Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1083 | 1084 | (Page 1085) | 1086 | 1087 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Mhe. Juma Zuberi Homera,akiwa na baadhi ya wakulima wa Korosho
   Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Mhe. Juma Zuberi Homera,akishiriki kumwagilia miche ya zao la Korosho kwenye vitalu


  Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Mhe. Juma Zuberi Homera, jana desemba  27,2016 alikwenda CDC kujiridhisha na uandaaji wa miche za mikorosho kwa msimu mpya wa Kilimo 2016/2017 na hatimaye kuridhishwa na maandalizi ya miche ya mikorosho iko ya kutosha na itaanza kusambazwa Kwa mujibu wa utaratibu wa uendelezaji wa zao hilo.

  Lakini pia ametoa maelekezo kwa maafisa elimu. alisema, "maafisa elimu wanapaswa kuhakikisha wana kwenda sambamba katika uzalishaji wa zao hili la biashara wilayani Tunduru kwa upande wa shule za msingi na sekondari kwa kuandaa hekari 5 za mikorosho kila shule maafisa kilimo, watendaji wa Kata na vijiji wanapaswa kusimamia zoezi hili na mbegu hizo watagawiwa bure kama mradi wa EK na kuhusu uzalishaji wa mbegu mwaka huu ni mzuri zaidi ukilinganisha na mwaka jana. 
   
  Mfano, kitalu cha CDC kina miche zaidi ya 79,000, kangomba zaidi ya miche 49,000, Mbesa zaidi ya miche 25,000, Nalasi zaidi ya miche 20,000, Namasakata zaidi ya miche 20,000, Misechela zaid ya miche 25,000, Muhuwesi 15000, Majimaji zaidi ya miche 10,000, Namiungo zaidi ya miche 15,000, Nandembo zaidi ya miche 15000, na kitanda zaidi ya miche15000 kazi kwetu wanatunduru mbegu hizi za kisasa zinazaa baada ya miaka 3".

  Alisisitiza, "lakini pia ni mbegu bora kuhusu minada mpaka sasa wanunuzi mnada wa 4,5,6, wameshalipa bado kuwafikishia vyama vya msingi baada ya kufanya ukokotozi "TWENDE NA MKOROSHO WANGU UCHUMI WANGU" tusisahau kupanda mazao ya Chakula kama mahindi, mpunga, mihogo nk. Tumuunge mkono Rais wetu Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika kuinua kilimo nchini na chenye tija kwa wananchi wanyonge na wa hali ya chini. HAPA KAZI TU mungu ni Mwema"

  0 0


   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye ni mbunge wa Ruangwa akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Manokwe katika wilaya ya Ruangwa ambao walijitokeza kumsikiliza mbunge wao alipokuwa anawahimiza kufanya kazi ilikujileta maendelo katika wilaya ya ruangwa Waziri mkuu yupo Jimboni Ruangwa kwa ziara ya kikazi
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye ni mbunge wa Ruangwa akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Manokwe katika wilaya ya Ruangwa ambao walijitokeza kumsikiliza mbunge wao alipokuwa anawahimiza kufanya kazi ilikujileta maendelo katika wilaya ya ruangwa Waziri mkuu yupo Jimboni Ruangwa kwa ziara ya kikazi . 

   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye ni mbunge wa Ruangwa akisalimiana na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Manokwe katika wilaya ya Ruangwa ambao walijitokeza kumsikiliza mbunge wao alipokuwa anawahimiza kufanya kazi ilikujileta maendelo katika wilaya ya ruangwa Waziri mkuu yupo Jimboni Ruangwa kwa ziara ya kikazi.
   Wananchi wa kijiji cha Nga’u kilichopo wilaya ya Ruangwa wakiwa wamejikinga  mvua kwakutumia viti wakati wakimsikiliza mbungewao Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa akiwahutubia kwa ajili yakuhimiza shughuli za maendeleo jimboni Ruangwa Mkoani Lindi.Picha na Chris Mfinanga


  0 0

  Disemba 19 hadi 25 mwaka huu, Mchungaji Josephine Miller (wa tatu kushoto) kutoka Marekani alikuwa akifundisha na kuhubiri katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza. 

  Baada ya huduma hiyo, jana Disemba 27, wenyeji wake (pichani) wakiongozwa na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo, Dkt.Daniel Moses Kulola (wa sita kulia) na Mama Mchungaji Mercy Kulola (wa tano kulia), walimtembeza Mchungaji Miller katika hifadhi ya Taifa Serengeti ili kujionea vivutio mbalimbali vilivyopo katika fidhahi hiyo.
  Na BMG
  Waumini wa EAGT Lumala Mpya wakifurahia uwepo wao ndani ya hifadhi
  Mchungaji Josephine Miller kutoka Marekani (kulia) akifurahia uwepo wake ndani ya hifadhi ya Serengeti. Kushoto ni Mwanahabari na Blogger wa Lake Fm Mwanza, George Binagi
  Pundamilia, nyumbu na nyati wakiwa kwenye makundi ndani ya hifadhi ya Serengeti
  Mama na Mwana
  Twiga na upendo wao, hawaachani
  Matukio yakiendelea kunaswa katika eneo la Viboko na Mamba
  Tembo ndani ya hifadhi ya Serengeti
  Simba mjamzito
  Hili ni daraja la waya ndani ya hifadhi ya Serengeti, ni katika eneo lenye Viboko wengi. Kulia ni Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kulola akiwa na Mwanahabari George Binagi
  Mchungaji Josephine Miller akipanda daraja la kunesanesa, limetengenezwa kwa kama imara ya chuma Daraja la kunesanesa
  Ni muda wa chakula ndani ya hifadhi ya Serengeti huku pia Watalii wa Ndani na Watalii wa Nje, wakifurahia pamoja uzuri wa hifadhi ya Serengeti.

  Watanzania wametakiwa kuongeza hamasa ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini ikiwemo hifadhi za Taifa ili kufurahia rasilimali walizotunukiwa na Mwenyezi Mungu.

  Mchungaji Josephine Miller kutoka nchini Marekani aliyasema hayo jana wakati wa ziara yake ya kutembelea hifadhi ya Taifa ya Serengeti ili kujionea vivutio mbalimbali vya wanyama katika hifadhi hiyo.

  Alisema alipokuwa katika hifadhi mbalimbali barani Afrika ikiwemo za Afrika Kusini na Zimbabwe, alikuwa akisikia kuhusu uzuri wa hifadhi ya Serengeti hivyo amefurahia kutembelea hifadhi hiyo akisema kwamba hilo lilikuwa ni chaguo lake la pili baada ya kuonana na watu wa bara la Afrika.

  Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, Dkt.Daniel Kulola, alisema ni vyema Mamlaka ya Hifadhi za Taifa TANAPA ikaongeza hamasa kwa Watanzania kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini ili kuukuza zaidi utalii wa ndani huku akiomba suala la miundombinu ya barabara kuboreshwa ili watalii.

  Kumbuka Mtanzania hulipa Tsh.11,800 pamoja na VAT kwa mtu mzima ili kuingia katika hifadhi ya Serengeti. Wageni hulipa dolla 70 ikikadiliwa kuwa Tsh, laki moja na elfu hamsini na nne. Hakika watanzania wanayo furusa kubwa kutembelea vivutio vya vya utalii.


  0 0

  MEYA wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita anatarajia kuwa mgeni rasmi katika fainali za kuwania Kombe la Diwani wa Tabata yanayotarajia kuanza Januari nane mwakani kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Tabata.

  Akizungumza juzi, Diwani wa Kata ya Tabata, Patrick Assenga alisema ufunguzi wa mashindano hayo mgeni rasmi anatarajia kuwa Meya wa Ilala Charles Kuyeko.

  Assenga alisema kabla ya kuanza kwa mashindano hayo, Januari 3 anatarajia kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu shiriki 16 vikiwemo jezi na mipira kwa washiriki.

  Aseenga alisema mashindano hayo yatashirikisha timu mbili za mitaa nane ambako mitaa yenyewe ni pamoja na Tabata, Kisiwani, Msimbazi, Msimbazi Magharibi, Mtambani, Mandela, Matumbi na Tenge.

  Assenga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mipango miji wa jiji la Dar es Salaam alitaja zawadi kwa mshindi wa kwanza ni ng’ombe mkubwa na mpira, mshindi wa pili atazawadiwa ng’ombe na mpira na mshindi wa tatu atazawadiwa mipira na jezi.

  Aidha Assenga alisema katika ufunguzi wa mashindano hayo atawashirikisha wachezaji wa zamani kama akina Jella Mtagwa, Peter Tino na wengineo kwa lengo la kuwapa heshima kwa waliyoifanyia Tanzania miaka iliyopita.

  Assenga alisema hamasa hiyo itasaidia wachezaji wa sasa kuongeza hamasa kwa akina Mbwana Samatta ili wasijutie mchezo huo.

  0 0  Na.Vero Ignatus Arusha.

  Mahakama kuu kanda ya Arusha imesikiliza maombi ya rufaa yayaliyowasilishwa na upande wa jamhuri na ule wa mshtakiwa Godbless Lema ambapo pande zote mbili wamekubaliana kusikilizwa rufaa ya upande wa jamhuri ambapo upande wa serikali wameiomba mahakama kuwasilisha kwa hati ya maandishi hapo kesho tarehe 30 disemba 2016 

  Aidha rufaa hizo ni pamoja na ile ya upande wa Jamhuri kutoridhika na maamuzi ya Jaji Dkt. Modesta Opiyo la kuwapa siku kumi (10) upande wa mshtakiwa Lema kufaili notisi ya rufaa ,na upande wa mshtakiwa ni ile ya kupinga uamuzi wa mahakama ya chini kushindwa kumpa Lema masharti ya dhamana

  Jaji aliyekuwa anasikiliza kesi ya rufaa hizo Salma Magimbi amesema kuwa mara baada ya upande wa jamhuri kuleta rufaa kwa njia ya maandishi upande wa mshtakiwa Lema wataijibu tarehe 30 desemba 2016 ambapo tarehe 2 januari watakutana pande zote kwa ajili ya kufanya majumuisho na maamuzi ya rufaa hiyo yatatolewa tarehe 4 januari 2017

  Hata hivyo baada ya kusikiliza rufaa hizo mahakama imeibua hoja yenyewe na kuwapa kazi mawakili wa pande zote mbili kuangalia kuwa notisi iliyowasilishwa na mahakama ya chini imekidhi matakwa ya kisheria?

  Kwa upande wa wakili wa mshtakiwa Peter Kibatala amesema kuwa kwa upande wao wameiomba mahakama kusubirisha rufaa yao ili wasikilize kwanza rufaa ya upande wa jamhuri kwani rufaa zote zimegongana na zinaelekea sehemu moja 

  "Unajua leo rufaa mbili zimegongana ile ya upande wa jamhuri na ile ya kwetu sisi,hivyo basi sisis tumeiomba mahakama kusitisha rufaa yetui isikilizwe ile ya serikali kwanza,kwani rufaa zote zinaelekea upandemmoja ,wandege apande ndege na wa basi apande basi "alisema Kibatala.

  Hata hivyo mbunge huyo wa Arusha mjini Godbless Lema amerudishwa rumande hadi hapo maamuzi yatakapotolewa na mahakama. 


  0 0

   
   Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Dkt Leonard Maboko (Katikati)akiwa na Mkuu wa kitengo cha Sheria Bi Elizabeth Kaganda(Kushoto)Pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Uraghibishi Bw Jumanne Issango(Kulia)Wakiongea na Waandishi wa Habari Kuhusu Takwimu za Hali ya Virusi vya  Ukimwi na Ukimwi kwa Tanzania kwa Kulinganisha na hali ya Dunia na ya Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika.
   Akizngumza na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Mikutano wa TACAIDS leo jijini Dar es salaam.Picha na Yasir Adam Blog ya Jamii⁠⁠⁠⁠

  Na Anthony John Glob Jamii.

  TAKWIMU zinaonyesha kuwa maambukizi mapya ya ukimwi yamepungua ikiwemo kwa watoto kwa asilimia 50% japokuwa bado ni janga kubwa kwa Dunia,Afrika na Tanzania hivyo nguvu zaidi inahitajika kupambana na ugonjwa huo.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo hii Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania Leonard Maboko amesema kuwa mapambano dhidi ya virusi vya Ukimwi yanatakiwa kuwa endelevu haswa katika maeneo yanayoonyesha kuathirika zaidi ili kutokomeza maambukizi mapya.

  " wakati maambukizo mapya yameshuka kwa asilimia 50 miongoni mwa watoto duniani 290,000 wapya waliambukizwa mwaka 2010 na watoto wapya 150,000 waliambukizwa Mwaka 2015 maambukizo mapya kwa watu wazima hayajashuka tangu 2010 duniani" amesema Maboko.

  Aidha maboko ameongeza kuwa Dunia imejiweke lengo la kutokomeza Ukimwi kama janga ifikapo mwaka 2030 kupitia Shirika la umoja wa mataifa linalo ratibu mapambano dhidi ya Ukimwi (UNAIDS) kwakuanza kutoa dawa za kufubaza virusi vya ukimwi mara tu mgonjwa anapogundulika kuwa na Ugonjwa huo.

  Wakati Huo Huo Mkurugenzi huyo alitumia fursa hiyo kuwaasa watanzania kutokubweteka na mafanikio ya takwimu kushuka kwa maambukizi ya virusi vya Ukimwi na badala yake kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

  0 0

  RC ATOA WIKI MBILI WANANCHI WAJENGE VYOO
  *Msako wa DC kupita Jan. 15 mwakani
  *Asiye na choo kutozwa faini ya sh. 50,000

  MKUU WA MKOA wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi ametoa wiki mbili kwa wakazi wa jimbo la Ruangwa kuhakikisha kuwa wanajenga vyoo ili kujiepusha na ugonjwa wa kipindupindu.

  Amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Bw. Joseph Mkirikiti afanye msako wa nyumba kwa nyumba ifikapo Januari 15, 2017 na endapo atakuta kuna mkazi wa kijiji chochote hajajenga choo, basi atozwe faisi ya sh. 50,000 mara moja.

  Ametoa a leo (Jumatano, Desemba 28, 2016) wakati akizungumza na wananchi wa vijiji vya Namilema, Mbuyuni, Nandandara, Namkonjera, Muhuru, Chikundi na Chibula wilayani humo ambako alikuwa akiwasalimia wananchi kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu azungumze na wakazi wa vijiji hivyo.

  Waziri Mkuu yuko Ruangwa kwa siku nne kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka na ameamua kutumia muda huo kuwasalimia wananchi wa jimbo lake na kuhimiza kazi za maendeleo.

  Mkuu huyo wa Mkoa amesema wakulima wengi wamevuna korosho msimu na baadhi yao wamelipwa vizuri, hivyo hawana budi kutumia sehemu ya fedha hizo kujenga vyoo ili kujiepusha na magonjwa ya mlipuko na hasa kipindupindu.

  “Hili ni agizo la Serikali siyo yangu binafsi kwa hiyo ni amri halali. Kikilipuka kipindupindu, naanza na Mkuu wa Wilaya kabla na mimi sijaulizwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu au Mheshimiwa Rais,” amesema.

  Katika hatua nyingine, Bw. Zambi amewahimiza wakazi wa vijiji hivyo wapande miche ya mikorosho katika msimu huu wa kilimo pindi mvua zitakapoanza kwani iliyopo imekaa kwa zaidi ya miaka 50 na sasa haizai matunda ya kutosha.

  “Mkoa wetu una mpango wa kubadilisha miti ya mikorosho kwani mingi ni ya zamani na imelkaa kwa zaidi ya miaka 40 hadi 50 na hivi sasa haina tija kwenye mazao yake. Mti mzuri wa korosho unazaa hadi kilo 40 lakini hii iliyopo sasa hivi inatoa kilo 10 tu,” amesema.

  Amesema Serikali imeagiza kila kijiji kiandae miche 5,000 kwa mwaka na kuwapa wananchi kwa bei nafuu na mpango huo tumeshaanza kuutekeleza.

   
                              
  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMATANO, DESEMBA 28, 2016.

  0 0  0 0

  darassa-dar-live-4
  darassa-dar-live-5
  darassa-dar-live-6
  darassa-dar-live-7
  Nyomi la mashabiki wakimshangilia Darassa.
  darassa-dar-live-8
  darassa-dar-live-9
  darassa-dar-live-10
  darassa-dar-live-11
  darassa-dar-live-12
  darassa-dar-live-13
  darassa-dar-live-14
  Darassa akigonga shoo ya bure Viwanja vya Karume leo.
  darassa-dar-live-15
  darassa-dar-live-16
  darassa-dar-live-17
  darassa-dar-live-18
  Mashabiki wakisukuma gari la Darassa.

  darassa-dar-live-1
  Meneja Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers ambao ni waandaaji wa shoo ya R.O.M.A na Darassa, Abdallah Mrisho akitoa ufafanuzi kwa wanahabari waliokuwepo Viwanja vya Karume jijini Dar, leo kuhusu shoo hiyo.
  darassa-dar-live-2
  Meneja wa Dar Live na mratibu wa mpambano huo, Juma Mbizo akitoa maelezo kuhusu shoo hiyo kwa wanahabari.
  darassa-dar-live-3
  Rapa Darassa akizungumza na wanahabari kuelekea shoo hiyo.  MWANAMUZIKI wa Hip Hop anayefanya poa kwa sasa hapa Bongo, Shariff Thabeet ‘Darassa’, leo amefanikiwa kuisimamisha Ilala alipokutana na mashabiki wake kabla ya Jumamosi hii hajapanda kwenye Jukwaa la Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam.

  Darassa na Roma, kwa pamoja watapanda katika Jukwaa la Dar Live kwenye Mkesha wa Mwaka Mpya ili kumaliza ubishi wa nani mkali wa michano katika pambano la Nichane Nikuchane.

  Akiwa kwenye Viwanja vya Karume jijini Dar, leo, Darassa aliisimamisha Ilala pale alipotoa burudani fupi ikiwa ni kionjo kabla ya shoo yenyewe kamili ya siku hiyo.

  Akizungumza na mashabiki wake, Darassa alisema: “Mashabiki zangu, siku hiyo ya Mkesha wa Mwaka Mpya mnachotakiwa kufanya ni kuja kwa wingi pale Dar Live kushuhudia miujiza nitakayoifanya kwani siku zote naamini huwa nafanya miujiza kila ninapopanda jukwaani.”

  Naye Meneja wa Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers ambao ni waandaaji wa pambano hilo, Abdallah Mrisho, alisema: “Shoo hii inayoenda kufanyika ni ya tofauti, kama tujuavyo R.O.M.A na Darassa kwa sasa ndiyo habari ya mjini hasa kwenye Muziki wa Hip Hop, hii ni mara ya kwanza kwa Darassa kupanda kwenye Jukwaa la Dar Live, hivyo mashabiki ni fursa yenu kujumuika naye siku hiyo."

  Katika hatua nyingine, Meneja wa Dar Live na mratibu wa mpambano huo, Juma Mbizo, alisema: “Kwa kiingilio cha Sh 5,000, mashabiki watapata fursa ya kuingia na kushuhudia mpambano huo mkali ambao rasmi utaanza saa 7 mchana mpaka majogoo.”

  Mbali na wakali hao kupanda jukwaani siku hiyo, pia wengine watakaotoa burudani ni pamoja na Kundi la Muziki wa Taarab la Jahazi, Juma Nature, Makhirikhiri, MC Darada, Topido, ID Classic, H-Mbizo na wengine wengi.

  Mpaka Home; Haya Ndo' Maisha Halisi ya Darassa, Tazama Anavyopika Msosi Gheto


  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na vikongwe wa kijiji cha Nandandala wilayani Ruangwa baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara kijijini hapo akiwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguzi la Ruangwa , Desemba 28, 2016.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Namilema wilayani Ruangwa akiwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguzi, Desemba28, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Nandandala wilayani Ruangwa akiwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguzi la Ruangwa Desemba 28, 2016.

  Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Namilema wialyani Ruangwa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao akiwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguzi la Ruangwa Desemba 28, 2016.

  Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Namkunjera wilayani Ruangwa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kijijini hapo akiwa katika ziara ya jimbo lake la Ruangwa Desemba 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

   Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo akiangalia
  kitanda ambacho kinatumiwa na akina mama wajawazito wakati wa
  kujifungua katika Hospitali ya wilaya ya Itigi mkoani singida wakati
  alipofanya ziara ya kushtukiza. Kulia kwake ni Dkt. Mary Rume Kaimu
  Mganga Mkuu wa Wilaya Itigi na anayefuatia ni Mkuu wa wilaya Manyoni
  Geoffrey Mwambe.
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo
  akimsikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Itigi Pius Luhende
  wakati alipokuwa akitoa maelezo ya namna walivyojipanga kushughulikia
  kero ya wodi ya wazazi katika Hospitali ya wilaya ya Itigi mkoani
  singida.
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo akipata
  maelezo toka kwa Agnesi Katumbo juu ya kusitishwa kwa kutolewa kwa
  risiti za kielectroniki ambayo ni kinyume na utaratibu wa Serikali na
  kutoa wiki moja kurudisha huduma hiyo ambayo ni chanzo cha kupotea kwa
  fedha za Serikali.
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo akipata
  maelezo toka Mkuu wa wilaya Manyoni Geoffrey Mwambe wakati wa ziara
  yake aliyoifanya wilayani humo Manyoni na Halmashauri ya Itigi,
  alieleza juu ya changamoto za wahamiaji, uharibifu wa mazingira na
  tatizo la utoro wa wanafunzi ambalo linasababishwa na wazazi zaidi
  katika wilaya hiyo, walio kaa kulia kwake ni Mkurugenzi wa Halmashauri
  ya Manyoni Edward C. Fussi na anayefuata ni Mwenyekiti wa Halmashauri
  ya Manyoni Moses Matonya.
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo
  akisisitiza jambo kwa Wakuu wa Idara na baadhi ya watumishi wa
  Halmashauri ya Manyoni (hawapo pichani) juu ya uwajibikaji kwa vitendo
  na sio kwa mazoea ili kuleta ufanisi sehemu za kazi walio kaa kushoto
  kwake ni Mkuu wa wilaya Manyoni Geoffrey Mwambe, Mwenyekiti wa
  Halmashauri ya Manyoni Moses Matonya na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manyoni Edward Fussi

  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo
  akimpima uzito mmoja wa watoto katika hospitali ya wilaya ya Manyoni
  alipotembelea hospitali hiyo wilayani manyoni leo hii.

  ……………..

  NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  (Tamisemi), Selemani Jafo, amefanya ziara katika halmashauri mpya ya
  Itigi na Manyoni huku akibaini uwepo wa changamoto mbalimbali hususan
  upungufu wa dawa katika Kituo cha Afya Itigi na Hospitali ya wilaya ya
  Manyoni mkoani Singida.

  Akizungumza katika ziara hiyo, Jafo amesema mara baada ya kutembelea
  Halmashauri hizo amebaini changamoto za dawa katika kituo cha afya
  Itigi pamoja na vifaa katika chumba cha mama huku akisema zipo
  changamoto ambazo zinazotakiwa kutatuliwa ndani ya halmashauri hiyo.

  Jafo akizungumza kuhusu suala la upatikanaji wa dawa, amesema tatizo
  hilo linaonekana ni kikwazo kutokana na watendaji kushindwa kutumia
  fedha za dharura wanazopewa na serikali kununulia dawa na vifaa tiba.

  “Naziagiza Halmashauri hizi kuhakikisha zinaweka kipaumbele uboreshaji
  wa vituo vya afya kwa kununua dawa nyingi na vifaa vingine tofauti na
  kusubiri zinazotoka Bohari ya Madawa (MSD),”amesema Naibu Waziri huyo

  Amewaagiza watendaji wa idara mbalimbali kuhakikisha wanashirikiana na
  mkurugenzi wa Itigi ili kutimiza wajibu wao na kuifanya halmashauri
  hiyo kuwa bora na kuwaonya kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

  “Kila mtumishi ahakikishe anajali muda wa kazi na kuacha tabia ya
  kutoenda kwa ratiba ya kazi, watumishi wa Tamisemi wanatakiwa
  kujiamini katika kazi zao na kuacha uoga ama kufanya kazi hadi pale
  wanapofuatiliwa hasa kwenye miradi mbalimbali,”amesema

  Kadhalika, Naibu Waziri huyo amewataka wahasibu kuacha tabia ya
  kuabudiwa kutokana na kuamua kuidhinisha fedha hadi pale
  watakapojisikia na kusababisha miradi mingi kukwama na mingine kufa.

  Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa hospitali ya wilaya ya Manyoni, Dk.
  Francis Mwanisa, amesema hospitali hiyo inakabiliwa na upungufu wa
  dawa licha ya kupokea wagonjwa kutoka sehemu mbalimbali nje ya wilaya
  hiyo.

  0 0
  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewahimiza wakazi wa vijiji saba wilayani Ruangwa waharakishe kufyatua matofali ili waanze ujenzi wa zahanati na yeye atawachangia mabati.

  Ametoa ahadi hizo leo (Jumatano, Desemba 28, 2016) wakati akizungumza na wananchi wa vijiji vya Namilema, Mbuyuni, Nandandara, Namkonjera, Muhuru, Chikundi na Chibula na viongozi wa wilaya ya Ruangwa, mkoa wa Lindi ambako anapita kuwasalimia wananchi wa jimbo lake na kuhimiza kazi za maendeleo. Waziri Mkuu yuko Ruangwa kwa siku nne kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka.Amesema sera ya Serikali ni kuwa na zahanati kwa kila kijiji na kituo cha afya kwa kila kata na kwamba umefika wakati wa kuanza kutekeleza kaulimbiu ya jimbo hilo inayosema “Ruangwa kwa maendeleo, inawezekana.”

  Katika kuhimiza ujenzi wa zahanati hizo, amechangia mabati kati ya 50 na 150 kwa kila kijiji na akawahimiza wahakikishe wanakamilisha mapema ujenzi wa maboma ili aweze kutimiza ahadi yake ya mabati.

  Amesema katika awamu iliyopita, alikazania sana suala la elimu kwa kusimamia ujenzi wa nyumba za walimu na madarasa kwenye shule ambazo hazikuwa na madarasa ya kutosha. Pia alisimamia ukarabati wa majengo chakavu katika baadhi ya shule.

  “Kuanzia awamu hii na miaka minne iliyobakia, mkakati wangu ni kusimamia upatikanaji wa maji safi na suala la kuboresha sekta ya afya katika jimbo zima nikishirikiana na uongozi wa Halmashauri yetu,” amesema.Pia amemwagiza Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Dk. Japhet Simeo ahakikishe anawasiliana na viongozi wa vijiji hivyo ili wapatiwe michoro ya ramani zilizoidhinishwa na Wizara ya Afya.

  Wakati huohuo, Mkurugenzi wa kampuni ya Umemejua ya Baraka Solar Specialist, Bw. Ansi Mmasi amesema atajitolea kuweka mfumo wa umemejua wa watts 300 pamoja na nyaya zake kwenye zahanati inayotaka kujengwa kwenye kijiji cha Namilema.Alisema anaishukuru kwa kuwapa kazi makandarasi wazawa na akawataka wakandarasi wenzake watumie vifaa bora na imara pindi wanapopewa kazi ya kutoa huduma na taasisi mbalimbali ikiwemo halmashauri na idara za Serikali.

  “Tujitahidi kufanya kazi hizi kwa weledi na tutumie vifaa bora na imara ili watu wanaotarajia huduma zetu waweze kuridhika na kuendelea kuwa na umani na wakandarasi wazawa kwamba tunaweza kufanya kazi nzuri na zenye ubora unaotakiwa,” amesema.

  Naye Mkurugenzi wa kampuni ya ujenzi ya Wanyumbani Construction, Bw. Fakihi J. Bakili alisema atachangia mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa zahanati hiyo ya kijiji cha Namilema. Pia alichangia mifuko 100 kwenye zahanati ya kijiji cha Manokwe na mifuko mingine 50 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Chikundi.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMATANO, DESEMBA 28, 2016.

  0 0

  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt.Medard Kalemani, akizungumza jambo wakati wa Mkutano wake na wananchi wa Kata ya Ngwanseri,wilaya ya Muleba, wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Mradi wa REA Awamu ya Pili.
  Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Ruyango,akizungumza jambo wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt.Medard Kalema ni kukagua utekelezaji wa Mradi wa REA Awamu ya Pili.Wengine katika picha ni baadhi ya Viongozi wa Halmashauri hiyo,Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, REA,TANESCO, na Wakandarasi wanaotekeleza mradi husika.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt.Medard Kalemani, akizungumza jambo wakati wa Mkutano wake na wananchi wa Kijiji cha Kishuro,Kata ya Ngenge Wilaya ya Muleba, Mkoa wa Kagera. Dkt.Kalemani amefanya ziara Wilayani humo ya kukagua Mradi utekelezaji wa Mradi wa REA Awamu ya Pili na kueleza mipango ya Serikali kutekeleza Awamu ya Tatu ya mradi husika.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt.Medard Kalemani, (Wa tatu kushoto) katika picha ya pamoja na Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini, Prof.Anna Tibaijuka (wa pili kushoto),Mkuu wa wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Ruyango,(wan ne kushoto)pmoja na Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, REA,TANESCO, na Wakandarasi wanaotekeleza mradi wa REA Awamu ya Pili.
  Mmoja wa Wananchi katika akiuliza jambo wakati wa mkutano wa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt.Medard Kaleman
  Wananchi wa Kata za Ngwanseri na Ngenge wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Dkt.Medard Kalemani na ujumbe wake wakati wa ziara yake a kukagua utekelezaji wa Mradi wa REA Awamu ya Pili wilayani Muleba.


  Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini Prof.Anna Tibaijuka (kulia) akiteta jambo na Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Dkt.Medard Kalemani ( katikati) mara baada ya kumaliza mkutano wake na wananchi wa Kijiji cha Kishuro. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhandisi Richard Ruyango.


  Wananchi wa Kijiji cha Kishuro Wilaya ya Muleba, wakisoma Jarida la Wakala wa Nishati Vijijini (REA), wakati wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Dkt.Medard Kalemani (hayupo pichani) akieleza utekelezaji wa Mradi wa REA Awamu ya Pili na mipango ya Serikali ya kutekelza REA Awamu ya Tatu.


  Na Asteria Muhozya, Muleba

  Imeelezwa kuwa, Serikali imepanga kutumia Nguzo za Zege katika utekelezaji wa Mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini Awamu ya Tatu, unaotarajia kuanza kutekelezwa kuanzia mwezi Januari, 2017 chini ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

  Hayo yamebainishwa kwa nyakati tofauti na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa mradi wa REA Awamu ya Pili katika Kata za Ngenge na Ngwanseri, Wilayani Muleba Mkoani Kagera, pamoja na kueleza mipango ya Serikali katika utekelezaji wa mradi husika Awamu ya Tatu.

  Dkt. Kalemani amesema kuwa, lengo la kutumia nguzo hizo za zege ni kutokana na uimara wake utakaowezesha upatikanaji umeme wa uhakika na kuepuka kuchomwa na kuongeza kuwa, tayari nguzo hizo zimeanza kutumika katika Mkoa wa Kilimanjaro.

  Akizungumzia utekelezaji wa REA Awamu ya Pili, amesema Serikali imetekeleza mradi huo kwa kasi kubwa kutokana na dhamira yake ya kuhakikisha kuwa, ifikapo mwaka 2025 asilimia 75 ya Watanzania wawe wameunganishwa na nishati hiyo ambayo ni kichocheo cha shughuli za kiuchumi.

  “ REA awamu ya pili imekamilika kwa kiwango kikubwa. Vipo baadhi ya vijiji havijafikiwa kutokana na dosari ndogo ndogo lakini tutavikamilisha kuwezesha utekelezaji wa Awamu ya Tatu. Hata katika Wilaya hii vipo na tayari nimemwelekeza Mkandarasi kukamilisha kazi hiyo haraka,”amesisitiza Dkt. Kalemani.

  Akielezea mipango kwa Awamu ya Tatu, amesema kuwa, Serikali imelenga kuhakikisha kuwa, awamu hiyo inavifikia vijiji vyote ambavyo havikuunganishwa katika Awamu ya Pili, visiwa vyote, Taasisi mbalimbali, Sehemu zinazotoa Huduma za Kijamii zikiwemo za Afya, shule na visima vya maji.

  Aidha, alisema kuwa, kukamilika kwa utekelezaji wa Miradi Ujenzi wa njia za Kusafirisha umeme wa Msongo Mkubwa wa kV 400 kutoka Iringa hadi Shinyanga kupitia Dodoma na Singida kutawezesha upatikanaji wa umeme wa uhakika pamoja na kuchochea uchumi wa viwanda hususan katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

  Wakati huo huo, Dkt. Kalemani ametumia fursa hiyo kuzitaka Halmashauri zote nchini kushirikiana na TANESCO kuweka utaratibu shirikishi ambao utawawezesha wananchi kupata huduma za kuunganishiwa nishati hiyo kupitia utaratibu wa kuanzisha madawati ya TANESCO katika maeneo yatakayotambuliwa ili kuwawezesha wananchi kupata huduma hiyo kwa urahisi.

  “TANESCO na Halmashauri, pangeni namna ya kuwawezesha wananchi kufikiwa kwa urahisi na huduma za kunganishwa nishati ya umeme. Mkubaliane kupanga siku maalum ambayo wananchi watahudumiwa. Serikali inataka kila mwananchi apate umeme, hivyo tuweke utaratibu ambao utarahisisha na kuwezesha azma hiyo kufikiwa kwa haraka,” amesisitiza Dkt. Kalemani.

  Pia, Dkt. Kalemani amewataka Wakandarasi wote wakati wa utekelezaji wa miradi ya Awamu ya Tatu kuhakikisha kuwa, wanajitambulisha katika Halmashauri na Mamlaka nyingine ili waweze kutambulika ili kuepusha udanganyifu.

  Vilevile, Dkt. Kalemani ameitaka TANESCO kuwaidhinisha Wakandarasi wote watakaofanya kazi ya ‘wiring’ katika nyumba za wananchi katika utekelezaji wa REA Awamu ya Tatu ikiwemo kutoa orodha zao ili kuwapunguzia wananchi kero ikiwemo kuwaepusha na utapeli unaofanywa na baadhi ya wasiowaaminifu.

  Akizungumzia Sekta ya Madini, Dkt. Kalemani amewahamasisha wachimbaji wadogo wadogo kujiunga katika vikundi ikiwemo kujisajiri katika Ofisi za Madini zilizopo katika maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kuwawezesha wachimbaji hao kuomba ruzuku kupitia vikundi pindi zinapotolewa na Serikali.

  Katika ziara ya kutembelea Kata hizo, Dkt. Kalemani ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Mhandisi Richard Ruyango, Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, REA, TANESCO na Wakandarasi wanaotekeleza mradi wa REA Awamu ya Pili Wilayani humo.

  0 0


  0 0

  Matroni wa Kituo cha Afya cha Murangi, Sabina Daudi akitoa shukrani kwa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) baada ya kupokea vifaa kwa ajili ya kituo hicho.

  Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akizungumza kabla ya kukabidhi vifaa. Wa kwanza kushoto ni Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Thadeus Makwanda na katikati ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Murangi, Dkt. Josephat Karambo. 
  Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akiwasili katika Kituo cha Afya cha Murangi kwa ajili ya kukabidhi vifaa mbalimbali. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Vicent Naane.
  Baadhi ya Vitanda ikiwa ni miongoni mwa vifaa vilivyokabidhiwa katika Kituo cha Afya cha Murangi.
  Mbunge wa Musoma Vijijini na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesikitishwa na wizi wa dawa na uharibifu wa baadhi ya vifaa katika Kituo cha Afya cha Murangi, Musoma Vijijini na kuagiza wahusika wachukuliwe hatua.

  Agizo hilo alilitoa hivi karibuni wakati akikabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya afya ikiwemo vitanda maalum 10, baisikeli za wagonjwa na vifaa vingine kutoka kwa wafadhili wa Australia kwa ajili ya Kituo hicho na kushuhudiwa na wananchi mbalimbali kutoka maeneo tofauti ya jimbo hilo.

  Awali kabla ya makabidhiano ya vifaa hivyo, alipokea taarifa kutoka kwa wananchi kuhusiana na wizi wa dawa uliomhusisha mlinzi wa Kituo hicho pamoja na tukio la kuharibiwa kwa gari la wagonjwa alilokabidhi mwezi Machi mwaka huu.

  Taarifa husika ilimkasirisha Profesa Muhongo na hivyo kuagiza wahusika wote wachukuliwe hatua za kisheria haraka iwezekanavyo ili iwe fundisho kwa wenye tabia za namna hiyo.Akizungumzia gari hilo, Profesa Muhongo alisema lilitolewa na Serikali ya Japan kwa ajili ya wananchi wa jimbo la Musoma Vijijini lengo likiwa ni kusaidia wananchi hao kuondokana na usumbufu waliokuwa wakiupata.

  Aliongeza kuwa Serikali hiyo ya Japan ilimuahidi magari mengine zaidi ikiwa gari hilo litatunzwa vizuri na kutumika kwa shughuli iliyokusudiwa.“Hii ni aibu kubwa, hata wafadhili watatushangaa na kutucheka, dawa nyingi tulipewa na wafadhili na gari ile tulikabidhiwa ikiwa bado mpya na kwa Tanzania gari za namna hiyo zipo mbili tu, ni hapa na Muhimbili,” alisema.

  Mbali na hilo aliongeza kuwa Serikali ya Japan ilitoa kiasi cha shilingi milioni 170 kwa ajili ya kuboresha Kituo hicho na kuongeza kuwa atamuomba Balozi wa Japan nchini kufanya ukaguzi wa matumizi ya fedha hiyo.Aliwaagiza Madiwani kufuatilia kubaini hatua iliyofikiwa ya matumizi ya fedha hiyo na alisema endapo itadhihirika kuna ubadhirifu wa aina yoyote hatua za kisheria zichukuliwe ikiwa ni pamoja na kurejesha fedha hizo.

  Profesa Muhongo alisema anashangazwa kupewa taarifa hiyo na wananchi huku viongozi wakiwa kimya bila kuonesha hatua walizochukua na hivyo aliwataka Madiwani kutokuwa waoga katika kuwachukulia hatua wanaofanya ubadhirifu.Aidha, Profesa Muhongo aliwaagiza Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Thadeus Makwanda na Kaimu Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Murangi, Dkt. Josephat Karambo kuhakikisha hadi kufikia Tarehe 15 mwezi ujao gari hilo liwe limetengemaa.

  0 0


   Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita a kizungumza na wajumbe wa halmashauri ya jiji na menejiment ya soko la kariakoo baada ya kufanya ziara yake Jana. 
  Mjumbe wa halmashauri ya jiji ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kawe Halima Mdee akichangia jambo mara baada ya kuwasilishwa kwa taarifa ya soko hilo.

    Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akisikiliza taarifa ya soko iliyokuwa ikisomwa Mbele ya wajumbe wa halmashauri hiyo. 

  Ziara ya Meya wa jiji la Dar es SalaamIsaya Mwita, imebaini kuwepo kwa wizi wa fedha katika vizimba vya soko la kariakoo jambo ambalo limeonyesha kulinyima jiji mapato kwa kipindi kirefu.

  Hatua hiyo imekuja baada ya wajumbe wa kamati ya Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kufanya ziara ya kukagua mali za jiji ambapo ikiwa ni mwendelezo wa ziara zilizowahi kufanyika hapo awali.

  Katika kikao hicho ambacho kilifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa soko la kariakoo, Meneja Mkuu wa shirika la soko la Kariakoo Hetson Kips shirika hilo likabaliwa na tatizo la uwezo mdogo wa kifedha jambo linalofanya kushindwa kumudu kuendesha shirika hilo.

  Akizungumza katika kikao hicho, Meya wa Jiji Isaya Mwita licha kuonyesha kukerwa na hali aliyoiona katika soko hilo alimueleza mejena huyo kwamba asifanye mchezo na ujio huo kwani atafanya kwa vitendo nasio kupita tu.

  Isaya alisema anachotaka kukiona ni kwamba wafanye kila njia ili kuhakikisha kwamba jiji linapata fedha badala ya wizi ambao wanaufanya kwani kila kitu kinachoendelea ndani ya soko hilo anafahamu.

  “ Leo tunaongea kirafiki, sitaki kuongea sana, sitawawajibisha hata mmoja, ila kunasiku mtajikuta hampo hapa , narudia tena tukienda mbali zaidi kwa wizi huu ambao mnaufanya hali itakuwa mbaya” alisema Meya Isaya.

  Alifafanua kwamba, hili jambo halijaisha, siku ambayo nitapita tena hakafu jiji pesa hazija ingia ,hali itakuwa mbaya, fanyeni jitihada za kuliwezesha jiji, lipate pesa, msiseme kwamba hakuna pesa mnaendesha soko kwa hasara.

  Awali akisoma taarifa ya soko hilo, Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko Kariakoo, Hetson Kips alisema kwamba wanakabiliwa na tatizo la uwezo mdogo wa kifedha jambo linalofanya kushindwa kumudu shuguli za uendeshaji.

  Alisema hali hiyo ndio imefanya shirika hilo kushindwa kulipa madeni yake kwa wakati na kwamba kwa sasa shirika linakabiliwa na madeni yaliyotokana na huduma mbalimbali yaliyofanywa na wakandarasi wa vipindi vilivyopita.

  Alisema sheria ya shirika hilo ambayo imeshapitwa na wakati imesababisha baadhi ya wafanyabiashara kukataa kuingia mikataba ya upangaji na kuwa wagumu kulipa viwango vya kodi stahiki vitakavyoendana na wakati sambamba na kukidhi gharama za sasa za kiuendeshaji.

  “ Gharama vidogo vya kodi ya pango na ada ya kutumia soko vimekuwa haviendani na hali halisi ya soko kibiashara , pamoja na jitihada za shirika hilo kupandisha viwango kutoka shilingi 8,000 hadi 10,550 ofisi za maduka mwaka 2016 hadi 2017 kwa mita za mraba hadi shilingi 12,500, 14,750 kwa mita mraba kwa ” alisema Meneja.

  Katika taarifa hiyo ilieleza kwamba shirika hilo linamilikiwa na wanahisa wawili ambao ni Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam ambayo inamiliki hisa asilimia 51 ambazo pia hadi sasa hazijalipwa na hazina inayomiliki asilimia 49 na kwamba shirika halipati ruzuku serikalini.

  Taarifa hiyo ilionyesha kuwakera wajumbe wa kikao hicho na kumtaka Meneja aache kuwadanganya kwakuwa ukweli halisi wa jambo hilo wanaujua.

  Diwani wa Kata ya Mbezi Hamfrey Sambo alihoji kwamba “ awali mliwahi kusema kwamba jiji halina hisa na leo hii mnasema kwamba jiji linahisa, uhalali huo mmeutoa wapi” alihoji Sambo.

  Mbali na hivyo, Sambo pia alisema anatambua kwamba vizimba vya kariakoo havipangishwi kwa bei ambayo wanaizungumza mbele ya wajumbe wa kikao na kwamba kuna mapato makubwa ambayo yanapatikana ila kutokana na ujanja ujanja uliopo ndio umefikia hatua hiyo ya jiji kukosa mapato.

  “ Natambua kabisa kwamba hapa mnatupiga pesa nyingi, kuna ujanja ujanja ambao unafanyika , na humu tunajua wapo wakubwa ambao wanavizimba vyao humu, lakini sasa unaposema kwamba kuna hasara ambayo inapatikana hatukuelewi, tunaomba utuambie ukweli” alisisitiza Sambo.

  Mejena Hetson alisema kwamba tangu afike hapo anamiezi miwili , na kwamba tayari ameanza kufanya mazungumzo na menejimenti ya soko hilo na kwamba kikao kitakachofanyika kesho kitakuja na majibu ya mkanganyiko huo.

  Alisema si jambo hilo tu, lakini pia wapo wafanyabiashara wengine ambao mikataba yao imekwisha lakini wanaendelea kufanyabiashara na mbaya zaidi mikataba hiyo inaonekana kusainiwa mara mbili, jambo ambalo alisema ni changamoto kwao.

  Lakini alisema kuwepo kwa hali hiyo kunamfanya kushindwa kuchukua mamuzi, huku wakati mwigine akifikiri kuvunja kwa mikata ya watu hao ili apangishe watu wengine.

  Kwaupande wake Diwani Mariam Mtemvu alishauri kwamba ili kuepukana na hali hiyo, ni vema uongozi huo ukafanya kazi ya kutembelea wafanyabiashara waliopo kwenye vizimba hivyo na kuingia nao mkataba badala ya wale ambao wanakuja kufanya mazungumzo nao kwani kufanya hivyo kutapunguza hali ya wizi wa mapato.

  “ Mfanye jambo, watu ambao wanakuja kuomba vizimba tunafahamu kwamba nawao wanapangisha watu, sasa ili kuondoa hili na jiji likapata mapato, wazungukieni wote ambao wanafanya biashara hapa, muongee nao ndio hao muwape mikataba, watakubali kodi kuongezeka, hawa ambao wanakataa tayari walishawapandishia hivyo hawawezi kurudi

  0 0


  Mpendwa Mteja,
  YAH: KUFUNGWA KWA BENKI SIKU YA JUMAMOSI, 31/12/2016
  Tunapenda kukujulisha kwamba benki itafungwa siku ya Jumamosi, tarehe 31/12/2016. kwaajili ya kupisha uboreshaji wa mfumo wa kiufundi wa benki na huduma zitarejea kama kawaida siku ya jumatatu, tarehe 2/01/2017.
  Ijumaa, 30 Desemba 2016
  Tutakuwa wazi kuanzia saa                           2: 30 Asubuhi -10:00 Jioni
  Jumamosi, 31 Desemba 2016
  Tutafunga kupisha uboreshaji wa mfumo wa kiufundi wa Benki
  Jumatatu , 2 Januari 2017
  Kurejea kwa Huduma
  Unashauriwa kufanya miamala yote ya muhimu kabla ya siku tajwa hapo juu, ili kuepusha ucheleweshaji usio wa lazima.
  Huduma za kibenki kwa njia ya mtandao (Internet Banking), ATMs na Visa cards zitaendela kupatikana kama kawaida katika kipindi tajwa hapo juu.
  Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza na tunawahakikishia dhamira yetu ya kuendelea kuwahudumia ipasavyo. Kwa maelezo Zaidi tafadhali tembelea tawi letu lolote lililo karibu nawe au piga 0782 262 291.
  Tunakutakia Heri ya Mwaka Mpya wa 2017.
  Imetolewa na Utawala
  28.12.2016

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole   Bi Mugwe Mbabe ambaye ni Mke mkubwa wa Marehemu Mzee Maarufu Admirabilis Mbabe Manyama(82) mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Chato mkoani Geita.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa pole Bi. Regina Mbabe mke mdogo wa Marehemu Mzee Maarufu Admirabilis Mbabe (82) Manyama mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Chato mkoani Geita.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Deodatus Manyama wakwanza (kushoto) ambaye ni mdogo wa marehemu Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama(82) mara baada ya kuwasili nyumbani kwa Marehemu Chato mkoani Geita.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Bi. Mugwe Mbabe mke mkubwa wa Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Chato mkoani Geita.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini daftari la maombolezo mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama (82) Chato mkoani Geita
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na kutoa pole katika msiba huo wa Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama mara baada ya kuwasili nyumbani kwake Chato mkoani Geita
   Mdogo wa Marehemu Deodatus Manyama kimshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwapa pole na  kuwafariji kufuatia msiba wa Mpendwa wao Marehemu Mzee Admirabilis Mbabe Manyama
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wafiwa katika msiba huo Chato mkoani Geita.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka msibani mara baada ya kutoa pole. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wananchi akitokea katika msiba huo Chato mkoani Geita.
  PICHA NA IKULU

  0 0

  Na Fredy Mgunda,Iringa .

  MAKUNDI maalumu yanayohusisha vijana, walemavu na wanawake wa mjini Iringa walioingia katika mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa 2015 wakitoa masikitiko yao ya namna vyombo vya habari vilivyowapa nafasi finyu katika mchakato huo.

  Makundi hayo yalikuwa yakijadili ripoti ya tathmini ya jinsi vyombo vya habari (televisheni, magazeti na redio) vilivyoripoti habari zao wakati wakitia nia na kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo iliyofanywa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA).

  Dora Nziku anatoa malalamiko yake kwa kuvilaumu vyombo vya habari mkoani iringa kwa kutowapa nafasi wanawake,walemavu hata wale wasio na kipato kwa kuwa waandishi wengi walikuwa wanajali maslai kuliko ukubwa wa habari
  “Naona kama wanawake tuliathiriwa zaidi katika mchakato huo kwani habari zetu hazikupata nafasi kama ilivyo kwa wagombea wengine hasa wanawake,” alisema Diwani wa Viti Maalumu Iringa Mjini, Dora Nziku (CCM).

  Nziku alisema imekuwa ni jambo la kawaida kwa baadhi ya wanahabari kuomba hela kwa wagombea na viongozi wa kisiasa ili waweze kutoa habari zao.“Pamoja na kuwapa hela wakati mwingine habari hizo hazitoki na mimi ni mmoja wa wahanga wa hilo, nimewahi kuita wanahabari, wakaniomba hela lakini hawakutoa habari zangu na nadhani hazikutoka kwasababu mimi ni mwanamke,” alisema diwani huyo bila kutaja wanahabari hao.

  Naye Agusta Mtemi aliyekuwa mgombea udiwani viti maalumu mjini Iringa (CCM) alisema katika kinyang’anyiro hicho aliwashinda kwa kura 266 wagombea wenzake zaidi ya 10 lakini katika mazingira tata alionekana kama mshindi namba mbili na kukosa nafasi ya kuwawakilishi wanawake wenzake katika Baraza la Madiwani la Jimbo la Iringa Mjini.

  Naye Imelta Mhanga kijana aliyegombea udiwani viti maalumu (CHADEMA) mjini Iringa alilaumu mchakato ndani ya chama akisema unawanyima uhuru wa kuongea na vyombo vya habari hasa wanapofanyiwa figisufigisu.“Ndani ya taasisi kuna vitisho, kwamba shughuli za chama ni siri ya chama, hazitakiwi kutoka nje. Kwahiyo tunaogopa kukutana na wanahabari,” alisema huku akipinga kwamba wanahabari wanataka fedha mara zote ili kutoa habari zao.

  Kwa upande wake, Selekti Sinyagwa ambaye ni mlemavu wa miguu aliyegombea udiwani viti maalumu ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) alisema; “kwa kweli walemavu tunabaguliwa sana katika mchakato wa kupata viongozi, jambo hili linatufanya tujione kama ni jamii tofauti na jamii tunayoishi nayo.”

  Afisa Miradi wa TAMWA, Reonida Kanyuma alisema taasisi hiyo iliangalia namna makundi hayo yalivyoripotiwa katika vyombo vya habari ili kwa kushirikiana na wadau waje na suluhisho litakaloondoa tofauti zilizopo.“Tulifanya ufuatiliaji katika mchakato huo, na kuona jinsi wanawake, walemavu na vijana walivyoripotiwa katika vyombo hivyo vya habari ikilinganishwa na wagombea wanaume katika nafasi za udiwani, ubunge na urais waliopewa nafasi,” alisema.

  Alisema kwa kuwa mwisho wa uchaguzi mmoja ni mwanzo wa uchaguzi mwingine, vyombo vya habari havipaswi kuwabagua wagombea kwa kuangalia udhaifu wao au mfumo dume na badala yake vitoe fursa sawa kwa kuzingatia uwezo na dhamira waliyonayo katika kuwatumikia watu wengine.

  “Ni matarajio ya TAMWA na wadau wote wa maendeleo kwamba sekta ya habari itatenda haki kwa kutoa nafasi sawa kwa wagombea wote katika chaguzi zijazo,” alisema.
  Baadhi ya washiriki walikuwa wakijadili ripoti ya tathmini ya jinsi vyombo vya habari (televisheni, magazeti na redio) vilivyoripoti habari zao wakati wakitia nia na kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi Mkuu wa 2015 na mjadala huo uliongozwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA).

older | 1 | .... | 1083 | 1084 | (Page 1085) | 1086 | 1087 | .... | 1898 | newer