Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46313 articles
Browse latest View live

KIDOKEZO CHA MAKALA: MAISHA YA WATU NA RASILIMALI WALIZOPEWA NA MWENYEZI MUNGU.

$
0
0
Baadhi ya akina mama wa Kijiji cha Ikonongo wilayani Kishapu, wakitoka Kliniki, ambapo baiskeli ni chombo kikuu cha usafiri katika wilaya hiyo.
#BMGHabari
Upendo Hotel ni moja ya hoteli kubwa zilizoko katika Kijiji cha Nyenze wilayani Kishapu.
Baadhi ya wakazi wa wilaya ya Kihapu wakimuaga mwandishi wa habari hii (hayupo pichani).

Baadhi ya wakazi wa vijiji vinavyozunguka na mgodi wa almasi katika wilaya ya kishapu mkoani shinyanga, wameelezea kutoridhishwa na uwepo wa wawekezaji wa madini katika wilaya hiyo kutokana na mchango wao mdogo kwenye shughuli za kimaendeleo.

Wakizungumza na Lake Fm, wakazi hao wamesema bado vijiji vingi wilayani kishapu vinakumbwa na changamoto kadhaa ikiwemo ukosefu wa huduma za afya, maji, miundombinu ya umeme pamoja na barabara, na kwamba wajibu wao kimaendeleo umekuwa mdogo ikilinganishwa na neema ya madini iliyopo katika wilaya hiyo.

Akizungumzia wajibu wa wawekezaji hususani wa madini katika maeneo mbalimbali nchini, Mwanasheria kutoka Taasisi ya Demokrasia na Utawala Bora ADLG, Carolina Tizeba, amesema sheria ya madini ya Mwaka 2010, kifungu cha 10 inawataka wawekezaji kuwajibika kwa ajili ya maendeleo ya jamii kwenye maeneo waliyowekeza.

USIKOSE KUFUATILIA MAKALA YA "MAISHA YA WATU NA RASILIMALI WALIZOPEWA NA MWENYEZI MUNGU" HIVI KARIBUNI, KUPITIA 102.5 LAKE FM MWANZA NA BMG HABARI.

TSN YAADHIMISHA MIAKA 10 YA GAZETI LAKE LA HABARILEO

$
0
0
 Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) Wachapaji wa magazeti ya Daily News, Sunday News, Habarileo, Habarileo Jumapili na Spotileo imeadhimisha miaka 10 tangu kuanza kwa gazeti la Habarileo mnamo Desemba 21,2006 kwa kukata keki huku Uongozi wa Kampuni hiyo ukitangaza shamra shamra za mwezi mmoja wa kusherehekea kuzaliwa kwa gazeti hilo.

Aidha ili kushirikiana na wadau wengine, Kampuni imetangaza punguzo la asilimia 30 kwa mteja atakeatangaza tangazo lake ndani ya siku 30 za shamrashamra katika gazeti la Habarileo.
 Miongoni mwa wageni maalum waliohudhuria sherehe hizo ni Mhariri Mtendaji wa zamani wa TSN, Isack Mruma (wapili kulia) ambaye kwa sasa ni Ofisa wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambaye alishiriki kukata keki pamoja na Mhariri Mtendaji wa sasa Dk Jim Yonaz (wapili kushoto) na Naibu Mharidi Mtendaji, Tuma Abdallah. Kushoto akishuhudia ni Meneja Mauzo na Masoko, Januarius Maganga. 
 Naibu Mharidi Mtendaji, Tuma Abdallah akimlisha keki Kaimu Mhariri wa Gazeti la Habarileo, Nicodemus Ikonko.
 Shangwe za miaka 10 ya Habarileo.
 ME wa zamani wa TSN Isack Mruma akilishwa keki na ME wa TSN Dk Jim Yonazi.BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI.
 Ilikuwa ni furaha sana kwa viongozi hawa .
 Isack Mruma akimlisha keki Dk Jim Yonazi.
 Isack Mruma akizungumza katika shamra shamra hizo na kuelezea changamoto mbalimbali alizokumbana nazo tangu kuanza kwa gazeti hilo.
 Wafanyakazi wa TSN wakifuatailia
 Mruma akizungumza na viongozi wa TSN kumsikiliza kwa makini.
 Isack Mruma akiagana na wafanyakazi wa gazeti la Habarileo ambao wengi wao alianza nao gazeti hilo.
 Dk Jim Yonazi (kushoto) akimsindikiza Isack Mruma
Picha ya pamoja ilipigwa.

ZIARA YA SHAKA MISENYI NA BUKOBA MJINI YAFANA

$
0
0
 Kaimu Katibu Mkuu Uvccm Shaka Hamdu Shaka Alipo tembezwa na Mkuu wa Wilaya ya Kyelwa Kuona Athari zilizo tokana  na Mvua ya Mawe  Zilizo Wakumba Wananchi wa kijiji Kangenyi Kata ya Kieluwa Wilayani Kyelwa
vcm-1
Mhandisi wa Maji wilaya Misenyi ABdallah Gendaheka wa tatu kutoka kushoto akitoa maelezo mbele ya kaimu katibu mkuu wa UVCCM na msafara wake walipoutembelea mradi huo wa maji ambao kati ya vituo 15 ni vituo vi8tu vinavyotoa na saba kwa mwaka mmoja na miezi miwili sasa vimeharibik
vcm-2
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM  Shaka Hamdu Shaka akipata maelezo toka kwa Afisa Mfawidhi wa Mpaka wa Mutukula Bw.Samwel Mori wilayani Misenyi Mkoani Kagera alipotembelea katika mpaka huo kuangalia shughuli za kihuduma katika mpaka huo.
vcm-3
 Mapokezi ya Kaimu Katibu Mkuu Uvccm Shaka Hamdu Shaka  alipo Wasili Bukoba Mjini
vcm-4
Watendaji na wakuu wa Idara katika Halmashauri ya Manispa ya mji wa Bukoba wakimsikiliza Ndg:Kaimu Katibu Mkuu Uvccm Shaka Hamdu Shaka alipotembelea Manispaa hiyo
vcm-5
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kagera Ndg:Yahya kateme wa tatu toka kushoto alipoingia na mgeni wake Kaimu Katibu Mkuu Uvccm Shaka Hamdu Shaka wa pili kushoto katika  kiwanda cha uzalishaji maji safi  Bunena Spring Water katika manispaa ya mji wa bukoba wa nne kulia ni mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya bukoba mjini Ashraf kazinja
vcm-6
Katibu wa UVCCM Mkoa wa Kagera  Dismas Zimbihire wa kwanza kulia akiongoza msafara na kumfikisha Kaimu katibu mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka katika eneo la uzakishaji Maji na ufungaji wa chupa katika kiwanda cha  Bunena Spring Water kilichopo katika manispaa ya mji wa bukoba.
vcm-7
Makundi ya Vijana wajasiriamali wakiwemo Mamalishe,bodaboda,na machinga walipompokea kwa shangwe na hoihoi  Kaimu Katibu Mkuu Uvccm Shaka alipokwenda kuwatembelea katika soko la machinjioni kwenye manispaa ya mji wa bukoba.
vcm-9
 Kaimu katibu wa Idara ya Hamasa,Sera,Utafiti na Mawasiliana UVCCM Mtemi Slyvester yaredi akizungumza na makundi ya wajasiriamali katika manispaa ya mji wa bukoba kabla ya kumkaribisha Kaimu katibu mkuu UVCCM
vcm-10
 ”Nimefarijika saana na ziara ya mkoa wa Kagera,nimefurahi kuwakuta viongozi wa chama,Serikali kuu na Halmashauri za wilaya wakifanya kazi bega kwa bega kwa lengo la kuhudumia wananchi na kutekeleza matakwa ya sera za CCM zilizoainishwa katika ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020”Shaka alimueleza mkuu wa mkoa wa Kagera Meja jenerali Salum kijuu alipomtembelea ofisini kwake
vcm-11
”Nimekua nikifuatilia ziara zenu kwa karibu sana,nimeridhika na uibuwaji wenu wa maswala yenye manfaa,kuzindua miradi ya kimaendeleo lakini pia kuzungumza na wanachama wenu katika vikao vya ndani vya kisiasa.Changamoto mlizoziona serikali itaendelea kuzifanyia kazi na kupata utatuzi,tutasiliba na kuziba mianyayote inayopitisha wahamiaji haramu na kukomesha vitendo vya uhalifu,hatutashindwa kwa jambo lolote”Meja jenerali Kijuu alimueleza kaimu katibu mkuu UVCCM

​DC MUFINDI AFANYA ZIARA KIWANDA CHA CHAI KUFUATIA TISHIO LA KUFUNGWA KWA KIWANDA HICHO

$
0
0


 DC Jamhuri William na mmoja wa mameneja akipata maelezo ndani ya kiwanda.
 Mkuu wa usalama wa taifa wa Wilaya ya Mufindi  aliyevalia shati jeupe akichachangia hoja baada ya kukagua sehemu ya shehena ya mifuko mikubwa ya chai huku Mkuu wa wilaya JAMHURI WILLIAM mwenye vazi la suti nyeusi
 Mkuu wa Wilaya Jamhuri William pamoja na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wakitembezwa ndani ya kiwanda
 Ndani ya kiwanda cha MTC na hizi ni mitambo inayotumika kuchakata chai.
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa Wilaya ya Mufindi wakimsikiliza mmoja kati ya mameneja wa kiwanda hicho.

Na afisa habari Mufindi


Mkuu wa Wilaya ya Mufindi JAMHURI WILLIAM amefanya ziara katika kiwanda cha chai MTC kilichopo kijiji cha ITONA halmshauri ya Wilaya ya Mufundi baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa mwekezaji wa kiwanda hicho anakusudia kukifunga.

Mkuu wa Wilaya ameamua kufanya ziara kiwandani hapo akiwa na kamati yake ya ulinzi na usalama ya Wilaya ili kufanya mazungumzo na mwekezaji huyo ajue tatizo nini mpaka afikirie kufunga kiwanda na kuhatarisha maisha ya watu wa Mufindi ambao wanaendesha maisha yao kwa kutegemea kiwanda hicho kwani kiwanda hicho pekee kimeajiri zaidi ya watu elfu 50.

Baada ya mazungumzo marefu, mwekezaji huyo alimhakikishia mkuu wa Wilaya kuwa kiwanda hicho hakitafungwa licha ya changamoto za kiuchumi anazozipitia ambazo zimesababisha tanesko wakate umeme kwa kuchelewa kulipa bili ya mwezi mmoja ya Zaidi ya shilingi milioni 100, kisha akamuomba Mkuu wa Wilaya asaidie baadhi ya changamoto zinazotokana na masuala ya kisera.

Halmshauri ya wilaya ya Mufindi inajumla ya makapuni makubwa matano (5) yaliyowekeza kwenye viwanda vya kuchakata chai kutokana na hali ya hewa rafiki kwa kilimo cha chai.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA WAZIRI MKUU MAJALIWA IKULU JIJINI DAR

$
0
0
 Rais John Magufuli  akisalimiana na  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Ikulu jijini Dar es salaam Desemba 23, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Rais John Magufuli akiteta na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Ikulu jijini Dar es salaam, Desemba 23, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri `Mkuu)

  Rais John Magufuli akiteta na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Ikulu jijini Dar es salaam, Desemba 23, 2016. 
 Rais John Magufuli akizungumza na mtoto  Doreen Ndika ambaye aliambatana na baba yake, Jaji Dkt. Gerald Ndika ambaye aliyeapishwa na Rais `Ikulu jijini Dar es salaam Desemba 23, 2016 kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NEWZ ALERT....MPIGANAJI MWENZETU MPOKI BUKUKU AMEFARIKI DUNIA

$
0
0
 Mpiga picha maarufu Mpoki Bukuku amefariki dunia leo katika Taasisi ya Mifupa (MOI), alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano kwa Umma (MOI) Almas Jumaa.

"Ni kweli Mpoki amefariki dunia mchana huu, alipokelewa jana usiku baada ya kupata ajali ya gari maeneo ya Mwenge  ITV, taarifa zaidi tutazitoa baadaye," alisema Almas.

Mpoki Bukuku amewahi kufanya kazi kama Mpiga Picha Mkuu katika gazeti la Mwananchi, linalochapisha magazeti ya Mwananchi, The Citizen na Mwanaspoti. Pia amewahi kufanya kazi magazeti kadhaa likiwemo Majira na Nipashe.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEME PEPONI-AMIN

RAIS MAGUFULI AFANYA UAPISHO WA MWENYEKITI NEC, KAMISHNA WA MAADILI NA MAJAJI WA MAHAKAMA YA RUFANI

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Jaji Semistocles Kaijage kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) anayechukua nafasi ya Mhe. Jaji Mstaafu Damian Lubuva aliyemaliza Muda wake, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Mhe. Jaji Semistocles Kaijage akisaini hati ya kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa kiapo cha kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Jaji Mstaafu Hamid Mohamed Hamid kuwa Makamu kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapishaJaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Mhe. Jaji Harold Nsekela kuwa Kamishna wa Maadili katika Sekretariat ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Jaji Rehema Kiwanga Mkuye kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Jaji Sivangilwe Sikalaliwa Mwangesi kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi vitendea kazi Mhe. Jaji Dkt. Gerald Ndika kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhe. Jaji Jackobs Mwambegele kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
 Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa wakiwa katika picha ya pamoja na Majaji wa Mahakama za Rufani leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) (wakwanza kushoto) na aliyekuwa Mhe. Jaji Mstaafu Damian Lubuva aliyemaliza muda wake.

PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO

WIZARA YA VIWANDA,BIASHARA NA UWEKEZAJI YAPOKEA TUZO YA UBORA WA UWASILISHAJI WA TAARIFA YA FEDHA KWA MWAKA 2015

$
0
0
 Katibu Mkuu wa wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Dr. Adelhelm Meru, akipokea tuzo ya ushindi wa kwanza kwa kundi  la Wizara na Idara za Serikali ya ubora wa uwasilishwaji wa taarifa ya fedha kwa mwaka 2015 kutoka kwa mhasibu mkuu wa Wizara Bi. Rose Janeth Bandisa.
 Picha ya pamoja ya Katibu Mkuu wa wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Dr. Adelhelm Meru, wahasibu na wakaguzi wa ndani wa Wizara.
Tuzo ya ushindi wa kwanza kwa kundi la Wizara na Idara za Serikali ya ubora wa uwasilishwaji wa taarifa ya fedha kwa mwaka 2015. Tuzo hii hutolewa kila mwaka na bodi ya taifa ya wahasibu na wakaguzi (NBAA). Picha na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.


WATUMISHI WA WIZARA YA KATIBA WAKIPOKEA MAPENDEKEZO KUHUSU SHERIA YA NDOA YA 1971 NA SHERIA YA MSAADA WA KISHERIA

$
0
0
 Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Bw. Aloyce Mwogofi (aliyesimama kushoto) akiongea katika Kikao na watumishi wa Wizara hiyo wakati wakipokea taarifa ya mapendekezo ya sheria ya Ndoa ya 1971 na utungwaji wa sheria ya msaada wa kisheria, leo katika ukumbi wa wizara hiyo.
 Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria wakimsikiliza kwa makini mtoa  taarifa ya  mapendekezo ya sheria ya Ndoa ya 1971 na utungwaji wa sheria ya msaada wa kisheria Bw Sabath Cazmiry (wa tatu kushoto), leo katika ukumbi wa wizara hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Bw. Amon Mpanju (kushoto) akisisitiza jambo kwa watumishi wa Wizara hiyo wakati wa kikao cha kupokea  taarifa ya  mapendekezo ya sheria ya Ndoa ya 1971 na utungwaji wa sheria ya msaada wa kisheria leo, katika ukumbi wa wizara hiyo.

MUNGAI ASAIDIA YATIMA IRINGA MISAADA YA TSH MILIONI 4.5 KWA AJILI YA SIKUKUU YA KRISMAS

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela (kushoto ) na mfanyabiashara Geofrey Mungai wakiwa wamewapakata watoto yatima wa kituo cha Daily Bread Life Ministres cha Mkimbizi katika Manispa ya Iringa waliokuwa wametupwa na wazazi wao na kuchukuliwa na kituo hicho jana wakati Mungai alipofika kukabidhi chakula na nguo za sikukuu ya Krismas na mwaka mpya kwa watoto hao 
Mkuu wa wilaya ya Iringa Bw Kasesela akisalimiana na Geofrey Mungai kulia 









Bw Mungai akiwa na mmoja kati ya watoto yatima wanaolelewa kituo cha DBL 
Viongozi mbali mbali wakiwa katika picha ya pamoja na yatima wa kituo cha DBL kutoka kushoto ni mkurugenzi wa kituo hicho mchungaji Mpeli Mwaisumbe , mfadhili Geofrey Mungai , katibu wa CCM Iringa , mwenyekiti wa CCM Iringa mjini , mkuu wa wilaya ya Iringa Bw kasesela,mbunge viti maalum Iringa Ritta kabati ,diwani Dolla Nziku 

Mtoto wa mbunge Mwamoto Leah akitoa ahiadi yake ya Tsh 50000 kwa ajili ya kusaidia yatima 
katibu wa CCM Iringa mjini akiahidi kuchangia yatima hao 
Mbunge Kabati akiahidi kuchangia Tsh 500,000 kwa ajili ya Yatima hao



Na MatukiodaimaBlog .
WATOTO yatima wa kituo cha Daily Bread Life Ministres cha Mkimbizi katika Manispa ya Iringa na wale wa kituo cha Tosamaganga katika wilaya ya Iringa Iringa wapewa msaada wenye nguo na chakula msaada wenye thamamani ya Tsh milioni 3 kwa ajili ya sikukuu ya Chrismas na mwaka mpya .

pamoja na msaada huo wa chakula na mavazi pia Mungai aliahidi kuchangia Tsh milioni 1.5 kwa ajili ya ununuzi wa vyombo vya muziki katika kituo hicho na kufanya msaada wake kufikia Tsh milioni 4.5 


Huku mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela pamoja na kumshukuru mfanyabiashara huyo kwa kukumbuka yatima bado ametoa onyo kali kwa wanawake wote wanaotupa watoto kuwa ikibainika watachukuliwa hatua kali .






Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo Geofrey Mungai alisema imekuwa ni kawaida ya familia yake kila mwaka kusherekea sikukuu mbali mbali pamoja na watoto yatima kama sehemu ya kuikumbusha jamii kuwa na utamaduni wa kuwatazama yatima hao ambao tegemeo lao kubwa ni jamii inayowazunguka.






Mungai alisema kuwa suala la kulea yatima linapaswa kuwa ni jukumu la watanzania wote na kuwa ili kuwawezesha watoto hao kujisikia ni sehemu ya familia zenye wazazi ni vema jitihada za vituo vya yatima hapa nchini kuendelea kuheshimika zaidi.






Hata hivyo Bw.Mungai alisifu kazi nzuri inayofanywa na kituo hicho cha DBL katika kuendelea kuwalea watoto ha kimwili na kiroho na kuendelea kuwa miongoni mwa vituo bora vya kulea yatima katika mkoa wa Iringa.






Aidha aliwataka wananchi wengine kuendelea kufika katika kituo hicho na kusaidia kulea watoto hao kwa kutoa misaada mbali mbali kama njia ya kuwafariji na kuwalea watoto hao kuliko kuwaachia walezi wao pekee.






Hivyo alisema kwa mwaka huu amelazimika kutoa msaada wa nguo na chakula kwa kila kituo msaada wenye thamani ya Tsh milioni 1.5 na kuwa ataendelea kufanya hivyo kwa ajili ya watoto hao ili siku ya sikukuu nao waweze kufafana na watoto wengine ambao wanawazazi wao wote wawili .










Mkurugenzi mkuu wa kituo hicho mchungaji Mpeli Mwaisumbe Bw. Tukuswiga Mwaisumbe alisema kuwa kituo chake cha DBL kilichopo chini ya  usimamizi wa mchungaji Neema Mwaisumbe kina watoto yatima 43 na kuwa maendeleo ya kituo hicho yametokana na jitihada za wadau mbali mbali ambao wameendelea kujitolea kusaidia kituo hicho.






Alisema kuwa mbali ya familia hiyo ya Mungai kuendelea kutoa msaada wakati wa sikukuu mbali mbali kwa watoto hao bado michango yake imeendelea kuwa chachu kwa wadau wengine kujitokeza kusaidia watoto hao kwa misaada mbali mbali .






Hata hivyo alisema kuwa wadau wanaoendelea kusaidia kituo hicho ni wengi zaidi na kuwa kwa umoja wao kituo hicho kinaendelea kuthamini michango yao na kuomba kuzidi kujitolea zaidi kwa ajili ya watoto hao kwa ajili ya kuona watoto hao wanapata elimu Kituo hicho ambacho kina zaidi ya miaka 15 15 toka kuanzishwa kwake kimefanikiwa kuanzisha shule yake ya Sekondari iliyopo kijiji cha Mgera ambayo inapokea na watoto wengine kwa kuchangia ada ndogo zaidi kuzindua shule ya sekondari .






kama umeguswa na jitihada za wale wote wanaojitolea kusaidia yatima wa kituo hiki cha DBL mkimbizi Iringa unaombwa kuchangia mchango wako wowote kupitia namba hii ya mkurugenzi mtendaji wa kituo hiki mchungaji Mpeli kupitia huduma ya TIGO PESA 0719239936 na M-PESA ni 0754362536 na Mungu atakubariki na kukuongezea pale ulipopunguza.






Aidha alishukuru ushirikiano kubwa ambao umekuwa ukionyeshwa na wadau mbali mbali kama mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu ambae amekuwa akijitolea kusomesha baadhi ya watoto elimu ya msingi kwenye shule yake ya Star pia mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela  pamoja na wadau wengine mbali mbali .






Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Iringa Kasesela alisema kuwa hatapenda kuona katika wilaya yake watoto wanaendelea kutupwa ama kutelekezwa na wazazi wao baada ya kuzaliwa na kutaka wananchi kutoa ushirikiano kwa kuwafichua wale wote wanaotupa watoto .






Mkuu huyo wa wilaya kwa kushirikiana na mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati (CCM) kwa ajili ya kuungana na Mungai kusaidianbsp; watoto hao walichangia Tsh milioni moja 





















SABODO AMSHAURI RAIS MAGUFULI ABADILISHE FEDHA

$
0
0
Mfanyabiashara maarufu nchini, Mustafa Jaffar Sabodo akizungumza jijini Dar es Salaam, kuhusu wafanyabiashara wanaoficha fedha majumbani na kumshauri Rais John Magufuli abadilishe fedha. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA)
Sabodo akisisitiza jambo

Mfanyabiashara maarufu nchini, Jaffar Sabodo (73), amemshauri Rais John Magufuli abadilishe fedha ili kubana wafanyabiashara wakwepa kodi na kuficha fedha majumbani.

Aidha, amesema kutokana na utendaji wa Rais, haoni sababu za vyama vya upinzani kuendelea kumpinga, na badala yake waache siasa na waungane naye kujenga Tanzania mpya.

Kauli ya mfanyabiashara huyo iliungwa mkono na wachumi waliozungumza na gazeti hili kubainisha kuwa njia nzuri zaidi ni Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kupunguza masharti kwa benki, hasa viwango vya riba, ili riba kwenye benki iwe kubwa jambo ambalo litafanya watu wakiweka fedha benki wapate faida.

Sabodo alitoa ushauri huo jana alipozungumza na JAMBO LEO katika mahojiano maalumu nyumbani kwake Dar es Salaam, ambapo alisema licha ya hatua nzuri za Serikali ya Rais Magufuli kiuchumi na kwenye mapambano dhidi ya rushwa, ubadhirifu na ufisadi, wapo walioficha mabilioni ya fedha nyumbani badala ya benki ili kukwepa kodi.

“Rais anafanya kazi nzuri, lakini ni wengi walioficha fedha nyumbani. Watanzania wanakufa njaa, wengine wameficha fedha. Hapo nashauri Rais abadilishe fedha hasa noti za Sh 5,000 na Sh 10,000. Hatua hiyo itasaidia kukabili ubadhirifu unaofanywa na watu wenye nia mbaya, lakini pia inaweza kuokoa uchumi na kufikia ndoto ya kuwa na Tanzania Mpya,” alisema Sabodo.

Aliongeza: “Kwa maoni yangu, hatua hiyo ya kubadilisha fedha ichukue kati ya mwezi mmoja na mmoja na nusu, watabainika wengi walioficha fedha nyumbani na hali ya uchumi itabadilika.”

Akifafanua, Sabodo ambaye ni mzaliwa wa Lindi, alisema India, Pakistan na Venezuela ziliwahi kukumbwa na hali kama iliyopo sasa nchini, lakini hatua ya kubadilisha noti ilizisaidia kuimarisha uchumi na bajeti zao.

“Watu wanaiba fedha nyingi, wanazificha chini ya magodoro, ili kumaliza hali hiyo ni muhimu noti zikabadilishwa hali itakayomlazimisha kila aliyeficha fedha kuzitoa, hapo wapo watakaokimbia nchi,” alisema Sabodo huku akitaja baadhi ya watakaokimbia hatua hiyo ikichukuliwa.

Sabodo alitoa kauli hiyo wakati Rais Magufuli ameshatoa kauli kuwataka walioficha fedha majumbani kuziacha ziingie kwenye mzunguko huku akionya wasipofanya hivyo anaweza kuamua kuzibadili ili wakose mahali pa kuzipeleka. 

Magufuli alitoa kauli hiyo Septemba kwenye mkutano wa 14 wa mwaka wa wahandisi ambapo alisema watu hao wamekuwa na utaratibu wa kutoa fedha zao benki na kuzificha kwa kuogopa kuwa atabaini kiasi walichonacho.

Wachumi

Akizungumzia suala hilo, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (Sua), Profesa Damian Gabagambi alisema: “Kuendesha uchumi hakutakiwi nguvu sana. Uchumi unajengwa kwa imani, mtu yeyote anayeendesha uchumi anatakiwa kuijenga hiyo imani na ikuzwe.

“Chochote kinachofanyika na kuua imani kinavuruga uchumi, ukiona watu wanaficha fedha hilo si tatizo, ni kwamba kuna kitu ambacho ni tatizo, kuficha fedha ndio kujihami kwao.”

Alisema njia nzuri ya kufanya watu walioficha fedha kuzitoa, ni BoT kupunguza masharti inayowekea benki, hasa viwango vya riba, ili riba kwenye benki iwe kubwa, jambo ambalo litafawanya watu kutoficha fedha kwa maelezo kuwa wakipeleka fedha kwenye benki hizo, watapata faida.

Alisema riba inayotozwa kwenye benki inapangwa na BoT na kuitaka benki hiyo kufanya marekebisho ili kusaidia wanaoweka fedha kwenye benki kupata faida.

“Ila kama wana hakika fedha zimefichwa na wahusika hawawezi kuzitoa, njia pekee ni kutishia kuchapisha, ingawa hiyo ni njia ya haraka sana. Pamoja na hayo, muhimu ni kuhakikisha chanzo cha watu kuficha fedha kinajulikana,” alisema

Mhahidhi Mwandamizi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dk Haji Semboja alisema: “Katika uchumi ambao unakwenda vizuri na mamlaka zinazohusika na usimamizi wa fedha zinafanya kazi, suala hilo (kuficha fedha) haliwezi kujitokeza kwa maana mwenye fedha atajua jinsi ya kuziweka.

“Katika uchumi ambao watu wamekaa na kuhodhi fedha majumbani mwao ukitaka fedha hizo ziingie kwenye mzunguko basi unazibadilisha. Watu watazileta kwa nguvu maana hawatakuwa na ujanja. Ila kubadili fedha kuna sababu nyingi.”

Alisema sababu nyingine ni kutaka kubadili fedha ili kuwa na mwonekano mpya, pamoja na ubora wake ikiwa za awali zilikuwa zikichakaa mapema.

“Watu kukaa na fedha ndani ni kutoelewa mifumo ya kisasa ya kibiashara, watu wanaofanya hivyo ni wanaofanya shughuli ambazo haziko kwenye mfumo wa ulipaji kodi,” alisema.


Mfanyabiashara maarufu nchini, Mustafa Jaffar Sabodo akizungumza jijini Dar es Salaam, kuhusu wafanyabiashara wanaoficha fedha majumbani na kumshauri Rais John Magufuli abadilishe fedha. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA)
Sabodo akisisitiza jambo

Mfanyabiashara maarufu nchini, Jaffar Sabodo (73), amemshauri Rais John Magufuli abadilishe fedha ili kubana wafanyabiashara wakwepa kodi na kuficha fedha majumbani.

Aidha, amesema kutokana na utendaji wa Rais, haoni sababu za vyama vya upinzani kuendelea kumpinga, na badala yake waache siasa na waungane naye kujenga Tanzania mpya.

Kauli ya mfanyabiashara huyo iliungwa mkono na wachumi waliozungumza na gazeti hili kubainisha kuwa njia nzuri zaidi ni Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kupunguza masharti kwa benki, hasa viwango vya riba, ili riba kwenye benki iwe kubwa jambo ambalo litafanya watu wakiweka fedha benki wapate faida.

Sabodo alitoa ushauri huo jana alipozungumza na JAMBO LEO katika mahojiano maalumu nyumbani kwake Dar es Salaam, ambapo alisema licha ya hatua nzuri za Serikali ya Rais Magufuli kiuchumi na kwenye mapambano dhidi ya rushwa, ubadhirifu na ufisadi, wapo walioficha mabilioni ya fedha nyumbani badala ya benki ili kukwepa kodi.

“Rais anafanya kazi nzuri, lakini ni wengi walioficha fedha nyumbani. Watanzania wanakufa njaa, wengine wameficha fedha. Hapo nashauri Rais abadilishe fedha hasa noti za Sh 5,000 na Sh 10,000. Hatua hiyo itasaidia kukabili ubadhirifu unaofanywa na watu wenye nia mbaya, lakini pia inaweza kuokoa uchumi na kufikia ndoto ya kuwa na Tanzania Mpya,” alisema Sabodo.

Aliongeza: “Kwa maoni yangu, hatua hiyo ya kubadilisha fedha ichukue kati ya mwezi mmoja na mmoja na nusu, watabainika wengi walioficha fedha nyumbani na hali ya uchumi itabadilika.”

Akifafanua, Sabodo ambaye ni mzaliwa wa Lindi, alisema India, Pakistan na Venezuela ziliwahi kukumbwa na hali kama iliyopo sasa nchini, lakini hatua ya kubadilisha noti ilizisaidia kuimarisha uchumi na bajeti zao.

“Watu wanaiba fedha nyingi, wanazificha chini ya magodoro, ili kumaliza hali hiyo ni muhimu noti zikabadilishwa hali itakayomlazimisha kila aliyeficha fedha kuzitoa, hapo wapo watakaokimbia nchi,” alisema Sabodo huku akitaja baadhi ya watakaokimbia hatua hiyo ikichukuliwa.

Sabodo alitoa kauli hiyo wakati Rais Magufuli ameshatoa kauli kuwataka walioficha fedha majumbani kuziacha ziingie kwenye mzunguko huku akionya wasipofanya hivyo anaweza kuamua kuzibadili ili wakose mahali pa kuzipeleka. 

Magufuli alitoa kauli hiyo Septemba kwenye mkutano wa 14 wa mwaka wa wahandisi ambapo alisema watu hao wamekuwa na utaratibu wa kutoa fedha zao benki na kuzificha kwa kuogopa kuwa atabaini kiasi walichonacho.

Wachumi

Akizungumzia suala hilo, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (Sua), Profesa Damian Gabagambi alisema: “Kuendesha uchumi hakutakiwi nguvu sana. Uchumi unajengwa kwa imani, mtu yeyote anayeendesha uchumi anatakiwa kuijenga hiyo imani na ikuzwe.

“Chochote kinachofanyika na kuua imani kinavuruga uchumi, ukiona watu wanaficha fedha hilo si tatizo, ni kwamba kuna kitu ambacho ni tatizo, kuficha fedha ndio kujihami kwao.”

Alisema njia nzuri ya kufanya watu walioficha fedha kuzitoa, ni BoT kupunguza masharti inayowekea benki, hasa viwango vya riba, ili riba kwenye benki iwe kubwa, jambo ambalo litafawanya watu kutoficha fedha kwa maelezo kuwa wakipeleka fedha kwenye benki hizo, watapata faida.

Alisema riba inayotozwa kwenye benki inapangwa na BoT na kuitaka benki hiyo kufanya marekebisho ili kusaidia wanaoweka fedha kwenye benki kupata faida.

“Ila kama wana hakika fedha zimefichwa na wahusika hawawezi kuzitoa, njia pekee ni kutishia kuchapisha, ingawa hiyo ni njia ya haraka sana. Pamoja na hayo, muhimu ni kuhakikisha chanzo cha watu kuficha fedha kinajulikana,” alisema

Mhahidhi Mwandamizi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dk Haji Semboja alisema: “Katika uchumi ambao unakwenda vizuri na mamlaka zinazohusika na usimamizi wa fedha zinafanya kazi, suala hilo (kuficha fedha) haliwezi kujitokeza kwa maana mwenye fedha atajua jinsi ya kuziweka.

“Katika uchumi ambao watu wamekaa na kuhodhi fedha majumbani mwao ukitaka fedha hizo ziingie kwenye mzunguko basi unazibadilisha. Watu watazileta kwa nguvu maana hawatakuwa na ujanja. Ila kubadili fedha kuna sababu nyingi.”

Alisema sababu nyingine ni kutaka kubadili fedha ili kuwa na mwonekano mpya, pamoja na ubora wake ikiwa za awali zilikuwa zikichakaa mapema.

“Watu kukaa na fedha ndani ni kutoelewa mifumo ya kisasa ya kibiashara, watu wanaofanya hivyo ni wanaofanya shughuli ambazo haziko kwenye mfumo wa ulipaji kodi,” alisema.

MKUU WA WILAYA YA ILALA, SOPHIA MJEMA AKABIDHI ZAWADI ZA KAPU LA SIKUKUU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (katikati), akimkabidhi zawadi, Asha Soud ambaye ni mshindi la shindano la Kapu la Sikukuu Dar es Salaam leo, lililoendeshwa na Kampuni ya Multichoice Tanzania kwa kushirikiana na Kituo cha Redio cha EFM. Kutoka kulia ni msanii Haji Salum 'Mboto' Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Alpha Joseph na Mkurugenzi wa EFM, Francis Cizza.
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (katikati), akimkabidhi zawadi msanii Irene Paul.
 Maelekezo ya upokeaji wa zawadi hizo yakitolewa.
 DC Mjema akizungumza na wanahabari baada ya kukabidhi zawadi hizo.
 Washindi wa shindano hilo wakiwa katika picha ya pamoja.
 Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Alpha Joseph (kulia) akimkabidhi zawadi Kelvin Mhenzi
Washindi wakiondoka na zawadi zao.

Na Dotto Mwaibale

MKUU wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema ametoa zawadi mbalimbali kwa washindi 24 wa shindano la Kapu la Sikuu lililoendeshwa na Kampuni ya Multichoice Tanzania na Kituo cha Redio cha EFM.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi hizo Dar es Salaam leo DC Mjema aliwataka wananchi kuendelea kufuatilia kwa karibu vipindi mbalimbali vinavyotangazwa na kituo hicho ili waweze kujipatia zawadi kutokana na kujibu maswali yatokanyo na vipindi hivyo  na kuweza kupata zawadi kama walizopata wenzao katika kipindi hiki cha Sikukuu.

"Napenda kuwapongezwa EFM kwa shindano hili kwani linatoa msukumo kwa wananchi wa kusikiliza vipindi mbalimbali vyenye manufaa" alisema Mjema.

Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Alpha Joseph akizungumza katika hafla hiyo alisema kampuni hiyo kupitia kisambuzi chake cha DSTV imemwaga zawadi ya visambuzi vya kisasa vipatavyo 24 pamoja na vifurushi vya mwezi mzima kwa washindi wa shindano hilo la Kapu la Sikuu.

"Washindi hao wataweza kusherehekea Sikukuu ya krismas na mwaka mpya kwa kuangalia chaneli zaidi ya 70 za DStv ikiwemo mpira wa ligi ya Hispania (Laliga) na ligi ya Uingereza" alisema Joseph

Alpha alisema Multichoice Tanzania haijawatunuku washindi hao 24 wa kapu la Sikuu pekee bali watanzania wote kwa ujumla kwani hivi karibuni walishusha bei za vifurushi vyao kwa wastani wa asilimia 16, huku kifurushi maarufu cha DStv Bomba chenye chaneli zaidi ya 70 kikipunguzwa bei hadi sh.19,975 tu.

Zawadi hizo kwa washindi hao zilitolewa na wasanii waigiza maarufu nchini kama Muhogo Mchungu, Riyama Ali, Haji Salum Mboto na Hashim Kambi wanaoonekana katika Tamthilia ya Huba.

SUALA LA KUACHIANA VITI VYA KUGOMBEA UBUNGE NA UDIWANI KWA UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI (UKAWA)BADO KIZUNGUMKUTI ARUSHA

$
0
0
Mwenyekiti mwenza wa Ukawa James Mbatia akiwa na Viongozi wa CUF mkoa wa Arusha Mwenye shati la blue ni Katibu mkuu wa chama cha wananchi (CUF)mkoa wa Arusha Zuberi Mwinyi baada ya mazungumzo ya ushirikiano wa ukawa Hotel ya Safari jijini Arusha picha na Maktaba

                                       
                                   
                                        Na Mahmoud Ahmad Arusha.

Suala la kuachiana viti vya kugombea udiwani,ubunge  kwa umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA)bado kizungumkuti katika Kata ya Mateves wilayani Arumeru  ambapo CUF na CHADEMA wasimamisha wagombea hali inayopelekea kugawa kura za wagombea hao wa Ukawa.

Akizungumza na wanahabari Ofisini kwake Mkurugenzi wa Uchaguzi mkoa wa CUF Arusha Zuberi Mwinyi alisema kuwa wao wamesimamisha mgombea kwenye kata hiyo kutokana na mgombea wao kukubalika kwenye kata hiyo hivyo kuwataka wenzao kuwaachia kata hiyo kwani wanazo kata nyingi kwenye maeneo hayo.

Mwinyi alisema kuwa Tulikuwa na makubaliano ya kuachiana kata na nafasi za Ubunge lakini wenzetu vyama wenza bado wamekuwa na Tamaa ya kusimamisha wagombea kila inapotokea nafasi wemekuwa mbele kusimamisha wagombea bila kujali makubaliano hali inayopelekea sisi kama chama kuamua kusimamisha mgombea wetu eneo hilo.

Alisema kuwa sisi kama CUF tumewaachia wenzetu wa chadema kata zote za jiji la Arusha ambapo walishinda kata 24 na moja kuangukia mikononi mwa chama cha Mapinduzi (CCM), ili hali wao wameshindwa kutuachia kata hiyo moja kama wenza na kutusaidia kuweza kuwa na mwakilishi kwenye vikao vya kutnga sera je huku ni kujenga umoja au kubomoa.

“Tulikuwa na makubaliano ya kuachiana kata na nafasi za ubunge jambo hili limeonekana kushindikana kwa wenzetu kuwa na tamaa huku tukiwadanganya wananchi kwa wimbo wa ukawa ukawa kumbe si hivyo wenzetu wapo kimaslahi zaidi na uroho wa madaraka”alisema Mwinyi.

Akatanabaisha kuwa CUF lazima itachukuwa kata hiyo na kazi ndio imeanza ya kuhakikisha kata inaingia mikononi mwetu tukiwa na lengo la kukijenga chama kuhakikisha mwaka 2020 tunakuwa na viti zaidi vya udiwani na ubunge katika jiji la Arusha na mkoa kwa ujumla.

Suala la mgawanyo wa maeneo ya kugombea limekuwa likivichanganya vyama hivi licha ya kuwepo makubaliano yaliofanywa na vingozi wa vyama vine hali inayoonekana kutokuwa na muafaka katika jambo hili, mfano majimbo ya segerea chadema na cuf walisimamisha wagombea na kujikuta wakiangukia pua katika jimbo hilo,hali inayoonyesha hakuna makubaliano katika hilo.

“tumekuwa tukiongea kweye vikao bila hatua kuchukuliwa na wenzetu wamekuwa waongeaji wazuri kwenye vikao bila utekelezaji hali inayotuwiwa vigumu kukijenga chama na kuwa na viti vya wabunge na madiwani katika mkoa huu kutoka na hila za wenzetu”alisisitiza Mwinyi
Juhudi za wanahabari kuwatafuta viongozi wa CHADEMA mkoani hapa akiwemo Mwenyekiti wa chama na Katibu wa Kanda ya kaskazini wa chama hicho Amani Golugwa ziligonga mwamba baada ya simu zao kutokupokelewa kila walipopigiwa bado juhudi zinaendelea kuwatafuta ili waweze kujibu madai hayo.

RAIS DKT MAGUFULI NA MKEWE MAMA JANETH MAGUFULI WAMTEMBELEA ASKOFU MKUU POLYCARP KARDINALI PENGO

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiongea na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki Dar es salaam Muadhama Polycarp Kardinali Pengo walipomtembelea kumpa pole kufuatia kifo cha dada yake nyumbani kwake Kurasini jijini Dar es salaam leo Desemba 23, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiongea na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki Dar es salaam Muadhama Polycarp Kardinali Pengo walipomtembelea kumpa pole kwa kufiwa na dada yake nyumbani  kwake Kurasini jijini Dar es salaam leo Desemba 23, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa kwenye picha ya pamoja na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki Dar es salaam Muadhama Polycarp Kardinali Pengo walipomtembelea kumpa pole kwa kufiwa na dada yake nyumbani  kwake Kurasini jijini Dar es salaam leo Desemba 23, 2016

PICHA NA IKULU

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AHIMIZA ELIMU KWA WATOTO WA KIKE KASKAZINI UNGUJA

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi katika ufunguzi wa Madrasa ya Al-Madrasatul Munawwaratul Islamiyyah ya KilimaninTazari Zanzibar ikiwa sehemu ya ziara yake ya mkoa wa Kaskazini Unguja.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa Sheihiya ya Kilimani waliojitokeza kwa wingi kwenye ufunguzi wa Madrasa ya Al-Madrasatul Munawwaratul Islamiyyah ya KilimaninTazari Zanzibar ikiwa sehemu ya ziara yake ya mkoa wa Kaskazini Unguja.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki dua maalum mara baada ya zoezi la ufunguzi wa Madrasa ya Al-Madrasatul Munawwaratul Islamiyyah ya KilimaninTazari Zanzibar kukamilika ikiwa sehemu ya ziara yake ya mkoa wa Kaskazini Unguja.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia ramani ya msikiti mkubwa unaojengwa kwa nguvu za wananchi alipotembelea Uwanja wa Jitimai uliopo Kidoti mkoa wa Kaskazini Unguja.

...............................................................................


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wazazi na walezi wa Tanzania Zanzibar waache tabia ya kuwaoza wasichana wa kike wakiwa na umri mdogo bali wawasomeshe kwa ajili ya manufaa yao ya jamii kwa ujumla.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti wakati akizindua madrasa ya kisasa iliyojengwa kwenye eneo la Kilimani na kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa na ujenzi wa msikiti mkubwa kuliko yote nchini Tanzania unaojengwa katika eneo la Jitimai kidoti katika Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa michango ya wananchi katika siku yake ya kwanza ya ziara ya Kikazi Kisiwani Unguja.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kama wazazi na walezi watasomesha watoto wa kike elimu watakayopata itasaidia kwa kiasi kikubwa wasichana hao kufanya maamuzi sahihi na yenye tija katika jamii.

Amesisitiza kuwa pamoja na elimu kuwa ni haki ya msingi kwa mtoto wa kike hivyo ni muhimu kwa jamii nzima ya Zanzibar ihakikishe watoto wa kike wote wanapata elimu kwani watakuwa na uwezo wa kuchagua na kuandaa mustakbali wa maisha yao ya baadaye ikilinganishwa na hali ilivyo sasa kwenye baadhi ya maeneo.

Kuhusu elimu ya dini, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewahimiza wazazi na walezi kuwalea watoto katika maadili mema kwa kuzingatia maandiko matakatifu ya Mtume Mohammad (S.A.W).

Amesema vijana wengi wanaolelewa kwa kufuata misingi ya bora ya dini ni vigumu kurubuniwa na kujiingiza katika matendo yasiyofaa katika jamii.


BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

TUME YA MIPANGO YATEMBELEA KIWANDA CHA VINYWAJI CHA AZAM

$
0
0
 Meneja anayesimamia Ubora wa Bidhaa, Lilian Mwashigadi (aliyevaa koti jeupe) akiwaonesha maofisa wa ukaguzi wa miradi kutoka Tume ya Mipango hatua za mwisho za uzalishaji wa juisi katika kiwanda cha uzalishaji wa vinywaji kilichopo eneo la Mwandege Mkoani Pwani.
 Meneja anayesimamia Ubora wa Bidhaa, Bibi Lilian Mwashigadi (mwenye koti jeupe) akionesha mtambo unaotumika katika uzalishaji katika kiwanda hicho.
 Wataalam kutoka Tume ya Mipango wakimsikiliza Meneja anayesimamia Ubora wa Bidhaa, Bibi Lilian Mwashigadi wakati wa ziara ya Tume ya Mipango katika kiwanda cha uzalishaji wa vinywaji kilichopo eneo la Mwandege Mkoani Pwani.
 Meneja anayesimamia Ubora wa Bidhaa, Bibi Lilian Mwashigadi pamoja na wataalamu kutoka Tume ya Mipango wakiwa wameshika vichupa vidogo vinavyotanuliwa kwenye mitambo na kuwa chupa kubwa za kufungashia kunywaji aina ya Energy.
 Bidhaa ya vinywaji aina ya Energy katika hatua za mwishoni za uzalishaji.
 Bidhaa zikiwa zinapangwa baada ya kupitia hatua mbalimbalikatika katika kiwanda cha uzalishaji wa vinywaji kilichopo eneo la Mwandege Mkoani Pwani.
Baadhi ya mitambo ya  kiwanda cha uzalishaji wa vinywaji kilichopo eneo la Mwandege Mkoani Pwani. PICHA ZOTE NA ADILI MHINA, TUME YA MIPANGO

Na Adili Mhina, Pwani.
Tume ya Mipango imetembelea kiwanda cha vinywaji cha Azam kilichoko eneo la Mwandege Mkoani Pwani na kuonesha kuridhishwa na shughuli za uzalishaji za kiwanda hicho ikiwa ni moja ya mikakati ya kutekeleza malengo ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016/17-2020/21) wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.

Timu ya wataalamu wa Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Tume ya Mipango ilifanya mazungumzo na Meneja anayesimamia ubora wa bidhaa kiwandani hapo, Bibi Lilian Mwashigadi na kuelezwa kuwa kiwanda hicho kipo katika hali nzuri na kinaendelea na shughuli za kuzalisha bidhaa zenye ubora unaotakiwa katika kukidhi mahitaji ya soko. 

Bibi Mwashigadi alieleza kuwa kiwanda hicho ambacho kina jumla ya wafanyakazi 800 ambapo kati hao 500 ni ajira za moja kwa moja (direct labor) na 300 ni ajira zisizo za moja kwa moja (indirect labor) kina mikakati ya kuendelea kupanua soko la bidhaa zake kimataifa ambapo kwa sasa kinauza bidhaa katika nchi za Kenya na Rwanda. 

Kuhusu upatikanaji wa matunda ya kutosheleza kiwanda hicho, Meneja huyo alieleza kuwa hakuna changamoto kwani hapa nchini kuna matunda yenye ubora unaokidhi mahitaji ya viwanda na kiwanda chake kinategemea malighafi hiyo kutoka kwa wakulima wadogo wadogo kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Pamoja na hayo, Bibi Mwashigadi aliongeza kuwa kiwanda chake kimeendelea kununua matunda kwa bei nzuri ambayo inaendana na bei ya kawaida ya soko lengo likiwa ni kuhakikisha mkulima anaona faida ya kujishughulisha na kilimo cha matunda. 

Hata hivyo alitoa wito kwa Tume ya Mipango kuangalia namna ya kutengeneza sera itakayosaida kumnufaisha zaidi mkulima mdogo kwani kwa sasa madalali ndio wanaochukua matunda toka kwa wakulima na kupeleka kiwandani na mkulima anaishia kupata faida kidogo huku madalali wakiendelea kunufaika.

MWENYEKITI MPYA WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI JAJI SEMISTOCLES KAIJAGE AANZA KAZI RASMI.

$
0
0

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhan (kushoto) akimkaribisha Mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Semistocles Kaijage (kulia) kwenye Ofisi za Tume zilizoko Posta jijini Dar es salaam. Mhe. Jaji Semistocles Kaijage ameapishwa leo Ikulu jijini Dar es salaam kuiongoza Tume hiyo kwa kipindi cha miaka 5.

Watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakimpokea Mwenyekiti mpya wa Tume hiyo mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi Posta, jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Semistocles Kaijage (kulia) akiwa Ofisini kwake kwa mara ya kwanza mara baada ya kuapishwa leo. Mhe. Jaji Semistocles Kaijage ameteuliwa kuongoza Tume hiyo kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia tarehe 20 Desemba, 2016.


Mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Semistocles Kaijage (kushoto) akizungumza na Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ofisini kwake.
Mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Semistocles Kaijage akitoa ufafanuzi kwa vyombo vya Habari kuhusu majina 11 yaliyoteuliwa kugombea Ubunge katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Dimani Zanzibar na majina 72 ya wagombea Udiwani kwenye Kata 20 za Tanzania Bara. Picha/Aron Msigwa -NEC




RC SHINYANGA AFANYA ZIARA WILAYANI KISHAPU, AAGIZA MIRADI IKAMILIKE KWA WAKATI ULIOPANGWA

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kushoto) akikagua mojawapo ya nyumba za walimu zinazojengwa katika Shule ya Sekondari Mwamashele wilayani humo.
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kushoto) akisisitiza jambo wakati akizungumza na watendaji na Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya alipotembelea Kata ya Kiloleli. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya  Kishapu, Nyabaganga Taraba.
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (mbele) akitembelea mifugo ya mmoja wa wafugaji wilayani humo wakati wa ziara yake.
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Joseph Swalala alipowasili Kata ya Kiloleli.
 Mhandisi wa Ujenzi Wilaya ya Kishapu, Samson Pamphil (kushoto) akitoa maelezo kuhusu mradi wa ujenzi wa vyoo katika Kata ya Mwamamalasa kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack. Katikati ni Diwani wa kata hiyo, Justine Sheka.
 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (katikati) akizungumza na watendaji alipofika Kata ya Mwamalasa wakati wa ziara yake. Wengine pichani wa pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya  Kishapu, Nyabaganga Taraba, Diwani wa kata hiyo, Justine Sheka na  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Joseph Swalala.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Zainab Telack amefanya ziara katika Wilaya ya Kishapu na kukagua miradi ya maendeleo.
Katika ziara hiyo Telack alikagua ujenzi wa mradi wa nyumba za walimu kata ya  Kiloleli na vyoo kata za Mwamalasa, Masanga na Mwakipoya inayoendelea.
Aliagiza miradi hiyo iwe imekamilika kabla ya Desemba 31 mwaka huu huku akionya tabia ya wakandarasi kuchelewesha miradi ya maendeleo wakati tayari wamekwisha lipwa fedha.
“Nataka kuona miradi hii imekamilika na tunajua agizo hili lilishatolewa na Waziri wa TAMISEMI siku nyingi, wahandisi hamieni site kuhakikisha miradi inakamilika,” alisema Telack.
Aidha, mkuu huyo wa mkoa katika ziara hiyo ya siku moja akiwa ameambatana na wataalamu kutoka halmashauri ya wilaya na Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya aliwataka waendelee kusimamia miradi ya maendeleo.
Kwa upande mwingine alikemea utoro mashuleni huku akiagiza wazazi wasiopeleka watoto shule ifikapao Januari wakamatwe na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Alisema kuwa kwa sasa Serikali inaendelea na utaratibu wa kutoa elimu bure hivyo ni lazima wazazi wapeleke watoto shule kupata elimu na baadaye kulisaidia taifa.
“Nakuagiza mkuu wa shule hakikisha wanafunzi wote wanafika shule, hosteli ipo sasa kwanini wanafunzi hawafiki shule kwa hiyo nakupa kazi hiyo,” alisisitiza.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA BALOZI WA UTURUKI NCHINI MHE YASEMIN ERALP

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa Uturuki nchini Mhe. Yassemin Eralp  walipokutana kwa mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 23, 20176
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika picha ya kumbukumbu na  Balozi wa Uturuki nchini Mhe. Yasemin  Eralp walipokutana kwa mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 23, 20176.Wengine kutoka kushoto ni Balozi zuhura Bundala, Balozi Joseph Sokoine na Bw. Hassan Mwamweta wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa.PICHA NA IKULU

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI DEC 24

Viewing all 46313 articles
Browse latest View live




Latest Images