Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 9 | 10 | (Page 11) | 12 | 13 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Bondia Mtanzania Thomas Mashali kushoto akiwa amemgalagaza bondia Bernad Mackoliech na kwenda chini akimsubili ili amwendelezee kipondo wakati wa mchezo wao wa kugombania ubingwa wa Afrika Mashariki uliofanyika katika ukumbi wa Friends Conner, Manzese jijini Dar es Salaam na Mashali kuibuka na ushindi wa K,O katika raundi ya sita.

   Bondia Bernad Mackoliech wa kenya na Mtanzania Thomas Mashali wakioneshana ufundi wa kutupiana makonde wakati wa mchezo wao wa ubingwa wa Afrika Mashariki Mashali alishinda kwa K,O raundi ya sita.

  Baadhi ya mashabiki waliojitokeza katika mpambano huo wa ubingwa wa Afrika Mashariki

  Refarii Mark Hatia akimwesabia Bondia Bernad Mackoliech huku akimuamulu Thomas Mashalikwenda katika kona nyeupe baada ya kumtwanga konde zito lililomsababisha kulamba sakafu wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa Afrika Mashariki.
  Kamanda wa polisi mkoa wa Kipolisi wa kinondoni Charles Kenyela akimvisha ubingwa wa Afrika Mashariki bondia Thomas Mashali baada ya kumpiga Bernad Mackoliech wa Kenya kwa K,O Raundi ya 6 picha na wwww.superdboxingcoach.blogspot.com

  Refarii Mark Hatia akimwesabia Bondia Bernad Mackoliech huku akimuamulu Thomas Mashalikwenda katika kona nyeupe baada ya kumtwanga konde zito lililomsababisha kulamba sakafu wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa Afrika Mashariki picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com

  0 0


  ZAIDI ya abiria 25 waliokuwa wakisafiri na ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kutoka Kigoma kwenda Dar es Salaam wamenusurika kifo baada ya ndege aina ya Bombardier Dash 8-300 waliyokuwa wakisafiria kupasuka kioo ikiwa angani na hivyo kumlazimu rubani wake kutua kwa dharura.

  Hayo yamethibitishwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Kapteni Milton Lazaro, huku akiwataka wasafiri kutokuwa na hofu kwa matatizo hayo ni ya kawaida.

  Ndege hiyo ilikuwa ikifanya safari yake ya kwanza mkoani humo ikiwa ni miezi 10 baada ya ndege nyingine ya shirika hilo kuanguka na kuharibika mkoani Kigoma.

  Baadhi ya abiria waliokuwemo kwenye ndege hiyo Athumani Batumwa na Fred Mbassa, walisema ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 50, ilipata hitilafu ya kioo cha mbele kiasi cha dakika 30 baada ya kuruka kutoka Uwanja wa Ndege wa Kigoma.

  Kapteni Lazaro amekiri kutokea kwa hitilafu hiyo na amewaondoa hofu wasafiri juu ya tatizo hilo na kwamba ni sehemu ya matatizo yanayoweza kutokea kwa ndege yoyote.

  Alisema utaratibu unafanywa kuhakikisha abiria waliokuwa wakisafiri na ndege hiyo wanatafutiwa ndege nyingine ya kuwasafirisha hadi Dar es Salaam na kwamba hadi kufikia jana, abiria hao wangekuwa wameshatafutiwa ufumbuzi.

  Hata hivyo, ndege ya ATCL inaweza kuanza kufanyiwa marekebisho kuanzia leo baada ya kuwasili kwa vipuri.

  Hii ni mara ya pili kwa ndege ya ATCL mkoani Kigoma kupata hitilafu ikiwa inaelekea Dar es Salaam ambapo mapema mwaka jana moja ya ndege kampuni hiyo ilishindwa kuruka na kuserereka ambapo hadi sasa ipo kama chuma chakavu pembezoni mwa uwanja wa ndege mkoani hapa.

  0 0


  Natafuta mchumba kupitia blog yako. Mchumba ninayemtafuta naomba sana awe na miaka kuanzia 35 - 40. Awe mkristo, pia awe serious kwenye suala hili na maisha kwa ujumla ili Mungu akijalia tuingie kwenye ndoa. Awe na elimu ya chuo kikuu. Awe tayari kupimaukimwi.
  Aliye tayari naomba aniandikie kwenye:
   

  0 0


  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Iddi(kulia) na Afisa mwandamizi  kutoka katika kitengo cha elimu katika ofisi ya Benki ya Dunia nchini Bwana Nobuyuki Tanaka wakikata utepe wakati wa hafla ya ufunguzi wa Shule ya Sekondari ya Mlimani  Matemwe huko Zanzibar jana.Shule hiyo imejengwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Mainduzi Zanzibar na Benki ya Dunia. Picha na Freddy Maro wa Ikulu.

   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia vitabu vya masomo katika maktaba ya shule mpya ya Sekondari ya Mlimani Matemwe muda mfupi baada ya kuifungua rasmi jana.Kulia ni Ofisa mwandamizi kutoka ofisi ya Benki ya Dunia nchini anayeshughulikia masuala ya elimu Bwana Nobuyuki Tanaka na kushoto ni Mwalimu mkuu wa Shule hiyo Mohamed Mzee Choum.

  0 0

  Waziri wa nchi ofisi ya rais fedha uchumi na maendeleo Znz  Omary Yusuph Mzee akizungumza na waziri wa fedha uchumi na mipango wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt William Mgimwa wakati wa mkutano huo leo.
   Mwenyekiti wa mkutano kujadili changamoto za muungano mh. Mohamed Aboud Mohamed waziri wa nchi ofisi ya makamu wa pili wa Rais serikali ya mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti mwenza mh Samia Suluhu Hassan waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais muungano wakijadili jambo wakati wa mkutano huo .Picha zote na Ali Meja ofisi ya makamu wa Rais.
  Baadhi ya Mawaziri katika mkutano wa kujadili changamoto za muungano mjini zanzibar leo.

  ======  ======= ======= =======


  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar mh. Mohamed Aboud Mohamed, ameongoza kikao cha mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,kilichojadili masuala ya muungano mjini Zanzibar leo.


  Mambo mbali mbali yamejadiliwa katika kikao hicho, ikiwa ni pamoja na kupitia na kuthibitisha kumbukumbu za kikao cha Mawaziri kilichopita kilichofanyika mjini Dar es Salaam mwezi march mwka 2011, kupitia kumbu kumbu za kikao cha kamati ya pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Seriklai ya Mapinduzi ya Zanzibar. Mh. Aboud kama mwenyikiti wa kikao hicho cha mawaziri pia ameongoza mawaziri hao katika kupitia rasimu ya mwongozo wa ushiriki wa serilaki ya mapinduzi Zanziar katika masuala ya kimatifa katika hatua za awali.

  Pamoja na hayo mambo mengine yaliyojadiliwa ni pamoja na,kupokea mapendekezo kuhusu uratibu wa muda wa mgao wa ajira kwa taasisi za muungano kwa serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na kupitia taarifa ya utekelezaji wa masuala ya muungano.


  Aidha kikao hicho pia kimeweza kupitia hati za makubaliano ya hoja zilizopatiwa ufumbuzi, na agenda za kikao cha kamati ya pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar .


  Mwenyikiti Mh. Aboud ameongoza kikao hiki cha mawaziri kwa kushirikiana na mwenyekiti mwenza  ambae ni waziri wa nchi ofisi ya makamu wa raisi muungano mh. Samia Hassan Suluhu ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kikao cha kamati ya pamoja kati ya serikali ya jamhuri ya muungano wa tanzania na serikali ya mapinduzi Zanzibar kitakachofanyika kesho mjini zanzibar chini ya uwenyekiti wa  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mh Dkt Gharib Mohamed Bilal.


  NA EVELYN MKOKOI-ZANZIBAR

  AFISA HABARI OFISI YA MAKAMU WA RAIS.  0 0

  Mwakilishi kutoka kampuni ya Vannedrick Tanzania Ltd, ambao ni moja ya waandaaji wa tamasha hilo, Dino Debwe, akiongea na wanahabari (hawapo pichani).
  Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba, naye akiongea machache wakati wa mkutano huo na wanahabari.
  Baadhi ya wasanii wa filamu nchini kutoka kushoto ni Dk Cheni, Snura, Shamsa Ford na Shilole wakifuatilia mkutano huo.
  Sehemu ya wanahabari waliohudhuria mkutano huo uliofanyika katika hoteli ya Lamada Ilala jijini Dar leo.


  Kitalima Gerald na Khatimu Naheka 
  SHIRIKISHO la Filamu Tanzania (TAFF), limeandaa Tamasha la Wasanii litakalofanyika Januari 26, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, rais wa shirikisho hilo, Simon Mwakifwamba, alisema tamasha hilo wamelipa jina la Siku ya Ma-Star wa Filamu Tanzania, likiwa na lengo la kupata fedha za kujiendesha.

  Mwakifwamba alisema wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kukosa ofisi na vitendea kazi muhimu ndani ya ofisi kulingana na hadhi, hivyo wanakadiria kupata shilingi milioni 60 katika tamasha hilo. Alisema kwa kutambua hilo wameliandaa tamasha hilo wakiamini kupata wadau wengi wapenzi wa kazi zao. 

  Kiingilio kwa watoto kitakuwa Sh 2,000, wakubwa 7,000 na VIP 15,000. Tamasha litaanza saa 4:00 asubuhi. “TAFF tumeandaa Tamasha la Wasanii tulilolipa jina la Siku ya Ma-Star wa Filamu Tanzania, litakalofanyika Januari 26, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Dar Live.
  “Lengo ni kupata fedha kwa ajili ya kukabiliana na changamoto zinazotukabili, ikiwemo kuwa na ofisi kulingana na hadhi yetu na vitendea kazi muhimu ndani ya ofisi, tumekadiria kupata shilingi milioni 60 katika tamasha hilo linalotarajiwa kuanza saa nne asubuhi,” alisema Mwakifwamba.

  0 0  Jerry Silaa akisalimiana na wananchi Nzovwe Jijini Mbeya.(Picha kwa hisani ya Kalulunga Blog).


  Mjumbe wa NEC UVCCM Taifa Jerry Silaa akipigiwa saluti na Green Guard baada ya kuwasili.
  Mjumbe wa NEC UVCCM Taifa Jerry Silaa akisalimiana na wajumbe wa UVCCM mkoa wa Mbeya na pembeni yake ni Mwenyekiti wa UVCCM Mbeya Aman Kajuna.
  MNEC UVCCM Taifa Jerry Silaa akifungua semina ya siku mbili ya viongozi wa UVCCM mkoa wa Mbeya. Kushoto ni Aman Kajuna mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Mbeya.
  Jerry Silaa akigawa kadi za CCM viwanja vya Nzovwe Jijini Mbeya leo.
  Jerry Silaa akihutubia mamia ya wakazi wa eneo la Nzovwe jijini Mbeya.

  0 0

  Flightlink is a Scheduled and Corporate Air Charter Operator with bases in Dar Es Salaam and Arusha.
   
  The Company is made up of Experienced and talented general aviation professionals and providing strong foundation to achieve its VALUES & OBJECTIVES.
  Holder of Air Service License (ASL) and Air Operators Certificate (AOC) our primary VALUES and OBJECTIVES is to operate safe and secured air transport within Tanzania, Provide Quality Service, Be customer Oriented, Have Operational Eficiency with Team Spirit, Continuous improvement of our fleet and understanding customer requirements, be conscientious and responsible with sincerity.
   
  The Company Operates a Fleet of Cessna 208 Grand Caravans, Cessna 206 all fitted with Cargo pods for Schedule Flights and now introducing Cessna Citation 560 Twin Jet for VIP & Medevac Charters With the Introduction of Medevac Flights, Flightlink will strive to be the most comprehensive aeromedical company in Tanzania, Using Cessna Citation 560 (V) Aircraft Powered by Twin Pratt Whitney (JT15D) Turbo Fan Jet Engines, !tted with state of the Art Life Port Air Ambulance Kit.
  24Hrs Emergency Medevac and Repatriation services will be offered to those who live work and travel in Tanzania and Neighbouring Countries.
  Cessna Citation Centre in Wichita, KS, USA was the preferred choice to deliver and retrofit the Jet with the most advanced Avionics (ADVIZ) Glass Panel Cockpit and Navigation System. It is also fitted with TCAS II, EGPWS and enhanced Mod S Transponders. The aircraft comes with factory support for first in Tanzania of its type.
  Cessna Citation Centre and LifePort Inc., teamed up to assist Flightlink to prepare and Install Electrical wiring on Citation 560 Jet for Life Port Air Ambulance kit, an efficient and effective Medevac Kit Life Port Inc. is EASA recognised FAA Repair station; it has PMA, STC and TSO approvals from FAA.
  The Citation 560’s Interior and the kit is engineered to meet requirements of any medical mission (Casualty to Hospital Transfers).
  Medevac mission includes mechanisms like patient loading utility system, advance life support base unit, manual load system and Aero sled Stretcher for a smooth loading and ride for the patient.
   
  The Citation will also be used for Personalised VIP Air Charters. It is a solid, reliable private jet that can fly anywhere a mid-sized jet can go at the cost of light- jet travel.
   
  It’s comfortable and has a high performance speed of 850kph. Reliability of the Citation 560 Jet matches Cessnas highest standards in Private Jet Travel.
   
  It is spacious and can accommodate up to 8 passengers with great ease. Featuring a hot and cold beverage area, a well equipped mini bar, flushing toilet and a satellite phone (Aircel) and its baggage compartment is larger than other jets in its class.
   
  The Jet has 1900NM Range and Flies at FL410!

  For further information, 
  contact  Email: cmd@flightlink.co.tz
  Tel: +255 782 354448/9

  0 0  Meneja wa kinywaji cha Guinness.Davis Kambi akiongea.

   Meneja wa kinywaji cha Guinnes, Davis Kambi akipiga picha ya pamoja na washiriki wa shindano la Guinness Football Challenge wakati walipokuwa wakiagwa kwenye mgahawa wa City Sports Lounge Posta ,jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki .Washiriki hao wameondoka usiku wa kuamkia jana kuelekea nchini Afrika Kusini ambako watashiriki katika shindano hilo.
   Meneja wa kinywaji cha Guinnes, Davis Kambi akimkabidhi tiketi za ndege na hati za kusafiria kwa kiongozi wa  washiriki wa shindano la Guinness Football Challenge,Mohamed Kobembe kwenye hafla fupi iliyofanyika mwishoni mwa wiki ndani ya kiota cha maraha cha City Sports Lounge kilichopo katikati ya jiji la Dar.
   Meneja wa kinywaji cha Guinnes, Davis Kambi akitoa maelekezo machache kwa  washiriki wa shindano la Guinness Football Challenge,kwenye hafla fupi iliyofanyika mwishoni mwa wiki ndani ya kiota cha maraha cha City Sports Lounge kilichopo katikati ya jiji la Dar.
  Mmoja wa Wafanyakazi wa kampuni ya R&R,Peter Ngassa ambao ndio waratibu wa shindano la Guinness Football Challenge,akifafanua jambo kwa Wanahabari,kabla ya washiriki hao kukabidhiwa tiketi zao 

  0 0


  Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga 'Joe' pichani kushoto akichanganua jambo kwa Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti,Steve Gannon mara baada ya kutembezwa studio mpya na ya kisasa kabisa,iliyofungwa mjengoni humo,ambayo inatarajia kuanza kutumika hivi karibuni,Steve Gannon amefanya ziara fupi mwishoni mwa wiki na kutembelea vitengo vyote kampuni hiyo huku akijionea namna shughuli mbalimbali zinavyofanyika mjengoni humo.
  Steve Gannon akitazama picha za wasanii mbalimbali wa nje waliowahi kufika nchini Tanzania na kufanya maonesho yao kadhaa ndani ya ofisi za Prime Time Promotions Ltd.
  Mkurugenzi wa mambo ya utafiti na vipindi vya Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akifafanua jambo kwa Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti,Steve Gannon ambaye nae alikuwa akimsikiliza kwa makini.
  Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti,Steve Gannon akimuuliza jambo mtangazaji wa kipindi cha Power Breakfast,Gerald Hando kuhusiana na mambo mbalimbali ya kikazi,alipotembezwa kwenye studio ya ziada.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga 'Joe' pichani kushoto akifafanua jambo kwa Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti,Steve Gannon mara baada ya kufanya ziara fupi mwishoni mwa wiki na kutembelea vitengo vyote kampuni hiyo huku akijionea namna shughuli mbalimbali zikifanya mjengoni humo.
  Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti,Steve Gannon akizungumza jambo na baadhi ya wafanyakazi wa kitengo muhimu cha kampuni hiyo cha Masoko.
  Steve Gannon akisalimiana na Oparesheni Meneja wa Prime Time Promotions Ltd.Balozi Kindamba,mara alipotembelea ndani ya kampuni hiyo ambayo imekuwa ikijihusisha na matamasha mbalimbali likiwemo tamasha kubwa la Fiesta ambalo hufanyika kila mwaka.
  Steve Gannon akisalimiana na Gerald Hando
  Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti,Steve Gannon akioneshwa matoleo mbalimbali ya jariba la burudani la KITANGOMA linachapishwa na kampuni ya Prime Time Promotions.
  Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti,Steve Gannon akipeana mkono na Mmoja wa wafanyakazi wa Prime Time Promotions,Godliva Nicholaus mara alipowasili ndani ya ofisi za kampuni hiyo.
  Mkurugenzi wa mambo ya Masoko na Mauzo,Shebba Kusaga akifafanua jambo kwa Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti,Steve Gannon.
  Chief Editor wa Clouds TV,Bwa.Kanyopa akitoa maelezo mafupi kuhusiana na ufanyaji wao kazi ikiwemo na urushaji wa vipi kupitia Tv yao,Pichani kushoto ni Boss Joe akisikiliza kwa makini.
  Mkurungezi Mtendaji wa Kampuni ya bia ya Serengeti,Steve Gannon alitembezwa pia ndani ya chumba maalum cha kuandalia habari,hapa Mtangazaji wa kipindi cha Michezo Shaffih Dauda akifafanua jambo kwa Steve Gannon.

  Baada ya ziara kutembelea vitengo mbalimbali vya kampuni hiyo,pia Steve Gannon alipata wasaa wa kukaa meza moja na uongozi wa juu wa kampuni hiyo na kuzungumza machache,ikiwa ni sehemu ya mchakato wa ufanisi wa kikazi kwa mwaka mpya wa 2013. 

  0 0


  Prime Minister Mizengo Pinda cuts a ribbon to mark official opening of the first showroom in East Africa to stock BEKO products, a renowned electronic manufacturing brand from Turkey. The showroom which is housed at KIDA Plaza in Mikocheni B, Dar es Salaam is being managed by Modern Holdings (EA) Limited. On his left is Deputy Minister of Trade and Industry, Gregory Teu and on his left is Chairman of Modern Holdings (EA) Limited Anselm Minja followed by Ambassador of Turkey to Tanzania Ali Davutoglu.
  Prime Minister Mizengo Pinda shares a light moment with the Deputy Minister of Trade and Industry, Gregory Teu and Chairman of Modern Holdings (EA) Limited Anselm Minja after cutting a ribbon to mark official opening of the first showroom in East Africa which will stock and distribute BEKO products from Turkey. The showroom is which is housed at KIDA Plaza, Mikocheni B in Dar es Salaam will be managed by Modern Holdings (EA) Limited. 

  Director of sales for BEKO products, responsible Middle East, Africa and Turkic Republic, Murat Buyukerk shows Prime Minister Mizengo Pinda some of the products manufactured by the Turkish company shortly after Pinda launched the first showroom in East Africa which will stock and distribute BEKO products which is housed at KIDA Plaza in Mikocheni B, Dar es Salaam. The showroom is managed by Modern Holdings (EA) Limited. Right is Chairman of Modern Holdings (EA) Limited Anselm Minja.
   Lucky winners of a sweepstake which was done during the launch of the first showroom in East Africa which will stock and distribute BEKO products which is housed at KIDA Plaza in Mikocheni B, Dar es Salaam, poses for a group photo with some BEKO officials. Shop it stands for Modern Holdings (EA) Limited becomes the first in the East African region. The showroom is the first in East Africa is managed by Modern Holdings (EA) Limited.
   Director of sales of products AEG from Turkey Murat Buyukerk he showed Prime Minister Mizengo Pinda some products manufactured by the company immediately after the Pinda to launch the official shop of distributing products AEG lililofunguliwa in the building of Kida Plaza Mikocheni B, Dar es Salaam. Shop it stands for Modern Holdings (EA) Limited becomes the first in the East African region. Aliyefunga red eagle behind the Pinda is Chair of Modern Holdings (EA) Limited Anselm Minja.
   Director of sales for BEKO products, responsible Middle East, Africa and Turkic Republic, Murat Buyukerk shows Prime Minister Mizengo Pinda some of the products manufactured by the Turkish company shortly after Pinda launched the first showroom in East Africa which will stock and distribute BEKO products which is housed at KIDA Plaza in Mikocheni B, Dar es Salaam. The showroom is managed by Modern Holdings (EA) Limited. Right is Chairman of Modern Holdings (EA) Limited Anselm Minja.
  Prime Minister Mizengo Pinda discusses an issue with the Chair of Modern Holdings (EA) Limited Anselm Minja (left) during the launch of the first showroom in East Africa which will stock and distribute BEKO products which is housed at KIDA Plaza in Mikocheni B, Dar es Salaam.The showroom is managed by Modern Holdings (EA) Limited. Right is the Deputy Minister of Trade and Industry, Gregory Tue.
  Deputy Minister of Trade and Industry, Gregory Teu (left) inspects a TV set which was given to him as a gift after the launch of the first showroom in East Africa which will stock and distribute BEKO products which is housed at KIDA Plaza in Mikocheni B, Dar es Salaam. The showroom is managed by Modern Holdings (EA) Limited. On his left is BEKO Sales Director, responsible for Middle East, Africa and Turkic Republic Murat Buyukerk, followerd by the Chairman of Modern Holdings (EA) Limited Anselm Minja.  ========  ======  =======  ======


  BEKO extends its footprints to Tanzania, East Africa 

  By Correspondent.

  A renowned Turkish manufacturing company dealing with electronic appliances, BEKO has open its first showroom in the country in collaboration with Modern Holdings (EA) Ltd, making Tanzania a base for expansion of its footprints in East Africa.  

  While inaugurating the launch at KIDA Plaza in Mikocheni B, Dar es Salaam at the weekend, Premier Mizengo Pinda stressed the need to promote and strengthen the good bilateral relations between Tanzania and Turkey, making it more meaningful and beneficial. “We are determined to develop our bilateral relations with Turkey in every field and we are happy to see world class Turkish producers in our country,” said the PM.

  According to Premier, Turkey’s exports to Tanzania in 2011 were $170.7 million compared to $89.3 million posted in 2010. The top export categories were iron and steel ($63.1 million), petroleum products and related materials ($36.1 million), manufactures of metals ($11.1 million), commodities and transactions not classified elsewhere in the United States Standard International Trade Classification (SITC) ($8.2 million), paper or paperboard and articles of paper pulp ($7.1 million).

  While Tanzania’s exports to Turkey were $21.7 million in 2011, an increase of 52 per cent compared to $14.3 million in 2010. The top five export categories for 2011 were tobacco and tobacco manufactures ($13.2 million), transport equipment ($4.9 million), crude animal and vegetable materials ($1.2 million), textile yarn, fabrics, made-up articles and related products ($1 million), fish (not marine mammals, crustaceans, mollusc and aquatic invertebrates ($269,000).

  The trade surplus of goods with Turkey was $148.9 million in 2011, 50 per cent increase from $75.3 million in the previous year 2010. Prime minister called up on the Turkish companies to open more showrooms in Tanzania for their products in diverse cities like Arusha, Mwanza, Dodoma and Mbeya.

  He noted that the decision of BEKO to open showroom in the country is a clear sign of booming and constantly flourishing economy and standard of living in Tanzania, adding that this move will enable more Tanzanians to afford its products, hence, Turkey will continue to export more to Tanzania and Tanzanians will benefit more.

  However, Mr Pinda outlined challenges facing trade sector, including clearing of goods at Tanzania Ports Authority (PTA) and taxation issues under Tanzania Revenue Authority (TRA), saying the government is working hard to ensure a conducive environment for everyone doing business in Tanzania.

  He challenged Tanzania business companies to ensure they open showrooms for Tanzania products in Istanbul, Turkey, saying TCCIA, ministry of Industry, Trade and Marketing as well as Tanzania Investment Centre (TIC) can give guidance to businessmen to establish areas of interest.
  There is a big demand for showroom in Turkey such as in the country, he stressed.

  On his welcoming address, the Chairman of Modern Holdings East Africa Limited, Mr. Anselm Minja, who is the sole distributor of BEKO products in the region, mentioned that it is the aim of BEKO to establish a manufacturing plant in Tanzania, whose products will be exported to the neighbouring countries, hence making the products affordable to many consumers.   
    
  BEKO Sales Director for Middle East, Africa and Turkic Republic, Murat Buyukerk said, “We are active in more than 100 countries and become a choice of over 280 million people by our understanding of quality, high technology and smart solutions with our production plants in Turkey, Romania, Rusia and South Africa. We are targeting to become permanent in Tanzania and East Africa. We as BEKO & Grundig will be searching for opportunities of added value investments to Tanzania.”     

  On his side, Turkish ambassador to Tanzania, Mr Ali Davutoglu said there is enormous potential for greater bilateral cooperation between Tanzania and Turkey in areas such as trade, investments, joint business ventures and tourism, and Turkey is keen to further expand cooperation for the mutual benefit of the two countries.

  The envoy said the exchange of business and government delegations will go a long way in strengthening economic ties and promoting trade investment between the two countries.

  “I appreciate the Tanzania’s achievements in the field of economy, business and tourism. We will continue to support. BEKO’s effort is a transfer of technology and job creation in Tanzania,” he said.
  As bilateral ties forge ahead, people to people exchanges have become closer between the two countries, Mr Davutoglu concluded.

  0 0

  0 0


  Baadhi ya Wamiliki wa magazeti Tando walioko jijini Dar es Salaam, wakiwa katika picha ya pamoja walipokutana katika tafrija ya kuwaaga, ashiriki wa shindano la Guinness Football Challenge 2013. Kutoka kushoto ni Kassim Mbaruku, Fransic Dande, Josephat Lukaza, William Malecela, Ahmad Michuzi, John Bukuku, Henry Mdimu na Othman Michuzi ambaye amekaa chini ni Mroki Mroki a.k.a Father Kidevu.

  0 0


  WADAU wa muziki wa injili mkoani Tabora wamewaomba waandaaji wa tamasha la Pasaka nchini ambalo hufanyika kila mwaka kuhakikisha mwaka huu linafanyika mkoani humo.

  Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na kusainiwa na Samuel Ngosha kwa niaba ya mashabiki wa muziki wa injili mkoani Tabora, ilisema mwaka huu wameamua kupeleka mapema maombi kwa waandaaji ili tamasha hilo lifanyike mkoani humo.

  “Mikoa ya Mwanza, Dar es Salaam, Shinyanga na Dodoma imekuwa ikipewa kipaumbele sana katika tamasha, sasa tunawaomba waandaaji watukumbuke na sisi wa Tabora kwani pia ni mashabiki wakubwa wa muziki huo.

  Hata hivyo Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalii ya tamasha hilo, Alex Msama alisema wamekuwa wakipokea maombi mengi lakini bado hawajaanza maandalizi ya kulifanya.

  “Hatujakwenda hata kuomba kibali katika Baraza la Sanaa la Taifa, bado tupo katika mchakato wa kwenda kutafuta kibali, tukikipata mambo mengine yatafuata, kwa hiyo ni mapema sana kusema habari za tamasha, ila nikikutajia orodha ya mikoa inayoomba kuandaa utashangaa” alisema Msama.

  Tamasha la Pasaka mwaka jana lilifanyika Aprili 8, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ambapo miongoni mwa wasanii maarufu waliotumbuiza ni malkia wa muziki huo kutoka Afrika Kusini, Rebecca Malope.

  Wasanii wengine maarufu waliotumbuiza ni Rose Muhando, Solomon Mukubwa, Anastazia Mukabwa, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Christina Shusho, Atosha Kissava, Mwinjilisti Faraja Ntaboba, Ephraim Sekeleti, Maryanne Tutuma, kundi la Glorious Celebration na kwaya ya Kinondoni Revival.


  0 0

   Afisa Mwandamizi wa NSSF Kahama, Lusajo Enest (kushoto), akitoa elimu kuhusu mafao mbalimbali yanayotolewa na mfuko huo kwa wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu wakati wa Siku ya Wanafamilia.
   Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Taifa (NSSF) Kahama, Omari Mziya (kulia), akikabidhi hundi ya Milioni 2/- kwa Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa African Barrick Gold (ABG) Bulyanhulu, Dennis Hoof  ikiwa ni moja ya udhamini ya mfuko huo katika kufanikisha Siku ya Wanafamilia ya mgodi huo, iliyofanyika mgodini wilayani Kahama juzi. NSSF pia ilitoa jumla ya T-shirts 200.
  Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Taifa (NSSF) Kahama, Omari Mziya akizungumza kabla ya kukabidhi hundi.

  0 0

  Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Suleiman Kova akitoa maelezo kwa waandishi wa habari juu ya hatua zitakazochukuuliwa baada ya kupata taarifa hizo ambapo aliwaamuru wanafunzi hao wote kwapamoja kwenda Kigamboni kufuatilia tukio hilo kwa pamoja.

  Tunaimba! Tunavuka bure Tunavuka bure kwenye Pantoni.
  
  Pamoja na kutakiwa kupungua hapa wengine walizidi kuendelea kuingia na kukijaza kivuko hicho.

  Wanafunzi wa Chuop Cha Uongozi wa Fedha cha jijini Dar es Salaam (IFM) wakiwa mbele ya geti la Wizara ya Mambo ya ndani walipovamia leo majira ya saa nne nanusu asubuhi wakiwa na madai ya kutopewa ulinzi na jeshi la polisi kwenye makazi yao ya Hosteli za Kigamboni kutokana na kuvamiwa na majambazi mara kwa mara. Wanafunzi hao walidai siku ya Ijumaa walifanya kikao na jeshi hilo ili wawape ulinzi lakini suala la ajabu siku waliyofanya kikao na Jeshi hilo ndio siku waliovamiwa wenzao wawili wakiume na kubakwa hali iliyosababishwa wanafunzi hao kubakwa. Majambazi hao wamekua wakidai kupewa Laptop simu na fedha kama mwanafunzi akikataa humfanyia vitendo vya kulawiti.
  Ulinzi uliimarishwa nnje ya jengo la Wizara ya Mambo ya ndani kufuatia kadhia hiyo ya wanafunzi.

  Tembelea Libeneke la Mtaa kwa Mtaa Blog kwa picha zaidi


  0 0   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto Zanzbar Msham Abdulla Khamis akifungua mkutano wa tathmini ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2012  kwa niaba ya Waziri wa Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto Bi. Zainab Omar Mohammed leo mjini Zanzibar.Mkutano huo umewashirikisha viongozi na waratibu wa mbio za mwenge kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania bara na Zanzibar.
  Mwenyekiti wa mkutano wa tathmini ya Mbio za Mwenge wa Uhuru 2012 ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga (kulia) akiongoza mkutano huo leo mjini Zanzibar. Kushoto ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga  Ali Nassoro Lufunga mkoa ambao ulikua mwenyeji wa kilele cha mbio za Mwenge kitaifa kwa mwaka 2012.

   Baadhi ya washiriki wa mkutano wa tathmini ya Mbio za Mwenge mwaka 2012 wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa mkutano huo kuhusu , mafanikio, changamoto na namna ya kufanikisha shughuli za mbio za Mwenge nchini.
   Mratibu wa Mbio za Mwenge mkoa wa Iringa Bw. Atilio Mganwa akitoa mchango wake kuhusu uboreshaji wa shughuli za mbio za Mwenge nchini ambapo mkoa wa Iringa utakuwa mwenyeji wa kilele cha mbio za Mwenge kwa Mwaka 2013.
   Washiriki wa mkutano wa tathmini ya mbio za Mwenge mwaka 2012 kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania bara na Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo unaoendelea mjini Zanzbar. Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiendesha Kikao cha Muungano, kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar leo, Januari 14, 2013. Wa pili (kushoto) ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (wa pili (kulia) Ni Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (kushoto) ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samiah Suluhu na (kulia) ni Waziri wa nchi Ofsi ya Makamu wa pili wa Rais zanzibar, Mohamed Aboud. Picha na OMR
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Makamu wa pili wa Rais, Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, wakati Makamu alipokuwa akiendesha Kikao cha Muungano kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar leo, Januari 14, 2013.
   Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Sazi Salula (kulia) Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Eng. Ngosi Mwihava (katikati) na Mkurugenzi wa Muungano, Rajab Baraka (kushoto) wakifuatilia vifungu katika machapisho ya kujadili masuala ya Muungano, wakati wa kikao cha Muungano, kilichoendeshwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (hayupo pichani), kilichofanyika leo Januari 14, 2013, katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar. 

   Baadhi ya Mawaziri wakiwa ukumbini humo wakati wakifuatilia kikao hicho cha  Muumgano kilichoendeshwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (hayupo pichani), leo katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar.


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Samiah Suluhu, mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Muungano, kilichofanyika leo Januari 14, 2013 katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar. Picha na OMR.

  0 0

  Washiriki wa shindano la Guinness Football Challenge wakiwa katika picha ya pamoja tayari kwa ukaguzi wa kuingia Uwanja wa ndege wa Julius Nyerere kuelekea nchini Afrika ya Kusini kwa ajili ya kushiriki shindano la Guinness Football Challenge litalofanyika katika jiji la Johannesburg kwa muda wa siku kumi.      
   WASHIRIKI WAKIWA KATIKA HOTEL YA CITY INN KABLA YA KUANZA SAFARI YA KWENDA UWANJA WA NDEGE.
  Washiriki wa GFC wakihakiki nyaraka zao kabla ya kuondoka alfajiri kuelekea South Africa.

  0 0  Makamo wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Malim Seif Sharif Hamad amesema maoni yake juu ya madadiliko ya katiba ni maoni yake binafsi  kama Seif Sharif Hamad na kamwe yasihusishwe na chama chake wala serikali. Amesema maoni hayo hayawakilishi chama wala serikali kwani vyama na serikali vina nafasi yao maalum ya kutoa maoni yao.

  Hayo ameyasema leo huko Hoteli ya Bwawani wakati alipo kuwa na mkutano wa pamoja na wandisahi wa habari kuelezea yale aliyoyazungumza  na Tume ya kukusanya maoni  juu ya Katiba mpya  chini ya mwenyekiti wake Joseph Sinde Warioba yaliofanyika nyumbani kwake.

  Amesema kama ni mwananchi wa kawaida ameipongeza tume hiyo kwa kuweka utaratibu wa kusikiliza maoni hayo ambayo hapo baadae yatafanyiwa kazi kwa ajili ya kupata katiba ambayo  wananchi wanitaka.

  Ameongeza kuwa tume imetoa muongozo ambao wananchi wanaweza kujikita katika   maeneo makuu tisa yalio anishwa na Tume hiyo ambayo ni pamoja na Muundo wa Nchi na Taifa ndani ya Jamhuri ya  MuunganowaTanzania, mamboyenyewe ni HakizaBinadamu na Wajibu wa Wananchi,Ardhi,Maliasili,Mazingira,mihimili yaNchi,Watu,Utawala,Serikali,Bunge, Mahkama,Serikali za Mitaa, Muundo na Mamlaka yake,Vyombo vya Ulinzi na Usalama.

  Alisema yanapotazamwa kwa undani maeneo hayo itaonekana kwamba takriban mengi si mambo ya Muungano na hivyo hayawahusu wananchi wa Zanzibar ambao kwa mujibu wa Mkataba wa Muungano wa 1964 yanasimamiwa na Zanzibar yenyewe ambayo ina mamlaka kamili (exclusive jurisdiction) kuhusiana na mambo yote yasiyo mambo ya Muungano.

  Alisema maeneo ambayo yanaweza kuwahusu Wazanzibari kwa mfano misingi na maadili ya kitaifa, madaraka ya wananchi, mihimili ya utawala (Serikali, Bunge na Mahkama) na vyombo vya ulinzi na usalama, kuhusika kwao kutakuwa ni kwa kiasi kile yanapohusika na uendeshaji wa Muungano. “ Ndiyo kusema kwamba jambo lililo katikati ya mjadala kwa Wazanzibari katika mchakato huu ni Muungano wenyewe“alisema Malimu Seif.


  Mimi nimeamua kutoa changamoto kupitia waraka huu kwa kuitazama historia ya Muungano, jinsi ulivyoundwa, matatizo yanayoukabili, nafasi na hadhi ya Zanzibar katika Muungano na nini khatima ya Zanzibar na mustakbali wa Muungano katika mchakato huu tunaoendelea nao wa kupata Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano. Nitakayoyaeleza yanaweza yakaonekana ni machungu kwa wakati huu lakini yanaweza yakawa ndiyo ufumbuzi mjarab kwa siku zijazo”.

  Malimu seif ali ishukuru tume hiyo kufika kwake na kutoa mchango wake binafsi juu ya mchakato mzima wa ukusanyaji maoni kutafuta katiba mpya ya watanzania ifikapo 2014 mwaka ujao.

  Na Mwandishi wetu maelezo Zanzibar 14/1/2013

older | 1 | .... | 9 | 10 | (Page 11) | 12 | 13 | .... | 1898 | newer