Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1080 | 1081 | (Page 1082) | 1083 | 1084 | .... | 1898 | newer

  0 0  0 0

  Bwanaharusi Ndugu Samwel Makalobo akivishwa pete ya ndoa na Mke wake Given Mgaya katika kanisa la K.K.K.T Usharika wa Isanga jijini Mbeya .Picha na Keneth Ngelesi .
   JamiiMojaBlog,Mbeya


  HATIMAYE lile tukio lililovuta hisia za watu wengi la bibi harusi, Given Mgaya, kukimbiwa kanisani na mchumba wake siku ya harusi, limepatiwa jibu baada ya bwana harusi , Samwel Mwakalobo, kujirudi na kuamua kutimiza ahadi yake ya kufunga ndoa.

  Ndoa hiyo imefungwa leo  majira ya saa tisa Desemba 23  katika Kanisa la (K.K.K.T) Usharika wa Isanga na kufungishwa na Mchungaji, Mathias Andangile Mwakijungu, huku tukio hilo likishuhudiwa na idadi kubwa ya waumini na wananchi wa kawaida waliojitokeza kanisani hapo.

   Kabla ya  maharusi hao kula kiapo cha ndoa,Mchungaji Mwaijungu alitumia zaidi ya saa moja kutoa nasaha kwa maharusi kutokana na tukio lilotokea awali Disemba 16 mwaka huu baada ya Bwana harusi kuingia mitini bila kutoa sababu zozote.
  Bwanaharusi akisaini hati ya Ndoa mbele ya mchungaji wa kanisa hilo Ndugu Mathias Mwaijungu mara baada ya ndoa hiyo kufungwa rasmi Desemba 23  mwaka huu.
  Bibi harusi akisaini hati ya Ndoa mbele ya mchungaji wa kanisa hilo Ndugu Mathias Mwaijungu mara baada ya ndoa hiyo kufungwa rasmi Desemba 23  mwaka huu.


  Mbali na kutoa nasaha kwa maharusi,pia Mchungaji Mwaijungu alitumia fursa hiyo kuwaonya baadhi ya waumini na watu wengine kuacha tabia ya kueleza mambo yasiyo yajua tena bila kuwa na uhakika.

  Alisema tabia hiyo huenda ndiyo iliyosababisha tukio la kukwama kufungwa kwa ndoa hiyo baada ya baadhi waumini na watu wengine kwa maslai yao walimua kueleza uzushi ulio iibua taaruki kubwa.

  Baada ya nasaha hizo na kunukukuu baadkitakatifu cha Bihi ya maandiko kutoka kitabu Biblia ndipo ulipo fika muda kwa maharusi hao kutimiza ahadi ya kula kiapo cha uaminifu katika ndoa yao.


  Mara baada ya kufungisha ndoa hiyo nje ya kanisa hilo akizungumza na waandishi wa habari bwana harusi Mwakalobo alisema kuwa anawaomba radhi ndugu jamaa na marafiki na kwamba kilicho tokea ni mapito.

  “ndugu zangu nawadhibitishia kuwa alipangelalo mungu binadamu hawezi kulitengua ni kwe;li tuliopnga tarehe ile lakini sisi ni wanadamu mungu alipanga huu ulikuwa ni upepo ulipita na niwaombe radhi ndugu jamaa kwa hili liliotokea” alisema Mwakalobo

  Aidha katika hatua nyingine bibi harusi aligoma kuzungumzia suala hilo huku kwa kile alichokileza lile suala lililotokea kila kitu anamwachia Mungu.
  Bibi harusi akitabasamu kwa furaha baada ya kutoka kanisani
  Bwana na bibi harusi wakitoka kanisani
  Maharusi akitoka kanisani


  0 0


  0 0
 • 12/24/16--00:28: MARUFUKU DISKO TOTO-BASATA
 • Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambalo ni msimamizi wa sekta ya Sanaa na burudani nchini linawakumbusha wamiliki na waendeshaji wa kumbi za burudani kufuata sheria, kanuni na taratibu walizopewa kwenye vibali vyao vya uendeshaji wa kumbi.

  Wanaelekezwa kuhakikisha wanakuwa na vibali halali vya uendeshaji wa kumbi zao, kuzingatia muda wa matumizi wa ukumbi, kuepuka kelele zinazosumbua kwenye maeneo maalum hasa makazi ya watu na kuhakikisha ulinzi na usalama wa maisha ya watu na mali zao.

  Aidha, BASATA linawakumbusha wamiliki wote wa kumbi za sherehe na burudani kwamba ni marufuku kukusanya watoto katika kumbi zao kupitia kile kinachoitwa ‘Disko Toto’ katika msimu huu wa Sikukuu ya Christmas na Mwaka mpya ili kuepuka maafa yanayoweza kujitokeza.

  Uzoefu unaonesha kwamba, nyakati za sikukuu kama hizi wamiliki wa kumbi wamekuwa wakijisahau na kuandaa madisko ya watoto hali mbayo imekuwa ikisababisha maafa ambayo yangeepukika kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu.

  Aidha, baadhi ya wamiliki na waendeshaji wa kumbi wamekuwa wakijisahau na kuendekeza faida pasi na kujali maelekezo ya vibali vyao, wamekuwa wakijaza watu kupita viwango vya madaraja waliyopangiwa na BASATA.

  BASATA mamlaka inayotoa vibali vya kumbi za sherehe na burudani linasisistiza kwamba halitafumbia macho ukumbi wowote utakaokiuka maelekezo haya sambamba na kuruhusu maonesho machafu yenye kudhalilisha utu wa binadamu hasa yale yanayoonesha maungo ya ndani. Hatua kali na za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayekiuka maagizo haya.

  BASATA linawatakia wasanii na wadau wote wa 
  Sanaa Heri ya Christmas na Mwaka Mpya.

  SANAA NI KAZI TUIKUZE, TUILINDE NA KUITHAMINI
  Godfrey L. Mngereza

  KATIBU MTENDAJI, BASATA

  0 0

   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa(Mb)  akisalimiana na Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa kabla ya kuongea na Maafisa na askari wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Dar es Salaam alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua maandalizi ya ujenzi wa nyumba 320 za makazi ya Maafisa na askari wa Jeshi hilo katika eneo la Gereza Kuu Ukonga, Jiji la Dar es Salaam Disemba 24, 2016(wa kwanza kushoto) ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.
   Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Malewa akitoa maelezo mafupi kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim(hayupo pichani) namna Jeshi hilo lilivyojipanga katika kuhakikisha kuwa ujenzi wa nyumba hizo ambazo zinatarajiwa kujengwa katika eneo la Gereza Kuu Ukonga, Jijini Dar es Salaam unakamilika ipasavyo.
   Meneja Ujenzi wa Mamlaka ya Majengo nchini – TBA, Arch. Humphrey Killo akitoa maelezo ya kitalaamu kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua maandalizi ya ujenzi wa nyumba 320 za makazi ya askari katika eneo la Gereza Kuu Ukonga, Jiji la Dar es Salaam Disemba 24, 2016.
   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akikagua eneo la ujenzi wa nyumba hizo za makazi ya askari.

  0 0

  Mhe. Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ametuma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa, wapiga picha pamoja na Wanahabari wote nchini kufuatia kifo cha mwanahabari na mpiga picha Mpoki Bukuku (kushoto) kilichotokea jana tarehe 23 Desemba, 2016 katika Taasisi ya Mifupa (MOI) Jijini Dar es Salaam. 
  Mhe. Nape Nnauye pamoja na watendaji wa Wizara wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha mwanahabari huyo kwani ni pigo katika tasnia ya habari nchini. 
  Mhe. Waziri Nape amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha mwanahabari huyo na ameeleza kuwa, kifo chake ni pigo katika tasnia ya habari hususani katika picha kwasababu Marehemu wakati wa uhai wake ametoa mchango mkubwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo magazeti ya Majira, Business Times, The Guardian, Nipashe na Mwananchi na The Citizen.

  Wakati huo huo Mhe. Waziri ametuma salamu za rambirambi kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel pamoja na familia kufuatia kifo cha mtumishi wake Bw. Modest Mfutakamba Mfilinge (kulia) kilichotokea usiku wa kuamkia leo 24 Desemba, 2016. 
  Mungu azilaze roho za Marehemu mahali pema peponi. Amina.
  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,
  Dar es Salaam.


  24 Desemba, 2016.


  0 0

   Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Kimataifa ya CRJE Bw. Li Yi akimueleza Balozi Seif nia ya Kampuni yake ya kutaka kuibadilisha Zanzibar kimajengo endapo itaendelea kupewa tenda za Ujenzi walipokutana Mjini Beijing China.
  Balozi Seif akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Kimataifa ya CRJE  inayojenga Jumba la Treni Darajani Bw. Li Yi katika Hoteli ya Kimataifa ya Sheraton Mjini Beijing Nchini China. Nyuma ya Bwana  ni Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dr. Khalid Salum Mohamed.

  Na Othman Khamis Ame, OMPR
  Kampuni ya Kimataifa ya Uhandisi  inayoshughulikia miradi ya Ujenzi wa Bandari  na Madaraja Makubwa ya China { CHEC}   iko tayari wakati wowote kuanzia sasa kusubiri kuanza kwa harakati za ujenzi wa Bandari ya Mizigo ya Mpiga Duri Mjini Zanzibar.

  Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Kampuni hiyo Bwana Li Yi akiambatana na Timu ya wahandisi wa Kampuni hiyo wakati wa mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  hapo Ofisini kwake  Mjini Beijing Nchini China.

  Bwana Li Yi alisema Wataalamu na wahandisi wa Kampuni yake  wameshakamilisha taratibu zote za kufanya Utafiti wa ujenzi huo baada ya  kupewa nafasi hiyo kufuatia tenda iliyotolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ajili ya Mradi huo.

  Alieleza kwamba Kampuni hiyo kongwe Duniani iliyoasisiwa mwaka 1837 hivi sasa imebadilika kiutendaji  ndani ya kipindi cha miaka miwili  kwa kuzingatia zaidi sheria na taratibu wa Kimataifa kitendo chacho kimeleta mafanikio makubwa kwa  Kampuni kiasi cha kuweza kuaminiwa na Taasisi na Mataifa tofauti Duniani..

  Bwana Li Yi alisema CHEC kwa sasa ina uwezo wa kuendesha miradi ya Uvuvi, huduma za Maji, majengo ya bishara kubwa  { MALL }pamoja na miundombinu ya miradi ya umeme na hata kilimo.

  Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliufahamisha Uongozi wa Kampuni nhiyo ya CHEC  kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haina pingamizi yoyote kwa uwamuzi wao huo wa kujihusisha na miradi mengine ya kiuchumi.

  Balozi Seif  alisema chakuzingatia  zaidi katika miradi yao mipya  wanayotaka kuianzisha ni kuandika barua  za maombi na kuziwasilisha kwa Mamlaka inayohusika na Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar {ZIPA} kwa hatua zinazofaa.

  Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na Ujumbe wake  alifanya mazungumzo na Uongozi wa Kapuni ya Kimataifa ya Ujenzi ya CRJE ya Mjini China chini ya Mwenyekiti wake wa Kanda ya Afrika Bwana Hu Bo.

  Katika mazungumzo yao yaliyofanyika Hoteli ya Kimataifa ya Sheraton  Mjini Beijing Bwana Hu Bo alisema Kampuni ya CRJE imeamua kuibadilisha Zanzibar kimajengo mazuri yakiwa na hadhi ya kisasa inayokubalika Duniani endapo wataendelea kukabidhiwa  tenda za kazi hizo.

  Kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliyekiri uwezo mkubwa iliyonayo Kampuni hiyo ya Ujenzi ya CRJE baadaye mchana alionana kwa mazungumzo na Uongozi wa  Kampuni Kubwa  inayoongoza Duniani katika uendeshaji wa  Miradi ya Umeme ya TBEA.

  Balozi Seif  aliueleza Uongozi huo wa TBEA chini ya Makamu wa Rais wake Bwana Wang  Pinshan kwamba Wataalamu wa Taasisi hiyo wana fursa ya kuangalia namna  wanavyoweza kuisaidia Zanzibar katika huduma mbadala  ya nishati ya Umeme.

  0 0

  Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Saint Nicholas Jimbo Kuu Mwanza DVN, Lazaro Manjelenga, akiwafungisha ndoa Bwana Godfrey Sinyangwe na Bibi Esther Kiluma wote wa Jijini Mwanza, hii leo. Amesaidizana na Mchungaji Msaidizi wa Kanisa hilo, Joseph Samwel.
  #BMG
  Bwana Godfrey Sinyangwe na Bibi Esther Kiluma wakivishana pete ya ndoa
  Upendo wa dhati
  Bwana Godfrey Sinyangwe (kushoto) na Bibi Esther Kiluma, wakifurahia ndoa yao
  Wanapendana sana
  Bwana Godfrey Sinyangwe na Bibi Esther Kiluma
  Ndoa na iheshimiwe na watu wote
  Bwana Godfrey Sinyangwe na Bibi Esther Kiluma wakiwa ufukweni
  Ndoa yetu na idumu milele
  Baada ya ndoa pamoja na zoezi la kupiga picha katika ufukwe wa ziwa Victoria, shughuli usiku huu inafanyika Ukumbi wa Bugando Club.
  BMG inawatakia Maisha Mema.

  0 0

  Mchambuzi wa maswala ya jamii na siasa nchini Tanzania Mathias Canal (Picha na David Mtengile)

  Na Mathias Canal

  Katika sehemu ya maelezo yake Raisi wa 16 wa Marekani Bw Abraham Lincoln namnukuu aliwahi kusema kuwa Demokrasia ni mfumo wa serikali ambapo wananchi wote ni sawa mbele ya sheria na wanashiriki katika kufanya maamuzi ya kitaifa juu ya masuala ya umma. Wakati mwingine wananchi hushiriki moja kwa moja - hii ina maana kwamba wao hupiga kura moja kwa moja kwenye masuala kama vile katika chaguzi. 

  Kabla sijaanza kuzungumzia uchaguzi wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Tutazame Mwongozo wa kumteua muaniaji Urais nchini MarekaniKabla ya Wamarekani kuamua nani wanayemtaka awe rais ajaye, wao kwanza huteua nani atakayewania kiti hicho.

  Mchakato huo hungo'oa nanga kwa mchujo wa kamati za wajumbe ambapo wananchi hupata fursa ya kumchagua muaniaji kiti cha urais kwa tiketi ya chama cha Democratic au kile cha Republican.Mshindi wa mchujo huo huwakusanya wajumbe - hawa ni wanachama wenye nguvu ya kupiga kura kumchagua mgombea katika mikutano ya chama.

  Nchini Marekani inakumbukwa kuwa kulikuwa na upinzania mkali katika uchaguzi wa nafasi ya Rais kati ya vyama viwili ambapo ni Republican na Demokratic, Kwa upande wa Democrats upinzani mkali ulikuwa kati ya Hillary Clinton na Seneta Bernie Sanders ambaye alionekana nae kupata uungwaji mkono zaidi dhidi ya Clinton. Kwa upande wa Republican kulikuwa na wagombea kama Marco Rubio na Ted Cruz sambamba na Donard Trump aliyeibuka kuwa mshindi wa chama hicho na mshindi wa nafasi ya Urais wa Marekani.

  Tutakubaliana wote kwa pamoja kwamba Vyama vyote nchini Marekani vilisimamisha wagombea katika kura za awali kabisa ambao wote kwa pamoja walipigiwa kura na wajumbe wao hapakuwa na kura za Ndio na Hapana kwa maana ya Kivuli/Jiwe na Mtu sasa tutazame mchakato ulivyo kuwa kwenye vyama vinavyounda umoja wa katiba ya Wananchi UKAWA vikiongozwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA jinsi vilivyompata mgombea wake wa Urais.

  Julai 30, 2015 nikiwa natazama Luninga majira ya saa tatu na dakika moja usiku niliona katika kipindi cha Dira ya Dunia kinachorushwa na chombo cha habari cha BBC kupitia Televisheni ya Star Tv kikiarifu kuwa WANACHAMA wapya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa pamoja na na Juma Duni Haji wamepitishwa katika Mkutano Mkuu wa chama hicho kugombea ngazi ya urais na umakamu wa rais kwa asilimia 99.3 ambapo jumla ya wajumbe 2021 kati ya 2035waliotakiwa kuhudhuria kwenye mkutano huo, walipiga kura za NDIO kwa kuwa hapakuwa na wagombea wemngine na kuibua kishindo katika mkutano huo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

  Awali kabla ya kufanyika uchaguzi huu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mhe Freeman Alikael Mbowe Akizungumzia utaratibu wa kuteua mgombea huyo alisema kuwa, kwa mujibu wa katiba hiyo kifungu namba 7.16, mgombea urais pamoja na makamu wake wanateuliwa na sio kupigiwa kura.

  Yaani kama kuna mtu hakuelewa vyema hapo katika maelezo hayo naomba nimsaidie kwa hili naamini ataelewa vyema zaidi Mbowe alisema kuwa kwa mujibu wa katika huku akitaja kifungu Mgombea Urais hapigiwi kura na wajumbe bali anateuliwa. Hii ni kauli ya kishujaa nay a ubakaji wa Demokrasia kwa uwazi kabisa.

  Tujikumbushe Demokrasia ni nini kabla ya kuendelea na mjadala ili tuende sawa: Utawala wowote wa Demokrasia ni ule unaotokana na ridhaa ya wananchi, ambao kutokana na utaratibu waliojiwekea hufanya maamuzi ya kuwapata viongozi wao. Wananchi hushiriki moja kwa moja - hii ina maana kwamba wao hupiga kura moja kwa moja kwenye chaguzi. Tukubaliane sasa ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA hakuna Demokrasi kama ambavyo inahubiriwa katika vijiwe na majukwaa ya kisiasa. Na kama demokrasia ni pamoja na kushirikisha wananchi kufanya maamuzi kwa nini Mbowe aliamua yeye kwamba Lowassa na Duni wateuliwe sio kupigiwa kura na wajumbe zaidi ya 2000, kwa akili ya kawaida tu na karne hii unaweza kuwaambia watu fanyeni maamuzi kati ya Jiwe/kivuli na mtu...? Lakini katika hili sikuwaona vijana wa CHADEMA wakihoji wala wale wa Umoja wa Kizazi cha Kuhoji (UTG) wakihoji. Huenda walipitiwa hawakuliona hili sasa tuendelee.

  UCHAGUZI KANDA YA NYASA 

  Kwa kunukuu gazeti la Rai linalochapishwa na KAMPUNI ya New Habari (2006) Ltd ambayo pia inachapisha magazeti ya Mtanzania, Bingwa, Dimba na The African, la Disemba 8, 2016 liliandika habari ilikuwa na kichwa cha habari kilichosema UCHAGUZI CHADEMA NI ‘VITA’ KALI 

  ‘NI vita’, hivyo ndivyo tafsiri inapatikana kufuatia mvutano mkali ulioibuka ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kati ya Mchungaji Peter Msigwa na Patrick Ole Sosopi ambao walikuwa wanapambana kuwania nafasi ya uenyekiti kanda ya Nyasa.

  Msigwa ambaye ni Mbunge wa Iringa Mjini alipamba na kijana Machachari katika Siasa za Tanzania Patrick Ole Sosopi ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), kuwania Kanda hiyo ya Nyanda za Juu Kusini (Nyasa) inayojumuisha mikoa ya Iringa, Mbeya, Rukwa, Njombe na Songwe.

  Tangu maandalizi ya uchaguzi kanda nane za Chadema yalipoanza mwezi uliopita kulikuwapo na majibizano kati ya wafuasi wa wagombea hao wawili ambao kwa namna moja au nyingine wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kuanika madhaifu ya kila mgombea.

  Hata hivyo, Msigwa alionekana kushambuliwa zaidi na wafuasi wa Chadema Kanda ya Nyasa kutokana na madai mbalimbali ikiwamo tabia ya kutoshirikiana na wabunge wenzake katika kukijenga chama, pia kujiweka mbali na wabunge wa chama hicho kipindi walipokuwa wakipambana kutetea madai yao kwa Naibu Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson.

  Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia gazeti la RAI zinaeleza kuwa baadhi ya wabunge na viongozi wa chama hicho walionekana kusita kumuunga mkono Mbunge huyo kutokana na madai ya ubinafsi aliouonyesha katika kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu 2015 kwa kushindwa kushirikiana na makada wa chama hicho kuzunguka sehemu mbalimbali.

  Hata hivyo baadhi ya wafuasi wa Ole Sosopi walionekana kulalamika kutukanwa kwenye mitandao ya kijamii ambapo mmoja wao alisema: “Nimeshangaa sana watu kunifuata inbox na kunitukana hata wengine kutumia lugha ambayo si njema. Kumuunga mkono Sosopi ‘it’s just my perception.’ Kwa kuwa nina akili timamu siwezi kujibu matusi kama mlivyofanya “Imeniuma sana, nimeumia sana. Naomba niliweke wazi hili, Peter Msigwa ni Mbunge wangu, ni mlezi wangu na sina ugomvi naye. Sosopi na Msigwa wote ni Chadema na wote ni familia moja ndani ya chama chetu Chadema,” 

  SIKU YA UCHAGUZI WA KANDA YA NYASA

  Tarehe Disemba 22, 2016 ndio siku ambayo Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kilifanya uchaguzi huo lakini mapema asubuhi kabla ya kuanza kwa uchaguzi jina la Patrick Ole Sosopi liliondolewa katika kinyang’anyiro cha kugombeanafasi ya uenyekiti Kanda ya Nyasa na Uongozi wa Kamati kuu ya Chama hicho iliyokuwa inaongozwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Alkael Mbowe.

  Sosopi alipewa taarifa kwa njia yam domo kwamba jina lake limetolewa pasina kupewa hata maelezo kwa njia ya maandishi lakini pia taarifa hiyo alipewa asubuhi siku ya uchaguzi sio siku moja ama mbili kabla ya uchaguzi
  Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo ambaye kwa sasa ni katibu wa Nec, Itikadi na Uenezi wa  CCM Taifa Hamphrey Polepole aliwahi kusema kuwa Huu si wakati wa siasa za kutafuta uongozi; Ni wakati wa siasa za maendeleo na kujenga nchi hapo alikubaliana na dhana ya mfumo wa kupunguza madaraka kwa viongozi inayohubiriwa naserikali ya wamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ya kuwataka viongozi kuwa na cheo kimoja serikalini ikibidi kuwa na cheo kimoja pia kwenye chama cha siasa isiwe zaidi ya hapo.

  Kabla ya kuendelea naomba nikurejeshe katika kauli ya Mchungaji Peter Msigwa ya Mwaka 2015 aliyoisema kwamba “Raisi apunguziwe madaraka, na wakuu wa mikoa pia wana vyeo vingi sana wapunguziwe" by peter msigwa 2015.

  Lakini tutazame sasa vyeo alivyonavyo mchungaji Msigwa kwenye chama na seriakli kabla ya kutazama uchaguzi wa Mwenyekiti Kanda ya Nyasa ulivyoendeshwa
  Mchungaji Msigwa ni Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini
  Mchungaji Msigwa ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu Chadema
  Mchungaji Msigwa ni Mjumbe wa Baraza kuu Chadema
  Mchungaji Msigwa ni Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema
  Mchungaji Msigwa ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Iringa
  Mchungaji Msigwa ni Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa
  Mchungaji Peter  Simion Msigwa amekipata cheo cha sita ndani ya Chadema na kuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa baada ya wagombea wengine kuenguliwa, hivyo kuwa mgombea Pekee ambaye ni yeye Msigwa na Mgombea mwingine ambaye ni Jiwe/kivuli. Binafsi najiuliza sana lakini najiuliza kimya kimya hivi vikao vya vyeo hivyo vyote vya watu sita anahudhuriaje!


  Maana ya upatikanaji wa Mchungaji Msigwa kama Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyasa ni kwa njia ya kuteuliwa na sio kuchaguliwa lakini Demokrasia ambayo CHADEMA huihubiri ni wazi wamekuwa wakiivunja wao maana wanawanyima nafasi wagombea pendwa na kukata majina yao na hatimaye wanakubali mgombea mmoja ashindane na kivuli pamoja na kwamba hakubaliki.

  UCHAGUZI WA CHADEMA KANDA YA NYASA ULIKUWAJE BAADA YA MSIGWA KUBAKI MGOMBEA PEKEE AKISHINDANA NA KIVULI CHAKE MWENYEWE

  Kwa mujibu wa andiko la lililosomeka kama “NIMEAMINI MAISHA BILA UNAFIKI HAYAENDI”
  lililoandikwa na Mwalimu Pasaka Rucho mara baada ya mchakato mzima wa kumalizika na mshindi kutangazwa. Umeeleza tangu mchakato kuanza wajumbe walitaharuki sana kusikia taarifa ya kutolewa kwa jina la sosopi, tazama mchakato ulivyokuwa:
  Wajumbe halali ni 98
  Waliosusia 28
  Waliopiga kura ni 106
  Kura za ndio kwa msigwa 62
  Kura za hapana ambazo zilipigia kivuli cha mgombea ni 44

  Hii ikiwa na maana Ukichukua Kura 44 za Hapana dhidi ya Msigwa + na kura 28 za wajumbe waliosusia uchaguzi jumla yake ni =72 hivyo Sosospi tayari kama alikuwa mshindani alikuwa amejihakikishia ushindi kwa kura 78.

  Kura zilizoongezeka kwa zile zilizopigwa ni 8 maana wapiga kura waliongezeka kutoka wapiga kura halali 98 na kuwa na wapiga kura wasio halali 8 waliofanya idadi kuongezeka na kuwa na wapiga kura 106.
  Wajumbe waliopaswa kubaki ndani ukiondo waliokuwa wamekataa kuingia ndani ni 70
  98-28=70.

  Kwa maana halisi ni kwamba kulikuwa na wapiga kura 36 walioletwa na kuwa wajumbe wasio halali maana baada ya kura 44 za Hapana na wajumbe 28 kutoka ukumbini hivyo kulipaswa kupatikana kura za halali 28 ambazo ndizo kura za Ndio kwa Msigwa. 

  Hii inamaanisha kwamba katika hali ya kawaida hata kama wajumbe wale 28 wasingeingia kama walivyofanya Msigwa angeshinda kwa kura 26 tu kwa maana ya wajumbe waliopaswa kubaki ndani 70- wajumbe 44 waliomkutaa=26 ambayo ndio idadi ya kura za Msigwa katika uchaguzi huo.

  kwa ufupi kwa kutumia wajumbe halali katika uchaguzi kama Sosospi asingetolewa uchaguzi ungemalizika hivi:
  Sosopi 72 (73.5%)
  Msigwa 26 (26.5%)

  HITIMISHO

  Nianze kwa kumnukuu Dkt  Benson Bana wa Chuo Kikuu cha Dare s salaam ambaye amebobea katika masuala ya siasa alipokuwa akizungumza katika mkutano wa wadau wa siasa wa uimarishaji demokrasia ya vyama vingi. Alisema pamoja na mafanikio hayo bado kuna mapungufu mengi hasa ya kutokuwa na utamaduni wa vyama vingi, utamaduni unaoambatana na vyama kuwa na  aidolojia (itikadi), kukosekana kwa lugha za kistaarabu katika majukwaa ya siasa na hata mitafaruku ya ndani ya kivyama.

  Mfumo wa vyama vingi ni hali ya kuwa na chama zaidi ya kimoja,katika nchi moja.Madhumuni ya kuwa na vyama vingi vya siasa ni kuleta ushindani wa kisiasa,ili kuleta maendeleo ya nchi,upinzani wa kisiasa sio uadui kama watu wengi kwenye nchi zinazoendelea wanavyodhani,kuwa na vyama vingi ni kuongeza wigo wa demokrasia katika jamii huska. Hata hivyo mara kadha amesema kuwa ili nchi yetu iweze kupiga hatua ni dhahiri lazima kuwe na Upinzani imara unaochukia Rushwa, na Uminyaji wa Demokrasia.

  Binafsi sasa nakitoa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA katika Ukuzaji wa Demokrasi kwa kauli ya Mbowe kwa kusema kuwa Mgombea Urais hachaguliwi bali anateuliwa jambo ambalo ameliongoza pia kwa kumteua Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa Mchungaji Msigwa badala ya kuruhusu wajumbe kugombea na kuchagua kiongozi wanaomtaka.

  TANZANIA ina vyama vya siasa 21 vyenye usajili wa kudumu huku kikiwepo kimoja ambacho kina usajili wa muda. Vyama hivi vimepatikana baada ya mabadiliko madogo ya Katiba yaliyotoa fursa ya kurejesha mfumo wa vyama vingi katika nchi yetu mwaka 1992.

  Kufuatia mabadiliko haya, Chama cha Mapinduzi (CCM) ndicho kilichokuwa cha kwanza kupata usajili wa kudumu mwaka 1992, huku kikifuatiwa na vyama vipya vya CUF, CHADEMA,UMD, NCCR, NLD, UPDP, NRA, TADEA NA TLP vilivyopata usajili wa kudumu mwaka 1993.

  Vyama vingine na usajili wao kwenye mabano ni:  UDP (1994), Demokrasia Makini (2001), CHAUSTA (2001), DP (2002), APPT(2003), Jahazi Asilia (2004), SAU (2005), AFP (2009), CCK (2012), ADC (2012), CHAUMMA (2013) na ACT (2014). RNP ni chama pekee kilichopo katika orodha ya vyama visivyo na usajili wa kudumu.

  Katika vyama vyote hivi 21 mpaka sasa ni CHADEMA pekee ndicho kisichokuwa na Demokrasi kama ambavyo nimebainisha katika maeneo kadha wa kadha katika andiko langu.

  Mwandishi Henry Mwangonde Aprili 23, 2014 katika gazeti la The Citizen, alimnukuu Dk. Benson Banna Katika makala yake ya “Vyama vingi vimeisaidia Tanzania” na kuandika; “vyama vya siasa nchini Tanzania havina nguvu katika kutanua mianya ya demokrasia kutokana na kukosa sera nzuri, mikakati pamoja na tabia ya viongozi wa vyama hivi kutokutumia mtaji wa wanachama wao kuviendeleza badala yake kuwatumia kwa masilahi binafsi.” Kwa mujibu wa Dkt Bana katika makala hiyo; vyama hivi vimeshindwa kutanua miaya ya demokrasia kwa kuwa havina demokrasia ndani yake.

  Ni aibu kubwa sana kwa CHADEMA chama kinachojificha katika Mwamvuli wa Demokrasia katika Karne hii ya 21 kusimamisha mgombea Kivuli/Jiwe na Mtu…! Na bado kivuli kinapata kura 44? Watu 28 wanaishia mitini? Mtu anapata kura 66 naye anarudi kumsimulia Mkewe na Watoto kwamba ameshinda uchaguzi. 

  Sasa hapa wachambuzi na wajuzi wa Siasa watahoji Tofauti ya CHADEMA na Yule mtu waliompa umaarufu kwa kumuita Bwana Yule upo wapi…? Lakini nimkumbushe Msigwa na CHADEMA kuwa raha na uzuri wa kura za Ndio na Hapana ni pale amabapo mshindi anaibuka kidedea kwa kura nyingi sio unapata kura 62 wakati zinakukataa ni kura 44 huku kura zingine 28 zikisusia namna ya Demokrasia ndani ya Chama.

  Wakati vyama Vingine nchini vikiwa vinasonga mbele katika kuimarisha chaguzi zao za ndani ya Chama lakini CHADEMA wao wanarudi nyuma na kutoa mwanya kwa vyama vyenzake kusonga mbele.Naitazama CHADEMA kuanguka Kama umaarufu wa NCCR Mageuzi mwaka 1995.
  Nitafurahi sana kuona na kusikia kauli za vijana mbalimbali wa CHADEMA wakiwemo UTG wakihoji kuhusiana na Uminyaji wa Demokrasia ndani ya chao chao CHADEMA ili tuzijue rangi zao katika kuhoji na kujenga hoja.

  Mwandishi wa Makala haya ni Mathias Canal, Mchambuzi wa maswala ya jamii na siasa nchini Tanzania, Anapatikana kwa Barua Pepe ya canalmathias@gmail.com na kwa simu namba 0756413465

  0 0  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Mlezi wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wabunge, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka mkoa wa Kaskazini ,Wenyeviti na Makatibu wa Majimbo CCM Mkoa wa Kaskazini pamoja na Wenyeviti na Makatibu wa Jumuiya kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini B Kinduni.
  Wabunge, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka mkoa wa Kaskazini ,Wenyeviti na Makatibu wa Majimbo CCM Mkoa wa Kaskazini pamoja na Wenyeviti na Makatibu wa Jumuiya wakimsikiliza Mlezi wa CCM mkoa wa Kaskazini na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini B Kinduni.
  Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Mhe. Vuai Ali Vuai akihimiza Umoja na Mshikamano kwa Viongozi wa CCM mkoa wa Kaskazini Unguja wakati wa kikao cha kupokea tathmini ya uchaguzi wa mwaka 2015 kikao ambacho mgeni rasmi alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini B Kinduni.  .....................................................................................................

  Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi-CCM- Taifa ambaye pia Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wanachama na viongozi wa CCM katika mkoa Kaskazini Unguja wadumishe na kuimarisha ushirikiano miongoni mwao kama hatua ya kujenga chama imara.

  Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ametoa kauli hiyo katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kaskazini (B) Unguja wakati akizungumza kwenye kikao kilichojumuisha viongozi wa ngazi mbalimbali wa chama hicho kwa ajili ya kujadili mipango na mikakati ya kuimarisha chama hicho.

  Mjumbe huo amesisitiza kuwa kama viongozi wa chama hicho watadumisha ushirikiano na kuondoa tofauti zao watakijenga chama na kuongeza idadi kubwa ya wanachama wapya ikilinganishwa na hali ilivyo kwa sasa katika eneo hilo.Amesema baada ya kumalizika kwa uchaguzi Mkuu kazi iliyopo kwa sasa kwa viongozi wa CCM katika ngazi zote ni kuweka wanaweka mipango na mikakati madhubuti itakayoweza chama hicho kuendelea kushika dola.

  Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi-CCM-Taifa SAMIA SULUHU HASSAN ambaye pia ni Mlezi wa CCM katika mkoa wa Kaskazini Unguja amesema anaimani kubwa kuwa kuanzia sasa viongozi hao watajipanga ili kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020.

  Kuhusu uimarishaji wa jumuiya za Chama hicho, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wa CCM katika mkoa wa Kaskazini Unguja waimarishe jumuiya hizo ili ziweze kutekeleza majukumu ya kichama katika kila ngazi.

  Mjumbe huyo ameonya viongozi hao waache tabia ya kugombania madaraka kwenye chama bali washirikiane katika kuongeza idadi ya wanachama hasa vijana ndani ya Chama hicho.

  0 0

   Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akiwa amewabeba watoto, Editha  (kushoto) na Edina wa Kituo cha kulea watoto yatima cha CHAKUWAMA kilichopo Sinza jijini Dae es salaam jijini Dar es salaam  wakati alipotembelea kituo hicho na kutoa misaada mbalimbali leo  Desemba 24, 201
  MKE wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa ametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa makundi ya watoto yatima jijini Dar es Salaam ili kuwawezesha kufurahia sikukuu za mwisho wa mwaka. 

  Mama Majaliwa ametoa msaada huo leo (Jumamosi, Desemba 24, 2016) katika vituo vitatu vya CHAKUWAMA kilichopo Sinza, HISANI kilichopo Kigamboni na CHAMAZI kilichopo Mbagala. 

  Akikabidhi msaada huo ikiwemo mchele, sabuni, mbuzi, juisi na soda, Mama Majaliwa amesema ameona ni vema atoe msaada huo kwa watoto hao ili na wao waweze kufurahia sikukuu za mwisho wa mwaka kama ilivyo kwa watoto wengine. 

  Pia ametoa wito kwa makundi mbalimbali yenye uwezo katika jamii wawe na moyo wa kusaidia makundi yenye uhitaji. 
  Kwa upande wao, walezi wa vituo vya kulelea watoto yatima vya CHAKUWAMA na HISANI wamemshukuru mke wa Waziri Mkuu kwa msaada huo huku baadhi ya watoto wakisema msaada huo umewapa faraja kubwa. 

  Mlezi wa kituo cha CHAKUWAMA, Bibi Saida Hassan mbali ya kushukuru kwa msaada huo, amewaombea kwa Mwenyezi Mungu awape afya na nguvu za kuendelea kuwatumikia vizuri Watanzania. 

  Naye Mlezi wa kituo cha HISANI, Bi. Hidaya Mutalemwa ameiomba jamii iendelee kuyakumbuka makundi yenye uhitaji kwani bado yanakabiliwa na changamoto nyingi za kufanikisha ndoto zao ikiwemo kupata elimu.

  0 0


   Walimu wastaafu wakiimba wimbo wa Solidarity Forever
   Mwenyekiti wa chama cha walimu (CWT) Wilaya ya Makete Thobias Kasambala akizungumza kwenye hafla hiyo

   Walimu wa staafu wakisikiliza jambo


   Afisa elimu sekondari wilaya ya Makete jacob Meena akiwaasa wastaafu hao
   Katibu wa CWT wilaya ya Makete Elizabeth Petro akisoma taarifa fupi
   Mgeni Rasmi afisa elimu Msingi wilaya ya Makete Anthony Mpiluka akitoa hotuba yake kwa wastaafu hao
   Mgeni rasmi akiendelea na hotuba yake


   Mgeni rasmi akikabidhi zawadi ya bati 20 kwa wastaafu hao   Mwalimu Mstaafu akitoa neno la shukrani kwa CWT
  Picha zote na Edwin Moshi, Makete

  0 0


  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi mara baada ya kuwasili mkoani humo. Pia Rais Dkt. Magufuli anatarajiwa kushiriki katika Ibada ya Krismasi mkoani humo hapo Kesho
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili mkoani Singida na kupokelewa na Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi.
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akielezea ujio wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mkoani humo ambapo pamoja na mambo mengine atashiriki katika Ibada ya Siku ya Krismasi katika Kanisa mojawapo mkoani Singida. PICHA NA IKULU
  0 0


  Wish You And Your Family A Very Happy Christmas And A Prosperous New Year.

  0 0

   Askofu mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa, akisalimiana na muumini wa kanisa hilo Usahrika wa Azania Front, Violet Muro baada ya kumpatia zawadi ya ibada mkesha wa Krismasi iliyofanyika jana usiku jijini Dar es Salaam.
   Kwaya ya Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Akbano ikitumbuiza katika ibada iliyofanyika katika kanisa hilo jijini Dar es Salaam.
   Waumini wa Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano wakiwa kwenye ibada ya mkesha wa krismasi.
   Vijana wa Kanisa la KKKT la Azania Front wakiigiza igizo la kumbukumbu ya kuzaliwa Yesu Kristo.
   Kwaya ya Vijana ya KKKT usharika wa Azania Front ikitoa burudani.
   Kwaya ya vijana ya KKKT Usharika wa Azania Front ikiendelea kutoa burudani.
   Watoto wakishiriki ibada katika Kanisa la KKKT la Azania Front
   Askofu mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akimsalimia muumini wa kanisa hilo, Violet Njau aliyekuwa ameongoza na familia yake.
   waumini wakiwa nje ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri usharika wa Azania Front baada ya ibada hiyo.

  Kwaya ya Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph ikitoa burudani

  Na Dotto Mwaibale

  AMANI Duniani na hapa nchini hawezi kuletwa na matajiri bali italetwa na maskini wenye kumcha mungu.

  Hayo yalisemwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo wakati akiongoza ibada ya mkesha wa Krismasi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Dar es Salaam jana.

  "Amani duniani na hapa nchini haiwezi kuletwa na matajiri bali italetwa na maskini wamchao kristo" alisema Pengo.

  Alisema kila mmoja wetu mahali alipo akitekeleza wajibu wake ipasavyo atambue anakuwa anatekeleza amani.

  Askofu mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dk. Alex Malasusa alisema Sikukuu ya Krismasi inamaanisha ni amani na ndio maana watu mbalimbali wamekuwa wakipeana zawadi kuashiria amani hivyo akawaomba wakristo na watu wote kuendeleza amani nchini. 

  Katika ibada hiyo ya mkesha wa Krismasi waumini walimiminika kwenye makanisa ya Anglikana la Mtakatifu Albano, Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam la Mtakatifu Joseph na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Azania Front huku wakiburudishwa na nyimbo za kusifu mungu za kuzaliwa kristo.

  0 0

  Jana Disemba 24, 2016 ilikuwa siku ya furaha kwa Bwana Godfrey Sinyangwe (kushoto) pamoja na Bi.Esther Kiluma (kulia), baada ya kufunga ndoa takatifu katika Kanisa la Saint Nicholas Jimbo Kuu la Mwanza chini ya Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo, Lazaro Manjelenga aliyesaidiana na Mchungaji Joseph Samwel.

   Zifuatazo ni baadhi ya picha zikionesha matukio katika hafla ya ndoa hiyo iliyofanyika usiku wa kuamkia leo, ukumbi uliopo Bugando Jijini Mwanza.
  #BMG
  Maharusi wakikata keki
  Maharusi wakilishana keki, kwa upendo kabisa
  Best man wa bwana harusi, Kabuji Noah (kushoto) pamoja na Best lady wa bi.harusi, Huruma Ntangu (kulia) wakilishana keki
  Mshereheshaji, Mc.Lama, akifungua shampaini kwa ustadi wa hali ya juu
  Ndugu, jamaa. marafiki na wageni waaikwa wakiwapongeza maharusi
  Wazazi wa pande zote mbili wakiwa neno la wosia kwa maharusi
  Ndugu, jamaa, marafiki na wageni waalikwa wakitoa zawadi kwa maharusi
  Kapu la bibi kama kawaida
  Msosi ulipikwa kwa ustadi mkubwa
  Maharusi wakilishana chakula
  Wazazi wakipata chakula
  Ni wasaa wa kufungua mziki
  Burudani ikiendelea
  Hafla hii imefana sana, shukrani kwa wote waliofanikisha akiwemo Mwenyekiti wa sherehe, Erica Elias. BMG inawatakiwa kila la kheri kwenye ndoa yenu, Bwana Godfrey Sinyangwe pamoja na Bi.Esther Kiluma.
  Tazama picha za ndoa HAPA

  0 0


  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

  MKUU wa Wilaya Ilala, Sophia Mjema ameagiza polisi kuacha mara moja kuwanyanyasa waendesha bodaboda na kutaka polisi kutumia mashine ya EFD pale wanapotoa faini kwa bodaboda hao.

  Kutumia mashine za EFD kutawafanya waendesha bodaboda kulipa ndani ya siku saba kama wanavyofanya kwa wenye bodaboda.

  Hata hivyo amesema maagizo ya mkuu wa Mkoa ya askari mgambo na ulinzi shirikishi wafanye kazi na watendaji wa kata na kuhoji kuwa mgambo na ulinzi shirikishi wanapenda kazi ya kukamata bodaboda.

  Mkuu wa Wilaya ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa bonanza la bodaboda jana lililofanyika Pugu, Jijini Dar es Salaam, Sophia amesema kunyanyasika kwa bodaboda kunatokana na baadhi yao kutotambua umuhimu wa kazi zao.Alifafanua kuwa “Ulinzi shirikishi na mgambo ni marufuku kuwasumbua bodäboda, kwani wanayo haki ya kufanya kazi na kuishi kwa amani kama ilivyo”.

  Sophia amesema licha ya kuwepo kero za bodaboda kukamatwa inatokana na baadhi yao kutopewa elimu ya usalama barabarani hivyo lazima wapewe elimu hata wakikosea watajua.Amesema wakati umefika wa kazi za bodaboda kuheshimika kudharau kazi hiyo inafanya wafanye kazi bila uhakika.

  Hata hivyo amesema kutokana na kupata malalamiko atafanya mkutano kati ya bodaboda na jeshi la polisi kwa ajili ya kutoa elimu ya pamoja na kutatua sintofahamu zinazojitokeza kwa bodaboda.
  .Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akiwa katika pikipiki kabla ya uzinduzi wa bonanza la Bodaboda Pugu jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akizungumza na waendesha bodaboda katika uzinduzi wa bonanza Pugu, jijini Dar es Salaam.Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
  Mrakibu Msaidizi wa Jeshi Polisi (ASP),Charle’s Kanyunyu akizungumza katika uzinduzi wa bonanza jana Pugu, jijini Dar es Salaam.
  Katibu wa Bodaboda wa Kituo cha Mombasa, Athuman Omary, akitoa kero wanazokutana nazo katika madereva wa bodaboda katika uzinduzi wa bonanza jana Pugu, jijini Dar es Salaam.
  Sehemu mdereva wa Bodaboda wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya Ilala, Sophia Mjema katika uzinduzi wa bonanza la Bodaboda Pugu jijini Dar es Salaam.

  0 0


  DC Kinondoni Ally Hapi

  Ndugu wana Dar es Salaam,

  Kwa niaba ya serikali ya Mkoa wetu, napenda kuchukua fursa hii kwa dhati kabisa kuwatakia waumini wote wa kikristo na wana Dar es salaam kwa ujumla sikukuu njema ya Christmas yenye furaha, upendo, amani na utulivu.

  Ni muhimu wana familia kuchukua tahadhari za kiusalama katika siku hii ikiwemo kuongeza umakini na uangalizi wa watoto maeneo ya fukwe (beach) ili kuondoa uwezekano wa maafa, kutoondoka nyumbani bila kuacha angalau mtu mmoja mzima wa kubaki kutazama usalama wa nyumba na kuzidisha umakini katika matumizi ya barabara.

  Tusisite kutoa taarifa kwa jeshi letu la polisi pindi tunapoona viashiria vya uhalifu au kuvunjika amani katika maeneo tuliyopo.

  Nawasihi tutumie siku hii kuiombea nchi yetu iendelee kuwa ya amani na utulivu, na tuwaombee viongozi wetu akiwemo Rais wetu mpendwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli na wasaidizi wake wote ili waendelee kuitumikia nchi yetu vema. 

  Aidha tuwajali wagonjwa, walemavu, yatima na watu wasiojiweza katika maeneo yetu tunayoishi ili nao waweze kusherehekea siku hii kwa furaha.

  Mwisho nawatakia heri, furaha na amani katika sikukuu hii ya Christmas.

  ALLY HAPI
  KAIMU MKUU WA MKOA
  DAR ES SALAAM

  0 0


  Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (kushoto) akimkabidhi mmoja wa watoto wa kituo cha yatima 'Yatima Group Trust Fund Mbagala Chamazi mfuko wa unga, . TTCL imekabidhi msaada wa bidhaa mbalimbali vikiwemo mchele, sukari, mafuta ya kupikia, soda, maji ya kunywa na mbuzi kwa ajili ya sherehe za Siku Kuu ya Chrismass. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Kituo cha Yatima Group Trust Fund Mbagala Chamazi.
  Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (wa pili kushoto) akimkabidhi mbuzi Mkurugenzi Msaidizi wa Kituo cha Yatima Group Trust Fund Mbagala Chamazi. TTCL imekabidhi msaada wa bidhaa mbalimbali vikiwemo mchele, sukari, mafuta ya kupikia, soda, maji ya kunywa na mbuzi kwa ajili ya sherehe za Siku Kuu ya Chrismass.
  Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (wa tatu kulia) akimkabidhi mmoja wa watoto wa kituo cha watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi cha Kimara SUCA maji ikiwa ni moja ya bidhaa zilizotolewa. TTCL imekabidhi msaada wa bidhaa mbalimbali vikiwemo mchele, sukari, mafuta ya kupikia, soda, maji ya kunywa na mbuzi kwa ajili ya sherehe za Siku Kuu ya Chrismass.
  Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (kushoto) akimkabidhi mfuko wa unga Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi cha Kimara SUCA, Evans Tegete ikiwa ni baadhi ya msaada uliotolewa na kampuni hiyo. TTCL imekabidhi msaada wa bidhaa mbalimbali vikiwemo mchele, sukari, mafuta ya kupikia, soda, maji ya kunywa na mbuzi kwa ajili ya sherehe za Siku Kuu ya Chrismass.
  Picha ya pamoja ya baadhi ya watoto kutoka vituo vyote vilivyosaidiwa na viongozi wao.
  Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (wa pili kushoto) akimkabidhi mbuzi mmoja wa watoto wa kituo cha watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi cha Kimara SUCA. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho, Evans Tegete.
  Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (kushoto) akimkabidhi mmoja wa watoto wa kituo cha yatima 'Yatima Group Trust Fund Mbagala Chamazi sehemu ya msaada uliotolewa na kampuni ya TTCL kwa ajili ya sherehe za Siku Kuu ya Chrismass.
  Picha ya pamoja baada ya shughuli ya kukabidhi misaada hiyo.
  Baadhi ya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu wakibeba sehemu ya misaada waliyokabidhiwa na TTCL.

older | 1 | .... | 1080 | 1081 | (Page 1082) | 1083 | 1084 | .... | 1898 | newer