Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 108 | 109 | (Page 110) | 111 | 112 | .... | 1896 | newer

  0 0

  Alphonce Shabani wa Mtakuja Beach (kulia) akimtoka Haruna Athuman waf Sifa United wakati wa mechi ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars, mkoa wa Kinondoni, iliyochezwa kwenye uwanja wa Mwanamanyala Shule ya Msingi jijini Dar es Salaam leo Juni 24, 2013. Sifa United walishinda 5-2.
  Abdulazizi Haruna wa Mtakuja Beach na Hamir Sheh wa Sifa United wakiwania mpira wa juu wakati wa mechi ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars, mkoa wa Kinondoni, iliyochezwa kwenye uwanja wa Mwanamanyala Shule ya Msingi jijini Dar es Salaam leo Juni 24, 2013. Sifa United walishinda 5-2.
  Mshambuliaji wa Sifa United Haruna Athuman (kushoto) akichuana na Alex Simenga wa Mtakuja Beach wakati wa mechi ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars, mkoa wa Kinondoni, iliyochezwa kwenye uwanja wa Mwanamanyala Shule ya Msingi jijini Dar es Salaam leo Juni 24, 2013. Sifa United walishinda 5-2

  0 0

  Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Bi. Ingiahedi Mduma akiwa na washiriki wa nchi mbalimbali wakati wa matembezi ya hiari wakati wa kukamilisha maonesho ya wiki ya utumishi wa umma nchini Ghana.
  Watanzania wakiwa kwenye matembezi ya hiari pamoja na washiriki wa nchi zingine wakati wa kukamilisha maonyesho ya wiki ya utumishi wa umma Nchini Ghana.
  Washiriki wa Tanzania na washiriki wa nchi zingine wakisubiri kuanza kwa matembezi ya hiari wakati wa kuadhimisha maonesho ya wiki ya utumishi wa umma Nchini Ghana.

  0 0


   

  0 0


  Mbunge wa Monduli, ambaye pia ni waziri mkuu mstaafu, Edward Lowasa, akisalimiana na wanafunzi wa chuo kikuu cha UDOM waliotoka shule za sekondari za kata, wakati walipofika nyumbani kwake mkoani Dodoma kutoa shukrani zao kwa hatua waliyofikia kielimu.


  Hamida Salum mwanafunzi wa mwaka wa kwanza UDOM, akizungumza kwenye hafla hiyo Juni 25, 2013


  Mh. Lowasa katikati, Dkt. Mahanga (Kulia) na Parseko Korne wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi hao.


  Na Father Kidevu Blog, Dodoma.


  Wanafunzi wa Chuo Kikuu ch DODOMA, maarufu kama UDOM, ambao walifika hapo wakitokea zile shule za makabwela (Shule za Kata), wamemtaka Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowasa, achukue fomu za kugombea urais 2015 muda utakapowadia.

  Pia wameahidi kujichangisha fedha kwa ajili ya malipo ya fomu hizo endapo italazimika.  Kauli hiyo ya kwanza kutoka kwa makundi na watu wasiokuwemo ndani ya siasa, ilitolewa Jumatatu usiku nyumbani kwa Lowasa mjini Dodoma, wakati kundi nla wanafunzi hao walipofika kutoa shukrani zao kwa hatua waliyofikia ikiwa ni matunda ya shule hizo, ambazo muasisi wake ni mbunge huyo wa Monduli.


  “Mimi ninayofuraha kusimama hapa leo hii, nikiwa mtu tofauti, kwa maana ninayesoma elimu ya juu, baada ya kufanikiwa ,kuendelea na elimu ya sekondari kupitia shule za kata pale Kiluvya Dar es Salaam” anasema Hamida Salum ambaye kwa sasa ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza hapo UDOM.


  “Wewe ni jembe, kama uliweza kusimamia ujenzi wa shule za kata kwa kipindi kifupi cha miaka 2, ninahakika unaweza kufanya men gi zaidi endapo utakuwa rais wan chi hii” mwanafunzi mwingine wa mwaka wa kwanza, Clementina Ophoro alisema, kwenye salamu za mwanafunzi mmoja mmoja wakati wa utoaji shukrani kwa Lowasa.


  Lowasa wakati akiwa waziri mkuu wa Tanzania, kwenye mwanzoni mwa awamu ya n ne ya utawala wa rais Jakaya Kikwete, aliweza kusimamia ujenzi wa shule za kata kote nchini, ili kutoa nafasi zaidi za wanafunzi wa makabwela, walioishindwa kendelea na masomo kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na uhaba wa madarasa.  Kwa sasa shule hizo zimekuwa zikibezwa na watu mbalimbali kwa maelezo kuwa hazina walimu wa kutosha na uhaba wa vifaa vya kufundishia ikiwemo vyumba vya maabara.“Mimi ninawashangaa watu wanaosema kuwa eti shule za kata hazifai, kwa vile hazina walimu na vifaa. Haya maneno ni ya kupuuzwa, kwani binadamu hupaswi kukwepa changamoto za maisha” alisema mwanafunzi mwingine Victor Mafuru pia wa mwaka wa kwanza.


  Wanafunzi hao wa UDOM waliotoka kwenye shule za sekondari za kata, wameamua kuanzisha umoja wao kote nchini, ili kuendeleza ndoto za kuhakikisha kila mwanafunzi wa mtu masikini anapata elimu.

  Kwa kuanzia wanafunzi hao wapatao 600, wameahidi kufundisha bure kwenye shule za umma, wawapo likizo baadaye mwishoni mwa mwezi huu wa Juni.


  Kwa upande wake, Lowasa ambaye alikuwa pamoja na naibu waziri wa kazi na ajira, Dkt. Makongoro Mahanga, mbunge wa Kigoma mjini, Peter Serukamba, na mkuu wa mkoa wa Singida, Parseko Kone, aliwapongeza wanafunzi hao kwa moyo wao wa shukrani na kuwataka wasikatishwe tama na maneno yanayotolewa juu ya ubora wa shule hizo, kwani yeye binafsi anajivunia juhudi zake kupitia sera za chama cha Mapinduzi, zimeweza an galau kutoa wanafunzi wengi kutoka shule hizo kujiunga na vyuo vikuu.

  0 0


  Direcotor Credit Bureau Expansion- Creditino Group Mr.Hakon Stafansson speaking at the press conference today at Serena Hotel (left) is Mr.Davith Kahwa,Director-Creditino Tanzania.

  ========  =========  ========  =======

  On 6th June 2013, Creditinfo Tanzania Limited (CIT) received the licence to conduct credit reference business after satisfactorily met the conditions stipulated in the provisional licence that was granted by the Bank of Tanzania on October 2012 and demonstrated its readiness to commence business. This means that Creditinfo Tanzania, is the first company to receive a licence to operate a credit reference bureau in Tanzania issued under Section 48 of the Bank of Tanzania Act, 2006.


  Subsequently, on 12thJune 2013, Creditinfo Tanzania started to provide services to public and various categories of business that are denominated under the Act as being eligible to provide credit information to a Credit Reference Databank. These include banks and non-bank financial institutions, savings and credit schemes, micro-finance companies, any other finance company that are licensed and supervised by the Bank of Tanzania. Similar services are available for subscriptions to all other credit providers, he added.


  Speaking at the press conference today, Mr. Hakon Stefansson, on of the shareholders & Director Credit Bureau Expansion – Creditinfo Group said “Credit Reference Bureaus ensure responsible lending and borrowing, which is particularly important for the growing economies. Currently more than 45 banks have licenses issued by the Bank of Tanzania, and their successful development as well as successful development of country’s economy as a whole could be influenced by an adequate clients’ risk evaluation.  Credit reporting systems will improve credit risk and credit portfolio management, enhance financial supervision and financial sector stability and access to credit. We are delighted to have the opportunity to contribute to the Government of Tanzania’s efforts of creating sound financial infrastructures“.


  Mr. Davith Kahwa, Director– Creditinfo Tanzania said “We are also far advanced in negotiations with public information providers to access data that will allow us to develop value-added products. We anticipates that reliable, credible and accessible credit information will revolutionize the way credit decisions are made in Tanzania, facilitating effective risk management, quicker decisions and more accurate pricing of risks associated with credit decisions as well as reduced interest rates”


  Persons who had difficulties accessing credit due to a lack of collateral will now be better positioned to do so provided they can demonstrate an excellent credit history and credit score. For the first time Tanzanians now can obtain a copy of their credit report” Mr Kahwa added .The company will be investing heavily in training and the provision of technical oversight for the members of its user group, noting that a specialist in credit bureau systems and risk management will arrive in country in August to train our subscribers”

  "Creditinfo Tanzania is committed to differentiating itself by focusing not just on the core business of individual and corporate credit information but also introduction of automated credit scoring software tools and developing value-added products from publicly accessible data sources, packaging them and making them easily accessible to users," Mr Stefansson concluded…

  0 0

   Watoto yatima wa kituo cha Ngeze education center kilichopo maeneo ya kinondoni kwa  msisiri watajumuika na watoto wenzao katika tamasha la Raha za jana na leo linalojumuisha burudani ya bendi za muziki wa dansi.

  Wasanii nguli wa filamu na bongoflava wanaokubalika kwa watoto watakuepo kula,kuimba na kucheza na watoto wote watakaodhulia katika tamasha hilo amabapo kiingilio kwa watoto wadogo kitakuwa ni bure ambapo wazazi wao watalipa kiasi cha tshs 8,000 tu.

  Jumla ya bendi sita zitapanda jukwaani moja kuonyesha ukali wake,pia zile nyimbo mpya kutoka katika bendi hizo utazisikia zikipigwa live,bendi hizo ni Twanga Pepeta"African Stars",Mashujaa musica Band ikiongozwa na Chalz baba " wazee wa tuzo tano",Bantu group ikiongozwa na   ikiongozwa na "komandoo Hamza kalala".

  Bendi zingine ni King kikii"wazee sugu",OTTU jazz band"MSONDO",King Kikii "wazee sugu" na DDC Mlimani park "SIKINDE" tamasha hilo linatarajiwa kufanyika tarehe 6 mwezi wa saba katika viwanja vya posta vilivyopo kijitonyama jijini Dar es salaam.
   
   Milamgo ya viwanja hivyo itafunguliwa saa tano asubuhi ambapo michezo ya watoto itaanza na kuisha saa kumi na mbili jioni ambapo burdani za bendi zikiendelea mpaka usiku wa manane.

  0 0

  m2s breaking news

  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi muda huu ametangaza kuahirishwa kwa uchaguzi wa Udiwani katika kata za Elerai, Themi, Kaloleni na kimandolu Manispaa ya Arusha hadi tarehe 14/7/2013. Amesema sababu kuu ni hali ya amani bado sio nzuri ya kuruhusu uchaguzi kufanyika kwa sasa. Itakumbukwa kuwa Uchaguzi wa Kata Hizi ambao ulikuwa ufanyike tarehe 16/6 uliahirishwa hadi tarehe 30/6 kutokana na mlipuko wa bomu kwenye mkutano wa kufunga kampeni wa CHADEMA. Kampeni hazitakuwepo kwa kipindi hiki hadi tarehe ya Uchaguzi.  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia washiriki wa kutano, wakati akifungua rasmi Mkutano wa 24 wa mwaka wa nguvu za Atomiki Tanzania, wa Utafiti na Mfunzo ya ukuaji wa Teknolojia ya Sayansi ya Nyuklia, ulioanza leo Juni 25, 2013 katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha.
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa Utafiti wa Mitambo ya Nyuklia, Kitengo cha Matengenezo, Yesaya Sungita, wakati Makamu alipotembelea Taasisi ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, iliyopo eneo la Njiro jijini Arusha leo, Juni 25, 2013 baada ya kufungua mkutano wa 24 wa mwaka wa nguvu za Atomiki Tanzania, wa Utafiti na Mfunzo ya ukuaji wa Teknolojia ya Sayansi ya Nyuklia, ulioanza leo Juni 25, 2013 katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa msimamizi wa Mashine ya kutafiti Vyakula na Mazingira, Remigius Kawala, wakati Makamu alipotembelea Taasisi ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, iliyopo eneo la Njiro jijini Arusha leo, Juni 25, 2013 baada ya kufungua mkutano wa 24 wa mwaka wa nguvu za Atomiki Tanzania, wa Utafiti na Mfunzo ya ukuaji wa Teknolojia ya Sayansi ya Nyuklia, ulioanza leo Juni 25, 2013 katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha.
   Makamu wa Rais Dkt. Bilal, akionyeshwa baadhi ya maeneo ya Taasisi hiyo, wakati alipotembelea katika Taasisi hiyo iliyopo Njiro jijini Arusha.
   
   Baadhi ya washiriki wa Mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo leo, Juni 25, 2013 katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia na kusikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Kinga ya Mionzi, Ukaguzi wa  Vifaa, Dkt. Willbrod Muhogola, wakati Makamu alipotembelea Taasisi ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, iliyopo eneo la Njiro jijini Arusha leo, Juni 25, 2013 baada ya kufungua mkutano wa 24 wa mwaka wa nguvu za Atomiki Tanzania, wa Utafiti na Mfunzo ya ukuaji wa Teknolojia ya Sayansi ya Nyuklia, ulioanza leo Juni 25, 2013 katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania, iliyopo eneo la Njiro jijini Arusha, baada ya kuzungumza nao alipotembelea Taasisi hiyo leo Juni 25, 2013. Picha na OMR
  Picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano huo

  0 0

  Bw.Henry Kileo akiwa na watuhumiwa wenzake wa mashtaka ya Ugaidi yanayowakabili wakati walipofikishwa Mahakama ya Hakimu mkazi mkoani Tabora kwa mara ya kwanza.
  Wanachama wengine wa Chadema ambao wanahusishwa katika mashataka hayo ya Kigaidi ambapo imedaiwa kuwa watuhumiwa walifanya makosa hayo ya Ugaidi na kumjeruhi Bw.Mussa Tesha ambaye ni mwanachama wa CCM wakati wa kampeni za uchaguzi wa Ubunge wa jimbo la Igunga mnamo tarehe 9/9/2011 katika msitu wa Hanihani huko wilayani Igunga.
   Ulinzi katika Mahakama hiyo uliimarishwa ipasavyo.
   Henry Kileo akiwa ndani ya gari pamoja na watuhumiwa wenzake wanne wakisubiri kupelekwa Gereza la Mahabusu hadi watakapoletwa tena Mahakamani hapo mnamo tarehe 8/7/2013

  Na Josephat Isango wa Tanzania Daima.

  KAIMU Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mkoa wa  Dar es Salaam, Henry Kilewo, anashikiliwa  na polisi , akihusishwa na  tukio la kumwagiwa tindikali, Musa Tesha. Tesha alimwagiwa tindikali na watu wasiojulikana Septemba 9, mwaka juzi kwenye kampeni ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga, uliomuweka madarakani Dk. Kafumu Dalali.
  Akizungumza juzi na Tanzania Daima kabla ya kufika makao makuu ya Jeshi la Polisi, Kilewo alisema hajui anachoitiwa na kwamba anatekeleza wito wa jeshi hilo kuwa afike ofisini kwao. “Sijui ninachoitiwa, nimepigiwa simu naenda kutekeleza wito, nimesha wataarifu mawakili wangu ninaowaamini, kwa kuwa chochote kinaweza kutokea cha msingi Watanzania wapenda mageuzi waniombee kwa Mungu,” alisema Kilewo.
  Wakili wa Kilewo, Peter Kibatala, alisema baada ya mteja wake kuhojiwa kwa muda wa saa tano juzi alielezwa kuwa anapelekwa Igunga, mkoani Tabora kuunganishwa na watuhumiwa wengine katika kesi ya kutumia tindikali na kujeruhi.
  Kibatala alisema anasikitishwa na hatua ya jeshi hilo kumnyima dhamana mteja wake ilhali kosa wanalomtuhumu linadhaminika na kwamba hayo ni matumizi mabaya ya madaraka kumzuia mtu kwa zaidi ya saa 24 pasipo kumfikisha mahakamani. Wengine wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kutumia tindikali na kudhuru watu ni pamoja na  Oscar Kaijage wa Shinyanga na Evodius Justinian wa Bukoba.
  Evodius Justinian alikamatwa na  Jeshi la Polisi mjini Bukoba na kushikiliwa kwa siku kadhaa kabla ya  kusafirishwa hadi jijini Dar es Salaam. Kabla ya kusafirishwa na kufikishwa jijini Da r es Salaam, Justinian alieleza kuteswa na kupigwa na askari waliokuwa wakimzuia katika vituo mbalimbali kuanzia mjini Bukoba.

  0 0

   
   Nahodha wa timu ya Makumbusho United Hamza Mohamed akinyanua juu kombe la ubingwa wa Airtel Rising Stars, mkoa wa Kinondoni, baada ya kuibamiza timu ya Mtakuja 5-1 katika fainali ya mashindano hayo ngazi ya mkoa iliofanyika kwenye uwanja wa Mwanyamala shule ya msingi jijini Dar es Salaam leo Juni 25, 2013.
   Nahodha wa timu ya Makumbusho United Hamza Mohamed akipokea kombe la ubingwa wa Airtel Rising Stars, mkoa wa Kinondoni, kutoka kwa Ofisa Maendeleo wa TFF Bw. Salum Madadi baada ya kuibamiza timu ya Mtakuja 5-1 katika mchezo wa mwisho wa mashindano ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17 uliofanyika kwenye uwanja wa Mwanyamala shule ya msingi jijini Dar es Salaam leo Juni 25, 2013
   Wachezaji wa timu ya Makumbusho United wakishangilia baada ya kutwaa kombe la ubingwa wa Airtel Rising Stars, mkoa wa Kinondoni, kwenye uwanja wa Mwanyamala shule ya msingi jijini Dar es Salaam leo Juni 25, 2013. Makumbusho walishinda 5-1 dhidi ya Mtakuja.


  Baadhi ya mashabiki wa kishangilia timu zao katika michuano ya Mkoa ya Airtel Rising star 2013.
  ======  =======  ========
  Makumbusho mabingwa Airtel Rising Stars Kinondoni.

  Timu ya Makumbusho United imetawazwa kuwa mabingwa wa Airtel Rising Stars mkoa wa kisoka wa Kinondoni baada ya kuwafunga bila huruma Mtakuja Beach 5-1 katika mchezo wa fainali wa mashindano hayo ya vijana chini ya umri wa miaka 17. Mchezo huo ulifanyika kwenye kiwanja cha shule ya Msingi Mwananyamala jijini Dar es Salaam leo Juni 25 ,2013.

  Mabingwa hao wapya wa ARS ngazi ya mkoa walianza michuano hiyo kwa kishindo walipoitandika Sifa United 3-1 katika mchezo wa ufunguzi uliopigwa katika uwanjwa huo huo Jumapili. Katika mchezo wa leo, Makumbusho wamepata magoli kupitia kwa Premji Stephano (dk 12), Ally Amin (dk 35), Rashid Ngone (dk 38 na 71) na  Wllie Kalolo (dk 53) wakati Mtakuja walipata goli la kufutia machozi dakika ya 78 kwa njia ya penati iliyopigwa na Steven Munyu.

  Jijini Mbeya, timu ya Mbasco ilitoshana nguvu na timu ya Mbosa Jumatatu Juni 24 baada ya kutoka sare ya 3-3 katika mchezo wa vuta nikuvute wa Airtel Rising Stars. Mbasco walipata magoli yao kupitia kwa Jasco Mwaibabe (dk 20 na 50) na Joel Kasimila dakika ya 68. Mchezo huo ulifanyika kwenye kiwanja cha Magereza Mbeya. Kwa upande wao, Mbosa walipata magoli yao kupitia kwa Michael Mwashilanga (dk 5), Richard Kalinga (dk 49) na Enock Chikaonga (dk 9).

  Mjini Morogoro; timu ya Moro kids iliishinda Anglikana 3-0 katika mchezo mwingine wa Airtel Rising Stars ngazi ya mkoa uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya seconday ya Morogoro. Magoli ya Moro kids yaliwekwa kimiani na Abdul Rashid, Robert Nashon na Evans Nashon. Robert na Evans ni mapacha.

  Katika mkoa wa kisoka wa Ilalan, Msimamo Youth Academy walipata ushiindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Buguruni Youth Center katika mchezo mgumu iliofanyika kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam. Goli hilo la ushindi lilifungwa dakika za majeruhi na nahodha wa timu hiyo Rajab Mohamed katika dakika ya 89

  Mkoa wa kisoka waTemeke ulitarajiwa kuanza mechi zake za Airtel Rising Stars ngazi ya mkoa jana (leo) katika uwanja wa Twalipo na mkoa wa Mwanza vile vile ulitarajia kuanza mechi zake kwenye uwanja mkongwe wa Nyamagana jana (leo). 

  Programu hii ya Airtel Rising Stars ni ya Afrika nzima likiwa na lengo la kuendeleza na kukuza  mpira wa miguu katika bara la Afrika kwa vijana wanaochipukia waweze kupata nafasi ya kuendeleza vipaji vyao.

  Fainali za ARS Taifa vile vile zitatumika kuchagua timu bora za wavulana na wasichana ambao wataiwakilishaTanzania katika mashindano ya kimataifa ambapo nchi mwenyeji wa michuano hiyo itatangazwa mwezi ujao. Wachazeaji wengine watachaguliwa kwenda kwenye kliniki itakayoendeshwa na makocha kutoka klabu maarufu duniani ya Manchester United


  0 0

  942331_578714148840668_773339795_n
  Mjasirimali mchapakazi na Mbunge Kijana nchini Tanzania, Mohammed Dewji (MO) ametajwa katika jarida la Kimataifa la mabilionea duniani katika Nyanja za biashara (Forbes Africa Magazine) kama mjasirimali mwenye umri mdogo mwenye mafanikio ya kuigwa hapa Afrika na duniani kwa ujumla taarifa la Jarida hilo limeeleza.

  Kwa mujibu wa taarifa hizo toka kwa Jarida hilo la Forbes African Magazine linasema amekuwa Mtanzania wa Kwanza kupata kuhojiwa na (Forbes Magazine) mafaniko, changamoto na matatizo kadhaa kwenye uwanja wa biashara kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati.

  Mo akihojiwa na Jarida hilo alisema toka kwenye masaa mia moja kwa wiki na kutengeneza faida ya Millioni 85 dola za kimarekani! Ni mafanikio makubwa katika biashara Afrika. Anasema ni safari ya takribani miaka 12 ya ushindani wa kibiashara ndani ya mipaka ya Tanzania na Afrika kwa ujumla.

  “Nani anaweza kufikiri kwamba tunaweza kubadilisha biashara yetu toka Millioni 30 za kimarekani hadi dola Billioni 1.1 ndani ya miaka 12 tu,’ alinukuliwa akisema.

  0 0

   Mtuhumiwa akiwa ndani ya  chumba cha mganga na Mganga wake aitwae Yahaya tayari kwa kufanya mambo ya kishirikina.

  Mama mmoja pichani juu ajulilikanae kwa jina la Magreth Simon Nkwera,  amekamatwa kwa Mganga wa kienyeji akijaribu kutekeleza jaribio la kutaka kuwauwa baadhi ya watoto wa mumewe na baadhi ya ndugu zake huko kibaha maili moja mkoani Pwani na hivi sasa yupo katika kituo cha polisi Maili moja akisubiri kupandishwa kizimbani.  
   Mtuhumiwa huyo akiwa ndani ya gari la polisi baada ya kukamatwa akiwa na huyo Mganga wa Kienyeji. 
  Mtuhumiwa  ambaye ni mfanyakazi wa shirika la Nyumbu kibaha mkoani Pwani,akiwa anahojiwa na mzee wa ukoo wa Shirima,Afisa polisi jeshi daraja la Kwanza (woii mstaafu) Joseph Shirima mara baada ya kumkamata live kwa sangoma.Habari hii imetolewa na mwenyekiti wa ukoo wa shirima bwana Godilisten Hendrick Shirima.

  0 0

  IMG_2657

  Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Kanda ya Afrika Mashariki nchini Tanzania (ILO) Bw. Alexio Musindo amesema kupitia msaada kutoka Serikali ya Sweden wa kifedha ILO iliweza kuwahusisha wasichana na wavulana katika makundi mbalimbali wenye vipato vidogo kupata uelewa wa Afya ya Uzazi kupitia Makongamano, Semina na Mafunzo mbalimbali yaliyoendeshwa na shirika hilo la kazi Duniani.

  Ameongeza kuwa “tuliwasaidia kuwaunganisha na vikundi vya kuweka na kukopa ili waweze kupata mitaji midogo midogo ya kufungua biashara ndogo ndogo katika harakati za kuwafanya wajitegemee na kuepekana na vishawishi vya Ngono isiyokuwa Salama.

  Bw. Musindo amesisitiza Umuhimu wa TACAIDS kuandaa makongamano kama haya ili kuwawezesha wasichana na wavulana wadogo kupata ufahamu uelewa na mafunzo ya uzazi wa Afya na jinsi ya kuelewa mabadiliko yao ya kimaumbile.

  “Ni matumaini yangu mwingiliano huu wa Utamaduni wa kupambana na Ukimwi, Kinga na Uwezeshwaji wa Kiuchumi umefanyika vizuri, hasa katika kuyalenga makundi yaliyo katika mazingira magumu itasaidia kuongeza kasi ya kupunguza maambukizi mapya kama ilivyoripotiwa na ripoti ya UNAIDS mwaka 2012 Duniani kwamba maambukizi mapya yamepungua kwa Asilimia 20”. Amesema.
  IMG_2710
  Sehemu ya washiriki wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa leo kwenye Kongamano hilo.
  IMG_2731
  Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Jamii, Jinsia na Watoto Bi. Kijakazi Mtengwa akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo amesema mikakati ya kuwawezesha Wanawake Kiuchumi inaweza kupunguza hatari ya kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa Wanawake, Wasichana na Wavulana wadogo.

  Amesema Jamii lazima itambue kuwa juhudi zaidi zinahitajika ili nchini yetu iweze kufikia malengo ya 0.3 yaani Tanzania ambayo haina maambukizi mapya ya VVU, Ukimwi usiwe sababu ya vifo, vile vile pasipo unyanyapaa wala ukatili kwa mtu yeyote anayeishi na Virusi vya Ukimwi.
  IMG_2702
  Mwenyekiti wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dr. Fatma Mrisho akizungumza na washiriki amesema Takwimu zinazonyesha Wanawake wako katika hali ya hatari ya kuambukizwa zaidi kuliko wanaume ambapo mpaka sasa ni Asilimia Sita ya Wanawake nchini huambukizwa wakati wanaume ni Asilimia 3 nchini nzima.

  Dr. Mrisho alisisitiza umuhimu wa kumwezesha mwanamke kiuchumi kama ndio moja ya suluhisho la kumfanya kutokuwa tegemezi katika jamii.
  “Amesema takwimu zinazonyesha katika nchi nyingi za Kiafrika umaskini unachagia sana kuenea kwa Ukimwi maana Wanaume wengi hutumia umasikini wa Wasichana au Kinadada kuwarubini kwa fedha na kufanya nao Ngono isiyosalama”.

  Dr. Fatma Mrisho amepongeza juhudi za ILO na kuwataka mashirika mengine na wadau wa mapambano dhidi ya Ukimwi kuiga juhudi zilizofanywa na ILO za kuandaa makongamano ya kiuchumi ili kumwezesha Mwanamke na wavulana wadogo kujitambua na kuelewa jukumu lao katika mapambo ya VVU na Ukimwi nchini.
  IMG_2737
  Meza Kuu: Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Ukimwi Tanzania (UNAIDS) Dr. Hedia Belhadj, Mwakilishi kutoka TUCTA Bw. Hezron Kaaya, Katibu Mkuu wa Wizara ya Jamii, Jinsia na Watoto Bi. Kijakazi Mtengwa, Mwenyekiti wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dr. Fatma Mrisho, Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Kanda ya Afrika Mashariki nchini Tanzania (ILO) Bw. Alexio Musindo, Mkurugenzi wa Sera na Utetezi wa Chama cha waajiri Tanzania (ATE) Bi. Justina Lyela.
  IMG_2723
  Mwakilishi kutoka shirikisho la wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Bw. Hezron Kaaya alisisitiza mshikamano na umoja wa wafanyakazi katika mapambano ya VVU na Ukimwi sehemu za kazi. Bw. Kaaya amesisitiza majadiliano kama hayo yasiishie kwenye makabrasha bali wayatekeleze kwa vitendo ili kuleta matokeo chanya kwenye jamii.
  IMG_2721
  Mkurugenzi wa Sera na Utetezi wa Chama cha waajiri Tanzania (ATE) Bi. Justina Lyela akitoa nasaha zake kuhusu viwango sawa vya malipo ya mishahara kwa wafanyakazi nchini ili kuwakomboa wanawake na kipato kidogo makazini.
  IMG_2709
  Picha juu na chini ni sehemu ya washiriki kutoka ndani na nje ya nchini wa Kongamano la kuwawezesha Kiuchumi Wanawake, Wasichana na Wavulana dhidi ya Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi lililofanyika leo jijini Dar na kuratibiwa kwa pamoja kati ya ILO na TACAIDS.
  IMG_2632
  IMG_2654
  IMG_2741
  Washiriki wa Kongamano hilo wakiangalia baadhi ya machapisho mbalimbali ya VVU na Ukimwi.
  IMG_2745
  Picha juu na chini mgeni rasmi katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano hilo la siku moja lililofanyika jijini Dar es Salaam.
  IMG_2758

  0 0

  FAMILIA YA ZAINABU ABEID ALLY (BABY SHANGAZI HOTELI) YA MBEYA INAPENDA KUCHUKUA FURSA HII KUMKUMBUKA MAMA YAO MPENDWA ALIYEFARIKI USIKU WA TAREHE 5-06-2013 KATIKA HOSPITALI YA RUFAA JIJINI MBEYA NA KUZIKWA SIKU YA ALHAMISI TAREHE 6.06.2013.

  WATOTO WAKO POSTER, MABRUCK, ASHA, HAWA, HUSSEIN, HASIRA NA ABEID WANAUNGANA NA NDUGU NA JAMAA WALIOJITOLEA KWA HALI NA MALI KUHAKIKISHA MAMA YAO MPENDWA ANAPATA KILA AINA YA MSAADA ULIOKUWA UNAHITAJI MPAKA PALE MWENYEZI MUNGU ALIPOCHUKUA ROHO YAKE.

  KUMBUKUMBU YA KUTIMIZA SIKU YA 40 BAADA YA KIFO CHA MAMA YETU INATARAJIWA KUFANYIKA NYUMBANI KWAKE MAREHEMU MBEYA SIKU YA JUMAMOSI TAREHE 6.07.2013 WOTE MNAKARIBISHWA.

  MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALA PEMA PEPONI.
  AHSANTENI SANA

  0 0

   
   Meneja wa bia ya Serengeti Allan Chonjo (wa pili kulia) akiongea kwa njia ya simu na mshindi wa droo ya pili ya Winda na Ushinde  Mwl.Michael Valerian Mbuya katika mkutano na wana habari uliofanyika jana katika ofisi za Kampuni ya Bia ya Serengeti jijini Dar es Salaam, kushoto kwake ni Meneja mauzo  wa Push Mobile Rugambo Rodney, kulia kwake ni Afisa mwandamizi kutoka PWC Daniel Nnko na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Bahati Humudi Abdul Hussen(wa kwanza kushoto).
   Meneja wa bia ya Serengeti Allan Chonjo(katikati) akiongea na wana habari wakati wa kumtangaza mshindi wa droo ya pili ya Winda na Ushinde katika mkutano uliofanyikajana katika ofisi za Kampuni ya Bia ya Serengeti jijini Dar es Salaam. 
   Wakihakiki namba za simu za mshindi wa droo ya pili ya Winda na Ushinde iliofanyika jana katika ofisi za Kampuni ya Bia ya Serengeti, wa kwanza kulia ni Meneja wa bia ya Serengeti Allan Chonjo, Afisa mwandamizi kutoka PWC Daniel Nnko(katikati) na Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Bahati Nasibu Humudi Abdul Hussen(kushoto).

  ======  ========  =========

  MSHINDI WA DROO YA PILI KAMPENI YA WINDA NA USHINDE ATANGAZWA.

  Mshindi asherekea kitita cha 1,000,000 huku akiwapongeza kampuni ya bia ya Serengeti kwa promosheni hiyo. 


  25 Juni 2013, kampuni ya bia ya Serengeti imetangaza mshindi wa pili wa kampeni ya Winda na Ushinde ambae amejinyakulia kitita cha milioni moja baada ya kuchezesha droo yake ya pili. Droo hiyo ilichezeshwa katika ofisi za kiwanda hicho jijini Dar es Salaam huku ikishuhudiwa na mhakiki kutoka katika bodi ya uchezeshaji promosheni bwana Humud Abdul Hussein.


  Baada ya kupokea Michael Varelian Mbuya (29) ambae ni mwalimu wa sekondari kutoka Tabata Dar es salaam alionesha furaha yake na kubaki bumbuwazi kwa furaha. “Nina furaha isiyokifani kuwa mshindi wa promosheni hii ya Winda na Ushinde kutoka katika kampuni ya bia Serengeti na ntaitumia kufungua duka kwani ni ndoto yangu kubwa. Na najivunia kuitumia bia ya serengeti kwani ndio bia niipendayo na nawapongeza sana kampuni ya Serengeti kwa kuanzisha mashindayo haya na mpaka sasa nimeshajishindia bia nyingi pamoja na bia taslimu” alisema mshindi huyo.


  Akiongelea promosheni hii meneja wa kinywaji cha Serengeti Mr.  Allan Chonjo alisema “promosheni hii ni ya kipekee na mpaka sasa watu 110,000 wameshajishindia bia za bure na pesa taslimu ambazo ni shilingi 10,000 na100, 000/= na droo ya kwanza ilichezeshwa mwezi uliopita huku mshindi kutoka Moshi akiondoka na kitita cha milioni moja, pia promosheni hii inampa fursa mshindi kununua kile anachokitaka baada ya kujishindia fedha taslimu kwani tunaamini baadhi ya wateja wetu wana ndoto nyingi sana za mafanikio ila tatizo huwa ni pesa ili kitimiza ndoto zao.


  Lengo la kampuni yetu ni kuendeleza umoja na mshikamano  na wateja wetu kwa kuutambua na kuuthamini mchango wa wateja wetu kwani wao ni muhimili mkubwa katika kukuza na kuendeleza bai yetu ya Serengeti. Na sasa kampuni ya Serengeti inachezesha promosheni hii kutimiza azma yake ya kuinua uchumi wa wateja wao kama sehemu ya shukrani kwa wateja wake.


  Ni wakati wako ndugu mteja kushiriki mara nyingi uwezavyo na kuhakikisha unajishindia zaidi ya milioni saba. Ili kushiriki unatakiwa kufungua chini ya kizibo cha bia ya Serengeti na utakuta namba maalumu na unatakiwa kuituma kwenda namba 15317 na utapokea majibu.

  Tafadhari kunywa kistaarabu na ni maalum kwa 18+

  0 0

  Imeelezwa kuwa Zanzibar inaweza kukumbwa na Janga la uhaba wa Maji  ifikapo mwaka 2015 kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo watu kuharibu Vyanzo vya Maji.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud ameeleza hayo alipokuwa akizindua Kongamano la Kitaifa la kukabiliana na Maafa lililofanyika Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja.
  Amesema kuna Tafiti zimefanywa  na kuonesha hatari inayoikabili Zanzibar katika upatikanaji wa Maji na kwamba juhudi binafsi zinahitajika ili kukabiliana na hali hiyo.
  Aboud amesema Wasomi na Wataalam kwa ujumla wanapaswa kufahamu hali hiyo na kuisaidia Serikali katika kukabiliana na Upungufu huo badala ya kukaa kimya na kulaumu.
  “Wasomi wamekaa kimya sana hawatoi ushauri wa kitaalamu kwa Serikali juu ya nini kifanyike ili kuijengea uwezo Serikali na Jamii kwa ujumla kukabiliana na Majanga ” Alifafanua Aboud
  Ametolea Mfano wa Zao la Nazi linavyoendelea kupotea katika Visiwa vya Zanzibar na kusema kuwa Wataalamu wameshindwa kuja na namna bora ya kupata Minazi bora  inayozalisha zaidi na kuchukua eneo dogo kuliko Minazi iliyopo.
  Aidha Waziri Aboud amesisitiza  Idara ya Maafa kwa kushirikiana na wadau wengine  kuendelea kutoa Elimu ya kukabilaiana na Majanga  kwa jamii ili kupata jamii salama.
  “Ndugu wadau Elimu ni Muhimu kwa wananchi kuanzia ngazi ya chini hadi juu,kwa kukosekana Elimu ya Majanga baadhi ya wakati hata Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wanakuwa wagumu kupitisha Vifungu vya Bajeti za Idara,yote ni kiashirio cha uelewa mdogo juu ya Majanga” Aliongezea Aboud.
  Awali akimkaribisha Waziri Aboud, Mkurugenzi wa Idara ya Maafa alisema licha ya kukabiliwa na Changamoto mbalimbali Idara yake imejipanga vyema kuhakikisha inafanya majukumu yake ya msingi ikiwemo kukabiliana na Maafa.
  Amesema kwa Sasa Idara ya Maafa ina mpango wa kuainisha maeneo hatarishi katika Ramani  ili kusaidia ufahamu na namna ya kuweza kukabiliana na maafa pale  yanapotokea.
  Kongamano hilo la kitaifa la kukabiliana na maafa limendaliwa na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar  ambapo kwa siku mbili Washiriki kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali na Binafsi watajadili na namna bora ya kukabiliana na Majanga Zanzibar.
  Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar.
  IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR 26/06/2013

  0 0


  _DSC1179
  Ujumbe kutoka Ofisi za Umoja wa Mataifa Dar es Salaam, waandishi wa habari na watumiaji wa dawa za kulevya walioonyesha nia ya kuacha kutumia dawa hizo mjini Tanga, ambao wapo kwenye nyumba ya mafunzo ya kuwawezesha kuachana na dawa hizo (TANGA SOBER HOUSE) iliyopo Tanga. Ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga matumizi na biashara ya dawa za kulevya ambayo hufanyika 26 June kila mwaka. Kitaifa maadhimisho hayo yanafanyika mjini Dodoma.
    _DSC1238
  Picha juu na chini ni Afisa uhusiano wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama akiwasilisha ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu siku ya kimataifa ya kupinga matumizi na biashara haramu ya madawa ya kulevya kwenye kongamano la vijana kuhusu madawa ya kulevya mjini Tanga.
  _DSC1214
  _DSC1161
  Afisa habari wa kituo cha taarifa cha Umoja wa mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama akikabidhi Beji ya utambulisho kwa mmoja wa vijana aliyekaa miezi sita kwenye nyumba ya mafunzo ya waathirika wa madawa ya kulevya bila kutumia madawa hayo mjini Tanga katika kituo cha Tanga Sober House.
  _DSC1215
  Pichani juu na chini ni baadhi ya vijana wakifuatilia semina ya kupinga matumizi na biashara haramu ya madawa ya kulevya iliyoandaliwa na Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) kwa kushirikiana na TAYODEA.
  _DSC1215

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Mfalme Mswati wa (ii) wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam leo Juni 26, 2013. Mfalme Mswati wa ii, ametua nchini kwa ajili ya  kuhudhuria Mkutano wa 'Smat Patnership' unaotarajia kuanza Juni 28 mwaka huu. Picha na OMR
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Mfalme Mswati ii, baada ya  kuwasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam,  leo Juni 26, 2013. Mfalme Mswati wa ii, ametua nchini kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 'Smat Patnership' unaotarajia kuanza Juni 28 mwaka huu.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Mfalme Mswati ii, mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, leo Juni 28, 2013 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa 'Smat Patnership', unaotarajia kuanza Juni 28. Kushoto ni mke wa Mfalme Mswati. 

  0 0  0 0


older | 1 | .... | 108 | 109 | (Page 110) | 111 | 112 | .... | 1896 | newer