Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live

MSAMA AVIKUMBUKA VITUO VYA WATOTO YATIMA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Bw. Alex Msama akikabidhi msaada wa chakula kwa Bi.Zainab Bakari mlezi wa kituo cha kulea watoto yatima cha Maunga Yatima Centre kilichopo Kinondoni jijini Dar es salaam wakati alipotembelea kituoni hapo na kuzungumza na watoto, Msama aligawa chakula pia katika vituo vya Honorata Temeke, Shifaa Bunju na Mwandalio kilichopo Temeke Vetenary vyote vya jijini Dar es salaam.
 
Msama ametoa wito kwa watu mbalimbali wenye uwezo kwa namna yoyote wajitokeze kuwasaidia watoto yatima na wasiojiweza kwa kutoa misaada mbalimbali ili jamii hiyo nayo ifurahie msimu wa sikukuu kwa furaha kama wengine.
 Bw. Alex Msama akikabidhi msaada wa chakula kwa kituo cha Shifaa -Bunju.
 
  Bw. Alex Msama akiwaasa watoto wa kituo cha Honorata kutoka Temeke,wakasherehekee sikukuu kwa upendo na amani na kwa umoja wao wakamshukuru Mungu kwa kila jambo.
Bw. Alex Msama akikabidhi msaada wa chakula kwakituo cha Mwandalio cha Vetenary Temeke.

MUSOMA VIJIJINI WAJISIFU WALICHAGUA JEMBE,WAMMWAGIA SIFA PROF. MUHONGO

$
0
0

Mzee wa Kijiji cha Murangi- Musoma Vijijini, Clifford Biseko (kulia) akifungua rasmi mkutano wa kujadili uchumi na maendeleo ya Jimbo la Musoma Vijijini. Wa kwanza kushoto ni Mbunge wa Jimbo hilo, Profesa Sospeter Muhongo.
Madiwani wa Musoma Vijijini wakijitambulisha wakati wa mkutano wa Tathmini ya Maendeleo na Uchumi ya Jimbo la Musoma Vijijini. Wa kwanza kushoto ni Mbunge wa Jimbo hilo na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Wadau wa maendeleo ambao pia ni wazaliwa wa Musoma Vijijini lakini wanaishi nje ya hapo wakijitambulisha. +
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Musoma, Flora Yongolo akitambulisha watendaji mbalimbali kutoka kwenye halmashauri hiyo.


Baadhi ya wananchi wa Musoma Vijijini waliohudhuria mkutano huo wakimsikiliza Mbunge wao, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani).



Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini wamempongeza Mbunge wao na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kwa kufanya mambo makubwa ya kimaendeleo ndani ya mwaka mmoja.

Pongezi hizo zimetolewa na wananchi wa jimbo hilo wakati wa mkutano wa Tathmini ya Maendeleo na Uchumi ya jimbo uliofanyika hivi karibuni katika Kijiji cha Murangi, Musoma Vijijini na kushirikisha wananchi wa jimboni humo, madiwani, wadau wa maendeleo na watendaji wa Halmashauri husika.

Awali akifungua mkutano huo mzee wa Kijiji cha Murangi, Musoma Vijijini, Clifford Biseko alisema wanamusoma vijini wanajivunia maendeleo yanayodhihirika kila kukicha kutokana na mchango wa mbunge huyo. Aliongeza kwamba Profesa Muhongo ni mtu sahihi kwa nafasi hiyo na kuwa hawajuti kumchagua na wanamwombea afya njema ili azidi kushirikiana nao katika kusukuma gurudumu la maendeleo jimboni humo.

Alisema katika kipindi kifupi cha uongozi wake, wameshuhudia masuala makubwa ya maendeleo kwenye sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu, kilimo, sanaa na michezo. Akizungumzia suala la afya, Biseko alisema, Musoma Vijijini haikuwahi kuwa na gari hata moja la wagonjwa lakini tangu Profesa Muhongo awe Mbunge tayari jimbo hilo linayo magari manne.

Aliongeza kuwa Musoma vijijini haikuwahi kupata ugeni wa madaktari bingwa kwa ajili ya vipimo, ushauri na matibabu lakini kwa Profesa Muhongo hilo liliwezekana kwani alikaribisha madaktari bingwa kutoka ndani na nje ya nchi ambao walitoa huduma bila malipo.

Kuhusu suala la kilimo, Biseko alisema, tangu Profesa Muhongo achaguliwe, alisambaza tani kadhaa za mbegu za zao la mihogo na alizeti ili wananchi wajikwamue kwenye umasikini. Aliongeza kuwa, Profesa Muhongo alipeleka wataalamu mahiri wa kilimo kutoka ndani na nje ya nchi ili kufanya tathmnini ya kilimo bora ikiwa ni pamoja na kutoa ushauri wa kilimo bora.

Aidha, suala la elimu, Biseko alisema kuwa kulikuwa na uhaba wa madawati 8,000 kwa shule zote zilizomo jimboni humo na hilo lilitatuliwa bila wao kuchangishwa pia kusambaziwa shehena ya vitabu vya sayansi kwa shule zote. Biseko alimalizia kwa kuzungumzia sekta ya michezo na sanaa alisema kuwa Mbunge ameandaa mashindano mbalimbali na vilevile kugawa vifaa vya michezo kwenye vijiji mbalimbali jimboni humo jambo ambalo alisema limehamasisha sekta husika.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI MKOANI LINDI KWA ZIARA YA KIKAZI KATIKA WILAYA YA RUANGWA

$
0
0
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Lindi Godfrey Zambi mara alipowasili katika uwanja wa ndege wa Nachingwea kwa ajili ya ziara ya kikazi katika wilaya ya Ruangwa Mkoani lindi kushoto ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi  Alli Mohamed Mtopa
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na mkurugenzi wa Nachingwea (DED) Bakari Mohamedi Bakari katika kiwanja cha ndege cha Nachingwea wakati wa mapokezi ya waziri mkuu wilayani hapo waziri mkuu amefika kwa ziara ya kikazi katika wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi 
Waziri mkuu Kassim Majaliwa na mkewe Mery Majaliwa wakifurahia ngoma ya kikosi cha JKT  843KJ kilichopo Nachingwea ambacho kilikuwepo katika mapokezi ya Waziri Mkuu katika uwanja wa ndege wa Nachingwea .Picha na Chris Mfinanga

MAANDALIZI YA MAZISHI YA MPENDWA WETU MPOKI BUKUKU HUKO KIJIJINI KWAO MSALATO-MKOANI DODOMA

$
0
0
 Maziko ya Mpigapicha Mpoki Bukuku yanatarajibkufanyika leo Kijijini kwao Msalato Dodoma yalipo makazi ya mamavyake nabyalipo makaburi ya Familia likiwepo la Baba yake na kaka yake. Tayari waombolezaji wameshaanza kuwasili na taratibu za mazishi zinaendelea.
Wamama wa Kinyakyusa wakiimba kuzunguka Jeneza la Marehemu Mpoki Bukuku.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa nyumba ya muda ya Mpoki Bukuku.
Waombolezaji wakiwa katika eneo itakapofanyika ibada ya mazishi pamoja na eneo la makaburi.
Mpigapicha Mroki Mroki akisaini kitabu cha maombolezo, Msalato Dodoma.
Mpigapicha John Bukuku nae akisaini  cha maombolezo.
Mpigapicha Emmanuel Herman nae akisaini kitabu.
Mohamed Mambo, Mpigapicha nae akisaini Kitabu cha Maombolezo.

ASAKARI JESHI NA WANAHABARI WALIVYOSHEREHEKEA MIAKA 55 YA UHURU KATIKA KILELE CHA UHURU ,MLIMA KILIMANJARO.

$
0
0
Safari ya kuekea kilele cha Uhuru inaanza majira ya saa 5:00 usiku kwa kuianza safafri kutoka Kibo Hut.
Safari ilikuwa ni usiku kucha 
Jua likachomoka wakati safari ikiendelea.
Kadri kulivyokucha ndivyo washiriki walivyoendelea kupata nguvu ya kuendelea na safari ya kufika Uhuru Peak.
Matumaini yakaana kuonekana baada ya alama ya Gilmans Point kuanza kuonekana.
Mdogo mdogo ndo ilikua kauli ya kuongeza morali kwa wapandaji.
Gilmans Point hatiaye washiriki wakafika lakini hii ni hatua ya kwanza bado hatua mbili ili kufika Uhuru Peak.
Miongoni mwa waliofika Gilmans Point ni Naibuu Kamanda wa kikosi cha nchi kavu cha jeshi la Ulinzi ,Brigedia Jenerali ,Jairo Mwaseba.
Safari ya kueelkea Uhuru Peak ikaendelea.
Hatimaye wapandaji wakapita kituo chha Pili ambachi ni Stella na mongoni mwa waliofika hapa ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Balozi Charles Sanga.
a Safari ilivyoendelea kuelekea Uhuru Peak ,safu ya vilima vikiwa vyenye barafu ndio vilitawala eneo hilo.
Hatimaye safari ya siku sita ya Wanahabari na askari wa jeshi la Ulinzi ya kupanda Mlim Kilimanjaro kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanganyika ikafika tamati.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini aliykuwepo katika safari hiyo.

Waziri Mahiga apokea Dola elf 50,000 kwa ajili ya Waathirika wa Kagera

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi, Dkt. Augustine Mahiga akihutubia katika hafla ya makabidhiano ya mchango uliotolewa na Ubalozi wa Korea kwa ajili ya kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Kagera mwezi Septemba, 2016 na kusababisha madhara makubwa, Makabidhiano hayo yamefanyika leo katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere.Kushoto ni Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini, Mhe.Song Geum Young 
Waziri Mahiha akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya Dola za Marekani elf 50 (shillingi millioni 108) kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Korea, Mhe. Song.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo y Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga akiratibu hafla hiyo. 
Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia hafla ya makabidhiano, Kutoka kushoto ni Bw. Halmenshi Lunyumbu, Bw. Assah Mwambene, Bw. Ally Kondo na Bw. Freddy Maro. 
Hafla ya makabidhiano ikiendelea. 
Picha ya pamoja.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Serikali ya Jamhuri ya Korea imetoa msaada wa Dola za Marekani elf 50,000 takribani milioni 108 kwa fedha za Tanzania kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi lilitokea mkoani Kagera mwezi Septemba 2016.

Msaada huo ulikabidhiwa leo jijini Dar es Salaam na Balozi wa Korea nchini Tanzania, Mhe. Song Geum Young na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb) kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb).

Baada ya kupokea msaada huo, Dkt. Mahiga aliishukuru Serikali ya Korea na kuahidi kuwa msaada huo ataukabidhi kwa Mhe. Waziri Mkuu ili uweze kutumika kama ulivyokusudiwa.

Mhe. Mahiga alisema kuwa Korea imekuwa mbia mkubwa wa Tanzania tokea nchi hiyo ilipoanzisha mahusiano ya kidiplomasia na Tanznaia miaka 25 iliyopita. Alieleza kuwa katika kipindi hicho Tanzania imekuwa ikipokea misaada mbalimbali ya kiuchumi, kijamii na ya kibinadamu ukiwemo huu wa leo ulioelekezwa kwa waathirika wa tetemeko la ardhi la mkoani Kagera. 

Mhe. Waziri alitaja misaada ambayo Korea imeipatia Tanzania ni pamoja na ujenzi wa daraja la Malagarasi mkoani Kigoma, ujenzi wa hospitali ya kisasa ya Mloganzila na ujenzi wa hospitali ya uchunguzi wa afya ya Mama iliyopo Chanika. Aidha, Korea hivi karibuni itaanza ujenzi wa daraja la Selander ambalo linatarajiwa kuanzia ufukwe wa Coco, Oysterbay hadi maeneo ya hospitali ya Aga Khan, Upanga jijini Dar es Salaam.

Waziri Mahiga alibainisha pia kuwa Jamhuri ya Korea itatoa msaada mkubwa zaidi wa maendeleo kwa Tanzania kuliko nchi yeyote ya Afrika. Taarifa hiyo ilitolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea, Mhe. Yun Byung-se alipofanya naye mazungumzo kando ya Mkutano wa nchi za Afrika na Korea uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia tarehe 06 na 07 Desemba 2016.

Kwa upande wake, Balozi wa Korea nchini aliahidi kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania hususan kutoa atia misaada ya maendeleo ili iweze kutimiza azima ya Serikali ya awamu ya tano ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 27 Desemba 2016.

Tujue ' blood Group ' zetu - Maana Hatujui Siku na Saa- Zitto Kabwe

$
0
0
Usiku wa kuamkia tarehe 26 Desemba 2016 mke wangu alipata uchungu wa uzazi. Nikampeleka hospitali moja hapa Masaki. Hakuweza kujifungua siku hiyo bali tulikaa hospitali mpaka tarehe 27 Desemba, saa moja dk 45 asubuhi alipojifungua mtoto wetu wa kike Josina- Umm Kulthum. 

Masaa ya jioni tarehe 26/12/2016 nikiwa napiga soga na Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Msafiri Mtemelwa na shemeji yangu mmoja mbele ya hospitali, wakaja watu 3. Watu hao mmoja mwanaume na wengine wanawake walikuwa na mtoto mdogo. Mwanaume huyu alikuwa amembeba mtoto akiwa na taharuki kubwa na mama mmoja mtu mzima na mwengine wa umri wa miaka 30 hivi walikuwa wakilia. Wakaingia hospitalini kwa kasi. Tukaambiana pale kuwa huyu binti atakuwa mahututi. Tukaendelea na soga. 

Mara kina mama wale wakatoka, wanapiga mayowe "mtoto hana damu" na ilitakiwa damu ya haraka Group A+. Wenzangu hawakuwa group hilo au group linaloweza kupeana damu. Mimi sikuwa najua/kukumbuka Group langu. Nikawaambia kina mama wale kuwa ngoja nijaribu kupima group langu na pia kuona kama damu yangu inaweza kuokoa maisha ya mtoto yule malaika za mungu. Nikaingia maabara nikapima. 

Baada ya dakika 10 Hivi nikaitwa kuambiwa damu yangu ni group sawa na mtoto yule na kwamba ni safi inafaa wanitoe muda ule ule ili kumuwahi mtoto. Nikatoa nusu lita muda ule ule. Baadaye nikaenda kumjulia Hali mtoto yule, nikaambiwa anaitwa Rahma. Ana umri wa miaka 2 na miezi 3. Nikawatakia kheri wazazi wake ( kumbe yule mwanaume ndie baba wa mtoto na msichana mama yake. Yule bi mkubwa nadhani ni bibi ya Rahma, sina hakika).

Leo asubuhi baada ya mke wangu kujifungua, nikaenda kumwona Rahma wodini. Nimemkuta anaendelea vizuri, anakula na kuongea. Mola ampe umri mrefu zaidi yeye na wazazi wake. Amwondolee maradhi na akue katika maadili mema ya dini. 

Namshukuru mola kuniweka mahala sahihi na wakati sahihi hivyo kuweza kufanya ibada hii ya kumsaidia binti Rahma. Lau kama sikuwa nimechagua jina la binti yangu mapema, ningemwita Rahma. Hata hivyo inshallah Rahma atakuwa dada yake Umm Kulthum-Josina.

Naishauri Serikali itengeneze kanuni za kuhakikisha kila hospitali inakuwa na akiba ya damu ya kutosha na mgonjwa mwenye kuhitaji apewe kwanza damu kabla ya kutafuta watu wa kuchangia kiwango husika. Juhudi za kuchangia damu kwa hiari ziongezeke kama tufanyavyo wanachama wa ACT Wazalendo ambao kila mwaka  Wiki ya kwanza ya Mwezi Mei hujitolea damu kwa hiari kwenye hospitali za umma nchini kote. 

Pia nimepata somo kubwa kwamba ni muhimu Sana kujua Group lako la damu na kuwa na kumbukumbu nalo kwani inaokoa muda pindi damu ikitakiwa kwa haraka. Sasa najua Group langu, ilikuwa ni makosa makubwa na uzembe wa hali ya juu kwangu kutojua ' blood group ' yangu. Nawasihi Watanzania wenzangu na mie msiojua blood group, mjue sasa kwani hatujui Siku wala Saa.

Heri ya mwaka mpya 2017

Zitto Kabwe ( Baba Josina Machel)
27/12/201

WADAU KAZUMARI NA SADA WAUAGA UKAPERA JIJINI MWANZA

$
0
0
 Hatua ya Sada Almasi Shomary na mumewe Kazumari Malongo, harusi ilifanyika jijini Mwanza katika Msikiti Sheikh Amin Mtaa wa Rufiji na kufuatiwa na tafrija iliyofanyika katika Hoteli ya Gold Grest jijini Mwanza
Hatua ya Sada Almasi Shomary na mumewe Kazumari Malongo, harusi ilifanyika jijini Mwanza katika Msikiti Sheikh Amin Mtaa wa Rufiji na kufuatiwa na tafrija iliyofanyika katika Hoteli ya Gold Grest jijini Mwanza
Bibi Harusi Sada Almasi Shomary akikata keki wakati wa mnuso uliofanyika  katika Hoteli ya Gold Grest jijini Mwanza
Bi Harusi akizungumza jambo ukumbini humo mbele ya wageni mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo
Bwana Harsi Kazumari Malongo akimvalisha pete ya ndoa mkewe Bi' Sada Almasi Shomary na , katika tafrija iliyofanyika katika Hoteli ya Gold Grest jijini Mwanza





TAARIFA YA KUPOTEA KWA MTOTO DAMIAN JAMES WA KATORO MKOANI GEITA

Zantel watembelea wateja wao mjini Unguja

$
0
0
  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zantel Tanzania, Benoit Janin (katikati), akizungumza na  baadhi ya wateja na mawakala wa kampuni hiyo mjini Zanzibar nje ya Soko la Malindi jana, ili kupata mawazo yao juu ya ubora wa huduma na bidhaa za Zantel wazipatazo na jinsi ya kuzoboresha.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zantel Tanzania, Benoit Janin (katikati), pamoja na baadhi ya maofisa wa kampuni hiyo wakimsikiliza mmoja wa mawakala wao, Juma Abdallah Safi (kulia), nje ya Soko la Malindi, Zanzibar  jana, walipokwenda kuwatembvelea mawakala na wateja wa kampuni hiyo ili kupata mawazo yao juu ya ubora wa huduma na bidhaa za Zantel wazipatazo na jinsi ya kuzoboresha.     
  Mkuu wa Zantel, Mohamed Khamis Baucha (kulia), akizungumza na baadhi ya wateja wao nje ya soko la Malindi, Zanzibar jana  walipokwenda kuwatembvelea mawakala na wateja wa kampuni hiyo ili kupata mawazo yao juu ya ubora wa huduma na bidhaa za Zantel wazipatazo na jinsi ya kuzoboresha.     
 Meneja Biashara Wateja wa Makampuni wa Zantel Kassongo Faraji (kulia), Ofisa Mauzo na Usambazaji, Mabuga Abdallah (wa pili kulia), wakimsikiliza mmoja wa mawakala wa Zantel mjini Zanzibar jana walipokwenda kuwatembvelea mawakala na wateja wa kampuni hiyo ili kupata mawazo yao juu ya ubora wa huduma na bidhaa za Zantel wazipatazo na jinsi ya kuzoboresha.   
 Mkurugenzi wa Huduma ya Ezypesa ya Zantel, Hamad Shehe (katikati), akiwa na Mkurugenzi wa Mauzo wa kampuni hiyo, Herbert Louis (kushoto kwake),  wakimsikiliza mmoja wa mawakala wa Zantel mjini Zanzibar, Juma Abdallah Safi walipokwenda kuwatembvelea mawakala na wateja wa kampuni hiyo jana, ili kupata mawazo yao juu ya ubora wa huduma na bidhaa za Zantel wazipatazo na jinsi ya kuzoboresha.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zantel Tanzania, Benoit Janin (katikati) Mkuu wa Mauzo, Herbert Loius (kushoto kwake), pamoja na maofisa wengine wa kampuni hiyo   wakimsikiliza mmoja wa mawakala wa Zantel mjini Zanzibar, Juma Abdallah Safi (wa pili kulia),  walipokwenda kuwatembvelea mawakala na wateja wa kampuni hiyo jana, ili kupata mawazo yao juu ya ubora wa huduma na bidhaa za Zantel wazipatazo na jinsi ya kuzoboresha.  
Mkuu wa Mauzo wa Zantel, Herbert Louis (kushoto), akimpiga picha mmoja wa mawakala wao mjini Zanzibar, Salum Omar Ali (kulia) ili kumuonyesha ubora wa moja ya program za Zantel zinavyofanya kazi kupitia mtandao walipokwenda kuwatembvelea mawakala na wateja wa kampuni hiyo jana, ili kupata mawazo yao juu ya ubora wa huduma na bidhaa za Zantel wazipatazo na jinsi ya kuzoboresha. Wa pili kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zantel, Benoit Janin

MAREHEMU MPOKI BUKUKU AZIKWA NYUMBANI KWAO MSALATO MKOANI DODOMA

$
0
0
01
Alice Mama wa Marehemu Mpoki Bukuku akisaidiwa kuweka shada la maua katika kaburi la mwanaye Mpoki Bukuku wakati wa mazishi hayo yaliyofanyika Msalato nje kidogo ya mji wa Dodoma Marehemu Mpoki alifariki hivi karibuni jijini Dar es salaam kwa kugongwa na gari maeneo ya Mwenge.
1
Watoto wa Marehemu Mpoki Bukuku Junior akiongozana na wadogo zake wakiweka shada la maua katika kaburi la baba yao wakati wa mazishi yaliyofanyika Msalato nje kidogo ya mji wa Dodoma.
2
Junior akiwa ameshikili msalaba kwa majonzi wakati wa mazishi ya baba yake.
3
Mke wa Marehemu Mpoki Bukuku Bi. Lilian na watoto wake wakiaga mwili wa marehemu Mpoki Bukuku.
4
jeneza lenye Mwili wa marehemu Mpoki Bukuku likiteremshwa kaburini.
5
Mbunge wa Singida Mashariki Mh Lazaro Nyalandu akiweka udongo kwenye kaburi la marehemu Mpoki Bukuku.
6
Mke wa Marehemu Bi Lilian akiweka udongo kwenye kaburi la marehemu mumewe.
78
Viongozi wa Dini wakiwa katika ibada hiyo ya mazishi.
9
Ndugu na jamaa waombolezaji wakiomboleza kwa uchungu mkubwa.
1012
Naibu Waziri Anthony Mavunde pamoja na mbunge wa Singida Mashariki Mh. Razalo Nyalandu wakiombea mwili wa marehemu Mpoki Bukuku.
13
Waombolezaji wakiaga mwili wa marehemu
16
Junior akiaga mwili wa baba yake Marehemu Mpoki Bukuku.
1718
Mama wa Marehemu Mama Alice akiaga mwili wa mtoto wake mpendwa marehemu Mpoki Bukuku.
19
Waombolezaji wakiwa katika mstari wa kuaga mwili wa marehemu.
20
Naibu Waziri Anthony Mavunde pamoja na mbunge wa Singida Mashariki Mh. Razalo Nyalandu wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Mpoki Bukuku.
21
Naibu Waziri Anthony Mavunde akitoa salam za pole kwa wafiwa.
22
Naibu Waziri Anthony Mavunde akisaini kitabu cha maombolezo.
23
Mpiga picha wa magazeti ya Serikali TSN Habari Leo na Dairly News Bw. Mroki Mroki akitoa salamu za pole kwa wafiwa kwa niaba ya chama cha wapigapicha.
24
Bw. John Bukuku akitoa salamu za pole kwa wafiwa kwa niaba ya Wanamitandao
25
Mwenyekiti wa Press Club ya waandishi wa habari mkoani Dodoma Bw. Chidawali akitoa salamu zake kwa niaba ya wanahabari mkoani humo.
26
Mbunge wa Singida mjini Mh. Lazaro Nyalandu akitoa salam za pole kwa wafiwa.
27
Waombolezaji wakiwa katika mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu Mpoki Bukuku.

MWENYEKITI MPYA WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI ALIPOZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI NA WATENDAJI WA TUME

Kora ya ipiga jeki Serikali ya Tanzania msaada wa Dola elfu hamsini kusaidia waathirika wa tetemeko la Ardhi mkoani Kagera

$
0
0
Na Amina Kibwana-Globu ya Jamii
 
Serikali ya Tanzania imepokea pokea msaada wa hundi ya dola 50,000 (Dola elfu hamsini) kutoka katika  ubalozi wa jamuhuri ya Korea kwa ajili ya kukabiliana na  athari zilizotokana na tetemeko la ardhi Mkoani Kagaera, ili kuweza kurekebisha Miundo mbinu,makazi ya watu pamoja na shule.

Akizungumza na waandishi wa habari Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki kikanda na Kitaifa Dk.Augustine Mahinga amesema serikari ya korea ni mdau mkubwa  hasa ktk misaada ya  kimaendeleo, kiuchumi , ustawi wa jamii na katika misaada ya kibinadamu ikiwa ni pamoja kusimamia ujenzi wa hospitali ya logazila na chanika.

“Tumekuwa tukipokea misaada mbalimbali kutoka kwa marafiki lakini huu ni mchanngo wa hivi karibuni kutoka kwa wenzetu wa korea  ambapo leo nimepokea hundi hii kwa niamba ya waziri mkuu na serikali ya Tanzania kwa ujumla.”

Hata hivyo Dk mahinga aliongeza kuwa hundi hiyo ni zawadi kubwa kwa wanachi wetu hasa wa kagera  pamoja na kutoa shukrani zake kwa balozi wa korea na kuahidi kuwa kuendelea  kufanya kazi kwa pamoja.

Kwa upande wake balozi wa jamuhuri ya korea song Young amesema kuwa kutokana na ushirikiano wao wa muda mrefu Korea imeamua kutoa msaada huo, Korea imeamua kwamba katika kuendeleza ushirikiano wa maendeleo na nchi za afrika Tanzania itapewa kipaumbele na kuwa ni chi ya kwanza kwa afrika ili kudumisha ushirikiano kati ya Jamuhuri ya Korea na tanzania.

huu ni mwaka wa 25  tangu jamuhuri ya korea kuanzisha ubalozi wao nchini Tanzania,ambapo ili kudumisha ushirikiano huo,  Serikali ya Tanzania kupitia Rais wake Dk John Pombe Magufuli  nayo inatarajia kuanzisha  ubalozi wake huko soo mji mkuu wa korea kusini mapema mwaka 2017.

Dk.Shein akutana na Balozi Mdogo wa Oman

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Balozi Mdogo wa Oman katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayefanyia kazi zake Zanzibar Mhe,Ahmed Bin Humoud Al Habsi, alipofika Ikulu Mjini Unguja leo kujitambulisha.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akibadilishana mawazo na Balozi Mdogo wa Oman katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayefanyia kazi zake Zanzibar Mhe,Ahmed Bin Humoud Al Habsi, baada ya mazungumzo yao alipofika Ikulu Mjini Unguja leo kujitambulisha.Picha na Ikulu, Zanzibar.

WAZIRI MKUU AHOJI KUCHELEWESHWA KULIPWA KWA WAKULIMA WA KOROSHO

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema atamuita Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho, Bw. Hassan Jarufo ili aje amueleze ni kwa nini wakulima wa zao hilo wanacheleweshewa malipo yao kinyume na maagizo ya Serikali.

Ametoa kauli hiyo leo mchana wakati akizungumza na viongozi na watendaji wa mkoa wa Lndi mara baada ya kupokea taarifa ya mkoa huo kwenye Ikulu ndogo wilayani Nachingwea. Waziri Mkuu amewasili wilayani Nachingwea akiwa njiani kuelekea Ruangwa kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka.

“Niliagiza wanunuzi waje na bond (dhamana ya mauzo), waziweke benki ndipo waingizwe kwenye mnada. Kwa maana hiyo mnada ukimalizika, benki inakata fedha husika na kuingiza kwenye chama cha wakulima.”

“Hapa tatizo ni kwamba hatukusimamia vizuri zuala hili. Tulipaswa tujiridhishishe kwanza kama mnunuzi amelipa fedha benki. Tatizo la biashara hii watu wengi ni madalali, wanaangalia hali ikoje na wakibaini kuna cha juu, ndiyo anaagiza na kuamua kuja kulipa. Kama angekuwa amelipa benki, ile hela ya awali ingekatwa katika fedha ya dhamana aliyokwishaitoa,” amesisitiza.

Oktoba 16, 2016 wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja cha Sokoine wilayani Nachingwea, mkoani Lindi, Waziri Mkuu alisema alishatoa maelekezo tangu Aprili, mwaka huu kwamba wanunuzi wa korosho ni lazima watoe asilimia 25 ya malipo wanayotaka ili kuepuka tatizo la madalali kuingilia kati biashara hiyo.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi na Wakuu wote wa wilaya za mkoa huo wawahimize wakulima wapande miche mipya ya korosho kwa sababu mikorosho iliyopo imezeeka na haitoi mazao ya kutosha.

“Mnatakiwa muwahimize wananchi wapande miche mipya mara tu mvua zitakapoanza ili ianze kukua wakati wakusubiria kung’oa ile ya zamani. Nimeambiwa korosho bora hazipaswi kuzidi punje 190 ili zijae kwenye kilo  moja. Ubora wa miti ya korosho ukishuka na idadi ya punje pia inapungua,” amesema.

Amesema kigezo kikuu cha ununuzi wa korosho hivi sasa ni idadi ya punje na kwa Ruangwa na Nachingwea, idadi inakuwa kubwa kwa sababu punje zake ni ndogo. “Wenzetu wa Tandahimba walipanda miche mipya tangu miaka minne iliyopita kwa hiyo sasa hivi wanavuna korosho zenye ubora,” ameongeza.

Amempongeza Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk. Charles Tizeba kwa uamuzi wake wa kuvunja mfuko wa wakfu wa korosho (CIDTF) na akamtaka afute mifuko kama hiyo kwenye mazao mengine kama katani, chai na kahawa kwani inafanya kazi ambazo zinaweza kufanywa na bodi za mazao hayo.

“Waziri Tizeba alishaanza na zao la pamba, sasa aende kwenye mazao mengine ili fedha ambazo watu wa mfuko huu walikuwa wakizitumia kulipana posho tu, sasa ziende kwenye bodi kuhamasisha wakulima walime zaidi na ikibidi wapewe hata mashine za kupulizia dawa,” ameongeza.

WALIOFAULU NI LAZIMA WAENDE SEKONDARI – MAJALIWA

$
0
0
*Asema atafuatilia ajue kwa nini kuna tozo kwenye maghala ya Serikali

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haitavumilia kuona mamia ya vijana waliofaulu mitihani ya darasa la saba na kuchaguliwa kuingia kidato cha kwanza wanabaki nyumbani eti kwa kuwa hakuna madarasa ya kutosha.

“Serikali haitaridhika kuona vijana waliofaulu vizuri wanashindwa kwenda kidato cha kwanza. Halmashauri zilijua tangu mapema ni wanafunzi wanaenda shule za msingi kwa hiyo inataka kuona wote waliofaulu wanakwenda sekondari kwa asilimia 100,” amesema.

Ametoa kauli hiyo leo mchana wakati akizungumza na viongozi na watendaji wa mkoa wa Lndi mara baada ya kupokea taarifa ya mkoa huo kwenye Ikulu ndogo wilayani Nachingwea. Waziri Mkuu amewasili wilayani Nachingwea akiwa njiani kuelekea Ruangwa kwa mapunziko ya mwisho wa mwaka.

Amesema Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kutoa elimu ya bure kwa kila mtoto sasa iweje watoto wengine wanafaulu na wanashindwa kujiunga na elimu ya sekondari. “Tumesema elimu ni bure hakuna sababu ya kufanya wengine wasiende shule wakati azma ya Serikali ni kutoa elimu ya bure. Hakikisheni wote wanaingia katika chaguo la kwanza,” amesema.

Amewataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri ambazo zimefaulisha wanafunzi lakini hazina madarasa na madawati ya kutosha warudi mezani na kujipanga upya ili kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu wanapangwa na kuanza na wenzao katika chaguo la kwanza kwani wakisubiri chaguo la pili wanakuwa wamechelewa.

“Kama tumepokea vijana wengi kwenye udahili wa kidato cha kwanza, ni dhahiri kuwa ,tutapata Vijana wengi watakaomaliza kidato cha nne. Sote tunajua kuna agizo la kila tarafa kuwa na sekondari moja ya kidato cha tano na sita, nataka utekelezaji wa agizo hili usimamiwe kuanzia sasa.”

“Tafuteni moja kati ya shule kwenye tarafa zenu na ipandishwe hadhi kwa kuwekewa miundombinu inayotakiwa ya bwalo, jiko, mabweni, mifumo ya maji, madarasa na vyoo vya kutosha,” amesema.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema atafuatilia ili abaini ni kwa nini taasisi ya maghala ya Serikali inadai tozo kwa wakulima wanaohifadhi mazao kwenye maghala hayo.

Waziri Mkuu amesema atapitia sheria ya kuanzishwa kwa taasisi hiyo ili kuona kama inaruhusu tozo hizo na kuangalia sheria gani inawaruhusu kutoza kodi. Alihoji inakuwaje taasisi ya Serikali inatoza tozo kwenye maghala ambayo yamejengwa na wananchi.

Akitoa mfano kuhusu ghala la Liwale, Waziri Mkuu amesema: “Kuna viagency vimeanzishwa kazi yao ni kutoza mapato tu. Inakuwaje kunakuwa na taasisi imekaa tu na kuanza kutoza tozo kwa wananchi wanaotumia facility za Serikali. Sheria ya kutoza tozo imetokana na nini na hizo zinakwenda kwa nani, je srikali imeanza kufanya biashara?,” alihoji.

“Nimepata taarifa kuwa walikuja kuzuia mazao yasitoke hadi wao walipwe, hapana huu siyo utaratibu. Ni kwa nini tuwanyang’anye fedha wale waliojenga ghala? Wao walijenga ghala kutokana na ubunifu halafu unasema unawapa sh. 7/- kwa kilo wakati wewe umetoza sh.25/- kwa kilo moja. Hapana hilo halikubaliki,” amesisitiza.

Waziri Mkuu amesema kama Serikali inaruhusu kuwepo kwa tozo hizo kwa jambo ambalo wananchi wamelibuni wenyewe, basi ilipaswa kudai kodi na hiyo kodi ilitakiwa kukusanywa na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) na siyo vinginevyo.

Waziri Mkuu amesema atafuatilia wakala mbalimbali walioanzishwa kwenye wizara kwani kuna nyingine zinafanya kazi ambazo zilistathili kufanywa na idara kwenye wizara mama.

                            
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, DESEMBA 27, 2016.

Tanzania Kufungua Ofisi za Ubalozi Nchini Jamhuri ya Korea

$
0
0
Na: Frank Shija – MAELEZO.

Tanzania yadhamiria kuimarisha uhusiano baina yake na Jamhuri ya Korea kwa kufungua Ofisi zake za Ubalozi Mjini Seoul, nchini Korea.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga leo jijini Dar es Salaam wakati akipokea msaada wa Dola za Kimarekani 50,000 kwa ajili ya kusaidia urejeshaji wa miundombinu iliyoharibika kutokana na Tetemeko la Ardhi lilitokea Mkoani Kagera mnamo tarehe 9 Septemba 2016.

Balozi Mahiga amesema kuwa nchi ya Jamhuri ya Korea imekuwa na uhusiano mzuri na wa muda mrefu na Tanzania ambapo kupitia uhusiano huo imekuwa ikisaidia katika mambo mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya afya akitolea mfano Hospitali za Mloganzila na Chanika ambazo zote zimejengwa kwa ufadhili wa Shirika la Kimataifa la Mahusiano la Korea (KOICA).

“Korea imekuwa na Ofisi za Ubalozi hapa nchini kwa zaidi ya miaka 25 hivyo wameona ni wakati sasa kwa Tanzania kuwa na Ofisi yake Ubalozi nchini nnchini Korea,” Alisema Balozi Mahiga.

Kwa upande wake Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Bw. Song, Geum – Young amesema kuwa msaada huo unatokana na namna ambavyo waliguswa na janga la Tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera na kusababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu na makazi ya wananchi.

Ameongeza kuwa msaada huo ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi aliyoitoa kwa Rais Dkt. Magufuli alipomtembelea Ikulu na kumpa Pole mnamo tarehe 22 Septemba mwaka huu.
Balozi Song Geum-Young pia amemhakikishia Waziri Mahiga kuwa Korea itaendeleza na kuimarisha uhusiano wake na Tanzania na kwamba itatoa ushirikiano wa kutosha kufanikisha miradi ya maendeleo ambayo inatekelezwa hapa nchini ikiwemo ujenzi wa Daraja la Salender, Meli, Hospitali ya Mloganzila, Chanika na mingineyo.

PROF. MBARAWA AKUMBUSHA KAMPUNI ZA MAWASILIANO KUJISAJILI SOKO LA HISA

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu utekelezaji wa sheria ya EPOCA kulingana na mabadiliko yaliyofanywa katika Sheria ya Fedha No. 2 ya mwaka 2016, jijni Dar es Salaam.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amezitaka Kampuni za Mawasiliano kukamilisha taratibu za usajili katika Soko la Hisa la Dar es Salaam kwa kuuza asilimia 25 ya hisa zote kadri ya Sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana inavyoelekeza mwishoni mwa mwaka huu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Prof. Mbarawa ametaja kampuni hizo kuwa ni zile zenye leseni za mawasiliano zilizotolewa kabla ya tarehe 1 Julai 2016 kwa ajili ya Miundombinu ya Mawasiliano, Huduma za Mawasiliano, na Huduma za Matumizi.

“Watoa huduma wote wa Mawasiliano wajisajili na kuuza hisa zao kwa wananchi ndani ya mwezi wa Disemba”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Ameongeza kuwa kwa Kampuni zilizopata leseni baada ya tarehe mosi Julai, 2016 watatakiwa kutimiza sharti hilo la kisheria kwa kipindi kisichozidi miaka miwili tangu kusajiliwa.

Waziri Prof. Mbarawa amesisitiza kuwa Kampuni zitakazokiuka Sheria hiyo zitachukuliwa hatua za kisheria kupitia kifungu cha 21 (C) cha EPOCA, 2010.

Aidha, amewataka wananchi kutumia fursa hiyo kununua hisa hizo na kuwa sehemu ya wamiliki wa makampuni ya Mawasiliano ili kuongeza kipato na kushiriki katika maamuzi ya kampuni hizo.




Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMATANO DESEMBA 28, 2016

Mradi wa Umeme Vijijini (REA III) kufika Vijiji vyote nchini

$
0
0

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kwikuba kuhusiana na Mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akipokelewa na Mwenyekiti wa kijiji cha Kwikuba, Kamunyiro Kwibega.

Baadhi ya wananchi wakiagana na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) mara baada ya kumaliza kuzungumza nao
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani).

Serikali imesema vijiji vyote ambavyo havikufikishiwa huduma ya nishati ya umeme vitapata huduma hiyo kupitia Mradi mkubwa wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III).

Hayo yamesemwa hivi karibuni na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo katika ziara yake katika kijiji cha Kwikuba, Mkoani Mara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa Umeme Vijijini Awamu ya Pili (REA II) ambao unamalizika.

Katika maeneo mbalimbali aliyotembelea Waziri Muhongo alielezwa kuwa vijiji vya ndani havina umeme kwani umeme umeishia kwenye vijiji vilivyopo katika barabara kubwa na kwenye senta za biashara.

Waziri Muhongo alisema Serikali inatambua vijiji ambavyo havikufikishiwa huduma husika na hivyo aliwaasa wananchi katika vijiji hivyo kuwa na subira kwani lengo la Serikali ni kuhakikisha ndani ya miaka 10 vijiji vyote nchini view vimefikiwa na umeme.

Alisema Mradi huo wa REA III umetengewa zaidi ya trilioni moja ambayo ni mara tatu zaidi ya iliyotengwa kwa Mradi wa REA II ambao unamalizika kwa kuunganisha baadhi ya vijiji.

Aliongeza kuwa sasa hivi Serikali ipo katika utaratibu wa kuwapata Wakandarasi mahiri ambao watakabidhiwa jukumu la kutekeleza mradi huo ambao alisema ni mkubwa na wa kihistoria nchini.

Aidha akizungumzia mradi huo wa REA III, Meneja wa Kanda ya Ziwa wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Amos Maganga alisema mbali na kuunganisha vijiji vyote, lakini pia mradi huo umelenga kuhakikisha unamaliza mapungufu yaliyojitokeza katika REA II.

Alisema katika utekelezaji wa mradi wa REA II kuna mapungufu yaliyojitokeza kwa sababu mbalimbali ikiwemo kutokuwa na wigo mpana na hivyo kusababisha baadhi ya vijiji kurukwa na vingine kutofikiwa kabisa na vilevile uhaba wa baadhi ya vifaa katika maeneo mbalimbali.

Aliwaasa wananchi ambao vijiji vyao havijafikishiwa huduma ya nishati ya umeme kuwa na subira kwani mradi mkubwa wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) hautaacha kijiji.
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live




Latest Images