Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 106 | 107 | (Page 108) | 109 | 110 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Super Maya Baikoko kutoka Tanga wakifanya vitu vyao kwenye tamasha la siku ya muziki duniani lilifonyika jana kwenye viwanja vya posta Kijitonyama Dar es Salaam
   Mratibu wa Utamaduni wa Goethe Institut-Tanzania, Daniel Semheho (kulia) akiteja jambo na kiongozi wa kundi la Super Maya Baikoko Juma Nassoro (kushoto) katikati ni Mzungu Kichaa.
   Godzila
   Ben Paul
   Sarakasi pia zilikuwepo, kutoka makini kids
   Msanii Nyemo
   Barnaba na bendi yake
   Jhiko Man
  Kala Jeremiah

  Tamasha hilo liliandaliwa na umoja wa ulaya wa taasisi za utamaduni (EUNIC) na kudhaminiwa na Fastjet, Pepsi, Total na balozi za Ujerumani na Ufaransa.

  0 0

  Dr. Asha-Rose Migiro
  DAR ES SALAAM, Tanzania.

  NAIBU Katibu Mkuu Mstaafu wa Umnoja wa Mataifa, Dk. Ash-Rose Migiro amesifiwa kwa umahiri wa wake wa kutoingiza athari za kiingereza katika kiswahili, anapozungumza au kuhutubia, licha ya kuishi na kufanya kazi nje ya Tanzania kwa miaka mingi.

  Amesifiwa kwamba amekuwa akizungumza kiswahili fasaha kisichochanganywa na kiingereza, kwa athari za maneno au utamkaji kwenye mikutano ya hadhara au katika mazungunzo ya kawaida na watu.

  Sifa hizo zimetolewa leo na Mtaalam wa Kiswahili kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Mussa Kaoneka, katika kipindi cha lugha ya Kiswahili, kilichokuwa kikitangazwa na Kituo cha Radio One kilichopo Mikocheni, Dar es Salaam.

  "Hizi athari zinatokana na watu wengi kupenda kutukuza mno lugha za wenzetu, na tatizo limekuwa likidhaniwa kwamba huenda ni kitokana na mtu kuwa ughaibuni kwa mda mrefu, lakini mbona wapo baadhi ya Watanzania ambao wamekaa na kufanya kazi kwa muda mrefu nje, lakini wakizungumza Kiswahili utasuuzika moyo kwa jinsi wanavyokienzi wanapoongea", alisema Kaoneka na kuongeza;

  "Mmoja wa Watanzania hawa naomba  nimtaje, ni Dk. Asha-Rose Migiro aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, huyu ukimkuta anazungumza kwenye mikutano ya hadhara hata kwa kutumia hotuba ambayo hakuiandika, huwezi kumsikia amechanganya hata neno moja la kiingereza katika mazungmzo yake au kuzungumza kwa haiba ya kizungu.

  Kaoneka alisema, mbali ya hotuba, hata katika mazungumzo ya kawaida Dk. Asha-Rose ambaye kwa sasa ni Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, akiamua kuzungumza kiswahili ni kiswahili fasaha kisicho na mchanganyiko wa neno la Kiinereza hata moja.

  Katika kipindi hicho kilichorushwa kuanzia saa mbili asubuhi, kikiongozwa na mtangazaji Lugendo Madege, walikuwa wanajadili athari mbaya na nzuri za lugha nyingine kwenye Kiswahili katika zama hizi za utandawazi.

  Walisema, athari nzuri ni pamoja na Kiswahili kuweza kupata maneno mapya hasa ya majina ya vitu na teknbolojia ambavyo kabla ya udandawazi havikuwepo Tanzania na hivyo kulikuwa hakuna majina rasmi ya kuvitaja na athari mbaya ni baadhi ya watu kuchukua maneno ya Kiingereza na kuyapa tafsiri  ya 'sisisi' ambayo yanakiharibu Kiswahili.

  Kaoneka aliyataja baadhi ya maneno yanayotokana na tafsiri za aina hiyo kuwa ni 'Mwisho wa siku' linalotokana na neno la Kiingereza 'at the end of the day' ambalo kwa mujibu wa mtaalam huyo tafsiri yake sahihi ni 'hatimaye', na mtu kusema "siku hizi nafanyakazi na Benki, wakati usahihi ni "nafanyakazi benki".

  Alifafanua kuwa kusema, "nafanyakazi na Benki" ikimaanisha kuajiriwa Benki, siyo sahihi, kwa kuwa kutamka hivyo kuna maanisha kwamba mhusika na benki wanafanya kazi pamoja. IMEYATARISHWA NA BASHIR NKOROMO

  0 0

   kutoka kushoto, katibu mkuu ofisi ya makau wa Raisi Bwana Sazi Salula, waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais Muungano mh. Samia Suluhu Hassan, Mwenyekiti wa mkutano,Mh Ali Juma shamhuna waziri wa Elimu Zanzibar, akimuwakilisha  Wazri wa nchi ofisi ya makamu wa pili wa Rais Zanzibar kama mwenyekiti mwenza katika kikao cha kamati ya pamoja cha Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar cha kujadili changamoto za Muungano.
   Baadhi ya mawaziri wa Serikali ya mapinduzi Zanzibar katika kikao cha pamoja cha kujadili changamoto za muungano mjini Dodoma Leo
   pichani kushoto ni Waziri wa nchi Ofisi yamakamu wa Rais Muungano mh Samia Suluhu Hasan akiongoza kikao cha pamoja cha kujadili changamoto za muungano..mjini Dodoma leo.
  baadhi ya wakurugenzi kutoka Ofisi ya makamu wa rais wakifuatilia mazungumzo katika kikao cha pamoja cha kujadili changamoto za muungano kinachoendelea mjini Dodoma.Picha zote na Evelyn Mkokoi

  0 0


    Tatu bora ni katikati ni Redds Miss Kinondoni 2013 Lucy Tomeka, (shoto kwake) ni Prisca Clement, (kulia kwake) ni Phillios Lemi. 
   Warembo waliofanikiwa kuingia katika tano bora wakifurahia kwa pamoja, katikati ni Redds Miss Kinondoni 2013 Lucy Tomeka, (shoto kwake) ni Prisca Clement, (kulia kwake) ni Phillios Lemi. Wengone ni Sarah Paul (kwanza kulia) na Linda Joseph (kwanza kushoto).
   Mshindi wa Redds Miss Kinondoni 2013, Lucy Tomeka akivalishwa taji lake na mrembo aliyekuwa akilishikilia taji hilo Redds Miss Tanzania 2012/2013, Bright Alfred. Lucy Tomeka aliweza kuchukua taji hilo kwa kuweza kuwagalagaza wenzake wapatao 12 katika kinyang'anyiro hicho kilifanyika jana ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip jijini Dar.    
   Akivalishwa utambulisho wake.
   Showlove...

  0 0

   Jukwaa liko tayari kwa Show Babkubwa itakayoangushwa na Wasanii mbali mbali waliopo kwenye Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013 ndani ya Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma hivi sasa.ambapo leo hii ni sherehe ya wakazi wa Dodoma Kiburudani.
   Dj akiwa tayari tayari kwa kuangusha Bonge moja la Burudani.
   Mabaunsa wakiwa tayari washajipanga kwa kazi moja.


  0 0

   Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya,Linex akiwasalimia mashabiki na wapenzi wa Muziki waliofurika kwa wingi ndani ya Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma leo,ambapo usiku huu kulikuwa na bonge moja la Show ya Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013.
   Msanii aliejinyakulia Tuzo kadhaa za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013,Ommy Dimpoz akienda sambamba na timu yake ya Madansa wakitoa burudani ya kufa mtu ndani ya Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma usiku huu.
   Msanii Ben Pol akighani moja ya nyimbo zake.
   Msanii wa Hip hop Mwenye tuzo nne za Kilimanjaro Tanzania Music Awards  2013,Kala Jeremier akifanya vitu vyake usiku huu ndani ya Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
   Mashabiki hawakutaka kabisa kupitwa na taswira za show hii.
   Ni shangwe kwa kwenda mbele ndani ya Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma hivi sasa.   0 0


  Enie-Muyang-Tatah-founder and CEO

   Welcome  to !


  International African Festival Tübingen, Germany 2013

  Be part of 100.000 visitors at the largest Extravanganza !
   
   African Pilgrimage to Tübingen, Germany 2013 – outdoor & Entry Free

  International African Festival Tübingen proudly announces its 2013 season today, bringing together world class African lifestyle, music, food, exciting newcomers to the international stage from 8- 11 august 2013 – African Village (Festplatz) Open-air –Down town Tübingen, Germany.

  It is the fastest and largest growing Diaspora cultural event transforming the city of Tübingen in south of Germany into a pilgrim city, bringing African Diaspora worldwide irrespective of country of origin, gender and religious background , friends and well wishers of Africa together .

  More than 100.000 visitors are expected to attend International African Festival Tübingen 2013.This event promises a multi-dimensional exploration of interplay of authentic African culture and lifestyle -150 artists –live- featuring fresh sounds and voices –Ngoma Africa Band, Soweto Entsha, Wamali percussions, street arts, workshops and culinary expression.

  The Festival once again invites artist and audiences of all ages to experience African music, arts, culture and party, a mélange between traditional and modern Africa, bringing African hip-hop, Bongo Dansi,Kwaito,Afro-Pop,soukouss and African movies on the international stage Festival highlights will include- a grandiose opening ceremony lead by African children & youths, celebrities, African ambassadors rep.

   in Germany under the chairman ship of the Ghana Ambassador, program for families, panel discussion and late night events - the biggest African party in Germany, Stuttgart on Saturday night –form 22 o’clockfeaturing celebrities and Sunday will be special day for family – special church and Gospel day and closing ceremony Visual art is at the focus on our Festival and this year the African royal ballet is visiting all the way from Mali featuring Djiby & Basy Kouyate, dance styles and moves to support and build schools in Mali,   Christoffel-Blindemission project helping the blind to see in Africa, bongob trust and many more. 

  Stay updated on www.afrikafestival.net, follow and like us on facebook
  For more details you may  please contact:
  Madam Enie Muyang Tatah,CEO and Founder / Call +49-15210610374 /Email: kontakt@afrikafestival.net

  0 0


  Mwakilishi wa BOT,Bwa. Ephraim Mwasanguti  akitoa elimu kuhusu umuhimu wa kuweka hisa 
  ======  ===== ======

  WANACHAMA wa Benki ya wananchi Mufindi (MuCoBa) wameshauriwa kununua zaidi hisa katika benki hiyo ili kukuza mtaji wa benki na kufikia shilling billion mbili kiwango, ambacho kinahitajika katika benki kuu (BOT).
  Hayo yalisemwa na meneja mkaguzi wa Benki kuu Ephraim Mwasanguti wakati wa kikao cha kumi na nne cha wanahisa wa Benki ya Mufindi uliofanyika katika ukumbi wa southen highland ulioko mafinga.

  Mwasanguti alisema kuwa benki ikiwa na mtaji mzuri ina uwezekano wa kupunguza kukopa katika mabenki mengine na riba ya mwanahisa kuwa ndogo kutokana na benki kujiendesha yenyewe. Kwa upande wake mwenyekiti wa benki hiyo Attilio Muhole aliwataka wanahisa kutokuchukua gawio bali waendelee kununua hisa na kuwashawishi wanahisa kuwaleta wanunuzi wapya ili kukuza mtaji wa benki hiyo.

  Sambamba na hayo mkutano mkuu ulilizia gawio liwe shilingi 50 kwa hisa sawa na shilling million 44 ambapo ni asilimia 28 ya faida baada ya kodi.  0 0
 • 06/23/13--00:42: KUMEKUCHA TAMASHA LA ZIFF
 • ZIFF is East Africa’s largest film, music and arts festival, bringing new talents together from all over the world for a Zanzibar Tamasha.

  BONGO MOVIE AWARDS

  BONGO MOVIE AWARDS

  Awards at ZIFF 2013 will be awarded to Swahili/Bongo Movies  by ZUKU:
  ZIFF 2013 - General Program

  ZIFF 2013 - General Program

  OPENING FILM ZIFF 2013

  OPENING FILM ZIFF 2013...  0 0

  Mjumbe wa NEC Phares Magesa akiwa na Mwenyekiti wa TEWO SACCOS Mama Sophia Kinega mara baada ya kukagua ujenzi wa jengo la kitega uchumi la SACCOS hiyo mtaa wa Boko, Temeke

  0 0

  Mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa wa CHADEMA, (Kulia), na mbunge wa Iramba Magharibi, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Lameck Nchemba (Kushoto), wakinyoosheana vidole walipokutana mjini Dodoma kwenye semina ya wabunge kuhusu Ukimwi, iliyoandaliwa na chama cha wabunge walio katika mapambano dhidi ya UKIMWI (TAPAC), Jumamosi Juni 22, 2013.

  Kisa na mkasa wa hali hiyo ni pale Mchungaji Msigwa alipofoka kuwa, Mwigulu ndiye injinia wa machafuko kwenye shughuli za CHADEMA na kwamba ana uchu wa madaraka akitumia neno la kimombo "POWER HUNGRY", hali iliyopelekea Mwigulu kujibu mapigo kwa kusema, Mchungaji Msigwa anaweweseka. anayeshuhudia ni Mbunge wa Nyamagana CHADEMA, Ezekiel Wenje ambaye baadaye aliwaaamua na kuingia ukumbini. Hata hivyo mambo yaliendelea kuwa hivyo hivyo ndani ya ukumbi, hadi mama Anne Kilango Malecela alipowatuliza.

  Mwigulu Nchemba (Mwenye kofia ya Kichina, akiwa amezungukwa na wabunge wa CHADEMA, Peter Msdigwa (Kushoto), Ezekiel Wenje (Wapili kushoto), Said Arfi, Wakwanza kulia) na Vincent Nyerere.
  MWIGULU Nchemba, mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), akiwa kwenye mavazi rasmi yanayomtambulisha akiwa nje ya bunge, kofia ya jeshi la China na sklafu ya Tanzania.PICHA ZOTE KWA HISANI YA http://khalfansaid.blogspot.com


  0 0


  MWENYEKITI wa Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi Taifa (UVCCM), Sadifa Juma Hamisi, amepinga vikali kuwepo kwa mfumo wa serikali tatu kama inavyopendekeza rasimu ya katiba.
  Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma Hamisi (katikati) akiwa na mwenyekiti wa UVCCM kilimanjaro, Fredrick Mushi (kulia) na Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Aluu Segamba katika Hafla ya kutunuku Vyeti kwa wanachama wa UVCCM vyuo vikuu Kilimanjaro.

  Sadifa ameyasema hayo wakati akizungumza na wanachama wasomi wa UVCCM kutoka katika vyuo vikuu mkoani kilimanjaro katika hafla ya kuwaaga wasomi hao na ambapo pia ametunuku vyeti vya uanachama kwa wanafunzi 312 pamoja na kuwakabidhi kadi za uanachama wanachama wapya.

  Mwenyekiti wa UVCCM Kilimanjaro akiongoza maandamano kuelekea katika ukumbi wa CCM mkoa ambapo ndipo ilikofanyikia mkutano mkubwa wa UVCCM jana

  Mwenyekiti huyo ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Donge (CCM) zanzibar, amesema uwepo mfumo wa serikali tatu ni mzigo mkubwa kwani kutokana na uduni wa uchumi wan chi yetu itakuwa vigumu kuendesha serikali tatu kwa maana ya serikali ya Zanzibar, serikali ya Tanzania bara na ule wa muungano.
  Viongozi waandamizi wa CCM mkoani Kilimanajro katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa

  “Jamani tusidanganyane, kuendesha serikali tatu ni mzigo, kwa uduni wa uchumi wetu sidhani kama itakuwa rahisi kuendesha serikali tatu, kama kutakuwa na serikali tatu kuna hatari ya kuvunjika kwa muungano wetu huu maana uwezo kuchangia hatuna, tutajiingiza kwenye matatizo makubwa, vijana tuwe makini na tutumie taaluma zetu kuhimiza umuhimu wa kuwepo kwa muungano huu wa sasa,"
  Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma Hamisi Akipokea Maandamano ya Wanafunzi wa Vyuo vikuu Kilimanjaro ambao ni makada wa UVCCM mkoani Kilimanjaro

  Aidha Sadifa amewahimiza vijana kuwa mfano mzuri kwa jamii huku akiwahimiza kuwa waadilifu, wazalendo, kujiamini na kuwa na nidhamu hali ambayo itasaidia kuwepo kwa amani na usalama wa nchi.


  Amesema bila amani na muungano wa wananchi maendeleo hayawezi kupatikana katika nchi ambpo aliwataka vijana kuwa mtari wa mbele kuwaelimisha wananchi wa kawaida juu ya umuhimu wa kuenzi, kudumisha na kuimarisha muungano wa zanzibar na Tanganyika  kama njia pekee ya kuhakikisha nchi inakuwa na amani siku zote.

  Katibu wa UVCCM manispaa ya Moshi, Bwana Makwaiya akisakata Rumba muda mfupi baada ya maandamano kuwasili katika makao makuu ya CCM mkoa wa kilimanjaro

  “Vijana tuna wajibu kubwa wa kuwaenzi waliotuletea muungano wetu wa sasa, taaluma zetu ziwe dira ya jamii katika kuenzi, kudumisha na kuimarisha muungano wetu kwani ndio njia pekee ya kusaidia kudumisha amani na usalama wan chi yetu, tuepuke kujiingiza katika mkumbo wa wale wanaodai nchi haitatawalika,” amesema


  Hata hivyo Sadifa amewataka vijana kutodanganyika na vyama vinavyoeneza chuki na maandamano yasiyokuwa na msingi wowote huku akifafanua kuwa kisheria kuandamana na haki ya msingi lakini ifuate sheria na yassingilie haki za wengine.

  Sadifa akikabidhi cheti cha unachama kwa mwanafunzi wa chuo kikuu muccobs jana, jumla ya wanavyuo 312 walipata vyeti vya uanachama wa UVCCM

  “Chama pekee katika nchi hii ni CCM, kuna vyama vingine vimeanzishwa ambavyo mimi binafsi naviita ‘Saccos’, hauwezi ukajikopesha fedha kienyejienyeji kama alivyofanya Dk. Slaa! Vijana tuwe makini na saccos hizi ambazo ajenda zao ni kukopeshana na vurugu tu,” amesema Sadifa


  Kwa upande wake mwenyekiti wa shirikisho la wanafunzi wa vyuo vikuu wanachama wa CCM kilimanjaro, Wakati Mtulya akizungumzia changamoto wanazokumbana nazo, alisema kumekuwa na urasimu ndani ya bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, ambapo mikopo imekuwa ikitolewa kwa watu wasiostahili huku walengwa wakiendelea kutaabika.

   
  Mwenyekiti wa shirikisho la Vyuo Vikuu mkoani Kilimanjaro, Wakati Mtulya

  Amesema kuwa kumekuwa na mchezo ndani ya bodi hiyo, ambapo mikopo imekuwa ikitolewa kwa watoto wa matajiri huku wastahili ‘watoto wa wakulima’ wakibaki kuzungushwa na kuwekewa masharti magumu ya kupata mikopo hiyo jambo ambalo limekuwa likichangia kuwepo kwa vitendo vibaya miongoni mwa wanafunzi hao.

  Sadifa (aliyevaa suti) akiongoza vijana kucheza kwaito katika ukumbi wa CCM mkoa wa Kilimanjaro
  “Mikopo ni yetu, sio ruzuku, lazima tukopeshwe kwa wakati kwani lazima tutairudisha lakini jambo la kusikitisha, bodi hii imekuwa ikitoa mikopo kwa watoto wa masaki, huku sisi watoto wea mkulima tukiendelea kuzungushwa na kuwekewa masharti magumu ili kupata mikopo hiyo, hili ni tatizo,” amesema Mtulya (habari na TAIFA LETU.com). 

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na waumuni wa kanisa katoliki Emaus Centre Ubungo Jijini Dar walioshiriki katika ibada ya kupanda mbegu hivi karibuni. Mkuu huyo wa Mkoa alialikwa kama mgeni rasmi kuongoza zoezi hilo la kupanda mbegu ambalo lilifanikiwa kukusanya Tsh. Milioni 41.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na waumuni wa kanisa katoliki Emaus Centre Ubungo Jijini Dar es Salaam  ambapo aliwaasa  juu ya umuhimu wa kutunza amani iliyopo nchini kwa kujiepusha na mambo madogomadogo yanayoweza kuondoa amani iliyopo ikiwemo mijadala ya kuchinja ambayo ilishaanza kufanya machafuko nchini. Hata hivyo aliwaomba waumini hao kuwaombea wanasiasa wafanye kazi zao vizuri kwa haki, usawa na uwajibikaji badala ya kuishia kuwatupia lawama ambazo hazijengi.

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akishiriki kukusanya sadaka zilizokuwa zikitolewa na waumini wa kanisa katoliki Emaus Centre Ubungo Jijini Dar walioshiriki katika ibada ya kupanda mbegu hivi karibuni. Mkuu huyo wa Mkoa alialikwa kama mgeni rasmi kuongoza zoezi hilo la kupanda mbegu ambalo lilifanikiwa kukusanya Tsh. Milioni 41.
  Waumini wa kanisa katoliki kutoka sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam waliokuwa wamekusanyika "Emaus Centre" Ubungo kwa ajili ya ibada ya kupanda mbegu iliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya hivi karibuni.
  (Picha na Hamza Temba) Hamza Temba 2:56 PM (6 hours ago) to MUHIDIN, johnbukuku, me, haki.yako, Mroki, Maggid
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na waumuni wa kanisa katoliki Emaus Centre Ubungo Jijini Dar walioshiriki katika ibada ya kupanda mbegu hivi karibuni. Mkuu huyo wa Mkoa alialikwa kama mgeni rasmi kuongoza zoezi hilo la kupanda mbegu ambalo lilifanikiwa kukusanya Tsh. Milioni 41.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na waumuni wa kanisa katoliki Emaus Centre Ubungo Jijini Dar es Salaam  ambapo aliwaasa  juu ya umuhimu wa kutunza amani iliyopo nchini kwa kujiepusha na mambo madogomadogo yanayoweza kuondoa amani iliyopo ikiwemo mijadala ya kuchinja ambayo ilishaanza kufanya machafuko nchini. Hata hivyo aliwaomba waumini hao kuwaombea wanasiasa wafanye kazi zao vizuri kwa haki, usawa na uwajibikaji badala ya kuishia kuwatupia lawama ambazo hazijengi.

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akishiriki kukusanya sadaka zilizokuwa zikitolewa na waumini wa kanisa katoliki Emaus Centre Ubungo Jijini Dar walioshiriki katika ibada ya kupanda mbegu hivi karibuni. Mkuu huyo wa Mkoa alialikwa kama mgeni rasmi kuongoza zoezi hilo la kupanda mbegu ambalo lilifanikiwa kukusanya Tsh. Milioni 41.

  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akinadi kitabu cha Sumbawanga Ng'ara alichoandika yeye mwenyewe kwa waumini wa kanisa katoliki Emaus Centre Ubungo Jijini Dar (hawako pichani) walioshiriki katika ibada ya kupanda mbegu hivi karibuni, kitabu hicho kinachoelezea juu ya usafi na udhibiti wa mazingira Mkoani Rukwa na taifani kwa ujumla kilitumika pia kupandia mbegu. Mkuu huyo wa Mkoa alialikwa kama mgeni rasmi kuongoza zoezi hilo la kupanda mbegu ambalo lilifanikiwa kukusanya Tsh. Milioni 41.

  0 0

   Katibu wa Wabunge wa Tanzania Katika Bunge la Afrika Mashariki, Shy-Rose Bhanji akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu miswada mbalimbali iliyojadiliwa na bunge hilo kwa kipindi cha  mwaka mmoja. Kushoto ni mbunge wa bunge hilo, Abdullah Mwinyi. (Picha zote na Habari Mseto Blog)

   Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Abdullah Mwinyi akizungumza na waandishi wa habari leo. Kulia ni Katibu wa wabunge wa Tanzania katika bunge hilo, Shy-Rose Bhanji.

  DAR ES SALAAM, Tanzania

  KATIBU wa Wabunge wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki, Shy-Rose Bhanji, amejivunia harakati chanya alizoshiriki katika kipindi cha mwaka mmoja tangu kuanza kushiriki vikao vya bunge hilo Juni mwaka jana, huku akiielezea kuvutiwa na miswada miwili inayosubiri baraka za Marais wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.


  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Shy-Rose, alisema kuwa, yeye kama mbunge amejifunza mengi katika miezi 12 ya uwapo wake bungeni, huku akiitaja miswada hiyo kuwa ni sheria ya Udhibiti wa Uzito wa Magari Barabarani ‘Vehicle Load Contol Bill’ na Punguzo la Vituo vya Ukaguzi Mipakani ‘One Stop Border Posts Bill.’
                                                                                                                                                                                                                                                 

  Aliongeza kuwa, bunge hilo limeijadili kwa kina miswada hiyo, ambayo kwa sasa inasubiri maamuzi ya Marais wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, huku akitoa wito kwa wafanyabiashara kutumia fursa za Kijiografia za Afrika Mashariki ili kujiletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla.


  Shy-Rose alisema kuwa, sheria hizo zitakuwa na tija kubwa kwa wananchi na mataifa yanayounda Jumuiya ya Afrika Mashariki, kutokana na ughali wa ujenzi wa miundombinu ya barabara kwa sasa, lakini pia urasimu ulioshamiri katika vituo vingi vya ukaguzi wa abiria na mizigo mipakani kwa wanaotoka nchi moja kwenda nyingine.


  “Uhai wa barabara zetu Afrika Mashariki unategemea matumizi sahihi, yanayozingatia uzito wa magari kwa barabara husika. ‘Vehicle Load Control Bill’ ina kila kanuni itakayowabana madereva kuhakikisha wanatumia barabara kwa uzito sahihi wa mzigo garini, ili kuzifanya zidumu kwa muda mrefu,” alisema Shy-Rose.


  Aliongeza kuwa, mawasiliano ya barabara ndio mhimili wa maendeleo katika nchi yoyote na ili kudumisha barabara kuepuka ujenzi ghali wa mara kwa mara, sheria hiyo imependekeza uzito wa juu kabisa kwa magari yanayotumia barabara za Afrika Mashariki uwe ni tani 55 na sio zaidi.


  Alifafanua kuwa, muswada huo umezingatia mambo mengi, hasa kutokana na ukweli kuwa kabla ya hapo kila nchi ilikuwa na sheria yake ya uzito wa juu zaidi barabarani, huku nchi nyingine za Afrika Mashariki zikiwa hazina sheria hiyo na kuruhusu magari kubeba uzito wowote na kupita barabara yoyote.


  Kuhusu muswada wa ‘One Stop Border Posts Bill,’ Shy-Rose alisema kuwa, ni wazi kwamba jamii ya Wana-Afrika Mashariki, imechoshwa na urasimu mkubwa unaowakumba wanapohitaji kusafiri kutoka nchi moja kwenda nyingine, unaosababishwa na uwingi wa vituo vya ukaguzi wa abiria na mizigo yao, hivyo muswada huyo ni tiba ya kero hiyo.


  “Sheria hii ikipitishwa na kuridhiwa na Marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, itamaliza hadha za usafiri zisizo za lazima, wanazokabiliana nazo wananchi, kiasi cha kuchelewesha safari zao na kjurudisha nyuma harakati chanya za kujiletea maendeleo yao na nchi zao kwa ujumla,” alisema Shy-Rose.


  Kwa upande wake, Mbunge mwingine wa bunge hilo, Abdullah Mwinyi, alisema Jumuiya ya Afrika Mashariki imejikita kujiletea maendeleo kupitia nyanja tofauti, zikiwamo za Forodha, Soko Huria na Sarafu ya pamoja, ambapo Bunge hilo limejadili mengi yaliyo bora kuhusu Forodha na sasa wanaingia katika Soko Huria.  “Soko Huria ndio kiini halisi cha mafanikio ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Dalili za mafanikio kupitia nyanja hiyo zimeanza kuonekana, ambapo bidhaa nyingi za Afrika Mashariki zilizokuwa zikiuzwa huko Afrika Magharibi, kwa sasa zinaingia rasmi kwenye mzunguko wa nchi wanachama wa Afrika Mashriki na kuchangia maendeleo ya pamoja,” alisema Mwinyi.


  Aidha, Shy-Rose na Mwinyi wakatumia fursa hiyo kuwasilisha pole ya pamoja kati yao na wabunge wengine wa Bunge la Afrika Mashariki, kwa wahanga wa bomu jijini Arusha, ambako watu kadhaa walifariki dunia na wengine kujeruhiwa vibaya, huku wakilaani vikali shambulizi hilo lililoathiri watu wasio na hatia.


  “Tunaviomba vyombo vya dola kuhakikisha vinatumia kila njia kuwanasa waliohusika na kuwawajibisha kwa mujibu wa sheria. Tunawaomba wana Arusha na atanzania kwa ujumla kudumisha amani, upendo, utulivu na mshikamano miongoni mwa Watanzania,” walisisitiza wabunge hao.


  Kwa mujibu wa wabunge hao, vikao vijavyo vya bunge hilo vitafanyika kama ifuatavyo: Agosti 18 hadi 29, Oktoba 13 hadi 26 vikao vitakuwa jijini Arusha, huku Novemba 17 hadi Desemba 6 vikao vikiwa jijini Nairobi. Desemba 19 hadi 31, Januari 9 hadi Machi 22 na Mei 25 hadi Juni 6 mwakani vikao vyote vitafanyika jiji Arusha.

  0 0


  The comedy show is just around the corner and I've left this a little late, but please forward to your respective sites and make some noise about this event. Around 8 standup comedians on 1 stage cracking your ribs like nonsense, now at our new venue; East 24 Bar & Grill (former Arcade). The logos have been attached just in case you need to use them creatively ; ))

  Hope to see some of your faces there!!

  Best Regards,


  Evans.

  0 0

   Mkuu wa Kitengo Cha Ukaguzi wa Mikataba katika Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Steven H. Issack alipotembelea banda la wizara ya fedha kutaka kupata ufafanuzi juu ya uanzishwaji wa mikopo kwa watumishi wa umma kutoka kwa Mhasibu Mkuu wa Serikali,  kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mikopo Bi. Christine Ngonyani na kulia ni Bi. Miriam Mnzava Nchini Ghana.

   Mkuu wa Kitengo cha Mikopo wa Wizara ya Fedha kutoka kwa Mhasibu Mkuu wa Serikali Bi. Christine akiwaeleza wananchi wa Ghana jinsi idara ya  Mhasibu Mkuu wa Serikali inavyosaidia Watumishi wa Umma katika kupata Mikopo. 
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Celina O. Kombani alipotembelea Banda la Wizara ya fedha katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.

   Washiriki kutoka Nchi mbalimbali walipotembelea katika makumbusho ya taifa ya Ghana.

   - Washiriki wa Maonesho ya Wiki ya Utumishiwa Umma kutoka Tanzania na nchi nyingine wakifurahia ushiriki katika maonesho hayo Nchini Ghana. 
   Mwakilishi kutoka Wizara ya Fedha chini ya Mhasibu Mkuu wa Serikali Bi. Miriam Mnzava alipotembelea banda la Zimbabwe wakati wa maonesho hayo.  
   Msemaji wa Wizara ya Fedha akiwa ameambatana na washiriki wengine kutoka wizara ya fedha wakiwa kwenye banda la Zimbambwe wakibadilishana uzoefu juu ya utendaji kazi katika nyanja mbalimbali walipokuwa Nchini Ghana.

  Afisa Tawala Mwandamizi Bw. E. Ndofi kutoka kwa Mhasibu Mkuu wa Serikali Wizara ya Fedha, akitoa ufafanuzi kuhusu watumishi wa Idara na Vitengo vilivyopo kwa Mhasibu Mkuu wa Serikali wakati wa maonesho ya wiki ya utumishi wa umma Nchini Ghana .Picha zote naScolaMalinga-Wizara ya fedha, Tanzania

  0 0

  UKITAKA KUISOMA SIMULIZI HII KWA UNDANI ZAIDI INGIA

  0 0


   Makamu wa pili wa Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Ally Iddy akipokea vifaa mbalimbali vya michezo kwa timu za baraza la wawakilishi za mpira wa miguu na pete toka kwa Meneja masoko wa kinywaji cha Grandmalt  Fimbo Mohamed Butallah kwenye makabidhiano yaliyofanyika kwenye ukumbi la baraza la wawakilishi Zanzibar, kushoto kwake ni mwenyekiti wa timu ya Baraza la wawakilishi mheshimiwa Hamza Hassan Juma. Picha kwa Hisani ya Intellectuals Communications Limited.
    Makamu wa pili wa Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Ally Iddy pichani kati akiwashukuru Grand Malt kwa msaada mkubwa walioutoa wa vifaa mbele ya Wanahabari (hawapo pichani),wakati alipokuwa akipokea vifaa mbalimbali vya michezo kwa timu za baraza la wawakilishi za mpira wa miguu na pete toka kwa Meneja masoko wa kinywaji cha Grandmalt  Fimbo Mohamed Butallah kwenye makabidhiano yaliyofanyika kwenye ukumbi wa baraza la wawakilishi Zanzibar. kushoto kwake ni mwenyekiti wa timu ya Baraza la wawakilishi mheshimiwa Hamza Hassan Juma.  
   Meneja masoko wa kinywaji cha Grandmalt  Fimbo Mohamed Butallah akizungumza machache kwenye makabidhiano ya vifaa vya michezo kwa   Makamu wa pili wa Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Balozi Seif Ally Iddy wakati alipokuwa akipokea vifaa mbalimbali vya michezo kwa timu za baraza la wawakilishi za mpira wa miguu na pete yaliyofanyika kwenye ukumbi la baraza la wawakilishi Zanzibar, kushoto kwake ni mwenyekiti wa timu ya Baraza la wawakilishi mheshimiwa Hamza Hassan Juma.
  ==========  ====== ========
  TIMU za Baraza la Wawakilishi za mchezo wa soka na netiboli, mwishoni mwa wiki zilikabidhiwa vifaa vya michezo vya aina mbalimbali ili kuziwezesha kushiriki mashindano mbalimbali kwa uwezo zaidi.
  Vifaa hivyo vilitolewa na kinywaji kisicho na kilevi cha Grand Malt, ambao walisema kutokana na kuamua kuwekeza katika michezo Zanzibar, waliona ni vema kuvikabidhi pia kwa timu za Baraza la Wawakilishi ili wajumbe wake waweze kuwa sehemu ya maendeleo ya michezo hapa nchini.
  Akikabidhi vifaa hivyo kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Idd, Meneja Masoko wa Grand Malt, Fimbo Butallah alisema, wataendelea kuwekeza katika miichezo kwani wanaamini itatoa fursa kubwa kwa watu mbalimbali kushiriki na hata kuongeza kipato kwao.
   “Grand Malt ikiwa ni wadhamini wakuu wa Ligi Kuu ya Zanzibar, iliona vema ikatoa msaada huu wa vifaa vya michezo kwa timu za Baraza la Wawakilishi, ili wajumbe wake wawe sehemu ya kuendeleza michezo hapa nchini,” alisema.
  Akipokea msaada huo, Balozi Seif aliishukuru Grand Malt na kuiomba pia idhamini sherehe za Mapinduzi Zanzibar na akataka zitayarishwe mbio fupi ambazo wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi watashiriki, huku akiahidi atakuwa mmoja wao.
   “Grand Malt ni kinywaji cha afya kwasababu hakina kilevi, naomba waendelee kutusapoti katika mambo mbalimbali na tukumbuke michezo ni afya, hivyo pia ingekuwa vema mngeaa mbio fupi kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, nami naahidi nitashiriki,” alisema.

  Grand Malt kinywaji kisicho na kilevi kwa sasa ndio wadhamini wakuu wa Ligi Kuu ya Zanzibar.

  0 0

   Mmoja wa washiriki wa shindano la Bibi Bomba awamu ya pili Bi.Anna Nicholaus akikabidhiwa fulana yenye jina lake na mmoja wa Waratibu wa shindano hilo,AJ Jonathan,wakati wa utambulisho rasmi wa washiriki hao mapema jana jioni mbele ya Wanahabari (hawapo pichani),uliofanyika kwenye ukumbi wa alliance française,jijini Dar.Aidha pia washiriki hao wapatao ishirini walipata nafasi ya kusaini mikataba yao na pia kuelezwa utaratibu mzima wa mchakato wa Bibi Bomba 2013.
   Bi.Anna Nicholaus akivalishwa fulana yake ya ushiriki kutoka kwa mmoja wa waratibu wa shindano hilo lenye msisimko mkubwa,Asmah Makau.
   Mshiriki mwingine wa shindano la Bibi Bomba.Bi.Tabitha Tungaraja akishukuru Mungu mara baada ya jina lake kutajwa na kuingia kwenye ushiriki wa shindano hilo,mbele ya baadhi ya waratibu wa shindano zima
   Pichani wa pili kushoto ni Meneja wa Clouds TV ambao ndio warushaji wa shindano la Bibi Bomba season 2,Bwa.Lee Ndayisaba akifafanua jambo mbele ya washiriki wa shindano hilo na wanahabari (hawapo pichani) kuhusiana uendeshaji na mchakato mzima wa shindano hilo ambalo limekuwa na msisimko mkubwa kwa watazamaji.Shoto ni mmoja wa waratibu wa shindano hilo Babuu wa Kitaa (Clouds TV),tatu shoto ni wawakilishi wa shirika la USAID,Bi.Naomi Kaspar pamoja na Dkt.May Bukuku, ambao wametoa mchango mkubwa kufanikisha maandalizi ya shindano hilo. 
   Baadhi ya washiriki wa shindano la Bibi Bomba awamu ya pili 2013 wakiwa ndani ya ukumbi wa alliance française wakisiliza mchakato mzima wa utaratibu wa shindano hilo.
  Baadhi ya Mabibi Bomba wakifurahi jambo.Picha na Michuzijr.Blogspot.com

  Shindano hilo lilianza mchakato wake wa usaili katika viwanja vya Leaders  Club, ambapo Mabibi zaidi ya 60 walijitokeza aidha kati yao waliingia katika mchujo wa awali na kupatikana Mabibi 20 ambao wameendelea kupigiwa kura hadi hii leo.


  Shindano la Bibi Bomba season 2 limezinduliwa rasmi hapo jana katika ukumbi wa Alliance Française, ambapo bibi 20 wanaingia rasmi katika kinyanganyiro cha kumtafuta bibi Bomba kwa mwaka 2013.

  "siku zote panapokuwa na watu wengi lazima vituko, kero ama ubabe lazima vinanafasi ya kujitokeza ili kutimiza ule msemo wa kiswahili unaosema “penye wengi kuna mengi” ..tunatarajia msisimko wa aina yake katika mashindano haya kwa mwaka huu.


  tofauti pia na mwaka jana ambapo shindano hili lilidumu kwa mwezi mmoja,na mwaka huu Bibi bomba itachukua takriban miezi 3.Mengi mtayapata wakati kipindi kikiwa kinaruka kuanzia saa mbili na nusu usiku",alimaliza kusema Lee wa Clouds TV ,kituo ambacho kitakuwa kikirusha shindano hilo.

  0 0

   Ofisa Uhusiano wa Airtel TanzaniaJane Matinde akipiga penati kuashiria
  uzinduzi rasmi ya Airtel Rising Stars Mkoa wa Kinondoni.
   Ofisa Uhusiana wa Airtel Tanzania akikagua timu kabla ya mechi kuanza.
   Mchezaji chipukizi wa timu ya soka ya Sifa United ya Manzese Abuu
  Mohamed (kushoto) akichuana na mchezaji wa Makumbusho United Shabani
  Idd wakati wa mechi ya ufunguzi wa mashindano ya vijana chini ya umri
  wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars, Mkoa wa Kinondoni, iliyofanyika
  uwanja wa mpira wa shule ya msingi Mwanamanyala jijini Dar es Salaam
  Juni 23, 2013. Makumbusho United walishinda 3-1
   Mchezaji wa timu ya soka ya Sifa United ya Manzese Yassin Saleh
  (kulia) akichuanana na Shaban Idd wa Makumbusho United wakati wa mechi
  ya ufunguzi wa mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya
  Airtel Rising Stars, Mkoa wa Kinondoni, iliyofanyika uwanja wa mpira
  wa shule ya msingi Mwanamanyala jijini Dar es Salaam Juni 23, 2013.
  Makumbusho United walishinda 3-1

  Mshambuliaji Ally Amin wa Makumbusho United (kulia) Abuu Mohamed wa
  Sifa United ya Manzese wakipambana vikali wakati wakati wa mechi ya
  ufunguzi wa mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel
  Rising Stars, Mkoa wa Kinondoni, iliyofanyika uwanja wa mpira wa shule
  ya msingi Mwanamanyala jijini Dar es Salaam Juni 23, 2013. Makumbusho
  United walishinda 3-1.

  =======  =======  ====== ======

  Michuano ya Airtel Rising Stars yaanza Rasmi -Makumbusho yaibamiza Sifa 3-1

  Timu ya Makumbusho United imeanza vema mashindano ya vijana chini ya
  umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars mkoa wa kisoka wa Kinondoni
  baada ya kuibamiza timu ya Sifa United ya Manzese 3-1 katika mechi
  iliyokuwa na ushindani mkubwa iliyopigwa kwenye uwanja wa Mwananyamala
  shule ya msingi jijini Dar es Salaam leo Jumapili, Juni 23 2013.

  Ilikuwa ni Sifa United walioanza kufunga goli katika dakika ya 16
  wakati mchezaji wao hatari Jumbe Evon alipowatoka walinzi wa
  Makumbusho United na kuachia shuti kali iliyotinga wavuni moja kwa
  moja na kuibua hamasa kubwa kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo
  waliofika uwanjani kushuhudia mchezo huo. Goli hili lilidumu hadi
  mapumuziko.

  Baada ya kupata maelekezo kutoka kwa kocha wao, wachezaji wa timu ya
  Makumbusho United walikianza kipindi cha pili kwa kasi kubwa na juhudi
  zao zilizaa matunda dakika tatu ndani ya kipindi cha pili wakati
  mchezaji mwenye kasi Willy Kalolo alipoipatia timu yake goli la
  kusawazisha.

  Goli hilo la kusawazisha lilibadilisha kabisa sura ya mchezo huku
  vijana wa Manzese wakipambana kupata goli la kuongoza lakini walinzi
  wa Makumbusho walikuwa imara. Ilikuwa dakika ya 55 ambapo Makumbusho waliandika goli la pili kupitia kwa Ally Amin ambaye alipiga shuti kali na kuingia wavuni kabla ya Kalolo kufunga goli la tatu daikia ya
  70 na kuzima ndoto za Sifa United za kushinda mechi hiyo

  Michuano hiyo ya kusaka vipaji vya wanasoka chipukizi inaendelea kesho
  Jumatatu Juni 24 katika uwanja huo huo ambapo timu ya Mtakuja Beach
  itapambana na Sifa United.

  Katika mkoa wa kisoka wa Ilala, Buguruni Youth Center (BYC) kesho Juni
  24 watakuwa na kibarua kigumu watakapopambana na Bomubomu katika mechi ya kukata utepe itakayofanyika kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa
  Secondari jijini Dar es Salaam. Kila upande umetamba kwamba utaibuka
  na ushindi.

  Wakati michuano hii inaendelea, makocha watakuwa na kibarua kigumu cha kuchagua wachezaji ishirini bora kuunda timu za mikoa kwa ajili ya
  fainali za Taifa zitakazopigwa katika uwanja wa kumbukumbu ya Karume
  jijini Dar es Salaam kuanzia julai 2 2013.

  Mkoa wa Temeke ambao ndio mabingwa watetezi wa ARS Taifa wanatarajia
  kuanza mashindano haya ngazi ya mkoa siku ya Jumanne Juine 25. Mikoa
  mingine inayoshiriki Airtel Airtel Rising Stars mwaka huu ni Morogoro,
  Mwanza, Mbeya, Tanga, Kigoma na Ruvuma.

  Programu hii ya Airtel Rising Stars ni ya Afrika nzima likiwa na lengo
  la kuendeleza na kukuza mpira wa miguu katika bara la Afrika kwa
  vijana wanaochipukia waweze kupata nafasi ya kuendeleza vipaji vyao.

  Fainali za ARS Taifa vile vile zitatumika kuchagua timu bora za
  wavulana na wasichana ambao wataiwakilishaTanzania katika mashindano
  ya kimataifa ambapo nchi mwenyeji wa michuano hiyo itatangazwa mwezi
  ujao. Wachazeaji wengine watachaguliwa kwenda kwenye kliniki
  itakayoendeshwa na makocha kutoka klabu maarufu duniani ya Manchester
  United

older | 1 | .... | 106 | 107 | (Page 108) | 109 | 110 | .... | 1898 | newer