Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1084 | 1085 | (Page 1086) | 1087 | 1088 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (Kushoto) akimpatia Zawadi ya Ramani ya Tanzania Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake, Dkt. Tonia Kandiero (Kulia).
  Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake, Dkt. Tonia Kandiero (Kulia aliyesimama) akizungumza wakati alipotembelea TADB. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga.
  Afisa anayeshughulikia masuala ya kijinsia katika Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania, Bibi Beatrice Mrema akitoa neno la Shukrani kwa Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake, Dkt. Tonia Kandiero.
  Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake, Dkt. Tonia Kandiero (Wapili kulia mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti na maafisa waandamizi wa TADB.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (Katikati) akimkaribisha Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake, Dkt. Tonia Kandiero (Kulia). Kushoto ni Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji Fedha wa TADB, Bw. Albert Ngusaru.
  Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake, Dkt. Tonia Kandiero (Kulia) akisaini Kitabu cha Wageni wakati alipotembelea TADB. Anayemtazama ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga.
  Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji Fedha wa TADB, Bw. Albert Ngusaru (Aliyesimama) akizungumza wakati Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake, Dkt. Tonia Kandiero alipotembelea TADB.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (Aliyesimama) akizungumza wakati Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake, Dkt. Tonia Kandiero alipotembelea TADB.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (Wapili kulia aliyesimama) akihimiza jambo wakati Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake, Dkt. Tonia Kandiero alipotembelea TADB.
   

  0 0

  Leo Disemba 29, 2016 ni siku ya furaha kwa ndugu, jamaa na marafiki wa kijana Jackson John Binagi, wa Kenyamanyori Tarime mkoani Mara (wa tatu kushoto),aliyefunga ndoa na Bi.Monica Syaga wa Mogabiri Tarime, Mara.
  Maharusi na wapambe wao, pamoja na ndugu, jamaa na marafiki
  Maharusi na wapambe wao
  Maharusi katika ubora wao
  Wazazi wa bibi harusi wakiongozwa na baba, wakimpa baraka bibi harusi
  Ni furaha kwa ndugu, jamaa na marafiki kucheza ngoma ya asili ya kikurya (Ritungu) kwenye harusi hiyo.

  0 0

  Taasisi ya MO Dewji Foundation imeweza kuwakumbuka watoto wanaopatiwa matibabu ya magonjwa ya kansa katika kituo cha Tumaini la Maisha kilichopo ndani ya Hospitali ya Taifa Muhimbili, Jijini Dar es Salaam. Katika kusheherekea sikukuu za mwisho wa mwaka ikiwemo kuingia mwaka mpya wa 2017, MO Dewji Foundation imeweza kutembelea watoto wa kituo hicho cha Tumaini la Maisha na kutoa zawadi kwa watoto hao ili kuwasaidia katika kipindi wawapo kituoni hapo wakiendelea na kliniki ya matibabu yao.
  Kwa zaidi ya miaka mitatu MO Dewji Foundation imekuwa ikitoa ufadhili na mahitaji mbalimbali ikiwemo chakula kwa watoto hao, mafunzo kwa watoto hao wawapo kituoni hapo, gharama za usafiri kwa watoto kuja na kurejea kutoka mikoa mbalimbali kwa ajili ya matibabu yao katika wodi yao iliyopo Hospitalini hapo Muhimbili. Katika tukio hilo, Mo Dewji Foundation waliweza kutoa vitu mbalimbali kama zawadi kwa ajili ya kusaidia mahitaji ya kituo hicho. 
  Miongoni mwa vitu hivyo ni pamoja na unga wa ngano, sabuni za kunawia mikono, sabuni za kuogea, doti za khanga, mafuta ya kupikia na vitu vingine vingi. Kwa upande wake, Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez amewatakia kila lakheri watoto na wazazi wa kituo hicho katika kuingia mwaka mpya ambapo pia aliwahakikishia wafanyakazi wa kituo hicho kuwa taasisi yao itaendelea kusaidia kituo hicho.
  Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez akimkabidhi Mwalimu Leonard ambaye ni mwalimu anayetoa elimu kwa watoto wenye kansa wanaopatikana kituoni hapo.
  Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez akikabidhi zawadi hiyo kwa mmoja wa wafanyakazi wa kituo hicho cha TLM
  Mkuu wa Taasisi ya MO Dewji, Barbara Gonzalez akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kituo hicho, pamoja na baadhi ya watoto hao wa TLM.
  Mratibu wa Miradi wa MO DEWJI Foundation, Catherine Decker akiwa pamoja na watoto wa TLM, wakati wa tukio hilo la kuwafariji watoto pamoja na kutoa zawadi.
  Mwalimu Leonard wa TLM akiwa na mmoja wa watoto wa kituo hicho wakati wa tukio hilo la kutoa zawadi.
  Jengo la TLM

  0 0


  Mbunge wa jimbo la Kilolo Venance Mwamoto wa tatu kulia akiongozana na kamati yake ya mfuko wa jimbo kukagua miradi ya kimaendeleo na kuchangia miradi hiyo pichani ni jengo la maabara ambalo limekwama kuendelea katika shule ya Sekodari Ipeta

  Mbunge Mwamoto akitazama shughuli za ujenzi wa vyoo katika shule ya Msingi Iramba

  Mbunge wa kilolo Venance Mwamoto akikagua ujenzi wa choo cha wanafunzi shule ya Msingi Iramba jana wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa miradi mbali mbali jimboni humo  Mwamoto akikagua ujenzi wa kituo cha Afya Ukumbi

  Shimo la choo shule ya Sekondari Ipeta

  Vyumba vya madarasa shule ya msingi Italula

  Vyoo vya zamani vya wanafunzi shule ya Msingi Kidabaga

  Ujenzi wa vyoo vya kisasa shule ya Msingi Kidabaga ukiendelea  Majengo ya shule ya Msingi Kidabaga

  Nyumba ya mwalimu Kidabaga shule ya Msingi  Maabara ya shule ya sekondari Ipeta ikiwa imesimama ujenzi wake


  Choo cha mwalimu mkuu shule ya Msingi Mdeke Kilolo


  Na MatukiodaimaBlog


  MBUNGE wa jimbo la Kilolo mkoani Iringa Venance Mwamoto amechangia zaidi ya Tsh milioni 20 kwa ajili ya kukamilisha miradi mbaali mbali ya kimaendeleo ikiwemo ya ujenzi wa vyoo vya wanafunzi ,madarasa ,nyumba za walimu na Zahanati katika jimboni hilo huku akiwataka viongozi wa serikali za vijiji na kata kuhakikisha wanakamilisha ujenzi huo kwa wakati na ubora .


  Pamoja na kuwataka viongozi hao kusimamia ujenzi huo amesema atachukua hatua kali kwa kiongozi yeyote wa serikali ya kijiji ama kata ambaye atatafuna fedha hizo za ukamilishaji wa miradi hiyo ya kimaendeleo jimboni humo.


  Mbunge huyo aliyasema hayo jana wakati alipofanya ziara ukaguzi wa miradi 9 inayoendelea kwa nguvu za wananchi na Halmashauri ya wilaya ya Kilolo na kueleza kuvutiwa na miradi hiyo japo kunahitajika msukumo wa haraka katika umaliziaji wa miradi hiyo hasa ile ya vyoo vya wanafunzi ili kuwawezesha wanafunzi hao pindi shule zinapofunguliwa kuwa na vyoo bora.


  Alisema kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya kwa mvua kuchelewa kunyesha katika maeneo mbali mbali ya wilaya ya Kilolo tofauti na miaka mingine ameona ni vema kuwapunguzia makali ya michango wananchi wake na badala yake sehemu ya michango ambayo walipaswa kuchangia ili kukamilisha miradi hiyo kuibeba yeye kupitia mfuko wa jimbo kwa kuchangia fedha hizo.


  Kwani alisema ni rahisi kwa wananchi kuchangia nguvu zao kwa kushirikia katika ujenzi huo wa miradi hiyo kuliko kushiriki kutoa fedha jambo ambalo kwa wananchi hao ni sawa na kuwatesa kutokana na wengi wao waliuwa wakiishi kwa kutegemea kilimo na hadi sasa matumaini ya kupata fedha kwa njia ya kilimo yametoweka baada ya mvua kushindwa kunyesha .


  "Ninawaombeni sana wananchi wangu kwa sasa ninyi mshiriki zaidi katika maendeleo kwa kuchangia nguvu zenu na mimi niwaunge mkono kwa kuchangia fedha ili kuifanya miradi hii ikamilike kwa wakati"


  Hata hivyo alisema kuna baadhi ya maeneo wananchi wanachangamoto kubwa ya barabara hasa zile zilizopo chini ya Halmashauri kuwa barabara hizo zitafanyiwa matengenezo na ile ya Tanrod kutoka makao makuu ya wilaya ya Kilolo hadi Ndiwili mpakani mwa jimbo la Kalenga inaanza kujengwa kwa kiwango cha lami mapema mwakani na kuwa kuanzia January ujenzi huo utaanza kwani barabara hiyo ipo katika ilani ya uchaguzi ya CCM.


  Mbunge Mwamoto alisema kuwa kwa suala la ujenzi wa Zahanati na vituo vya afya wananchi wamejitahidi kwa maeneo mbali mbali aliyopita kukagua ujenzi umefikia hatua nzuri na kutolea mfano ujenzi wa Zahanati ya Masege ambao jengo lake bado kuezekwa na nyumba ya mganga ipo katika hatua ya kuanza kupandisha kuta kuwa kukamilika kwa Zanahati hiyo kutawawezesha wananchi hao ambao walikuwa wakilazimika kufuata matibabu Kibengu na Usokami wilaya ya Mufindi wataweza kutibiwa katika Zanahati hiyo.


  Alisema katika ziara yake hiyo aliyoambatana na wajumbe wa mfuko wa jimbo kupitia fedha za mfuko wa jimbo Kijiji cha Mdeke ambako kuna ujenzi wa vyoo vya wanafunzi amechangia Tsh milioni 1 na kwenye ujenzi wa nyumba ya mwalimu amechangia Tsh milioni 2 , sekondari ya Ipeta kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya wanafunzi amechangia Tsh milioni 2, shule ya Msingi Kidabaga amechangia Tsh milioni 3 kwa ajili ya vyoo na nyumba ya mwalimu ,Wangama amechangia Tsh milioni 1 kwa ajili ya ukarabati wa madarasa ,Kitongoji cha Ifiga amechangia Tsh milioni 1 kwa ajili ya kuanzisha mkondo B wakati ujenzi wa Zahanati na nyumba ya Mganga Masege amechangia Tsh milioni 5

  Mbunge Mwamoto alisema ujenzi wa kituo cha Afya Ukumbi amechangia Tsh milioni 2 na katika ujenzi huo nguvu za wananchi ni Tsh milioni 35 na Halmashauri ni Tsh milioni 10 huku ujenzi wa vyumba vyamadarasa shule ya Msingi Italula amechangia Tsh milioni 2 hata hivyo alisema atafanya ziara ya ukaguzi na uchangiaji wa miradi ya maendeleo katika jimbo zima ili kupitia mfuko huo wa jimbo miradi yote iweze kupata mgao huo.

  0 0

  Dereva boda boda Kasian Haule ambaye alimpakia Denis Komba na nyoka wake.
  ...................................
  Tukio lililo zua taharuki kwa wakazi wa songea mkoani Ruvuma na kupewa nafasi kubwa katika vyombo vya habari vya Tanzania na nje ya Tanzania pamoja na mitandao ya kijamii, huku likiacha gumzo midomoni mwa watu, kuhusiana na kifo cha DENIS KOMBA kufariki dunia baada ya nyoka wake aliyekuwa anasadikiwa kummiliki, kuuawa na wananchi DESEMBA 26 MWAKA HUU, majira ya saa 4 na nusu usiku , katika maeneo ya hospital ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma. Ruvuma TV imezungumza na KASIANI HAULE, ambaye ndiye dereva boda boda aliyekuwa kakodiwa na marehe DENISI KOMBA Bonyeza hiyo Video upate ukweli wa tukio.

  0 0


  Mbunge wa Jimbo la Tanga(CUF) Mussa Mbaruku amewatakia heri ya sikukuu ya mwaka mpya wakazi wa Jimbo lake na kuwataka wajitume zaidi ili kuweza kupata mafanikio.

  Akitoa salamu hizo kwenye ofisi yake wakati akizungumza na waandishi wa habari leo,Mbunge Mussa aliwataka wananchi hao kutambua kuwa wanashirki kwenye shughuli za kimaendeleo ili kuweza kujikwamua kiuchumi.

  Alisema licha ya kushiriki huo lakini pia wakulima watambue katika kipindi hiki wanapaswa kutayarisha mashamba yao ili kuweza kulima kilimo cha kisasa chenye tija.

  Aidha pia aliwataka kuhakikisha wanawajibika kusafisha maeneo yao ili yaweze kuwa na muonekana mzuri ili waweze kuepukana na magonjwa ya milipuko yanayoweza kutokana na kuwepo kwa hali hiyo.“Lakini pia ni niwatake halmashauri ya Jiji la Tanga kuhakikisha wanasafisha maeneo yao kwa kuondoa takataka “Alisema Mbunge Mussa.

  Sanjari na hilo Mbunge huyo pia aliwataka wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kwenye Jimbo lake kuhakikisha wanaongeza bidhii kwenye masomo ili waweze kufanya vizuri kwenye mitihani yao

  “Niwaambie wanafunzi wakati wanapokuwa shuleni acheni masuala ya michezo badala yake hakiksheni mnazingatia elimu kwani ndio mkombozi mkubwa kwenye maisha yenu ya sasa na baadae “Alisema.

  habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

  0 0

  Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa

  *Asema wanaotaka fedha wataipata shambani

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa Ruangwa na mkoa mzima wa Lindi wachangamkie fursa ya kulima mihogo na alizeti kwa sababu mazao hayo yana uhakika wa soko.

  Alitoa wito huo wakati akizungumza na wananchi wa vijiji mbalimbali vya wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi ambako anapita kuwasalimia wananchi wa jimbo lake na kuhimiza kazi za maendeleo. Waziri Mkuu yuko Ruangwa kwa siku nne kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka.

  “Nimekuja na fedha, wangapi wanataka kupata fedha?” alihoji Waziri Mkuu katika mikutano yake na kuitikiwa “Sisi” na umati wa watu walionyoosha mikono juu kuonesha kuwa wako tayari kupokea fedha hizo. Mikutano hiyo ilifanyika kwenye vijiji vya Namilema, Mbuyuni, Nandandara, Namkonjera, Muhuru, Chikundi, Chibula na Matumbu.

  “Mnataka fedha siyo? Fedha iko shambani! Nimewaletea fursa ya mwekezaji anayetaka kununua mihogo yote katika mkoa huu,” alisema Waziri Mkuu na kusababisha kicheko kwa watu waliokuwa wakinyoosha mikono yao.

  “Limeni mtu mmoja mmoja au jiungeni kwenye vikundi ili mpate ekari tatu hadi nne kwa sababu mna uhakika wa soko. Mwekezaji huyu anataka kununua mihogo yote na ya wilaya hii peke yake haitoshi kiasi ambacho anataka. Kwa hiyo tumekubaliana na wabunge wenzangu kwamba kiwanda hiki kitajengwa Nanjilinji ambako ni katikati ya mkoa ili iwe rahisi kusomba na kupeleka mazao hayo,” alisema.

  Waziri Mkuu alisema eneo la Nanjilinji lililoko wilayani Kilwa, linafikiwa kwa urahisi na wakazi wote kutoka Kilwa, Nachingwea, Ruangwa, Lindi Vijijini na Liwale.

  Akifafanua zaidi, alisema mwekezaji aliyepatikana (bado ni mapema kumtaja) yuko tayari kufuata mazao waliko wakulima na atakuwa akiwalipa hukohuko. “Yeye anachotaka ni mihogo ya kutosha, ndiyo maana nawasisitizia muanze kulima zao hili kwa wingi cha msingi mfuate kanuni bora za kilimo,” aliongeza.

  Wakati huohuo, Waziri Mkuu amewataka wakazi hao walime zao la alizeti kwa wingi kwa sababu amekwishapatikana mwekezaji wa kununua zao hilo na kwa bei nzuri.

  “Nilipokwenda Singida nilikutana na mmiliki mmoja wa kiwanda cha kusindika mafuta ya alizeti akasema anahitaji kununua zao hilo kwa wingi kwa sababu inayozalishwa kule haitoshi. Ameshakuja hapa na kuangalia ardhi ya hapa amesema inafaa kwa zao hilo,” alisema.

  “Yeye atawaletea mbegu na kila ekari moja inahitaji kilo tano. Ukivuna kila ekari unapata magunia 20 na kila gunia lina uwezo wa kutoa lita 20. Bei ya dumu mojala lita 20 ni sh. 60,000 kwa hiyo katika ekari yako moja una uhakika wa kupata sh. milioni 1.2. Hata ukitoa gharama ya kulima na palizi, bado huwezi kukosa walau sh. milioni moja kwa kila ekari.”

  Alimwagiza Mkuu wa Idara ya Kilimo (Umwagiliaji na Ushirika) wa wilaya hiyo, Bi. Violeth Byanjweli afanye kazi ya kuratibu ni wakazi wangapi wana mashamba ya alizeti na wangapi wako tayari kuanzisha kilimo hicho ili mbegu zitakapoletwa iwe ni rahisi kuwasambazia huko waliko.

  “Hiki kilimo ni cha miezi mitatu tu na palizi yake ni mara moja tu. Kwa hiyo mvua za Januari zikianza, changamkieni hiyo fursa na baada ya miezi mitatu kila mtu atakuwa na hela yake badala ya kusubiria korosho ambazo mnavuna mara moja kwa mwaka,” alisisitiza.

                              
  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  ALHAMISI, DESEMBA 29, 2016.

  0 0


  Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora (kulia) akimsikiliza Diwani wa Kata ya Buguruni Mhe. Adam Fugame (Kushoto) wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua ujenzi wa mfereji wa maji taka katika eneo la Ilala Bungoni, Jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw. Palela Msongela (kushoto) akiongea na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora mara baada ya kukagua ujenzi unaoendelea katika mfereji wa kupitisha maji taka eneo la Ilala Bungoni.
  Gervas wa Kampuni ya Dezo Civil Contractors Co. Ltd akifanunua jambo kwa Prof Kamuzora, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, katika eneo la Temeke ambapo Kampuni hiyo imepewa kazi ya kusafisha na kujenga mfumo wa maji taka. Katikati ni Bw. Motongori Chacha, Afisa Mazingira Manispaa ya Temeke.
  Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora (kushoto) akimsikiliza Bi. Ukende Mkumbo kutoka Taasisi ya Mwalimu Nyerere Kigamboni akifafanua hatua za ujenzi wa ukuta katika eneo lao. Katikati ni mwakilishi kutoka Kampuni ya Dezo Civil Contractors Co. Lt
  Sehemu ya Ukuta wa Obama/Ocean Road ukarabati ukiendelea


  Na Lulu Mussa

  Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora ameuagiza ungozi wa Dezo Civil Constractors Co. Ltd kuhakikisha ujenzi wa Miundombinu ya maji taka katika Manispaa za Ilala na Temeke unakamilika kwa muda uliopangwa na kwa ubora wa hali ya juu kwa kuzingatia makubaliano yaliyopo katika mkataba.

  Akikagua ujenzi unaoendelea wa miundombinu hiyo, katika Wilaya ya Ilala eneo la Bungoni, Prof. Kamuzora amemtaka Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw. Palela Msongera kuhakikisha changamoto zinazojitokeza katika ujenzi huo zinatatuliwa mara moja ikiwa ni pamoja na utupaji wa taka maji na taka ngumu katika mfereji huo unaojengwa.

  Awali Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw. Palela Msongela alimueleza Katibu Mkuu kuhusu changamoto zinazohusu mazingira hususan uhaba wa miundombinu ya mifumo ya maji taka na ujenzi wa makazi holela unaosababisha udhibiti hafifu wa taka.

  Aidha, Prof. Kamuzora amewataka watendaji wa Manispaa ya Ilala kuwaelimisha wananchi juu ya athari zinazoweza kujitokeza kwa kutiririsha maji machafu kuwa ni pamoja na milipuko ya magonjwa hususan kipindupindu na kuhatarisha afya za wakazi hao.

  Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Buguruni Bw. Adam Fugame amemhakikishia Prof Kamuzora kuwa ataongea na wananchi katika Kata yake na kusisitiza matumizi sahihi ya sheria ndogondogo za mitaa walizojiwekea ikiwa ni pamoja na kuwatoza faini wananchi wanaokiuka taratibu hizo.

  “Nikuhakikishie, kwa kupitia mikutano na vikao na wananchi katika Kata yangu, tutazidi kusisitiza juu ya jambo hili na kuweka sheria kali zaidi kwa watakao kaidi”. Alisisitiza Mhe. Diwani Fugame

  Ujenzi huo wa Ukuta wa (Obama/Ocean Road na Kigamboni) na Miundombinu ya maji taka katika Manispaa za Ilala na Temeke unatekelezwa chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais chini ya Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi. Mradi huu unafadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira (UNEP). Kampuni ya Dezo Civil Contractors ndio inafanya ujenzi huu na unatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni na kazi zinatarajiwa kukamilika mwezi Julai 2017.


  (Picha na Habari na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Ofisi ya Makamu wa Rais.)

  0 0


  0 0

  Na Rhoda Ezekiel- Kigoma,

  KAMATI ya usalama na maadili na kamati ya siasa ya Wilaya ya Kasulu imetoa adhabu kwa Mbunge wa Viti maalumu wa Mkoa wa kigoma,Josephin Ngezabuke na madiwani sita wa Halmashauri ya mji wa Kasulu kwa tuhuma za kuchochea mgogoro wa madiwani kumpinga Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu kwamba aondolewe hafai.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari jana katibu muenezi wa Wilaya ya Kasulu Masoud Kitowe alisema kumekuwa na mgogoro Mkubwa uliodumu kwa miezi mitano wa Baadhi ya madiwani wa Act na CCM waliomuandikia barua Mkurugenzi ya kudai Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Kasulu aondolewe hafai na Chama Cha mapinduzi hakikupatiwa barua hiyo ambayo ingeweza kuwasaidia kujua chanzo cha tatizo nini.

  Alisema katika mgogoro huo madiwani wa CCm walio shiriki ni watano na kati ya hao mmoja ambaye ni Seleman diwani wa kata ya Kumnyika amepewa adhabu ya kalipio ambayo ataitumikia kwa miezi 18 kwa kosa na kushiriki kuandika barua ya kumkataa mwenyekiti wa Halmashauri hiyo wakati jambo hilo bado halijajadiliwa katika Kikao cha Chama kwamujibu sisi kama chama tulipo pata taarifa kutoka kwa Mkurugenzi tuliwaita madiwani walio husika na kupewa onyo.

  Aidha kitowe alisema madiwani wanne waliojiorodhesha kwenye barua ya kushiriki kumpinga Mwenyekiti huyo kamati ya siasa pia imetoa adhabu ambayo kwa Mujibu wa Sheria za Chama cha mapinduzi hairuhusiwi kuitangaza hazarani nao watatumikia adhabu hiyo kwa miezi 12.

  Alisema Madiwani hao walipo hojiwa walikili mgogoro huo una chochewa na baadhi ya watu ambao ni Diwani wa Kata ya Murusi Steward Zinduse ambae alikuwa akigombea nafasi ya Mwenyekiyi wa halmashauri akashindwa pamoja na Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Kigoma Josephini Ngezabuke nao pia wamepewa adhabu ambayo hairuhusiwi kitangazwa kwa mujibu wa sheria na barua walishapewa zinazo elezea adhabu zao.

  Hata hivyo Kitowe alitaja sababu zinazo pelekea Mbunge huyo kumkataa Mwenyekiti wa halmashuri ni kwamba aliwahi kumuomba meya wa kasulu ashiriki vikao vya halmashauri ya Mji wa Kasulu baada ya kukataliwa kwakuwa ni mjumbe wa Baraza la madiwani kakonko alijenga chuki na Mwenyekiti huyo ,jambo la pili alimuomba mea amuite Everina diwani wa viti maalumu kwa madai avuliwe madaraka ya udiwani viti maalumu kutokana na migogoro ya kifamilia kati yake na diwani huyo wa viti maalum.

  "Kwa mbunge wetu huyu migogoro ni kawaida yake ukiona kasulu kuna migogoro ujue kuna watu wanaochochea, ikumbukweMwaka 2010 kamati ya Siasa ya Mkoa ilimpa azabu ya kalipio mbunge huyo kutokana na migogoro kwakuwa yeye anadai anawatu juu watatengua adhabu hiyo ndio maana anaendelea na migogoro hiyo inayo pelekea Halmashauri kushindwa kufanya Shughuri za maendeleo suala ambalo hatulifurahii sisi kama Chama.

  Alisema Madiwana hao watano baada ya kupewa adhabu waliachana na mgogoro huo lakini mpaka sasa Mbunge huyo pamoja na Diwani wa Kata ya Murusi alie kosa nafasi hiyo bado wanaendeleza Mgogoro huo suala ambalo halina masilahi katika chama zaidi ya kudhohofisha halmashauri yetu ya Mji wa Kasulu.

  Kwa upande wake Mbunge wa Viti maalumu Josephin Ngeza buke alisema hawezi kwenda kwenye halmashauri ya kasulu kuingia kwenye kikao na kufanya vurugu kwakuwa sheria ninazifahamu ninauwezwa kufanya vurugu hata nikiwa nje siwezi kupiga kura sehemu mbili yeye ni Mjumbe wa Halmashauri ya kakonko anacho hitaji ni yeye kupewa heshima kama Mbunge wa Mkoa anapo fika katika Halmashauri ya Wilaya ya kasulu nikeshimike kama Mbunge.

  " mimi sio kwamba simuhitaji Mweenyekiti sina shida na mwenyekiti wala kurudi kwenye Baraza la mji wa kasulu mimi nitabaki Kakonko lakini ninacho hitaji niheshima mimi kama mwenyekiti wa UWT na Mbunge wa Mkoa mzima,Siwezi kuleta malalamiko yangu kwamba mtu kanifanyia vurugu nyumbani kwangu nisisikilizwe na hata Zinduse mwenyewe amekwisha ridhika na Mwenyekiti",alisema Ngezabuke.

  0 0

  By Jumia Travel Tanzania

  The coming of the science and technology era, in specific the internet sphere has changed tremendously how companies advertise their products and services worldwide.These new media platforms have granted power to customers to testify, criticise and comment on what their experiences with products and services.

  A while ago majority of advertisers concentrated predominantly on traditional modes of advertisement such as television and radio, a one-way communication stream. This did not provide room for customers to share their experiences, question, criticise or comment on products.

  However recently, companies have shifted their focus to online advertising and more engaged based approaches. Most companies have invested a lot on website building as well as their official social media pages such as facebook, twitter and instagram.

  Investing in online media has helped thousands of brands grow because of the reasonable number of followers, likes, viewers, engagements and influence it has within the digitized community. Customers are attracted to companies with a huge influence in their community encouraging them to purchase its products and services.

  The travel and hospitality industry has seen this movement towards technological advancement recently. Online marketing platforms allow customers to survey hotels online as though they are physically there. Moreover, it enables customers to share their experiences towards the services they were provided with.

  Jumia Travel (www.travel.jumia.com), Africa's No.1 hotel booking website, allowing you to get the best prices for more than 25,000 hotels in Africa and more than 200,000 hotels around the world, has encouraged several hotels by awarding certificates for Customers’ Selection due to higher number of positive reviews their received from their customers throughout 2016.

  Speaking on the importance of these awards Jumia Travel Tanzania country manager, Ms. Fatema Dharsee noted that, “These awards are crucial to the growth of business as they keep one aware on how customers rate your hotel and services when they visit. For many years now, word of mouth has been the dominant tool considered when purchasing a product or service because people are highly convinced with the experience felt by their friends or close ones. Through our online hotel booking platform, customers are able to share experience of the hotels they stayed, comment on the services provided to them, criticize as well as offer suggestions to areas in need of improvements.”

  “Now it is the time for hoteliers to recognize how powerful customers’ ratings through online media platforms are for the growth of their business. Online media engagements, especially positive reviews from the customers who experienced good services are enough to market your business since they are authentic and genuine. Therefore, i would like to urge hotel managers who received these certificates to make sure they are following very closely and working effectively on customers’ reviews to improve their services.” Concluded Ms. Dharsee

  Hotels which received the certificates for Customers’ Selection are such as Jafferji House & Spa Hotel and Garden Lodge both from Zanzibar Island; while from Dar es Salaam are Peacock Hotel, Butterfly Hotel and Golden Tulip Hotel.


  0 0  #Bei za umeme zimepanda kwa 8.5% badala ya 18.19% iliyopendekezwa na TANESCO.

  #Ongezeko la bei ya huduma za umeme limetokana na kuzidi kwa gharama za uzalishaji wake.

  #Shirika la umeme Zanzibar (ZECO) ambalo linanunua umeme wa jumla kupeleka Zanzibar limeongezewa 5.7% ya bei ya umeme.

  #Ongezeko hilo halitaathiri wateja wa majumbani ambao matumizi yao hayazidi uniti 75 kwa mwezi.

  #Kundi la TIb linalohusisha viwanda vidogo,mabango na minara ya mawasiliano litakua na tozo ya mwezi ya shilingi 5,520.

  #Bei hizo zitaanza kutumika Januari Mosi mwaka 2017.

  #TANESCO inatarajia kufanya maboresho ya msongo wa umeme na kutekeleza miradi mipya ya kuunganisha wateja ili kuboresha huduma za umeme.

  IMEANDALIWA NA IDARA YA HABARI (MAELEZO).

  0 0


  Kutokana na kuendelea kushamiri kwa migogoro ya wakulima na wafugaji hapa nchini ,mbunge wa chalinze Mh RIDHIWANI KIKWETE ameiomba serikali kuchukua hatua stahiki ili kulinda raia wake dhidi ya migogoro hiyo...
  Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Kitonga kata ya Vigwaza mbele ya mkuu wa mkoa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo, Ridhiwani amesema katika kijiji hicho kuna wafugaji ambao wameingiza mifugo kwenye ranchi pamoja na kijijini pasipo kufata taratibu za kisheria,jambo ambalo limekuwa kero kubwa kwa wakulima wa kitonga,hivyo ni vema serikali ikachukua hatua stahiki juu ya jambo hilo..
  kama ilivyoandikwa kwenye vitabu vya dini kuwa ombeni nanyi mtapewa,kilio cha mbunge ridhiwani kikapokewa vyema na mkuu wa mkoa Mhandisi Ndikilo kwa kutoa siku 30 ,kwa wafugaji waliovamia maeneo ya wakulima kuondoa mifugo yao haraka iwezakanavyo,"Mlipokuja hamkugonga hodi hvyo na mnapoondoka msituulize mtaenda wapi,haiwezekani ufugaji wako mtu mmoja uwe kero kwa jamii inayokuzunguka hii si sawa"...alisema Ndikilo
  RC Ndikilo katika hatua nyingine ameagiza wakuu wa wilaya kuhakikisha wafugaji wote waliongiza mifugo hiyo kuondoka haraka iwezekanavyo, licha ya wafugaji katika kijiji cha kitonga kudai kuwa wana ngombe wapatao laki 5,lakini ukweli unaonesha kuwa kuna zaidi ya kiasi hicho,huku akimtaka mmoja wafugaji anayeonekana kuwa mbabe kijiji hapo aliyefahamika kwa jina moja la leki kuhakikisha anatii agizo la kuondoka ndani ya mwezi mmoja haraka iwezekanavyo..
  akionekana kuchukizwa zaidi na vitendo vya wafugaji kuwanyanyasa wakulima ndikilo amesema ni vyema wafugaji wakaelewa kuwa kila mmoja ana wajibu wa kutii sheria ili watu waishi kwa amani na upendo..
  kwaupande wake mbunge wa chalizne mara baada ya kauli ya mkuu wa mkoa akawataka wananchi wa chalinze kutoa ushirikiano kwa serikali ili kurahisisha zoezi la kuondolewa kwa mifugo iliyoiungia kinyemela..
  Wafugaji wa kwanza kuingia mkoa wa pwani waliiongia mwaka 1940 ambao walikuwa wamasai na tangu hapo ukawa mwanzo wa pwani kuwa na mifugo...
  wanakijiji cha Kitoga wakisikiliza katika mkutano wa kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha Kitoga kata ya Vigwaza Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga akizungumza katika mkutano wa kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha Kitoga kata ya Vigwaza Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga akizungumza kwa wananchi katika mkutano wa kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha Kitoga kata ya Vigwaza Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo akitoa maelekezo kwa wanakijiji baada ya kufika katika kijiji cha Kitonga kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji. Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa katika mkutano wa kutatua migogoro ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha Kitoga kata ya Vigwaza

  0 0

   Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (katikati) akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro wilayani Ngorongoro mkoani Arusha jana katika ziara yake ya kufuatilia utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu. Kulia ni Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Freddy Manongi na Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha (kushoto). 
   Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani (kulia) akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro wilayani Ngorongoro mkoani Arusha jana katika ziara yake ya kufuatilia utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu,  ametoa wiki mbili kwa watumishi wenye mifugo na majengo ndani ya eneo la mamlaka ya hifadhi hiyo kujiandikisha kwa uongozi wa mamlaka hiyo ikiwa ni mkakati wa utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu. 

  Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha akichangia katika mkutano huo. Alieleza kuwa salama ya Hifadhi ya Ngorongoro itategemea uwekaji wa mizania sawa baina ya uhifadhi na maendeleo ya wananchi wa eneo hilo.

   Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Freddy Manongi (katikati) akizungmza katika mkutano huo. Kushoto ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Prof. Alexandre Songorwa (kulia).

   Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo, Mfaume Taka (kushoto) akizungumza kwenye mkutano huo.

   Sehemu ya watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro wakiwa kwenye mkutano huo.

  ................................................................................................
  NA HAMZA TEMBA - WMU
  ....................................................

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo Makani ametoa wiki mbili na siku tano kwa watumishi wote wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) wenye mifugo na majengo ya kudumu  ndani ya eneo la hifadhi hiyo kuorodhesha majina yao kwa uongozi wa mamlaka hiyo  na kusalimisha taarifa ya kile wanachokimiliki ndani ya eneo hilo ikiwa ni sehemu ya mkakati wa utekelezaji maagizo ya Waziri Mkuu  aliyoyatoa kwa uongozi wa mamlaka hiyo.


  Ametoa agizo hilo jana wakati akizungumza na watumishi wa Mamlaka hiyo mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na Ngorongoro katika kikao alichokiitisha kwenye ukumbi wa makao makuu ya NCAA yaliyopo katika wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha kwa ajili ya kufuatilia changamoto za uhifadhi na utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliyoyatoa kwa mamlaka hiyo hivi karibuni akiwa ziarani mkoani Arusha.


  Anasema miongoni mwa maagizo yaliyotolewa na Waziri Mkuu ambayo yameshaanza kufanyiwa kazi ni pamoja na kuondolewa mifugo yote maeneo ya Kreta, kuhakikisha upatikanaji wa maji na chumvi kwa ajili ya mifugo na wananchi, idadi ya mifugo kutambuliwa na kupigwa chapa pamoja na kutambua idadi ya wananchi ndani ya eneo la mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro na kupewa hati za utambuzi.


  “Mpaka ikifika wiki ya pili ya mwezi januari, tarehe 15, kila mtumishi ambaye yeye binafsi ana mifugo ndani ya eneo hili, maana tunaanzia nyumbani, Conservator (Mhifadhi) uweke utaratibu wa kupokea taarifa kutoka kwao, kila mmoja aweze kudeclare (kutangaza) umiliki wake wa mifugo ndani ya eneo la hifadhi, ng’ombe, mbuzi, kondoo.


  "Lakini pia kila mtumishi ambaye ana nyumba ya kudumu ndani ya hifadhi, iliyojengwa kwa matofali, mabati, zege nakadhalika atuambie, na mimi nishauri tu kuwa muwazi itakusaidia. Kwasababu haiwezekani sisi tuanze kuwaambia watu wengine, wewe kwanini umejenga nyumba ya kudumu hapa, wakati tunapowaonyesha vidole na wengine sisi tunazo, hatuwezi kwenda kuwaambia wengine, wewe kwanini una mifugo humu 200,000, 2000, 1000 au 500 wakati wengine sisi humu tuna mifugo zaidi yao hata mara mbili", alisisitiza Makani.


  Alisema kuwa, kwa wale waajiriwa wapya wapewe elimu juu ya malengo na majukumu mahsusi ya taasisi hiyo pamoja na miiko yake ambayo ni pamoja na uwepo wa maeneo maalum ya uhifadhi yasiyoruhusiwa mifugo na majengo ya kudumu.


  Amewataka watumishi wa mamlaka hiyo kusoma kwa makini madhumuni ya kuanzishwa kwa mamlaka hiyo pamoja na majukumu makhsusi iliyopewa ili kufanya vizuri zaidi katika uhifadhi endelevu wa Hifadhi hiyo huku wakitambua kuwa wao ndio wenye jukumu la kwanza la kuhakikisha kuwa taasisi hiyo inastawi.


  Katika hatua nyingine Naibu Waziri Makani ametoa muda wa wiki mbili kwa uongozi wa NCAA kumkabidhi taarifa ya mpango mkakati wa utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu. "Zile wiki mbili nilizozisema, ule mpango mkakati wa utekelezaji wa maagizo ya waziri mkuu, sina maana kwamba tutaanza kutekeleza kwenye wiki mbili, hivi tunavyoendelea kutekeleza kwa maana yapo mambo mengine hapa utekelezaji wake ni wa muda zaidi ya hizo wiki mbili, nataka nipate mpango kazi wa utekelezaji wa maagizo hayo tuujadili na kuufanyia kazi kwa haraka".


  Alisema miongoni mwa changamoto kubwa za uhifadhi katika eneo hilo kwa sasa ni wingi wa mifugo pamoja na majengo ya kudumu ndani ya eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro jambo lililohatarisha uhifadhi endelevu wa hifadhi hiyo.


  Kwa upande wake Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dkt. Freddy Manongi amesema jukumu kuu la kuazishwa kwa mamlaka hiyo ni kuendeleza uhifadhi wa wanyamapori na malikale, utalii na jamii iliyopo ndani ya Eneo la Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.


  Akizungumzia changamoto  alisema kuna uhaba wa chakula kutokana na wananchi wa eneo hilo kuzuiliwa kulima kisheria, malalamiko kuhusu wanyama wakali kuwashambulia wananchi na ongezeko la magonjwa mbalimbali huku mengi yakisababishwa na muingiliano wa wananchi na  wanyamapori.   0 0

  Daraja la mto wa MUHUWESI ambalo wachimbaji wadogowadogo wanafanya kazi hiyo ya kuchimba madini hali ambayo itapelekea kuhabomoka kwa daraja hilo

  Sehemu ambayo wachimbaji hawa wanachimba

  Baadhi ya wachimbaji(Habari na Ruvuma Tv)


  0 0


  0 0

  Ndugu Watanzania, Kama mnavyofahamu kuwa ibara ya 132(4) na (5) na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Sheria namba 13 ya mwaka 1995 inataka viongozi wote wa umma kujaza fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni. 
   
  Tamko hilo huwasilishwa Sekretariat ya Maadili ya Viongozi kabla ya mwisho wa kila mwaka. Kama nifanyavyo siku zote, nawajulisha rasmi kwamba nimetimiza matakwa hayo ya katiba na sheria kuhusu Maadili ya Viongozi.

  Inafahamika kuwa Chama Cha ACT Wazalendo, kwa mujibu wa Katiba yake na Azimio la Tabora, kimeelekeza kuwa Viongozi wake wote waweke wazi kwa Umma Tamko la Mali, Madeni na Maslahi. Kwa kufuata masharti ya Katiba ya Chama Cha ACT Wazalendo natangaza rasmi fomu zangu nilizowasilisha Leo Sekretariat ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

  Ni matumaini yangu kwamba itafikia wakati Daftari la Rasilimali na Madeni la Viongozi wa Umma litakuwa linawekwa wazi kwa Umma ili wananchi waweze kujua Mali, Madeni na Maslahi ya Viongozi wao na pale ambapo kiongozi ametoa habari zisizo sahihi au kuficha mwananchi aweze kutoa Taarifa kwenye Sekretariat na Baraza la Maadili liweze kufanya kazi yake ipsavyo.

  Mfumo wa kuweka wazi Rasilimali na Madeni ya Viongozi wa Umma ni mfumo endelevu na muhimu kwenye vita vita dhidi ya ubadhirifu na ufisadi. Mataifa kadhaa duniani hutumia mfumo huu ( public disclosure of leaders' assets and liabilities) kuwezesha mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi. Nchini Uingereza na Kanada kwa mfano, daftari la matamko ya Rasilimali na Madeni ya Viongozi lipo wazi kwa kila mwananchi kuona na huuzwa kwenye duka la vitabu la Bunge.

  Namsihi Sana Rais John Pombe Magufuli kusaidia kufanya mabadiliko makubwa ya Sheria ya maadili ya Viongozi ili kurejesha na kuboresha Miiko ya Viongozi katika kuimarisha vita dhidi ya ufisadi nchini. Rais aliahidi kuweka wazi Mshahara wake alipokuwa anazungumza katika kipindi cha 360 cha Clouds TV. Ninamkumbusha afanye hivyo na pia aweke wazi Mali, Madeni na Maslahi yake ya Kibiashara ili awe mfano kwa Viongozi wengine Nchini.

  Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto, Mb

  Kigoma Mjini
  30/12/2016

  0 0

  Wezi walivunja na kuingia katika nyumba ya aliyekuwa mshambuliaji wa Manchester City Carlos Tevez viungani mwa mji wa Bueno Aires nchini Argentina siku ya Jumapili na kuiba wakati nyota huyo alipokuwa nchini Uruguay kufunga ndoa.

  Maafisa wa polisi wanasema kuwa Tevez hakuwasilisha ripoti kwa polisi kuhusu wizi huo hivyobasi haijulikani ni nini kilichoibiwa.

  Tevez na mke wake tayari wameondoka na kuelekea Mexico kwa fungate yao.Polisi wanasema kwamba waligundua kuhusu wizi huo siku ya Jumanne baada ya kuwaona wanahabari wamekusanyika nje ya nyumba hiyo ya nyota huyo wa Argentina.

  Wanasema kuwa wezi wengi waliingia katika nyumba hiyo ambayo Tevez na familia yake walikuwa wamekodi huku wakisubiri nyumba yao ambayo ilikuwa inafanyiwa ukarabati.

  Inadaiwa wezi hao waliingia nyumba hiyo kupitia eneo ambalo ukarabati huo ulikuwa ukifanywa.Baada ya Tevez kuarifiwa kuhusu wizi huo, alirudi nyumbani kwake kwa helikopta .

  Aliukuta mlango wa nyumba yake uko wazi huku vitu vikiwa vimepekuliwa.Tevez baadaye alisafiri kuelekea Mexico kama alivyopanga kwa fungate yake na mpenziwe wa utotoni Vanesa Masilla.

  Wawili hao waliokutana wakiwa na umri wa miaka 13 na ambao wana wasichana wawili, walifunga ndoa katika sherehe ya kawaida siku ya Ahamisi mjini Bueno Aires.
   

  0 0

  MAMLAKA ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji, (EWURA), imetangaza ongezeko la bei ya umeme kwa asilimia 8.5%.

  Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlamgosi, (pichani), ongezeko hilo la bei ni kufuatia maombi ya Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO), ambalo liliwasilisha maombi EWURA ya kutaka ongezeko la bei kwa asilimia 18.19, ifikapo Januari mwaka 2017.


  Akitangaza bei hizo mpya jijini Dar es Salaam, leo Mkurugenzi Mkuu huyo wa EWURA amesema, baada ya kufanya uchambuzi wa kina, Mamlaka yake imefikia uamuzi wa kuongeza asilimia 8.5 itakayoanza kutumika Januari Mosi, 2017 kutokana na kuongezeka kwa gharama za uzalishaji wake.

  Shirika la umeme Zanzibar (ZECO) ambalo linanunua umeme wa jumla kupeleka Zanzibar limeongezewa kwa asilimia 5.7% ya bei ya umeme.

  Hata hivyo ongezeko hilo halitaathiri wateja wa majumbani ambao matumizi yao hayazidi uniti 75 kwa mwezi.

  Kundi la TIB linalohusisha viwanda vidogo, mabango na minara ya mawasiliano litakua na tozo ya mwezi ya shilingi 5,520.

  Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), linaendelea kufanya maboresho ya miundombinu ya umeme na kutekeleza miradi mipya ya kuunganisha wateja ili kuboresha huduma za umeme nchini.

  0 0


  Diwani wa viti maalumu Chadema kata ya Mang’ola ,Maria Patrice aliyevaa kitenge akiwa na baadhi ya wananchi wa wilaya ya karatu leo katika kituo cha polisi mjini kati Jijini Arusha.Picha na Vero Ignatus blog.
  Baadhi ya wananchi kutoka wilaya ya karatu wakiwa nje ya kituo cha polisi mjini kati leo.Picha na Vero Ignatus Blog.


  Vero Ignatus,Arusha

  Sakata la viongozi wa Chadema na wananchi wa vijiji  vinne wilayani Karatu Mkoani Arusha wamekamatwa na polisi kwa kosa la kuchoma mashine ya kuvutia maji ni kufuatia hatua za baadhi ya watu kukaidi amri ya Waziri Mkuu aliyetaka mashine hizo zote kuondolewa katika chanzo cha maji kilichokuwa na mgogoro wa muda mrefu.

  Waziri Mkuu,Kassimu Majaliwa Mnamo desemba 5 mwaka huu,alimwagiza Mkuu wa wilaya ya Karatu, Theresia Mahongo kuhakikisha kabla ya saa 12 jioni nay eye kumaliza kikao na wananchi awe ameziondoa mashine hizo zilizowekwa katika chanzo cha maji.

  Mbali ya hilo Waziri Mkuu aliagiza chanzo hicho cha maji kutunzwa na mashine zote ziwe umbali wa mita 500 na mto utunzwe kwa mita 60 tofauti na hapo hatua kali zichukuliwe.Kufuatia agizo hilo vifaa hivyo na vingine viliondolewa vyote kwa kusimamiwa na Mkuu wa wilaya Karatu mwenyewe na jeshi la polisi wilaya ya Karatu.

  Diwani wa viti maalumu Chadema kata ya Mang’ola ,Maria Patrice akizunzgumza na waandishi wa habari leo amesema kuwa baada ya agizo hilo kutekelezwa walirudi katika vikao vya jumuiya ya uongozi wa vijiji saba vya kata mbili za Mang’ola na Qaedenti kwa ajili ya kufanya maazimio ya agizo la Waziri Mkuu.

  Amesema vijiji vyote viliafiki agizo hilo na kuahidi kutunza chanzo hicho cha maji umbali wa wa mita 500 kutoka katika chanzo hicho na mita 60 kutoka kwenye mto.Patrice ameendelea kueleza kuwa maazimio hayo yalikubaliwa na viongozi na wananchi wa vijiji vyote kwani kiliagizwa na Waziri Mkuu ni msisitizo kwani katika vikao vya nyuma vya vijiji hivyo hayo yote yalikubaliwa katika vikao.

  Alisema cha kushangaza baadhi ya viongozi na madiwani kukamatwa kwani ndio waliokuwa mstari wa mbele kuhakikisha wananchi wanatii amri ya Waziri Mkuu.Diwani huyo alisema kuwa aliambiwa kuwa baadhi ya wananchi wamerudisha mashine na vifaa vingine katika chanzo hicho cha maji na kufikia hatua ya wananchi wengine kukasirishwa na kitendio hicho cha kudharau mamlaka za juu zilizoagiza.

  ‘’Baadhi ya watu waliokamatwa hawahusiki kabisa na uchomwaji wa mashine hizo kwani polisi imeamua kukamata hovyo hovyo ila mie ninachojuwa desemba 26 na 27 mwaka huu baadhi ya wananchi walialikwa kufanya usafi katika chanzo hicho na kwa kuw amaji yalikuwa yakipungua siku hadi siku’’alisema diwani huyo

  Mkazi mwingine wa Kata ya Mang’ola aliyeomba kutotajwa jina lake alisema kuwa mgogoro huo ni wa muda mrefu sana kutoka mwaka 2007 na kijiji cha Qaedenti ndio chanzo mgogoro huo kwani wamekuwa waghumu kutii maagizo ya viongozi wa juu wa serikali pindi wanapotakiwa kukaa umbali wa mita 500 kutoka katika chanzo hicho cha maji.

  ‘’wamekuwa wakileta vurugu kila mara kwa sababu ya madai kuwa chanzo hicho ni chao lakini sio kweli kwani chanzo hicho hutoa huduma ya maji kwa vijiji saba bila ya kuwa na ubaguzi wowote’’alisema mwananchi huyo

  Alisema kuchomwa kwa mashine ni kutokana na wananchi kupatwa na hasira na jazba za baadhi ya wananchi kurudisha mashine na vifaa vingine katika chanzo hicho cha maji na kudharau agizo la Waziri Mkuu.

  Wakati huo huo Mbunge wa Jimbo la Karatu ,Willy Qambalo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu ,Jubillet Manyenyo wameachiwa kwa dhamana na wametakiwa kuripoti kituo kikuu cha polisi Arusha januari 4 mwakani.Wengine waliokamatwa na bado wanahojiwa na polisi Arusha ni pamoja na diwani wa kata ya Baray ,Thomas Darabe na diwani wa kata ya Mang’ola Lazaro Emmanuel .

  Kamata kamata hiyo imewakumba wananchi wengine ambao ni pamoja na Godwin Mussa,Safari Awak,George Pius,Baridi John,Bartazar Lohay,Jafari Thiophil,Vicent Airo ,sebastian Mosses na Daniel Ninida.Wengine waliokamatwa na polisi ambao ni ndugu ni pamoja na ndugu wawili ambao ni pamoja na Charles Lameck na Chrisopher Lameck .

  Habari kutoka ndani ya jeshi la polisi zinasema kuwa baada ya kuchukuliwa maelezo kwa watuhumiwa hao 15 majalada yanapelekwa katika ofisi ya Mwansheria wa serikali kwa ajili ya kufungua kesi.

older | 1 | .... | 1084 | 1085 | (Page 1086) | 1087 | 1088 | .... | 1897 | newer