Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46193 articles
Browse latest View live

KATIBU TAWALA MKOANI MARA AHITIMISHA MAFUNZO KWA WADAU WA FILAMU MKOANI HUMO.

0
0
Katibu Tawala mkoa wa Mara, Adoh Mapunda (katikati) akizungumza hii leo kwenye kilele cha mafunzo ya siku tatu kwa wadau wa filamu mkoani humo. Mafunzo hayo yalianza juzi Disemba 14,2016 kwenye ukumbi wa shule ya Sekondari Mara Mjini Msoma.

Yaliandaliwa na Bodi ya Filamu nchini kwa lengo la kuwajengea welezi wanatasinia wa filamu ili kuzalisha kazi zenye ubora na hivyo kukidhi ushindani katika soko la ndani na nje ya nchi ambapo zaidi ya washiri 200 walionufaika na mafunzo hayo wamepatiwa vyeti. Tayari mafunzo ya aina hiyo yamefanyika mikoa ya Morogoro na Mwanza na yataendelea katika mikoa mingine.
#BMGHabari
Wanatasnia wa filamu mkoani Mara wakimsikiliza Katibu Tawala mkoani humo, Adoh Mapunda, wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa wanatasnia hao. Ameahidi kutoa fulana (Tshirt) 250 kwa ajili ya wanatasnia wa filamu mkoani Mara waliohudhuria mafunzo hayo ambapo zitawasaidia hususani kuwa na sare ya aina moja wakikutana kwa pamoja
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi.Nuru Millao, amesema sekta ya filamu ina mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa wanatasnia wake na taifa kwa ujumla hivyo Bodi za filamu mikoani zihakikishe zinasimamia maendeleo ya tasnia hiyo.
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Bi.Joyce Fisso, amebainisha kwamba wadau wa filamu wakiwemo watayarishaji, waongozaji, wahariri pamoja na waigizaji wamefundishwa vyema mafunzo hayo ili kuzalisha kazi bora.
Mgeni rasmi, Katibu Tawala mkoani Mara, Adoh Mapunda (wa pili kulia), akipokea cheti cha utambuzi kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi.Nuru Millao
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi.Nuru Millao, akipokea cheti cha utambuzi
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Bi.Joyce Fisso
Mmoja wa wakufunzi wa mafunzo hayo, Bi.Deograsia Ndunguru, kutoka Chuo Kikuu Dodoma, akipokea cheti cha utambuzi kutoka Bodi ya Filamu nchini.
Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba, akipokea cheti cha utambuzi kutoka Bodi ya Filamu nchini.
Mwanahabari Genoveva kutoka Idara ya Habari Serikalini, akipokea cheti cha utambuzi kutoka Bodi ya Filamu nchini.
Katibu wa Chama cha Waigizaji mkoani Mara, Johnson Ibambai, akipokea cheti cha utambuzi kutoka Bodi ya Filamu nchini.
Mwakilishi wa Mkuu wa Shule ya Sekondari Mara, akipokea cheti cha utambuzi kwa niaba yake kutoka Bodi ya Filamu nchini.
Mwanahabari Amicus Butunga, akipokea cheti cha utambuzi kwa niaba ya TBC kutoka Bodi ya Filamu nchini.
Mwanahabari George Binagi akipokea cheti cha utambuzi kwa niaba ya 102.5 Lake Fm kutoka Bodi ya Filamu nchini.
Katibu Tawala mkoa wa Mara, Adoh Mapunda (mwenye suti) na viongozi wengine wakiwa pamoja na washiriki wa mafunzo ya filamu mkoani Mara wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Katibu Tawala mkoa wa Mara, Adoh Mapunda (mwenye suti) na viongozi wengine wakiwa pamoja na washiriki zaidi ya 200 wa mafunzo ya filamu mkoani Mara wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Mwigizaji Dan Msimamo kutoka Tarime amesema mafunzo hayo yatawasaidia kuinua ubora wa filamu mkoani Mara na hivyo kukuza soko lake
Mwigizaji Justar Lucas kutoka Tarime amesema mafunzo hayo yamewaongezea weledi na kutambua kwamba filamu ni ajira na ikitumika vyema husaidia kukuza kipato cha wanatasnia wa filamu na taifa kwa ujumla.
Mwigizaji Innocent Mbalwa kutoka Bunda ameishukuru Serikali kupitia Bodi ya Filamu kwa kutoa mafunzo hayo ambapo amesema yatafungua milango mipya kwenye tasnia ya filamu mkoani Mara.
Mwigizaji Jackline James kutoka Musoma amesema mafunzo hayo yamemsaidia kutambua kwamba filamu ni ajira tofauti na alivyokuwa akidhani awali kwamba tasnia hiyo ni sehemu ya burudani.
******************
Katibu Tawala mkoani Mara, Adoh Mapunda, amewahimiza wanatasnia wa filamu mkoani humo kuwa wabunifu katika uzalishaji wa kazi zao ili kupanua soko la filamu ndani na nje ya nchi.

Mapunda ametoa rai hiyo hii leo, wakati akihitimisha mafunzo ya siku tatu kwa wanatasnia wa filamu mkoani Mara, yaliyoandaliwa na Bodi ya Filamu nchini ili kukuza welezi katika uzalishaji wa kazi bora na zenye maudhui yanaykubalika katika jamii.

"Ubunifu ndio unahitajika hivi sasa, watu wengi wanahitaji ubunifu binafsi na siyo "kucopy" na "kupaste" kazi za wengine". Amesisitiza Mapunda na kuongeza kwamba serikali itatoa ushirikiano wa dhati katika kuboresha tasnia hiyo ya filamu kwani hivi sasa hutoa ajira na kukuza uchumi kwa taifa.

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nuru Millao, ameziagiza Bodi za Filamu za mikoa kuhakikisha kwamba zinatimiza wajibu wake ipasavyo ili kuboresha zaidi sekta hiyo.

Naye Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fisso, amewahimiza wadau wa filamu mkoani Mara wakiwemo watayarishaji, waongozaji, wahariri pamoja na waigizaji walionufaika na mafunzo hayo, kuyatumia vyema ili kukuza soko lao la filamu.

Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba, amewasisitizia hao kutumia mafunzo hayo ili kuzalisha filamu na vipindi vya luninga vyenye ubora ili kunufaika na uhitaji uliopo.

Akisoma maazimio ya wanatasnia wa filamu mkoani Mara, Katibu wa Chama cha Waigizaji mkoani humo, Johnson Ibambai, ametaja baadhi ya maazimio hayo kuwa ni pamoja na kuiomba serikali kuweka mitaala ya filamu kuanzia shule za msingi na vyuo vya ufundi VETA ili kusadia utoaji wa elimu hiyo ya filamu.
Tazama picha zaidi HAPA

Waziri wa Elimu aitunuku nishani Global Education Link

0
0
WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Stadi, Profesa Joyce Ndalichako ameitunuku nishani ya uzalendo kampuni ya Global Education Link (GEL) kutokana na mchango inaotoa katika maendeleo ya elimu nchini.

Nishani hiyo aliitoa leo wakati akizindua mkutano mkuu wa 11 wa Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari nchini (TAHOSSA) mkoani Dodoma. 
Mkurugenzi wa Global Education Link (kulia) akipokea tuzo kutoka kwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na ufundi Stadi Prof. Joyce Ndalichako.

Rais wa Wakuu wa Sekondari Tanzania (TAHOSSA), Bonus Ndimbo alisema GEL imekuwa ni mdau mkubwa wa maendeleo katika elimu, sio tu kwa TAHOSSA hata kwa nchi kwa ujumla.

“Tunaipongeza sana Global Education Link, kwani imekuwa karibu na jamii, imekuwa karibu na sekta ya Elimu na maendeleo ya nchi kwa ujumla,” alisema Katibu Mkuu wa TAHOSSA Diana Matemu.Global Education Link ni kampuni iliyoanzishwa Mwaka 2006 kwa lengo la kuwaunganisha wanafunzi wa Tanzania wanaotaka kusoma vyuo vikuu vya nje.

Tangu imeanza shughuli zake kwa miaka 10 sasa, zaidi ya wanafunzi 5400 wamefaidika kwa kuunganishwa na vyuo mbalimbali vilivyoko Marekani, Canada, Uingereza, Afrika Kusini, Ukraine, India, Urusi, Malaysia, China na nyinginezo. 
Mkurugenzi Mkuu wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel akizungumza na Wakuu wa Sekondari Tanzania baada ya kupewa nafasi ya kipekee ya kuwawakilisha wadau mbalimbali wa elimu waliokaribishwa katika mkutano huo mbele ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Ufundi stadi Prof Joyce Ndalichako.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA) wakimsikiliza Mkurugenzi wa Global Education Link, Abdulmalik Mollel (hayuko pichani).

Akizungumza baada ya kukabidhiwa nishani hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel alishukuru na kusema anafanya hivyo kwa lengo la kusaidia Serikali na Watanzania kwa ujumla katika kuharakisha maendeleo nchini.

Kikubwa ambacho Mkurugenzi wa GEL alisema ni kuwa mpango wa mafunzo kwa wanafunzi utasaidia kuwafanya wanafunzi kuchagua kozi ambazo zitakuwa na tija kwao na taifa kwa ujumla.

Mkurugunzi wa Idara ya Habari MAELEZO HASSAN ABBAS ALAMBA NONDOZZZZ YA PhD

0
0
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO - Dkt. Hassan Abbass akikitunukiwa Shahada yake ya Uzamivu ya Mawasiliano ya Umma (PhD) kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT) wakati wa Mahafali ya 16 ya chuo hicho leo Jijini Mwanza.
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO - Dkt. Hassan Abbass akipokea shada la maua mara baada ya kutunukiwa Shahada yake ya Udaktari wa Mawasiliano ya Umma kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT) wakati wa Mahafali 16 ya chuo hicho leo Jijini Mwanza.
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO - Dkt. Hassan Abbass (kushoto) akifurahia jambo na mmoja wa Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT) Fr. Francis Ng’atigwa mara baada ya kutunukiwa Shahada yake ya Udaktari wa Mawasiliano ya Umma kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Tanzania (SAUT) wakati wa Mahafali 16 ya chuo hicho leo Jijini Mwanza
Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO - Dkt. Hassan Abbass (wanane kutoka kushoto mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu wenzake mara baada ya kutunukiwa Shahada yake ya Udaktari wa Mawasiliano ya Umma kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Tanzania (SAUT) wakati wa Mahafali 16 ya chuo hicho leo Jijini Mwanza.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO DKT. ASHATU KIJAJI AHIMIZA MAENDELEO VIJIJINI

0
0
Mkuu wa mradi wa Agra, ambaye pia ni Mhadhiri katika Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini-Dodoma, Dkt. Mark Msaki (kushoto), akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (Katikati) wakati akikagua maonesho ya taaluma, huduma na bidhaa kabla ya kutunuku tuzo mbalimbali kwa wahitimu 829 katika Mahafali ya 30 ya Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Kituo cha Mwanza. Kushoto kwa Dkt. Kijaji na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula (Mb).
Mwanafunzi wa kiume wa Stashahada Mwaka wa Pili wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Kituo cha Mwanza, akielezea kuhusu mafunzo wanayoyapata chuoni hapo na namna elimu hiyo inavyosaidia kuendeleza vijiji walivyokwenda kufanya mazoezi kwa vitendo mkoani Mwanza, wakati Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (Hayupo pichani) alipotembelea na kukagua maonesho hayo ya taaluma, huduma na bidhaa zinazotolewa na chuo hicho.


Mwanafunzi wa kike wa Stashahada Mwaka wa Pili wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Kituo cha Mwanza, akielezea kuhusu mafunzo wanayoyapata chuoni hapo na namna elimu hiyo inavyosaidia kuendeleza vijiji walivyokwenda kufanya mazoezi kwa vitendo mkoani Mwanza, wakati Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) alipotembelea na kukagua maonesho hayo ya taaluma, huduma na bidhaa zinazotolewa na chuo hicho.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto), akionesha moja ya machapisho yaliyotolewa na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini wakati alipotembelea na kukagua maonesho ya taaluma, huduma na bidhaa kabla ya kutunuku tuzo mbalimbali kwa wahitimu 829 katika Mahafali ya 30 ya Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Kituo cha Mwanza.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto), akisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mkufunzi wa Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini Bw. Ezekiel Kanire, (aliyeshika kipaza sauti) wakati alipotembelea na kukagua maonesho ya taaluma, huduma na bidhaa kabla ya kutunuku tuzo mbalimbali kwa wahitimu 829 katika Mahafali ya 30 ya Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Kituo cha Mwanza. Kushoto kwa Dkt. Kijaji na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula (Mb).
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto), akiangalia kipeperushi chenye maelezo ya faida za kutumia kitunguu swaumu kwa binadamu wakati Mkulima wa zao la vitunguu swaumu kutoka Wilayani Mbulu Mkoani Manyara, Bw, Boniface Bura, (aliyeshika kipaza sauti), akitoa maelezo namna Chuo chas Mipango ya Maendeleo Vijijini kilivyomsaidia kuongeza thamani ya zao hilo, wakati Naibu waziri huyo alipotembelea na kukagua maonesho ya taaluma, huduma na bidhaa zinazotolewa na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Kituo cha Mwanza.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto), akisikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na mkulima wa zao la vitunguu swaumu kutoka Wilayani Mbulu Mkoani Manyara, Bw. Boniface Bura, (aliyeshika kipaza sauti), alipotembelea na kukagua maonesho ya taaluma, huduma na bidhaa zinazotolewa na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Kituo cha Mwanza, kabla ya kutunuku tuzo mbalimbali kwa wahitimu 829 wa Chuo hicho wakati wa Mahafali ya 30 yaliyofanyika mara ya tano katika Kituo hicho cha Mwanza.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto), akipokea zawadi ya Kitunguu swaumu kilichosindikwa, kwaniaba ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli iliyotolewa na Mkulima wa zao hilo kutoka Wilayani Mbulu Mkoani Manyara, Bw. Boniface Bura, anayenufaika na mradi wa kuwawezesha wakulima vijijini wa Mivaraf, ikiwa ni ishara ya kuunga mkono Jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano ya Viwanda.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto), akizungumza na vyombo vya habari baada ya kumaliza kutembelea na kukagua maonesho ya taaluma, huduma na bidhaa kabla ya kutunuku tuzo mbalimbali kwa wahitimu 829 katika Mahafali ya 30 ya Chuo Cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Kituo cha Mwanza.


(Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)

BELLE 9 AZINDUA WIMBO WAKE MPYA WA 'GIVE IT TO ME' USIKU HUU JIJINI DAR

0
0
 Msanii wa Muziki wa kizazi Kipya, Abelnego Damian maarufu kama Belle 9 akizungumza wakati wa uzinduzi wa wimbo wake mpya uliofahamika kwa jina la  'Give It To Me' usiku huu. Kulia ni Mdau wa Muziki wa Kizazi Kipya na Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete. Hafla hii imefanyika usiku huu katika bustani ya Nyumba ya Mbunge huyo, Kawe jijini Dar.
 Mbunge Jimbo la Chalinze na Mdau wa Muziki wa Kizazi Kipya, Ridhiwani Kikwete akizungumza machache ikiwemo na kumpongeza msanii huyo,katika hafla ya uzinduzi wa Video yake ya  wimbo mpya  uliofahamika kwa jina la  'Give It To Me' Jijini Dar es salaam leo.
 Baadhi ya Wasanii mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo wakimpongeza msanii mwenzao Belle 9 

YANGA YA LWANDAMINA YAIGARAGAZA JKT RUVU 3-0

0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

MABINGWA watetezi wa ligi kuu Vodacom Yanga imefanikiwa kupanda hadi kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Ruvu jioni ya leo Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi 36 baada ya kucheza mechi 16 na kuishusha Simba iliyomalizia kileleni mzunguko wa kwanza kwa pointi zake 35. 

Winga Simon Msuva aliweza kuwa nyota wa mchezo huio baada ya kufanikiwa kuifungia timu yake goli mbili katika dakika ya 57 na 90 huku lingine akipiga pande safi linalomshinda beki Michael Aidan na kuingia nao nyavuni dakika ya 38.

JKT Ruvu waliweza kucheza kandanda safi na wakionekana kutumia mashuti ya mbali kuweza kujaribu nafasi ya kufunga huku mshambuliaji wake Atupele Green akikosa nafasi mbili za wazi.

Mkurugenzi wa Ufundi wa Yanga, Mholanzi Hans van der Pluijm alikuwepo jukwaa kuu kufuatilia mchezo, wakati kiungo mpya kutoka Zambia, Justin Zulu pia akiwa jukwaani kwa sababu bado hajapatiwa kibali cha kufanya kazi nchini. 

Baada ya mchezo, kocha msaidizi Juma Mwambusi amesema kuwa waliingia uwanjani na mpango wakushinda na wamefaniklisha hilo ingawa mchezo ulikuwa mgumu sana kwao.


Mechi hiyo ilichezeshwa na Hery Sasii akisaidiwa na Hellen Mduma na Kassim Mpanga wote wa Dar es Salaam.

Matokeo mengine ni:
Mwadui 1-0 Toto Africans Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Mbeya City 0-0 Kagera Sugar Uwanja wa Sokoine, Mbeya na Ruvu Shooting 1-1 Mtibwa Sugar Uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Pwani.

Kikosi cha Yanga kilikuwa; 
Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Haruna Niyonzima, Mwinyi Hajji Mngwali, Kelvin Yondan, Vincent Bossou, Simon Msuva, Thabani Kamusoko/Geoffrey Mwashiuya dk84, Donald Ngoma, Amissi Tambwe/Said Juma ‘Makapu’ dk55na Deus Kaseke/Obrey Chirwa dk90
.
JKT Ruvu: Hamisi Seif, Michael Aidan, Edward Charles, Yussuf Chuma, Kelvin Nashon/Naftal Nasho dk66, Rahim Juma, Ally Bilal/Mussa Juma dk77, Hassan Dilunga, Najim Magulu, Atupele Green/Saad Kipanga dk77 na Edward Joseph.
Kikosi cha Yanga SC leo dhidi ya JKT Ruvu FC
Kikosi cha JKT Ruvu SC leo dhidi ya Yanga FC 
Mshambuliaji wa Yanga SC,Deus Kaseke (katikati) akiwatoka mabeki wa timu ya JKT Ruvu leo katika uwanja wa Uhuru mchezo uliomaizika kwa Yanga SC kuibuka na ushindsi wa goli 3-0 leo jijini Dar es Salaam. 
Mshambuliaji wa timu ya JKT Ruvu ,Naftal Nashon (wakwanza kulia) akimtoka beki wa timu ya Yanga leo katika uwanja wa Uhuru mchezo uliomaizika kwa Yanga SC kuibuka na ushindsi wa goli 3-0 leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba akijadiliana jambo na Mbunge wa Chalinze, Ridhiwan Kikwete wakati wa mechi ya ligi kuu kati ya JKT Ruvu na Yanga leo Jijini Dar es salaam.
Kiungo mpya kutoka Zambia, Justin Zulu (katikati) akiwa jukwaani kwa sababu bado hajapatiwa kibali cha kufanya kazi nchini. 
Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.


VIJANA 150 WAKUTANA KAHAMA KWENYE BONANZA LA MICHEZO LILILOANDALIWA NA AGPAHI

0
0

Vijana wanaotoka katika halmashauri za wilaya ya Kahama Mji,Ushetu,Msalala na Manispaa ya Shinyanga wamekutana katika bonanza la michezo lililoandaliwa na Shirika la Kitanzania lisilo la kiserikali la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI.
Bonanza hilo la michezo limejumuisha vijana 150 wenye umri kati ya miaka 14-19 wanaotoka katika klabu za vijana zilizoundwa na zinasimamiwa na shirika la AGPAHI kwa kushirikiana na halmashauri za wilaya husika.
Akifungua bonanza hilo katika uwanja wa taifa mjini Kahama leo Jumamosi Desemba 17,2016,mgeni rasmi Dr. Anthony Kasomelo kutoka hospitali ya mji wa Kahama,alisema bonanza hilo ni kwa ajili ya vijana kufurahi,kufahamiana,kupata marafiki wapya,kuonyesha vipaji na kujifunza. 
"Vijana hawa wanatoka kwenye vikundi 12 vilivyopo katika halmashauri nne za mkoa wa shinyanga,ambazo ni Msalala,Kahama mji,Ushetu na manispaa ya Shinyanga", alisema Kasomelo.
Dr. Kasomelo alitumia fursa hiyo kulipongeza shirika la AGPAHI kwa kuendelea kuwa karibu na vijana huku akiwaasa vijana hao kuendelea kuwa wafuasi wazuri wa huduma za afya ili kuboresha afya zao ili waweze kutimiza ndoto zao.

Aidha alitoa wito kwa viongozi wa halmashauri za wilaya kuendelea kutoa ushirikiano kwa shirika la AGPAHI hasa katika kutekeleza majukumu ya kuwasaidia wananchi katika huduma za afya hususani kwa watu wanaopata tiba na matunzo ili huduma zipatikane katika ubora na ziwe rafiki kwa wananchi. 
Awali akizungumza katika bonanza hilo, Afisa mradi wa watoto kutoka Shirika la AGPAHI mkoa wa Shinyanga, Jane Kashumba alisema wafadhili wa bonanza hilo ni shirika la Uingereza linalofadhili huduma za kuboresha maisha ya watoto (Children's Investment Fund Foundation -CIFF).
Kashumba alibainisha kuwa shirika la AGPAHI limeanzisha klabu 12 za vijana zenye wastani wa vijana 20 - 70 walio katika rika balehe. 
"Lengo la vikundi hivi ni kuwakutanisha vijana kila mwezi ili waweze kujifunza pamoja masuala mbalimbali ikiwemo masuala ya msukumo rika kwa vijana,kushirikiana katika kutatua changamoto zao na njia za kujikinga na maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi vijana hao wameendelea kunufaika na elimu hiyo",alieleza Kashumba. 

Miongoni mwa michezo iliyochezwa na vijana hao ni pamoja mpira wa miguu,kuvuta Kamba,mbio za magunia,kukimbiza kuku ,kuimba nyimbo na kucheza muziki ambapo washindi waliibuka na zawadi mbalimbali. 

Bonanza hilo limehudhuriwa na wadhibiti wa Ukimwi kutoka halmashauri za wilaya,wasimamizi wa klabu za vijana,wafanyakazi wa shirika la AGPAHI na wadau mbalimbali wa michezo na mambo ya afya. 
Angalia matukio katika picha yaliyojiri uwanjani hapa chini
Afisa mradi wa watoto kutoka Shirika la AGPAHI mkoa wa Shinyanga, Jane Kashumba akizungumza wakati Bonanza la michezo katika uwanja wa taifa wa mjini Kahama
Mgeni rasmi Dr. Anthony Kasomelo kutoka hospitali ya mji wa Kahama akifungua bonanza hilo la vijana lililokutanisha vijana 150 ambapo mbali na kulipongeza shirika la AGPAHI alitumia fursa hiyo kuwaasa vijana hao kupenda shule
Katikati ni mgeni rasmi Dr. Anthony Kasomelo akizungumza wakati wa kufungua bonanza la michezo.Kushoto ni Mhudumu wa jamii pia Afisa tabibu kutoka kituo cha afya cha Kolandoto katika manispaa ya Shinyanga Maryciana Bruno ,aliyeinama kulia ni Mganga mfawidhi zahanati ya Segese Denis Ngatale
Mgeni rasmi Dr. Anthony Kasomelo akiteta jambo na Jane Kashumba 
Timu ya mpira wa miguu kutoka halmashauri ya manispaa ya Shinyanga wakijiandaa kuanza mchezo baina yao na timu kutoka halmashauri ya wilaya ya Ushetu,Msalala na Kahama Mji. 
Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu kutoka manispaa ya Shinyanga wakiwa na walezi wao na maafisa kutoka AGPAHI 
Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu kutoka halmashauri ya wilaya ya Ushetu,Msalala na Kahama Mji wakipiga picha kabla ya mchezo 
Wachezaji wa timu ya halmashauri ya wilaya ya Kahama Mji,Ushetu na Msalala wakiwa na walezi wao na maafisa kutoka AGPAHI 
Dawati la ufundi timu ya Kahama Mji,Ushetu na Msalala. 
Mchezo kati ya Kahama Mji,Ushetu na Msalala ukiendelea 
Mchezo unaendelea ambapo hadi kipenga cha mwisho kinapulizwa Kahama mji walikuwa wanaongoza kwa kuibamiza timu ya manispaa ya Shinyanga bao 4-1 
Mbio za magunia ukiendelea kati ya vijana wa kike kutoka manispaa ya Shinyanga(waliovaa nguo za bluu) na wasichana kutoka Kahama Mji,Ushetu na Msalala zikiendelea 
Mbio za magunia zikiendelea ambapo hadi mwisho wa mchezo mshindi wa kwanza alikuwa Esther Peter kutoka Ushetu (aliyevaa nguo nyeupe),wa pili Elizabeth Busheye kutoka manispaa ya Shinyanga(wa kwanza kulia) 
Mbio za magunia upande wa vijana wa kiume kutoka manispaa ya Shinyanga (waliovaa nguo za bluu) na wasichana kutoka Kahama Mji,Ushetu na Msalala zikachukua nafasi 
Mchezo unaendelea,ambapo hadi mwisho wa mchezo mshindi wa kwanza alikuwa Ali Seleman,wa pili Isack Kiwila 
Mchezo wa kufukuza kuku upande wa vijana wa kike ukiendelea
Vijana wakiendelea kukimbiza kuku
Helena Daudi kutoka manispaa ya Shinyanga akiwa amebeba kuku baada ya kufanikiwa kumkamata na kisha kuondoka naye kama zawadi ya ushindi
Vijana wa kiume nao walifukuza kuku
Kijana Peter Kulwa naye akaondoka na kuku baada ya kufanikiwa kumkamata
Mchezo wa kuvuta kamba nao ulikuwepo,picha ni kushoto ni vijana wa kike kutoka Kahama mji,Ushetu na Msalala wakijiandaa kushindana kuvuta kamba na vijana wa kike kutoka manispaa ya Shinyanga(kulia).Waliopo katikati ni Dr. Anthony Kasomelo kutoka hospitali ya mji wa Kahama na Afisa mradi wa watoto kutoka Shirika la AGPAHI mkoa wa Shinyanga, Jane Kashumba wakitoa maelekezo kwa vijana hao kabla ya mchezo huo wa kuvuta kamba
Vijana kutoka manispaa ya Shinyanga wakijiandaa kuvuta kamba
Katika mchezo huo wa kuvuta kamba vijana kutokaUshetu,Msalala na Kahama Mji waliibuka washindi
Vijana wa kiume kutoka Kahama Mji,Ushetu na Msalala wakijiandaa kushindana kuvuta kamba dhidi ya vijana kutoka manispaa ya Shinyanga
Vijana kutoka manispaa ya Shinyanga wakikazana kuvuta kamba ingawa hata hivyo walishindwa katika mchezo huo
Vijana kutoka manispaa ya Shinyanga wakiimba shairi
Walezi wa vijana na vijana wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea uwanjani
Vijana kutoka Kahama mji wakiimba 
Kulia ni Dr. Selemani Wambili kutoka Zahanati ya Kagongwa wilayani Kahama na mlezi wa vijana kituo cha Segese katika halmashauri ya Msalala wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Vijana wakiwa eneo la tukio 
Vijana kutoka manispaa ya Shinyanga wakicheza muziki
Vijana wakionesha kipaji cha kucheza
Kijana akiimba wimbo 
Vijana wakishindana kucheza muziki
Wajumbe wa kamati ya kutoa zawadi kwa washindi katika michezo iliyofanyika uwanjani wakijadili jambo kabla ya kuanza kugawa zawadi kwa washindi.Aliyekaa kushoto ni Dr. Selemani Wambili kutoka Zahanati ya Kagongwa,kulia kwake ni mhudumu wa jamii kutoka kituo cha Kolandoto Maryciana Bruno.Waliosimama wa kwanza ni kushoto ni mlezi wa watoto kituo cha Kambarage Glory Assey akifuatiwa na mlezi wa watoto kituo cha hospitali ya Kahama mji Flora Selutongwe.Kulia ni mgeni rasmi Dr. Anthony Kasomela akijiaandaa kupokea majina ya washindi ili awape zawadi
Mgeni rasmi Dr. Anthony Kasomelo akitoa zawadi ya kombe kwa Timu ya Kahama mji,Ushetu na Msalala walioibuka washindi baada ya kuifunga timu ya manispaa ya Shinyanga bao 4-1
Vijana wakifurahia baada ya kupewa zawadi ya kombe
Vijana waliofunga magoli manne na kuipa ushindi timu ya Kahama mji,Ushetu na Msalala wakipokea zawadi ya saa kila mmoja
Vijana kutoka manispaa ya Shinyanga wakipokea zawadi kombe kwa kuibuka wachezaji bora wa muziki
Mgeni rasmi Dr. Anthony Kasomelo akimkabidhi zawadi ya saa Esther Peter kutoka Ushetu aliyekuwa mshindi wa kwanza katika shindano la mbio za magunia
Mshindi wa pili mbio za magunia upande wa vijana wa kike Elizabeth Busheye kutoka manispaa ya Shinyanga akipokea zawadi ya saa
Mshindi wa kwanza mbio za magunia upande wa vijana wa kiume Ali Seleman kutoka manispaa ya Shinyanga akipokea zawadi ya saa
Mshindi wa pili mbio za magunia Isack Kiwila kutoka manispaa ya Shinyanga akishikana mkono na mgeni rasmi kabla ya kupokea zawadi ya saa
Kijana aliyeonesha kipaji cha kucheza muziki akipokea zawadi ya begi
Mlezi wa vijana katika kituo cha hospitali ya mkoa wa Shinyanga Elizabeth Lubasha akijiandaa kupokea vifaa vya shule ikiwepo soksi na kalamu kwa ajili ya vijana anaowalea
Mlezi wa vijana katika kituo cha Segese Kanzaga Fabian akipokea vifaa vya shule kwa ajili ya vijana wake
Mlezi wa watoto kituo cha hospitali ya Kahama mji Flora Selutongwe akiwa amebeba zawadi ya soksi na kalamu kwa ajili ya vijana anaowalea
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

VJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI DESEMBA 18, 2016

0
0
Add caption

Vyuo India vyaeleza vinavyoweka ulinzi vyuoni

0
0
BAADHI ya maofisa kutoka vyuo vikuu vya India ambao wamekuwa wakishirikishi maonyesho ya vyuo vya nje yaliyofanyika tarehe 14 hadi 15 Desemba Dodoma, wameeleza namna vyuo nchini mwao vinavyoweka kipaumbele katika ulinzi wa wanafunzi wao.

Ofisa kutoka Chuo Kikuu cha Lovely (LPU), Love Kumar alisema, katika maonyesho hayo yaliyoandaliwa na Kampuni ya wakala wa vyuo vya nje, Global Education Link (GEL) kuwa kwa mfano katika chuo chake kuna kamera nyingi zilizofungwa katika maeneo mbalimbali kuchunguza kila kinachoendelea.

“Tunatamani kuona watu wanakuja kwetu na kusoma kwa amani, India ni nchi ya amani. Hata hivyo tumeweka zaidi ya kamera 4000 kuhakikisha kila kitu kinaangaliwa kwa ufasaha” aliongeza Kumar.

Naye Mratibu wa wanafunzi wanaotoka nje kutoka Chuo Kikuu cha Maharishi Markandeshwar, Rashmi Garg alisema hali ni hivyo pia katika chuo hicho. Alifafanua kwamba sababu ya kufunga vifaa vya ulinzi ni kuendelea kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa.
Mojawapo ya majengo ya Chuo Kikuu cha Lovely nchini India. Global Education Link (GEL) ni mwakilishi rasmi wa chuo hiki hapa nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel, aliwahakikisha Watanzania kwamba kampuni yake inafanya inaloweza kuhakikisha Watanzania wengi zaidi wanakwenda nje ya nchi kupata ujuzi ambao watarudi nao nchini kwa ajili ya kusaidia kukuza maendeleo.

SUALA LA UKEKETAJI MKOANI MARA BADO NI CHANGAMOTO KUBWA

0
0
Baadhi ya wasichana wakitoka kukeketwa wilayani Tarime mkoani Mara, kumbuka mwezi Disemba, kila baada ya miaka miwili, ni msimu wa ukeketaji na tohara kwa baadhi ya Koo za Wakurya.
#BMGHabari
Pamoja na juhudi za Serikali, Wanaharakati na Watetezi wa haki za binadamu (Wanawake na Wasichana) katika kuhakikisha kwamba suala la ukeketaji linatokomezwa katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo mikoa ya Mara na Arusha, bado suala hilo ni pasua kichwa kwani linafanyika, iwe kwa uwazi ama usiri.

Mtandao wa Binagi Media Group umeshuhudia baadhi ya wakazi wa wilaya ya Tarime wakisherehekea msimu huu wa ukeketaji (Mwezi Disemba kwa baadhi ya koo, ikiwemo Watimbaru) ambapo wasichana wadogo wanafanyiwa ukeketaji.

Shamra shamra zinafanyika hadharani licha ya Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Glorious Luoga, kuonya kwamba yeyote atakayebainika kujihusisha na ukeketaji atachukuliwa hatua za kisheria.

Baadhi huamini kwamba msichana akikeketwa huleta heshima kwake na kwa familia na huwa tayari kwa ajili ya kuolewa na hivyo kuwapatia wazazi mahari (ng'ombe). Hatua hii husababisha baadhi ya mabinti kukosa fursa ya kuhitimu masomo yao na kujikuta wakiolewa, Aidha kwa kupenda ama kulazimishwa na wazazi/walezi wao. 

Suala la unyanyapaa miongoni mwa wasichana waliokeketwa na ambao hawajakeketwa ni jambo ambalo pia huongeza msukumo wa wasichana kutaka kukeketwa. Mbaya zaidi, unyanyapaa huo huenda hadi kwa baadhi ya wanaume kukataa kuwaoa wale ambao hawajakeketwa na hivyo kusababisha ugumu wa kutokomeza suala hilo.

Tayari Ngariba mmoja aitwaye Angelina ppCharles (50) amehukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani kwa kosa la kumfanyia ukeketaji mmoja wa wasichana wilayani humo huku wengine wawili wakidaiwa kukabiliwa na kesi ya aina hiyo. Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya Wilaya ya Tarime, Mhe.Martha Mpaze.

Wakati hayo yakiendelea, zipo kauli mbalimbali wilayani Tarime kwamba hivi sasa wasichana hawakeketwi kama zamani bali wakifika eneo la tukio hupakwa unga kwenye uso na maumbile yao na kufanyiwa matambiko ya kimila na shughuli huishia hapo na kinachofuata ni shamra shamra za kucheza ngoma ya ritungu na kurejea nyumbani.

Hata hivyo utafiti uliofanywa mwishoni mwa mwaka jana na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, TAMWA kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linalojihusisha na idadi ya watu duniani, UNFPA, kwenye mikoa 13 nchini ikiwemo Mara, umebaini kwamba katika maeneo mengi nchini, wanajamii wanazo mbinu mpya za kuhakikisha wanatimiza malengo yao ya kukumbatia mila potofu ikiwemo ukeketaji.

 Utafiti huo ulibaini kuwa, suala la kuwapaka unga usoni wasichana wilayani Tarime ni kuuficha tu ukweli kwamba wasichana hao hawakeketwi wakati ukweli ni kwamba hukeketwa.

Itoshe tu kusema kwamba, elimu zaidi inahitajika ili kuwanusuru wasichana wanaotoka kwenye makabila yanayojihusisha na ukeketaji kwani madhara yake ni makubwa ikiwemo kupoteza damu nyingi, kupata madhara kabla na baada ya kujifungua, kupoteza uwezo wa kufurahia tendo la ndoa, uwezekano wa kupata maambukizi ya magonjwa ikiwemo Virus vya Ukimwi na wakati mwingine kupoteza maisha.
Inaelezwa kwamba msichana anayekeketwa hulipia kiasi cha shilingi elfu 35 hadi 40 ambapo wazee wa kimila hugawana pesa hiyo na mangariba hivyo inawezekana suala hili linakuwa na ugumu kutokomezwa maana ni sehemu ya ujira kwa wazee na mangariba hao.
Inadhaniwa kwamba zaidi ya wasichana 3,000 kwa Koo moja ya kabila la Wakurya hukeketwa kwa kila msimu. Kabila la Wakurya lina Koo 13.
Wakazi wa Wilaya ya Tarime wanasema, msukumo wa ukeketaji umepungua kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na miaka ya nyuma. Wanasema suala la elimu juu ya madhara ya ukeketaji pamoja na mwingiliano wa makabila mbalimbali ya ndani na nje ya mkoa wa Mara, umesaidia japo kwa kiasi kidogo kupunguza ari ya ukeketaji.
Kataa Ukeketaji, haina umuhimu kufurahia mila na tamaduni zenye athari katika jamii. Vyombo vya ulinzi na usalama vinapaswa kuwakama na kuwafungulia mashtaka.
Wakati haya yanaendelea, zaidi ya wasichana 250 kutoka maeneo mbalimbali mkoani Mara na Arusha, wamehifadhiwa katika kituo cha kuwahifadhi wasichana waliokimbia ukeketaji cha Masanga kilichopo wilayani Tarime.

BMG inaamini kwamba, Imani humalizwa kwa Imani. Suala la Ukeketaji ni Imani hivyo itolewe elimu yenye uhusiano wa kiimani ikiwemo maandiko matakatifu (dini) hatua ambayo itasaidia kuwanusuru wasichana wengi na suala hilo la ukeketaji.

TIMU YA KIJITONYAMA VETERANS WAFANYA MKUTANO WA KUPATA VIONGOZI WAPYA

0
0
 TIMU ya Kijitonyama Veterans yenye maskani yake Kijitonyama, leo imefanya uchaguzi mkuu na kupata viongozi wapya wa kuingoza timu hiyo kwa kipindi cha miaka mitano.

Nafasi zilizokuwa zikigombewa ni tisa, ambapo katika nafasi ya Mwenyekiti aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo muda uliopita, Lupyana Michael, ameendelea kubaki katika nafasi hiyo baada ya kupigiwa kura na wajumbe na kuongoza dhidi ya mpinzani wake, Petro Malima .

Pia aliyekuwa Katibu Mkuu wa Timu hiyo Amon Petro, naye ameendelea kubaki katika nafasi hiyo baada ya kuibuka na kura nyingi zaidi ya mpinzani wake, Evodius Mtawala

Naye Mratibu wa timu hiyo, Majuto Omary,pia ameendelea kubaki katika nafasi hiyo baada ya kuibuka kidedea dhidi ya mpinzani wake Evans Malla, 

Kwa mujibu ya utaratibu wa Timu hiyo, kutokana na mapendekezo ya Wajumbe, katika uchaguzi, majina mawili yanayopigiwa kura na mmoja kati yao anayepata kura nyingi ndiye anapaswa kuwa kuwa kiongozi katika nafasi husika na anayefuatia kwa kura anakuwa msaidizi.

VIONGOZI WALIOCHAGULIWA:-

MWENYEKITI:  Lupyana Michael
MAKAMU MWENYEKITI: Malima Petro

KATIBU MKUU: Amon Petro
KATIBU MSAIDIZI: Evodius Mtawala

MRATIBU MKUU: Majuto Omary
MTARIBU MSAIDIZI: Evans Malla

MWEKAHAZINA MKUU: Othaman Hussein 
MWEKA HAZINA MSAIDIZI: Sweetbert Mwombeki

MSEMAJI WA TIMU: Muhidin Sufiani (Mafoto)

 Baadhi ya wajumbe wakipitia vifungu vya katiba wakati wa uchaguzi huo.

Zaidi ya wanawake 900 wajasiriamali wapigwa msasa

0
0
· Kwa mafunzo ya kibiashara na huduma za kifedha kutoka Vodacom Tanzania,Technoserve, ExxonMobil

Zaidi ya wanawake 900 wanaomiliki biashara ndogo ndogo wamehitimu mafunzo ya ujuzi wa biashara na huduma za kifedha kupitia mradi wa Business Women Connect (BWC) unaofadhiliwa na ExxonMobil Foundation na kutekelezwa kwa ushirikiano baina ya TechnoServe, Vodacom Tanzania, Benki ya Dunia (kitengo cha Gender Innovation) pamoja na kitengo cha Maendeleo ya Dunia.(Centre for Global Development).

Mradi wa BWC ulizinduliwa Octoba mwaka 2015 ukiwa na lengo la kuwasaidia wanawake 3,000 wanaomiliki biashara ndogo ndogo kujiongezea kipato kupitia huduma ya Vodacom ya M-Pawa pamoja na kuwapatia mafunzo ya ujuzi wa biashara na uelewa wa huduma za kifedha. Mradi huu umelenga wanawake wa mikoa ya Dodoma na Mbeya.

Sherehe za mahafali ya wahitimu hawa zilifanyika mwishoni mwa wiki mkoani Dodoma na Mbeya na kuhudhuriwa na mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa akimwakilisha Rehema Madenge na Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya akimwakilisha Mariam Mtunguja.

Wahitimu walimaliza mafunzo ya miezi 3, wakiwa wamepata ujuzi wa jinsi ya kupanua biashara na faida, ufanisi katika kazi, kutunza kumbukumbu za fedha, uandaaji wa biashara pamoja kuweka akiba salama kupitia M-Pawa.

Utafiti uliofanya na InterMedia na Benki ya Dunia unaonyesha kuwa asilimia 70 ya watanzani wanamiliki simu za mikononi, wakati asilimia 60 bado hawapo kwenye mfumo rasmi wa kutunza pesa benki. Wakati wanawake wakiathirika zaidi na ufinyu wa nafasi za kutumia mfumo wa kuhifadhi fedha kupitia simu za mikononi, hivyo kuwazuia kukuza biashara zao.

Wakati huo huo, tafiti inaonyesha kuwa wanawake ni watunzaji wazuri wa fedha hata wenye kipato kidogo au kisicho cha uhakika, wanawake wanaweza kutunza asiimia 10 mpaka 15 ya mapato yao hivyo kuwapa urahisi wa kutumia M-Pewa wanawake wanajiongezea uwezo wa kudhibiti pesa zao, kukuza vipato na kuwekeza kwenye familia na biashara zao.

“Tunaamini kuwa wanawake wanaomiliki biashara ndogo ndogo wakipewa ujuzi wa kutunza fedha pamoja na ujuzi wa kibiashara wanaweza kupata nafasi za kukuza biashara. Kukua kwa mitaji yao ya biashara hakuwanufaishi wao peke yao bali pamoja na familia zao na jamii kwa ujumla,” alisema Mkurugenzi wa TechoServe Tanzania, Dr Alexandra Mandelbaum.

‘Tumefurahi kuona mradi ukifikia hatua hii muhimu, tunapoendelea kutafiti manufaa yanayoweza kuletwa na huduma za akiba kwa simu na mafunzo ya biashara kwa wanawake. Tafiti mbalimbali zinaonyesha kwamba wanawake ni kiungo muhimu kwenye maendeleo ya jamii na mradi huu unaleta mwanya wa kuongeza wigo wa kiuchumi kwa wanawake wanaofanya biashara ndogondogo, kitu ambacho kitaboresha maisha yao hivyo kuwawezesha kuboresha jamii zinazowazunguka’ Aliongea Mark Fraser, Rais wa EMEPTL (ExxonMobil Exploration and Production Tanzania Limited)

Kwa updande wake Afisa mkuu wa huduma za kifedha wa Vodacom Tanzania, Sitoyo Lopokoiyit alisema, “Tunafurahi kushirikiana na wadau wa maendeleo kama Technoserve na ExxonMobil Foundation kuhakikisha kuwa makundi yote kwenye jamii yanaingia kwenye mfumo rasmi wa kifedha kupitia huduma za Vodacom. Ushirikiano huu una mchango mkubwa kwenye juhudi za Vodacom za kuwaleta watanzania wengi karibu zaidi na huduma bora za kifedha’

PROF. MBARAWA AAGIZA BARABARA YA MAKUTANO-NATA KM50 KUKAMILIKA

0
0
Ujenzi wa barabara ya Makutano-Nata KM 50 inayojengwa kwa kiwango cha lami, wilaya ya Butiama, mkoani Mara ukiendelea.



Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maagizo kwa Mhandisi Mshauri Eng. Domicus Mapunda wa Kampuni ya Ujenzi ya Mbutu Bridge JV inayojenga barabara ya Makutano-Nata KM 50 kwa kiwango cha lami mkoani Mara wakati alipokagua mradi huo.


Mhandisi Mshauri Eng. Domicus Mapunda wa Kapuni ya Ujenzi ya Mbutu Bridge JV akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu mradi wa ujenzi wa barabara ya Makutano-Nata KM 50 inayojengwa kwa kiwango cha lami mkoani Mara wakati alipokagua mradi huo.
Kaimu Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Musoma Bi. Faraja akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), ramani ya eneo la kiwanja cha ndege hicho, alipokagua kiwanja hicho mkoani Mara.Muonekano wa barabara ya changarawe ya kuruka na kutua ndege katika Kiwanja cha Ndege cha Musoma.Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Musoma Bi. Faraja kuhusu eneo litaloongezwa kiwanja hicho, mkoani Mara.

………….

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewapa miezi minne Wakandarasi Wazawa wa Kampuni ya Ujenzi ya Mbutu Bridge JV inayojenga barabara ya Makutano-Nata kukamilisha km 18 kati ya 50 za barabara hiyo kwa kiwango cha lami.

Agizo hilo limetolewa na Waziri huyo, alipokuwa akikagua mradi huo wa barabara inayoanzia makutano kupitia Butiama, Nyamuswa hadi Sanzate ambao upo katika mkoa wa Mara, na kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wake ambayo imesuasua kwa takriban miaka 3 sasa.

“Nataka mwezi Aprili mwakani sehemu ya barabara hii iwe imeshakamilika kwa kiwango cha lami na wananchi waanze kufurahia matunda yake, hatuwezi kusubiri kwa muda wote huo kuwavumilia kukamilisha mradi huu”, amesema Prof. Mbarawa.

Amesisitiza kuwa nia ya Serikali ya kuboresha barabara hiyo ni kupunguza gharama za usafirishaji, kuboresha makazi, kukuza uchumi kwa maeneo yaliyo kando ya Barabara hiyo na kuhamasisha utalii kwenye mbuga za Wanyama za Serengeti na Ngorongoro.

Naye, Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Mkoa wa Mara Eng. Japherson Nnko amesema kuwa barabara hiyo itakapomalizika itakuwa na njia ya magari yenye upana wa mita6.5, mabega ya barabara ya mita 1.5 kila upande na Daraja kubwa la Kyarano lenye urefu wa mita 37.5.

Katika hatua nyingine, Serikali imesema itawapa kipaumbele makandarasi wazawa kuweza kushiriki katika mradi wa ujenzi wa reli mpya ya kisasa (Standard Gauge), inayotarajiwa kuanza hivi karibuni katika maeneo mbalimbali nchini.

Aidha, Serikali imewataka Makandarasi hao kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa kwa kuomba zabuni za ujenzi huo na kuziimarisha kampuni zao ikiwemo kuwa na vifaa vilivyo bora ili kupambana na soko la kibiashara na makandarasi wa nje.

Sambamba na hayo, Waziri Prof. Mbarawa amekagua Uwanja wa Ndege wa Musoma na kusema kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha inapanua na kujenga kwa kiwango cha lami uwanja huo hususani njia ya kuruka na kutua ndege kutoka KM 1.6 ya sasa hadi KM 1.8 ili kuruhusu ndege kubwa zenye uwezo wa kubeba abiria 70 kutua katika uwanja huo.

Waziri Prof. Mbarawa amemaliza ziara yake ya siku mbili mkoani Mara ambapo amekukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wizara yake katika Wilaya ya Bunda, Butiama, Musoma Mjini na Serengeti.

Imetolewa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli aungana na wana Parokia wenzake kusali ibada ya Jumapili

0
0

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea komuniyo kutoka kwa Padre Paul Haule wa Kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
1Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa katika Ibada ya Jumapili katika Kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam. wa kwanza kulia kwake ni Dada yake Ester Enock na anayefuata ni Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa. 

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akifuatilia Mahubiri yaliyotolewa na Padre Paul Haule wa Kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akifuatilia Mahubiri yaliyotolewa na Padre Paul Haule wa Kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akizungumza na baadhi ya waumini akiwemo muuza magazeti maarufu Bw. Bonge nje ya Kanisa la Mtakatifu Petro, Oysterbay Jijini Dar es Salaam.

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa nje ya Kanisa la Mtakatifu Petro, Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
 


Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli leo Jumapili ameungana na Wakristo wenzake wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Petro iliyopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam ikiwa ni wiki kadhaa tangu alipougua na kulazwa hospitali.

Akiwa mwenye afya njema na furaha Mama Magufuli aliyekuwa pamoja na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wamesali ibada ya asubuhi katika kanisa hilo na baadaye kusalimiana na waumini nje ya kanisa.

Baada ya kumalizika kwa Ibada, baadhi ya Waumini wa Kanisa hilo wameelezea furaha yao ya kumuona Muumini mwenzao akiungana nao katika ibada na wamemuombea afya njema.

"Nimejisikia furaha sana kumuona Mama Magufuli amekuja Kanisani akiwa na afya njema na uso wa bashasha, na ninamuombea kwa Mungu aendelee kumsimamia" amesema Mama Mabula.

"Nimeshukuru sana kumuona Mama yangu Mama Magufuli, Mwanajumuiya mwenzangu leo Kanisani, huku afya yake ikiwa imetengemaa zaidi, tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu na tunamuombea aendelee kumpigania afya yake izidi kuwa imara" amesema Thomas Simon.

"Kwa kweli siku ya leo kwangu mimi ninafuraha sana kwa kumuona Mama akiwa kanisani, na zaidi Mama wote wawili kwa sababu pia amekuja Mke wa Mhe. Waziri Mkuu, kwa hiyo kwetu sisi ni furaha sana kama Parokia, tunafurahi sana tunaposhirikiana na viongozi wetu" ameongeza Epifania Ngonyani.

Mwezi uliopita Mama Janeth Magufuli aliugua na kulazwa katika wodi ya Sewahaji iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alipata matibabu kwa siku mbili na kisha kuruhusiwa.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWAKUNA WAPINZANI KIKAO CHA MAJUMUISHO ZIARA YA ARUSHA

0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika kikao cha majumuisho ya ziara yake ya mkoa wa Arusha kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha, Desemaba 18, 2016. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika kikao cha majukmuisho ya ziara yake ya mkoa wa Arusha kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha, Desemaba 18, 2016. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo  na kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Arusha, Lekule Laiza.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  Baadhi ya Wenyeviti wa halmashauri  za mkoa wa Arusha wakisikiliza kwa makini hotuba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ya majumuisho ya ziara yake ya mkoa  huo  kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha Desemba 18, 2016. 
 Wabunge wa Arusha wakifuhia hotuba ya majumuisho ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ya kuhitimisha ziara yake ya mkoa huo kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha , Desemba 27, 2016. Kutoka kushoto ni  Mbunge wa Arumeru Magharibi, Gipson Mesiek, Mbunge wa Viti Maalum Amina Mollel na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Baadhi ya Wenyeviti wa halmashauri  za mkoa wa Arusha wakisikiliza kwa makini hotuba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ya majumuisho ya ziara yake ya mkoa  huo  kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha Desemba 18, 2016. 9Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Baadhi ya Wenyeviti wa halmashauri  za mkoa wa Arusha wakisikiliza kwa makini hotuba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ya majumuisho ya ziara yake ya mkoa  huo  kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha Desemba 18, 2016. 9Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari, akionyesha ishara ya kukubaliana na maneno ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipotoa hotuba ya majumuisho ya ziara yake mkoani Arusha kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Desemba 28, 2016. Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum, Amina Mollel.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (kushoto) wakizungumza na Mbunge wa Monduli, Julius Kalanga (wapili kulia) na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Monduli, Isaac Joseph (kulia) baada ya Waziri Mkuu kumaliza kikao cha majumuisho ya ziara yake mkoani Arusha kwenye ukumbi wa Mkuu wa mkoa huo, Desemba 18, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (kushoto) wakizungumza na Mbunge wa Monduli, Julius Kalanga (wapili kulia) na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Monduli, Isaac Joseph (kulia) baada ya Waziri Mkuu kumaliza kikao cha majumuisho ya ziara yake mkoani Arusha kwenye ukumbi wa Mkuu wa mkoa huo, Desemba 18, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (kushoto) wakizungumza na Mbunge wa Monduli, Julius Kalanga (wapili kulia) na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Monduli, Isaac Joseph (kulia) baada ya Waziri Mkuu kumaliza kikao cha majumuisho ya ziara yake mkoani Arusha kwenye ukumbi wa Mkuu wa mkoa huo, Desemba 18, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Meya wa jiji la Arusha,Mstahiki,Kalisti Lazaro  (kulia) baada ya kumaliza mkutano wake wa majumuisho ya ziara ya Arusha kwenye ukumbi wa Mkuu wa mkoa wa Arusha, Desemba 28, 2016.  Wapili kushoto ni Mbunge wa Arumeru Magharibi, Gipson Mesiek na wapili kulia ni Mbunge wa Monduli, Julius Kalanga.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na  Meya wa jiji la Arusha, Mstahiki   KalistiLazaro (wapili kulia) na  wabunge wa upinzani waliohudhuria katika mkuano wake wa ajumuisho ya ziara ya mkoa wa Arusha kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Desemba 28, 2016. Wengine kutoka kushoto ni Mbunge wa Arumeru Magharibi, Gipson Mesiek, Mbunge wa Monduli, Julius Kalanga na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na  Meya wa jiji la Arusha, Mstahiki   KalistiLazaro (wapili kulia) na  wabunge wa upinzani waliohudhuria katika mkuano wake wa ajumuisho ya ziara ya mkoa wa Arusha kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Desemba 28, 2016. Wengine kutoka kushoto ni Mbunge wa Arumeru Magharibi, Gipson Mesiek, Mbunge wa Monduli, Julius Kalanga na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari.

WAZIRI MKUU AUNDA TUME YA KUCHUNGUZA TAARIFA ZA UHAMISHO WA FARU JOHN,AAGIZA KABURI LAKE LITAFUTWE.

0
0
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imeunda tume kuchunguza taarifa inayoelezea utaratibu uliotumika kumhamisha faru John kutoka Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Sasakwa Black Rhino Sanctuary iliyoko kwenye Hifadhi ya Grumeti Serengeti pamoja na kutafuta kaburi la faru huyo.

Amesema timu hiyo ya wataalamu tayari imeshafika Sasakwa  VIP Grumet kwa ajili ya kutafuta kaburi na kuchukua vinasaba vya masalia ya faru John na kisha watakwenda kwenye Hifadhi ya Ngorongoro kuchukua vinasaba vya watoto wake  na kuvilinganisha na pembe hiyo ili  kubaini kama kweli pembe aliyopelekewa ni  ya faru John au laa.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumapili, Desemba 18, 2016) wakati wa majumuisho ya ziara yake ya kikazi mkoani Arusha. Ziara hiyo ililenga kukagua utekelezaji wa shughuli za maendeleo na kuona utoaji wa huduma kwa wananchi. 

"Tume niliyounda kwa ajili ya uchunguzi wa faru John imetua VIP  Grumet Serengeti kujiridhisha kama kuna kaburi la faru John na kama lipo wachukue vinasaba na baada ya hapo watakwenda Creter na kuchukua vinasaba vya watoto wa faru John na kuvipima kwa pamoja. Lengo ni kutaka kubaini kama pembe iliyowasilishwa kwangu Disemba 9 mwaka huu ni ya faru John,” amesema.

Waziri Mkuu amesema wakati faru John akiwa V I P Grumet taarifa zilisema ni mgonjwa na daktari alipompima mara ya kwanza akabaini faru huyo hakuna na ugonjwa wowote.”Daktari alimpima tena kwa mara ya pili taarifa zikasema tena si mgonjwa  ghafla wakasema amekufa. Hili  haliwezekani,”.

Waziri Mkuu amesema ameiagiza timu hiyo kufanya kazi ya uchunguzi wa taarifa hizo kikamilifu kwa sababu Serikali imetumia fedha nyingi kuwaleta faru hao kutoka nchini Afrika Kusini. Ni lazima nyara hizo za Serikali zilindwe kwa manufaa Taifa. 

Waziri Mkuu alipokea taarifa inayoelezea utaratibu uliotumika kumhamisha faru John kutoka Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Sasakwa Black Rhino Sanctuary iliyoko kwenye Hifadhi ya Grumeti Desemba 9, 2016 katika kikao kilichofanyika kwenye makazi ya Waziri Mkuu Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe na baadhi ya watendaji wa wizara yake, Baada ya kupokea taarifa hiyo Waziri Mkuu alisema taarifa hiyo itafanyiwa kazi na wataalamu wa ofisi yake.Akisoma taarifa hiyo mbele ya Waziri Mkuu, Prof. Maghembe alisema hadi kufikia Desemba 2015 wakati faru John anahamishwa alikuwa na watoto 26 (sawa na asilimia 70.2) ya faru wote waliokuwepo ndani ya kreta. 

“Kati ya faru 37 waliokuwepo ndani ya kreta, watoto wake walikuwa 26 sawa na asilimia 70.2. Uamuzi wa kumuondoa John ulikuwa ni muhimu ili kuwezesha kuongezeka kwa faru weusi na kupunguza tatizo la ‘inbreeding’ ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro,” alisema Waziri Maghembe. Baada ya kuhamishiwa Sasakwa, Waziri Maghembe alisema Julai 10, 2016 afya ya faru John ilianza kudorora na alikufa tarehe 18 Agosti, mwaka huu.

 Taarifa hiyo iliandaliwa na Kamati ya Taifa ya Kuwalinda Tembo na Faru. Kamati hiyo inaundwa na Mkurugenzi Mkuu wa TAWIRI, Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Mkurugenzi Mkuu wa NCAA na Mhifadhi Mkuu wa Ngorongoro.

 Akikabidhi pembe za faru huyo mbele ya Waziri Mkuu, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Kupambana na Ujangili wa Wanyamapori, Bw. Robert Mande alimweleza kwamba pembe kubwa ya faru John ilikuwa na uzito wa kilo 3.6 na pembe ndogo ilikuwa na uzito wa kilo 2.3.

Desemba 6, mwaka huu, akiwa ziarani mkoani Arusha, Waziri Mkuu aliuagiza uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), umletee nyaraka zote zilizotumika kumhamisha faru maarufu kwa jina la ‘John’ kutoka kwenye hifadhi hiyo ifikapo Alhamisi, Desemba 8.

Alitoa agizo hilo alipotembelea ofisi za makao makuu ya NCAA zilizoko wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha na kuzungumza na watumishi wa mamlaka hiyo pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wafugaji ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani humo.


IMETOLEWA NA:                                                         
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, DESEMBA 18, 2016.  

Newz Alert:Msanii Darassa na wenzake wanusurika kifo baada ya kupata ajali kahama,mkoani Shinyanga.

0
0


 Baadhi ya Wananchi wakilitazama gari hilo baada ya kupata ajali
Muonekano wa gari alilopata nalo ajali Msanii huyo na Wenzake,
Habari zilizoifikia Globu ya Jamii hivi punde zinaeleza kuwa Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo ambaye ametokea kutikisa kwa kiasi kikubwa kupitia ngoma yake kali ya Muziki, Sharrif  Thabit ‘Darassa’ amenusurika kifo baada ya kupata ajali mbaya maeneo ya Ntobo barabara ya kuelekea Mgodi wa Bullyanhulu Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Habari zimeeleza kuwa ndani ya gari hilo aina ya Toyota Harrier yenye namba za usajili T503 DGQ, ambalo dereva hakufahamika mapema, Darassa alikuwa ameambatana na Director wake, Hanscana pamoja na producer wake, Abba Process na wote wametoka salama.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Darassa amethibitisha kupata ajali hiyo, na kama aonekanavyo kwenye hiyo clip ya video sehemu ya tukio ya ajali hiyo akimshukuru Mungu kwa kutoka salama yeye pamoja na wenzake. 

Chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana mpaka sasa.

MSIMAMO WA LIGI

0
0

WAZIRI LUKUVI ATUA MKOANI MARA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI

0
0
Na Hassan Mabuye .

(Kitengo cha Mawasiliano - Wizara ya Ardhi)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi anaendelea na Ziara zake za utatuzi wa Migogoro ya Ardhi nchini, ambayo imejikita zaidi katika kutatua migogoro ya ardhi ya Mikoa ya kanda ya Magharibi, Kaskazini na ile ya Kanda ya Ziwa hapa nchini.

Mhe. Lukuvi kwa siku ya jumatatu tarehe 19 Desemba 2016 atatua migogoro ya ardhi ya wilaya ya Musoma mkoani Mara na siku ya jumanne tarehe 19 Desemba 2016 atatua migogoro ya ardhi ya wilaya ya Bunda mkoani Mara.

Katika ziara hiyo Waziri Lukuvi atakutana na wananchi wa Musoma mjini na wananchi wa Bunda walio na kero za migogoro ya ardhi na kuzitatua pamoja na kutembelea miradi inayosimamiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika wilaya ya Musoma.

Aidha, Mhe. Lukuvi baada ya ziara hiyo anatarajiwa kuwasili mkoani Arusha ambapo pia atatua migogoro ya ardhi inayoukabili mkoa huo.
Hadi sasa Mhe. Lukuvi ndani ya mwezi huu wa Desesmba ameishatatua migogoro ya ardhi ya Mkoa wa Kigoma na wilaya zake za Kigoma mjini, Kasulu na Kibondo na katika Mkoa wa Shinyanga na wilaya zake za Kishapu na Shinyanga mjini na katika mkoa wa Geita amefanya ziara wilayani Chato.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiongea na wananchi walio na migogoro ya ardhi wakati wa ziara zake mikoani.
Muonekano wa Halmashauri ya Musoma Mjini.

Zanzibar na kampuni ya ZTE ya China zimetiliana saini Mkataba wa ushirikiano katika uendelezaji wa miradi

0
0
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi (kushoto)  na Rais wa Kampuni ya ZTE ya Mji wa Shengzhen Nchini China Bwana Zhang Rejun kulia wakitia saini Mkataba wa ushirikiano katika uendelezaji wa miradi itakayotumia mfumo wa Teknolojia ya Kisasa ya Mawasiliano  Makao Makuu wa ZTE Mjini Shengzhen China.
 Balozi Seif kushoto akibadilishana hati na Rais wa ZTE Bwana Zhang Rejun baada ya kutia saini Mkataba wa Ushirikiano wa uendelezaji wa miradi itakayotumia mfumo wa Teknolojia ya Kisasa ya Mawasiliano.
Mtaalamu wa Ufundi wa Kampuni ya ZTE Bibi Radhika Devi wa kwanza kutoka Kushoto akimkaguza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif na Ujumbe wake katika vitengo mbali mbali ndani ya Makao Makuu ya  Kampuni hiyo Mjini Shengzheng. Kushoto ya Balozi Seif ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Mh. Mohamed Ahmed Salum na Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bibi Asha Ali Abdulla.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Kampuni ya Kimataifa ya Mitandao ya Kisasa ya Mawasiliano ya ZTE ya Mji wa Shengzhen Nchini Jamuhuri ya Watu wa China zimetiliana saini Mkataba wa ushirikiano katika uendelezaji wa miradi itakayotumia mfumo unaokubalika Kimataifa kwa hivi sasa.

Miradi hiyo itakayotumia  mfumo waTeknolojia ya Kisasa { TEHAMA } ni pamoja na Mradi wa Mawasiliano Serikalini { E Goverment } huduma za umeme, usafiri, miji mipya, afya pamoja na huduma za Kijamii ikiwemo utaratibu wa udhibiti wa ukusanyaji wa Mapato ya Serikalini.

Saini ya Mkataba huo imetiwa na Rais wa Kampuni ya ZTE Bwana Zhang Rejun wakati upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ambaye yuko Nchini China kwa ziara rasmi ya Kiserikali ya siku Tano.

Akizungumza na Uongozi wa Kampuni hiyo ya ZTE kwenye Makao Makuu yake Mjini Shengzhen Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Zanzibar inaendelea kuipa fursa zaidi Kampuni ya ZTE katika mtazamo wake wa miradi ya maendeleo inayotarajia kuanzisha hapo baadaye.

Balozi Seif alisema hatua hiyo ya Serikali imekuja kutokana na Uongozi wa juu wa Kampuni ya ZTE kuonyesha juhudi kubwa za kuendelea kuunga mkono harakati za kuimarisha miradi ya Maendeleo zinazotekelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliishukuru na kuipongeza Kampuni ya ZTE kwa kasi kubwa ya uwajibikaji wa watendaji wake  katika mfumo wa Teknolojia ya kisasa ya mawasiliano unaoonekana kukubalika na Mataifa mengi Duniani zikiwemo pia Nchi za Bara la Afrika.

Balozi Seif aliutolea mfano mradi Mkubwa  wa mawasiliano Serikalini                      {E Goverment } ambao ulisimamiwa na Kampuni hiyo kwa upande wa Zanzibar ukikamilika katika awamu ya kwanza.

Viewing all 46193 articles
Browse latest View live




Latest Images