Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA RASMI BARABARA YA BARIADI-LAMADI KM 71.8 BARIADI MKOANI SIMIYU

0
0
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe  na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka pamoja na Waziri wa Ujenzi Profesa Makame Mbarawa kuashiria ufunguzi wa barabara ya Barabara ya Bariadi-Lamadi yenye kilometa 71.8.
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiweka jiwe la ufunguzi wa barabara ya Bariadi-Lamadi yenye kilometa 71.8 wengine katika picha ni  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Luhaga Mpina, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, Mwenyekiti wa CCM Simiyu Titus Kamani na Mbunge wa Bariadi Andrew Chenge.
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Bariadi kabla ya kufungua rasmi barabara ya Bariadi-Lamadi, katika mkoa wa Simiyu.
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi wa Bariadi mara baada ya kumaliza kufungua barabara ya Bariadi-Lamadi yenye urefu wa kilometa 71.8.

 PICHA NA IKULU

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO ALHAMIS JANUARI 12, 2017

0
0


COSATO CHUMI ATATUA TATIZO LA MASHUKA KATIKA ZAHANATI,VITUO VYA AFYA NA HOSPITALI ZA JIMBO LA MAFINGA MJINI

0
0
Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akikabidhi mashuka kwenye moja ya Zahanati ilikuwa na upungufu wa mashuka katika kata ya Isalavanu wakati wa ziara yake ya kukagua na kugundua changamoto za zahanati za jimbo la mafinga mjini
 Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi kushoto akiwa na katibu wake pamoja na mfanyakazi wa zahanati matanana wakati wa ziara yake
 Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi akiwasalimia wananchi wa kata ya Isalavanuwakati wa ziara yake
Mbunge wa mafinga mjini akitandika moja ya shuka kati ya mashuka aliyoyagawa katika zahanati mbalimbali katika jimbo lake ,Mashuka hayo yametolewa na mfuko wa bima ya afya NHIF
Na fredy mgunda,Iringa

Mbunge wa jimbo la mafinga mjini Cosato Chumi ametoa jumla ya mashuka mia moja (100) kwenye zahanati,vituo vya afya na hospitali ya mafinga kwa lengo la kuboresha huduma za kiafya kwa wananchi wanaopata huduma katika maeneo hayo.

Akizungumza na blog hii mbunge huyo alisema kuwa aliomba mashuka kutoka mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF)kwa lengo la kuboresha huduma za kiafya katika jimbo la mafinga mjini.

“Zahanati na vituo vya afya vingi vinachangamoto nyingi lakini moja wapo ni kukosekana kwa mashuka ya kutosha kwenye maeneo mbalimbali ya kiafya hivyo nilichukua jukumu la kwenda mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF)kuomba  msaada wa mashuka na namshukuru mungu wamenisaidia na kunipa mashuka haya yote”. Alisema Chumi

Aidha Chumi aliwataka watendaji wa sekta ya afya katika jimbo la mafinga kuwahudumia wagonjwa kwa weledi wao ili kuifanya kada hiyo kuondokana na changamoto ambazo zimekuwa zikiwakumba mara kwa mara kutoka kwa wananchi.

“Nimeleta mashuka haya naomba mtumie na kuyatunza ili yaweze kudumu kwa muda mrefu kwa kuwa ni mashuka yenye ubora wa hali ya juu kama mnavyoyaona lakini boresheni huduma kwa kutoa huduma nzuri kwa wananchi hapo ndio wananchi watafurahia serikali yao”.Alisema Chumi

Chumi aliwashukuru mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF)kwa kuwapa mashuka hayo ambayo yamefanikiwa kutatua changamoto ya ukosefu wa mashuka katika jimbo la mafinga na amewaomba wazidi kuwasaidia wananchi wa jimbo hilo.

Kwa upande wao viongozi wa zahanati hizo walimshukuru mbunge wa jimbo hilo Cosato Chumi kwa kujituma na kutafuta njia za kutatua changamoto kwenye zahati zote za jimbo la Mafinga mjini tofauti na ilivyokuwa hapo awali kwa viongozi wengine.

“Unaona toka ameingia madarakani amekuwa akiwaleta viongozi mbalimbali wa serikali ili kutafuta njia za kutatua changamoto za huduma za afya,alimleta naibu waziri wa wizara ya afya na maendeleo ya jamii Hamis Kigwangala na wengine wengi kwenye sekta nyingine”. Walisema viongozi hao

Baadhi ya madiwani waliendelea kujivunia juhudi za mbunge wao kwa kazi kubwa anayoifanya kuwaletea maendeleo katika jimbo la Mafinga Mjini ambapo hapo awali ilikuwa vigumu kushudia  mbunge akijituma kama anavyofanya Cosato Chumi

Naye mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Mafinga Charle Makoga amesema kuwa changamoto ya huduma ya afya katika vijiji vya jimbo la Mafinga ni mbaya na inahitaji juhudi binafsi kuwasaidia wananchi na kuongeza kuwa tatizo la umeme ni kubwa katika vijiji ambavyo havipokupata umeme wa REA awamu ya kwanza na pili na ndio sababu inayosababisha huduma za kiafya kudorola katika baadhi ya vijiji.

Toeni huduma bora kwa Wanachama wetu- Kaimu Mkurugenzi Mkuu NHIF

0
0
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw. Bernard Konga akimjulia hali mwanachama wa Mfuko aliyelazwa hospitalini hapo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bw. Bernard Konga akiongozana na baadhi ya wakurugenzi wa Mfuko na uongozi wa Hospitali ya Kairuki walipotembelea maeneo mbalimbali ya hospitalini hapo kuangalia huduma zinazotolewa kwa wanachama wa Mfuko.
Bw. Konga akiwasikiliza wanachama wa Mfuko waliokuwa wakipata huduma za matibabu hospitalini hapo.Ziara ikiendelea katika maeneo ya Hospitali ya Kairuki
Ziara ikiendelea katika maeneo ya Hospitali ya KairukiAkiendelea kupata maelezo ya huduma hospitalini hapo
Bw. Konga akipata maelezo ya namna wagonjwa wanavyopokelewa
Wakipata maelezo kutoka katika chumba cha kuchakata madai ya huduma zilizotolewa kwa wanachamaMeneja wa Idara ya Ukjaguzi wa Kairuki akitoa maelezo ya huduma mbele ya wanachama na uongozi wa NHIF.

…………………………………………………………………………

Na Grace Michael

KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Bernard Konga amezitaka Hospitali zote nchini zinazohudumia wanachama wake kuhakikisha zinatoa huduma bora na zinazostahili kwa wanachama ikizingatiwa ukweli kwamba wamekwishazilipia huduma hizo kabla ya kuugua.

Aidha amewahakikishia wanachama wa Mfuko kwamba, Mfuko umejipanga kuwahudumia na kutatua kero wanazokabiliana nazo wakati wa kupata huduma ili wajivunie huduma walizolipia.

Bw. Konga amesema hayo wakati alipofanya ziara ya kujionea namna wanachama wa Mfuko wanavyohudumiwa katika Hospitali ya Kairuki mjini Dar es Salaam ambapo mbali na kuona huduma pia alipata fursa ya kuzungumza na wanachama waliofika hospitalini hapo kupata huduma.

Akizungumza na wanachama katika Hospitali ya Kairuki, Bw. Konga alisema kuwa ameamua kuanza ziara ya kutembelea hospitali zote ili kukutana na wanachama, kusikiliza kero zao pamoja na kuzungumza na watoa huduma kwa lengo la kutatua matatizo yaliyopo na kujenga uhusiano bora.

“Nimeamua kuanza rasmi ziara hizi za kikazi kuwaona moja kwa moja wanachama wanahudumiwa ili nizungumze nao na kupata maoni kutoka kwao…wanachama kwangu ndio kipaumbele cha kwanza kwa kuwa ndio wametupa dhamana ya kuwahudumia na kukaa na fedha zao hivyo binafsi sitakubali kuona mwanachama akipata huduma hafifu”. Alisema Bw. Konga.

Alisema kuwa kitendo cha kutoka na kusikiliza wanachama kitasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha huduma lakini pia kukutana uso kwa uso na wananchi ambao Mfuko unawahudumia.

Wakizungumza mbele ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyo baadhi ya wanachama waliokuwa wakipata huduma hospitalini hapo, kwanza wameupongeza Mfuko kwa hatua hiyo ya kuamua kutoka nje kwa lengo la kukagua huduma lakini pia kwa maboresho mbalimbali ambayo yamefanywa na Mfuko.

“Hii kazi ambayo umeianza Mkurugenzi Mkuu ni nzuri sana na tunaomba pia hata vituo vya chini kwa maana ya Zahanati navyo vitembelewe ili kuwekewa utaratibu mzuri zaidi…matatizo bado yapo lakini kwa kiasi kikubwa mmejitahidi sana kuyatatua,” walisema wanachama hao.

Kwa upande wa Mwanachama wa Mfuko ambaye anahudumiwa na Mfuko chini ya Fao la Wastaafu Injinia Emmanuel Olekambainei ambaye alifika hospitalini hapo kwa ajili ya kupata huduma za macho, naye aliupongeza Mfuko na kumtaka Kaimu Mkurugenzi Mkuu kuangalia zaidi huduma ambazo haziko katika kitita cha mafao.

Aidha Injinia Olekambainei alisema kuwa huduma za afya hususan zinazotolewa na Mfuko zimeboreshwa na hasa katika kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya tano. “Nawapongeza kwa kweli maana kuna mabadiliko makubwa na inatokana na kasi ya Serikali yetu hivyo hongereni sana maana mimi mwenyewe napata huduma hapa kwa mwamvuli wa ustaafu chini ya NHIF,” amesema Bw. Olekambaini.

Akizungumza na Uongozi wa Hospitali ya Kairuki,Bw. Konga alisema kuwa ni muda muafaka kwa Mfuko kushirikiana kwa karibu na watoa huduma kwa lengo la kutoa huduma bora kwa wanachama wa Mfuko.

Kwa upande wa Uongozi wa Hospitali ya Kairuki ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu Dr. Asser Mchomvu, alisema kuwa hawana matatizo na uhusiano kati yao na Mfuko kwa kuwa wanatambua mchango katika kuboresha huduma zao.

“Tuwe wazi kuwa bila NHIF hatuwezi kujiendesha hata siku moja na wagonjwa tunaowahudumia hapa zaidi ya asilimia 90 ni wanachama wa NHIF hivyo tunao wajibu wa kuhakikisha kwamba Mfuko hauyumbi kwa namna yoyote vile vile kwetu wanachama wa NHIF ndio wateja wetu wakubwa hivyo tunawathamini na kuwaheshimu sana,” alisema.

Alisema kuwa changamoto za kiutendaji kati yao na Mfuko zikiwemo za bei za huduma, mifumo na ulipaji wa madai wataendelea kushirikiana kwa pamoja ili kuhakikisha haziwakwamishi kutoa huduma kwa wanachama.

Akihitimisha ziara hiyo Bw. Konga alitoa wito kwa wanachama wote kuhakikisha wanatoa taarifa wakati wowote wanapokutana na changamoto wakati wa kupata huduma za matibabu.

LEO NI SIKU YA KUZALIWA KWA MDAU MUGANYIZI BISHEKO

0
0
Leo Januari 12, 2017 ni siku ya kuzaliwa kwa Ofisa Masoko Mwandamizi wa Bank of Africa Tanzania, Muganyizi Bisheko... Wote kwa pamoja tunapenda kukutakia heri na fanaka. Mwenyezi Mungu akujalie maisha marefu.

Mfumo wa Uhifadhi Data, Nishati Jadidifu kuanzishwa

0
0
Wizara ya Nishati na Madini kupitia Mradi wa Kuwajengea Uwezo  Wataalam wa Nishati na Tasnia ya Uziduaji  (CADESE: Capacity  Development  in the Energy Sector  and Extractive Industries), inatarajia kuanzisha mfumo wa uhifadhi data  kwa ajili ya nishati  jadidifu  ujulikanao kama  Tanzania  Renewable Energy Management  Information System (TREMIS)  utakaowezesha wawekezaji ndani na nje ya nchi  kubaini fursa za uwekezaji zilizopo katika  sekta ya nishati jadidifu.

Hayo yameelezwa na  Msimamizi wa Mradi wa Kuwajengea Uwezo  Wataalam wa Nishati na Tasnia ya Uziduaji  (CADESE), Paul Kiwele katika ziara ya maandalizi ya mfumo huo jana, Kahama mkoani Shinyanga.
 Mtaalam kutoka Sehemu ya Nishati Jadidifu- Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Stephan Kashushura (kushoto) akizungumza na mtaalam  kutoka kampuni ya vifaa vya umeme jua ya Mobisol, Devis Mtete (kulia) mjini Kahama mkoani Shinyanga tarehe 11 Januari, 2017
 Mtaalam kutoka Sehemu ya Nishati Jadidifu- Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Stephan Kashushura (kushoto) akizungumza na mtaalam  kutoka kampuni ya vifaa vya umeme jua ya Mobisol, Devis Mtete (kulia) mjini Kahama mkoani Shinyanga tarehe 11 Januari, 2017
Mtaalam kutoka kampuni ya vifaa vya umeme jua ya Zola, Omary Raymond (katikati) akielezea shughuli za kampuni yake kwa Mtaalam kutoka Sehemu ya Nishati Jadidifu- Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Stephan Kashushura (kulia). Kushoto ni Msimamizi wa Mradi wa Kuwajengea Uwezo  Wataalam wa Nishati na Tasnia ya Uziduaji  (CADESE) chini ya  Wizara ya Nishati na Madini, Paul Kiwele. 

Walimu Karatu kurejeshewe Fedha za Vitambulisho vya Kazi – RC Gambo

0
0

 Na Nteghenjwa Hoseah, Karatu 

MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Theresia Mahongo kuhakikisha fedha za walimu wa shule za sekondari na msingi zilizokatwa na halmashauri ya wilaya hiyo kwaajili ya vitambulisho vya kazi zinarudishwa. 

 Mhe. Gambo alitoa agizo hilo jana wilayani Karatu wakati alipokuwa akizungumza na walimu hao kwenye ukumbi wa shule ya sekondari Karatu Boys ili kujua changamoto wanazokutana nazo na jinsi ya kuzitatua ikiwemo madeni ya likizo, upandaji wa madaraja. 

 Alihoji ni kwanini walimu hao wakatwe Sh. 6000 kwa ajili ya kutengenezewa vitambulisho vya kazi wakati ni haki yao kama watumishi na waajiriwa wa halmashauri hiyo na ni haki yao kupata vitambulisho vya kazi bure; Mwajiri anao wajibu wa kumtengenezea kila mtumishi Kitambulisho cha kazi.  Alimwagiza DC Mahongo kuhakikisha anafuatilia na kumchukulia hatua watumishi wa halmashauri hiyo waliowakata walimu hao wa msingi na sekondari kiasi hicho cha fedha kwa ajili kuwachukulia hatua. 
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (aliyesimama) akifungua Kikao cha walimu alichokiitisha ili kuskiliza changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi wakati wa ziara yake Wilayani Karatu.
 Walimu wa shule za msingi na Sekondari wanaofanya kazi katika Halmashauri ya Karatu wakifuatilia kikao kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha wakati wa ziara ya kikazi.
1.     Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo akiongea na walimu wa Shule za Msingi na Sekondari katika Wilaya ya Karatu. 

NICHAGUENI NITAWALETEA MAENDELEO - MGOMBEA UDIWANI WA CCM KATA YA KIJICHI

0
0

Na 
Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

MGOMBEA wa Udiwani wa Kata ya Kijichi kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Tausi Milanzi amesema kuwa wananchi wamchague ili aweze kufanya kazi ya maendeleo ya Kijichi.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa Kampeni, Tausi amesema  yuko tayari kuwatumikia wananchi na sio jambo lingine hivyo anahitaji kura ndio itakayomuwezesha  kuwapa maendeleo.

Amesema vijana ndio wenye maamuzi hivyo watumie fursa ya kupiga kura ili aweze kushirikiana na vijana hao katika maendeleo.Tausi amesema kuwa yeye ni mwanamke mwenye uchungu wa maendeleo hivyo anaomba kura ndio aweze kutimiza malengo hayo.

Naye  Mbunge wa Mkuranga,na Katibu  Msaidizi  wa Kamati ya Wabunge wa  Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Ulega amesema wananchi wa kijichi wamchague Tausi kwa ajili ya maendeleo.
 Mgombea  wa Udiwani wa Kata ya Kijichi kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Tausi Milanzi akizungumza na wananchi wa kitongoji cha Sayari wakati wa kuomba kura leo.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
 Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam,Afidu Luambano akizungumza na wakazi  wa Kijichi wakati mkutano wa hadhara  wa  kuomba kura ya Mgombea wa Udiwani wa Kata ya Kijichi kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Tausi Milanzi leo katika mkutano wa hadhara wa kuomba kura.
 Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza wakati wa akimnadi Mgombea wa Udiwani wa Kata ya Kijichi kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Tausi Milanzi leo katika mkutano wa hadhara wa kuomba kura.
 Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega akiwa ,amemshika mkono Mgombea wa Udiwani wa Kata ya Kijichi kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Tausi Milanzi leo katika mkutano wa hadhara wa kuomba kura.

 Mbunge wa Mbagala, Issa Mangungu akizungumza na wakazi  wa Kijichi wakati mkutano wa hadhara  wa  kuomba kura ya Mgombea wa Udiwani wa Kata ya Kijichi kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Tausi Milanzi leo katika mkutano wa hadhara wa kuomba kura.

MISS UNIVERSE TANZANIA 2016 AONDOKA NCHINI KUSHIRIKI MASHINDANO YA MISS UNIVERSE NCHINI PHILIPINES

0
0
Mrembo wa Miss Universe Tanzania 2017 Jihan Dimachk ameondoka jana  alfajiri na ndege ya Oman Air kuelekea Manilla nchini Philipines kwa ajili ya kushiriki Mashindano ya Miss Universe. 

Jihan Dimachk aliyetwaa taji la Miss Universe Tanzania mapema mwezi Novemba mwaka jana anaenda kuiwakilisha Tanzania akiungana na wenzake kutoka nchi mbalimbali Ulimwenguni kuwania taji hilo. 

 Jihan Dimachk ameondoka akiwa amejiandaa vyema ikiwemo kisaikolojia, kimazoezi na kimavazi akishirikiana na wataalam mbalimbali kutoka hapa nchini. 

 Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communications  ambaye pia ndio Mkurugenzi na Muandaaji mkuu wa Kitaifa wa mashindano haya Maria Sarungi Tsehai amewashukuru wadau mbalimbali kwa kujitoa na kushiriki katika kuhakikisha mrembo wetu anatayarishwa vyema. 
 Mrembo wa Miss Universe akikabidhiwa bendera ya Taifa na Bi.Joyce Hagu akimwakilisha mkurugenzi wa kitengo cha sanaa.
 
 Miss Univere Tanzania Jihan Dimachk akiwa na Miss Universe Kenya Marry Esther Were uwanja wa ndege wa JK Nyerere wakati wakisubiri ndege kwa ajili ya kuanza safari.(katikati yao ni matron/mlezi wa Miss Universe Tanzania Happy Kimbe akiwatakia baraka za mwisho na ushindi mwema.)
Washiriki wa shindano la Miss Universe Tanzania wakimtakia kila la kheri kinara wao katika mwendelezo wa mshindano haya.

MAJ.GEN.GAUDENCE; UJANGILI KWA SASA UMEPUNGUA NCHINI

0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi akizungumza katika mkutano huo.luv1
Picha ya pamoja
……………………………………………………………………………………….
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii amesema kwa kiasi kikubwa cha  ujangili umepungua nchini na kwamba meno ya tembo yanayokamatwa kwa sasa ni masalia ya zamani.
Aliongeza kuwa kinachohitajika kwa sasa ni kuendelea kufuatilia kuwa nani anaua,nani anatoa porini na nani mnunuzi ili wote wakamatwe na hatua kali zichukuliwe dhidi yao ili iwe fundisho.
Katika hatua nyingine Katibu Mkuu amepongeza hatua ya nchi ya China kuua soko la manunuzi ya meno ya tembo ,jambo ambalo alisema litafanikisha zaidi ujangili kupungua.
Alisema si tu china bali kuna nchi nyingine ambazo zinajihusisha na manunuzi hayo zinatakiwa kuunga mkono usitishwaji huo ili uuaji wa wanyama hai uishe kabisa.
Aidha, Milanzi amesema serikali imeweka mpango mkakati mpya wa kuhakikisha ujangili unaendelea kudhibitiwa kwa hali ya juu.
Pia amewataka watumishi wa Mamlaka ya Usimamamizi wa Wanyamapori (TAWA) wametakiwa kutojifungia maofisini na badala yake kuingia kufanya kazi katika maeneo yao kazi yaani ‘field’ hapo ndipo mafanikio yatatokea.
Hayo aliyasema jana wakati akizungumza kwenye mkutano ulioandaliwa na Mamlaka ya Usimamizi wa wa Wanyamapori Nchini (TAWA) walipokutana na  wahifadhi wakuu kwa lengo la kuweka mkakati wa udhibiti wa ujangili.
Alisema kila mfanyakazi na kila mtu aliyepo katika mamlaka hiyo anatakiwa kujitafakari yeye mwenyewe kwa utendaji wake.
Alisema hakuna sababu ya kushindwa kukabiliana na ujangili na huku akiwataka kusiwe na sababu kukosa hiki wala kile kinachohitajika ni mambo ya maendeleo pekee.
Hata hivyo alisema kuna watumishi ambao wanajihusisha na ujangili lakini hafikirii kama wote ni watu wabaya bali wenye kasoro hiyo wapo hivyo watumishi wema wasikubali wakawavurugwa na wengine.
Naye Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali (DPP) Biswalo Mganga amesema watu ya 200 wamekamatwa katika kipindi cha mwaka jana kutokana makosa ya kukutwa na nyara mbali mbali za Serikali.
Pia zaidi ya milioni 800-900 zilipatikana kutokana na faini za watu wanaokutwa na nyara za serikali sambamba na walioshindwa kulipa faini kufungwa miaka 20-25.
Alisema kati ya watuhumiwa hao endapo wote wangefanikiwa kutoa faini na kutofungwa kiasi cha shilingi bil 164 zingekusanywa na kwamba hiyo inaonesha ni jinsi gani udhibiti unaendelea kwa kasi .
Biswalo alisema kutokana na takwimu hizo kwa mwaka huu hawatategemea kutokea tena kwani idadi hiyo ilikuwa kubwa na inatisha kwa taifa.Alisema kila mmoja anajukumu la kulinda maliasili za serikali ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za wahalifu hao ili ziweze kushughulikiwa haraka na kufunguliwa mashitaka.
Kaimu Mkurugenzi wa TAWA,  Martini Loibooki alisema vita ya ujangili ni kubwa hivyo inahitaji kuongeza nguvu ili kuwazuia waharifu wenye ushawishi.Alisema wanafahamu kuna watumishi wengine wanahusika katika ujangili hivyo katika mwaka huu wanatakiwa kuacha mara moja.
‘’Hadi sasa kuna watumishi wanne ambao wanachunguzwa kujihusisha na hilo na endapo wakibainika hatua mbalimbali za kisheria zitachukuliwa,’’alisema.Naibu wa Mkuu wa Jeshi la Polisi Abdulrahman Kaniki alisema ni jukumu kwa jeshi la Polisi kulinda rasilimali za taifa ili vizazi vijavyo viweze kuona kuliko kuadithiwa.
Alisema ni muhimu kuona wanajipangaje hasa katika kuwa na mahusiano mazuri kwa sekta mtambuka katika kuhakikisha ujangili unakwisha.lisema ni vyema kuwakamata watuhumiwa kuwepo na ushahidi wenye taarifa sahihi ,ili hatua dhidi yao ziweze kuchukuliwa bilakuonewa.
Naye mhifadhi mkuu wa Pori la Akiba la Selous Henock Msocha alisema mafunzo haya ni sahihi kwa kuwa wanakumbushana mambo mengi na kuwafanya wajirekebishe kwa kile walichokosea awali.
Mwenyekiti wa bodi ya TAWA meja Mstaafu Hamis Semfuko,alisema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na maeneo ya kuwaweka watuhumiwa.Pia alisema rushwa ni malalamiko ya wengi na miongoni mwa watumishi wanajihusisha na uhalifu.
Alisema ufanisi unahitajika na kujibidiisha ili kuongeza kasi ya utendaji kazi kwa TAWA.

WAFANYAKAZI BENKI YA POSTA TANZANIA TAWI LA MBEYA WASHEREKEA SHEREHE ZA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA KUSHIRIKI ZOEZI LA USAFI KITUO CHA AFYA KIWANJA MPAKA

0
0
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Posta Tanzania Tawi la Mbeya wakishiriki zoezi la usafi katika kituo cha Afya kiwanja Mpaka jijini Mbeya ikiwa ni sehemu ya kusherekea miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar .

Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Posta Tanzania Tawi la Mbeya wakishiriki zoezi la usafi katika kituo cha Afya kiwanja Mpaka jijini Mbeya ikiwa ni sehemu ya kusherekea miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar ambapo pia wakabidhi vifaa vya usafi katika kituo hicho cha Afya .

Zoezi la usafi likiendelea

Erick Mwaigomole Mfanyakazi Benki ya Posta Tanzania Tawi la Mbeya akishiriki kikamilifu shughuli za usafi katika kituo cha Afya Kiwanja Mpaka jijini Mbeya kama sehemu ya kusherekea Miaka 53 ya Mapinduzi Zanzibar.

Zoezi la Usafi likiendelea........




Meneja Msaidizi Benki ya Posta Tanzania Tawi la Mbeya  Joseph Nzilla akizungumza na waandishi wa habari kuhusu zoezi la usafi ambalo limehusisha wafanyakazi wote wa benki ya posta tawi la mbeya kama sehemu ya kusherekea miaka 53 ya Mapinduzi Zanzibar Leo January 12, 2017.
Picha baadhi wa wafanyakazi benki ya Posta Tanzania Tawi la Mbeya ambao wameshiriki zoezi la usafi katika kituo cha afya kiwanja mpaka jijini Mbeya ikiwa sehemu yao ya kusherekea miaka 53 ya Mapinduzi Zanzibar.
Meneja Msaidizi Benki ya Posta Tanzania tawi la Mbeya  Joseph Nzilla akimkabidhi vifaa vya usafi mganga mfawidhi kituo cha afya kiwanja Mpaka Stella Moses kama sehemu ya mchango wao ili kuendeleza zoezi la usafi katika kituo hicho.
Wafanyakazi wa Benki ya Posta Tanzania Tawi la Mbeya katika picha ya pamoja mara baada ya kushiriki zoezi la usafi katika kituo cha Afya kiwanja Mpaka jijini Mbeya ikiwa sehemu ya kusherekea sherehe za Miaka 53 ya  mapinduzi Zanzibar.

MVUA YAZUA BALAA SHINYANGA, NYUMBA ZAIDI YA 20 ZAEZULIWA NA UPEPO MKALI

0
0

Nyumba zaidi ya 20 zimeezuliwa na upepo mkali wakati mvua ikinyesha usiku huu wa Januari 11,2017 katika manispaa ya Shinyanga.(Habari na RUVUMATV)

Hadi sasa bado haijafahamika kama kuna vifo ingawa mamlaka husika haijatoa taarifa kuhusu tukio hilo, mvua hiyo iliambatana na upepo mkali pia imejeruhi watu kadhaa katika kata ya Kitangiri manispaa ya Shinyanga.

Diwani wa kata ya Ngokolo kupitia chama cha Demoklasia na Maendeleo(CHADEMA) Emmanuel Ntobi akipewa maelezo na mmoja wa wahanga ambaye amejeruhiwa na paa la nyumba.

Diwani wa kata ya Ngokolo kupitia chama cha Demoklasia na Maendeleo(CHADEMA) Emmanuel Ntobi amefika katika baadhi ya maeneo yaliyoathiriwa na kujionea uharibifu uliojitokeza kufuatia mvua hiyo

Nyumba zaidi ya 20 pia madarasa manne na ofisi ya walimu katika shule ya msingi Viwandani zimeezuliwa. Amewaomba wasamaria wema kufika katika eneo hilo ili kutoa msaada kwa wananchi waliothirika na mvua hiyo.

Nyumba zilizoharibiwa na mvua .

 

Diwani wa kata ya Ngokolo kupitia chama cha Demoklasia na Maendeleo(CHADEMA) Emmanuel Ntobi akipewa maelezo na mmoja wa wahanga ambaye amejeruhiwa na paa la nyumba.

WAZIRI MKUU AZINDUA SACCOS YA MELINNE

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kufungua SACCOS ya Melinne mjini Zanzibar ikiwa ni moja ya shamrashamra za sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar Januari 11, 2017.
Waziri Kassim Majaliwa , viongozi mbalimbali wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakimsikiliza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd wakati alipozungumza baada ya Waziri Mkuu kufungua SACCOS ya Melinne mjini Zanzibar Januari 11, 2017.
Baadhi ya wananchama wa SACCOS ya Melinne ya Zanzibar wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kufungua ukumbi wa SACCOS hiyo Januari 11, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Idd baada ya kufungua ukumbi wa SACCOS ya Melinne ya Zanzibar Januari 11, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mama Asha Seif Idd kabla ya kufungua ukumbi wa SACCOS ya Melinne mjini Zanzibar ikiwa ni moja ya shughuli za sherehe ya Mapinduzi ya Zanzibar Januari 11, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wanachama wa SACCOS ya Melinne ya Zanzibar baada ya kufungua ukumbi wao Januari 11, 2017. Kulia kwake ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd.

(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa Melinne saccos kuhakikisha wanakuwa wawazi na kutoa taarifa za hesabu za umoja huo kila wakati ili wanachama waweze kuwa na takwimu sahihi.

Alitoa agizo hilo jana jioni (Jumatano, Januari 11, 2017) wakati akizindua saccos hiyo yenye mtaji wa zaidi ya sh. bilioni moja kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Dk. John Magufuli ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinguzi Matukufu ya Zanzibar.

Waziri Mkuu alisema viongozi hao wanatakiwa kuwa wawazi kwa wanachama wenzao jambo ambalo litawajengea uaminifu hivyo kuwezesha umoja huo kudumu na kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Alisema vyama vingi vya ushirika nchini vimekufa kutokana na viongozi wake kutokuwa waaminifu hivyo Serikali hatokubali kuona suala hilo linatokea katika umoja huo kwani litakwamisha maendeleo.

Aidha, Waziri Mkuu aliwapongeza wananchi hao kwa kuanzisha saccos hiyo kwani wameweza kutimiza ndoto ya Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume ya kuondokana na umasikini, dhuluma na unyonge.

Waziri Mkuu alisema saccos hiyo itawawezesha baadhi ya wanachama kuanzisha miradi ya ujasiriamali na wengine kuongeza mitaji hivyo kukuza biashara zao na kuondokana na umasikini.

Awali, Waziri Mkuu alizindua ukumbi wa kisasa wa mikutano unaomilikiwa na saccos hiyo na kuwapongeza wananchi hao kwa kubuni miradi ya maendeleo itayowaongezea kipato na kuweza kujikwamua kiuchumi.

Hata hivyo aliwataka wanachama hao kuendeleza mshikamano wao na kuendelea kushirikiana na Serikali ambayo imejipanga kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kutoa mikopo ya ujasiriamali hasa kwa walio katika vikundi vya uzalishaji.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu aliwashauri wanachama wa umoja huo kufikiria uwezekano wa kuanzisha viwanda ili kukuza mitaji yao. Pia vitawezesha umoja kuongeza za fursa za ajira nchini.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMIS, JANUARI 12, 2017.
Share

KILELE CHA MIAKA 53 YA MAPINDUZI ZANZIBAR

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Dk.Ali Mohamed Shein akiwa katika Gari Maalum huku akiongozwa na Pikipiki za Polisi, akiwangia mkono wananchi waliohudhuria  katika Kilele cha Sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,Sherehe zilizofanyika leo huko Uwanja wa Amaan Mjini Unguja.
RINGA 1
Gwaride la Farasi likimsindikiza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Dk.Ali Mohamed Shein alipoingia katika akiwa Uwanja wa Amaan Mjini Unguja leo katika Kilele cha Sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Sherehe hizo zilihudhuriwa na Viongozi mbali mbali pamoja na Vyama vya Siasa. 
RINGA 2
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Dk.Ali Mohamed Shein akiwa katika Gari Maalum huku  akiwangia mkono wananchi waliohudhuria  katika Kilele cha Sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,Sherehe zilizofanyika leo huko Uwanja wa Amaan Mjini Unguja. 
RINGA 3
 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Lt.Co.Khamis Mohamed Adam  wakati akikagua Gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama katika Uwanja wa Amaan Mjini Unguja leo katika sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanziba. 
RINGA 4
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Lt.Co.Khamis Mohamed Adam  wakati akikagua Gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama katika Uwanja wa Amaan Mjini Unguja leo katika sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanziba. 
RINGA 5
 
 Baadhi ya Watendaji kutoka Idara mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi wakiwa katika sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanziba,zilizofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Mjini Unguja. 
RINGA 6
 
Baadhi ya Wanachama cha Mapinduzi CCM waliohudhuria katika  sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanziba,zilizofanyika leo katika Uwanja wa Amaan Mjini Unguja,wakifuatilia kwa makini taratibu za Sherehe hizo ambazo zilihudhuriwa pia na wanachama wa Vyama vyengine vya Siasa. 
RINGA 7
 
 Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe,Dkt.Amani Abeid Karume akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud (katikati) alipowasili katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja leo wakati wa Sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar(kulia) Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mji wa Unguja,Abrahman Khatib. 
RINGA 8
 
 Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamin Willium Mkapa na Mkewe Mama Anna Mkapa (katikati)  walipowasili katika Uwanja wa Amaan Studium Mjini Unguja leo wakati wa Sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar  (wa pili kulia) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud. 
RINGA 9

 Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Kassim Majaliwa  Majaliwa alipowasili katika Uwanja wa Amaan Studium katika Sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar zilizofanyika leo,[Picha na Ikulu.]12/01/2017.

Walimu Karatu kurejeshewe Fedha za Vitambulisho vya Kazi ‘Gambo’

0
0

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (aliyesimama) akifungua Kikao cha walimu(hawapo pichani) alichokiitisha ili kuskiliza changamoto zinazowakabili na kuzitaftia ufumbuzi wakati wa ziara yake Wilayani Karatu.AUKO 1
Walimu wa Msingi na Sekondari wanaofanya kazi katika Halmashauri ya Karatu wakifuatilia kikao kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha wakati wa ziara ya kikazi.
AUKO 2
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo akiongea na walimu wa Shule za Msingi na Sekondari katika Wilaya ya Karatu.
………..
Nteghenjwa Hoseah, Karatu
MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Theresia Mahongo kuhakikisha fedha za walimu wa shule za sekondari na msingi zilizokatwa na halmashauri ya wilaya hiyo kwaajili ya vitambulisho vya kazi zinarudishwa.
Mhe. Gambo alitoa agizo hilo jana wilayani Karatu wakati alipokuwa akizungumza na walimu hao kwenye ukumbi wa shule ya sekondari Karatu Boys
ili kujua changamoto wanazokutana nazo na jinsi ya kuzitatua ikiwemo madeni ya likizo, upandaji wa madaraja.
Alihoji ni kwanini walimu hao wakatwe Sh. 6000 kwaajili ya kutengenezewa vitambulisho vya kazi wakati ni haki yao kama watumishi na waajiriwa wa halmashauri hiyo na ni haki yao kupata vitambulisho vya kazi bure; Mwajiri anao wajibu wa kumtengenezea kila mtumishi Kitambulisho cha kazi.
Alimwagiza DC Mahongo kuhakikisha anafuatilia na kumchukulia hatua watumishi wa halmashauri hiyo waliowakata walimu hao wa msingi na sekondari kiasi hicho cha fedha kwa ajili kuwachukulia hatua.
“Eti vitambulisho vyenu mmetozwa hela kwa sababu gani wakati ni bure, sasa nasema aliyehusika na kuwatoza Sh, 6000 kwaajili ya vitambulisho vyenu vya kazi atachukuliwa hatua kwanini muwafanye walimu kama shamba la bibi hamuwaonei huruma jamani, wanadai malipo yao na hata vitambulisho vya kazi pia muwakate hela zao hii siikubali”
Pia Mhe. Gambo aliwaondoa hofu walimu hao kuwa serikali ya mkoa wa Arusha itahakikisha kuwa madeni yote yanayodaiwa na walimu hao yatashughulikiwa ili waweze kufundisha vyema wanafunzi hao
Awali walimu hao baadhi walisema wengine wanatembea umbali mrefu kwaajili ya kutoa elimu huku wanafunzi nao kwenye baadhi ya shule wakishindwa kuhudhuria masomo yao kwa wakati sababu njiani wanakutana na wanyamapori.
Pia Mwalimu Joakim Petro akisema awali alisimamishwa kazi kwa mizengwe na baadaye kurudishwa kazini na kuamriwa kupewa Sh, milioni 3. 5 kama madai ya usumbufu na mshahara yake lakini tangu mwaka juzi hajapewa fedha zake
Pia fedha za walimu za Sacco zaidi ya Sh, milioni 11.3 za walimu ambazo ni makato yao hawazioni na hata wakitaka kuzikopa wanaelezwa hazina sasa zimekwenda wapi.
Awali, Mkuu wa Wilaya hiyo, Mahongo alisema anafuatilia suala hilo ili kujua ni mtumishi gani wa halmashauri alichukua fedha hizo kwakushirikiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Waziri Morice ili kuchukua hatua kali za kinidhamu

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUENDELEA KUSIMAMIA RASILIMALI KWA MASLAHI YA WANANCHI WAKE.

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akiongea na wananchi wakati wa sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar ambapo alisema mbali za jitihada zilizofanywa na serikali hiyo katika kuinua maisha ya wazanzibar ameahidi kuendelea kusimamia rasilimali ili zitumike kwa maslahi ya wananchi wote.
PINDU 2
2-Makamo wa Pili wa Rais Zaznzibar Balozi Seif Ali Idd akiongea na wananchi wakati wa sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar ambapo alisema serikali ya mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuweka jitihada ili kuendelea kujenga uchumi za Zanzibar kwa maslahi ya wananchi.
PINDU 3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akiwasalimia wananchi walijitokeza katika sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.
PINDU 5
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akiimba wimbo wa Taifa katika sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.
PINDU 6
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akikagua gwaride katika sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.
PINDU 7
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akisalimiana na viongozi wastaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.
PINDU 8
Vikundi mbalimbali, Asasi za Kiraia,Vyama vya Siasa,Mikoa,Wizara na Taasisi za Serikali wakipita mbele Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein katika sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.
PINDU 13
Vikosi mablimbali vya Jeshi la Polisi vikipita mbele Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein katika sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.
PINDU 14
Vijana vya halaiki wakiwa katika umbo linaloonesha miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.
PINDU 16
Kikosi cha Kwata la KimyaKimya wakionesha onesho wakati wa sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.
PINDU 18
Komando wa Jeshi la Wananchi Tanzania akishuka katika kamba katika sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.
PINDU 19
Kikosi cha Makomandoo wa Jeshi la Wananchi Tanzania wakionesha onesho wa namna ya kuakibiana na vikwazo mbalimbali wawapo kazini katika sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.
PINDU 20
Askari wa Kikosi cha Mbwa, akionesha namna mbwa anavyoweza kuruka vikwazo mbalimbali katika kukabiliana na wahalifu katika sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.
………..
Na: Frank Shija – MAELEZO
ZANZIBAR imeadhimisha miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu huku ikiwa imepiga hatua mbalimbali za kimaendeleo na utoaji wa huduma bora za kijamii.
Hayo yamebainishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein wakati akihutubia wananchi katika sherehe za maadhimisho ya Mapinduzi leo katika uwanja wa Amani, Unguja, Zanzibar.
Dkt. Sein amesema kuwa siku ya Mapinduzi ni muhimu sana katika historia ya Zanzibar kwani ndiyo siku ambayo Wazanzibar walipokuwa huru katika nchi yao na kuweza kufanya shughuli mbalimbali za kujiletea maaendeleo.
“Tukiwa tunasherehekea miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ni vyema tukajivunia maendeleo yaliyopatikana na yanayoendelea kupatikana.”Alisema Dkt. Shein.
Akitaja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana tangu Mapinduzi Matukufu yatokee tarehe 12 Januari 1961, Dkt. Shein amesema kuwa mafanikio makubwa yamepatikana katika sekta za elimu kwa kuwa na ongezeko la shule kutoka shule 752 mwaka 2015 hadi kufikia 843 mwaka 2016.
Ongezeko hilo limeenda sambamba na ongezeko la udahili wa wananfunzi ambapo umeongezeka kutoka wanafunzi 384,000 hadi kufikia 424,000 mwaka 2016.
Katika sekta ya afya kumekuwa na mafanikio ya kuongezeka kwa vituo vya afya kwa asilimia 13.4 ambapo mwaka 2015 kulikuwa na Vituo vya Afya 134 hadi kufikia sasa jumla ya Vituo 152 vimepatikana.
Mafanikio mengine ni pamoja na upatikanaji wa ajira 2658 zilizotokana na miradi mbalimbali iliyozindulia katika kipindi hiki cha maadhimisho ya siku ya Mapinduzi, kukua kwa Sekta ya Utalii kwa ongezeko la watalii kwa asilimia 13 huku ikichangia pato la taifa kwa asilimia 27.
Huduma za kijamii zimezidi kuboreshwa huku upatikanaji wa maji safi na salama umeendelea kutatuliwa ambapo miradi ya maji imeekuwa ikitekelezwa ikiwemo kuchimba visima vipya 9 na kuvifanyia ukarabati visima vya zamani.
Kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd amesema kuwa Mapinduzi haya yamekuwa chachu ya kuleta maendeleo kwa kuwa yamewaweka Wazanzibar kuwa huru katika kutekeleza shughuli zao za kujiletea maendeleo.
Zanzibar imeadhimisha miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar huku ikiwa imepiga hatua kubwa za kimaendeleo ambapo katika shamra shamra za maadhimisho haya jumla ya miradi 32 ya maendeleo imezinduliwa huku mingine 16 ikiwekwa jiwe la msingi tayari kwa utekelezaji wake, hayo yote ni matunda yatokanayo na Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ambayo baadaye yalizaa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA BARABARA YA MWIGUMBI-MASWA (50.3) MKOANI SIMIYU

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Barabara ya Mwigumbi-Maswa (Km 50.3) katika Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka watatu kutoka kulia Waziri wa Ujenzi Profesa Makame Mbarawa wakwanza kulia pamoja na viongozi wengine.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengiene  akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Mitambo itakayotumika katika ujenzi wa mradi wa Barabara ya Mwigumbi-Maswa (Km 50.3).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza maelezo ya mradi wa ujenzi wa Barabara ya Mwigumbi-Maswa (Km 50.3) kutoka kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS  Mhandisi Cristianus Ako kabla ya kuweka jiwe la msingi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Maswa kabla ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa wa Barabara ya Mwigumbi-Maswa (Km 50.3), mkoani Simiyu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri wa Ujenzi Profesa Makame Mbarawa mara baada ya kuwasili Wilayani Maswa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza mkuu wa mkoa wa Simiyu Antony Mtaka mara baada ya kuwasili Wilayani Maswa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri wa TAMISEMi na Kazi maalumu kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Haji Omari Heri kabla ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara hiyo ya Mwigumbi-Maswa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Waziri wa TAMISEMi na Kazi maalumu kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Haji Omari Heri wakimwagilia maji mti mara baada ya kuupanda baada ya uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya Mwigumbi-Maswa (Km 50.3), mkoani Simiyu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka saini kwenye Ubao kwa kutumia Chaki zinazotengenezwa na Kiwanda cha Chaki cha Maswa Mkoani Simiyu. Rais Dkt. Magufuli aliwapongeza wenye kiwanda hicho na kuwashauri kukipanua zaidi ili kiweze kuwafikia Watanzania wengi wenye mahitaji ya Chaki.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia Wakazi wa Maganzo mkoani Shinyanga mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia Wakazi wa Maganzo mkoani Shinyanga mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili mkoani Simiyu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wakazi mbalimbali wa Maswa mara baada ya kumaliza kuwahutubia Wilayani humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wakazi mbalimbali wa Maswa mara baada ya kumaliza kuwahutubia Wilayani humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkuu wa mkoa wa Simiyu Antony Mtaka wakiangalia utengenezwaji wa Chaki katika kiwanda cha Chaki cha Maswa mkoani Simiyu. PICHA NA IKULU

RAIS DKT. MAGUFULI AHUTUBIA WANANCHI WA SHINYANGA KATIKA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MIAKA 53 MAPINDUZI YA ZANZIBAR

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kuwasalimia wananchi wa Shinyanga waliofika katika uwanja wa mpira wa Kambarage katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar mkoani humo.
3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kuwahutubia wakazi wa Shinyanga katika kilele cha Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Kambarage mkoani humo.
2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Shinyanga katika kilele cha maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Kambarage mkoani humo.
4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono Kwaya ya KKKT Shinyanga mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.
PICHA NA IKULU

FURAHIA OFA HIZI ZA 'TRAVEL WEDNESDAY' KUTOKA JUMIA TRAVEL

0
0

Na Jumia Travel Tanzania


Kila siku ya Jumatano ya kila wiki, Jumia Travel (www.travel.jumia.com) huwa inawaletea wateja ofa za punguzo la bei kutoka hoteli mbalimbali nchini Tanzania ambazo hudumu mpaka siku ya Ijumaa.
Ofa hizi humuwezesha mteja kuchagua na kulipia sehemu anayoitaka kwa njia ya mtandaoni au pindi atakapowasili hotelini. Lengo kubwa ni kumuwezesha kila mtu kufurahia utajiri wa sehemu lukuki za kuvutia zinazopatikana kila kona ya nchi kwa gharama nafuu.

Ikiwa ni wiki ya pili tu tangu tuauanze mwaka mpya wa 2017, hoteli zifuatazo zimetoa ofa ya punguzo la bei kuwavutia watu kwenda kufurahia huduma mbalimbali walizonazo.

Mermaids Cove Beach Resort & Spa

Hoteli hii ya kifahari inapatikana Visiwani Zanzibar umbali wa mwendo wa saa moja kutoka mji wa Stone Town ikiwa inapakana na mandhari nzuri ya kuvutia ya bahari ya Hindi. Ukiwa pale unaweza kufurahia huduma kama vile intaneti ya bure, mgahawa uliosheheni vinywaji na vyakula vya kutosha, sehemu ya kufanyia mazoezi, michezo ya kufurahisha, ukumbi wa mikutano na duka dogo la manunuzi.

Nashera Hotel

Hii ni sehemu mojawapo ya zile zinazovutia na unaweza kuanza mwaka huu mpya kwa kwenda kuitembelea. Nashera ni hoteli ya kifahari inapatikana mkoani Morogoro ikiwa inatazamana na mandhari nzuri ya safu ya milima ya Uluguru. Baadhi ya huduma zilizopo ni pamoja na vyakula vya kitanzania na kigeni, simu, vifaa vya kujitengenezea chai au kahawa, sehemu za mapumziko, mashine za kukaushia nywele na ulinzi wa kutosha kwa ajili ya usalama wako na mali zako.  

New Kwetu Hotel 

New Kwetu Hotel inapatikana katika eneo tulivu la Kisosora mkoani Tanga lenye mandhari nzuri na bustani ya kuvutia. Ukiwa hapo utafurahia huduma nzuri za vyakula vya asili na kigeni, mgahawa wenye vinywaji mbalimbali, kufuliwa nguo, usafiri wa kukupeleka uwanja wa ndege na eneo kubwa la kuegeshea magari.

Hoteli zingine zinazotoa ofa hizi ni pamoja na Jangwani Sea Breeze Resort, Golden Tulip Hotel na Skippers Haven za jijini Dar es Salaam pamoja na Paradise Beach Resort na Golden Tulip Zanzibar Boutique Hotel za visiwani Zanzibar.
Kupata taarifa na kufahamu mengi zaidi juu ya hoteli hizi unaweza kutembelea Jumia Travel (www.travel.jumia.com) ili kuweza kuperuzi sehemu utakayoipendelea. 

MLIPUKO WA INJILI KUTOKA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA.

0
0
Ni mlipuko wa injili na habari njema takatifu kwa watu wote.
Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo nyuma ya Soko Kuu la Sabasaba, Ilemela Jijini Mwanza, chini ya Mchungaji na Mwinjilisti wa Kitaifa na Kimataifa, Dkt.Daniel Moses Kulola, linawakaribisha watu wote kwenye ibada zake.

Kila Jumapili ibada ya kwanza inaanza saa 12:00 asubuhi, ibada ya pili saa 1:00 kamili na ibada ya tatu ni saa 4:30 asubuhi huku ibada za katikati ya wiki zikifanyika jumatano na ijumaa kuanzia saa 10:00 alasiri.

Njoo ukutane na nguvu ya Mungu kutoka kwa wapakwa mafuta wa Bwana, wakiongozwa na Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola ambaye huduma zake zimefanyika Baraka katika mikoa mbalimbali nchini na hata nchi za nje ikiwemo Kenya, Rwanda, Burundi, DRC Congo, Zambia, Malawi, Dernimark, Sweden, Marekani na nyinginezo nyingi.

Njooni nyote wenye kujawa na misukosuko maishani ikiwemo kuteswa na majini, uchawi, kutozaa, maombezi ya kazi na biashara huku mkibarikiwa na kwaya mbalimbali ikiwemo Havila Gospel Singers, Revival Kwaya, New salvation na Hot spear choir bila kuwasahau waimbaji kama Sarah Emmanuel,  Aggness Akrama, Happy Shamawele,  Mitagato, Ndangeji, paschal, Allen, God's Reign, Samuel Daniel Kulola mzee wa Vocal bila kusahau huduma ya Kusifu na Kuabudu inayopigwa mubashara yaani #Live.

Kama hiyo haitoshi, Mahubiri, Mafundisho na Maombezi ya Mchungaji Daniel Moses Kulola yatakujia Mubashara kwa njia ya mtandao kupitia Facebook kila siku ya alhamisi kuanzia saa tisa kamili mchana kwenye ukurasa wake uitwao Daniel Moses Kulola.
Kwa msaada na ushauri wa kiroho, piga simu nambari 0767 74 90 40 na Mungu atakubariki.
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live




Latest Images