Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

BENKI YA BARCLAYS YAFANYA SEMINA YA CAREER FAIR (UDBS) CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

$
0
0

vote for susan luendo

Redds Miss Kanda ya Mashariki kufanyika Juni 29

$
0
0
MASHINDANO ya Redds Miss Kanda ya Mashariki yatafanyika Juni 29 Nashera Hotel mkoani Morogoro kwa kushirikisha jumla ya warembo 14.
Mkurugenzi wa kampuni ya Nikalex Ltd, Alex Nikitas aliwataja warembo hao ambapo wapo kambini hotel ya Starwing Hotel chini ya mkufunzi, Kudra Lupatu kuwa ni Muzne Abduly (19), Ummy Mohamed (21), Sabra Islam (19) na Diana Laizer ambao wote wanatoka Morogoro.
Warembo ambao wanatoka Mtwara kwa mujibu wa Nikitas ni Ivony Stephen (22), Purkeriah Ndovi (21), Zulfa Semboja (19) na wa Lindi ni Janeth Awet (19), Zainab Shaaban (23) na  Sophia Mganga (21). Wanaotoka mkoa wa Pwani ni Elizabeth Perty (22), Suleiyah Abdi (22)  na Easther Albert (20).
Nikitas alisema kuwa maandalizi ya mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Redds Original, Dodoma Wine, CXC Africa, Nyumbani Park, Usambara Safari Lodge, Michuzi Blog, Clouds Media Group, Chilakale Resorts, Nashera Hotel, Starwing Lodge, Simple car Rental, Big Solution na Mikocheni Resort Centre yamekwisha kamilika na warembo watatembelea sehemu mbali mbali mkoa wa Morogoro na kufanya kazi za jamii.
“Tumejiandaa vziuri na warembo kwa sasa wapo kambini wakijifua kwa ajili ya shindano hilo, warembo watatu wataiwakilisha kanda hiyo katika mashindano ya Redds Miss Tanzania ambayo yatafanyika mwezi Septemba,” alisema Nikitas.
Alisema kuwa wamejipanga vilivyo kwa ajili ya mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kuwa na ushindani mkali kutoka kwa warembo wote.

MAONI YA WADAU KUHUSU SERA MPYA YA ARDHI

$
0
0
  
 Mkuu wa Wilaya ya Kusini Haji Makungu Mgongo akifungua warsha ya sera ya Taifa ya Ardhi iliyowashirikisha Masheha wa Wilaya hiyo. Kushoto ni Mratibu wa Mradi wa SMOLE Saleh Kombo na kulia ni mkufunzi wa warsha Mlenge Hassan.

masheha wa wilaya ya kusini wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya Haji Makungu Mgongo (hayupo pichani) alipokuwa akifungua warsha ya sera ya ardhi katika afisi ya Wilaya Makunduchi. (Picha na Ramadhani Ali- Maelezo Zanzibar)
========   ========  ========
Masheha wa Wilaya mbili za Mkoa wa Kusini Unguja wameshauri kuwepo Mahakama ya Ardhi na kitengo cha usajili wa Ardhi kuanzia ngazi ya wilaya katika Sera mpya ya ardhi inayoandaliwa ili kupunguza migogoro mingi inayoikabili sekta hiyo.

Ushauri huo wameutoa katika Warsha ya kuelimisha na kukusanya maoni ya wadau kwa ajili ya sera ya Taifa ya Ardhi iliyoandaliwa na Mradi wa usimamizi endelevu wa ardhi na Mazingira (SMOLE) awamu ya pili Afisi ya Wilaya Kusini Makunduchi na  Halmashauri ya Wilaya ya Kati Dunga.
Wamesema matatizo ya ardhi hasa vijijini yamekuwa makubwa na ufumbuzi wake huchukua muda mrefu kutokana na kukosa vitengo inavyoshughulikia ardhi na Mahamakama ya ardhi katika ngazi za Wiaya.

“Kesi zinazohusu ardhi ni nyingi na mahakama ya ardhi ipo mjini hili ni tatizo kubwa hivyo sera mpya inayoandaliwa ifikirie kuanzisha mahakama za ardhi kuanzia ngazi ya Wilaya,” alisema Sheha wa Chwaka Msaraka  Pinja.

 Katika Sera mpya ya Ardhi  inayotayarishwa, Masheha wa Wilaya ya Kusini  na Kati wamependekeza sheria za ardhi ambazo hivi sasa zinasimamiwa na  taasisi  tano ziwekwe katika taasisi moja ili kupunguza urasimu katika kuzitekeleza.

Taasisi hizo ni Idara ya Ardhi na Usajili,  Idara ya Misitu na Mali  zisizohamishika,Idara ya  Mipango miji na vijiji, Idara ya upimaji na ramani na Idara ya   Mazingira.

Sheha wa shehia ya Mzuri Khamis Ramadhani ameshauri sheria za ardhi  zilizopo zifanyiwe mapitio upya na ikiwezekana zipunguzwe kwani hivi sasa ni nyingi na utekelezaji wake unapelekea kuwa  mgumu.

Aidha viongozi hao wa shehia wametaka sera ya ardhi iweke wazi idadi ya Eka ambazo mtu mmoja anatakiwa azimiliki kwa shughuli za  maendeleo na  watu wanaojikusanyia maeneo makubwa ya ardhi yachukuliwe na kupewa watu ambao hawana ardhi.

“Kuna baadhi ya watu wanamiliki mashamba makubwa kila sehemu na wala hawayatumii, wakati umefika yachukuliwe na serikali na wapewe wananchi wengine  kwa shughuli za kilimo na maendeleo mengine,” alipendekeza sheha Mumeangu.

Aidha wameishauri Serikali kuanzisha majengo ya ghorofa na tabia ya kuuziwa ardhi wageni  ama kukodishwa kwa miaka mingi iachwe na wamependekeza kipindi cha kukodishwa  ardhi kisizidi miaka 20.

Mratibu wa mradi wa SMOLE  Saleh Kombo amewaeleza viongozi wa Wilaya hizo mbili kwamba serikali kwa kushirikiana na serikali ya Finland  imo katika mchakato wa kutayarisha Sera  rasmi ya ardhi katika kusimamia ardhi ndogo iliyopo  ikiwa ni  juhudi  za kupunguza umaskini kupitia MKUZA awamu ya pili na amewashauri kushiriki kikamilifu katika mchakato huo.

Amesema Serikali imechukua uwamuzi huo kwa kujua kuwa  ardhi  ni rasilimali kubwa katika nchi na ardhi ya  Zanzibar imekuwa ikipungua kwa kasi kutokana na mmongonyoko wa fukwe wakati idadi ya watu imekuwa ikiongezeka kwa kasi. 
              
  NA RAMADHANI ALI – MAELEZO ZANZIBAR    

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.  24/6/2013

Wadhamini wa Ligi kuu ya Vodacom kukabidhi zawadi Julai 3

$
0
0
 Meneja Uhusiano wa nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim, Akizungumza na waandishi wa habari    ( Hawapo pichani) Wakati akitangaza tarehe ya utoaji wa zawadi za ligi kuu ya Vodacom zitakazo tolewa julai 3 jijini Dar es Salaam,  Zawadi hizo ni za jumla ya shilingi Milioni 200 zitakazotolewa kwa vipengele mbalimbali kwa timu za ligi hiyo

Waandishi wa habari wakimsikiliza meneja Uhusiano wa nje wa kampuni ya Vodacom Tanzania Salum Mwalim ( Hayupo pichani)  Wakati akitangaza tarehe ya utoaji wa zawadi za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara zitakazo tolewa julai 3 jijini Dar es Salaam.

=======  =======  ========
Vodacom kukabidhi zawadi ligi kuu Julai 3 Dar es Salaam 24 Juni, 2013 ..... Wadhamini wakuu wa Ligi kuu soka Tanzania Bara Kampuni ya Vodacom imetangaza kuwa itakabidhi zawadi kwa washindi wa ligi hiyo Julai 3 jijini Dar es salaam.


Vodacom imekuwa ikisubiri kumalizika kwa hekaheka za timu ya taifa - Taifa Stars za kusaka nafasi ya kushiriki fainali za kombe la dunia mwakani nchini Brazil hali iliyochelewesha tukio la kukabidhi zawadi hizo kwa mabingwa pamoja na wote waliofanya vema katika msimu wa 2012/2013 

"Tulikuwa tukisbiri wakati muafaka wa kufanya hivyo kwani tangu kumalizika kwa ligi mwezi uliopita mwelekeo wa taifa ulikuwa ni kuipa ari na nguvu timu yetu ya taifa katika kusaka tiketi ya kufuzu kushiriki fainali za kombe la dunia mwakani nchini Brazil." Alisema Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim.

Mwalim amesema  maandalizi yote ya zoezi hilo yamekamilika kwani hakukuwa na sababu nyingine ya kutokabidhi zawadi mara tu baada ya ligi kumalizika zaidi ya timu ya taifa - taifa stars.



Mwalim amesema hafla ya utoaji wa zawadi inahitaji ushiriki wa wadau mbalimbali wa soka nchini wakiwemo wachezaji wa vilabu ambao miongoni mwao wamo kwenye kikosi cha Stars, viongozi wa TFF na walimu wa timu ya taifa ambao wote hao kwa pamoja walikuwa na jukumu moja tu la kuhakikisha Stars inafuzu kwenda Brazil na hivyo isngekuwa vema kuingiza maandalizi ya jambo jingine katikati ya juhudi hizo.

Mwalim ametumia nafasi hiyo kuvishukuru vilabu pamoja na Shirikisho la Soka - TFF na kamati ya ligi kwa uvumulivu wao wakati wote ambapo Vodacom ikisubiri kupatikana kwa muda mufaka wa kukabidhi zawadi.
"Tendo la kukabidhiwa zawadi ni moja ya matendo makuu kabisa kwa yeyote anaeshinda, tumeona uvumilivu mkubwa na wenzetu walituelewa wakati tulipowashauri kutoa nafasi kwa Stars bila kuharibu concetratiuon ya taifa. Tumeonesha umoja wetu."



Mbali ya mabingwa timu ya Yanga ambayo watakabidhiwa kitita cha fedha cha Sh 70 Milioni zinahusisha pia zawadi za wachezaji na wadau wengine mmoja mmoja walioonesha umahiri kwenye maeneo yao. 
Vodacom itakabidhi zawadi za fedha taslimu takribani Sh. 200 Milioni  kwa mabingwa Yanga na Azam, Simba na Kagera Sugar zilizoshika nafsi ya pili hadi ya nne. 


Wengine watakaonufaika na zawadi za fedha ni Mlinda mlango bora, mwamuzi bora, mwalimu bora, timu iliyoonyesha nidhamu na mfungaji bora. Vodacom imekuwa ikiidhamini ligi kuu ya soka ya Tanzania bara kwa zaidi ya misimu mitano sasa huku ikiiwezesha ligi hiyo kuimarika na kuwa ya ushindani kadri miaka inavyosonga mbele.

ZITTO AALIKWA KWENYE TAMASHA LA ASPEN IDEAS 2013

$
0
0

MBUNGE WA Kigoma Kaskazini, Ndugu Zitto Z. Kabwe amealikwa
kuhudhuria tamasha la tisa la Aspen la mwaka huu huko Marekani.
Tamasha hilo linawaleta pamoja watu mashuhuri kutoka nyanja mbalimbali
duniani.

Lengo kubwa la tamasha ni kuwawezesha washiriki kubadilishana mawazo
kuhusiana na masuala mbalimbali ambayo wana uzoefu nayo. Ushiriki katika tamasha hilo utamwezesha Zitto kukutana na kubadilishana
mawazo na magwiji wa masuaka mbalimbali duniani.  Ratiba iliyotolewa na waandaaji inaonyesha kuwa tamasha hilo  litakaloendeshwa kwa muda wa wiki moja kuanzia Juni 26, limegawanyika
katika sehemu mbili.

Kama ilivyo kwa miaka iliyopita, tamasha hilo litahusisha majadiliano ya
pamoja, ya vikundi pamoja na ya mtu mmoja mmoja. Pia washiriki watakuwa na fursa ya kukutana na wabunifu na wataalamu wa nyanja mbalimbali na kubadilishana nao mawazo. Mijadala itahusu mambo ya kijamii, siasa, mahusiano ya kimataifa, watoto na vijana pamoja na namna ya kukabiliana na changamoto kubwa zinazoikabili dunia hivi sasa.

Vile vile kutakuwa na maonyesho ya vitabu pamoja na mikutano na
waandishi wa habari maarufu kutoka Marekani. Washiriki pia watapata
fursa ya kujifunza kupitia filamu na michezo ya kuigiza.

“Nimefurahi kupata mwaliko huu na nimekubali kushiriki kwa sababu
kwangu mimi hii ni nafasi adhimu sana na kupanua uelewa wangu wa
masuala mbalimbali, pia ni fursa kubwa ya kueleza maoni yangu kwa
waalikwa mbali mbali. Nina uhakika kuwa watu nitakaokutana na
kubadilishana nao mawazo na uzoefu watasaidia kupanua uelewa wangu wa
masuala kadhaa”, alisema Zitto alipotakiwa kufafanua umuhimu wa
tamasha hilo kwa vijana.

Baadhi ya watu maarufu watakaotoa mada katika tamasha hilo ni pamoja na
Majaji washiriki wa Mahakama Kuu ya Marekani Stephen Breyer na
Elena Kagan, Mwakilishi Eric Cantor, Rais wa Kituo cha Brady Dan
Gross, Rais wa Chama cha Wamiliki wa Bunduki Marekani David Keene,
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Susan Rice; Rais wa Taasisi
ya Taasisi ya Kulinda Rasilimali, Frances Beinecke; Mkurugenzi mwenza
wa Boies, Schiller & Flexner LLP David Boies, Waziri wa kazi wa zamani
Elaine Chao, Waziri wa Usafirishaji Ray LaHood, Meya wa New Orleans
Mitch Landrieu, Waziri wa Fedha wa zamani Hank Paulson, Gavana wa
zamani wa Minnesota Tim Pawlenty, Mshauri wa Chama cha Republican
Karl Rove na Rais wa Shirikisho la Walimu Marekani Randi Weingarten.

KUHUSU TAASISI YA ASPEN.

Taasisi ya Aspen inajihusisha na masuala ya elimu na sera ambayo ina
makao makuu katika jiji la Washington, Marekani. Lengo lake kuu ni
kuendeleza maadili ya kiuongozi. Pia taasisi hii ni kama kituo cha
kuwezesha kutafuta ufumbuzi wa masuala magumu.
Taasisi ina matawi kadhaa baadhi yakiwa huko Aspen, Colorado na Wye
River huko Maryland. Pia Taasisi ina ofisi katika jiji la New York. Pia taasisi
ina mtandao mkubwa wa washiriki duniani kote.

Maandalizi ya tamasha la Grand Malt Tanzania Open Film Festival yazidi kunoga.

$
0
0

HUKU zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kufanyika kwa Tamasha la Wazi la Filamu Tanzania, maarufu kama ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’ ambalo litafanyika katika Viwanja vya Sahara jijini Mwanza, maandalizi yake yamezidi kupamba moto.

Mratibu wa Tamasha hilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Sophia Records, Musa Kissoky, alisema kwa sasa kila kitu kimekamilika na kinachosubiriwa ni kuanza kwa tamasha hilo Jumatatu ijayo.


Kissoky alisema, tamasha hilo ambalo litakuwa la bure kwa watu wote na kushirikisha mastaa wa filamu hapa nchini, litakuwa la aina yake kwani vitu vitakavyofanyika vitakuwa si vya kawaida.  “Kwa sasa maandalizi yamekamilika kwa asilimia 90, yaani tunaleta kitu tofauti ambacho watu watashangaa, ndio maana mpaka sasa wengi wanapigwa na bumbuwazi kuhusu kile tutakachofanya siku hiyo,” alisema.

Naye Meneja wa kinywaji cha Grand Malt walio wadhamini wakuu wa tamasha hilo, Consolata Adam, alisema wameamua kufanya kweli zaidi kwani wanataka kuona Watanzania wanapata kitu chenye uhakika. “Tumejipanga katika hili na wala hatutanii kwani tunataka kuwawezesha wakazi wa Mwanza na maeneo ya jirani kuhudhuria tamasha hili kwa wingi . Tunawakaribisha watu wote wenye mapenzi na filamu zetu za Tanzania kufika na kushuhudia tamasha hili ambalo mwaka huu limeboreshwa zaidi,” alisema Consolata.

Naye Meneja Habari na Mawasiliano wa TBL, Edith Mushi, alisema, kutokana na ubora wa kinywaji cha Grand Malt hata tamasha hilo litakuwa la aina yake na litakaloiteka mikoa yote ya Kanda ya Ziwa. “Tumeona jinsi wananchi wanavyozipenda filamu za Tanzania, maarufu kama ‘Bongo Movies’ na jinsi walivyo na kiu ya kuwaona wasanii wa filamu ana kwa ana, sasa kazi kwao kuwashuhudia na kuona tamasha bora zaidi,” alisema.

Tamasha la Filamu la Grand Malt linatarajiwa kuanza Julai 1-7, mwaka huu huku kukiwa na filamu mbalimbali zitakazooneshwa katika kipindi hicho. Filamu zote hizo ni kutoka Tanzania.Wasanii wakali wa Bongo Muvi wakiwemo Aunty Ezekiel, Vicent Kigosi ‘Ray’, Jacqueline Wolper, Irene Uwoya, Jacob Steven ‘JB’, Mahsein Awadh ‘Dk Cheni’na  Issa Mussa ‘Cloud’ ni baadhi ya wasanii walioahidi kufanya kweli pia katika tamasha hilo.


Tamasha hilo la filamu limedhaminiwa na kinywaji cha Grand Malt kisicho na kilevi ambacho kinazalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA (TCRA) KANDA YA MASHARIKI WATOA SEMINA YA MAWASILIANO KWA WADAU WAO KATIKA WILAYA YA BAGAMOYO

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Ahamed Kibozi akihutubia wakati wa uzinduzi rasmi wa semina ya wadau wa huduma za Mawasiliano iliyowalenga wawakilishi wa jumuiya mbalimbali za vijiji na vitongoji vya Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani.aliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzanizi(TCRA ) Kanda ya Mashariki hivi karibuni.Katikati ni Mkurugenzi wa Huduma za Mawasiliano wa TCRA, Dk.Raynold Mfungahema na Kushoto ni Meneja wa Kanda ya Mashariki Mhandisi Oscar Mwanjesa.
Mkurugenzi wa Huduma za Mawasiliano Dk.Raynold Mfungahema akitoa mada ya Haki na wajibu wa watumiaji wa huduma za mawasiliano wakati wa semina ya watumiaji wa huduma za mawasiliano iliyofanyika katika chuo cha sanaa cha Bagamoyo kwa kuwashilikisha wawakilishi wa jumuiya mbalimbali za vijiji na vitongoji vya Wilaya ya hiyo.
Afisa wa Idara ya Posta wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA,Bi,Ccilia Sylvester,akitoa mada juu ya mfumo mpya wa anuani za posta semina ya wadau wa huduma za Mawasiliano iliyowalenga wawakilishi wa jumuiya mbalimbali za vijiji na vitongoji vya Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani.aliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzanizi(TCRA ) Kanda ya Mashariki wakiwakatika foleni ya kujiandikisha wakati wakuingia katika semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha sanaa Bagamoyo.


Swala to Sponsor ten students at the Dept. of Geology, University of Dar es Salaam

$
0
0
Swala Oil and Gas (Tanzania) Limited (“Swala”) is pleased to announce a new scholarship scheme to sponsor ten students at the Department of Geology, University of Dar es Salaam.  This scheme is part of Swala’s commitment to the development of local capacity able to fully participate in Tanzania’s hydrocarbon economy. 

Students wishing to attend a university course must apply to the Tanzania Commission for Universities (www.tcu.go.tz) or the National Council for Technical Education (www.nacte.go.tz).  Once selected for a course, students may apply for national grants to assist them in their studies.

Swala invites applications for its scholarship scheme from students wishing to start a Geology degree at the University of Dar es Salaam in the 2013/2014 academic year.  Students with outstanding academic results are invited to send a CV together with copies of their academic results and the names of two referees to Swala Oil and Gas (Tanzania) Limited DSMscholarship@swala-energy.com


Applications must be received by the 30thJune 2013.  No applications shall be considered after that date.

Successful candidates will be notified by the 7th of July 2013.



Dr. David Mestres Ridge, Swala’s CEO said “With Tanzania’s success in gas exploration and on-going oil exploration, we collectively need to build the local capacity to support and develop such a nationally important industry.  This means developing human resources, and particularly the next generation of Tanzanian geoscientists.  
Whilst the oil industry in Tanzania already contributes significant sums to local development, in a programme administered by the Tanzanian Petroleum Development Corporation, we felt it appropriate to add to that effort in partnership with the University of Dar es Salaam.”

MTANGAZAJI JOYCE KIRIA AOMBA AFAHAMISHWE ALIPO MUMEWE HENRY KILEO

$
0
0

TGNP yakabidhi Vifaa vya Mawasiliano Vituo vya Taarifa na Maarifa

$
0
0
 Ofisa katika Kitengo cha Habari na Mawasiliano TGNP, Deogratius Temba, akikabidhi vifaa hivyo kwa wanakituo hicho.
======  =======  ========= 
MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP),  umepanua wigo wa mawasiliano kwa makundi ya pembezoni hasa wanwake kwa kuwapatia vifaa vya teknolojia ya habari na Mawasiano (TEHAMA) kwaajili ya kupashana habari katika Kituo cha taarifa na maarifa Mkambarani Morogoro Vijijini.

Akikabidhi vifaa hivyo vyenye dhamani ya zaidi ya shilingi Milioni 1.9, Ofisa katika Kitengo cha Habari na Mawasiliano TGNP, Deogratius Temba, amesema kuwa  shirika hilo limeamua kutoa vifaa hivyo kwaajili ya kuhakikisha makundi yaliyoko pembezoni hasa wanawake wanafikiwa kwa kupata taairfa sahihi kwa wakati muafaka na kuwawezesha pia wao kutoa taraifa walizo nazo katika ngazi ya jamii.

“Huu ni mradi unaowezesha sauti za jamii kusikika,  kuanzishwa kwa ‘Sauti ya Jamii’ kunawezesha  sauti za wanawake wengi kupewa taarifa na kutoa na kusikika, Tunajua hii itawezesha wanawake wengi  kupaaza sauti zao na kupambana na matukio ya ukatili wa kijinsia pamoja na changamoto nyingine zilizoibuliwa wakati wa Utafiti raghibishi mwaka 2012 na tamasha la Jinsia la mwaka 2012 hapa Mkambatani” alisema Temba

Alisema kuwa TGNP kwa muda mrefu imekuwa ikitumia TEHAMA kwa ajili ya mawasiliano, kuwafikia wadau mbalimbali, kujenga nguvu za pamoja   katika kuleta mabadiliko chanya.  Matumizi ya ujumbe mfupi wa simu  (SMS) imekuwa ni  moja ya TEHAMA ambayo  inatumika kwa wingi katika ngazi ya jamii.

“Kwa mantiki hii TGNP imeona fursa kubwa ya kutumia ujumbe mfupi  kama nyenzo ya  kusaidia kuunganisha nguvu katika kuhabarishana na kuchukua hatua za kwajibisha  mamlaka na kuleta mabadiliko chanya” aliongeza.

Sauti ya jamii itatumia  teknolojia  ya bulk SMS yaani kutuma ujumbe  mfupi wa simu kwa kutumia computer kwa watu wengi zaidi ya 10,000 kwa wakati mmoja.  Sauti ya jamii  itasaidia  kupashana habari  kupitia kituo cha taarifa na maarifa cha jamii kwenda wa wadau mbali mbali wakiwemo wanaharakati waliohusika katika Utafiti wa mwaka jana, madiwani,  Wanajamii wa Mkambarani, kamati mbalimbali  za maendeleo Mkambarani,  viongozi wa serikali za mtaa , kata hadi wilaya, madiwani na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali.   

Makamu Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Mkambarani, Teresia Berege, alisema kuwa kuwepo kwa Kituo hicho na vifaa hivyo vya kisasa kutasaidia  kurahisisha mawasiliano, upashanaji wa taarifa na kupata habari kwa haraka itakuwa ni ukombozi kwa watoto na wanawake na kuwaweka katika mazingira bora ya kupata maendeleo.

Naye Diwani wa kata ya Mkambarani, danile Shawa alisema kuwa wanaharakati wa Mkambarani wanapaswa kutumia vizuri vifaa vilivyotolewa na TGNP ili vilete ufanisi na maendeleo kwa wakazi wa kata hiyo.

“ninawashauri mtumie vema hivi vitu, kwa hapa kwetu Mkambarani hii ni fursa ya pekee, tumepiga hatua sasa, tekonoljia ilikuwa nyuma sasa TGNP imewawezesha mnakwenda na wakati, mtumie vizuri kwa uaminifu na unagalifu na msitume taarifa ambazo hazina ukweli” alisema Diwani.

NALIZIMIA KINOMA HILI SONGI LA Abdul kiba ft Ali kiba liitwalo Kidela..!

muonekano wa taswira kadhaa ndani ya zanzibar.

JOHNNIE WALKER MENTORSHIP

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Steve Gannon(kulia) na mdau Mr. Paul(kushoto) wakiwa wameshika chupa ya Johnnie Walker blue label. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Steve Gannon (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na Afisa mawasiliano wa SBL Bi. Hawa (wa pili kulia) wakiwa na wadau  Paul(kulia) na Mac(kushoto) waliohudhuria katika hafla ya ‘Johnnie Walker Mentorship’ iliyoandaliwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti waliohudhuria hafla hiyo
Mabalozi wa kinywaji cha Johnnie Walker kutoka Kampuni ya Bia ya Serengeti  wakionesha wageni waalikwa moja ya aina ya Johnnie Walker.
Baadhi ya wageni waliohidhuria hafla ya Johnnie Walker Mentorship wakifuatilia kwa makini namna ya utumiaji wa Whisky aina ya Johnnie Walker kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Steve Gannon(hayupo pichani).
Mtaalamu wa cocktail Mr. Mikey, akimimina mchanganyiko wake murua kabisa uliotokana na vinywaji vya Johnnie Walker Mentorship maalum kwa hafla hiyo iliyofanyika Escape Club jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Steve Gannon akiwa amepozi na chupa ya Johnnie Walker blue label. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Steve Gannon(kushoto) akiwa na baadhi ya wageni waliojumuika kuonja na kutofautisha ladha mbalimbali za vinywaji vya Johnnie Walker
 Mmoja wa mabalozi wakuu wa kinywaji cha Johnnie Walker Danis Ssebo akiwamiminia wageni waalikwa kinywaji cha John Walker Black label waweze kukionja na kujua ladha yake katika hafla ya ‘Johnnie Walker Mentorship’ iliyoandaliwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Steve Gannon (kulia) akizungumza jambo mbele ya baadhi ya wageni waliojumuika kuonja na kutofautisha ladha mbalimbali za vinywaji vya Johnnie Walker

MAMBO YALIVYONOGA TBL'S FAMILY DAY DAR

$
0
0
 Wasanii wa kikundi cha  sanaa cha Afrigay Talent Base cha Magomeni Dar es Salaam, kikitumbuiza wakati wa hafla ya wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tvanzania (TBL), kufahi pamoja na familia zao Kunduchi Water Park, Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Fedha wa TBL, Kelvin (kulia), akimkabidhi George Magombeka zawadi ya saa ya ukutani baada ya kuwa mshindi wa riadha katika bonanza hilo la kukata na shoka lililofanyika Kunduchi, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Meneja Uhusiano Mambo ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Emma Oriyo (kulia) akimkabidhi zawadi  .Mbwana Milanzi baada ya kuwa mshindi wa kwanza wa mbio za magunia katika hafla ya Siku ya wafanyakazi wa TBL kufurahi na familia zao kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi, Kunduchi Dar es Salaam
 Meneja Uhusiano Mambo ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Emma Oriyo  akimkabidhi zawadi  .mmoja wa washindi wa riadha kwa upande wa wananwake. Kulia ni Mhandisi Ujenzi wa TBL, John Malisa.
 Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakifurahi na familia zao kwa kucheza kushindana kuvuta kamba katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, Kunduchi Dar es Salaam, wakati wa sherehe 'Tbl's Family Day'.
 Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakifurahi na familia zao kwa kucheza soka katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, Kunduchi Dar es Salaam juzi, wakati wa sherehe 'Tbl's Family Day'.



 Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakifurahi na familia zao kwa kucheza soka katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, Kunduchi Dar es Salaam juzi, wakati wa sherehe 'Tbl's Family Day'.

 Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakifurahi na familia zao kwa kucheza soka katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, Kunduchi Dar es Salaam juzi, wakati wa sherehe 'Tbl's Family Day'.

 Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakifurahi na familia zao kwa kushindana mbio za magunia katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, Kunduchi Dar es Salaam, wakati wa sherehe 'Tbl's Family Day'.
 Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakifurahi na familia zao kwa kushindana mbio za magunia katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, Kunduchi Dar es Salaam juzi, wakati wa sherehe 'Tbl's Family Day'.
 Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakifurahi na familia zao kwa kucheza mpira wa wavu katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, Kunduchi Dar es Salaam, wakati wa sherehe 'Tbl's Family Day'.

 Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakifurahi na familia zao kwa kucheza mpira wa wavu katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, Kunduchi Dar es Salaam, wakati wa sherehe 'Tbl's Family Day'.

 Wato wa familia za wafanyakazi wa TBL, wakifurahi kwenye moja ya mabwawa ya kuogelea

 Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakifurahi na familia zao kwa kushindana kucheza mpira wa kikapu ndani ya maji eneo la  Kunduchi Dar es Salaam juzi, wakati wa sherehe 'Tbl's Family Day'.
 Mneja wa Kiwanda cha TBL, Dar es Salaam, Calvin Martine akimkabidhi zawadi mmoja wa wattoto waliofanya vizuri kwenye michezo
 Mmoja wa watoto akichorwa usoni wakati wa hafla hiyo
 Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), wakifurahi na familia zao kwa kushindana kucheza mpira wa kikapu ndani ya maji eneo la  Kunduchi Dar es Salaam juzi, wakati wa sherehe 'Tbl's Family Day'.
                                                          Sasa ni wakati wa maakuli

                                                        Ni msosi kwa kwenda mbele
 Muziki wa dansi nao haukukosa
Wakishuhudia mambo burudani mbalimbali zilizokuwa zinatolewa katika hafla hiyo

Hali si Shwari Ndani ya Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU).

$
0
0
 
 Kaimu Mwenyekiti wa TEKUASA Amani Simbeye akifungua mkutano kati ya waandishi wa Habari na Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU)

Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU)  wakifuatilia kwa umakini kikao  hicho wakati kikiendelea.




















  Kaimu Mwenyekiti wa TEKUASA Amani Simbeye pamoja na katibu wake wakisikiliza kwa umakini wahadhiri wakichangia hoja



















  Mmoja wa Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU) , akikazia jambo  ya yale ambayo yalikuwa yamezungumzwa
 Mmoja wa Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU), akitila  mkazo na kujibu swali ambalo liliulizwa na mmoja wa waandishi wa Habari.


















Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU) wakipiga piga Meza kuashiria kuunga MKONO Hoja ilizo somwa.


















 Kikao kikiwa kinafungwa kwa Sala


















 Waahadhiri wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU)  wakiwa wanaimba wimbo wa Solidarity .
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Dr. Daniel Mosses Akiwa anauficha Uso akihofia kupigwa picha na kuhojiwa na waandishi wa Habari kuhusiana na Mgogoro unao endelea  Chuoni hapo 

***************

HALI si Shwari  Ndani ya Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU) baada ya Uongozi wa Chama cha Wahadhili wa Chuo hicho (TEKUASA) na wanachama wake kutangaza mgomo wa kutotunga mitihani ya kufungia Mhula, Mitihani ambayo inatarajiwa kufanyika Julai Mosi Mwaka huu kwa kile walichodai Menejimenti ya Chuo kutotoa majibu ya matatizo yao.

Mgomo huo  umetangazwa leo na Kaimu Mwenyekiti wa Tekuasa Amani Simbeye katika Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Chuo hicho kilichopo  Block T kata ya Iyela Jiji na Mkoa wa Mbeya na kuhudhuriwa na zaidi ya Wahadhili 30.

Simbeye amesema kuna mambo mengi na changamoto za elimu inayotolewa Chuoni hapo ambazo Menejimenti ya Chuo inahusika moja kwa moja hivyo kuhatarisha mustakabali wa Elimu Nchini hususani inayotolewa Chuoni hapo ambapo ameongeza kuwa zaidi ya yote ni kukosa ushirikishwaji wa maamuzi yanayohusu Taaluma.

Kwa taarifa zaidi na madai ya Wahadhili hao hadi kupelekea kususia kutunga mitihani ya kumaliza muhula inatarajiwa kufanyika Julai Mosi Mwaka huu yameandikwa kwenye  barua hapo chini lakini habari kamili itawajia baadaye kwa Lugha ya Kiswahili endelea kuwa nasi.

zaidi ya milioni 14 zakusanywa kwenye HARAMBEE YA UJENZI WA SEKONDARI ISAPULANO MAKETE

$
0
0
Na James Festo, Makete
 
Zaidi ya shilingi milioni 14 zimekusanywa katika harambee ya ujenzi wa shule ya sekondari ya kata ya Isapulano wilayani Makete mkoani Njombe, inayoendelea kujengwa katani hapo
 
Akisoma risala kwa mgeni rasmi Mratibu elimu kata ya Isapulano Bw. Nahomu Tweve amesema katika ujenzi huo wamekutana na changamoto kadahaa zikiwemo ukosefu wa michango kutoka kwenye vijiji vya vingine vilivyopo katika kata hiyo ambavyo ni Ivilikinge na Luvulunge kutokana na mgogoro wa ujenzi wa makao makuu ya kata, pamoja na halmashauri ya wilaya kutotoa mchango wa fedha katika ujenzi huo
 
Amesema thamani ya vitu na fedha zilizochangishwa katika harambee hiyo jumla ya sh. Milioni kumi na nne mia moja kumi na tatu elfu na mia mbili ambazo ni fedha taslimu, ahadi pamoja na vifaa vya ujenzi zikiwemo bati
 
Amevitaja vifaa vilivyochangishwa kuwa ni mifuko 164 ya saruji, pamoja na bati 164 kutoka kwa wananchi vyote vikiwa na tahamani ya zaidi ya shilingi milioni 7
 
Kwa upande wake Bi Jackline Mroso aliyemuwakilisha mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Makete ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi, alivishukuru vikundi vyote vilivyoshiriki katika hamasa ya harambee hiyo ambapo pamoja na hayo yeye binafsi aliahidi kuchangia sh. 200,000/=, daftari boksi tano na kalamu boksi tano
 
Pia alisema halmashauri imeguswa na harambee hiyo na wameamua kuchangia bati 60 ambazo zitaatumika kwa aajili ya ujenzi huo
 
Awali katika ufunguzi wa harambee hiyo Afisa mtendaji wa kijiji hicho Bw. Alimivu Sanga alibainisha sababu zilizopelekea kufanya harambee ya ujenzi wa shule hiyo kuwa ni kupunguza msongamano wa wanafunzi katika shule jirani ya Iwawa sekondari, kupunguza idadi ya wanafunzi wengi walioko mitaani walioacha shule kwa sababu ya umbali
 
“Wapo wanafunzi wengi waliopo mitaani walikata tamaa ya kuendelea na shule kutokana na umbali uliopo kutoka hapa Isapulano kwenda Iwawa sekondari ama Kitulo sekondari, kwa hiyo ujenzi wa shule hii utasaidia kuondoa kero kama hizo ukizingatia hapa isapulano ni katikati ya Iwawa na Kitulo” alisema Sanga
 
Diwani wa kata hiyo mh. Aginiwe Mahenge amewashukuru wadau walioshiriki katika harambee hiyo na kusema kuwa ujenzi wa shule si kwa manufaa yao pekee bali ni kwa wilaya nzima kwa kuwa watoto watakaokuja kusoma shuleni hapo manufaa yake yatakuwa kwa wanamakete wote
 
Lengo la harambee hiyo lilikuwa ni kukusanya shilingi milioni 150 ili kukamilisha ujenzi wa shule hiyo ambapo kwa matarajio yao wanakusudia ianze kupokea wanafunzi kuanzia januari 2014

Young Tanzanian Computer Programmer Lands $328,000 Victory

$
0
0
(L) Eric Mutta. is a 29 year-old Tanzanian software engineer who recently secured over half a billion shillings (equivalent to $328,000) in grant funding. The grant was awarded on the 18th June 2013  software startup Problem Solved Ltd, founded in 2008. It comes from the Financial Services Deepening Trust (FSDT – www.fsdt.or.tz) as part of the competitive SME Finance Innovation Challenge Fund, in which Problem Solved Ltd defeated 13 companies to emerge the winner.(C)Sosthenes Kawe Technical Director of (FSDT) (R) Christian Mpalanzi SME FINACE INNOVATION CHALLENGE FUND
 =======  =======  ======= =====
The objective is to improve the way Small & Medium Enterprises (SMEs) keep financial records by providing them with an affordable and user-friendly accounting package called Minishop. Better financial records make it easier to apply for loans that can be used to grow the business, increase employment and contribute to government revenues.

Of the 130,000 SMEs in Tanzania that should keep electronic financial records, only 900 currently do so (i.e. less than one percent). I will be using the funds to close this gap, by hiring up to 7 employees, purchasing 500 laptops to be bundled and sold with Minishop, and developing other supporting systems (mobile payment collection).

I would like to thank the FSDT for supporting this new approach to solving the long-standing problem of SME access to finance. Participating in the second round of the challenge has made my company stronger and I encourage other entrepreneurs, young and old, to give it their best and apply in the upcoming third round.

For more information visit www.tzaccounting.com and direct enquires to me viaeric@tzaccounting.com and to FSDT via info@fsdt.or.tz

SHEREHE ZA KUAPISHWA SKAUTI MKUU WA CHAMA CHA SKAUTI TANZANIA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM JUNI 23, 2013

$
0
0
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha  Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza akisubiri kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi baada ya kumuapisha Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza baada ya kumuapisha Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi vitendea kazi Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza baada ya kumuapisha  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza baada ya kumuapisha  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akivishwa skafu na skauti kabla ya kumuapisha Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza akisubiri kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha na  Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza baada ya kumuapisha  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim, Jaji Kiongozi Fakih Jundu na Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza baada ya kumuapisha  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha na  Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza pamoja na viongozi wa maskatu na skauti  baada ya kumuapisha  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha na  Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza na familia yake baada ya kumuapisha  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha na  Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza pamoja na waheshimiwa wabunge ambao ni maskauti  baada ya kumuapisha  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na skauti Ismail Aden Rageh na wabunge maskauti  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha na  Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza pamoja na wanachama wa UWT wilaya ya Ilala  baada ya kumuapisha  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha na  Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza na viongozi wa skauti nchini baada ya kumuapisha  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na skauti Livingstone Lusinde ambaye pia ni Mbunge wa Mtera  Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
 Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania mteule Mhe. Mwantumu Mahiza akisubiri kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijiandaa kuvishwa skafu na skauti kabla ya kumuapisha Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania Mhe. Mwantumu Mahiza akisubiri kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 23, 2013

Wasanii watamba tamasha la filamu Grand Malt

$
0
0
WASANII mbalimbali watakaoshiriki katika Tamasha la Tamasha la Wazi la Filamu Tanzania, maarufu kama ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’ ambalo litafanyika katika Viwanja vya Nyamagana jijini Mwanza, wameanza kutoa tambo zao.
Tamasha hilo linatarajiwa kuanza Jumatatu ijayo, ambapo kutakuwa na maonyesho mbalimbali ya filamu pamoja na burudani za muziki kutoka bendi ya Extra Bongo, pamoja na ngoma za asili. Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wasanii hao walisema tamasha hilo litawafungua macho wengi ikiwa pamoja na kupata kujua kile ambacho wanakifanya wakati wakirekodi sinema zao.
Msanii mahiri wa filamu, Aunty Ezekiel alisema atakuwepo Mwanza kipindi chote cha tamasha hilo na akataka mashabiki wafike kwa wingi kushuhudia filamu kali zaidi ambazo amezicheza katika siku za karibuni, ambazo zitaonyeshwa bure.
“Mimi ndiye mkali wao, Watanzania waje kushuhudia kile ambacho tumekifanya,” alisema Aunty Ezekiel, kauli ambayo iliungwa mkono na Jacqueline Wolper aliyedai naye atakuwepo, ila ndiye pia anayejiamini ni ‘mzuri’ zaidi katika mambo ya filamu.
Irene Uwoya alitamba atafunika wengi katika tamasha hilo, huku Vicent Kigosi ‘ray’ na Jacob Steven ‘JB’ nao wakijinasibu watafanya vitu adimu zaidi katika tamasha hilo linalosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wengi wa filamu hapa nchini.
Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Choki alitamba watafanya kweli zaidi siku ya uzinduzi kwani watapiga vibao vipya na kutoa shoo mpya kwa mashabiki watakaojitokeza kipindi chote cha tamasha hilo. “Tumejiandaa vya kutosha, tuna shoo mpya na ya aina yake, ambayo si ya kukosa. Waje tu waone Extra Bongo itakachofanya ni nini,” alisema Choki.
Mratibu wa Tamasha hilo aliye pia Mkurugenzi wa Sophia Records, Musa Kissoky, alisema kwa sasa kinachosubiriwa ni siku ya tamasha tu na kusema wasanii wengi wa filamu watakuwepo hapo. “Kwa sasa maandalizi yamekamilika kwa asilimia 90, yaani tunaleta kitu tofauti ambacho watu watashangaa, ndio maana mpaka sasa wengi wanapigwa na bumbuwazi kuhusu kile tutakachofanya siku hiyo,” alisema.
Naye Meneja wa kinywaji cha Grand Malt walio wadhamini wakuu wa tamasha hilo, Consolata Adam, alisema wameamua kufanya kweli zaidi kwani wanataka kuona Watanzania wanapata kitu chenye uhakika. “Tumejipanga katika hili na wala hatutanii kwani tunataka kuwawezesha wakazi wa Mwanza na maeneo ya jirani kuhudhuria tamasha hili kwa wingi . Tunawakaribisha watu wote wenye mapenzi na filamu zetu za Tanzania kufika na kushuhudia tamasha hili ambalo mwaka huu limeboreshwa zaidi,” alisema Consolata.
Tamasha la Filamu la Grand Malt linatarajiwa kuanza Julai 1-7, mwaka huu huku kukiwa na filamu mbalimbali zitakazooneshwa katika kipindi hicho. Filamu zote hizo ni kutoka Tanzania.
Tamasha hilo la filamu limedhaminiwa na kinywaji cha Grand Malt kisicho na kilevi ambacho kinazalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa kushirikiana vyema na ISAMILO LODGE ya Mwanza
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live


Latest Images