Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1085 | 1086 | (Page 1087) | 1088 | 1089 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Msajili wa Hazina Dk.Oswald Mashindano akikabidhiana na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya AICC Balozi Dk.Ladislaus Komba mkataba wa makubaliano ya utekelezaji wa mkakati wa mwaka kati ya Taasisi za Serikali na Zisizo za Serikali kupitia msajili wa Hazina.
  Msajili wa Hazina Dk.Oswald Mashindano akizungumza jambo na baadhi ya wajumbe kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam(UDSM)na Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya Kitropiki Tanzania.(TPRI) wakati wa hafla ya makabidhiano ya makubaliano ya utekelezaji wa mkakati wa mwaka kati ya Taasisi za Serikali na zisizo za Serikali kupitia msajili wa hazina.
  Msajili wa Hazina Dk.Oswald Mashindano akikabidhiana na mwakilishi kutoka Mfuko wa Umoja wa Dhamana ya Uwekezaji Tanzania mkataba wa makubaliano ya utekelezaji wa mkakati wa mwaka kati ya Taasisi za Serikali na Serikali kupitia msajili wahazina .Nyuma ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Umoja wa Dhamana ya Uwekezaji Tanzania Bw.James Washima.
  Wajumbe mbalimbali kutoka Bodi yaWakurugenzi ya AICC na Mfuko wa Umoja wa Dhamana ya Uwekezaji  Tanzania wakimskiliza Msajili wa Hazina Dk.Oswald Mashindano (hayupo pichani) wakati wa makubaliano ya utekelezaji wa mkakati wa mwaka kati ya Taasisi za Serikali na Serikali kupitia msajili wa hazina.
  MsajiliwaHazinaDk.Oswald Mashindano akikabidhiana na mwakilishi kutoka Taasisi ya Utafiti wa Viuatilifu vya Kitropiki  Tanzania (TPRI) mkataba wa makubaliano ya utekelezaji wa mkakati wa mwaka kati yaTaasisi za Serikali na Serikali kupitia msajili wa hazina.
  Mhadhiriwa Chuo Kikuu cha Dar essaalaam Prof. Paramagamba Kabudi akitia saini mkataba wa makubaliano ya utekelezaji wa mkakati wa mwaka kati yaTaasisi za Serikali na Serikali kupitia msajili wa hazina leo Jijini Dar esSalaam.Kushoto kwake ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar esSalaam Profesa Rwekaza Mukandara


  PichanaDaudiManongi-MAELEZO.

  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku kulia akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kikundi cha Golani Shutashuta,Saidi Bakari  wakati alipokwenda akikagua mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji eneo la Golani Shutashuta Kata ya Pande Jijini Tanga jana wakati alipofanya ziara ya kuwatembelea kuona namna wanavyotekeleza majukumu yao na changamoto ambazo zinawakabili
  Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku akikangalia naamna mradi huo unavyopandwa

  Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku akikagua mradi huo leo mara baada ya kuwasilia kwenye eneo hilo
  Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku akikagua hoho wakati alipokuwa akitembelea mradi huo wa kilimo cha Umwagiliaji wa Kikundi cha Golani Shutashuta eneo la Kata ya Pande Jijini Tanga
  Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku akikagua hoho wakati alipokuwa akitembelea mradi huo wa kilimo cha Umwagiliaji wa Kikundi cha Golani Shutashuta eneo la Kata ya Pande Jijini Tanga
  Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku
  Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku akikagua tikitiki maji wakati alipotembelea mradi wa umwagiliaji leo wa  Kikundi cha Golani Shutashuta eneo la Kata ya Pande Jijini Tanga

  Mbunge wa Jimbo la Tanga,Alhaji Mussa Mbaruku akipata tunda la tikiti maji mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea kilimo cha Umwagiliaji wa Kikundi cha Golani Shutashuta eneo la Kata ya Pande Jijini Tanga katikani ni mwandishi wa gazeti la tanzania Daima Tanga Mbaruku Yusuph.Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa Ruangwa wakati alipowasili kwenye uwanja wa Ofisi ya CCM ya wilaya hiyo kuhutubia mkutano wa hadhara Desemba 30, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Ofisi ya CCM ya wilaya ya Ruangwa Desemba 30, 2016.
  Baadhi ya wananchi wa mji wa Ruangwa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Ofisi ya CCM ya wilaya hiyo mjini Ruangwa Desemba 30, 2016.
  Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Nandagala wilayani Ruangwa wakigalagala kuonyesha furaha katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye uwanja wa Ofisi ya CCM ya wilaya ya Ruangwa, Desemba 30, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea zawadi ya mkeka kutoka kwa wananwake wa Ruangwa katika mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye uwanja wa Ofisi ya CCM ya wilaya ya Ruangwa Desemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0


  Kwa mujibu wa kifungu cha 40 (6) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Tume ilipokea Rufaa moja ya kupinga Uteuzi wa Mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF) katika Uchaguzi Mdogo wa Bunge Jimbo la Dimani – Zanzibar.
   Rufaa hiyo ilikatwa na Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bwana Juma Ali Juma akipinga Maamuzi ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Dimani aliyemthibitisha Mgombea wa Chama Cha Wananchi (CUF) Bwana Abdul Razak Khatib Ramadhani kuwa ni mgombea halali.
   Rufaa hiyo ilikuwa na sababu mbili ambazo ni:- (i) Hakurudisha Fomu za Uteuzi kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na sheria na (ii) Hakudhaminiwa na Chama cha Siasa kugombea Ubunge. Katika kikao chake cha leo tarehe 30 Desemba, 2016, Tume imepitia Rufaa hiyo na kuona sababu zilizotolewa na mkata Rufaa hazina nguvu ya kisheria, kwa kuwa, Mgombea wa CUF amerudisha Fomu za Uteuzi kwa mujibu wa sheria na taratibu.
  Pia, Fomu zake za Uteuzi zimesainiwa na kugongwa muhuri wa Katibu wa Wilaya ya Magharibi B. Kwa mantiki hiyo, Tume imekubaliana na Uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Dimani – Zanzibar.  Hivyo, Mgombea wa CUF amekidhi vigezo na uteuzi wake ni halali na aendelee na kampeni za kugombea nafasi ya Ubunge wa Jimbo hilo.

  Aidha, kwa mujibu wa kifungu cha 44 (5) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, Tume imepokea Rufaa tatu; kutoka Kata ya Kijichi – Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Mkoa wa Dar es Salaam, Kata ya Misugusugu – Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Mkoa wa Pwani na Kata ya Ihumwa – Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma, Mkoa wa Dodoma.

  Kata ya Misugusugu Halmashauri ya Mji Kibaha, Rufaa ilikuwa ni ya Mgombea wa CHADEMA Bwana Gasper Melkiory Ndakidemi dhidi ya mgombea wa Chama cha Mapinduzi CCM Bwana Bogasi Hussen Ramadhani.

  Katika Kata ya Kijichi, Rufaa ilikuwa ni ya mgombea wa CUF Bi. Khadija Abdallah Shamas dhidi ya mgombea wa CHADEMA Bwana Fredrick Felician Rugaimukamu.
  Kata ya Ihumwa Rufaa ilikuwa ni ya Mgombea wa CHADEMA Bwana Magawa Edward Juma dhidi ya maamuzi ya Msimamizi wa Uchaguzi.Tume katika kikao chake cha leo tarehe 30 Desemba, 2016 imepitia Rufaa zote na imeamua ifuatavyo:

  Rufaa ya mgombea wa CHADEMA Bwana Gasper Melkiory Ndakidemi katika Kata ya Misugusugu Halmashauri ya Mji Kibaha na ya mgombea wa CUF Bi. Khadija Abdallah Shamas katika Kata ya Kijichi,  hazina mashiko ya kisheria na zimekataliwa.  Hivyo, Tume inakubaliana na Maamuzi ya Wasimamzi wa Uchaguzi wa Halmashauri hizo na wagombea waendelee na Kampeni kwa mujibu wa Ratiba.

  Kuhusu Rufaa ya Mgombea wa CHADEMA kutoka Kata ya Ihumwa, Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma. Tume, imepokea barua ya Msimamizi wa Uchaguzi, Manispaa ya Dodoma, ikiwa imeambatishwa na barua ya Mgombea wa CHADEMA kuiondoa Rufaa yake na kwamba anakubaliana na maamuzi ya Msimamizi wa Uchaguzi ambayo yalimuengua. Pia, leo Tume imepokea barua za kujitoa Ugombea za wagombea wa CHADEMA na ACT - WAZALENDO katika Kata ya Ihumwa. Kwa maana hiyo Rufaa iliyokuwa imekatwa na mgombea wa CHADEMA Kata ya Ihumwa imeondolewa kwa kuwa mkata Rufaa ameiondoa na amejitoa ugombea kabla haijasikilizwa.

  Mwisho, Tume inavisisitiza Vyama vya Siasa, Wagombea na Wananchi wote wa maeneo yenye Uchaguzi Mdogo kufanya Kampeni za kistaarabu kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Maadili ya Uchaguzi.
  Imetolewa na:-
  Jaji Mkuu (Mst. Znz) Hamid M. Hamid
  MAKAMU MWENYEKITI
  TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
  30/12/2016

  0 0

  SHIRIKA la Ndege la Etihad kupitia Kitengo chake cha Uhandisi (Etihad Airways Engineering) kwa kushirikiana na Lental Textiles AG wamezindua maabara ya kipekee ya kwanza Mashariki ya Kati kwa ajili ya wateja wa kanda hiyo walio sekta ya anga na waendeshaji mashirika ya uzalishaji na ubunifu.

  Maabara hiyo ambayo ipo ndani ya kituo cha uhandisi cha Shirika la Ndege la Etihad karibu kabisa na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abu Dhabi itakuwa inatoa huduma mbalimbali   ikiwemo vipimo vya kuwaka kwa moto, joto, moshi n.k.

  Aidha, maabara hiyo itaenda sambamba na hadhi ya ubora wa Kimataifa ISO 17025  na vipimo vyote vitafanyika kwa mujibu wa Kanuni za Anga za imataifa FAR/CS25.853.

  Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Uhandisi cha Shirika la Ndege la Etihad Jeff Wilkinson alisema, “Tunatoa huduma zilizotukuka kwenye matengenezo ya ndege na ufumbuzi wa kiuhandisi katika soko la anga duniani na kwa ajili ya aina zote za ndege za kibiashara.

  “Kupitia ushirikiano wetu huu na Lantal, itakuwa rahisi sasa na haraka kwa kwa wateja wa sekta ya anga katika Ukanda kupata huduma bora za vipimo katika kituo chetu cha Abu Dhabi,” alisema.

  Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Lantal, Dkt. Urs Rickenbacher alisema, “Maabara yetu ya Lantal kwa ajili ya vipimo nchini Uswisi inajulikana vema kwa huduma zake bora na haraka.  Kwa sasa tunalo soko kubwa barani Ulaya na sasa maabara yetu hapa Abu Dhabi tukishirikiana na Kitengo cha Uhandisi cha Shirika la Ndege la Etihad (Etihad Aiways Engineering) litatuwezesha kutoa huduma kwa ukaribu zaidi na wateja wetu wa Mashariki ya Kati,”.

  0 0

  Na Amina Kibwana,Globu ya jamii

  Halmashauri ya manispaa ya kinondoni imezindua utekelezaji wa mradi wa uboreshaji wa jiji la dar es salaam kwa kusaini mkataba wenye thamani ya bilioni 22 na mkandarasi kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya barabara.

  Akizungumza na waandishi wa habari maeneo ya makumbusho kata ya kijitonyama leo,Mstahiki meya wa Manispaa hiyo Benjamini Sitta amesema kuwa mpango wa mradi huu unalenga  kuboresha miundombinu ya barabara ambayo itasaidia kupunguza msongamano wa magari, kuondoa adha ya mafuriko na kuongeza thamani ya makazi ya watu pamoja na kupinguza umaskini.

  "Katika uboreshaji wa miundombinu barabara zitajengwa kwa lami nzito na huduma nyingine za watumiaji wa barabara kama maeneo ya waendao kwa miguu,taa za barabarani,mitaro ya majia pamoja na alama za vivuko ambavyo vitambadilisha sura ya manispaa ya Kinondoni na jiji la Dar es Salaam kwa ujumla."

  Aidha meya ametaja  barabara ambazo Zitahusika katika mpango huu ni pamoja na soko la makumbusho km1.45,MMK km 0.9,Nzasa km 1.25, Viwandani km 1.68 na Tanesko soko la samaki ambazo zitajengwa ndani ya mwaka mmoja na kwa kiwango  cha juu.

  Kwa upande wake mkandarasi kutoka Estim Construction Jagdish Bhudia amesema kuwa watajenga barabara kwa kiwango kinachotakiwa kama kwa kutumia lami nzito ili ziweze kudumu kwa muda mrefu bila kuharibika.

  Hata hivyo mstahiki meya wa manispaa ya kinondoni ameongeza kwa kuwataka wanachi wote wa manispaa hiyo kutoa ushirikiano wa kutosha katika mradi huu ambao unalenga kuboresha miundombinu  na kuimarisha huduma za kiuchumi, kibiashara na kijamii.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amelazimika kuendesha harambee ya papo kwa papo ma kuchangisha sh.milioni 138.26 ili kufanikisha ujenzi wa shule mpya ya sekondari wilayani Ruangwa.

  Hatua hiyo hiyo inafuatia wingi wa wanafunzi waliofaulu mtihani wa darasa la saba na kuchaguliwa kuingia kidato cha kwanza lakini hawakufanikiwa kupata nafasi katika mkupuo wa kwanza.

  “Katika kikao cha Halmashauri ya Wilaya cha hivi karibuni ilionekana kuna haja ya kujenga shule mpya ya sekondari ili kukabiliana na wingi wa watoto waliofaulu mtihani wa darasa la saba na kuchaguliwa kuingia kidato cha kwanza. Tunawashukuru sana wenzetu ambao wametoa maeneo yao bure ili shule ijengwe haraka,” amesema.

  Katika harambee iliyofanyika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Ruangwa leo mchana (Ijumaa, Desemba 30, 2016), Waziri Mkuu amefanikisha kupatikana kwa fedha kiasi cha sh. milioni 120.65 na mifuko 550 ya saruji  na mabati 360 (vyenye thamani ya sh. milioni 17.61) ambavyo vitatumika kujenga madarasa manne ya kidato cha kwanza yanayotakiwa kuwa yamekamilika ifikapo Januari 15, 2017.

  Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa, Bw. Andrea Chezue, jumla ya watoto 319 walichaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza lakini walikosa nafasi sababu ya ukosefu wa madarasa na walitakiwa kusubiri hadi chaguo la pili ambalo kwa kawaida hufanyika Februari, kila mwaka.

  “Wanafunzi waliofaulu na kukosa nafasi jumla yao ni 319 lakini kwa hapa Ruangwa mjini ni 179 na waliobakia 140 wanatoka kwenye kata za jirani za Nachingwea na Mandarawe. Shule hii ya sekondari itahudumia kata tatu. Kwa hiyo Halmashauri imepanga kujenga madarasa manne hapa mjini ili watoto wote waweze kuanza mara moja,” amesema.

  Mkurugenzi huyo amesema ili kupunguza tatizo hilo mwakani, wataendeleza ujenzi wa madarasa manne manne waweze kuwa na mikondo minne kwa kila kidato. “Halmashauri ya Ruangwa imetenga sh. milioni 75, wananchi wa Kata ya Ruangwa wametoa sh. milioni 1.2 na wananchi wa kata ya Nachingwea wametoa sh. milioni 2.25,” amesema.

  Waziri Mkuu ambaye ni mbunge wa jimbo hilo, amechangia sh. milioni 33 kutoka kwenye mfuko wa jimbo ili kuharakisha ujenzi wa madarasa mawili ya kuanzia. Wengine waliochangia harambee hiyo ni kampuni ya Paco Gems Ltd, (sh. milioni 6), Baraka Solar (sh. milioni moja), Ofisi ya Mkuu wa Mkoa (sh. milioni 1), Kampuni ya Asamalema (sh. milioni 1) na mfanyabiashara wa Ruangwa, Bw. Abdallah Namkudai (sh. 200,000).

  Wengine ni kampuni ya wanyumbani construction mifuko 100 ya saruji, kampuni ya Lindi Jumbo (mabati 100 na mifuko 100 ya saruji), kampuni ya madini ya Nazareth (mifuko 150 ya saruji), kampuni ya URANEX inayochimba madini ya Graphite (mabati 260), mgodi wa dhahabu wa Namungo (mifuko 100 ya saruji) na Kampuni ya ujenzi ya Nahungo Construction Ltd. (mifuko 100 ya saruji).

  Waziri Mkuu amewashukuru wote waliojitolea kuchangia ujenzi wa shule hiyo. Amerejea jijini Dar es Salaam jioni hii.

  IMETOLEWA NA
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  IJUMAA, DESEMBA 30, 2016.

  0 0


  Na Jumia Travel Tanzania

  KUJA kwa maendeleo ya sayansi na teknolojia hususani mtandao wa intaneti kumebadilisha kwa kiasi kikubwa mienendo ya matangazo ya utoaji wa huduma mbalimbali duniani na hii ni kutokana na uwezo wake wa kuwaruhusu wateja kutoa ushuhuda, kukosoa au kutoa maoni juu ya walichohudumiwa na kujionea.

  Tofauti na kipindi cha nyuma kidogo ambapo wataalamu wa masoko walikuwa wanatumia zaidi njia za luninga na redio kuwafikia wateja wao, siku hizi mfumo wa intaneti unapewa kipaumbele zaidi kutokana na namna unavyofikia watu wengi zaidi ndani ya muda mfupi, kwa haraka na gharama kidogo.

  Matangazo ya luninga na redio yanaweza kuwa hayana ushawishi mkubwa ukilinganisha na mtandao wa intaneti kwani hivi sasa makampuni yanaweza kuwasilisha bidhaa na huduma zao na kupokea majibu kujua kwamba zinakubalika au la. Hali hiyo ni dhahiri kutokana na makampuni mengi kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika teknolojia na rasilimali watu katika kusimamia tovuti na kurasa zao rasmi za mitandao ya kijamii kama vile facebook, twitter, instagram na mingineyo.

  Kupitia tovuti na kurasa hizo za mitandao ya kijamii biashara na huduma nyingi zinafanya vizuri kutokana na ushawishi wao kwenye mitandao kutokana na namna ambavyo zinazungumziwa vizuri na watu wengi. Lakini pia husaidia kampuni hizo husika kuwasiliana moja kwa moja na wateja wao kwa sababu wateja huwasilisha maoni yao moja kwa moja mtandaoni tofauti na luninga au redio ambazo hutoa fursa ya kuona au kusikiliza tu matangazo.
  Vivyo hivyo hali hii inaweza kusaidia sana ukuaji wa sekta ya utalii na ukarimu kama vile huduma za hoteli na malazi ambazo hujitangaza zaidi kupitia namna wateja wanavyozizungumzia.

  Jumia Travel (www.travel.jumia.com) kampuni unaongoza kwa huduma za hoteli mtandaoni barani Afrika umezitunuku vyeti hoteli kadhaa ambazo zilizopendekezwa na kutembelewa ndani ya wateja wengi kipindi cha mwaka mzima wa 2016.

  Akizungumzia juu ya umuhimu wa vyeti hivyo Meneja Mkazi wa Jumia Travel Tanzania, Bi. Fatema Dharsee amesema kuwa, “Vyeti hivi vina umuhimu mkubwa kwani ni viashiria vikubwa vya namna hoteli yako inatathminiwa vipi na wateja pindi wanapoitembelea. Siku zote wateja huambizana huduma wanazozipata sehemu za biashara wanazotembelea na kutokana na ushuhuda huo ndio na wengine hushawishika kutembelea pia. Kupitia mtandao wetu wateja wanayofursa ya kutoa maoni juu ya hoteli walizozitembelea, huduma walizopatiwa, mapungufu waliyoyaona na maboresho ambayo wangependa yafanyiwe kazi.”

  “Imefikia mahala sasa ni lazima wataalamu wa masoko watambue mchango na ushawishi walionao wateja kwenye kukua kwa biashara zao kwani nguvu yao ni kubwa zaidi ya matangazo wanayoyalipia kupitia luninga na redio au njia nyinginezo. Maneno au ushuhuda unaotolewa na wateja unatosha kwa kiasi kikubwa mtu kutumia bidhaa au huduma yako kwani ni halisi kutokana na mtu kuitumia au kupatiwa huduma hiyo husika. Hivyo ningependa kutumia fursa hii kuwataka mameneja wa hoteli waliokabidhiwa vyeti hivi kuichukulia hali hii kama ni changamoto kwao kwa kufuatilia maoni ya wateja yanayoachwa kwa njia ya mtandao na kuyafanyia kazi.” Alihitimisha Bi. Dharsee.

  Hoteli ambazo zimepatiwa vyeti hivyo ni pamoja na Jafferji House & Spa Hotel na Garden Lodge za visiwani Zanzibar, Golden Tulip Hotel, Peacock Hotel na Butterfly Hotel zote za jijini Dar es Salaam.


  0 0
  0 0

  Na: Frank Shija – MAELEZO

  WADAU waombwa kujitokeza na kuongeza kasi ya udhamini wa miradi inayotekelezwa kwa malengo ya kukwamua jamii kuondokana na changamoto mbalimbali wanazo kabiliana nazo.

  Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu wa Mradi wa Binti Jitambue Bi. Lilian Boniface wakati wa mkutano wao na wahandishi wa habari kuhusu tathmini ya utekelezaji wa mradi huo kwa kipindi cha miezi 11.

  Awali akifafanua changamoto walizokumbana nazo katika utekelezaji wa mradi huo Lilian amesema uhaba wa rasilimali fedha imekuwa kikwazo kikubwa kwao katika kutekeleza kwa ufasaha malengo ya mradi huo katika baadhi ya maeneo.

  “Nitumie fursa hii kutoa wito kwa Serikali na wadau wote wa maendeleo kutoa ufadhili kwa ajili kuimarisha utekelezaji wa mradi huu wa “Binti Jitambue” ili wasichana wengi zaidi waweze kunufaika na mradi huu muhimu kwao,” alisema Lilian.

  Kwa upande wake Meneja wa Mradi wa Binti Jitambue, Sara Bedah Akwisombe amesema kuwa licha ya changamoto wanazokumbana nazo wamefanikiwa kuwafikia watoto wa kike wenye umri kati ya miaka 10 hadi 16 wapatao 4000 nakuwapatia elimu juu ya Afya ya uzazi,, makuzi na kujitambua.

  Aliongeza kuwa tathmini ya mradi huo imebaini kuwa takribani asilimia 80 ya wazazi hawapati muda wa kukaa na kuwaelimisha watoto wao juu ya masuala mbalimbali yanayohusu malezi na makuzi.

  Katika kutekeleza azma hiyo mwaka 2017 mradi huu pia utatekelezwa katika mkoa wa Tanga ikiwa ni muendelezo wa jitihada za kuwasaidia watoto wa kike kujitambua na kutambua thamani na fursa zao katika jamii.

  Binti Jitambue ni mradi ambao umeanzishwa tarehe 30 Januari, 2016, kwa lengo la kusaidia utipatikanaji wa elimu ya afya ya uzazi, malezi na makuzi, elimu ya kujitambua utu na thamani kwa watoto wa kike, ambapo awamu ya kwanza umetekeleza katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Kirimanjaro chini ya uratibu wa Taasisi ya Tanzania Youth Vision Association (TYVA) ya jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi.

  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr Rehema Nchimbi ametoa wito kwa watumishi wa Umma Mkoani humo kuingia mwaka 2017 wakiwa na uelewa sahihi wa malengo ya serikali ya awamu ya Tano ya kuwatumikia wananchi kwa uweledi na kutatua matatizo yao kwa kasi ili kuinua maisha ya wananchi na Maendeleo ya Mkoa huo.

  Mwaka 2017,tunataka tupige hatua kubwa zaidi kupitia raslimali zetu ambazo zitawezesha maendeleo katika Mifugo, Ukulima Mazao ya Kisasa, Ufugaji Nyuki, Ufugaji Samaki, Uvunaji wa Maji ya Mvua, Utunzaji wa Mazingira na Usindikaji wa Mazao kwa malengo ya ujumla ya kumuendeleza mwananchi na kutosheleza mahitaji ya Wanasingida na Soko la Dodoma Makao Makuu ya Nchi. Tunafanikiwa iwapo wananchi wote, watendaji na Viongozi wote tutashirikiana na kuwajibika kwa uwaminifu, uwadilifu na uweledi. Aliongeza Dr Nchimbi

  Dkt Nchimbi amewataka wanchi wote wa Mkoani Singida washerekee Mwaka Mpya kwa amani bila kufanya mambo yeyote yatakayo ashiria uvunjifu wa amani ili kuufanya Mkoa huo kuwa ni kielelezo cha Utulivyo na amani na kuwafanya wageni wanaoingia Singida wasiwe na hufu na masha juu ya usalama wao.

  Nawashauri wananchi wa Mkoa wangu wa Singida kuukaribisha mwaka mpya kwa kwenda kwenye nyumba za ibada na kumshukuru Mungu kwa Uzima aliotupatia na pia kuombea Mkoa wetu wetu na Nchi kwa ujumla ili Mungu azidi kutukirimia neema zake, kwa wale watakao jaribu kuleta fujo napenda kuwaambia kuwa Jicho na Sikio la Serikali hapa Singida liko makini na watashughulikiwa kikamilifu. Alimalizia Mh Dr Nchimbi


  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akizungumza jambo wakati wa mkutano wa kujadili matumizi ya fedha za Mfuko wa Jimbo. Kushoto ni wajumbe wa Kamati ya Mfuko wa Jimbo la Musoma Vijijini.
  Baadhi ya wananchi wa Kata ya Tegeruka, Musoma Vijijini waliohudhuria mkutano wa kujadili matumizi ya fedha za Mfuko wa Jimbo hilo.
  Katibu wa Mfuko wa Jimbo la Musoma Vijijini na Afisa Mipango wa Wilaya ya Musoma, Mukama Rugina (aliyesimama) akizungumza wakati wa mkutano wa kujadili matumizi ya fedha za mfuko huo.
  Diwani wa Kata ya Tegeruka, Benjamin Maheke (aliyesimama) akizungumza wakati wa mkutano wa kujadili matumizi ya fedha za mfuko wa Jimbo la Musoma Vijijini.

  Wajumbe wa Kamati ya Mfuko wa Jimbo la Musoma Vijijini wameagizwa kuhakikisha wanakagua utekelezaji wa miradi ya kilimo ya vikundi vilivyokabidhiwa vifaa kutoka kwenye mfuko huo ili kujiridhisha.

  Agizo hilo limetolewa hivi karibuni na Mbunge wa Jimbo hilo, Profesa Sospeter Muhongo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati husika wakati wa mkutano wa hadhara wa kuainisha matumizi ya fedha za Mfuko wa Jimbo kwa Awamu ya Pili uliofanyika katika kijiji cha Tegeruka, Musoma Vijijini.

  Ilielezwa kwamba Awamu ya kwanza ya fedha zilizotolewa kwa ajili ya Mfuko wa Jimbo hilo ni shilingi milioni 70,820,000 ambazo zilitumika kwa matumizi mbalimbali ikiwemo shilingi milioni 20,000,000 kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Murangi.

  Fedha zingine ni milioni 27,500,000 ambazo zilitumika kwa ajili ya kurekebisha nyumba na madarasa yaliyokuwa yameezuliwa na upepo kwa shule mbili za msingi, milioni 22,500,000 ilitumika kununulia mashine za umwagiliaji, mbegu za mbogamboga na matunda pamoja na dawa za kilimo na shilingi 820,000 zilitengwa kwa ajili ya kuwezesha ufuatiliaji.

  Profesa Muhongo alisema ni jukumu la Kamati husika kuhakikisha fedha imetumika kwa matumizi yaliyokubaliwa na aliagiza vikundi vyenye miradi ya kilimo ambayo haijaanza vinyang’anywe vifaa vilivyokabidhiwa na vipewe vikundi vingine vyenye vyenye nia dhabiti ya kuendeleza kilomo.

  “Tembeleeni hivi vikundi, mkikuta havijaanza kutumia vifaa tulivyowapatia mvinyanga’anye na vifaa hivyo vigawiwe kwenye vikundi vyenye nia ya dhati,” aliagiza Profesa Muhongo.Akizungumzia Awamu ya Pili ya Mfuko wa Jimbo, Profesa Muhongo alisema Mfuko wa Jimbo umepokea kiasi cha shilingi milioni 38,479,000 ambazo alisema Kamati husika kwa kushirikiana na wananchi pamoja na madiwani wamependekeza zitumike kwa ajili ya kuboresha kilimo.

  Alisema shilingi milioni 16,000,000 zitatumika kwa ajili ya kununulia mbegu za kisasa za mihogo za mkombozi kiasi cha vipando 532,000 ambazo zitagawiwa kwenye Kata 21 kwa ajili ya vijiji 68, na shilingi milioni 21,900,000 itatumika kununulia mashine 21 za kukamulia alizeti. 

  Aliongeza kuwa hapo awali alisambaza mbegu za alizeti za majaribio kiasi cha kilo 4000 ambazo alisema zimeonesha mafanikio na hivyo aliongeza mbegu zilizoboreshwa kutoka Arusha kiasi cha kilo 5000 ambazo pia zilisambazwa.

  Alisema ili kujiongezea kipato kutokana na kilimo cha alizeti, wameamua badala ya kuuza mbegu, wakulima hao watauza mafuta na ndiyo sababu ya kutenga kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya mashine hizo ambazo alizielezea kuwa ni za kuzungusha kwa mikono na hazihitaji mafuta wala umeme.

  “Hizi nilitoa fedha yangu na sio katika mfuko wa jimbo; na kukitokea mapungufu nifahamisheni nijazilizie,” alisema.Akizungumzia utaratibu wa mashine hizo, alisema kila Kata itakabidhiwa mashine yake na kwamba zitafungwa kwenye ofisi za kata chini ya usimamizi wa Afisa kilimo.

  0 0


  Bw. Venanti Kagombora wa Bunju Dar es Salaam anasikitika kutangaza kifo cha baba yake mzazi Omulangira Cornel Kagombora, kilichotokea leo katika Hospitali ya Serikali ya Mkoa, mjini Bukoba. 

  Habari ziwafikie watoto wake Verdiana Kagombora na Prosper Kagombora wa TEXAS Marekani, mkwe wa marehemu Bw. Justin Lambert wa Dar es Salaam na Father Mushuga wa Ibalaizibu Bukoba. Mazishi yafanyika Jumapili, tarehe 1 Januari, 2017 nyumbani kwake Katika kijiji cha Bulembo kitongoji cha Katoma Kamachumu, Kagera.

  0 0

   Mkuu wa wilaya ya Songea Pololeti   Mgema akionyesha moja ya sehemu ambayo moto bado unawaka .
   Hiyo ndiyo hali halisi ya ofisi jinsi ilivyoungua kwa ndani
   Nyaraka za serikali ya kijiji cha Mtyangimbole zikiwa zimeteketea kwa moto na kubaki majivu tu.
   Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya madaba Shafii Mpenda wa kwanza kushoto akiwa anafatilia jambo katika mkutano wa wanakijiji ambao ulifanyika baada ya kumaliza kuzima moto
  Mkuu wa wilaya ya Songea Pololeti   Mgemaakizungumza na wakazi wa kijiji cha Mtyangimbole  baada ya zoezi la kuzima moto kumalizika. Kwa undani wa habari hii angalia hiyo video. (Habari na RUVUMA TV)

  0 0


  NA HAMZA TEMBA -WMU.

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani amesema hakuna mamlaka nyingine ya Serikali chini ya ofisi ya waziri mkuu yenye mamlaka ya kutoa tamko au ufafanuzi kuhusiana na Faru John kwa sasa kwakua jambo hilo bado lipo kwenye uchunguzi.

  Amesema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari katika tarafa ya Loliondo, Wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya siku mbili wialayani humo kwa ajili ya kufuatilia changamoto za uhifadhi pamoja na utekelezaji wa maagizo wa Waziri Mkuu aliyoyatoa hivi karibuni akiwa ziarani mkoani Arusha.

  Amesema miongoni mwa maagizo aliyoyatoa Waziri Mkuu katika ziara hiyo ni kuwasilishwa kwa taarifa ya inayoelezea utaratibu uliotumika kumuhamisha Faru John kutoka Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Sasakwa Black Rhino Sanctuary iliyoko kwenye Hifadhi ya Grumeti pamoja na kuwasilishwa kwa pembe zake ambapo baadae aliunda tume ya kuthibitisha ukweli wa taarifa hiyo.
  .
  "Ripoti hii ya uchunguzi ni mali ya Waziri Mkuu atakayeweza kutoa ripoti hii nje kwa ajili ya matumizi  ya kila mmoja wetu ni Waziri Mkuu, kwa maana ya mamlaka, kwa hiyo hakuna mamlaka nyingine yeyote ya Serikali chini ya Waziri Mkuu yenye uhalali wa kutoa tamko au ufafanuzi wa jambo hili, mpaka pale Waziri Mkuu atakapokamilisha kusoma ripoti kwa kina kwa kutumia wataalam wake, kufanya vipimo kama ambavyo tunasikia amevipeleka kwa mkemia mkuu wa Serikali, pamoja na udadavuzi wa ripoti.

  "Kwa kipindi hiki nnapozungumza, zaidi ya kwamba tunasubiri maagizo au maelekezo au muelekeo sasa juu ya jambo hili kutoka ofisi ya Waziri Mkuu, hakuna jambo jingine ambalo Wizara inaweza kufanya wala kusema kuhusiana na suala la Faru John, hatuna mamlaka hiyo", amesema.

  Akizungumzia tukio la hivi karibuni la baadhi ya watumishi wa wizara kuonekana kwenye chombo kimoja cha habari wakitoa ufafanuzi juu ya jambo hilo amesema "Mimi kwa sasa nnachoweza kusema kwa chochote kilichofanyika kama kuna utaratibu umetumika kuwafanya waweze kwenda mbele ya vyombo vya habari, kwenda kutoa taarifa hizo, lakini pia tukijua kabisa kwamba wao sio wasemaji wa wizara na wala kwa level  (hatua) ya jambo lenyewe pale lilipofikia wao hawana mamlaka ya kuweza kutosha kulizungumzia jambo hilo, sasa kwanini limekua hivo jana ni jambo ambalo tunalifanyia kazi, bila shaka walipoitwa pengine hawakuambiwa sawasawa wanaenda kuzungumzia nini",.

  "Kama wizara tutachukua sasa muda wa kuweza kuzungumza nao tujue nini kilitokea lakini kimsingi baada ya hiki nnachokisema hapa sasahivi ieleweke hivo na taifa zima kwa ujumla kuwa hakuna tunachoweza kusema sasa hakuna tunachoweza kufanya sasa mpaka uchunguzi unaofanyika chini ya ofisi ya waziri mkuu ukamilike mpaka waziri mkuu asome aridhike na taarifa yetu na aweze kuina taarifa ile inafaa kwa namna gani na kama kuna maagizo mengine atayatoa baada ya hatua hiyo.

  Wakati huo huo ametoa wito kwa wananchi kuwa na subira juu ya taarifa sahihi za faru John "Unaweza kusikiliza habari kutoka vyanzo vingi tu, lakini ukishapata habari usiifanyie kazi haraka haraka bila ya kujiridhisha juu ya ubora wa taarifa unayoipata, wawe na subira, wananchi waendelee kusubiri, si waliapata taarifa ya faru John kupitia kwa Waziri Mkuu?, busara ya kawaida inasema kwamba wangesubiri kutoka kwa Waziri Mkuu au mtu atakayekasimiwa madaraka na Waziri Mkuu atasema kitu kingine kinachofuatia baada ya pale na si vinginevyo".

  Katika hatua nyingine Naibu Waziri Makani ameunda kamati maalum ya kuushulikia mgogoro wa muda mrefu katika  pori tengefu la Loliondo baina ya wananchi, wawekezaji na hifadhi hiyo. Hatua hiyo imekuja ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya waziri mkuu ya kuwakutanisha wadau katika eneo hilo kumaliza mgogoro huo.

  Kamati hiyo imehusisha taasisi za serikali, asasi za kiraia, viongozi wa dini, wazee wa kimila (Leigwanan), viongozi wa vijiji, wajumbe wa kamati teule za vijiji, wawakilishi wa wanawake na vijana. Ameunda pia kamati ya kuandaa kanuni za kundesha vikao  vya kamati hiyo.

  "Kuna watu humu ndani na hata nje ambao hawataki tumalize migogoro Loliondo, nitoe rai kwao, waache chokochoko. Wananchi muone umuhimu wa jitihada za Serikali kumaliza changamoto hii na kutuunga mkono", alisema Makani.
   Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (kulia) akizungumza katika kikao cha wadau wanaohusika na mgogoro wa pori tengefu la Loliondo alichokiitisha katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, katika tarafa ya Loliondo wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha jana. Kupitia kikao hicho aliunda kamati maalum ya kutatua mgogoro wa muda mrefu wa pori tengefu la Loliondo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Mfaume Taka.
   Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (kulia) akizungumza katika kikao hicho.
  Baadhi ya wadau wanaohusika na mgogoro wa pori tengefu la Loliondo wakiwa kwenye mkutano huo.

  0 0

   Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea cheti maalum cha kutambua mchango wake katika kukijenga na kukiimarisha Chama cha Mapinduzi wilayani Ruangwa kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Lindi, Ali Mtopa katika mkutano wa hadahara aliouhutubia mjini Ruangwa Desemba 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha Cheti Maalum  cha kutambua mchango wake katika kukijenga na kukiimarisha Chama cha Mapinduzi wilayani Ruangwa alichokabidhiwa na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Lindi, Ali Topa   (kulia) katika mkutano wa hadhara aliouutubia mjini Ruangwa Desemba 30, 2016. Kushoto ni Katibu wa CCM wa wilaya ya Ruangwam Issa Njinjo.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya Shilingi milioni sita kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Pacco GEMS Limited, Bw. Mahendra Bardiya katika harambee  ya kuchangia ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari wilayani Ruangwa ambapo jumla ya shilingi milioni 138.26 zilichangwa. Harambee hiyo ilifanyika sambamba na  mkutano wa hadhara uliohutubia wa Waziri Mkuu mjini Ruangwa, Desemba 30, 2016.
  Wananchi wa Ruangwa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara mjini Ruangwa, Desemba 30, 2016.

  0 0


   Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dk.Valentino Mokiwa (katikati), akiwaongoza waumini wa kanisa hilo Archidikonari ya Kinondoni kufanya usafi katika viwanja vya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala Dar es Salaam leo asubuhi wakati kanisa hilo lilipotoa msaada wa vitanda na magodoro katika hospitali hiyo vyote vikiwa na thamani ya sh.milioni 12.
   Waumini wa kanisa hilo wakiendelea na kufanya usafi.
   Takataka zikipelekwa eneo maalumu.
   Takataka zikipelekwa kutupwa.
   Waumini wa kanisa hilo wakipiga picha mbalimbali za tukio hilo.
  Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dk.Valentino Mokiwa (kulia), akipanda mti nje ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala, wakati alipowaongoza waumini wa kanisa hilo  kutoa msaada wa magodoro na vitanda vya wagonjwa pamoja na kufanya usafi wa mazingira Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto anayemsaidia kupanda mti ni Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dk.Daniel Nkungu na wengine ni waumini wa kanisa hilo.  
   Kiongozi wa  kanisa hilo wilaya ya Kinondoni Achidikin Con Mathew Maigwa (kulia), akipanda mti.
  Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dk. Daniel Nkungu (kulia), akipanda mti.
   Ofisa  Afya wa Hospitali hiyo, Amina Pole (kushoto), 
  akipanda mti.
   Waumini wa kanisa hilo na viongozi wao wakiwa kwenye 
  tukio hilo.
   Askofu Dk. Valentino Mokiwa akimkabidhi moja ya kitanda kati ya 15,  Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Daniel Nkungu.
  Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Daniel Nkungu akitoa neno la shukurani kwa niaba ya Serikali baada ya kupokea msaada huo.

  Na Dotto Mwaibale

  ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Angilikana Tanzania, Dk Valentino Mokiwa amesema migogoro ya kisiasa inayoibuka hivi sasa inaweza kuhatarisha hali ya amani nchini.

  Dk. Mokiwa ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam leo wakati akiwaongoza waumini wa  kanisa hilo Archidikonari ya Kinondoni kutoa misaada ya vifaa tiba na kufanya usafi wa mazingira katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala.

  "Migogoro ya kisiasa ambayo imeanza kuzuka hivi sasa inaweza kuhatarisha amani ya nchi ni vizuri viongozi wanaovutana wakutana na kuweka mambo sawa" alisema Mokiwa.

  Alisema migogoro ya kisiasa inayoendelea inaweza kusababisha kutoweka kwa amani hivyo ni jukumu la viongozi husika kuliangalia jambo hilo kwa karibu na kulitafutia ufumbuzi.

  Alisema nchi yetu inahitaji amani na utulivu na kuondokana na matukio ya kuogopesha akitolea mfano miili ya watu saba iliyokutwa ndani ya viroba vilivyotupwa mto Ruvu Bagamoyo mkoani Pwani.

  Alisema matukio kama hayo yanaweza kuwafanya wananchi kukimbia nchi yao kwa hofu hivyo inatakiwa kila mmoja wetu kuwa na hofu ya mungu.

  Akizungumzia msaada uliotolewa na kanisa hilo katika hospitali hiyo  ambao ni  vitanda 15,magodoro 20, mashuka 40 na viatu vya tahadhri jozi 30 vyenye thamani ya Sh12 milioni alisema kanisa hilo kwa muda mrefu limekuwa likifanya maombi ya kuwaombea viongozi wa nchi na kutoa misaada ya kijamii hususan katika sekta ya afya, elimu na maeneo mengine.

  Mokiwa alisema wananchi wanapokuwa katika afya bora ndipo wanapoweza kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo hivyo kuinua uchumi wao na taifa kwa ujumla.

  Mkuu wa  kanisa hilo wilaya ya Kinondoni Achidikin Con Mathew Maigwa alitoa mwito kwa wadau wa maendeleo kote nchini kuwa na moyo wa kusaidia watu wenye uhitaji kama wanavyotoa michango ya harusi na sherehe nyingine.

  Alisema ni jukumu la kima mmoja wetu wa kusaidia jamii na si kuiachia serikali pekee na ndio maana kanisa hilo limekuwa likifanya hivyo kama neno la mungu linavyoelekeza kuwa tupendane kwani unapokwenda kumfariji mgonjwa inasaidia kumpa hali ya unafuu.


  Akizungumza kwa niaba ya serikali na Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dk. Daniel Nkungu alilishukuru kanisa hilo kwa msaada huo na kusema inazidisha ari ya kazi kwa wafanyakazi na kuwafariji wagonjwa ikiwa na kuwafanya wapate nafuu na kupona  haraka.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifanya mazoezi ya viungo kwenye viwanja vya makazi yake jijini Dar es salaam ikiwa sehemu ya kuendeleza kampeni yaKitaifa ya kudhibiti Magonjwa yasiyo ya kuambukiza  aliyoizindua tarehe 17 Desemba, 2016 katika viwanja vya Leaders Club.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Ally Hapi na Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa Oyster bay Ndugu Zefrin Lubuva ikiwa sehemu ya kuendeleza kampeni yaKitaifa ya kudhibiti Magonjwa yasiyo ya kuambukiza  aliyoizindua tarehe 17 Desemba, 2016 katika viwanja vya Leaders Club.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Ally Hapi na Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa Oyster bay Ndugu Zefrin Lubuva pamoja na wasaidizi wake ikiwa sehemu ya kuendeleza kampeni yaKitaifa ya kudhibiti Magonjwa yasiyo ya kuambukiza  aliyoizindua tarehe 17 Desemba, 2016 katika viwanja vya Leaders Club.

  0 0

  Na Frank Mvungi (MAELEZO) 

  Serikali imesema hakuna uhaba wa dawa ya usingizi katika Hospitali ya Rufaa Bombo Mkoani Tanga kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini kuwa hali hiyo inachochea kuzorota kwa huduma za upasuaji.

  Akifafanua suala hilo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt. Asha Mahita amesema kuwa taarifa kuwa huduma za upasuaji katika hosipitali hiyo zimesimama si za kweli na ukweli ni kwamba huduma zinaendelea kama kawaida. 
   
  “Huduma za upasuaji katika Hosipitali yetu zinaendelea kama kawaida na hakuna tatizo kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari” Alisisitiza Dkt. Mahita.

  Akifafanua zaidi Dkt. Mahita alisema kuna mgonjwa mmoja tu ambaye upasuaji wake ulisogezwa mbele kutokana na sababu za kitabibu na si kwa sababu ya kukosekana kwa dawa ya usingizi.
   
  Aliongeza kuwa sababu zinazoweza kusababisha kuahirishwa kwa upasuaji wa mgonjwa aliye kwenye ratiba ni pamoja na uwepo wa wagonjwa wengi wa dharura hali inayoweza kuchangia nguvu kubwa kuelekezwa katika kuhudumia wagonjwa hao wakiwemo wahanga wa ajali.

  Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imekuwa ikichukua hatua mbalimbali katika kuwahudumia wananchi na kuhakikisha kuna dawa za kutosha na vifaa tiba katika hospitali na vituo vya kutolea huduma hapa nchini.

  0 0

  Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Maruzuku katika Kata ya Mnyamani Buguruni Manispaa ya Ilala, kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Jabiri Sanze (kulia), akimkabidhi sare za shule mtoto, Hamad Ali Dar es Salaamleo, ambaye ataanza darasa la kwanza mwezi huu. Serikali ya mtaa huo imetoa sare za shule, daftari na penseli kwa  watoto 200 watakaoanza darasa la kwanza mwaka huu wa 2017. Katikati ni mama wa mtoto huyo, Farida Rashid.
  Mtoto Issa Athumani akipokea msaada huo. Katikati mama yake Halima Issa.
  Mtoto Asnat Mashaka akipokea msaada huo. Nyuma yake ni mama yake, Arat Hamisi
  Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mnyamani Jafari Mrisho (kushoto), akizungumza kwenye tukio hilo.
  Katibu Kata wa Kata ya Mnyamani (CUF), Omari Simba (kulia), akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo.
  Wazazi na walezi wakiwa na watoto wao wakisubiri kupokea msaada huo.
  Vifaa hivyo vikiandaliwa kabla ya kukabidhiwa watoto.
  wazazi na walezi wakiwa kwenye hafla hiyo.
  wazazi na walezi wakiwa kwenye hafla hiyo.
  Watoto na wazazi wao wakisubiri msaada huo.
  Na Dotto Mwaibale

  SERIKALI ya Mtaa wa Maruzuku katika Kata ya Mnyamani Buguruni Manispaa ya Ilala kupitia Chama cha Wananchi (CUF), imetoa sare za shule kwa watoto 200 wanakaoanza darasa la kwanza mwezi Januari ili kuleta msukumo wa masomo katika mtaa huo.

  Akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada huo Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa mtaa huo, Jabiri Sanze alisema wanaziunga mkono jitihada za Rais Dk.John Magufuli za kuhakikisha kila mwanafunzi anapata elimu bure na katika mazingira bora.

  "Tumeamua kutoa msaada huu mdogo kwa watoto 200 waliopo katika mtaa wetu ili kutoa hamasa kwa wazazi na walezi kwani kipindi hiki cha mwezi Januari kinachangamoto kubwa na mahitaji mengi ya shule kwa wanafunzi" alisema Sanze.

  Sanze alitaja msaada huo kuwa ni mashati ya shule, madaftari na penseli za kuandikia ambapo aliwaomba wazazi wasaidie eneo la sketi, kaputura, viatu na mabegi.

  Alisema watoto walionufaika na msaada huo ni wavulana 86 na wasichana 114 wote kutoka katika mtaa wa Maruzuku.

  Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mnyamani Jafari Mrisho aliupengeza uongozi wa mtaa huo kwa mpango huo wa kuwasaidia watoto hao wanaotarajia kuanza darasa la kwanza na akawaomba wadau wengine wa maendeleo kujitokeza kusaidia ili kuwafikia watoto wote wa mitaa mitatu ya kata hiyo ambayo ni Mji Mpya, Mbarouk na Mnyamani.

  Mjumbe wa mtaa huo Haroub Mussa aliwataka wazazi wa watoto waliopata msaada huo kutunza sare hizo na kuwa serikali ya mtaa itaendelea kushirikiana na wananchi na kuhakikisha watoto wote wanaopaswa kuanza darasa la kwanza wanakwenda shuleni.

older | 1 | .... | 1085 | 1086 | (Page 1087) | 1088 | 1089 | .... | 1897 | newer