Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live

Airtel, VETA kuwafikia vijana wa Vijiji vinavyonufaiaka na Mradi wa Umeme vijijini (REA), kupitia mtandao wa simu VSOMO

0
0
 Diwani wa Bungu, Mhe. Ramadhan Mpendu (kushoto)  akihamasisha wakazi wa Bungu kujiunga na VSOMO inayowezesha kutoa mafunzo ya ufunzi stadi kutoka VETA kwa njia ya simu za mikononi kwa kushirikiana na Airtel katika semina iliyofanyika katika ofisi ya kata ya Bungu katika wilaya ya Rufiji.
 Mhandisi wa Shirika la umeme Tanzania TANESCO, Christopher Mbwiga (kushoto) akiwaelekeza wanakijiji wa kata ya Bungu juu ya mradi wa kusambaza umeme vijijini na kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi na kusoma kozi ya umeme kutoka VETA kupitia application ya simu za mkononi VSOMO itayosaidia kupata mafunzo yatayopelekea kupata ajira kwenye mradi huo katika semina iliyofanyika ofisi ya kata ya Bungu wilayani Rufiji mkoani Pwani.
 Afisa Mwendelezaji biashara SIDO, Stephen Bondo (kulia) akielekeza juu ya fursa za kibiashara  kwa wanakijiji wa kata ya Bungu wilayani Rufiji zitokanazo na mradi wa kusambaza umeme vijijini REA na kuhamasisha wananchi kusoma kozi mbalimbali kutoka VETA kupitia application ya VSOMO itayosaidia kupata ajira na kujiajiri, katika semina iliyofanyika ofisi ya kata ya Bungu wilayani Rufiji.
 Mkuu wa Chuo cha VETA Kipawa, Mhandisi Lucius R. Luteganya (wapili kushoto) akielezea utaratibu wa mafunzo ya ufundistadi kwa vutendo kupitia mradi wa Airtel na VETA wa unaotoa mafunzo ya ufunzi stadi kwa njia ya simu za mikononi, ujulikanao kama  VSOMO kwa wanakijiji wa kata ya Bungu katika semina iliyofanyika katika ofisi ya kata hiyo katika wilaya ya Rufiji, mkoani Pwani.
 Mratibu wa kozi fupi na ujasiriamali VETA kipawa, Gosbert Kakiziba (kulia) akijibu nswali kutoka kwa wanakijiji juu ya kozi zipatikanazo kwenye application ya VSOMO inayowezesha kutoa mafunzo ya ufunzi stadi kutoka VETA kwa njia ya simu za mikononi kwa kushirikiana na Airtel katika semina iliyofanyika katika kata ya Bungu wilayani Rufiji.
Albert Sahoya, Balozi wa Airtel kupitia mradi wa mafunzo ya stadi za ufundi kupitia mtandao wa simu ya mkononi yajulikanayo kama “VSOMO” yaani VETA SOMO, akitoa elimu ya jinsi ya kupakua application na kujiunga na mafunzo hayo kwa wanakijiji wa kata ya Bungu wilayani Rufiji.

Mamlaka ya ufundi stadi Nchini VETA kupitia chuo chake cha VETA Kipawa kimeanza kutoa mafunzo ya ufundi wa Umeme, ufundi wa simu za Mkononi, ufundi wa kuchomelea vyuma (welding) n.k katika vijiji vitakavyo nufaika na mradi wa Umeme Vijijini (REA) kwa kutumia njia ya mafunzo kwa njia ya simu ya Mkononi (VSOMO), mfumo uliobuniwa kwa pamoja kati ya Airtel na VETA na kuzinduliwa June 7, 2016.

Hayo yamesemwa katika uzinduzi wa program ya VSOMO uliobeba kauli mbiu (FURSA INAKUFUATA ULIPO) uliofanyika viwanja vya ofisi ya kijijini za kata ya Bungu Wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani na Mkuu wa Chuo cha VETA Kipawa Eng. Lucius Luteganya kwamba “mfumo huu wa mafunzo (VSOMO), wanafunzi watajifunza nadharia kwa njia ya simu ya mkononi (smartphone) kwa kupakua bure mfumo huu wa VSOMO kutoka kwenye google play store ambapo msomaji atafanya mitihani ya kupima ufahamu wa somo kwa kutumia simu hiyo ya mkononi na hatimae mafunzo kwa vitendo kwa walio faulu nadharia, mafundi wa chuo cha VETA watawafuata wakiwa na karakana inayotembea (Mobile workshop) ili kutoa mafunzo ya vitendo kwa wale waliofaulu nadharia tu.

Eng, Luteganya aliongeza kuwa “Katika makubaliano yaliyofikiwa na wadau wengine, EWURA watatoa leseni kwa mafundi wa umeme watakaohitimu katika kozi ya UMEME, SIDO watatoa mafunzo ya ujasiliamali yanayoambatana na fursa za umeme kwa wanavijiji husika, na mwisho orodha ya wahitimu itapelekwa REA, TANESCO na kwenye Board ya wakandarasi ili mashirika na makampuni yatakayopewa kandarasi yaweze kuwatumia katika kujenga miundo mbinu (Wakandarasi), kutunza miundo mbinu (Tanesco) na REA”.

Katika uzinduzi wa Program hii (FURSA INAKUFUATA ULIPO) kwa wakazi wa vijiji vya Kata ya Bungu wilaya Rufiji Mkoani Pwani wadau wote VETA wakiwakilishwa na Mkuu wa Chuo cha VETA Kipawa Eng. Lucius Luteganya na timu yake, Airtel wakiwakilishwa na Bi. Hawa Bayumi Manager wa Airtel Fursa, SIDO wakiwakilishwa na Mr. Stephen Bondo, EWURA wakiwakilishwa na Chief Inspector Eng. Simon , Tanesco wakiwakilishwa na Eng. Mbwiga Chimala walipata mapokezi makubwa kutoka kwa wananchi na viongozi wa kata ya Bungu.

Nao baadhi ya Wananchi wameeleza kufurahishwa na mpango huo na kwamba mara nyingi wamekuwa wakishindwa kupata mafunzo kutokana na vyuo vya ufundi kuwa mbali lakini kwa sasa wanaona fursa hii imewafuata hivyo ni jambo muhimu katika maisha yao."Kusema ukweli haya mambo kwetu ni muhimu sana na mara nyingi tumekuwa tukishindwa kupata mafunzo kama haya kutokana na upatikanaji wake kuwa mgumu maana vyuo hadi usafiri kwenda Dar es salaam jambo ambalo ni gumu kwetu," Khamis Shaban-Mkazi wa Bungu

Nae Ramadhani Mpendu Diwani wa Kata ya Bungu ameeleza kufurahishwa na mpango huo huku akiwasisitiza viongozi wenzake kutoa elimu kwa wananchi ili wachangamkie fursa.hiyo muhimu na kuondoa malalamiko ya kuporwa ajira. Mfumo huu wa mafunzo utaendelea katika vijiji vingine vitakavyonufaika na mradi huu.

MBUNGE RITTA KABATI KUKARABATI SHULE YA MSINGI AZIMIO

0
0
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya iringa Abeid Kiponza,mbunge wa viti maalumu mkoani iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela wakiwa katika moja ya madarasa ya shule ya msingi Azimio wakati wa kujadili jinsi gani ya kutatua changamoto za shule hiyo
Mbunge wa viti maalumu mkoani iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akikagua miundombinu ya shule ya msingi Azimio sambamba na wananchi na viongozi wa shule hiyo.
Hili ni moja kati ya madarasa ya shule ya msingi Azimio ambalo lipo taabani kabisa na likiwa linakaribia kuanguka kutokana na kuwa na nyufa nyingi ambazo ni kubwa sana


Hili ni moja kati ya madarasa ya shule ya msingi Azimio ambao linaonekana afadhari kidogo na kuwashawishi viongozi mbalimbali kuketi na kujadili maswala ya kutatua changamoto za shule hiyo ambapo madarasa mengine yapo taabani kuliko hili.

Na fredy mgunda,Iringa


Mbunge wa viti maalum mkoani Iringa Ritta Kabati anatarajia kukarabati shule ya msingi ya Azimio iliyopo manispaa ya Iringa kutokana na uchakavu wa majengo hayo.

kizungumza wakati wa ukaguzi wa miundombinu ya shule hiyo mbunge Kabati alisema ni aibu kwa shule kongwe kama hiyo kuwa miundombinu mibovu kama hiii.Kabati aliongeza kuwa shule hiyo imeharika hovyo na inahitaji msaada wa haraka kuikarabati kwa kuwa wananfunzi wanasoma katika mazingira magumu na kudumisha elimu ya wanafunzi hao.

“Hii shule imeanza sawa na siku niliyozaliwa mimi lakini ukiiangalia imechakaa na imechoka hivyo sina budi kuanza kuikarabati shule hii kwa kuwa ni aibu kwangu haiwezakani shule ikawa manispaa ya iringa halafu ikawa katika muundo huuu”alisema kabati

Aidha Kabati alisema kuwa hadi kufikia siku ya ijumaa ya tarehe 23 mwezi wa kumi na mbili atahakikisha anakarabati shule yote ili iwe katika ubora unaotakiwa kama shule nyingine zilizopo manispaa ya iringa.

“Tunashule bora sana hapa manispaa ya iringa lakini hii ya Azimio imekuwa katika hali mbaya sana ni jukumu langu kama mbunge wa mkoa wa iringa kutatua changamoto mbalimbali zinazoukabili mkoa wangu”alisema Kabati

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alisema haiwezekani shule ya azimio ikawa katika mazingira mabovu ya miundombinu kama yale hiyo hadi kufikia siku ya ijumaa atahakikisha anakarabati shule hiyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

Naye mkuu wa shule ya msingi Willfrid Chotipembe alimshukuru mbunge wa viti maalum Ritta Kabati pamoja na mkuu wa wilaya kwa kufika shuleni hapo na kuahidi kutatua changamoto zinazoikabili shule hiyo.

SUMATRA Yaunda Kikosi Kazi Kudhibiti Upandishaji Holela wa Nauli Kipindi cha Sikukuu za Mwisho wa Mwaka.

0
0
 Na Lilian Lundo,MAELEZO-Dar es Salaam

MAMLAKA ya Usimamizi wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) imeunda kikosi kazi maalum kwa ajili ya kudhibiti upandashaji holela wa  nauli kwa mabasi yaendayo mikoani wakati wa kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka.

Hayo yamesemwa leo na Meneja Mawasiliano wa Mamlaka hiyo David Mziray wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari  hii, akieleza namna mamlaka hiyo inavyodhibiti upandaji wa nauli za mabasi yaendayo mikoani.

“Kuna timu ambazo ziko katika vituo vyote vya mabasi makubwa katika kila mkoa, timu hizo zinathibiti masuala ya nauli, usalama wa magari , kuhakikisha leseni za mabasi pamoja na muda uliopangiwa kuondoka vituoni,” alifafanua Mziray.

Aliongeza kuwa mamlaka hiyo imeruhusu mabasi yanayobeba abiria 40 na kuendelea kuomba leseni za muda  za kusafirisha abiria katika mikoa ambayo ina wasafiri wengi zaidi katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka.

Kwa mujibu wa Mziray alisema mabasi hayo yatakuwa yakikaguliwa kwanza ndipo yanapewa leseni za muda pamoja na kupangiwa nauli ambazo watatozwa abiria kutokana na mkoa ambao gari hilo litakwenda.

Akizungumzia kikosi kazi hicho, Mziray alisema kuwa mwanzoni mwa wiki hii timu iliyoko kituo cha mabasi cha Ubungo ilikamata mabasi manne ambayo yalipandisha nauli kwa abiria na kuchukuliwa hatua za kisheria.
MWISHO

Arusha wafurahia kompyuta za Bayport

0
0

Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Kampuni ya mikopo ya Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa (kushoto), akimkabidhi Ofisa Utumishi wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, Emelda Kisosi, kompyuta kwa ajili ya kusaidia ufanisi wa kazi ofisi zao kama sehemu ya kujitolea kwa jamii. Kulia ni Ofisa TEHAMA wa Halmashauri ya Wilaya Arumeru, Edna Mwaipiana. 


Na Mwandishi Wetu, Arusha

HALMASHAURI ya Wilaya Arumeru, mkoani Arusha, jana imepokea kompyuta mbili zilizotolewa msaada na Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, kama sehemu ya ushirikiano na kusaidia na kukuza ufanisi wa kikazi kwa watumishi wa umma wilayani humo.

Kompyuta hizo zinatoka ikiwa ni siku chache baada ya Mkoa wa Morogoro nao kupokea msaada kama huo kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa watumishi wa umma.

Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo, Mercy Mgongolwa katikati akizungumza jambo katika makabidhiano hayo yaliyofanyika leo jijini Arusha. Kulia ni Ofisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya Arumeru, Emelda Kisosi.

Akizungumza katika makabidhiano hayo leo jijini Arusha, Mratibu wa Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Mercy Mgongolwa, alisema wamefikisha kompyuta mbili katika wilaya hiyo kama orodha ya mahitaji waliyopokea kutoka Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Alisema anaamini kwa kufikisha kompyuta hizo, kutachangia ufanisi wa kikazi kwa kutumia vyema teknolojia ya kompyuta iliyokuja kupanua wigo wa utendaji bora wa kazi kwa Tanzania nzima kwa hali ya kupanga, kutatibu na kuhifadhi kumbukumbu muhimu za kiutendaji wakati wote.

Picha ya pamoja baada ya makabidhiano ya kompyuta hizo.
Mercy Mgongolwa akikabidhi nyaraka za kompyuta hizo.

“Huu ni mwendelezo mzuri wa ugawaji wa kompyuta 205 tulizonunua zenye thamani ya Sh Milioni 500, ambapo tayari kompyuta 125 zimefikishwa Makao Makuu ya Utumishi na wao kutuelekeza eneo na idadi ya ugawaji kwenye halmashauri za nchi yetu,” alisema.

Naye Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya Arumeru, Imelda Kisosi, aliwashukuru Bayport kwa kujitolea vifaa hivyo muhimu vitakavyowapatia urahisi watendaji hao kuchapa kazi kwa nguvu zote ili wilaya yao isonge mbele.

“Msaada huu ni mkubwa mno kwetu hivyo tunawashukuru na kuwaahidi ushirikiano wa hali ya juu sanjari na kuwataka Bayport waendelee kuwa karibu na jamii yetu kama njia ya kuwapatia maendeleo Watanzania wote, hususan wa wilayani kwao Arumeru, mkoani Arusha,” alisema Kisosi.

Bayport Financial Services ni taasisi ya mikopo inayojitolea kwa hali na mali  ambapo mbali na kununua kompyuta hizo 205, pia imekuwa ikishiriki kujenga madarasa katika shule mbalimbali, hali inayochangia kwa kiasi kikubwa kupanua kiwango cha elimu nchini.

Huduma znazotolewa na Bayport ni pamoja na mikopo ya fedha taslimu kwa watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni binafsi, mikopo ya viwanja, mikopo ya fedha kwa njia ya simu za mikononi maarufu kama ‘Nipe Boost’, Bima ya Elimu kwa Uwapendao na nyinginezo zinazopatikana katika ofisi zao za matawi 82 katika mikoa na wilaya mbalimbali za Tanzania Bara.

MULTICHOICE TANZANIA YAWAKUMBUKA YATIMA WA KITUO CHA AL-MADINA JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
 
 Na Amina Kibwana-Globu ya Jamii.
 
Kampuni ya Multichoice Tanzania imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vevye thamani ya shilingi milioni 5 kwenye kituo cha watoto yatima cha Al Madina kilichopo Tandale kwa tumbo, kwa ajili ya mahitaji ya sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Maharage Chande amesema kuwa wanaushirikiano wa muda mrefu na kituo hicho, ndio maana wameamua kuja kuleta zawadi mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia katika sikukuu pamoja na kuwalipia kodi ya nyumba wanayoishi.

“Leo tunatoa vyombo vipya vya kulia chakula,nguo, vyakula pamoja na sare za wanafunzi 50 kwa ajili ya watoto ambao ni wanafunzi”

Kwa upande wake mlezi wa watoto katika kituo hicho Kurutumu Yusuph ameeleza baadhi ya changamoto zinazowakabili katika kituo hicho ni pamoja ulipaji kodi ya nyumba, sare za shule pamoja na ada.

Hata hivyo Kurutumu alitoa shukrani zake kwa Multichoice Tanzania kwa kushirikiana nao kwa kipondi kirefu na kuwapatia msaada pale wanapohitaji ili kukidhi changamoto zinazowakabili..

"Ni kweli dstv wanatusaidia kwa mambo mengi hivyo tunawashukuru sana na tunamuomba M/mungu awape moyo wa kuendelea kutusaidia" amesema kuruthumu.

Kituo cha watoto yatima cha Al Madina kina jumla ya watoto 61, wasichana 25 na wavulana 36 kimeanza kupata msaada kutoka katika Kampuni ya Multichoice Tanzania tangu mwaka 2009 hadi sasa ambapo mnamo mwezi wa sita mwaka huu kituo kilipelekewa cherehani 5 kwa ajili ya kujipatia kipato.


Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande (kulia), akizungumza kabla ya kukabidhi msaada huo. Kushoto ni mama mlezi wa kituo hicho, Kuluthum Yusuf.

Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande (kushoto), akimkabidhi sare za shule mama mlezi wa kituo hicho, Kuluthum Yusuf.
Bwana Chande akimkabidhi mlezi wa kituo hicho mafuta ya kula. Wengine ni wafanyakazi wa Multichoice Tanzania na watatu kushoto ni Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Alpha Joseph.

Mlezi wa kituo hicho, Kuluthum Yusuf (kushoto), akimuonesha nguo zinazotengenezwa na kituo hicho kupitia mradi wao wa ushonaji ambao kwa kiasi kikubwa umetokana na msaada kutoka katika kampuni hiyo ya Multichoice Tanzania.Picha na Dotto Mwaibale.

ULEGA ASHRIKI UJENZI WA ZAHANATI YA KIJIJI CHA KIBAMBA WILAYANI MKURANGA

0
0
 Wakazi wa kijiji cha Kibamba kilichopo Kata ya Mipeko wamempongeza Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega Kwa kushiriki katika ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho ikiwa ni sehemu ya ahadi Yake.

Pia amesema mapema mwezi uliopita Mbunge huyo alitembelea kijiji chao nakukuta changamoto kubwa ya huduma ya Afya hivyo alitoa ahadi Kwao kwamba atahakikisha Zahanati inajengwa kijijini hapo.

Akizungumza kijijini hapo jana kwa niaba ya wananchi wezake mkazi Sharrifa Mkumbo alisema kuwa Ulega anaonesha kwamba yeye ni Kiongozi wa watu kwani anastahili kupongezwa.

"Tunashukuru sana kwakweli Baba huyu Mungu aendelee kumlinda kwani tunaamini siku chache zijazo tunakwenda kupata suluhisho la Afya katika kijiji chetu."alisema Sharrifa.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji hicho Salum Mlango aliwaeleza wananchi kuwa Mbunge wanayo na zaidi ni kuendelea kutoa ushirikiano kwake nakudai kuwa alihaidi kushiriki msingi wa ujenzi wa Zahanati hiyo na leo ametimiza.

"Ndugu waandishi kama mnavyoona wenyewe wananchi wamehamasika na leo Mbunge amekuja mwenyewe kushiriki nasi."alisema .
 
 Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Kibamba katika Ujenzi wa Zahanati katika Kijiji hicho Wilayani Mkuranga
 Mbunge wa Mkuranga Bw Abdallah Hamisi Ulega Akishiriki katika Ujenzi huo wa Zahanati katika Kijiji cha Kibamba Wilayani Mkuranga.
 Akiongea na Mmoja Wa Wanakijiji cha Kibamba kuhusiana na Ujenz huo wa Zahanati kijijini hapo
  Mbunge wa Mkuranga Bw Abdallah Hamisi Ulega Akishiriki kubeba matofali kwa ajili ya Ujenzi huo wa Zahanati katika Kijiji cha Kibamba Wilayani Mkuranga.
 Akiongea na Mmoja Wa Wanakijiji cha Kibamba kuhusiana na Ujenz huo wa Zahanati kijijini hapo

UTEKELEZAJI WA BARABARA ZA TANROADS MKOA WA KAGERA

0
0
TANROADS Mkoa wa Kagera inasimamiwa na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Kagera Eng. Andrew. L. Kasamwa. Mkoa wa Kagera una barabara zenye urefu wa km 1917.59 kati ya km 7505.42 zilizo mkoa wa Kagera. Kati ya hizo km 862.88 ni Barabara Kuu na km 1052.71 ni Barabara za mkoa.

Afisa Habari wa TANROADS Bi. Aisha Malima amemtembelea Meneja wa TANROADS Kagera leo tarehe 22. 12. 2016 kuangalia utekelezaji wa ujenzi wa barabara za TANROADS mkoani Kagera. Moja ya mradi waliotembelea ni Kyaka – Bugene – Kasulo Lot1: sehemu ya Kyaka – Bugene yenye km 59.1 inayojengwa kwa kiwango cha lami. 

 Aidha barabara hii itakuwa na daraja moja, box makalavati 11 na makalavati ya pipe 132 na inafadhiliwa kwa asilimia mia moja na Serikali ya Tanzania. Mhandisi Mshauri akiwa TECU na kazi ya ukandarasi utekelezwa na Kampuni ya CHICO.

Katika taarifa fupi ya Meneja wa TANROADS Kagera amesema “Hadi sasa barabara hii imekamilika kwa asilimia 97.2 ambayo ni km 57 na sasa bado kama km 2 tu ili mradi ukamilike na tunatarajia kukamilika Februari 2017”.

Aidha meneja aliongeza kwa kusema “Hali ya barabara ziliyo chini ya TANROADS mkoa wa Kagera zipo katika hali nzuri na wastani na barabara moja tu ya Rusumo – Lusahunga ambayo imeisha muda wake wa matumizi ndiyo iko katika hali mbaya. Hata hivyo katika mwaka huu wa fedha 2016/17 tumetengewa fedha kiasi cha shilling billion 5 ili kuifanyia matengenezo kwa sehemu zilizo katika hali mbaya zaidi ili iendelee kupitika kwa usalaama huku tukisubiri ukarabati mkubwa”.

Katika ziara hii Bi. Aisha Malima aliomba wananchi wa mkoa wa Kagera wakiwemo madereva walinde miundombinu ya barabara na samani za barabarani kwani zinajengwa kwa fedha nyingi za kodi zetu. Aliongeza kwa kusema “Kumekuwa na uharibifu wa barabara ambapo madereva kumwaga mafuta barabarani, kupiga jeki katika barabara za lami, kugonga nguzo za madaraja , kuiba alama za barabarani na makalavati ya chuma n.k.”
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Kagera Eng. Andrew Kasamwa (katikati) akipewa taarifa mradi wa Kyaka – Bugene (km 59.1) kutoka kwa Kaimu Mhandisi Mshauri – Eng. Hatibu Kapombe (TECU). Pamoja katika mkutano ni Bi. Aisha Malima – Afisa Habari TANROADS na Wakandarasi CHICO.
Bi. Aisha Malima Afisa Habari wa TANROADS akisalimiana na Mhandisi Mshauri wa Mradi wa Kyaka – Bugene (km 59.10) Eng. Hatibu Kapombe.
Kazi ya ujenzi wa barabara zikiendelea katika mradi wa Kyaka – Bugene eneo la Kishoju escarpment.
Meneja wa TANROADS Kagera Eng. Andrew Kasamwa (kushoto) akikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Kyaka – Bugene eneo la Kishoju Escarpment.
Daraja la Mwisa lililokamilika katika barabara ya Kyaka – Bugene.

MRADI WA GREEN VOICES WAFANIKISHA UTENGENEZAJI WA JIKO LA UMEME-JUA MOSHI

0
0

Mgeni rasmi katika uzinduzi wa jiko la umeme-jua, Robert George, ambaye ni Ofisa Ushirika wa Manispaa ya Moshi, akisikiliza maelezo ya namna jiko hilo linavyofanya kazi kutoka kwa Mkurugenzi wa Uhawilishaji Teknolojia wa Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini – CAMARTEC, Mhandisi Noela Byabachwezi. Kushoto kwa Noela ni mshiriki kiongozi wa mradi wa Green Voices Moshi, Farida Makame. Wengine pichani ni washiriki wa kikundi hicho. Uzinduzi wa jiko hilo lililotengenezwa na CAMARTEC kwa ufadhili wa Green Voices ulifanyika hivi karibuni mjini Moshi.
Jiko la umeme-jua ambalo limetengenezwa na CAMARTEC kwa ufadhili wa mradi wa Green Voices Tanzania kwa ajili ya kikundi cha akinamama wa TAWOCA Moshi. Jiko hilo linafaa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi pamoja na uharibifu wa mazingira.
Wanakikundi wa TAWOCA Green Voices Moshi wakihakikisha jinsi joto la jua linavyosaidia kupika kwa kutumia jiko la umeme-jua. Kushoto ni mgeni rasmi katika uzinduzi wa jiko hilo, Robert George, ambaye ni Ofisa Ushirika wa Manispaa ya Moshi.
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa jiko la umeme-jua, Ofisa Ushirika wa Manispaa ya Moshi, Robert George, pamoja na akinamama wakisikiliza maelezo ya namna jiko hilo linavyofanya kazi kutoka kwa Mkurugenzi wa Uhawilishaji Teknolojia wa Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini – CAMARTEC, Mhandisi Noela Byabachwezi.

Mhandisi Noela Byabachwezi, mwenye kofia kulia, akionyesha kwa vitendo jinsi jiko la umeme-jua linavyofanya kazi.
Ofisa Ushirika wa Manispaa ya Moshi, Robert George – kulia – akisikiliza maelezo mbalimbali ya akinamama wa TAWOCA Green Voices Moshi kabla ya kuzindua jiko la umeme-jua.


Picha ya pamoja.



VIUNGA vya ukumbi wa Aroma mjini Moshi vimesheheni akinamama wengi katika siku hii ya Jumamosi, kama ilivyo kawaida kwa siku kama hiyo, ambapo wote wanaonekana kuwa na nyuso za furaha kutokana na mijadala inayoendelea.

Lakini tofauti na Jumamosi nyingine ambapo akinamama wa kikundi cha Wamama wa Kahawa ambao ni wanachama wa Tanzania Women Coffee Association - TAWOCA mjini humo kujadili masuala mbalimbali ya ujasiriamali, siku hii inaonekana kuwa ya tofauti kwa sababu licha ya idadi ya akinamama kuongezeka, lakini kuna tukio kubwa na muhimu ambalo limewakutanisha.

"Leo tunazindua rasmi jiko la umeme-jua, yaani parabolic solar cooker, ambalo kupitia udhamini wa mradi wa akinamama wa Green Voices, hatimaye limeweza kupatikana baada ya jithada za miezi kadhaa," ndivyo anavyoanza kuelezea Farida Makame, mshiriki kiongozi wa mradi wa Green Voices wa kikundi hicho, huku akionyesha kifaa kinachofanana na dish kama la satellite ambacho katikati yake kumewekwa sufuria inayong’aa kama taa kubwa ya umeme.

Anasema kwamba, jiko hilo linaweza kupika kila aina ya chakula kwa kutumia mionzi ya jua ya moja kwa moja bila kuathiri mazingira.

"Kwa kutumia jiko hili maana yake huhitaji kutafuta mkaa wala kuni, hivyo kuokoa misitu ambayo inateketea kila siku kutokana na ukataji wa miti kwa ajili ya kutafuta nishati ya kupikia," anaongeza.

Farida, ambaye pamoja na akinamama wengine 14 – wakiwemo wanahabari watano wanawake – walipatiwa mafunzo ya takriban miezi miwili jijini Madrid, Hispania mapema mwaka huu wa 2016, anasema kwamba lengo la kubuni na kutengeneza jiko hilo la umeme-jua ni kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi pamoja na kupambana na uharibifu wa mazingira.

Anaeleza kwamba, haikuwa kazi rahisi kwake kukamilisha ubunifu wake, wazo ambalo aliliwasilisha akiwa mafunzoni, na kwamba ndiyo maana mradi wake umechelewa kutokana na kuhitaji teknolojia zaidi.

"Tumeanzisha huu mradi baada ya kukaa na akinamama wa TAWOCA na kuwauliza changamoto mbalimbali zinazowakabili katika maisha yao, moja ya changamoto ni upatikanaji wa kuni na mkaa, gesi na umeme.

"Kwahiyo tukaangalia kama kuna njia mbadala ambayo akinamama wanaweza kuitumia na ikawa nafuu na pia kiafya, kwa sababu njia ya kutumia umeme-jua ina manufaa sana kiafya, kwa hiyo tukaungana na wenzetu wa Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini, CAMARTEC, kwa sababu ndio watafiti wa mashine na zana za kilimo, ili kutengeneza jiko hili linalotumia nishati ya jua," anasema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uhawilishaji Teknolojia wa CAMARTEC, Mhandisi Noela Byabachwezi anasema imekuwa ni fursa kubwa kwao kufanya kazi na mradi wa Green Voices, kwani wameweza kutengeneza kwa mara ya kwanza jiko hilo ambalo limewapa hamasa wahandisi wa kituo hicho kuliboresha zaidi kwani linaonekana kuwa na manufaa makubwa.

Anakiri kwamba, ingawa wanabuni teknolojia mbalimbali ikiwemo kutengeneza majiko na makaushio yanayotumia umeme-jua, lakini hiyo ndiyo mara ya kwanza kwa kituo hicho kutengeneza jiko linalotumia nguvu ya jua moja kwa moja.

"Hivi sasa tunafanya utafiti kama tunaweza kulitengeneza dogo lakini lenye nguvu au kutengeneza jiko linaloweza kukunjwa na kuhifadhiwa kirahisi kwa sababu hili ni kubwa na inakuwa shida ikiwa mtu hana nafasi kubwa ya kuhifadhia," anasema Mhandisi Noela.

Akizungumzia kuhusu ufanisi wake, Noela anasema kwamba, jiko hilo ni rafiki mkubwa wa mazingira na lina uwezo mkubwa wa kupika na hata kuoka vyakula vya aina zote ikiwa tu kutakuwepo na jua la kutosha.

Kwa maeneo kame na yenye jua kali kama mikoa ya Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga na hata Dar es Salaam, jiko hilo linafaa sana kutumiwa bila shida, anaongeza mhandisi huyo.

Aidha, anafafanua kwamba, jiko hilo linaweza kupika chakula kwa ajili ya watu wengi na kwamba ni jukumu la jamii kugeukia matumizi ya jiko hilo lisilotumia mafuta wala nishati nyingine kwa sababu siyo tu linapunguza gharama, lakini pia linaokoa misitu kwa vile miti haitakatwa ikiwa watakuwa wanalitumia.

"Jambo jingine la muhimu ni kwamba, upikaji kwa kutumia jiko la umeme-jua mara nyingi hufanyika nje na katika mazingira ambayo yanahitaji matumizi madogo ya mafuta na kuni, au hatari ya ajali za moto na inaokoa afya za wanajamii, hususan akinamama pamoja na kuyalinda mazingira yetu," anaongeza Mhandisi Noela.

"Kama unavyoliona, jiko hili limetengenezwa kwa vifaa maalum vikiwemo vioo, ambavyo vinang’aa na kuakisi mwanga wa jua, vimepangwa kitaalam na mwanga huu unapoakisiwa unakwenda moja kwa moja kwenye sufuria ambayo kutokana na joto lake, chakula chochote kinachopikwa kinaiva bila wasiwasi wowote. Kama jua litakuwepo la kutosha, joto linalozalishwa na jiko hili linaweza kufikia hadi nyuzijoto 400 °C."

Kwa mujibu wa mhandisi huyo, vyakula vinavyopikwa kwa kutumia jiko la aina hiyo ni vyema vikawa katika maumbile madogo ili kusaidia kuiva haraka na kwamba muda wa chakula kuiva unategemea na vifaa unavyotumia, kiwango cha jua, na kiasi cha chakula kinachopikwa.

Faida kubwa za utumiaji wa jiko la umeme-jua zinatajwa kwamba, mbali ya kuokoa mazingira, ni uwezo wa kupika vyakula vigumu, kukaanga nyama, kupika supu, kuoka mikate na kuchemsha maji kwa muda mfupi.

Hata hivyo, jiko hilo linahitaji zaidi uwepo wa jua, kwani ndiyo chanzo cha joto linalofaa kupikia.

Mmoja wa wanakikundi hicho, Esther Moshi, amesema kupatikana kwa jiko hilo kutawakomboa wanawake wengi ambao mara nyingi ndio wanaokabiliwa na changamoto ya utafutaji wa nishati za kupikia kama kuni na mkaa.

"Tunashukuru mradi wa Green Voices kwa sababu unalenga kumkomboa mwanamke kutokana na adha ya upatikanaji wa nishati ya kupikia, kama majiko haya yatatengenezwa kwa wingi na kila familia kulipata, hakika yatakuwa mkombozi na yatasaidia kuokoa mazingira, " anasema.

Fatima Aziz Faraji ni mwenyekiti wa Chama cha TAWOCA, amesema ni muhimu kwa wanawake kuzidisha umoja wa vikundi ili waweze kusonga mbele na akaupongeza mradi huo kwamba utakuwa mkombozi si kwa wanawake pekee, bali jamii nzima.

Mgeni rasmi katika uzinduzi wa jiko hilo, Robert George, ambaye ni Ofisa Ushirika wa Manispaa ya Moshi, ameupongeza mradi wa Green Voices pamoja na akinamama hao na akahimiza kuwa, ni vyema kutumia teknolojia ambazo ni rafiki wa mazingira.

Amesema akinamama ndio waathirika wakubwa wa matumizi ya nishati za kupikia, na kwamba ndio wanaoongoza kupata madhara kiafya, hasa wanapotumia mkaa na kuni.

"Jitihada hizi za wenzetu wa Green Voices zinapaswa kuongezwa, kwa sababu zinalengo siyo tu kumkomboa mwanamke, bali kulinda mazingira yetu ambayo yanazidi kuteketea kila uchao kutokana na ukataji wa misitu kwa madhumuni ya kutafuta kuni na mkaa.

"Akinamama wanaathirika sana, wengine utakuta macho mekundu kutokana na moshi wa kuni, na wanapokuwa wazee ndio wanaoshambuliwa na watu wengine wasio na utu kwamba eti ni wachawi kwa sababu macho yao ni mekundu, lazima kutumia teknolojia mbadala kuwanusuru mama zetu, " alisema.

Hata hivyo, aliwataka akinamama hao kushikamana pamoja katika shughuli zao ili waweze kujiletea maendeleo, kwani umoja ni nguvu.

Kwa upande wake, Mratibu wa Mradi wa Green Voices Tanzania, Bi. Secelela Balisidya, amesema, mradi wa jiko la umeme-jua ni sehemu ya miradi 10 inayotekelezwa chini ya Green Voices ambapo Tanzania ndiyo pekee iliyopendekezwa kutekeleza mradi huo unaofadhiliwa na Taasisi ya Mfuko wa Wanawake wa Afrika, , ambayo inaongozwa na makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandez de la Vega Sanz.

Hata hivyo, taasisi hiyo inafadhili miradi 15 ya wanawake katika nchi 12 barani Afrika ambayo imeonyesha mafanikio, huku mradi wa Green Voices ukitajwa kuwa na mafanikio makubwa katika kipindi kifupi.

Kwa mujibu wa Bi. Secelela, Mradi wa Green Voices unatekelezwa katika mikoa sita ya Tanzania Bara ambayo ni Dar es Salaam, Pwani, Mwanza, Kigoma, Morogoro na Kilimanjaro.

“Miradi hiyo ni kilimo cha miti ya matunda mkoani Kigoma, kilimo cha viazi lishe visiwani Ukerewe mkoani Mwanza, Ufugaji Nyuki mkoani Morogoro na Pwani, ukaushaji wa mbogamboga kwa kutumia nishati ya jua mkoani Morogoro, usindikaji wa vyakula mbalimbali kutokana na muhogo mkoani Pwani, kilimo hai cha mbogamboga, na kilimo cha uyoga mkoani Dar es Salaam, mradi wa majiko banifu mkoani Pwani na mradi huu wa utafiti wa jiko linalotumia nishati ya jua mkoani Kilimanjaro,” anafafanua Secelela.

Anasema, lengo kubwa la mradi wa Green Voices ni kupaza sauti za akinamama kueneza ujuzi wao wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi ili jamii nzima ya kitanzania iweze kujifunza zaidi na kuzitumia mbinu hizo katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi.

Serikali kupitia taasisi na idara zake zilizo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Wizara ya Maendeleo ya Jamii imekuwa ikiendesha program mbalimbali za mafunzo ya ufundi ikiwemo utengenezaji wa majiko banifu na sanifu kama inayoendelea katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Malampaka wilayani Maswa.

Hata hivyo, bajeti ndogo imekuwa changamoto kubwa kukwamisha kuwafikia wananchi wengi na kuwapatia elimu ya aina hiyo.

MKUU WA WILAYA YA UBUNGO ALAKIAPO LEO JIJINI DAR ES ESALAAM

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amemuapisha Kisari Matiku Makori kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kufuatia uteuzi uliofanywa na Rais Magufuli kwa Wakuu wa Wilaya hivi karibuni.
Akimuapisha Mkuu huyo wa Wilaya RC Makonda ameeleza kuwa wananchi wa Ubungo wanamatumaini na uteuzi wake na lengo kuu la kuanzisha wilaya ya Ubungo ni kusogeza huduma za wananchi karibu hivyo inabidi ahakikishe anatatua changamoto zao kwa kuwafuata huko waliko na asiridhike na ripoti anazoletewa ofisini kwani kumekuwepo na changamoto kubwa ya uwajibikaji hivyo inabidi hajiridhishe kwanza.

Katika hatua nyingine RC Makonda amewaagiza wakuu wa wilaya wote kutoruhusu wananchi kubomolewa nyumba zao mpaka kuwepo hukumu halali ya mahakama kwani wananchi wamekuwa wanaonewa na kudhulumiwa haki zao, hivyo wakuu wa wilaya kwa kushirikiana na jeshi la polisi wahakikishe haki inatendeka kwa kufuatilia ukweli na kujiridhisha kwa kuzikagua nyaraka husika.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya huyo Makori ameomba ushirikiano kwa viongozi wenzake ili aweze kutimiza majukumu yake kikamilifu na kuahidi kuwa atafanya siasa za kuleta maendeleo ili kila mwananchi anufaike na rasilimali zilizopo.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akimwapicha Mkuu wa Wilaya ya Ubungo,Kisari Matiku Makori kufuatia uteuzi uliofanywa na Rais Magufuli kwa Wakuu wa Wilaya hivi karibuni. Leo jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
 Mkuu wa Wilaya ya Ubungo,Kisari Matiku Makori akila kiapo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda  kufuatia uteuzi uliofanywa na Rais Magufuli kwa Wakuu wa Wilaya hivi karibuni. Leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akimkabidhi katiba na ilani ya chama cha mapinguzi (CCM) Mkuu wa Wilaya ya Ubungo,Kisari Matiku Makori mara baada ya kumwapisha leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa wilaya wa mkoa wa Dar es Salaam,leo
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya jiji la Dar es Salaam.


KIUNGO WA ZAMANI WA TAIFA STARS ATHUR MWAMBETA ANAOMBA MSAADA

0
0

Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii.

Kiungo wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania na Simba Sports iliyokuwa ikiitwa Senderland ,Athur Mwambeta amewaomba wadau mbalimbali wa mchezo wa soka nchini na Chama cha Mapinduzi (CCM) kumsaidia kupata chombo cha usafiri kitakachomtoa sehemu moja mpaka nyingine mara baada ya kukatwa miguu yote miwili kutokana na maradhi yanayomkabili.


Mwambeta amesema hayo leo jijini Dar es Salaam katika mahojiano maalum na Globu ya jamii katika hospitali ya Taifa Muhimbili, ambapo amelazwa katika jengo la Kibasila ward namba 11, ambapo anaendelea na matibabu mara baada ya kukatwa mguu ijumaa iliyopita.


"Nimeugua maradhi haya pindi tu nilipoacha kucheza mpira hali iliyopelekea kukatwa mguu wangu wa kwanza mwaka 2015 na mwaka huu ijumaa iliyopita ndipo nilipokatwa mguu wangu wa pili na kubaki kama hivi mnavyoniona, kwani siwezi tena kusogea kutoka sehemu moja kwenda nyingine kama ilivyokuwa awali hivyo kwa yoyote anaeweza kunisadia naomba ajitokeze " amesema Mambeta.


Amesema kuwa anaomba wadau kumchangia kupitia nambari hii 0714435312 ili aweze kujikwamua katika changamoto mbalimbali za kimaisha.


Pia alitoa wito kwa wapenzi na wanachama wa CCM kujitokeza kumsadia kwani wao ni moja ya watu waliokuwa wahamasishaji wakubwa kupitia TANU mpaka ilipozaliwa CCM walitumia mpira kama sehemu ya hamasa.
 Wachezaji wa zamani wakiongozwa na Kitwana Manara wakimjulia hali,Athur Mwambeta,ambaye amekatwa miguu yote miwili



DCB YAIBUKA KIDEDEA SEKTA NDOGO NA KATI ZA KIBENKI KWA MWAKA 2015

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

BENKI ya DCB yaibuka kidedea kwa kupata zawadi ya kwanza kwa sekta ya benki ndogo na kati kwa ubora wa uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za hesabu kwa mwaka 2015.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam,Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Edmund Mkwawa amesema kuwa hii ni tuzo inayoandaliwa kila mwaka na bvodi ya uhasibu Tanzania (NBAA) ambapo yalianza toka mwaka 2011.

Mkwawa amesema kuwa katika kipindi cha miaka minne benki ya DCB imeweza kufanya vizuri kwa kushika nafasi tatu za juu na kuwa moja ya miongoni mwa benki zinazofanya vizuri na  katika uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za hesabu na kwa mwaka 2015 imeweza kushika namba moja.

Amesema kuwa benki yao inafuata miongozo ya utawala bora na kuwataka wawekezaji kuwa na imani juu ya usalama wa fedha zao walizoziwekeza na kuahidi kuendeleza mafanikio hayo kiujumla.

Mkwawa ameweka wazi mafanikio ya benki hiyoikiwemo ni kutimiza miaka 14 ya utoaji huduma bora za kibenki kwa wajasiliamali, kuongezeka kwa matawi kutoka mawili mwaka 2005 hadi matawi tisa 2016 na mwakani 2017 wanatarajia kufungua tawi la 10 mkoani Dodoma.

Mafanikio hayo ni pamoja na kuwa na mtaji imara wa bilioni 32 na upanuaji na uboreshaji wa huduma za kisasa kwa wateja wetu kupitia mawakal ambapo watawezesha wateja kupata huduma mbalimbali za kibenki kupitia mawakala walioidhinishwa na DCB katika vitongoji kwa kupitia DCB PESA inayotarajiwa kuanza Januri 2017.
 Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Edmund Mkwawa akizungumza na waandishi wa habari juu ya zawadi waliyoipata kwenye sekta ya benki ndogo na kati kwa ubora wa uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za hesabu kwa mwaka 2015.
  Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Edmund Mkwawa  akiwa ambebebelea zawadi waliyoipata ya sekta ya benki ndogo na kati kwa ubora wa uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za hesabu kwa mwaka 2015, pamoja na viongozi wengine wa benki hiyo.
   Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Edmund Mkwawa akionyesha kifaa kitakachokuwa kinatumiwa na mawakala wa benki hiyo katika mfumo utakaoenda wa DCB PESA unaotarajiwa kuanza Januari 2017.
Mawakala wa DCB wakiwa makini kusikiliza.

JESHI LA POLISI LAIMARISHA ULINZI KUELEKEA SIKUKUU ZA MWISHO WA MWAKA

0
0

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Jeshi la polisi limesema limeimarisha ulinzi kuelekea sikukuu za  Kristimasi na mwaka mpya hili kudhibiti vitendo vya uharifu .

Akizungunza leo, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba amesema jeshi la polisi katika kipindi cha sikukuu kuna watu wanajipanga kufanya uhalifu hivyo jeshi la polisi litafanya doria za kutosha.

Amesema kumbi zote zinazofanya starehe za kupiga mziki ziingize watu kutokana na ukumbi na watakaozidisha watachukuliwa hatua.

Afande Advera amesema wataondesha vyombo vya moto wataobainika  wametumia vilevi watachukuliwa kwani nia yao  nikutaka kusababisha ajali.

Aidha amesema wazazi wanatakiwa kufanya ulinzi kwa watoto wao kutokana na watoto kupotea katika siku za sikuu na kusababisha vituo vya polisi kuwepo kwa watoto hao.

Hata hivyo amesema  wananchi watoe ushirikiano kwa jeshi la polisi pale wanapohisi kuna watu wanaashiria kufanya uhalifu.

 Advera amesema kuwa wale ambao watatoa taarifa zikashindwa kutekelezeka wawasiliane na ngazi ya juu ili hatua ziweze kuchukuliwa kwa watu waliofanya uzembe.
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba

TAARIFA YA MATOKEO YA MITIHANI YA NBAA ILIYOFANYIKA 2016

0
0

BAR YA KWETU PAZURI TABATA YAFUNGWA KWA KUDAIWA KUTOKUKIDHI VIGEZO.

0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto ameagiza kufungwa kwa ukumbi maarufu wa Starehe ujulikanao kwa jina la Kwetu Pazuri Tabata kutokana na kushindwa kukidhi vigezo.

akizungumza na Globu ya jamii mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku mbili ,Kumbi la Moto amesema kuwa wameamua kufunga ukumbi huo mara baada ya kufanya na ukaguzi na kujiridhisha kuwa haijakidhi vigezo.

"Tumefanya ukaguzi na kumchukua Meneja wa Bar hiyo na kumfikisha kituo cha Polisi Ukonga Stakishari kwa ajili ya kufunguliwa mashataka na baadae kufikishwa mahakamani"amesema Kumbilamoto.

Amesema kuwa mara baada ya kutoka katika kituo hicho ,alifikishwa kituo cha Polisi kati na kukubali kulipa faini ya Milioni mbili na kukukiri makosa ya kufanya kazi ya Night Club bila kuwa na leseni huku akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Aidha tumewaonya juu ya tabia yao ya kupanga viti karibu na barabara jambo ambalo ni kinyume cha sheria za Tanroads, " hivyo  tumeamua tuifunge mpaka hapo watakapo jipanga upya",Kumbi la Moto amesema na kuongeza kuwa kwa muda mrefu watu walikuwa wakilalamika juu ya sehemu hiyo lakini hatua zilikuwa zinachelewa kuchukuliwa, hivyo nimefika katika eneo la tukio na kujionea hali halisi na kuamua kuifunga Bar hiyo.

Aidha katika ziara hiyo pia amekagua ujenzi wa maabara ya Zahanati ya kata ya vingunguti ambayo inatarajia kukamilika hivi karibuni.

MAJALIWA APOKEA MSAADA WA MAAFA YA TETEMEKO LA ARDHI KAGERA

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea msaada wa shilingi milioni 10 kutoka   Askofu Mkuu wa Kanisa la EAGT,  Dkt. Brown  Mwakipesele  ukiwa ni mchango  wa kanisa hilo kwa  waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye makazi yake , Oysterbay jijini Dar es salaam Desemba 22, 2016. Katikati ni Mchungaji Pray God Mgonja wa kanisa hilo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu Mkuu wa kanisa la EAGT,  Dkt. Brown Mwakipesile kabla ya kupokea msada wa shilingi milioni 10 uliotolewa na kanisa hilo kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika  kwenye makazi ya Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Desemba 22, 2016. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Askofu Mkuu wa Kanisa la EAGT, Dkt.  Brown Mwakipesile kabla ya kupokea msaada wa Shilingi milioni 10 ukiwa ni mchango wa kanisa hilo kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam, Desemba 22., 2016.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea fedha taslimu sh. milioni 10 kutoka Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) zikiwa ni msaada kwa ajili ya watu waliopatwa na maafa kutokana na tetemeko la ardhi mkoani Kagera.

Makabidhiano ya mchango huo yamefanyika leo mchana (Alhamisi, Oktoba 22, 2016) kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay, jijini Dar es Salaam.

Akikabidhi mchango huo, Askofu Mkuu wa Kanisa la EAGT, Dk. Brown Mwakipesile amesema kanisa hilo limeona lina wajibu wa kuisadia Serikali kuwapunguzia machungu watu waliopatwa na maafa kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera, Septemba 10, mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 17.

“Tumeona ni vema kanisa la EAGT lishiriki kuisadia Serikali kuwafariji wananchi waliopata maafa kutokana na tetemeko hilo. Tumeona ni wajibu wetu kwa sababu waliopatwa na maafa ni watu wetu wote. Tunawaombea wote waliopatwa na shida waweze kupata nafuu mapema zaidi,” amesema.

Askofu Mkuu Dk. Brown ametumia fursa hiyo kuipongeza Serikali kwa kusimamia vema suala hilo tangu lilipotokea hadi sasa na kuongeza kuwa wanamuomba Mwenyezi Mungu awape nguvu viongozi wa Serikali ya awamu ya tano ili waweze kutimiza majukumu yao ipasavyo.

“Ukiacha hili la tetemeko, tumeona jinsi Serikali ilivyosimamia vizuri suala la madawati hadi sasa kuna baadhi ya maeneo wamevuka hadi malengo. Tunamshukuru Mheshimiwa Rais Magufuli na Serikali nzima kwa kusimamia jambo hilo vizuri,” amesema.

Amesema kanisa hilo linatoa shukrani nyingi kwa Mheshimiwa Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa jitihada zinazofanywa na Serikali yake kukabili mambo mbalimbali yanayowagusa wananchi walio wengi.

Akitoa shukrani kwa Baba Askofu Mwakipesile na viongozi wa kanisa hilo aliombatana nao, Waziri Mkuu ameahidi kuwa Serikali itahakikisha michango hiyo inafikishwa Kagera kwa walengwa. “Nawashukuru sana kwa jinsi mlivyoguswa na kuamua kuwachangia wenzetu waliopatwa na maafa, tutahakikisha inawafikia walengwa,” amesema.

Waziri Mkuu amesema anawashukuru sana viongozi wa dini zote kwa jinsi wanavyoisadia Serikali kuwahudumia wananchi kupitia sekta mbalimbali. “Tunatambua juhudi zinazofanywa na taasisi za dini zote kuunga mkono juhudi za Serikali, tunafarijika mno na tunawashukuru sana,” ameongeza.

Amemuomba Askofu huyo pamoja na viongozi wengine wa dini wawaombee kwa Mungu viongozi waliopo madarakani ili awape hekima na busara na awawezeshe kuwaongoza vema Watanzania.

Tetemeko hilo la ardhi liliharibu miundombinu ya barabara, shule, zahanati na kujeruhi watu 440. Pia lilisababisha nyumba 2,063 kuanguka huku nyingine 14,081 zikiwa katika hali hatarishi na 9,471 zikipata uharibifu mdogo huku wananchi 126,315 wakihitaji misaada mbalimbali.

                            
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 - DAR ES SALAAM
ALHAMISI, DESEMBA 22, 2016.

Rais Magufuli ateua Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na pia ateua Majaji

0
0
Katibu Mkuu kiongozi Balozi John Kijazi akitangaza uteuzi wa viongozi ya Tume ya Uchaguzi, Tume ya Maadili na Majaji wa Mahakama ya Rufaa Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 22, 2016


PICHA NA IKULU


VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO IJUMAA DESEMBA 23, 2016

0
0

HOUSE FOR RENT AT MBEZI BEACH SHOPPERS '

0
0
Its a nice beach view house 8 Bedrooms, Large space for dining, Nice modern Kitchen, Large Green Garden, fully Air Condition.

The house is located Mbezi beach Shoppers.

Contact 0713 882 800





SERIKALI YAVIPIGA JEKI VIKUNDI 73 VYA UVUVI NCHINI

0
0
Na Frank Mvungi,MAELEZO-Dar es Salaam

SERIKALI kupitia Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi imetoa kiasi cha Tsh. Milioni 440 katika mwaka 2015/16 kwa  vikundi 73 vya uvuvi ili  kuiwezesha sekta ya uvuvi kuongeza tija na kuchangia kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa Viwanda nchini.

Hayo yamesemwa jana Jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Yohana Budeba wakati wa mahojiana maalum katika Kipindi cha “TUNATEKELEZA” kinachoratibiwa na Idara ya Habari (MAELEZO) kurushwa hewani kupitia Kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC).

Dkt. Budeba alisema Serikali imekusudia kuinua mchango wa sekta ya uvuvi kwa kuviwezesha vikundi vya wafugaji kuendesha shughuli zao kwa ufanisi mkubwa kwa kuvipatia ruzuku na mikopo kutoka katika taasisi mbalimbali za kifedha ikiwemo mabenki na mifuko ya hifadhi za jamii.

“Wizara inashirikiana na Halmashauri za Wilaya nchini katika kuwapatia fedha vikundi vyote vya wafugaji samaki waliopo katika ushirika, ambapo asilimia 40 hutolewa na Serikali ikihusisha ruzuku ya zana bora za uvuvi ikiwemo injini, nyavu na chakula cha samaki” alisema Dkt. Budeba.

Kwa mujibu wa Budeba alisema katika kuhamasisha ujenzi wa uchumi wa viwanda nchini kupitia mchango wa sekta hadi kufikia sasa Serikali imeanisha jumla ya viwanda 48 vya usindikaji samaki nchini, ikiwemo viwanda vidogo 36 vilivyopo katika ukandwa wa pwani wa bahari ya hindi, viwanda 11 vilivyopo kanda ya ziwa na kiwanda kimoja kilichopo katika ukanda wa ziwa Tanganyika.

Aidha Dkt. Budeba alifafanua kuwa katika kuwajengea uwezo vikundi hivyo, Serikali imekusudia kuajiri Maafisa Ugani katika kila kata nchini, hatua inayolenga kuongeza thamani ya mazao ya uvuvi na kuweza kutumika kama pato na lishe kwa wananchi.

Akizungumzia kuhusu maendeleo ya sekta hiyo, Dkt. Budeba alisema mpaka sasa Tanzania ina jumla ya mabwawa 22,000 yenye uwezo wa kuzalisha tani 10,000 za samaki, ambapo katika kipindi cha miaka mitano ijayo Serikali imekusudia kuvuna tani 50,000 za samaki, hatua inayolenga kuiwezesha nchi kujitosholeza na akiba ya samaki.

Akifafanua zaidi, Dkt. Budeba aliongeza kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wanafuga kitaalamu zaidi, ambapo Serikali inaendelea kutoa mafunzo kwa wataalamu wake katika vituo vya kutotoleshea vifaranga vya samaki vilivyopo Mbegani, Nyegezi na Igunga.

Alisema mikakati iliyopo kwa sasa ni pamoja na kuwawezesha wavuvi kukopa kutoka Benki ya Kilimo ili  kuwawezesha kuzalisha samaki na pia kuanzisha ufugaji wa Samaki katika maeneo mbalimbali kwa kutumia mfumo wa vizimba.

Dkt. Budeba alisema katika kuvutia wawekezaji katika sekta hiyo tayari Serikali imetoa amesema leseni 76,000, hatua inayolenga kuongezeka kiwango cha uzalishaji wa samaki nchini.

Alibainisha kuwa miongoni mwa changamoto zinazoikabili Wizara hiyo kwa sasa ni pamoja na uhaba wa Maafisa ugani, ambapo kwa sasa ina maafisa ugani 800 ingawa mahitaji halisi ni maafisa ugani 16,000.

TAASISI YA UTAFITI YA MAGONJWA YA BINADAMU KILIMANJARO (KCRI) YAWAKUMBUKA WATOTO WANAOLELEWA KITUO CHA UPENDO NA WALIOLAZWA KCMC.

0
0
Wafanyakazi wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu Kilimanjaro (KCRI) wakiwa katika picha ya pamoja na zawadi walizopeleka katika kituo cha kulelea Watoto Yatima cha Upendo cha mjini Moshi.
Zawadi ya Kei iliyotolewa kwa watoto wa kituo cha Upendo cha mjini Moshi.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Kilimanjaro,(KCRI) Profesa Blandina Mbaga akisalimiana na Msimamizi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Upendo cha mjini Moshi Sister Yasinta walipofika kwa ajili ya kutoa zawadi kwa watoto wa kituo hicho.
Msimamizi wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha Upendo cha mjini Moshi,Sister Yasinta Diwi akiwaeleza historia ya kituo hicho wafanyakazi wa taasisi ya utafiti ya magonjwa ya binadamu Kilimanjaro (KCRI).
Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu Kilimanjaro (KCRI) Prof Blandina Mbaga akizungumza na Mkurugenzi wa fedha Hosptali ya Rufaa ya KCMC,Hilda Mungure (katikati) na Elizabeth Msoka.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu Kilimanjaro (KCRI) wakiwa wamebea zawadi kwa ajili ya watoto wa kituo cha Upendo cha mjini Moshi.
Msimamizi wa Kituo cha Upendo cha mjini Moshi ,Sista Yasinta Diwi akiwaongoza watoto wanaolelewa katika kituo hicho kuwaimbia wageni waliofika katika kituo hicho kwa ajili ya kutoa zawadi. 
Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu Kilimanjaro (KCRI) akitoa zawadi kwa watoto wa kituo hicho. 
Wafanyakazi wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu Kilimanjaro (KCRI) wakifurahia na watoto wanaolelewa katika kituo cha Upendo cha mjini Moshi.
Mfanyakazi wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Kilimanjaro (KCRI) Anita akiwapa vipande vya Keki watoto wanaolelewa katika kituo cha Upendo cha mjini Moshi.
Mtoto Mwenye Umri wa wiki tatu anayelelewa katika kituo cha watoto cha Upendo baada ya kupelekwa kituoni hapo kufuatia mama wa mtoto huyo kuwa na ugonjwa wa akili. 
Mkurugenzi wa Taasisi ya Magonjwa ya Binadamu Kilimanjaro (KCRI) Prof Blandina Mbaga akizungumza muda mchache kabla ya kuwaona watoto waliolazwa katika Hosptali ya Rufaa ya KCMC.
Wafanyakazi wa Taasisi ya Utafiti ya Binadamu Kilimanjaro (KCRI) wakitoa zawadi kwa watoto waliolazwa katika wodi za watoto Hosptali ya Rufaa ya KCMC.
Wafanyakazi wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu Kilimanjaro (KCRI) wakirejea mara baada ya kutoa zawadi katika kituo cha Upendo na watoto waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
Viewing all 46202 articles
Browse latest View live




Latest Images