Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1088 | 1089 | (Page 1090) | 1091 | 1092 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke (kushoto) wakiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Ihungo mkoani Kagera. Shule hiyo inajengwa upya kufatia kuathirika na tetemeko la Ardhi lililotokea mkoani humo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitazama wakati Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke alipokuwa akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Ihungo mkoani Kagera. Wakwanza kushoto ni Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa uingereza hapa nchi Sarah Cooke wakikagua ujenzi wa majengo ya Shule ya Sekondari ya Wavulana Ihungo mkoani Kagera.
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo nchini (TBA) Elius Mwakalinga akitoa maelezo ya mradi huo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa ukaguzi.
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo nchini Elius Mwakalinga akitoa maelezo ya mradi huo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa ukaguzi.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Bukoba mjini(CHADEMA) Wilfred Lwakatare mara baada ya kuwasili katika shule ya Sekondari Ihungo mkoani Kagera
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Charles Masinde mmoja wa wanachi mkoani Kagera aliyeamua kujenga nyumba yake mwenyewe mara baada ya tetemeko. Rais Dkt. Magufuli amemuahidi mwananchi huyo kuwa atampatia mabati 30 kwa ajili ya kuezekea nyumba yake.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifafanua jambo wakati alipokuwa akikagua majengo ya shule ya Sekonadri ya Wavulana Ihungo ambayo yanajengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitabu cha wageni pamoja na balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke mara baada ya kuwasili katika uwanja wa mkutano katika Shule ya Sekondari Ihungo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa maeneo ya Ihungo Sekondari Mkoani Kagera hawapo pichani mara baada ya kukagua na kuweka jiwe la msingi katika Shule ya Sekondari Ihungo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu wakitoka kwenye ukaguzi wa shule ya Sekondari Omumwani mkoani Kagera. PICHA NA IKULU.

  0 0

  Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wakazi wa Bukoba mjini mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili mkoani Kagera.
  Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wakazi wa Muleba mkoani Kagera mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili mkoani humo.
  Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wakazi wa Muganza Wilayani Chato mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili mkoani Kagera. PICHA NA IKULU


  0 0

  Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Anglikana Jimbo la Tarime mkoani Mara, akiongoza ibada ya mazishi ya marehemu, bibi Catherine Seba Marwa (89). Mazishi yamefanyika hii leo katika Kata ya Kenyamanyori wilayani Tarime.
  Na BMG
  Ndugu, jamaa na marafiki wakiuaga mwili wa marehemu
  Mtoto wa marehemu (kushoto) akiwa na shemeji yake, wakiweka shada
  Viongozi wa dini wakiweka mashada
   Marehemu, bibi Catherine Seba Marwa (89), enzi za uhai wake. Mola aipumzishe roho ya marehemu, mahala pema, peponi, Amina!


  0 0  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (katikati) akizungumza na vikundi vya wanawake na vijana kutoka katika Jiji la Arusha kabla ya Kukabidhi hundi za Mikopo ya robo ya kwanza na ya Pili kwa mwaka wa Fedha 2016/2017.

  Nteghenjwa Hosseah, Arusha

  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo amefungua mafunzo ya ujasiriamali kwa vikundi vinavyokopeshwa na kutoa mikopo kwa vikundi 85 vya wanawake na vikundi 40 vya vijana kutoka katika kata zote za Jiji la Arusha.

  Akikabidhi hundi zenye thamani ya Sh Mil 624 kwa vikundi hivyo ikiwa ni mikopo ya robo ya kwanza na ya pili kwa mwaka wa fedha 2016/2017 Mhe. Gambo amewataka kinamama na vijana kutumia fedha hizo kwa shughuli zilizokusudiwa ili ziweze kuleta manufaa na kuwatoa katika lindi la umasikini.

   “Mikopo hii inatolewa ili kuendeleza shughuli za kijasiriamali ambazo ndizo zilizopelekea mkidhi vigezo vya kupata Fedha; Nimatumaini yangu fedha hizi zitawawezesha kuongeza mitaji yenu na kuwapa ari ya kujituma zaidi huku mkizingatia nidhamu ya pesa ili muweze kuzirejesha kwa wakati na makundi mengine waweze kupata fedha hizo”Alisema Rc Gambo.
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(Katikati) akikabidhi hundi ya Tsh Mil 425 kwa wawakilishi wa Wanawake Bi. Mariamu Okash(Kata ya Kati) na Rose Charles(Kata ya Olorieni).

  Aliongeza kuwa tofauti na mikopo hii ya halmashauri baada ya kuwawezesha vijana waendesha boda boda kwa kuwapatia Pikipiki 200 kundi litakalofuata ni wakinamama ambao watanufaika na Fedha zitakazorejeshwa na vijana hao kwa kupewa mitaji midogomidogo kadiri ya uhitaji.

  Aidha Rc Gambo alimuagiza Mkurugenzi wa Jiji kuunda timu maalumu ya kuchunguza utoaji wa Mikopo kwa Kipindi cha Miaka mitatu kama ilifuata taratibu, vikundi vilivyonufaika kama ni hai  na hali ya urejeshaji.

  Naye Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mhe. Kalisti Lazaro Bukhay ambaye alishiriki katika zoezi  la utoaji mafunzo na kukabidhi hundi amesema Kikundi ambacho hakitarejesha fedha zote za mkopo ama kuchelewesha marejesho kwa namna yeyote ile hakitapatiwa mkopo katika mwaka unaofuata ila wale watakaofanya vizuri katika biashara zao na kukuza mitaji wataongezewa kiasi cha kukopa kulingana na hali ya shughuli zao.
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Mrisho Gambo akikabidhi hundi ya Tsh Mil 199 kwa wawakilishi wa Vijana Amos Kosani (Daraja II) na Janeth Prosper (Kata ya Unga Ltd).

  Mikopo hiyo inayotolewa kwa mujibu wa Sheria na miongozo inayoelekeza  asilimia kumi ya Mapato ya ndani ya Halmashauri kutolewe kama Mikopo ya riba nafuu kwa vikundi vya wananwake na vijana na kwa  jiji la Arusha kiasi kinachotakiwa kutolewa ni Bil 1.2 kwa Mwaka huu wa Fedha hivyo kiasi kilichotolewa ni kwa kipindi cha nusu mwaka.

   Fedha hizo zinatolewe kwenye Saccos au Vicoba vyenye nguvu katika Kata husika ili kurahisisha usimamizi na urejeshaji wa mikopo hiyo. Hivyo Saccos na Vicoba ndizo zinazokopesha vikundi vilivyoainishwa na Kamati ya Maendeleo ya Kata (WDC) kwa riba ya asilimia 10 na wao hubaki na asilimia 8 kwa ajili ya shughuli za uendeshaji na kurejesha Halmashauri riba ya asilimia 2 tu.
  Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Eng. Gaston Gasana (kwanza kulia) akitoa taarifa fupi ya Utoaji wa Mikopo ya Wananwake na Vijana kwa robo ya kwanza na ya Pili kwa mwaka wa Fedha 2016/2017 kwenye hafla ya kukabidhi hundi za mikopo hiyo.
  Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro(Kwanza kushoto) akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo kukuabidhi hundi kwa vikundi vya Wanawake na Vijana wa Jiji la Arusha.
  Vikundi vya Wanawake na Vijana kutoka Kata mbalimbali za Jiji la Arusha wakimskiliza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (hayupo Pichani) kabla ya kukabidhiwa Mikopo inayotokana na asilimia kumi ya mapato ya ndani.

  0 0


  Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Zubery Mwombeji.

  ....................

  Kijana anayejulikana kwa jiana la Patrick Malindisa ( 29 ) mkazi wa Namanyigu kata ya mshangano Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma,anashikiliwa na jeshi kwa kusadikiwa kumuua baba yake mzazi anitwaye Atanasi Malindisa. Mkasa Mzima huu hapa.


  0 0

   hawa ni baadhi ya wananchi wa kabila la kimasai ambalo linakaliwa na tuhuma za kuozesha wasicha wenye umri mdogo.
  hili ni jengo la shirika lisilo la kiserikali la Ilula Ophan program (IOP)

  Na Fredy Mgunda,Iringa
   
  Shirika lisilo la kiserikali la Ilula Ophan program (IOP) limeendelea kukemea na kutoa elimu juu ya ndoa za utotoni kwa kuwa zinarudisha maendeleo nyuma ya wasichana wa jamii ya kimasai.

  Akizungumza na blog hii Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Ilula Ophan program (IOP) Edson Msigwa alisema kuwa tatizo la ndoa za utotoni katika kabila la wamasai bado ni kubwa.

  Msigwa alieleza jinsi gani wanavyofanya shughuli za kukemea na kutoa elimu juu ya ndoa za utotoni katika jamii ya wamasai

  “Tunajitahidi kuwafikia jamii zote za wilaya ya kilolo mkoani iringa kwa lengo la kutoa elimu lakini tunakumbana na changamoto kutoka kwa wazazi ambao bado wana mila potofu hasa huku umasaini”alisema Msigwa

  Aidha Msigwa alisema kuwa kila siku ndoa za utotoni zinaongezeka huko vijijini  na kuitaka serikali kukubali takwimu wanazozitoa kwa kuwa zinaukweli.

  “Sisi hapa Ilula Ophan program (IOP) tunaishi na wasichana wa kabila la kimasai wafanikiwa kukimbia kuozeshwa wakiwa na umri mdogo hebu mwangalie huyo motto joyce alivyo alitakiwa aolewe na umri huu wa miaka kumi nan ne je unafikiri ni haki jamiii inatakiwa kubadili na serikali inatakiwa kuongeza juhudi kulitatua hili”alisema Msigwa

  Naye mmoja wa wasichana wa kimasai aliyekimbia kuolewa akiwa na umri mdogo Joyce Hassani alisema kuwa msichana wa kimasai wakimaliza elimu ya msingi wanalazimishwa kuolewa na familia yake.

  “Mimi na mwenzangu tumemaliza shule tu wametupeleka kucheza ngoma kisha kutaka kutuozesha lakini mungu mwema tulifanikiwa kukimbia na kufika hapa Ilula Ophan program (IOP) japo kuwa wanaume wa kimasi wanakuja hapa kituoni mara kwa mara kutaka kutuiba turudi kule umasaini ili tukaolewe hasa kaka zangu”alisema joyce

  Joyce ameiomba serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali kusaidia kupambana na mila potofu zinazowapotezea malengo wasichana wa kimasai.“Angalia tunavyoteseka saizi tunaishi kama watoto yatima wakati wazazi wetu wapo na wana afya zuri kabisa lakini tatizo kubwa sisi wasichana wadogo wa kimasai tunaolewa tukiwa na umri mdogo sana tunaomba jamii iamuke na kutusaidia kutatua tatizo hilo.”alisema Joyce

  Zipo sababu nyingi na ushahidi mwingi wa kisayansi, unaonyesha kuwa, ndoa na mimba katika umri mdogo ni hatari kwa afya na mstakabali wa maisha yake na mtoto wake.
  Wasichana wanaopata ujauzito na kujifungua katika umri mdogo wengi wao pia hupata tatizo la fisitula - Vescovaginal fistula.

  Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na chama cha waandishi wahabari wanawake (TAMWA) umeonesha kuwa katika mwaka 2012-2013 matukio 228 ya mimba na matukio 42 ya ndoa za utotoni yaliripotiwa nchini tanzania.

  0 0


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Bukoba mjini(CHADEMA) Wilfred Lwakatare mara baada ya kuwasili katika shule ya Sekondari Ihungo mkoani Kagera.

  0 0


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Bukoba mjini(CHADEMA) Wilfred Lwakatare mara baada ya kuwasili katika shule ya Sekondari Ihungo mkoani Kagera.

  0 0

  Kamanda wa bendi ya Ngoma Africa aka FFU ya kule nchini Ujerumani, mwanamuziki Ebrahim Makunja aka Ras Makunja mapema leo ametembelea ofisi ya Michuzi Media Group jijini Dar es Salaam na kukutana na Ankal Issa Michuzi  pichani kulia pamoja na Ahmad Michuzi (Michuzi Jr) kushoto.
  Kamanda wa bendi ya Ngoma Africa aka FFU ya kule nchini Ujerumani, mwanamuziki Ebrahim Makunja aka Ras Makunja mapema leo ametembelea ofisi ya Michuzi Media Group jijini Dar es Salaam na kukutana na Ankal Issa Michuzi  pichani kulia pamoja na Ahmad Michuzi (Michuzi Jr) kushoto,pamoja na Cathbeth Kajuna

  0 0

   Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw.kailima Ramadhani akifungua mafunzo ya siku 3 ya Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya jimbo na Kata na Maafisa wa Uchaguzi leo mjini Dodoma. 
  Baadhi ya Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya jimbo na Kata na Maafisa wa Uchaguzi wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kutekeleza majukumu yao wakati wa Uchaguzi mdogo utakaofanyika Januari 22, 2017 leo mjini Dodoma. Picha na Aron Msigwa - NEC

  Na. Aron Msigwa - NEC
  TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI imewataka Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi wa Uchaguzi mdogo wa Udiwani utakaofanyika katika Kata 20 za Tanzania Bara na Ubunge katika jimbo la Dimani Visiwani Zanzibar Januari 22, 2017 kuzingatia Sheria, Kanuni na Maadili ili Uchaguzi huo uwe Huru na wa Haki.

  Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhan wakati akifungua mafunzo ya siku 3 ya Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya jimbo na Kata na Maafisa wa Uchaguzi leo mjini Dodoma.

  Mkurugenzi Kailima amewataka Wasimamizi hao kuzingatia matakwa ya Katiba, Sheria, Kanuni na miongozo mbalimbali katika kushughulikia mambo yatakayojitokeza wakati wa uchaguzi huo.

  Katika kutimiza majukumu yao wawe tayari kutoa ufafanuzi juu masuala mbalimbali kwa kuzingatia sheria na kutokuwa tayari kukubali kuyumbishwa na mtu yeyote atakayekiuka miongozo, sheria na kanuni za Uchaguzi.

  Amewataka Wasimamizi hao watende mambo yote kwa kuzingatia kanuni na Sheria na kutoa maamuzi sahihi kwa mustakabali wa Taifa na kuwasisitiza kuepuka kutoa upendeleo katika maamuzi wanayoyafanya na wasikubali kuyumbishwa na matakwa ya baadhi ya watu.

  Amewaeleza kuwa milango ya Tume iko wazi pale watakapohitaji ufafanuzi huku akitoa wito kwa Wasimamizi hao kuwasiliana na watendaji wa Tume katika mambo yanayowatatiza ili wapate ufafanuzi.

  Aidha, amewataka wawe makini na hatua ya utangazaji wa matokeo kwa kutoa taarifa kwa wananchi mara kwa mara juu ya hatua zinazoendelea vituoni wakati wa ukusanyaji wa matokea ili kuwaondolea wasiwasi pindi wanapoona matokeo yamechelewa kutolewa.

  " Hili naomba nilisisitize, mnapoona baadhi ya taratibu hazijakamilika tokeni nje muwaambie wananchi nini kinaendelea ili wawe na taarifa na hii itawaongezea imani wananchi wanaosubiri matokeo na kuepusha vurugu vituoni" Amesisitiza Bw.Kailima.

  Amesema kuwa mfumo wa Uchaguzi wa Tanzania ni wa uwazi kwa kuwa kila chama kinakuwa na Wakala anayesimamia maslahi ya chama chake wakati wa uchaguzi, pia uwazi katika hatua zote za uchaguzi ikiwemo upigaji wa kura, uhesabuji wa Matokeo na ujumlishaji wa matokeo ambayo hulinganishwa na vishina.

  Kwa upande wa Mawakala wa Vyama vya Siasa watakaoshiriki katika Uchaguzi mdogo amesisitiza kuwa wanatakiwa kuzingatia maadili ikiwemo kuepuka kutoa matokeo ambayo hawajaruhusiwa kuyasema wakati wa zoezi la upigaji wa kura na wanatakiwa kuapa kiapo cha kutunza siri na kujaza fomu kwa mujibu matakwa ya kikanuni.

  " Wakala Chama cha Siasa haruhusiwi kutangaza matokeo kwa mgombea wake wakati zoezi la kuhesbu kura likiendelea kituoni, na hili nalilisisitiza Mawakala wote ni lazima waape kiapo cha kutunza Siri, ni matakwa ya kikanuni, wakala asiyeapa na kujaza fomu asipewe ridhaa ya kuwa wakala wa chama cha siasa ndani ya kituo" Amesisitiza Bw. Kailima.

  Amesema kila Chama kitakuwa na Mawakala wa aina tatu kwa maana ya Wakala wa Kupiga kura, Wakala wa kuhesabu kura, Wakala wa kujumlisha kura na Kutangaza Matokeo ambao watakua na jukumu la kulinda maslahi ya vyama vyao na wagombea wawapo kituoni, kumsaidia msaidizi wa kituo pamoja na kuangalia taratibu zinavyokwenda kituoni.

  Amesisitiza kuwa maamuzi ya kituo yatatolewa na Msimamizi wa kituo na Wakala ambaye hatakubaliana na maamuzi hayo atajaza fomu namba 16 kuonyesha kuridhika au kutokuridhika.

  Kuhusu mafunzo amesema yanalenga kuwajengea uwezo Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya jimbo na Kata na Maafisa Uchaguzi kuelewa Misingi, Sheria na Wajibu wa namna bora ya kutekeleza majukumu yao katika usimamizi wa hatua zote za uchaguzi ikiwemo upigaji wa kura na utangazaji wa matokeo.

  Ameongeza kuwa Wasimamizi na Waratibu hao watafundishwa maadili ya kuzingatia wakati wakitekeleza majukumu yao ikiwemo maadili ya uchaguzi,maelekezo kwa wasimamizi ya Uchaguzi, wajibu wao, majukumu ya makarani , taratibu za kupiga kura, kuhesabu kura, kujumlisha kura na kutangaza matokeo, kuandaa taarifa za uchaguzi pamoja na masuala mbalimbali kuhusu uchaguzi huo.


  Akizungumzia kuhusu Rufaa za mapingamizi ya wagombea amesema kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 44 (5) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa Sura ya 292, Tume ilipokea Rufaa za wagombea kutoka Kata mbalimbali ikiwemo ya Kijichi - Manispaa ya Temeke, Misugusugu- Halmashauri ya mji Kibaha, Pwani na Kata ya Ihumwa Manispaa ya Dodoma.

  Amesema katika kikao cha Tume cha Desemba, 30, 2016 Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitoa maamuzi ya Rufaa zote kwa haki na kwa kuzingatia kanuni, taratibu, miongozo na sheria zinazosimamia Uchaguzi ikiwemo Rufaa ya Kata ya Ihumwa, Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma ambayo imeondolewa kwa kuwa mkata Rufaa ameiondoa mwenyewe na amejitoa katika ugombea Udiwani kabla Rufaa yake haijasikilizwa.

  Kwa Upande wa Rufaa ya jimbo la Dimani, Zanzibar Bw. Kailima ameeleza kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa mujibu wa kifungu cha 40 (6) ilipokea Rufaa ya mgombea wa Chama Cha Mapinduzi ya kupinga maamuzi ya Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo kumthibitisha mgombea wa Chama cha Wananchi CUF kwamba ni mgombea halali katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Dimani, Zanzibar.

  Bw. Kailima ameeleza kuwa katika kikao cha Maamuzi cha Tume cha kupitia Rufaa za wagombea, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilikubaliana na Uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo kuwa mgombea wa Chama cha Wananchi CUF aliyewekewa pingamizi na mgombea wa CCM amekidhi vigezo na uteuzi wake ni halali hivyo anaweza kuendelea na kampeni za kugombea nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo.

  " Napenda nisisitize kuwa maamuzi yote yaliyofanywa na Tume yamezingatia Kanuni, Taratibu, Sheria na miongozo inayosimamia chaguzi, hali hii ya wagombea kukubali maamuzi ya Tume inatujengea msingi imara wa kuendelea kufanya vizuri zaidi kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 huku tukitimiza majukumu yetu kwa mujibu wa sheria bila kupendelea" Amesisitiza Bw.Kailima.


  0 0


  0 0

  Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa atawasili mkoani Ruvuma kesho kwa ziara ya siku tano ambapo katika ziara hiyo atapita kukagua miradi mbalimbali ndani katika wilaya ya Mbinga na wilaya ya Songea Halmashauri ya Madaba. Kwa undani wa habari hii hii hapa video yake. 


  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga akimkabidhi cheti mmoja ya mhitimu ambaye ni mtoto aliyekimbia ukeketaji kwenye jamii yake na kujiunga na Kituo cha Kulea Watoto waliokimbia Kukeketwa cha (ATFGM-Massanga)

  Vijana wakifanya igizo la kupinga Ukeketaji dhidi ya watoto.
  Mkurugenzi wa Kituo cha Kulea Watoto waliokimbia Kukeketwa cha (ATFGM-Massanga) Sister Stella Mgaya akiongea wakati wa mahafali mahafali ya wasichana 46 waliokimbia ukeketaji na kushukuru juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na uongozi wa wilaya ya Tarime kukabiliana na tatizo hilo na kuendelea kuomba wadau kujitokeza kuwaendeleza watoto wanaohitimu kituoni hapo.
  Mkuu wa Wilaya ya Bunda Bi.Lydia Bupilipili akiongea wakati wa mahafali mahafali ya wasichana 46 waliokimbia ukeketaji na kuwasisitiza wazazi na walezi kubadilika na kuachana na imani potofu ya ukeketaji ili kuwawezesha kutimiza malengo yao.
  Mangariba wastaafu(Kina Mama na Kinababa Wakisasa) wakila kiapo cha kuacha na kutoendelea na ukeketaji.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga akimkabidhi Moja ya Ngariba Mstaafu (Mama wa Kisasa) cheti kutoka cha mafunzo waliyopewa baada ya kuachana na ukeketaji.
  Mkurugenzi wa Kituo cha Kulea Watoto waliokimbia Kukeketwa cha (ATFGM-Massanga) Sister Stella Mgaya akimkabidhi Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga cheti cha utambuzi katika harakati za kukabiliana na ukeketaji.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga akiwakabidhi Mangariba wastaafu(Kina Mama na Kinababa Wakisasa) vitendea kazi watakavyotumia katika shughuli zao mpya baada ya kuachana na ukeketaji na kuamua kujiwekeza katika ujasiriamali.
  Mkurugenzi wa Kituo cha Kulea Watoto waliokimbia Kukeketwa cha (ATFGM-Massanga) Sister Stella Mgaya akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Watoto kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi.Margareth Mussai.
  Mkuu wa Wilaya ya Tarime Bw. Glorious Luoga akiongea wakati wa mahafali ya watoto waliokimbia kukeketwa na kujiunga katika kituo Watoto waliokimbia Kukeketwa cha (ATFGM-Massanga) ambapo aliwataka wazazi wanaowatenga na kuwalazimisha kuwakeketa watoto waliohitumu mafunzo kuacha tabia hiyo kwani watachukuliwa hatua kali za kisheria.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga akiongea wakati wa mahafali ya watoto waliokimbia kukeketwa na kujiunga katika kituo Watoto waliokimbia Kukeketwa cha (ATFGM-Massanga) ambapo alisisitiza kuwa serikali itaendelea kuwachukulia hatua wazazi na jamii inayoendelea na kitendo kiovu cha ukeketaji kwa watoto wa kike.

  Mkurugenzi wa Kituo cha Kulea Watoto waliokimbia Kukeketwa cha (ATFGM-Massanga) kilichopo Tarime Vijijini Sister Stella Mgaya akimkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga alipofika wakati wa mahafali ya wasichana 46 waliokimbia ukeketaji. 
  Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga akisaini kitabu cha wageni alipofika katika Kituo cha Kulea Watoto waliokimbia Kukeketwa cha (ATFGM-Massanga) pembeni ni Mkurugenzi wa Kituo hicho Sister Stella Mgaya.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga akitembelea maeneo mbalimbali katika Kituo cha Kulea Watoto waliokimbia Kukeketwa cha (ATFGM-Massanga).
  Baadhi ya watoto waliokimbia ukeketaji wakiwa katika maandano kuelekea eneo walilofanyia mahafali. 
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga na Mkuu wa Wilaya ya Tarime Bw. Glorious Luoga wakiwaongoza watoto waliokimbia ukeketaji kwenye maandamano wakati wa mahafali leo Tarime. 
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga na Mkuu wa Wilaya ya Tarime Bw. Glorious Luoga wakiangalia baadhi ya bidhaa vilivyotengenezwa na Mangariba waliostaafu (kina mama na Baba wakisasa) wakati wa mahafali ya wasichana 46 waliokimbia ukeketaji.
  Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Sihaba Nkinga akiteta jambo na Mkurugenzi wa Kituo cha Kulea Watoto waliokimbia Kukeketwa cha (ATFGM-Massanga) Sister Stella Mgaya
  PICHA NA IDARA YA HABARI 


  0 0


  Mkuu wa Mkoa Godfrey Zambi akiwa anaongea na wanakijiji wa Kijiji cha Makanjiro

  Mkuu Wa Wilaya ya Ruangwa Joseph Mkirikiti akiwa anaongea na wananchi wa kijiji cha Mandawa(Na: Mwanakheri Ahmed wa Ruvumatv.com)


  …………………………………
  Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi amepiga marufuku kufanyika kwa shughuli zozote zile za kimila zinazotumia chakula kuanzia mwezi wa huu wa Disemba mpaka Mei 2017.

  Shughuli hizo ni pamoja na Unyago, Ndoa na Ngoma za Majini. Alisema shughuli hizo zinazofanywa na Wananchi zimekuwa zinatumia chakula kingi hali hii inaweza kupelekea kutokea kwa janga la njaa mkoani hapo.
  Mkuu huyo wa Mkoa wa Lindi aliwataka Wananchi kuwa wavumilivu na waelewa kwani janga la njaa halichagui Mkoa bali matumizi mabovu ya chakula yanaweza kuleta janga hilo kwa Wananchi wote.

  “Sitaki kuwa Mkuu wa Mkoa ambaye Mkoa wangu umekutwa na janga la njaa kwani hii ni aibu kubwa hivyo Watu wawe makini katika matumizi ya chakula hata kama chakula wanalima kwa nguvu zao wenyewe“.

  Wakati huo huo Mhe. Zambi aliwataka Wananchi wa Ruangwa wajenge vyoo imara na vya matumizi ya muda mrefu, ili kuweza kujiepusha na maradhi ya Kipindupindu kama ambavyo yanaikabili Wilaya ya Kilwa.

  Aidha, Mkuu wa Mkoa aliwataka Watendaji wa vijiji kusimamia zoezi la kila Mwananchi wa eneo lake anakuwa na choo imara na Mtu atakaekaidi kufanya ujenzi wa choo cha nyumbani kwake basi achukuliwe hatua za kisheria.

  Vilevile aliwasa Wananchi kuwa na matumizi mazuri ya pesa wanazoipata za kuuza korosho au fidia wanazolipwa na kuacha matumizi mabovu ya pesa hizo kama ambaVyo inafanywa na baadhi ya Watu.

  Mhe. Zambi aliwakata Wananchi kutumia pesa wanazozipata katika kutengeneza maisha yao kama katika kusomesha Vijana wao na kujenga nyumba imara kwa ajili ya familia zao.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya posho mbalimbali zisizokuwa za kisheria zinaelekezwa katika miradi ya maendeleo.

  Ametia agizo hilo leo (Jumanne, Januari 3, 20017) wakati akizungumza na watumishi wa Manispaa ya Kigamboni akiwa katika ziara yake ya kikazi.

  “Kuanzia sasa marufuku Wakurugenzi kutoa posho zisizotambulika kisheria zikiwemo za mazingira magumu, kujenga uwezo na vitafunwa katika halmashauri zenu na badala yake fedha hizo zitumike kwenye miradi ya maendeleo,” amesema.Agizo hilo litawezesha Jiji la Dar es Salaam kuokoa sh bilioni 130 zilizokuwa zitumike na Halmashauri na Manispaa za jiji hilo, ambazo kwa sasa zitaingizwa kwenye miradi na shughuli za maendeleo.

  Aidha, Waziri Mkuu amewataka watumishi wa umma nchini kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na kuacha kutumia fedha kinyume cha utaratibu na watakaobainika Serikali haitosita kuwachukulia hatua kali za kisheria.

  “Katika halmashauri zetu kila mtumishi anashiriki katika ukusanyaji wa mapato hadi walinzi, lakini mwisho wa siku vitafunwa huliwa na wachache wanaojiita wakubwa huku wengine wakisikilizia kwa nje. Jambo hili haliwezekani,” amesisitiza.Waziri Mkuu amesisitiza kwamba Mkurugenzi yeyote atakayebainika kulipa posho hizo baada ya siku ya leo atakuwa amejifukuzisha kazi.

  Aidha, ameagiza fedha zilizokuwa zikitolewa kwa madiwani kwa ajili ya kuhamasisha maendeleo zisitolewe moja kwa moja kwa madiwani na badala yake zipelekwe kwenye kata husika na zifuatiliwe matumizi yake.

  Hata hivyo, Waziri Mkuu amezionya halmashauri zote nchini kuhakikisha kuwa kila fedha zinayopelekwa kwenye halmashauri hizo inatumika kama ilivyokusudiwa na atakayebainika kutumia kinyume hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.Pia amewataka watumishi wote wa umma nchini kuwajibika ipasavyo na kuhakikisha wanawatumikia vyema mwananchi ikiwa ni pamoja na kuepuka vishawishi na kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa na ufisadi.

  Wakati huo huo, Waziri Mkuu ametoa siku tatu kwa watumishi 10 wa halmashauri hiyo ambao wamehamishiwa kutoka wilaya ya Temeke wawe wameripoti katika Manispaa hiyo, vinginevyo watakuwa wamejifukuzisha kazi.

  Awali Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Bw. Hashim Mgandilwa wakati akiwasilisha taarifa ya wilaya hiyo kwa Waziri Mkuu, alisema hadi sasa asilimia 98 ya watumishi waliotakiwa kuhamia kwenye halmashauri hiyo wameripoti isipokuwa 10 na hakuna taarifa zozote juu yao.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  L. P. 3021,
  JUMANNE, JANUARI 3, 2017

  0 0

   
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifungua pazia kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa VERDE-MARINE HOTEL Mtoni Mjini Magharibi,hoteli ya kisasa yenye hadhi ya nyota 5 inayojengwa na kampunui ya ujenzi ya Bakhresa Group of Companies,ikiwa ni katika shamra shamra za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar,(kulia) Mwenyekiti wa Bakhresa Group of Companies Bw.Said Salim Bakhresa.[Picha na Ikulu.] 03/01/2017.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es salaam akiwa katika ziara ya wialaya ya Kigamboni Januari 3, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa wialya ya Kigamboni baada ya kuwasili wilayani humo kwa ziara ya siku moja. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0


  Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akiongoza waombolezaji kuaga mwili wa marehemu Kenan Mhaiki Rubani Mstaafu wa ndege za marais wa Tanzania wakati wa shughuli ya kuaga mwili wake iliyofanyika Kunduchi, jijini Dar es Salaam Januari 2 2017. Mwili wa marehemu umesafirishwa leo kwenda Songea Mjini Mkoani Ruvuma kwa mazishi yanayotayarajiwa kufanyika Januari 4, Makaburi ya Matogoro. (Imeandaliwa na Robert Okanda blogspot)
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Leonard Chamriho akitoa salamu kwa niaba ya serikali wakati wa ibada ya misa na shughuli ya kumuaga marehemu Kenan Paul Mhaiki.

  Katibu Mkuu Kiongozi wa zamani, Balozi Ombeni Sefue akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Kenani Mhaiki Rubani Mstaafu wa ndege za marais wa Tanzania wakati wa shughuli ya kuaga mwili wake iliyofanyika Kunduchi, jijini Dar es Salaam jana. Mwili wa marehemu umesafirishwa jana kwenda Mkoani Ruvuma kwa mazishi yanayotayarajiwa kufanyika Januari 4 2017. soma zaidi hapa

  0 0


  Na Omary Mngindo, Ruvu

  MBUNGE wa Jimbo la Chalinze Mkoa wa Pwani Mwanasheria Ridhiwani Kikwete Jan 3 amewatembelea wafanyabiashara katika kijiji cha Ruvu Darajani, Kata ya Vigwaza Halmashauri ya Chalinze Mkoa wa Pwani huku akiwaomba wawe wanahudhulia mikutano inayoitishwa na viongozi wao.

  Ridhiwani amefika kwenye kijiji hicho kwa lengo la kushuhudia utekelezaji wa agizo lililotolewa na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Alhaj Hemed Mwanga linalowataka wenyeviti wa vijiji na vitongoji wilayani humo kuitumia siku ya Jan 3 kuwa maalumu kwa ajili ya kuwasomea wananchi wao mapato na matumizi ili wananchi wao watambue makusanyo na matumizi yake.

  Hata hivyo Ridhiwani alipofika mweAnye Makao ya ofisi ya kijiji hicho kinachongoza na Kambona Kwalo na ofisa Mtendaji wake Williamu Jeuli, mkutano haukufanyika kwa madai ya wananchi hao kugoma kusomewa wakidai kwanza lizungumzwe suala la mgongano unaohusha ardhi kati ya wananchi haona mmoja wa wakazi anateishi jijini Dar es Salaam wakidai ni la muda mrefu huku kukiwa hakuna utekelezaji wake.

  Baada ya kushindikana kufanyika kwa mkutano huo, Mwanasheria huyo aliamua kufanya ziara ya papohapo ya kuwatembelea wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao katupika soko la Ruvu Darajani ambapo pia alitumia fursa hiyo kuwaomba vijana kuwa na utamaduni wa kuhudhulia mikutano ya setikali ya kijiji kwani ndipo sehemu ya kuibua miradi kwenye eneo lao.

  Akizungumza na vijana hao Ridhiwani alisema kwamba kwa utaratibu ambao vijana na baaddhi ya wakazi hao ya kutohudhulia mikutano kwenye eneo lao kutawafanya kukikosesha maendeleo kwa sababu kila jambo la maendeleo linaibuliwa kwenye mikutano hivyo ni vema wakaweka itikadi zao pembeni katika masuala yanayohusu maendeleo.

  “Vijana wenzangu katika suala linalohusu maendeleo tuweke pembeni itikadi zetu binafsi, kwani katika maeneo yeyote ambayo mnayaona au kuyasikia yana mafanikio makubwa, chanzo kikuu ni watu wake kuitikia wito wa kuhudhuria mikutano kwani hapo ndipo wanapokaa na kukubalia jambo gani lifanyike au la, kwa utaratibu ambao mnauendeleza wa kutohudhulia mikutano mtaendelea kukidhohofisha kijiji chetu,” alisema Mwanasheria huyo.

  Alimalizia kwa kuwaomba wajitokeze kwa wingi siku ya Alhamisi katika mkutano utaofanyika kwenye ofisi ya kijiji chao ili waweze kuibua miradi yakimaendeleo badala ya kukaa vijiweni na kuendeleza migomo ya kutofika kwenye mikutano kwani hatua hiyo isiyo na yija itaendelea kukikosesha maendeleo kijiji chao.
  Mbunge wa jimbo la Chalinze, Halmashauri ya Chalinze Mkoa wa Pwani Mwanasheria Ridhiwani Kikwete akizungumza na baadhi ya wakaazi wa kijiji cha Ruvu Darajani alipokwenda kwa ajili kusikiliza mkutano wa kusomwa mwa mapato na matumizi ya kijiji ikiwa ni utekelezji wa agizo lililotolewa na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Alhaj Hemed Majid la kuwataka viongozi wote wa vijiji vinavyounda wilaya hiyo kuitumia siku ya Jan 3 kuwasomea mapato na matumizi wannchi wao, hata hivyo mkutano huo umesogezwa mpaka Alhamisi ya Jan 5.
  Mbunge wa jimbo la Chalinze, Halmashauri ya Chalinze Mkoa wa Pwani Mwanasheria Ridhiwani Kikwete akiwaunga mkono wafanyabiashara wa samaki wa kukaanga wanaofanya biashara zao katika eneo la Ruvu Darajani pembezoni kidogo mwa barabara Kuu ya Dar es Salaam- Chalinze, Morogoro- Segera, alipowatembelea kushuhudia wanavyofanya shughuli zao hizo. 
  Mbunge Ridhiwani Kikwete akiwasikiliza wafanyabiashara waaouza bidhaa mbalimbali hapa wauza bidhaa jamiyambogamboga wakizungumza na mbunge wao.

older | 1 | .... | 1088 | 1089 | (Page 1090) | 1091 | 1092 | .... | 1898 | newer