Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1090 | 1091 | (Page 1092) | 1093 | 1094 | .... | 1898 | newer

  0 0

  0 0


  Wakwanza kushoto ni ndugu Amin Mongi,akifuatia na  pili kushoto ni Katibu wa Arusha Press Club(APC) ndugu Amir Mongi (bwana harusi mtarajiwa)akiwa na mkewe mtarajiwa ,Wa kwanza kulia  bi Millen Amin ,siku ya sendof Jijini Arusha.Picha na Vero Ignatus Blog


  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Vifaa vipya vya kufanyia kazi katika Bandari ya Malindi Mjini Unguja leo ikiwemo  Makontena ya mizigo mizito wakiwepo na Viongozi mbali mbali,  ikiwa ni shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
  ruge-1
  Vifaa vipya vya kufanyia kazi Bandarini ikiwemo Makontena ya mizigo mizito inayowasili katika Bandari ya Malindi Mjini Unguja,leo vimezinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)  katika  shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. 
  ruge-2
  Vifaa vipya vya kufanyia kazi Bandarini ikiwemo Makontena ya mizigo mizito inayowasili katika Bandari ya Malindi Mjini Unguja,leo vimezinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)  katika  shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ikulu.
  ruge-3
  0665 ///// Vifaa vipya vya kufanyia kazi Bandarini ikiwemo Makontena ya mizigo mizito inayowasili katika Bandari ya Malindi Mjini Unguja,leo vimezinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)  katika  shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ikulu.
  ruge-4
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji Mhe,Ali Abeid Amani Karume,alipowasili katika Bandari ya Malindi Mjini Unguja  katika Uzinduzi wa  Vifaa vipya vya kufanyia kazi Bandarini ikiwemo Makontena leo,ikiwa ni shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(katikati) Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe,Ayoub Mohamed Mahamoud,[Picha na Ikulu.
  ruge-5
  0729 ////// Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Cpt.Abdalla Juma,alipowasili katika Bandari ya Malindi Mjini Unguja  katika Uzinduzi wa  Vifaa vipya vya kufanyia kazi Bandarini ikiwemo makontena ya mizigo mizito leo,ikiwa ni shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
  ruge-6
  1086 /// Baadhi ya Viongozi wa Serikali waliohudhuria katika Uzinduzi wa Vifaa vipya vya kufanyia kazi Bandarini ikiwemo makontena ya mizigo mizito leo,ikiwa ni shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
  ruge-7
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akipata bmaelezo kutoka kwa  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Cpt.Abdalla Juma,kuhusu utendaji wa Vifaa vipya vya kufanyia kazi katika    Bandari ya Malindi Mjini Unguja  mara baada ya Uzinduzi uliofanyika leo,ikiwa ni shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
  ruge-8
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwasha   Mashine ya Reach Stacker yenye uwezo wa kunyanyua Tani 45  wakati alipokuwa akikagua  Vifaa vipya vya kufanyia kazi   katika Bandari ya Malindi Mjini Unguja  mara baada ya Uzinduzi rasmi alioufanyika leo,ikiwa ni shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,[Picha na Ikulu.] 04/01/2017. 

  0 0   Katika Karne ya sasa vijana wengi wamekuwa na tabia ya kutafuta uhodari  wa nani zaidi kwenye tasnia ya mapenzi,  hivyo wakati kijana anapo jikita kwenye mapenzi kama unavyo jua mapenzi yalivyo na nguvu,  anashindwa kuvumilia na kujiwekea misimamo yaani kutulia na msichana ambaye tayari kamfanyia uchunguza wenye kina.

  Tamaa! ni mbaya, kupenda sio vibaya ila unapaswa kufanya uchunguzi kabla ya kupenda na sio kutamani! Ili ujue  ulipo penda ni sahihi au laa!. Unaweza kupenda ulipo tamaniwa  shida ndipo huanza, sio hivyo tu unaweza ukapenda mzuka /jini/shetani nk. Mwishowake huwa ni majuto.

  Kumbuka umakini na msimamo katika mapenzi  vinamsaada mkubwa sana katika karne hii (usipende usicho kijua) Ukitazama hiki kipande cha video kilicho andaliwa 2017 na Vicent Petro  a.k.a Mr. Kiraka, Ziada Mgwassa a.k.a “Zaydar”  & Moses,  utajifunza kuwa sio kila kinacho ng’aa ni dhahabu!. Tunaomba support yako kwenye video hii ili iwafikie walengwa wetu! Asante.   0 0


  .Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jaffo akizungumza na watumishi wa afya katika Hospitali ya Mkuranga mapema jana alipofanya ziara katika Wilaya hiyo .
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jaffo akipata maelezo ya Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega juu ya wananchi kulalamikia upatikanaji wa dawa katika Hospitali ya Mkuranga katika Mkutano wa hadhara uliofanyika hivi karibuni.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jaffo akielezwa na mgonjwa, Emiliana shila aliyefika katika Hospitali Mkuranga akiwa na vifaa Tiba na Dawa alizoambiwa akanunue nje mapema jana.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jaffo akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga jana  alipofanya ziara katika Wilaya hiyo
  Mbunge wa Mkuranga , Abdallah Ulega akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga leo katika ziara Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jaffo.
  Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Hassan Sanga akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga leo katika ziara Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jaffo.
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jaffo akiwasili katika Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga ikiwa ni ziara ya yake kuangalia utoaji wa huduma katika hospitali hiyo.
  Wafanyakazi wa Halmashauri ya Mkuranga pamoja wajumbe wa Baraza la Madiwani wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Selemani wakati ziara aliyoifanya leo. picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
  Muonekano wa Wodi ya Wazazi Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga ambapo Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jaffo alifnya ziara jana .
  Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jaffo akiwa na kitabu cha stakabadhi za malipo ambazo kwa sasa hazitumiki katika sehemu za huduma za serikali leo anaeshuhudia tukio hilo ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mkuranga, Juma Abeid (kulia).


  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  NAIBU Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jaffo amemuagiza Katibu Tawala Mkoa wa Pwani kuunda Tume ya kuchunguza upotevu wa fedha za dawa katika Hospitali ya Mkuranga, Mfumo wa ukusanyasaji wa mapato kwa kutumia stakabadhi.

  Jaffo ametoa agizo hilo wakati alipokutana na watendaji wa Halmashauri ya Mkuranga leo, amesema serikali ilitoa sh. milioni 258 kwa ajili ukarabati wa Hospitali kati ya hiyo , Sh. milioni 86 ya kununulia dawa lakini dawa zilizonunuliwa katika Hospitali hiyo ni za sh. Milioni 22 na fedha iliyobaki haina majibu

  Amsema wananchi wanahitaji dawa kutokana na fedha wanayochangia katika huduma ya afya kukosa dawa kwao suala ambalo sio matarajio yao.
  Jaffo amesema kuwa ukusanyaji mapato katika hospitali ya Mkuranga sio mzuri kutokana na kutumia mfumo makaratasi ikilinganishwa na sehemu nyingine kutokana na kutumia mashine za Kieletroniki.

  Amesema Hospitali ya Mkuranga inakusanya mapato ya sh. Milioni 2.7 kwa mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana sh. milioni 2.1 ambapo ongezeko lake ni sh. 600, 000 wakati Hospitali zingine zinakusanya zaidi ya sh. milioni 20.

  Mwitikio wa kufika kwa Naibu Waziri Jaffo kulitokana na ombi la Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega ambaye alifanya ziara katika vijiji 90 na malalamiko ya wananchi ni ukosefu wa dawa katika Hospiali ya Wilaya, Vituo vya Afya pamoja na Zahanati.

  Hata hivyo, Jaffo ametoa agizo la Kisima cha Mwarusembe ndani ya siku tatu awe amepata majibu ya kuridhisha kutokana wananchi kukosa maji kwa muda mrefu. Nae Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega amesema wananchi wanaweza kuondokana na tatizo la kukosa dawa kutokakana watendaji kufuata taratibu za uombaji

  0 0

   
  Na Abel Daud,KIGOMA 

  Kupitia jitihada za zinazofanywa na Asasi,taasisi,makampuni na watu binafsi,kwa kuunga mkono juhudi za Serikali kwa lengo la kukamilisha huduma mbalimbali kwa Umma ,Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma amepokea jumla ya mataili 05 yenye thamani ya shilingi millioni mbili na laki nane ili kuboresha gari la polisi la kituo cha Nguruka kata ya Nguruka wilayani Uvinza.

  Akipokea mataili hayo yaliyotolewa na kanisa la Pool of Sloam,kwa niaba ya Naibu kamishina wa polisi Mkoani Kigoma,Ferdinand Mtui,mkuu wa polisi wilaya ya Uvinza Amedeus Malenge amesema kuwa kitendo kilichofanywa na kanisa hilo kitasaidia kuifikia jamii kwa wakati hasa wahalifu.

  Kwa upande wake Kuhani UFAHAMU HAKIKAZI ambaye alimwakilisha kiongozi mkuu wa kanisa hilo hapa nchini,amesema kuwa baada ya kupata taarifa ya uhitaji wa mataili hayo,kanisa limechukua hatua hiyo kwa kuwa kanisa na Serikali hufanya kazi pamoja katika kukamilisha huduma za kijamii.

  Aidha kuhani.HAKIKAZI ameongeza kuwa ,kupitia mahitaji ya kuboreshwa kituo cha polisi kilichopo kijijini humo,amesema kuwa amelichukua na atalifikisha kwa uongozi wa kanisa ili kuona namna linavyoweza kufanyiwa ufumbuzi wa kuboresha kituo hicho.

  Nao viongozi wa kijijini humo akiwemo mwenyekiti wa kijiji cha nguruka Bw.Mosha Mohamed na mwenyekiti wa kitongoji cha nguruka kusini Hamis Kiliza,wamesema kuwa kwa kuwa huduma ya polisi inauhitaji mkubwa kwa jamii,mataili hayo yatasaidia kupunguza uhalifu kwa kuwa kazi sasa zitafanyika kwa wakati huku wakiomba kuboreshwa tena kwa kituo hicho cha polisi kwa kuwa sasa hakitoshi kutoa huduma kulingana na wingi wa wahalifu wanaowekwa ndani ya kituo hicho.
   Kuhani Ufahamu akipeana mkona na Mkuu wa Polisi wilaya ya Uvinza mara baada ya kumkabidhi mataili hayo.
    Wakijadili.jambo nje ya kituo hicho cha polisi Nguruka
  Matairi hayo yaliyokabidhiwa katika kituo hicho cha polisi Nguruka


  0 0


  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa na viongozi waandamizi wa CCM katika boti ya wakati wakiwa safarin kwenda Zanzibar kwenye uznduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Dmani, mkoa wa mjini Magharibi, leo. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole na kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstafu Lubinza na Katibu wa NEC Oganaizesheni Muhammed Seif khatib
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa na viongozi waandamizi wa CCM katika boti wakati wakiwa safarin kwenda Zanzibar kwenye uznduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Dmani, mkoa wa mjini Magharibi, leo. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole na kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstafu Lubinza na Katibu wa NEC Oganaizesheni Muhammed Seif khatib
  Msaidizi wa Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Msami akiwa na Msimamizi Mkuu wa Blog ya Taifa ya CCM, Ndugu Nkoromo, katika boti wakati wakienda Zanzibar na Viongozi hao.

  0 0

  Baada ya kusomewa taarifa ya mkoa wa Ruvuma na mkuuwa mkoa huo Dokta Binilith Mahenge katika ikulu ndogo ya Songea , Waziri mkuu wa Jamhuri ya Tanzania Kassim Majaliwa akatoa maagizo matatu ambayo ambayo mkoa wa ruvuma unatakiwa kuyatekeleza. Kwa undani wa habari hii hii hapa video yake.

  0 0

   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  na mkewe Mery Majaliwa wakiweka shada la maua katika kaburi la aliye kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali Kapteni  Kenan Mhaiki  aliyefariki tarehe 31/12/2016 na kuzikwa tarehe 4/1/2017 kijijini kwao Matogoro Mkoani Ruvuma
   Waziri mkuu Kassim Majaliwa  akitoa salamu za serikali katika misa ya kumuombea marehemu Kapteni Kenan Mhaiki iliyofanyika katika kanisa la Jimbo kuu Katoliki la Songea  Parokia ya Mtoto Yesu  Matogoro, Songea
   Mjane wa Marehemu  Kapteni Kenan Mhaiki  akiweka shada la maua katika kaburi la mume wake
   Watoto wa Marehemu Kapteni Kenan Mhaiki wakiweka Mashada ya maua katika kaburi la Baba yao

  Jeneza lenye mwili wa marehemu Kapteni Kenan Mhaiki wakati wa misa ya kumuombea katika kanisa la Jimbo kuu Katoliki la Songea  Parokia ya Mtoto Yesu  Matogoro, Songea. Picha na Chris Mfinanga

   
  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameongoza mamia ya wakazi wa mji wa Songea na kata ya Matogoro kuuaga mwili wa aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA), Kapteni Keenan Mhaiki katika ibada iliyofanyika kwenye parokia ya Mt. Teresia wa Mtoto Yesu iliyoko Matogoro, mjini Songea.

  Waziri Mkuu ambaye ameshiriki msiba huo kwa niaba ya Serikali, pia alishiriki mazishi ya Kapteni Mhaiki ambaye pia alikuwa rubani wa ndege za Serikali yaliyofanyika kwenye makaburi ya parokia ya Matogoro.

  Akizungumza kwenye ibada ya mazishi mara baada ya kutoa heshima za mwisho, leo jioni (Jumatano, Januari 4, 2017), Waziri Mkuu aliwasilisha salamu za rambirambi kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli na Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan.

  “Msiba huu ni wetu sote na umetugusa wote. Ni msiba mzito kwa wanafamilia na kwa Serikali pia. Kapteni Mhaiki amekuwa rubani wa ndege za Serikali kwa muda mrefu na amewaendesha viongozi wa kitaifa kuanzia awamu ya kwanza hadi awamu ya tano. Kwa niaba ya Serikali tunawapa pole sana,” amesema.

  “Ninawaomba wafiwa wote hasa mke wa marehemu na watoto tushikamane katika kipindi hiki na tuendelee kuwa wavumilivu huku tukimuombea Baba yetu apate pumziko la milele,” amesema.

  Kapteni Mhaiki alifariki dunia Desemba 31, 2016 katika hospitali ya Agha Khan jijini Dar es Salaam. Alilazwa katika hospitali hiyo, kabla ya sikukuu ya Krismasi, kwa ugonjwa wa saratani ya ini.

  (mwisho)

  IMETOLEWA NA
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  JUMATANO, JANUARI 4, 2017.

  0 0
  Afisa Uhusiano Airtel Tanzania Jane Matinde akizungumza na waandishi wa habari juu ya kuanza kwa kliniki ya mpira wa miguu ya Airtel Rising Stars inayoshirikisha wachezaji nyota 65 waliochaguliwa kutoka katika msimu wa sita wa michuano hiyo, cliniki ya mafunzo inategemea kuanza wiki ijayo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa maendeleo wa soka la vijana Ayoub Nyenzi.
     Mkurugenzi wa Ufundi TFF Salum Madadi akiongea na waandishi wa habari wakati wa kutangaza kuanza kwa kliniki ya Airtel Rising Stars wiki ijayo jijini Dar es Salaam, kliniki hiyo itashirikisha wachezaji nyota 65 waliochaguliwa kutoka katika msimu wa sita wa michuano hiyo. Kulia ni kocha wa timu ya taifa ya vijana Oscar Milambo, wa pili kulia mwenyekiti wa maendeleo wa soka la vijana Ayoub Nyenzi na Afisa Uhusiano Airtel Tanzania Jane Matinde.
  Kocha wa timu chini ya miaka 17 Oscar Milambo akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza kuanza kwa kliniki ya soka ya Airtel Rising Stars inayoshirikisha wachezaji nyota 65 waliochaguliwa kutoka katika msimu wa sita wa michuano hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa maendeleo wa soka la vijana Ayoub Nyenzi, na wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Ufundi TFF Salum Madadi na kushoto Afisa Uhusiano Airtel Tanzania Jane Matinde.
   

  Kliniki ya soka ya Airtel Rising Stars iyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa inatarajiwa kuanza Jumatatu, Januari 16 kwenye uwanja wa Karume huku wavulana 40 na wasichana 25 waliofanya vyema kwenye michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars 2016 wakishiriki. Kufanyika kwa kliniki hiyo kutakuwa ni hitimisho ya michuano ya Airtel Rising Stars msimu wa sita.

  Kliniki hiyo itakuwa ya siku sita na itaendeshwa na makocha wa timu ya soka ya taifa Oscar Milambo akisaidiwa na Kim Paulsen kwa wavulana huku wasichana wakifundishwa na kocha mkuu wa Kili Queens Sebastian Nkoma.

  Akizungumzia maandalizi ya kliniki hiyo, Mwenyekiti wa Maendeleo ya soka la vijana kutoka Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF), Nyenzi Ayoub alisema “kliniki hiyo itatoa fursa kwa vijana kujifunza mbinu mpya za mpira, na kupata mafunzo kutoka kwa makocha wazoefu ili kuongezewa vipaji vyao. ‘Sisi TFF tumefanya maandalizi yote ya kliniki na tumeichukua kwa uzito wa hali ya juu kwa kuwa ndio njia sahihi ya kupata wachezaji wa timu zetu za taifa, Serengeti Boys na Taifa Queens’, alisema Ayoub.

  Tunaamini ya kwamba kliniki haitakuwa na mafanikio kwa wachezaji tu bali na timu zetu kupata wachezaji walio bora. Tumekuwa tukishuhudia wachezaji wazuri wenye vipaji kwenye kila msimu wa Airtel Rising Stars. Nachukua nafasi hii kuzishauri klabu zetu za mpira wa miguu kujitokeza kuangalia wachezaji wakati wa siku sita za kliniki hii ya Airtel Rising Stars, aliongeza Ayoub.

  Kwa upande wake, kocha mkuu wa timu ya Taifa ya vijana chini wa umri wa miaka 17 Oscar Milambo alisema, ‘Wachezaji watafundishwa nidhamu ya mpira, ndani na nje ya uwanja, jinsi kumiliki mpira mbele ya mchezaji wa timu pinzani, kutoa pasi za uhakika pamoja na mafunzo ya nadharia. Sambamba na hayo wachezaji pia watakuwa na fursa ya kukutana na wenzao na hii itakuwa na hamasa kwao kwani wengi wao itakuwa mara ya kwanza kupata mafunzo kutoka kwa makocha. Milambo aliongeza kuwa vijana hao watafundishwa jinsi mchezaji anavyotakiwa kujitunza kwa manufaa ya kuendelea kutunza kipaji chake.

  Akizungumza juu ya kliniki hiyo, Afisa Uhusiano Airtel Tanzania Jane Matinde alisema michuano ya Airtel Rising Stars 2016 imekuwa na mafanikio makubwa na kuwa kufanyika kwa kliniki kutahitimisha Airtel Rising Stars msimu wa sita na kufungua pazia kwa maandalizi ya Airtel Rising Stars msimu wa saba. Michuano ya Airtel Rising Stars mwaka 2016 tuliunganisha na promosheni ya kampuni ya Airtel ya ‘Airtel Fursa’ ambayo ni maalum kwa kuwawezesha vijana kufanikisha malengo yao.

  Matinde aliongeza kuwa Airtel inajivunia kuwa sehemu ya mradi huu wa kukuza vipaji vya soka kwani imesaidia kubadilisha soka la Tanzania. Airtel Rising Stars inalenga kutafuta vipaji chipukuzi kuanzia ngazi ya chini mpaka ngazi ya Taifa, kampeni yetu ya Airtel Fursa inalenga kuwainua vijana na kuwawezesha kufikia ndoto zao inaenda sambamba na program hii ya Airtel Rising Stars na tunajisikia furaha kuendelea kuwafikia vijana katika Nyanja mbalimbali aliongeza Matinde.

  Wachezaji zaidi ya 1000 wavulana na wasichana walishiriki kwenye michuano ya Airtel Rising Stars 2016 kutoka mikoa ya Mwanza, Morogoro, Mbeya, Arusha, Kinondoni, Ilala, Temeke,Lindi na Zanzibar.

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiongea na wazee wa kimila kutoka koo tano mkoani Mara ambapo amewapongeza kwa kazi ya kuelimisha jamii inayowazunguka juu ya madhara ya ukeketaji kwa watoto wa kike na tohara mara mbili kwa watoto wakiume, Katikati ni Mtumishi Jukwaa la Utu wa Mtoto(CDF) Bi. Kambibi Kamugisha, kushoto ni Katibu Tawala Tarime Bw. John Marwa na Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Watoto kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi.Margareth Mussai.
  Mzee wa Kimila kutoka Koo ya Bukira Mzee Sinda Nyangore akiongea na na Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga ambapo alishauri serikali na mashirika mengine kutoa elimu katika vipindi vyote vya mwaka na kuacha utaratibu wa kutoa elimu katika msimu wa ukeketaji kwenye koo mbalimbali.
  Mzee wa Koo ya Bukenye Mzee Elias Maganya akiongea na Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga ambapo alimuomba Katibu Mkuu kuangalia uwezekano wa kuwezeshwa kutembea Koo hadi Koo kwa ajili ya kuelimisha jamii kuhusu madhara ya ukeketaji.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiwa katika picha ya pamoja na wazee wa kimila kutoka koo tano za Bukenye,Nyabasi,Bukira,Butimbaru na Buhunyaga leo Mjini Tarime
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiongea na watoto wa kike walio katika mradi unaotekelezwa na Jukwaa la Utu wa Mtoto(CDF) wa kuwawezesha kijasiriamali watoto waliokimbia vitendo vya ukeketaji.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiagana na watoto wa kike walio katika mpango wa kuwezeshwa kijasiriamali na Jukwaa la Utu wa Mtoto(CDF)
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Jukwaa la Utu wa Mtoto(CDF) na watoto wakike walio katika mradi huo.

  Na Hassan Silayo-MAELEZO

  Wazee wa Kimila kutoka Koo Tano Mkoani Mara wamemuomba Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga kuwawezesha kutembea Koo hadi Koo kwa ajili ya kuelimisha jamii kuhusu madhara ya ukeketaji.

  Akiongea wakati walipokutana na Katibu Mkuu aliyepo Wilayani Tarime Mzee wa Koo ya Bukenye Mzee Elias Maganya alisema kuwa walishapata elimu kutoka kwenye Jukwaa la Kulinda Utu wa watoto(CDF) na changamoto ni jinsi ya kuzifikia koo nyingine Mkoani huko ili kuwezesha kuondoa kabisa mila hiyo.

  “Tumechoka vitendo vya ukatili kwa watoto na vitendo visivyoturishisha sisi kama wazee, tutafanya kila jitihada kuweza kuondokana na vitendo hivi, tunahitaji ushiriki zaidi wa serikali na asasi nyingine zishirikiane na CDF ili kwa pamoja tuweze kufikia lengo tuliloliweka” Alisema Mzee Elias

  Akitolea ufafanuzi suala hilo Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga amesema kweli upo umuhimu wa kutekeleza suala hilo la kupeleka elimu juu ya madhara ya ukeketaji ili kuweza kuwasaidia watoto wakike.

  Naye Mzee wa Kimila kutoka Koo ya Bukira Mzee Sinda Nyangore ameishauri serikali na mashirika mengine kutoa elimu katika vipindi vyote vya mwaka na kuacha utaratibu wa kutoa elimu katika msimu wa ukeketaji kwenye koo mbalimbali.

  Katika Ziara hiyo Katibu Mkuu Sihaba Nkinga alitembelea maeneo mbalimbali ikiwemo Dawati la Jinsia katika wilaya hiyo na kujionea namna wanavyofanya kazi na jinsi wanavyokabiliana na changamoto mablimbali.

  Aidha Bi. Sihaba aliwatembelea watoto wa kike waliopo katika mpango wa uendelezwaji kijasiriamali unaotekelezwa na Jukwaa la Kulinda Utu wa watoto(CDF) katika kata ya Manga Wilayani Tarime Mkoani Mara.

  0 0

  Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii Malinyi.

  Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi ni moja ya Wilaya mpya hapa nchini zilizoundwa kutokana na ukubwa wa mkoa wa Morogoro kwa lengo la kuzidi kuongeza huduma za kiserikali kwa wananchi walio pembezoni hili kupunguza gharama za wananchi kutembea umbali mrefu.

  Malinyi ambayo imezaliwa kutoka katika Wilaya Mama ya Halamashauri ya Wilaya ya Ulanga ambayo ilionekana kubwa kuliko kawaida na kushindwa kukidhi kuwahudumia wakazi wa malinyi kutokana na umbali wa kijiografia.
  Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Malinyi ,Marcelin Ndimbwa, akikagua ujenzi wa madarasa ambayo yamejengwa kwa ajli ya watoto wa wafugaji Rumbanga.

  Marceline Ndimbwa ni Mkurugenzi wa kwanza katika halmashauri hiyo mpya kuteuliwa na Rais wa awamu ya tano Daktari John Pombe Magufuli ili kuhakikisha maendeleo ya wilaya hiyo yanafanana na sehemu nyingine.

  Ndimbwa amekuwa ni mkurugenzi wa halamashauri hiyo huku akikabiliana na changamoto kubwa ya mgogoro wa ardhi baina ya wakulima na wafugaji na changamoto ya miundombinu ya elimu katika jamii kubwa ya wafugaji.

  Ndimbwa anasema kuwa Rumbanga ni moja ya maeneo ambayo hayapo mbali na mji wa Malinyi lakini yamekuwa na jamii kubwa ya wafugaji wa kabila la kisukuma huku wakiwa na changamoto ya kutokuwa na shule ya msingi, Sekondari na huduma za afya.

  Ndimbwa anasema kuwa mbali na changamoto zote hizo lakini ameamua kuanza na changamoto kubwa ya kutokuwepo na shule ya msingi katika eneo hilo la Rumbanga.
  “kiukweli hali sio nzuri katika eneo la Rumbanga kwani shule iliyopo ni ya nyasi ambayo imejengwa na wanakijiji wenyewe na aina walimu wa kufundisha zaidi vijana wawili ambao wamemaliza kidato cha nne na kuamua kujitolea katika kuwafundisha wadogo zao ambao wapo kuanzia darasa la kwanza mpaka la nne”amesema Ndimbwa.

   Ndimbwa anasema kuwa mara baada ya kuona mazingira hayo wakaona ni ulazima wa kuamua kujenga shule hiyo kuwa ya kisasa kutokana changamoto ya umbali kufata shule ambayo ipo kilometa 34 kutoka hapo Rumbanga na wanafunzi hao kutakiwa kutembea kwenda na kurudi katika shule ya msingi Mwembeni hali iliyochangia watoto wengi kuacha masomo na watoto wa kike kupata ujauzito katikati ya masomo na kulazimika kuacha shule.

  Anataja kuwa katika hatua za awali zilizochukuliwa na halmashauri yake katika kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi na  sera ya Rais Magufuli ya kupata elimu bure na sio bure tu bali iliyobora kwa wanafunzi, Serikali ya Wilaya imeamua kubuni arambee kutoka kwa jamii ya wafugaji na kutenga fedha kadhaa kwa ajili ya kujenga majengo ya kisasa ya shule ya msingi Rumbanga ambayo imeanza kutokana na jitahada za watu wa jamii hiyo ya wafugaji.

  “hatua ya kwanza niliyochukua ni kuchukua fedha za zilizotengwa kwa ajili ya kwenda Simiyu kuzima mwenge kiasi cha shilingi milioni 4 zipelekwe Rumbanga kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo hivyo kuongeza hali ya mwamko kwa wakazi wa kijiji hicho chenye jamii ya wafugaji” anasema Ndimbwa.

  Ndimbwa anasema wanafunzi hawa pindi shule zitakapofungua awatasoma tena katika mabanda ya nyumba za nyansi kama ilivyokuwa awali hivyo watakingi katika madarasa ya kisasa kama ilivyo kwa watoto wengine wa Tanzania.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Malinyi, Nasoro Liguguda amesema kuwa uamuzi huo wa mkurugenzi wa mtendaji wa halmashauri umekuja wakati muafaka kwani jamii kubwa ya watoto wa wafugaji walikuwa wakiteseka kwa kupata elimu bora kutokana na wao kupendelea kuishi pembezoni na kuanzisha miji mipya.

  Anasema wafugaji hao ambao kwa sasa wameamua kuishi malinyi hapo ni vyema nao wakapata stahiki zao za huduma za jamii kama ilivyo kwa jamii ya wakulima hili kupunguza migogoro.

  Nae katibu wa kamati ya ujenzi wa shule hiyo, Joseph Paschal wanashukuru halmashauri kwa kuweza kuwapatia fedha za kujenga shule hiyo ambayo ni tumaini jipya kwa wakazi wa Rumbanga .

  Anataja kuwa wakazi wa kijiji hicho walikuwa wakikumbwa na chngamoto nyingi wakati wa masika pindi wanapohitaji kwenda shule kutokana na kushindwa kuvuka mto Rumbanga ambao mara zote uwa unajaa maji hivyo kukusa masomo kwa kipindi chote.

  Kwa upande wake mkurugenzi Ndimbwa amesema kuwa serikali imekwisha ridhia kuiweka shule hiyo katika mpango ujao wa bajeti lakini kwa sasa shule hii itakuwa kama shule dada ya shule ya miembeni mpaka hapo itakapo pata usajili kamili.

  Hivyo ametaja wazi kuwa shule hiyo ambayo itakuwa na miundombinu ya kisasa na ujenzi wa choo bora ambacho kitajengwa sambamba na Zahanati ya Lumbanga ambayo itajenga jirani na eneo hilo la shule.
  Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Malinyi ,Marcelin Ndimbwa, akikagua madarasa ambayo yamejengwa kwa ajli ya watoto wa wafugaji Rumbanga.
  Mkurugenzi wa malinyi,Marcelin Ndimbwa, akionyesha choo kilichokuwa kikitumiwa na wanafunzi hao.
  sehemu ya ubao wa kufundishia wa shule hiyo ya manyasi.
  mkurugenzi wa malinyiMarcelin Ndimbwa akitoka darasani katika shule ya msingi Rumbanga.
  Wanafunzi wakiwa darasani.

  0 0

  "I've had a couple people in my life try and OWN my life and lease it out to me every so often - I hated that. It broke me..."

  NAIROBI, JANUARY 5 - One of Kenya's top media personalities Adelle Onyango is among the 100 most influential young people in Kenya.

  Adelle is know for her various uplifting, inspirational and mentorship campaigns like Sisterhood.

  "It's an honor because some of the other nominees amaze me with their level of self awareness, not influence, like Lupita! But...argh ... why is it always so deep with me?" Adele quipped.

  "I don't know who I influence because I'm just on this wild journey of self actualization that I just happen to share - If it happens to influence you - I hope it influences you to want to start and stay true to YOUR journey. You dig? But that's not the reason I am me."

  Adelle opened up about how importance of being self aware.

  "I've had a couple people in my life try and OWN my life and lease it out to me every so often - I hated that. It broke me," Adele revealed.

  "But I built myself right back up and I fuckin love me! Do you know how POWERFUL that is for me! That's why I SHARE! It's a celebration, what's mine, is mine again."
   


  0 0

  Na Daudi Manongi-MAELEZO

  SERIKALI kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu,Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu kwa kushirikiana na Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi – VETA wanaendesha mpango wa kutathmini na kurasimisha ujuzi uliopatikana nje ya Mfumo rasmi wa Mafunzo.

  Kwa mujibu wa Taarifa ya Katibu Mkuu wa Kazi, Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Eric Shitindi, imesema kuwa mpango huo unatoa fursa ya kufanyiwa tathmini ya ujuzi, kupewa mafunzo, kuziba upungufu na kisha kutunukiwa cheti.

  Taarifa hiyo inaeleza kuwa sifa za mwombaji wa mafunzo hayo ni pamoja na uzoefu usiopungua miaka mitano na umri usiozidi miaka 45. Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa fani mbalimbali zitakazohusika ni Uashi, Useremala, Ufundi Magari (makenika), upishi, uhudumu wa hoteli, Bar na Migahawa.

  Ili kufanya maombi waombaji wanatakiwa kufika katika ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa, Mji au Wilaya iliyoko karibu ili kuchukua fomu za kujaza maombi bila malipo yeyote na maombi hayo kuwasilishwa kuanzia tarehe 5 hadi 25 Januari 2017.

  Taarifa hiyo imeongeza kuwa mchakato wote wa tathmini na urasimishaji wa ujuzi utagharamiwa na Serikali na pia watakaokidhi sifa, vigezo na masharti watajulishwa kwa ajili ya usaili kuanzia Tarehe 10 Februari 2017.

  0 0


  Na Jumia Travel Tanzania


  Mwaka 2016 umekwisha na kuupatia kijiti 2017 kuanza safari ndefu ya miezi 12 ijayo huku sekta ya utalii ikiwa kinara kwa kuiingizia serikali fedha za kigeni kiasi cha dola za Kimarekani bilioni 2.2.


  Takribani watalii 1,020,816 wameingia nchini katika kipindi cha Januari mpaka Oktoba mwaka 2016 kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango.

  Tukiwa tunauanza mwaka huu mpya ambapo watu wanamalizia mapumziko yao ili kurudi sehemu zao za kazi, Jumia Travel (www.travel.jumia.com) inapenda kukufahimisha juu ya aina za wasafiri na mahitaji yao.

  Biashara ya hoteli inajumuisha aina tofauti za makundi ya wateja kama vile wasafiri wa kibiashara na kujiburudisha. Makundi haya yana mahitaji tofauti na ili ufanikiwe katika biashara basi huna budi kuhakikisha kuwa unakidhi haja zao.

  Wasafiri wa kibiashara mara nyingi huzingatia mambo yafuatayo:

  Eneo ni muhimu: Wasafiri wa kibiashara huzingatia sana kigezo hiki kutokana na kuwa na ratiba inayowabana. Kwa mfano, hoteli kuwa karibu na ukumbi wanapofanyia mikutano ni muhimu kwani huwarahisishia kuwahi mapema au kufika kwa haraka. Hivyo ni muhimu kwa wamiliki wa hoteli kuzingatia kigezo hiki pindi wanapozitangaza hoteli zao.

  Kuunganishwa muda wote: Wafanyabiashara wanapendelea hoteli ambayo itawawezesha vifaa vyao kama kompyuta au simu kuunganishwa na umeme au mtandao wa intaneti muda wote. Hii huwarahisishia kufanya kazi zao pamoja na kuwaunganisha na wafanyabiashara wenzao.

  Uaminifu: Wamiliki wanatakiwa kujikita kwenye kujenga uaminifu na wateja wao hususani wafanyabiashara ili kuwavutia kuja tena na tena. Mara nyingi wasafiri wa aina hii hupendelea kwenda sehemu wanayoiamini hivyo huwawia vigumu kutafuta pengine kutokana na kubanwa na vikao au ratiba zao za kazi.

  Upatikanaji wa huduma zote kwa pamoja: Hapa inamaanisha huduma kama vile kifungua kinywa, kunyoosha nguo au huduma zote ambazo mfanyabiashara anaweza kuzipata kujiandaa kwenda kwenye shughuli zake mapema asubuhi. Hivyo basi hoteli ambayo inatoa huduma hizo inayo fursa kubwa ya kupendelewa na wasafiri wengi.

  Wasafiri wa kujiburudisha wao hupendelea huduma zifuatazo:

  Bajeti kwao ni kigezo kikubwa: Kundi hili la watalii huzingatia sana kupata bei nzuri kwenye hoteli watakayofikia ili kujiburudisha. Siku zote huhakikisha wanazingatia unafuu wa gharama katika kipindi chote watakachokitumia.

  Huzingatia watu wanaizungumziaje hoteli husika: Mara nyingi kundi hili likitaka kufanya maamuzi ya kusafiri hutafuta ushauri au maoni kutoka kwa familia, marafiki au wenza wao. Maoni kutoka kwa watu wao wa karibu yana ushawishi mkubwa katika maamuzi yao. Wamiliki wa hoteli wanapaswa kulizingatia hili kwa kuyafanyia kazi maoni yanayoachwa na wateja wao kwa njia mbalimbali kama vile mtandaoni.

  Huvutiwa na ofa maalumu: Hakuna mtu asiyependa ofa na kwa sababu wasafiri wa aina hii lengo lao kubwa ni kuburudika, basi wanazingatia sana kigezo hiki pindi wanapochagua hoteli ya kufikia. Kwa kulitambua hili hoteli zinatakiwa kuwa wabunifu wa kuweka ofa za kipekee na zinazovutia kundi hili la wateja.

  Hupendelea hoteli zinazotoa vitu vya ziada kwa wateja wao: Kwenye biashara lazima kuwe na utofauti ili kuwavutia wateja. Wasafiri wa aina hii wanapendelea pia vitu vya ziada ambavyo ana uhakika akienda hoteli nyingine hatovipata. Huduma kama vile bwawa la kuogelea, sehemu ya mazoezi, michezo ya kwenye maji au mgahawa ambao unasifiwa na wengi kwa kuwa na chakula kitamu.

  Ili kuwa na biashara yenye mafanikio, ni muhimu kutambua mahitaji na matakwa ya wateja wako. Jumia Travel (www.travel.jumia.com) inakukumbusha kuwa hali hiyo pia ni sawa na kwa biashara ya hoteli au sehemu yoyote inayotoa huduma ya malazi. Sio tu ni muhimu kujua mahitaji ya wateja bali pia ni lazima kujua aina ya wateja unaowahudumia.

  0 0


  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Rodrick Mpogolo akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mjini Magharibi, Aziza Mapuri baada ya msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kuwasili Bandari ya Zanzibar leo
  "NAAM TUMEWASILI KWA MUDA SAHIHI" Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimwambia Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Zanzibar Vuai Ali Vuai baada ya kuwasili Bandari ya Zanzibar leo
  Katibu Mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole (kushoto) baada ya kuwasili Bandari ya Zanzibar
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo (kushoto) alipowasili Bandari ya Zanzibar leo

  Humphrey Polepole akilakiwa baada ya msafara wa Kinana kuwasili Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui leo
  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mjini Magharibi Aziza Mapiri akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuhusu hali ya kampeni za uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Dimani walipokuwa katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar leo


  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na msafara wake wakitazama eneo alilouliwa muasisi wa Mapinduzi ya zanzibar, Hayati Abeid Amani Karume katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar, leo

  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiagwa na viongozi wakati akitoka Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar kwenda kwenye mapumziko kabla ya kwenda kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Dimani leo jioni. Picha zote na Bashir Nkoromo 


  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (watano kulia) na ujumbe wake wa viongozi waandamizi kutoka makao makuu ya CCM, wakiwa kwenye chumba cha nahodha walipokuwa wakisafiri kwa boti ya mwendokasi kutoka Dar es Salaam, kwenda Zanzibar kwa ajili ya kushiriki uzinduzi wa kampeni za CCM, uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Dimani, leo. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo

  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akihoji moja ya kifaa cha kuongozea boti ya mwendo kasi kinavyofanya kazi.

  Karibu Zanzibar

  0 0

  Mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze, Saidi Zikatimu, akizungumzia mikakati waliyojiwekea kuwalipa posho wenyeviti wa vijiji na vitongoji sanjali na kuinua mapato ya ndani (Picha na Mwamvua Mwinyi)
  ………………………………………………………………………

  Na Mwamvua Mwinyi,Chalinze

  HALMASHAURI ya mji mdogo wa Chalinze,mkoani Pwani,imetenga kiasi cha sh.mil 36 katika kipindi cha mwaka 2016/2017 kwa ajili ya kuwalipa posho wenyeviti wa vijiji na vitongoji katika halmashauri hiyo.

  Kati ya fedha hiyo wenyeviti hao wanalipwa kila mmoja sh.30,000 kwa mwezi hadi mwezi july mwaka huu itakapokoma bajeti hiyo.

  Akizungumzia kuhusiana na mpango huo,kwa waandishi wa habari mjini hapo,mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Chalinze ,Said Zikatimu ,alisema halmashauri hiyo imeamua kuwalipa posho wenyeviti hao kwani wanafanyakazi kubwa ndani ya miaka mitano bila kuambulia chochote.

  Alisema wameshirikiana na mbunge wa jimbo la Chalinze,Ridhiwani Kikwete,kuona namna ya kuwatupia jicho wenyeviti hao wa vijiji na vitongoji .

  Aidha Zikatimu alieleza kwamba ,fedha hizo zitawawezesha wenyeviti hao kujikimu na kuondokana na hali ya kuuza ardhi za vijiji kwa visingizio vya kukosa posho ama mishahara.Alibainisha ,fedha hiyo pia itaweza kuwasaidia wenyeviti hao kuwa na morali na ari ya kuchapakazi kwenye maeneo yao na wamejipanga kila mwaka watakuwa wakitenga fedha hizo.

  “Kiasi hiki cha sh.mil.36 ni fedha watakazolipwa hadi july 2017 na bajeti inayofuata tutaangalia kama kuna uwezekanao wa kuongeza kiasi kilichopangwa katika bajeti hii ama ibakie kiasi kilichotengwa kwenye bajeti hii”alifafanua Zikatimu.Hata hivyo Zikatimu alisema ,wanachotarajia ni wenyeviti hao kuendelea kuwa wasimamizi wazuri katika vyanzo vya mapato na kuachana na tabia ya kuuza maeneo ya vijiji kinyume na taratibu.

  Alisema wanawahamasisha kusimamia vyanzo vya mapato ili kuinua makusanyo hasa ya vyanzo vya ndani ikiwemo vizuizi mbalimbali vya pembezoni na ndani ya mji huo.Mwenyekiti huyo alitoa wito kwa halmashauri nyingine nchini kuwaangalia wenyeviti hao kwani kwa Chalinze imeshaleta tija ndani ya miezi sita tangu kuanza kwa mpango huo.

  Aliiomba serikali na halmashauri hizo ziangalie namna ya kuwatengea fedha wenyeviti wa vijiji na vitongoji kama ilivyo kwa madiwani na wabunge wanavyotengewa posho wakimaliza muda wao,ili waweze kuwa na moyo wa kufanya kazi pasipo kukosa chochote.

  “Halmashauri ni sehemu ya kwanza na serikali kuu ni sehemu ya pili,hivyo halmashauri zionyeshe nia ili serikali ilione hili,kwa kuwapa kipaombele ya kuwatengea fedha bila kuwaacha”

  Zikatimu alisema wenyeviti hao wanasimamia chaguzi mbalimbali na ilani ya CCM hivyo waangaliwe katika suala hilo ili waweze kujiona ni viongozi wanaoaminika kwenye maeneo yao.

  0 0

    Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipata maelezo ya mradi wa maji  kutoka kwa mkurugenzi wa Halimashauri ya  Madaba Bwana Safi Mpenda Waziri Mkuu ameuzindua mradi huo ambao umejengwa katika kijiji cha Magingi wilaya ya Songea,  Mradi ambao una uwezo wa kutoa lita 200000 (laki mbili) na kuhudumia zaidi ya watu 5000 (Elfu tano) katika Halmashauri ya madaba, Songea

   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimtwisha ndoo ya maji Bibi Leonara Kibuno ikiwa ni ishara ya uzinduzi  wa mradi huo ambao umejengwa katika kijiji cha Magingi wilaya ya Songea,Mradi ambao una uwezo wa kutoa lita 200000 (laki mbili) na kuhudumia zaidi ya watu 5000 (Elfu tano) katika Halmashauri ya madaba, Songea
  Waziri mkuu Kassim Majaliwa akiwa hutubia wananchi wa halimashauri ya Madaba.Picha na Chris Mfinanga

  0 0

     Baadhi wa Wafugaji wakiwa wanakunywa maji na juisi walizopelekewa kama msaada baada ya kuokolewa na Askari wanyamapori wa Pori la Akiba la Selous,  Kanda ya Kaskazini Mashariki  Kingupira  baada ya kutelekezwa kwa muda wa  siku tano na mtu mmoja waliyemtaja kwa  jina maarufu la Mzigua aliyewarubuni kwa kuwaonyesha njia za mkato ndani ya Pori hilo ( Picha na Lusungu Helela-Wizara ya Maliasili na Utalii) 
    Baadhi ya Mzoga wa ngombe uliopatikana ndani ya Pori la Akiba la Selous,  Kanda ya Kaskazini Mashariki  Kingupira  baada ya Wafugaji 50  waliotelekezwa kwa muda wa  siku tano na mtu mmoja waliyemtaja kwa  jina maarufu la Mzigua aliyewarubuni kwa kuwaonyesha njia za mkato ndani ya Pori hilo na kisha kuwakimbia( Picha na Lusungu Helela-Wizara ya Maliasili na Utalii)
     Mmoja wa  wafugaji aliyepotea na  kutelekezwa ndani ya Pori la Akiba la Selous,  Bw. Lisesi Cherehani aliyekuwa na ng’ombe 180 na punda mmoja akiangalia mmoja wa ng'ombe wake aliyekufa kwa kukosa  maji ya kunywa kwa muda  wa siku tano kwenye Kanda ya Kaskazini Mashariki katika Pori la Akiba la Selous ( Picha na Lusungu Helela-Wizara ya Maliasili na Utalii)
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence  Milanzi (katikati) akipata taarifa kutoka kwa  Meneja wa Mradi wa Pori la Akiba la Selous    Bw. Enock Msocha (wa tatu kushoto)  mara baada ya  kuwasili kwa ajili ya kuwatembelea  Wafugaji 50 waliokolewa na Askari wanyamapori baada ya kutelekezwa  na mtu mmoja waliyemtaja kwa  jina maarufu la Mzigua aliyewarubuni kwa kuwaonyesha njia ya mkato ndani ya Pori hilo na kisha kuwakimbia ( Picha na Lusungu Helela-Wizara ya Maliasili na Utalii)  Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Askari wa Wanyamapori wa Pori la Akiba la Selous, Kanda ya Kaskazini Mashariki Kingupira imewaokoa wafugaji 50 waliokuwa wakiwapitisha jumla ya ng’ombe 1780, kondoo 200 na punda 6 baada ya kutelekezwa kwa muda wa siku tano na mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la Mzigua aliyewarubuni kwa kuwaonyesha njia za mkato ndani ya Pori hilo wao bila kujua na kuamua kuwakimbia.

  Bw. Lisasi Cherehani ambaye ni mmoja wa wafugaji hao alisema ‘’tulimpa Mzigua kiasi cha zaidi ya shilingi 5,000,000 kutoka kwa wafugaji kama malipo ya kutufikisha eneo la Ilonga mkoani Morogoro tukitokea vijiji vya Ndundunyekanza, Kipungila na Chumbi vilivyopo wilayani Rufiji mkoani Pwani kwa makubaliano kuwa atatupitisha njia fupi ya mkato tutakayotembea kwa muda wa siku tano tu, hatukujua anatutupitisha ndani ya pori hili. ‘’

  Baada ya kutelekezwa, wafugaji hao ambao walikuwa katika hali mbaya waliomba msaada kwa ndugu zao ambao waliwasiliana na Uongozi wa Pori la Akiba la Selous ambao kwa haraka walifanya jitihada za kuokoa maisha yao ikiwa ni kuwapa huduma ya kwanza, maji, uji pamoja na kuwakimbiza hospitalini kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi aliwatembelea wafugaji hao jana kwa ajili ya kuwapa pole na kuwapelekea chakula yakiwemo maji pamoja na unga.

  Aidha, Milanzi aliagiza Wafugaji hao waachiwe huku akitoa wito kwa wananchi kuacha kupita maeneo ya Hifadhi kwa vile ni kosa kisheria na wale wote watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria na kuahidi kuwa mtu huyo aliyewa danganya kwa kuwapitisha ndani ya Hifadhi hiyo ni lazima akamatwe kwa udi na uvumba.

  ‘’Sisi kama Serikali kitu cha kwanza ni ubinadamu tumewahudumia na hivyo natoa tamko la kuwaachia wafugaji wote waliopotea ndani ya Pori hili kwa vile mateso waliyoyapata na mali waliyoipoteza ni kubwa sana baada ya kudanganywa kwa na kupitishwa ndani ya Pori la Akiba la Selous.’’ Alisema Milanzi

  Mmoja wa wafugaji aliyekuwa katika msafara huo na aliyekuwa akiwasiliana kwa njia ya simu , Bw. Lisesi Cherehani akielezea namna walivyotelekezwa katika pori hilo, alisema kuwa walianza safari hiyo siku ya jumatano ambapo walikuwa wakitembea usiku na mchana kwa muda w siku tano bila kujua wanapitishwa ndani ya Hifadhi hiyo ndipo wakaanza kushikwa na kiu kwa vile maji waliyokuwa nayo yaliwaishia na kila walipokuwa wakijaribu kumuuliza aliyewapitisha njia hiyo alikuwa akiwambia baada muda mfupi watakutana na maji hata hivyo waliendelea na safari bila mafanikio ndipo walipoanza kuanguka na baadhi ya wafugaji walianza kunywa mikojo yao pamoja na damu za kondoo kwa ajili ya kuokoa maisha yao.

  Aliongeza kuwa, wasingekuwa Askari wanyamapori ambao walikuja kuwapa msaada wa kibinadamu kwa kuwapatia maji pamoja na kuwanyesha uji wangeweza kufa wote.‘’Nawashukuru sana askari wanyamapori kwa kutuhudumia bila wao leo hii msingemkuta mtu yeyote hapa tungekuwa tayari tumeshakufa.’’ Alisema Bw. Cherehani.

  Mfugaji mwingine, Mbaga Mahila aliwashukuru sana Askari wanyampori kwa utu waliouonesha tokea mwanzo walipowaokoa hadi hapo walipofikia na kuitaka jamii ibadilishe mtazamo wa kuwaona askari wanyamapori kama watu katili jambo ambalo halina ukweli wowote.

  Pia, Masanje Hambe aliiomba Serikali iwasamehe kwa kuwa wametambaua kosa la kuingia ndani ya Pori la Akiba la Selous kinyume cha sheria lakini hata hivyo hawakujua kuwa wanapitishwa ndani ya hifadhi hiyo.

  Awali, Mkuu wa Kanda ya Mashariki Kingupira, Bw. Paschal Mrina alisema wamepata taarifa za wafugaji hao kutoka kwa Wasamaria wema na Uongozi wa wilaya ya Rufiji kuwa kuna wafugaji wamepotelea ndani ya hifadhi hiyo na kwa bahati nzuri kulikuwa na mfugaji mmoja aliyekuwa na simu ndipo wakaanza kuwasiliana naye na kuunda kikosi maalum cha doria kwa ajili ya kuwaokoa.

  Kwa mujibu wa Mkuu wa Kanda hiyo alisema wamefanikiwa kuwaokoa wafugaji wote na ilionekana mizoga saba na wengine ambao hawakuonekana taratibu za kuanza kutafuta zimeandaliwa

  Alielezea njia walizotumia kuokoa wafugaji hao ni kuwa waliunda vikosi vitatu vya doria ambapo kikosi cha kwanza kilifanya doria kwa njia za miguu, kikosi cha pili kilfanya doria kwa njia za magari na kikosi cha tatu kilifanya doria kwa kutumia ndege kwa ajili ya kubaini walipo.

  Kwa upande wake, Katibu wa Chama cha Wafugaji, Bw. Magembe Makoye alitumia fursa hiyo kuiomba Serikali kuacha kuwafukuza wafugaji katika maeneo waliyopo badala yake wawatafutie maeneo mbadala ili kuthibiti matukio kama hayo ambayo yamepelekea hasara na mateso makubwa kwa wafugaji.

  Pori la Akiba la Selous lina ukubwa wa kilomita za mraba 50,000 na limegawanywa katika kanda nane huku Kanda ya Mashariki Kipungira ikiwa moja kati ya kanda kubwa yenye kilomita za mraba 7,650, Shughuli zinazofanyika katika Pori hilo ni Utalii wa picha na pamoja na uwindaji

  0 0

  Na Amina Kibwana-Globu ya Jamii.
   
  Wizara ya ardhi,nyumba na maendeleo ya Makazi kupitia idara ya nyumba imepewa jukumu la kusimamia mfuko wa mikopo ya Nyumba kwa watumishi wa serikari kwa lengo la kuwawezesha watumishi wake kujenga,kununua au kukarabati nyumba kupitia mkopo huo mwenye masharti nafuu.

  Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Idara ya nyumba Michael Mwalukasa amesema kuwa mfuko huu ulianzishwa kwa ajili ya kusaidia na kuwawawwzesha watumishi wa serikali wanaoishi mjini na vijijini kupata mkopo wa nyumba wenye masharti nafuu kwa ajili ya kujenga au kununua nyumba.

  Ameongeza kuwa mfuko huo unatoa mikopo kuanzia milioni 20 kwa riba ya asilimia tatu ambao muda wa juu wa kurejesha mkopo huo ni miaka thelasini(30) katika kipindi cha utumishi kabla ya kustaafu au anapoacha utumishi kwa sababu zozote zile.

  Mwalusaka amesema kuwa kuna sifa mbalimbali  za kupata mkopo huu ikiwa ni pamoja na mkopaji ni lazima awe mtumishi wa serikali, raia wa Tanzania,aliyeajiriwa kwa masharti ya kudumu na kuthibitishwa kazini pamoja na kuwa na hati ya kiwanja ambacho kitamuwezesha kupata mkopo kwa ajili ya kujenga.

  Kwa upande wake Mkurugenzi msaidizi mikopo ya nyumba Lucy Kabyemera ameeleza faida za mikopo hiyo kwa watumishi wa  serikali ikiwa ni pamoja na kuwawezesha watumishi kupata mikopp yenye riba nafuu, kuweza kumiliki nyumba kwenye maeneo yenye hadhi,kuchochea kasi ya maendeleo kwenye miji na wilaya mbalimbali pamoja na kutoa fursa kwa watumishi kumiliki nyumba kwa kadri ya matakwa yao.

  "Faida zipo nyingi sana kwani pamoja na kunufaika na mikopo baadhi ya wakopaji pia wameendelea kunufaika na ushauri wa kutumia technologia ya bei nafuu ya ujenzi kutokana na tafiti zilizofanywa na taasisi iliyopo chini ya Wizara (NHBRA)."

  Kabyemera ameongeza kwa kusema kuwa ujenzi wa nyumba unahitaji gharama nyingi hivyo ndio maana wameamua kutoa mikopo hasa kwa watumishi wa serikali ili iweze kuwasaidia kwa kuwapa fedha taslimu ya shilingi milioni 20.

  Mfuko wa Mikopo ya Nyumba ni moja wapo ya vyombo vilivyoanzishwa na serikali mara baada ya nchi kupata uhuru mnamo mwaka 1963 kupitia waraka wa watumishi wa serikali na.8 na badae kuendeshwa kupitia waraka wa watumishi wa serikali na.4 wa mwaka 1965.
  Mkurugenzi wa Idara ya Nyumba Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Michael Mwalukasa akizungumza na Waandishi wa Habari Leo Jijini Dar es salaam kuhusu mfuko wa kuwawezesha watumishi wa Serikali kumiliki Nyumba ambapo zaidi ya watumishi 2000 wameshanufaika na mikopo yenye riba nafuu ya asilimia 3 ili kuwawezesha kumiliki nyumba bora. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Mikopo ya Nyumba Bi Lucy Kabyemera na Kushoto
  Mkurugenzi Msaidizi Mikopo ya Nyumba,Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi Lucy Kabyemera akifafanua kwa waandishi wa habari kuhusu faida wanazopata watumishi wa Umma kutokana na mikopo inayotolewa na Serikali ili kuwawezesha kumiliki makazi bora. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Nyumba Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Michael Mwalukasa.Picha na Frank Mvungi-Maelezo.


older | 1 | .... | 1090 | 1091 | (Page 1092) | 1093 | 1094 | .... | 1898 | newer