Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46194 articles
Browse latest View live

WALIOUZA KIWANJA CHA SHULE WACHUKULIWE HATUA-MAJALIWA

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Bw. Rashid Taka na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw. Raphael Siumbo kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua watendaji wote watakaobainika kuhusika katika uuzwaji wa kiwanja cha shule ya msingi Waso.

Ametoa agizo hilo jana jioni (Alhamisi, Desemba 15, 2016) wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kata ya Waso Wilaya ya Ngorongoro akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Arusha.

Waziri Mkuu alisema Serikali haiwezi kuvumilia kuona watendaji wachache wasiokuwa waadilifu  wanamega kiwanja cha shule na kukiuza kwa maslahi yao, hivyo aliwataka viongozi hao kufuatilia na kumpa taarifa ya hatua za kisheria walizochukua kwa wahusika.

“Mkuu wa wilaya na Mkurugenzi hapa kuna malalamiko ya viwanja fuatilieni viwanja hivyo vinavyolalamikiwa na wananchi ni viwanja gani je hiyo ya kwamba mmeuza viwanja vya shule ameuziwa nani,” alisema.

Aidha, Waziri Mkuu amemtaka Bw. Taka ahakikishe Mkuu wa Idara ya 
Ardhi, Maliasili na Mzingira, Bw. Switbeth Byorushengo anatekeleza majukumu yake ipasavyo. Ametoa agizo hilo baada ya wananchi kudai Ofisa huyo ameshindwa kufanya kazi na kumuomba Waziri Mkuu aondoke naye.
Alisema Bw. Byorushengo anatakiwa kuhakikisha halmashauri hiyo inapima viwanja vya kutosha na kutoa hati kwa wananchi ili waweze kupata maeneo ya kujenga makazi na shughuli zingine za kijamii.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alimuagiza Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Bw. Byorushengo kuhakikisha halmashauri hiyo inaanza ujenzi wa hospitali ya wilaya na ifikapo Aprili, 2017 awe amepewa taarifa za ulipofikia ujenzi huo.Kwa upande wake Mkurugenzi huyo alisema tayari wapo katika mchakato wa ujenzi wa hospitali ya wilaya ambapo wametenga sh. milioni 800 za kuanzia.

Akizungumzia kuhusu mgogoro wa ardhi kati ya vijiji vya Tarafa ya Loliondo na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Waziri Mkuu alitoa muda wa siku 30 kwa uongozi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Nchini (TANAPA) wawe wamekamilisha uhakiki wa mpaka huo.

Naye Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi ambaye ni Mbunge wa Ngorongoro Mheshimiwa William Ole Nasha alimuomba Waziri Mkuu kuwasaidia kutatua mgogoro huo wa ardhi kwa kuwa ni wa muda mrefu na unakwamisha shughuli za maendeleo.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Bw. Mrisho Gambo alisema Wilaya ya Ngorongoro inachangamoto nyingi ikiwemo ya ardhi na sasa kuna mgogoro kati ya Kampuni ya Thomson Safari na wananchi ambao wanadai kuwa ardhi hiyo ilichukuliwa kinyemela na mwekezaji huyo bila ya wao kushirikishwa.

Alisema baada ya ziara ya Waziri Mkuu kumalizika mkoani hapa atarudi wilayani Ngorongoro kwa ajili ya kutatua kero mbalimbali ikiwemo ya ardhi na matumizi mabaya ya fedha zinazotolewa na wawekezaji ambazo matumizi yake hayajulikani.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, DESEMBA 16, 2016. 

DARASA: SINA UGOMVI NA SAIDA KAROLI

0
0


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Mwanamuziki wa muziki wa kufokafoka (Hip Pop) nchini, Darasa amekana kuwa yeye amewahi kukutana na msanii wa muziki wa asili utoka mkoani Kagera, Saida Karoli na kuzungumza nae biashara yoyote ya muziki.

Darasa amesema hayo alipokuwa akizungumza na kituo kimoja cha habari hapa nchini na kusema wimbo wake sio wa midundo ya Saida Karoli bali ni midundo ya kitamaduni la kabila la kihaya.

“Midundo ya muziki na Saida Karoli ni vitu viwili tofauti hivyo mtayarishaji wangu Abba kapiga kwa hisia zake lakini mtu mmoja akasema kwanini tusimshirikishe saida karoli kwa kuwa yeye ni mtu wa huko huko lakini hilo alikufanikiwa” Amesema Darasa.

Amesema kuwa mtu anatakiwa kuchukua midundo ya Saida karoli na kusikiliza marimba yaliyopigwa katika wimbo wangu wa muziki na kuona tofauti.

Ameongeza kuwa mara baada Diamond kutoa wimbo wa Salome ndipo wazo la kumshirikisha Saida Karoli likafa hivyo ndio akajitokeza, Ben Paul na yeye kama msanii mkubwa kaamua kuitendea haki nyimbo ndio mnaona leo Baraka za nyimbo kukubarika kila mtu.

Amemaliza kwa kusema kuwa anamshukuru mungu kwa kuwezesha wimbo huo kupenya kila mahali hasa kwa kuvunja rekodi kwa kuwa wimbo wa kwanza wa muziki wa kufokafoka kuweza kuchezwa mpaka kwenye Kitchen Paarty.

NEWZ ALERT:RAIS MAGUFULI ATENGEUA UTEUZI WA MKURUGENZI MKUU WA NIMR DKT. MWELE MALECELA

0
0
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR) Dr Mwele Malecela

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI DESEMBA 17, 2016

0
0

SIMBACHAWENE AFAFANUA AGIZO LA RAIS MAGUFULI KUHUSU 'WAMACHINGA

0
0
Serikali imewaagiza Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Mamlaka ya Serikali za Mitaa wameagizwa kuhakikisha wanatekeleza agizo la Rais Dk.John Magufuli la kuwatafutia maeneo ya kufanyia biashara Wafanyabiashara ndogo ndogo ‘wamachinga’ na si kuwaacha wafanye biashara zao kiholela.

Kauli hiyo ilitolewa leo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), George Simbachawene alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma.

Amewataka wakuu hao kuwawekea Wamachinga utaratibu wa kupangiwa maeneo ya shughuli zao yenye wateja wa kutosha, miundombinu rafiki na washirikishwe katika michakato yote wakati wa maandalizi ya maeneo hayo.

Amefafanua kuwa Rais Magufuli alisitisha zoezi la kuwaondoa kiholela wamachinga kutoka katika maeneo wanayofanyia biashara zao kwasasa hadi pale mamlaka husika zitakapoandaa maeneo maalum kwa ajili yao.

“Maagizo ya Rais yameonesha namna anavyowapenda na kuwathamini wamachinga na aliweka msisitizo wasiondolewe mpaka pale yatakapotengwa maeneo mbadala,”amesema Simbachawene.

Amebainisha utaratibu wowote wa kuwapangia maeneo mapya uzingatie ushirikishwaji ili kuondoa msuguano wakati wa kuwahamisha na kwamba pale inapowezekana wapangiwe maeneo ya katikati ya mji ikibidi kuteua mitaa mahsusi kwa utaratibu utakaowekwa ili wafanye biashara zao.

Pamoja na maelezo hayo, Simbachawene amesema Rais alisisitiza kwamba maagizo yake juu ya wamachinga hayana maana kuwa kwasasa wamachinga wafanye biashara zao kwenye barabara za kupita magari na watembea kwa miguu au kwenye hifadhi za barabara.

Amewasisitiza wakuu hao kujipanga kutekeleza maagizo ya rais kwa ufasaha, weledi na umakini mkubwa ili kuwasaidia wamachinga kufanya biashara zao na kujipatia kipato na kuzitaka mamlaka za serikali kuheshimu shughuli zao.

Wakati huo huo, Simbachawene amewaagiza Makatibu Tawala wa Mikoa ya Rukwa na Arusha watafute shule ndani ya mikoa yao na kuwapanga wanafunzi ambao wameondolewa shule za sekondari Makuyuni na Milundikwa ambazo majengo yake yamerudishwa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT).
Amesema serikali imelazimika kuwaondoa wanafunzi 254 wa shule ya Makuyuni wa kidato cha kwanza hadi cha tatu na katika shule ya Milundikwa wanafunzi 120 wa kidato cha tano na sita.

Pia amesema walimu na watumishi wasio walimu ambao walikuwa wakifundisha katika shule hizo wapangiwe kwenye shule watakazopelekwa wanafunzi hao.

Ametaka utekelezaji huo wa agizo hilo ufanyike kabla shule hazijafunguliwa januari 2017 na lizingatie kutowavuruga wanafunzi wa kidato cha sita ambao tayari wamesajiliwa kufanya mtihani wa Taifa mwezi mei, 2017.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene  akitoa ufafanuzi kwa Umma kuhusu agizo alilolitoa Rais Dkt John Magufuli  hivi karibuni juu ya kusitisha zoezi la kuwahamisha Wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu Wamachinga, kulia kwake ni Mkurugenzi Idara ya Tawala za Mikoa TAMISEMI Susan Chekani na kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI (Afya) Dk. Zainab Chaula.

VODACOM NA TECNO WAWALETEA PHANTOM 6 NA TECNO PHANTOM 6+ KWA BEI NAFUU

0
0
Kaimu Mkurugenzi wa  Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Domician Mkama (katikati) akionyesha moja ya simu za Tecno Phantom 6 na Tecno Phantom 6+, kwenye hafla ya  uzinduzi wa simu hizo uliofanywa kwa Ushirikiano wa Tecno Mobile Tanzania jijini Dar es Salaam leo Desemba 16, 2016. Kushoto ni Afisa Mauzo Mwandamizi wa Tecno Mobile  Tanzania, William Motta na kulia ni Mkuu wa Bidhaa wa Vodacom Tanzania, Samson Mwongela. 
  Kaimu Mkurugenzi wa  Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania, Domician Mkama (katikati) akizungumza na waandishi wa habari  huku akionyesha moja ya simu za Tecno Phantom 6 na Tecno Phantom 6+, kwenye hafla ya  uzinduzi wa simu hizo uliofanywa kwa Ushirikiano wa Tecno Mobile Tanzania jijini Dar es Salaam leo Desemba 16, 2016. Kushoto ni Afisa Mauzo Mwandamizi wa Tecno Mobile  Tanzania, William Motta na kulia ni Mkuu wa Bidhaa wa Vodacom Tanzania, Samson Mwongela.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na Tecno Mobile  Tanzania ,wakionyesha simu aina ya Tecno Phantom 6 na Tecno Phantom 6+ zilizopo kwenye maboksi, wakati wa hafla ya uzinduzi wa simu hizo  jijini Dar es Salaam leo Desemba 16,2016.

BANDARI TANGA YAIFUNGA MTWARA MABAO 43-16 MCHEZO WA PETE KATIKA MICHUANO YA BANDARI

0
0
Wachezaji wa timu za Bandari ya Dar es Salaam  na Makao Makuu wakichuana kwenye mchezo wa mpira wa kikapu uliochezwa kwenye uwanja wa Bandari Tanga ambao ulimalizika kwa Bandari Dar kuibuka na ushindi wa vikapu 50 -47
 Wachezaji wa timu za Bandari ya Dar es Salaam  na Makao Makuu wakichuana kwenye mchezo wa mpira wa kikapu uliochezwa kwenye uwanja wa Bandari Tanga ambao ulimalizika kwa Bandari Dar kuibuka na ushindi wa vikapu 50 -47
 Wachezaji wa kuvuta kamba timu ya Bandari ya Tanga wakichuana dhidi ya Makao Makuu mchezo umalizika kwa Tanga kuibuka na ushindi wa seti 2-0 mchezo uliochezwa viwanja vya Shule ya Sekondari Popatlaly mjini Tanga
TIMU ya Mpira wa Pete ya Bandari ya Tanga leo wameweza kuibuka na ushindi wa mabao 43-16 dhidi ya Bandari ya Mtwara kwenye michuano ya Bandari inayoendelea mjini Tanga.

Mchezo huo ambao ulichezwa kwenye viwanja vya Bandari mjini hapa ambapo mpaka timu zote zinakwenda mapumziko Bandari Tanga ilikuwa ikiongozwa kwa mabao 23 -17 dhidi ya Mtwara.

Halikadhalika Tanga wakiweza kuibuka pia na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Makao  Makuu kwenye mchezo wa mpira wa miguu uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya sekondari Popatlaly mjini hapa.Katika mchezo mwengine uliochezwa kwenye uwanja huo timu ya Bandari ya Dar es Salaam iliweza kuibuka na ushindi dhidi ya Makao Makuu kwa mabao 36-13.

Wakati huo huo,Timu ya Bandari ya Dar es Salaam imeweza kuibuka na ushindi wa vikapu 50 -47 dhidi ya Makao Makuu kwenye mchezo wa mpira wa kikapu uliochezwa kwenye dimba hilo la Bandari mjini hapa.

Kwenye mchezo mpira wa miguu uliozikutanisha Bandari Mtwara na Maziwa Makuu ambapo timu hizo mpaka dakika 90 zilijikuta zikigawana pointi moja moja baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1.Ili kuonyesha wana umahiri mkubwa kwenye michezo Bandari Tanga wanaume waliweza kuibuka na ushindi wa seti 2-0 dhidi ya Makao Makuu kwenye mchezo wa kuvuta kamba.

Wakati wanaume wakiibuka na ushindi huo wanawake nao waliweza kuwaunga mkono wenzao kwa kuibuka na ushindi wa seti 2-0 dhidi ya Makao makuu kwenye mchezo wa kuvuta kamba uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Popatlaly.

Mashindano hayo ambayo yalifunguliwa jana na Mkurugenzi wa Bandari nchini (TPA) Deusdedit Kakoko ambaye aliwataka wanamichezo hao kuzingatia nidhamu na maarifa kwenye michezo yao ili kupata ushindi.

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

Namna ya kuepuka matumizi makubwa ya fedha kipindi cha sikukuu

0
0

 Na Jumia Travel Tanzania

Kwa kawaida kipindi cha sikukuu ni wakati ambao watu wengi huwa na matumizi makubwa ya fedha kwa ajili ya kusherehekea pamoja na wapendwa wao, famila, jamaa na marafiki.

Jumia Travel (www.travel.jumia.com) ingependa kukushauri kwamba ni vema ukawa na mpango madhubuti unaoeleweka wa namna gani pesa yako itakavyotumika ili pindi mwaka mpya utakapoingia uwe mwenye furaha na sio huzuni. 

Tenga bajeti mapema.

Kuna namna nyingi za kutenga bajeti kwa ajili ya matumizi yako kama vile manunuzi ya zawadi kwa watoto, wazazi, kutoa msaada pengine na mengineyo ndani ya nyumba. Endapo utapanga mapema itakusaidia sana kujua utahitajika kutumia kiasi gani kipindi hiki badala ya kukurupuka sikukuu zinapowadia.

Fuatilia mwenendo wa matumizi yako.

Kutenga bajeti pekee tu haitoshi bila ya kuwa na mbinu sahihi ya kufuatilia mwenendo mzima wa jinsi pesa inavyotumika. Tenga pembeni bajeti ya sikukuu kwa kufungua akaunti ya benki ili isiingiliane na ya matumizi ya kawaida. Unaweza kutumia mbinu mbalimbali kuhakikisha unafanikiwa katika hili, kwa mfano kuwa na programu ya simu, ambayo utakuwa unaweza kufuatilia kwa ukaribu mwenendo wa matumizi na kiasi cha pesa kilichobaki popote na muda wowote ulipo.

Punguza matumizi yasiyokuwa na tija.

Unaweza kuepuka au kupunguza matumizi ambayo si ya lazima ndani ya kipindi hiki ili kufidia gharama kwenye vitu vingine. Kwa mfano, kama ulikuwa na mazoea ya kwenda na familia yako kwenye hoteli ya kifahari kwa ajili ya mapumziko kila wikendi pengine gharama yake ni TSHS 100,000/- kwa wiki ambayo ni sawa na TSHS 400,000/- kwa mwezi, unaweza kuacha kwa mwezi huu ili kuitumia kwa mambo mengine.

Pendekeza utaratibu wa kununuliana zawadi kwa siri.

Kwa bahati mbaya familia nyingi za kiafrika sio wenyeji wa utamaduni huu wa kununuliana zawadi kwa siri au ‘Secret Santa’ kama inavyojulikana kwa lugha ya Kiingereza.  Mbinu hii ina manufaa makubwa sana kama utataka kuepuka gharama kubwa za kumnunulia zawadi kila mwanafamilia, kwa mfano, pengine una baba, mama, kaka, dada, binamu, wajomba na mashangazi unaweza ukautambulisha utaratibu wa kila mtu kumnunulia zawadi mwenzio kwa siri na kumkabidhi siku ya sikukuu. Nadhani inaweza kuleta msisimko zaidi na kila mtu akafurahia.

Epuka mila zitakazokugharimu
Kuna baadhi ya makabila bado yana taratibu ambao huwalazimu wanakoo kukutana kwa pamoja ifikapo kila mwisho wa mwaka. Watu hulazimika kusafiri na kutumia gharama kubwa kwa karamu ambazo huandaliwa na kujikuta mwaka unaanza wakiwa hawana fedha za kutosha. Unaweza kuepuka hayo yote kwa kufanya vitu vya kawaida ambavyo familia yako itavifurahia na kuvipenda.

Kuwa mwangalifu na ofa za mauzo.

Inabidi kuwa makini sana na ofa zinazotolewa na wauzaji wa bidhaa mbalimbali ndani ya kipindi hiki cha sikukuu. Wafanyabiashara ni werevu sana kwani hutumia mbinu mbalimbali za kuuza bidhaa zao kwa kuweka mabango makubwa ya ‘Ofa Ofa!’ huku bei ikiwa ni ileile sawa na siku za kawaida. Kuepuka hili unapaswa kufanya tafiti mapema kwa kutembelea maduka au mitandao ili kujua kama ni kweli kuna unafuu kwenye hizo bei zinazotangazwa.

Jitahidi kutokuzidisha manunuzi yako.

Kutokana na ofa kemkem ndani ya kipindi hiki cha sikukuu wateja wengi hujikuta njia panda kwa kushindwa kujizuia kuzidisha manunuzi wanayoyafanya. Inashauriwa kuwa na orodha pamoja na bajeti ya vitu unavyotaka kwenda kuvinunua ili pindi umalizapo usizidishe kwa kutamani vingine. Kama ikiwezakana fanya manunuzi mapema kabla ya sikukuu yenyewe ambapo kutokana na punguzo kubwa la bei ukajikuta unataka kununua kila bidhaa.

Mwisho kabisa Jumia Travel (www.travel.jumia.com) inakukumbusha kufanya tathmini ya pesa na matumizi uliyoyafanya ili kujua kama ulikuwa ndani ya bajeti kama ulivyojipangia au la. Kwa kufanya hivyo, utakuwa na mkakati mzuri wa kuanza mwaka mpya bila ya msongo wa mawazo. 

How to avoid over budgeting during the festivities

0
0

By Jumia Travel Tanzania

Usually, the festive season is a time when most people spend a lot of money for travelling, shopping, and buying gifts for their loved ones, family, and friends.

Jumia Travel (www.travel.jumia.com) would like to give you a piece of advice on how to plan your festivals effectively, in order to start the New Year with a smile rather than a panic.

Set aside your budget
There are various ways to plan your festive budget for expenditures such as for buying gifts, shopping or a charitable donation. It is advisable to have a prior plan or a list of items and their respective budget instead of waiting until the actual days of festivals.

Track your expenditures
To set aside a budget is not enough unless you establish a close tracking system of expenditures so as to be aware on how your money is spent. This also can be attained by having a separate bank account for a festive season apart from your current one. To facilitate easy tracking you are advised to install bank programs on your mobile phone or have an excel sheet that you will be able to get access to wherever and whenever you are.    

Cut-down unnecessary expenses
If you had a tendency of taking out your family every weekend, maybe for a swim or cinema you can stop at least on this month and instead use that money on other issues such as buying gifts, shopping or decorating the house during this festive season.

Introduce a ‘Secret Santa’
Unfortunately, most African families are not familiar with ‘Secret Santa.’ This technique could save you with some expenses if you will try to introduce it into your family. Let’s say there are a couple of family members and each of them buy a gift for his/her ‘Secret Santa’ such as parents, grandparents, sisters, brothers, cousins, in-laws, and neighbors. You will cut down costs by avoiding buying gifts to all members of the family and turn the moment to be very exciting and memorable.

Avoid costly traditions
There are still some of the tribes embrace a tradition that requires family members to gather every end of the year and throw a spectacular party. Therefore, people incur costs to travel with their families. To avoid this situation, you can do simple things to your family and they will be very delighted.

Be careful with sales offers
You have to be extra-careful with the sales offers during this festive season. Sales persons are very clever when it comes to push sales under the ‘Sales Discount’ taglines. Those tricks might entice you to purchase a lot of products unwillingly, so make sure you know what you are going to buy when you visit a shop.  

Try not to exceed your shopping
Festive season is the time when most customers find themselves at purchasing dilemmas, whereby there are thousands of sales offers targeting them in every shopping mall they enter. You are advised to have a list of items you want to buy as well as their respective budget and if possible do a shopping before the actual festive days if you know that you will not be able to control yourself from more buyings.

Lastly but not least, Jumia Travel (www.travel.jumia.com) would like to advise you to do an evaluation on the purchases you make during the entire festive season, so as to determine if you operated under the set budget or if you exceeded. This will help you to know if you will start a new year with a smile or some debts to clear.

KAMPUNI YA NAMAINGO KUGAWA SUNGURA 600 KWA WAJASIRIAMALI DAR

0
0
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Namaingo Business Agency, Biubwa Ibrahim (kulia0 na Meneja Mradi wa Sungura wa kampuni hiyo, Amos Misinde wakionesha kwa wanahabari, Dar es Salaam jana,  baadhi ya sungura 600 zitakazogawiwa leo kwa Wajasiriamali 2000. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)


Na Richard mwaikenda
KAMPUNI ya Namaingo, kugawa sungura 600 kwa Wajasiriamali 2000 Dar es Salaam leo, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa nchini.

Mpango huo ulitangazwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Namaingo Business Agency, Biubwa Ibrahim katika mkutano na waandishi wa habari eneo la mradi huo wa Sungura eneo la Majohe, Dar es Salaam jana.

Alisema kuwa walengwa watakaonufaika na mradi huo, ni Wakulima  3000 waliojiunga katika vikundi vya ushirika 30 kutoka katika wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam ambapo kila kikundi kina wakulima 50.

Biubwa alisema  kwa kuanzia ni vikundi 20 vya ushirika vyenye Wajasiriamali 2000 ndiyo watakaogawiwa sungura leo na wengine 1000 watafuata baada ya sungura hao kuzaliana. Kila kikundi kipatiwa sungura wazazi 27 na dume watatu.

"Hadi sasa tuna vikundi  30 vya ushirika, tutaanza mradi na vikundi 20 vitakavyopatiwa sungura kama mbegu ya kuzalisha kwa ajili ya kupatiwa vikundi vingine 10 vilivyobakia," alisema Biubwa. 

Alisema kuwa ndani ya miezi mitano sungura wazazi 540 watakuwa wamezaa mara tatu, hivyo kuwa na watoto 9,720. Jumla hiyo inatokana na kila sungura mzazi mmoja kuzaa watoto 6.

Alisema mpango utakaofuata ni kila mwanachama kugawiwa sungura 8 kwa ajili ya kuendeleza ufugaji na kupata kipato kitakachosaidia katika maisha yao.

Akielezea faida ya ufugaji wa sungura, Meneja wa Mradi huo, Amos  Misinde alisema kuwa nyama ya sungura inahitajika sana na kwamba hadi sasa zinahitajika tani 5 za nyama hiyo kwa wiki. Sungura wakifugwa kwa uangalizi mzuri mmoja anaweza kufikisha uzito wa kilo 8 ambapo kilo moja ya nyama ni sh. 8,500.

Wanahabari walipata wasaa wa kutembezwa kwenye mabanda kuwaona sungura hao walioingizwa nchini wiki hii kutoka Kenya.
Sungura hao wapo chini ya uangalizi wa watalaamu kutoka Rabbit Republic ya Kenya, Suma JKT na Namaingo Business Agency pamona na watalaam wengine kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA).




 Biubwa akimwingiza mmoja wa  sungura kwenye banda eneo la Majohe, Gongo la Mboto, Dar es Salaam
 Biubwa akifafanua jambo mbele ya wanahabari alipokuwa akielezea kuhusu mradi huo
 Wanahabari wakisikiliza kwa makini wakati Biubwa akizungumza nao
 Meneja Mradi wa Sungura wa Kampuni ya Namaingo, Amos Misinde akionesha sungura waliokwenye mabanda tayari kuwagawia wajasiriamali leo
 Mabanda yenye sungura
 Sungura wanaosubiri kuwekwa kwenye mabanda
 Sungura akila majani
 Meneja Masidizi wa Mradi wa Sungura, Denis Rugezia akiwa na sungura tayari kumpanga kwenye moja ya mabanda
 Mmoja wa wafanyakazi akiwapeleka sungura kwenye mabanda. Sungura hao wamewasili kutoka Kenya.

 Mtaalamu kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA), akiwanesha wanahabari sungura dume
 Mmiliki wa Kamanda wa Matukio Blog, Richard Mwaikenda akiangalia mabanda yenye sungura
 Mmiliki wa Bongo weekend blog Khadija Kalili akikagua mabanda hayo
 Mmoja wa wanufaika wa mradi huo akiwa kwenye mabanda hayo
Makao Makuu ya Mradi wa Sungura eneo la Majohe, Dar es Salaam.

SERIKALI MKOANI SIMIYU YAAGIZA SHULE ZA SERIKALI KUTUMIA CHAKI ZINAZOTENGENEZWA MASWA

0
0

Na Stella Kalinga, Simiyu.

Serikali Mkoani Simiyu imeagiza Shule zote za Serikali Mkoani humo kuhakikisha kuwa ifikapo Januari 09 mwaka 2017 zinatumia Chaki zinazotengenezwa Wilayani Maswa.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka wakati wa ziara yake aliyoifanya  wilayani Maswa kwa lengo la kukagua ujenzi wa Miundombinu ya shule  ikiwa ni pamoja na vyumba vya madarasa.

“Kuanzia Januari 09 mwakani shule zitakapofunguliwa Wakuu wa Shule, Walimu wakuu na Wazabuni wanaofanya kazi na shule za  Serikali  wahakikishe wananunua chaki zinazotengenezwa na Vijana wa Wilaya ya Maswa. Haya ni maelekezo na hayajadiliki”, alisema Mtaka.

Mtaka amewataka Wananchi Mkoani Simiyu kujenga utamaduni wa kupenda na kuthamini vitu au bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.
Mkuu huyo wa mkoa ameongeza kuwa Maono ya Serikali ya Mkoa ni kuzalisha bidhaa zote ambazo malighafi yake yanapatikana hapa nchini na kubadili mtazamo na fikra za Watanzania walio wengi wanaoamini kuwa  bidhaa bora ni zile zinazotengenezwa nje ya nchi.

Mtaka amewataka Viongozi wa Kisiasa kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Watendaji wa Serikali katika ngazi zote, ili waweze kufikia azma ya Mkoa wa Simiyu  kuwa Mkoa kiongozi kwa kutekeleza kwa Vitendo Ilani ya Chama cha Mapinduzi , ikiwa ni pamoja na kuifikia Tanzania ya Viwanda kwa kuanzisha viwanda vidogo hususani vya kuyaongezea thamani mazao yanayozaliswa mkoani humo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa (kulia) akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka (wa pili kulia) alipotembelea Shule ya Msingi Maswa kukagua ujenzi wa Vyumba vya madarasa  wakati wa ziara yake wilayani humo.
 Kiongozi wa kikundi cha Simiyu Umoja Arts Group cha Wilayani Maswa, Ally Kazembe  (kulia) akitoa maelezo juu ya utengenezaji wa sabuni kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (wa tatu kulia) alipotembelea kikundi hicho wakati wa  ziara yake wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa,Mhe.Dkt. Seif Shekalaghe akizungumza na wananchi wa wilaya hiyo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa MODECO wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

MKURUGENZI WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI BW.KAILIMA RAMADHAN AFAFANUA SHERIA, KANUNI,TARATIBU NA MAADILI YA KUZINGATIWA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA DIMANI -ZANZIBAR

0
0

TGNP yakutanisha watendaji kujadili changamoto sera za maji, elimu na afya

0
0
Mwasilisha mada (wa pili kulia) akijadiliana jambo na baadhi ya watendaji na wataalamu kutoka sekta za Maji, Afya na Elimu pamoja na wale wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati wa warsha hiyo iliyoandaliwa na TGNP Mtandao. Mwasilisha mada (wa pili kulia) akijadiliana jambo na baadhi ya watendaji na wataalamu kutoka sekta za Maji, Afya na Elimu pamoja na wale wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati wa warsha hiyo iliyoandaliwa na TGNP Mtandao.Sehemu ya watendaji na wataalamu kutoka sekta za Maji, Afya na Elimu pamoja na wale wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakijadiliana jambo katika warsha iliyoandaliwa na TGNP Mtandao. Sehemu ya watendaji na wataalamu kutoka sekta za Maji, Afya na Elimu pamoja na wale wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakijadiliana jambo katika warsha iliyoandaliwa na TGNP Mtandao.Mwasilisha mada (wa pili kulia) akijadiliana jambo na baadhi ya watendaji na wataalamu kutoka sekta za Maji, Afya na Elimu pamoja na wale wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati wa warsha hiyo iliyoandaliwa na TGNP Mtandao. Mwasilisha mada (wa pili kulia) akijadiliana jambo na baadhi ya watendaji na wataalamu kutoka sekta za Maji, Afya na Elimu pamoja na wale wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati wa warsha hiyo iliyoandaliwa na TGNP Mtandao.Sehemu ya watendaji na wataalamu kutoka sekta za Maji, Afya na Elimu pamoja na wale wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakijadiliana jambo katika warsha iliyoandaliwa na TGNP Mtandao. Sehemu ya watendaji na wataalamu kutoka sekta za Maji, Afya na Elimu pamoja na wale wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakijadiliana jambo katika warsha iliyoandaliwa na TGNP Mtandao.Meneja Idara ya Ujenzi wa Nguvu za Pamoja, TAPO kutoka TGNP Mtandao, Grace Kisetu (kushoto) akizungumza na washiriki wa warsha hiyo. Meneja Idara ya Ujenzi wa Nguvu za Pamoja, TAPO kutoka TGNP Mtandao, Grace Kisetu (kushoto) akizungumza na washiriki wa warsha hiyo.Mwasilisha mada akizungumza na washiriki wa warsha hiyo. Mwasilisha mada akizungumza na washiriki wa warsha hiyo.Watendaji na wataalamu kutoka sekta za Maji, Afya na Elimu pamoja na wale wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya majadiliano. Watendaji na wataalamu kutoka sekta za Maji, Afya na Elimu pamoja na wale wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya majadiliano.

 MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) inakutanisha watendaji mbalimbali na wataalamu kutoka sekta za Maji, Afya na Elimu pamoja na wale wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuangalia changamoto za kijinsia zilizopo kwenye sera za sekta tajwa. 

Watendaji hao na wataalamu wanaoungana na wengine kutoka Halmashauri zote za jiji la Dar es Salaam pamoja na wanajamii kuangalia changamoto za kijinsia lengo likiwa ni kuboresha zaidi huduma ndani ya sekta hizo. Akizungumza katika warsha iliyowakutanisha wataalamu hao Meneja Idara ya Ujenzi wa Nguvu za Pamoja, TAPO kutoka TGNP Mtandao, Grace Kisetu alisema lengo kubwa la majadiliano hayo ni kushauriana namna bora ya utekelezaji wa sera katika sekta hizo zinazotegemewa zaidi na jamii. Wataalamu hao watatoka na kikosi kazi cha wataalamu ambacho pamoja na mambo mengine kitaweka mikakati ya pamoja ili kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa sera kwa wadau anuai. --

WAZIRI UMMY ATOA TAMKO KUHUSU UGONJWA WA ZIKA NCHINI

0
0

Rais Magufuli amteua Prof. Yunus D. Mgaya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NIMR

0
0
 Mkurugenzi Mkuu mpya wa NIMR,Prof. Yunus D. Mgaya


MPOGOLO AKAGUA MALI ZA CHAMA LEO MJINI DODOMA, LUHWAVI AMKABIDHI KILA KITU HADI MSAIDIZI

0
0
 Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akimpa maelezo Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo, kuhusu jengo la mikutano la CCM, lililopo Kilimani mjini Dodoma wakati Naibu Katibu Mkuu huyo mpya alipotembelea jengo hilo akiwa katika ziara ya kukagua mali za CCM, leo. Kushoto ni Mkuu wa Utawala Makao Makuu ya CCM, Innocent Msena na kulia ni Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Utumishi na Uendeshaji Makao Makuu ya CCM Filbert Mdaki.
 Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akimpa maelezo Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo, kuhusu jengo la mikutano la CCM, lililopo Kilimani mjini Dodoma wakati Naibu Katibu Mkuu huyo mpya alipotembelea jengo hilo akiwa katika ziara ya kukagua mali za CCM, leo. kulia ni Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Utumishi na Uendeshaji Makao Makuu ya CCM Filbert Mdaki.
 Mafara wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo ukiwa mbele ya jengo hilo la mikutano la CCM
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo, akimoji jambo, Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM-Bara Rajabu Luhwavi baada ya kukagua jengo hilo, akiwa katika ziara ya kukagua mali za Chama, leo mjini Dodoma.
KIWANJA
🔻
 Meneja wa Miliki wa Makao Makuu ya CCM, Abdallah (kulia) Msangi akimpatia maelezo Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo (wapili kushoto), alipoenda kukagua kiwanja cha CCM kilichopo eneo la Kilimani mjini Dodoma, akiwa katikaziara ya kukagua mali za Chama, leo mjini Dodoma. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi.
 Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Utumishi na Uendeshaji Makao Makuu ya CCM Filbert Mdaki akiongeza maelezo kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo alipoenda kukagua kiwanja cha CCM kilichopo eneo la Kilimani mjini Dodoma, akiwa katikaziara ya kukagua mali za Chama, leo mjini Dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi, akimuonyesha mwisho wa shamba la CCM, Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo (wapili kulia), Naibu Katibu Mkuu huyo alipoenda kukagua kiwanja hicho kilichopo eneo la Kilimani mjini Dodoma, akiwa katikaziara ya kukagua mali za Chama, leo mjini Dodoma, leo.

NYUMBA YA CCM YA NAIBU KATIBU MKUU-BARA
🔻
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akiwasili kukagua nyumba ya CCM ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, akiwa katika ziara ya kukagua mali za Chama, mkoani Dodoma, leo
 Mkuu wa Utawala Makao Makuu ya CCM, Innocent Msena akimpa maelezo Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo, aliyefika kukagua nyumba ya Chama atakayoishi, akiwa katika ziara ya kukagua mali za Chama mjini Dodoma, leo
 Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Utumishi na Uenedeshaji Filbert Mdaki akionyesha sehemu ya jikoni, wakati Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo alipokagua nyumba ya CCM ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, akiwa katika ziara ya kukagua mali za Chama leo mjini Dodoma. Kushoto ni Luhwavi
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo akikagua meza kwenye jiko, alipokuwa akikagua nyumba ya CCM ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, akiwa katika ziara ya kukagua mali za Chama mjini Dodoma leo. Kulia ni Msaidizi Msaidizi wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Mbwana Kambangwa.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo akikagua kabati la jikoni, alipokuwa akikagua nyumba ya CCM ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, akiwa katika ziara ya kukagua mali za Chama mjini Dodoma leo
 Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akimpa maelezo Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo wakati wakiizunguka kuikagua nyumba ya CCM ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Mpogolo alipokuwa katika ziara ya kukagua mali za Chama mjini Dodoma, leo.
 Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akimpa maelezo Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo baada ya kuikagua nyumba ya CCM ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Mpogolo alipokuwa katika ziara ya kukagua mali za Chama mjini Dodoma, leo.

KUKAGUA MAGARI WHITE HOUSE
🔻
 Msafara wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo na Rajabu Luhwavi, ukiwa umepumzika kwa mda katika jengo la White House la Makao Makuu ya CCM kabla ya kuanza kazi ya kukagua magari, Mpogolo alipokuwa katika ziara ya kukagua mali za Chama mjini Dodoma, leo.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rodrick Mpogolo (wapili kushoto), akipatiwa maelezo na Fundi wa magari, Ramadhani Mbelwa (kushoto), kuhusu hali ya magari yaliyoharibika, Mpogolo alipokuwa akikagua magari hayo akiwa katika ziara ya kukagua mali za Chama mjini Dodoma, leo.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo amhoji jambo Fundi wa magari ya Chama, Ramadhani Mbelwa (kushoto), alipokuwa akikagua magari mabovu ya Chama, akiwa katika ziara ya kukagua mali za Chama mjini Dodoma, leo. Kulia ni Luhwavi.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akionyeshwa gari lililofunguliwa boneti, kupata uthibisho wa gari tatizo la gari, alipokuwa akikagua magari mabovu ya Chama, akiwa katika ziara ya kukagua mali za Chama, leo mjini Dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akimshukuru Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi baada ya kumalizika kazi ya kukagua baadhi ya mali za Chama, mjini Dodoma leo.
KUNZIA SASA HUYU NDIYO BOSS WAKO, SIYO MIMI TENA: Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akimtambulisha aliyekuwa Msaidizi wake, Mbwana Kambangwa(kulia), kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo kabla ya kuagana, mwishoni mwa ziara ya Mpogolo kukagua mali za Chama, mjini Dodoma, leo. Picha zote na Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog

GARI LA MBUNGE WA MBEYA MJINI (SUGU) LAGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO

0
0
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (SUGU)


Na JamiiMojaBlog,Mbeya.

Mkazi wa Iyunga jijini Mbeya ambaye amefahamika kwa jina moja la Rechal (13) amefariki dunia mara baada ya kugongwa na gari , namba T161 CPP Toyota LandCruiser inayodaiwa kumilikiwa na Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi maharufu kwa jina la (SUGU), kwenye kivuko cha barabara (ZEBRA) na kumsababishia kifo chake papo hapo.

Tukio hilo limetokea leo Desemba 17  majira ya saa mbili asubuhi huko katika eneo la Iyunga Jijini hapa, wakati gari ya Mbunge huyo ikiwa njiani kuelekea uwanja wa ndege wa Songwe kwa ajili ya mapokezi ya kiongozi wa Kitaifa Freeman Mbowe.

Imeelezwa kuwa, gari hilo likiwa katika mwendokasi linadaiwa kukiuka sheria za barabarani kwa kutosimama kwenye kivuko cha barabara kinachowaruhusu watembea kwa miguu kuvuka na kumgonga mtoto huyo  na kusababisha kifo chake papo hapo.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wakizungumza , kwa nyakati tofauti , wamesema mtoto huyo akiwa na mama yake walikuwa wakivuka barabara baada ya magari ya upande wa  pili kusimama na kuwaruhusu watembea kwa miguu hao kuvuka.

Amesema, wakiwa katikati ya kivuko hicho mama wa marehemu alishangaa kuliona gari ya Mbunge hiyo ikija kwa kasi hivyo kumuachia mtoto wake aliyekuwa amemshika mkono na yeye kutafuta njia ya kujiokoa.

Wameeleza kuwa  licha ya dereva wa gari ya Mbunge kuona madereva wenzie wa magari yaliyokuwa yakitokea Mbalizi wakisimama kwa ajili ya kuwaruhusu watembea hao kuvuka lakini yeye akitokea mjini Mbeya alishindwa kutii sheria hiyo na kupita akiwa katika mwendo kasi.

“Madereva wenzie tumesimama ili mama na mtoto wavuke lakini yeye akiwa na haraka alipita tu, kwa kweli hii inauma sana, nasikia mtoto amepoteza maisha lakini mama amejeruhiwa na kwamba amekimbizwa hospitali Teule ya Ifisi kwa matibabu,”alisema mmoja wa mashuhuda hao.
Gari la Mbunge wa Mbeya mjini Mheshimiwa Joseph Mbilinyi (Sugu) Toyota Land Cruser T.161 CPP likiwa ofisi za Usalama barabarani jijini Mbeya baada ya kugonga mtembea kwa miguu na kusababisha kifo .

Kamanda wa  Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari akizungumza kwa njia ya simu amekiri kutokea kwa tukio hilo na kuthibitisha kifo cha mtoto huyo. Aidha Kivadashari ametaja jina la  dereva wa gari hiyo kuwa ni  Gabriel Endrew alimaarufu Dj BBG (43) mkazi wa Mwakibete jijini hapa.

 Amesema hilo  limetokea majira ya saa mbili asubuhi ambapo gari T161 CPP ilimgonga mtembea kwa miguu ambaye ni mtoto anayekadiriwa miaka 13 ambapo amefahamika kwa jina moja la Rechal na kumsababishia kifo wakati akikimbizwa hospitali .

Pia, aliongeza kuwa gari hiyo imekamatwa na dereva anashikiliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano na kwamba polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA KAMPENI YA KITAIFA YA KUDHIBITI MAGONJWA YASIYO YA KUAMBUKIZA LEO

0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa muda wa miezi mitatu kwa Halmashauri zote nchini kurudisha serikalini haraka maeneo ya michezo yaliyovamiwa na watu kwa ajili ya kufanya shughuli zao binafsi.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo baada ya kushiriki matembezi na kuzindua wa kampeni ya Kitaifa ya kudhibiti Magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwenye viwanja wa Leaders Club jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais ameonya kuwa kama watendaji wa mikoa na halmashauri watashindwa kurudisha maeneo hayo basi watenge haraka maeneo mengine kwa ajili ya wananchi kufanya mazoezi kama hatua ya kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

Katika kuunga mkono utaratibu wa kufanya mazoezi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewaagiza viongozi wa mikoa na wilaya zote kuweka utaratibu wa kufanya mazoezi angalau kwa mwezi mara Moja.

“Nitamke kuwa kila Jumamosi ya pili ya mwezi itakuwa siku ya mazoezi kwa afya kwa sababu mazoezi ni afya na nawaasa wananchi kufanya mazoezi na kuanzisha na kujiunga na vikundi vya mazoezi na serikali itatimiza wajibu wake wa kuweka mazingira mazuri ya kufanyia mazoezi kote nchini”Makamu wa Rais pia ameagiza watendaji wa Wizara ya elimu, Sayansi na Teknolojia kurudisha mchakamchaka mashuleni kulingana na maeneo yalivyo.

Amesema mchakamchaka utasaidia kuimarisha afya za wanafunzi na kukabiliana na magonjwa mbalimbali.
“Natoa rai utaratibu wa mchakamchaka katika shule zetu urudishwe mara Moja katika Muda ambao utaonekana ni mwafaka kwa shule husika”.Katika hatua nyingine, Makamu wa Rais ameiagiza Wizara ya Afya kukamilisha haraka mchakato wa kuunda kamati ya kushughulikia magonjwa yasiyo ya kuambukiza itakayojumuisha wadau kutoka wizara mbalimbali nchini.

Amesisitiza kuwa mchakato huo ni lazima ukamilike tarehe 1 machi mwaka 2017.Kwa upande wake, Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema magonjwa yasiyo ya kuambukiza yamekuwa yanaongezeka sana duniani kote hasa kwenye nchi zilizo chini ya Jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania ambapo magonjwa hayo mpaka sasa yanachangia asilimia 27 ya vifo Duniani.

Amesema utafiti uliofanyika mwaka 2012 uliohusisha wilaya 53 hapa nchini umeonyesha viashiria hatarishi vya magonjwa hayo ambapo asilimia 26 ya wananchi ni wanene kupita kiasi,asilimia 26 wana lehemu nyingi mwilini na asilimia 25.9 wanashinikizo kubwa la damu.

Utafiti huo pia ulionyesha kuwa asilimia 15.9 ya wananchi wanavuta sigara na asilimia 97.2 ya wananchi wanakula mboga mboga na matunda chini ya mara tano kwa siku.Waziri wa afya Ummy Mwalimu amesema watanzania wanaweza kukabiliana na magonjwa hayo kwa kufanya mazoezi ya viungo angalau mara tatu kwa wiki kwa muda wa nusu saa, kuzingatia ulaji wa vyakula unaofaa,kupunguza matumizi ya pombe kupita kiasi na kujiepusha na matumizi ya tumbaku.

Kwa upande wake Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi katika nasaha zake amewahimiza Watanzania kufanya mazoezi kwa ajili ya kulinda afya zao.Amesema kama watanzania watafanya mazoezi wataepukana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwemo ugonjwa wa moyo,kisukari,uti wa mgongo na mifumo ya neva na figo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Kudhibiti Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza kwenye viwanja vya Leaders Club.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Alhaji Ali Hassan Mwinyi akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Kitaifa ya Kudhibiti Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza ambapo aliwaambia wananchi walishiriki kwenye tukio hilo kuwa siri kubwa ya mafanikio yake ya kuonekana yupo imara ni mazoezi hivyo aliwataka wananchi wajenge tabia ya kushiriki na kufanya mazoezi kwani kutawaepusha na maradhi mengi .
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalim akihutubia kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuzindua rasmi Kampeni ya Kitaifa ya Kudhibiti Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akiongoza matembezi ikiwa sehemu ya kuhamasisha jamii kufanya mazoezi akiongozana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Alhaji Ali Hassan Mwinyi (kushoto) na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalim kabla ya kufungua Kampeni ya Kitaifa ya Kudhibiti Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza kwenye viwanja vya Leaders Club viongozi wengine walioshiriki matembezi hayo ni pamoja na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalah, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda .

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbali mbali mara baada ya kufungua wa Kampeni ya Kitaifa ya Kudhibiti Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza kwenye viwanja vya Leaders Club.

WAZIRI MKUU AENDELEA NA ZIARA YAKE MKOANI ARUSHA, AWATAKA WASIOENDELEZA MASHAMBA ARUMERU KUNYANG’ANYWA-MAJALIWA

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia burudani ya wanawake wa kimasai baada ya kuzindua mradi wa maji wa kijiji cha Ondenderet wilayani Arusha Desemba 27, 2016. kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa eneo la Kwamrombo wilayani Arusha ambao walijipanga kwa wingi barabarani na kumshawishi kusimama ili kuzungumza nao. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Arusha Desemba 27, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa kizungumza na wananchi wa kijiji cha Ormapinu wilayani Arusha ambao wlijipanga kwa wingi barabarani na kumshawishi kusismama ili kuwasikiliza. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Arusha Desemba 27, 2016.

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali itawanyang’anya ardhi wamiliki wote wa mashamba makubwa wilayani Arumeru ambao hawajayaendeleza kwa sababu wamekiuka mkataba wa umiliki.

Amesema Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa William Lukuvi atakuja mkoani Arusha kwa ajili ya kufanya mapitio ya mashamba yote makubwa ambayo hayajaendelezwa na kuyarudishwa Serikalini.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Desemba 17, 2016) wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Arumeru na wananchi wa kijiji Bwawani na kitongoji cha Mapinu katika kata ya Nduruma akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Arusha.

“Tufanya mapitio ya kila shamba ili kujua linamilikiwa na nani na alipewa lini na tangu alipokabidhiwa amefanya nini. Shamba lisiloendelezwa litarudisha kwa wananchi. Kama mtu ameshindwa kupata mtaji kwa muda wa miaka 10 atapata leo,” amesema.

Amesema Serikali haiko tayari kuona wananchi wakinyanyaswa kwa kukosa ardhi ya kilimo kwa sababu ya watu wachache kumiliki maeneo makubwa bila ya kuyaendeleza..

"Ninataarifa kwamba hapa Arumeru kuna baadhi ya wawekezaji wanamiliki mashamba makubwa na hawajayaendeleza. Wengine wanakodisha kwa wananchi ili kujipatia fedha kinyume na mikataba yao ya umiliki. Hatutawavumilia,” amesema.

BOFYA HAPA KWA PICHA NA HABARI ZAIDI

NAPE AFUNGUA MASHINDANO YA MICHEZO MBALIMBALI WILAYANI KARATU

0
0
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akipiga baruti juu kuashiria ufunguzi rasmi wa mashindano ya michezo mbalimbali yanayofanyika Wilayani Karatu (Karatu Sports Festival).
 Wanariadha wanaoshiriki mashindano ya michezo mbalimbali yanayofanyika Wilayani Karatu wakijandaa kuanza kukimbia wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo uliofanywa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye Disemba 17/2016.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na baadhi ya washiriki wa mashindano ya michezo mbalimbali yanayofanyika Wilayani Karatu.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na baadhi ya washiriki wa mashindano ya michezo mbalimbali yanayofanyika Wilayani Karatu.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na baadhi ya washiriki wa mashindano ya michezo mbalimbali yanayofanyika Wilayani Karatu.
Viewing all 46194 articles
Browse latest View live




Latest Images