Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1086 | 1087 | (Page 1088) | 1089 | 1090 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Uongozi wa Coastal Union kutoka mkoani Tanga inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara, unawataka wapenzi wake waliopo Dar es Salaam kesho (Jumapili Januari 1, 2017) kufika uwanja wa Karume zilipo ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ili kushuhudia timu mpya na yenye uwezo wa hali ya juu. 

  Kwa mujibu wa Meneja wa timu Hilal Said, vijana wa sasa ni wapya nah ii ni mechi ya pili tangu mzunguko wa pili uanze. Hivyo usajili mpya umeonyesha mwanga na vijana wanapiga soka la uhakika. 

  “Naweza kusema sisi hatustahili kucheza na timu za ligi daraja la kwanza, hata ligi kuu hakuna timu ya kutufunga kwa sasa tumekua level nyingine kabisa. Inafika wakati hata tukifanya mechi za majaribio tunaona kama tunazionea timu tunazocheza nazo. 

  “Hivyo nawaomba wapenzi wa soka si lazima wawe wa Coastal Union tu bali mpenzi yeyote anayependa kuona soka la uhakika aje Karume kesho Jumapili. Tunafungua mwaka kwa kuichapa Kimondo mabao yasiyo na idadi,” alisema Hilal. 

  Coastal Union inayoshika nafasi ya tano katika kundi B kwa sasa ina point sita huku Kimondo FC kutoka beya ikishika mkia kwenye kundi hili.
  Mchezo uliopita Coastal Union ilitoka sare ya 1-1 dhidi ya Polisi Morogoro katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro huku mashabiki wa soka mkoani humo wakisifia kiwango kikubwa kilichoonyeshwa na wachezaji wa Coastal Union. 

  Katibu wa Coastal Union, Tahbit Abuu, aliweka wazi kuwa kwa sasa timu yoyote itakayoingia katika anga zao watarajie kichapo kwani wanataka kuhakikisha mechozote sita zilizobaki wanashinda ili kujiweka katika nafasi nzuri. 

  “Tunataka turudi ligi kuu, hakuna namna nyingine zaidi ya kuendeleza kichapo popote pale iwe nyumbani au ugenini, kwa sababu timu ya ushindani tunayo na uwezo tunao, hatuna sababu ya kuwa wanyonge,” alisema. 

  Wachezaji wa Coastal Union wameshawasili jijini Dar es Salaam tangu Ijumaa ambapo wamefichwa katika kambi maalumu kwenye moja ya fukwe za Bahari ya Hindi tayari kwa mechi ya Jumapili.

  Habari hii imetolewa na msemaji wa Klabu Hafidh Kido
  0713 593894

  0 0
  TAARIFA KWA UMMA

  UONGOZI wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Shinyanga (SPC),na baadhi ya waandishi wa habari wilayani Kahama,wamekutana na mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu ili kupata muafaka wa tatizo la kukamatwa na kufikishwa mahakamani mwandishi wa habari wa kujitegemea Paul Kayanda.

  Kikao hicho cha usuluhishi kilichofanyika leo Jumamosi Desemba 31,2016 katika ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo,kimehudhuriwa pia na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Kahama.

  Kayanda alikamatwa jana Desemba 30,2016 na kufikishwa mahakamani kwa agizo la Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akimtuhumu kuandika habari za kumdhalilisha na kuzisambaza kwenye barua pepe mbalimbali za vyombo vya habari.

  Katika kikao ,Uongozi wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga ,ulimuomba mkuu wa wilaya Nkurlu kutaka kufahamu kilichomsukuma kuchukua maamuzi hayo,na nini ushauri wake juu ya suala hilo lakini pia kumsikiliza mwandishi Paul Kayanda.

  Baada ya kusikiliza pande zote mbili,kikao kilibaini kuwepo kwa mapungufu katika habari iliyoandikwa na Kayanda kuhusu habari ya laptop mbili zilizoibiwa nyumbani kwa mkuu huyo wa wilaya.

  Mkuu huyo wa wilaya alikiri kuwepo kwa tukio la wizi nyumbani kwake lakini mwandishi huyo aliandika habari kwa kuingilia uhuru binafsi wa kiongozi huyo akielezea watu wanaoingia na kutoka nyumbani kwake lakini maisha anayoishi na kijana wake.

  Kwa kuangalia maslahi mapana ya umma kutokana na kutegemeana katika kusukuma maendeleo ya jamii baina ya uongozi wa serikali na waandishi wa habari ,kikao kimemtaka Kayanda kumwomba radhi mkuu huyo wa wilaya kwa kuingilia uhuru wake binafsi na kuuhusisha na habari ya wizi wa laptop badala ya kujikita kwenye tukio la wizi wa laptop pekee.

  Kikao pia kimebaini kuwa pamoja na mapungufu ya mwandishi, ni ukweli ulio wazi kuwa mkuu huyo wa wilaya aliibiwa kompyuta mpakato (lap top) mbili nyumbani kwake na kuagiza vijana watatu wakamatwe kwa mahojiano polisi akiwemo mmoja anayeishi nyumbani kwake japo ameelezea kuwa hakujua walishikiliwa kwa siku ngapi.

  Mkuu huyo wa wilaya pia alieleza kukerwa na ujumbe mfupi wa maandishi kwa njia simu ya mkononi (sms) alizodai kutumiwa na Kayanda kwa kutumia simu nyingine (tofauti na anayotumia) zenye lugha ya kumtuhumu na kumdhalilisha.Hata hivyo kikao hakikuona kuwepo kwa ushahidi wa moja kwa moja kuthibitisha kama ni za mwandishi huyo kweli au la huku kikao kikiomba sms hizo zifuatiliwe ili wamiliki wa namba hizo wajulikane .

  Baada ya kujadiliana kwa kina katika kikao hicho kilichodumu kwa muda wa saa mbili,Kayanda amemwomba mkuu wa wilaya msamaha kwa mapungufu yaliyojitokeza katika habari hiyo aliyoiandika, na mkuu wa wilaya ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Kahama amekubali kumsamehe mwandishi huyo akiahidi kufuata taratibu zingine kuondoa kesi mahakamani na kutaka kusafishwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii ilikoandikwa habari hiyo.

  Nkurlu amesema anatambua kazi nzuri inayofanywa na waandishi wa habari wilaya ya Kahama na mkoa wa Shinyanga kwa ujumla katika kuandika habari zinazohusu serikali na akaomba kudumishwa kwa ushirikiano uliopo baina ya viongozi wa serikali na waandishi wa habari ili kusaidia kuharakisha maendeleo ya wananchi huku akiwasisitiza waandishi wa habari kuzingatia weledi katika kazi zao.

  Aidha Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga imewasisitiza waandishi wa habari kuzingatia weledi na kufuata maadili katika kutekeleza majukumu yao ili kuepuka migongano isiyokuwa na tija kwa umma.

  Pia tunawashauri wadau wote wa habari pindi inapotokea kuingia katika mgogoro wowote ama na waandishi wa habari au chombo cha habari si vyema kwenda mahakamani moja kwa moja bali wawasiliane na viongozi wa klabu za waandishi wa habari katika mkoa husika ili kusuluhishana na kuwekana sawa.

  Imetolewa na
  Kadama Malunde
  MWENYEKITI –SPC

  Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu,waandishi wa habari na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Kahama wakiwa katika kikao cha usuluhishi

  Waandishi wa habari wakiwa katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kahama

  Kikao kinaendelea

  Waandishi wa habari wakiondoka katika ofisi ya mkuu wa wilaya baada ya kikao kumalizika.

  0 0

  Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii Kilombero

  Ujenzi Wa Daraja la mto kilombero ni moja ya vitu vinavyotajwa na vilivyopo katika vinywa Vya wakazi wa eneo hili kukuza uchumi wa Wilaya ya Malinyi na Ulanga.

  Ujenzi Wa daraja hilo ambao umekamilika kwa asilimia 80 unatarajiwa kuongeza  matumaini makubwa kwa wakazi wa Wilaya hizi mbili, ambazo kwa kiasi kikubwa hutegemea biashara ya mchele Kama ndio uti wa mgongo wa mapato.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Chalinze wa Malinyi, Marcelin Ndimbwa amesema daraja hilo litafungua Biashara upya kwa kasi kutokana maeneo hayo kufikiwa na vyombo vya usafiri kwa saa 24 .

  Amesema Wilaya hizi mbili zilikuwa zinadumaa kutokana na kutofikika kwa urahisi ,lakini kwa muonekano huo kila mmoja ana matumaini na serikali ya awamu ya tano ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli.

  Mmoja wa wakazi wa Ifakara Said Lumisha amesema kila mfanyabiashara ana imani na serikali ya awamu ya tano,kwani kila mmoja anahitaji kusafirisha Mchele mwingi, ila wanashindwa kutokana na tatizo la miundo mbinu ikiwemo kivuko.

  Ametaja kuwa mzigo wa kupakiwa kwenye Lori,unapakiwa nusunusu kutokana na kivuko kutokuwa na uwezo mkubwa, lakini siku chache maroli makubwa yataweza kufika mpaka Ulanga na Malinyi kwa urahisi na zaidi.

  Ametaja uwepo Wa daraja hilo kuwa utafungua njia ya basi kwenda Songea kupitia Malinyi kwani njia ni fupi kuliko kuzunguka Iringa,Anataja kuwa watu Wa mikoa ya kusini wakihitaji kwenda Dodoma hawatakuwa na haja ya kupitia Dar es salaam kwani daraja hili likikamilika mambo mengi ya kimaendeleo yatafunguka,


  Muonekano wa daraja la Kilombero kwa mbali ambalo inaelezwa kwa asilimia 80 limekwishakamilika


  Sehemu ya ujenzi wa daraja hilo muhimu ukiendelea

  0 0
  0 0

  Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Zubery Muhombeji amewataka wanaruvuma kusherekea sherehe za kuupokea mwaka katika hali ya amani na utulivu kwa undani zaidi wa habari hii msikilize kupitia video hii


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Bw. Ashraf Ramadhani, mlemavu kutoka Bukoba mkoani Kagera, aliyemtembelea kijijini kwake Chato mkoani Geita ambapo alikaa na kumsikiliza changamoto za kimaisha anazokumbana nazo.

  0 0  0 0

  Siku ya Alhamis tarehe 29/12 Bw. Wasia Maya kutoka mjini Houston , Texas aliamua kuachana na kambi ya makapera na kufunga ndoa na Bi. Laila Martin. Harusi hiyo ilifanyika nyumbani kwa Bw. Wasia na kuhudhuriwa na Watanzania wengi waishio katika jiji la Houston na miji ya jirani. Ijumaa ya tarehe 30/12 kulifanyika Nikka Dinner katika ukumbi wa Pakwan uliopo kwenye makutano ya barabara za HW6 na Beechnut . Pata picha za Harusi na Nikka Dinner hapa chini.
  Bw. Wasia na Bi. Laila siku ya ndoa yao
  Maharusi wakiwa na sura za furaha   Bw. Wasia na mkewe Bi. Laila
  Bibi Harusi Bi. Laila

  Bw. Wasia

  Bi. Laila  Bw. Wasia akiwa kaka Said Nassor

  Kaka Mohamed Msika , Bw. Wasia Maya na kaka Said Nassor

  Maharusi
  Kaka Ally Mjungu akiwa na Bw. Wasia Maya  Kaka Ally Mjungu , Bw. Wasia Maya na Uncle Shebby Pambwe  Bwana Wasia akiozeshwa 

  The 1st kiss
  NIKKA DINNER


  Kaka Ramadhan Machapati, Kaka Kassim Daffa na Kaka Abdul

  Bi. Amina na Bi. Zainab
  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amewaomba radhi wale wote aliokwaluzana nao mwaka 2016 kwa njia moja au nyingine kwani yeye ni binadamu si maraika hivyo hajakamilika.

  Kasesela ameongezea na kusema kuwa katika kuhakikisha mambo yanakwenda sawa lazima mtapishana lugha na watu ndipo mambo yaende sawa, pia amewataka wana Iringa kusherekea mwaka mpya kwa njia ya amani na tulivu kwa undani wa habari hii angalia hiyo video.


  0 0

  Wakazi wa mji wa Lindi wakifanya usafi wa mazingira katika mitaa na barabara zinazozunguka hospitali ya mkoa huo Desemba 31, 2016. Walifanya hivyo kuitikia agizo la Rais John Pombe Mgufuli la kuwataka watanzania kutumia muda wa asubuhi kila Jumamosi kufanya usafi wa mazingira. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba Desiderius Rwoma mara baada ya kuwasili katika Kanisa Kuu la Jimbo katoliki Bukoba mkoani Kagera.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akibusu mkono wa Askofu Msaidizi Jimbo Katoliki la Bukoba Askofu Methodius Kilaini mara baada ya kuwasili katika Kanisa Kuu la Jimbo katoliki Bukoba mkoani Kagera kwa ajili ya Ibada.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekea katika katika Kanisa Kuu la Jimbo katoliki Bukoba mkoani Kagera mara baada ya kuwasili na kupokewa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba Desiderius Rwoma (katikati) pamoja na Askofu Msaidizi Jimbo Katoliki la Bukoba Askofu Methodius Kilaini wa kwanza (kulia).
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika ibada ya mwaka mpya katika Kanisa Kuu la Jimbo katoliki Bukoba mkoani Kagera.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba Desiderius Rwoma mara baada ya Ibada.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na waumini wa Kanisa Kuu la Jimbo katoliki Bukoba mkoani Kagera mara baada ya Ibada.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisali katika kaburi la Marehemu Kadinali Rugambwa mara baada ya Ibada kanisani hapo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba Desiderius Rwoma mara baada ya kushiriki Misa ya Mwaka mpya kanisani hapo. Katikati ni Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba Askofu Methodius Kilaini.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha Wageni Kanisani hapo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba Desiderius Rwoma kushoto pamoja na Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba Askofu Methodius Kilaini.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na masista kanisani hapo mara baada ya Ibada. PICHA NA IKULU.

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilith Mahenge akiwa katika boti ya kisasa inayotumiwa na idara ya maliasili na uvuvi wilaya ya Nyasa kabla ya kuzunguka ziwa Nyasa kuangalia vivutio mbalimbali vya utalii katika wilaya ya Nyasa mkoani humo,kushoto ni mkuu wa wilaya ya Nyasa Esabila Chilumba.
  Naibu waziri wa elimu na mafunzo mhandisi Stella Manyanya kushoto akimsikiliza askofu wa kanisa la Anglikana Doyasisi ya Ruvuma Raphael Reuben Haule ndani ya boti la Mv Matema linalofanya safari zake kati ya kijiji cha Liuli na maeneo mengine ndani ya ziwa Nyasa,katikati mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilith Mahenge.
  Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilith Mahenge katikati akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Tamasha la kuvitangaza vivuutio vya utalii katika wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma jana,kulia mkuu wa wilaya ya Mbinga Kosmas Nshenye,wa pili kulia mkuu wa wilaya ya Nyasa Esabila Chilumba na kushoto nmbunge wa jimbo la Nyasa Stella Manyanya.
  Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilith Mahenge akiangalia kahawa ya kopo inayolimwa katika wilaya ya Nyasa na kusindikwa katika kiwanda cha kukoboa kahawa cha Mbinga ambayo ni moja kati ya rasimali na utajiri uliopo katika wilaya Nyasa,kulia ni mkuu wa wilaya ya Nyasa Esabela Chilumba na kushoto Mbunge wa jimbo la Nyaa na naibu waziri wa elimu Stella Manyanya.
  Naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Nysasa mkoani Ruvuma mhandisi Stella Manyanya kulia na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mafia mkoani Pwani Erick Mapunda wakiangalia makapu yanayotumika kubebea dagaa katika ziwa nyasa wakati wa Tamasha la kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika wilaya ya Nyasa.
  Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilith Mahenge akizungumza jana na wananchi, watendaji wa serikali na wageni kutoka nje ya mkoa huo(hawapo pichani) waliofika katika uzinduzi wa Tamasha la kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika wilaya ya nyasa mkoani humo,kulia ni mkuu wa wilaya ya Nyasa Esabila Chilumba na kushoto mbunge wa jimbo la Nyasa ambaye pia ni naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Mhandis Stella Manyanya.
  Nahodha wa boti ya kisasa iliyonunuliwana serikali kwa ajili ya kufanya kazi ya doria ya uvuvi haramu na kusaidia shughuli ya uokoaji katika ziwa nyasa Baraka Mguhi akimsaidia kuvaa jakti maalum(life jacket)mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Binilith Mahenge kabla ya kuzunguka ziwa nyasa kuangalia vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo katika wilaya ya Nyasa.

  0 0

  MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) umefanikiwa kulipa vituoni madai yanayotokana na huduma za afya kwa wakati  zaidi ya bilioni 5.1 kwa mwaka wa fedha 2015/2016 sawa na asilimia 148.
  Malipo hayo yamesaidia huduma kuboreshwa kwenye vituo mbalimbali ikiwemo watoa huduma kuhamasika na uelewa juu ya mfuko huo .

  Hayo yalisemwa hivi karibuni na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga(NHIF) Ally Mwakababu (Pichani )wakati akitoa taarifa ya utendaji wa mfuko huo kwa waandishi wa habari mkoani hapa.

  Ambapo alisema kwenye kipindi cha mwaka 2014/2015 walilipa kiasi cha zaidi ya bilioni 3.5 hali inaonyesha ongezeko kwa mwaka huu.
  Alisema pamoja na malipo kuongezeka lakini bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo huduma za afya vijijini imekuwa kikwazo sanjari na upatikanaji wa dawa vituoni.

  Aidha alisema lakini pia kuongezeka kwa magonjwa yakiwemo ya ukimwi ikiwemo upungufu wa watumishi katika sekta ya afya. “Lakini changamoto nyengine ni ugonjwa wa ukimwi kwa wanachama ni chanzo cha magonjwa nyemelezi na lakini pia halmashauri hazijachangamkia mikopo ,vifaa tiba,ukarabati na dawa kwenye vituo vyao “Alisema.

  Aidha alisema katika kuhakikisha uhai wa mfuko huo unakuwa endelevu mfuko huo uliamua kufanya ukaguzi kwenye vituo vinavyoashiria wizi na udanyanifu.

  “Katika kipindi hicho mfuko umefanikiwa kuokoa kiasi cha zaidi ya milioni 83.6 kutokana na ukaguzi maalumu 29 zilifanyika kwenye vituo 22 kutokana na kuona vinaashiria vya hujuma au uadanyanyifu wa huduma kwa wanachama wa Bima ya Afya “Alisema.

   “Kaguzi hizo zilifanyika kwenye vituo vya serikali 10 sawa asilimia 45,vituo vya madhehebu ya dini 8 sawa na asilimia 36 na vituo vya watu binafsi 4 sawa na asilimia 19 “Alisema.

  Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tangaraha

  0 0

  Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa KamatiKuu ya CHADEMA Taifa Mh Edward Lowassa akizungumza na waumini wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Monduli Arusha  katika misa maalamu ya mwaka mpya 2017 ambapo amewataka watanzania wote bila kujali itikadi zao  kufanya kazi kwa bidii.

  Mh Lowassa ameshiriki ibada hiyo akiambatana na familia yake pamoja na baadhi ya viongozi wa chama na Serikali Mkoani Arusha na Jimbo la Monduli  wakiwemo Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mh Kalisti Lazaro,  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli Mh  Isack Joseph , Wakili John Mallya  na viongozi wengine. 

  Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Taifa Mh Edward Lowassa, mama Regina Lowassa akisalimiana na  mchungaji wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Monduli Arusha  Laison Saning'o katika Ibada  maalamu ya mwaka mpya 2017.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Taifa Mh Edward Lowassa akisalimiana na  mchungaji wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Monduli Arusha  Laison Saning'o katika  Ibada  maalamu ya mwaka mpya 2017.
  Wakili John Mallya (aliyeshika biblia) akisoma neno kwenye biblia katika Ibada ya mwaka mpya katika  Kanisa la KKKT Dayosisi ya Monduli Arusha.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Taifa Mh Edward Lowassa akizungumza na waumini wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Monduli Arusha  katika misa maalamu ya mwaka mpya 2017
  Mtoto mkubwa wa Mh Lowassa, Fred Lowassa (mwenye shati jeupe) akiwa na waumini wengine katika Ibada ya mwaka mpya katika  Kanisa la KKKT Dayosisi ya Monduli Arusha leo.
  Mtoto mkubwa wa Mh Lowassa, Fred Lowassa (mwenye shati jeupe) akiwa na waumini wengine katika Ibada ya mwaka mpya katika  Kanisa la KKKT Dayosisi ya Monduli Arusha leo.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria kuanza kwa ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kabyaile Misenyi Mkoani Kagera. Wengine katika picha ni Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage, Waziri  Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Vija Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama pamoja na Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako wakiwa wameshika utepe huo.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahi  mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika Kituo cha Afya cha Kabyaile Misenyi Mkoani Kagera.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua maeneo ya ujenzi wa kituo hicho cha Afya cha Kabyaile kilichopo Misenyi mkoani Kagera.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua maeneo ya ujenzi wa kituo hicho cha Afya cha Kabyaile kilichopo Misenyi mkoani Kagera.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua maeneo ya ujenzi wa kituo hicho cha Afya cha Kabyaile kilichopo Misenyi mkoani Kagera.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua maeneo ya ujenzi wa kituo hicho cha Afya cha Kabyaile kilichopo Misenyi mkoani Kagera.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katika eneo la mradi wa ujenzi wa kituo hicho cha Afya cha Kabyaile kilichopo Misenyi mkoani Kagera.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katika eneo la mradi wa ujenzi wa kituo hicho cha Afya cha Kabyaile kilichopo Misenyi mkoani Kagera.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katika eneo la mradi wa ujenzi wa kituo hicho cha Afya cha Kabyaile kilichopo Misenyi mkoani Kagera.
  Moja ya majengo katika mradi huo wa kituo cha Afya cha Kabyaile kilichopo Misenyi mkoani Kagera.  
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika eneo la Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kabyaile Misenyi Mkoani Kagera.
  PICHA NA IKULU

  0 0

  Papa Francis
  Mwinjilisti wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Mtaa wa Kivule, Ukonga Dar es Salaam Michael Mgaya (wa pili kushoto) akiwa na wazee wa kanisa hilo baada ya kumalizika kwa ibada. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

  Na Richard Mwaikenda
  KIONGOZI Kanisa la Katoliki Duniani, Papa Francis amekubali mwaliko wa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 500 ya kuasisiwa kwa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Duniani.

  Taarifa hiyo imetangazwa leo wakati wa Ibada ya Jumapili ya kuukaribisha mwaka mpya katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Mtaa wa Kivule Ukonga, Dar es Salaam.

  Maadhimisho hayo yatafanyika hivi karibuni eneo ambapo kanisa hilo liliasisiwa nchini Ujerumani ambapo kutakuwa na shamrashamra za kila aina zitakazoshuhudiwa na wageni kutoka nchi mbalimbali.

  Kwa hapa nchini maadhimisho hayo yatafanyika katika Chuo cha Dini cha Makumira, mkoani Arusha, ambapo mnara wa kumbukumbu utajengwa. Kanisa hilo liliasisiwa mwaka 1557.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Juma Homera amesema watendaji wa Vijiji ambao sio waadilifu kutokana na kupokea rusha kutoka kwa wafugaji kwa lengo la kuwapa makazi katika vijiji , ndiyo chanzo cha migogoro hiyo katika ya wakulima na wafugaji. Kwa undani wa habari hii bonyeza hii video.Habari na RUVUMA TV.


  0 0

  Na Lulu Mussa
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba hii leo amefanyia ziara ya kikazi ya kukagua hatua za ujenzi katika miradi inayofadhiliwa na Ofisi yake.

  Akiwa katika Wilaya ya Ilala, Waziri Makamba ametembelea ujenzi wa Mfereji wa kupitishia maji taka katika eneo la Ilala Bungoni na kuongea na wananchi wa eneo hilo.

  Waziri Makamba ameugiza uongozi wa Dezo  Civil Constractors Co. Ltd kuhakikisha ujenzi wa Miundombinu ya maji taka katika Manispaa za Ilala na Temeke unakamilika kwa muda uliopangwa na kwa ubora wa hali ya juu kwa kuzingatia makubaliano yaliyopo katika mkataba.

  “Nataka mradi huu uwe wa mfano kwa ubora na viwango vya hali ya juu, ikiwa ni jitihada za kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabianchi, kwa kuweka mfumo mzuri wa kukusanya maji taka na kuyaelekeza sehemu stahiki” Makamba alisisitiza.

  Aidha, Waziri Makamba amewataka wakazi wanaozuka eneo hilo kuacha mara moja utupaji wa taka maji na taka ngumu katika mfereji huo unaojengwa, na kumuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw. Palela Msongela kutoa adhabu kali kwa yeyote atakayekiuka agizo hilo.
  “Kwa kupitia kamati za Mazingira za vitongoji na sheria ndogo ndogo mlizojiwekea hakikisheni kuwa hifadhi ya mazingira inazingatiwa kwa mstakabali wa vizazi vya sasa na vizazi vijavyo.”

  Pia, Waziri Makamba amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kuhakikisha Wakandarasi wanaopewa kazi za ukusanyaji wa taka, wanakuwa na vifaa na uwezo wa kutosha kwa kuhakikisha taka zote zinazolewa kwa wakati ili kuepuka mrundikano wa taka katika makazi ya watu.

  “Natoa wito pia kwa vijana wa maeneo haya kuunda vikundi vidogo vya kuzoa taka ili kuwa chanzo cha ajira kwenu.” Makamba alisisitiza.
  Waziri Makamba ameliagiza Baraza la Taifa La Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira -  NEMC kutembelea eneo hilo la Ilala Bungoni na kutoa maelekezo kwa Gereji bubu  zinazokiuka hifadhi na usimamizi wa Mazingira kwa kufanya shughuli zao pembezoni mwa mfereji unaojengwa.

  Ujenzi wa Ukuta wa (Obama/Ocean Road na Kigamboni) na Miundombinu ya maji taka katika Manispaa za Ilala na Temeke unatekelezwa chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia  Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi na  unafadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira (UNEP). Aidha, Kampuni ya Dezo Civil Contractors ndio inafanya kazi ya ujenzi huu na kazi zinatarajiwa kukamilika mwezi Julai 2017.

  Waziri Makamba katika ziara yake hii leo ametembelea Ilala Bungoni, Mtoni kwa Azizi Ali, Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Kutembelea eneo la Ujenzi wa Ukuta Barabara ya Obama.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiongea na Diwani wa Kata ya  Buguruni Mhe.  Adam Fugame (katikati) wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua ujenzi wa mfereji wa maji taka katika eneo la Ilala Bungoni jijini Dar es salaam
   Sehemu ya Mfereji wa Maji taka unaojengwa eneo la Ilala Bungoni chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia  Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi na  unafadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira (UNEP).
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiongea na Wananchi wakazi wa Ilala Bungoni, mara baada ya kukagua ujenzi wa mrefeji wa maji taka 
  Mwakilishi wa UNOPS Bw Bernard Omondi akifanunua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba katika eneo la Temeke - Mtoni kwa Azizi Ali ambapo kazi ya kusafisha na kujenga mfumo wa maji taka inaendelea. 

   Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora ( wa tatu kutoka kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba mara baada ya ziara ya kukagua hatua za ujenzi kwa miradi inayosimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.  Kulia ni Bw. Kanizio Manyika Afisa Mazingira Mkuu na Msimamizi wa Mradi na Bw. Richard Muyungi Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira.


  0 0

   Mhandisi Felchesmi Mramba


  0 0

  Naibu Spika wa Bunge, Dk.Tulia Akson, akipeperusha bendera ya Taifa wakati wa mkesha mkubwa wa kitaifa wa dua maalumu uliofanyika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam jana. Dk.Akson alimwakilisha Rais Dk.John Magufuli kwenye mkesha huo ambaye alikuwa mgeni rasmi.
  Naibu Spika wa Bunge, Dk.Tulia Akson (katikati), Mratibu wa mkesha huo Askofu Godfrey Malesi na Askofu Damas Kenasi (kulia), wakishiriki kuomba katika mkesha huo.
  Waimbaji wa Kwaya ya Mass ya Sinza jijini Dar es Salaam wakiimba nyimbo za kumsifu mungu.
  Watoto waimbaji wa Kwaya ya Mass ya Sinza jijini Dar es Salaam wakifanya vitu vyao kwenye mkesha huo.
  Waumini wakiwa wameinua mikono kwenye mkesha huo.
  Maombi yakiendelea.
  Wananchi wakisubiri kuupokea mwaka mpya wa 2017 katika uwanja huo.
  Shamrashamra za kuupokea mwaka mpya.
  Mwaka mpya wa 2017 ukipokelewa.
  Wananchi wakiwa wamelala wakisubiri kuupokea mwaka mpya.

  Na Dotto Mwaibale

  NAIBU Spika wa Bunge Dk. Tulia Akson amesema Tanzania mpya na yenye matokeo chanya kwa mwaka 2017 inawezekana hivyo akamataka kila mmoja wetu kufanyakazi kwa bidii ili kuliletea taifa maendeleo.

  Dk.Akson aliyasema hayo kwa niaba ya Rais Dk.John Magufuli wakati akihutubia kwenye mkesha mkubwa wa kitaifa wa dua maalumu uliofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam jana.

  "Tanzania mpya na nchi mpya yenye matokeo chanya kwa mwaka 2017 inawezekana" alisema Akson

  Akson alimwakilisha Rais Dk.John Magufuli alikuwa mgeni rasmi kwenye mkesha huo mkubwa ulioandaliwa na makanisa mbalimbali ya kiroho.

  Akinukuu baadhi ya maneno kutoka katika kitabu cha biblia cha Nyakati mungu ataiponya nchi iwapo kila mtu atamuita kwa jina lake na kujinyenyekesha na kuomba na kuziacha njia mbaya.

  "Tukimuita mungu kwa jina lake na kujinyenyekesha kwa kuacha kutenda mambo mabaya mungu ataiponya nchi yetu" alisema Akson.

  Mratibi wa mkesha huo Askofu Godfrey Malesi alisema hivi sasa kila Januari Mosi mikoa 17 hapa nchini imekuwa ikifanya mkesha huo ikiwepo na Zanzibar kwa ajili ya kuwaombea viongozi wa nchi na taifa kwa ujumla.

  "Mungu amekuwa akijibu maombi yetu tangu tuanze kuomba kupitia mkesha huu tulipoanza jijini Dar es Salaam mwaka 1997" alisema Malesi.

  Alisema tangu wakati huo wamekuwa wakiiombea nchi iwe na amani na kuondokana na ufisadi na kumpata Rais atakayeifanya Tanzania iwe mpya ambapo amepatikana Rais Dk.John Magufuli ambaye ameifanya nchi kuwa na muelekeo mpya.

  Alisema lengo lao ni kuhakikisha mkesha huo unafanyika katika mikoa yote na kila eneo la nchi yetu.

  Mkesha huo uliopambwa na nyimbo kutoka kwaya ya Mass ya Sinza jijini Dar es Salaam na Brass Band ya Polisi ulihudhuriwa na viongozi wa dini kutoka nchi za jirani za Rwanda na Burundi ambao walipata fursa ya kuzungumzia umuhimu wa nchi kuwa na amani.

older | 1 | .... | 1086 | 1087 | (Page 1088) | 1089 | 1090 | .... | 1898 | newer