Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

NSSF YASHIRIKI UZINDUZI WA KAMPENI YA 'AFYA YAKO MTAJI WAKO'

$
0
0
 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akiongoza wananchi katika matembezi ya hisani wakati wa uzinduzi wa  Kampeni ya Kitaifa ya Kudhibiti Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza  kwenye viwanja vya Leaders Club, iliyolenga kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi na upimaji wa Afya katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.
Maofisa wa NSSF wakiwa katika picha ya pamoja katika banda lao. Kutoka kushoto ni Ofisa Matekelezo, Abeid Abdulaziz, Ofisa Mwandamizi Uhusiano na Masoko, Amina Mmbaga, Ofisa Uhusiano na Masoko, Kiamba Rajab.
Wananchi wakiwa katika banda la NSSF.
 Wananchi wakipata maelezo juu ya Mafao yatolewayo na NSSF.
 Wananchi wakipata ufafanuzi juu ya mafao ya NSSF.
Ofisa Mwandamizi Uhusiano na Masoko wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Amina Mmbaga (wa pili kulia), akitoa ufafanuzi kwa watu waliojitokeza katika banda la NSSF.
Ofisa Matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abeid Abdulaziz (kulia), akitoa maelezo kwa wanachama wapya wa NSSF juu ya mafao yatolewayo na shirika hilo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Kudhibiti Magonjwa Yasiyo Ambukiza.
Ofisa Matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abeid Abdulaziz (kulia), akitoa maelezo kuhusu fao la matibabu (SHIB), linalotolewa na mfuko huo kwa wananchi waliofika katika uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Kudhibiti Magonjwa Yasiyo Ambukiza jijini Dar es Salaam
Ofisa Matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abeid Abdulaziz (kulia), akitoa maelezo kuhusu fao la matibabu (SHIB), linalotolewa na mfuko huo kwa wananchi waliofika katika uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Kudhibiti Magonjwa Yasiyo Ambukiza jijini Dar es Salaam
Kiamba Rajab akimwandikisha mwanachama mpya wa NSSF.
Wanachama wakiandikishwa.
Wanachama wapya wa NSSF wakijiandikisha. 
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalim akiwa ameongozana na Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Amina Mmbaga.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalim akisalimiana na Ofisa Matekelezo wa NSSF, Abeid Abdulaziz.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalim (kushoto), akisalimiana na Ofisa Uhusiano NSSF, Kiamba Rajab, wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Kudhibiti Magonjwa Yasiyo Ambukiza na kudhaminiwa na NSSF. Katikati ni Ofisa Matekelezo wa NSSF, Abeid Abdulaziz
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalim akisoma vipeperushi vinavyoelezea taarifa za mfuko wa NSSF alipotembelea banda la shirika hilo. 
Maofisa wa NSSF wakimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalim akizungumza na maofisa wa NSSF alipotembelea banda lao.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalim (wa tatu kushoto), akiwa katika picha ya pamoja. 

BARABARA YA LOLIONDO-MTO WA MBU KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kuhusu utekelezaji wa miradi ya miundombinu alipowatembelea ofisini kwao.
Muonekano wa barabara ya Changarawe ya Loliondo – Mto wa Mbu KM 218 inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Manyara
Mkazi wa Kijiji cha Sale, Bw. Michael Nagwianye mkoani Manyara akitoa maoni kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa mara baada ya kukagua barabara ya Loliondo – Mto wa Mbu KM 218 inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami.

……………….


Serikali imesema ipo katika hatua za mwisho za kuanza ujenzi wa Barabara ya Loliondo- Mto wa Mbu yenye urefu wa KM 218 itakayojegwa kwa kiwango cha lami ili kurahishisha usafiri na usafirishaji wa mizigo kwa wananchi wa mikoa ya Mara, Manyara, Arusha na Mwanza.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa katika kijiji cha Sale, wilayani Ngorongoro mara baada ya kukagua barabara hiyo ambayo ni kiungo kati ya mikoa hiyo minne na nchi jirani ya Kenya.

“Tumeshatangaza Zabuni kwa ajili ya ujenzi wa barabara hii, mapema mwakani zitafunguliwa ili kumpata mkandarasi ambae atajenga barabara hii kwa kiwango kilichobora”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Aidha,Waziri huyo amefafanua kuwa ujenzi wa barabara hiyo utatekelezwa kwa awamu mbalimbali ambapo awamu ya kwanza itahusisha ujenzi wa barabara ya kutoka katika kijiji cha Waso – Sale yenye urefu wa KM 49.

Ameongeza kuwa barabara hiyo ikikamilika itaungana na ile ya Makutano-Nata yenye urefu wa KM 50 iliyopo Wilaya ya Butiama, mkoani Mara na itasaidia kupunguza kero ya usafiri na kufungua mikoa hiyo kibiashara kwa wakazi wa maeneo hayo.

Amewataka wananchi wa maeneo hayo kutoa ushirikiano kwa mkandarasi atakayepata zabuni hiyo ili kumrahisishia kumaliza mradi huo kwa wakati na viwango vinavyokubalika.

Kwa upande wao wakazi wa Kijiji cha Sale wamemuelezea Waziri Changamoto wanazozipata katika barabara hiyo na kuiomba Serikali kuharakisha mradi huo kwani utasaidia kuongeza pato katika Sekta ya Utalii na kurahisisha huduma za kijamii.

“Barabara hii ni ya muhimu sana kwani tumeteseka kwa muda mrefu, huduma za kijamii kama kumsafirisha kutoka nyumbani mpaka kwenye kituo cha afya ilikuwa ikituchukua muda mrefu kutokna na ubovu wa miundombinu”, amesema Bw. Elias Badiani.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

MHE. DKT. POSSI AITAKA JAMII KUHESHIMU HAKI ZA WATU WENYE ULEMAVU

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mhe. Selemani Mzee (wa kwanza kulia) wakati wa ziara yake katika shule ya Masasi yenye kuhudumia wenye ulemavu Mkoani Mtwara.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi (wa kwanza kushoto) akiwa katika ziara ya kuangalia maeneo ya shule ya Masasi inayohudumia wanafunzi wa mahitaji maalum wakati wa ziara yake mkoani Mtwara.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akikagua moja ya bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalum la Shule ya Masasi Mkoani Mtwara
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akionesha namna ya kutumia Kurunzi ya mwanga wa jua kwa baadhi ya wazee wenye ukoma wanaoishi katika Kambi ya Mkaseka Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara na kuwapatia wazee hao kurunzi 20 kwa kila nyumba.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe.Halima Dendego akimweleza Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi historia fupi ya mkoa huo wakati wa ziara yake mkoani hapo.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi (wa sita kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara mara bada ya kumaliza ziara yake mkoani hapo.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari katika ziara yake alipotembelea Shule na Makazi ya wazee Wilayani Masasi mkoa wa Mtwara.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).

……………..

Na. Mwandishi Wetu

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu, Mhe. Dkt. Abdallah Possi ameitaka jamii kuzingatia haki na usawa kwa watu wenye ulemavu nakuondokana na imani potofu za kuona watu wenye ulemavu hawana uwezo wa kufanya shughuli za maendeleo.

Mhe. Possi ameyasema hayo kwa nyakati tofauti alipotembelea Vituo na Shule zinazohudumia watu wenye mahitaji maalum vya Nandanga, Rasi Bula, Shule ya msingi Nyangao mkoani Lindi pamoja na makazi ya wenye ulemavu na Ukoma ya Mkaseka, Chuo cha wenye Ulemavu cha Mtapika, shule ya Lulindi na Masasi mkoani Mtwara.

Katika ziara hiyo Mhe.Possi alisisitiza jamii zibadili mitazamo hasi juu ya masuala ya haki na usawa kwa watu wenye ulemavu kwa kuwashirikisha katika shughuli zote na kuwapa vipaumbele vya fursa sawa.

“Ninasisitiza jamii ibadili mitazamo dhaifu juu ya haki na usawa wa kuwashirikisha watu wenye ulemavu kwani wana uwezo wa uzalishaji endapo tutawapa fursa sawa kama ilivyokuwa kwa wakina mama walipoachwa nyuma muda mrefu ila jamii imeona fursa ndani yao, iwe hivyo hivyo kwa watu wenye ulemavu” alisema.

Aidha Waziri Possi ameweka mkazo juu ya kuwahusisha na kutokuwaona kuwa ni kundi la kuachwa nyuma na kama tegemezi.

“sheria zipo wazi kabisa zinazotuelekeza juu ya haki na usawa kwa watu wenye ulemavu kwa mujibu wa matakwa ya Sheria ya watu wenye Ulemavu namba 9 ya mwaka 2010 inayoeleza haki za watu wenye Ulemavu kuwahudumia kwa haki na usawa na kuboresha maeneo muhimu ikiwemo fursa za kielimu, ajira, kiuchumi na kijamii,” alieleza.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Joseph Mkirikiti alikiri kuyapokea yote aliyoeleza Mhe.Waziri katika ziara yake na kuipongeza Serikali kwa juhudi za kuisaidia jamii bila kujali hali zao na tofauti zao.

“Ninaipongeza Serikali ya Awamu ya Tano inayowajali wanyonge na kujali haki zao pamoja na mhe. Waziri kwa kuona umuhimu wa kututembelea wana Ruangwa na tunaahidi kukuweka katika kumbukumbu zetu maana umewagusa wakazi wa Mtwara hususani wazee na watu wenye ulemavu.”Alisisitiza Mkuu wa Wilaya hiyo.

Nae Afisa Mfawidhi kituo cha Kulelea wazee wenye ukoma cha Mkaseka Bw. Cleophace Nguli aliiomba Serikali kuendelea kuwakumbuka watu wenye ulemavu ikiwa ni watu waliosahaurika na kuendelea kupongeza hatua zilizopo kwa sasa.

Tume ya Mipango yaridhishwa na Mpango wa kuboresha Kiwanja cha Ndege Mtwara kwa kiwango cha Kimataifa

$
0
0

Kaimu Katibu Mtendaji kutoka Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (aliyevaa suti) akiwa pamoja na maofisa wa mamlaka ya viwanja vya ndege na wa Tume ya Mipango wakielekea kukagua maeneo mbalimbali ya kiwanja hicho.
Meneja wa Teknolojia na Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini , Bw. Abdulatif Min-Hajj (aliyekaa kulia kwa Kaimu Katibu Mtendaji) akielezea mpango wa kuboresha kiwanja cha ndege Mtwara mbele ya timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Tume ya Mipango.
Kaimu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango Bibi Florence Mwanri akitoa ushauri kwa maofisa wa mamlaka ya viwanja vya ndege juu ya umuhimu wa kuwa na hati miliki ya eneo hilo.
Mchumi Mkuu kutoka Tume ya Mipango, Bibi Salome Kingdom akiongea jambo na Bw. Daniel Werema kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, wengine ni Mhandisi Omary Othman (aliyevaa t-shirt) na Bw. Hekima Chengula kutoka Tume ya Mipango.
Sehemu ya barabara inayotumika katika kutua na kuruka ndege (Runway) ya Kiwanja cha Mtwara. Urefu wa barabara hiyo ni mita 2258 na ina upana wa mita 30.

……………..

Na Adili Mhina, Mtwara.

Katika kutekeleza Malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, Mamlaka ya viwanja vya Ndege imedhamiria kufanya maboresho katika Kiwanja cha Ndege Mtwara kwa kiwango cha Kimataifa ili kuendelea kuimarisha huduma za usafiri wa anga nchini.

Mapango huo umeelezwa hivi karibuni na Meneja wa Teknolojia na Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini , Bw. Abdulatif Min-Hajj wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya Kiwanja hicho kwa Kaimu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri alipofanya ziara katika kiwanja hicho ikiwa ni mfululizo wa ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo unaofanywa na timu kutoka Tume ya Mipango.

Meneja huyo alieleza kuwa mradi huo amabao ni mpango wa muda mrefu unaolenga katika kufanya upanuzi wa kiwanja pamoja na ujenzi wa jengo la kisasa kwa ajili ya abiria upo katika hatua za awali ambapo mkandarasi mshauri tayari amewasilisha rasimu ya taarifa ya mpango mkuu (maste plan).

“Katika mradi huu kiwanja cha Mtwara kitapanualiwa na kufikia code 4E ambapo kitakuwa na uwezo wa kuhudumia ndege kama A340-200. Katika ujenzi wa jengo la abiria, kwa awamu ya kwanza tutajenga jengo lenye mita za mraba 6570 ili kufikia mahitaji ya mwaka 2023 na awamu ya pili tunatarajia kuwa na jengo la mita za mraba 10,880 ili kukidhi mahitaji ya abiria kwa mwaka 2033”, alieleza Meneja huyo.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Florence Mwanri alieleza kuwa Dira ya Taifa ya Maendeleo inasisitiza kuwa na vianzio mbalimbali vya uchumi na kuwepo kwa miundombinu ya kutosha kuiwezesha Tanzania kuingia katika nchi za kipato cha kati. Hivyo, mradi huo utasaidia kuimarisha uchumi wa nchi sambamba na kuongeza ufanisi katika usafiri wa anga.

Aliongeza kuwa upanuzi wa kiwanja hicho utakapokamilika sio kwamba tu utasaidia usafiri wa anga peke yake bali kwa upande mwingine utafungua fursa mbalimbali za uwekezaji kwa sekta binafsi na kusaidia kuongeza uchumi kwa watanzania.

“Nimeelezwa kuwa mradi huo ukikamilika kutajitokeza fursa za uwekezaji kama kujenga mahoteli makubwa ya hadhi ya nyota tano, kujenga eneo la biashara, ujenzi wa maduka na migahawa ya kisasa, ujenzi wa visima vya mafuta ya ndege, kutakuwa na jengo kubwa la kuhifadhia mizigo, na majengo ya kutengenezea ndege. Hizi zote ni fursa zitakazosaidia kuinua uchumi wa wananchi wetu,” alieleza.

Hata hivyo Mwanri alishauri kuwa pamoja na kuwa na malengo mazuri ya muda mrefu mamlaka ya hiyo inapaswa kuendelea kutekeleza malengo yake ya muda mfupi katika kutatua changamoto za miundombinu ya barabara za ndege kiwanjani hapo ili kuendelea kuimarisha huduma za usafiri huku akishauri mamlaka hiyo kufanya jitihada za haraka kupata hati miliki pamoja na kufikiria kujenga uzio katika eneo la kiwanja hicho.

“Mnapaswa kuendelea kutekeleza mipango ya muda mfupi wakati mnasubiri mradi mkubwa utekelezwe. Najua katika bejeti yenu ya sasa mtaendelea kukarabati miundombinu ili ndege ziendelee kutua na kuondoka kwa usalama. Vile vile angalieni namna ya kupata hati miliki na kujenga uzio wa eneo lote kwa ajili ya usalama na kuwadhibiti watu wenye tabia ya kuvamia maeneo”, Alieleza Mwanri.

NASSARI ASIFU UTENDAJI WA SERIKALI YA AWAMU YA TANO

$
0
0
 MBUNGE wa jimbo la Arumeru Mashariki, Mheshimiwa Joshua Nassari amepongeza na kusifu  jitihada kubwa zianazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuwaletea maendeleo wananchi wa maeneo mbalimbali nchini wakiwemo wa jimbo lake.
Kufuatia hatua hiyo Mheshimiwa Nassari ameahidi kushirikiana bega kwa bega na Serikali ili kuhakikisha maendeleo yanakuwa endelevu.
Mheshimiwa Nassari ametoa pongezi hizo leo (Jumapili, Desemba 18, 2016) mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye alikuwa katika majumuisho ya ziara yake ya siku 10 ya kikazi mkoani Arusha.
Mbunge huyo ambaye alilazimika kuja nchini kwa dharura akitokea masomoni nchini Uingereza ili kumuwahi Waziri Mkuu, amesema ameridhishwa na hatua za utatuzi wa migogoro ya ardhi zinazochukuliwa na Serikali.
Amesema ziara ya Waziri Mkuu mkoani Arusha, imesaidia kutibu majeraha na makovu makubwa yalitokana na matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana.”Kama kuna kiongozi ambaye hawezi kuunga mkono jitihada hizi za kuwaletea maendeleo watu wetu, atakuwa na matatizo,” amesema.
Ameongeza kuwa kitendo cha Waziri Mkuu kuweka mikakati ya kushughulikia migogoro ya ardhi iliyodumu kwa miaka mingi ni ushahidi tosha kwamba Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuwasaidia wananchi wa kawaida.
Mheshimiwa Nassari amesema mwaka 1952 wazee wa Meru walimtuma mtu kwenda Uingereza kuomba uhuru wa wananchi wa Arumeru ili waweze kujitawala na kumiliki ardhi yao kutoka kwa wakoloni.
Amesema wazee hao walichukua uamuzi huo baada ya kuchoshwa na vitendo vya unyanyasaji vilivyokuwa vinafanywa na wakoloni dhidi yao. Lakini miaka 55 imepita tangu nchi ipate Uhuru bado migogoro na mateso hayo yapo.
Hivyo amempongeza Waziri Mkuu kwa kuamua kuitafutia ufumbuzi changamoto ya ardhi wilayani Arumeru jambo ambalo litawawezesha wananchi kupata ardhi kwa ajili ya kuendesha shughuli zao za kimaendeleo zikiwemo za  kilimo na ufugaji.
Waziri Mkuu jana (Jumamosi, Desemba 17, 2016) alifanya ziara katika wilaya ya Arumeru ambapo alisema Serikali itawanyang’anya ardhi wamiliki wote wa mashamba makubwa wilayani Arumeru ambao hawajayaendeleza kwa sababu wamekiuka mkataba wa umiliki.
Alisema Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa William Lukuvi atakuja mkoani Arusha kwa ajili ya kufanya mapitio ya mashamba yote makubwa ambayo hayajaendelezwa na kuyarudishwa Serikalini.
 “Tufanya mapitio ya kila shamba ili kujua linamilikiwa na nani na alipewa lini na tangu alipokabidhiwa amefanya nini. Shamba lisiloendelezwa litarudisha kwa wananchi. Kama mtu ameshindwa kupata mtaji kwa muda wa miaka 10 atapata leo,” amesema.
Amesema Serikali haiko tayari kuona wananchi wakinyanyaswa kwa kukosa ardhi ya kilimo kwa sababu ya watu wachache kumiliki maeneo makubwa bila ya kuyaendeleza..
“Ninataarifa kwamba hapa Arumeru kuna baadhi ya wawekezaji wanamiliki mashamba makubwa na hawajayaendeleza. Wengine wanakodisha kwa wananchi ili kujipatia fedha kinyume na mikataba yao ya umiliki. Hatutawavumilia,” alisema.
Alisema wilaya ya Arumeru inaongoza kwa migogoro ya ardhi na maeneo mengi yametwaliwa na mtu mmoja mmoja na baadhi yao wamekuwa wakilitumia vibaya Jeshi la Polisi kwa kuwanyanyasa wananchi wanaokatiza au kulima kwenye maeneo hayo, ambapo aliwataka polisi kuacha tabia hiyo mara moja.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, DESEMBA 18, 2016.  
                                        

WAKULIMA WATAKIWA KUTUMIA PEMBEJEO ASILIA KUKUZA KILIMO HAI

$
0
0
 
Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO
Wataalamu wa kilimo wamewataka wakulima mkoani Morogoro kutumia pembejeo za asili ili kuepuka kemikali zenye sumu zinazotokana na pembejeo za viwandani ambazo zinaathiri usalama wa chakula.

Rai hiyo ilitolewa hivi karibuni mjini Morogoro katika mafunzo ya siku moja yaliyoandaliwa na Shirika la PELUM Tanzania wakishirikiana na Shirika la TOAM kupitia Mradi wa Masuala ya Kilimo Unaozingatia Utunzaji wa Mazingira.

Akifungua mafunzo hayo, Mratibu wa Shirika linalohamasisha utunzaji wa bionuwai ya kilimo Tanzania (TABIO), Abdallah Ramadhani amesema kuwa  lengo la mafunzo hayo ni kuweza kutoa elimu juu ya umuhimu na matumizi sahihi ya pembejeo za asili kwa ajili ya kukuza na kuendeleza kilimo hai nchini hasa kwa kuangalia njia zinazotumika kutengeza mbolea na madawa ya asili ili kuhakikisha wakulima nchini wanaachana na matumizi ya viuatilifu vya viwandani ambavyo vina kemikali.

“Viuatilifu vyenye kemikali za kuua wadudu waharibifu zenye thamani ya Dola za Kimarekani Bilioni 30 humwagwa kwa makusudi katika mazingira ya dunia kila mwaka, sehemu kubwa ya viuatilifu hivyo ni vile vyenye sumu kali ambazo zina athari za moja kwa moja kwa afya ya binadamu, wanyama pori pamoja na vyanzo vya chakula ndio maana tunawashauri wakulima kuacha kutumia pembejeo za aina hiyo”,alisema Ramadhani.

Akibainisha baadhi ya madhara yatokanayo na viutalifu hivyo toka viwandani, Ramadhani amesema kuwa pamoja na kuathiri afya na usalama wa viumbe hai, viuatilifu hivyo vinatumiwa bila ya kuwa na vifaa kinga pia huchafua mzingira na hata kuua viumbe wengine wasiokusudiwa.

Ameongeza kuwa, baadhi ya viuatilifu hivyo vina athari za muda mrefu kwa binadamu ikiwemo matatizo ya uzazi, dosari za kuzaliwa, kuvuruga mfumo wa homoni na kuharibu mfumo wa kinga.

Kwa upande wake Meneja wa Viwango na Ubora toka Kampuni ya Guavay inayotengeza mbolea aina ya HAKIKA Organic Fertilizer, Latifa Mafumbi amewasihi wakulima kuendelea kutumia pembejeo za asili kwa kuwa hazina madhara kuanzia kwa mtengenezaji, ardhi, mimea, viumbe, wadudu wanaorutubisha ardhi pamoja na mlaji.

Amesema kuwa kama mtaalamu, kwa sasa anaendelea kufanya uchunguzi kwenye zao la nyanya ili kubaini tofauti iliyopo kwenye zao hilo kama atatumia mboleaya kiwandani yenye kemikali na mbolea iliyotengenezwa kiasili kwani tafiti nyingi za awali zinaonyesha kuwa matumizi ya mbolea za asili hutoa mazao bora.

Naye mkulima mshiriki, Pius Paulini amebainisha kuwa kilimo hai kinachotokana na matumizi ya pembejeo za asili (mbolea na madawa) kimekuwa kikiongeza rutuba kwenye ardhi hivyo kuwasaidia wakulima kulima kwenye eneo moja kwa kipindi kirefu pasipo kuhamahama.

Amefafanua kuwa mimea hustahimili mabadiliko ya tabianchi tofauti na viuatilifu vya viwandani vilivyojaa kemikali yenye sumu na kuchangia kwa asilimia kubwa kufifisha ubora wa ardhi na hata kuua wadudu ambao wanasaidia kurutubisha mimea shambani.

PELUM ni shirika linalohamasisha utunzaji na matumizi bora ya ardhi kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi ili kuepuka athari kwenye kilimo na shirika la TOAM ni shirika linalohamasisha Kilimo Hai Tanzania.

Global Education Link yaanzisha dawati maalum la kuwasaidia wahitimu wa vyuo

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel, akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, tawi la Mbeya.
Ofisa anayehusika na wanafunzi wa nje kutoka Chuo Kikuu Cha Lovely, (LPU), Love Kumar akizungumza na wanafunzi wa Chuo kikuu cha Mzumbe, tawi la Mbeya.
 

Kampuni ya Global Education Link (GEL) ambayo ni wakala wa vyuo vya nje ya nchi, imetangaza kuanzisha dawati maalum kwa ajili ya kuwasaidia wahitimu wa vyuo na vyuo vikuu nchini kuanzia tarehe 15, Januari, 2017. 

Hayo yalisemwa leo (tarehe 17 Desemba, 2016) na Mkurugenzi Mkuu wa GEL, Abdulmalik Mollel alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe tawi la Mbeya. “Azma yangu ni kuona dawati hilo linaleta majibu juu ya wahitimu wanaomaliza vyuo lakini wanakosa ajira au wanasemwa kwamba hawaajiriki,” alisema Mollel. 

Kwa mujibu wa Mollel, mojawapo ya majukumu ya dawati yatakuwa ni kuangalia namna ya kuwaingiza wahitimu hao katika mfumo wa mafunzo maalum ya vitendo kwenye makampuni yaliyoko ndani au nje ya nchi kwa muda mfupi kama vile miezi mitatu, minne au sita ili kuwafanya waweze kuajirika au kujiajiri wenyewe. 

“Tayari tumeshaanzisha mawasiliano na baadhi ya makampuni kwa ajili ya kuanzisha mpango huo” aliongeza Mollel na kufafanua kuwa kwa wanafunzi wanaosoma nje ya nchi, suala la mafunzo kwa vitendo kwao sio tatizo, bali mafunzo hayo yanawahusu zaidi wahitimu wa vyuo vya ndani, ambao wengi wao wanaonekana kutopikwa vizuri kwa ajili ya kuingia kwenye soko la ajira. 

Kwa mujibu wa Mollel wahitimu wanaotaka kuingia katika mpango huo wa mafunzo wanaweza kujiandikisha moja kwa moja kupitia website ya kampuni hiyo (www.gel.co.tz). Fomu zitaanza kupatikana rasmi kuanzia mwishoni mwa mwezi huu. Aidha wanaweza kutembelea katika matawi ya kampuni hiyo yaliyoko Arusha, Mwanza, Mbeya, Zanzibar na makao makuu yake yaliyoko ndani ya Uwanja wa Sabasaba, Dar es Salaam.

Kampuni JUNACO yazindua kifaa cha kisasa cha kuzima moto Dar.

$
0
0
1
George Michael Mtaalam kutoka kampuni inayotengeneza vifaa vya kuzima moto FirePro ya Cyprus akionyesha moja ya kifaa cha kuzima moto kinachoweza kufungwa katika mitambo mbalimbali chenye uwezo wa kuzima moto katika hatua za awali kabisa kabla ya kuwa mkubwa wakati alipokuwa akielezea ubora wa vifaa hivyo katika kupambana na majanga ya moto kwenye uzinduzi ulifanyika Bwalo la Polisi Oysterbay jijini Dar es salaam mwishono mwa wiki.
2
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kushoto), akimsikiliza George Michael Mtaalam kutoka kampuni inayotengeneza vifaa vya kuzima moto FirePro ya Cyprus wakati alipokuwa akitoa maelezo ya jinsi vifaa hivyo vinavyoweza kuzima moto katika mitambo wakati wa uzinduzi uliofanyika kwenye Bwalo la Polisi Oysterbay jijini Dar es salaam, wa pili kutoka kushoto ni Justin Lambert Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Junaco Group Campanies na wa tatu ni Fikili S. Salla Kamishna wa Divisheni ya Usalama dhidi ya moto Jeshi la Zimamoto.
3
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kushoto), akimsikiliza George Michael Mtaalam kutoka kampuni inayotengeneza vifaa vya kuzima moto FirePro ya Cyprus wakati alipokuwa akitoa maelezo ya jinsi vifaa hivyo vinavyoweza kuzima moto katika mitambo wakati wa uzinduzi uliofanyika kwenye Bwalo la Polisi Oysterbay jijini Dar es salaam, wa pili kutoka kushoto ni Justin Lambert Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Junaco Group Campanies
4
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kushoto), akimsikiliza George Michael Mtaalam kutoka kampuni inayotengeneza vifaa vya kuzima moto FirePro ya Cyprus wakati alipokuwa akitoa maelezo ya jinsi vifaa hivyo vinavyoweza kuzima moto katika mitambo wakati wa uzinduzi uliofanyika kwenye Bwalo la Polisi Oysterbay jijini Dar es salaam , wa pili kutoka kushoto ni Justin Lambert Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Junaco Group
5
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya (kushoto), akimpongeza George Michael Mtaalam kutoka kampuni inayotengeneza vifaa vya kuzima moto FirePro ya Cyprus mara baada ya kumaliza kutoa maelezo yake mbele ya wageni waalikwa wakati wa uzinduzi uliofanyika kwenye Bwalo la Polisi Oysterbay jijini Dar es salaam, katikati ni Justin Lambert Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Junaco Group Campanies
6
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Biashara wa Kampuni ya JUNACO Group Of Companies Limited Bw. Anic Kashashaakizungimza katika uzinduzi huo.
7
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa kifaa hicho cha Firepro mwishoni mwa wiki.
8
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya , Justin Lambert Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Junaco Group Campanies na George Michael Mtaalam kutoka kampuni inayotengeneza vifaa vya kuzima moto FirePro ya Cyprus wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo
9
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya , Justin Lambert Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Junaco Group Campanies na George Michael Mtaalam kutoka kampuni inayotengeneza vifaa vya kuzima moto FirePro ya Cyprus wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo

................................................................................

Kampuni ya JUNACO Group of Companies mwishoni mwa wiki ilizindua kifaa cha kisasa kinachotumika kuzima moto kwenye makazi ya watu na mitambo kinachofahamika kama ‘FirePro’ ikiwa ni uvumbuzi unaolenga kukabiliana na janga hilo hatari.

Akizungumza wakati wa hafla maalum ya uzinduzi wa kifaa hicho iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na kuhuduriwa pia na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambao ya Ndani Balozi Hassani Simba Yahya, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo ya nchini hapa nchini , Bw Justine Lambert alisema matumizi ya kifaa hicho miongoni mwa watanzania yatasaidia kutaondoa athari za uharibifu wa mali na vifo vitokanavyo na majanga ya moto kwenye makazi ya watu.

“Uvumbuzi na ujio wa kifaa hiki ni ishara kwamba athari zitokazo na majanga ya moto ambayo yamekuwa yakiripotiwa kupoteza maisha ya watanzania na kusababisha umasikini kutoka na uharibifu wa mali sasa linakwenda kwisha,’’ alisema Bw Lambert huku akiongeza kuwa wao kama sekta binafsi wana wajibu wa kuisaidia serikali kukabiliana na changamoto zinazowakabili wananchi wake.

Alisema mbali na suala la kuhakikisha usalama wa watanzania, uwepo wa kifaa hicho pia utaongeza ajira kwa wadau wote watakaohusika kwa namna moja au nyingine katika mauzo ya kifaa hicho hapa nchini.“ Ndani ya miaka minne ijayo Junaco Group of Companies tunarajia kutengeneza ajira zipatazo 780 zitakazohusisha wauzaji, wasambazaji na wataalamu wa kufunga kifaa hiki kote nchini,’’ alisema.

Kwa upande wake balozi Simba ambae alimuwakilisha waziri wa wizara hiyo Bw Mwigulu Nchemba alisema serikali imekuwa ikiridhishwa sana hasa pale inapopokea taarifa za uwepo wa teknolojia mpya zinazolenga kutatua changamoto zinazowakibili wananchi wake kuisalama kama hiyo ya uzinduzi wa kifaa cha ‘FirePro’ huku akitoa wito kwa kampuni hiyo kutumia fursa za kiuwekezaji kuanzisha kiwanda cha kutengeneza vifaa kama hivyo hapa nchini.

“Ujio wa kifaa hiki hapa nchini ni wazi kuwa utakuwa na matokeo chanya kijamii na kiuchumi kwasababu mbali na kulinda usalama wa wananchi na mali zao lakini pia utazalisha ajira zaidi ya 800... hongereni sana naimani mtafikiria pia kuanzisha kiwanda kitakachowezesha uzalishaji wa vifaa hivi hapa nchini,’’ alisema.

Kwa mujibu wa Meneja Maendeleo wa Mradi huo Bw, George Michael, teknolijia iliyotumika kutengeza kifaa hicho ni bora zaidi kwa nchi zinazoendelea na ni rafiki pia kwa mazingira.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMATATU DESEMBA 19, 2016

Zantel wafanya kazi za kijamii kwa kusafisha mazingira ya Forodhani Zanzibar

$
0
0
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zantel Tanzania, Benoit Janin (wa tatu kulia), akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo wakifanya usafi eneo la Forodhani mjini Zanzibar mwishoni mwa wiki ikiwa ni sehemu ya juhudi za Zantel  kujitolea kufanya kazi za jamii.. Mara baada ya kufanya usafi, Zantel ilikabidhi vifaa mbalimbali vya kufanyia usafi vyenye thamani ya zaidi ya shs milioni 3 kwa uongozi wa serikali ya mji huo  kama sehemu ya kurudisha sehemu ya mapato yao  kwa jamii wanayofanya nayo biashara.
 Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohamed Khamis (kulia) akikabidhi vifaa mbalimbali vya kufanyia usafi  kwa mwakilishi wa manispaa,  Khamis Msabah vilivyotolewa na Zantel ikiwa ni sehemu ya juhudi zao kufanya kazi za kijamii na kurudisha sehemu ya faida waipatayo kwa jamii. Awali ofisa mtendaji wa kampuni hiyo akiwa na baadhi ya wafanyakazi walifanya usafi katika eneo la Forodhani,  visiwani humo.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zantel Tanzania, Benoit Janin (kulia), akitoa zawadi ya vocha kwa wateja waliokuwa wakihudumiwa katika kituo cha huduma kwa wateja cha Vuga mjini Zanzibar ikiwa ni moja ya kuonyesha shukrani kwa wateja wao. Ofisa huyo pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo walikuwa visiwani humo mwishoni mwa wiki ambapo walitembelea wateja na wakala wao na baadae kufanya shughuli za kusafisha mazingira eneo la Forodhani na pia kukabidhi vifaa vya kufanyia usafi kwa uongozi wa manispaa ya mji humo ikiwa ni mwendelezo wa shughuli a kuhudumia kijamii. Kulia kwake ni Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohamed Khamis Baucha. 
Baadhi ya wafanyakazi wa Zantel wakishiriki zoezi la kufanya usafi eneo la Forodhani mjini Zanzibar ikiwa ni sehemu ya juhudi za kampuni hiyo kujitolea kufanya kazi za kijamii.

Barclays yafungua tawi jipla la kisasa katika jengo la Alpha House jijini Dar es Salaam

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Tanzania, Abdi Mohamed (katikati), Afisa Usambazaji wa Barclays Africa Group Limited, Vimal Kumar (kulia) na Mkurugenzi wa Biashara Reja reja wa benki hiyo nchini, Kumaran Pather wakikata utepe kuashiria  uzinduzi rasmi wa tawi jipya la kisasa la benki hiyo lililopo katika jengo la Alpha House kando ya Barabara ya New Bagamoyo, jijini Dar es Salaam.
 Afisa Usambazaji wa Barclays Africa Group Limited, Vimal Kumar (katikati), akifungua pazia kuashiria uzinduzi wa tawi hilo. Pamoja naye ni Mkuu wa Mtandao wa Matawi wa Benki ya Barclays Tanzania, John Beja.
 Mkuu wa Mtandao wa Matawi wa Benki ya Barclays Tanzania, John Beja (mbele), akionyesha sehemu mbalimbali za tawi jipya la kisasa la benki hiyo lililopo katika jengo la Alpha House, kando ya Barabara ya New Bagamoyo wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa tawi hilo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wanaoangalia kutoka kushoto ni, Afisa Usambazaji wa Barclays Africa Group Limited, Vimal Kumar, Mkurugenzi Mtendaji wa Barclays Tanzania, Abdi Mohamed, Meneja wa tawi hilo, Nicholaus Mukanya, Mkurugenzi wa Biashara Reja reja wa benki hiyo nchini, Kumaran Pather na Mkuu wa kitengo cha IT, Dakshit Pandya.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Tanzania, Abdi Mohamed (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi rasmi wa tawi jipya la kisasa la benki hiyo lililopo katika jengo la Alpha House kando ya Barabara ya New Bagamoyo, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto kwake ni  Afisa Usambazaji wa Barclays Africa Group Limited, Vimal Kumar na Mkurugenzi wa Biashara Reja reja wa benki hiyo nchini, Kumaran Pather.

 Baadhi ya maofisa wa Barclays pamoja na wageni wengine wakipiga picha ya kumbukumbu katika hafla hiyo.
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki ya  Barclays Tanzania, Aron Luhanga (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Biashara Reja reja wa benki hiyo nchini, Kumaran Pather (kushoto), wakiwa na baadhi ya wateja na wageni wengine waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa tawi hilo.

BANDARI TANGA YAIBUKA WASHINDI WA JUMLA MICHEZO YA TANO USIMAMIZI WA BANDARI TANZANIA

$
0
0
Kapteni wa timu ya Bandari Tanga, Abdalla Abdulla, akipokea kombe la Ubingwa wa jumla na Kaimu Mkurugenzi Usimamizi wa Bandari Tanzania, Mussa Msabimana mara baada ya kumalizika michezo hiyo iliyoshirikisha timu za Tanga, Dar Makao Makuu, Mtwara na Bandari za Maziwa.


Tangakumekuchablog
Tanga, MICHEZO ya tano ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (INTERPORTS GAMES) yamemalizika kwa timu ya Bandari ya Tanga kuibuka Mabingwa wa jumla. 

Timu ya Bandari ya Tanga imeibuka kwa kunyakua vikombe 7 ikifuatiwa na Bandari Makao Makuu Dar es Salaam kwa kujinyakualia vikombe 7 ambapo Bandari Mtwara na Bandari za Maziwa kila mmoja kujinyakulia kikombe kimoja kimoja. Akikabidhi vikombe na zawadi mbalimbali kwa washindi Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, Mussa Msabimana ,aliwapongeza washiriki hao kwa kuonyesha umahiri katika michezo mbalimbali. 

Alisema mbali ya umri wao kwenda juu lakini walikuwa wakionekana kama vijana ambao wanaweza kucheza timu yoyote inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara. “Nimefarijika kuwaoma wafanyakazi wenzangu umri tofauti mukicheza mpira na kushindwa kutofautisha kijana na mzee, munakimbia uwanjani kama Messi na Ronaldo” alisema Msabimana
Aliwataka wanamichezo hao ambao ni watumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania kuwa wamoja na kuwa na mshikamano ili kuweza kuyafikia malengo waliojiwekea.

Mshindi wa bao kutoka Bandari Makao Makuu Dar es Salaam, Mwinyi Sultan, akikabidhiwa kombe na Kaimu Mkurugenzi wa Mmlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, Mussa Msabimana baada ya kuibuka msindi wa mchezo huo wakati wa michezo iliyofanyika Tanga kwa siku 4 viwanja mbalimbali Mkoani humo.
Wachezaji wa timu ya Bandari Tanga michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, Netboll, kurusha Tufe, kuvuta kamba na riadha wakishangilia ushindi wa jumla mara baada ya kukabidhiwa kombe lao na Kaimu Mkurugenzi Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mussa Msabimana. Bandari Tanga imeibuka mshindi wa jumla na kunyakua vikombe 6.





Wachezaji wa timu ya Bandari Makao Makuu Dar es Salaam wakishangilia ushindi mara baada ya kukabidhiwa vikombe vyao kwa michezo mbalimbali, Bandari Makao Makuu walinyakua vikombe 7. Raha ya Ushindi Bandari Mkao Makuu.Dar es Salaam,

NYUMBA, GARI NA PIKIPIKI VINAUZWA BEI NI NAFUU SANA CHANGAMKIA FURSA HIYO

$
0
0

Mwonekano wa nyumba hiyo.
Gari linalouzwa lipo katika hali nzuri.
Pikipiki inayouzwa ipo katika hali nzuri.

NYUMBA INAUZWA IPO WILAYA YA TEMEKE KATA YA CHAMAZI KARIBU NA UWANJA WA MPIRA WA AZAM NI SEIF CONTAINED NA INA MASTER ROOM NA CHUMBA KIMOJA CHA KULALA, SEBURE, JIKO NA CHOO NA BAFU LA NDANI, BEI NI SHILINGI MILIONI 19, MBALI YA NYUMBA HIYO PIA KUNA GARI PAMOJA NA PIKIPIKI VINAUZWA KWA MAWASILIANO PIGA SIMU NAMBA 0687-347676 AU O759-239338.

Tanzania ya Viwanda; NSSF, PPF waanza kutekeleza ujenzi wa kiwanda cha sukari.

$
0
0
 Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu,  Jenister Mhagama (kushoto) na Waziri wa Fedha na Mpango, Dr. Phillip Mpango (katikati) wakijadili masuala pamoja na wakurugenzi wakuu wa mifuko hifadhi ya jamii ya NSSF na PPF,  Profesa Godius Kahyarara na Bw.William Erio pamoja na Mbunge Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki Omari Mgumba (kulia) kuhusiana na mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha sukari kitakachojengwa katika eneo la Mkulazi, mkoani Morogoro ikiwa ni  uwekezaji wa pamoja  wa mifuko hifadhi ya jamii ya NSSF na PPF wakati viongozi hao walipotembelea mradi huo mwishoni mwa wiki.
 Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu,  Jenister Mhagama na Waziri wa Fedha na Mpango, Dr. Phillip Mpango wakikagua ujenzi wa barabara   inayoelekea sehemu ya mradi ambayo inafanyiwa ukarabati mkubwa na kampuni ya ujenzi ya SUMA JKT.
 Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu,  Jenister Mhagama na Waziri wa Fedha na Mpango, Dr. Phillip Mpango wakikagua ujenzi wa barabara   inayoelekea sehemu ya mradi ambayo inafanyiwa ukarabati mkubwa na kampuni ya ujenzi ya SUMA JKT.
 Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu,  Jenister Mhagama (wa tatu kushoto) na Waziri wa Fedha na Mpango, Dr. Phillip Mpango (katikati) wakifuatilia maelezo kutoka kwa muwakilishi wa kampuni ya Mkulazi Holding inayotekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha sukari kitakachojengwa katika eneo la Mkulazi, mkoani Morogoro ikiwa ni  uwezeshaji wa pamoja  wa mifuko hifadhi ya jamii ya NSSF na PPF wakati viongozi hao walipotembelea mradi huo mwishoni mwa wiki. 
 Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu,  Jenister Mhagama (wa tatu kushoto) na Waziri wa Fedha na Mpango, Dr. Phillip Mpango (katikati) wakifuatilia maelezo kutoka kwa muwakilishi wa kampuni ya Mkulazi Holding inayotekeleza mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha sukari kitakachojengwa katika eneo la Mkulazi, mkoani Morogoro ikiwa ni  uwezeshaji wa pamoja  wa mifuko hifadhi ya jamii ya NSSF na PPF wakati viongozi hao walipotembelea mradi huo mwishoni mwa wiki. 
 aziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu,  Jenister Mhagama (kushoto) na Waziri wa Fedha na Mpango, Dr. Phillip Mpango (katikati) wakimsikiliza Mbunge Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki Omari Mgumba (kulia) ambae jimboni kwake ndipo unatekelezwa  mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda hicho.
 Wananchi wa kijiji cha Kidunda, kata ya Mkulazi, wilaya ya Morogoro Vijijini wakikaribisha ugeni huo muhimu. Kukamilika kwa mradi huo kunatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 100,000 huku kipaumbele kikiwekwa zaidi kwa wakazi wanaoishi maeneo jirani na mradi.
 Wananchi wa kijiji cha Kidunda, kata ya Mkulazi, wilaya ya Morogoro Vijijini wakikaribisha ugeni huo muhimu. Kukamilika kwa mradi huo kunatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 100,000 huku kipaumbele kikiwekwa zaidi kwa wakazi wanaoishi maeneo jirani na mradi.
 Wananchi wa kijiji cha Kidunda, kata ya Mkulazi, wilaya ya Morogoro Vijijini wakikaribisha ugeni huo muhimu. Kukamilika kwa mradi huo kunatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 100,000 huku kipaumbele kikiwekwa zaidi kwa wakazi wanaoishi maeneo jirani na mradi.
 Washirika muhimu! Wakurugenzi wakuu wa mifuko hifadhi ya jamii ya NSSF na PPF,  Profesa Godius Kahyarara (kulia) na Bw.William Erio (kushoto) wakisikiliza hotuba ya  Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu,  Jenister Mhagama alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kidunda, kata ya Mkulazi, wilaya ya Morogoro Vijijini mwishoni mwa wiki.
 Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu,  Jenister Mhagama akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kidunda, kata ya Mkulazi, wilaya ya Morogoro Vijijini wakati alipotembelea mradi huo mwishoni mwa wiki ambapo aliwahakikishia wakazo hao kuhusiana na utekelezaji wa mradi huo huku akiwaahidi kuwa mradi utatoa kipaumbele zaidi kwa wakazi wa eneo hilo hususani vijana.

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu,  Jenister Mhagama (wa pili kulia) na Waziri wa Fedha na Mpango, Dr. Phillip Mpango (wa tatu kulia) walipotembelea bwawa la Kidunda lililopo kijiji cha Kidunda, kata ya Mkulazi, wilaya ya Morogoro Vijijini. Mawaziri hao walipokea ombi la kuwezesha ujenzi wa daraja litakalounganisha kijiji hicho na Wilaya ya Kisarawe, Mkoa wa Pwani ili kurahisisha mawasiliano baina ya mikoa hiyo miwili.



 Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu,  Jenister Mhagama (kushoto) na Waziri wa Fedha na Mpango, Dr. Phillip Mpango (kulia) wakijipongeza baada ya kukamilisha ziara hiyo muhimu. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa mfuko hifadhi ya jamii wa NSSF Profesa Godius Kahyarara.
Waziri wa Fedha na Mpango, Dr. Phillip Mpango (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkuu wa mfuko hifadhi ya jamii wa PPF  Bw.William Erio





MIFUKO ya hifadhi ya jamii ya NSSF na PPF imeanza utekelezaji wa awali wa mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha sukari kitakachojengwa katika eneo la Mkulazi, mkoani Morogoro ikiwa ni jitahada ya mifuko hiyo kwa pamoja kuunga mkono muelekeo wa serikali ya awamu ya tano wa kuwekeza kwenye uchumi wa viwanda.

Kukamilika kwa kiwanda hicho kinachotajwa kuwa kitakuwa ni kikubwa zaidi Afrika Mashariki, kutaongeza uzalishaji wa sukari wa hapa nchini ambapo zaidi ya tani laki mbili (200,000) zitakuwa zikizalishwa kwa mwaka sambamba na kutoa ajira zaidi ya 100,000 kwa hatua ya awali.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kidunda, kata ya Mkulazi, wilaya ya Morogoro Vijijini wakati alipotembelea mradi huo mwishoni mwa wiki, Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu,  Jenister Mhagama aliekuwa ameambatana na Waziri wa Fedha na Mpango, Dr. Phillip Mpango, mbali na kuipongeza mifuko hiyo, aliwahakikishia wakazo hao kuhusiana na utekelezaji wa mradi huo huku akiwaahidi kuwa mradi utatoa kipaumbele zaidi kwa wakazi wa eneo hilo hususani vijana.

“Mradi huu una ushawishi mkubwa kutoka kwa Rais John Magufuli kutokana na adhma yake ya kuibadili Tanzania kuwa nchi ya viwanda na umekuja kwa wakati muafaka. Nataka huu uwe wa mfano,’’ alisema Waziri Mhagama ambae pia aliambatana na Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk Stephen Kebwe, Mbunge Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki Omari Mgumba pamoja na wawakilishi wa kampuni ya Mkulazi Holding inayosimamia utekelezaji wa mradi huo pamoja na viongozi wengine wa serikali.
Waziri Mhagama aliwaomba watekelezaji wa mradi huo kuainisha  mapema aina ya rasilimali watu watakaohitajika kwenye mradi ili waanze kuandaliwa mapema kuepuka suala la kuagiza wataalamu kutoka nje ya nchi kuja kufanya kazi ambazo zingeweza kufanywa na wataalamu wa ndani iwapo wangeandaliwa mapema.

Kwa upande wake Waziri Mpango alisema tayari serikali imeshatenga sh bilioni 17 katika mwaka wa fedha 2016/2017 kwa ajili ya kumalizia fidia na mipaka kwa wakazi wanaoishi kwenye shamba la miwa kwa ajili ya kiwanda hicho lenye ukubwa wa ekari 63,000.

“Lengo kubwa hapa ni kuzalisha sukari itakayotuwezesha kukidhi mahitaji yetu ya ndani na kuuza nje ya nchi pamoja na bidhaa ambatano ikiwemo ethanol. Pia nitoe wito kwa vijana wa eneo hili kuhakikisha wanakuwa katika vikundi ambavyo vitawawezesha kutekeleza kwa urahisi miradi mbalimbali ikiwemo kuanzisha mashamba yatakayosaidia kuongeza malighafi kwa kiwanda hiki,’’ alisema.

Zaidi Dk. Mpango aliwataka viongozi wa serikali wilayani humo wakiwemo wahandisi  kuhakikisha wanatoka maofisini ili kukagua ujenzi wa miundombinu inayoambatana na mradi huo ikiwemo barabara inayojengwa na kampuni ya ujenzi ya SUMA JKT kuelekea eneo la mradi.

“Ile barabara ndio itatumika kusafirisha bidhaa mbalimbali kutoka na kuelekea kiwandani na iwapo itatengenezwa chini ya kiwango kutokana na uzembe tu wa kushindwa kumsimamia mkandarasi hatutaelewana,’’ alisema Dk Mpango huku akiionya kampuni ya SUMA JKT kutekeleza mradi huo kwa viwango vya ubora ili kulinda imani ya serikali kwa makampuni ya umma katika  utekelezaji wa miradi yake mbalimbali.

Kwa upande wake Dr Kebwe mbali na kuahidi kuusimamia vema mradi huo hadi kukamilika kwake, alitoa wito kwa vijana wa eneo hilo kuhakikisha  wanafanya kazi badala ya kuwategemea zaidi wakina mama na wazee kwenye shughuli za uzalishaji.

“Ninazo takwimu zinazoonyesha kuwa katika kata hii wakina mama na wazee ndio wanaofanya kazi zaidi kuliko vijana na kwa mujibu wa takwimu hizo wakina mama na wazee wanafanya kazi kwa asilimia 68 huku vijana mpo…mbadilike!,’’ alionya.

ZIARA YA KAIMU KATIBU MKUU UVCCM TAIFA SHAKA WILAYANI NGARA MKOA WA KAGERA

$
0
0
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akizindua Mradi wa kikundi cha Vijana wajasiliamali cha Ufugaji wa Nyuki na Shamba la Upandaji wa Miti katika kijiji cha Nyaruku Wilayani Ngara.
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akikagua Mradi wa Usambazaji wa Umeme Vijijini katika kijiji cha Nyankenda ikiwa ni Utekelezaji wa Ilani ya CCM 2015_2020
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akikagua Ukamilishaji wa Agizo la Utengenezaji wa Madawati katika Shule ya Msingi Rulenge Jinsi lilivyo Kamilika kama alivyotoa agizo Mhe:Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akikagua eneo la Shamba la kikundi cha Mpaji ni Mungu Youth group kinacho jishughulisha na Ufugaji wa Nyuki na Ulimaji wa Mazao Mbali mbali ya Chakula
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akionyeshwa Bidhaa mbali mbali zinazo zalishwa na kikundi cha Mpaji ni Mungu Youth group
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akimkabidhi mmoja kati ya Wazee 25 waliopokea Vyeti Vya Matibabu ya bure kwa wazee katika kijiji cha kijiji cha Mumiramila Wilayani Ngara.
Mwandishi wa Gazeti la Uhuru Bw.Antari Sangali pamoja na wazee wakijiji cha Mumilamila Wilayani Ngara wakimsikiliza kwa makini Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka (MNEC)alipo kua akigawa Vyeti kwaajili ya Matibabu ya Bure kwa wazee.
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka (MNEC) alipo zindua Mradi wa Shamba la Uvccm wilayani Ngara kwa ajili ya Shughuli Mbali mbali za kilimo kwa Vijana Wilayani humo ikiwa ni Utekelezaji wa agizo lake alilotoa kwa Makatibu wote kuandaa miradi Mbali mbali ili kukwamua Vijana kiuchumi kama kauli Mbiu yake isemayo” SIASA NA UCHUMI”
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akiwasili katika Kijiji Cha BENACO Wilayani Ngara, Shaka yupo kwa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM 2015_2020
Mwenyekiti wa uvccm Mkoa wa Kagera Bw. Yahya Kateme akizungumza kumkaribisha Ndg: Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka Kuzungumza na Wajumbe wa Baraza la UVCCM pamoja na Wajumbe wa Sekretariet ya CCM Wilayani Ngara.
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka (MNEC)akizungumza na Wajumbe wa Baraza la UVCCM pamoja na Wajumbe wa Sekretariet ya CCM Wilayani Ngara Katika Kikao Cha Ndani Kilicho Fanyika katika Ukumbi wa Engubenako Wilayani Ngara.
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akizungumza na Wajumbe wa Baraza la UVCCM pamoja na Wajumbe wa Sekretariet ya CCM Wilayani Ngara Katika Kikao Cha Ndani Kilicho Fanyika katika Ukumbi wa Engubenako Wilayani Ngara
 

TPDC YATOA SHILIONI MILIONI 10 WAKAZI WA PUGU-MAJOHE

$
0
0

Diwani wa kata ya Majohe Bw.Waziri Mwanavyale akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa msaada wa shilingi milioni 10 toka kwa Shirika la Petroli Nchini (TPDC) kwa ajili ya kujenga Ofisi ya Serikali ya Mtaa.Kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) Mhandisi Kapulya Musomba na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bi.Elizabeth Thomas.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bi.Elizabeth Thomas akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiwa msaada wa shilingi milioni 10 toka kwa Shirika la Petroli Nchini(TPDC) kwa ajili ya Ulinzi mzuri wa Bomba la Gesi linalopita jirani yao.
Kaimu Mkurugenzi Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) Mhandisi Kapulya Musomba akizungumza na wananchi wa Pugu Majohe kabla ya kuwakabidhi shilingi milioni 10 kwa ajili ya kujenga Ofisi ya Serikali ya Mtaa.
Kaimu Mkurugenzi Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) Mhandisi Kapulya Musomba akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 10 kwa ajili ya kujenga Ofisi ya Serikali ya Mtaa,katikati ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bi.Elizabeth Thomas. Wakazi wa Majohe ni wadau wa Bomba la Gesi linalotokea Mtwara hadi Dar es Salaam.
Wakazi wa Pugu Majohe wakifurahi kupatiwa hundi ya shilingi milioni 10 kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Serikali ya Mtaa . Wakazi wa Majohe ni wadau wa Bomba la Gesi linalotokea Mtwara hadi Dar es Salaam. Picha na Daudi Manongi-MAELEZO.

Na Daudi Manongi-MAELEZO.
SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) limeipatia shilingi milioni 10 Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa mji Mpya iliyopo Pugu Majohe Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Serikali hiyo.

Akizungumza katika hafla hiyo leo Jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi wa Shirikahilo, Mhandisi Kapulya Musomba alisema wakazi wa Pugu-Majohe wameamua kutoa fedha hizo kutokana na wakazi wa eneo hilo kupitiwa na bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.

“TPDC hatuwezi kulinda bomba hili la Gesi kila mahali linapopita, wadau hawa wamekuwa ni sehemu ya kulinda bomba hili wanalinda pia uchumi wa nchi kwa sababu gesi hii pia inatumika kuzalisha umeme wa viwanda” Alisema Musomba.

Aidha Mhandisi Musomba ametoa wito kwa wananchi wa Pugu Majohe kuacha kuchimba mchanga karibu na bomba hilo kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanaharibu miundombinu ya bomba hilo.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bi.Elizabeth Thomas ameishukuru TPDC kwa kuwawezesha kupata kiasi hicho kwani kitawasaidia katika ujenzi wa Ofisi hizo na pia katika maendeleo ya Pugu Majohe na kuwaomba kuendelea kusaidia katika maeneo tofauti ya Wilaya ya Ilala.

Nae Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa mji Mpya-Majohe Bw.Geofrey Chacha amesema kuwa wamejiskia faraja sana kwa kupata msaada huo kutoka TPDC kwani utaweza kusaidia kumalizia ujenzi wa Ofisi zao.

Mchango huu umetupa nguvu katika kuwahamasisha wananchi katika eneo hili kuweza kuwa walinzi wazuri wa miundombinu hii ambayo inagusa maslahi ya Taifa letu” alisema Chacha.

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA VIONGOZI WA CHAMA CHA WAFANYABIASHARA WA CHINA JIJINI DAR E SALAAM

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewakaribisha wawekezaji kutoka nchini China kuja kuwekeza nchini katika maeneo mbalimbali ikiwemo uvuvi katika bahari,madini, utalii, ujenzi wa viwanda na miundombinu.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Watendaji Wakuu wa makampuni makubwa kutoka nchini China ambao walikuja hapa nchini kutafuta fursa za uwekezaji.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wawekezaji hao kuwa Tanzania ni nchi salama kwa ajili ya kuwekeza kutokana na amani iliyopo na kwa sasa Serikali inaendelea na mkakati kuondoa vikwanzo vinavyokwamisha uwekezaji ikiwemo ukiritimba na rushwa nchini.

Amesema Tanzania na China zinamahusiano mazuri na ya muda mrefu hivyo ni muhimu mahusiano hayo yakaendelea kuimarishwa zaidi kama hatua ya kukuza biashara kati ya nchi hizo mbili kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa Tanzania na China.Amesisitiza muhimu wa kuimarishwa kwa ushirikiano kati ya Chama cha Wafanya Biashara wenye Viwanda na Wakulima nchini (TCCIA) na Chama cha Wafanya biashara kutoka China kama hatua ya kuimarisha kwa angalia fursa bora za uwekezaji kati ya China na Tanzania.

Makamu wa Rais pia ameishukuru nchi ya China kwa kuichangua Tanzania kuwa miongoni mwa nchi Nne za bara la Afrika kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda.Kwa upande wao, Watendaji hao wa makampuni makubwa kutoka nchini China wamesema kwa sasa wapo mbioni kujenga kiwanda kikubwa cha kutengeneza vifaa tiba katika eneo la Mbagala jijini Dar es Salaam na wameshapewa ekari 160 kwa ajili ya kujenga kiwanda hicho.

Watendaji hao wameiomba serikali ya Tanzania isaidie kuhakikisha pindi mradi huo utakapoanza kujengwa huduma za msingi ikiwemo umeme na maji zinapatikana kwa urahisi kwenye eneo hilo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa Chama Cha Wafanyabiashara wa China nchini Tanzania ambao walimtembelea ofisini kwake leo.

BINTI WA KITANZANIA ANYAKUA TUZO YA MJASIRIAMALI BORA AFRIKA

$
0
0
Makamu Mwenyekiti wa TPSF,Salum Shamte akimkabidhi Mshindi wa Tuzo ya Mjasiliamali Bora Afrika, Jennifer Shigholi cheti cha kumtambua katika Taasisi hiyo ya TPSF kama Mjasiriamali Mahiri.
Mshindi wa  tuzo ya African entrepreneurship, Jennifer Shigholi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, kulia ni makamu Mwenyekiti wa bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania Salum Shamte. 
Makamu Mwenyekiti wa TPSF,Salum Shamte akitoa shukrani kwa  Mshindi wa Jennifer Shigholi.


Na Anthony John Globu Jamii.

Binti wa Kitanzania, Jennifer Shigholi ameibuka kuwa Mjasiriamali katika Bara la Afrika(African Enterprenuership Awards) katika Mashindano yaliyofanyika Desemba 5 Nchini Morroco.

Shigholi amewahasa Vijana  kuendelea kudhubutu na kutumia fursa mbalimbali zilizopo nchini ilikuweza kujikomboa kichumia na badala yake kuacha kulalamika na kuchukua hatua za uthubutu kwa kuwa kila kitu kinawezekana kama mtu akimua.

Pia amesema kuwa Serikali imempatia eneo la kujenga Kiwanda kikubwa zaidi ilikuweza kutoa ajira kwa vijana hapa Nchini.

Hivyo hivyo Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania TPSF Salum Shamte, amesema Mjasiliamali huyo ameleta heshima kubwa  katika nchini yetu na sisi kama Sekta binafsi tutafanya naye kazi bega kwa bega ilikumsaidia  kuweza kuendeleza biashara zake.

" Jennifer ni Mfano wa kuigwa na Vijana wengine kwa Ujasiliamali wake Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania inampongeza kwa Ushindi wake kwenye tuzo za Ujasiliamali barani Afrika na kuiletea nchi yetu heshima kubwa haswa wanawake" amesema

RAIS DKT. MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA WAKUU WA WILAYA WAWILI NA WAKURUGENZI WATATU WA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA

$
0
0
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi akizungumza na vyombo vya habari wakati wa kutangaza uteuzi wa Wakuu wa Wilaya wawili na Wakurugenzi watatu wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, uliofanywa na Rais Dkt. Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 19 Desemba, 2016 amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya wawili na Wakurugenzi watatu wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Kisare M. Makori kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Bw. Kisare M. Makori anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Humphrey Polepole ambaye hivi karibuni ameteuliwa kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Itikadi na Uenezi.

Halikadhalika, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Avod Mmanda Herman kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara iliyopo katika Mkoa wa Mtwara.
Bw. Avod Mmanda Herman anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Khatib M. Kazungu ambaye hivi karibuni ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Ramadhan Geodrey Mwangulumbi kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga iliyopo Mkoani Shinyanga.

Bw. Ramadhan Geodrey Mwangulumbi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Lewis Kalinjuna ambaye anastaafu kwa mujibu wa Sheria.
Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw Rojas John Romuli kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda iliyopo katika Mkoa wa Katavi.
Bw. Rojas John Romuli anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ngalinda Hawamu Ahmada aliyefariki dunia hivi karibuni.

Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Rashid K. Gembe kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga iliyopo katika Mkoa wa Tanga.

Bw. Rashid K. Gembe anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Mkumbo Emmanuel Barnabas ambaye uteuzi wake ulitenguliwa hivi karibuni.
Uteuzi wa huu unaanza mara moja na wateule wote wanatakiwa kuripoti Makao Makuu ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) mara wapatapo taarifa hii.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
19 Desemba, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA WENYEVITI WA BODI KWA BAADHI YA TAASISI SERIKALI

$
0
0

Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.


Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>