Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1089 | 1090 | (Page 1091) | 1092 | 1093 | .... | 1897 | newer

  0 0  0 0


  0 0

   Kushoto ni Katibu  wa UVCCM wilaya ya Longido Isaya Karakara, Katibu Hamasa wa UVCCM mkoa wa Arusha Neema Emmanuel  na Mjumbe Baraza Kuu  UVCCM Mkoa wa Arusha Robert Kaseko w akikabidhi msaada kwa Mmiliki wa kituo cha kulelea Watoto yatima cha Masai Foundation  Joyce Kabati

   Kushoto ni Katibu  wa UVCCM wilaya ya Longido Isaya Karakara, Katibu Hamasa wa UVCCM mkoa wa Arusha Neema Emmanuel  na Mjumbe Baraza Kuu  UVCCM Mkoa wa Arusha Robert Kaseko w akikabidhi msaada kwa Mmiliki wa kituo cha kulelea Watoto yatima cha Masai Foundation  Joyce Kabati.Habari picha na Woinde Shizza,Arusha.

  Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Longido umetembelea kituo cha Watoto yatima na Wanaoishi katika mazingira magumu cha Masai Foundation kilichopo mji mdogo wa Namanga na kutoa msaada wa vyakula pamoja na vifaa mbalimbali.

  Mjumbe Baraza Kuu  UVCCM Mkoa wa Arusha Robert Kaseko Amesema kuwa wameamua kushirikiana na jamii katika kusaidia watoto ikiwa ni moja kati ya michango wanayoitoa ili kutosheleza mahitaji muhimu yanayohitajika katika kituo hicho.

  Robert Amesema kuwa jukumu la kuwasaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu ni la kila mwanajamii hivyo jamii inapaswa kujitoa kusaidia watoto hao.

  Katibu Hamasa wa CCM mkoa wa Arusha Neema Emmanuel amesema kuwa vijana hao wameamua kujitoa kutoa msaada kwa jamii ili kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu hivyo ameiomba jamii kujitokeza kwa wingi kuwasaidia watoto hao.

  “Hawa ni watoto wetu sote kila mtu anapaswa kuona kuwa ana jukumu la kuwasaidia hawa watoto ili waweze kufanikisha ndoto zao”  Neema

  Katibu  wa UVCCM wilaya ya Londigo Isaya Karakara na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya Tulli Lemanga aliyejitolea kuwakatia bima ya afya watoto wanaolelewa katika kituo hicho wamesema  kuwa vijana hao wataendelea na utamaduni huo mara kwa mara katika kuunga mkono juhudi za serikali katika kutatua changamoto za watoto.

  Mmiliki wa kituo hicho Joyce Kabati amewashukuru vijana hao kwa kutembelea watoto hao jambo ambalo linaleta faraja kwa watoto hao ambao na wanamahitaji mbalimbali ambayo yamewasilishwa na vijana hao.


  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuhakikisha eneo la Kisarawe II linakuwa na umeme wa uhakika ili kuwezesha viwanda na wananchi wa eneo hilo kupata nishati hiyo. 

  Alitoa agizo hilo jana jioni (Jumanne, Januari 3, 2017) wakati alipotembelea kiwanda cha Milkcom kinachozalisha bidhaa za maziwa na kiwanda cha Watercom kinachozalisha maji vilivyoko katika kata ya Kisarawe ii wilayani Kigamboni akiwa katika ziara yake ya kikazi. 
  “Waziri wa Nishati ahakikishe eneo hili linapata umeme wa uhakika ili kuviwezesha viwanda hivi kufanyakazi vizuri jambo litakaloongeza uzalishaji. Pia wananchi wanaoishi katika maeneo haya nao watanufaika na upatikanaji wa nishati hiyo,” alisema. 

  Waziri Mkuu alisema amefarijika na jitihada za muwekezaji huyo za kuungamkono mkakati wa Serikali ya awamu ya Tano wa kuifanya Tanzania kujenga uchumi wa viwanda utakaoliwezesha Taifa kufikia uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025. 

  Awali, Msemaji wa Viwanda hivyo, Aboubakar Faraj akisoma taarifa ya viwanda hivyo kwa Waziri Mkuu alisema moja ya changamoto zinazowakabili ni pamoja na upatikanaji wa umeme wa uhakika jambo linasababisha kupanda kwa gharama za uzalishaji. 

  “Punde umeme unapokatika tunalazimika kutumia majenereta kwa muda mrefu. Hii husababisha ongezeko la gharama za uzalishaji ambazo huumiza kiwanda kwa sababu haiwezekani kumtwisha mzigo huu mlaji,” alisema. 

  Faraji alisema changamoto nyingine ni miundombinu ya barabara ambayo usababisha wateja wengi kushindwa kufika kwenye viwanda hivyo kwa urahisi, hivyo aliiomba Serikali kuwatatulia kero hilo. 
  Aliongeza kuwa kwa sasa viwanda hivyo vimeajiri watu zaidi ya 1,800, ambapo alisema endapo Serikali itawahakikishia upatikanaji wa umeme na barabara wataongeza ajira kwa asilimia 25 ifikapo mwaka 2018. 

  Mapema Waziri Mkuu alizindua wodi ya wazazi katika Zahanati ya Kisarawe ii iliyojengwa kwa ufadhili wa kampuni ya mafuta ya Oilcom. Wodi hiyo yenye vyumba vitatu itawapunguzia akinamama kusafiri umbali mrefu kutuata huduma hiyo.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S.  L. P. 3021,


  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga akiongea wakati wa mahafali ya watoto waliokimbia kukeketwa na kujiunga katika kituo Watoto waliokimbia Kukeketwa cha ATFGM-Massanga
  NA HASSAN SILAYO-MAELEZO 
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Bi. Sihaba Nkinga amekemea vitendo vya ukeketaji kwa watoto wa kike nchini na kuahidi kuwachukulia hatua kali za kisheria wale watakaobainika. 

   Akiongea wakati wa Mahafali ya watoto 46 waliokimbia kukeketwa na kujiunga na Kituo cha kulea watoto hao cha ATFGM Kilichopo Masanga Tarime Vijijini Bi.Sihaba alisema kuwa suala la ukeketaji ni kinyume na sheria za nchi na haki za binadamu na ni suala lenye madhara kwa maisha ya watoto. 

   “Hatukubaliani na suala hili kwani linarudisha maendeleo ya nchi yetu,suala hili pia linachangia kurudisha fikra za vijana wetu na kubatilisha ndoto za vijana wetu, tunao muda wa kujirekebisha na kama tulikuwa tunaendelea basi turudi nyuma”Alisema Bi. Sihaba. 

  Katibu Mkuu huyo amesema kuwa jamii inayo wajibu wa kulinda na kuendeleza mila zenye kuleta maendeleo na kuacha kulinda na kukumbatia mila zinathoathiri maisha ya binadamu kwani sio suala sahihi kwani mila nyingine zinagharimu maisha ya vijana wetu. 

   Akizungumza katika mahafali hayo Mkuu wa Wilaya ya Tarime Mhe. Glorious Luoga amewakemea wazazi watakaothubutu kuwakeketa wasichana wanaotoka katika kituo hicho baada ya mafunzo na wale watakao watakaowatahiri watoto wa kiume kwa mara ya pili baada ya kufanyiwa tohara salama hospitalini. 

   “Niwaeleze wazazi na walezi, wapo wanaowalazimisha kuwafanyia tohara ya pili watoto wa kiume baada ya kufanyiwa tohara salama, atakayegundulika kufanya tukio hilo tutamshughulikia kwa kumchukulia hatua kali za kisheria ili aone uchungu anaoupata mtoto wakati wanawatahiri kwa mara ya pili” Alisema Mhe. Luoga. 

   Naye Mkuu wa Wilaya ya Bunda Bi. Lydia Bupilipili amewasihi wazazi kuacha tabia ya ukeketaji na kuwapeleka watoto shule ili waweze kutimiza malengo yao kwani kila mtoto ana talanta aliyopangiwa na mungu hivyo kufanya hivyo kuwakeketa na kuwazuia kwenda shule ni kukatisha malengo yao. 

  Mkurugenzi wa Kituo cha Kulea Watoto waliokimbia Kukeketwa cha (ATFGM-Massanga) Sister Stella Mgaya ameshukuru juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na uongozi wa wilaya ya Tarime kukabiliana na tatizo hilo na kuendelea kuomba wadau kujitokeza kuwaendeleza watoto wanaohitimu kituoni hapo. 

   “Tunashukuru jitihada za Wilaya ya Tarime wamekuwa nasi bega kwa bega ila tunaomba wadau wengine ikiwemo serikali kwani baada ya mafunzo watoto hawa wamekuwa wakitengwa na familia zao na kuacha kuwapa mahitaji ya msingi hivyo kulazimu kituo kugharamia masomo japo sio kwa kiwango cha kuridhisha” Alisema Sister Mgaya. 

   Wakisoma Risala kwa mgeni rasmi muwakilishi wa wahitimu hao Magreth Daniel ameiomba serikali kuendelea kuwasaidia hasa baada ya mafunzo na kuepuka kutengwa na familia pia kuendelea kuwachukulia hatua za kisheria wazazi,walezi na mangariba wanaojishughulisha na vitendo vya ukeketaji. 
   Kituo cha Kulea Watoto waliokimbia Kukeketwa cha ATFGM-Massanga kwa mwaka jana kimepokea watoto 300 kutoka katika maeneo ya Tarime,Rorya,Bunda, Loliondo na baadhi kutoka nchi jirani ya Kenya.

  0 0

  Usiku wa kuamkia mwaka mpya wa 2017 Bw. Wasia na Bi. Laila waliandaa mnuso wa nguvu wa  Harusi yao kwenye Ukumbi wa Taj Hall ulioko Savoy Drive jijini Houston, Texas, Marekani.  Pata taswira  za tukio hilo hapa chini.
  Newly Wed Mr. Wasia akiwa na Mkewe Bi. Laila na kijana wao Zion
  Bw. Wasia Maya na Bi. Laila Martin

  Lovely couple 
  Zion akiwa na Baba na Mama 
  0 0

  Msemaji wa Polisi, Advera Bulimba – ACP

  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu ametuma timu ya Maofisa  wa Polisi ikiongozwa na Kamishna wa Polisi Jamii Mussa Alli Mussa kwenda Zanzibar kushughulikia kero na malalamiko ya wananchi juu ya vitendo vya udhalilishaji na ukatili kwa watoto/wanawake ambavyo vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara.

  Timu hiyo imepewa jukumu la kuchunguza vitendo hivyo vya udhalilishaji na kiini chake na hatimaye kuja na mpango mkakati wa kuzuia vitendo hivyo ikiwemo kuwakamata  wahusika na kuwafikisha mahakamani.

  IGP Mangu amewataka wananchi wa Zanzibar, Taasisi za kiserikali na Taasisi za kiraia zilizopo Zanzibar kutoa ushirikiano kwa timu hiyo ili kukomesha vitendo hivyo ambavyo ni kinyume na maadili ya Watanzania.

  Imetolewa na:
  Advera John Bulimba - ACP
  Msemaji wa Jeshi la Polisi.

  Makao Makuu ya Polisi.

  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Tanga(CUF)Mussa Mbaruku akimuelekeza namna ya kuitumia Baiskeli ya kutembelea mkazi wa Mtaa wa Tongoni Jijini Tanga,Mwinchumu Ally jana mara baada ya kumkabidhi ikiwa ni ahadi aliyemuahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka juzi .
  Mbunge wa Jimbo la Tanga(CUF) Mussa Mbaruku kulia akimkabidhi baikeli mkazi wa Mtaa wa Tongoni Jijini Tanga,Mwinchumu Ally jana ambaye anamatatizo ya ulemavu wa miguu kwa ajili ya kutembelea ikiwa ni kutimiza ahada aliyomuahaidi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwakajuzi,Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

  0 0

  1
  Nasieku Kisambu Mkurugenzi wa Mipango Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA) akizungumza katika mafunzo ya Haki za Wanawake na Jinsi ya kufanya utetezi katika ngazi ya Kitaifa, Kikanda na Kimataifa yakiwa na lengo la kuongeza uelewa wa misingi ya kulinda na kutetea haki za wanawake na watoto Kitaifa , Kikanda na Kimataifa.

  Kuelewa mifano iliyopo katika Kanda, Kikanda na kimataifa inayolinda haki za wanawake , Haya ni mafunzo yanayolenga kujenga uwezo wa Taasisi zinazotetea haki za wanawake kutumia fursa zilizopo katika mikataba, Taasisi na mifumo ili kuweza kubadilisha sera na sheria kandamizi na kutetea haki za wanawake. 

  Mafunzo hayo yanayofanyika kwenye hoteli ya Courtyard Upanga jijini Dar es salaam yameandaliwa na Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) na kwa ushirikiano na mashirika mengine yanayotetea haki za wanawake na watoto ambapo wadau mbalimbali kutoka katika taasisi hizo wameshiriki katika mafunzo hayo
  2
  Maria Matui Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake Wanasheria Tanzania (TAWLA) akifungua mafunzo hayo ya siku mbili yanayofanyika kwenye hoteli ya Courtyard Upanga jijini Dar es salaam.
  3
  Mkufunzi wa Mafunzo hayo Dk. Clemence Mashamba akitoa mada wakati wa mafunzo hayo yanayoendelea kwenye hoteli ya Courtyard Upanga jijini Dar es salaam.
  45
  Christina Kamili Mkurugenzi Mtedaji wa Shirika la Tanzania Network Of Legal And Providers akifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa na Mkufunzo wa Mafunzo hayo Dk. Clemence Mashamba hayupo pichani.
  06
  Baadhi ya washiriki mbalimbali wa mafunzo hayo wakifuatilia mada zilizokuwa kititolewa na mkufunzi huyo.
  6
  Christina Kamili Mkurugenzi Mtedaji wa Shirika la Tanzania Network Of Legal And Providers akifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa na Mkufunzo wa Mafunzo hayo Dk. Clemence Mashamba hayupo pichani.
  07
  Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada mbalimbali katika mafunzo hayo.
  7008
  Mkufunzi wa mafunzo hayo Dk Clemence Mashamba akiwa na Dotto Joseph Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya National Oganization For Legal Assistance (Nola)
  08
  Maria Matui Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake Wanasheria Tanzania TAWLA akipitia nyaraka za mmbalimbali za mafunzo hayo.
  8
  Washiriki wa Mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja.

  0 0

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na mkuu wa mkoa wa ruvuma Mhandisi Binilis Mahenge mara alipowasili katika uwanja wa ndege wa Ruvuma kwa ziara ya kikazi kulia ni mke wa mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mama Mahenge
  Waziri mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Kaimu Jaji Mfawidhi wa Songea Mh Salima Chikoyo ambaye alikuwepo katika uwanja wa ndege wa Ruvuma katika mapokezi ya waziri mkuu Kushoto ni Naibu waziri wa maliasili na utali Mhandisi Ramo Makani na kushoto ni katibu tawala wa mkoa wa Ruvuma Hassani Bndeheko Waziri mkuu amewasili mkoani Ruvuma kwa ziara ya kikazi. Picha na Chris Mfinanga

  0 0

   Meneja mauzo Airtel mkoa wa Dodoma, Hendrick Bruno (kushoto) akiongea na Fikiri Chinji (kulia) anayejishughulisha na ufundi seremala  juu ya maendeleo na changamoto za biashara baada ya kuwezeshwa na Airtel kupitia mpango wake wa Airtel FURSA “Tunakuwezesha”, wakati Airtel ilipotembelea kwenye karakana yake katika Mtaa wa Ng’ong’ona manispaa ya Dodoma ili kujionea maendeleo yake pamoja kupanga jinsi ya kuboresha zaidi biashara yake.
  Meneja mauzo Airtel mkoa wa Dodoma, Hendrick Bruno (kulia) akishuhudia matumizi ya moja ya vifaa alivyowezeshwa kijana Fikiri Chinji anayejishughulisha na ufundi seremala kwa kupitia mpango wa Airtel
  FURSA “Tunakuwezesha” miezi tisa iliyopita, wakati Airtel ilipotembelea kwenye karakana yake katika Mtaa wa Ng’ong’ona manispaa ya Dodoma ili kujionea maendeleo yake pamoja kupanga jinsi ya kuboresha zaidi biashara yake.


  Kampuni na Taasisi mbalimbali hapa nchini zimeaswa  kuiga mfano wa Kampuni ya simu za mkononi ya  Airtel Tanzania kwa kuwawezesha vijana mbalimbali  kujiajiri wenyewe kupitia   mradi wa Airtel Fursa, ili kupunguza tatizo la Ajira hapa nchini.

  Hayo yamebainishwa na mmoja kati ya waliofaidika na mradi wa Airtel Fursa kijana mjasiriamali anayejihusisha na  fani ya ufundi seremala  Fikiri Chinji aishie katika kijiji cha Ng'ong'ona manispaa ya Dodoma wakati alipotembelewa na Airtel ili kutadhimini maendeleo yake.

  Fikiri alisema wapo vijana wengi ambao wapo mtaani wakitafuta ajira na wengine wakikumbwa na changamoto za mitaji ili kuendesha biashara zao, program kama hii ya Airtel Fursa ni vyema ikafanywa na makampuni mengi ili kuinua uchumi wa vijana  jamii nan chi kwa ujumla

  Mpaka sasa nawashukuru sana Airtel kwa kuniwezesha mtaji ambao umeweza kuinua biashara yangu, kupitia program hii nimeweza kutanua biashara yangu ya ufundi selemala na kuanzisha biashara ya welding. Sambamba na kutanua biashara pia nimeweza kuajiri vijana  saba na kuongeza vifaa vingine zaidi, nawashukuru Airtel kwa kunishika mkono.”

   Akizungumza katika eneo hilo Afisa Airtel kanda ya kati, Hendrick  Werner amesema kijana Fikiri Chinji ameweza kupiga hatua kwa kuongeza vifaa vingine toka alipowezeshwa na Airtel Fursa, kukuza biashara pamoja na kutengeneza ajira kwa vijana wengine na  kuwataka vijana wengine kuiga mfano wa fikiri kwa  kuanzisha vikundi mbalimbali na kuwatafuta wadau  watakao wawezesha kupita program mbalimbali ikiwemo hii ya Airtel Fursa.

  Airtel Fursa ni mradi wa kijamii wenye dhumuni la kuhamasisha vijana, kuwapa nafasi ya kujiendeleza kibiashara na ujuzi utakoawawezesha kuimarisha biashara zao. Pambana group ni kikundi kingine kilichonufaika na mradi wa Airtel Fursa Dodoma ambacho kina vijana zaidi ya 15.

  0 0

    Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nyakaboja wilayani Busega katika Mkutano wa hadhara kwa lengo la kuwahamasisha kuanza kutekeleza mpango wa kilimo cha umwagiiaji wilayani humo.
   Mkuu wa Wilaya ya Busega Tano Mwera akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Nyakaboja wilayani humo katika Mkutano wa hadhara kwa lengo la kuwahamasisha wananchi kuanza kutekeleza mpango wa kilimo cha umwagiiaji wilayani humo.
  Afisa Ardhi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Simiyu, Bibi.Grace Mgombera akitoa ufafanuzi wa juu masuala ya ardhi yaliyowasilishwa na wananchi wa Kijiji cha Nyamikoma B wilayani Busega  kama kero kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka katika mkutano wa hadhara uliofanyik kjijini hapo.
   Diwani wa Kata ya Kabita wilayani Busega akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Nyakaboja wilayani humo katika Mkutano wa hadhara kwa lengo la kuwahamasisha wananchi kuanza kutekeleza mpango wa kilimo cha umwagiiaji wilayani humo.
   Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (wa pili kulia) akisaini kitabu mara baada ya kuwasili katika Kijiji cha Nyakiboja kata ya Kabita wilayani Busega  kabla ya kuwahutubia wananchi wa eneo hilo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo.
  Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Nyamikoma B Kata ya Kabita, wilayani Busega wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka katika Mkutano wa hadhara kuwahamasisha kuingia na kuanza kutekeleza mpango wa kilimo cha umwagiiaji wilayani humo.
   Baadhi ya Maafisa wa Sekretarieti ya Mkoa walioambatana na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka katika ziara yake ya kuwahamasisha wananchi wa Busega kutekeleza mpango wa kilimo cha umwagiliaji.


  Na Stella Kalinga, Simiyu

  Serikali Mkoani Simiyu  imewashauri wakulima wote wilayani Busega  wenye mashamba yaliyo karibu na ziwa Victoria kuorodhesha jumla ya ekari za mashamba waliyonayo ili waweze kusajiliwa na kuingizwa katika mpango wa  kilimo cha umwagiliaji kinachotarajiwa kuanza mapema mwaka huu.


  Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka katika ziara yake maalum ya kuwatembelea wananchi wa vijiji vilivyopo  kandokando ya ziwa Victoria Wilayani Busega, ambapo ameanza na vijiji vya Nyamikoma na Nyakaboja  kata ya Kabita.


  Mtaka alisema endapo wakulima watakuwa tayari kufanya  kilimo cha umwagiliaji  kwa kufuata ushauri wa kitaalamu na kutumia mbegu bora watapata mazao mengi yatakayokubalika katika soko la ndani na nje ya Mkoa ikiwa sambamba na  na kujikwamua kiuchumi.


  Alieleza kuwa  lengo la serikali  ya Mkoa ni kuhakikisha dhana ya mapinduzi ya kilimo kwa mfumo wa umwagiliaji inatekelezwa kwa vitendo kwa kuwapatia elimu ya kitaalamu wakulima ili waweze kuzalisha mazao bora na mengi yanayotosheleza soko la ndani ya nchi na kupunguza uagiziaji mazao nje ya Mkoa.


   “Tumekuja kama mkoa kuzungumza na wananchi ili wale watakaokuwa tayari waanze kutekeleza. Ni lazima tufanye maamuzi ya kufanya mapinduzi ya kilimo kama watu tulio kandokando ya ziwa Victoria ili uwepo ziwa utunufaishe” amesema Mtaka.


  Aidha alifafanua kuwa kilimo hicho katika maeneo ya  Wilaya ya Busega  kitahusisha mazao ya Mpunga,  mboga mboga, mahindi na mazao jamii ya mikunde, hivyo wakulima kwa kushirikiana na Serikali wanatakiwa kuendelea kubuni mbinu  mbalimbali za uzalilishaji mazao hayo kwa wingi ili kwenda sambamba na fursa ya masoko ya ndani na nje ya nchi hasa kwa mazao ya mikunde.


  Mtaka ameongeza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi imetoa fedha katika Taasisi za fedha kwa ajili ya shughuli za kilimo, hivyo akawashauri wananchi kujiunga katika vikundi ili iwe rahisi kuwatambua na kuwawezesha kwa pembejeo na miundombinu  ya kilimo cha umwagiliaji kulingana na makubaliano yatakayowekwa.


  Hata hivyo Mkuu huyo wa Mkoa amewasihi vijana nchini kujiajiri wenyewe kupitia kilimo hicho kwa lengo la kupambana na changamoto ya ukosefu wa ajira badala ya kukimbilia mijini wakati fursa za kujiajiri zipo nyingi vijijini.


  Kwa upande wake Mkulima wa kilimo cha mpunga Charles Malombo kutoka  katika kijiji cha Nyakaboja alisema licha ya serikali kuwa na mpango mzuri kwa kuwapatia matumaini makubwa ya mafanikio katika kilimo cha umwagiliaji bado wanahitaji msaada wa kitaalamu utakaowasaidia kutumia teknolojia ya kisasa  katika umwagiliaji maji  ya ziwa Victoria ili waweze kupata mazao mengi zaidi ya wanayopata kwa sasa.


  Naye Samuel Chochomo ambaye ni Mkulima wa mazao mbali mbali ya Mboga mboga alikiri kilimo hicho ndicho kitakachowatoa wakulima na wananchi katika janga la njaa

    

  Alieleza kuwa   kilimo cha kutumia teknolojia ya umwagiliaji maji ni kizuri na  hakitegemei msimu wa mvua, wakulima wanaweza kulima wakati wote kama  wakiwa na miundombinu mizuri ya upatikanaji wa maji kutoka Ziwani na mipira imara ya kusambazia maji.


  Wilaya ya Busega ni wilaya pekee Mkoani Simiyu iliyo na maji ya uhakika ya Ziwa Victoria na eneo la takribani ekari 7200 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji.  0 0

   Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhan akitoa ufafanuzi kuhusu uwekaji wa kituturi cha kupigia kura wakati wa mafunzo ya Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo na Kata watakaosimamia uchaguzi mdogo wa Madiwani utakaofanyika katika kata 20 za Tanzania Bara na Ubunge katika jimbo la Dimani  Januari 22, 2017 leo mjini Dodoma.
  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhan akionyesha mfano wa namna ya kuweka vituturi vya kupigia kura vituoni ili kuwawezesha wananchi kupiga kura kwa wakati wa mafunzo ya Wasimamizi wa Uchaguzi mdogo wa Madiwani utakaofanyika katika kata 20 za Tanzania Bara na Ubunge katika jimbo la Dimani  Januari 22, 2017.
   Kaimu Naibu –Uendeshaji wa Uchaguzi, Bi. Irene Kadushi Tutah  akiwasilisha mada kuhusu Kujumlisha na Kutangaza Matokeo ya Ubunge na Madiwani wakati wa mafunzo ya Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo na Kata watakaosimamia uchaguzi mdogo utakaofanyika Januari 22, 2017.
   Washiriki wa mafunzo ya Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo na Kata kutoka Kanda ya Kaskazini na Pwani wakiendelea na mafunzo ya kuwajengea uwezo wasimamizi hao wakati uchaguzi mdogo wa Madiwani utakaofanyika katika kata 20 za Tanzania Bara na Ubunge katika jimbo la Dimani  Januari 22, 2017.
    Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo wakiwemo Wakurugenzi wa Halmashauri wakifuatilia kwa makini mafunzo ya Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo na Kata watakaosimamia uchaguzi mdogo Januari 22, 2017 mjini Dodoma. Picha na Aron Msigwa - NEC

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Arusha  Mhe. Mrisho Gambo akifungua kikao cha Wadau wa Elimu Mkoa wa Arusha
   Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akishirikiana na wataalamu kuweka mitambo sawa kwa ajili ya wadau wa Elimu kuwasilisha taarifa.
   Viongozi wa Halmashauri ya Ngorongoro wakifuatilia Kikao cha Wadau wa Elimu
   Wadau wa Elimu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Karatu
       Kaimu Afisa Elimu Mkoa Ndg. Emmanuel Mahondo akiwasilisha taarifa ya Elimu Mkoa wakati wa Kikao cha wadau wa Elimu kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

  0 0

  Na Angella Msangi,Dar Es Salaam

  WAKAZI wa jiji la DAR ES SALAAM wamepongeza huduma mbali mbali za matibabu zinazotolewa kwenye Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo kwenye hospitali ya TAIFA ya MUHIMBILI,ambapo wamesema kuwa kwa sasa matibabu ya moyo yamepata ufumbuzi tofauti na miaka mingine ilivyokuwa hapa nchini.

  Wakizungumza hospitalini hapo, baadhi ya wananchi hao waliokuwa katika nyuso za furaha mara  baada ya kupata huduma nzuri, wameeleza kuwa hospitali hiyo inafaa kuwa mfano wa kuigwa kutokana na namna ya huduma zinavtolewa kuanzia madaktari mpaka wauguzi na watoa huduma wa kawaida.

  REUBEN MTAITA (79) mkazi wa KONGOWE nje kidogo ya jiji la DAR ES SALAAM amesema tangu ameanza kutibiwa katika hospitali hiyo ameweza kupata nafuu kwa matatizo ya moyo yanayomsumbua, huku akibainisha kuwa huduma ziko katika viwango na hujutii kupata matibabu katika hospitali hiyo.

  “Ni kweli na wazi hospitali hii inatoa huduma bora kabisa , hata namna madaktari wanavyokuhudumia inatia moyo, na kwamba wako karibu na wagonjwa kuhakikisha unapata matibabu sahihi”alisema MTAITA

  Kwa upande wake mkazi wa TEMEKE KHADIJA OMARY(30) amesema anafuraha huduma za hospitali hiyo na kwamba tangu aanze kutibiwa ameona unafuu mkubwa na kwamba hali yake inazidi kuimirika.

  “Huduma zipo kwenye ubora na wagonjwa tuna hudumiwa bila ubaguzi hili jambo limenifurahisha kabisa”alisema KHADIJA.

  Baadhi ya madaktari, BASHIR NYANGASA na GEORGE LONGOPA wamesema kwamba wanajitahidi kwa uwezo wao kuhakiksha wagonjwa wanapata matibabu ya uhakika na yenye viwango vya juu ili kuhakikisha wagonjwa wa moyo wanakuwa salama .

  “Tunajitahidi kwa uwezo wetu kuwahudumia wagonjwa wote wanaofika katika taasisi yetu katika kiwango cha hali ya juu na kama ulivyoona mwenyewe, wagonjwa wanaridhika na matibabu wanayopata” alisema Dkt.NYANGASA alipokuwa akizungumza na Mwandishi wa habari hii

  Naye mkurugenzi mkuu wa taasisi hiyo ya MOYO YA JAKAYA KIKWETE Professa Mohamed Janabi, amesema kwamba ,katika hospitali hiyo wanaendelea kutoa huduma zilizo bora na kuwashauri wananchi nchini kujiuga na huduma za bima afya ili kuweza kumudu gharama za ugonjwa wa moyo katika matibabu na vipimo vyake.

  “Mwananchi akiwa kwenye mpango wa bima ya afya ni rahisi sana ana unafuu katika kutibwa kwani ni gharama kubwa , lakini mtu anapokuwa amejiunga katika mfuko wa bima ya taifa unaweza kugharimia “ alisema Dkt.Janabi.

  Amesema kwa sasa hospitai hiyo iamdelea na maboresho mbali mbali hasa katikaeneo la huduma kwa wateja ambapo amesema wafanyakazi waliopo katika idara hiyo wanapataiwa mafunzo mbali mbali ya kuweza kuhudumia wagnjwa wanaokuja katuka taasisi hhiyo.

  Kwa mujibu wa Dkt.Janabi mpaka sasa taasisi hiyo iliyoanzishwa mwaka 2015 mwaka jana iliweza kufanya upasuaji wa moyo kwa wagonjwa wenye jumla ya 973 ambapo ameongeza kuwa hospitali hiyo imepunguza kwa asilimia 80 kwa wagonjwa kwenda nje ya nchi kutibiwa na badala yake hutibiwa hapa nchini katka hospitali hiyo kutokana na wataalamu waliopo . 
  Hata hivyo amesema mbali na wagonjwa wa hapa nchin kutibiwa katika hosptali hiyo pia wagonjwa kutoka nchini za Comoro,Burundi,Congo na Uganda wamekuwa wakitibiwa katika taasisi hiyo.

  0 0


   Afisa Uendeshaji wa PSPF, Hadji Hamisi Jamadari, akitoa ufafanuaiz kuhusu kazi zifanywazo na Mfuko huo, hususan uchangiaji wa hiari, (PSS), mwishoni mwa seina ya mafunzo ya siku mbili, kwa watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kitengo cha sheria, iliyomalizika leo Januari 4, 2017. Baada ya semina hiyo wanasheria hao zaidi ya 35 walijiunga na Mfuko huo kupitia mpangio huo wa PSS.

  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
  WATUMISHI wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kitengo cha sheria, wamejiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF baada ya kuhudhuria semina ya mafunzo ya siku mbili iliyomalizika leo Januari 4, 2017.

  Semina hiyo iliandaliwa na Mfuko huo kufuatia ombi la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makodna, kutaka wanasheria wa ofisi yake, wapewe semina ili kuwajengea uwezo wa kutatua kero za wananchi ambao ni wanachama wa Mfuko huo watakaofika Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa kwa shida zinazohusiana na masuala ya Mafao na Pensheni.

  Katika senmina hiyo iliyoanza Januari 3, 2017, wanasheria hao walipatiwa ufafanuzi wa kina kuhusu shughuli namajukumu yanayotekelezwa na PSPF.
  Meneja wa PSPF huduma kwa wateja, Bi.Leila Magimbi, alitaja majukumu hayo kuwa ni pamoja na  kutambua na kusajili wanachama wapya, kukusanyan michango na kutunza taarifa za michango ya wanachama, kuwekeza michango katika vitegauchumi mbalimbali na kulipa mafao.

  Shughuli nyingine zinazotekelezwa na Mfuko huo ni kulipa mafao kwa wanaostahili kwa mujibu wa sheria, kutunza kumbukumbu za wanachama na wastaafu, kuangalia upya ubora wa mafao na kufanya tathmini ya Mfuko na kuweka mikakati endelevu, aliongeza Bi. Magimbi.

  Pia wanasheria hao walipata fursa ya kuelezwa aina za wanachama wa PSPF ambao ni Watumishi wa Umma, sekta binafsi ambao hawa watachangia katika mfumo wa uchangiaji wa lazima na watu wote walio katika sekta isiyo rasmi, ambao wao watachangia katika Mfumo wa uchangiaji wa Hiari.

  Aidha faina apatazo mwanachama wa PSPF, kwa mujibu wa Kaimu Meneja Mafao, Bw.Haji Moshi, ni pamoja na Fao la uzazi, mkopo wa elimu, mkopo kwa mwajiriwa mpya, mikopo ya viwanja, mikopo ya nyumba, mkopo wa fedha taslimu, mikopo kwa wastaafu yenye masharti nafuu, mafao ya muda mrefu, fao la ulemavu, fao la mirathi, fao la kufukuzwa au kuachishwa kazi, na bima ya afya.

  Akifunga semina hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, amewataka wanasheria hao kutumia busara wanapohudumia wananchi kwani kwa kufanya hivyo itawasaidia kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi kama ilivyokusudiwa.

  “Huko mtakutana na watu wa aina mbalimbali, wengine wamesoma zaidi yenu, wengine hawakupata fursa ya kusoma kama nyinyi, kwa hivyo mnao wajibu wa kutunmia busara katika kuhudumia wananchi wa kada tofauti tofauti.” Aliwaasa Bw. Mayingu.

  Aidha mwakilishi wa wanasheria hao, Bi.Georgia Ephraim Kamina, amesema semina hiyo imekuwa na manufaa makubwa kwao, na kuishukuru PSPF kwa kuandaa semina hiyo na kuuomba uongozi wa Mfuko, kujenga mahusiano ya kudumu baina ya Mfuko na wanasheria hao katika utendaji kazi wao wa kuhudumia wananchi.
  Afisa Masoko Mwandamizi wa PSPF, Bw. Magira Werema, akifafanua masuala kadhaa yahusuyo shughuli za Mfuko na faida zake kwa wanachama
   Afisa wa idara ya Pensehni ya Mafao wa PSPF, Bw.Andrew Dayson akitoa mada
   Kaimu Meneja wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS), wa Mfuko huo, Bi.Sophia Mbilikira, akielezea faida za kuwa mwanachama kupitia uchangiaji wa hiari
   Baadhi ya washiriki (wanasheria), wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa na wataalamu wa PSPF
   Baada ya kuelewa "somo" hatimaye ilifika wakati wa wanasheria hao kujiunga na Mpango wa uchangiaji wa Hiari, (PSS), na hapa wanajaza fomu


   Obote Simon, akikabidhiwa kadi ya kujiunga na uanachama wa PSPF, kupitia mpango wa PSS, kutoka kwa Kaimu Meneja wa PSS, Bi. Sophia Mbilikira
   Bw. Mahfoudh K. Mohammed (kushoto), akipokea kadi yake
   Bw. Emmanuel S. Nyanza, (kushoto), akipokea kadi yake
   Bw. Albert Nyange, (kushoto), akipokea kadi yake
   Kongozi wa Wanasheria wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Georgia Sphraim Kamina, akizunguzma
   Bi. Kissa, akiuliza swali kuhusu mikopo ya elimu

   Meneja Masoko na Uhusiano wa PSPF, Bi. Costantina Martin, (kulia), akiwa amejiungana wanasemina wakati semina hiyo ikielekea ukingoni


   Sehemu ya utunzaji nyaraka kwenye mfumo wa makabati yanayoendeshwa kielektroniki

   Msaidizi maalum wa Mkuu wa Mkoa wa Dares Salaam, Bw. Daniel P. Jenga, (kushoto), akifurahia kuonyeshwa faili lake ndani ya dakika moja
   Afisa wa PSPF akiwa kazini
   Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu akitoa nasaha zake wakati wa kufunga semina hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma na uendeshaji, Bi. Neema Muro
   Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu akitoa nasaha zake mbele ya wanasemina hao wakati wa kufunga semina hiyo
   Wanasemina wakitembelea kitengo cha kutunza kumbukumbu cha PSPF

   Meneja Huduma kwa Wateja, PSPF, Bi. Leila Magimbi

  0 0

   Naibu waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Masauni akiwa na Mkuu wa Magereza kamishna Juma Malewa wakizungumza  na Waandishi  wa Habari leo katika gereza la Ukonga Jijini Dar es salaam.
   .Naibu Waziri  wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Masauni akizungumza jambo na  Mratibu wa Ujenzi wa Nyumba za Askari Magereza Bw. Julious Chege  katika gereza hilo la Ukonga,jijini Dar.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamad Masauni akizungumza jambo na Kaimu kamishna wa Jeshi la Magereza Juma Malewa,mara baada ya kukagua Kiwanda cha kutengeneza Samani Katika gereza la Ukonga.
   

   Na Anthony John Glob Jamii.

  NAIBU Waziri  mambo ya Ndani  Mhandisi Hamad Masauni amelitaka jeshi la zimamoto na  Uhamiaji kutoshona sare zao za uraiani, badala yake wakashone katika jeshi  la Magereza ili kubana matumizi ya serikali.

  Masauni ameyasema hayo  leo katika  ziara yake ya kutembelea  Magereza Ukonga,jijini Dar, ambapo amekagua  Kiwanda  cha Magereza kinachojishughulisha na ushonaji wa nguo za wafungwa na nguo za askari Magereza.

  Sanjari na hayo Mhandisi Masauni ametoa wito  kwa Watanzania kwa kununua  bidhaa mbali mbali zinazo tengenezwa na jesi la Magereza ili kuunga mkono kwa kazi nzuri wanazozifanya.
   
  Aidha amewapongeza askari wa jeshi la  Magereza kwa kujitolea kujenga nyumba zao bila kusubiri serikali kuwajengea na kuwaahidi kuwa Serikali itaandaa bajeti Mwakani ili kumalizia maeneo machache yaliyo baki.

  Naye   kaimu Mkuu wa Magereza  Kamishina Msaidizi . Juma Malewa amesema Jeshi hilo linakabiliwa na uhaba wa vitendea kazi  kama mashine za  kushonea nguo, na mashine za za ufundi selemala , ukosefu wa mtaji wa kuendesha shughuli za kilimo,  hivyo amesema pindi serikali itakapo wawezesha watajitosheleza kwa chakula na mahitaji mengine.

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana leo ameongoza mazishi ya aliyekuwa Katibu wa CCM wilaya ya Monduli mkoani Arusha, Jacob Nkomola, yaliyofanyika Mtoni Kijichi, Temeke Dar es Salaam.

  Katika mazishi hayo walikuwepo piaa viongozi wengine wa ngazi ya juu wa CCM, wakiwemo Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu. Ngemela Lubinza.

  Nkomola ambaye alifariki juzi jijini Dar es Salaam, mwili wake ulitangulia kuagwa nyumbani kwake, Mtoni Kijichi na baadaye kupelekwa katika Kanisa la Kianglikana, Mtoni Kijichi kabla ya kuzikwa katika makaburi yaliyopo Kijichi  saa kumi jioni. Kuona mfululizo wa picha tangu kuagwa mwili hadi maziko, tafadhali/>BOFYA HAPA

  0 0

  Waziri mkuu Kassim Majaliwa leo amewasili mkoani Ruvuma na kupokelewa na Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa , wakuu mbali mbali waidara , viongozi wa dini na wakazi wa mkoa huo. Tizama mapokezi yake uwanja wa denge wa mkoa wa ruvuma katika video hii pia tutakuletea taarifa ya mkoa wa ruvuma pamoja na maagizo ya waziri mkuu aliyoyatoa katika kikao kilichofanyika ukumbi wa ikulu ndogo ya songea.

  0 0


  *Asema kama tabia hiyo ilikuwepo, mwisho wake ni jana

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Wakurugenzi wote wa Halmashauri na Manispaa nchini kuacha kutoa fedha taslimu na kuwapa madiwani ili zikafanye kazi za maendeleo.

  Badala yake amewataka waandae mfumo maalum wa kutoa fedha hizo kama zinavyotolewa fedha za mfuko wa Jimbo ambazo ni maalum kwa wabunge lakini zinatumika kwa shughuli za maendeleo jimboni.

  Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumatano, Januari 4, 2017) wakati akizungumza na viongozi na watendaji wa mkoa wa Ruvuma mara baada ya kupokea taarifa ya mkoa huo kwenye Ikulu ndogo Manispaa ya Songea.

  “Nimepata taarifa kuwa fedha za maendeleo kwa madiwani zinakabidhiwa mkononi. Hapana. Msiwape fedha mkononi, bali zifuate mfumo wa utoaji fedha wa Serikali. Kama mlikuwa na matumizi ya aina hiyo, mwisho wake ni jana,” amesisitiza.

  “Fedha za mfuko wa Jimbo ni za Mbunge lakini hapewi mkononi bali zinapelekwa kwenye Halmashauri na yeye anahusika kwenye kikao cha maamuzi. Anakubaliana na madiwani wenzake ni miradi ipi ipatiwe fedha, ambayo mara nyingi inakuwa imekwishaidhinishwa na vikao husika,” ameongeza.

  Alisema makusanyo ya fedha yanayofanywa na Halmashauri hayana budi kuangaliwa pia na jinsi fedha hizo zinavyotumiwa. “Lazima tukishakusanya tuangalie tumepata kiasi gani, siyo kukaa na kuamua kutoa sh. laki tano tano kwa kila diwani. Suala la matumizi ni muhimu sana, ni lazima fedha hizo ziende kwenye miradi ya maendeleo,” amesisitiza.

  Amesema kuna baadhi ya watu wanaamua kugawana fedha kwa kigezo cha maendeleo lakini wanaishia kutumia fedha hizo kwa kigezo cha kujengeana uwezo (capacity building). “Hii si sahihi na jana nimepiga marufuku posho za aina hii pamoja na fedha za vitafunwa kwa sababu zinaishia kwa wakubwa wachache na waliozikusanya hawapati chochote,” ameongeza.

  Akizungumzia kuhusu ukusanyaji wa mapato kwenye Halmashauri, Waziri Mkuu amewataka waangalie baadhi ya makampuni ambayo yanajitokeza kutoa vifaa vya kukusanya ushuru lakini wanatumia software ambazo zinawanufaisha na wao pia.

  “Tumieni watu wenu wa TEHAMA kukagua mifumo hii kwani kuna baadhi ya watu wanaoleta zile mashine siyo waaminifu. Watu wa TEHAMA wazikague na kujiridhisha kuwa hakuna mianya ya wizi. Tumegundua wako wanaokusanya fedha, lakini asilimia 80 inangia kwenye akaunti za Halmashauri na asilimia 20 inapelekwa sehemu wanayoijua wao. Ukiangalia unaona mapato yanaongezeka lakini kumbe pia unaibiwa. Jaribuni kuchunguza na mjiridhishe na hizo software zao,” amesisitiza.


  IMETOLEWA NA
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  JUMATANO, JANUARI 4, 2017.

older | 1 | .... | 1089 | 1090 | (Page 1091) | 1092 | 1093 | .... | 1897 | newer