Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

Waziri Mhagama azindua Bodi mpya ya NEEC

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Bi.Jennista Mhagama akisisitiza jambo katika kikao cha uzinduzi wa Bodi mpya ya Baraza la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi(NEEC). Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Dkt.John Jingu na kushoto ni katibu mtendaji wa NEEC,Bi.Beng’i Issa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Bi.Jennista Mhagama akikabidhi nyenzo za kazi kwa Mwenyekiti wa bodi ya Baraza la Uwezeshaji wananchi kiuchumi(NEEC), Dkt. John Jingu katika kikao cha uzinduzi wa bodi hiyo mpya ya Baraza. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na W,alemavu Bi.Jenista Mhagama akikabidhi nyenzo za kazi mmoja wa wajumbe wa Bodi ya Baraza la Uwezeshaji wananchi kiuchumi(NEEC), Prof.Samuel Wangwe katika kikao cha uzinduzi wa Bodi mpya ya Baraza hilo.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC),Bi.Beng’i Issa akizungumza jambo katika kikao cha uzinduzi wa Bodi mpya ya Baraza hilo. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Bi.Jennista Mhagama na wapili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya NEEC, Dkt. John Jingu


SERIKALI  imeridhishwa  na utekelezaji wa sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi na kuiagiza Bodi mpya ya Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kufanya kazi karibu na watendaji baraza hilo ili kufikia malengo yake.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Bi.Jennista Mhagama, amesema serikali ina imani kubwa na bodi mpya ya Baraza na hivyo kulitaka kutekeza majukumu yake kwa uwazi na ufanisi.
 “Jukumu lenu kubwa ni kushauri na kuelekeza utendaji wa majukumu ya Sekretarieti ya Baraza ili waweze kuchochea Uwezeshaji unaotekelezwa na taasisi za umma na zile zile za binafsi,”alisema Bi.Mhagama wakati akizindua Bodi mpya ya Baraza juzi jijini Dar es Salaam.
Waziri Mhagama alisema kuwa Serikali inaimani kubwa Mwenyekiti na Wajumbe wote wa Baraza na pasipo shaka  uzoefu wenu katika masuala mbalimbali ya Uwezeshaji yataiwezesha Serikali kufikia ndoto yake ya kuona Mwananchi amewezeshwa katika maeneo yote muhimu hasa katika uchumi.
 ”Dhana nzima ya Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya mwaka 2004 ni kuona kuwa sehemu kubwa ya uchumi wa Tanzania inamilikiwa na watanzania wenyewe,” alisema na kuongeza kuwa jukumu la bodi ni kuhakikisha nafasi kubwa ya uwezeshaji inatolewa kwa makundi yote hasa yale yenye uwezo mdogo na kuwapa nafasi zaidi wanyonge.
 Alisema yote haya yanawezekana tukishirikiana kwa pamoja katika kutekeleza azma ya serikali ya kukuza uchumi imara kwa wananchi unaoweza kuhimili ushindani katika soko la dunia katika mazingira ya utandawazi.
“Ni vizuri Baraza likawapa elimu  wananchi juu ya utunzaji fedha ili waweze kupata mitaji ya kuendeleza au kuanzisha miradi ya biashara kwani utunzaji fedha ni njia mojawapo ya kumkomboa mwananchi katika umaskini,” alisisitiza.
Waziri alilitaka Baraza kuandaa mfumo wa kufuatilia Maendeleo ya shughuli za kiuchumi na mfumo wa Menejimenti ya Habari za Uwezeshaji ili kuwa na taarifa sahihi katika maswala ya uwezeshaji nchini.
“Kupitia Madawati ya Uwezeshaji kuanzia Wizarani, Idara na Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa fuatilieni kwa ukaribu Taarifa za utekelezaji wa Miradi na Programu za Uwezeshaji kutoka katika Madawati hayo,” alisisitiza Bi.Mhagama
 Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya NEEC, Dkt. John Jingu alisema sera ya uwezeshaji italitekeleza kwa vitendo na kuhakikisha wananchi wanapiga hatua kiuchumi na nchi kufikia uchumi wa kati kama sera inavyoeleza.“Tutajitahidi kuwa wabunifu katika kutatua changamoto zitakazojitokeza ili kuhakikisha malengo ya serikali yanatekelezeka kikamilifu,” alisema Dkt. Jingu
Alisema ushirikiano ndio nyenzo pekee katika kufanikisha malengo ya serikali ya kuwawezeshaji wananchi kiuchumi  linafanikiwa kwa kiwango kikubwa.Naye Katibu Mtendaji wa NEEC, Bi.Beng’i Issa alisema mambo muhimu ambayo Waziri amesisitiza ni kufanya kazi kwa pamoja ili kuwafikia wananchi wengi zaidi hasa wanyonge.
“baraza litaendelea kuhamasisha na kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kujiunga na SACCOS na VICOBA pamoja na kuweka akiba pia kutengeneza mpango wa utekelezaji wa programu ya ushiriki wa watanzania katika uwekezaji(LOCAL CONTENT).

Kamati ya gesi, mafuta Tanzania Bara, Zanzibar kuundwa

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Mhandisi Kapuulya Msomba ( wa tano kushoto, waliokaa mbele) akielezea majukumu ya shirika hilo katika kikao cha Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Zanzibar, Salama Aboud Talib aliyeambatana pamoja na ujumbe.
Mkurugenzi wa Mkondo wa Chini wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dk Wellington Hudson akieleza jambo katika kikao hicho.
Kaimu Mkurugenzi wa Mkondo wa Juu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Venosa Ngowi akielezea shughuli za utafiti zinavyofanyika katika shirika hilo.
Kaimu Mkurugenzi wa Mkondo wa Juu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Venosa Ngowi akielezea shughuli za utafiti zinavyofanyika katika shirika hilo.
Kaimu Mkurugenzi wa Mkondo wa Juu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Venosa Ngowi akielezea shughuli za utafiti zinavyofanyika katika shirika hilo.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati, waliokaa mbele) na Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Zanzibar, Salama Aboud Talib ( wa pili kutoka kushoto, waliokaa mbele wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji kutoka Wizara husika.



Na Greyson Mwase, Dar es Salaam.

Wizara ya Nishati na Madini kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Zanzibar zinatarajia kuunda Kamati Maalum kwa ajili ya kuandaa Mpango wa ushirikiano kati ya Tanzania Bara na Zanzibar katika sekta za gesi na mafuta.

Hayo yalielezwa mwishoni mwa wiki na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo katika kikao chake na Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Zanzibar, Salama Aboud Talib aliyeambatana na Ujumbe wake.

Wengine waliohudhuria kikao hicho ni watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA) na Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta (PURA).

Profesa Muhongo alisema lengo la kamati hiyo ni kujadili maeneo ya kushirikiana pamoja na kubadilishana uzoefu katika sekta za gesi na mafuta

Alisema kuwa, kamati hiyo itashirikisha Wataalam kutoka katika taasisi za Sheria, Ardhi, Kodi, Gesi na Mafuta chini ya Makatibu Wakuu wa sekta husika kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.Waziri Muhongo alisema kuwa, uwepo wa kamati hiyo utachochea Zanzibar kuwa na taasisi kama TPDC na nyingine hivyo kupelekea ukuaji wa sekta ya gesi na mafuta.

Alisisitiza kuwa, Serikali ya Tanzania Bara kupitia Wizara ya Nishati na Madini ipo tayari kushirikiana na Serikali ya Zanzibar pamoja na kubadilishana uzoefu katika masuala ya gesi na mafuta.Profesa Muhongo alishauri Serikali ya Zanzibar kuandaa wataalam wa mafuta na gesi kwa kuwasomesha katika ngazi za diploma na shahada katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo cha Madini Dodoma (MRI).

Akiongeza kuwa, Serikali ipo tayari kutoa ufadhili kwa wanafunzi wa Zanzibar wanaofanya vizuri katika masomo ya Sayansi kwa ajili ya kusomea shahada ya uzamili katika vyuo vya ndani na nje ya nchi.Naye Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Zanzibar, Salama Aboud Talib, alimshukuru Waziri Muhongo kwa utayari wa Wizara ya Nishati na Madini katika kushirikiana na Wizara yake kwenye shughuli za mafuta na gesi

Alisema kuwa, kamati itakayoundwa itapelekea mambo kwenda kwa kasi na kuwa na data za pamoja zinazotokana na utafiti wa mafuta na gesi na kupanga Mikakati ya kuvutia wawekezaji kutoka nje ya nchi.

Kamati za Umoja wa Walimu na Wazazi wa Shule za Msingi Zarudisha Nidhamu Shuleni.

$
0
0
Lilian Lundo - MAELEZO

Kamati za Umoja wa Walimu na Wazazi (UWW) katika Shule za Msingi za Serikali nchini zimefanikiwa kudhibiti utoro, nidhamu na kutofanya vizuri kwa baadhi ya Wanafunzi katika shule hizo kwenye mitihani yao ya kumaliza Elimu ya Msingi. Lilian Lundo wa Idara ya Habari (MAELEZO) anaelezea.

Mwaka 2015 Serikali kupitia Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (Education Quality Improvement Programme –Tanzania (EQUIP-T), ilianzisha Kamati za Umoja wa Walimu na Wazazi (UWW) katika shule za msingi nchini kwa lengo la kujenga uhusiano mzuri kati ya Walimu na Wazazi ikiwa ni njia mojawapo ya kuinua ubora wa elimu.

Aidha, Kamati hizo zilipewa jukumu la kufuatilia maendeleo ya Kitaaluma kwa Wanafunzi, kubuni miradi mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya shule na kubuni klabu mbalimbali ambazo zitawashirikisha Wananfuzi katika kujadili masuala ya kijamii na hivyo kuwavutia Wanafunzi kupenda masomo.

Mpango huo ambao awamu ya kwanza ulianza katika mikoa ya Dodoma, Kigoma, Lindi, Mara, Simiyu, Shinyanga na Tabora, umeleta mafanikio makubwa kimaendeleo ya kitaaluma darasani, kuongezeka kwa nidhamu na kudhibiti utoro jambo ambalo pia limeongeza ufaulu katika mitihani yao ya Elimu ya Msingi.

Kwa mujibu wa wa Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Uhelela iliyoko Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma Bw. Dankan Kamwela, mpango huo umepata mafanikio makubwa katika shule yake ambapo imefanikiwa kupunguza utoro kutoka Wanafunzi 127 sawa na asilimia 30 kwa siku mwaka 2015 hadi Wanafunzi 12 sawa na silimia 8 kwa siku mwaka 2016.

Ameelezea kwamba, kwa kuitumia Kamati ya Umoja wa Walimu na Wazazi (UWW) wamekuwa wakifanya vikao mara kwa mara kwa kuwashirikisha Wazazi na Wanafunzi kujadili maendeleo ya Shule ikiwa ni pamoja na wajibu wa Walimu, Wazazi, na Wanafunzi kwa ujumla.

Amesema, kufuatia vikao hivyo ilibainika kuwa iko haja ya kuweka mikakati itakayosaidia kurekebisha kasoro zote zilizoonekana kuchangia kushuka kwa maendeleo ya kitaaluma, utoro na nidhamu ambavyo kwa pamoja vinasabisha kutofanya vizuri kwa Wananfunzi katika mitihani yao kwenye shule zilizo katika Kata hiyo. 

Kwa upande wake, Afisa Elimu Mkoa wa Mara Bw. Hamis Lissu amesema ufaulu wa darasa la saba mkoani humo umekuwa ukipanda mwaka hadi mwaka kuanzia mwaka 2014. Ameeleza kuwa mwaka huo mkoa wa Mara ulikuwa katika nafasi ya 25 kati ya mikoa 25. Mwaka 2015 mkoa wa Mara ulishika nafasi ya 17 kati ya 25 na mwaka 2016 umeshika nafasi ya 13 kati ya mikoa 26.

Mratibu Elimu Kata wa Chamwino, Chitema Simango amesema kuwa Kamati hiyo imewezesha kwa kiasi kubwa ushiriki wa Wazazi katika maendeleo ya shule ambapo kabla ya kuanzishwa Umoja huo Walimu walikuwa wakiachiwa ufuatiliaji wa maendeleo ya Wanafunzi pamoja na shule lakini kwa sasa Wazazi na Walimu wanashirikiana kwa katika kufuatilia maendeleo ya Wanafunzi na shule kwa ujumla.

Vile vile amesema kuwa UWW umeleta uwazi katika mapato na matumizi ya Shule ambayo yanabandikwa katika mbao za matangazo za shule husika na Wazazi wanapewa nafasi ya kuhoji juu ya mapato na matumizi hayo.

Aidha ametoa ushauri kwa Maafisa Elimu, Waratibu Elimu Kata na Walimu Wakuu katika mikoa ambayo bado haijaanzisha Kamati za UWW kuanzisha Kamati hizo katika shule zao ili kuleta mabadiliko ya uendeshaji wa shule za msingi za Serikali kwa kuishirikisha jamii. Kwani kupitia UWW Walimu na Wazazi wanajadiliana kwa pamoja na kukubaliana namna ya kuboresha taaluma ya Wanafunzi katika shule husika na hata katika kusimamia miradi ya shule.

Pia amesema kuwa Wazazi wanaposhirikiana na walimu inapelekea Wanafunzi kuwa na nidhamu ya hali ya juu kutokana na mwanafunzi asiye na nidhamu au mtoro anakosa pakukimbilia kwani mwalimu na mzazi wamekuwa kitu kimoja.

Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania (Education Quality Improvement Programme -Tanzania) EQUIP-T ni mpango unaosimamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kudhaminiwa na Serikali ya Uingereza. Mpango huu ni wa miaka minne ambao ulianza mwaka 2014 katika mikoa ya Dodoma, Tabora, Simiyu, Shinyanga, Kigoma, Mara na Lindi.

Mpango huo umejikita katika kuinu ubora wa Elimu Shule za Msingi katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo kwa walimu wa madarasa ya awali mpaka la tatu katika kuwajengea uwezo katika ufundishaji, utoaji wa vifaa vya kufundishia, uanzishwaji wa kamati za walimu na wazazi pamoja na mafunzo ya uongozi kwa walimu wakuu, kamati za shule pamoja na umoja wa walimu na wazazi.

Kaya 227 za wafugaji Simanjiro zanufaishwa na mradi wa maji kutoka TanzaniteOne

$
0
0
Wakazi wa Kijiji cha Losoito Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakiwa kwenye mradi wa bomba linalohifadhi maji yanayotumiwa na wanakijiji hao uliogharamiwa na kampuni ya TanzaniteOne, (kushoto) ni ofisa mahusiano wa kampuni hiyo Halfan Hayeshi.

Kaya 277 za wananchi 1767 wa Kijiji cha Losoito, Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wenye tatizo kubwa la ukosefu wa maji, wanatarajia kuondokana na changamoto hiyo baada ya kampuni ya TanzaniteOne kuwapatia maji.

Ofisa mahusiano wa kampuni ya madini ya Tanzanite ya wilayani humo TanzaniteOne Halfan Hayeshi alisema hivi sasa mradi huo umefikia asilimia 85 ili umalizike na kuzinduliwa ila wanachi wanapata maji.

Hayeshi alisema wananchi wa eneo hilo wanaendelea kupata huduma ya maji ila mradi kamili haujakamilika kwani wanahitaji kuweka mabomba urefu wa mita 500 ili kufikisha maji hayo karibu zaidi na jamii eneo la shule ya msingi Losoito.

“Tunatarajia kuweka mabomba ya urefu wa mita 500 ili kufikisha mradi huu karibu zaidi, ila hivi sasa wananchi wanapata huduma hiyo ya maji kwani awali tuliambiwa tufikishe mradi huo kwenye eneo la sasa ulipo,” alisema Hayeshi.

Alisema wanatarajia kuzindua mradi huo hivi karibuni baada ya kuwapa taarifa Katibu tawala wa mkoa huo Eliakim Maswi na mkuu wa wilaya hiyo Zephania Chaula, ambao ndiyo wataukabidhi kwa wananchi wa kijiji hicho cha Losoito.

Alisema mifugo na jamii ya eneo hilo hivi sasa wanafaidika na huduma hiyo ya maji na mara baada ya kununuliwa kwa rola sita za mabomba ya maji yatakayoweza kuwekwa katika mita 500 zilizobaki yatafika kwenye shule hiyo.

Ofisa mtendaji wa kijiji hicho Ngatayai Mollel alishukuru uongozi wa kampuni ya TanzaniteOne kwa kufanikisha mradi huo wa maji, utakaowasaidia wananchi wa eneo hilo, ambao kwa muda mrefu walikuwa wanakabiliwa na tatizo la maji.

Mollel alisema kijiji hicho kilichoanzishwa mwaka 2009 hivi sasa kina wakazi 1767 chenye kaya 277 kilikuwa na wakati mgumu wa kupata huduma ya maji ila hivi sasa wananchi wameondokana na changamoto ya maji iliyowasumbua.

Hata hivyo, alitoa ombi la wananchi wa eneo hilo kujengewa zahanati kwani inawalazimu kutembea umbali mrefu kupata huduma ya afya pindi wanapougua hivyo kuwa tatizo hasa kwa wanawake na watoto.

Mmoja kati ya vijana wanaolinda mradi huo wa maji ili mabomba yasiibiwe Daniel Solomon, alisema wamepeana zamu ya kulinda kila siku watu watatu ili miundombinu isiharibiwe na jamii ya eneo hilo ifaidike na maendeleo hayo.

“Wakina mama walikuwa wanatembea umbali mrefu wa kilomita 20 kila siku kwenda na kurudi mji mdogo wa Mirerani, kwa kutumia wanyamakazi punda, ila hivi sasa wanaondokana na tatizo hilo la muda mrefu,” alisema Solomon.

Vijana wajasiriamali watakiwa kutokata tamaa

$
0
0

Afisa masoko Airtel mkoa wa Arusha Geoffrey Sayore (kushoto) akipata maelezo juu ya faida za ng’ombe aliyewezeshwa kijana mjasiriamali anayejishughulisha na ufugaji Jonathan Tarimo (kulia) na Airtel kupitia mpango wake wa Airtel FURSA “Tunakuwezesha” baada ya kumtembelea katika Kijiji cha Migungani ‘B’ wilayani Monduli mkoa wa Arusha na kujionea maendeleo yake pamoja kupanga jinsi yakuboresha zaidi biashara yake.
Jonathan Tarimo (kushoto) kijana mjasiriamali anayejishughulisha na ufugaji akimwonyesha Afisa masoko Airtel mkoa wa Arusha Geoffrey Sayore (kulia) ndama wa mmoja wa ng’ombe aliyewezeshwa na Airtel kupitia mpango wake wa Airtel FURSA wakati Airtel ilipomtembelea ili kujionea maendeleo yake katika Kijiji cha Migungani ‘B’ wilayani Monduli mkoa wa Arusha.

 

Vijana wanaojishughulisha na ujasiriamali wametakiwa kutokata tamaa na matatizo mbalimbali wanayokumbana nayo wakati wa shughuli zao.wito huo umetolewa na mfugaji Jonathan Tarimo mkazi wa mkazi wa Migungani kata ya Mto wa Mbu wilaya ya Monduli mkoani Arusha anayejishughulisha na ufugaji

kijana huyo miezi mitano iliyopita aliwezeshwa kupitia mpango wa Airtel FURSA msimu wa pili kwa kupatiwa ng’ombe wawili, banda la kisasa na mafunzo ya biashara.Akiongea na maofisa wa Airtel waliotembelea katika mradi wake wa ufugaji ili kujionea maendeleo ya biashara yake alisema kwamba amepata matatizo katika shughuli yake baada ya ng'ombe aliyekuwa anampa maziwa kufa.

“nawashukuru sana Airtel kwa kunisaidia kufikisha hapa nilipo sasa, maana nlikuwa na ngo’mbe mmoja tu na Airtel kupitia Airtel Fursa kwa kunipatia ngombe wawili ambapo mmoja alizaa na nikawa nauza maziwa kwa wingi lakini baadae alifariki kutokana na ugonjwa. Kwahiyo nikawa nimebakiwa na ng’ombe wawili na ndama.

Kwa sasa ndama anaendelea vizuri na huyu ngo’mbe mwingine niliyewezeshwa anamimba. Kwasasa changamoto kubwa ni kutafuta chakula kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa nimekuwa nikienda umbali mrefu ili kupata chakula cha mifugo yangu”.

alisema, pamoja na adha aliyoipata, aliwaasa vijana wenzangu tusikate tamaa na kuendelea kutafuta fursa mbalimbali zitazoweza kufikisha katika malengo yao hata kama wakipata changamoto mbalimbali

Naye Afisa masoko Airtel mkoa wa Arusha Geoffrey Sayore alisema, Jonathan amekuwa ni mfano mzuri wa kijana aliyewezeshwa na Airtel FURSA na kuweza kupiga hatua kwenye biashara yake pamoja na changamoto mbalimbali zinazomzunguka.

Nawasihi vijana wanapopata fursa waweze kuzitumia vizuri ili ziwasaidie kuongeza kipato na kutoa ajira kwa jamii inayowazunguka. Lengo letu sisi Airtel ni kuhakikisha vijana wanafaidika na mradi huu wa Airtel Fursa na ndio maaana tunafanya ziara hii kutadhimini mafanikio , changamoto na maeneo ya kuwawezesha zaidi ili kuzifikia ndoto zao na kuwawezesha vijana wengi zaidi.

Airtel FURSA ni mradi wa kijamii kutoka Airtel Tanzania wenye lengo la kuwawezesha vijana wajasiriamali kwa kuwapatia vitendea kazi na elimu ya ujasiriamali ili kuboresha biashara zao.

VITUKO USWAHILINI: AVAA DERA LA MKEWE BAADA YA KUPIGIWA SIMU YA HELA!

$
0
0
Uswahilini ni sehemu ambayo inaongoza kwa vituko, ugomvi na maneno ya shombo. Wahenga  walisema kuishi kwingi ndio kuona mengi,  Haraka Haraka haina baraka  hii misemo inamaanaisha ukiishi sehemu tofauti tofauti utaona vitu vingi na kujifunza pia. Haraka haraka haina baraka hii imebeba maana ya kwamba ukienda haraka unaweza kukosea au kusahau kitu muhimu.


Tumia dakika zako chache kuitazma short video, ya uswahilini iliyo chezwa na Vicent Petro (Mr.Kilaka) Husina, Moses & Ziada Mgwassa (Zaydar). Endelea kusapport sanaa ya Tanzania tunaamini bila wewe hatuwezi fika popote thanks. Kwa maelezo na taarifa yeyote wasiliana nasi kwenye 0658161950.

MVUA YAWAATHIRI WANANCHI WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA

$
0
0


Mkazi wa Kijiji cha Ndubi kilichopo wilayani Rungwe mkoani Mbeya, Julius Mwambola (kulia), akionyesha migomba iliyoangushwa kutokana na mvua iliyonyesha wilayani humo mwishoni mwa wiki. Kulia kwake ni mke wake Nabwike Swebe.
Migomba ikiwa imeanguka kutokana na mvua hizo.

Mwanahabari Dotto Mwaibale, akichukua taarifa ya athari ya mvua hiyo kutoka kwa mkazi wa Kijiji cha Ndubi, Ambokile Mwangosi.

Nyumba ya Kikongwe, Gwanaloli Ndapapa ikiwa imeezuliwa paa na mvua hiyo ya upepo.
Kikongwe Maria Kamendu (85), akiwa ameshika paa la nyumba ya jirani yake Gwanaloli Ndapapa iliyobomolewa na mvua iliyonyesha mwishoni mwa wiki katika Kijiji cha Ndubi wilayani Rungwe mkoani Mbeya na kuharibu migomba na baadhi ya nyumba.


Dotto Mwaibale, Mbeya

WAKAZI wa Vijiji vya Ndubi, Mpuguso Kata ya Kisondela Tarafa ya Pakati wilayani Rungwe mkoani Mbeya wameathiriwa na mvua kubwa iliyoambatana na upepo ambayo imeezua baadhi ya mapaa ya nyumba na kuangusha migomba.

Akizungumza kuhusu tukio hilo mkazi wa Kijiji cha Ndubi, Ambokile Mwangosi alisema wamepata pigo kubwa kutokana na mvua hiyo iliyonyesha mwishoni mwa wiki kutokana na migomba mingi kuanguka hivyo kutishia tishio la njaa.

"Siwezi kuelezea kwa undani tathmini ya athari ya mvua hii lakini tumepata pigo kwani kaya nyingi migomba imeangushwa na mvua hiyo" alisema Mwangosi.Mkazi mwingine wa kijiji hicho Julius Mwambola alisema mvua hiyo imeangusha migomba yake 100 yenye thamani ya sh.250,000.

"Tumeathiriwa kwa kiasi kikubwa na mvua hii kwani mimi binafsi migomba iliyoangushwa na upepo wa mvua hiyo ni zaidi ya 100" alisema Mwambola.Mkazi mwingine wa Kijiji cha Mpuguso kitongoji cha Nkuju, Tulinagwe Naswila alisema mvua hiyo imeangusha migomba yake 40 yenye thamani ya sh.200,000.

Alisema mvua hiyo ilianza kunyesha saa saba mchana na ilidumu kwa muda wa saa moja na kuleta athari kubwa ya kubomoa baadhi ya nyumba na kuharibu migomba."Mvua ilikuwa kubwa ambayoiliharibu migomba na kuezua paa za nyumba kadhaa na kubomoa nyumba ya mjane mmoja aliyemtaja kwa jina la Gwanaloli Ndapapa (85).

Jitihada za kumpata Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Julius Chalya ili kuzungumzia suala hilo zilishindikana baada ya kupigiwa simu mara kadhaa bila ya kupokelewa.

WANAWAKE MKO WAPI UCHAGUZI MDOGO?

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.


Hivi karibuni Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilitangaza kufanya uchaguzi mdogo wa Ubunge pamoja na Udiwani kwa sehemu mbalimbali nchini ambazo viongozi wake wamefariki au wamepoteza sifa za kuendelea kuongoza wananchi katika sehemu husika.

Uchaguzi huo unategemewa kufanyika Januari 22 mwaka 2017 katika Jimbo la Dimani lililopo Zanzibar pamoja na Kata 20 ambazo zipo kwenye Halmashauri 19 za Tanzania Bara.

Mnamo Desemba 2016, NEC ilifanya uteuzi wa wagombea watakaogombea katika uchaguzi huo ambapo walioteuliwa kugombea Ubunge katika Jimbo la Dimani ni 11 ambao wote ni wanaume na kwa upande wa wagombea udiwani katika Kata mbalimbali za Tanzania Bara ni 71 ambapo wanaume ni 67 na wanawake ni watano.

Kwa kuangalia takwimu hizi chache tu zinatosha kutupatia majibu kuwa katika uchaguzi huu wanawake hawajajitokeza kabisa kugombea nafasi hizo wakati asilimia kubwa ya wanawake nchini wana sifa za kugombea nafasi hizo. Kwa uchaguzi huu wanawake wamewaangusha Watanzania wengi ambao wana amini kuwa wanawake wakipewa nafasi wanaweza kuzitendea haki.

Kumekuwa na wadau wengi duniani wanaotetea haki za wanawake kila kukicha kuhakikisha wanawake wanakuwa na haki sawa na wanaume kwenye nyanja mbalimbali zikiwemo za uongozi, kazi pamoja na elimu.

Pamoja na utetezi huo kushika kasi hadi kufanya jamii nzima kuamini kuwa wanawake wanaweza lakini bado wanawake wengi wanajirudisha nyuma kwa kutojiamini kama wanaweza kushika nyazfa mbalimbali za uongozi nchini.

Haina ubishi kuwa wanawake waliopata bahati za kuchaguliwa kuwaongoza wananchi katika sehemu mbalimbali wanafanya kazi nzuri katika kuhakikisha wananchi wao wanapata haki zao na kuishi maisha bora.

Kwa sababu uongozi ni kitu endelevu, nawashauri wanawake kutumia fursa ya sasa kujipanga vyema ili kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi ujao hivyo kuweza kuwaongoza wananchi na kufanya mageuzi makubwa yatakayoleta tija kwa nchi na kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye maendeleo.

Pia wanawake kutofikiria kushiriki nafasi za kuteuliwa peke yake badala yake wanatakiwa wawe mstari wa mbele kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ili kuwasemea wanawake wenzao katika nyanja mbalimbali kama vile Bungeni na katika Mikutano ya Kimataifa.

Wanawake wanamatatizo mengi ambayo yanahitaji kusemwa ili yaweze kutatuliwa. Matatizo hayo yametokana na mila na desturi ambazo zimekuwepo tangu enzi za mababu, ambazo ni ukeketaji kwa watoto wa kike, ndoa za utotoni, ukatili kwa wanawake, ubaguzi wa elimu kwa watoto wa kike na matatizo mengine mengi.

Matatizo hayo yote hayawezi kutatuliwa bila ushiriki wa wanawake katika nyazfa mbalimbali ambao watatumika kama daraja katika kuwakilisha matatizo yao hivyo kuwakomboa wanawake wenzao ambao bado wana mila na desturi za kizamani ambazo ni kandamizi kwa maendeleo yao.

TTCL yadhamini michuano ya vyuo Soka la Ufukweni

$
0
0



Mkuu wa Biashara Kanda ya Dar es salaam wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Jane Mwakalebela (wa tatu kushoto) akimkabidhi nahodha wa timu ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es Salaam (CBE), Ally Rabi (wa tatu kulia) fedha shs 600,000/- pamoja na laini za TTCL za 4G LTE zenye muda wa maongezi wa simu na intaneti (10GB) kwa muda wa mwezi mmoja baada ya kuibuka washindi wa Mashindano ya Mpira wa Miguu wa Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer'. CBE ilikifunga Chuo cha Ardhi mabao 2-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika Ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa timu ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es Salaam (CBE), wakiwa katika picha ya kumbukumbu na Mkuu wa Biashara Kanda ya Dar es salaam wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Jane Mwakalebela (wa nne kushoto) mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya fedha shs 600,000/- pamoja na laini za TTCL za 4G LTE zenye muda wa maongezi wa simu na intaneti (10GB) kwa muda wa mwezi mmoja baada ya kuibuka washindi wa Mashindano ya Mpira wa Miguu wa Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer'. CBE ilikifunga Chuo cha Ardhi mabao 2-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika Ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam.
Meneja Uhusiano wa TTCL, Nicodemus Mushi (wa pili kushoto mbele) akizungumza kwa niamba ya Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri W. Kindamba kwenye hafla ya uzinduzi wa mashindano ya Soka la Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer' yaliofanyika jijini Dar es Salaam kwenye ufukwe wa Coco Beach na kushirikisha vyuo mbalimbali vya jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Biashara Kanda ya Dar es Salaam wa Kampuni ya TTCL, Jane Mwakalebela akiwa katika uzinduzihuo.
Mkuu wa Biashara Kanda ya Dar es salaam wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Jane Mwakalebela (katikati) akimkabidhi kiasi cha fedha shilingi laki nne (400,000/-) pamoja na laini za TTCL za 4G LTE zenye muda wa maongezi wa simu na intaneti (5GB) kwa muda wa mwezi mmoja nahodha wa timu ya Chuo cha Ardhi (kulia) baada ya kuibuka washindi wa pili wa Mashindano ya Soka la Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer' yaliyoshirikisha vyuo mbalimbali vya jijini Dar es Salaam chini ya uratibu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF). Mashindano hayo yalifanyika Ufukwe wa Coco Beach jana. Kulia ni Bw. Dimo Dibwe muandaaji wa mashindano hayo.
Baadhi ya waamuzi wa Mashindano ya Soka la Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer' yaliyoshirikisha vyuo mbalimbali vya jijini Dar es Salaam wakijadiliana jambo kabla ya mechi kuendelea.
Mapambano mbalimbali ya mechi za Mashindano ya Soka la Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer' yakiendelea.
Mapambano mbalimbali ya mechi za Mashindano ya Soka la Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer' yakiendelea.
Mapambano mbalimbali ya mechi za Mashindano ya Soka la Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer' yakiendelea.
Mapambano mbalimbali ya mechi za Mashindano ya Soka la Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer' yakiendelea.
Wakati mashindano hayo yakiendelea wanafunzi wa vyuo waliendelea kujishindia zawadi mbalimbali. Kushoto ni Ofisa Masoko wa TTCL, Eric Muganda akimkabidhi vocha ya muda wa maongezi wa thamani ya shs10,000/- baada kushinda moja ya michezo iliyoambatana na zawadi kwa wanafunzi waliokuwa wakishiriki mashindano ya soka la ufukweni.
Baadhi ya timu zilizoshiriki Mashindano ya vyuo Soka la Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer' zikishangilia baada ya kushinda mechi za awali.
Mbwembwe za mabingwa...! Mabingwa wa Mashindano ya Vyuo Soka la Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer' wakiwa katika moja ya pozi mara baada ya kutangazwa kuwa mabingwa.
Kikosi cha Timu ya Chuo cha Ardhi ambao waliibuka washindi wa pili katika Mashindano ya Soka la Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer' yaliyoshirikisha vyuo mbalimbali vya jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa TTCL ambao ni wadhamini wa mashindano hayo.

KAMPUNI ya Simu nchini Tanzania (TTCL) imedhamini mashindano ya Soka la Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer' yaliozikutanisha timu za mchezo huo kutoka vyuo mbalimbali vya jijini Dar es Salaam. Akizungumza katika ufunguzi wa mashindano hayo jana jijini Dar es Salaam Meneja Uhusiano wa TTCL, Nicodemus Mushi kwa niamba ya Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri W. Kindamba alisema kudhamini kwa mashindano hayo ni mwendelezo wa kampuni hiyo kuiunga mkono Serikali kukuza michezo anuai nchini. 

Alisema TTCL inatambua kuwa michezo inamanufaa makubwa kwa jamii hasa kundi la vijana kwani licha ya kuwakinga na baadhi ya magonjwa na kudumisha ushirikiano baina yao, pia ni sehemu ya ajira ambayo imekuwa ikiwapatia baadhi yao vipato halali na kuendesha maisha yao vizuri. 

Alibainisha michezo ina faida nyingi ikiwemo kuwafanya washiriki kuwa watu wenye afya njema ya viungo mbalimbali vya mwili, afya ya akili na uwezo mkubwa wa kukabiliana na changamoto za maisha hivyo kujenga jamii ya watu wenye afya na furaha wakati wote jambo ambalo ni zuri kwa jamii nzima. "...Kimsingi kwetu TTCL ni siku muhimu ambapo kwa mara nyingine, tunaungana na Wanamichezo kufanikisha tukio hili kwa udhamini wetu wenye nia ya kuithibitishia jamii kuwa kampuni ya TTCL ni mali yao, ipo kwa ajili yao na inatimiza kwa vitendo mpango wake wa kuipatia jamii huduma bora za Mawasiliano ya simu na intaneti zenye kiwango cha juu kabisa cha ubora na gharama nafuu.

 "TTCL ni Wadau wakubwa wa sekta ya Michezo nchini. Wafanyakazi wa TTCL wanao utaratibu wa kushiriki michezo mbali mbali na mabonanza ya kila mara ili kujenga afya zao na kuongeza ushirikiano miongoni mwao. TTCL tunaamini kuwa, Michezo ni afya na kiungo muhimu cha mahusiano mema sehemu za kazi," alisema Mushi akimuwakilisha Kindamba katika uzinduzihuo. 

Aidha aliongeza kuwa tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa, watoto na vijana wanaoshiriki katika michezo mbalimbali katika shule zao hujiepusha na matumizi ya madawa ya kulevya, pombe, sigara na vitendo vya ngono ikilinganishwa na wale ambao hawajihusishi au kushiriki katika michezo, huku zikibaini wanafunzi wa kike wanaojihusisha na michezo katika ngazi mbali mbali za elimu kuwa na maendeleo mazuri ya kitaaluma jambo ambalo linapaswa kusisitizwa. 

Alisema TTCL inaahidi kuendelea kushirikiana na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo pamoja na Vyama vya Michezo na Vikundi mbali mbali katika kuendeleza sekta ya michezo. Ametoa wito kwa Wanamichezo na Wananchi kwa ujumla kuiamini kampuni hiyo ya kizalendo na kuiunga mkono kwa kutumia huduma na bidhaa za TTCL. "Nunueni laini za simu za TTCL, pigeni simu na kutuma ujumbe mfupi kupitia line hizi, nunueni vifurushi vya data vya TTCL ili muweze kuperuzi mitandaoni, mpate habari, elimu na burudani katika ubora na kasi ya hali ya juu.

 Hakika, TTCL imerejea, msisubiri kuhadithiwa, fanyeni maamuzi sasa. Hakikisheni kuwa mnakuwa miongoni mwa wale wanaofaidika na huduma bora za TTCL ambazo zina thamani halisi ya fedha zenu," Michuano hiyo iliyoratibiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) kupitia kocha wa taifa wa mpira wa ufukweni nchini ikiwa na lengo kupata wachezaji chipukizi wa mchezo huo ilishirikisha vyuo vya CBE, Chuo cha Ustawi wa Jamii, Chuo cha IFM, Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Chuo cha NIT, DIT, TIA, Chuo cha Kodi cha TRA -ITA na Chuo cha Ardhi. Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es Salaam (CBE) ndio kiliibuka washindi wa Mashindano ya Mpira wa Miguu wa Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer' yaliyoshirikisha vyuo mbalimbali vya jijini Dar es Salaam chini ya uratibu wa TFF.

Rais Dkt. Magufuli awasalimia wakazi wa Chato Mjini, pia atembelea Shule ya Msingi aliyosoma Chato

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika benchi la kibanda cha kupigia kiwi (Shoe Shine) pamoja na wakazi wengine wa Chato katika eneo maarufu kama Stendi za zamani Chato mkoani Geita. Kibanda hicho cha Kiwi ndicho Rais Dkt. Magufuli alichokuwa akisafishiwa viatu  vyake kabla ya kuwa Rais, pia ni sehemu ambayo alikuwa akipenda kukaa na  kubadilishana mawazo na wakazi wa Chato wakati akiwa mapumzikoni kipindi cha Nyuma.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Chato mkoani Geita. Shule hiyo ya Msingi Chato ndiyo Rais Dkt. Magufuli alisoma kuanzia darasa la kwanza mpaka Darasa la Saba. Rais Dkt. Magufuli amewaasa Wanafunzi hao kusoma kwa bidii kwasababu yeye pia alisoma shuleni hapo. Picha na Mpigapicha Maalum
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Chato mkoani Geita. Shule hiyo ya Msingi Chato ndiyo Rais Dkt. Magufuli alisoma kuanzia darasa la kwanza mpaka Darasa la Saba. Rais Dkt. Magufuli amewaasa Wanafunzi hao kusoma kwa bidii kwasababu yeye pia alisoma shuleni hapo. Picha na Mpigapicha Maalum.

WATAKAOZIDISHA NAULI ABIRI KUKIONA-SUMATRA TANGA.

$
0
0

MAMLAKA ya Usimamizi wa vyombo vya usafiri wa nchi kavu na Majini (Sumatra) mkoani Tanga kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani wameanza operesheni maalumu kwa madereva wanaozidisha abiria na nauli kwenye mabasi yanayotoka  mikoa mbalimbali ikiwemo kanda ya kaskazini.

Hatua inafuatia idadi kubwa ya abiria ambao wanatoka mikoa hiyo kurejea mkoani Tanga na maeneo mengine hivyo baadhi ya mabasi wanapandisha nauli kiholea na kuzidisha abiria.

Hayo yalisemwa na Ofisa Sumatra Mkoani Tanga, Dkt Walukani
Luhamba (Pichani Juu) wakati akizungumza na mtandao huo ambapo alisema waliamua operesheni hiyo ili kuweza kudhibiti masuala hayo ambayo yamekuwa yakiwapa wakati mgumu wananchi wanaotumia vyombo hivyo kwa ajili ya matumizi yao.

Operesheni hiyo inafanyika kwenye maeneo ya Mombo,Korogwe, Mkata na Segera ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha wanakabiliana na hali hiyo ili kuweza kuikomesha kwa madereva wenye tabia kama hiyo.

Dkt Walukani alisema katika kuhakikisha wanazibiti operesheni hiyo hivi sasa wanamshikilia dereva wa basi la Hood Issa Kayela (30) linalofanya safari zake kutoka mkoani Arusha kuelekea Mbeya anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika kituo cha Mkata wilayani Handeni mkoani Tanga kwa kosa la kuzidisha abiria zaidi ya idadi aliyotakiwa kubeba.

Alilitaja basi hilo lilikuwa na namba za usajili T.779 AVL Scania aina ya Torino lilikuwa likitokea mkoani Arusha kuelekea Mbeya ambapo baada ya kumkamata walimpelekwa mahakamani na baada ya kufika huko akukosa dhamana amerudishwa mahabusu na baade ya wiki mbili anatarajiwa kupandishwa kizimbani.

Akizungumza hatua inayofuata,Dkt Walukani alisema baada ya hapo dereva huyo kukaa kwenye kituo hicho kutokana na kukosa dhamana atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili na ikibainika anamakosa kutokana na sheria za Sumatra atafungwa mwaka mmoja au miwili jela.

“Ukiangalia basi hilo la hood lilikuwa linapaswa kupakia abiria 51 lakini lilipokamatwa eneo la mkata wilayani Handeni  lilikuwa na abiri 80 jambo ambalo ni hatari sana “Alisema.

 “Kutokana na hali hiyo dereva wa basi hilo alipelekwa mahakamani na alikosa dhamani na hivi sasa anashikiliwa kwenye kituo cha Polisi Mkata kwa ajili ya kufikishwa mahakamani na ikithibitisha ana kosa basi atalazimika kwenda Jela mwaka mmoja au miwili hii itakuwa fundisho kwa madereva wengine wenye tabia kama hii “Alisema.

Dkt Walukani alisema baada ya hapo dereva huyo alikaa kwenye kituo hicho baada ya kukosa dhamana atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili na ikibainika anamakosa kutokana na sheria za Sumatra atafungwa mwaka mmoja au miwili jela.

Naye kwa upande wake, Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoani   Tanga, Nassoro Sisiwayah alisema operesheni hiyo itakuwa endelevu kwa kufanyika kwenye maeneo mbalimbali mkoani Tanga ikiwemo Mombo, Korogwe, Mkata na Segera lengo kubwa kuhakikisha sheria za usafirishaji zinafuatwa.

Alisema katika operesheni hiyo wanazibiti nauli kwenye mabasi y mikoani ambayo hivi sasa kwa asilimia kubwa watu wengi wanarudi kutoka mikoa ya kaskazini ambapo ulanguzi wa nauli umekuwa ukitumika.

Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha Blog

SERIKALI YATAKIWA KUJIPANGA KATIKA UJIO WA VIWANDA –TPSF

$
0
0
 
.Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Sekta Binafsi Nchini (TPSF), Godfrey Simbeye akizungumza na waandishi habari juu ujio wa viwanda 200 vya China kuhamishiwa Nchini iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Kitengo cha Masuala ya Uwekezaji na  Maendeleo  ya Biashara wa TPSF, Edward Furaha akizungumza na waandishi habari juu ujio wa viwanda iliyofanyika  jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye.
 
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

MFUKO wa Sekta Binafsi nchini (TPSF) umesema ujio wa viwanda 200 kutoka nchini China,Serikali inatakiwa kujipanga kupokea viwanda hivyo kwani vitachangia kukua kwa uchumi pamoja na ajira nchini.
 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye amesema China kwa sasa ni nchi yenye mitaji mikubwa kuliko nyingine duniani hivyo lazima kuongeza mahusiano zaidi ili kuweza kunemeeka  nao katika kuelekea uchumi wa kati wa viwanda kufikia 2025.
 
Simbeye amesema viwanda vingi vya China vimefikia hatua ya kuweza kuhamishwa katika sehemu mbalimbali katika Bara la Afrika na kuendelea na uzalishaji kutokana na uhakika wa rasilimali watu pamoja na malighafi.

Amesema  kutokana na uwekezaji wa viwanda hivyo suala la maeneo tengefu  liangaliwe kimkakati   katika kufanya maandalizi  ya viwanda hivyo pamoja na vingine vitakavyojengwa.Simbeye amesema nchi ya China ina uwezo mkubwa wa mitaji kuliko maeneo mengine duniani na Tanzania inaelekea katika uchumi wa viwanda  zilizowawezesha  kufanya mapinduzi ya viwanda.
 
Aidha amesema ujio wa Waziri wa Mambo ya Nchi wa China nchini  ni sehemu ya kuchangamkia fursa kwa karibu kwa kuongeza uhusiano uzidi kudumu ambao wenye maendeleo baina ya nchi mbili.
 

MWAKYEMBE ATEMBELEA MAHAKAMA MAALUM YA RUSHWA NA UHUJUMU UCHUMI

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe akiangalia chumba cha kuendeshea kesi katika mahakama ya makosa ya rushwa na uhujumi uchumi alipoitembelea leo
 Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe akiangalia chumba cha kuendeshea kesi katika mahakama ya makosa ya rushwa na uhujumi uchumi alipoitembelea leo
  Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe akimsikiliza kaimu mkuu wa mahakama hiyo Kanda ya Dar es Salaam Mhe. Jaji Winnie Koroso alipokuwa akiatoa taarifa ya utendaji wa mahakama hiyo  alipoitembelea leo
 Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza baada ya kufanya ziara katika Mahakama malum ya makosa ya Rushwa na Uhujumu uchumi Kanda ya Dar es Salaam leo
Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe akiangalia kitabu ambacho huingizwa orodha ya mashauri yaliyofunguliwa katika Mahakama maalum ya makosa ya rushwa na ufisadi alipoitembelea leo.



Waziri wa mambo ya katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe ametembelea Divisheni Maalum ya Mahakama inayojishughulisha na makosa ya rushwa na uhujumu uchumi nchini Kanda ya Dar es Salaam na kujionea namna inavyoendesha shughuli zake.

Akizungumza katika ziara hiyo Waziri Dkt Mwakyembe amewataka watendaji wa mahakama hiyo kuzingatia lengo la uanzishwaji wa mahakama hiyo ili kuleta tija na ufanisi uliofanywa kuanzishwa kwake.

“Mahakama hii ni chombo maalum kilichoundwa ili kushughulikia masuala ya rushwa na uhujumu uchumi ndani ya muda mfupi, nyinyi kama watendaji hamna budi kuongeza bidii na kuhakikisha mashauri yote yanayoletwa katika mahakama hii yanamalizika ndani ya muda mfupi huku mkizingatia haki za kila mmoja na hivyo kufanikisha lengo la kuanzishwa kwake ”,alisema Dkt Mwakyembe

Aidha alisema uanzishwaji wa mahakama hiyo ulilenga kuifanya Tanzania kupunguza utendaji wa makosa ya aina hiyo au kuyamaliza kabisa na kuongeza kuwa kwa hali ilivyo sasa inaonekana kuwa uhalifu wa aina hiyo umepungua.

Kutokana na kupungua kwa makosa hayo mhe. Waziri alisema anafikiria kuandaa mpango wa kupunguza kiwango cha gharama za makosa ambayo yatapelekwa mbele ya mahakama hiyo . “Inaonekana yale makosa ya ufisadi mkubwa hakuna kwa sasa na hili no moja ya lengo la kunazisha mahakama hii na kwa hali hiyo nafikiria kuja na mpango wa kupunguza kiwango cha thamani ya makosa ambayo kitakuwa ni chini ya kile kilichowekwa awali cha sh. Bilioni moja,” alisema Dr. Mwakyembe.

Akizungumza katika kikao hicho Kaimu Mkuu wa Mahakama hiyo Maalum Mhe. Jaji Winnie Korosso alisema mahakama hiyo ina uwezo wa kupunguza kiwango cha thamani ya makosa husika yanayopaswa kupelekwa na kuongeza kuwa mahaklama hiyo pia inao uwezo wa kusikiliza kesi zote zinazohusiana na nyara za serikali bila ya kujali thamani yake.

“Mahakama hii inao uwezo wa kupunguza kiwango cha thamani ya mashitaka yanayoletwa hapa, pia ijulikane wazi kuwa mashitaka yote yanayohusu nyara za taifa yanaweza kuletwa katika mahakama hii wakati bila ya kujali thamani yake,”alisema Mhe. Koroso 

Akiongelea utendaji kazi wa mahakama hiyo Mhe Jaji Koroso alisema mpaka sasa mahakama hiyo imeshasikiliza maombi ya dhamana tisa ambapo sita yameshafanyiwa kazi na maombi mengine yanaendelea kushughulikiwa. 

Amesema mahakama hiyo iko katika kanda zote 14 za Mahakama Kuu nchini na hivyo mashauri yanayostahili kusikilizwa na mahakama hiyo yanaweza kupokelewa na kusikilizwa nchi nzima kupitia kanda hizo na sio kwam,ba iko Dar es Salaam pekee.

Aliasema kwa kuwa mahakama hiyo ni maalum mashauri yanayopelekwa yanatakiwa yawe yamemalizika ndani ya miezi tisa (9) na hivyo hazina budi kuendeshwa kwa haraka ili kufanikisha lengo la kusikilizwa kwa haraka na hivyo kusaidia taifa.

UZINDUZI WA MRADI WA UJENZI WA MIUNDOMBINU MAENEO HURU YA UCHUMI FUMBA.

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein na Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa wakifungua pazia kama ishara ya Uzinduzi wa Mradi wa Ujenzi wa Miundombinu katika maeneo huru ya Uchumi huko Fumba Wilaya ya Magharibi "A" Mkoa Mjini Magharibi leo, sambamba na uwekaji wa jiwe la msingi nyumba za kuishi katika shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar(Picha na Ikulu)

RAIS MAGUFULI KUFANYA ZIARA MKOANI SIMIYU

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) katika mkutano aliotisha kwa lengo la kuwajulisha ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli mkoani Simiyu.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtakakatika Mkutano aliotisha kwa lengo la kuwajulisha ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mkoani Simiyu.

Na Stella Kalinga, Simiyu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli anatarajia kufanya ziara ya siku mbili Mkoani  Simiyu, kuanzia tarehe 11/01/2017 hadi tarehe 12/01/2017.

Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake leo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka amesema, Tarehe 11/01/2017 Rais Magufuli ataweka jiwe la Msingi katika Hospitali ya Mkoa wa Simiyu katika Mtaa wa Nyaumata Halmashauri ya Mji wa Bariadi na kufungua barabara ya Lamadi-Bariadi.

Mtaka amesema baada ya kuweka jiwe la msingi la Hospitali ya Mkoa na kufungua barabara ya Lamadi–Bariadi Mhe. Rais atazungumza na  wananchi wa Bariadi katika Uwanja wa Shule ya Msingi Somanda, mahali lilipo jiwe la ufunguzi wa barabara hiyo.

Aidha, Mtaka ameongeza kuwa Siku ya tarehe 12/01/2017 Mhe.Rais atatembelea kiwanda cha kutengeneza Chaki kilichopo Wilayani Maswa na baadaye ataweka jiwe la msingi katika barabara ya Mwigumbi-Maswa ambapo pia atazungumza na wananchi wa Wilaya ya Maswa.

“Kwa niaba ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu,napenda kuwaalika wananchi wote wa mkoa wetu kujitokeza kwa wingi kumlaki na kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli katika maeneo yote atakayopita”  amesema Mtaka.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA

$
0
0
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, SACP Ahmed Msangi

Watanzania Tumuunge Mkono Rais Magufuli Kujenga Uchumi Wa Viwanda

$
0
0
Katika hotuba yake ya kwanza Mhe.  Rais  wa Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akifungua Rasmi Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alisema kwamba Serikali yake itaweka mkazo mkubwa katika ujenzi wa Viwanda.

“Viwanda tunavyovikusudia ni vile ambavyo sehemu kubwa ya malighafi yake itatoka ndani, hususani kwenye sekta za kilimo, mifugo, uvuvi, madini na maliasili nyingine,” alifafanua Rais Magufuli

Viwanda hivyo  vitatakiwa kuzalisha bidhaa ambazo zitatumiwa na watu wengi nchini kama vile nguo, viatu, mafuta ya kupikia ili kuwa na uhakika wa soko la ndani kabla ya kufikiria soko la nje.

Licha ya Serikali kuweka mkazo katika uanzishwaji wa viwanda nchini lakini bado watanzania wamekuwa na fikra potofu juu ya bidhaa zinazotengenezwa ndani ya nchi, wengi wao wanashusha thamani ya  bidhaa hizo na kuziweka katika  kundi la bidhaa zisizo na ubora huku wakikimbilia bidhaa za nje ya Tanzania.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango alipotembelea maonyesho ya Viwanda yaliyofanyika  kuanzia tarehe 07  hadi 11 Desemba 2016 alisema kwamba Tanzania haitaweza kuwa Tanzania ya Viwanda ikiwa watanzania wenyewe hawathamini bidhaa zinazotengenezwa ndani ya nchi.

Dkt. Mpango alitoa mfano wa mashine zinazotengenezwa na SIDO ambazo zimekuwa zikidharaulika kwamba hazina ubora wakati huo huo mashine hizo zimetengenezwa kwa kuzingatia mazingira ya nchi yetu na gharama yake ni ya chini ukilinganisha na zile zinazotengenezwa nje ya nchi.

“Haiwezekani hata jembe la mkono liagizwe toka nje wakati kuna viwanda ndani ambavyo vinauwezo wa kutengeneza majembe katika kiwango cha juu.” Alisema Dkt. Mpango.

Ni muda wa watanzania kubadilika na kuunga mkono Serikali ya Awamu ya Tano kwa kununua bidhaa zinazotengenezwa ndani ya nchi ili kuipeleka nchi kuwa na uchumi wa viwanda hatimaye kufikia uchumi wa kati.

Kamwe Tanzania haitaweza kufikia uchumi wa viwanda ikiwa sisi wenyewe tunakimbilia bidhaa zinazotoka nje ya Tanzania.

Ifike hatua tuone bidhaa zetu ni bora zaidi kuliko bidhaa kutoka nje ya nchi. Nchi nyingi zimeendelea kutokana na kuthamini bidhaa ambazo zimekuwa zikitengenezwa ndani ya nchi.

Mfano ni Nchi ya Japan, ambayo imekuwa ikifanya vizuri katika uchumi wa viwanda, mafanikio hayo yametokana na wajapani wenyewe kutokana na imani ambayo wamejiwekea kwamba hakuna bidhaa inayotengenezwa Dunia yenye ubora zaidi ya bidhaa zinazotengenezwa nchini kwao.

Kwa kupenda bidhaa zinazotengenezwa ndani kutaamsha morali kwa uanzishwaji wa viwanda vingi hapa nchini, kwani watu wengi wamekuwa wakihofia kuanzisha viwanda vidogo vidogo kwa hofu ya kukosa masoko ya bidhaa zao na wengine wakihofia gharama ya uanzishwaji wa viwanda.

Ambapo wengi wetu tumekuwa tukitafsiri kiwanda kama ni kuwa na mashine kubwa, zenye gharama kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa mbalimbali, na kusahau kuwa kiwanda kinaweza kuundwa kwa kuwa na cherehani nne tu.

Hivyo basi, kwa kuwa na cherehani nne peke yake, tayari watu wanne wanakuwa wamepata ajira na kujikomboa kiuchumi.

Hivyo uchumi huu wa viwanda ni fursa kubwa kwa vijana katika kutengeneza ajira badala ya kusubiri ajira kutoka Serikalini au Mashirika Binafsi.

Ambapo Mhe. Rais katika hotuba yake ya kufungua Bunge la 11 alisema kuwa ifikapo mwaka 2020 idadi ya ajira itokanayo na viwanda ifikie asilimia 40 ya ajira zote zitakazokuwepo nchini wakati huo.

KARIMJEE JIVANJEE FOUNDATION REWARDS YOUNG SCIENTISTS 2016

$
0
0
Diana Sosoka and Nadhra Mresa (All photos: Daniel Mbega of MaendeleoVijijini Blog)

Diana and her father, Sosoka Paul
Young Scientists Tanzania (YST) Executive Director, Dr Gozbert Kamugisha
Dr Kamugisha with scholarships
Diana Sosoka, Nadhra Mresa and their teacher Mr Rashid Namila.




By Daniel Mbega of MaendeleoVijijini Blog.


Dar es Salaam: THE Karimjee Jivanjee Foundation (KJF) has rewarded Diana Sosoka and Nadhra Mresa from Mtwara Girls Secondary School for being overall winners of the Young Scientists Tanzania (YST) Awards in 2016.

Speaking at a press event to send off the winners to Dublin, Ireland, the KJF Team said the winners would receive scholarship from the foundation to study at any local university when they complete their high school education.

They both take a combination of Chemistry, Biology and Geography and aspire to be medical doctors.The students are travelling to Dublin today to attend the BT Young Scientists and Technology Exhibition, an Irish annual school students’ science competition, which aims at encouraging interest in science in primary, and secondary schools.

Speaking at the event, the students thanked their school teacher, Mr. Rashid Namila their Biology teacher, whom they said has been a fundamental to their success.They also thanked the YST, led by Dr. Gozbrt Kamugisha, and the KJF for making their dreams come true.

“Our innovation was based on a locally made incubator to help the women around our school to raise chicken after seeing them come to our school every day to seek for leftovers sue to the poverty situation that has engulfed them,” they said, adding that their technology has inspired various people around Mtwara and across the country to go and learn.

Ms. Eliavera Timoth, the Foundation’s Deputy Marketing Manager, speaking on behalf of KJF Manager Ms. Devota Rubama, said KJF was a non-governmental organization that was registered in 2009 and commenced its operation in 2010 with commitment to support the Tanzanian community, specifically improving education sector.

“The education sector is the core charity notably by providing scholarships to young Tanzanians to be able to accomplish their studies at university level,” she was quoted as saying, adding that the scholarships were provided to students under the category of science in an effort to join hands with to government initiatives, targeting on encouraging students to pursue science subjects.

“We are eager to ecourage and support Tanzania young students to be able to develop various innovative skills through science for the betterment of the nation,” she said.

Speaking of the YST scholarships, Ms. Eliavera said since 2012 the Foundation has provided 17 scholarships to students in the categories of overall winners and winners in special school in need.

“Every year KJF provide 4 schholarships to winner of YST awards to study at university level. We have already provided scholarships to students from Kibosho Secondary School (2012 – 3 scholarships overall winners); Ilongelo Secondary School of Singida (2013 – 2 overall winners scholarships); and Fidel Castro –Pemba (2013 – 2 special school in need scholarships),” Ms. Eliavera said.

Other scholarships were Lumumba Secondary School – Zanzibar (2014 – 2 overall winners); Ngongo Secondary School – Lindi (2014 – 2 special school in need scholarships); Mzumbe Secondary School – Morogoro (2015 – 2 overall winners); Nasa Secondary School – Simiyu (2015 – 2 special school in need); Mtwara Girls (2016 – 2 overall winners); and Binza Secondary School – Simiyu (2016 – 2 special school in need scholarships).

However, Ms. Eliavera said, KJF is planning to launch a dual Masters’ degree in African Cinservation at the University of Glasgow, Scotland and Nelson Mandela University – Afican Institution of Science and Technology in Arusha.

The programme, according to her, is for two years and KJF will provide three scholarships for students to study two terms at Glasgow University and eight terms at Nelson Mandela University.


“The Foundation has been giving scholarships to Doctors to graduate for a Masters’ degree programme in Paediatric Oncology at Muhimbili University of Health and Alllied Sciences (Muhas), two doctors graduated in 2015 and one in 2016,” Ms. Eliavera said.


The Honorary Chairman of Karimjee Jivanjee Group of Companies in Tanzania, Hatim Karimjee said: “We are very honoured to support the Young Scientists Tanzania Award because we believe that education is very important to the future development of Tanzania, and also because science education in particular can open opportunities for higher level career development.”


KJF is the primary vehicle for the Karimjee family’s charitable work.


The mission of the Foundation is to invest in education as a means to enhance the economic development of Tanzania.

At present, many young Tanzanians continue to benefit from scholarships from KJF, which enable them to follow their dreams and to make a greater contribution to Tanzania as a result of their education.

In addition to these scholarships, the Foundation also supports Read International and others; works with Wonder Workshop and is working to boost the capacity for management of pediatric oncology in Tanzania.

Hatim Karimjee said, although KJF’s main focus at the moment is funding educational institutions to improve education capacity, the Karimjee family established several charitable trusts in the 1950’s before independence.

“We have built many schools, hospitals, dispensaries, mosques and community centres. The most famous of our donations is the Karimjee Hall. We built and donated this building to the Dar es Salaam Municipal Council in 1957 as a Town Hall. It was later adapted to become the official seat of Parliament. Independence was declared in Karimjee Hall on 9th December 1961,” he said.

Other important donations by the Karimjee family have been the Usagara Secondary School in Tanga (Formerly Karimjee Secondary School), the Karimjee Clin in Mnazi Mmoja – Dar es Salaam, the old Karimjee Hospital in Zanzibar and the recent donation of 100 desks to Mkwakwani Secondary School in Tanga, a donation that was made to support the Government’s effort to offset the existing countrywide shortage of desks in primary and secondary schools.

The Karimjee Jivanjee Foundation is funded by donations from Toyota Tanzania, one of Tanzania’s biggest and compliant taxpayers, which is celebrating its 50th anniversary as the sole and authorized Toyota distributor in Tanzania since 1965.

(Prepared by www.maendeleovijijini.blogspot.com)

MBUNGE COSATO CHUMI: UMEME CHANZO CHA KUDHOROTESHA HUDUMA BORA ZA AFYA KATIKA JIMBO LA MAFINGA MJINI

$
0
0
 Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi kulia akisikiliza kilio cha wafanyakazi wa zahanati na vituo vya afya alipotembelea kujionea na kusikiliza changamoto za huduma za afya katika jimbo lake ili kuzitafutia ufumbuvi na kuboresha huduma hiyo.

Na fredy mgunda,Iringa
MBUNGE wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi alifanya ziara ya kuzitembelea zahati,vituo vya afya na hospitali za jimbo hilo kwa lengo la kujionea changamoto za kiafya. 

Akiwa katika ziara hiyo alikumbana na changamoto ya kukosekana kwa umeme katika baadhi zahati za jimbo hilo na kuahidi kulipeleka tatizo hilo bungeni ili litafutiwe ufumbuzi mapema.

Akizungumza na blog hii Chumi alisema tatizo la umeme katika vituo na zahati ni kubwa hivyo inahitajika nguvu ya ziada kutatua tatizo la umeme ili kuboresha afya za wananchi wake pamoja na huduma ya mama na mtoto.

“Hii inasikitisha sana hebu angalia zahati zinavifaa vyote mhimu ila umeme ndio tatizo hatuwezi kupata huduma bora kama hakutakuwa na umeme tunaelekea bungeni nitaenda kuongea na waziri husika ili kutatua changamoto hii” alisema Chumi

Aidha mh chumi alisema kuwa anapenda kuhakikisha kuwa umeme wa REA awamu ya tatu unazifikia zahati zote pamoja na vijiji husika kwa kuwa serikali inalengo la kusambaza umeme vijiji vyote nchi nzima hivyo hata vijiji vya jimbo la Mafinga Mjini vimo katika mpango huo.

Nao baadhi ya Wananchi walimpongeza mbunge huyo kwa kazi kubwa anayoifanya kuwaletea maendeleo katika jimbo la Mafinga Mjini ndani ya mwaka mmoja tu amefanya vitu vingi vizuri tofauti na matarajio ya watu wengi.

“Angalie nyie waandishi wa habari Mbunge Cosato Chumi kwa mwaka moja tu ametengeneza barabara karibi a zote za jimbo huku nyingine zikiwekwa rami,amehangaikia swala la maji tunaona matumaini,swala afya ndio kafanya vitu vingi,michezo ndio mechi zinaendelea na mambo mengine mengi huyu mbunge ni wakuigwa kwa juhudi zake” walisema wananchi

Wananchi hao waliongeza kuwa swala la umeme mbunge wetu ametueleza vizuri sana hivyo tunaimani ya maneno na vitendo yake kuwa analishughurikia kwa umuhimu mkubwa.

Baadhi ya madiwani wa jimbo hilo walisema kuwa kuwa mbunge huyo amekuwa akiwasaidia kutatua changamoto nyingi za kitendaji na kuifanya kazi yetu ya udiwani kuwa rahisi kutokana na mambomengi anayafanya mbunge wetu Cosatio chumi.

“Tunamshukuru Mbunge wetu kwa kuwasaidia wananchi taa za sola kwa vijiji ambavyo havina umeme hizo ni juhudi zake binafsi na sio hilo kafanya mambo mengi sana hadi sasa tunajiona tupo kwenye halmashauri kongwe kumbe ni halmashauri mpya” walisema baadhi ya wadiwani 

Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Mafinga Charle Makoga amesema kuwa changamoto ya umeme ni kubwa katika vijiji ambavyo havipokupata umeme wa REA awamu ya kwanza na pili na ndio sababu inayosababisha huduma za kiafya kudorola katika baadhi ya vijiji.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMANNEJANUARI 10, 2017

Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images