 2017 kwa kuondoa dosari zote zilizojitokeza hapo awali na kusababisha kuahirishwa mwaka jana.

  Lengo la mchezo huo ilikuwa ni kumuenzi aliyekuwa mchezaji wa timu ya soka ya vijana chini ya miaka 20 ya Mbao Fc inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Isamail Khalifan Mrisho ambaye Disemba 04 mwaka jana, alifariki dunia akiwa uwanjani kwenye mchezo baina ya na timu yake na Kagera Sugar huku kiingilio kilichopatikana kwenye mchezo huo kikiwasilishwa kwa familia ya mchezaji huyo.

  Mchezo huo uliandaliwa na taasisi ya soka nchini iliyomlea mchezaji huyo ya The Football House kwa ushirikiano wa karibu na taasisi ya Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Mama Angelina Mabula iitwayo Angeline Foundation.

  Hadi dakika 90 zinatamatika, timu ya kombaini ya Nyamagana iliibuka mshindi kwa ushindi wa mabo2-1. Mabao ya Nyamagana yalifungwa na Rajesh Kotecha na Kuzaifa Mdabiru huku Ilemela wakipata bao la kufutia machozi baada ya mchezaji wa Nyamagana Jefta John kujifunga.
  Mkuu wa wilaya ya Ilemela, Dkt.Leonald Masele, alisema wilaya yake imejipanga kuhakikisha inaendeleza mchezo wa soka ambapo imeanzisha timu kwa kila soko la machinga wilayani humo hatua ambayo itasaidia kuukuza mchezo huo.
  Mkurugenzi wa taasisi ya The Football House, Mbaki Mutahaba, alisema taasisi hiyo itaendelea kumuenzi mchezaji wake Ismail Khalifan Mrisho huku akiwasisitiza vijana kutumia vyema vipaji walivyonavyo kama ilivyokuwa kwa Mrisho ambaye ameacha alama ya soka nyuma yake baada ya umauti kumkuta.
  Kaka wa marehemu Ismail Khalifan Mrisho, aitwaye Athman Kitwana, akitoa salamu za shukurani kwa niaba ya familia kwa namna ambavyo wadau mbalimbali walivyojitoa kumwendeleza kipaji chake, kusaidia kwenye msiba wake na namna wanavyoendelea kumuenzi baada ya umauti.
  Wazazi wa marehemu Ismail Khalifan Mrisho, kushoto ni Rehema Mfaume (mama) na kulia ni Khalifan Mrisho (baba). 


  0 0

  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Ijumaa Januari 13,2017 amefungua rasmi viwanda viwili mkoani Shinyanga. 
  Rais Magufuli amefungua Kiwanda cha kutengeneza vifungashio vya bidhaa mbalimbali ikiwemo mifuko ya Sandarusi cha Fresho Investment Company Limited na kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited kinachojihusisha na uzalishaji wa vinywaji baridi ikiwemo soda,juisi na maji. 
  Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,ndugu Kadama Malunde ametusogezea picha 45 wakati wa uzinduzi wa viwanda hivyo
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Katikati ni rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika kiwanda cha kutengeneza vifungashio vya bidhaa mbalimbali ikiwemo mifuko ya Sandarusi cha Fresho Investment Company limited kilichopo katika manispaa ya Shinyanga,kulia ni mkurugenziwa kiwanda hicho Freddy Shoo.
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika kiwanda cha kutengeneza vifungashio vya bidhaa mbalimbali ikiwemo mifuko ya Sandarusi cha Fresho Investment Company Limited kilichopo katika manispaa ya Shinyanga
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia kwa kuwapungia mkono wananchi wa mkoa wa Shinyanga waliofika katika kiwanda Fresho Investment Company Limited kushuhudia uzinduzi rasmi wa kiwanda hicho 
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika kiwanda hicho.Kulia kwake ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack,akifuatiwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kushikana mkono na mkurugenzi wa kiwanda cha Fresho Investment Company limited Freddy Shoo baada ya kuweka jiwe la msingi kuashiria uzinduzi wa kiwanda hicho
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijiandaa kukata utepe kuashiria kufungua rasmi kiwanda cha kutengeneza mifuko ya sandarusi cha Fresho Investment Company Limited.
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Rais Magufuli akikata utepe kuashiria kufungua rasmi Kiwanda cha kutengeneza mifuko ya Sandarusi cha Fresho Investment Company Limited cha Mkoani Shinyanga.Kushoto wa kwanza kushoto ni mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini Stephen Masele,wa tatu ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.Wa kwanza kulia ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack,akifuatiwa na mbunge wa jimbo la Kishapu Suleiman Nchambi,mkurugenzi wa kiwanda hicho Freddy Shoo
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ndani ya kiwanda cha Fresho Investment Company Limited akiongozwa na mkurugenzi wa kiwanda hicho Freddy Shoo
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Mkurugenzi wa kiwanda cha Fresho Investment Company Limited Freddy Shoo (kushoto) akimwonesha rais Magufuli jinsi uzalishaji wa vifungashio/mifuko ya sandarusi unavyofanyika katika kiwanda hicho
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Rais Magufuli akiangalia mifuko ya sandarusi katika kiwanda hicho
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Rais Magufuli akiangalia mifuko/vifungashio vya bidhaa mbalimbali vilivyotengenezwa katika kiwanda hicho
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Mkurugenzi wa kiwanda cha Fresho Investment Company Limited Freddy Shoo akimwelezea rais Magufuli namna mitambo ya kisasa iliyopo katika kiwanda hicho inavyofanya kazi katika kiwanda hicho
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Mkurugenzi wa kiwanda cha Fresho Investment Company Limited Freddy Shoo akiteta jambo na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza baada ya kufungua kiwanda cha Kiwanda cha kutengeneza vifungashio vya bidhaa mbalimbali ikiwemo mifuko ya Sandarusi cha Fresho Investment Company Limited ambapo alisema kiwanda hicho ni kizuri na cha kisasa huku akimpongeza mmiliki wa kiwanda hicho Freddy Shoo ambaye ni Mtanzania kwa kuunga mkono jitihada za serikali kuifanya Tanzania kuwa ya viwanda
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Viongozi mbalimbali wakimsikiliza rais Magufuli ambaye alitumia fursa hiyo kuwataka watanzania wengine wenye pesa kujitokeza kuwekeza katika viwanda ili kuhakikisha kuwa uchumi wa nchi unakua na wananchi wanapata ajira
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Tunamsikiliza rais Magufuli
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Viongozi mbalimbali wakiongozwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack (mwenye ushungi mweupe katikati) wakimsikiliza rais Magufuli
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blogHapa ni ndani ya kiwanda cha kutengeneza vinywaji baridi ikiwemo soda,maji na juisi cha Jambo Food Products Company Limited.Katikati ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia mitambo ya kisasa iliyopo katika kiwanda hicho ambacho awamu ya kwanza ya ujenzi wake ulianza mwaka 2015 na kukamilika Juni 2016 kwa kuanza na uzalishaji wa vinywaji baridi ikiwemo soda,Malta,Fresh Juice,Energy drinks na maji kikiwa na uwezo wa kuzalisha tani 200 kwa siku 
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Kushoto ni mkurugenzi wa kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited Salum Khamis maarufu Salum Mbuzi akimweleza rais Magufuli namna kiwanda hicho kinavyofanya kazi.Pamoja na mambo mengine alisema awamu ya pili ya ujenzi itakamilika Oktoba 2017 ambapo kiwanda hicho kitaweza kusindika na kufungasha matunda yote yaliyopo kanda ya ziwa Victoria
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Mkurugenzi wa kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited Salum Khamis maarufu Salum Mbuzi ambaye ni mbunge wa Meatu mkoani Simiyu akimwelezea rais Magufuli jinsi mfumo wa komputa unavyofanya kazi katika shughuli za uzalishaji katika kiwanda hicho cha vinywaji baridi 
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Rais Magufuli akiwa katika kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited cha mkoani Shinyanga ambacho asilimia 100 ya umiliki wake ni watanzania wazawa
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blogRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia soda zilizozalishwa katika kiwanda hicho zikiwa tayari kwa ajili ya matumizi
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Mkurugenzi wa kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited Salum Khamis maarufu Salum Mbuzi akitoa hotuba fupi kuhusu kiwanda hicho.Alisema uwekezaji utakapokamilika mwezi Oktoba mwaka huu,utakuwa na thamani ya dola 125,000,000.Mbuzi aliwataja waliofanikisha katika ujenzi wa kiwanda hicho kuwa ni Benki ya CRDB (Tanzania),COMMERZ Bank (Germany),Krones (Germany),Volvo(Tanzania) na EKN Bank ( Sweden) 
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Mkurugenzi wa kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited Salum Mbuzi alimshukuru rais Magufuli kufungua kiwanda hicho na kuahidi kuendelea kuunga mkono kwa vitendo jitihada za serikali ya awamu ya tano kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda 
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Wananchi wakimsikiliza Mkurugenzi wa kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited Salum Mbuzi ambapo alisema tayari kiwanda hicho kimetoa ajira rasmi 365 na zisizo rasmi 500 na matarajio ni kufikia ajira 2500 pindi uwekezaji utakapokamilika na kwamba hivi sasa bidhaa zao wanauza ndani ya nchi na wanatarajia kupanua masoko ya nje ya nchi kwa nchi za Burundi,Rwanda na Kongo
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited ambapo aliupongeza uongozi wa kiwanda hicho kumuunga mkono kwa vitendo kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa nchi ya viwanda badala ya kuendelea kutegemea viwanda vya nje ya nchi. 
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alieleza furaha yake kuona mkoa wa Shinyanga ukiwa kituo cha uzalishaji wa vinywaji huku akiwapongeza viongozi wa mkoa wa Shinyanga kwa kumuunga mkono kwa vitendo na kuahidi kuwasaidia wawekezaji wazawa kupata mikopo katika benki mbambali ili wawekeze zaidi wananchi wapate ajira
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Rais Magufuli alisema wawekezaji wazawa katika viwanda viwili alivyovifungua mkoani Shinyanga wameonesha uzalendo wa kweli kwa nchi yao na kuwataka watanzania kutoogopa kuanzisha viwanda hata kama vingekuwa vidogo namna gani
  Wananchi wakimsikiliza rais Magufuli
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Kulia ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akifuatiwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na Mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam ambaye pia ni mwenyekiti wa ALAT taifa wakimsikiliza rais Magufuli 
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Wa kwanza kulia ni mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Stephen Masele akifuatiwa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Erasto Kwilasa na mkurugenzi wa kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited Salum Mbuzi wakifuatilia hotuba ya rais Magufuli
  Wananchi wakimsikiliza rais Magufuli
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Katikati ni Kamanda wa polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akiwa na askari polisi wakati rais Magufuli akizungumza katika kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akigawa soda kwa wananchi zilizozalishwa katika kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited kilichopo katika manispaa ya Shinyanga 
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wananchi wakati akigawa soda kwa wananchi zilizozalishwa katika kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Rais Magufuli akiendelea kugawa soda kwa wananchi
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akigawa soda kwa viongozi mbalimbali wa mkoa wa Shinyanga wakiwemo viongozi wa madhehebu ya dini
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiendelea kugawa soda
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Rais Magufuli akiendelea kugawa soda
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Rais Magufuli akigawa soda kwa kikundi cha wacheza ngoma
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifungua soda kutoka katika kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akinywa soda kutoka katika kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited cha mkoani Shinyanga-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia utamu wa soda kutoka katika kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akionesha soda kutoka katika kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited
  Rais John Pombe Magufuli viwanda Shinyanga malunde1 blog
  Wananchi wakiwa wamesimama baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuondoka katika kiwanda cha Jambo Food Products Company Limited baada ya kufungua kiwanda hicho
  Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

  0 0

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bw. Felix Lyaniva anayemfuatia kulia wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia wazee na Watoto wakati wa uzinduzi wa mazoezi mkoa huo katika wilaya ya Temeke yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bw. Felix Lyaniva anayemfuatia kulia wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanamazoezi wakati wa uzinduzi wa mazoezi mkoa huo katika wilaya ya Temeke yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na wanamazoezi wa mkoa wa Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa mazoezi mkoa huo katika wilaya ya Temeke yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.

  Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bw. Felix Lyaniva kushoto akiongea na wanamazoezi wa mkoa wa Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa mazoezi mkoa huo katika wilaya ya Temeke yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bw. Felix Lyaniva wa pili kulia wakiongoza mazoezi wakati wa uzinduzi wa mazoezi katika mkoa huo uliofanyika wilaya ya Temeke yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.

  ……………………………………………………………………

  NA Ally Daud-WIZARA YA AFYA.

  MASHINDANO ya vikundi vya kufanya mazoezi yanatarajiwa kuanza hivi karibuni jijini Dar es salaam na mikoa mingine ili kutekeleza kauli na agizo la Mhe. Makamu wa Rais wa Awamu ya Tano Bi. Samia Suluhu Hassan alilolitoa wakati anazindua kampeni ya kitaifa ya kufanya maoezi Desemba 17 2016.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa ufunguzi wa mazoezi ya hiari mkoa wa Dar es salaam yaliyofanyika katika wilaya ya Temeke.

  “Hata kama zawadi ikiwa ng’ombe lazima kipatiane kikundi kimoja cha mazoezi ambacho ni bora kuliko vikundi vingine mkoa mpaka kitaifa ili kuwafanya watanzania waepuke magonjwa yasioambukiza kwa kupenda mazoezi.

  Aidha Mhe. Ummy amesema kuwa kampeni hiyo ya kufanya mazoezi inalenga zaidi kupunguza gharama za kutibu ugonjwa huo na badala yake kuwataka watazania kufany mazoezi siku tatu katika wiki ngalau kwa dakika 30 il kujikinga na magonjwa yasiomabukiza.

  Kwa upande wake Mkuu Wa wilaya ya Temeke Bw. Felix Lyaniva amesema kuwa mazoezi hayo yamewahamasisha na wamepanga kila ijumaa wafanyakazi wote wa umma wanatakiwa kufanya mazoezi ili kujikinga na magonjwa yasioambukiza.

  Aidha Bw. Lyaniva amesema kuwa wtanzania wanapaswa kufanya mazoezi ili kuweza kujipunguzia gharama za matibabu ya magonjwa yasioambukiza ili kujenga taifa lenye wananchi wenye afya imara.

  Kampeni hiyo ya kufanya mazoezi ya kitaifa ina lengo la kujikinginga na magonjwa yasioambukiza kam vile kisukari, magonjwa ya moyo, saratani, shinikizo la damu na magonjwa ya mfumo wa hewa.

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida Miraji Mtaturu akimwagilia maji kwenye mti alioupanda katika shule ya sekondari Unyihati iliyopo wilayani humo ikiwa ni uzinduzi wa wa upandaji miti kiwilaya uliofanyika leo huku ikibeba kauli mbiu isemayo panda miti ikutunze.

  Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida Miraji Mtaturu akishirikiana na Kaimu Afisa misitu wa Wilaya hiyo Bosco Ndunguru kuweka udongo kwenye mti alioupanda katika shule ya sekondari Unyihati wilayani humo ikiwa ni uzinduzi wa upandaji miti kiwilaya uliofanyika leo huku ikibeba kauli mbiu isemayo panda miti ikutunze.  Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida Miraji Mtaturu akipanda mti katika shule ya sekondari Unyihati wilayani humo ikiwa ni uzinduzi wa upandaji miti kiwilaya uliofanyika leo huku ikibeba kauli mbiu isemayo panda miti ikutunze.  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida, Miraji Mtaturu akizungumza na watendaji wa Wilaya hiyo na wananchi baada ya kuzindua upandaji miti.

  …………….  MKUU wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida Miraji Mtaturu ameziagiza kaya zote zilizopo katika wilaya hiyo kupanda miti 10 kwa mwaka na kuitunza ili kukabiliana na ongezeko la joto la dunia.

  Agizo hilo linahusisha pia vijiji na taasisi zilizopo wilayani humo.

  Akizungumza baada ya uzinduzi wa upandaji miti kiwilaya uliofanyika katika shule ya sekondari ya Unyahati mkuu wa wilaya huyo alisema lengo la wilaya ni kupanda miti 550,000 kwa mwaka.

  “Naelekeza kila tarafa kuwa na kitalu cha miche ya miti ili iwe rahisi wananchi kupata miche na kutimiza lengo tulilojiwekea”,amesema Mtaturu.

  Mbali na hilo ameitaka halmashauri kuweka sheria ndogo ili kusaidia utekelezaji wa mipango ya idara ya misitu waliyojiwekea.

  Ametaja changamoto iliyopo katika utunzaji wa mazingira kuwa ni ufugaji holela na ukame na kuwataka wananchi kuepuka kufanya shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo vya maji.

  Mtaturu amewapongeza wadau wa mazingira kwa kuendelea kushirikiana na serikali katika utunzaji wa mazingira.

  Kauli mbiu ya uzinduzi huo ni panda miti ikutunze ambapo katika uzinduzi wamefanikiwa kupanda miti ipatayo 2500.

  0 0


  Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kaskazini na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa mkoa wa Kaskazini A, Unguja wakati wa Kufungua Mafunzo maalum ya Viongozi na watendaji wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake wa ngazi ya Matawi, Wadi na Majimbo
  Wana CCM wa Kaskazini A wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye mafunzo ya Uongozi yaliofunguliwa na Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kaskazini na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kaskazini A Unguja, Ndugu Juma Haji akihutubia kabla ya kumkaribisha Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kaskazini na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kufungua mafunzo maalum ya Uongozi yaliofanyika Mkokotoni Unguja kwenye Chuo cha Amali.
  ...................................................................

  Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa ambaye pia Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wa CCM katika Mkoa Kaskazini (A) Unguja kuwachukulia hatua stahiki wanachama ambao wanakisaliti na kuhujumu shughuli katika hatua ya kujenga CCM mpya.

  Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduz i(CCM) Taifa SAMIA SULUHU HASSAN ametoa kauli hiyo wakati anafungua mafunzo maalum ya viongozi na watendaji wa CCM na Jumuiya zake wapatao 556 katika ngazi ya matawi, wadi/tarafa na majimbo katika Mkoa wa Kaskazini (A) Unguja.

  Samia Suluhu Hassan amesema kuwa hatua hiyo itasaidia chama kuimarisha shughuli zake kwa sababu chama kitakuwa na watu waadilifu na wenye nia ya kukisaidia CCM kusonga mbele na kupata ushindi mkubwa katika chaguzi zijazo.

  Amesisitiza wanachama na viongozi wa CCM kote nchini waendelee kuweka mipango na mikakati imara itakayowezesha chama kuendelea kupata ushindi mkubwa na kushika dola.

  Mjumbe huyo ambaye pia ni Mlezi wa CCM katika mkoa wa Kaskazini A Unguja amesema Umoja na Mshikamano miongoni mwa wananchama na viongozi ndio silaha madhubuti itakayowezesha chama hicho kuimarisha shughuli zake na kuongeza maradufu idadi ya wanachama nchini.

  Amesema kwa sasa Viongozi watakiwa kujielekeza katika kufufua na kuimarisha jumuiya za chama ambazo katika baadhi ya maeneo hazifanyi kazi vizuri ili zianze kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia kanuni na taratibu za chama.

  Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi(CCM) Taifa pia ameendelea kuonya baadhi ya viongozi waache tabia ya kutengeneza makundi ya ndani ya chama kwa ajili ya kusaka madaraka bali wawe mstari wa mbele katika kujenga umoja na mshikamano ndani ya chama.

  Kuhusu mafunzo, Samia Suluhu Hassan amewahimiza viongozi wanaopata mafunzo hayo kuyatumia vizuri ili kuhakikisha wanaporudi kwenye maeneo yao wanafanya kazi kwa bidii na kwa uaminifu mkubwa.

  Amesema kwa sababu Serikali iliyopo madarakani inatekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi ni muhimu kwa viongozi wa chama katika ngazi zote washirikiane na viongozi wa Serikali katika maeneo husika ili kuhakikisha miradi ya maendeleo ya wananchi inafanyika kwa ubora unaotakiwa kulingana na thamani ya fedha.

  0 0

   Waziri  wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati), akihutubia katika Maadhimisho ya Siku ya Familia ya Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Gift Msuya,Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi, Kamanda wa Polisi Kinondoni, Suzan Kaganda na Meya wa Manispaa hiyo, Benjamini Sitta.
   Waziri  wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akimkabidhi zawadi Mkaguzi wa Polisi, David Mabula.
   Ofisa wa Polisi Hamad akikabidhiwa zawadi na Waziri Nchemba.
   Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Sajeni, Moses Alphance Sinyagwa akipongezwa baada ya kukabidhiwa zawadi ya pikipiki kutokana na ufanyakazi bora.
   Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ali Hapi akitoa neno la shukurani katika maadhimisho hayo.
   Maofisa wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni wakiwa katika shindano ya kumkamata kuku kwenye maadhimisho hayo.
   Maofisa wa jeshi la polisi wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
   Waziri Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.
   Waziri Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa polisi waliotunukiwa vyeti.
   Hapa Waziri Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na wadau 
  kutoka akampuni yaliyodhamini maadhimisho hayo.
   Bendi ya Jeshi la Polisi ikitoa burudani.
  Askari polisi, jamaa zao na waandishi wa habari  wakiwa kwenye hafla hiyo.

  Na Dotto Mwaibale

  WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amesema Serikali itaendelea kupambana wa waingizaji na wauzaji wa dawa za kulevya nchini.

  Mwigulu alitoa kauli hiyo wakati akihutubia katika Maadhimisho ya Siku ya Familia ya Polisi Mkoa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam leo ambapo alikuwa mgeni rasmi.

  "Serikali imejipanga  kupambana na dawa za kulevya ambazo zimekuwa janga la kitaifa ambapo vijana wengi wanakuwa waanga wakubwa'' alisema Mwigulu.

  Mwigulu alisema serikali ya awamu ya tano haitamfumbia macho mtu yeyote atakaye kwamisha jitihada za kupambana na uhalifu nchini ambao wamepanga kuupunguza kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2019.

  Aliongeza kuwa kanuni na sheria zilizowekwa na mkoloni ambazo zinazotumika ndani ya jeshi la polisi zimekuwa na changamoto kubwa kwa askari polisi. 

  Akitolea mifano kadhaa alisema askari polisi aliyekosa nyumba ya kuishi ya jeshi hilo anapaswa kupewa fedha za kulipia pango nje ya kambi ya polisi na suala hilo si la kumuonea huruma askari husika bali ni haki yake.

  Alisema kwa upande wa askari polisi aliyeumia au kupoteza kiungo wakati wa mapambano dhidi yake na wahalifu askari huyo anapaswa kulipa fidia yake kwa wakati badala ya kuunda tume ya kuchunguza jinsi alivyoumia akiwa katika mapambvano hayo.

  "Mambo mengine hayahitaji mpaka uwe na elimu kubwa askari amepambana na majambazi mbele ya watu lakini majambazi hayo yamemjeruhi fidia yake anashindwa kulipwa eti mpaka iundwe tume haya si mambo ya ajabu" alihoji Mwigulu.

  Alisema kwa muda mrefu askari anapopangiwa kituo cha kazi amekuwa akijigharamia kwa nauli na fedha za kujikimu kwa zaidi ya miezi mitatu na zaidi bila ya sababu za msingi.

  Alisema hali hiyo kama askari husika anakuwa si mzalendo anaweza kujiingiza katika tamaa na kutumia silaha aliyonayokufanya uhalifu hivyo akaomba wahusika kuliangalia jambo hilo kwa karibu kwani mshahara na posho kwa askari hao ni haki yao.

  Mwigulu alisema serikali kupitia Rais Dk. John Magufuli imejipanga kuweka mazingira mazuri kwa askari polisi ikiwa ni pamoja na kujengewa nyumba na kuona namna ya kubadilisha sheria ambazo zinaonekana hazina tija kwa wakati huu katika kuliongoza jeshi hilo.

  0 0

   Joseph Mwanukuzi akiwa amepozi na mke wake Mariam wakati wa Ibada ya Ndoa yao iliyofanyika katika Kanisa la St. Peter Oysterbay jijini Dar es Salaam leo.
  Joe na mke wake wakielekea kula kiapo cha ndoa.
  Joseph akimvisha pete ya ndoa mke wake Mariam.
  Mariam akimvisha pete ya ndoa mume wake Joseph.
  Jose akimkumbatia mke wake baada ya kuvalishana pete za ndoa.
  Josephna Mariam wakioneesha pete zao za ndoa.
  Mmeona....
  Bwana na Bi. harusi wakiwa katika pozi.
  Mapozi.....

  Wakiwa na kila aina ya furaha.
  Bwana harusi akihakikisha Bi. harusi anakuwa katika hali ya kupendeza muda wote.
  Akiweka sawa vazi la Bi. harusi.
  Bwana harusi akiweka saini cheti cha ndoa.
  Bi, harusi akiweka saini cheti cha ndoa.
  Maharusi wakionesha shahada zao za ndoa.
  Joseph na Mariam wakitoka kwa furaha baada ya kufunga ndoa takatifu katika kanisa la St. Peter Oysterbay jijini Dar es Salaam leo.
  Ndugu na jamaa wakiwapongeza.
  Picha ya pamoja.


  Picha ya pamoja.
  Bi. harusi akiwa amepozi kwa picha.
  Mapozi.
  Wakiwa katika pozi.
  Ni furaha tupu.
  Busu takatifu....
  Maharusi wakitoka kanisani.

  0 0

  Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akipokea msaada wa mfano wa hundi ya shilingi milioni kumi kwa ajili ya ujenzi wa Skuli ya ngambwa uzi kutoka kwa Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Ndg. Waziri Barnabas, hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika ukumbi wa Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja Dunga.
  Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said (mwenye koti) akipokea msaada wa mfano wa hundi ya shilingi milioni kumi kwa ajili ya ujenzi wa Skuli ya msingi Ngambwa uzi kutoka kwa Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Ndg. Waziri Barnabas, mwenye tai kulia Afisa Elimu wa Wilaya ya Kati Unguja Ndg. Makame Haji na kushoto kwa Mwakilishi Sheha wa Ngambwa Ndg. Amour Ali Mussa na Mratibu wa Shughuli za Serikali SMZ  Wilaya ya Kati Unguja Ndg. Khamis Foum. hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika ukumbi wa Ofisi Kilimo Gunga Wilaya ya Kati Unguja.

  Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Wilaya ya Kati Unguja akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa hundi ya shilingi milioni kumi kutoka kwa Kaimu Meneja wa Benk ya NMB Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa Skuli ya Msingi Ngambwa kisiwa cha Uzi Wilaya ya Kati Unguja na kutowa shukrani kwa msaada wao huo kutowa kwa ajili ya jamii kuwapatia watoto wao majengo ya skuli katika eneo lao. Benk ya NMB itejenga jengo la Skuli hiyo katika Kijiji cha Ngambwe Uzi.

  Kaimu Meneja wa Benk ya NMB Waziri Barnabas akizungumza na Uongozi wa Wilaya ya kati Unguja kuhusuana na kuguswa kwa hali ya kijiji hicho cha ngambwa watoto kupata elimu yao ya msingi masafa marefu na makazi yao. kushoto Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Wilaya ya Kati Ungja. 
   Afisa Elimu Wilaya ya Kati Unguja Ndg. Makame Haji, akitowa shukrani kwa uongozi wa Benk ya NMB kwa msaada wao huo kuwakumbuka Wakazi wa Ngambwa kuwapatia msaada kwa ajili ya kumalizia jengo la Skuli yao ya Msingi. ilioazwa msingi na wananchi wa kijiji hicho. 
  Mratibu Shughuli za Serikali ya SMZ Wilaya ya Kati Unguja Ndg Khamis Foum akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi msaada huo kwa ajili ya maendeleo ya ujenzi wa jengo la Skuli ya Msingi Ngambwa Uzi. na kutowa shukrani kwa Mwakilishi na Mbunge wa Jimbo la Tunguu kwa msaada wao kufanikisha shughuli hiyo ya ujenzi wa Skuli hiyo kuwapunguzia masafa marefu watoto wa ngambwa kufuati masomo katika eneo la uzi.
  Maafisa wa Benk ya NMB wakiwa katika ukumbi wa mkutano wakishuhudia hafla hiyo ya makabidhiano.
  Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akimkabidhi zawadi ya embe za boribo za muyuni Kaimu Meneja Mkuu wa NMB Waziri Barnabas, baada ya hafla hiyo ya kukabidhi cheki ya shilingi milioni kumi kwa ajili ya ujenzi wa Skuli ya Msingi Ngambwa.  

  Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Wilaya ya Kati Unguja Mhe, Simai Mohammes Said akimkabidhi zawadi ya mananasi ya Zenj Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Ndg Waziri Barnabas, baada ya hafla ya kukabidhi cheki shilingi milioni kumi kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa Skuli ya Msingi Ngambwa Uzi Wilaya ya Kati Unguja.
  Imetayarishwa na OthmanMapara. Blog.
  Zanzinews.com
  Mob. 0777424152. Or 0715424152.  

  0 0

  MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo wa tatu kutoka kulia akishiriki kwenye mazoezi ya Jogging leo kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani humo ikiwa ni kuunga mkono agizo la Makamu wa Rais Samia Suluhukulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza,Desderia Haule

   MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati mwenye hijabu akishiriki kwenye mazoezi hayo kwa ajili ya kuimarisha miili yao na kujenga afya.


   MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati mwenye hijabu akishiriki mazoezi ya kuruka ikiwa ni kuunga mkono agizo la Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu leo kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani Muheza   MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati mwenye hijabu akishiriki kwenye kukumbia ikiwa ni kufanya Jogging inayofanyika kila mwezi wilayani humo kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza, Desderia Haule wa kwanza kushoto ni Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mathew
   MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati mwenye hijabu katika Jogging ambayo hufanyika kila Jumamosi ya kwanza ya  mwezi kwa ajili ya kuimarisha miili na kuwaweka fiti wa kwanza kulia ni Mwandishi wa Azam TV mkoani Tanga,Mariam Shedafa akishiriki mazoezi hayo.
  MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati mwenye hijabu akiteta jambo na Mganga Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mathew mara baada ya kumalizika mazoezi hayo.
  MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kumalizika kwa Jogging hiyo.
  MKUU wa Wilaya ya Muheza Mhandisi Hajat Mwanasha Tumbo amewaagiza watendaji wa kata na Vijiji kuhakikisha wanatenga maeneo  ya viwanjavya michezo ili kuwezesha vijana kushiriki kwenye michezo jambo ambalolinaweza kuwasaidia kupata ajira na kuweza kujikwamua kimaisha.

  Agizo la Mkuu wa Wilaya hiyo alilitoa leo wakati akiunga mkonokampeni ya Makamu wa Rais Samia Suluhu ya kufanya mazoezi kila Jumamosi ya pili ya mwezi lengo likiwa kuimarisha afya na miili yawatumishi na vijana ili kuepukana na magonjwa yasiyoambukizwa ambayoyanaweza kuwanyemelea.

  Alisema kutokuwepo kwa viwanja vya kutosha Wilayani humo kunapunguzafursa kwa wananchi na vijana wengi kutokufanya mazoezi na hatakuonyesha vipaji vyao ambavyo vingeweza kuwa sehemu ya kujipatiaajira.

  “Michezo ni afya na ajira,kuongeza idadi ya viwanja kutatuongezea
  mchango mkubwa wa kukuza vipaji na kufungua fursa za ajira kwa vijanawengi ambao asilimia kubwa wapo mtaani wakiwa wanakabiliwa na ugumu wamaisha”Aliseam Hajat Tumbo.

  Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo (DMO) Mathew Mganga alisemakuwa kumekuwepo na ongezeko kubwa la magonjwa wa magonjwayasiyoambukizwa kutokana na kutokuwepo na utaratibu wa kufanya mazoezihasa kwa watumishi wa Serikali.
   
  Alisema ili kuweza kukabiliana na magonjwa hayoyasiyoambukizwa kamaugonjwa wa Moyo,sukari na shindikizo la damu lazima kauli ya makamu waRais ya kuhamasisha kufanyike mazoezi nchi nzima itekelezwe kwavitendo na si maneno.

  “Laima tubadilike kwa kufanya mazoezi ili kupunguza magonjwa hayoambayo yamekuwa pigo kwa wananchi na hasa watumishi waUmma,inatulazimu tupambane kukabiliana na hali hiyo kwa kufanyamazoezi mara kwa mara ili kuboresha afya zetu”Alisema Dk Mathew.

  Naye Katibu Tawala Wilaya hiyo Desderia Haule ambae pia ni Mwenyekitiwa Baraza la Michezo Wilya alisema zoezi hili litakuwa ni endelevu naSerikali itatenga maeneo ya kutosha ya viwanja kwa ajili mazoezi nakukuza vipaji vya vijana .
  Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

  0 0

  Mkuu  wa mkoa  wa  Iringa  Amina  Masenza  katikati   wa  pili kulia  akiwa na mbunge  wa   viti  maalum mkoa  wa Iringa  Ritta  Kabati (CCM)  wakiongoza mazoezi  kwa wanawake  watumishi na  wasio  watumishi  pamoja na  baadhi ya  wanaume  leo  katika  uwanja  wa Samora  mazoezi  ambayo  yataendelea  kila jumamosi  mjini hapa Picha  zote na MatukiodaimaBlog
  Baadhi ya  askari  wanawake  walioshiriki  mazoezi  leo   uwanja  wa Samora  Iringa
  Wanawake na wananchi  wakitoka  uwanja wa  samora  katika  mazoezi leo
  Mazoezi  kwa afya  yako
  Mmoja  ya  wanajeshi  Bw  Kimbavala  aliyeshiriki  kutoa mazoezio  leo
  DC Kasesela  akiwa katika  picha ya  pamoja na  watumishi wa Tanesco  Iringa  walioshiriki mazoezi
  Mazoezi  yakiendelea  kwa wote
  RC  Iringa  wa  tatu  kushoto  akifuatiwa na mbunge Kabati
  RC  akionyesha  uwezo  katika mazoezi
  DC  Richard  Kasesela  akiwajibika katika mazoezi
  Kasesela  akionyesha  mazoezi  leo  uwanja wa  samora  Iringa
  Afisa  habari  Manispaa ya  Iringa  Sima Bingileki  katikati  akishiriki mazoezi
  Baadhi ya  maofisa  watendaji kata  wakiwa katika mazoezi
  vyombo  vya ulinzi na usalama  mkoa  wa  Iringa  nanvyo vyashiriki mazoezi  kwa  kuzunguka  mtaani mji  wa Iringa
  RPC  Julius  Mjengi kulia  akiongoza  mazoezi  kwa askari  polisi na majeshi  mengine mkoa  wa Iringa
  Ni mazoezi kwa  wote  mkoa  wa  Iringa  Picha  zote na MatukiodaimaBlog

  0 0

  Mkurugenzi wa Multichoiuce Tanzania  Maharage Chande akizungumza wakati wa kuwakaribisha waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbaliu nchini wakati wa ufunguzi wa kombe la mataifa Afrika yanayofanyika Gabon
  Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania Shumbana Walwa akuzngumza wakati wahafla ya waandishi wa habari pamoja na kuangalia ufunguzi wa kombe la mataifa Afrika AFCON kwa oamoja leo Jijini Dar es salaam

  baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika hafla hiyo leo Jijini Dar es salamm.


  Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania Shumbana Walwa (Katikati) akijadiliana jambo na John Bukuku (kulia) wakati wa hafla ya waandishi wa habari pembeni ni Othman Michuzi.

  Bendi alikwa wakitumbuiza kwenye hafla ya waanidhi wa habari leo Jijini Dar es salaam.


  Mkurugenzi wa Multichoiuce Tanzania  Maharage Chande akiwa pamoja na wafanyakazi wengine wakampuni hiyo wakati wa hafla ya waandishi wa habari iliyofanyika leo Jijini Dar es salaam.
  Ahmad Michuzi akisaini katika kitabu cha wageni wakati wa hafla ya waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam.

  Waandisi wa habari kwa pamoja na wafanyakazi wa Multichoice Tanzania wakiburudika wka pamoja katika hafla ya waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam.  Waaandishi wa habari wakishuhudia kwa pamoja uzinduzi wa michuano hiyo leo Jijini Dar es salaa.Picha na Emanuel Masaka

older | 1 | .... | 1100 | 1101 | (Page 1102) | 1103 | 1104 | .... | 1897 | newer