Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1071 | 1072 | (Page 1073) | 1074 | 1075 | .... | 1898 | newer

  0 0

  0 0

  Usiku wa manane katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa J.K.Nyerere jijini
  Dar es salaam jana usiku jicho la kamera ya paparazi lilimzoa mwanamuziki
  Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja ambaye alikuwa ndio kwanza katua kutokea nchini Ujerumani,mwanamuziki huyo wa kimataifa anayeiongoza bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa Band aka FFU Ughaibuni,alipokumbana na paparazi akutaka maneno zaidi.bali alipakiwa katika gari moja jeusi aina na Noa na kutokomea aliko tokomea,ubuyu umedokeza kuwa bendi hiyo ipo likizo kwa muda wa miezi miwili ,likizo hiyo imetokana na kufanya tour miaka miwili bila mapumziko,Kiongozi huyo wa Ngoma Africa band inawezekena yupo nyumbani Tanzania labda kwa likizo kama inavyodhaniwa,Any way Kikamanda Ketu Ras Makunja karibu nyumbani,

  0 0


  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia), na Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), mkoa wa Mwanza Eng. Fredinand Mishamo (kushoto), wakiingia katika Kivuko cha MV TEMESA wakati alipokagua kivuko hicho kinachotoa huduma kati ya Kijiji cha Luchelele na Irunda, mkoani Mwanza.
  Muonekano wa Kivuko cha MV TEMESA kinachotoa huduma zake katika Kijiji cha Luchelele na Irunda, mkoani Mwanza. Kivuko hicho kina uwezo wa kubeba abiria 80, magari 5 kwa wakati mmoja.
  Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), mkoa wa Mwanza Eng. Fredinand Mishamo (kulia), akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), kuhusu hali ya utendaji wa kivuko cha MV TEMESA wakati alipokagua kivuko hicho kinachotoa huduma kati ya Kijiji cha Luchelele na Irunda, mkoani Mwanza.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akielekezwa na Nahodha Mkuu wa kivuko cha MV TEMESA (kulia), wakati alipokagua kivuko hicho, mkoani Mwanza.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Luchelele, mara baada ya kukagua kivuko cha MV TEMESA kinachotoa huduma kati ya Kijiji hicho na Irunda, mkoani Mwanza
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa Kampuni ya Nyanza Road Works inayojenga kwa kiwango cha lami barabara ya Usagara-Kisesa yenye urefu wa KM 16, mkoani Mwanza.
  Mkandarasi wa Kampuni ya Nyanza Road Works (wa pili kulia), akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kuhusu hatua ya ujenzi iliyofikiwa ya barabara ya Usagara-Kisesa yenye urefu wa KM 16 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Mwanza. Wa pili kushoto ni Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), mkoa wa Mwanza Eng. Marwa Rubirya.
  Muonekano wa sehemu ya barabara ya Usagara-Kisesa yenye urefu wa KM 16 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Mwanza. Barabara hiyo inatarajiwa kukamilika Mwezi Februari mwakani.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wafanyakazi wa taasisi za wizara hiyo alipokutana nao mkoani Mwanza.

  ………………….

  Serikali imesema ipo katika hatua za mwisho kuanza ujenzi wa Daraja la Kigongo – Busisi lenye urefu wa kilometa 3.2 litakalounganisha eneo la Kigongo na Busisi, wilayani Misungwi Mkoani Mwanza .

  Kauli hiyo imetolewa mkoani Mwanza na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa wakati akizungumza na watumishi wa Taasisi za Wizara hiyo ambapo pamoja na mambo mengine amesema tayari Serikali imetenga fedha kwa ajili ya kutekekeleza kazi hiyo.

  “Serikali ina nia ya dhati kwa wananchi wake katika kuhakikisha wanapata miundombinu iliyobora kwa maendeleo yao, hivyo basi wananchi wa mkoa huu mtarajie kupata daraja jingine kubwa la Kigongo-Busisi”, amesema Waziri Mbarawa.

  Ameongeza kuwa kuhusu suala la ununuzi wa meli mpya ya kisasa itakayotoa huduma mkoani Mwanza na Bukoba, tayari Serikali imeshatenga fedha na majadiliano kwa ajili ya ununuzi wa meli hiyo yataanza wiki ijayo.

  Prof. Mbarawa amewataka watumishi hao kuwa wabunifu na kufanya kazi kwa haraka, uadilifu na uwazi ili kuboresha utendaji na kwenda sambasamba na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano.

  Katika hatua nyingine, Waziri Prof. Mbarawa ametembelea Kivuko cha
  Mv Temesa kinachotoa huduma kati ya Kijiji cha Irunda na Luchelele mkoani Mwanza na kumtaka Meneja wa kivuko hicho kuhakikisha anasimamia wananchi katika kuilinda na kuitunza miundombinu ya kivuko hicho.

  Pia amemtaka Meneja huyo kufunga mifumo ya kielektroniki ili kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato.

  Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme Nchini (TEMESA), mkoani Mwanza, Eng. Fredinand Mishamo, amemhakikishia Waziri huyo kuboresha hali ya miundombinu ya ukusanyaji wa mapato ili kivuko hicho kijiendeshe chenyewe bila kutegemea ruzuku kutoka TEMESA Makao Makuu.

  Aidha, Waziri Prof. Mbarawa ametembelea barabara ya Usagara – Kisesa (km 16), na kutoridhishwa kwa hatua ya ujenzi wake, hivyo kumtaka Mkandarasi wa Kampuni ya ujenzi ya Nyanza Roads Works anayejenga barabara hiyo kumaliza ujenzi wake ifikapo mwezi Februari mwakani.

  Waziri Prof. Mbarawa amehitimisha ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani Mwanza ambapo ametembelea na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wizara yake.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

  0 0

  Tanga, MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Deudence Kakoko, amewataka wafanyakazi wa mamlaka hiyo kufanya kazi kwa bidii ili kwenda kasi ya Serikali ya awamu ya Tano.
  Akifungua michezo ya Tano ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (INTERPORTS GAMES) viwanja vya shule ya Sekondari ya Popatlal Tanga jana, Kakoko, alisema kila mfanyakazi wa Mamlaka hiyo anapaswa kujua wajibu wake.

  Alisema kasi hiyo iende sambamba na uboreshaji wa utoaji huduma bandarini na kuwa kivutio kwa wageni ili kuweza kuitumia kwa kushusha shehena zao bandari za Tanzania.
   

  Michezo hiyo inashirikisha wafanyakazi wachezaji kutoka Tanga ambao ni wenyeji, Dar es Salaam,, Mtwara na Bandari za Ziwa.


  0 0

   WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itazifutia usajili Taasisi zote zisizokuwa za Kiserikali (NGO’s) zilizoko kwenye Tarafa ya Loliondo zinazofanyakazi kinyume na katiba zake na sheria ya nchi ambapo ametoa miezi sita zijitathimini kama zinafanya kazi ya kuhudumia jamii au la.

  Pia ameahidi kumpeleka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika Taraha hiyo ya Loliondo kwa lengo la kuzifanyia ukaguzi NGO hizo ili kubaini kiasi cha fedha wanazopata kama zinalingana na matokeo ya kazi za kijamii inazofanya katika Tarafa hiyo.

  Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Desemba 15, 2016) wakati akizungumza na Wakurugenzi wa NGO na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Arusha.

  Amesema NGO nyingi zimekuwa zikipata bajeti kubwa ya fedha lakini masuala ya maendeleo wanayoyafanya katika eneo hilo hayalingani na bajeti halisi wanazopata.”Loliondo pekee kuna NGO zaidi ya 30 ila zilizokuwa ‘active’ ni 15 tu kuna nini Loliondo? Na baadhi yake zinafanya kazi ya kuchochea eneo hili lisiwe na amani,”.

  Waziri Mkuu ameongeza kuwa “watu wote wanaoshirikiana na NGO hizo zinazochafua taswira ya nchi tutawashughulikia. Mnawavalisha watoto kandambili zilizotobona na miguu michafu kisha mnawapiga picha mnazituma kwenye mitandao na kusema umasikini wa Tanzania ndio huo. Hatutawavumilia watu wa namna hii,” amesisitiza.                                                    

  Amesema NGO nyingi zimekuwa zikilalamikiwa kutokana na kufanya kazi kinyume na mikataba yake ya usajili na miongoni mwa NGO hizo ni pamoja na PWC inayopata sh. bilioni 2.5 kwa mwaka, UCRT inayopata sh. bilioni 1.5 kwa mwaka, Oxfarm Tanzania inayopata sh. bilioni 1.7 kwa mwaka.

  “Nitafuatilia kwa karibu kuona kazi wanazozifanya kwani zinapata fedha nyingi kwa mwaka. Lazima tujenge nidhamu kwa wote wanaopata fedha kwa lengo la kuisaidia jamii. Wote wanaojihusisha na shughuli nje ya mikataba yao wabadilike ndani ya miezi sita. Wafuate kanuni, sheria na taratibu za nchi,” amesema.

  Amesema Serikali haiwezi kufanya kazi bila ya wadau ila haiitaji wadau wanaofanya mambo kinyume cha taratibu, ambapo amezitaka NGO hizo kusajiliwa na Wakala wa Usajili wa Kampuni (BRELA) ili ziweze kutambulika kisheria na ofisi zake kujulikana badala ya hivi sasa kuwa na ofisi za mifukoni.

  Awali, Waziri Mkuu alizungumzia na wananchi wa kijiji cha Ololosokwan ambapo alisema  mgogoro wa ardhi kati ya wananchi wa Tarafa la Loliondo na wawekezaji unaolikabili eneo hilo Waziri Mkuu mesema Serikali itahakikisha mgogoro huo uliodumu kwa muda mrefu unamalizika haraka.

  Aidha, amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Bw. Mrisho Gambo kukutana na uongozi wa wilaya ya Ngorongoro na kamati ya wananchi iliyoundwa kwa ajili ya kuboresha uhifadhi ili kumaliza mgogoro huo na kisha kumpelekea taarifa.

  “Haiwezekani Waziri Mkuu aje kumaliza mgogoro wa ardhi Loliondo wakati kuna viongozi hapa. Mimi nimemuagiza Mkuu wa mkoa aje akutane na wawekezaji na wananchi ili kuzungumza na kuupatia ufumbuzi mgogoro huu na atakayeshindwa ndiye nitakayemshughulikia,” amesema.

  Amesema Serikali itahakikisha migogoro ya ardhi inamalizika nchini ili kuwawezesha wananchi kufanya shughuli zao kwa amani na utulivu. “Naomba tushirikiane katika kutatua changamoto hii ya migogoro ya ardhi kwani suala hili limeahidiwa katika ilani ya uchaguzi ya CCM,”.

  Wakati huo huo, Waziri Mkuu amepiga marufuku tabia ya baadhi ya wananchi kuingiza ng’ombe kiholela kutoka nje ya nchi kwa kuwa kitendo hicho kinachangia kuwepo kwa migogoro ya ardhi. 

  Katika kuhakikisha suala hilo linadhibitiwa Waziri Mkuu amemtaka Mkuu wa wilaya hiyo, Bw. Rashid Taka kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo kuimarisha ulinzi katika mipaka kwa kuongeza doria ili kudhibiti uingiaji holela wa mifugo.
  Naye Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe alisema  eneo la Loliondo ni muhimu sana kwa ajili ya ikolojia ya wanyama pamoja na maji kwani hifadhi ya Serengeti inategemea zaidi eneo hilo.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMATANO, DESEMBA 15, 2016.  


  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na watumishi wa   serikali na Halmashauri  ya Wilaya ya  Ngorongoro uliopo  kwenye ukumbi wa halmashauri  hiyo iliyopo Wasso  Desemba 15, 2016.  Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   1A7872, 1a7873,   Baadhi ya watumishi wa   serikali na  halmashauri   ya wilaya ya  Ngorongoro    wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo uliopo Wasso wilayani Ngorongoro Desemba 15, 2016. (Picha  na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Waandishi wa Habari walioshiriki changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara wakinyanyua kuashiria kuanza safari hiyo atika lango la Marangu.
  Safari ya kupanda ikaanza katika lango la Marangu majira ya saa 5 asubuhi kila mmoja akiwa na nguvu za kutosha na shauku ya kutzama madhari ya Mlima Kilimanjaro ambao siku ya kwanza safari inaanza kwa kupita katika msitu mnene.
  Wapandaji waliokuwa wamevalia nguo za kuzuia baraidi mapema wakati safari ya kupanda mlima inaanza baadae kidogo kidogo walilazimika kuzipunguza kwa sababu pindi unapotembea joto la mwili pia huongezeka.
  Safari ya kupanda mlima kwa kundi hili la Wanahabari na Askari wa jeshi la Ulinzi (JWTZ) wakiongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu,George Waitara lilikuwa pia na ulinzi wa kutosha. 
  Safari ya kupanda vilima vidogo ndani ya Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro iliendelea.
  Maeneo mengine yalikuwa ni ya Madaraja na Mito.
  Hatimaye safari kafika eneo la Kisambioni ikiwa ni nusu ya safari ya kuelekea katika kituo cha Mandara ,eneo ambalo hutumika kwa ajili ya kupata chakula.
  Baadae safari ya kuelekea kituo cha Mnadara ikaendeleo.
  Maeneo mengine Washiriki walilazimika kupumzika kwa ajili ya kupata nguvu mpya ya kuendelea na safari.
  Majira ya saa 12 jioni hatimaye Safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa siku ya kwanza ikafika katika kituo cha Mandara na washiriki wakapata nafasi ya kupata picha ya pamoja na kupumzika kwa ajili ya siku ya pili kuendele na safari ya kwenda kituo cha Horombo.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii aliyekuwa katika safari hiyo.

  0 0

   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia), akiwasikiliza Viongozi Waandamizi kutoka Kampuni ya ‘Solar Securities’ ya Uingereza, Nicholas Richardson ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji (katikati) na Manoli Yannaghas – Mkurugenzi (kushoto); walipomtembelea ofisini kwake hivi karibuni kwa lengo la kuonesha nia yao ya kuwekeza kwenye sekta ya umeme nchini.
   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akisisitiza jambo katika kikao baina yake na Ujumbe kutoka Kampuni inayojishughulisha na masuala ya nishati mbadala kutoka Uingereza, ‘Solar Securities (hawapo pichani)
   Mbunge wa Shinyanga Mjini, Stephen Masele (kulia), akifurahia jambo wakati wa kikao baina ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Ujumbe kutoka Kampuni inayojishughulisha na masuala ya nishati mbadala kutoka Uingereza, ‘Solar Securities (hawapo pichani). Masele ni mshirika wa Kampuni hiyo. Kulia ni Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia Nishati Mbadala, Jacob Mayala.

  Kutoka Kulia ni Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia Nishati Mbadala, Jacob Mayala, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Solar Securities Nicholas Richardson, Mkurugenzi wa kampuni hiyo Manoli Yannaghas, Mbunge wa Shinyanga Mjini Stephen Masele na Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia Umeme, Mhandisi Innocent Luoga, wakiwa katika kikao ambacho Ujumbe kutoka Kampuni husika ulionesha nia kuwekeza kwenye sekta ya nishati nchini.  Kutoka Kulia ni Kaimu Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia Nishati Mbadala, Jacob Mayala, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Solar Securities Nicholas Richardson, Mkurugenzi wa kampuni hiyo Manoli Yannaghas, Mbunge wa Shinyanga Mjini Stephen Masele na Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia Umeme, Mhandisi Innocent Luoga, wakiwa katika kikao ambacho Ujumbe kutoka Kampuni husika ulionesha nia kuwekeza kwenye sekta ya nishati nchini.  Na Veronica Simba
  Ujumbe kutoka Kampuni inayojishughulisha na masuala ya nishati mbadala kutoka Uingereza, ‘Solar Securities’, umemtembelea Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ofisini kwake na kufanya mazungumzo kuhusu nia yao ya kuwekeza kwenye sekta ya nishati hapa nchini.
  Viongozi waandamizi kutoka Kampuni hiyo, Nicholas Richardson (Mkurugenzi Mtendaji) na Manoli Yannaghas (Mkurugenzi), walimweleza Waziri Muhongo kuwa lengo lao ni kuwekeza nchini kwa kuzalisha umeme wa jua.
  Akitoa mwongozo wa nia iliyowasilishwa na Ujumbe huo, Profesa Muhongo aliwaeleza kuwa, Serikali imeanzisha utaratibu mpya wa uwekezaji nchini hususan katika sekta ya nishati, ambapo wawekezaji walioonesha nia ya kuwekeza watashindanishwa kwa uwazi na wale watakaokidhi vigezo ndiyo watapata fursa ya kuwekeza.
  Alisema kuwa, kwa kuanzia, mwongozo wa utaratibu huo mpya kwa upande wa sekta ndogo ya gesi na mafuta uko mbioni kukamilika na utafuatiwa na miongozo husika kwa sekta nyingine za nishati.
  Alitumia fursa hiyo kuwaalika wawekezaji wote wenye nia ya kuwekeza katika sekta husika kuutumia ipasavyo mwongozo husika pindi utakapokuwa tayari ambapo alisema utasambazwa duniani kote ili waweze kuelewa vyema fursa za uwekezaji katika sekta hiyo.
   Vilevile, alieleza kuwa, Serikali hususan wizara yake, imefanya mabadiliko katika utaratibu wa majadiliano baina yake na wawekezaji wanaoonesha nia za kuwekeza nchini, ambapo sasa majadiliano yatatumia muda mfupi tofauti na ilivyokuwa zamani ili kuleta tija kwa pande zote mbili.
  “Awali, tulikuwa tukipoteza muda mrefu katika majadiliano. Sasa majadiliano yanachukua muda mfupi na kufikia makubaliano,” alisisitiza.
  Profesa Muhongo alimwagiza Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia Umeme, Mhandisi Innocent Luoga, kufuata utaratibu huo wenye kutumia muda mfupi kwa kuandaa kikao kitakachohusisha pande zote likiwemo Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na wataalam kutoka wizarani, kujadili maombi yaliyowasilishwa na Kampuni hiyo ili kufikia muafaka ndani ya muda mfupi.


  0 0

  Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii.

   Mwanzilishi na Mtendaji Mkuu wa Mtandao wa JamiiForums Maxence Melo amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka matatu.

  Maxence amesomewa shtaka la kwanza na la pili chini ya hakimu mfawidhi  Victoria Nongwa, Kosa la kwanza ni kuzuia na kuharibu data ambazo jeshi la Polisi wamekuwa wakizihitaji kwa ajili ya uchunguzi chini ya kifungu cha 22 cha Cyber Act. Kosa la pili ni kushindwa kutoa ushirikiano kwa jeshi la Polisi na kuharibu uchunguzi chini ya kifungu cha 22 cha sheria ya makosa ya mtandaoni.

  Kosa la tatu ambalo amesomewa na hakimu mkazi, Godfrey Mwambapa ni la kumiliki 'Website' ambayo aina Domain ya Tanzania kinyume na kifungu cha 7 cha sheria ya EPOCA.

  Mshtakiwa alifanikiwa kupata dhamana ya makosa mawili. 

  Hata hivyo Maxence alirudishwa mahabusu mara baada ya taratibu za dhamana katika kosa la tatu kushindwa kukamilika kutokana na mmoja wa wadhamini kutokuwa na barua inayomtambulisha kwa hakimu kutoka taasisi anayofanyia kazi. Hata alipofanikiwa kufanya hivyo muda wa mahakama uikuwa umekwisha.
   Mwanzilishi na Mtendaji Mkuu wa Mtandao wa JamiiForums, Maxence Melo akiongozwa na Askari Polisi wakati alipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es salaam leo, kusomewa mashtaka yanayomkabili kama inavyosomeka hapa chini>  0 0


  0 0

  Wananchi Wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni wamehamasishwa kujiunga na mfuko wa afya ya jamii CHF ili kupunguza gharama za matibabu na kuwa na uhakika wa kupata matibabu wakati wote pindi huduma ya Afya inapohitajika.

  Hayo yalisemwa na Afisa Tawala Wilaya Bi. Upendo Magashi alipokuwa kwenye kampeni  ya uhamasishaji wa wananchi  kujiunga na kuwa wanachama wa mfuko wa afya ya jamii wa hiari  CHF ili kupunguza gharama za matibabu, uliobeba kauli mbiu ya KUKU MMOJA MATIBABU MWAKA MZIMA.

  Aliwaeleza wananchi kuwa, kuku mmoja anayegharimu shilingi 10000, anaweza kusaidia kaya moja yenye watu sita kujiunga na mfuko wa  Afya ya jamii CHF, ambao watapata matibabu bure kwenye vituo vya Afya kwa ngazi ya Wilaya mwaka mzima. Aliwataka waratibu wa mfuko wa Afya CHF, Wataalamu wa afya, na viongozi mbalimbali kuendelea kutoa elimu na kuwahamasisha wananchi ili kuweza kuwasaidia juu ya umuhimu wa mfuko huo ikiwa ni pamoja na kujibu  hoja zao kwa kuzitafutia ufumbuzi.

  Mganga Mkuu wa Halmashauri ya  Wilaya ya Handeni Bw.Credianus Mgimba aliwaeleza wananchi kuwa faida mojawapo kubwa ya kujiunga na mfuko wa CHF ni kusaidia upatikanaji wa dawa za kutosha kwenye vituo  vya huduma za afya. Wanachama wakiwa wengi itasaidia uwepo wa dawa za kutosha kwani fedha itakayokusanywa itakuwa nyingi itakayosaidia upatikanaji wa dawa mbalimbali  na wanachama wakiwa wachache tatizo la upungufu wa dawa halitakwisha.

  Aidha  wananchi walielezwa kuwa kuwa kuna thamani kubwa sana wakiwa wanachama wa mfuko wa afya ya jamii  hasa kwa kaya zisizojiweza kwani husaidia katika kipindi kigumu iwapo mgonjwa atakosa fedha za matibabu. kwa kutumia kadi ya  CHF ataweza kupata matibabu tofauti na kutokuwa mwanachama hali ambayo wakati mwingine hupelekekea hata mtu kupoteza uhai kwani wananchi wengi  hawana uwezo wa kujigharamia matibabu. Lengo ni kuhakikisha kila mwananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni  anakuwa na uhakika wa huduma ya afya.

   Wananchi walisisitizwa pia kuwahudumia wazee kwani kumekuwa na changamoto za huduma ya Afya kwa wazee hasa linapokuja suala zima la matibabu. Wameelezwa  kuwa ili wazee waweze kuhudumiwa kila kijiji kinapaswa kuchangia laki mbili (200,000) ili iweze kusaidia dhana ya huduma bure ya afya kwa wazee ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa dawa zinazolenga wazee peke. Mpango huo umepitishwa na baraza la madiwani lililofanyika mwisho mwa mwezi wa kumi na moja hivyo utekelezaji wake unatarajiwa kuanzia januari mwaka 2017.

   Faida za  mfuko huo wa  Afya ya jamii CHF ni pamoja na kupunguza gharama kama za kufungua faili, kumuona daktari na kununua dawa hauta kuwepo hali itakayopelekea uhakika wa afya kwa familia nzima.
    
  Mpaka sasa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni ina kaya wanachama  22,532 wa mfuko wa afya ya jamii CHF, Malengo ni kufikia kaya wanachama  26,152 ifikapo June 2017. Uhamasishaji huo ulifanywa kwenye kata saba za Halmashauri ya Wilaya ya Handeni ambapo mwananchi aliyejiunga siku ya uhamsishwaji alitengenezewa na kupewa kadi papohapo. Kata hizo ni  Segera, Kiva, Kabuku, Komkonga,Kang’ata, Mkata na Kwamsisi.

  Kampeni hii inaongozwa na Mhe. Mkuu wa Wilaya na ni  endelevu lengo likiwa ni kuwafikia wananchi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni. Awamu ya kwanza imemalizika.

  ...............................
  Alda Sadango
  Afisa Habari,Halmashauri ya Wilaya Handeni.


   Afisa Tawala Wilaya Bi. Upendo Magashi akizungumza na wananchi wa Kata ya Kabuku kuhusu faida za CHF
   Bi.Upendo Magashi akitoa mfano kwa kumzawadia mmoja wa wananchi wa kata ya Segera elfu kumi iliyomuwezesha kujiunga na CHF
   Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. Credianus Mgimba akizungumza na wananchi wakati wa uhamasishaji
   Mwenyekiti wa Bodi ya Afya Bw. Salumu Masokola akiwaeleza wananchi umuhimu wa mfuko wa afya ya jamii  CHF.
   Mwenyekiti kamati ya Elimu, Afya na Maji Bw. Joel Mabula akiwahamasisha wananchi wakati wa kampeni hiyo
   Mratibu wa mfuko wa Afya ya jamii CHF wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. Godfrey Vedasto akiwaeleza wananchi faida za CHF.
  baadhi ya wananchi walioshiriki kampeni ya uhamasishaji wa CHF
  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga kwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Mhe. Balozi Dkt. Amina Mohammed wakisaini Makubaliano ya Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya. Makubaliano hayo yamesainiwa kufuatia Kikao cha Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JCC) kati ya Tanzania na Kenya kilichofanyika tarehe 1 hadi 3 Desemba, 2016 ambapo masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya nchi hizi mbili yalijadiliwa na kukubaliwa. Masuala ya ushirikiano ni pamoja na kilimo, uchukuzi, utalii, nishati na madini na uvuvi. Hafla hiyo fupi ya uwekaji saini makubaliano hayo imefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Desemba, 2016. 
  Waziri Mahiga na Waziri Mohammed wakibadilishana makubaliano hayo mara baada ya kusaini. 
  Waziri Mahiga akizungumza katika hafla hiyo.Katika hotuba yake Mhe. Mahiga alisisitiza kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana kwa karibu na Kenya na kwamba makubaliano yaliyosainiwa yataimarisha mahusiano hayo kwa kuboresha mazingira ya uwekezaji, kurahisisha ufanyaji biashara na kuongeza fursa za ajira kwa vijana wa nchi hizi mbili. 
  Waziri Amina naye akizungumza kwenye hafla hiyo. Katika hotuba yake aliahidi Kenya kuendelea kushirikiana na Tanzania kwa karibu katika masuala yote yaliyokubaliwa. 
  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi akitoa neno la shukrani katika hafla hiyo ya uwekaji saini Makubaliano ya Tume ya Pamoja ya Ushirikiano 
  Sehemu ya wajumbe kutoka Kenya waliohudhuria hafla ya uwekwaji saini wa Makubaliano ya Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya. Kulia ni Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Chirau Ali Mwakwere 
  Sehemu ya ujumbe wa Tanzania nao wakishuhudia uwekwaji saini katika makubaliano ya tume ya pamoja ya ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya. Kushoto ni Balozi Samwel Shelukindo, Mkurugenzi wa Idara ya Afrika akifuatiwa na Bw. Stephen Mbundi, Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masahriki 
  Mshereheshaji ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga akiwakaribisha wageni wakati wa hafla ya uwekaji saini Makubaliano ya Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya. 
  Sehemu ya maafisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Waandishi wa Habari waliohudhuria hafla hiyo. 
  Picha ya Pamoja

  0 0

  *Aagiza arudishwe Longido kujibu tuhuma zinazomkabili

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi aliyekuwa Mwekahazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido, Bw. Issai Mbilu ambaye kwa sasa amehamishiwa Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma na kuagiza arudishwe haraka na kuja kujibu tuhuma za ubadhilifu sh. milioni 642.4 za miradi zinazomkabili.

  “Tunaendelea kudhibiti na kuweka nidhamu ndani ya Serikali. Ukiharibu Longido usitegemee kuhamishiwa wilaya nyingine tunamalizana hapa hapa. Hatuwezi kuhamisha ugonjwa hapa na kuupeleka wilaya nyingine hivyo Mwekahazina huyu arudishwe haraka Longido,” amesisitiza.

  Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Ijumaa, Desemba 16, 2016) wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Arusha.

  Pia amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega kumuandikia barua Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) akimuomba amrudishe Mwekahazina huyo katika kituo chake cha kazi cha zamani ili aweze kujibu tuhuma zinazomkabili.

  Amesema Serikali haitamvumilia mtumishi wa idara yoyote atakayeharibu jambo halafu kuhamishwa sehemu nyingine, “hivyo naagiza kuanzia sasa nimemsimamisha kazi Mwekahazina huyu na arudi hapa kujibu kwanini ameleta hasara ya hizi fedha. Na nyie watumishi wengine hili liwe funzo kwenu,” amesema.

  Amesema miradi mingi ya maendeleo inakwama kwa sababu ya baadhi ya watumishi kuweka mbele maslahi binafsi badala ya kuzingatia maadili ya utumishi, hivyo amewaagiza Wakuu wa Idara wafuatilie kwa makini miradi inayotekelezwa katika maeneo yao kama inalingana na thamani halisi ya fedha zilizotolewa.

  Akizungumzia kuhusu kushamiri kwa biashara haramu ya dawa za kulevya wilayani Longido, Waziri Mkuu amewaagiza wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya kufanya kufanya msako wa nyumba hadi nyumba na kuwakamata wote watakaokutwa wanafanya biashara hiyo.

  “Wilaya hii ina sifa mbaya ya kuwa kitovu cha kusafirisha dawa ya kulevya zikiwemo bangi na mirungi. Hivyo nawaagiza wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama waendeshe msako kwa kila nyumba na atakayekamatwa achukuliwe hatua. Dawa za kulevya zinadhohofisha nguvu kazi ya Taifa,”.

  “Ukivuta bangi unapishana na kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu kwani unakwenda kulala jambo ambalo hatuwezi kulikubali. Watakaokutwa wanauza au kununua mirungi na bangi wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa pamoja na kutaifisha magari yanayotumika kubeba bidhaa hiyo haramu,” amesema.

  Awali, Mkuu wa Wilaya hiyo Bw. Daniel Chongolo akisoma Taarifa ya Wilaya amesema Longido inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kutumika kama njia kuu ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya bangi na mirungi kwenda nchi jirani ya Kenya ambako biashara hiyo imehalalishwa.

  Changamoto nyingine ni ukosefu wa hospitali ya wilaya hali inayofanya wananchi kwenda kutibiwa Kenya, ambapo Waziri Mkuu alisema haiwezekani wakakosa hospitali ya wilaya hivyo amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuhakikiusha anatenga fedha za ujenzi huo.

  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Serikali ipo mbioni kujenga kiwanda cha kuchakata madini ya magadi soda ili yawe na ubora na thamani kubwa. Ametoa kauli hiyo aliposimamishwa na wananchi katika kijiji cha Loonolwo kilichopo Kata ya Gelai Merugoi Wilayani Longido akitokea wilayani Ngorongoro.

  Amesema lengo la kujenga kiwanda hicho ni kuwawezesha wananchi wa wilaya hiyo hasa akinamama wanaoishi karibu na Ziwa Natron linalotoa magadi hayo waweze kunufaika na uwepo wa ziwa hilo.

  Waziri Mkuu amesema ujenzi wa kiwanda hicho utawezesha vijana na akinamama hao wanaouza magadi maeneo ya pembezoni mwa barabara katika ziwa Natron kupata ajira kwa kuwa kitazalisha ajira zaidi ya 500 katika wilaya hizo mbili za Longido na Ngorongoro.

  Pia amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Bw. Mrisho Gambo kushirikiana na wataalam wake kufanya tathimini ya uhaba wa chakula katika wilaya za Longido na Ngorongoro ili Serikali ijue Mkoa wa Arusha una ukosefu wa chakula kwa kiasi gani.

  "Gambo fanya tathimini ya hali ya njaa katika wilaya hizi mbili ili tuweze kuwasaidia wananchi hawa. Hata hivyo nawaomba wananchi mtunze kiasi cha chakula mlichonacho na marufuku tumia nafaka kwa ajili ya kupika pombe,” amesema.

  Awali, wananchi hao waliokuwa na mabango mbalimbali walilalamikia kero ya mipaka ya ardhi kati ya vijiji vya wilaya za Longido na Ngorongoro, ambapo Waziri Mkuu alimuagiza Afisa Ardhi Mkoa wa Arusha, Bw. Hamdoun Mansour kwenda katika vijiji hivyo vya mpakani na kukutana na viongozi wa kimila ili kumaliza mgogoro huo.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  IJUMAA, DESEMBA 16, 2016. 

  0 0


  Na Antony John Globu ya Jamii

  Kutokuielewa sheria kumeonekana kunaleta changamoto kubwa kwa jamii hali inayosababisha wananchi kukosa hakizao na kusababisha mlundikano wa kesi mahakamani.

  Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za mkuu wa mkoa leo, mkuu wa mkoa wa Dar es salaam,Paul Makonda amesema kutokana na changamoto hiyo serekali imeamua kupeleka wanasheria vijana watakao jitolea katika wilaya zote za dar es salaam ili kuwasaidia wananchi katika maswala ya kisheria.

  Makonda amesema kati ya changamoto zinazo wakabili wananchi wengi ni pamoja na malaamiko ya rushwa katika vyombo vinavyo toa haki, ucheleweshwaji wa kesi mahakamani, migogoro ya ardhi, migogoro ya ndoa, miradhi na waajiri kuwaachisha kazi waajiriwa bila kufuata taratibu.

  Aidha amewaambia wanasheria hao wametakiwa kutoa msaada wa kisheria kwa watu na makundi ya watu wasio na uwezo katika mashauri ya madai ya jinai, kushuhulikia malalamiko mbalimbali juu ya utoaji haki kutoka kwa wananchi na kuwaelekeza pamoja na kuwaelimisha wapi waende kupata suluhu ya haki zao.

  Hata hivyo mkuu huyo wa wilaya amesema swala la uandikaji wa miradhi ni changamoto kwa jamii hivyo nivyema wananchi wakapata msaada huo wa kisheria ili kupunguza changamoto mbalimbali za mashauri yanayohusiana na maswala ya miradhi.

  ‘’kati ya mambo munayotakiwa kufanya yaani wajibu wenu pia nipamoja na kuandika nyaraka tofauti za kisheria kama kuandika wosia, mikataba pamoja na kutoa msaada kwa njia ya simu’’ amesema makonda.
  Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wanasheria vijana watakao jitolea katika wilaya zote za Dar es salaam ili kuwasaidia wananchi katika maswala ya kisheria leo jijini Dar es Salaam. picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
  Mkuu wa Wilaya Temeke Mh.Felix Lyaniva akimshukuru Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwa ubunifu wake wakupeleka wanasheria katika kila wilaya zote za Dar es salaam ili kuwasaidia wananchi katika maswala ya kisheria leo jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wilaya na wanasheria leo jijini Dar es Salaam.

  0 0


  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akikaribishwa na Katibu wa Sekretarieti, Anamringi Macha, alipowasili leo jioni Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma kukabidhiwa rasmi Ofisi na aliyekuwa Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Ruhwavi.
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akikaribishwa na Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi alipowasili Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma leo jioni kwa ajili ya Luhwavi kumkabidhi Ofisini. Katikati ni Katibu wa Sekretarieti, Anamringi Macha.  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo (watatu kushoto), akifuatana na viongozi waandamizi wa CCM, kwenda ukumbini kwenye mazungumzo baada ya kuwasili Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma leo jioni kukabidhiwa ofisini. Kushoto ni Katibu wa Sekretarieti, Anamringi Macha, na wapili ni Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Ruhwavi
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM-Bara, Rajabu Luhwavi, wakisalimia Makatibu Muhtasi wa Ofisi ya Katibu Mkuu wa CCM na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, walipoingia katika ofisi ya Makatibu Muhtasi hayo kabla ya Mpogolo kufanya kikao na viongozi waandamizi wa Makao Makuu hayo ya CCM. Kushoto ni Evalida Mafuta na Elizabeth Mhina.
  Mpogolo na Luhwavi wakiwasili ukumbini kuzungumza na viongozi waandamizi wa Makao Makuu ya CCM.
  Mpogolo akisaini Kitabu cha wageni kabla ya mazungumzokuanza. Kulia ni Luhwavi


  Katibu wa Sekretarieti ya CCM, Anamringi Macha akikaribisha ugeni kabla ya mazungumzo ya Mpogolo na watumishi waandamizi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma
  Viongizi wakiwa tayari kwa kikao hicho na Mpogolo

  Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akizungumza kabla ya kumkaribisha Mpogolo kuzungumza

  Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Rajab Luhwavi akimkaribisha kuzungumza, Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo akizungumza na viongozi waandamizi wa Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma leo. katika mazungumzo hayo Mpogolo amewataka viongozi hao kumpa ushirikiano ili kuongoza vizuri, huku akisisitiza kuwa atakuwa akifanyakazi kwa kufuata mstari ulionyooka,na pale atakapokuwa akilazimika kusema hatakuwa akimung'unya maneno. Kulia ni Luhwavi.
  Katibu Msaidizi Mkuu katika Idara ya Utawala Ndigu Mdaki akitoa shukrani kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli kuwaletea CCM Mpogolo.
  Katibu Msaidizi Ndugu, Kazidi naye akitoa shukrani na maneno machache baada ya kupewa nafasi ya kuzungumza mwishoni mwa mazungumzo hayo
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo (watatu kushoto-walioketi) na Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi wakiwa katika picha ya kumbukumbu na viongozi hao waandamizi wa makao makuu ya CCM mwishoni mwa mazungumzo
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Mpogolo na Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM-Bara, Luhwavi wakiwa kakatika Ofisi ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, tayari kwa makabidhiano ya ofisi hiyo huku viongozi waandamizi wa Makao makuu ya CCM wakishuhudia.PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO-theNkoromo Blog

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Londoluo  waliomsimamisha akiwa njiani kutoka Loliondo kwenda Longido  mkoani Arusha Desemba 16, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa wilaya ya Longido baada ya kuwasili  kwenye Ofisi za Halmashauri hiyo Desemba 16, 2016.
   Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa  akizungumza na watumishi wa serikali na halmashauri ya wilaya ya Longido  kwenye ukumbi wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere  uliopo kwenye Ofisi za halmashauri hiyo Desemba 16, 2016.
    Baadhi ya watumishi wa serikali na halmashauri ya wilaya ya Longido  wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere uliopo kwenye Ofisi za halmashuri hiyo Desemba 16, 2016.
   Waziri  wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe  akiwasalimia  watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Longido kabla ya kumwalika Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa kuzungumza nao kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo wa Julius Kambarage Nyerere Desemba 15, 2016.
   Mkuu wa Wilaya ya  Longido , Daniel Chongolo,  akisoma taarifa ya maendeleo ya wilaya hiyo mbele ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye ukumbi wa halmashuri hiyo wa Julius Kambarage Nyerere Desemba 16, 2016.

  0 0

   Baadhi ya ng’ombe wa maziwa wa mradi wa ufugaji ngo’ombe na uzalishaji wa maziwa unaoendeshwa na watawa eneo la Narunyu wakiwa katika banda.
   Bi Yasinta Mrose (Mtawa) akimwonesha Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Florence Mwanri hatua za awali za kutengeneza gesi kwa kutumia kinyesi cha ng’ombe.
   Kaimu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, Florence Mwanri akiwa ndani ya chumba ambapo gesi inazalishwa (gesi ipo ndani ya turubai lililojaa ndani ya chumba hicho linaloonekana chini).
   Mwonekano wa Kiwanda cha kuzalisha nishati inayotokana na kinyesi cha ng’ombe.
  Ndama wanaofugwa katika mradi wa ufugaji ngo’ombe na uzalishaji wa maziwa unaoendeshwa na watawa eneo la Narunyu wakiwa katika banda.
  PICHA ZOTE NA ADILI MHINA, TUME YA MIPANGO

   Kaimu Katibu Mtendaji  Tume ya Mipango Bibi Florence Mwanri anayeongoza timu ya ukaguzi wa miradi kutoka Tume ya Mipango akielekea kukagua mradi wa ufugaji ngo’ombe na uzalishaji wa maziwa unaoendeshwa na watawa katika eneo la Narunyu wilayani Lindi. Kulia ni Bi, Yasinta Mrose (Mtawa) ambaye anasimamia upande wa mifugo.
   Kaimu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri akitoa ushauri kwa uongozi wa mradi ufugaji ngo’ombe na uzalishaji wa maziwa (ambao ni watawa) katika moja ya mabanda ya ng’ombe wa maziwa. Wengine ni maofisa wa Serikali walioambatana na Kaimu Katibu Mtendaji huyo.

  Na Adili Mhina, Lindi
  Tume ya Mipango imefanya ziara katika mradi wa ufugaji ngo’ombe na uzalishaji wa maziwa unaoendeshwa na watawa eneo la Narunyu wilayani Lindi na kushauri uongozi wa mradi huo kutumia fursa za mikopo ya kilimo ili kupanua wigo wa uzalishaji wa mazao ya mifugo pamoja na kuongeza uzalishaji wa nishati ya umeme kwa kutumia kinyesi cha wanyama.

  Mradi huo umekuwa ukizalisha maziwa na nyama kwa ajili ya biashara huku nishati ya umeme kwa ajili kuendesha shughuli za kiwanda hicho ikiwa inazalishwa kutokana na kinyesi cha wanayama hao.

  Kwa sasa uzalishaji umepungua baada ya kiwanda kushindwa kuzalisha nishati ya umeme ya kutosha na kuanza kutegemea umeme wa tanesco ambao kwa mujibu wa mmoja wa wasimamizi wa mradi huo, Bi Yasinta Mrose umesababisha gharama za uzalishaji kuongezeka. 

  Changamoto nyingine ni  kuharibika kwa baadhi mashine zinazotumika kuandaa malisho ya ngo’ombe, ukosefu wa soko la karibu kwa mazao ya nyama na maziwa, pamoja na uhaba wa maeneo kwa ajili ya malisho ambapo kwa sasa mradi una zaidi ya ng’ombe 400. 

  Kutokana na changamoto hizo, Kaimu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango Bibi Florence Mwanri aliueleza uongozi huo kuwa ni vyema wafanye taratibu za kuomba mkopo hususani katika benki ya kilimo ili waweze kuongeza mtaji, uzalishaji na kupanua soko. 

  “Huu ni mradi mzuri na msirudi nyuma katika uzalishaji wenu, nawashauri mkae mjadiliane muone namna ya kupata mkopo ili muweze kununua mashine za kisasa na muongeze uzalishaji. Bila kuchukua hatua hizo mnaweza mkashangaa mradi unakufa wakati unafaida kwenu na hata kwa wananchi wanaowazunguka,” alieleza.

  Kuhusu changamoto ya soko la karibu, Mwanri alieleza kuwa uongozi unapaswa kufikiria kuzalisha maziwa na kutengeneza bidhaa zinazotokana na maziwa na kusafirisha nje ya wilaya ya Lindi kwani soko bado ni kubwa.

  Aliongeza kuwa hatua iliyofikiwa ya kuzalisha umeme wa kutosha kuhudumia shughuli zote za uzalishaji kiwandani hapo ni nzuri na Serikali inaiunga mkono jitihada za sekta binafsi katika kukuza maendeleo ya uchumi ikiwa ni njia ya kutekeleza malengo ya Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016/17-2020/21). 

  “Nimefarijika sana kusikia mlikuwa mnazalisha umeme wa kuwatosheleza, mmejitahidi kutekeleza mpango wa Taifa wa Maendeleo kwa vitendo. Tume ya Mipango inatambua na kuunga mkono jitihada zenu hivyo nawasihi shirikianeni na Halmashauri kufanya kila linalowezekana ili shughuli zenu ziendelee zaidi ya mlivyokuwa mnazalisha huko nyuma,” aliongeza.


  0 0


  0 0

   Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akisalimiana na baadhi ya wazee wanaoishi katika kambi ya kulelea wazee ya Rasi Bula mkoani Lindi wakati wa ziara yake kujionea hali halisi ya kituo hicho.
   Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akiwa katika ziara ya kuangalia mazingira ya Shule ya kulelea watu wenye ulemavu ya Nyangao mkoani Lindi kulia kwake ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bw.Richard Mponda.
   Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akizungumza na baadhi ya walimu wa shule ya msingi ya Nyangao alipotembelea kuona hali halisi ya mazingira ya wanafunzi wenye wahitaji maalum Desemba 15, 2016.
    Mwalimu wa wasiona shule ya nyangao Bw.Nassoro Kambona akielezea changamoto wanazokabiliana nazo kazini kwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi (hayupo pichani) wakati wa ziara yake shuleni hapo.
   Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akijibu hoja za wazee wenye ukoma na mahitaji maalum katika kambi yao ya Nandanga wilayani ruangwa mkoa wa Lindi alipofanya ziara yake Desemba 15, 2016
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akitoa maagizo kwa baadhi ya watendaji wa Serikali wakati ya ziara yake Wilayani Lindi alipotembelea shule na Vituo vya kulelea watu wenye mahitaji maalum.
   Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Shaibu Ndemanga akizungumza wakati wa kikao cha kumkribisha Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi wakati wa ziara yake Mkoani hapo Desemba 15, 2016.
   Mwenyekiti wa Chama cha Wasioona Lindi Bw.Musa Bakari akizungumza changamoto zao kwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi wakati wa ziara yake mkoani Lindi Desemba15, 2016
  (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu Mhe.Jenista Mhagama

  Na Daudi Manongi 
  WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe.Jenista Mhagama amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Bw. Majid Mwanga kuhakikisha ana tatua mgogoro wa  ujenzi wa barabara ya Kiwangwa-Mabohelo  yenye urefu wa kilomita 15 na kumalizika mwishoni mwa mwezi huu.

  Ameyasema hayo jana Wilayani  wakati alipotembelea  miradi inayotekelezwa na Halmashauri  ya Wilaya ya Chalinze na Bagamoyo  kwa ufadhili wa Programu ya  Miundombinu ya  Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini(MIVARF)  inayosimamiwa na chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

  “Serikali ya Awamu ya Tano ina lengo kubwa la kuwasaidia wananchi hususani wakulima ili wafikiwe na miundombinu ili kupambana na umaskini na kuboresha masuala ya masoko yao na hivyo kuwaongezea kipato”, Alisema Mhagama.

  Aidha Mhe. Mhagama alisema kuwa asili ya miradi ya ufadhili wa Programu ya Miundombinu ya  Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) iliyo  chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu haina fidia hivyo  anashangaa kuona ni kwanini ujenzi vipande hivyo vitatu vya barabara vinachelewa kukamilika hadi kufikia leo.

  Ameongeza kuwa pesa za kumalizia mradi huo zipo na kusema kuwa tatizo kubwa lililopo ni kukosekana kwa mawasiliano kati ya Halmshauri za Bagamoyo na Chalinze na kuwaagiza Viongozi wa Halmashauri hizo chini na kumaliza mgogoro huu mara moja ili  wananchi wafanikishe lengo kuu la mradi huo ambao ni umwagiliaji.

  Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mhe.Ridhiwani Kikwete alisema kuwa tatizo kubwa  linalofanya mradi huo kutokamilika ni kutoshirikishwa kwa wananchi  na kuitaka halmashauri ya Bagamoyo kukaa pamoja na wao ili kupata ufumbuzi wa kudumu.

  Naye Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Bw.Majid Hemed Mwanga aliahidi kulipatia ufumbuzi tatizo la mgogoro huo ndani ya muda alioagizwa  kwa kuwashirikisha madiwani wote.

older | 1 | .... | 1071 | 1072 | (Page 1073) | 1074 | 1075 | .... | 1898 | newer