Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1070 | 1071 | (Page 1072) | 1073 | 1074 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Chama cha Madereva wa Serikali Tanzania (CMSP) mara baada ya kukutana na viongozi hao kwa lengo la kujadili masuala ya kiutendaji ofisini kwake leo.

  0 0

  The Board of Directors of the African Development Fund (ADF) has approved a loan of UA 67.27 million (USD 93.51 million) to the United Republic of Tanzania for on-lending to the Tanzania Agricultural Development Bank (TADB). The funding will contribute to supporting Tanzania’s agriculture sector and achieving the country’s development goals.
  The TADB is a national development finance institution, the mission of which is to develop the agriculture sector in Tanzania. The sector provides employment for about 67% of the population and has a very big potential for expansion given the abundance of arable land and the availability of inland water resources. However, the sector needs to be developed if Tanzania is to achieve sustainable economic development and poverty reduction. 
  Specifically, in order for the country to achieve the Sustainable Development Goals and its Tanzania Development Vision 2025, the agriculture sector must sustainably grow at over 10% per annum. Unfortunately, over the past ten years, the sector has grown at an average of 4.4% per annum and contributed an average of 29.3% of Gross Domestic Product (GDP). These rates have recently declined to 3.2% per annum and 26% of GDP (Q2 2016), respectively.
  A major problem facing the country’s agriculture sector is the unavailability of medium to long-term finance to support, among other things, agricultural production, processing and marketing. The TADB is designed to address this through the provision of much-needed funding to a sector that is key to the country’s development.
  Concluding his remarks following the Board discussions, the AfDB President Akinwumi Adesina underscored that: “The TADB is expected to play a key role in facilitating attainment of sustainable food self-sufficiency and food security in Tanzania and in promoting and supporting the transformation of agriculture from subsistence to commercial farming in order to effectively and sustainably contribute to inclusive economic growth and poverty reduction.”

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo wakati alipowasili kwenye  uwanja wa ndege wa Kiltaro katika tararafa ya Loliondo kuendelea na ziara yake wilayani Ngorongoro Desemba, 15, 2016. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wanawake wa Kimasai wakati alipotembelea Kituo mafunzo ya kazi za mikono na utamaduni kilichojengwa na UNICEF katika kijiji cha Ololosokwan kilichopo Loliondo wilayani  Ngorongoro Desemba 15, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama kazi mbalimbali za mikono hasa mapambo yanayotengenezwa na wanawake wa kimasai katika kijiji cha Ololosokwan katika tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro wakati alipotembelea Kituo cha Mafunzo ya kazi za mikono na utamaduni  kijijini  hapo Desemba 15, 2016.
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwa ndani ya nyumba ya asili ya wamasai maarufu kwa jina la Emanyatta katika kijiji cha Ololosokwan  kwenye tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro Desemba 15, 2016.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoka ndani ya nyumba ya asili ya wamasai maarufu kwa jina la emanyatta katika kijiji cha Ololosokwan kwenye tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro Desemba 15, 2016. 
   Wananchi wa kijiji cha Ololosokwan  kwenye tarafa ya  Loliondo wilayani Ngorongoro  wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipowasalimia akiwa ktika ziara ya wilaya ya Ngorongoro Desemba 15, 2016. 
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wanchi wa kijiji cha Ololosokwan katika tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro akiwa katika ziara ya mkoa wa Arusha Desemba 15, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  NA EVELYN MKOKOI  - DSM .

  Tawi la baraza la wafanyakazi katika Ofisi ya makamu wa Rais limetakiwa kuwa ndo sehemu sahihi ya kujadili na kutatua migogoro ya wafanyaki na siyo majukwaa ya siasa.

  Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Nchi anayeshughulikia masuala ya Muungano na Mazingira Mhe January Mkamba, Lipokuwa akizungumza na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi katika Ofisi ya Makamu wa Rais Mtaa wa Luthuli jijini dar es Salaam.

  Mhe.Makamba alisema kuwa vikao vya baraza la wafanyakazi vimekuwepo kisheria na ni muhimu wajumbe kukaa pamoja kujadili masuala ya msingi yanyowahusu watumishi kwani wao ndo waliowachangua hivyo, majadiliano yanayokuwepo katika vikao hivyo ni nyenzo muhimu ya kuondoa migogoro na migomo mahala pa kazi.

  “Nyie ni miongoni mwa watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais ambao kwa namna moja au nyingine mmeaminiwa na kukabidhiwa dhamana ya kuwawakilisha wenzenu katika chombo hiki muhimu, katika kuamua na kushauri Baraza juu ya masuala mbalimbali yanayolenga kuleta ufanisi na utulivu ndani ya Ofisi yetu.alisisita Makamba”.

  Aidha, Waziri Makamba alisema kwamba, Lengo la vikao vya Baraza ni kuleta ufanisi wa utendaji kazi mahala pa kazi kwa ajili ya manufaa ya Taifa kuelekezana, kushauriana na kukumbushana, kuhusu majukumu ya ofisi na ushiriki wa wafanyakazi katika kuyatekeleza na kuyasimamia, na aliongeza kwa kusema kuwa ni fursa ya kipekee ya kutafakari utendaji wa kazi na majukumu ya Ofisi kwa ujumla.

  Kikao hicho cha baraza la wafanyakazi cha Ofisi ya makamu wa Rais kimudhuriwa na wawakilishi kutoka TUGHE Taifa na Mkoa na Wawakilishi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Zanzibar. 
  Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rias Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akizungumza na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi la Ofisi ya Makamu wa Rais leo Jijini Dar es Salaam kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Professor Faustine Kamuzora na kulia ni Katibu wa Baraza hilo Bw. Isaya Kisiri.
  Katibu wa baraza la wafanyakazi Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Isaya Kisiri akifungua mkutano wa baraza hilo uliofanyika katika Ofisi ya Makamu wa wa Rais Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam.  (kushoto) ni Katibu Mkuu mstaafu Bw. Mubarak Abdul Wakil.
   Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Professor Faustin Kamuzora akimkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba aliyekaa katikati, katika Mkutano wa Baraza la wafanyakazi cha Ofisi Hiyo uliyofanyika Leo Jijini Dar es Salaam.
   Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Makamu wa Rais wakiimba kwa pamoja wimbo wa wafanyakazi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa wajumbe wa Baraza la wafanyakazi Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dar es Salaam leo.
  Katika Picha Sehemu ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais katika Mkutano wa baraza hilo jijini Dar Es Salaam leo. ( Picha na habari na Evelyn Mkokoi wa OMR)

  0 0

  Waendesha Boda Boda wakisubir abiria

  Na. Ahmad Mmow, Nachingwea.

  Waendesha pikipiki za kusafirisha abiria (bodaboda) wilayani Nachingwea wameaswa wasikubali kutumiwa na wanasiasa nakufanywa ngazi ya kufikia malengo yao yakisiasa.

  Wito huo ulitolewa hivi karibuni na mkurugenzi mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali ya kupambana na umasikini na utunzaji mazingira (APEC), Respicius Timanywa.Wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya usalama barabarani iliyofanyika katika kijiji cha Chiola wilaya ya Nachingwea.

  Timanywa alisema madereva bodaboda ni kundi lenye nguvu katika jamii kutokana na kuundwa na vijana. Hivyo baadhi ya wanasiasa wamekuwa natabia ya kuwalaghai ili wawaunge mkono kwa kuwataka washiriki kutekeleza vitendo vya uvunjifu wa sheria. Ikiwamo kushiriki maandamano na mikutano isiyo halali.

  Mkurugenzi huyo ambae taasisi yake inashugulika pia na kupunguza maafa kwa waendesha pikipiki, alisema vijana hawana budi kukataa kutumika kufanya vitendo vitakavyo vuruga amani na utulivu uliopo nchini kwa maslahi ya wanasiasa.


  Badala yake wajiwekee malengo ya kufikia maendeleo kwakufanya kazi kwa juhudi na maarifa."Anzisheni vikundi vya ujasiriamali na fungueni akaunti ili muweze kuungwa mkono na serikali, muweze kukopeshwa kupitia fedha za mifuko ya vijana na wanawake," alisisitiza Timanywa.

  Aidha alitoa wito kwa serikali iwatambue waendesha bodaboda kuwa nimiongoni mwa watu wanaoweza kuchangia uchumi wa taifa kupitia kazi wanayofanya, iwapo wataandaliwa mazingira mazuri ya kufanya kazi yao. Alibainisha mchango wa vijana hao utatokana na kodi kupitia kazi wanayofanya. Hata hivyo kwa mazingira ya sasa wanajiona kama wametengwa.

  "Sasa hivi hawana sehemu ya maalumu ya kuegesha pikipiki zao na hawana vituo, wanapigwa na jua na mvua ikinyesha wanahangaika, serikali iwajengee vituo wanaweza kuwa walipaji wazuri wa kodi," alisema Timanywa.Alisema kunahaja ya vijana wanaohitimu mafunzo kupewa leseni haraka ili waanze kulipa kodi na kuchangia pato la taifa. Hasa katika kipindi hiki ambacho serikali ipo katika harakati kubwa za kuleta maendeleo ya nchi kupitia ukusanyaji makini wa mapato na kuziba mianya wizi na ufisadi.

  Mbali na hayo, mkurugenzi huyo alitoa wito kwa serikali pitia jeshi la polisi kuendelea kutoa ushirikiano na taasisi ili kuendelea kuwapa elimu waendesha bodaboda. Kwani wasipopata elimu wataendelea kuwa chanzo cha ajali nakusababisha madhara kwa taifa kutokana na kupoteza nguvu kazi.Akiongeza kusema hata waendesha bodaboda watakuwa hawanufaiki na kazi hiyo. Kwasababu sehemu kubwa ya mapato yao yatatumika kulipa faini kwa kukiuka sheria za usalama barabarani.

  Nae ofisa tawala wa wilaya ya Nachingwea, Stephen Mbije, ambae alimuwakilisha mkuu wa wilaya hiyo, aliwaasa vijana hao kujiunga na mfuko wa jamii wa bima ya afya ili waweze kupata matibabu kwa gharama nafuu. Huku akiwaomba waanzishe vikundi vya ulinzi shiriki vya jamaii, ili kukabilina uhalifu katika maeneo yao.

  Kwa upande wake, katibu wa washiriki hao, Deograsia Litimba, alisema licha ya mafunzo hayo kuwafanya wazielewe sheria za usalama barabarani lakini pia yamesababisha wabaini kuwa sababu ya mahusiano hafifu baina yao na jeshi la polisi ni wao kutozitambua sheria.

  Huku akibainisha kuwa mafunzo hayo ambayo yalitolewa na APEC kwa kushirikiana na jeshi hilo yamesababisha wawe na mahusiano mema nakuwa wanafamilia. Mafunzo hayo ya wiki moja yalikuwa na washiriki 220 waliotoka katika za Mkoka, Kipara Mtua, Kipara Mnero, Chiola, Marambo, Ruponda na Mnero Ngongo.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza nawafanyabiashara ndogo ndogo marufu kama Machinga mtaa wa Kongo na kusikiliza kero zao leo jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza wafanyabiashara wa soko kuu la Kariakoo nakusikiliza kero zao leo jijiji Dar es Salaam.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akiwa na viongozi mbalimbli akikagua soko la Kariakoo.
  Ofisa Tawala wa wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo akifafanua jambo katika mkutano wawafanyabiashara ndogo ndogo Machinga mtaa wa Kongo leo jijiji Dar es Salaam.
  Wafanyabiashara na wananchi wakimsikiliza mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
  WAFANYABIASHARA ndogo ndogo wa Kariakoo wametakiwa kuuza bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya ndani ili kukuza uchumi wa viwanda. Hayo ameyasema leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipokutana na wafanyabiashara wandogo wandogo wa Kariakoo, amesema bidhaa zinazozalishwa katika viwanda vya ndani zikipata soko nchi itapata mapato pamoja na kukuza uchumi wa nchi yetu.

  Amesema serikali iko pamoja na wamachinga kuhakikisha wanafanya biashara kwa mujibu wa sheria kwa kuuza vitu vyenye ubora na wakibaini kuwepo kwa vitu ambavyo vinahatarisha maisha ya watanzania watachukuliwa hatua mara moja.

  Makonda amesema ni marufuku wageni kutoka nje ya nchi kufanyabiashara ya umachinga katika jiji la Dar es Salaam wao wanatakiwa kuleta utaalam tu. Aidha amewaasa wamachinga kuwafichua wale ambao wanaweka rebo katika bidhaa wakati hawazalishi wenyewe.

  Makonda amesema katika maeneo ambayo wanafanyia kazi wamachinga kufuata sheria na kanuni zilizowekwa bila kuharibu utaratibu.


  0 0

  Kampuni ya Intaneti ya Yahoo inasema wavamizi wa mitandao waliiba data za zaidi ya ya watumiaji wake bilioni moja.

  Tukio hilo linaaminika kufanyika mnano mwaka 2013.
  Katika taarifa yake, Yahoo inasema uvamizi huo wa taarifa muhimu ni tofauti na ule ulioripotiwa mwezi Septemba mwaka huu, ambapo wavamizi hao waliiba taarifa kutoka kwenye akaunti mbalimbali za watumiaji zaidi ya milioni mia tano.

  Imeongeza kuwa data zilizoibiwa zinajumuisha majina, anuani, namba za simu,tarehe za kuzaliwa pamoja na nywila (namba za siri).
  Lakini kadi za malipo sambamba na akaunti za benki hazikuingiliwa.

  Tazama hii video hapa chini

  0 0  0 0

  Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Nandi Mwiyomella(kushoto)akimsikiliza Msanii wa muziki wa kizazi kipya wa bongo fleva,Diamond Platinumz(kulia)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa hafla fupi ya kutanga tamasha la”Nogesha Upendo”yatakayofanyika Disemba 24 katika fukwe za Jangwani Sea Breeze jijini Dar es Salaam na Disemba 25 Iringa katika uwanja wa Samora chini ya udhamini wa Vodacom Tanzania.
  Msanii wa muziki wa kizazi kipya wa bongo fleva,Diamond Platinumz(katikati)akipiga selfie na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania mara baada ya mkutano na waandishi wa habari(hawapo pichani)kuhusiana na tamasha la”Nogesha Upendo”litakalofanyika Disemba 24 katika fukwe za Jangwani Sea Breeze jijini Dar es Salaam na Disemba 25 Iringa katika uwanja wa Samora chini ya udhamini wa Vodacom Tanzania.
  Baadhi ya wasanii wa nembo ya WCB wakiongozwa na Diamond Platinumz wakiwasili katika makao makuu ya Vodacom Tanzania,yaliyopo Mlimani city jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na tamasha la”Nogesha Upendo”litakalofanyikaDisemba 24 katika fukwe za Jangwani Sea Breeze jijini Dar es Salaam na Disemba 25 Iringa katika uwanja wa Samora chini ya udhamini wa Vodacom Tanzania.

  Katika mwendelezo wake wa kuwapatia wateja wake na watanzania wote kwa ujumla burudani za sikukuu, Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na wasanii wa WCB imeandaa matamasha mawili ya kukata na shoka ambayo yatafanyika katika msimu huu wa sikukuu.

  Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Nandi Mwiyomella, alisema matamasha hayo makubwa ya muziki wa kizazi kipya yatafanyika katika mikoa ya Dar e salaam na Iringa chini ya wasanii Diamond Platinumz, Rayvanny , Rich Mavoko, Harmonize na Queen Darleen.

  “Kama mnavyoelewa msimu huu huwa umeambatana na shamrashamra mbalimbali za sikukuu na mitoko ukiwa na familia yako, Desemba 24 kutashushwa shoo ya Nguvu katika fukwe za Jangwani Sea Breeze Hotel ambapo kutakua na tamasha la kihistoria la “Vodacom Wasafi Beach Party” na Iringa tamasha litafanyika siku ya Krismasi katika uwanja wa Samora na Matamasha yote yataanza saa nane mchana”.Alisema.

  Mwiyombella alisema burudani hii ya muziki inakwenda sambamba na promosheni ya Nogesha Upendo ya Vodacom inayolenga kuwapatia wateja wote wa mtandao wa Vodacom zawadi za sikukuu ikiwa ni shukrani kwa wateja ambapo pia wateja wanayo fursa ya kujishindia tiketi za bure za kushiriki katika matamasha haya makubwa katika msimu huu wa sikukuu.

  “Ili kujishindia tiketi ya bure anachotakiwa kufanya mteja wa Vodacom ni kupiga*149*01# kisha nunua kifurushi chochote cha Vodacom na moja kwa moja utakua umeingia katika droo ya kuweza kujishindia tiketi yako. Zawadi nyingine kem kem kupitia promosheni ya Nogesha Upendo ni fedha taslimu , muda wa maongezi, Vifurushi vya intaneti (Mb)”.Alisema.

  Naye Msanii wa muziki wa kizazi kipya anayetamba katika anga za kimataifa,Diamond Platinumz akiongea kwa niaba ya wasanii wa WCB alitoa wito kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam na Iringa kujitokeza kwa wingi siku ya shoo hizo kwani zitakuwa ni shoo za kihistoria katika mikoa hii miwili kufanywa na Vodacom kwa kushirikiana na WCB,Napenda kuwahakikishia mashabiki wetu kwamba tutakamua vilivyo tukiwa na wasanii wenzangu wote wa WBC kwa “Kunogesha Upendo” Alisisitiza Diamond.

  0 0

    Katibu mkuu wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji, anayeshughulikia Biashara na uwekezaji mhe. Prof. Adolf Mkenda (katikati) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi. Halima Dendegu alipomtembelea leo ofisini kwake na kuanza ziara yake mkoani humo.
   Katibu mkuu wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji, anayeshughulikia Biashara na uwekezaji Mhe. Prof. Adolf Mkenda (kushoto) akizungumza jambo na kaimu mkurugenzi wa bodi ya Korosho Tanzania, Hassan M. Jarufu. Katibu mkuu yuko katika ziara ya kusikiliza changamoto za korosho, maghala, vipimo na masoko mkoani Mtwara.
    Katibu mkuu wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji, anayeshughulikia Biashara na uwekezaji Mhe. Prof. Adolf Mkenda akikagua karakana ya ukaguzi wa mizani katika ofisi ya Wakala wa Vipimo Mkoani Mtwara.
  Katibu mkuu wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji, anayeshughulikia Biashara na uwekezaji mhe. Prof. Adolf Mkenda

  0 0

  Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF) limeadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa (1946-2016) likiwa na kauli mbiu ya Kwa Kila Mtoto, Tumaini. Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Bi. Maniza Zaman alisema shirila lao kwa kipindi cha miaka 70 limekuwa likifanya kazi za kuwasaidia watoto ambapo malengo yao ni kuhakikisha watoto wanaishi maisha bora na kuwawezesha kufikia malengo ambayo wanatamani kuyafikia. 
  Mwakilisha wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini, Bi. Maniza Zaman akielezea kazi ambazo UNICEF imekuwa ikizifanya kwa miaka 70 tangu kuanzishwa na mafanikio ambayo wameyapata.

  "Hii ni siku muhimu kwetu kufikisha miaka 70, ni muhimu kwa sababu ya malengo ambayo yamewekwa ya kujenga dunia ambayo kila mtoto atapata haki zake za kimsingi bila kumuacha hata mmoja nyuma ni muhimu sababu ya uwepo wenu kujadili umuhimu wa watoto ambao utatoa matumaini mapya kwa kila mtoto Tanzania, "Kwa miaka 70 UNICEF imekuwa ikiwatetea watoto, kwa pamoja tukishirikiana na wadau wetu kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha tunaboresha maisha ya kila mtoto duniani kote. Mpango wetu upo wazi kuwa kuhakikisha kila mtoto anapata nafasi ya kufikia malengo yake," alisema Zaman. Nae Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema UNICEF ni washirika wazuri wa serikali kutokana na programu ambazo wamekuwa wakitoa kwa watoto na kuwaomba kuendelea kushirikiana na serikali ili kuboresha maisha ya watoto nchini. 
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza faida ambazo Tanzania imepata kutokana na uwepo wa UNICEF nchini pamoja na kumshukuru Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi kwa kusaini mkataba ambao uliwaruhusu UNICEF kuingia nchini kwa ajili ya kuwasaidia watoto.

  "Serikali ya Tanzania itaendelea kulinda na kutetea haki za watoto na katika utekelezaji wa hili tunawashukuru sana UNICEF kwa programu ambazo wamekuwa wakizifanya, watoto wa Tanzania wamefaidika sana na programu ambazo UNICEF mnazitoa na serikali itaendelea kushirikiana na UNICEF kuwasaidia watoto nchini," alisema Mwalimu. Kwa upande wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN), Alvaro Rodriguez alisema UNICEF imesaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha maisha ya watoto duniani kote tangu ilipoanzishwa na kupitia mpango wa SDGs ni matumaini ya UN kuwa serikali ya Tanzania kwa kushirikiana nanyi zitaendelea kushirikiana ili kuwasaidia watoto. 
  Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN), Alvaro Rodriguez akielezea jinsi UNICEF ambavyo natekeleza mipango ya Umoja wa mataifa kwa kuanza na mpango wa kwanza wa Millenium Development Goals (MDGs) ambao ulimalizika mwaka 2015 na mpango wa sasa wa maendeleo endelevu (Sustainable Development Goals - SDGs).

  "Mchango wa shirika hili la watoto ni mkubwa, muhimu na wenye thamani kubwa sana katika dunia ya leo na kesho, kwa miaka 15 iliyopita tulikuwa na mpango wa MSDs ambao ulishughulikia changamoto ambazo zinawakabili watoto na sasa kuna mpango wa SDGs ambao tumekusudia ufanye mageuzi makubwa kwa maendeleo ya baadae ya binadamu wakiwepo watoto, na Tanzania kama mwanachama wa UN ina wajibu wa kuhakikisha inafanikisha hilo," alisema Rodriguez. 
  Rais wa pili wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi akitoa pongezi kwa UNICEF kwa kazi ambazo wanafanya za kuwasaidia watoto ili waishi katika mazingira bora.

  Nae mgeni wa heshima katika maadhimisho hayo, Rais wa pili wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi aliipongeza UNICEF kwa kufikisha miaka 70 na kusema kuwa "Nilihusika kukubali UNICEF kufanya kazi nchini na leo sijuitii hilo kwa kazi ambayo mnaifanya, niwatie moyo muendelee na kufanya kazi kwa kuwasaidia watoto." 
  Baadhi ya watu waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 70 ya kuanzishwa shirika la UNICEF.

  0 0


  0 0

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiongea na wadau mbalimbali katika uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es Salaam leo.
   Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akizindua Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es Salaam leo.
   Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dr. Albina Chuwa akiongea na  wadau mbalimbali katika Uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es Salaam leo.
   Meneja wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii Sylivia Meku akielezea kwa wadau wa afya Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es Salaam leo.
   Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dr. Albina Chuwa kabla ya uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es Salaam leo, katikati ni Kaimu Katibu Mkuu  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dr. Mohamed Ally.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja wadau mbalimbali wa Takwimu na Afya katika uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa Afya ya Mzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa Mwaka 2015-16 Tanzania jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Benjamin Sawe- Maelezo)

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
  Waziri wa Afya na Maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto, Ummy Mwalimu, amesema kuwa Utafiti unasema kuwa kiwango cha maambukizi ya Malaria kwa watoto chini ya mwaka mmoja kuwa malaria bado ni mojawapo ya magonjwa yanayoongoza kwa kusababisha vifo vya watoto Nchini.

  Ummy amesema hayo jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa taarifa ya utafiti wa afya ya uzazi na mtoto na Malaria Tanzania ya mwaka 2015-16 (TDHS-MIS), katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.

  “ asilimia kubwa ya vifo vya watoto na akina mama wajawazito. Kiwango cha maambukizi ya malaria kwa watoto chini ya mwaka mmoja kimeongezeka kutoka asilimia 14 mwaka 2015/16 ukilinganisha na asilimia (9) ya mwaka 2010 kwa kutumia kipimo cha kutoa matokeo kwa haraka yaani Rapid Diagnostic Tests (RDT)” amesema Waziri Ummy.

  Ameongeza kuwa anatambua kwamba, suala hili limeshaanza kufanyiwa kazi ndani ya Wizara na niwaombe wadau wote tushirikiane kwa pamoja katika kuendeleza juhudi zilizopo za kuhakikisha Malaria inamalizwa hapa Tanzania. Hivyo natambua Mpango wa Kudhibiti Malaria Tanzania (NMCP) upo katika utekelezaji wa awamu nyingine ya kusambaza vyandarua katika Kaya za Tanzania, tunategemea juhudi hizi na nyingine zinazofanywa na wadau wengine zitachangia kupunguza kiwango cha Malaria hapa nchini.

  Katika hatua nyingine Waziri Ummy ameweza kuzungumzia tatizo la Mimba za utoto kwa watoto wa kike walio na miaka 15 hadi 19 na kusema kuwa matokeo yanaonesha kuwa asilimia 27 ya wasichana wenye umri wa miaka 15 hadi 19 wa mwaka 2015/16 wameshaanza kuzaa kulinganisha na asilimia 23 ya mwaka 2010.

  Ameongeza kuwa bado hii ni changamoto ambayo sote kwa pamoja tunatakiwa kukabiliana nayo kwa kutoa elimu zaidi ili kupunguza kiwango hiki na kuwezesha watoto wa kike waweze kupata muda wa kusoma na kujiendeleza katika kujiandaa na maisha yao ya baadae. Hivyo, Serikali itaendelea kutoa elimu juu ya madhara yanayoweza kutokea kwa wasichana kuzaa wakiwa bado wadogo

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamko Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Auai wakiwa katika Kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.
   Wajumbe wa Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar wakiwa katika kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja,chuini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamko Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamko Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiendesha Kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja,(kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Auai.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamko Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiendesha Kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.
  Baadhi ya Wajumbe wa Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar wakimsikiliza Mwenyekiti wa kikao hicho cha siku moja Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamko Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein,kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja (Picha na Ikulu.)

  0 0  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi , Marceline Ndimbwa amelazimika kufanyia kazi nje ya ofsi kutokana kukumbwa na majukumu ya kusimamia ujenzi wa madarasa ili kuenenda na kasi ya Rais John Pombe Magufuli aliyemuagiza kumaliza ujenzi huo ndani ya mwezi huu.

  Katika hali isiyo ya kawaida Mkurugenzi huyo ambaye ameonekana katika eneo la ujenzi akiendelea na kazi zingine za kiofsi huku akiwa na lundo la mafaili ambayo alikuwa akiyasaini hili kuweza kuruhusu shughuli zingine za kiofisi zikiendelea.

  Kwa upande wake Mkurugenzi huyo alipo ulizwa juu ya swala hilo amesema kuwa jambo ni la kawaida katika mazingira ya kazi,kwani jambo moja haliwezi kukwamisha shughuli nyingine zisiendelee wakati wananchi wana mahitaji ya haraka.

  Amesema kuwa Rais alimuagiza kuhakikisha kuwa ujenzi huo unakamilika kwa wakati hivyo yeye kama mteule anahakikisha kuwa anatekeleza agizo hilo kwa wakati hili watu wa Malinyi waweze kunufaika na ahadi za Rais Magufuli.

  Amemaliza kwa kutoa wito kwa wakazi wa malinyi kuwa na imani na serikali yao ambayo kipaumbele chake ni kutumikia wanyonge kwa kurekebishe miundombinu ya elimu kwa kipindi kifupi.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Khatibu Malimi Kazungu kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wa pili kutoka kulia, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango wakwanza kushoto, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Doto James wakwanza kulia pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Khatibu Malimi Kazungu Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU  0 0

   
  Wyre has a new music video out #wyreworkandplay

  Kevin Waire better known as Wyre Da Love Child is a Kenyan R&B and reggae musician from known from the some of the most popular groups in music history- Necessary Noize and East African Bashment Crew as well as a solo artist.

  With four albums out, namely “Defination of a Love Child”, “10 Years Wiser”, “Re-Wyred” and he recently released “Lion” just to be sure of cementing his well founded legacy.

  Giving something new this time the dancehall maestro teams up with popular turn table doctor DJ Protege to bring you this fire hit release,“Work and Play” the new song is a simple feel good track that this two musical geniuses have teamed up together to remind you to have fun after work.The video was shot in the US,Atlanta.

  Produced by Dj Protege and the video directed by Morgan Cashboy Films based in Atlanta,US watch the video here

  Follow Muziki Kenya & Wyre on twitter here


  0 0


  Mkurugenzi wa Mradi wa Ujenzi Kijiji cha Utalii Matemwe Zanzibar Pennyroyal Gibraltar Limited Zanzibar Amber Resort Mr. Saleh Mohammed Said akizungumza kabla ya kuaza kwa hafla hiyo ya utilianaji wa Saini ya Ujenzi wa Mradi huo na Kampuni ya MCC Overseas Ltd ya China, hafla hiyo ya utianaji wa saini hyo umefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Park Hyyat Shangani Zanzibar.
  Mkurugenzi wa Mradi wa Ujenzi Kijiji cha Utalii Matemwe Zanzibar Pennyroyal Gibraltar Limited Zanzibar Amber Resort Mr. Saleh Mohammed Said akizungumza kabla ya kuaza kwa hafla hiyo ya utilianaji wa Saini ya Ujenzi wa Mradi huo na Kampuni ya MCC Overseas Ltd ya China, hafla hiyo ya utianaji wa saini hyo umefanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Park Hyyat Shangani Zanzibar.kulia Mkurugenzi Mkuu wa Pennyroyal Gibraltar Limited Mr Brian Thomson akiwa na Mwenyekiti wa Kampuni ya MCC Overseas Limited ya China Mr Leo Zou.wakiwa katika ukumbi wa hafla hiyo.
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Pennyroyal Gibraltar Limited "Zanzibar Amber Resort" Mr Brian Thomson na kulia Mwenyekiti wa Kampuni ya MCC Overseas Limited ya China Mr. Leo Zou, wakitiliana saini ya ujenzi wa Mradi huo wa Kijiji cha Utalii Matemwe Zanzibar Mkoa wa Kaskazini Unguja. akishuhudia utilianaji wa saini hiyo katikati Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar Mr. Khamis Mussa.
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Pennyroyal Gibraltar Limited "Zanzibar Amber Resort" Mr Brian Thomson na kulia Mwenyekiti wa Kampuni ya MCC Overseas Limited ya China Mr. Leo Zou, wakibalishano mikatabaa hiyo baada ya kusaini.ujenzi wa Mradi huo wa Kijiji cha Utalii Matemwe Zanzibar Mkoa wa Kaskazini Unguja. akishuhudia utilianaji wa saini hiyo katikati Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar Mr. Khamis Mussa.
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Pennyroyal Gibraltar Limited "Zanzibar Amber Resort" Mr Brian Thomson, akizungumza wakati wa hafla hiyo ya utilianaji wa saini iliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Park Hyyat Shangani Zanzibar na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali katika hafla hiyo.
  Mwenyekiti wa Kampuni ya MCC Overseas Limited ya China Mr. Leo Zou, akizunguma baada ya hafla ya utilianaji wa saini ujenzi wa mradi wa Kijiji cha Utalii cha Matemwe Zanzibar
  Wageni waalikwa wakifuatila hafla hiyo ya utilianaji wa saini baina ya Pennyroyal Gibraltar Limited na MCC Overseas Limited ya China itakayojenga majengo ya Mradi huo huko Matemwe Zanzibar. Mkoa wa Kaskazini Unguja.
  Wawakilishi wa Kampuni ya MCC Overseas limited ya China wakifuatilia hafla hiyo.
  Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar Ndg Khamis Mussa akizungumza baada ya hafla hiyo utilianaji wa saini baina ya Kampuni ya Pennyroyal na MCC Overseas.
  Waalikwa wakiwa katika hafla hiyo.
  Wageni waalikwa wakifuatilia hafla hiyo
  Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar Ndg Khamis Mussa akimsikiliza Mwenyekiti wa MCC Overseas Mr. Leon Zou, wakibadilishana mawazo baada ya hafla hiyo.
  Muwekezaji wa Mradi wa Pennyroyal Zanzibar Mr Brian Thomson akizungumza na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar Ndg Khamis Mussa, baada ya kumalizika kwa hafla ya utilianaji wa saini.

  Wafanyakazi wa Pennyroyal wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaslizika kwa hafla hiyo.
  Mkurugenzi Mkuu Pennyroyal Mr Brian akibadilisha mawazo na wageni wakati wakati wa kupata viburudisho katika viwanja vya hoteli hiyo.
  Wageni waalikwa wakiwa katika viwanja vya hoteli Park Hyyat wakipata vitafunio baada ya hafla hiyo.
  Kikundi cha Taarab cha Dulla Ganuni kikitoa burudani wakati wa hafla hiyo. katika viwanja vya Park Hyyat Shangani Zanzibar


  Imeandaliwa na OthmanMapara.blog.


  Zanzinews.com


  othmanmaulid@gmai.com


  0777 424152 0715424152


  0 0

  Bi.Deograsia Ndunguru ambaye ni Kaimu Mkuu wa Idara ya Sanaa na Habari, Chuo Kikuu Dodoma UDOM, hii leo akiwasilisha mada kwenye mafunzo ya siku tatu kwa wanatasnia wa filamu na maigizo mkoani Mara, yaliyoanza jana ukumbi wa shule ya Sekondari Mara. Mafunzo hayo yameandaliwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia Bodi ya Filamu nchini.
  #BMGHabari
  Mtendaji Mkuu Taasisi ya Sanaa Bagamoyo, Dkt.Herbert Makoye, hi leo akiwasilisha mada kwenye mafunzo ya siku tatu kwa wanatasnia wa filamu na maigizo mkoani Mara, yaliyoanza jana ukumbi wa shule ya Sekondari Mara.
  Wanatasnia wa filamu na maigizo mkoani Mara wakifuatilia mada kutoka kwa Mtendaji Mkuu Taasisi ya Sanaa Bagamoyo, Dkt.Herbert Makoye.
  Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Bi.Joyce Fissoo (kushoto), akizungumza wakati wa mafunzo hayo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo jana. Baada ya ufunguzi alishiriki na wadau wengine mafunzo hayo.
  Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, akizungumza kwenye mafunzo kwa wadau wa filamu na maigizo mkoani Mara, hii leo. Kutoka kushoto ni Mtendaji Mkuu Taasisi ya Sanaa Bagamoyo, Dkt.Herbert Makoye, Bi.Deograsia Ndunguru ambaye ni Kaimu Mkuu wa Idara ya Sanaa na Habari, Chuo Kikuu Dodoma UDOM na Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Bi.Joyce Fissoo
  Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba (kuhoto) akiwa pamoja na Afisa Utamaduni Halmashauri ya Musoma Vijijini, Twalib Kamugisha (kulia) wakifuatilia mafunzo kwa wanatasnia wa filamu na maigizo mkoani Mara.
  Afisa Utamaduni Halmashauri ya Musoma Vijijini, Twalib Kamugisha (kushoto) akiwa pamoja na Katibu wa Chama cha Waigizaji mkoani Mara TDFAA, Johnson Ibambai maarufu kama Dunia (kulia), wakifuatilia mafunzo kwa wanatasnia wa filamu na maigizo mkoani Mara
  Wanatasnia wa filamu na maigizo mkoani Mara, wakiwa kwenye mafunzo ya filamu yanayotolewa na Bodi ya Filamu mkoani humo.
  Bodi ya Filamu nchini imewataka wadau wa sekta hiyo kuwasilisha miswada ya kazi zao ili kukaguliwa kabla ya kuanza kuigiza ili kuondona na usumbufu wa kuzifungia kazi zisizo na maadili.

  Katibu Mtendaji wa bodi hiyo, Joyce Fissoo, ametoa kauli hiyo kwenye mafunzo ya siku tatu kwa wanatasnia ya filamu mkoani Mara, yanayofanyika Mjini Musoma.

  Amesema hatua hiyo itasaidia kuondoa usumbufu wa ambao umekuwa ukijitokeza kwa baadhi ya miswada ya filamu kurekodiwa kabla ya kukaguliwa na baadaye filamu zake kuzuiliwa wakati wa kuingia sokoni hivyo kuibua usumbufu mkubwa.

  Wakiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo, Dkt.Herbert Makoye kutoka Taasisi ya Sanaa Bagamoyo pamoja na Deograsia Ndunguru kutoka Chuo Kikuu Dodoma, wamewahimiza wanatasnia wa filamu kuzingatia weledi katika uandaaji wa kazi zao kwa kuzingatia maudhui bora pamoja na maandalizi yanayokidhi uhitaji.

  Washiriki wa mafunzo hayo wameelezea umuhimu wake ambapo wamesema yatawasaidia kuboresha uzalishaji wa kazi zao ikiwemo kuzingatia maudhui bora tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
  Bonyeza HAPA kujua zaidi

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya mambo ya Nje wa Slovenia hapa nchini, Stanslav Vidovic, aliyemtembelea leo, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo, Desemba 15, 2016. (Picha na Bashir Nkoromo)
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya mambo ya Nje wa Slovenia hapa nchini, Stanslav Vidovic, aliyemtembelea leo, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo, Desemba 15, 2016. (Picha na Bashir Nkoromo).

older | 1 | .... | 1070 | 1071 | (Page 1072) | 1073 | 1074 | .... | 1897 | newer