Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

RAIS MAGUFULI AUAGIZA UONGOZI WA MKOA WA SHINYANGA KUFUTA USAJILI WA MRADI WA TRIPLE S.

$
0
0
Na: Frank Shija - MAELEZO

Rais wa Jmamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Shinyanga kumfutia usajili mwekezaji wa Kiwanda cha Nyama, Kampuni ya Triple S na badala yake watafute mwekezaji mwingine.

Agizo hilo limetolewa leo Mjini Shinyanga wakati akiwahutubia wananchi wa mji wa huo ambapo yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi iliyoambatana na sherehe ya kuadhimisha miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

“Futeni usajili wa mradi wa Triple S, haiwezekani mwekezaji hakashindwa kuendesha kiwanda kwa zaidi ya miaka 10 sasa afu tuendelee kumkumbatia, tafuteni mwekezaji mwingine, mkishindwa semeni Serikali iweke hela, ili uzalishaji uendelee,” alisisitiza Rais Magufuli.

Aliongeza kuwa mwekezaji huyo amekuwa mbabaishaji kwani tangu kipindi yeye (Rais Magufuli) alipokuwa Waziri wa Uvuvi na Mifugo alimfahamu na alimpa maelekezo cha kusikitisha hakuna jambo aliloendeleza ikiwemo kuanza kwa uzalishaji.

Akizungumzia sababu ya kufanya maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar katika upande huu wa Bara Rais Magufuli amesema kuwa Tanzania ni moja, na kuongeza kuwa chimbuko halisi la uwepo wa Taifa la Tanzania ni Mapinduzi ya Zanzibara mabapo miezi michache tu baada ya kufanyika kwa mapinduzi hayo Tanganyika na Zanzibar ziliungana na kuzaliwa kwa Taifa la Tanzania.

Kwa upande wake Waziri wa TAMISEMI na Kazi maalumu kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Haji Omari Heri amesema wao kama Wazanzibar wamefarijika sana kwa kitendo cha Serikali ya Awamu ya Tano kuamua kushiriki maadhimisho ya Mapinduzi Matukufu kwa kusherehekea katika upande wa Bara kitu ambacho akijawahi kufanyika kabla.

Aliongeza kuwa ujio wake umetokana na ukweli kwamba Tanzania ni nchi moja hivyo Rais Magufuli alivyoeleza nia yake ya kuadhimisha Maapinduzi huku Bara, Rais Dkt. Shein alimteua aje kumwakilisha na kueleza kuwa maefarijika sana na kusema Tanzania ni yetu sote na tutaendelea kuwa wamoja.

Rais Dkt. Magufuli yuko ziarani Mkoani Shinyanga ambapo kesho anatarajiwa kufungua viwanda kadhaa vilivyopo mkoani hapo, baadhi ya viwanda hivyo ni pamoja na Kiwanda cha Vinywaji Baridi (maji) cha Jambo, Kiwanda cha Mafuta na vingene.


MAADHIMISHO YA MIAKA 53 YA MAPINDUZI YALIVYOFANYIKA LEO ZANZIBAR

$
0
0
 Makomandoo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania  wakionyesha uwezo wao wa kupigana bila silaha katika Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye wawnja wa Aman Januari 12, 2017. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
  Makomandoo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania  wakionyesha  jinsi matofari yanavyoweza kuvunjwa juu ya kichwa katika maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa Aman, Januari 12, 2017. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
 Komandoo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania akiwa  amelala  juu ya misumari  huku wenzake wakipita juu yake ikiwa ni moja ya maonyesho ya ukakamavu yaliyoonyeshwa na Makomandoo hao katika maadhimisho ya  miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa Aman Januari 12. 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Rais wa  Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein  akihutubia katika kilele cha Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa Aman   Januari 12, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

 Rais Mstaafu wa Zanzibar, Aman Karume akiteta na  Rais Mstaafu wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete katika maadhimisho ya miaka  53 ya Mapinduzi  ya Zanzibar  zilizofanyika kwenye uwanja wa Aman Zanzibar Januari 12, 2017.  
  Baadhi ya waandamanaji wakishangilia  wakati walipopita mbele ya Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed  Shein katika maadhimisho ya  miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa Aman, Zanzibar Januari 12, 2017.
 Mmoja wa wananchi wa Zanzibar akimsikiliza kwa makaini Rais wake, Dkt. Ali Mohammed Shein  wakati alipohutuba katika Maadhimisho ya  miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar  kwenye uwanja wa Aman Januari 17, 2017.
 Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein, Makamu wa Rais, Samia Suluhu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Sif Idd wakifuatilia kwa makini gwaride  la Maaddhisho ya miaka 53  ya Mapinduzi ya Zanzibar kwenye uwanja wa Aman, Januari 12, 2017
 Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi cha Zanzibar akipita   kwa ukakamavu mbele ya  mgeni rasmi Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein  katika gwaride la kuadhimisha miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari 12, 2017.



VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO IJUMAA JANUARI 13, 2017

SBL inalaani kusambazwa kwa video isiyo na maadili kwenye mitandao ya kijamii

$
0
0
TAARIFA KWA UMMA Dar es Salaam Januari 13, 2017- Kampuni ya Bia ya Serengeti inapenda kuwataarifu wateja wake na umma na kwa ujumla kuwa kuna video isiyo na maadili inaiyosambazwa katika mtandao ya kijamii ikionesha msanii akiigiza na kuimba wimbo wenye mahadhi ya taarabu mbele ya bango lenye nembo ya bia Serengeti Premiur Lager. 
 
Tunapenda kuweka bayana kuwa onesho la msanii huyo halikuidhinishwa wala kudhaminiwa na SBL Pia msanii huyo sio sehemu na hajawahi kuwa mmoja wa mawakala wetu wanaotoa huduma za kutangaza bidhaa zetu.
 
 Video hiyo ambayo haizingatii maadili ya sanaa inatoa picha mbaya jambo ambalo ni kinyume na sera ya SBL ya kuzingatia maadili mema katika shughuli za kutangaza bidhaa zake. Aidha ikumbukwe kwamba SBL imekuwa mstari wa mbele katika kulinda na kusimamia maadili katika shughuli zake za kijamii ikiwa ni pamoja na kuhamasisha unywaji wa pombe kistaarabu.
 
 Tunauhakikishia umma na wateja wetu kuwa SBL inafanya shughuli zake za kijamii kwa kuangalia mambo yenye tija kwa jamii na sio vinginevyo. Tunapenda kuwashukuru sana wateja wetu na umma kwa ujumla kwa kuendelea kushirikiana nasi.
 
 Imetolewa na Mkurungezi wa Mahusiano 
Serengeti Breweries Limited.

WATANZANIA WATANO WACHAGULIWA KUWA MABALOZI WA KUWAINUA WANAWAKE KIUCHUMI DUNIANI

$
0
0
“BINGWA WA MABADILIKO” au “CHAMPION FOR CHANGE” ni kauli mbio iliyoanzishwa kwenye shindano lililoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maswala ya wanawake (UN-WOMEN) lenye lengo wa kuwapata vijana watakaoweza kushirikiana na serikali za nchi zao kuwainua wanawake kiuchumi.

Maombi zaidi ya 4000 kutoka kona zote za dunia yalitumwa kwa shirika hilo na ni vijana 170 tu ndio waliobahatika kuchaguliwa wakiwemo vijana watano kutoka Tanzania.

Vijana hao waliofanikiwa kuchaguliwa kuwa mabalozi wa “CHAMPION FOR CHANGE” ni Agnes Mgongo, Doris Mollel, Hassani Tozir, Catherine Ruge pamoja na Sadick Lungendo.

Mabalozi hawa watashirikiana na serikali kwa kwa hamasa na mafunzo mbalimbali ili  kuwainua na kuwawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi. 

Hivyo basi wadau wote kwenye njanja tofauti tofauti wanaombwa kuwaunga mkono mabalozi hawa kwa kushiriki kwenye midahalo au mahojiano kwa kupitia kwenye mtandao mkubwa kijamii ulioanzishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maswala ya wanawake (UN-WOMEN) unaoitwa “JOIN THE MOVEMENT” kwa kufuatisha kiunganishi (link) hapa chini kujisajili na kuanzisha mijadala yako.


https://www.empowerwomen.org/en/join-the-movement

SIASA ZA CHUKI NA CHAFU HAZIWEZI KULETA MAENDELEO KATIKA TAIFA LETU

$
0
0
 Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF), Mhandisi Shaban Kaswaka (kushoto), akimtambulisha kwa wananchi Mgombea Udiwani kupitia chama hicho Kata ya Kijichi, Abdallah Shamas katika mkutano wa kampeni uliofanyika eneo la Mwanamtoti Temeke jijini Dar es Salaam jana.
 Mgombea Udiwani kupitia chama cha CUF wa Kata ya Kijichi, Abdallah Khalid Shamas akihutubia katika mkutano huo.
 Wasanii wa kundi la Sanaa la Mwamuko wakitoa burudani kwenye mkutano huo.
 Wafuasi wa CUF wakimkaribisha mgombea udiwani wa Kata ya Kijichi wakati alipokuwa amewasili kwenye mkutano wake wa kampeni.
 Meza kuu katika mkutano huo.
 wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.
 Sera za CUF zikitolewa.
 Mkutano ukiendelea.
Wafuasi wa chama cha CUF wakiinua mikono kukubali kumpigia kura mgombea wa chama hicho.

Na Dotto Mwaibale

MGOMBEA  Udiwani  Kata ya Kijichi kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Abdallah Khalid Shamas amewataka wananchi na wagombea wenzake kuacha siasa za chuki na chafu ili kuiletea maendeleo kata hiyo na taifa kwa ujumla.

Shamas alitoa ombi hilo wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika eneo la Mwanamtoti Kijichi Dar es Salaam jana wakati akijinadi kwa wapiga kura.

"Siasa  chafu za chuki na  zinazowatenganisha wananchi kutokana na itikadi za vyama vyao hazifai na haziwezi kuleta maendeleo katika kata hiyo na taifa kwa ujumla" alisema Shamas.

Alisema siasa chafu zilizokuwepo katika eneo hilo la Mwanamtoti zilifikia hatua ya kugawana makaburi jambo ambalo lilikuwa ni hatari katika kushirikiana.

Akizungumzia baadhi ya vipaumbele vyake iwapo atachaguliwa kuwa diwani wa kata hiyo alisema cha kwanza ni kuhakikisha eneo la Mwanamtoti wanapata shule ya msingi ambayo itawasaidia watoto wa eneo hilo kutotembea umbali mrefu wa kwenda shuleni.

Alitaja kipaumbele chake cha pili ni kuhakikisha eneo hilo linapata zahanati pamoja na kukaa na wataalamu wa taasisi za fedha kuona namna ya kuanzisha Saccos au chombo cha fedha ili kuweza kutoa fursa kwa wananchi wa kata hiyo kukopa na kufanikisha maendeleo yao.

Mgombea huyo amewaomba wananchi wa eneo hilo Januari 22, mwaka huu wamchague ili awatumikie baada ya kata hiyo kukosa maendeleo kwa zaidi ya miaka 20.

Uchaguzi huo mdogo wa ngazi ya udiwani unafanyika katika kata hiyo kufuatia aliyekuwa diwani kufariki dunia mapema mwaka jana na nafasi hiyo kuwa wazi.

NAIBU WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU KAZI VIJANA NA AJIRA ATHONY MAVUNDE ATEMBELEA MIRADI MBALI MBALI YA VIJANA WAJASILIA MALI WILAYANI MBOZI MKOANI SONGWE.

$
0
0
Mhe Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Athony Peter Mavunde wa tatu kushoto akionyeshwa na kupata maelekezo juu ya ufugaji wa Samaki na Msimamizi wa Kituo cha Maendeleo ya Vijana SASANDA Ndg Martin kambisi wa Pili kushoto.

Mhe Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Athony Peter Mavunde akizungumza na Vijana wajasilia mali wakulima na wafugaji wanaopata Mafunzo juu ya kilimo bora na Ufugaji wa kisasa katika Kituo cha maendeleo ya Vijana SASANDA kilichopo Wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe.

Mhe Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Athony Peter Mavunde akikagua duka la dawa baridi Moja kati ya Mradi wa Vijana wa kikundi cha MELANAKO kilichopata Mkopo wa shiling Milion Saba toka Wizarani.

Mhe Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Athony Peter Mavunde akitazama bidhaa za ujasiliamali Asali pamoja na Dawa ya Kusafishia chooni vinavyo zalishwa na kikundi cha Vijana wajasilia mali MELANAKO kilichopo wilayani Mbozi mkoani Songwe.


Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mhe:Athony Peter Mavunde wa kwanza kulia akipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya mbozi ambae pia ni kaimu Mkuu wa Mkoa wa Songwe mhe:John Palingo mara baada ya kuwasili Mkoani Songe.

Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mhe:Athony Peter Mavunde wa pili kiushoto akiongozwa na Kaimu RAS wa Mkoa wa Songwe Ndg:Samwel Razaro kusalimiana na Watumishi mbalimbali wa serikali alipo wasili katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Songwe,

Kaimu Afisa Elimu wa Mkoa wa Songwe Ndg:Samwel Mshana akimsomea Mhe Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Athony Peter Mavunde Taarifa ya Maendeleo ya Mkoa wa Songwe alipo kutana na kuzungumza na watumishi Mbalimbali wa serikali mkoani Songwe.


Nawaomba Viongozi wa Halmashauri kwanza Ndani ya Halmashauri zetu mhakikishe mmetenga Maeneo ya Shughuli za kilimo kwa vijana, pili Kusimamia Urasimishwaji wa Saccos kwa kila Halmashauli, tatu Kusimamia kwa Uadilifu mkubwa juu ya Fedha za Mikopo kwa vijana kuhakikisha zinawafikia walengwa na Nne kwenda kasi katika utekelezaji wa Falsafa ya Serikali ya Awamu ya tano Juu ya Uchumi wa Viwanda”Aliyasema hayo Mhe Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Athony Peter Mavunde wakati akizungumza na Watumishi Mbali mbali wa Serikali Mkoani Songwe. .

Mhe Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Athony Peter Mavunde akikagua Mradi wa Ufugaji wa Ng’ombe wa kisasa alipotembelea Kituo cha maendeleo ya Vijana SASANDA chenye vikundi vya vijana 12 vyenye jumla ya Vijana 200 wanaojifunza shughuli mbali mbali za kilimo na Ufugaji wa kisasa.

MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA YASHAURIWA KUHAMASISHA MATUMIZI YA VITAMBULISHO VYA TAIFA KATIKA HUDUMA NCHINI

$
0
0
Mhe. Mwinyiusi A. Hassan, Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “A” akiweka saini kwenye kitabu cha wageni alipotembelea banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA kwenye Maonesho ya 53 ya Sherehe za Mapinduzi Zanzibar viwanja vya Miasara Zanzibar.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA, Ndg. Andrew W. Massawe akisaliana na Ndg. Aboubakar Mikidadi Othuman mwananchi aliyetembelea banda la NIDA kupata huduma ya Usajili.

Ndg. Abdulaziz Juma Mtumwa (kushoto) Afisa Msajili Msaidizi – NIDA akimsajili Ndg. Aboubakar Mikidadi Othuman kupata kitambulisho cha Taifa baada ya kupokea maelezo ya kina toka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA.

Dr. Hamed Rashid Hikmany; Mkuu wa chuo Kikuu cha Abdulrahman Al-Sumait Memorial akiweka saini kitabu cha wageni alipotembelea banda la maonesho la Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa Zanzibar
Mmoja wa wananchi akipata maelezo ya kina kuhusu muonekano mpya wa Kitambulisho cha Taifa alipofika kutembelea banda la NIDA Maisara – Zanzibar.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA Ndg. Andrew W. Massawe akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi kwenye banda la Mamlaka ya Vitambulisho NIDA- Maisara Zanzibar.

……………


Maonesho ya sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar yameendelea leo kwenye viwanja vya Maisara – Zanzibar, ambapo wananchi wameendelea kumiminika kwa wingi kwenye banda la maonesho la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kusajiliwa, kuchukua vitambulisho vyao na kupata elimu kuhusu umuhimu na faida za Vitambulisho vya Taifa.

Miongozi mwa wageni waliotembelea banda hilo ni Mhe. Mwinyiusi A. Hassan, Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “A”, Dr. Hamed Rashid Hikmany; Mkuu wa chuo Kikuu cha Abdulrahman Al-Sumait Memorial, ambao wamepongeza kazi nzuri inayofanywa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa na kupendekeza Vitambulisho vya Taifa kuanza kutumika katika shughuli mbalimbali ili kupunguza utitiri wa vitambulisho.

“Tuimarishe utendaji na tufanye kazi kwa malengo na kwa kufanikisha utendaji kwa kuendelea kuwa karibu zaidi na Serikali za Wilaya, Shehia na wananchi” alisisitiza Mkuu wa Wilaya.

Aidha; Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Dr. Andrew W. Massawe naye amejumuika na wananchi wa Zanzibar kwa kutembelea na kukagua shughuli zinazofanyika kwenye banda la NIDA Maisara- Zanzibar na kushiriki kuzungumza na kujibu hoja za wananchi wa Zanzibar walio kuwepo kwenye banda la NIDA kupata huduma. Wananchi hao wameonyesha kufarijika na utendaji wa Mkurugenzi huyo na kuelekeza furaha yao kwa jinsi alivyojitoa na kushirikiana na wafanyakazi wake katika kujibu hoja mbalimbali za wananchi.

Akizungumza wakati akijibu hoja za wananchi, Bwana Masssawe amepongeza wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye banda la NIDA kupata huduma na ufafanuzi kuhusu Vitambulisho vya Taifa; na kuipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na wananchi kwa jumla kwa kutimiza miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

“NIDA tunaahidi kuendelea kuwa karibu zaidi na wananchi kwa kuendelea kutoa huduma nzuri zaidi kwa wananchi; lengo letu tuhakikishe kila Raia mwenye umri wa miaka 18 na kuendelea anapata kitambulisho chake, pamoja na kuwasajili Wageni, Wakimbizi wenye sifa za kuishi nchini kama sheria ya Usajili na Utambuzi wa watu inavyoelekeza” Amesisitiza

Maonesho ya sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar yalianza tarehe 07 Januari na yatamalizika Jumamosi tarehe 14 Januari 2017 viwanja vya Maisara Zanzibar, NIDA ikiwa miongoni mwa taasisi zinazoshiriki kwa kutoa huduma za Utambulisho kwa wananchi na usawaji wa Vitambulisho kwa wananchi ambao wamekamilisha taratibu za usajili.

ZIARA YA MSIMAMIZI WA CADESE KATIKA MRADI WA UMEME JUA WA MAJARIBIO, HOSPITALI YA WILAYA NYAMAGANA, MWANZA

$
0
0
Mratibu wa Mradi wa Umeme Jua wa Majaribio katika hospitali ya wilaya ya Nyamagana, Amin Abdallah (kushoto mbele) akimwongoza Msimamizi wa Mradi wa Kuwajengea Uwezo Wataalam wa Nishati na Tasnia ya Uziduaji (CADESE), Paul Kiwele (kulia mbele) pamoja na wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini katika ziara kwenye mradi huo.
Mratibu wa Mradi wa Umeme Jua wa Majaribio katika hospitali ya wilaya ya Nyamagana, Amin Abdallah (kulia) akielezea mfumo wa kuongozea vifaa vya umeme jua katika hospitali ya wilaya ya Nyamagana.
Mratibu wa Mradi wa Umeme Jua wa Majaribio katika hospitali ya wilaya ya Nyamagana, Amin Abdallah (kushoto) akionesha mita maalum ya kuruhusu umeme kuingia na kutoka kwenye Gridi ya Taifa.
Mratibu wa Mradi wa Umeme Jua wa Majaribio katika hospitali ya wilaya ya Nyamagana, Amin Abdallah ( wa pili kutoka kulia) akionesha karabai zinazotumia umeme jua zilizotolewa na mradi huo kwa wavuvi wa soko la samaki la Mwaloni jijini Mwanza.
Mmoja wa wavuvi katika soko la samaki la Mwaloni jijini Mwanza, Joseph Athony (kushoto) akielezea manufaa ya karabai zinazotumia umeme jua zilizotolewa na Mradi wa Umeme Jua wa Majaribio.

Sehemu ya wodi za wagonjwa katika hospitali ya wilaya ya Nyamagana iliyofungwa umeme jua.
Mratibu wa Mradi wa Umeme Jua wa Majaribio katika hospitali ya wilaya ya Nyamagana, Amin Abdallah, (kulia) akielezea maendeleo ya mradi huo kwa Msimamizi wa Mradi wa Kuwajengea Uwezo Wataalam wa Nishati na Tasnia ya Uziduaji (CADESE), Paul Kiwele ( wa pili kutoka kulia). Wengine ni wataalam kutoka Sehemu ya Nishati Jadidifu, Wizara ya Nishati na Madini.
Mratibu wa Mradi wa Umeme Jua wa Majaribio katika hospitali ya wilaya ya Nyamagana, Amin Abdallah (kulia) akieleza jambo kwa Mtaalam kutoka Sehemu ya Nishati Jadidifu- Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Stephan Kashushura (katikati). Kushoto ni Nasra Mohamed kutoka Wizara hiyo.

WATANZANIA WATANO WACHAGULIWA KUWA MABALOZI WA KUWAINUA WANAWAKE KIUCHUMI DUNIANI

$
0
0
“BINGWA WA MABADILIKO” au “CHAMPION FOR CHANGE” ni kauli mbio iliyoanzishwa kwenye shindano lililoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maswala ya wanawake (UN-WOMEN) lenye lengo wa kuwapata vijana watakaoweza kushirikiana na serikali za nchi zao kuwainua wanawake kiuchumi.

Maombi zaidi ya 4000 kutoka kona zote za dunia yalitumwa kwa shirika hilo na ni vijana 170 tu ndio waliobahatika kuchaguliwa wakiwemo vijana watano kutoka Tanzania.

Vijana hao waliofanikiwa kuchaguliwa kuwa mabalozi wa “CHAMPION FOR CHANGE” ni Agnes Mgongo, Doris Mollel, Hassani Tozir, Catherine Ruge pamoja na Sadick Lungendo.

Mabalozi hawa watashirikiana na serikali kwa kwa hamasa na mafunzo mbalimbali ili  kuwainua na kuwawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi. 

Hivyo basi wadau wote kwenye njanja tofauti tofauti wanaombwa kuwaunga mkono mabalozi hawa kwa kushiriki kwenye midahalo au mahojiano kwa kupitia kwenye mtandao mkubwa kijamii ulioanzishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maswala ya wanawake (UN-WOMEN) unaoitwa “JOIN THE MOVEMENT” kwa kufuatisha kiunganishi (link) hapa chini kujisajili na kuanzisha mijadala yako.


https://www.empowerwomen.org/en/join-the-movement

NAIBU WAZIRI MAKANI ALIVYOPANIA KUMALIZA MGOGORO ULIODUMU ZAIDI YA MIAKA 25 LOLIONDO

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (wa pili kushoto) akioneshwa Ramani ya Kijiji cha Ololosokwan na Diwani wa Kata hiyo, Yanick Ndoinyo alipotembelea kijiji hicho hivi karibuni kuona changamoto za uhifadhi. Kulia ni Kaimu Mwenyekiti wa Kijiji cha Ololosokwan, Emmanuel Salteimoi. 
Kundi la mifugo likiwa ndani ya Pori Tengefu la Loliondo, karibu kabisa na mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (kulia) akizungumza katika kikao cha wadau wa mgogoro wa Pori Tengefu la Loliondo alichokiitisha katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Tarafa ya Loliondo mkoani Arusha hivi karibuni.

NA HAMZA TEMBA - WMU
............................................................................

Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais, Dkt. John Pombe Magufuli mara tu ilipoingia madarakani mwezi Oktoba mwaka juzi ilitoa vipaombele vyake kadhaa vya kutelezwa na wizara zake mbalimbali huku Wizara ya Maliasili na Utalii ikikabidhiwa majukumu mazito matatu ya kutekeleza katika kipindi cha uongozi wake. 

Majukumu hayo yaliyotolewa na Rais Magufuli wakati wa hotuba yake ya kwanza ya kulihutubia bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma, ni yale ya kuhakikisha kuwa wizara hiyo inakomesha vitendo vya ujangili, kuongeza mapato ya serikali na kushuulikia utatuzi wa migogoro ya mipaka kwenye maeneo ya hifadhi nchini. 

Wizara ya Maliasili na Utalii, imesema kuwa imejipanga kuhakikisha kuwa malengo yake ya uhifadhi wa Maliasili, Malikale na Kuendeleza Utalii pamoja na utekelezaji wa vipaombele ilivyopewa na Serikali ya awamu ya tano kuwezesha kufikia malengo hayo yanatimia kwa wakati.

Kwa upande wa utatauzi wa migogoro kwenye maeneo ya hifadhi nchini, Wizara hiyo imejipanga kuwashirikisha wadau wote wanaohusika na migogoro hiyo kwa kukaa nao pamoja kwenye vikao vya majadiliano na kuweka mikakati ya pamoja ya kufikia suluhu ya migogoro hiyo kwa faida ya Serikali na wadau wote wanaohusika.

Hivi karibuni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani alifanya ziara ya kiutafiti katika Hifadhi ya Ngorongoro pamoja na Pori Tengefu la Liliondo, lengo kuu la ziara hiyo ikiwa ni kuona uhalisia wa changamoto zilizopo pamoja na kupata taarifa sahihi kutoka kwa wadau husika, alifanya hivyo bila ya kujitambulisha kwa lengo la kupata taarifa sahihi kuhusiana na migogoro hiyo.

Akiwa katika Tarafa ya Loliondo alitembelea kijiji cha Ololosokwan, Pori Tengefu la Liliondo, sehemu ya mpaka wake na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na eneo la muwekezaji, kampuni ya Ortello Business Corporation (OBC) na kampuni ya &Beyond (Kleins Camp).

Akiwa katika eneo hilo alizungumza na viongozi wa kijiji cha Ololosokwan ambao waliwasilisha changamoto kadhaa ikiwemo ongezeko la mifugo kutoka nchini Kenya na vijiji jirani hususani wakati wa kiangazi kwa ajili ya kutafuta malisho na uelewa tofauti wa mpaka baina ya vijiji na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Diwani wa Ololososkwan, Yanick Ndoinyo alisema uhifadhi umekuwa ukiwanufaisha kwa kiasi kikubwa kwa kuwa kupitia utalii kijiji hicho hupata fedha taslim zaidi ya shilingi milioni 300 kwa mwaka kupitia mikataba ya wawekezaji na mgao kutoka Serikalini.

Pamoja na mchango huo amesema “wawekezaji wa eneo hili wamekuwa wakitekeleza miradi ya jamii ambapo wamechimba visima vinne, wamejenga madarasa mawili na kisima kingine kinajengwa jirani na kata hii, lakini kampuni zote kwa ujumla zinatoa ajira kwa wanavijiji, kwahiyo kwakweli sisi ni kijiji ambacho tumeona manufaa ya utalii “

Ndoinyo alisema fedha hizo zimekuwa zikisaidia kusomesha watoto masikini kuanzia elimu ya awali hadi chuo kikuu, kusaidia ujenzi wa zahanati na huduma nyingine za jamii.

Kwa upande wa kampuni ya Ortello Business Corporation (OBC) ambao wamewekeza katika pori hilo kupitia Afisa Mahusiano wao, William Parmat walisema changamoto kubwa inayowakabili ni ya wananchi kuingiza mifugo katika eneo la uwekezaji jambo linalosababisha uharibifu mkubwa wa mazingira ikiwemo wanyamapori kutoweka.

Muwekezaji huyo alisema wapo tayari kuweka makubaliano ya uhifadhi na wananchi pamoja na kusaidia kujenga miundombinu ya huduma za jamii. Alisema changamoto ya mifugo imesababishwa na msukumo wa baadhi ya asasi za kiraia kwa wananchi kwamba Serikali inataka kuchukua pori hilo hivyo waingize mifugo yao kwa ajili ya kulilinda.

Naibu Waziri Makani aliuahidi uongozi wa kijiji cha Ololosokwan pamoja na wawekezaji hao kuwakutanisha wadau wote wanaohusika na mgogoro wa pori hilo kwa ajili kujadili changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.

Akiwa kwenye Pori Tengefu la Loliondo na kwenye mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti alishuhudia makundi ya mifugo ikiwa ndani ya pori hilo na mingine ikizagaa maeneo ya mpakani na Hifadhi hiyo. Alielezwa na Viongozi wa Wilaya ya Ngorongoro kuwa, mifugo hiyo huingizwa kwa ajili ya malisho wakati wa usiku kwenye hifadhi ya Serengeti. 

Inaelezwa kuwa eneo la Pori Tengefu la Loliondo lina umuhimu wa pekee katika uhifadhi kwa sababu ni sehemu ya mazalia ya wanyamapori, mapito ya wanyamapori na vyanzo vya maji. Kutokana na sababu hizo, eneo hilo linapaswa kuendelea kuhifadhiwa ipasavyo, kwa kuwa linachangia kwa kiwango kikubwa kuimarisha mfumo wa ikolojia ya Hifadhi ya Serengeti.

Siku chache baada ya ziara hiyo ya kiutafiti, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alifanya ziara ya kikazi mkoani Arusha na kuwaagiza viongozi wa Serikali kukaa pamoja na wadau wanaohusika na migogoro ya ardhi katika Tarafa ya Loliondo na kuitafutia suluhu ya kudumu.

Baada ziara hiyo ya Waziri Mkuu, Naibu Waziri Makani aliendelea na ziara yake katika tarafa ya Loliondo ambayo aliikatisha kupisha ziara Waziri Mkuu. Mara hii ziara hiyo ikihusisha pia ufuatiliaji wa maagizo ya Waziri Mkuu aliyoyatoa kwenye ziara yake mkoani Arusha.

Aliwasili Loliondo kwa ajili ya kuweka mkakati wa kumaliza changamoto ya mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miaka 25 kati ya mwekezaji, wanavijiji, mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs), suala la mifugo, uharibifu wa mazingira na utata wa mpaka wa Hifadhi ya Serengeti na Loliondo.  

Tarehe 29 Desemba, 2016 alifanya mkutano na wadau wanaohusika moja kwa moja na mgogoro wa Loliondo, mkutano huo ulifanyika katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Tarafa ya Loliondo, Kupitia mkutano huo aliunda kamati maalum ya kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogoro huo.

Kamati hiyo inahusisha taasisi za serikali, asasi za kiraia, viongozi wa dini, wazee wa kimila (Leigwanan), viongozi wa vijiji, wajumbe wa kamati teule ya vijiji 15 ya mpango bora wa matumizi ya ardhi na uendelezaji wa uhifadhi na wawakilishi wa wanawake na vijana. Aliunda pia kamati ya kuandaa kanuni za kundesha vikao vya kamati hiyo.

Naibu Waziri huyo aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa kamati hiyo, na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Rashid Mfaume Taka akateuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti.  

“Kamati ya kanuni itumie muda wa wiki mbili hadi kufikia tarehe 17 Januari, 2017 iwe imeshakamilisha rasimu ya kanuni ili tarehe 18 Januari, 2017 tuzipitie, tuzijadili na kuzipitisha. Hatua itakayofuata ni mawasilisho ya taarifa mbalimbali kutoka kwa wadau pamoja na majadiliano”, alisema Makani.

Aliagiza pia taarifa mbalimbali za kamati zilizowahi kushuulikia mgogoro huo miaka ya nyuma na mapendekezo yake pamoja na taarifa mbalimbali za sheria za uhifadhi na vijiji kwa ajili ya kusaidia majadiliano hayo ziwasilishwe.

Kikao hicho kilikubaliana kazi hiyo ifanyike ndani ya miezi mitatu hadi kufikia tarehe 31 Machi, 2017 iwe imekamilika na muafaka upatikane kwa ajili ya kuishauri Serikali namna bora ya kumaliza mgogoro huo.

Wadau wote walikubaliana kushiriki vikao vya majadiliano huku wengine wakipongeza hatua iliyofikiwa na Serikali ya kutaka kumaliza mgogoro huo, hata hivyo Naibu Waziri Makani alitoa angalizo kwa wadau hao; "Kuna watu humu ndani na hata nje ambao hawataki tumalize migogoro Loliondo, nitoe rai kwao, waache chokochoko.

“Wafikishiwe salamu, tutawabaini, tutawakamata na kuwashitaki kwa kosa la kukwamisha jitihada za Serikali kuwaletea wananchi maendeleo yao, Wananchi muone umuhimu wa jitihada za Serikali kumaliza changamoto hii na kutuunga mkono”, alisema Makani.

Akizungumza katika mkutano huo, mchangiaji mmoja ambaye hakutambulisha jina lake alisema “Eneo hili Loliondo lenye kata saba na vijiji 15 lilikosekana dawati la pamoja, kwa mfumo huu tutaenda mbele, Taasisi nyingi zimekuwa zikipotosha umma kuhusiana na taarifa za Loliondo, tutashukuru kuona tunapata muafaka kupitia kamati hii iliyoundwa leo”

Changamoto ya Mgogoro wa Pori Tengefu la Loliondo ni mkwamo kwa maendeleo ya wananchi wa Loliondo na Taifa kwa ujumla, Kila mwananchi wa Loliondo ana nafasi kubwa  ya kuhakikisha mgogoro huu unafikia tamati kwa kushirikiana na Serikali na wadau wengine. Kila mmoja atimize wajibu wake mgogoro huu utakuwa historia na Loliondo itakua salama na kupiga hatua kimaendeleo.

HALMASHAURI YA MUFINDI YAPITISHA BAJETI YA BILIONI 60.7

$
0
0
Baraza maalum la madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, limejadili na kupitisha mapendekezo ya bajeti ya halmshauri hiyo, yenye jumla ya Sh. bilioni 60.7 kwa mwaka wa fedha wa 2017- 2018 huku kiasi kikubwa cha fedha hiyo ikikielekezwa kwenye miradi ya maendeleo.

Taarifa iliyotolewa na kitengo cha habari na mawasilino cha halmshauri ya Wilaya ya Mufindi, imebainisha sehemu kuu mbili za bajeti hiyo, ambapo jumla ya shilingi bilioni 4.9 zimetengwa kwa matumizi ya kawaida, wakati bilioni 14.5 zikielekezwa kwenye miradi ya maendeleo.

Taarifa hiyo imevitaja vyanzo vya mapato hayo, kuwa ni makusanyo ya halmashauri, fedha kutoka serikali kuu, wafadhili, taasisi za kijamii sanjari na nguvu za wananchi.

Akizungumza wakati wa kuhailisha kikao hicho, mwenyekiti wa halmshauri ya wilaya ya Mufindi Mh. Festo Mgina amemtaka Mkurugenzi mtendaji pamoja na wataalamu wake kuhakikisha wanaisimamia na kuitetea bajeti kwa hoja zenye mashiko katika ngazi ya Mkoa na Taifa ili malengo ya kuharakisha maendeleo ya halmashauri yafikiwe kwa wakati na akawahimiza watumishi na madiwani kushirikiana katika ukusanyaji wa mapato.

Kupitishwa kwa bajeti ya na baraza la madiwani, ni kwa mujibu wa sheria ya fedha yaserikali za mitaa namba 9 ya mwaka 2013. Aidha bajeti hiyo imezingatia mwangozo wa kitaifa wa bajeti wa 2017/ 2018, ilani ya uchaguzi ya chama tawala CCM ya 2015/2020, mpango wa maendeleo wa Taifa wa mwaka 2017/2018 huku mambo mengine yakiwa ni malengo ya maendeleo endelevu, dira ya Taifa ya maendeleo 2025 pamaja na maelekezo ya kisekta na mpango wa maendeleo ya miaka mitano.
 Mkurugenzi Mtendaji wa halmshauri Profesa Riziki Shemdoe akiwashukuru madiwani mara baada ya kuipitisha bajeti ya 2017/2018
 Mwenyekiti wa halmashauri Festo Mgina akizungumza kabla ya kuhailisha kikao cha baraza la bajeti. 
madiwani wakifuatilia mwenendo wa upitishaji bajeti kwenye makablasha.

SERIKALI YAWASHAURI WANAMICHEZO KUZINGATIA MKATABA WA KIMATAIFA WA UDHIBITI WA DAWA NA MBINU ZA KUONGEZA NGUVU MICHEZONI KWA MAENDELEO YA MICHEZO NCHINI.

$
0
0

Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Mohamed Kiganja akizungumza na wadau, walimu na viongozi wa vyama vya michezo nchini wakati wa ufunguzi wa mkutano wenye lengo la kutoa mafunzo kwao kuhusu madhara ya matumizi ya dawa na mbinu za kuongeza nguvu michezoni uliofanyika katika Ukumbi ulipo katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam leo Januari 13,2017.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge akisisitiza jambo kwa wadau, walimu na viongozi wa vyama vya michezo nchini wakati wa ufunguzi wa mkutano wenye lengo la kutoa mafunzo kwao kuhusu madhara ya matumizi ya dawa na mbinu za kuongeza nguvu michezoni uliofanyika katika Ukumbi ulipo katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo Januari 13,2017.

Baadhi ya wadau, walimu na viongozi wa vyama vya michezo nchini wakifuatilia watoa mada wakati wa mkutano wenye lengo la kutoa mafunzo kwao kuhusu madhara ya matumizi ya dawa na mbinu za kuongeza nguvu michezoni uliofanyika katika Ukumbi ulipo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam leo Januari 13,2017.Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM .

Na Raymond Mushumbusi WHUSM

Wanamichezo nchini wameshauriwa kuzingatia mkataba wa kimataifa wa dawa na mbinu za kuongeza nguvu michezoni ili kuwezesha kuiendeleza sekta ya michezo kwa kutoa washindi wanaostahili katika mashindano mbalimbali.

Ushauri huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye katika risala iliyosomwa kwa niaba yake na katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa(BMT) Bw. Mohamed Kiganja katika ufunguzi wa mkutano wa wadau,walimu na viongozi wa vyama vya michezo wenye lengo la kujadiliana kuhusu Mkataba wa kimataifa wa udhibiti wa dawa na mbinu za kuongeza nguvu michezoni.

Bw. Mohamed Kiganja ameongeza kuwa ili kufanikisha maendeleo ya michezo nchini yako mambo muhimu ya kuzingatia kudhibiti na kuzuia matumizi ya dawa na mbinu za kuongeza nguvu michezoni.

Ameyataja mambo hayo kuwa ni utoaji wa elimu kwa wanamichezo kuhusu madhara ya utumiaji wa dawa za kuongeza nguvu michezoni sanjari na utoaji wa adhabu kali kwa watakaobainika kutumia dawa au mbinu za kuongeza nguvu michezoni.

“Ushindi wowote unaopatikana baada ya mchezaji kutumia dawa ama mbinu nyingine yoyote chafu mbali ya kutokuwa haramu lakini pia inamyima ushindi yule mchezaji ambaye hatumii dawa na inapelekea kutokuwepo kwa ushindani wa kweli katika mashindano” alisistiza Bw. Kiganja.

Aidha Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Moshi Kimizi amesema kuwa lengo la mkutano huo ni kutoa mafunzo kwa viongozi wa michezo ambapo itasaidia kuipeleka elimu hiyo kwa wanamichezo walio chini ya vyama vyao.

Pia ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kuendelea kushirikiana na wadau ili kupata Sheria itakayoendana na mkataba huo wa kimataifa ili kuiendeleza sekta ya michezo kwa manufaa ya wanamichezo na taifa kwa ujumla.

“Niiombe Serikali kupitia Wizara yenye dhamana ya michezo kuendelea kushirikiana na wadau wa michezo na wanamichezo kudhibiti matumizi ya dawa za kuongeza nguvu michezoni ili kulinda heshima ya michezo na taifa kwa ujumla” Alisisitiza Dkt Kimizi.

Mkutano huo ulioandaliwa na Tume ya Taifa ya UNESCO ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Habari utamaduni Sanaa na Michezo wenye lengo la kutoa mafunzo ya siku moja kwa wadau, walimu na viongozi wa vyama vya michezo nchini kuhusu madhara ya matumizi ya dawa na mbinu za kuongeza nguvu michezoni umehusisha takriban washiriki 100 kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Mkutano wa Waziri Muhongo na Kamati ya Wachimbaji na Wanunuzi wa Jasi na Makaa ya Mawe Tanzania

$
0
0
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo hivi karibuni alikutana na wajumbe wa Kamati ya Wazalishaji na Wanunuzi wa Madini ya Jasi na Makaa ya Mawe Nchini katika Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam.

Masuala mbalimbali kuhusiana na biashara ya madini hayo kwa ujumla yalijadiliwa kwa lengo la kuleta tija kwa pande zote na Taifa kwa ujumla.

Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi waandamizi wa Wizara ambao wamo ndani ya Kamati husika akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Profesa James Mdoe, Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje na Makamishna Wasaidizi wa Madini kwenye Kanda zinazozalisha madini husika.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akizungumza kwenye mkutano na Kamati ya Wachimbaji na Wanunuzi wa Jasi na Makaa ya Mawe Tanzania. Wa kwanza kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Dangote, nchini Tanzania, Harpreet Duggal akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Devakumar Edwin.
Kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati husika, Profesa James Mdoe, Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje na Kamishna Msaidizi wa Madini, Kanda ya Kusini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani). 
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Wazalishaji (Wachimbaji) na Wanunuzi wa Madini ya Jasi na Makaa ya Mawe waliohudhuria mkutano huo. 
Baadhi ya wajumbe kutoka Kampuni ya Dangote wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani). Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Dangote, Devakumar Edwin, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Dangote, nchini Tanzania, Harpreet Duggal. 
Wawakilishi kutoka Kampuni inayochimba Makaa ya Mawe ya Tancoal waliohudhuria mkutano huo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu, Jim Shedd, Mkuu wa Masoko, Emmanuel Constantinides na Mkurugenzi Mtendaji, Mark McAndrew wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani).

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA VIWANDA VIWILI MKOANI SHINYANGA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akiwa amechuchumaa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali pamoja na wafanyakazi wa Kiwanda hicho cha Kutengeneza mifuko ya Sandarusi mkoani Shinyanga.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akikata utepe kuashiria kufungua rasmi Kiwanda cha kutengeneza vinywaji cha Jambo food product mara bada ya kukizindua mkoani Shinyanga.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akisikiliza maelezo kutoka kwa mmiliki wa kiwanda cha kutengeneza vinywaji cha Jambo food product  Salum Hamis Mbuzi mara bada ya kukizindua mkoani Shinyanga.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akimsikiliza mmiliki wa wa kiwanda hicho cha Fresho,  Fred Shoo kuhusu malighafi ya kutengenezea mifuko ya Sandarusi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akiangalia moja ya hatua ya utengenezaaji wa mifuko ya Sandarusi katika kiwanda hicho cha Fresho mkoani Shinyanga.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akiangalia moja ya hatua ya utengenezaaji wa mifuko ya Sandarusi katika kiwanda hicho cha Fresho mkoani Shinyanga.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akiangalia moja ya hatua ya utengenezaaji wa mifuko ya Sandarusi katika kiwanda hicho cha Fresho mkoani Shinyanga.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akiwa amechuchumaa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali pamoja na wafanyakazi wa Kiwanda hicho cha Kutengeneza mifuko ya Sandarusi mkoani Shinyanga.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akiwagawia vinywaji viongozi mbalimbali wa dini mara baada ya kuzindua kiwanda hicho mkoani Shinyanga.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akiwagawia vinywaji kikundi cha ngoma za asili cha mkoani Shinyanga mara baada ya kuzindua kiwanda hicho cha Vinywaji mkoani Shinyanga.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akiwasalimia kwa kuwapungia mkono wakazi wa Igunga mkaoni Tabora. PICHA NA IKULU


Rais MAGUFULI avionya Vyombo vya Habari Vinavyoandika Habari za Uchochezi

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 13 Januari, 2017 ameyaonya magazeti mawili yanayoandika habari za uchochezi na kupotosha wananchi kwa kuwa vinahatarisha amani ya nchini.

Rais Magufuli ametoa onyo hilo wakati akikagua na kufungua Kiwanda cha Jambo cha kuzalisha vinywaji baridi mkoani Shinyanga.
Rais Magufuli amesema Serikali haitayavumilia magazeti hayo mawili kwa kuandika habari za uchochezi ambazo zinaweza kuhatarisha amani ya nchi kama ilivyotokea katika nchini ya Rwanda na kupelekea mauaji ya kimbari nchini humo.

''Serikali ya kutumbua majipu haiwezi kuacha kutumbua magazeti yanayofanya mambo ya uchochezi hatuwezi kuiacha Tanzania ikawa dampo la eneo la kuweka maneno ya uchochezi chini ya utawala wangu hilo halitakuwepo kuna magazeti mawili tu kila ukisoma wao ni kuchochea tu ikizungumzwa habari hii wao wanageuza hii nasema na nataka wanisikie siku zao zimeshafika kama wanasikia wasikie wasiposikia  wasisikie lakini magazeti mengine na vyombo vyote vingine vinatoa uchambuzi mzuri sana''.

Rais Magufuli amesema Serikali yake haiwezi kuvumilia kuona amani ya nchi inahatarishwa na magazeti mawili kwani amani ndio chimbuko la maendeleo ya taifa lolote duniani.

Amesema bila kuwepo kwa amani hakuna mwekezaji atakayeweza kuja kuwekeza nchi, hata wawekezaji wa ndani watashindwa na hivyo kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.

Rais Magufuli amesema uwepo wa amani nchini ndio uliowezesha wawekezaji wa Kiwanda cha Fresho cha kutengenezea mifuko ya kubebea bidhaa za chakula nchini na kiwanda cha Jambo cha kuzalisha vinywaji baridi mkoani Shinyanga kujengwa mkoani hapo kwani bila amani visingeweza kujengwa.

Aidha ameitaka Benki ya Uwekezaji Nchini TIB na Taasisi nyingine za fedha kutoa mikopo kwa wawekezaji wanaotaka kuwekeza katika viwanda badala ya kuwakopesha wanasiasa ambao hutumia fedha wanazokopa kwa matumizi yasiyowanufaisha watanzania waliowengi.

Rais Magufuli ameupongeza uongozi wa mkoa wa Shinyanga kwa kuanza kutekeleza kwa vitendo azma ya Serikali ya kutaka Tanzania ya viwanda kwa kujenga viwanda vingi mkoani humo ikiwa ni pamoja na viwanda hivyo viwili alivyovizindua katika siku yake ya mwisho ya ziara mkoani Shinyanga.

Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano, Ikulu
Shinyanga

13 Januari 2017.

Wadau mbalimbali wapongeza Nishati na Madini kwa mfumo wa TREMIS

$
0
0

Na Greyson Mwase, Mwanza.
Wadau mbalimbali wa vifaa ya umeme jua kutoka katika mikoa ya Mwanza na Kagera wamepongeza Wizara ya Nishati na Madini kwa kuanzisha mfumo mpya wa uhifadhi data na utoaji taarifa kwa ajili ya nishati jadidifu ujulikanao kama Tanzania Renewable Energy Management Information System (TREMIS) wenye lengo la kutangaza fursa za uwekezaji katika nishati jadidifu nchini.

Mfumo wa TREMIS unaratibiwa na Mradi wa Kuwajengea Uwezo Wataalam wa Nishati na Tasnia ya Uziduaji (CADESE) kwa kushirikiana na Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini.

Wakitoa pongezi hizo katika kikao cha maandalizi ya mfumo huo kilichofanyika jijini Mwanza leo wamesema kuwa mfumo huo utawezesha shughuli za kampuni zao kufahamika ndani na nje ya nchi na kupata wabia wa kushirikiana nao katika bishara ya vifaa vya umeme jua.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, mmiliki wa kampuni ya kusambaza vifaa vya umeme jua ya Kaguta General Supplies yenye makazi yake Bukoba mkoani Kagera, Justin Kamlali amesema kuwa mfumo wa TREMIS utawawezesha kufahamika ndani na nje ya nchi.

Alisema kuwa biashara ya vifaa vya umeme jua imekuwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na kutofahamika na kupelekea wateja kutokuwa na imani na huduma zao.

“Baada ya ya mfumo huu kukamilika na kuunganishwa na tovuti ya Wizara, wadau na wawekezaji wengi kutoka ndani na nje ya nchi watakaotembelea tovuti ya wizara watapata fursa ya kuona taarifa za kampuni zetu na kuwa na imani ya kufanya kazi pamoja nasi tofauti na zamani”. Alisema .

Aliongeza kuwa kutokana na kampuni nyingi zinazojihusisha na biashara ya vifaa vya umeme jua kutokuwa na tovuti imekuwa ni vigumu kwa biashara zao kufahamika na watu wengi zaidi mbali na kutumia vyombo vya habari vilivyopo katika mikoa hiyo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji kutoka kampuni ya Rex Energy, Francis Kibhisa alisema kuwa mfumo wa TREMIS ni mkombozi kwa wamiliki wa kampuni ndogo zinazojihusisha na vifaa vya umeme jua na nishati jadidifu ambapo watapata soko ndani na nje ya nchi kutokana na kufahamika kwao

Alisisitiza kuwa mfumo huo utawezesha wawekezaji kutoka nje ya nchi kufahamu maeneo ya uwekezaji zaidi katika eneo la nishati jadidifu na kuja kuwekeza nchini.

Mradi wa CADESE unaofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Maendeleo (UNDP) ulianzishwa mwaka 2014 na unatekelezwa na Wizara ya Nishati na Madini kwa kushirikiana na wadau wengine kama Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Taasisi ya Uongozi na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF).
 Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Styden Rwebangila akielezea  faida za mfumo wa uhifadhi data na utoaji  taarifa kwa ajili ya nishati jadidifu (TREMIS)  mbele ya wadau  wa nishati jadidifu (hawapo pichani)
 Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Styden Rwebangila (mbele) akielezea  faida za mfumo wa uhifadhi data na utoaji  taarifa kwa ajili ya nishati jadidifu (TREMIS) mbele ya wadau  wa nishati jadidifu.
 Msimamizi wa Mradi wa Kuwajengea Uwezo  Wataalam wa Nishati na Tasnia ya Uziduaji  (CADESE), Paul Kiwele (kushoto) akifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa katika kikao hicho. Kulia ni Nasra Mohamed kutoka Wizara ya Nishati na Madini.
 Sehemu ya wajumbe na wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, wakifuatilia maelezo  yaliyokuwa  yanatolewa na Kamishna Msaidizi- Nishati Jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Styden Rwebangila (hayupo pichani)
 Mtaalam kutoka Kitengo cha Teknolojia ya  Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Justin Chankan akiwasilisha  rasimu ya mfumo wa TREMIS katika kikao hicho.
Wadau wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa katika kikao hicho

NEC YATOA UFAFANUZI WA MALALAMIKO YA UKIUKWAJI WA MAADILI YA UCHAGUZI YALIYOTOLEWA NA ACT-WAZALENDO

$
0
0
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Ramadhani Kailima akitoa Ufafanuzi kuhusu malalamiko ya ukiukwaji wa maadili ya Uchaguzi yaliyotolewa na Chama cha ACT WAZALENDO.

Na. Aron Msigwa –NEC.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekishauri Chama cha ACT – Wazalendo na Vyama vingine vyenye wagombea wa Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Dimani na Udiwani katika Kata Ishirini (20) za Tanzania Bara ,kuwasilisha malalamiko ya ukiukwaji wa Maadili ya Uchaguzi kwenye Kamati za Maadili zilizo katika maeneo yao.

Akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Bw. Kailima Ramadhan amesema NEC imepata taarifa kupitia Vyombo mbalimbali juu ya malalamiko ya Chama Cha ACT-Wazalendo kuvilalamikia Vyombo vya Dola pamoja na Watendaji wa Umma kufanya vitendo vyenye muelekeo wa kukipendelea Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Bw. Kailima amesema taarifa ya Chama hicho iliyotolewa kwenye Vyombo vya Habari Januari, 12 2017, imeeleza kuwa Watendaji wa Halmashauri ya Geita waliwakusanya Wazee katika Kata ya Nkoma waje na Vitambulisho vyao vya kupigia Kura kwa lengo la kuwapatia huduma ya afya bure jambo linalolalamikiwa na ACT- Wazalendo kwa madai kwamba Watendaji hao wana lengo la kuwahadaa Wazee hao ili wakipigie Kura Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Aidha, amesema katika malalamiko yake Chama cha ACT Wazalendo kimeibua tuhuma za wananchi kupokwa kadi za kupigia Kura ili wasiweze kushiriki katika uchaguzi mdogo utakaofanyika Januari 22, 2017.

Mkurugenzi Kailima amesisitiza kuwa ni kosa chini ya kifungu cha 88 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na kifungu cha 100 cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 mtu kumiliki kadi ya kupigia kura isiyokuwa yake.

“Natoa wito kwa wananchi wote kwamba, ni kosa chini ya kifungu cha 88 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na kifungu cha 100 cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 mtu yeyote kumiliki kadi ya kupigia kura isiyokuwa yake” Amesema.

Amefafanua kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuzingatia sehemu ya 5.4 ya Maadili ya Uchaguzi inavikumbusha Vyama vya Siasa kuwa iwapo vitakuwa na malalamiko ya ukiukwaji wa Maadili ya Uchaguzi katika Uchaguzi Mdogo wa Udiwani viwasilishe malalamiko hayo kwenye Kamati ya Maadili ngazi ya Kata ndani ya saa 72 tangu kutokea kwa tukio linalolalamikiwa.

“ Sehemu ya 5.4 ya Maadili ya Uchaguzi yayosainiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Serikali na Vyama Vya Siasa inaeleza wazi muda wa kuwasilisha malalamiko kwa kuvitaka vyama au wahusika wenye malalamiko yoyote kuyawasilisha kwa maandishi kwenye Kamati ya Maadili ya Uchaguzi ya ngazi husika ndani ya saa 72 tangu kutokea kwa tukio” Amesisitiza Kailima.

Amesisitiza kuwa iwapo Chama cha Siasa au Mgombea hataridhika na maamuzi ya Kamati ya Maadili ngazi ya Kata, kwa kuzingatia sehemu ya 5.7 (a) ya Maadili ya Uchaguzi anatakiwa awasilishe rufaa yake kwa Msimamzi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo ndani ya saa 24 tangu maamuzi ya Kamati ya Maadili ngazi ya kata kutolewa.

Aidha, Bw. Kailima amebainisha kuwa kama Chama cha Siasa hakikuridhika na maamuzi ya Kamati ya Maadili ngazi ya Jimbo, bado kwa kuzingatia sehemu ya 5.7 (b) na (c) kinayo fursa ya kuwasilisha Rufaa yake katika Kamati ya Maadili ngazi ya Taifa au ngazi ya Rufaa ambayo ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

“ Tunavishauri Vyama vya Siasa na Wagombea kuzingatia matakwa ya Maadili ya Uchaguzi katika kuwasilisha malalamiko yao ya ukiukwaji wa maadili ya Uchaguzi, kwa mujibu wa sehemu ya 5.7(e) ya Maadili ya Uchaguzi, pale ambapo Chama cha Siasa au Mgombea hakuridhika na maamuzi ya Kamati ya Rufaa atakuwa na fursa ya kuwasilisha malamiko yake Mahakamani baada ya Uchaguzi kwa mujibu wa Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292”.

Amesisitiza kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaendelea kuwasihi viongozi wa Vyama vya Siasa na Wadau wengine wa Uchaguzi kuendelea na Kampeni za kistaarabu na kuzingatia Sheria, Kanuni na Maadili ya Uchaguzi na kwamba inaendelea kufuatilia kwa karibu kila hatua ya Uchaguzi na hasa Kampeni huku akisisitiza kuwa haitasita kuchukua hatua kwa mtu yeyote atakayekiuka Sheria za Uchaguzi.

DKT SHEIN AHUDHURIA TAARAB RASMI YA KUSHEHEREKEA MIAKA 53 YA MAPINDUZI

$
0
0
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana  na  Mshauri wa Rais masuala ya Utamaduni Mhe, Chimbeni Kheir Chimbeni jana alipowasili katika viwanja vya Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi alipohudhuria katika Taarab rasmi ya kusherehekea Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Mhe, Rashid Ali Juma (kushoto) Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi(kulia) na Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kasim Majaliwa Majaliwa (wa pili kulia) pamoja na Viongozi wengine wakiwa katika  Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi  katika Taarab rasmi ya kusherehekea Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyofanyika jana.
 Wake wa Viongozi wakuu wa Nchi wakiwa katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi  katika Taarab rasmi ya kusherehekea Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyofanyika jana iliyopigwa na Kikundi cha Taifa.
 Baadhi ya Viongozi na Waalikwa mbali mbali wakiwa katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi  katika Taarab rasmi ya kusherehekea Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyofanyika jana iliyopigwa na Kikundi cha Taifa.
 Kikundi cha Taifa cha Muziki wa Taarab kikitumbuiza kwa Wimbo unaosema "Khofu yako Iondoke"ilyoimbwa na Profesa Moahmed Ilyas katika sherehe za Taarab rasmi ya kusherehekea Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyofanyika jana, mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (Picha na Ikulu).

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA OFISI YA MAKAMU WA RAIS

Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images